(Mchungaji, mzee wa kanisa, au shemasi anaweza kufanya huduma hii). Ushauri umetolewa kwamba, kadiri inavyowezekana, mazishi yafanywe siku isiyo ya Sabato. Lakini kama ni lazima kufanya mazishi siku ya Sabato, basi watu waangalie ili mazishi yasizuie huduma za kawaida katika nyumba ya Mungu. Washiriki na watu walio katika madarasa ya ubatizo wafundishwe kwamba wakati wa huduma ya mazishi ya Kikristo tunaweza kuonesha kwa utulivu imani yetu katika ahadi ya siku ya ufufuo wakati wa kuja kwa Bwana Yesu Kristo; na kwa hiyo haifai, wala si vizuri kufuata mila na desturi za wasioamini katika kuomboleza kwa ajili ya marehemu.
Huduma Kanisani—Watu wakiisha kuketi kanisani omba sala fupi ya kwamba Mungu afariji kila mtu kwa ahadi yake ya ufufuo, na hivyo kuondoa giza liletwalo na mauti. Kisha mafungu ya Maandiko Matakatifu yatasomwa, machache ama mengi, kwa kadiri ya umri na maisha ya marehemu. Kwa kawaida somo litakuwa na mafungu yafuatayo: “Mwanadamu aliyezaliwa na mwanamke, siku zake za kuishi si nyingi, naye hujaa taabu. Yeye huchanua kama vile ua, kisha hukatwa; hukimbia kama kivuli, wala hakai kamwe ... Mtu akifa, je, atakuwa hai tena? Mimi nitangoja siku zote za vita vyangu, hata kufunguliwa kwangu kunifikilie. Wewe ungeita, nami ningekujibu; ungekuwa na tamaa ya kazi ya mikono yako” (Ayubu 14:1,2,14,15). “Wewe, Bwana, umekuwa makao yetu, kikazi baada ya kizazi. Kabla haijazaliwa milima wala hujaiumba dunia, na tangu milele hata milele ndiwe Mungu. Wamrudisha mtu mavumbini, usemapo, rudini, enyi wanadamu. Maana miaka elfu machoni pako ni kama siku ya jana ikiisha kupita, na kama kesha la usiku ... Siku za maisha yetu miaka sabini, na ikiwa tuna nguvu miaka themanini, na kiburi chake ni taabu na ubatili, maana chapita upesi tukatokomea mara ... Basi, utujulishe kuzihesabu siku zetu, tujipatie moyo wa hekima” (Zaburi 90:1-4,10,12). “Angalieni nawaambia ninyi siri, hatutalala sote, lakini sote tutabadilika, kwa dakika moja, kufumba na kufumbua, wakati wa parapanda ya mwisho; maana parapanda italia, na wafu
watafufuliwa, wasiwe na uharibifu, nasi tutabadilika. Maana sharti huu uharibikao uvae kutokuharibika, na huu wa kufa utakapovaa kutokufa, hapo ndipo litakapokuwa lile neno lililoandikwa Mauti imemezwa kwa kushinda. Ku wapi, Ewe mauti kushinda kwako? U wapi, ewe mauti uchungu wako? Uchungu wa mauti ni dhambi na nguvu za dhatnbi ni torati. Lakini Mungu na ashukuriwe atupaye kushinda kwa Bwana wetu Yesu Kristo” (I Wakorintho 15:5157). Ni vyema kutoa historia kidogo ya marehemu. Baada ya hapo kuwe na hubiri fupi. Simulia maisha ya Kikristo ya marehemu kuwasaidia walio hai, ukionesha tumaini lenye baraka na hakika ya kumshinda adui wa mwisho ambaye ni mauti. Sisitiza ahadi za injili zinazowafariji wenye huzuni na tangaza ujio wa pili wa Kristo kama “tumaini lenye baraka” la vizazi vyote. Kisha sala fupi ifuate, yenye shukurani kwa wema wote wa Mungu kwa marehemu, kwa matumaini kwamba hakuna cho chote katika vipawa vizuri vya Mungu kitakachopotea, ya kuwa katika siku ya ufufuo vitu vyote vyema vinavyoondolewa sasa vitarudishwa, na kwamba mateso yote ya hapa duniani yakoma kabisa. Omba kwamba watu wote watambue ufupi wa maisha, wakiona kweli ubatili wa mambo yote ya dunia, na uhakika wa ufufuo, ukionesha mambo ya hakika ya milele, ili watu wote waliopo ambao wangali dhambini waamke. Ombea familia ya marehemu na ndugu zake waliobaki; tena ombea kazi ya injili duniani iishe na mwenye kutoa uzima arudi upesi na kuleta kutokufa. Kisha kuwe na wimbo, na ombi la baraka na kufunga huduma.
Huduma ya Mazishi Kaburini—Maiti inaposhushwa kaburini mhudumu atasoma Maandiko Matakatifu yafuatayo: “Mimi ndimi huo ufufuo, na uzima. Yeye aniaminiye mimi ajapokufa atakuwa anaishi” (Yohana 11:25). “Usiogope, Mimi ni wa kwanza na wa mwisho, na aliye hai, nami nalikuwa nimekufa, na tazama ni hai hata milele na milele. Nami ninazo funguo za mauti na za kuzimu” (Ufunuo 1: 17,18). “Nikasikia sauti kutoka mbinguni ikisema, Andika, Heri wafu wafao katika Bwana tangu sasa. Naam, asema Roho, wapate kupumzika baada ya taabu zao; kwa kuwa matendo yao yafuatana nao” (Ufunuo 14:13).
“Lakini ndugu, hatutaki msijue habari zao waliolala mauti, msije mkahuzunika kama wengine wasio na matumaini. Maana, ikiwa twaamini kwamba Yesu alikufa akafufuka, vivyo hivyo na hao waliolala katika Yesu, Mungu atawaleta pamoja naye. Kwa kuwa twawaambieni haya kwa neno la Bwana, kwamba sisi tulio hai, tutakaosalia hata wakati wa kuja kwake, Bwana, hakika hatutawatangulia wao waliokwisha kulala mauti. Kwa sababu Bwana mwenyewe atashuka kutoka mbinguni pamoja na mwaliko, na sauti ya Malaika mkuu na parapanda ya Mungu; nao waliokufa katika Kristo watafufuliwa kwanza. Kisha sisi tulio hai tuliosalia, tutanyakuliwa pamoja nao katika mawingu, ili tumlaki Bwana hewani; na hivyo tutakuwa pamoja na Bwana milele. Basi farijianeni kwa maneno hayo” (I Thes.4:13-18).
Kuweka Maiti Kaburini—Mhudumu atasema maneno haya: “Kwa sababu imempendeza Mwenyezi Mungu katika upendo wake na hekima yake kumruhusu ndugu yetu mpenzi alale katika Kristo, nasi kwa moyo wa huruma twaweka mwili wake ardhini; udongo kwa udongo, majivu kwa majivu, mavumbi kwa mavumbi; katika tumaini la hakika, lisilo na shaka katika ufufuo wa uzima wa milele katika Yesu Kristo Bwana wetu; ambaye wakati wa ufunuo wake wa utukufu “ataubadili mwili wetu wa unyonge, upate kufanana na mwili wake wa utukufu, kwa uweza ule ambao kwa huo aweza hata kuvitiisha vitu vyote viwe chini yake” (Wafilipi 3:21). Kisha mhudumu atatamka: “Nikasikia sauti kubwa kutoka katika kile, kiti cha enzi ikisema, Tazama, masikani ya Mungu ni pamoja na wanadainu, naye atafanya masikani yake pamoja nao, nao watakuwa watu wake. Naye Mungu mwenyewe atakuwa pamoja nao. Naye atafuta kila chozi katika macho yao, wala mauti haitakuwapo tena; wala maombolezo, wala kilio, wala maumivu hayatakuwapo tena; kwa kuwa mambo ya kwanza yamekwisha kupita” (Ufunuo21:3,4). Kisha atafunga kwa ombi.
RATIBA YA MAZISHI
1. Kutoa mwili {wimbo}
2. Kufungua Ibada na wimbo namba.....
3. Ombi
4. Risala
5. Neno la Mungu
6. Ombi
7. Kuaga mwili
Malaloni
Nyimbo
Ombi
Neno
Ombi
Shukurani kutoka kwa:
Kiongozi wa Kanisa
Mwanafamilia
Kiongozi wa serkali au zengo
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni