Jumatano, 17 Januari 2018

AFYA

DAWA KUMI AMBAZO HAZITUMIKI KABISA KIPINDI CHA UJAUZITO…




Tunaendelea na makala zetu za siri za afya bora na leo tutaongelea dawa ambazo jamii yetu huzitumia mara kwa mara kujitibu magonjwa mbalimbali na hupatikana kirahisi mtaani


Lakini bahati mbaya baadhi ya dawa hizo hazitakiwi kupewa kwa wajawazito kabisa kulingana na madhara makubwa yanayoambatana na dawa hizo kwa mtoto aliyepo tumboni.


Zifuatazo ni dawa hizo.




Albendazole; hii ni dawa ya minyoo ambayo hutumika mara kwa mara kujitibu lakini ni dawa mbaya sana kwa akina mama wajawazito kwani una uwezo wa kutoa mimba kabisa hivyo mebendazole hutumika kama mbadala.




Gentamycin: hii ni dawa ambayo iko kwenye mfumo wa sindano tu, mara nyingi hutumika kutibu magonjwa ya mfumo wa mkojo. Dawa hii huharibu kabisa mishipa ya fahamu kitaalamu kama auditory nerve ambayo hutufanya sisi kusikia. Hivyo matumizi ya dawa hii huweza kusababisha mototo kuzaliwa akiwa hasikii yaani kiziwi.




Ciproflaxin; hii ni dawa ambayo hupatikana kwenye mfumo wa vidonge na sindano, mara nyingi hutumika kutibu typhoid, UTI au magonjwa ya njia za mkojo na magonjwa baadhi ya zinaa. Dawa hii huharibu ukuuji wa mifupa ya mtoto na huweza kutoa mtoto asiyetembea mwishoni.




Doxycline: hii ni dawa ambayo hupatikana kwa mfumo wa dawa za kumeza kitaaalamu kama capsules, dawa hizi ni antibiyotiki yaani hutumika kuua bakteria wa aina tofauti. Bahati mbaya huweza kuingilia mfumo wa utengenezaji wa mtoto ikitumika miezi mitatu ya mwanzo na kusababisha kuzaliwa na motto mwenye viungo pungufu au zaidi.




Dawa ya mseto ya malaria au ALU; dawa hii ni salama kipindi chote cha ujauzito isipokua miezi mitatu ya kwanza ambapo dawa hii huweza kuingilia ukuaji wa maumbile ya kwanza ya mtoto[organogenesis} na kutoa motto asiye na viungo vya kawaida.




Metronidazole au fragile; hii dawa ipo kwenye kikundi cha antibayotiki yaani hushambulia bakteria. Dawa hii hutumika mara nyingi kuua minyoo ya amiba na kutibu magonjwa ya mfuko wa uzazi wa mwanamke na ikitumika miezi mitatu ya kwanza ya ujauzito huingilia mfumo wa utengenezaji wa viungo vya mtoto.




Mesoprostol: hii ni dawa ambayo iko kwenye kikundi maarufu cha prostanglandins analogue, hutumika sana kuongeza njia ya mlango wa uzazi kipindi cha kujifungua na pia hutumika kutibu madonda ya tumboni hivyo matumizi ya dawa hii kipindi cha ujauzito yana madhara makubwa mno ikiwemo kutoa mimba kabisa.




Aspirin: hii ni dawa ya maumivu ambayo humezwa mara kwa mara na hupatikana kirahisi tu, lakini dawa hii ina uwezo wa kusababisha kuvuja kwa damu nyingi hasa mama akipata matatizo flani ya uzazi kama placenta previa. Sio dawa nzuri sana kipindi cha ujauzito.




Praziquantel: hii ni dawa inayotumika kutibu minyoo flani inayopatikana kwenye sehemu za maji yaliyotuama, ni hatari sana kwa wamama wajawazito kwani huiingilia mfumo wa ukuaji wa mtoto.




Furesamide: hii ni dawa ambayo inapatikana kwenye kikundi cha diuretic.. mara nyingi hutumika kushusha ongezeko la maji nje ya mfumo husika wa damu [oedema] na kutibu presha kubwa ya damu. Sio dawa nzuri kwa akina mama wajawazito kwani wajawazito hua na presha ya chini kidogo hivyo huweza kuishusha chini kabisa[intravascular volume depletion].






Mwisho: usitumie dawa yeyote kipindi cha ujauzito bila ushauri wa daktari kwani ni hatari sana kwa maisha yako na mtoto wako kwa ujumla.




MAMA MWENYE VVU ANAZAAJE MTOTO ASIYE NA VVU?






Mama mwenye vvu anaweza kuzaa mtoto asiye na vvu endapo njia zote zinazoweza kumweka mtoto katika hatari ya kupata maambukizi zitazuiwa.







Ni vyema tukatambua kuwa mtoto anaweza kupata maambukizi toka kwa mama katika njia tatu muhimu.Njia hizo ni pamoja na mtoto anapokuwa tumboni,wakati wa kuzaliwa na wakati wa kunyonya maziwa ya mama.Hatari zaidi ni pale mama anapokuwa na idadi kubwa ya vvu katika damu na akawa anaugua mara kwa mara.Kwa jinsi hii usalama wa mtoto tumboni unakuwa ni mdogo na anaweza akapata maambukizi akiwa tumboni hasa pale mfuko wa uzazi unapokuwa dhaifu kiasi cha kuruhusu damu ya mama ichanganyike na ile ya mtoto.Maambukizi ya mama kwenda kwa kwa mtoto kwa njia hii ni kwa kiasi kidogo tu.Endapo kiasi cha vvu katika damu ya dawa ya kumkinga mtoto,hali ya mama itakuwa nzuri na uwezekano wa mtoto kupata maambukizi kwa njia hii huwa mdogo.




Wakati wa kuzaliwa mtoto anaweza kupata maambukizi toka kwa mama kama atapata michubuko mwilini mwake na mama akawa na michaniko katika njia ya uzazi.Asilimia kubwa ya watoto wanaozaliwa hupata maambukizi kwa njia hii.Kwa jinsi hii kama kiasi cha vvu ni kidogo katika damu ya mama mtoto anaweza kuwa salama kwani ngozi ya mtoto mara nyingi huwa imekingwa na aina Fulani ya mafuta yanayoweza kuzuia michubuko japo anaweza akapata michubuko kidogo.




Wakati wa kunyonyesha mama anashauriwa kutompa mtoto chakula kingine hadi hapo atakapomuachisha kulingana na muda uliokubaliwa wa kunyonyesha.Hii ni kulinda ukuta wa ndani ya tumbo la chakula ambao ni laini na unalindwa na utando mwepesi usipate kuchubuliwa na chakula kigumu hivyo kupitisha vvu vinavyokuwepo katika maziwa ya mama mwenye maambukizi.

Huduma zinazopatikana kliniki kwa ajili wajawazito wenye vvu

Elimu ya vvu na ukimwi
Huduma ya ushauri nasaha juu ya kuishi na maambukizi ya vvu,lishe na namna ya kuzuia maambukizi mapya
Elimu ya namna ya kumkinga mtoto asipate maambukizi ya vvu
Kuangalia maendeleo ya mtoto tumboni na baada ya kuzaliwa
Dawa maalumu za kumkinga mtoto dhidi ya vvu
Ushauri juu ya uzazi salama katika hali ya maambukizi ya vvu
Huduma ya upimaji wa vvu kwa watoto
Huduma za maambukizi ya vvu kama vile kupima cd4,na vipimo vingine vinavyohusiana
Mafunzo juu ya kukubaliana na changamoto mbalimbali za maisha
Kuanzishwa dawa za ARVs kama wametimiza vigezo

ARV zinavyomkinga mtoto na maambukizi


Jinsi dawa za kuzuia maambukizi kwa mtoto zinavyofanya kazi:






Kwa mama: zinapunguza idadi ya virusi katika damu hivyo kufanya afya ya mama iendelee kuimarika na kupunguza uwezekano wa kumwambukiza mtoto






Kwa mtoto: inakuwa ni kama kinga baada ya hatari ya kuambukizwa(PEP)kuteketeza kiasi Fulani cha maambukizi anayoweza kupata akiwa tumboni.






ARV na dawa za kumkinga mtoto na maambukizi


Dawa za ARV na zile za kumkinga mtoto kutopata VVU hazipaswi kuchanganya kwa sababu dawa zinazotumika kumkinga mtoto dhidi ya VVU zimo ndani ya dawa za ARVs.






Tofauti kati ya ARVs na dawa za kumkinga mtoto na maambukizi


Tofauti ni kwamba mama mjamzito ambaye hajatimiza vigezo vya kuanza kutumia ARVs anapewa aina moja ya dawa za ARVs kumkinga mtoto wakati yule aliyetimiza vigezo anatumia dawa aina tatu.






Kuendela na dawa za kumkinga mtoto baada ya ujauzito:


Mama anayetumia dawa za kumkinga mtoto kama hajatimiza vigezo vya kuanza dawa za ARVs ataacha kutumia dawa hiyo mara baada ya kujifungua. Endapo atakuwa ametimiza vigezo ataanza kutumia dawa za ARVs ataendelea kutumia dawa hizo kama kinga kwa mtoto na tiba kwake maisha yake yote.






Dawa za kumkinga mtoto zinazuia maambukizi kwa mtoto kwa kiasi gani?


Kwa mama anayetumia dawa za kumkinga mtoto dhidi ya vvu uwezekano wa kuzaa mtoto asiye na maambukizi ya vvu ni asilimia hamsini kwani kuna vigezo vingi vinavyohitajika kuzingatiwa hadi mtoto azaliwe bila maambukizi ya vvu kama ilivyoelezwa hapo juu.Hata hivyo mpango wa kuzuia maambukizi toka kwa mama kwenda kwa mtoto unaonekana kufanikiwa kwa kiasi kikubwa hasa baada ya maambukizi kwa watoto wachanga kupungua miongoni mwa wamama wanaotumia mpango huo,wamama wengi wanaotumia dawa ya kumkinga mtoto au walioko kwenye dawa za ARV na ambao wanafuata ushauri wa kitaalamu wanajifungua watoto wasio na maambukizi ya vvu kuliko hapo awali.




JINSI YA KUJIKINGA NA KUONDOA HARUFU MBAYA MDOMONI(HALITOSIS)!














WATU wengi husumbuliwa na tatizo la kunuka mdomo bila hata kujijua hivyo kuwa kero kwa wenzao na wakati mwingine hujishushia hadhi mbele ya jamii. Mara nyingi ugonjwa wa kunuka mdomo (Halitosis) husababishwa na uchafu wa kinywa na ulaji wa vyakula usiosahihi lakini ni tatizo linalotibika.

Ni rahisi kulizuia na kuliondoa tatizo la kunuka mdomo iwapo utaamua kufuata kanuni za usafi wa kinywa na unywaji wa maji kwa kufuata kwa makini muongozo ufuatao:


KUPIGA MSWAKI

Kitu cha kwanza kufanya ni kupiga mswaki kwa ukamilifu kila uamkapo asubuhi. Wakati wa kupiga mswaki, utatakiwa siyo tu kusugua meno, bali pia ulimi, sehemu ya katikati hadi karibu na koromeo kwa kusugua vizuri.

Vile vile kila uamkapo baada ya kulala mchana au jioni, hakikisha unapiga mswaki, kwani bakteria wa kinywani, hutawala kinywa kila ulalapo. Mara baada ya kupiga mswaki na kusugua ulimi sawaswa, hakikisha unasukutua vizuri kwa maji, kwani hapa ndipo baadhi ya watu hukosea kwa kupiga mswaki bila kusukutua kwa maji.


KUNYWA MAJI MENGI

Maji ni muhimu sana karibu kila eneo la mwili wa binadamu. Unywaji wa maji ya kutosha kila siku utakusaidia kudhibiti na hatimaye kuondoa tatizo la kunuka mdomo. Unywaji wa maji mengi ni muhimu, hasa kwa wale watu wenye ugonjwa wa kukauka midomo (xerostomia).


Mara nyingi harufu itokayo mdomoni, hutokea tumboni na siyo kinywaji peke yake kama unavyoweza kudhani. Hivyo, kama tumbo litakuwa chafu, hata kama utasafisha kinywa vizuri bado harufu mbaya inaweza kuendelea kutoka.


Harufu mbaya ya tumboni hutokea pale tumbo linapokuwa chafu kutokana na kutopata choo kwa muda mrefu. Miongoni mwa mambo yanayochangia kukosekana kwa choo kwa muda mrefu ni pamoja na tabia ya kutokunywa maji ya kutosha kwa siku, hivyo hakikisha unakunywa maji, kiasi kisichopungua






lita moja na nusu hadi mbili au zaidi, kutegemeana na kazi unazozifanya.

Ukiwa na tatizo la kukaukiwa maji mwilini kila mara, mwili hujaribu kutumia njia zake za kiasili kupunguza uzalishaji wa mate ili kuhifadhi maji kwa ajiili ya matumizi mengine, kitendo hicho huchangia kunukisha mdomo kwa sababu ndani ya mate huwa kuna kinga muhimu dhidi ya baktetria wanaonukisha kinywa.


Kwa upande mwingine, ili kuzuia kinywa kunuka pale mdomo unapokuwa umekaukiwa na mate, ni vizuri kutafuna vitu kama bazooka au ‘chewing gum‘ yoyote ili kuzalisha mate ambayo huhitajika katika kudhibiti bakteria.




Pia kama tatizo hili limezidi unaweza kutumia dawa kama MEDORAL NA HYDROGEN PEROXIDE MOUTH WASH.


Mwisho, hakikisha unasukutua sawaswa baada ya kula chakula chochote, hata kama ni juisi isipokuwa unapokunywa maji tu ya kawaida. Bila shaka, ukizingatia haya, tatizo ulilonalo la kunuka mdomo litataoweka na kubaki historia.





Bamia Huweza Kusaidia Wagonjwa Wa Vidonda Vya Tumbo

Muungwana Blog · 14 hours ago


Mtandao wa healthandcure.com unawanukuu wataalamu wa afya wakieleza kuwa watu wanaosumbuliwa na maradhi kadha wa kadha ya mfumo wa chakula kama vile vidonda vya tumbo na mengine yanayofana na hayo wanaweza kupata ahuweni au kupona kabisa ikiwa watakula bamia.

Unafahamu kuwa kwa kula bamia unaweza ukawa umejiondoa katika hatari ya kupata maradhi mbalimbali?


Mtandao wa healthandcure.com unawanukuu wataalamu wa afya wakieleza kuwa watu wanaosumbuliwa na maradhi kadha wa kadha ya mfumo wa chakula kama vile vidonda vya tumbo na mengine yanayofana na hayo wanaweza kupata ahuweni au kupona kabisa ikiwa watakula bamia.

Wataalamu hao wanaendelea kuzitaja faida nyingine zinazotokana na ulaji wa bamia ni pamoja na kuboresha uwezo wa macho kuona.


Bamia ni chanzo kizuri cha Vitamin A na beta carotene ambavyo ni virutubisho vinavyosaidia kuboresha uwezo wa kuona.


Bamia inasaidia kuweka kawaida kiwango cha sukari mwilini na nyuzinyuzi zake zinasaidia kurahisisha ufyonzwaji wa sukari mwilini.


Pia hudhibiti pia kiwango cha lehemu mwilini na hasa pale inapokuwa mtu ametumia vyakula vingi vyenye mafuta.


Husaidia pia kulainisha choo. Vilevile ni mboga ambayo kwa Waafrika huongeza hamu ya kula na hata kurahisisha kazi ya kumeza.


Wataalamu wanaeleza kuwa ina virutubisho vinavyoweza kupambana na bakteria wanaoshambulia utumbo na kusababisha vidonda vya tumbo.


Pamoja na haya yote bamia huimarisha mifupa, huongeza kinga dhidi ya magonjwa ya figo, saratani pamoja na pumu.


Faida nyingine ya kutumia Bamia hii hapa

Chimbuko la Bamia ni Abyssinia (Ethiopia) Kisha ikaenea Duniani kote.


1. Michirizi na utonvu unaopatikana katika Bamia, husaidia kusawazisha Kisukari kwa kuzuia kiwango cha Sukari inayotumika katika mwili kutoka kwenye utumbo mkubwa.


2. Utelezi wa bamia huchuja uchafu unaoingia katika Kolestorali (cholesterol) na asidi ya Nyongo unaoingia kutoka kwenye Ini ambao usipo dhibitiwa huenda ikasababisha matatizo ya ki-afya.


3. Bamia husaidia kulainisha Utumbo mkubwa (large intestines) kutokana na kazi yake ya kulainisha choo.


4. Bamia hutumika kwa kutibu vidonda vya Tumbo inasaidia kusawazisha Asidi.

Magonjwa Maalum


Asidi ya Kujirudia rudia na Kufunga Choo

Tafuna vipande sita vya Bamia bila kutumia dawa nyigine kilasiku na Asidi ya Kujirudia rudia na kufunga choo kutakwisha, inashusha Sukari kutoka 135 hadi 98


Pumu

Bamia ina Vitamin C ambayo inawafana watoto wanaougua ugonjwa wa pumu kupumua vizuri wanapoitumia. Nusu kikombe ya Bamia iliyopikwa huwa na miligramu 13 ya vitamin C.


Kidonda Ndugu (Cancer)

Bamia husaidia kuweka Utumbo kuwa na hali nzuri hivyo kupunguza uwezakano wakuugua ugonjwa huu wa Kansa hasa kwenye utumbo mkubwa.


Mishipa midogo ya Damu Kula Bamia kwa wingi kunasaidia kuimarisha Mishipa midogo ya Damu.


Cataracts

Nusu kikombe cha Bamia iliyopikwa inakua na kiwango cha 460 IU ya vitamin A.ambayo inapunguza uwezakano wa kupata ugonjwa wa mtoto wa jicho (cataracts).


Usongo (Depression) na Kukosa Nguvu. Bamia ni mboga bora zaidi kwa wale wanaojisikia dhaifu, Kuchoka na wanao athirika na Usongo (depression).






UTANGULIZI:






Elimu ya kweli ni ufunuo wa tabia yake na uwezo wake na kazi ya kuonyesha kuwa kila kiumbe kimeubwa na Mungu na kutangaza utukufu wake. ZABURI 19:1- 7, ISAYA 37: 16, 46:5, 44: 6, 46 :9






Kila kiumbe kiliumbwa na yeye mwenyewe malaika mwanadamu ni kazi ya Mungu AYUBU 38:5 – 7, MWANZO 1: 26 -27






Hivyo hukanusha masomo ya nadharia za watu, zinazofundishwa kuwa dunia ni kipande kilicho meguka kwenye mwezi, huu ni uongo, Mungu aliumba dunia, na mwezi nyota, jua vyote ni kazi ya Mungu.


MWANZO 1: 1- 5, 14 – 19 , ISAYA 66:2, AYUBU 36:26 .


Hivyo tunakanusha uvumi wa kusema kwamba vitu hivi vilitokea tu . Pia mwanadamu naye ni kazi ya Mungu aliumbwa hakuna kiumbe kilichotokana na kingine .


MWANZO 2: 7 ZABURI 139: 23 – 25, 8: 3- 9.










Hii ndiyo Elimu ya kweli ya kujua kazi ya Mungu kama mwanzo wa vitu vyote, na ukuu wake na mamlaka yake ya uumbaji, hata hivyo tuelewe kuwa mwanadamu aliumbwa na si uibukaji kama wengi wanavyoelewa .






Ni mhimu sana kujifunza kuujua mwili wetu na kujua kila kiungo kinavyofanyakazi tena kwa kushirikiana na vingine . Wengi wamekuwa walemavu wa viungo, na wengine kufa kwa kutumia viungo vyao vibaya 1 WAKORINTHO 6:12 – 20






Ni wajibu wa kila mtu, kwa ajili yake mwenyewe, na kwa ajili ya watu wengine, kujua kabisa kanuni zinzohusiana na afya njema, na kuzifuata kwa bidii na uaminifu. Inawapasa wote kufahamu kabisa umbo hili la ajabu – yaani mwili wa mwanadamu. AFYA NA RAHA UK 10, 39 – 42.






Uasi wa sheria za mwili ni uasi wa sheria za maadili kwa maana kwa hakika Mungu ndiye mwanzilishi wa sheria za mwili. Kama alivyo mwanzilishi wa sheria za maadili. Sheria yake imeandikwa kwa kidole chake na kwa kila mshipa wa fahamu kwa kila msuli na kwa kila uwezo wa akili na mwili, ambao umewekwa kwa mwanadamu.VIELELEZO VYA MAFUNDISHO YA KRISTO,: UK 268 KUTOKA 31 : 18






Mvuto wa akili kwa mwili, Pia ule wa mwili kwa akili, zitiliwe makazo. Nguvu ya umeme ya akili ikitiwa nguvu na shughuli za kiakili, hutia nguuvu mfumo wote hivyo huwa msaada wa thamani sana katika kukinga magonjwa. ELIMU YA KWELI UK 144 -147






Unapojifunza jinsi mwili unavyofanya kazi, uzingatiaji makini uelekezwe kwenye uwezo wa kubadilika na jinsi viungo vinavyotegemeana. Kadri moyo wa kupenda kwa mwanafunzi utakavyoamshwa na kuongozwa na kuona umhimu wa elimu ya kukua na kukomaa kimwili, mwalimu atafanya mengi kusaidia kukua ipasavyo na mazoea sahihi. Miongoni mwa mambo ambayo yapaswa kulengwa kwanza lingekuwa hali sahihi katika yote mawili kukaa na kusimama. Mungu alimuumba mwanadamu mnyoofu na anapenda awe siyo tu na yale ya kimwili, bali faida za kiakili na maadili. ELIMU YA KWELI 145. MHUBIRI 7:29






INI, LIVER NATURAL REMEDIES UK. 357- 58, 361 – 62




Ini ni kiungo muhimu sana ndani ya mwili wa binadamu. Ini hufanya kazi ya kutengeneza protini kuondoa sumu ndani ya damu na kusambaza kiwango cha damu inayohitajika kila sehemu ya viungo vya mwanadamu na kupambana na kinukari za sumu zinazoingizwa mwilini.


Ini seli nyekundu za damu zilizokufa.


Hugeuzwa na ini kuwa pigmenti za nyongo ambazo huipa nyongo rangi yake. Pigmenti hizo huingia kwenye chakula njia ya chakula na baadaye kuchanganyika na kinyesi. Ini pia hupambana na sumu zinazongia mwilini. Simu zinapozidi uwezo wake hulifanya ini kusinyaa, na kushidwa kufanya kazi vizuri na kusababisha makovu. Ini linapokuwa limeathilika namna hiyo, hushindwa kufanya kazi zake za kawaida kama vile kutengeneza (Protein) na kuondoa sumu ndani ya damu na hivyo husababisha shinikizo la juu la damu ndani ya mishipa ya damu.


Uvujaji wa damu ndani kwa ndani kunaweza kutukea na pia mkusanyiko wa maji ndani ya tumbo na tumbo kuvimba.






Vitu vinavyoharibu ini na kulifanya lishindwe kazi vizuri


Ø Kula chakula kisicho na virutubisho nafaka zilizokobolewa.


Ø Matumizi ya nyama, kahawa, majani ya chai, pombe, uvutaji wa hewa yenye sumu


Ø Samaki kwa mtu anayetumia samaki kwa wiki mara 2 huzuia utendaji kazi wa mafuta ya ini


Ø Kutumia vidonge, sukari, soda, juisi, chakula chenye sumu pia na homa ya njano. WALAWI 3:4 -11






TIBA


Ø Tumia kwa wingi matunda ya apples


Ø Celery chukua kijiko kimoja weka kwenye glasi moja ya maji ya moto kunywa 2x2 kwa siku


Ø Tumia chai ya Rosemery










ACHA KUTUMIA


Nicotine, alchohol, caffeine, fishi, fowl, meat, salt, soft drinks, sugar foods, lea NK










KIDNEY PROBLEMS – MATATIZO YA FIGO






NATURAL REMEDIES UK 397-398
Figo au mafigo ni viungo vinavyohusika kuchuja maji ndani ya mwili na kuyabalansi yakae kwenye uwiano ulio sawa. Kiungo hiki (viungo) kina ushirikiano mkubwa sana na kibofu cha mkojo. Mafigo yanaposhindwa kufanya kazi vizuri husababisha matatizo ya kuvimba miguu, kujaa maji sehemu ya malengelenge ya maji sehemu yoyote ya mwili hata yasipotakiwa kuwepo.


Figo ni ogani iliyo nyuma ya fumbatio figo linaumbo la harangwe.


Kuna fiigo mbili moja upande wa kulia na la pili upande wa kushoto wa uti wa m gongo, kwenye kila


M,WALAWI 8:16


figo kuna mshipa unaingia na kutoa. Ule unatoka huitwa vena ya renali, na ule unaingia huitwa ateri ya renali. Damu kuingia kwenye figo kupitia ateri za renali figo huchuja damu inayoingia na kuondoa urea, chumvichumvi na maji ya ziada.






Taka mwili zilizochunjwa na figo husafilishwa kwenda kwenye kibofu kupitia ureta.


Ureta ni mlija utakao kwenye figo hadi kwenye kibofu cha mkojo. Kazi yake ni kupitisha mkojo toka kwenye figo hadi kwenye kibofu, Kibofu cha mkojo ni mfumo unaokusanya mkojo kutoka kwenye figo. Baada ya kibofu kujaa, misuli yake husinyaa na kuusukuma mkojo nje kupitia ureta.





VYANZO


Ø Kula chumvi mbichi


Ø Vinywaji, pombe, soda, juisi


Ø Kuunga chumvi mbichi kwenye chakula yaani kuongeza chumvi


Ø Mawe ndani ya mafigo






TIBA


ACHA KUTUMIA


Soft drinks, caffeine, chocolate, cocoa, pepper, Nuts, nyama, chumvi.






BANDAMA


SPLEEN NATURAL REMEDIES UK 2102




Bandama ni kiungo muhimu sana kwa mwanadamu pia kuingo aina ya nyama kinachohifadhi damu na kutunza kama alivyo kwa viungo vingine. Kiungo hicho hushirikiana na viungo vingine. Kiungo hiki kikiungua au kupata matatizo ni hatari.





















































































KONGOSHO






4. Kongosho ni kiungo pia muhimu kwa kutengeneza kiwango cha sukari inayotakiwa mwilini kinapaswa kutunzwa kwa makini sana. Kongosho inapozidiwa na kazi yake husababisha sukari kusambaa mwilini na mtu kupatwa na ugonjwa wa kisukari.





Dalili za kuonyesha kongosho halifanyi ni


Ø Ugonjwa wa kisukari


Ø Kupungua uzito


Ø Kukonda kwa haraka sana


Ø Kukojoa san, mkojo wa mara kwa mara


Ø Mkojo wa sukari sukari






Vyanzo vikubwa


Juisi za viwandani, soda, chumvi, sukari, nyama, mayai, apple, ndizi, maziwa, sigara, pombe, tikiti maji, na jamii ya vitu vyenye sukari


Mtu anayetumia soda x2 kwa wiki husababisha kansa ya kongosho.




































































































NYONGO BILE DUCT MFEREJI WA NYONGO GALL BLADER- KIBOFU NYONGO










Nyongo ni kiungo kinachozalisha tindi kali (URIC ACID) inayowekwa kwenye chakula kabla ya kuyeyushwa kama kund wadudu chakula hakiwezi kuyeyushwa kama nyongo haijadondosha, tindi kali kwenye chakula. Viungo hivi hufanya kazi kwa kushirikiana na kila kiungo kwa kazi ya na utaratibu kula kwa wakati usio badilika na moja ya kutunza kiungo hiki na kukifanya kifanye kazi vizuri na kutokula ovyo ovyo.


Mojawapo ya madhara yanayotokana na kula bila utaratibu. Madonda ya tumbo. Kuchacha kwa chakula tumboni, kuharisha, kutapika, hewa chafu, tumbo kujaa gesi, kukosa hamu ya chakula.




























































































































STOMACH – TUMBO MFUKO WA CHAKULA NATURAL REMEDIES UK 355










Tumbo ni kiungo muhimu kwani hupokea chakula kinachotoka mdomoni na kukifinyanga (kuyeyusha) kiungo hiki ni kimeumbwa kwa muundo wa taulo ni muhimu sana kukitunza kiungo hiki kazi yake ni kubwa na nzito. Chakula kinacholiwa hakiwezi kuingia kwenye mfuko wa chakula huanzia kwenye kiungo hicho baada ya kukifinya mpaka kwenye utumbo mpana, madhara waliyonayo watu wengi ni kwa kula vibaya na kunywa vibaya yamekifanya kiungo hiki kuwa dhaifu na mengi ku la bila utaratibu, kula na kunywa maji. Wengi hunywa vinywaji vikali sana kiasi kwamba vinatoboa utumbo na kutokuwa na kiasi katika kula. Iwako 10:23


Isaya 55:2 (Wak 6:12 – 13, 19- 20


Madhara Taifodi husababisha madonda ya tumbo, mawazo, Amiba aina zote za minyoo kwani hutoboa utumbo na kushiba sana.


Pombe, majani ya chai, sigara, juisi za kemikali na soda unga uliokobolewa na vyakula vya kuangiza nyama zaburi 18:27- 33 zaburi 106:15






Ili kutunza kiungo hiki ni vema kula chakula cha asili na juisi za nanasi, apple, machungwa, papai, embe nk na mboga za majani zaburi 104:13- 15 Ayubu 28:5 Zaburi 136:25, 147:8-9 Ayubu 38:41




















































INTESTINE UTUMBO MPANA NA MWEMBAMBA






Utumbo mpana na mwembamba hufanya kazi kwa pamoja kazi kwa pamoja baada chakula kuingia na hutoka kwenye tumbo na kufyonzwa na utumbo mpana hapo hufanyika kazi ya kuchambua vitamini na madini na virutubisho protini inayohitajika mwilini hapo ini linahusika kongosho na kama chakula kina maji kazi ya kuchuja maji na mafigo pia huhusika ubongo huratibu shughuli nzima ya uyeyushaji kwani kwani huamrisha viungo vyote shughuli hii huchukua takiribani masaa 4-6 kulingana na aina ya chakula.






Mucous membrane - Kiwamba ute sehemu ya kiwamba cha seli inayozunguka mfereji wa chakula.


Sehemu ya chakula kinacholiwa, humeng’enywa na kusharabiwa mwilini. Sehemu iliyobaki ambayo ni chakula ambacho hakikumeng’enywa na kusharabiwa mwilini, husafilishwa hadi kwenye utumbo mpana. Mabaki hayo ambayo yamechanganyika na pigmenti za nyongo hutolewa nje kama kinyesi.


Chakula kilichosharabiwa mwilini huchanganyika na kemikali kuzalisha nishati. Baadhi ya dutu zinazotokana na mchanganyiko huo hazina manufaa kwa mwili . Dutu hizo huitwa takamwili ambazo ni pamoja na kabonidayoksaidi, kompaundi za natrojeni, maji na pigmenti za ini.


Ogani zitumikazo kutoa taka mwili ni mapafu, figo, ngozi na ini.










Baada ya vitamini, madini, protini na vitu muhimu kuchuliwa na kubaki makapi husafirishwa kwa njia ya utumbo mwembamba (mrefu) hadi kwenye lango la haja kubwa na mtu kujisaidia Marko 7: 18- 20 kwa muda huu wa masaa 4- 6 mtu hatakiwi kula chochote mpaka baada ya masaa 6 5-6 kula ndani ya masaa haya ni kujiletea magonjwa mengi sana sana.




BLADDER – KIBOFU CHA MKOJO






Kibofu ni kiungo mfano wa bilika kazi yake ni kutunza na kuhifadhi mkojo, maji baada ya kuchujwa vizuri na figo maji taka hupelekwa kwenye kibofu kupitia milija inayounganisha figo na kibofu au bilika.


Maji taka yanapofika kwenye birika husafirishwa kwenye mishipa hadi kwenye,uume, uke kisha maji hayo humwagika nje, au kutoka nje hutwa kukojoa, paa hapa kuwa na kiungo kidogo kama mfumo wa (mashine engine ) inayosukuma mkujo kubana mkojo kwa muda mrefu bila kukojoa huathiri kibofu (birika) na kuuwa mashine ya kusukuma mkojo otoke nje .Madhara haya huenda na kuharibu mafigo.


Kutumia vinywaji vikali, juisi, soda, pombe, viroba nk ni kuuwa mashine ya kibofu cha mkojo. Madhara yake ni:-


Ø Kupasuliwa


Ø Kuwekewa mpira wa kukojolea


Ø Kushindikana kabisa


Ø Kifo


Ni vyema kuthamini viungo vyetu kwani ni zawadi tuliyopewa na Mungu 1WAKORINNTHO 12:12-26



































































REPRODUCTIVE: WOMEN MFUMO WA UZAZI WA MWANAMKE, NATURAL REMEDIES UK. 640






Mfumo wa uzazi wa mwanamke ni moja kati ya viungo muhimu na nyeti, kwa kazi uzalishaji watu au kuzaliana mwanzo 1:28, 4:1.


Huu ni mfumo ambao Mungu aliumba kwa ajili ya kuendeleza uzao wa mwanadamu ili watu wasingie katika swala la kujamiana, kabla ya ndoa. Waebrania 13:4 Mathayo 19:4-6 kwa maneno hayo tendo la ndoa kabla ya kuoa au kuolewa ni kosa la jinai mbele za Mungu katika hili Mungu akataza yafuatayo.






Ø Kuharibu ubikira torati 22:20-21, 17c 4-7


Ø Kufanya tendo kabla kuowa au kuolewa ni dhambi Walawi 21:7 na mume wake mwenyewe wako 7:1


Ø Wasiingie kwa jamaa wako wa karibu. Walawi 18:6-18 torati 27:20, 22-23


Ø Magomvi na mauji na mafarakano


Ø Usingia kwa mke wa mwingine Walawi 20:10


Ø Masumbufu na majuto


Ø Ndoa jinsia moja ni laana Walawi 18:22


Ø Kulala na kiumbe Walawi 18:23 torati 27:21


Ø Usilale na mwanamke ikiwa kwenye siku zake Walawi 18:19






Hivyo Mungu alikusudia ndoa iwe baina ya mme na mke.


Mfumo wa via vya uzazi vya mwanamke ni kama ifuatavyo


Ø Ovari (2) mirija ya falopia, uke ovari hutoa mayai au kuzalisha gamete uke mwanamke ana ovari mbili moja chini ya kila figo Walawi 12:2, 15:19, 25


Ø Mrija wa falopia husafirisha gameti uke kutoka kwenye ovari


Ø Uterasi mji wa mimba ni mahari ambapo kitoto hutunzwa na kukua hadi kuzaliwa.


Ø Seviksi- kilango cha uterasi mlango au misuli mviringo ya seviksi.


Ø Uke – ni sehemu ambayo mtoto hutoke wakati wa kujifungua na ndipo na mbegu za kiume gamete ume hupitia wakati wa kujamiiana na kutoka nje ya mwili.


Kuziba kwa husababisha madhara ya kukosa mtoto, siku za hedi maumivu makali kama zikitoka wakati mwingine damu hutoka kidogokidogo na kuleta maumivu makali sana, wakati mwingine mhusika anaweza kuzimia na kufanya zinaa kinyume na utaratibu. Matatizo mengine ni kama kansa ya kizazi. Baadhi ya vipodozi ni hatari huleta madhara makubwa, kula vibaya, kuvaa vibaya wengi wamepata ugumba (tasa) kwa kujiletea wenyewe au wazazi wao Torati 7:14, 28:18 na mimba kuharibika kutumia dawa za nywele na kilimu ni hatari dawa za nywele huharibu vitamini c sumu kilimu huleta saratani ya ngozi.























REPRODUCTIVE: MEN MFUMO WA UZAZI WA MWANAUME NATURAL REMEDIES UK 634






Mfumo wa uzazi wa wanaume ni kuzaliana na kuongeza watu duniani Mungu alimuumba mwanaume na mwanamke mwanzo 1:27 watu huzaliana kwa njia ya kujamiana kwa mwanaume/mke Wakorinntho. Mfumo wa mwanaume






Ø Korodani, korodani hutengeneza na kuhifadhi gamete za kiume, korodani hutengeneza homoni inayosababisha wakati wa kubalehe (korodani) Walawi 212


Ø Mirija ya manii, mirija ya manii hupitisha gameti za kiume kutoka kwenye korodani kwenda kwenye uume na kutoka nje. Ayubu 10:10 Walawi 15:16-18


Ø Uume, kwenye uume kuna mrija uitwao urethra ambao hupitisha manii






























































1. VIUNGO VYA KICHWA (HEAD SYSTEM).






1. UBONGO NERVOUS SYSTEM


A. Colebrum - ubongo wa mbele


B. Celebelem – Ubongo wa kati


C. Medulla Oblangata – Ubongo wa nyuma


























“Sikiliza, Ee Israel; Bwana, Mungu wetu, Bwana ndiye nawe mpende Bwana Mungu wako, Kwa moyo wako wot, na kwa roho yako, na kwa nguvu zako zote”. K. TORATI 6:4 -5


“Linda moyo wako kuliko yote uyalindayo maana ndiko zitokako chemichemi za uzima”MITHALI 4:20 -23


“Mimi ni Mungu wa Ibrahim, na Mungu wa Isaka, na Mungu wa Yakobo? Mungu sio Mungu wa wafu, bali wa wawaliyo hai”MATHAYO 22:32














A. Ubongo wa mbele au ubongo mkubwa. Sehemu hii inahusika na utawara wa


matendo yote ya hiari hasa yale yanayo husiana na kufikiri, Busara na kumbukumbu. Sehemu hii pia huhusika na kuona, kusikia, kunusa na kuonja.






B. Ubongo wa kati au ubongo mdogo : Sehemu hii huratibu mijongeo katika mwili, sehemu hiyo ndiyo inayohusika na kuweka mwili uwe katika hali ya msawazo kiumbo.






C. UBONGO WA NYUMA – MEDULLA OBLANGATA.


Sehemu hii hutawara matendo yote yasiyo ya hiari katika mwili, kwa mfano, kupumua, mapigo ya moyo, kutanuka na kusinyaa kwa mishipa ya damu na mmeng’enyo wa chakula katika njia ya chakula .


Sehemu iliyo kubwa, tata na yenye kazi nyingi zaidi ya ubongo mkubwa. Uso wake umekunjamana sifa ambayo huongeza eneo lake. Uso wa ubongo wa nyuma ndiye sehemu ya chini zaidi ya ubongo na imeunganishwa na ubongo wa kati na ugwe mgongo.Mithali 17:2-22, Mithali 16:23, Mithali 15:13 – 15 Mithali 3:8


















2. MACHO - EYE.






Jicho hushikiwa kwenye nafasi yake kwa misuli. Misuli hii huuweza kuzungusha mboni ya jicho kwa ajili ya kutazama sehemu mbalimbali. Kuna Neva moja itwayo neva ya Optike inayo unganisha jicho na ubongo sehemu kuu za jicho ni:


Lenzi - hupanuka na kusinyaa ili kufokasi taswira ya kitu kwenye retina


Retina - hupeke nuru na kuunda taswira ya kitu


Mboni – Pupili ni shimo katika mboni


Konea -Ni sehemu ya mbele inayowezesha kuona miale ya mwanga kupenya






Mucus in eye:Ute ute aina ya kemikali zinto inayoteleza inayotokana na tezi ute yenye kazi ya kulinda tishu za tabaka –nje zisikauke, na pia kuzuia viumbe na maradhi visidhuru jicho.














“Macho yako yatazame mbele, na kope zako zitazame mbele yako sawasawa. Ulisawazishe pito la mguu wako, na njia zako zithibitike, usingeuke kwa kuume wala kwa kushoto; ondoa mguu wako maovuni”, MITHALI 4:25-27






“Nilifanya agano na macho yangu; basi nawezaje kumuangalia msichana? AYUBU 31: 1, 16: 9-10, ZABULI 121: 1, 123: 1- 2






Eye strain - Uchovu wa macho , Computer eyestrain – ucovu wa kokotoa macho


Mucus in eye – uteute wa jicho, Yellow eys- macho ya njano, Puffy eyes (Bags undrs eyes) - mpumuo uhemaji wa mfumo wa macho, Itchy eyes - Mwasho wa macho, red eyes (Blood shol eyes) macho mekundu au damu kwenye macho


Black eyes – Macho meusi. NATURALA REMEDIES UK 301

















3. PUA






Pua zina seli zenye uwezo kuhisi kemikali .Kuna seli zinazotoa, kamasi ambalo lina unyevu kemikali zinazoyeyeshwa na unyevu huu hushitua seli hizi na kupeleka taarifa kwenye ubongo. Pia pua huhusika na mfumo wa upumuaji kutoa hewa nje na kuingiza ndani kwa kushirikiana na mapafu na sehemu nyingine zenye matundu .Mwanzo 2:7


























4. ULIMI.


Ulimi unaseli onji ambazo huonja na kuamua kama kiti ni kitamu, kichungu au chenye chachu. Pia ulimi unamsuli unazungusha nma kuufanya uwe na uwezo wa kumuwezesha mtu kutoa matamushi au tamushi .Pia ulimi umo ndani ya mdomo.Mithhali 4: 24, Mithali 6:2 Hata meno Zaburi 37:12.


“Nalisema nitazitunza njia zangu nisije nikakosa kwa ulimi wangu; nitajitia lijamu”..............ZABURI 39:1-3






“Vivyo hivyo ulimi nao ni kiungo kidogo, nao hujivuna majivuno makuu........... YAKOBO 3:5










5. SIKIO -EAR.






Sikio ni ogani ya kusikiliza na kusawazisha kuna migawanyo mitatu mikuu.


v Sikio la nje – Sikio la nje hukusanya sauti


v Sikio la kati – Sikio la kati lina hewa na dirisha lenye umbo la yai ambalo huelekea kwenye sikio la ndani .


v Sikio la ndani – Katika sikio la ndani kuna koklea ambayo huhisi sauti itakanayo na mitetemo kwa kutumia neva ya akausteka.


“Mwanangu, sikiliza maneno yangu; tega sikio lako, uzisikie kauli zangu....MITHALI 4:20-24


































6. MENO .






Meno teeth meno ni viungo pia mhimu kwa ajili ya kazi kutafuna wakati wa kula ni vema kuyatunza meno . Mtahayo 22:13 meno hushikiliwa na misili aina ya miziz, au nyuzinyuzi. Nyuzinyuzi hizi zinapopata hitirafu mtu hupatwa na tatizo la usafi wa meno ni mhimu kwa ulinzi, na kula vyakula vyenye virutubisho.


Wengi wanaopatwa na ugonjwa wa meno ni wale, wanatumia, pipi, barafu, au vitu vya baridi soda, pombe, ugoro, sukari, nyama maana nyama inapoliwa nyuzi nyuzi za nyama hepenya nyufa za maunganishio ya meno, wengi huchokonoa kwa njiti, au mti vyote hivi ni vyanzo vya matatizo ya meno






“Amenilalua katika gharabu zake,na kunionea; amesaga-saga meno juu yangu; AYUBU 16: 9, 5-8








MFUMO WA KIFUA.






a. MOYO - Unafanya kazi ya kusukuma damu au kupampu. Na damu kuzunguka mwilini, kazi ya moyo ni ya mhimu maana kiungo hiki ni cha thamani kwa maana katika viungo hiki ndicho kiungo kisicho pumzika kinafanya kazi tangu kuumbwa kwa mtu hadi kifo ni yetu kukitunza . Pia unamishipa midogo ya kusafilisha damu pia moyo unapampu mbili.






1. Upande wa juu – Pampu hii inasukuma damu kwenda juu kwa kushirikiana na mapafu kunyumbua


2. Nyingine upande wa chini- Hii pampu hizi zinapo shindwa kufanyakazi magonjwa ya presha ya kupanda – kushuka kutumia vyakula vyenye vichocheo huleta kiherehere cha moyo, moyo kupanuka, mafuta kwenye mishipa ya damu ya moyo. Moyo kushindwa kufanya kazi, acha kutumia singira, sukari za viwandani, na juisi chumvi bichi, nyama, samaki pombe, mavazi ya kubana mwili, viatu vyenye kisingino kilefu sana, sembe, ngano iliyokobolewa, na isiyo ya asili.






“Maana wewe ndiwe uliyeniumba mtima wangu, ........ Zaburi 139:13


Presha ya juu, Presha ya chini, Kupanuka kwa moyo, Kusinyaa kwa mshipa ya moyo, Mafuta kwenye mshipa ya moyo, Kiherehere cha moyo, Kuziba kwa pampu ya juu ya moyo, Kuziba kwa pampu ya chini ya moyo.


b. MAPAFU.






Mapafu hufanya kazi ya kuchunja hewa na mapafu kunyumbuka. Kazi ya kuondoa hewa chafu, na kuunda mfumo kwenye mfumo wa hewa safi. Na kuondoa uchafu kwenye mfumo hewa, mavumbi, moshi, na mazingira yenye hewa chafu n.k


Inashirikiana na sehemu zenye matundu ya mwili, na mfumo wa ngozi. Pia mapafu yana mishipa aina ya tawi na mfumo wa nyuzi nyuzi. Mapafu yanaposhindwa kufanyakazi mtu hupata tatizo la kupumua kwa shida na kufanya kazi ya moyo kuwa ya shida sana Huduma ya uponyaji uk 165.






Kukohowa, Madonda kooni kuziba kwa mirija ya mapafu. Ni vema mtu kukaa mahali penye hewa safi na kujenga nyumba zenye madirisha ya kuingiza, hewa, na mwanga wa jua. Kutumia sigara majani ya chai, kahawa ni hatari sana, na kutumia aina ya vinywaji vikari vyakula vyenye vichocheo ni hatari pia. Habakuki 2:15- 16, Isaya 5:11- 12 .






kwa mfano magonjwa


1. Saratani ya mapafu,


2. Athima (Pumu)


3. Kupumua vibaya


4. Kuvimba mishipa


5. Madonda kooni






Pia kuvaa nguo za kubana kifua husababisha tatizo la moyo, Kutayarisha
KIWAMBA MOYO DIAPHRAGM






Kiungo hiki huunganika na vena cava kwa umbo la mfano wa misitari ya mikononi kiungo hiki na viungo vingine huninginia kwneye kiungo, kama vile moyo, mapafu, mafingo kwenye kiungo hiki huanganisha mishipa yote mikubwa inayosfili kwenye vidole vya mikono na minguu. Huungana sup, vena cava. Na inf vena cava. Na renal inayounganisha figo ya kulia na vena cava na upande wa kushoto .













MFUMO WA MIFUPA NA VIUNGO VINGINE KWA UJUMLA .BASIC ANATOMY.






Huu ni mfumo unajumuisha mbavu, mapaja miguu, mikono, mafuvu, vibandiko vya aina ya parastiki, vinavyofunga kama vile mabega, sehemu za siri, kwa jinsia zote.


Mungu alimumba mwadamu kwa ustadi mwanadamu ni kazi ya Mungu. Zaburi 100:3, Ayubu 10:8 -9, Isaya 45: 9 -10, Ezekiel 37: 4- 9.


Skull – Fuvu la kichwa


Spine – Uti wa mgongo


Humenus – Mfupa kubwa utakao begani hadi kwenye mkono






Nyonga






Tezi za ovari ziko katika nyonga ya mwanamke ziko tezi mbili za ovari.










Paji la uso.






Uso ni sehemu ya paji likionyesha muonekano wa mtu.


1. Kama mtu amekasilika au kuwaza uso hukunjamana kuonyesha hari ya mtu isiyo ya kawaida, mwanzo 4......hasira gadhabu, mithali 15:18 .





2. Uso wa mtu mwenye muunekano wa faraja huu ndio uso wenye afya mithali 15:13, Mithali 14:30, Mithali 15:30

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

HUDUMA ZA MAZISHI

Huduma ya Mazishi  (Mchungaji, mzee wa kanisa, au shemasi anaweza kufanya huduma hii). Ushauri umetolewa kwamba, kadiri inavyowezekana, maz...