Jumatano, 17 Januari 2018

KIASI KWA KILA JAMBO

HASARA ZA KUPENDA KUPITA KIASI




Kupenda ni jambo muhimu katika maisha ya mwanadamu, kwa sababu asilimia kubwa ya matendo ya mtu huongozwa na mapenzi. Miongoni mwetu kuna watu wanapenda waume/wake zao, mali, watoto, magari vyakula, vinywaji, michezo na pengine aina fulani ya maisha.

Baadhi yetu tuko tayari kupoteza maisha kama tutaachwa na wapenzi au kukosa mambo tuliyoyapenda. Pamoja na kwamba moyo hupata maumivu pale mazuri yanapokosekana, bado kuna ukweli juu ya madhara ya kujitakia yanayoweza kuepukwa na mtu anayeumia kwa kiwango cha kukosa usinginzi, kulia mara kwa mara kiasi cha kushindwa kufanya kazi zake kama kawaida.

Kupenda kwa kiwango cha kushindwa kujizuia na kuvumilia ni hatari kwa afya ya mwanadamu, kwani uchunguzi unaonesha kuwa watu wengi wanaosumbuliwa na ugonjwa wa vidonda vya tumbo, moyo na wale wenye magonjwa yasiyoonekana kitalaamu pamoja na wanaokufa ghafla ni athari za msongo wa mawazo utokanao na kukosa mazuri wanayohitaji katika maisha yao.(Jiulize ni kipi kinachokutia simanzi moyoni mwako).

Kisaikolojia kuutesa moyo kwa sababu mpenzi wako kakukataa ni matokeo ya kufikiri vibaya kwani ushahidi uliopo miongoni mwetu unaonesha kuwa mapenzi si kitu cha kudumu kwa miaka mingi na anayesema anaweza kupenda jambo moja milele kwa kiwango kilekile ni mtu anayejiwekea mtengo utakaomnasa mwenyewe na kumtesa.

Watu wengi tunaowaona wakipagawa baada ya kupewa talaka na waume zao au kuondolewa mambo fulani waliyokuwa wanayapenda ni wale walioyachukulia mapenzi kama kitu cha kudumu kisichoweza kubadilika, huku wakisahau ukweli kuwa wanayopenda kwa wakati huo hawakuzaliwa nayo na wala hawakuyapenda kabla.

Licha ya kuwepo kwa umuhimu wa kujiaminisha katika kupenda kwa msingi wa muda mrefu, mtu hatakiwi kukataa mabadiliko yanapotokea kwani ni wazi kwamba tuliyopenda tulipokuwa watoto si yale tunayopenda sasa. Hivyo ni jukumu la kila mtu anayetaka kuwa salama na maumivu ya moyo ya kumkosa ampendaye ni kuwa tayari kubadilika kutoka kupenda kitu cha awali mpaka kijacho, kuliko kung’ang’ania wazo moja na kujitesa nalo.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

HUDUMA ZA MAZISHI

Huduma ya Mazishi  (Mchungaji, mzee wa kanisa, au shemasi anaweza kufanya huduma hii). Ushauri umetolewa kwamba, kadiri inavyowezekana, maz...