Jumanne, 9 Januari 2018

NYIMBO ZA KRISTO



001 - U Mtakatifu,

1
U Mtakatifu! Mungu Mwenyezi!
Alfajiri sifa zako tutaimba,
U Mtakatifu, Bwana wa huruma,
Mungu wa vyote, hata milele.

2
U Mtakatifu! Na malaika,
Wengi sana wanakuabudu wote.
Elfu na maelfu, wanakusujudu,
Wa zamani na hata milele.

3
U Mtakatifu! Ingawa giza,
Lakuficha fahari tusiione,
U Mtakatifu! Wewe peke yako,
Kamili kwa uwezo na pendo.

002 - Twamsifu Mungu

1
Twamsifu Mungu, Mwana wa upendo,
Aliyetufia na kupaa juu.

CHORUS:
Aleluya! usifiwe, Aleluya! Amin;
Aleluya! usifiwe, utubariki.

2
Twamsifu Mungu, Roho Mtukufu,
Akatufunulia Mwokozi wetu.

3
Twamsifu Mwana, aliyetufia,
Ametukomboa na kutuongoza.

4
Twamsifu Mungu, wa neema yote,
Aliyetwaa dhambi akazifuta.

5
Tuamshe tena, tujaze na pendo,
Moyoni uwashe moto wa Roho.

003 - Mungu Atukuzwe

1
Mungu atukuzwe, kwa mambo makuu,
Upendo wake ulitupa Yesu,
Aliyejitoa maisha yake,
Tuwe nao uzima wa milele.

CHORUS:
Msifu, msifu, dunia sikia,
Msifu, msifu watu wafurahi,
Na uje kwa Baba, kwa Yesu Mwana,
Ukamtukuze kwa mambo yote.

2
Wokovu kamili, zawadi kwetu,
Ahadi ya Mungu kwa ulimwengu,
Wanaomwamini na kuungama,
Mara moja wale husamehewa.

3
Alitufundisha mambo makuu,
Alihakikisha wokovu wetu,
Lakini zaidi ajabu kubwa,
Yesu atakuja na tutamwona.

004 - Jina la Yesu, Salamu

1
Jina la Yesu, salamu! lisujudieni,
Ninyi mbinguni, hukumu na enzi mpeni.
Ninyi mbinguni, hukumu na enzi mpeni.

2
Enzi na apewe kwenu, watetea dini;
Mkuzeni Bwana wenu, na enzi mpeni.
Mkuzeni Bwana wenu, na enzi mpeni.

3
Enyi mbegu ya rehema, nanyi msifuni
Mmeponywa kwa neema, na enzi mpeni.
Mmeponywa kwa neema, na enzi mpeni.

4
Wenye dhambi kumbukeni, ya msalabani.
Kwa furaha msifuni, na enzi mpeni.
Kwa furaha msifuni, na enzi mpeni.

5
Kila mtu duniani msujudieni,
Kote-kote msifuni, na enzi mpeni.
Kote-kote msifuni, na enzi mpeni.

6
Sisi na wao pamoja tu mumo sifani.
Milele sifa ni moja, ni enzi mpeni.
Milele sifa ni moja, ni enzi mpeni.

005 - Na Tumwabudu Huyo Mfalme

1
Na tumwabudu huyo Mfalme,
Sifa za nguvu zake zivume;
Ni ngao, ni ngome, Yeye milele,
Ndizo sifa zake kale na kale.

2
Tazameni ulimwengu huu,
Ulivyoumbwa, ajabu kuu;
Sasa umewekwa pahali pake,
Hata utimize majira yake.

3
Kwa ulinzi wako, kwetu Bwana,
Twakushukuru, U mwema sana;
Hupewa chakula kila kiumbe,
Kila kitu kina mahali pake.

4
Wanadamu tu wanyonge sana,
Twakutumaini Wewe, Bwana;
Kamwe haupungui wako wema,
Mkombozi wetu, Rafiki mwema.

006 - Kumekucha kwa Uzuri

1
Kumekucha kwa uzuri, nafumbua macho,
Baba amenihifadhi, ni wake mtoto.

2
Bwana niwe leo kutwa, ulinzini mwako,
Nisamehe dhambi, niwe mikononi mwako.

3
Roho wako anikae, moyoni daima,
Anitakase nione, uso wako mwema.

007 - Mungu Msaada Wetu

1
Mungu Msaada wetu, tangu miaka yote,
Ndiwe tumaini letu, la zamani zote.

2
Kivuli cha kiti chako, ndiyo ngome yetu,
Watosha mkono wako, ni ulinzi wetu.

3
Kwanza havijakuwako, nchi na milima,
Ndiwe Mungu, chini yako twakaa salama.

4
Na miaka elfu ni kama, siku moja kwako;
Utatulinda daima, tu raia wako.

5
Bwana Msaada wetu tangu miaka yote,
Mlinzi wetu na ngome, daima, milele.

008 - Unisikie Ninapolia

1
Unisikie ninapolia, uje Mkombozi,
Moyo wangu hukutazamia, uje Mkombozi.

CHORUS:
Nimepotea mbali na kwangu, nimetanga peke
yangu, Unichukulie sasa kwako, uje Mkombozi.

2
Sina pahali pa kupumzika, uje Mkombozi,
Unipe raha, nuru, uzima, uje Mkombozi.

3
Nimechoka, Njia ni ndefu uje Mkombozi,
Macho yako kuona nataka, uje Mkombozi.

4
Bwana, daima hutanidharau, uje Mkombozi, Kilio
changu utanijibu, uje Mkombozi.

009 - Mwumbaji Mfalme

1
Mwumbaji Mfalme, vitu vyote vyako,
Ni kwa ukarimu wako ninabarikiwa,
Ni kwa ukarimu wako ninabarikiwa.

2
Uliyeniumba, Nakutegemea,
Sina budi kuzisifu hisani zako kuu,
Sina budi kuzisifu hisani zako kuu.

3
Nitatoa Nini? Kwanza vyote vyako,
Upendo wako wadai moyo wa shukrani,
Upendo wado wadai moyo wa shukrani.

4
Nipewe neema, Niwe na uwezo,
Wa kuishi kwako, Bwana siku zangu zako,
Wa kuishi kwako, Bwana siku zangu zako.

010 - Kristo wa Neema Yote

1
Kristo wa neema yote, imbisha moyo wangu,
Mifulizo ya baraka, inaamsha shangwe kuu,
Unifunze nikupende, nikuandame kote,
Moyo wangu ukajae, furaha na tumai.

2
Namshukuru sana Bwana, aniwezesha huku.
Salama aniongoza, hata kule nyumbani,
Yesu alinitafuta, njiani mbali kwake,
Akatoa damu yake, nipone hatarini.

3
Kweli mimi mwiwa mkubwa, wa neema daima
Wema wako unifunge, zaidi kwako Bwana,
Ili nisivutwe tena, kukuacha ee Mponya,
Nitwalie moyo wangu, uwe wako kamili.

011 - Sauti Zote Ziimbe

1
Sauti zote ziimbe, jina la Yesu li heri!
Sifa za Mfalme Mungu, jina la Yesu li heri!

CHORUS:
Jina li heri, jina li heri, jina la Yesu li heri!
Jina li heri, jina li heri, jina la Yesu li heri!

2
Hofu zote latuliza, jina la Yesu li heri!
Mwenye dhambi hukubali, jina la Yesu li heri!

3
Huvunja nguvu za dhambi, jina la Yesu li heri!
Damu yake hutakasa, jina la Yesu li heri!

4
Sauti yake ni tamu, jina la Yesu li heri!
Wafu nao hufufua, jina la Yesu li heri!

5
Lugha maelfu zitaimba, jina la Yesu li heri!
Astahili Mwana-Kondoo, jina la Yesu li heri!

012 - Msifu Mungu


Msifu Mungu wa neema,
Enyi viumbe po pote;
Wa juu pia sifuni,
Baba, Mwana naye Roho!

013 - Umetuahidi

1
Umetuahidi, kwamba wawili, watatu kwa jina lako
wakija, Utawabariki, kwa hivi leo twapiga magoti
nyumbani pako.

CHORUS:
Yesu uje kwetu, utubariki;
Yesu uje kwetu, uwe karibu.

2
Umekuwa nasi, siku nyingine, tunakuhitaji mpaka mwisho,
Uje Mkombozi, tupe neema, tusikie Yesu, utubariki.

3
Uje utawale sauti zetu, nyimbo nazo sala, uziagize.
Imani izidi, ikamilike, pendo liwe safi na njia nuru.

014 - Nitembee Nawe

1
Nitembee nawe Mungu, alivyotembea Henoko,
Mkono wangu uushike, unene nami kwa pole,
Ingawa njia siioni, Yesu nitembee nawe.

2
Siwezi tembea pekee, pana dhoruba angani,
Mitego ya miguu elfu, adui wengi hufichwa,
Uitulize bahari, Yesu nitembee nawe.

3
Ukinishika mkono, anasa kwangu hasara,
Kwa nguvu nitasafiri, ‘tautwika msalaba,
Hata mji wa Sayuni, Yesu nitembee nawe.

015 - Nena Rohoni Yesu

1
Nena rohoni Yesu, nena kwa upole,
Sema kwangu kwa pendo, “huachwi upweke,”
Fungua moyo wangu, nisikie mara,
Jaza roho na sifa, sifa zako Bwana.

CHORUS:
Kila siku unene, vile kwa upole.
Nong’oneza kwa pole, upole wa pendo,
“Daima utashinda, uhuru ni wako.”
Nisikie maneno, “huachwi upweke.”

2
Nena kwa wana wako, waonyeshe njia,
Wajaze kwa furaha, fundisha kuomba,
Wajifunze kutoa, maisha kamili,
Wahimize ufalme, tumwone Mwokozi.

3
Nena kama zamani, ulipoitoa,
Sheria takatifu, niishike pia,
Nipate kutukuza Wewe Mungu wangu,
Mapenzi yako tena, daima kusifu.

016 - Bwana Ninakuhitaji

1
Bwana ninakuhitaji, Ni mpofu, maskini,
Unishike mkononi, kwako napata nguvu.

CHORUS:
Kila saa, kila saa, Bwana ninakuhitaji,
Kila saa, kila saa, unilinde kila saa.

2
Univike na mavazi, ya usikivu wako,
Nguo zangu zote chafu, nazitamani zako.

3
Wewe ukiniongoza, nitakwenda salama,
Nenda nami siku zote, u nuru na uzima.

4
Na ikiwa huko mbele, sehemu yangu ngumu,
Au ikiwa furaha, unilinde kila saa.

017 - Si Mimi, Kristo

1
Si mimi, Kristo astahili sifa,
Si mimi, Kristo ajulikane,
Si mimi, Kristo katika maneno,
Si mimi, Kristo kwa kila tendo.

2
Si mimi, Kristo kuponya huzuni,
Kristo pekee, kufuta machozi,
Si mimi, Kristo kubeba mzigo,
Si mimi, Kristo kutoa hofu.

3
Kristo pekee, pasipo kujisifu,
Kristo pekee, na nisizungumze,
Kristo pekee, na hakuna kiburi,
Kristo pekee, sifa yangu ife.

4
Kristo pekee, mahitaji atoe,
Si mimi, Kristo, kisima changu,
Kristo pekee, kwa mwili na kwa moyo,
Si mimi, Kristo, hata milele.

018 - Mwokozi Kama Mchunga

1
Mwokozi kama mchunga, utuongoze leo,
Ututume malishoni, fanya tayari boma,
Bwana Yesu peke yako, umetuvuta kwako.

2
Tu wako uwe rafiki, uwe mlinzi wetu,
Kundi lako ulilinde, tusivutwe na dhambi,
Bwana Yesu tusikie, tukiomba samehe.

3
Umetuahidi kwamba utakubali watu,
Utawahurumia na, utawapa neema,
Bwana Yesu tunapenda, kuwa wako mapema.

019 - Msalabani pa Mwokozi

1
Msalabani pa Mwokozi, hapo niliomba upozi,
Moyo wangu ulitakaswa, na asifiwe.

CHORUS:
Na asifiwe, na asifiwe,
Alinikomboa kwa damu, na asifiwe.

2
Chini ya mti msumbufu, niliomba utakatifu,
Alinikomboa kwa damu, na asifiwe.

3
Kwa ajabu ninaokoka, Yesu anakaa moyoni;
Mtini alinifilia, na asifiwe.

4
Damu ya Yesu ya thamani huniokoa makosani,
Huniendesha wokovuni, na asifiwe.

020 - Mungu Wetu Yeye Mwamba

1
Mungu wetu yeye mwamba, kimbilio taabuni,
Msaada penye shida, ulio karibu sana.

CHORUS:
Mwamba wetu kutupumzisha, yu kivuli kuburudisha,
Huongoza katika njia, kimbilio taabuni.

2
Mchana usiku yeye, kimbilio taabuni,
Hivyo hatutaogopa, kwani yu karibu sana.

3
Iwayo yote Yeye tu, kimbilio taabuni,
Twamjua Yeye mlinzi, aliye karibu sana.

4
Mungu wetu ficho kwetu, kimbilio taabuni,
Siku zote uwe boma, lililo karibu sana.

021 - Baba Twakujia

1
Baba twakujia, uwe msaada,
Uwe kimbilio, twakusihi,
Dunia ni giza, tukitengwa nawe,
Tufariji hapa, Baba yetu.

CHORUS:
Baba twakujia, tu dhaifu, na usituache, tusikie.

2
Salama tulinde, kati ya taabu,
Uwe raha yetu, mashakani.
Roho yasumbuka, Baba tujalie,
Twakuomba sana, tupe nguvu.

3
Neema utupe, tukubali kwako,
Moyo wetu linda, safarini,
Tuongoe mbele, tupate kushinda,
Na kufika ng’ambo, kule kwako.

022 - Usinipite

1
Usinipite Mwokozi, unisikie,
Unapozuru wengine, usinipite.

CHORUS:
Bwana, Bwana, unisikie,
Unapozuru wengine, usinipite.

2
Kiti chako cha rehema, nakitazama,
Magoti napiga pale, nisamehewe.

3
Sina ya kutegemea, ila wewe tu,
Uso wako uwe kwangu, nakuabudu.

4
Wewe tu u Mfariji, sina mbinguni,
Wala duniani pote, Bwana mwingine.

023 - Yesu Furaha ya Moyo

1
Yesu furaha ya moyo, hazina ya pendo na nuru.
Yote yatupendezayo, yasilinganishwe nawe.

2
Kweli yako ya daima, wawajibu wakwitao,
Ni siku zote u mwema, kwao wakutafutao.

3
U Mkate wa Uzima, kupokea ni baraka,
Twanywa kwako u kisima, roho zikiburudika,

4
Mwokozi twakutamani, kwako roho hutulia,
Twakushika kwa imani, nawe watubarikia.

5
Yesu, ndiwe kwetu mwanga, tufurahishe daima,
Giza la dhambi fukuza, uwe mwanga wa Uzima.

024 - Jina Lake Yesu Tamu Tukilisikia

1
Jina lake Yesu tamu, tukilisikia,
Hutupoza tena hamu, hutuondolea.

2
Roho iliyoumia, kwalo hutibika,
Chakula njaani pia, raha tukichoka.

3
Jina hili ni msingi, ngao, ngome, mwamba,
Kwa hili napata vingi, kwangu ni akiba.

4
Yesu, Mchunga, Rafiki, Mwalimu, Kuhani,
Mwanzo, Mwisho, na Amina, mali yangu yote!

5
Moyo wangu hauwezi, kukusifu kweli,
Ila sifa zangu hizi, Bwana zikubali.

025 - Taji Mvikeni

1
Taji mvikeni, taji nyingi sana,
Kondoo mwake kitini, Bwana wa mabwana,
Nami tamsifu, kanifia mimi,
Ni Mfalme mtukufu, Bwana wa mbinguni.

2
Taji mvikeni, Mwana wa Bikira;
Anazovaa kichwani, aliteka nyara,
Shilo wa manabii, Mchunga wa watu,
Shina na tanzu ya Yese, wa Bethlehemu.

3
Taji mvikeni, Bwana wa Mapenzi;
Jeraha zake ni shani, ni vito vya enzi,
Mbingu haina, hata malaika,
Awazaye kuziona, pasipo kushangaa.

4
Taji mvikeni, Bwana wa salama,
Kote-kote duniani, vita vitakoma,
Nayo enzi yake, itaendelea,
Chini ya miguu yake, maua humea.

026 - Tutokapo Tubariki

1
Tutokapo tubariki, utupe kufurahi,
Tuwe na pendo lako, neema ya kushinda.
Nawe utuburudishe, tukisafiri chini.

2
Twatoa sifa shukrani, kwa neno la Injili,
Matunda yake wokovu, yaonekane kwetu,
Daima tuwe amani, kwa Kweli yako Bwana.

3
Siku zeku zikizidi, tuzitoe kwa Yesu,
Tuwe na nguvu moyoni, tusichoke njiani,
Hata tutakapoona, Utukufu wa Bwana.





026a  MUNGU MTUKUFU

God the Omnipotent
1
Mungu mtukufu, aliyeumba Pepo kuvuma na radi kali;
Toa neema unapotawala, tupe amani Bwana wa wema.

2
Mungu wa neema, nchi imeacha Amri tukufu na Neno lako,
Hasira zako zisituharibu, tupe amani, Bwana wa wema.

3
Mwumbaji wa haki, watu wabaya wamedharau utukufu wako,
Lakini wema wako utadumu; endesha kweli Bwana wa wema.

4
Tunakutolea Ibada, safi kwa ajili ya Wokovu wako,
Hivi tunaziimba sifa zako, wako uwezo na utukufu.

027 - Tena Mwokozi Twalitukuza

1
Tena Mwokozi twalitukuza,
Jina lako lenye kupendeza,
Twangojea neno la amani,
Kabla hatujakwenda nyumbani.

2
Tupe amani njiani mwetu,
Wewe u mwanzo u mwisho wetu,
Dhambini kamwe isiingie,
Midomo ikutajayo wewe.

3
Utupe amani usiku huu,
Ili gizani kuwe nuru kuu,
Tulinde kwa kuwa kwako Bwana,
Usiku ni sawa na mchana.

4
Tupe amani ulimwenguni,
Ndiyo dawa yetu majonzini,
Na ikitwita sauti yako,
Tupe amani milele kwako.

028 - Jina Lake Yesu Tamu

1
Jina lake Yesu tamu, lihifadhi moyoni,
Litakufariji ndugu, enda nalo po pote.

CHORUS:
Jina la thamani,
(Jina la ) (thamani)
Tumai la dunia,
Jina la thamani,
(Jina la thamani–tamu)
Furaha ya mbinguni.

2
Jina la Yesu lafaa, kama ngao vitani,
Majarabu yakisonga, omba kwa jina hili.

3
Jina hili la thamani, linatufurahisha,
Anapotukaribisha, na tunapomwimbia.

4
Mwisho wa safari yetu, tutakapomsujudu,
Jina hili tutasifu, furaha ya mbinguni.

029 - Yesu Nakupenda

1
Yesu nakupenda u mali yangu,
Anasa za dhambi sitaki kwangu,
Na Mwokozi aliyeniokoa,
Sasa nakupenda kuzidi pia.

2
Moyo umejaa mapenzi tele,
Kwa vile ulivyonipenda mbele,
Uhai wako ukanitolea
Sasa nakupenda kuzidi pia.

3
Ulipoangikwa msalabani,
Tusamehewe tulio dhambini,
Taji ya miiba uliyoivaa,
Sasa nakupenda kuzidi pia.

4
Mawanda mazuri na masikani,
Niyatazamapo huko mbinguni,
‘Tasema na taji nitakayovaa,
Sasa nakupenda kuzidi pia.

030 - Yesu Unipendaye

1
Yesu unipendaye, kwako nakimbilia,
Ni wewe utoshaye, mwovu akinijia.
Yafiche ubavuni, mwako maisha yangu,
Nifishe bandarini, wokoe moyo wangu.

2
Ngome nyingine sina, nategemea kwako,
Usinitupe Bwana, nipe neema yako,
Ninakuamania, mwenye kuniwezesha,
Shari wanikingia, vitani wanitosha.

3
Nakutaka Mpaji, vyote napata kwako,
Niwapo mhitaji, utanijazi vyako,
Nao waangukao, wanyonge wape nguvu,
Poza wauguao, uongoze vipofu.

4
Bwana umeniosha, moyo kwa damu yako,
Neema ya kutosha, yapatikana kwako,
Kwako Bwana naona, kisima cha uzima,
Mwangu moyoni Bwana, bubujika daima.

031 - Niimbe Pendo Lake

1
Niimbe (niimbe) pendo lake, pendo la (pendo la) Yesu
Bwana, Sababu (Sababu) alitoka, kwa Baba akafa.

CHORUS:
Niimbe (niimbe) pendo lake, sifa kuu (sifa kuu) nitatoa,
Akafa (akafa) niwe hai, niimbe pendo lake.

2
Machozi (machozi) alitoa, ijapo (ijapo) sijalia,
Maombi (maombi) yangu bado, aniombeapo.

3
Upendo (upendo) mkubwa huo! Dunia (dunia) haijui,
Msamaha (samaha) kwa kosa, kubwa kama langu.

4
Hapana (hapana) tendo jema, ambalo (ambalo) nilitenda,
nataka (nataka) toka leo, nimwonyeshe pendo.

032 - Ninao Wimbo Mzuri

1
Ninao wimbo mzuri, tangu kuamini,
Wa Mkombozi mfalme, tangu kuamini.

CHORUS:
Tangu kuamini, jina lake ‘tasifu,
Tangu kuamini, nitalisifu jina lake.

2
Kristo anitosha kweli, tangu kuamini,
Mapenzi yake napenda, tangu kuamini.

3
Nina ushuhuda sawa, tangu kuamini,
Unalofukuza shaka, tangu kuamini.

4
Ninalo kao tayari, tangu kuamini;
Nililorithi kwa Yesu, tangu kuamini.

033 - Karibu Sana

1
Karibu sana univute, karibu sana daima niwe,
Bwana napenda unishike, unilinde nisitengwe nawe,
Unilinde nisitengwe nawe.

2
Karibu sana sina kitu, sina sadaka kwa Bwana Yesu,
Isipokuwa moyo wangu, uutakase katika damu,
Uutakase katika damu.

3
Karibu sana wewe nami ninafurahi kuacha dhambi,
Anasa zote na kiburi, nipe niliyemsulibisha,
Nipe niliyemsulibisha.

4
Karibu ssana hata mwisho, hata mbinguni nisimamapo,
Daima dawamu niwepo, nitakapoona uso wako,
Nitakapoona uso wako.

034 - Nipe Habari za Yesu

1
Nipe habari za Yesu, kwangu ni tamu sana,
Kisa chake cha thamani, hunipendeza sana,
Jinsi malaika wengi, walivyoimba sifa,
Alipoleta amani, kwa watu wa dunia.

CHORUS:
Nipe habari za Yesu, kaza moyoni mwangu,
Kisa chake cha thamani, hunipendeza sana.

2
Kisa cha alivyofunga, peke yake jangwani,
Jinsi alivyolishinda, jaribu la Shetani,
Kazi aliyoifanya, na siku za huzuni,
Jinsi walivyomtesa; yote ni ya ajabu.

3
Habari za Msalaba, aliposulubishwa,
Jinsi walivyomzika akashinda kaburi,
Kisa chake cha rehema, upendo wake kwangu,
Aliyetoa maisha, nipokee wokovu.

035 - Nimekombolewa na Yesu

1
Nimekombolewa na Yesu, na sasa nimefurahi,
Kwa bei ya mauti yake, mimi ni mtoto wake.

CHORUS:
Kombolewa! Nakombolewa na damu,
Kombolewa! mimi mwana wake kweli.

2
Kukombolewa nafurahi, kupita lugha kutamka,
Kulionyesha pendo lake, mimi ni mtoto wake.

3
Nitamwona Mfalme wangu, katika uzuri wake,
Ambaye najifurahisha, katika torati yake.

4
Najua taji imewekwa, mbinguni tayari kwangu,
Muda kitambo atakuja, ili alipo niwepo.

036 - Ni Siku Kuu

1
Ni siku kuu, siku ile, ya kumkiri Mwokozi,
Moyo umejaa tele, kunyamaza hauwezi.

CHORUS:
Siku kuu! Siku kuu! ya kuoshwa dhambi zangu kuu,
Hukesha na kuomba tu, ananiongoza miguu,
Siku kuu! siku kuu! ya kuoshwa dhambi zangu kuu.

2
Tumekwisha kupatana, mimi wake, yeye wangu,
Na sasa nitamwandama, nikiri neno la Mungu.

3
Moyo tulia kwa Bwana, kiini cha raha yako,
Huna njia mbili tena, uwe naye uendako.

037 - Pendo Lako Ee Mwokozi

1
Pendo lako Ee Mwokozi, hushinda pendo zote,
Kaa nasi ndani yetu, furaha ya mbinguni,
Yesu u rehema tupu, safi na kusamehe,
Mfariji mwenye huzuni, yaondoe machozi.

2
Roho yako ya upendo, tuma kwa kundi lako,
Hebu tuirithi raha, iliyoahidiwa,
Uondoe moyo mbaya, u mwanzo, tena mwisho,
Timiza imani yetu, ili tuwekwe huru.

3
Yesu uje kwetu sasa, tupokee huruma,
Rudi kwetu tena kamwe, usituache pekee,
Tungekutukuza leo, pamoja na malaika,
Imba na kutoa sifa, ingia kwa ibada.

4
Sasa Bwana kazi yako, imalize moyoni,
Takasa hekalu lako, wokovu kamilisha,
Safisha viumbe vyako, katika wakati huu,
Tupumzike toka dhambi, tuingie mbinguni.

038 - Nasifu Shani ya Mungu

1
Nasifu shani ya Mungu, mweneza bahari,
Muumba pia wa mbingu, jua nyota mwezi,
Ni tukufu yako shani, mtengeza mambo,
Ya nyakati na zamani, yasiyo na mwisho.

2
Kadiri ya nionayo, ya kusifu Mungu:
Nchi niikanyagayo, na hayo mawingu,
Hakuna hata unyasi, usiokukuza,
Na upepo wavumisha, au kutuliza.

3
Nami kwa mkono wako, naongozwa sawa,
Ni pato nikusifupo, kukwomba ni dawa,
Umenizingira nyuma, na mbele baraka,
Maarifa ya ajabu, yanishinda mimi.

039 - Ati Kuna Mvua Njema

1
Kuna mvua ya baraka, Bwana nimesikia,
Unawamwagia wote, bure wanaipata.

CHORUS:
Na mimi, Na mimi, Bwana uninyeshee?

2
Sinipite Baba Mwema, dhambini nimezama,
Rehema ni za daima, Bwana, unioneshe.

3
Sinipite, Yesu mwema, niwe nawe daima,
Natamani kukwandama, Bwana, unichukue.

4
Sinipite, Roho Mwema, Mpaji wa uzima,
Nawe shahidi wa wema, Bwana wema unipe.

040 - Njoo, Roho Mtukufu

1
Njoo Roho Mtukufu, uoshe moyo wangu,
Utakase nia yangu, njoo nijaze sassa.

CHORUS:
Roho Mtukufu njoo, nijaze sasa,
Utakase nia yangu, njoo nijaze sasa.
2
Ujalize moyo wangu, ijapo sikuoni,
Nami ninakuhitaji, njoo nijaze sasa.
3
Nimejaa udhaifu, nainamia kwako,
Roho Mtukufu sasa, nitilie na nguvu.
4
Unioshe nifariji, niponye nibariki,
Unijaze moyo wangu, ndiwe mwenye uwezo.

041 - Roho Mtakatifu

1
Roho Mtakatifu, kiongozi amini,
Utushike mkono, tulio wasafiri,
Utupe kusikia, sauti ya upole,
“Msafiri fuata, naongoza nyumbani.”

2
Wewe ndiwe rafiki, msaada karibu,
‘Situache shakani, Na tukiwa gizani,
Utupe kusikia, sauti ya upole,
“Msafiri fuata, naongoza nyumbani.”

3
Siku zetu za kazi, zikiwa zimekwisha,
Wala hatuna tamaa, ila mbingu na sala,
Utupe kusikia, sauti ya upole,
“Msafiri fuata, naongoza nyumbani.”

042 - Ewe Roho wa Mbinguni

1
Ewe Roho wa mbinguni, maombi sikia!
Makao yako yafanye, mioyoni mwetu.

2
Kama nuru tupenyeze, giza uondoe,
Siri yako tuione, na amani yako.

3
Kama moto tusafishe, choma dhambi yetu,
Roho zetu ziwe zote, hekalu la Bwana.

4
Kama umande na uje, utuburudishe,
Moyo mkavu utakuwa, ni wenye baraka.

5
Kama upepo Ee Roho, katika pentekoste
Ukombozi utangaze, kwa kila taifa.

043 - Furaha Gani

1
Furaha gani na ushiriki, nikimtegemea Yesu tu,
Baraka gani tena amani, nikimtegemea Yesu tu.

CHORUS:
Tegemea, salama bila hatari,
Tegemea, tegemea Mwokozi Yesu.

2
Nitaiweza njia nyembamba, nikimtegemea Yesu tu,
Njia ‘tazidi kuwa rahisi, nikimtegea Yesu tu.

3
Sina sababu ya kuogopa, nikimtegemea Yesu tu,
Atakuwa karibu daima, nikimtegemea Yesu tu.

044 - Hakuna Rafiki Kama Yesu

1
Hakuna rafiki kama Yesu, hakuna, hakuna,
Tabibu mwingine wa rohoni, hakuna, hakuna.

CHORUS:
Yesu ajua shida zetu, daima ataongoza,
Hakuna rafiki kama Yesu, hakuna, hakuna,

2
Wakati ambapo hapo yeye, hapana, hapana,
Wala giza kututenga naye, hapana, hapana.

3
Aliyesahauliwa naye, hakuna, hakuna,
Mkosaji asiyempenda, hakuna, hakuna.

4
Kipawa kama Mwokozi wetu, hakuna, hakuna,
Ambaye atanyimwa wokovu, hakuna hakuna.

045 - Mlimani Pana Mwanga

1
Mlimani pana mwanga, mwanga wa jua zuri,
Shambani na baharini, jua tukufu liko,
Mwanga ulio mkubwa, umo moyoni mwangu,
Kwa kuwa Yesu alipo, hapa pana mwangaza.

CHORUS:
Mwangaza ulio mzuri, mwanga umo moyoni,
Akiwapo Bwana Yesu, pana mwanga moyoni.

2
Kama mavazi kikuu, ninavua huzuni,
Nguo nzuri za furaha, umenipa za kuvaa,
Nakuandama rohoni, hata nyumba ya juu,
Iliyopambwa vizuri, katika pendo lako.
3
Ulinikomboa Yesu, maisha yangu mali,
Vyote ni vyako Mwokozi, daima nikusifu,
Nakuandama rohoni, hata nyumba ya juu,
Iliyopambwa vizuri, katika pendo lako.

046 - Miguuni Pake Yesu

1
Miguuni pake Yesu, maneno yake tamu,
Pahali palipo heri, niwepo kila siku.
Miguuni pake Yesu nakumbuka upendo
Na hisani yake kwangu, vimenivuta moyo.

2
Miguuni pake Yesu, hapa mahali bora,
Pa kuweka dhambi zangu, mahali pa pumziko.
Miguuni pake Yesu, hapa nafanya sala,
Kwake napewa uwezo, faraja na neema.

3
Unibariki Mwokozi, ni miguuni pako,
Unitazame kwa upendo, nione uso wako.
Nipe Bwana nia yake, ili ionekane,
Nimekaa na Mwokozi, aliye haki yangu.

047 - Ni Heri Kifungo

1
Ni heri kifungo kinachotufunga,
Mioyo yetu kwa pendo pendo la Kikristo.

2
Mbele ya Baba tunatoa sala,
Hofu nia masumbufu yetu ni mamoja.

3
Tunavishiriki matata na shida,
Na mara nyingi twatoa chozi la fanaka.

4
Tunapoachana moyoni twalia,
Lakini tutakutana mwisho mbinguni.

048 - Ninakupenda Zaidi

1
Ninakupenda zaidi, ya vyote vingine;
Kwani umenipa raha, na amani Bwana.

CHORUS:
Nusu haijatangazwa (tangazwa) ya upendo wako,
Nusu haijatangazwa (tangazwa) damu hutakasa
(takasa).

2
Nakujua u karibu, kuliko dunia,
Kukukumbuka ni tamu, kupita kuimba.

3
Kweli wanifurahisha, na nitafurahi,
Pasipo upendo wako naona huzuni.

4Itakuwaje Mwokozi, kukaa na wewe,
Ikiwa ulimwenguni tuna furaha hii?

049 - Ninaye Rafiki

1
Ninaye rafiki naye, alinipenda mbele,
Kwa kamba za pendo lake, nimefungwa milele,
Aukaza moyo wangu, uache ugeuzi,
Ninakaa ndani yake, Yeye kwangu milele.

2
Ninaye Rafiki ndiye, aliyenifilia,
Alimwaga damu yake, kwa watu wote pia,
Sina kitu mimi tena, nikiwa navyo tele,
Pia vyote ni amana, ndimi wake milele.

3
Ninaye Rafiki naye, uwezo amepewa,
Atanilinda mwenyewe, juu ‘tachukuliwa,
Nikitazama mbinguni, hupata nguvu tele,
Sasa natumika chini, kisha juu milele.

4
Ninaye Rafiki naye, yuna na moyo mwema,
Ni Mwalimu Kiongozi, mlinzi wa daima,
Ni nani wa kunitenga na mpenzi wa mbele?
Kwake nimetia nanga, ndimi wake milele

050 - Mungu Awe Nanyi Daima

1
Mungu awe nanyi daima, hata twonane ya pili,
Awachunge kwa fadhili, Mungu awe nanyi daima.

CHORUS:
Hata twonane juu, hata twonane tena kwake,
Hata twonane juu, Mungu awe nanyi daima.

2
Mungu awe nanyi daima, awafunike mabawa,
Awalishe, awakuze, Mungu awe nanyi daima,

3
Mungu awe nanyi daima, kila wakati wa shida,
Awalinde hifadhini, Mungu awe nanyi daima.

4
Mungu awe nanyi daima, awabariki na pendo,
Ambalo halina mwisho, Mungu awe nanyi daima.

051 - Yesu Mwokozi

1
Yesu Mwokozi, kwa hakika, hunipa furaha na amani,
Mrithi wa wokovu wake, natakaswa kwa damu yake.

CHORUS:
Habari hiyo wimbo wangu, daima nitamsifu Yesu.
Habari hiyo wimbo wangu, daima nitamsifu Yesu.

2
Nijitoapo nina raha, na kwa imani namwona Bwana,
Aniletea malaika, wananilinda niokoke.

3
Hali na mali anatwaa, katika Yesu nabarikiwa,
Nikimngoja kwa subira, wema wake unanitosha.

052 - Nipe Biblia

1
Nipe Biblia nyota ya furaha,wapate nuru wasafirio,
Hakuna la kuzuia amani, kwani Yesu alituokoa.

CHORUS:
Nipe Biblia neno takatifu, nuru yake itaniongoza,
Sheria na ahadi na upendo, hata mwisho vitaendelea.

2
Nipe Biblia nihuzunikapo, ikinijaza moyoni dhambi,
Nipe neno zuri la Bwana Yesu, nimwone Yesu
Mwokozi wangu.

3
Nipe biblia nipate kuona, hatari zilizo duniani,
Nuru ya neno lake Bwana Yesu, itaangaza njia ya kweli.

4
Nipe Biblia taa ya maisha, mfariji tunapofiliwa,
Unionyeshe taa ya mbinguni, nione utukufu wa Bwana.

053 - Napenda Kuhubiri

1
Napenda kuhubiri, habari ya Yesu,
Ya Bwana wa fahari, na pendo lake kuu.
Kuhubiri napenda, kwa hali na mali,
Mwenyewe nimeonja, najua ni kweli.

CHORUS:
Napenda kuhubiri, kisa cha Bwana Yesu,
Cha Bwana wa fahari, na pendo lake kuu.

2
Napenda kuhubiri, mambo ya ajabu,
Na tukiyafikiri, yapita dhahabu,
Kuhubiri napenda, ya yaliyonifaa,
Nami sana napenda, hayo kukwambia.

3
Napenda kuhubiri, hunifurahisha,
Tamu yake habari, haiwezi kwisha,
Napenda kuhubiri, wa gizani nao,
Hawana mhubiri, wa kueleza chuo.

4
Kuhubiri napenda, hata wajuao,
Kusikia hupenda, kama wenzi wao,
Nako kwenye fahari, nikiimba wimbo,
Nitaimba habari, ya Mwokozi huyo.

054 - Nataka nimjue Yesu

1
Nataka nimjue Yesu, na nizidi kumfahamu,
Nijue pendo lake tu, wokovu wake kamili.

CHORUS:
Zaidi zaidi, nimfahamu Yesu,
Nijue upendo wake, wokovu wake kamili.

2
Nataka nione Yesu, na nizidi kusikia,
Anenapo kitabuni, kujidhihirisha kwangu.

3
Nataka tena zaidi, daima kupambanua,
Mapenzi yake nifanye, yale yanayompendeza.

4
Nataka nikae naye, kwa mazungumzo matamu,
Nizidi kuwaonyesha, wengine wokovu wake.

055 - Twapanda Mapema

1
Twapanda mapema, na mchana kutwa,
Mbegu za fadhili, hata jioni,
Twangojea sasa, siku za kuvuna,
Tutashangilia, wenye mavuno.

CHORUS:
Wenye mavuno, wenye mavuno,
Tutashangilia, wenye mavuno,
Wenye mavuno, wenye mavuno,
Tutashangilia, wenye mavuno.

2
Twapanda mwangani, na kwenye kivuli,
Tusishindwe na baridi na pepo;
Punde itakwisha, kazi yetu hapa,
Tutashangilia, wenye mavuno.

3
Twapanda kwa Bwana, mbegu kila siku,
Tujapoona taabu na huzuni,
Tuishapo shinda, atatupokea,
Tutashangilia, wenye mavuno.

056 - Walio Kifoni

1
Walio kifoni nenda waponye,
Uwatoe walio shimoni,
Wanaoanguka uwainue,
Habari njema uwajulishe.

CHORUS:
Walio kifoni, waokoeni,
Mwokozi yuko huwangojea
2
Wajapokawia anangojea,
Awasubiri waje tobani,
Mwokozi hawezi kuwadharau,
Huwasamehe tangu zamani.
3
Na ndani ya moyo wa mwanadamu,
Huwamo shida tena huzuni,
Lakini kwa Yesu kuna rehema,
Kuwaponya na kuwaokoa.
4
Walio kifoni nenda waponye,
Kazi ni yetu zawadi iko,
Nguvu kuhubiri Bwana hutoa,
Kwa subira tuwavute sasa.

057 - Usiikatae Kazi

1
Usiikatae kazi, yake Bwana,
Ukae tayari, kuifanya kazi,
Uende po pote, Mungu akwitapo,
Nawe utaona, furaha kazini.

CHORUS:
Njoo we, usiikatae, Njoo we, uifanye kazi,
Usiikatae kazi yake Bwana, ili hatimaye,
usikatazwe juu.

2
Usiikatae, kazi yake Bwana,
Kwa nini kawia, fanya kazi leo,
Mavuno meupe, wachache wavuni,
Onyesha furaha, kwa kazi ya Bwana.

3
Usiikatae kazi, yake Bwana,
Kukataa pendo, kwako ni hatari,
Saa ya rehema, Yesu akiomba,
Ziungame dhambi, zifutwe mbinguni.

058 - Leo Ninafikiria

1
Leo ninafikiria nchi nzuri, ninayotaka kuiona,
Nisimamapo karibu na Mwokozi, tajini zitakuwa nyota?

CHORUS:
Sijui tajini mwangu kama nyota, zitang’aa kila wakati.
Nitakapoamka katika majumba, zitakuwa nyota tajini?

2
Kwa nguvu za Bwana nitafanya kazi, nitavuta roho za
watu, Ili niwe na nyota katika taji, Bwana anapotupa tunu.

3
Nitakuwa na furaha nikimwona, kuweka miguuni pake,
Watu waliovutwa kwa ajili ya kazi yangu na roho yake.

059 - Fanyeni Kazi Zenu

1
Fanyeni kazi zenu, usiku si mbali,
Kesheni saa zenu, vumilieni,
Kwa Yesu tumikeni, na hiyo Injili,
Sana wahubirini, watu wa mbali.

2
Fanyeni kazi zenu, giza lasogea,
Na wengi wenzi wenu, wamo gizani,
Msipoteze moja, dakika ni hizi,
Bwana atarejea, mwisho wa kazi.

3
Fanyeni kazi zenu, hivi jua lachwa:
Wote walio kwenu apenda Mungu
Na sisi tumjuaye na tuwafundishe
Ili Yesu ajaye tumfurahishe.

060 - Pengine Siyo Mlimani

1
Pengine siyo mlimani, utakaponiita,
Pengine siyo baharini, wala palipo vita,
Lakini unaponiita, na njia siijui,
Bwana nitajibu ni tayari, kwenda uniagizapo.

CHORUS:
Ukiwa pamoja nami Bwana, mlimani baharini,
Niende utakaponiita; na fuata uendako.

2
Pengine leo kuna neno, neno tamu la pendo,
Ambalo Yesu anataka, ninene kwa upole,
Ukiwa pamoja nami Bwana, nitamtafuta leo,
Yule aliyepotea mbali, nitasema upendavyo.

3
Pahali pako bila shaka, pa kuvuna shambani,
Kazi niwezayo kufanya, kwa Yesu Mkombozi,
Hivi nikikutegemea, kwa kuwa wanipenda,
Mapenzi yako nitayafanya, na niwe upendavyo.

061 - Nimemwona Rafiki

1
Nimemwona rafiki, wa thamani kubwa,
Ananipenda kwa ‘pole, kwa pendo amini,
Kuishi kutengwa naye, la, huku siwezi,
Tunakaa pamoja, Bwana nami.

2
Pengine ninachoka, mimi mdhaifu,
Ndipo ninamtegemea, alivyoalika,
Huniongoza njiani, pahali pa nuru,
Twatembea pamoja Bwana nami.

3
Namweleza huzuni, mimi mdhaifu,
Vile vinavyosumbua, vinavyopendeza,
Huniagiza kutenda, yanayonipasa,
Twatembea pamoja, Bwana nami.

4
Ajua natamani, kuwavuta watu,
Hivyo ananipeleka, kutangaza Neno,
Nitangaze pendo lake, kwa nini akafa,
Twahubiri pamoja, Bwana nami.

062 - Napenda Kitabu Chake

1
Napenda kitabu chake, kilichotoka mbinguni,
Barua kwangu ya Bwana, ujumbe wake wa pendo.

2
Humo ndani ya kitabu, sura ya Yesu naona,
Karatasi zimekuwa, nyayo zake za kiongozi.

3
Neno lake tamu sana, kama asali naona,
Natamani kulionja, ni mkate wa uzima.

4
Mapenzi yake mwumbaji, yanafunuliwa humo,
Hazina kuu ya hekima, utajiri wa ajabu.

5
Mwangaza wa ulimwengu, angaza humo moyoni,
Uwe mwandamizi pote, taa ya hatua zangu.

063 - Niuonapo Msalaba

1
Niuonapo Msalaba, Kristo aliponifia,
Kwangu pato ni hasara, kiburi nakichukia.

2
Na nisijivune Bwana, ila kwa sadaka yako,
Upuzi sitaki tena, zi chini ya damu yako.

3
Tazama kichwani kwake, mikononi na miguu,
Huzuni pendo twaona, vyabubujika daima.

4
Vitu vyote vya dunia, si sadaka ya kutosha,
Pendo zako zaniwia, nafsi mali na maisha.

064 - Piga Panda ya Injili

1
Piga panda ya injili, onyesha watu wote,
Ili anayesikia, atubu aokoke.

CHORUS:
Piga panda ya injili, uipige kwa nguvu,
Mungu amekuagiza, mateka wawe huru.

2
Uipige vilimani, kwa kila tambarare,
Pande zote miji yote, isikie injili.

3
Uipige mipakani, barabarani pia,
Iwatangazie wote, wanaitwa na Baba.

4
Uipige watu wengi, wataka wawe huru,
Waambie kwamba Yesu, asema “Njoni kwangu.”

065 - Twendeni Askari

1
Twendeni askari watu wa Mungu, Yesu yuko mbele,
tumwandame juu, Ametangulia Bwana vitani,
twende mbele kwani ndiye amini.

CHORUS:
Twendeni askari, watu wa Mungu,
Yesu yuko mbele, tumwandame juu.

2
Jeshi la Shetani likisikia, jina la Mwokozi litakimbia,
Kelele za shangwe zivume pote, ndugu inueni zenu sauti.

3
Kweli kundi dogo watu wa Mungu, la watakatifu ni letu fungu,
Hatutengwi nao moja imani, tumaini moja na moja dini.

4
Haya mbele watu nasi njiani, inueni mioyo nanyi sifuni,
Heshima na sifa yake Mfalme. juu hata chini sana zivume.

066 - Roho Yangu Amka Sasa

1
Roho yangu amka sasa, mara jitahidi,
Shindano ni lake Bwana, zawadi ni taji.

2
Sauti ni yake Mungu inayokuita,
Ndiyo aliyekirimu, taji ya uzima.

3
Mashahidi ndio wengi, wanaokuona,
Ya nyuma usifikiri, bali mwendo kaza.

4
Bwana umetuanzisha, katika shindano,
Kwa vile tunaposhinda, ushindi ni wako.

067 - Kesha Roho Yangu

1
Kesha roho yangu, adui maelfu
Hujaribu kuangusha, kuvuta dhambini.

2
Ukeshe uombe, ili usishindwe,
Fanya vita kila siku, omba msaada.

3
Kushinda ni bado, ulinde silaha,
Usiache kupigana, hata una taji.

068 - Umtetee Mungu Duniani

1
Umtetee Mungu duniani, ijapo pepo kali zavuma,
Mwambani pekee pana nguvu, dhambi ikilemea.

CHORUS:
Tusimame imara katika mwamba,
Mwamba wa Kristo pekee,
Ndipo salamani tutasimama,
Kule kitini pa enzi.

2
Itetee haki kwa bidii, kwa moyo mnyofu wa imani,
Mwambani pekee utashinda, wingi wa upotovu.

3
Itetee kweli itadumu, ijapokawia itashinda,
Mwambani pekee pana raha, yaishapo tufani.

069 - Cha Kutumaini Sina

1
Cha kutumaini sina, ila damu yake Bwana,
Sina wema wa kutosha, dhambi zangu kuziosha.

CHORUS:
Kwake Yesu, nasimama,
Ndiye mwamba, ni salama,
Ndiye mwamba, ni salama.

2
Njia yangu iwe ndefu, yeye hunipa wokovu,
Mawimbi yakinipiga, nguvu zake ndiyo nanga.

3
Damu yake na sadaka, nategemea daima,
Yote chini yakiisha, Mwokozi atanitosha.

4
Nikiitwa hukumuni, rohoni nina amani,
Nikivikwa haki yake, sina hofu mbele zake.

070 - Wapenzi wa Bwana

1
Wapenzi wa Bwana, ije raha yenu,
Imbeni nyimbo za raha, imbeni nyimbo za raha,
Za ibada yenu, za ibada yenu.

CHORUS:
Twenenda Zayuni, mji mzuri Zayuni,
Twenenda juu Zayuni,
Ni maskani ya Mungu.

2
Wasiimbe wao wasioamini,
Watoto wa Mungu ndio, watoto wa Mungu ndio,
Waimbao chini, waimbao chini.

3
Twaona rohoni, baraka za Mungu,
Tusijafika mbinguni, tusijafika mbinguni,
Kwenye utukufu, kwenye utukufu.

4
Tutakapomwona, masumbuko basi,
Huwa maji ya uzima, huwa maji ya uzima.
Furaha halisi, furaha halisi.

071 - Kesha Ukaombe

1
Kesha ukaombe, panapo nafasi,
Wakati si mwingi, kwa hiyo ukeshe,
Mwili ni dhaifu, adui hodari,
Karibu atakuja, Bwana wa arusi.

CHORUS:
Kesha, Omba, Kesha, Omba,
Kesha kaombe gizani, mchana daima kesha.

2
Fukuza usingizi, fukuza mashaka,
Ahadi ni yako, raha ya milele,
Bwana alikesha, kwa ajili yako,
Jasho lake likawa, matone ya damu.

3
Yesu umkubali, awe nguvu zako,
Silaha uzivae, adui karibu,
Sasa nafasi iko, isipite bure,
Bila kukawia, Masihi yuaja.

072 - Jenga Juu ya Mwamba

1
Tutajenga juu ya mwamba, wa Yesu mwamba wa kale,
Tutavumilia kishindo, tufani ivumapo.

CHORUS:
Tutajenga juu, (Tutajenga juu ya mwamba mkuu)
Tutajenga juu, (Tutajenga juu ya mwamba mkuu)
Tutajenga juu ya mwamba mkuu, juu yake Yesu.

2
Wengine hujenga katika, mchanga wa ulimwengu,
Wengine katika mawimbi, ya anasa za dhambi.

3
Jenga nawe juu ya mwamba, msingi pekee wa kweli,
Tumai lake litadumu, tumai la wokovu.

073 - Nakaza Mwendo Mbinguni

1
Nakaza mwendo mbinguni, kila siku napanda juu,
Naomba nikisafiri, Bwana uniongoze juu.

CHORUS:
Bwana uniinue juu, kwa imani hata mbingu,
Juu kuliko dunia, Bwana uniongoze juu.

2
Moyo wangu hautaki, kukaa palipo shaka,
Wengine wapenda chini, nia yangu ni kupanda.

3
Nataka kupanda juu, nisishindwe na adui,
Kwa imani nasikia, sauti ya washindaji.

4
Kupanda juu nataka, niuone utukufu,
Hata mwisho nitaomba, Bwana uniongoze juu.

074 - Niambie Ee Mlinzi

1
Niambie Ee mlinzi, je, kumepambazuka ,
Utukufu wa Zayuni, pana dalili zake?
Msafiri uondoke, utazame mbinguni,
Kiunoni ujifunge, ni kucha alfajiri.

2
Mlinzi, inamulika, nuru njiani mwako,
Dalili za kuja kwake, kwamba siku karibu,
Panda itakapolia, itawaamsha wafu,
Watakatifu wa Mungu, kuwapa kutokufa.

3
Mlinzi ione nuru, ya mwaka wa Sabato,
Sauti zinatangaza, ufalme ni karibu,
Msafiri ninaona, mlima wa zayuni,
Mji wa Yerusalemi, nayo fahari yake.

4
Kwenye mji wa dhahabu, anaketi Mfalme,
Katika kiti kizuri, huku anatawala,
Pana amani po pote, mashamba husitawi,
Na ardhi ina rutuba; mito ni mitulivu.

5
Mlinzi twakaribia, nchi iliyo nzuri,
Twende mbele tufurahi, nchi inachangamka,
Sikieni kuna wimbo, wa waliookoka,
Kaza mwendo ujiunge, na kundi kubwa hili.

075 - Msingi Imara

1
Msingi imara ninyi wa Bwana,
Umewekwa kwenu kwa neno lake,
Nini zaidi atasema Bwana,
Imani yenu ipate kuzidi?

2
Wambiwapo vuka maji ya giza,
Mito ya mashaka haitazidi,
Takuwapo nawe nikuwezeshe,
Shida upatazo zisikutishe,

3
Utakapopishwa ndani ya moto,
Nguvu nitakupa, upate pato,
Huteketezwi ila taka zako,
Na zitasalia dhahabu zako.

4
Na mtu aliyenitegemea,
Nguvu za Jehanamu zijapotisha,
Kamwe kwa adui sitamtia,
Mtu wangu kamwe sitamuacha.

076 - Mrithi Ufalme

1
Mrithi ufalme kwani walala?
Karibu wokovu wasinzia?
Amka simama uvae silaha,
Haraka sana saa zapita.

2
Mrithi ufalme mbona ‘kawia?
Mbona hupokei zawadi?
Haya uvae Mwokozi yuaja,
Haraka umlaki afikapo.

3
Mataifa makuu ya dunia,
Yapigana na kujiangusha,
Usizihofu dalili, mrithi,
Ishara zote hazikawii.

4
Sitazame anasa za dunia,
Kwani hayo yapita upesi,
Zivunje kamba zinazokufunga,
Mrithi ufalme njoo karudi.

5
Inua kichwa tazama mbele tu,
Mfalme aja na utukufu,
Jua laonekana milimani,
Warithi ufalme furahini.

077 - Je! Mlinzi Ukutani

1
Je mlinzi ukutani, wa mji wa Zayuni,
Habari zake usiku, asubuhi karibu?
Kuna dalili za kupambazuka?
Kuna dalili za kupambazuka?

2
Katika safari yetu, twaona nchi kavu?
Tutalala baharini, bandari bado mbali?
Kweli kweli, tutaona ufalme?
Kweli kweli, tutaona ufalme?

3
Tunaona nuru yake, nyota ya asubuhi,
Nyota tukufu na safi, inang’aa mbinguni,
Furahini, wokovu u karibu,
Furahini, wokovu u karibu.

4
Tumetazama ramani, kweli pwani si mbali,
Twende mbele, kwa upesi tutaona bandari,
Furahani, imbeni nyimbo zenu,
Furahani, imbeni nyimbo zenu.

078 - Mpaka Lini Bwana

1
Mpaka lini Bwana, utakaa mbali?
Kumetuchosha moyo, kukawia hivi,
Utatujia lini, ili tufurahi,
Katika ile nuru, kuja kutukufu?

2
Mpaka lini Yesu, utaacha watu,
Uliowakomboa, wawe na mashaka?
Wachache waamini, kwamba utarudi,
Wachache wa tayari, Bwana kukulaki.

3
Waamshe watu wako, tangaza ujumbe,
“Mwe watakatifu, Bwana yu karibu,”
Utatujia lini, ili tufurahi,
Katika ile nuru, kuja kutukufu?

079 - Nataka Imani Hii

1
Nataka imani hii, imani imara,
Ambayo haitetemi kitu chote wakati wa shida,
Wakati wa shida.

2
Isiyonung’unikia, huzuni taabu;
Lakini katika saa ya matata humwamini Mungu,
Humwamini Mungu.

3
Imani inayong’aa, katika tufani,
Isiyoogopa giza wala shida njaa na hatari,
Njaa na hatari.

4
Haiogopi dunia, kudharau kwake,
Haiangushwi na hila, nayo dhambi na udanganyifu,
Na udanganyifu.

5
Bwana nipe imani hii, hivi nitaweza
Kuonja hapa chini ulimwenguni kurithi furaha,
Kurithi furaha.

080 - Tupe Moto wa Uhai

1
Tupe moto wa uhai, uliowaka zamani,
Uliowaongoza juu, wazee watakatifu.

2
Wapi roho iliyokaa, moyoni mwa Ibrahimu?
Kadhalika ndugu Paulo, aliwezeshwa na moto.

3
Kwani neema haina, nguvu siku hizi sawa,
Kama wakati wa Musa, Ayubu na wa Eliya?

4
Zamani za kale Bwana, kumbuka na kwa rehema,
Zihuishe roho zetu, kwa Roho Mtakatifu.

081 - Siku Sita Zimepita

1
Siku sita zimepita, Sabato tena karudi,
Shangilie roho yangu, itukuze kwa busara.

2
Msifuni awapaye, pumziko tamu wachovu,
Kwake roho yatulizwa, kupita siku nyingine.

3
Moyo wetu ufurahi, na kutoa shukurani,
Ujalizwe raha ile, yasiyopitika kamwe.

4
Raha hiyo ya rohoni, ni amana ya pumziko,
Ambalo limewekwa juu, kikomo cha masumbuko.

082 - Ni Siku ya Furaha

1
Ni siku ya furaha, ni siku ya nuru,
Nasi twaona raha, kuja kushukuru,
Leo watu wa Mungu, wadogo wakubwa,
Hukaribia mbingu, ilipo baraka.

2
Leo ndiyo bandari, nasi twawasili,
Hiyo bustani nzuri, ya nyingi fadhili,
Kijito cha baridi, kimefanya ziwa,
Na kiu ikizidi, twanywa maridhawa.

3
Leo ngazi na iwe, ifikayo juu,
Mawazo na yasiwe, ya duniani tu,
Leo ni kujilisha, chakula cha mbingu,
Na kujifurahisha, kwa mambo ya Mungu.

083 - Ewe Skuli ya Sabato

1
Ewe shule ya Sabato, u pazuri sana,
Moyo wangu wanivuta, nije kwako leo.

CHORUS:
Sabato, ni nzuri, Sabato, ni nzuri,
Moyo wangu wanivuta, nije kwako leo.

2
Moyo wangu mpotovu, hapa una raha,
Ndipo nimwonapo Yesu, nije kwako leo.

3
Hapa Yesu mwenye pendo, aniita pole,
Nimtolee moyo Yeye, nije kwako leo.

084 - Ikumbuke Kote Sabato

1
Ikumbuke kote, Sabato ya Bwana,
Siku tamu na bora, kupita nyingine,
Yatuletea raha, na furaha kweli,
Mwanga wake hung’aza, urembo wa Yesu.

CHORUS:
Karibie karibie, Sabato tamu,
Karibie Yesu pia, Bwana wa raha.

2
Itakase kweli, ukamsifu leo,
Yeye aliyesema, “Mimi ndiye njia,”
Nasi tukimfuata, Mkombozi hapa,
Atatunywesha tele, maji ya uzima.

3
Siku ya nderemo, tupishe wakati,
Tukimwimbia Yesu, rafiki mpendwa,
Mponya wetu leo, u mwema ajabu,
Ukae kwetu Bwana, moyoni daima.

085 - Salama Tumepita

1
Salama tumepita, safarini juma hii,
Tumwendee Mwokozi, atubariki sasa,
Siku hiyo ya raha, siku bora ya juma,
Siku hiyo ya raha, siku bora ya juma.

2
Utupe nuru leo toka hazina yako,
Ondoa dhambi zetu, tupokee na pendo,
Mikono yapumzika, tuishi ndani yako,
Mikono yapumzika, tuishi ndani yako.

3
Twakusanyika hapa, tusifu jina lako,
Ukaribie kwetu, tupe neema Bwana,
Utamu tusikize, wa raha ya milele,
Utamu tusikize, wa raha ya milele.

4
Injili yako leo, ishike wenye dhambi,
Itupe nguvu nyingi, iponye wenye shida,
Mioyo yetu shangaza, vyakula utulishe,
Mioyo yetu shangaza, vyakula utulishe.

086 - Ukaribie Tena

1
Ukaribie tena, ewe siku ya raha,
Roho yakusalimu, kama mwanga wa mbingu.

2
Raha yako tulivu, yafurahisha moyo,
Yatuliza taabu, hata waisha mwendo.

3
Ee siku takatifu, ya sifa na maombi,
Na kutuhekimisha, baraka yako kubwa.

087 - Siku ya Sabato

1
Siku ya Sabato, siku takatifu,
Watu wako Mungu wetu, waipenda sana.

2
Uliitakasa, uliibariki,
Siku hiyo ya Sabato, siku yako Bwana.

3
Nasi tubariki, tukikuabudu,
Katika siku ya raha, siku yako Bwana.

4
Halafu mbinguni, pamoja na Wewe,
Tunataka kuzishika, Sabato za Bwana.

088 - Siku Hii ya Sabato

1
Siku hii ya Sabato, tamu kufikiri,
Juu ya Mungu na mbingu, kuacha dunia.

2
Tamu kusikia neno, toka mhubiri
Anayefundisha toba, tupate uzima.

3
Katika vita na dhambi, ikiwa twashindwa,
Yeye atatupa nguvu, aonaye moyo.

089 - Bwana Asubuhi

1
Bwana asubuhi kucha, nitakuinua,
Sauti yangu kuomba, nipate baraka.

2
Nakuomba roho yako, niongozwe nayo,
Nifanye yanipasayo, na mapenzi yako.

3
Wanaokutegemea, u Mlinzi wao,
Matumaini wanayo, utayatimiza.

4
Na kwa wingi wa fadhili, nyumbani mwako juu,
Nitaingia na wimbo, pale kusujudu.

090 - Mapya Ni Mapenzi

1
Mapya ni mapenzi hayo,, asubuhi tuonayo,
Saa za giza hulindwa, kwa uzima kuamka.

2
Kila siku mapya pia, rehema wema na afya,
Wokovu na msamaha, mawazo mema furaha.

3
Tukijitahidi leo, na mwendo utupasao,
Mungu atatueleza, yatakayompendeza.

4
Mambo yetu ya dunia, Bwana atayang’aria,
Matata atageuza, yawe kwetu ya baraka.

5
Yaliyo madogo haya, Bwana tukimfanyia,
Yatosha tutafaidi, huvuta kwake zaidi.

6
Ewe Bwana siku zote, tusaidie kwa yote,
Mwendo wetu wote vivyo, uwe kama tuombavyo. 

091 - Kaa Nami

1
Kaa nami, ni usiku tena, usiniache gizani, Bwana,
Msaada wako haukomi, nili peke yangu, kaa nami.

2
Siku zetu hazikawi kwisha, sioni la kunifurahisha,
Hakuna ambacho hakikomi, usiye na mwisho kaa nami.

3
Nina haja nawe kila saa, sina mwingine wa kunifaa,
Mimi nitaongozwa na nani, ila wewe Bwana kaa nami.

4
Sichi neno uwapo karibu, nipata lo lote si taabu,
Kifo na kaburi haviumi, nitashinda kwako kaa nami.

5
Nilalapo nikuone wewe, gizani mote nimulikiwe,
Nuru za mbinguni hazikomi, siku zangu zote, kaa nami.

092 - Magharibini Jua

1
Magharibini jua, limekwisha kushuka,
Mwezi na nyota sasa, vinamsifu muumba wa usiku .

CHORUS:
Mungu Mtukufu, Mungu mkuu,
Wote juu mbinguni, na wanadamu chini twakusifu.
2
Mpaji wa uhai, ukaaye mbinguni,
Utuhifadhi sisi, tufahamu gizani u karibu.
3
Mapenzi yako makuu, yawe nasi usiku,
Tuli usingizini, kucha vivyo rohoni tushukuru.
4
Na utakapokuja, na nguvu kutawala,
Mungu wangu kubali, kunipeleka mimi uliko juu.

5
Baba Mwana Roho, Mungu wetu,
Wote juu mbinguni, na wanadamu chini twakusifu.

093 - Jua la Rohoni Mwangu

1
Jua la rohoni mwangu, mpendwa Mwokozi wangu,
Usiku giza hapana, ukiwa karibu Bwana.

2
Nikipata usingizi, nijaze fikara hizi,
Ni tamu sana, nilale pendoni mwako milele.

3
Kaa nami ewe Bwana, usiku kama mchana,
Nisiishi mbali nawe, ni uhai kuwa nawe.

4
Kama mtoto mnyonge, ameshawishwa atange,
Mtafute ewe Bwana, ujirudishie tena.

5
Wagonjwa wape amani, waneemeshe maskini,
Waliao, Mtulizi, wape wote usingizi.

6
Asubuhi tutokapo, tukaribie tulipo,
Twingiapo duniani, tuwe mwako mkononi.

094 - Po pote Mashamba Yajaa

1
Po pote mashamba yajaa, tele nafaka pevu,
Po pote yang’aa meupe, bondeni na nyandani.

CHORUS:
Mwenye mavuno twasihi, upeleke wavuni,
Wayakusanye mazao, hata kazi yaishe.

2
Wapeleke uchaoni, waende na jotoni,
Hata jua lishukapo, wakusanye ko kote.

3
Enyi wakazi wa bwana, yaleteni mazao,
Na jioni ingieni, kwake na furaha kuu.

095 - Sikieni Neno

1
Sikieni neno la Mungu wetu, zileteni zaka kwa hazina
Leteni na mioyo yenu yote, mibaraka itakuja.

CHORUS:
Zileteni zaka kwa hazina, kanijaribu sasa nazo,
Nitakupeni mibaraka, zaidi ya nafasi ya kupewa.

2
Wataka Roho Mtakatifu kwako? Uzilete zaka kwa hazina
Ukae karibu na Bwana wako, ndipo utabarikiwa.

3
Je, una kasoro na Bwana wako? Uzilete zaka kwa hazina,
Uzilete kama alivyosema, ndipo utabarikiwa.

4
Ushukuru Bwana na moyo wote, unapoleta zaka ghalani,
Usadiki ahadi zake zote, ndipo utabarikiwa.

5
Tuimbe sote nyimbo za furaha, tunapoleta zaka ghalani,
Tuimbe kabisa na furaha kubwa, kwani tutabarikiwa.


096 - Mali Yako Sasa

1
Mali yako sasa, Bwana, tunatoa,
Hatuna yaliyo yetu, yote ni vipaji.

2
Sisi watumishi, twaungama deni,
Tungeirudisha kwake, iliyo ya Bwana.

3
Utusaidie, upendo kujua,
Kwa ajili yao wote, walio gizani.

4
Neno tumaini, na kutegemea,
Kwamba lote tufanyalo, tulifanye kwako.


097 - Sioshwi dhambi Zangu

1
Sioshwi dhambi zangu, bila damu yake Yesu,
Hapendezewi Mungu, bila damu yake Yesu.

CHORUS:
Hakuna kabisa, dawa ya makosa,
Ya kututakasa, ila damu yake Yesu.

2
La kunisafi sina, ila damu yake Yesu,
Wala udhuru tena, ila damu yake Yesu.

3
Sipati patanishwa, bila damu yake Yesu,
Hukumu yanitisha, bila damu yake Yesu.

4
Sipati tumaini, bila damu yake Yesu,
Wema wala amani, bila damu yake Yesu.

5
Yashinda ulimwengu, hiyo damu yake Yesu,
Na kutufikisha juu, hiyo damu yake Yesu.

098 - Nilikupa Wewe

1
Nilikupa wewe, damu ya moyoni,
Ili wokolewe, winuke ufuni.

CHORUS:
Nimekunyima ni wewe? Umenipa nini?
Nimekunyima ni wewe? Umenipa nini?

2
Nilikupa miaka yangu duniani,
Upate inuka, kuishi mbinguni.

3
Nimekuletea, huku duniani,
Pendo na wokovu, vyatoka mbinguni.

4
Nipe siku zako, udumu mwangani,
Na taabu yako, wingie rahani.

CHORUS:
Nafsi nafsi pendo mali, twae Imanweli.
Nafsi nafsi pendo mali, twae Imanweli.

099 - Twende kwa Yesu

1
Twende kwa Yesu mimi nawe, njia atuonya tuijue,
Imo chuoni na mwenyewe, hapa asema njoo,

CHORUS:
Na furaha tutaiona, mioyo ikitakata sana,
Kwako Mwokozi kuonana, na milele kukaa.

2
“Wana na waje,” atwambia, furahini kwa kusikia,
Ndiye Mwokozi wetu hasa, na tumtii njoni.

3
Wangojeani? Leo yupo, sikiza sana asemapo,
Huruma zake zitwitapo, ewe kijana njoo.

100 - Kuwatafuta

1
Kuwatafuta wasioweza, kuomba wamrejee Yesu,
Kuwaambia maneno yake “Njooni kwangu nawapenda.”

CHORUS:
Nitakwenda (Nitakwenda) niwatafute wapotevu
(wapotevu) wageuke, waingie (Waingie) katika zizi
la Mwokozi (la Mwokozi)Yesu Kristo.

2
Kuwatafuta wasioweza, waonyeshwe Mwokozi wetu,
Kuwaongoza wapate wote, uzima ule wa milele.

3
Kazi hiyo nataka kufanya, leo nimesikia mwito,
Kuwainua waangukao, waletwe kwake Yesu njia.

101 - Yesu Akwita

1
Yesu akwita akwita wewe, uje leo, uje leo,
Kwani kusita akwita wewe, unatanga upeo,

CHORUS:
Msikie, msikie, Yesu akwita, ujitoe moyo sasa.

2
Waliochoka na wapumzike, uje leo, uje leo,
Wenye mizigo wenye huzuni, wapate mapumziko.

3
Anakungoja uliye yote, uje leo, uje leo,
Uliyekosa usijifiche, woshwe uvikwe nguo.

4
Yesu asihi wakawiao, waje leo, waje leo,
Watafurahi waaminio, amka upesi njoo.

102 - Mlangoni Pa Moyo

1
Mlangoni pa moyo, mgeni! (amesimama)
Amesimama pale, mgeni! (amesimama)
Umkaribishe sasa, umkaribishe mwana,
Wa Baba wa upendo, mgeni!(umkaribishe)

2
Moyo wako kwa Bwana, fungua. (fungulieni)
Asikuache mbali, fungua. (fungulieni)
Umkubali Rafiki, roho atafariji,
Naye atakutunza, fungua. (fungulieni)

3
Usikie sauti, ya Bwana. (uisikie)
Uyachague mambo, ya Bwana. (mambo ya Bwana)
Ufungue mlango, usimwambie bado:
Jina lake tumai, yu Bwana. (jina la Bwana)

4
Na ufungue moyo, kwa Bwana (fungulieni)
Utapewa msaada, wa Bwana (msaada wetu)
Uzuri utavikwa dhambi ataondoa,
Ukifungua moyo. kwa Bwana (fungulieni)

103 - Yesu Huita kwa Upole

1
Yesu huita kwa upole mwingi, atwita wewe nami,
Moyoni mwetu hungoja hukesha, hukungojea wewe

CHORUS:
“Njoni, kwangu, mliochoka njoni”
Yesu huita kwa upole mwingi, akwita, “uje kwangu”.

2
Atuombeapo usikawie, hutuombea sisi,
Usidharau wema na huruma, huruma kwetu sisi.

3
Siku za maisha hupita hima, hupita kwako kwangu,
Usiku waja kifo kinakuja, huja kwao na kwangu.

4
Fikiri juu ya upendo wake, upendo kwako kwangu;
Dhambi zetu amekwisha samehe, msamaha ni wetu.

104 - Yesu Aliniita, “Njoo”

1
Yesu aliniita “Njoo, Raha iko kwangu,
Kichwa chako ukilaze, kifuani mwangu,”
Nilikwenda kwake mara, sana nilichoka,
Nikapata kwake raha, na furaha tena.

2
Yesu aliniita “Njoo, kwangu kuna maji,
Maji ya Uzima bure, unywe uwe hai.”
Nilikwenda kwake mara, na maji nikanywa,
Naishi kwake na kiu, kamwe sina tena.

3
Yesu aliniita “Njoo, dunia i giza,
Ukiitazama nuru, ‘takung’arizia.
Nilikwenda kwake mara, yeye jua langu,
Ni kila wakati mwanga, safarini mwangu.

105 - Mchungaji mpenzi

1
Mchungaji mpenzi, hukuita uje,
Katika zizi lake, panapo salama,
Akina wanawake, waume vijana,
Yesu aliye kweli, huwaita kwake.

CHORUS:
Huita kwa moyo wa huruma, ‘uliyepotea uje kwangu,’
Hivi kukungoja anadumu, Bwana Yesu mchunga.

2
Akatoa maisha, kwa ajili yetu,
Ataka wapotevu, waje kwake sasa,
Tusijihatarishe, kwake tu salama,
Sikia wito wake, mchungaji wetu.

3
Tusikawie tena, adui shetani,
Kama mbwa wa mwitu, atatuharibu,
Tunaitwa na Yesu, mkombozi wetu,
Tuingie zizini, panapo nafasi.


106 - Ukitafuta Mali

1
Ukitafuta mali, huna wasaa kwa Yesu?
Kwa matendo ya haki, huna wasaa kwa Yesu?
Anasa za dunia, mambo yako ya raha,
Haya unatafuta, huna wasaa kwa Yesu?

2
Mambo yanakusonga, kwake huna nafasi?
Watekwa na dunia, kwake huna nafasi?
Humwoni m-langoni, anapopiga hodi?
Daima hukusihi, kwake huna nafasi?

3
Saa ni za thamani, kwake hamnayo kazi,
Wala hamfanyi bidii, kwake hamnayo kazi?
Hamkufikia kwao, waliomo shimoni,
Na waliopotea, kwake hamnayo kazi?

4
Na wazaa majani tu? Huna tunda kwa Yesu?
Mikono i mitupu, huna tunda kwa Yesu?
Huna chembe kwa ghala, kazi yako kulipa,
Wala huna furaha unapomwona Yesu.

107 - Sauti ni yake Bwana

1
Sauti ni yake Bwana, “Kwenda nani tayari?
Mavuno yanakawia, nani atayavuna?
Kwa kudumu anaita, zawadi atatoa,
Nani atakayejibu, “Nipo Bwana nitume.”

2
Kama huwezi safari, hata nchi za mbali,
Pana watu karibuni, wasiomjua Yesu,
Kama huwezi kusema, jinsi ya malaika,
Waweza kuutangaza, upendo wa Mwokozi.

3
Ingawa huwezi kuwa, mkesha mlangoni,
Ukiwatolea watu, nafasi ya uzima,
Kwa sala na kwa sadaka, watoa msaada,
Kama Haruni mwaminifu, kuinua mikono.

4
Roho za watu zikifa, Bwana akikuita,
Usiseme kwa uvivu, “Hakuna kazi kwangu.”
Kwa furaha anza kazi, ile aliyokupa,
Ukajibu mara moja, “Nipo Bwana, nitume.”

108 - Tumesikia Mbiu

1
Tumesikia mbiu, Yesu huokoa;
Utangazeni kote, Yesu huokoa.
Tiini amri hiyo, nchini baharini,
Enezeni mbiu hii, Yesu huokoa.

2
Imba nawe askari, Yesu huokoa,
Kwa nguvu ya kombozi, Yesu huokoa,
Imbeni wenye shida, unapoumwa moyo,
Mauti imeshindwa, Yesu huokoa.

3
Mawimbini uenee, Yesu huokoa,
Wenye dhambi jueni, Yesu huokoa,
Visiwa na viimbe, vilindi itikeni,
Na nchi shangilia, Yesu huokoa.

4
Upepo utangaze, Yesu huokoa,
Mataifa yashangaa, Yesu huokoa,
Milimani, bondeni, sauti isikike,
Ya wimbo wa washindi, Yesu huokoa.

109 - Anisikiaye

1
Anisikiaye aliye yote, sana litangaze wajue wote,
Duniani kote neno wapate, atakaye na aje!

CHORUS:
Ni “atakaye,” ni “atakaye,”
Pwani hata bara, na litangae,
Ni Baba mpenzi alinganaye, atakaye na aje.

2
Anijiliaye Yesu asema, asikawe aje hima mapema,
Ndimi njia kweli ndimi uzima, atakaye na aje.

3
Atakaye aje, ndiyo ahadi, atakaye hiyo haitarudi,
Atakaye lake ni la ahadi, atakaye na aje.


110 - Mlango Uko wa Wema

1
Mlango uko wa wema, mlango wazi huo,
Yesu ameufungua, na hakuna kufunga.

CHORUS:
Mlango wazi ajabu, uliachwa wazi kwangu.
Kwangu, Kwangu? Wazi wazi kwangu.

2
Mlango hukaa wazi, watu waokolewe.
Maskini na matajiri, wa mataifa yote.

3
Maadam mlango wazi, rafiki kaza mwendo,
Msalaba ukubali, amana ya upendo.

4
Msalaba tutabeba, daima na furaha,
‘Pendo wa Yesu hushinda, tunainama kwake.

111 - Tabibu Mkuu

1
Tabibu mkuu huyu, Yesu mwenye huruma,
Atuletaye faraja, Yesu Mwokozi wetu.

CHORUS:
Imbeni malaika, sifa za Bwana wetu,
Jina la pekee kwetu, ni la Yesu Bwana.

2
Mwana Kondoo msifuni, msifuni Mwokozi;
Hatia zote na dhambi, huziondoa Yesu.

3
Hakuna jina jingine, linalofaa sifa,
Au kutufurahisha, isipokuwa lake.

4
Naye atakapokuja, na utukufu wake,
Tutafurahi milele, kukaa kwake Bwana.

112 - Wewe umechoka sana?

1
Wewe umechoka sana? Wataka raha?
Kwake Yesu utapata msaada.

2
Alama anazo yeye? Sana makovu,
Ya mikono na miguu na mbavu.

3
Naye amevikwa taji, kichwani mwake?
Taji kweli alivikwa miiba.

4
Huku nikimfuata, nipate nini?
Maonjo nje na ndani - amani.

5
Kwamba namwandama yeye, mwisho ni nini?
Kurithi furaha naye - milele.

113 - Damu Imebubujika

1
Damu imebubujika, ni ya Imanweli,
Wakioga wenye taka, husafiwa kweli.

2
Ilimpa kushukuru, mwivi mautini,
Nami nisiye udhuru, yanisafi ndani.

3
Kondoo wa kuuawa, damu ina nguvu,
Wako wote kuokoa, kwa utimilivu.

4
Bwana tangu damu yako, kunisafi kale,
Nimeimba sifa zako, ‘taimba milele.

5
Bwana, umenikirimu, nisiyestahili
Kwa damu yako sehemu, ya mali ya kweli.

6
Nikubali kukwimbia, mbinguni milele.
Mungu nitamsifia, jina lako pekee.

114 - Yesu Mwokozi

1
Yesu Mwokozi ili nitakaswe, nataka moyo uwe enzi yako,
Ukiangushe kilichoinuka, unioshe sasa niwe mweupe.

CHORUS:
Mweupe tu, ndiyo mweupe,
Ukiniosha nitakuwa safi.

2
Bwana Yesu sasa unitazame, unifanye niwe dhabihu hai,
Najitoa kwako na moyo vyote, unioshe sana niwe mweupe.

3
Bwana kwa hiyo nakuomba sana, nakungojea miguuni pako,
Wanaokuja hutupi kamwe, unioshe sasa niwe mweupe.

115 - Naendea Msalaba

1
Naendea msalaba, ni mnyonge mpofu,
Yapitayo naacha, nipe msalaba tu.

CHORUS:
Nakutumaini tu, ewe Mwana wa Mungu;
Nainamia kwako, niponye sasa Bwana.

2
Nakulilia sana, nalemewa na dhambi,
Pole Yesu asema, “Nitazifuta zote.”

3
Natoa vyote kwako, nafasi nazo nguvu,
Roho yangu na mwili, viwe vyako milele.

4
Kwa damu yake sasa, amenivuta sana,
Upendo hubidisha, nimtafute Mwokozi.

116 - Bwana Ninataka Hili

1
Bwana ninataka hili, kwa kuwa nimechafuka,
Kwa moto au kwa maji, unisafishe kabisa.

CHORUS:
Unisafishe Mwokozi, ndani na nje kwa moto,
Utakavyo ili dhambi, ife kwangu ife kwangu.

2
Kupewa hekima yote, itakuwa tunu kubwa,
Lakini moyo safi ni, bora kwangu bora kwangu.

3
Mpaka moyo ni safi, siwezi kuyafahamu,
Mambo mazuri ya mbingu, mambo mazuri ya mbingu.

117 - Wamwendea Yesu?

1
Wamwendea Yesu kwa kusafiwa? kuoshwa kwa damu ya Kondoo?
Je, neema yake umemwagiwa? Waoshwa kwa damu ya Kondoo?

CHORUS:
Kuoshwa, kwa damu itutakasayo ya Kondoo,
Ziwe safi nguo nyeupe sana, waoshwa kwa damu ya Kondoo?

2
WamwandamadaimaMkombozi? waoshwakwadamuyaKondoo?
Yako kwa Msulubiwa mavazi? waoshwa kwa damu ya Kondoo?

3
Atakapokuja Bwana-arusi, uwe safi katika damu!
Yafae kwenda mbinguni mavazi, waoshwa kwa damu ya Kondoo?

4
Yatupwe yalipo na takataka, uoshwe kwa damu ya Kondoo, Huoni
kijito chatiririka, uoshwe kwa damu ya Kondoo

118 - Nilipotoka Kabisa

1
Nilipotoka kabisa, sasa narudi,
Nikakawia dhambini, Bwana narudi.

CHORUS:
Narudi nyumbani, daima kwako,
Kwa upendo nipokee, naja nyumbani.

2
Nikasusurika sana, sasa narudi,
Mwenye uchungu natubu, Bwana narudi.

3
Nimechoka maovuni, sasa narudi,
Pendo lako lanivuta, Bwana narudi.

4
Ndilo tumaini langu, sasa narudi,
Yesu alinifilia, Bwana narudi.

5
Damu yake yanitosha, sasa narudi,
Unioshe kenyekenye, Bwana narudi.

119 - Yesu Anasema

1
Yesu anasema, “Wewe huna nguvu,
Kesha ukaombe, na uje mwanangu.”

CHORUS:
Alilipa bei, nawiwa naye,
Dhambi ilitia waa, aliiondoa.

2
Bwana nimeona, uwezo wako tu,
Waweza takasa, mioyo michafu.

3
Sina kitu chema, kudai neema,
Hivi nitafua, mavazi kwa damu.

4
Ninaposimama, juu ya mawingu,
Taji nitaweka, miguuni pa Yesu.

120 - Msalaba wa Yesu

1
Msalaba wa Yesu, nikae karibu,
Pale pana chemchemi, ya kuponya dhambi.

CHORUS:
Pale msalaba, msalaba wake,
Huo ni sifa yangu, kwa maisha yote.

2
Karibu msalaba, nalitetemeka,
Pendo likaniona, likanirehemu.

3
Unikumbushe Yesu, nikuone pale,
Niupate upendo, na kuvutwa nao.

4
Karibu msalaba, kwa kutegemea,
Kukesha na kungoja, nitakaa pale.

121 - Katika Wenye dhambi

1
Katika wenye dhambi, ndimi mkuu wao,
Ila Yesu akaja, kwa dhambi alikufa,
Akamimina damu, niupate uzima.

2
Ajabu! Pendo lake, pendo lililo kuu,
Pendo lisilo mwisho, lidumulo milele,
Lililonitafuta, ingawa sikumpenda.

3
Ingawa ni mbaya, Kristo ni vyote kwangu,
Ajua haja zangu, huzuni zangu zake,
Hata katika vita, akiwapo salama.

122 - Yote Namtolea Yesu

1
Yote namtolea Yesu, moyo wangu ni wake,
Ninavutwa na upendo, kwa hivyo najitoa.

CHORUS:
Yote kwa Yesu, yote kwa Yesu,
Upendo wako hushinda, Yesu natoa.

2
Yote namtolea Yesu, nainamia pake,
Nimeacha na anasa, kwako Yesu nipokee.

3
Yote namtolea Yesu, nifanye niwe wako,
Nipe Roho yako, Bwana, anilinde daima.

4
Yote namtolea Yesu, nami naona sasa,
Furaha ya ukombozi, nasifu jina lake.

123 - Yesu kwa Imani

1
Yesu kwa imani, nakutumaini, peke yako,
Nisikie sasa, na kunitakasa, ni wako kabisa
Tangu leo.

2
Nipe nguvu pia, za kusaidia, moyo wangu,
Ulikufa wewe, wokovu nipewe, nakupenda wewe,
Bwana wangu.

3
Hapa nazunguka, katika mashaka, na matata,
Palipo na giza, utaniongoza, hivi nitaweza kufuata.

124 - Umechoka? Je, Umesumbuka?

1
Umechoka je umesumbuka? mwambie Yesu sumbuko
lako, Unayalilia yapitayo? mwambie Yesu pekee.

CHORUS:
Mwambie Yesu sumbuko lako, yu rafiki amini,
Hakuna rafiki kama yeye, mwambie Yesu pekee.

2
Je, machozi yakulengalenga? mwambie Yesu sumbuko
lako, Walemewa na dhambi rohoni? mwambie Yesu pekee.

3
Waogopa shida na majonzi? mwambie Yesu sumbuko lako,
Wasumbukia mambo yajayo? mwambie Yesu pekee.

4
Kuwazia kifo kukutisha? mwambie Yesu sumbuko
lako, Watamania ufalme wake? mwambie Yesu pekee.

125 - Uniangalie

1
‘Uniangalie’ atwambia, Yesu aliyetufia,
Msalabani ni uzima, hapa utaipata hazina.

CHORUS:
Kutazama Kalwari, kutazama Kalwari,
Ni kupewa kuishi, kuutazama mti.

2
Ninapojaribiwa ghafula, Shetani hatanitega,
Nikitazama msalaba, nguvu nitaipata kwa Bwana.

3
Msalaba nitautazama, kila wakati daima.
Ahadi nitategemea, hivi kabisa sitaanguka.

126 - Nina Haja Nawe

1
Nina haja nawe, kila saa,
Hawezi mwingine, kunifaa.

CHORUS:
Yesu nakuhitaji, vivyo kila saa,
Niwezeshe Mwokozi, nakujia.

2
Nina haja nawe, kaa nami,
Na maonjo haya, hayaumi.

3
Nina haja nawe, kila hali,
Maisha ni bure, uli mbali.

4
Nina haja nawe, nifundishe,
Na ahadi zako, zifikishe.

5
Nina haja nawe, mweza yote,
Ni wako kabisa, siku zote.

127 - Nionapo Amani Kama Shwari

1
Nionapo amani kama shwari, au nionapo shida,
Kwa hali zote umenijulisha, ni salama rohoni mwangu.

CHORUS:
Salama rohoni, ni salama rohoni mwangu.

2
Ingawa Shetani atanitesa, nitajipa moyo kwani,
Kristo ameona unyonge wangu, amekufa kwa roho yangu.

3
Dhambi zangu zote wala si nusu, huwekwa msalabani,
Wala sichukui laana yake, ni salama rohoni mwangu.

4
Ee Bwana himiza siku ya kuja, panda itakapolia,
Utakaposhuka sitaogopa, ni salama rohoni mwangu.

128 - Namwandama Bwana

1
Namwandama Bwana, kwa alilonena, njia zangu huning’azia
Na nikimridhisha, atanidumisha, taamini nitii pia.

CHORUS:
Kuamini, njia pekee ni hii,
Ya furaha kwa Yesu, amini ukatii.

2
Giza sina kwangu, wala hata wingu, yeye mara huviondoa,
Woga wasiwasi, sononeko basi, huamini nitii pia.

3
Masumbuko yote, sikitiko lote, kwa mapenzi hunilipia,
Baa dhara dhiki, vivyo hubariki, taamini nitii pia.

4
Mimi sitajua, raha sawasawa, ila yote Yesu kumtoa,
Napata fadhili, na radhi kamili, taamini nitii pia.

5
Nitamfurahia, na kumtumaini, majumbani na njia-njia;
Agizo natenda; nikitumwa huenda, huamini, nitii pia.

129 - Kumtegemea Mwokozi

1
Kumtegemea Mwokozi, kwangu tamu kabisa,
Kukubali neno lake, nina raha moyoni.

CHORUS:
Yesu Yesu namwamini, nimemwona thabiti,
Yesu Yesu yu thamani, ahadi zake kweli.

2
Kumtegemea Mwokozi, kwangu tamu kabisa,
Kuamini damu yake, nimeoshwa kamili.

3. Kumtegemea Mwokozi, kwangu tamu kabisa,
Kwake daima napata, uzima na amani.

4. Nafurahi kwa sababu, nimekutegemea,
Yesu mpendwa rafiki, uwe nami dawamu.

130 - Yesu Kwetu ni Rafiki

1
Yesu kwetu ni rafiki, wambiwa haja pia,
Tukiomba kwa Babaye, maombi asikia,
Lakini twajikosesha, twajitweka vibaya,
Kama tulimwomba Mungu, dua alisikia.

2
Una dhiki na maonjo? unamashaka pia?
Haifai kufa moyo, dua atasikia,
Hakuna mwingine mwema, wa kutuhurumia,
Atujua tu dhaifu, maombi asikia.

3
Je hunayo hata nguvu, huwezi kwendelea,
Ujapodharauliwa, njaporushwa pia,
Watu wakikudharau, wapendao dunia,
Hukwambata mikononi, dua atasikia.

131 - Namtegemea Mungu

1
Namtegemea Mungu niwapo, humo barani na baharini,
Yeye wa mbinguni anilinda, Baba wa mbinguni anilinda.

CHORUS:
Namwamini, Mungu anitunza (anitunza)
Milimani (milimani) au baharini (baharini), baharini
Moyo wangu (moyo wangu) aulinda (aulinda),
Baba wa mbinguni anilinda.

2
La waridi alinawirisha, na huyo tai juu angani,
Nami kweli ananilinda, Baba wa mbinguni anilinda.

3
Tunduni mwa simba namwamini, kwenye vita ama gerezani,
Motoni na furikoni, Baba wa mbinguni anilinda.

4
Bondeni mwa giza na upweke, mchunga wangu yu anilinda,
Kwa upole aniongoza, Baba wa mbinguni anilinda.




131a Kwa Mahitaji ya Kesho

Lord for Tomorrow and Its Needs
1
Kwa mahitaji ya kesho, sina ombi,
Unilinde nisitende dhambi leo, 
Nisiseme neno baya, Mkombozi, 
Nisifikiri uovu, leo hivi.

2
Ningefanya kazi sawa, na kuomba, 
Ningekuwa mtu mwema, kila saa, 
Mapenzi yako nifanye, na kutii, 
Nitoe mwili dhabibu, leo hivi. 

3
Kama leo ningekufa, kwa ghafula, 
Nitegemee ahadi, zako Bwana, 
Kwa mahitaji ya kesho, sina ombi,
Uniongoze nishike, leo hivi. 

132 - Bwana ni Mchunga

1
Bwana ni mchunga sitahitaji,
Majani mabichi malisho yangu.
Ananinywesha maji matulivu,
Atanirudisha nikipotea.

2
Nipitapo bondeni mwa mauti,
U mlinzi wangu sitaogopa,
Fimbo yako yatosha kunilinda,
Ukinifariji sina hasara.

3
Kati ya mateso meza waandaa,
Na kikombe changu kinafurika,
Umenipaka kichwani mafuta,
Nitaulizaje zaidi kwako?

4
Wema na fadhili zinifuate,
Siku zangu zote hata milele,
Nami nitakaa nyumbani mwa Bwana,
Katika ufalme wa pendo lake.

133 - Po pote na Yesu

1
Po pote na Yesu nina furaha, anitumako Yesu ndiyo raha,
Asipokuwako hapanifai, akiwapo Yesu mimi sitishwi.

CHORUS:
Po pote, po pote, sina mashaka,
Po pote na Yesu, naweza kwenda.

2
Akiwapo Yesu si peke yangu, na nijapotupwa akali wangu
Ajaponiongoza njia mbaya, niwapo na Yesu ninashukuru,

3
Akiwapo Yesu naweza lala, naweza pumzika hata kiyama,
Kisha nitakwenda kwake milele, akiwapo Yesu furaha tele.

134 - Tafuta Daima Utakatifu

1
Tafuta daima utakatifu, fanya urafiki na watu wote,
Nena siku zote na Bwana wako, baraka uombe kwa kila jambo.

2
Tafuta daima utakatifu, uwe peke yako ukimwabudu,
Ukimwangalia Mwokozi wako, utabadilishwa kama alivyo.

3
Tafuta daima utakatifu, kiongozi wako awe Yesu tu,
Katika furaha au huzuni, dumu kumfuata Yesu Mwokozi.

4
Tafuta daima utakatifu, umtawaze roho moyoni mwako,
Akikuongoza katika haki, hufanywa tayari kwa kazi yake.

135 - Saa Heri ya Maombi

1
Saa heri ya maombi, sasa kwako tunarudi,
Sumbuku ya kuondoa, shida zetu na pungufu,
Taabuni mara nyingi, roho zetu zimepona,
Mashakani tumeshinda, wakati wa saa tamu.

2
Saa heri ya maombi, twapeleka dhiki zetu,
Kwake aliyeahidi, kubariki wenye haja,
Huagiza tumwendee, tutegemee neno lake,
Hivyo tumwekee yote, wakati wa saa tamu.

3
Saa heri ya maombi, tutazidi kuingia,
Bomani mwetu na ngome, hata tuishapo mwendo,
Yesu atatusikia, tutamtafuta daima,
Na tutakapokutana, tutamwona-saa tamu.

136 - Unifundishe Baba

1
Unifundishe Baba, ile njia ya sala,
Uniendeshe sana, niwe kama Yesu.

CHORUS:
Niwe kama Yesu, niwe kama Yesu,
Uniongoze baba, niwe kama Yesu.

2
Unipe pendo baba, watu kuwaokoa,
Nyumbani na mjini, niwe kama Yesu.

3
Na unifahamishe, wakati ndio mfupi,
Unibidishe Bwana, niwe kama Yesu.

137 - Saa Heri ya Sala

1
Saa heri ya sala, tunapojidhili,
Kama tukija kwake Yesu rafiki,
Tukiwa na imani, kwamba yu mlinzi,
Waliochoka sana, watapata raha.

CHORUS:
Saa ya sala, iliyo heri,
Waliochoka sana, watapata raha.

2
Saa heri ya sala, ajapo Mwokozi,
Ili awasikie watoto wake,
Hutwambia tuweke, miguuni pake,
Mizigo yetu yote, tutapata raha.

3
Saa heri ya sala, wawezapo kuja,
Kwa Bwana Yesu wanaojaribiwa,
Moyo wake mpole, atawarehemu,
Waliochoka sana, watapata raha.

4. Saa heri ya sala, tutakapopewa
Mibaraka ya roho tukimwamini,
Kwa kuamini kweli, hatutaogopa,
Waliochoka sana, watapata raha.

138 - Nitakuandama Kote

1
Nitakuandama kote, nitakapoangizwa.
Wewe ukiniongoza, nami nitaandama.

CHORUS:
Nitakuandama kote, naam ulinifia,
Kwa neema yako Bwana, napenda kuandama.

2
Njia ijapoparuza, kwa miiba na fujo,
Ulitangulia mbele, nami nitaandama.

3
Nijapokuta taabu, na majaribu kote,
Nakumbuka shida yako, nami nitaandama.

4
Nijapoona ukiwa, na mateso makali,
Wewe uliyatikiza, nami nitaandama.

5
Ijapo wanipeleka, vilindini mwa giza,
Wewe uliyatikiza, nami nitaandama.

139 - Uliniimbie Tena

1
Uliniimbie tena, neno la uzima,
Uzuri wake nione, neno la uzima,
Neno hili zuri, lafundisha kweli.

CHORUS:
Maneno ya, uzima ni, maneno mazuri,
Maneno ya, uzima ni, maneno mazuri.

2
Kristo anatupa sote, neno la uzima,
Mwenye dhambi asikie, neno la uzima,
Latolewa bure, tupate wokovu.

3
Neno tamu la injili, neno la uzima,
Lina amani kwa wote, neno la uzima,
Litatutakasa, kwa haki ya mwana.

140 - Nitwae Hivi Nilivyo

1
Nitwae hivi nilivyo, umemwaga damu yako,
Nawe ulivyoniita, Bwana Yesu sasa, naja.

2
Hivi nilivyo si langu, kujiosha roho yangu,
Nisamehe dhambi zangu, Bwana Yesu sasa, naja.

3
Hivi nilivyo sioni, kamwe furaha moyoni,
Daima ni mashakani, Bwana Yesu sasa, naja.

4
Hivi nilivyo kipofu, maskini na mpungufu,
Wewe ndiwe u tajiri, Bwana Yesu sasa, naja.

5
Hivi nilivyo mimi tu, siwezi kujiokoa,
Na wewe hutanikataa, Bwana Yesu sasa, naja.

6
Hivi nilivyo, mapenzi yamenipa njia wazi,
Hali na mali sisazi, Bwana Yesu sasa, naja.

141 - Chini ya Msalaba

1
Chini ya msalaba, nataka simama,
Ndio mwamba safarini, wa kivuli chema,
Ni kweli kwa roho yangu, ni tuo kamili,
Tatua mzigo wangu, wakati wa hari.

2
Hapa ni pema sana, ni ngome kamili,
Hapa yameonekana, mapenzi ya kweli,
Kama alivyoonyeshwa, Yakobo zamani,
Msalaba umekuwa, ngazi ya mbinguni.

3
Na Yesu Msalabani, walimkemea,
Alikufa niokoke, niliyepotea,
Naona ajabu sana, ya mambo mawili,
Jinsi alivyonipenda, nisiyestahili.

4
Atakayeonana na, Yesu mbinguni,
Njia yake aanzapo, ni Msalabani;
Wokovu upo hapa tu, mwingine hapana,
Kisha kuna furaha kuu, pamoja na Bwana.

142 - Nasikia Mwito

1
Nasikia mwito, ni sauti yako,
Nikasafiwe kwa damu, ya kwangikwa kwako.

CHORUS:
Nimesogea, mtini pako,
Unisafi kwa damu, ya kuangikwa kwako.

2
Ni mnyonge kweli, umenipa nguvu,
Ulivyonisafi taka, ni utimilivu.

3
Yesu hunijuvya, mapenzi imani,
Tumai amani radhi, hapa na mbinguni.

4
Napata wokovu, wema na neema,
Kwako Bwana nina nguvu, na haki daima.

143 - Baba Sina Msaada

1
Baba sina msaada ila kwako pekee,
Kama kwangu ungefichwa, nifanyeje Baba?

CHORUS:
Sasa hivi naamini, Yesu alikufa,
Aliimwaga damu yake, nitoke dhambini.

2
Naamini mwana wako, nipe nguvu zako,
Nijazie mahitaji, katika saa hii.

3
Ni furaha gani kwangu, kukuona uso,
Nijue sauti yako, nipate neema.

144 - Ni Wako Bwana

1
Ni wako Bwana, ninasikia, unaponena nami,
Lakini kweli, nataka kwako, nizidi kusogea.

CHORUS:
Bwana vuta, (vuta) nije nisongee,
Sana kwako mtini,
Bwana vuta, (vuta) nije nisogee,
Pa damu ya thamani.

2
Niweke sasa, nikatumike, kwa nguvu za neema,
Uyapendayo, nami nipende, nizidi kukwandama.

3
Nina furaha, tele kila saa, nizungumzapo nawe,
Ninanena kama kwa rafiki, nikipiga magoti.

145 - Ulimwengu Siutaki

1
Ulimwengu siutaki, namtaka Bwana Yesu,
Dunia hunidanganya, Yesu yu mwaminifu.

CHORUS:
Rehema ni ya ajabu, pendo bila kipimo,
Wokovu mkamilifu, amana ya uzima.

2
Ulimwengu siutaki, namtaka Bwana Yesu,
Kati ya dhoruba kali, yeye wimbo mtamu.

3
Ulimwengu siutaki, namtaka Bwana Yesu,
Safarini duniani, yeye furaha yangu.

4
Ulimwengu siutaki, namtaka Bwana Yesu,
Msalaba naamini, hata namwona Yesu.

146 - Twae Wangu Uzima

1
Twae wangu uzima, sadaka ya daima,
Twae saa na usiku, zikutukuze huku.

2
Twae mikono nayo, ifanye upendayo,
Twae yangu miguu, kwa uongozi wako tu.

3
Twae sauti yangu, niimbe kwa Mungu tu,
Itwae na midomo, ijae neno lako.

4
Twae dhahabu pia, na yote ya dunia,
Twae yangu hekima, upendavyo tumia.

5
Nia itwae Mungu, haitakuwa yangu,
Twae moyo ni wako, uwe makazi yako.

6
Twae mapenzi yangu, sifa za moyo wangu,
Twae kabisa nafsi, niwe wako halisi

147 - Tawala Ndani Yangu

1
Tawala ndani yangu, ee Yesu mfalme,
Uwe kwangu majibu, kwa maswali yangu,
Uishi ndani yangu, wewe mwongozi,
Utumishi ni wangu, wako utukufu.

2
Hekalu nimetoa, umelisafisha,
Sasa fahari yako, imulike ndani,
Dunia iwe kimya, mwili sasa uwe,
Mtumwa mtulivu, wa kukutii tu.

3
Viungo vyake mwili, vyote vyakungoja,
Tayari vikiitwa, kwenda kusimama,
Bila manung’uniko, au malaumu,
Au kusumbuliwa, pasipo majuto.

4
Niwe na utulivu, pasipo haraka,
Tayari kungojea, maagizo yako,
Tawala ndani yangu, ee Yesu mfalme,
Uwe kwangu majibu, kwa maswali yote.
148 - Univute Karibu

1
Univute karibu Baba, unikumbatie,
Unisogeze kifuani, nataka pumziko.

CHORUS:
Univute karibu, (Vuta univute karibu)
Kwa kamba za upendo, (Kwa kamba, kamba za upendo)
Univute (Kwa kamba za upendo, univute karibu)
Karibu nawe. (Univute karibu)

2
Univute Mwokozi wangu, na tusiachane,
Mikono yako juu, yangu leo niione.

3
Univute kwa roho yako, nifanane nawe,
Unioshe unihuishe, niwe safi huru.


149 - Kuwa Wake Yesu

1
Kuwa wake Yesu, je ni kusudi lako?
Ungeenda naye, njia nyembamba?
Unataka aubebe, mzigo wako?
Awe Mwongozi wako.

CHORUS:
Uwezo wake unakutosha, na damu yake itakusafi,
Kwa vile ukubali ni bora, afanye mapenzi yake nawe.

2
Unataka kuitika, anapokwita?
Kupata amani, kwa kumpa vyote?
Wataka uwezo, usianguke kamwe?
Awe Mwongozi wako.

3
Wataka raha katika, ufalme wake?
Ungeshinda kwa majaribu yote?
Ungefanya kazi yake, vizuri sana?
Awe Mwongozi wako.

150 - Hasha Maneno Mabaya

1
Hasha maneno mabaya, yasitoke kinywani
Moyo mwema uzuie, ndimi zisichafuke.

CHORUS:
“Nanyi pendeni,” asema Yesu,
(mpendane) (mpendane)
Kama mwanzo alivyotupenda,
“Nanyi pendeni,” asema Yesu,
(mpendane) (mpendane)
Wana tiini amri hii (amri heri hii).

2
Pendo ni mtakatifu, urafiki mzuri,
Visiharibike mara, kwa kunena vibaya.

3
Tusinene kwa hasira, inazaa huzuni,
Pendo lako ee Mwokozi, linatosha tushinde.

151 - Huniongoza Mwokozi

1
Huniongoza Mwokozi, ndipo nami hufurahi,
Niendapo pote napo, ataniongoza papo.

CHORUS:
Kuongoza hunishika, kwa mkono wa hakika,
Nitaandamana naye, Kristo aniongozaye.

2
Pengine ni mashakani, nami pengine rahani,
Ni radhi ijayo yote, yupo nami siku zote.

3
Mkono akinishika, kamwe sitanung’unika,
Atakachoniletea, ni tayari kupokea.

4
Nikiisha kazi chini, sitakimbia mauti,
Kushinda ni ya hakika, nikiongozwa na Baba.

152 - Karibu na Wewe

1
Karibu na wewe, Mungu wangu,
Karibu zaidi, Bwana wangu,
Siku zote niwe, karibu na wewe,
Karibu zaidi, Mungu wangu.

2
Mimi nasafiri, duniani,
Pa kupumzika, sipaoni,
Nilalapo niwe, karibu na wewe,
Karibu zaidi, Mungu wangu.

3
Yote unipayo, yanivuta,
Pa kukaribia nitapata,
Na nielekezwe, karibu na wewe,
Karibu zaidi, Mungu wangu.

4
Na kwa nguvu, zangu nikusifu,
Mwamba uwe, maji ya wokovu,
Mashakani niwe, karibu na wewe,
Karibu zaidi, Mungu wangu.

5
Na nyumbani juu, Baba yangu,
Nikinyakuliwa, toka huko,
Kwa furaha niwe, pamoja na wewe,
Karibu zaidi, Mungu wangu.

153 - Fikira Moja tu

1
Fikira moja tu, hurejea tena,
Nimekaribia mbingu, zaidi ya jana.

CHORUS:
Karibu na, kwetu mbingu,
Karibu na kwetu sasa,
Nikwone karibu.

2
Karibu na kwetu, na kwenye makao,
Kiti cha enzi cha Mungu, pahali pa mto.

3
Kamilisha Yesu, kuamini kwangu,
Nikifika mwisho wangu, nikwone karibu.

154 - Yanipasa Kuwa Naye

1
Yanipasa kuwa naye, Mwokozi Bwana wangu,
Akiwa karibu nami, napata nguvu kweli.

CHORUS:
Moyo hauogopi, wala kutikisika.
Nitakwenda apendapo, kwa kuwa anilinda.

2
Yanipasa kuwa naye, kwani nategemea,
Anaweza kufariji, na maneno matamu.

3
Yanipasa kuwa naye maisha yangu yote,
Yakiwapo majaribu, na mashaka yo yote.

4
Yanipasa kuwa naye, katika njia zangu,
Macho yake yaongoza, hatua zangu zote.

155 - Njiani Huniongoza

1
Njiani huniongoza, Yesu wangu Mwokozi,
Rehema hatapunguza, milele kiongozi,
Ina raha kwandamana, duniani daima,
Nijaposumbuka sana, yeye hutenda vyema.

2
Njiani huniongoza, hupunguza matata,
Nikiugua hupoza, na njaa ninashiba,
Lichokapo guu langu, nguvu zikapungua,
Jiwe lilo mbele yangu, hunibubujikia.

3
Njiani huiongoza, kwa pendo lililo kuu,
Mwisho atanituliza, kwake Baba yangu juu,
Nikivikwa kutokufa, nikae na Mwokozi,
Nitamsifu sana sifa, kweli ni kiongozi.

156 - Uniongoze Yehova

1
Uniongoze Yehova, ni msafiri chini,
Ni mnyonge u hodari, nilinde kwa mkono.
Unitunze, unilinde, unionyeshe njia.

2
Na kisima cha uzima, maji ya utabibu,
Fungua na moyo wangu, ninywe na kuponyeka,
Uninyweshe, unilishe, hata nimetosheka.

3
Wakati wa kuuvuka, ule mto Yordani,
Hofu yangu hufariji, nione uso wako,
Nyimbo shangwe, nyimbo shangwe, nitaimba daima.

157 - Mfalme yu Mlangoni

1
Mfalme yu mlangoni, ndiye aliyetufia,
Mara wote wampendao, atawakusanya.

CHORUS:
Yuaja, yuaja, mlangoni anasimama,
Anakuja, anakuja, kuja kwake karibu.

2
Dalili za kuja kwake, zinazidi kutimizwa,
Karibuni wateule, watamlaki Bwana.

3
Sitafute duniani, amani wala furaha,
Mpaka Bwana arudi, dhambi kuondoa.

4
Tutakaa na Mwokozi, makaoni ya milele,
Daima tutafurahi, kuwa watu wake.

158 - U mwendo Gani Nyumbani?

1
U mwendo gani nyumbani? Mlinzi akanijibu,
“Usiku sasa waisha, macheo karibu,”
Usihuzunike tena, bali ulemee mwendo,
Hata ushike ufalme, kule mwangani juu.

2
Na tena niliuliza, nchi yote ikajibu,
“Sasa mwendo watimika, milele karibu,”
Usihuzunike tena, ishara kuu zasonga,
Na viumbe vyangojea, sauti ya Bwana.

3
Nikamwuliza shujaa, ndivyo kanitia moyo,
“Shikilia mapigano, kitambo yaisha,”
Usihuzunike tena, kazi ifanywe kwa moyo;
Tumeahidiwa tunu tuishapo shinda.

4
Siyo mbali na nyumbani, fikara tamu njiani,
yatupoza roho nayo, yafuta machozi,
Usihuzunike tena, kitambo tutakutana,
Wenye furaha kamili, nyumbani mwa Baba.
159 - Anakuja Upesi

1
Anakuja upesi Yesu Bwana wetu, msafiri mbali na kwao,
Alisema dhahiri “Nitakuja tena,” amina na uje Ee Bwana.

CHORUS:
Yuaja, Yesu atarudi sasa, anakuja duniani,
Wasafiri wote watapumzika, Yesu anaporudi tena.

2
Makaburi yote wafu wanapolala, yatafunguliwa tena,
Na maelfu pale wataondoka tena, wasione machozi kamwe.

3
Hatutatengana na hao tena huko, nyimbo nzuri tutaimba,
Watakusanyika toka kila kabila, miguuni pa Mwana Kondoo.

4
Aleluya amin aleluya tena, upendo wake unashinda,
Tutamsifu milele hata tutashangaa, jinsi alivyotukomboa.


160 - Watakatifu Kesheni

1
Watakatifu kesheni, nguvu za mbingu zagonga,
Washeni taa tayari, kwa kurudi kwake Bwana.

CHORUS:
Yuaja, Yesu mfalme, yuaja mwenye fahari,
Yesu yuaja enzini, karibu Yesu uje.

2
Piga mbiu tangazeni, habari ya ukombozi,
Ya mponya wa upendo, nayo nguvu ya samaha.

3
Falme nyingi zaangushwa, panda ya saba yalia;
Tangaza neema yake, kabla ya kupita saa.

4
Mataifa yapotea, nchi zajaa uchungu,
Kristo anaharakisha, unabii unatimizwa.

5
Wenye dhambi njoni sasa, Kristo awapatanishe,
Mbio twaeni neema, kitambo muda waisha.

161 - Piga Panda

1
Piga panda na ya makelele, Yesu yuaja tena,
Ipaze sauti imba sana, Yesu yuaja tena.

CHORUS:
Anakuja, anakuja, Yesu yuaja tena.

2
Itoe mwangwi sana vilima, Yesu yuaja tena,
Yuaja kwa utukufu mwingi, Yesu yuaja tena.

3
Itangazwe mahali po pote, Yesu yuaja tena.
Mwokozi aliyetufilia, Yesu yuaja tena.

4
Kuona machafuko twajua, Yesu yuaja tena,
Mataifa yakasiriana, Yesu yuaja tena.

5
Maradhi hofu hutuhubiri, Yesu yuaja tena.
Taabu, njaa hutulilia, Yesu yuaja tena.

162 - Tumaini Liko

1
Tumaini liko la thamani kuu,
Kupita anasa tupu zake ulimwengu.

2
Pana nyota nzuri nuru itoayo,
Kwetu wakati wa kifo ndio ufufuo.

3
Zikiumwa roho na hofu mashaka,
Sauti hutuambia Mungu hutupenda.

4
Kutoka Kalwari sauti hunena,
Nyota ni nuru ya mbingu tumaini letu.

163 - Pengine Ni Saa

1
Pengine ni saa ya kupambazuka, mishale ya jua
ipenyapo giza, kwamba atakuja Yesu mtukufu,
awapokee wake.

CHORUS:
Bwana itakuwa lini, tutakapoimba,
“Anakuja, Bwana Yesu, Aleluya, Amin,
Aleluya, Amin?”

2
Pengine mchana pengine jioni, pengine usiku wa
manane, giza litatoweka kwa fahari akija, awapokee
wake.

3
Majeshi yake yataimba ‘hosana,’ na watakatifu
waliotukuzwa, watamsifu kwa kuwa amekuja,
awapokee wake.

4
Furaha tukiitwa pasipo kufa, pasipo kuona maradhi
machozi, kuchukuliwa winguni kwa fahari,
akija kwa watu wake.

164 - Unakaribia Wakati

1
Unakaribia wakati wa kuja kwa Yesu,
Atawachukua watu wake nyumbani juu.

CHORUS:
Tunaiona mishale ya nuru inayopenya giza,
Tunaiona mishale ya nuru ya ufufuo.

2
Injili inatangazwa pote kwa mataifa,
Bwana wa Arusi atakuja na tarumbeta.

3
Pamoja na malaika zake Bwana arudi,
Awapeleke waaminifu wasife tena.

4
Wapenzi waliotengwa kale watakutana,
Machozi yao wenye huzuni yatafutika.

165 - Ahadi Tamu

1
Ahadi tamu kwa waamini, tazama nakuja upesi sana,
Uwe imara hatari kubwa, ndugu usilale, bali ukeshe.

CHORUS:
Uihifadhi imani yako, dunia mpya itatolewa.
Njoo ingia furaha yangu, taji zinangoja, uwe imara.

2
Tutakesha na kutoa sala, atakuja kama mwivi kwa wengi,
Ya kwamba yu karibu twajua, ila hatujui ni siku gani.

3
Tunategemea neno lake, ambalo latangaza kuja kwake,
Tumaini letu ni ahadi, “naja karibuni,” uwe imara.

166 - Furaha kwa Ulimwengu

1
Furaha kwa ulimwengu, Bwana atakuja.
Kila moyo umpokee, viumbe imbeni,
Viumbe imbeni, viumbe vyote imbeni.

2
Na Bwana atatawala, watu na waimbe,
Miti milima na mawe, kariri furaha,
Kariri furaha, kariri furaha kubwa.

3
Atatawala kwa wema, atawafundisha
Mataifa haki yake, ajabu za pendo,
Ajabu za pendo, ajabu za pendo lake.

167 - Yesu Bwana Mwokozi

1
Yesu Bwana Mwokozi, aishi milele,
Najua kwamba yupo, pamoja na mimi;
Sauti nasikia, rehema naona,
Wakati namhitaji, yupo nami.

CHORUS:
Yu hai, yu hai, yu hai Bwana Yesu,
Atembea, azungumza nami siku zote.
Yu hai, yu hai, kutoa uzima,
Hivi ndivyo nijuavyo,
Yu hai ndani yangu.

2
Ulinzi wake upo, naona dhahiri,
Miguu ichokapo, sikati tamaa,
Najua aniongoza, katika dhoruba,
Siku ya kuja kwake, nitamwona.

168 - Tarumbeta ya Mwana

1
Tarumbeta ya Mwana itakapolia mara,
Milele itakapopambazuka,
Nao wa haki watakapokusanyika ng’ambo,
Majina yaitwapo lo! niweko.

CHORUS:
Majina yaitwapo lo, Majina yaitwapo lo,
Majina yaitwapo lo, Majina yaitwapo lo niweko.

2
Siku ile watakatifu watakapoamka,
Nakuondoka huru kaburini,
Watakapokusanyika makaoni kule juu,
Majina yaitwapo lo niweko.

3
Tutende kazi ya Yesu mchana kutwa kwa bidii,
Tutangaze kote pendo lake kuu,
Nayo kazi itakapotimika hapa chini,
Majina yaitwapo lo niweko.

169 - Hapo Yesu Atakapoita

1
Hapo Yesu atakapoita, mataifa mbele yake,
Tutashindaje kwenye hukumu, mbele ya kiti cha enzi.

CHORUS:
Atakusanya ngano ghalani, atatupa mbali makapi,
Tutashindaje hukumuni, siku kuu ya kiyama?

2
Je tutasikia neno tamu, “Vema wewe mtumwa mwema,”
Ama wenye uchungu na hofu, tutakatazwa ufalme?

3
Atakubali tu kwa furaha, watoto wake wapendwa,
Atawapa mavazi meupe, wakae kitini pake.

4
Hivyo tukeshe nasi tungoje, wenye taa zinazowaka,
Tutakapoitwa arusini, tuwe tayari kumlaki.

5
Roho ikielekea mbingu, twangoja wenye saburi,
Hata safari yetu iishe, tukae kwake milele.

170 - Siitafuti Mali

1
Siitafuti mali, wala utajiri,
Nataka kwa yakini, nipate Mwokozi.
Chuoni mwa ufalme, niambie Yesu,
Jina langu yakini, je limeandikwa?

CHORUS:
Je limeandikwa? Jina langu huko?
Kitabuni mbinguni, je, limeandikwa?

2
Dhambi zangu ni nyingi, ni kama mchanga,
Lakini damu yako, mwokozi yatosha,
Kwani umeahidi, zijapo nyekundu,
Zitakuwa nyeupe, ilivyo theluji.

3
Mji mzuri sana, wa majumba makuu,
Walipo malaika, mji bila ovu,
Wakaapo walio, na mavazi safi,
Je limeandikwa, jina langu huko.

171 - Imeanzishwa Hukumu

1
Imeanzishwa hukumu mbinguni, tutasimamaje pale,
Apimapo Mungu Hakimu, kila wazo na tendo?

CHORUS:
Tutasimamaje sote katika siku kuu ile?
Dhambi zetu zitafutika, ama zitatuangusha?

2
Wametangulia wafu kupimwa, kitambo ndipo wahai,
Watapokea neno la mwisho, vitabuni mwa Mungu.

3
Tutasimamaje usiku ule, siri zetu kila moja,
Zafunuliwa toka vitabu, Yesu atusaidie!

172 - Mfalme Wetu Atuita

1
Mfalme wetu atuita, tukae karamuni kwake,
Itakuwaje nasi kule, Bwana ajapo?

CHORUS:
Bwana ajapo ndugu, Bwana ajapo,
Itakuwaje na sisi, Bwana akija?

2
Atavikwa vizuri sana, taji badala ya miiba,
Kweli tukeo la fahari, Bwana ajapo.

3
Kwa furaha awakubali, wenye mavazi ya arusi,
Tu wa heri tukimridhisha, Bwana ajapo.

4
Kutakuwako na utengo, watalia waliomwasi,
Cha kutisha kipindi kile, Kristo ajapo!

5
Mfalme utupe neema, sisi tunapokungojea,
Tusiogope kukuona, ujapo Bwana.

173 - Hatujui Saa

1
Hatujui saa ya kuja kwa Bwana, lakini dalili zasema
karibu, Atakaporudi lakini kwa kweli, hatujui saa.

CHORUS:
Atakuja, kwa vile tukeshe,
Atakuja, Mwokozi aleluya,
Atakuja kwa fahari, ya baba yake,
Hatujui saa.

2
Pana nuru kwao wapendao haki, pana kweli katika chuo
cha Mungu, Unabii hufundisha kuja kwake, hatujui saa.

3
Tutakesha na tutaomba daima, tutafanya kazi mpaka
akija, Tutaimba na tutasoma ishara, hatujui saa.

174 - Sijui Atakapokuja

1
Sijui atakapokuja, mchana au usiku,
Labda saa ya alasiri, pengine ni alfajiri,
Hutwambia tuwe tayari, taa zetu tusizime,
Ili ajapo atukute, tuwe tukimngoja Yeye.

CHORUS:
Tu... kimngoje.......a,
(Kukesha tunakungoja Wewe)
Tu... kimngoja.......a,
(Kukesha tunakungoja Wewe)
Tu... kimngoje........a,
(Kukesha tunakungoja wewe)
Twakesha twamngoja Yeye.

2
Nakumbuka huruma zake, bei ya wokovu wetu,
Aliacha nyumba tukufu, awafilie wabaya,
Ninadhani itampendeza, kama sisi watu wake,
Tukionyesha pendo letu, tuwe tukimngoja Yeye.

3
Ee Yesu Mwokozi mpendwa, wajua nalihifadhi,
Tumaini la kukuona, la kukaribishwa nawe,
Ukija kwa watu wengine, kama mhukumu wao,
Kwangu utakuwa rafiki, nakesha nakungojea.

175 - Nitaonana na Yesu

1
Nitaonana na Yesu, uso kwa uso kweli,
Siku ile shangwe tele, nikimwona Mwokozi.

CHORUS:
Tutaonana kwa macho, huko kwetu mbinguni,
Na kwa utukufu wake, nitamwona milele.

2
Sasa siwezi kujua, jinsi alivyo hasa,
Bali atakapokuja, nitamwona halisi.

3
Mbele yake yafukuzwa, machozi na huzuni,
Kipotovu kitanyoshwa, fumbo litafumbuka.

4
Uso kwa uso hakika, palepale furaha,
Nitafurahi kabisa, nikimwona Mwokozi.

176 - Ati twonane Mtoni?

1
Ati twonane mtoni? Maji mazuri ya mbingu,
Yanatokea mwangani, penye kiti cha Mungu.

CHORUS:
Naam twonane mtoni, watakatifu kwenu ni mtoni,
Tutakutanika kule mtoni, penye kiti cha Mungu.

2
Tukitembea mtoni, na Yesu mchunga wetu,
Daima tu ibadani, usoni pake kwetu.

3
Tukisafiri mtoni, tutue ulemeao,
Wema wa Mungu yakini, una taji na vazi

4
Kwang’ara sana mtoni, cha Mwokozi ni kioo,
Milele hatuachani, tumsifu kwa nyimbo.

5
Karibu sana mtoni, karibu tutawasili,
Mara huwa furahani, na amani ya kweli.

177 - Kazi Yangu Ikiisha

1
Kazi yangu ikiisha, nami nikiokoka,
Na kuvaa kutokuharibika,
Nitamjua Mwokozi, nivukapo ng’amboni,
Atakuwa wa kwanza kunilaki.

CHORUS:
Nitamjua, nitamjua, nikimwona uso kwa uso,
Nitamjua, nitamjua, kwa alama za misumari.

2
Kuona uso wake, kutanipa Furaha,
Furaha isiyo ya kukomesha,
Nitamsifu Mwokozi, kwa rehema na pendo,
Vilivyonipa pahali mbinguni.

3
Nao waliokufa, katika Bwana Yesu,
Nitawaona tena huko juu,
Lakini nifikapo, kwake huko mbinguni,
Nataka kumwona Mwokozi kwanza.

4
Milangoni mwa mji, Bwana atanipisha,
Pasipo machozi wala huzuni,
Nitauimba wimbo, wa milele lakini,
Nataka kumwona Mwokozi kwanza.

178 - Ukingoni Mwa Yordani

1
Ukingoni mwa Yordani, ninaangalia,
Bara nzuri ya Kanaani, ninayotamani.

CHORUS:
Tutakaa pamoja na Yesu,
Katika pwani yenye raha,
Tutaimba wimbo wa Musa na Kondoo,
Milele hata milele.

2
Bara ile ina nuru, nuru ya milele,
Kristo jua hutawala, hufukuza giza.

3
Nitapafikia lini, na kubarikiwa,
Penye ufalme wa Baba, na kumwona uso.

4
Furaha yangu rohoni ni kuchukuliwa,
Siyaogopi mawimbi katika Yordani.

179 - Wavunaji Watafurahi

1
Wavunaji watafurahi, pale watakaporudi,
Wakiyaleta mavuno, hata Yerusalemu.

CHORUS:
Furaha wataipata, furaha hata milele,
Furaha wataipata, wakati wa mavuno.

2
Na siku ile tutaimba, kumshukuru na kumsifu,
Bwana Yesu jumbe wetu, kule Yerusalemu.

3
Wavunaji watafurahi, makaoni mwa milele,
Yaliyowekwa tayari, kule Yerusalemu.

180 - Pana Mahali Pazuri Mno

1
Pana mahali pazuri mno, twapaona kwa mbali sana,
Baba yetu angoja pale, amepanga makao yetu.

CHORUS:
Kitambo tu bado, tutakutana ng’ambo pale,
Kitambo tu bado, tutakutana ng’ambo pale.

2
Tutaimba pale kwa moyo, nyimbo tamu za wenye heri,
Na rohoni hatutaona, tena haja ya kupumzika.

3
Kwa Baba yetu mkarimu, tutatoa shukrani sana,
Kwa kipaji cha pendo lake, na baraka anazotupa.

181 - Mahali pa Maji

1
Mahali pa maji mazuri, maji ya uzima,
Anapotungojea Yesu, tutakaribishwa.

CHORUS:
Mahali pa maji mazuri, penye maji ya uzima,
Tutakaa na Mwokozi, chemchemi ya uzima.

2
Tunapochoka safarini, tamu kupumzika.
Panapo maji ya uzima, yatufurahisha.

3
Una kiu? uje kwa Yesu, utaburudishwa,
Yesu yu maji ya uzima, unywe uokoke.

182 - Mchana Hauishi

1
Mchana hauishi, mjini mzuri,
Mji hautapita, na hapana giza.

CHORUS:
Machozi yatafutwa, kifo hakuna kule,
Hawahesabu siku, na hapana giza.

2
Milango ni ya lulu, mjini mzuri,
Dhahabu njia zake, na hapana giza.

3
Milango haifungwi, mjini mzuri,
Mto ni wa uzima, na hapana giza.

4
Hawahitaji jua, mjini mzuri,
Mwana Kondoo nuru, na hapana giza.

183 - Furaha na Raha

1
Furaha na raha tutapata, furaha na raha tutapata,
Furaha na raha tutapata, Yesu anaporudi.

CHORUS:
Yesu anaporudi (rudi), Yesu anaporudi (rudi),
Furaha na raha tutapata, Yesu anaporudi.

2
Tutaimba nyimbo za shangwe kuu,
Tutaimba nyimbo za shangwe kuu,
Tutaimba nyimbo za shangwe kuu ,Yesu anaporudi.

3
Hapana machozi arudipo, hapana machozi arudipo,
Hapana machozi arudipo, kwa wateule wake.

184 - Vitu Vyote ni Sawa

1
Vitu vyote ni sawa, panapo pendo,
Kila sauti tamu, panapo pendo.
Pana amani pale, na furaha nyumbani,
Siku zote salama, panapo pendo.

CHORUS:
Panapo upendo, siku zote salama, panapo pendo.

2
Furaha i nyumbani, panapo pendo,
Hapana machukizo, panapo pendo,
Chakula ni kitamu, mashamba yasitawi,
Maisha ni kamili, panapo pendo.

3
Hata mbinguni juu, pana furaha,
Wakiona upendo, nyumbani mwetu.
Macho yanapendezwa, na viumbe vya Mungu,
Naye Mungu huona, panapo pendo.

4
Ee Yesu niwe wako, wako kabisa,
Ndipo patakuwako pendo nyumbani.
Nitakaa salama, sitaifanya dhambi,
Nitabarikiwa tu, panapo pendo.
185 - Mungu U Mapenzi

1
Mungu u mapenzi makamilifu, yapitayo fahamu za watu,
Twanyenyekea sisi wapungufu, wape baraka wapenzi wetu.

2
Ewe Mapenzi yasiyopimika, twawaombea kitini Mwako,
Wape mapenzi yasiyotindika, waliooana mbele yako.

3
Ewe uhai, wewe u dhamana, ya imani na matumaini,
Wape kuvumilia hapa sana wasiche maumivu mwishoni.

4
Wape furaha hiyo iwezayo, kutia nuru kwenye huzuni,
Wape amani hiyo itokayo, katika matata duniani.

5
Waende mbele kusaidiana, maisha yao ulimwenguni,
Hata mwisho, ni kuja kwake Yesu, wafurahi milele mbinguni.

186 - Tuonanapo na Rafiki

1
Tuonanapo na rafiki sote twafurahi,
Ila tumepaswa mwishowe kuagana tena.

CHORUS:
Hatutaagana tena nyumbani mbinguni,
Kwenye nchi tamu juu, hatutaagana.

2
Twatumaini kwa furaha tutaonana juu,
Na rafiki tulioaga tuishapo shinda.

3
Kule hatutatamka kamwe neno la kuaga,
Tutaimba daima tena nyimbo za furaha.

187 - Kufariki Naye Yesu

1
Kufariki naye Yesu, usingizi wenye heri,
Raha isiyofujika, kwa majonzi na adui.

2
Kufariki naye Yesu, lo ya kubwaga simanzi
Na kulala na amani, hata Bwana awatuze.

3
Kufariki naye Yesu, heri watakaoamshwa,
Wataona siku ile, utukufu wake Bwana.

4
Kufariki naye Yesu, wataamka aitapo,
Watapasua kaburi, na kutoka watukufu.


188 - Wimbi la Damu

1
Wimbi la damu ya Yesu, linatutakasa,
Aliumia kusudi, tupate uzima.

CHORUS:
Wimbi la damu naona, naingia natakaswa,
Bwana asifiwe sana, hutakasa hutakasa.

2
Damu inasema kwangu, nasikia mvuto,
Inasema moyo wangu, hutakaswa nayo.

3
Naondoka kutembea, kwa nuru ya mbingu,
Mavazi yamesafishwa, moyoni ni Yesu.

4
Neema ni ya ajabu, kutakaswa ndani,
Na kuwa naye Yesu tu, aliye Mwokozi.



189 - Mimina Upya

1
Mimina upya, nguvu toka juu,
Tupe pendo lako, ewe Mwokozi.

CHORUS:
Twakusihi sana, Yesu Mwokozi,
Tubatize upya, kwa Roho leo.

2
Kwako twalia, wenye maovu,
Osha moyo wetu, ututakase.

3
Kipaji cha juu, kitume kwetu,
Tubariki sasa, utufariji.

4
Isikilize, kwa moyo wazi,
Sauti ya Roho, ubarikiwe.
Meza ya Bwana

190 - Raha Yangu Yote, Bwana

1
Raha yangu yote Bwana, i mbavuni pako,
Mimi sina haja tena, ila kifo chako.

2
Mwokozi uliyekufa, nawe ndiwe Mungu,
Kifo chako ni kwa dhambi, ziondoe zangu.

3
Nioshe na niwe wako, nawe uwe wangu,
Nioshe damuni mwako, liwe fungu langu.

4
Nioshe si miguu tu, osha tangu nyayo,
Hata kichwa changu juu, na ndani ya moyo,

5
Na iwe kafara damu, nifanyapo kazi,
Hata imani itimu, nikuone Mwokozi.

191 - Mkate wa Mbingu

1
Mkate wa mbingu mega kwetu, ulivyotoa kwa thenashara,
Katika kitabu twakuona, Moyo unatweta kukutana.

2
Neno la ukweli libariki, tusikie mwito wa upole,
Vizuizi vyote vitakoma, tena tutapata uungwana.

3
Uzima na nguvu utanena, nakimbilia kukufuata,
Lakini mnyonge ndiye mimi: naye mshindaji ndiye wewe!

192 - Mwamba Wenye Imara

1
Mwamba wenye imara, kwako nitajificha,
Maji hayo na damu, yaliyotoka humu,
Hunisafi na dhambi, hunifanya mshindi.

2
Kwa kazi zote pia, sitimizi sheria.
Nijapofanya bidii, nikilia na kudhii,
Hayaishi makosa, ndiwe wa kuokoa.

3
Sina cha mkononi, naja msalabani,
Nili tupu nivike, ni mnyonge nishike,
Nili mchafu naja, nioshe nisijafa.

4
Nikungojapo chini, na kwenda kaburini,
Nipaapo mbinguni, na kukwona enzini,
Roho yangu na iwe, rahani mwako wewe.
193 - Sauti ya Mchungaji

1
Sauti ya Mchungaji, ninasikia jangwani,
Kondoo waliopotea, anawaita warudi.

CHORUS:
Leteni, leteni, leteni toka dhambini,
Leteni, leteni, waleteni kwa Yesu.

2
Nani atakayekwenda, amsaidie Mchungaji,
Awarudishe zizini, wasife bure gizani.

3
Usikose kusikia, sauti ya Mchungaji,
Kondoo waliopotea nenda na kuwatafuta.


194 - Twaomba Bwana

1
Twaomba Bwana, umpokee kama mhudumu,
Ambaye anajitoa, kuwa mtumishi.

2
Twaomba Bwana, umpokee kama mhudumu,
Neno lako alitoe, mwangaza kung’aa.

3
Mwokozi wetu, twaomba na umwandikie,
Kitabuni mwako, juu mjumbe wa injili.

4
Silaha zake, apewe kumshinda adui,
Vitani awe hodari, mpaka mauti.

5
Yeye ashindaye, Bwana kwa rehema yako,
Ile taji ya dhahabu, nawe utampa.
Kuweka Kanisa Wakfu

195 - Msingi wa Kanisa

1
Msingi wa Kanisa ndiye Yesu Bwana,
Kiumbe chake kipya akipenda sana,
Kutaka ‘kitafuta alishuka chini,
Naye kwa haja yake, akafa mtini.

2
Lina kila kabila kisha ndiyo moja,
Wokovu wake una Mwokozi mmoja,
Uzazi ni umoja moja tumaini,
Chakula ni kimoja, moja tumaini.

3
Watu hustaajabu kwa mashaka yote,
Yaipatayo nje hata ndani mwote,
Ila watakatifu humwomba wakikesha,
Usiku ni kilio, asubuhi raha.

4
Mashaka na taabu hata vita vyake,
Vyangoja matimizo ya amani yake,
Ndipo kwa macho yetu twone utukufu,
Kanisa ya kushinda, itastarehe juu

196 - Kitambo Bwana Yuaja

1
Kitambo Bwana yuaja, atafute kote
Vito vya thamani kubwa, mali yake kuu.

CHORUS:
Kama nyota tajini, vitang’aa sana,
Vito vizuri kweli, vyenye thamani.

2
Karibu atakusanya, vito kwa ufalme,
Vizuri vinavyong’aa, mali yake kuu.

3
Watoto wote wadogo, wampendao Yesu,
Ndiyo vito ving’aavyo, mali yake kuu,

197 - Anipenda ni Kweli

1
Anipenda ni kweli, Mungu anena hili,
Sisi wake watoto, kutulinda si zito.

CHORUS:
Yesu Mwokozi, ananipenda,
Kweli hupenda, Mungu amesema.

2
Kwa kupenda akafa, niokoke na kifo,
Atazisafi taka, sana ataniweka.

3
Anipenda kabisa, niuguapo sasa,
Anitunza mbinguni, niliyelala chini.

4
Kunipenda haachi, tu sote hapa chini,
Baada ya mashaka, kwake tanipeleka.

198 - Nilinawa Mikono

1
Nilinawa mikono, safi asubuhi,
Itende kazi kutwa, kwa Yesu Mwokozi.

CHORUS:
Kaza sana macho, njiani kote,
Utende kwa Yesu, kazi njema tu.

2
Natega masikio, nitambue wasaa,
Mikono na itende, upole daima.

3
Macho yangu yachunga, mikono kazini,
Ilindwe maovuni, impendeze Yesu.

199 - Upendo ni Furaha

1
Upendo ni furaha, ni kweli desturi,
Yake kuzisahihisha njia zetu zote.

CHORUS:
Yu pendo, tu watoto wake.
Yu pendo, mwana wa Mungu,
Na sisi tupendane, kama Baba Mungu,
Amri yake ndiyo hii, kupendana sana.

2
Duniani huzuni, ugonjwa mauti,
Kwa pendo tuwafariji wenye mahitaji.

3
Na atakapokuja, kutuchukua juu,
Tutaimbia milele pendo lake Yesu.

200 - Baba Yetu Aliye Mbinguni

1
Baba yetu aliye mbinguni, amenifurahisha yakini,
Kuniambia mwake chuoni, ya kuwa nami Yesu pendoni.

CHORUS:
Anipenda Mwokozi Yesu, anipenda, anipenda,
Anipenda Mwokozi Yesu, anipenda mimi.

2
Nimuachapo kutanga mbali, yeye yu vivyo hupenda kweli,
Hunirejeza kwake moyoni, kweli yu nami Yesu pendoni.

3
Anipenda, nami ninampenda, kwa wokovu alionitenda,
Akanifilia Msalabani, kwa kuwa nami Yesu pendoni.

201 Mungu Huona Vindege

1
Mungu huona videge, wanaoanguka,
Akiwapenda videge, vile hunipenda.

CHORUS:
Hunipenda, hunipenda, hunipenda pia,
Najua ananipenda, niliye mdogo.

2
Rangi ya namna nzuri, hupamba maua,
Akiyapenda maua, vile hunipenda.

3
Mungu aliyeviumba, videge, maua,
Hatasahau watoto, kweli huwapenda.

202 Sikia Mlio

1
Sikia mlio, pesa koponi
Zinalialia, zote kwa Yesu.

CHORUS:
Kuanguka kuanguka, pesa koponi,
Kila moja kwako, Yesu zipokee.

2
Huanguka pesa, toka mikono,
Sadaka kwa Yesu, ya kundi dogo.

3
Tulio wadogo, tuna haba tu,
Tuishapo kua, ‘tatoa zaidi.

4
Wenye mali chache, tumpe moyo,
Kwa furaha tupu, atakubali.

203 Siku Sita Fanya Kazi

1
Siku sita fanya kazi, ya saba ni kwa Yesu.
Hapo tunapopumzika, kwani ni yake Yesu.

CHORUS:
Moja mbili tatu nne, tano sita zote kwetu,
Lakini tutakumbuka, ya saba ni kwa Yesu.

2
Huonyesha ya kufanya, kwa kuwa ni ya Yesu,
Na atuonyesha njia, tutamfuata Yesu.

3
Tuombe kila Sabato, na kujifunza kwake,
Tutamtii daima, tutakaa na Yesu.

204 Kuwa na Yesu Nyumbani

1
Kuwa na Yesu nyumbani,
Furaha nyingi, Furaha nyingi,
Furaha nyingi.
Kuwa na Yesu nyumbani,
Furaha nyingi, Furaha nyingi.

2
Yesu yu ndani ya Baba,
Nyumba salama, nyumba salama, nyumba salama,
Yesu yu ndani ya Baba,
Nyumba salama, nyumba salama.

3
Yesu yu ndani ya Mama,
Nyumba salama, nyumba salama, nyumba salama,
Yesu yu ndani ya Mama.
Nyumba salama, nyumba salama.

4
Yesu ndani ya Watoto,
Nyumba salama, nyumba salama, nyumba salama,
Yesu ndani ya Watoto.
Nyumba salama, nyumba salama.

205 Msifu Mungu Ee Watoto

1
Msifu Mungu, ee watoto wote, yu pendo, Yu pendo,
Msifu, Msifu, ee watoto wote Mungu ni upendo.

2
Tunampenda, ee watoto wote, yu pendo, Yu pendo,
Tunampenda, ee watoto wote Mungu ni upendo.

3
Tumikeni, ee watoto wote. yu pendo, Yu pendo,
Tumikeni, ee watoto wote Mungu ni upendo.

206 Mwokozi Wangu Alinipenda

1
Mwokozi wangu alinipenda, maovu hayanitengi naye,
Alijitoa kuniponya, sasa mimi wake.

CHORUS:
Mimi wake kabisa, naye Yesu wangu,
Si kwa wakati huu tu, bali na milele.

2
Dhambini nilijidhili sana, Yesu akaja kunikomboa,
Akanitoa sumbukoni, sasa mimi wake.

3
Furaha nyingi moyoni mwangu, Bwana Yesu kuni-
fanya huru, Kunitwaa kwa damu yake, sasa m

207 Nani Ayafanya Maua

1
Nani ayafanya maua, maua,
Nani ayafanya, Mungu juu.

2
Nani apambaye machweo, machweo,
Nani ayapamba, ni Mungu.

3
Nani afanya theluji, theluji,

208 Mungu Afanya Upinde

1
Nani afanya upinde, namjua, namjua,
Mungu afanya upinde, nampenda kwa hiyo.

2
Mungu atuma upinde, ni bora mweupe,
Mungu atuma upinde, kwamba yu karibu.

209 Napenda Sana Kufika

1
Napenda sana kufika, skuli ya Sabato,
Napenda sana kufika, skuli ya Sabato.

2
Napenda sana kuimba, habari za Yesu,
Napenda sana kuimba, siku ya Sabato.

3
Napenda sana kutoa, sadaka kwa Yesu,
Napenda sana kutoa, siku ya Sabato.

4
Napenda sana kuomba, kwa Yesu kwa Yesu,
Napenda sana kuomba, siku ya Sabato.

5
Napenda sana kujua, maneno ya Yesu,
Napenda sana kujua, siku ya Sabato.

6
Napenda sana kusema, fungu la kariri,
Napenda sana kusema, siku ya Sabato.

210 Roho Wa Mungu Wangu

Roho wa Mungu wangu, nakuhitaji,
Roho wa Mungu wangu, nakuhitaji,
Uniunde, na unijaze,
Roho wa Mungu wangu, nakuhitaji.

211 Moyoni

Moyoni, moyoni, ingia moyoni Yesu.
Njoo leo, njoo kukaa, ingia moyoni Bwana.
Moyoni, moyoni, angaza moyoni Yesu,
Ng’aa leo, siku zote, angaza moyoni Bwana.

212 Mtazame Mwokozi

Mtazame Mwokozi,
Usoni mwake mzuri,
Mambo ya dunia hugeuka,
Uso wake tukiuona.

213 Niwe Nao Uzuri

Niwe nao uzuri wa Mwokozi,
Nazo huruma zake na usafi,
Roho Mtakatifu anibadilishe,
Aonekane Yesu ndani yangu.

214 Nataka Niwe Tayari

Nataka niwe tayari Bwana,
Nataka niwe tayari Bwana,
Furaha za ulimweng

215 Ulimwengu Wataka

Ulimwengu wataka kumwona Yesu,
Ulimwengu wataka kumwona Yesu,
Analeta furaha shangilio kutosha,
Ulimwengu wataka kumwona Yesu.

216 Moyoni Nijaze

Moyoni ‘nijaze,
Na Roho wa Yesu,
Nataka kujitoa,
Moyoni ‘nijaze.

217 Omba Sana Asubuhi

1
Omba sana asubuhi, omba sana mchana,
Omba sana na jioni, Bwana hutusikia.

2
Mungu hujibu maombi, asubuhi na mchana,
Hata hutungojea tena, wakati wa jioni.

3
Na tuimbe asubuhi, tena saa za mchana.

218 Yesu Mwokozi Mpendwa

Yesu Mwokozi mpendwa, hakuna mwingine,
Yesu Mwokozi mpendwa, Yesu Mwokozi mpendwa,
Nakutazama wewe pekee, Yesu Mwokozi mpendwa,

219 Pambazuka Nuru

Pambazuka nuru, siku mpya yaja,
Basi amkeni na kuimba, ninyi nyote,
Pambazuka nuru, siku mpya yaja

220 Kwa Heri

Kwa heri, Mungu awalinde,
Kwa heri, na awaongoze,
Kwa heri, na kuwapa ama

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

HUDUMA ZA MAZISHI

Huduma ya Mazishi  (Mchungaji, mzee wa kanisa, au shemasi anaweza kufanya huduma hii). Ushauri umetolewa kwamba, kadiri inavyowezekana, maz...