Kupenda fedha na mali kunaweza kutujia kutoka sehemu nyingi mbalimbali. Ellen G. White anaeleza hila ya Shetani ya kutushawishi kupitia kwa ujanja wa tamaa ya vitu. “Nenda uwafanye wamiliki wa ardhi na fedha kulewa kutokana na shughuli za maisha haya. Wasilisha ulimwengu mbele yao katika nuru ya uzuri wake wa juu kabisa, ili wapate kuweka hazina zao hapa, na kukaza upendo wao juu ya vitu vya dunia. Ni lazima tufanye kila tuwezalo kuwazuia wale wanaofanya kazi katika njia ya Mungu kupata mali za kutumia dhidi yetu. Fanya fedha ipatikane kwa watu wetu peke yao. Kadiri watakavyopata mali nyingi, ndivyo watakavyoudhuru ufalme wetu kwa kuchukua kutoka kwetu wale tuliowaweka chini yetu. Wafanye kusumbuka zaidi kuhusu fedha kuliko kujenga ufalme wa Kristo na usambazaji wa ukweli tunaouchukia, na hatutakuwa na haja ya kuhofu mvuto wao; kwa vile tunafahamu kuwa kila mtu mbinafsi, mwenye tamaa ataanguka chini ya uwezo wetu, na hatimaye atatengwa kutoka kwa watu wa Mungu.”—Counsels on Stewardship, uk. 154, 155.
Hila hii, kwa bahati mbaya, inaonekana kutenda kazi yake vyema. Hebu basi tuziangalie hatari hizi na kile ambacho Neno la Mungu linasema kwetu ili tuweze kuepuka mtego huu wa kiroho.
“Baadhi huipenda sana dunia hii kiasi kwamba [dunia] inameza upendo wao kwa ajili ya ile kweli. Kadiri wanavyoimiliki dunia hii shauku yao kwa ajili ya hazina za mbinguni hupungua. Kadiri wanavyomiliki vitu vya dunia hii, ndivyo wanavyoikumbatia kwao kwa karibu zaidi, kana kwamba wanaogopa mali yao waliyoitamani itachukuliwa kutoka kwao. Kadiri wanavyomiliki vitu vingi, ndivyo wanavyotoa kidogo sana kwa ajili ya watu wengine, kwa sababu kadiri wanavyokuwa navyo vingi, ndivyo wanavyojisikia kuwa maskini zaidi. Lo! Udanganyifu wa mali! Hawataona na kuhisi mahitaji ya njia ya Mungu.”—Ellen G. White, Spiritual Gifts, vol. 2, uk. 267.
“Divai Mpya” ya Ufalme
Wala hakuna mtu atiaye divai mpya katika viriba vikuukuu; ikiwa atia, ile divai mpya itavipasua viriba vile, divai ikamwagika, vile viriba vikaharibika. Bali hutia divai mpya katika viriba vipya. Marko 2:22.
T
unahitaji daima Kristo ajae katika nia zetu, na wakati wote tuondoe ubinafsi na dhambi ndani yetu. Yesu alipokuja ulimwenguni, viongozi wa Wayahudi walikuwa wamejawa Ufarisayo kiasi kwamba hawakuweza kupokea mafundisho yake. Yesu aliwafananisha na viriba vikuukuu ambavyo havikufaa kutiwa divai mpya toka katika msimu mpya wa divai. Ilimbidi atafute viriba vipya ambamo ataweka divai mpya ya ufalme wake. Hii ndiyo sababu aliwapa kisogo Mafarisayo, na kuchagua wavuvi wa hali ya chini wa Galilaya.
Yesu alikuwa mwalimu bora kabisa kuliko wote ambao ulimwengu umepata kuwa nao, na akachagua watu ambao angewaelimisha, na ambao wangeyaamini maneno yake, na kuwatuma kizazi hata kizazi hadi wakati wetu. Hivyo kwa Roho wake na Neno lake, atakuelemisha ili utende kazi yake. Kwa hakika kadiri unavyoondoa akilini mwako ubatili na upuuzi, hilo ombwe litajazwa na kile ambacho Mungu anangoja kukupatia - Roho wake Mtakatifu. Ndipo kutoka katika hazina njema ya moyo utatoa mambo mema, mawazo yenye ubora wa juu sana, na wengine watachukua maneno yako, na kuanza kumtukuza Mungu. Basi mawazo yako hayatajengwa katika ubinafsi. Hutakuwa mtu wa kujionyesha; hutakuwa ukitenda kibinafsi; bali fikra zako na matamanio yako yatakuwa kwa Kristo, na utawaonesha wengine yale ambayo yameangaza juu yako toka katika jua la haki.
Kristo alisema: “Mtu akiona kiu, na aje kwangu anywe.” (Yohana 7:37). Je, umemaliza maji yaliyo katika chemchemi? - La hasha; kwani maji yake hayaishi. Mara tu unahisi hitaji, unaweza kunywa, na kunywa tena. Daima chemchemi imejaa. Na mara unapokunywa maji ya chemchemi hii, hutahangaika kuzima kiu yako toka katika visima vilivyo pasuka vya ulimwengu huu; hutakuwa unatafuta kuelewa namna ya kupata anasa, vichekesho, vitu vya kukufurahisha, masihara. La hasha; kwa vile unakunywa katika kijito kiletacho furaha katika mji wa Mungu. Hivyo utakuwa na furaha tele; kwani Kristo atakuwa pamoja nawe, tumaini la utukufu. --Review and Herald, March 15, 1892.
Yesu alikuwa mwalimu bora kabisa kuliko wote ambao ulimwengu umepata kuwa nao, na akachagua watu ambao angewaelimisha, na ambao wangeyaamini maneno yake, na kuwatuma kizazi hata kizazi hadi wakati wetu. Hivyo kwa Roho wake na Neno lake, atakuelemisha ili utende kazi yake. Kwa hakika kadiri unavyoondoa akilini mwako ubatili na upuuzi, hilo ombwe litajazwa na kile ambacho Mungu anangoja kukupatia - Roho wake Mtakatifu. Ndipo kutoka katika hazina njema ya moyo utatoa mambo mema, mawazo yenye ubora wa juu sana, na wengine watachukua maneno yako, na kuanza kumtukuza Mungu. Basi mawazo yako hayatajengwa katika ubinafsi. Hutakuwa mtu wa kujionyesha; hutakuwa ukitenda kibinafsi; bali fikra zako na matamanio yako yatakuwa kwa Kristo, na utawaonesha wengine yale ambayo yameangaza juu yako toka katika jua la haki.
Kristo alisema: “Mtu akiona kiu, na aje kwangu anywe.” (Yohana 7:37). Je, umemaliza maji yaliyo katika chemchemi? - La hasha; kwani maji yake hayaishi. Mara tu unahisi hitaji, unaweza kunywa, na kunywa tena. Daima chemchemi imejaa. Na mara unapokunywa maji ya chemchemi hii, hutahangaika kuzima kiu yako toka katika visima vilivyo pasuka vya ulimwengu huu; hutakuwa unatafuta kuelewa namna ya kupata anasa, vichekesho, vitu vya kukufurahisha, masihara. La hasha; kwa vile unakunywa katika kijito kiletacho furaha katika mji wa Mungu. Hivyo utakuwa na furaha tele; kwani Kristo atakuwa pamoja nawe, tumaini la utukufu. --Review and Herald, March 15, 1892.
Moto Uwakao
Nami nikisema, Sitamtaja, wala sitasema tena kwa jina lake; basi, ndipo moyoni mwangu kumekuwamo kama moto uwakao, uliofungwa ndani ya mifupa yangu, nami nimechoka kwa kustahimili, wala siwezi kujizuia. Yer. 20:9.
M
ungu atagusa mioyo ya watu wa hadhi za chini ili watangaze ujumbe wa ukweli wa leo. Wengi wa aina hiyo wataonekana wakienda mbio huko na huko, wakibidishwa na Roho wa Mungu kuwapa nuru wale walio gizani. Ukweli ni sawa na moto mifupani ukiwapa shauku inayowaka kuwaangazia wale waketio gizani. Wengi, hata miongoni mwa wasio na elimu, watalitangaza Neno la Bwana. Watoto watasukumwa na Roho Mtakatifu kutoka kwenda kutangaza ujumbe wa mbinguni. Roho atamwagwa kwa wale walioradhi kutekeleza maelekezo yake. Wakiweka kando sheria zinazowafunga wanadamu na miondoko ya hadhari, watajiunga na jeshi la Bwana.
Katika siku za usoni watu wa maisha ya kawaida watavutwa na Roho wa Bwana kuacha ajira zao za kawaida na kwenda kutangaza ujumbe wa mwisho wa rehema. Wanapaswa kuandaliwa kwa ajili ya kazi kwa kasi kubwa kadiri iwezekanavyo, ili jitihada ziweze kuleta mafanikio. Wanashirikiana na mawakala wa mbinguni kwani wako radhi kutumika na kutumiwa katika huduma ya Bwana. Hakuna aliyepewa mamlaka kuwakwamisha watendakazi hawa. Wanatakiwa waagizwe kwenda kwa kasi ya Bwana wanapotoka kwenda kutimiza agizo kuu. Hakuna neno lolote la kuudhi wanalopaswa kunenewa kwani wanapanda mbegu ya injili katika mazingira yaliyojaa mikikimikiki ya dunia.
Vitu bora kabisa vya maisha – usahili, unyofu, ukweli, usafi, uadilifu usiochafuliwa—usioweza kununuliwa au kuuzwa; wako huru kuchanganyika na wasio na elimu kama wanavyochanganyika na wasomi, kwa mweusi au mweupe, kwa mkulima wa hali ya chini au kwa mfalme katika kiti chake cha enzi. Watumishi wanyenyekevu wasiotumainia nguvu zao wenyewe, bali watendao kazi kwa usahili, daima wakimtumaini Mungu, watashiriki furaha ya mwokozi. Maombi yao ya uvumilivu yataleta roho msalabani. Katika kushirikiana na jitihada za kujinyima, Yesu atagusa mioyo ya watu akifanya miujiza katika uongofu wa roho. Wanaume na wanawake watakusanyika katika ushirika kanisani. Nyumba za mikutano na shule zitaanzishwa. Mioyo ya watendakazi itajawa na furaha wakiona wokovu wa Mungu.--Testimonies, vol. 7, pp. 26-28.
Katika siku za usoni watu wa maisha ya kawaida watavutwa na Roho wa Bwana kuacha ajira zao za kawaida na kwenda kutangaza ujumbe wa mwisho wa rehema. Wanapaswa kuandaliwa kwa ajili ya kazi kwa kasi kubwa kadiri iwezekanavyo, ili jitihada ziweze kuleta mafanikio. Wanashirikiana na mawakala wa mbinguni kwani wako radhi kutumika na kutumiwa katika huduma ya Bwana. Hakuna aliyepewa mamlaka kuwakwamisha watendakazi hawa. Wanatakiwa waagizwe kwenda kwa kasi ya Bwana wanapotoka kwenda kutimiza agizo kuu. Hakuna neno lolote la kuudhi wanalopaswa kunenewa kwani wanapanda mbegu ya injili katika mazingira yaliyojaa mikikimikiki ya dunia.
Vitu bora kabisa vya maisha – usahili, unyofu, ukweli, usafi, uadilifu usiochafuliwa—usioweza kununuliwa au kuuzwa; wako huru kuchanganyika na wasio na elimu kama wanavyochanganyika na wasomi, kwa mweusi au mweupe, kwa mkulima wa hali ya chini au kwa mfalme katika kiti chake cha enzi. Watumishi wanyenyekevu wasiotumainia nguvu zao wenyewe, bali watendao kazi kwa usahili, daima wakimtumaini Mungu, watashiriki furaha ya mwokozi. Maombi yao ya uvumilivu yataleta roho msalabani. Katika kushirikiana na jitihada za kujinyima, Yesu atagusa mioyo ya watu akifanya miujiza katika uongofu wa roho. Wanaume na wanawake watakusanyika katika ushirika kanisani. Nyumba za mikutano na shule zitaanzishwa. Mioyo ya watendakazi itajawa na furaha wakiona wokovu wa Mungu.--Testimonies, vol. 7, pp. 26-28.
Madhara ya Kutotembea na Mungu
Basi Yesu akawaambia, Nuru ingaliko pamoja nanyi muda kidogo. Enendeni maadamu mnayo nuru hiyo, giza lisije likawaweza; maana aendaye gizani hajui aendako. Yohana 12:35.
Y
esu anasema, “ Enendeni maadamu mnayo nuru hiyo.” Kusanya miale yote, msiache hata mmoja. Weka katika vitendo kila kanuni ya kweli uliyofundishwa. Ishi kwa kila neno litokalo kinywani mwa Mungu, ndipo utamfuata Kristo kila aendako. Bwana anapowasilisha ushahidi mmoja baada ya mwingine na kutoa nuru moja baada ya nyingine, kwa nini watu wanasita kutembea katika nuru? Kwa nini watu wanapuuzia kutembea katika nuru kwa nuru kubwa zaidi?
Bwana hakatai kuwapa Roho Mtakatifu wale wamwombao. Usadikishwaji unapofika katika dhamira, kwa nini usisikilize, na kuitii sauti ya Roho wa Mungu? Kwa kila kusita na kuchelewa, tunajiweka katika mazingira ambayo inakuwa vigumu zaidi kwetu kukubali nuru ya mbinguni, na hatimaye inaonekana jambo lisilowezekana kushawishiwa na maonyo. Mdhambi anaseme kwa urahisi zaidi na zaidi, “Sasa enenda zako, nami nikipata nafasi nitakuita.” (Mdo 24:25).
Najua hatari ya wale wakataao kutembea katika nuru Mungu anapoitoa. Wanajiletelezea dhahama ya kutisha ya kuachwa wafuate njia zao wenyewe, kutenda watakavyo. Dhamiri inaendelea kuwa sugu hatua kwa hatua. Sauti ya Mungu inaonekana kufifia hatua kwa hatua na mtenda maovu huachwa kuishi kulingana na upumbavu wake. Kwa kiburi hukataa kila wito, hudharau mashauri yote na nasaha, na kujitenga mbali na kila majaaliwa yaliyotolewa kwa ajili ya wokovu wake, na sauti ya mtumishi wa Mungu haileti ushawishi wowote katika nia yake. Roho wa Mungu hana tena nguvu ya kumzuilia, na hukumu inatolewa, “Amejiungamanisha na sanamu; mwache.” (Hosea 4:17). O, ni giza na huzuni kiasi gani huo uhuru wake wa kukataa kabisa mwito wa Mungu! Inaonekana kwamba hali ya kutotambua kuwa anaelekea mautini ipo moyoni mwake. Huu ni mchakato ambao mtu anayekataa utendaji wa Roho Mtakatifu huupitia.--Review and Herald, June 29, 1897.
Bwana hakatai kuwapa Roho Mtakatifu wale wamwombao. Usadikishwaji unapofika katika dhamira, kwa nini usisikilize, na kuitii sauti ya Roho wa Mungu? Kwa kila kusita na kuchelewa, tunajiweka katika mazingira ambayo inakuwa vigumu zaidi kwetu kukubali nuru ya mbinguni, na hatimaye inaonekana jambo lisilowezekana kushawishiwa na maonyo. Mdhambi anaseme kwa urahisi zaidi na zaidi, “Sasa enenda zako, nami nikipata nafasi nitakuita.” (Mdo 24:25).
Najua hatari ya wale wakataao kutembea katika nuru Mungu anapoitoa. Wanajiletelezea dhahama ya kutisha ya kuachwa wafuate njia zao wenyewe, kutenda watakavyo. Dhamiri inaendelea kuwa sugu hatua kwa hatua. Sauti ya Mungu inaonekana kufifia hatua kwa hatua na mtenda maovu huachwa kuishi kulingana na upumbavu wake. Kwa kiburi hukataa kila wito, hudharau mashauri yote na nasaha, na kujitenga mbali na kila majaaliwa yaliyotolewa kwa ajili ya wokovu wake, na sauti ya mtumishi wa Mungu haileti ushawishi wowote katika nia yake. Roho wa Mungu hana tena nguvu ya kumzuilia, na hukumu inatolewa, “Amejiungamanisha na sanamu; mwache.” (Hosea 4:17). O, ni giza na huzuni kiasi gani huo uhuru wake wa kukataa kabisa mwito wa Mungu! Inaonekana kwamba hali ya kutotambua kuwa anaelekea mautini ipo moyoni mwake. Huu ni mchakato ambao mtu anayekataa utendaji wa Roho Mtakatifu huupitia.--Review and Herald, June 29, 1897.
NJIA IPI
Ingieni kwa kupitia mlango ulio mwembamba; maana mlango ni mpana, na njia ni pana
iendayo upotevuni, nao ni wengi waingiao kwa mlango huo. Bali mlango ni
mwembamba, na njia imesonga iendayo uzimani, nao waionao ni wachache. Mathayo
7:l3,l4.
Mbele yenu kuna njia mbili ----- njia pana iliyojaa anasa na njia nyembamba ya kujikana
nafsi. Katika njia pana unaweza kwenda na uchoyo wako, kiburi chako, na kuipenda
dunia kwako; lakini wale wanaokwenda katika njia ile nyembamba wanalazimika
kuweka kando kila mzigo mzito na dhambi zinazowazinga kwa upesi. Njia ipi
umechagua ----- je! ni njia ile iendayo kwenye mauti ya milele, au ni njia ile iendayo
kwenye utukufu na uzima wa milele? ----- YI, Feb.13, 1902.
Kamwe hapajapata kuwa na wakati wa kutisha sana katika historia ya ulimwengu huu
kama wakati huu tunaoishi sasa. Mambo yetu ya milele yako hatarini, ingetupasa nasi
kuamka na kuona umuhimu wa kufanya imara kuitwa kwetu na uteule wetu. Hatuwezi
kuthubutu kuyahatarisha mambo yetu ya milele kwa kudhani-dhani tu. Ni lazima tuwe
makini. Vile tulivyo, vile tufanyavyo, vile tutakavyofuata katika matendo yetu kwa
wakati ujao, hizo zote ni hoja za maana mno kwetu, nasi hatuwezi kuwa walegevu, watu
wasiojali, na wasiohusika. Kila mmoja wetu yampasa kujiuliza, "Je, umilele ni kitu gani
kwangu mimi?" Je! miguu yetu i katika njia ile inayokwenda mbinguni, au i katika njia
ile pana iendayo upotevuni?
Wale wanaofanikiwa katika maisha yao ya Kikristo watayahesabu mambo yote kuwa
hasara kwa ajili ya uzuri usio na kiasi wa kumjua Kristo. Ni wale tu wanaoendelea kukaa
ndani ya Kristo wawezao kujua maisha halisi yalivyo. Wanaitambua faida ya dini ya
kweli. Wameweka juu ya madhabahu ya kujitoa wakf talanta zao zote za mvuto wao na
mali yao pamoja na uwezo wao, huku wakiwa wanatafuta tu kuyajua mapenzi yake Yule
aliyewafia ili kuwakomboa. Wanajua kwamba njia wanayopaswa kusafiri imesonga, tena
ni nyembamba, na ya kwamba itawapasa kukutana na vipingamizi vingi pamoja namajaribu, hapo ndipo watakapovipinga vishawishi vilivyomo katika njia ile pana iendayo
upotevuni; walakini watazitambua nyayo za Yesu, na kukaza mwendo na kuifikilia mede
ya thawabu ya mwito mkuu wa Bwana na Mwokozi wao. Watachagua njia ile ya kifalme
iendayo mbinguni. ----- RH, Mei 26, 1981.
TUMEZUNGUKWA NA FADHILI ZAKE MUNGU Januari 3
Naye mtu mwovu ana mapigo mengi, Bali amtumainiye BWANA fadhili zitamzunguka.
Zaburi 32:10.
Mara nyingi tunadhani kwamba wale wanaomtumikia Mungu wanayo majaribu mengi
kuliko yule asiyeamini, na kwamba njia iliyowekwa kwa ajili yao ili kutembea humo
inaparuza.... Lakini, je! mwenye dhambi anafurahia anasa zake za kidunia pamoja na raha
zake pasipo kuwa na tatizo lo lote? La, hasha. Kuna nyakati ambapo mwenye dhambi
anasumbuka sana. Anamwogopa Mungu, ila hampendi.
Je! waovu hawakati tamaa,, hawana wasiwasi, hawapati hasara katika biashara zao za
kidunia, hawana umaskini [ukata] na dhiki? Wengi wao husumbuka na maradhi ya
kudumu, ila wao hawanaye Yule aliye na nguvu na uweza ambaye wangeweza
kumtegemea, wala hawana neema ile itiayo nguvu itokayo kwa mamlaka ile ya juu zaidi
ili kuwategemeza katika udhaifu wao. Wao wanazitegemea nguvu zao wenyewe.
Hawapati faraja yo yote wanapoangalia mbele, bali wanasumbuka sana kwa hofu ya
kutokuwa na hakika; na hivyo wanafumba macho yao na kufa, pasipo kuona raha yo yote
kwa kutazama mbele kwenye ile asubuhi [njema] ya ufufuo, kwa kuwa hawana tumaini
lo lote linalowatia moyo kwamba watakuwa na sehemu yo yote katika ufufuo ule wa
kwanza....
Mkristo anaweza kupatwa na maradhi, kukata tamaa, umaskini [ukata], shutuma, na
dhiki. Lakini awapo katikati ya mambo hayo yote anaendelea kumpenda Mungu,
anachagua kufanya mapenzi Yake, naye hathamini kitu kingine cho chote isipokuwa
kukubaliwa naye [Mungu]. Katika majaribu yake mbalimbali na mabadiliko katika
mandhari [hali mbalimbali] za maisha haya, anajua kwamba yuko Mmoja ajuaye hayo
yote. Mmoja atakayeweza kusikiliza kilio cha wenye huzuni na wenye dhiki, Mmoja
anayeweza kuguswa [moyo wake] na kila huzuni [yao] na kutuliza uchungu mkali uliomo
ndani ya kila moyo....
Katikati ya mateso hayo yote, Mkristo anayo faraja thabiti. Na kama Mungu ataruhusu
ateseke na maradhi ya kudumu yenye usumbufu mwingi kabla hajafumba macho yake na kufa, basi, anaweza kustahimili maumivu yote kwa moyo wa uchangamfu.... Yeye
anatafakari mambo yale yaliyo mbele yake huku akiwa amepata kitulizo cha kimbingu.
Pumziko fupi kaburini, na halafu Mpaji-Uzima wake atavivunjilia mbali vifungo vya
kaburi, atamtoa nje mateka huyo na kumtoa kwenye kitanda chake cha mavumbi akiwa
na hali ya kutokufa, asiweze kuona tena maumivu kamwe, wala huzuni, wala mauti. Ni
tumaini lililoje alilo nalo Mkristo! Hebu tumaini hilo la Mkristo na liwe langu mimi.
Hebu na liwe lako wewe. ----- Letter 18, 1859.
MIBARAKA YA KUTUCHANGAMSHA Januari 4
Jinsi zilivyo nyingi fadhili zako ulizowawekea wakuchao; Ulizowatendea wakukimbiliao
mbele ya wanadamu! Zaburi 31:19.
Mungu anaimwaga mibaraka yake katika njia yetu yote ili kuifanya safari yetu iwe ya
furaha na kuiongoza mioyo yetu kumpenda na kumsifu, Naye anatutaka sisi kuteka maji
yetu katika visima vya wokovu ili mioyo yetu ipate kuburudika. Twaweza kuimba
nyimbo za Sayuni, twaweza kuichangamsha mioyo yetu sisi wenyewe, tena twaweza
kuichangamsha mioyo ya wengine; tumaini letu laweza kuimarishwa, na giza kugeuzwa
kuwa nuru. Mungu hajatuacha sisi katika ulimwengu huu wa giza ----- kama wasafiri na
wageni watafutao nchi iliyo bora, ile ya mbinguni ----- pasipo kutupa sisi ahadi zake za
thamani ili kuufanya kila mzigo mzito [tuliobeba] kuwa mwepesi. Kingo za njia yetu
zimepambwa kwa maua mazuri ya ahadi [zake]. Yanachipua pande zote yakitoa harufu
nzuri sana. ----- Letter 27, 1886.
Ni mibaraka mingapi tunayoipoteza kwa sababu tunaidharau na kuipuuza [kutoitilia
maanani] mibaraka tunayopokea kila siku, tukiitamani sana ile ambayo hatunayo [kwa
sasa]. Fadhili za kawaida ambazo zinamwagwa huku na huko katika njia yetu
zinasahaulika na kuthaminiwa kidogo tu. Twaweza kujifunza mengi kutoka kwa vitu vya
kawaida katika viumbe vya asili. Ua lililo mahali penye giza na palipo duni hupokea
mwanga wote linaoweza kuupata, na kutoa majani yake. Ndege aliyefungiwa katika
kitundu anaimba katika kitundu cha gereza lake, ndani
ya nyumba zisizopata mwanga wa jua, kana kwamba yuko katika jengo la kimwinyi,
lenye mwanga wa jua. Mungu anajua iwapo sisi tutaitumia mibaraka yake kwa hekima na
kwa vizuri; kamwe hataweza kutupatia [mibaraka] hiyo ili tupate kuitumia vibaya.
Mungu anaupenda moyo wenye shukrani, unaoyasadiki kabisa maneno yake yenye ahadi,
ukijikusanyia faraja na tumaini na amani kutokana nayo; Naye atatufunulia sisi vina
virefu zaidi vya upendo wake. ----- RH, Aprili l2, 1887.Endapo tungelisifu jina takatifu la Mungu kama ipasavyo, basi, mwali wa moto wa
upendo ungewashwa ndani ya mioyo mingi.... Sifa kwa Mungu inapaswa kuwa mioyoni
mwetu daima na vinywani mwetu. Hii ndiyo njia iliyo bora sana ya kulipinga jaribu lile
la kushiriki katika maongezi yasiyofaa na ya upuuzi. ----- Letter 42, 1900.
Bwana angependa sisi tuwe tunatazama juu, na kuwa na shukrani kwake kwamba
mbingu iko.... Hebu na tuzishikilie sana kwa imani hai ahadi nyingi sana za Mungu, na
kuwa na shukrani kuanzia asubuhi mpaka usiku. ----- RH, Aprili 12, 1887.
HATARI ZA KUEPUKWA Januari 5
Ee BWANA, najua ya kuwa njia ya mwanadamu haimo katika nafsi yake; Kuelekeza
hatua zake si katika uwezo wa mwanadamu. Yeremia 10:23.
Barabara inayopitika katika Genge Kuu la Shujaa mwenye Cheo (Knight's Canyon),
ambalo sikuzote ni la hatari kwa msafiri asiyekuwa na uzoefu, mara nyingi huwa
halipitiki wakati wa majira ya mvua.* Tulishukuru sana kuwa na kiongozi katika sehemu
hii ya safari yetu. Sikudiriki kuangalia aidha kulia au kushoto ili kuiangalia mandhari ile
[hali ya eneo lile], bali, nikiwa nimeshikilia kamba zake kwa nguvu, na kumwongoza
farasi wangu katika njia ile nyembamba, nikamfuata kiongozi wetu. Uzembe mahali hapo
ungeleta kifo. Laiti kama farasi wetu angaliacha njia ile, tungeanguka chini ya genge lile
refu la wima mpaka kule bondeni chini.
Tulipokuwa tumepanda [juu ya farasi yule] na kusonga mbele kwa kimya kama watu
wasiopumua, niliweza kutafakari jinsi kielelezo kile cha kupanda farasi katika hali ile ya
hatari kilivyoelezea kwa nguvu jinsi maisha ya Mkristo yalivyo. Tunasafiri katika safari
yetu ya maisha tukiwa katikati ya hatari nyingi za siku za mwisho. Yatupasa kuwa
waangalifu kwa kila hatua [tunayokwenda], na kuwa na hakika kama tunamwandama
kiongozi wetu Mkuu. Tabia ile ya kuwa na mashaka, ukafiri, ubadhirifu, na uhalifu iko
kila mahali. Lingekuwa ni jambo rahisi kuziachilia hatamu za kujizuia nafsi, na kuanguka
chini ya genge refu la wima kwenda chini kwenye maangamizi ya hakika....
Upendo wa milele umetengeneza njia iendayo juu ambayo juu yake wale
waliokombolewa na Bwana wanaweza kupita toka duniani kwenda mbinguni. Njia ile ni
Mwana wa Mungu. Malaika viongozi wanatumwa kuiongoza miguu ile inayopotea.
Ngazi ile tukufu ya mbinguni [Yesu Kristo] imeshushwa chini katika njia ya kila mtu,
ikiweka kizuizi katika njia yake ya kwenda maovuni na kwenye upumbavu. Itampasakumkanyaga chini ya miguu yake Mkombozi wake aliyesulibiwa kabla [mtu huyo]
hajaenda mbele kwenye maisha yale ya dhambi. Sauti ya Baba yetu aliye mbinguni
inatuita, Njoo huku juu zaidi.... Wale walio wanyenyekevu, wanaomtegemea huongozwa
na kulindwa katika njia ile ya amani. Walakini Yule ambaye hekima yake haina kikomo
hamlazimishi ye yote kukipokea kipawa hicho cha Mbingu cha thamani kuu -----
hamlazimishi ye yote kutembea katika njia ile iliyotengenezwa kwenda juu kwa gharama
kubwa sana kama hiyo. Kila mmoja anaruhusiwa kuchagua yeye mwenyewe njia ile
nyembamba, iliyosimama wima iking'aa, iendayo mbinguni, au njia ile pana na njia rahisi
ambayo mwisho wake ni mauti. ----- ST, Jan.26, 1882.
_____________________________
* Taarifa hii ni ya safari kutoka Healdsburg kwenda St.Helena, California iliyofanywa na
Bibi White na rafiki yake, katika mwezi ule wa Desemba, 1881. Marafiki zao
walitangulia mbele wakiwa wamepanda farasi ili kuwaongoza katika upenyo wa hatari
kati ya magenge mawili milimani.
UPENDO UKAJENGA DARAJA Januari 6
Hili ndilo pendo, si kwamba sisi tulimpenda Mungu, bali kwamba Yeye alitupenda sisi,
akamtuma Mwanawe kuwa kipatanisho kwa dhambi zetu. 1 Yohana 4:10.
Upendo wa Mungu kwa ulimwengu huu haukudhihirishwa kwa sababu ya kumtuma
Mwanawe, bali kwa sababu aliupenda ulimwengu huu ndio maana alimtuma Mwanawe
ulimwenguni ili Uungu uliovikwa ubinadamu upate kuugusa ubinadamu, wakati Uungu
Wake unashikamana na Mungu. Japokuwa dhambi ilikuwa imefanya shimo kubwa kati
ya mwanadamu na Mungu wake, wema wake Mungu uliweka mpango wa kujenga daraja
juu ya shimo hilo kubwa. Je! alitumia vifaa gani? Sehemu yake Mwenyewe. Yule aliye
mng'ao wa utukufu wake Baba alikuja katika ulimwengu huu ulionyauka na kuharibika
vibaya kwa laana, na katika tabia yake ya Uungu, yaani, katika mwili wake wa mbinguni,
akaliziba shimo hilo kubwa.... Madirisha ya mbinguni yakafunguliwa na manyunyu ya
neema ya mbinguni yakadondoka katika ulimwengu wetu wenye giza kama vijito vya
uponyaji....
Mungu angekuwa ameitoa [neema yake] pungufu, sisi tusingaliweza kuokolewa. Lakini
Yeye alitoa kwa ulimwengu wetu [neema yake] kwa wingi mno hata isingeweza
kusemwa kwamba angetupenda zaidi [ya vile alivyotupenda]. Basi ni upumbavu ulioje
kwa msimamo ule uliochukuliwa [na watu fulani] kwamba kutakuwa na nafasi ya pili(second probation) baada ya ile ya kwanza kuisha kabisa. Mungu ametoa wema wake
wote... kwa kuimwaga mbingu yote kwa ajili ya mwanadamu katika kipawa hicho kimoja
kikuu [Yesu Kristo]. Ni kwa kuitambua thamani ya kafara [toleo] hii tu tunaweza
kumfahamu Mungu. Ni upana na kimo na kina kilioje cha upendo wake Mungu! Ni nani
miongoni mwa wanadamu wasiodumu milele awezaye kuufahamu?...
Mungu anamdai mwanadamu ampe mapenzi yake yote, moyo wake wote, roho yake
yote, akili yake yote, na nguvu zake zote. Anatoa madai yake kwa mtu mzima kama
alivyo, kwa sababu amemwaga hazina yake yote ya mbinguni kwa kutupa sisi vyote kwa
wakati mmoja, asibakize kitu cho chote kikubwa kuliko kile mbingu inachoweza
kufanya....
Ninapoanza kuandika juu ya somo hili, huwa naendelea tu kuandika, na kujaribu kuupita
ukingo wake wa nje, lakini nashindwa. Tutakapofika kwenye makao yale juu, Yesu
Mwenyewe atawaongoza wale waliovikwa mavazi meupe yaliyofuliwa na kufanywa
meupe katika damu ya Mwana-Kondoo mpaka atakapowafikisha kwa Baba yake. "Kwa
hiyo wako mbele ye kiti cha enzi cha Mungu, nao wanamtumikia mchana na usiku katika
hekalu lake, na Yeye aketiye katika kiti cha enzi atatanda hema yake juu yao." Ufunuo
7:15. ----- Letter 36a, 1890.
KIPAWA KIMOJA KIKUU MNO CHA MUNGU Januari 7
Mungu na ashukuriwe kwa sababu ya kipawa chake, tusichoweza kukisifu kama
ipasavyo.
2Wakorintho 9:15.
Wale wanaompokea Kristo kwa imani wataangaliwa na Mbingu kama lulu za thamani
ambazo mfanya biashara amezilipia gharama kubwa mno, na mawakala wake wa
kibinadamu wanaomwona Yesu watatambua kwamba wameipata hazina ya mbinguni.
Watakuwa na shauku ya kuuza vyote walivyo navyo ili kulinunua shamba hilo lenye
hazina hiyo. Wanapoutambua upendo huo wa Mungu, unapofunuliwa kwao mpango huo
wa wokovu, siri ya kujidhili kwake Kristo inapokuwa wazi sana kwao, wanapoiona
kafara aliyoitoa kwa ajili yao, hawahesabu kitu cho chote kuwa ni cha thamani mno kwao
kuweza kukiacha kwa ajili yake. Kadiri wanavyozidi kuongea juu ya upendo wa Mungu
wa ajabu, ndivyo unavyozidi kuwa mpana zaidi kwao, na Yule aliye mng'ao wa utukufu
wa Mungu anakuwa na utukufu mwingi mno kuweza kutazamwa kwa macho ya
binadamu anayekufa. Bwana Mungu wa mbinguni alikusanya utajiri wote wa malimwengu, na kuuweka chini
ili kuinunua lulu ile ya wanadamu waliopotea. Baba alitoa akiba yote ya mali yake na
kuiweka mikononi mwa Kristo ili mibaraka mingi sana ya mbinguni ipate kumwagwa juu
ya wanadamu walioanguka. Mungu asingeweza kuonyesha upendo wake mwingi sana
kuliko ule aliouonyesha kwa kumtoa Mwana wa kifuani mwake kwa ajili ya ulimwengu
huu. Kipawa hiki [Kristo] kilitolewa kwa mwanadamu ili kumthibitishia ya kuwa Mungu
hakuacha kufanya kitu cho chote ambacho angeweza kufanya, kwamba hakubakiza kitu
cho chote katika akiba yake, ila alimwaga mbingu yote katika kipawa kimoja kilicho
kikuu mno [kwa kumtoa Kristo]. Furaha ya sasa na ile ya milele ya mwanadamu
inategemea kuupokea kwake upendo huu wa Mungu, na kuzishika Amri [Kumi] za
Mungu.
Kristo ni Mkombozi wetu. Yeye ndiye Neno aliyefanyika mwili na kukaa kwetu. Yeye
ndiye ile Chemchemi ambayo kwayo twaweza kuoshwa na kutakaswa kutokana na
uchafu wetu wote. Yeye ndiye ile Kafara ya gharama kubwa mno ambayo ilitolewa kwa
ajili ya upatanisho wa mwanadamu. Ulimwengu ule wa mbinguni, malimwengu yale
ambayo hayakuanguka, ulimwengu wetu ulioanguka, pamoja na nguvu zote za uovu
zilizoungana HAWAWEZI KUSEMA kwamba Mungu angaliweza kufanya zaidi ya vile
alivyofanya kwa ajili ya wokovu wa mwanadamju. Kamwe kipawa chake hakiwezi
kupitwa na kiwango kingine cho chote, kamwe hawezi kuudhihirisha upendo wenye kina
kuliko huo. Kalvari inawakilisha kazi Yake timilifu....Bwana wetu angetaka wafuasi
wake wapendezwe sana na Mungu kwa njia ya ujuzi wa tabia yake kama Baba. ----- YI,
Okt. 17, 1895.
KUWAITA VIJANA WOTE! Januari 8
Maana ndiwe taraja langu, Ee Bwana MUNGU, Tumaini langu tokea ujana wangu.
----- Zaburi 71:5.
Yesu anamwita kila mpotevu, akisema, "Mwanangu, nipe moyo wako." Mithali 23:26....
Vijana hawawezi kuwa na furaha bila kuwa na upendo wa Yesu. Anangoja kwa huruma
kusikiliza maungamo ya wale walio watundu, na kuikubali toba yao. Anatazamia
kurudishiwa shukrani toka kwetu, kama vile mama anavyotazamia kuona tabasamu ya
kumtambua toka kwa mtoto wake ampendaye sana. Mungu aliye mkuu anatufundisha sisi
kumwita yeye Baba. Angependa sisi tuelewe jinsi moyo wake kwa dhati na kwa upole
unavyotupenda sana tunapokuwa katika maonjo na majaribu yetu....Vijana wangekuwa wanaendelea daima kukua katika neema, na katika ujuzi wa ile
kweli. Muumbaji wa vitu vyote, ambaye hazina zote za hekima anazo, ameahidi kuwa
kiongozi wao katika ujana wao. Yeye aliyezishinda nguvu zote za uovu kwa ajili yao
anawataka wamsujudie. Hapawezi kuwapo na ujuzi wa juu kuliko ule wa kumjua Yeye
ambaye kumjua vema ni uzima na amani; hakuna upendo ulio safi na wenye kina kuliko
upendo ule wa Mwokozi wetu.
Kuna majaribu kila upande kuinasa miguu ya wale wasiojihadhari. Vijana wale
wasiomcha Mungu, wenye matendo mabaya wanao mvuto wenye nguvu kuwaongoza
wengine katika njia zile zilizokatazwa. Hao ni miongoni mwa vibaraka wa Shetani
wanaofanikiwa sana.... Mara nyingi wapenda dunia hii watakuja katika vazi la kirafiki, na
kujaribu kuingiza desturi na matendo yake. Hebu kila askari wa kweli awe tayari
kuvipinga vishawishi hivyo.
Shetani hutushambulia mahali pale tulipo na udhaifu; lakini hatuna haja ya kushindwa.
Shambulio hilo laweza kuwa kali na la muda mrefu, lakini Mungu ameahidi kutupatia
msaada wake, na kwa nguvu zake sisi tunaweza kushinda.... Kanuni na ahadi za neno la
Mungu zitakupatia silaha zenye uwezo wa Mungu kumpinga adui huyo.... Shetani
atakanganyikiwa [atachanganyikiwa] na kushindwa anapokuta moyo wako
unajishughulisha na kweli ya Mungu. Pia mara kwa mara tunahitaji kuonekana kwenye
kiti kile cha neema. Maombi ya bidii na ya kudumu, yakiunganisha udhaifu wetu wa
kibinadamu na Uweza usio na kikomo wa Mungu, yatatupatia ushindi. ----- ST, Jan.19,
1882.
NI JUU YANGU MIMI KUCHAGUA Januari 9
Nanyi kama mkiona ni vibaya kumtumikia BWANA, chagueni hivi leo
mtakayemtumikia;... lakini mimi na nyumba yangu tutamtumikia BWANA. Yoshua
24:15.
Katika dunia yetu hii kuna makundi mawili. Moja ni la wale wanaomtazama Mwokozi
wao aliyesulibiwa na kufufuka. Jingine ni la wale wote ambao wamechagua
kutokuutazama msalaba, na kufuata maongozi ya vishawishi vyake Shetani. Kundi hili la
mwisho hujishughulisha sana na uwekaji wa vikwazo mbele ya watu wa Mungu, ili
kusababisha kuanguka kwao, na kuiacha njia ile ya utii na kuingia katika njia pana ya
uasi na mauti....Wengi huchagua dhambi kwa sababu Shetani anaionyesha kwa namna ambayo
inaonekana kuwa inapendeza kwa wale wasiojilinda na hila zake. Naye anaifanya kazi
yake kwa njia ya pekee kupitia kwa wanaume na wanawake wasiokuwa na maisha safi
ambao hujidai kuwa wao ni watoto wa Mungu. Kwa njia fulani au nyingineyo adui huyo
atatafuta namna ya kuwadanganya wote, yamkini hata walio wateule. Ni pale tu
tunapokuwa washiriki wa tabia ya uungu tunapoweza kuviepuka vishawishi viletavyo
uharibifu ambavyo huletwa kwetu na yule adui wa roho zetu.
Shetani anapotafuta namna ya kuvivunjilia mbali vizuizi vya roho zetu, kwa kutujaribu
ili tujifurahishe katika dhambi, yatupasa kuuhifadhi uhusiano wetu na Mungu kwa imani
iliyo hai, pamoja na kuwa na tumaini katika nguvu zake ziwezazo kutuwezesha sisi
kulishinda kila shambulio linalotusonga. Yatupasa kuukimbia uovu, na kutafuta haki,
upole, na utakatifu.
Wakati umefika kwa kila mmoja wetu kuamua ni upande wa nani tumesimama.
Mawakala wa Shetani watafanya kazi na kila moyo utakaokubali kushughulikiwa naye.
Walakini wapo pia wajumbe wa mbinguni wanaongojea kuwaletea mionzi inayong'aa ya
utukufu wa Mungu wale wote wanaopenda kumpokea. ----- MS 43, 1908.
Ni juu yetu sisi kuchagua iwapo tutahesabiwa pamoja na watumishi wake Kristo au
pamoja na watumishi wake Shetani. Kila siku tunaonyesha kwa tabia yetu tumechagua
kumtumikia nani....
Mpendwa msomaji kijana, umefanya uchaguzi gani? Kumbukumbu ya maisha yako ya
kila siku ikoje? ----- YI, Nov.21, 1883.
KIONGOZI SALAMA Januari 10
Basi Yesu akawaambia tena akasema, Mimi ndimi nuru ya ulimwengu, yeye anifuataye
hatakwenda gizani kamwe, bali atakuwa nuru ya uzima. Yohana 8:12.
Wote wanaosafiri katika njia ile iendayo mbinguni wanahitaji kuwa na kiongozi salama.
Hatupaswi kwenda kwa kufuata hekima ya kibinadamu. Ni haki yetu kuisikiliza sauti
yake Kristo ikisema nasi tunaposafiri katika safari ya maisha yetu, na maneno yake daima
ni maneno ya hekima....
Shetani anafanya kazi yake kwa juhudi kubwa sana ili kuzizingira na kuziangamiza roho
za wanadamu. Ameshuka chini kwa nguvu nyingi, akijua kwamba anao wakati mchache
tu wa kufanya kazi yake. Usalama wetu pekee ni kumfuata Kristo kwa karibu sana,
kutembea katika hekima yake, na kuitenda kweli yake. Hatuwezi kuutambua siku zote
kwa upesi utendaji wake Shetani; hatujui ni wapi anapotega mitego yake. Lakini Yesu
anazifahamu hila za chini chini za adui huyo, naye anaweza kuilinda miguu yetu ipate
kubaki katika njia zile zilizo salama.... "Mimi ndimi njia, na kweli, na uzima" (Yohana
14:6) Yesu asema. ----- Letter 204, 1907.Ingekuwa na faida gani njia ile ya moja kwa moja na ya hakika iendayo kule kwenye
utukufu, kama pasingekuwako na nuru yo yote ya ile kweli ambayo ingeiangazia njie ile,
ili wasafiri wapate kuitamani? Nuru inayoiangazia njia ile ingekuwa na faida gani kama
uzima usingekuwamo ndani ya watu wale wanaosafiri katika njia ile, yaani, katika safari
ile ya wasafiri kutoka duniani kwenda mbinguni? Wakiwa na usemi ule wa Kristo,
usemao, "Mimi ndimi njia, na kweli, na uzima," wale wote wanaomwamini Yesu,
Kiongozi wao, wanaweza kutembea kwa imani kwenda mbinguni, wakiwa na hakika
kwamba wamo katika njia ile iliyoelezwa katika Neno lake kuwa ndiyo njia. ----- Letter
63, 1893.
Wale waendao kwa utii wataijua kweli ilivyo.... Ili kuijua kweli, yatupasa kuwa tayari
kutii. Wale ambao mapenzi yao yako katika mambo ya dunia hii hawako tayari kuiacha
mipango yao kwa ajili ya mipango ya Kristo. Wanakwenda gizani, wasijue waendako.
Nuru ya thamani ya ile kweli huangaza ghafula juu ya njia ya kila mmoja anayeitafuta. --
--- MS 31, 1886.
WANA WA MFALME ALIYE MBINGUNI Januari 11
Tazameni, ni pendo la namna gani alilotupa Baba, kwamba tuitwe wana wa Mungu; na
ndivyo tulivyo. Kwa sababu hii ulimwengu haututambui, kwa kuwa haukumtambua
Yeye.
1 Yohana 3:1.
Hebu na asiwepo ye yote anayejisikia kwamba anashuka ngazi kwenda chini anapokuwa
mwana (mtoto) wa Mungu. Ni Mwana pekee wa Mungu aliyeshuka chini.... Akiacha
utukufu wake, ufalme wake, cheo chake cha juu, na kuuvika uungu wake na ubinadamu,
ili ubinadamu wake upate kuugusa ubinadamu wetu, na uungu wake upate kuushika
uungu, akaja hapa duniani, na kwa ajili yetu akafa kifo kile cha msalaba....
Kristo alitoa kafara kubwa mno. Alitoa uhai wake kwa ajili yetu. Alibeba juu ya moyo
wake wa uungu matokeo ya uvunjaji wetu wa Sheria ya Mungu. Aliiweka kando taji yake
ya kifalme, alikubali kushuka chini, hatua kwa hatua, na kuifikia hali ya wanadamu
walioanguka. Aliangikwa juu ya msalaba ule wa Kalvari, akafa badala yetu ili tupateuzima wa milele.... Je! linaonekana hilo kuwa ni jambo dogo kwake kuweza kuvumilia
yote hayo, ili sisi tupate kuitwa wana wa Mungu? Je! linaonekana kuwa ni jambo dogo
kwenu kuwa watu wa familia ya kifalme, wana wa Mfalme wa mbinguni, washiriki wa
urithi ule wa milele? ----- GCB, Aprili 23, 1901.
Huo ndio wema wake Mungu usiokuwa na kikomo kwamba kwa njia ya haki ya Yesu
Kristo hatuachilii tu [makosa yetu] bali hutusamehe na kutuhesabia haki, na kwa njia ya
haki yake Kristo anatuhesabia sisi haki hiyo, na kutuinua juu na kututukuza kwa
kutufanya sisi kuwa wana wake wa uchaguo [kupanga]. Tunakuwa watu wa familia ya
kifalme, yaani, wana wa Mfalme wa mbinguni. Anawainua juu wanaume na wanawake
kutoka katika hali yao duni na kuwatukuza katika haki hiyo.... Anawaita kuwa wao ni
johari zake, na hazina ya pekee kwake. Wao ni kumbukumbu ya neema na uweza wake,
na ukuu wake na utajiri katika utukufu wake. Kwa ajili hiyo, wao si mali yao wenyewe,
bali wamenunuliwa kwa thamani, na kwa njia ya kazi ile ya ajabu ya upatanisho wake
Kristo wameletwa karibu na kuwa na uhusiano wa karibu sana na Yesu Kristo. Wanaitwa
urithi wake, wana wake, viungo vya mwili wake, yaani, vya nyama na mifupa yake;
naam, wameunganishwa na Bwana kwa uhusiano wa ndani sana. ----- Letter 8, 1873.
KILA MTU MAANA YAKE MIMI Januari 12
Kwa maana jinsi hii Mungu aliupenda ulimwengu, hata akamtoa Mwanawe pekee, ili
kila mtu amwaminiye asipotee, bali awe na uzima wa milele. Yohana 3:16.
Yatupasa kutafakari juu ya upendo wa Yesu, utume wake na kazi yake kuhusiana na sisi
tukiwa kama mtu mmoja mmoja. Yatupasa kusema, Yesu alinipenda mimi hata akatoa
uhai wake kuniokoa. Baba ananipenda, "kwa maana jinsi hii Mungu aliupenda
ulimwengu, hata akamtoa Mwanawe pekee, ili kila mtu amwaminiye asipotee, bali awe
na uzima wa milele." Ni juu yetu sisi kujua kwa masharti gani Kristo anatuahidi kipawa
hicho cha uzima wa milele. Mimi najibu hivi, Kinategemea imani yetu. ----- ST, Aprili
24, 1893.
Kipawa hiki cha Mwana mpendwa wa Mungu huzifanya ahadi za Mungu kuwa zetu
kama dhamana. ----- MS 23, 1899.
Ni wangapi wawezao kusema, "Ananiokoa mimi"? Najua kwamba anataka mimi
niokoke. Ananiangalia mimi kama mtu wa thamani machoni pake, na kwa hiyo, najuakwamba mawazo yangu, maneno yangu, na matendo yangu, vyote hupita mbele yake na
kuchunguzwa. Kila kitu kilichonunuliwa kwa damu yake Kristo kina thamani machoni
pake Mungu. Kulingana na bei ile iliyolipwa kwa ukombozi wetu, sisi tuko chini ya
uwajibikaji wa kutoa mapenzi yetu yote kwake Kristo. Tunapaswa kumpa Mungu vyote
tulivyo navyo; na kwa kumpa Mungu vyote, je! yatupasa sisi kufikiri kwamba tunapata
hasara kubwa sana? ----- La, maana kwa kumpa talanta zetu, tunazizidisha mara mbili.
Kila kipaji alichotupa, kinaporudishwa kwake, kinapokea baraka yake, ili kiweze kuwa
na mvuto ulioongezeka katika kazi ya Mungu. Po pote pale ulipo, yakupasa kutambua
kwamba wewe u mali yake Kristo. ----- ST, Jan. 9, 1893.
Thamani ya kipawa hiki cha Kristo kwa ulimwengu huu ilizidi upeo wa mahesabu ya
kibinadamu, wala hakuna mamlaka yo yote ambayo ingeweza kushindana na Mungu kwa
kutoa kipawa ambacho kingekuwa na ulinganifu na hazina hii ya mbinguni iliyo ya
thamani kuliko zote. Ukuu wa kipawa hiki ulikuwa na lengo la kuwapatia wanadamu
jambo kuu la shukrani na sifa ambalo lingedumu kwa wakati wote na milele zote. Baada
ya kutoa kila kitu alichokuwa nacho ndani ya Kristo, Mungu anatoa madai yake ili apate
kupewa moyo, akili, roho, na nguvu za mwanadamu. Tukiiangalia hazina ambayo Mungu
ameitoa katika kipawa hiki chote na kikamilifu cha Kristo, tunaweza kushangilia,
tukisema: "Upendo ndio huu!" ----- YI, Des.l3, 1894.
MIKONDO YA NEEMA TELE Januari 13
Na Mungu aweza kuwajaza kila neema kwa wingi, ili ninyi, mkiwa na riziki za kila
namna siku zote, mpate kuzidi sana katika kila tendo jema." 2 Wakorintho 9:8.
Je! si jambo la ajabu kwamba sisi tunaweza kupokea mkondo wa neema tele kutoka kwa
Mungu, na kufanya kazi kwa mwafaka na Mungu? Mungu anataka nini kwetu sisi,
maskini, dhaifu, na wanyonge kama tulivyo hasa? Mungu anaweza kufanya nini nasi?
Kila kitu, iwapo tutakuwa tayari kuvisalimisha vyote. Mungu anampenda kila kijana.
Anajua yote kuhusu majaribu [maonjo] yako. Anajua kwamba unapaswa kupigana na
nguvu zile za giza, zinazojitahidi kuutawala moyo wa mwanadamu. ----- MS 8, 1899.
Kusudi la Mungu kwa watoto wake ni kwamba wanaume na wanawake wapate kukua
hata kufika kwenye cheo cha kimo cha utimilifu wa Kristo. Ili kuweza kufanya hivyo,
yatupasa kutumia vizuri kila nguvu ya akili, na roho na mwili wetu. Hatuwezi kupoteza
nguvu yo yote ya akili, wala ya mwili....Shetani ameyaita majeshi yake yote ya giza kuja kupigana na watakatifu. Hatuwezi kuwa
watu wasiojali kuhusiana na mashambulio yake. Anakuja kwa njia nyingi, nasi twapaswa
kuwa na utambuzi kamili wa kiroho, ili tupate kuweza kutambua anapotaka kuitawala
mioyo yetu. Mungu anawaita wale ambao juu yao nuru ya ile kweli inaangaza ili
wasimame katika jeshi lake. Anawataka waonyeshe uaminifu wao kwa kwenda katika
nuru ile aliyowapa. ----- MS 50, 1904.
Mungu anawataka ninyi kuzijua nafasi mnazozikalia kama wana na binti za yule Aliye
juu sana, yaani, watoto wa Mfalme wa mbinguni. Anawataka ninyi kuishi karibu sana
naye.... Jitengeni mbali na kila kitu cha kipuuzi. Msifikiri kwamba mnapaswa
kujifurahisha kwa anasa hii au anasa ile. Amueni kwamba mtakuwa upande wake Bwana.
Ushikilieni kwa nguvu mkono wa Mungu wenye uwezo.... Zitawaleni tabia zenu. Tieni
lijamu na hatamu. Semeni, "Nampenda Bwana, nami nimeamua kutumia kila chembe ya
akili yangu kwa kazi yake."...
Iwapo wewe utasimama chini ya bendera yenye damu ya Mfalme Imanueli, ukifanya
kazi yake kwa uaminifu, basi, huna haja kamwe ya kuanguka chini ya jaribu lo lote; kwa
maana Mmoja anasimama kando yako ambaye anaweza kukulinda usianguke. ----- MS 8,
1899.
TAZAMA UISHI Januari 14
Na kama vile Musa alivyomwinua yule nyoka jangwani, vivyo hivyo Mwana wa Adamu
hana budi kuinuliwa; ili kila mtu amwaminiye awe na uzima wa milele katika yeye.
Yohana 3:14,15.
Fundisho lile lile ambalo Kristo alimwagiza Musa kuwapa wana wa Israeli jangwani
linawahusu watu wote wanaoteseka chini ya pigo la dhambi. Kutoka katika wingu lile
kama wimbi Kristo alizungumza na Musa, akamwambia atengeneze nyoka ya shaba na
kuiweka juu ya mti, na kisha kuwaamuru wote walioumwa na nyoka zile za moto
kutazama na kuishi. Vipi iwapo, badala ya kutazama kama vile alivyowaagiza Kristo,
wangesema hivi, "Mimi sisadiki hata kidogo kwamba kutazama huku kutaniletea jema lo
lote. Nina maumivu makali sana kutokana na kuumwa na nyoka huyu mwenye sumu.Utii ndilo lengo lililotakiwa kufikiwa, bila kusimama na kuuliza sababu au sayansi ya
kitendo kama hicho. Neno la Kristo lilikuwa hivi, "Tazama, uishi."...
Tunataka kuwa na maoni dhahiri juu ya umuhimu wa Yesu kwetu sisi. Tunataka kuwa
na picha dhahiri kuhusu ushindi ule uliopatikana kwa ajili yetu. Aliziharibu falme na
nguvu na kuzidhihirisha mbele ya watu. Alivivunja vifungo vya kaburi na kutoka nje
kuutwaa uhai wake tena ambao alikuwa ameutoa kwa ajili yetu. Alipaa juu, akiwa
ameteka mateka na kuwagawia wanadamu vipawa. Mateso yote hayo aliyastahimili kwa
ajili yetu sisi.... Yeye atakuwa Msaidizi wetu, naye atakuwa ngome yetu wakati wa taabu.
Angepaswa kuonekana katika maisha yetu ya Kikristo kuwa anatutosha kabisa, yaani,
Mwokozi wetu kwa wakati huu wa sasa.
Tazama tu na kuishi. Tunamvunjia Mungu heshima tunaposhindwa kusonga mbele
kutoka chumba cha chini cha giza la mashaka kwenda juu kwenye chumba cha tumaini
na imani. Nuru inapong'aa kwa ukali wake wote, hebu na tumshike Yesu Kristo kwa
mkono wenye nguvu wa imani. Usiendelee tena kuyakuza mashaka yako kwa kuongelea
juu yake na kuyaingiza katika mioyo ya wengine, na kwa njia hiyo kuwa wakala wa
Shetani kwa kuzipandikiza mbegu hizo za mashaka. Ongea juu ya imani, ishi kwa imani,
jizoeze kuwa na upendo kwa Mungu; toa ushahidi wako kwa ulimwengu kuhusu yale
yote ambayo Kristo amekutendea . Lihimidi jina lake takatifu. Simulia habari za fadhili
zake; zungumza juu ya rehema zake, na kusimulia juu ya uweza wake. ----- MS 42, 1890.
KIPIMO CHA JUU SANA Januari 15
Mwivi haji ila aibe na kuchinja na kuharibu; mimi nalikuja ili wawe na uzima, kisha
wawe nao tele. Yohana 10:10.
Ni ukamilifu ulioje ulioelezwa katika maneno haya, "Mimi ndimi nuru ya ulimwengu."
Yohana 8:12. "Mimi ndimi chakula cha [mkate wa] uzima." Yohana 6:35. "Mimi ndimi
njia, na kweli, na uzima." Yohana 14:6. "Mimi ndimi Mchungaji Mwema." Yohana
10:14. "Mimi nalikuja ili wawe na uzima, kisha wawe nao tele." Yohana 10:10. Uzima
huu ndio tunaopaswa kuwa nao, tena yatupasa kuwa nao TELE. Mungu atauvuvia uhaihuu ndani ya kila mtu anayeifia nafsi yake na kuwa hai kwa Kristo. Lakini kujikana nafsi
kabisa kunatakiwa. Jambo hilo lisipotokea, basi, tutakuwa tunachukua pamoja nasi uovu
ambao unaathiri furaha yetu. Lakini nafsi inaposulibiwa, hapo ndipo Kristo anapoishi
ndani yetu, na uwezo wa Roho unaambatana na juhudi zetu.
Natamani tungekuwa kama vile Mungu anavyotaka tuwe ----- nuru kamili katika Bwana
wetu. Tunahitaji kukifikia kipimo cha juu zaidi, lakini hatuwezi kamwe kufanya hivyo
mpaka nafsi yetu iwe imewekwa juu ya madhabahu, yaani, mpaka tuwe tumemruhusu
Roho Mtakatifu kututawala, kutubadilisha tabia zetu na kututengeneza upya kwa mfano
wake Mungu....
Kila siku yatupasa kujitoa wakf ili kumtumikia Mungu. Yatupasa kuja kwa Mungu kwa
imani.... Twahitaji kujinyenyekeza wenyewe mbele zake Mungu. Ni nafsi ambayo
tunapaswa kupambana nayo kwanza. Moyo wako uukosoe kwa karibu sana. Uchunguze
kuona ni kitu gani hasa kinachomzuia Roho wa Mungu asiweze kufanya kazi yake kwa
uhuru. Yatupasa kumpokea Roho Mtakatifu. Hapo ndipo tutakapokuwa na nguvu ya
kushinda pamoja na Mungu.
Kule kuikiri kweli tu hakutoshi. Kila siku yatupasa kuishi kulingana na kweli hiyo.
Yatupasa kujifungia wenyewe ndani pamoja na Mungu, tukisalimisha mambo yetu yote
kwake. Kule kuzisikiliza tu kweli zile kuu na tukufu za Neno hakutoshi. Yatupasa
kujiuliza sisi wenyewe swali hili, Je! Kristo anaishi ndani ya moyo wangu kwa imani?
Yeye peke yake ndiye awezaye kutuonyesha shida yetu na kutufunulia sisi ukuu na uzuri
wa kweli yake. Mahali pale pa madhabahu ya kujikana nafsi ----- mahali ambapo
pamechaguliwa pa kukutana Mungu na mwanadamu ----- hapo ndipo tunapopokea toka
mkononi mwa Mungu ile tochi ya mbinguni inayouchunguza moyo [Roho Mtakatifu],
ikifunua haja yake kuu ya kukaa humo Kristo. ----- MS 9, 1899.
KUWA HODARI KATIKA BWANA Januari 16
BWANA ni nuru yangu na wokovu wangu, Nimwogope nani? BWANA ni ngome ya
uzima wangu, Nimhofu nani? Jeshi lijapojipanga kupigana nami, Moyo wangu
hautaogopa. Vita vijaponitokea, Hata hapo nitatumaini. Zaburi 27:1,3.
Tunapita katika nchi ya adui. Adui wako kila upande kuzuia kusonga mbele kwetu.
Wanamchukia Mungu pamoja na wale wote wanaomfuata na kuchukua jina lake. Lakiniwale walio maadui zetu ni maadui za Bwana wetu, na ijapokuwa wao wanazo nguvu na
ni werevu, hata hivyo yule Kiongozi [Kamanda] Mkuu wa Wokovu wetu anayetuongoza
anaweza kuwashinda kabisa. Kama vile jua liyatawanyavyo mawingu katika njia yake,
hivyo ndivyo lile Jua la Haki [Kristo] litakavyoweza kuviondoa vipingamizi vyote
vinavyokwamisha maendeleo yetu. Twaweza kuzichangamsha roho zetu kwa
kuyaangalia mambo yale yasiyoonekana ambayo yatatutia moyo na kutuchangamsha
katika safari yetu....
Iwapo tunamshikilia kwa nguvu kwa imani iliyo hai, tukisema pamoja na Yakobo,
"Sikuachi" (Mwanzo 32:26); iwapo tutamsihi, tukisema, "Usinitenge na uso wako, Wala
Roho [w]ako Mtakatifu usiniondolee," (Zaburi 51:11), basi, ahadi kwetu ni hii,
"Sitakupungukia kabisa, wala sitakuacha kabisa."...
Tumesoma kisa cha mwana wa mfalme aliyekuwa na tabia nzuri ambaye siku zote
alitembea na picha ya baba yake aliyoiweka karibu na moyo wake; na wakati wa matukio
muhimu, ilipokuwapo hatari ya kumsahau, alichukua picha hiyo na kuiangalia, huku
akisema, "Hebu na nisitende jambo lo lote lisilofaa kulingana na tabia bora sana ya
baba." Sisi kama Wakristo, Mungu ana madai juu yetu ambayo kamwe, kamwe
tusingeweza kuyasahau hata kwa dakika moja tu; na kwa vile sisi tu watoto wake wa
uchaguo [kupanga], tungekuwa waangalifu kutofanya kitu cho chote ambacho
kitadhalilisha au kushusha hadhi ya mwito wetu mtakatifu, kwa kuwa tumo miongoni
mwa familia ile ya kifalme. Mungu ametufanya sisi kama vyombo vyake vya heshima,
tayari kwa kila kazi njema. "Watu wale niliojiumbia nafsi yangu, ili wazitangaze sifa
zangu." Isaya 43:21. Watu wa Mungu wanaitwa kilemba cha kifalme, yaani, taji. Shetani
kwa hamu kubwa angetaka kuikamata hazina yake Bwana, lakini Mungu ameihifadhi
salama hata Shetani hawezi kuipata. "Nawe utakuwa taji ya uzuri katika mkono wa
BWANA, na kilemba cha kifalme mkononi mwa Mungu wako." Isaya 62:3. Sisi tu
salama, salama kabisa mbali na hila za yule adui tunapokuwa na imani isiyotikisika kwa
Mungu. ----- Letter 8, 1873.
MALAIKA WA KUTULINDA Januari 17
Kwa kuwa atakuagizia malaika zake wakulinde katika njia zako zote. Zaburi 91:11.
Laiti kama sisi sote tungaliweza kujua jinsi mbingu ilivyo karibu sana na dunia! Watoto
waliozaliwa humu duniani hawajui, kwamba wanao malaika wa nuru kama wenzi wao;kwa maana wajumbe hao kutoka mbinguni wametumwa kuwahudumu wale
watakaourithi wokovu. Shahidi huyo wa kimya anamlinda kila mtu anayeishi, akitafuta
kumpata na kumleta kwa Kristo. Malaika hawamwachi kamwe yule anayejaribiwa kuwa
mateka wa adui yule anayetaka kuziangamiza roho za watu endapo angeruhusiwa
kufanya hivyo. Maadam tumaini linaendelea kuwapo, mpaka hapo watakapompinga
Roho Mtakatifu kwa maangamizi yao ya milele, wanadamu hulindwa na viumbe hao
wenye hekima watokao mbinguni. ----- MS 32a, 1894.
Laiti kama wote wangeweza kumtazama Mwokozi wetu wa thamani kama alivyo hasa,
yaani, kama MWOKOZI. Hebu mkono wake na ulivute kando pazia lile linalouficha
utukufu wake hata tusiweze kuuona. Linamwonyesha akiwa mahali pake pa juu na
patakatifu. Tunaona nini? Mwokozi wetu, si katika hali ya ukimya na kutoshughulika.
Amezungukwa na wenye hekima wale wa mbinguni, makerubi, na maserafi, elfu kumi
mara elfu kumi ya malaika. Viumbe hivyo vyote vya mbinguni wanalo kusudi moja tu
juu ya yote, ambalo wana hamu nalo sana ----- kanisa lake katika ulimwengu huu wa
uharibifu.... Wanamtumikia Kristo chini ya agizo lake la kuwaokoa kabisa wale wote
wanaomtazama Yeye na kumwamini. ----- 7 BC 967,968
Malaika wale wa mbinguni wametumwa kuwachunga kondoo wa malisho yake Kristo.
Wakati ambapo Shetani na mitego yake idanganyayo angeweza kuwadanganya yamkini
hata walio wateule, malaika hao wanatoa mivuto ambayo inaweza kuwaokoa watu hao
wanaojaribiwa endapo watalitilia maanani Neno la Bwana, wakitambua hatari yao, na
kusema, "Hapana, sitaki kuingia katika mpango huo wa hila ulioandaliwa na Shetani.
Ninaye Kaka yangu Mkubwa kwenye kiti kile cha enzi mbinguni, ambaye amenionyesha
kuwa ananipenda, nami sitaki kuuhuzunisha moyo wake wa upendo." ----- 7BC 922..
Kuishi katikati ya nguvu hizi zinazopingana, kwa kutumia imani na maombi, tunaweza
kuiwata waje upande wetu halaiki ya malaika kutoka mbinguni ili waandamane nasi, hao
watatulinda sisi tusiweze kuathirika na kila aina ya mvuto unaotushawishi kufanya
mabaya. ----- Letter 258, 1907.
AHADI KWA WALE WANAOTII Januari 18
Sasa basi ikiwa mtaitii sauti yangu kweli kweli, na kulishika agano langu, hapo ndipo
mtakapokuwa tunu kwangu kuliko makabila yote ya watu; maana dunia yote pia ni mali
yangu. Kutoka 19:5.Ahadi hii haikutolewa kwa Israeli peke yao bali kwa wote wanaolitii Neno la Mungu.
Wale wanaoishi katikati ya hatari za siku za mwisho wanaweza kutambua kwamba kama
vile kweli ilivyowaunganisha na Mwokozi wao mwanzoni mwa maisha yao, ndivyo Yeye
aliye mwasisi [mwanzilishi] na mtimizaji wa imani yao atakavyoitimiza kazi ile
aliyoianza kwa ajili yao. Mungu wetu ni mwaminifu, ambaye ametuita katika ushirika wa
Mwana Wake. Wanaume na wanawake wanaposhirikiana na Mungu katika kuifanya kazi
ile aliyowapa, wanasonga mbele toka katika nguvu ya awali kwenda katika nguvu nyingi
zaidi. Wanapojizoeza kuwa na imani ya kawaida, wakiamini kwamba siku kwa siku
Mungu hatashindwa kuwaimarisha katika Kristo, Mungu anasema kwao kama
alivyosema kwa Israeli ya zamani: "Kwa maana wewe u taifa takatifu kwa BWANA,
Mungu wako; BWANA Mungu wako, amekuchagua kuwa watu wake hasa, zaidi ya
mataifa yote walioko juu ya uso wa nchi." Kumbukumbu la Torati 7:6.
Hivyo ndivyo Mungu anavyoweza na anavyotaka kuwaongoza wote wanaotaka
kuongozwa. Anatamani kumfundisha kila mmoja fundisho lile la kumtegemea Yeye
daima, imani ile isiyotikisika na utii ule usiouliza maswali. Anamwambia kila mmoja,
Mimi ni Bwana Mungu wako. Tembea pamoja nami, nitaijaza njia yako na nuru....
Lakini Mungu anataka utii kwa amri zake zote. Njia ya pekee ambayo kwayo
inawezekana kwa wanadamu kuwa na furaha ni kwa kutoa utii wao kwa Sheria za ufalme
wake Mungu [Amri Kumi].
Uzima, pamoja na haki zake na vipawa vyake, ni karama ya Mungu. Hebu na tukumbuke
ya kwamba vyote tulivyo navyo vinatoka kwa Mungu, navyo vinapaswa kutolewa wakf
kwake kwa ukamilifu na kwa hiari. Paulo anasema hivi kwa mkazo, "Nayahesabu
mambo yote kuwa hasara kwa ajili ya uzuri usio na kiasi wa kumjua Kristo Yesu, Bwana
wangu; ambaye kwa ajili yake nimepata hasara ya mambo yote nikiyahesabu kuwa kama
mavi ili nipate Kristo; tena nionekane katika Yeye, nisiwe na haki yangu mwenyewe...
bali haki ile itokayo kwa Mungu, kwa imani." Wafilipi 3:8,9. Kuyaachilia mbali mawazo
yetu, yaani, mapenzi yetu, ni muhimu tukitaka kuwa na umoja na Kristo katika Mungu.
Vyote tulivyo navyo na jinsi tulivyo kimaumbile ni lazima kuviweka miguuni pake
Kristo. ----- MS 17, 1899
USALAMA WETU PEKEE Januari 19Kuwaogopa wanadamu huleta mtego; Bali amtumainiye BWANA atakuwa salama.
Mithali 29:25.
Wewe u salama tu kwa kadiri unavyomtegemea Mungu. Tunaye adui aliye macho sana
wa kupigana naye.... Yeye [Kristo] aliona kwamba isingaliwezekana kwa mwanadamu
kumshinda adui huyo mwenye nguvu kwa kutegemea nguvu zake mwenyewe, kwa hiyo,
alikuja katika mwili kutoka kwenye majumba ya kifalme kule mbinguni na kustahimili
kwa ajili ya mwanadamu jaribio lile lile aliloshindwa Adamu kustahimili.... Kristo
alimshinda Shetani, akifanya uwezekano kwa mwanadamu uwepo wa kushinda kwa nafsi
yake mwenyewe katika jina lake Kristo. Walakini ushindi huo unaweza kupatikana tu
katika jina lake Kristo, kwa njia ya neema yake. Unapolemewa na mizigo mizito,
unaposongwa sana na majaribu, hisia na tamaa za moyo wako usioongoka zinapopiga
makelele kutaka kushinda, maombi yako ya bidii, yaani, maombi yasiyokoma, katika jina
lake Kristo humleta Yesu upande wako kama msaidizi wako, na kwa njia ya jina lake
unapata ushindi, na Shetani anashindwa kabisa.....
Nawashihi sana mpate kumtegemea Mungu. "Mpingeni Shetani, naye atawakimbia.
Mkaribieni Mungu, naye atawakaribia ninyi." Yakobo 4:7,8. Maisha ya Kikristo ni
maisha ya mapambano, kujikana nafsi, na ushindi. Ni vita inayoendelea daima na
kusonga mbele. Kila tendo la utii kwa Kristo, kila ushindi uliopatikana dhidi ya nafsi, ni
hatua moja ya kusonga mbele kwenda kwenye utukufu na ushindi ule wa mwisho.
Mchukue Kristo awe Kiongozi wako, naye atakuongoza kwa salama katika njia yako.
Njia yako huenda ikawa inaparuza na kuwa na miiba, na miinuko yake huenda ni mikali
kupanda juu, ikihitaji kazi ya jasho ifanyike. Unaweza kulazimika kusonga mbele ukiwa
umechoka sana, yaani, ukiwa unatamani sana kupumzika. Unaweza kulazimika
kuendelea kupigana vita unapojisikia umeishiwa nguvu, na kuendelea kutumaini
unapokata tamaa, lakini, pamoja na Kristo kama Kiongozi wako, huwezi kuipoteza njia
ile ya uzima wa milele. Huwezi kushindwa kukifikia kiti kile cha enzi kando ya Kiongozi
wako huyo, ambaye nyayo zake mwenyewe ziliipitia njia hiyo inayoparuza ambayo i
mbele yako, akiisawazisha njia hiyo kwa ajili ya miguu yako. Endapo wewe utakifuata
kiburi chako na tamaa ya kutaka makuu kwa ajili ya nafsi yako wewe tu, basi, mwanzoni
utaona mambo hayo yakikupendeza, lakini mwisho wake ni uchungu na huzuni.
Unaweza kufuata uchoyo, ambao utaweza kukupa tumaini kubwa sana lakini
utayasumisha na kuyafanya maisha yako kuwa machungu sana. Kumfuata Kristo ni
salama. Hataziruhusu nguvu zile za giza kuudhuru hata unywele mmoja wa kichwa
chako. Mtumainie Mkombozi wako, nawe utakuwa salama. ----- Letter 1b, 1873.
NURU AU KIVULI? Januari 20 Ole wao wasemao kwamba uovu ni wema, na kwamba wema ni uovu; watiao giza
badala ya nuru, na nuru badala ya giza; watiao uchungu badala ya utamu, na utamu
badala ya uchungu! Isaya 5:20.
Mungu ni nuru, na ndani yake hamna giza hata kidogo. Kama pasingalikuwapo na nuru,
basi, pasingekuwapo na kivuli cho chote. Lakini wakati kivuli huja kutokana na jua,
hakisababishwi na jua. Ni kizuizi fulani kinachofanya kivuli. Kwa hiyo giza halitokani na
Mungu, bali ni matokeo ya kitu fulani kilichoingia kati ya mtu na Mungu.... Kutoijali
nuru ambayo Mungu ametoa kunaleta matokeo ya hakika. Kunaleta kivuli, yaani, giza
ambalo ni nene zaidi kwa sababu ya nuru ile iliyokwisha kutumwa.... Endapo mtu
anajiondoa mwenyewe kutoka katika nuru na ushuhuda, na kuanguka chini ya hila za
Shetani zenye ushawishi mwingi, basi, yeye mwenyewe anajiwekea pazia la kutoamini
kumzunguka pande zote, hata nuru isiweze kutofautishwa na giza. Nuru zaidi pamoja na
ushahidi kwake vingekuwa havieleweki. Kadiri ushahidi unavyozidi kuwa mwingi,
ndivyo hali ile ya kutojali inavyozidi kuwa kubwa. Jambo hilo litamwongoza mtu huyo
aliyedanganyika kusema kwamba giza ni nuru, na kweli ni uongo. ----- MS 56, 1898.
Shetani anafanya kazi yake daima akiwaongoza watu kuikataa nuru. Ni hatua moja tu
kutoka kwenye njia ile nyofu kwenda kwenye njia ile iliyochepuka kando yake, ambamo
Shetani ndiye kiongozi, na ambamo nuru ni giza tupu, na giza ni nuru.... Ni jambo la
hatari kuufungua moyo usiweze kuamini, kwa maana kitendo hicho kinamfukuzilia mbali
Roho wa Mungu kutoka moyoni, na mashauri ya Shetani ndiyo yanayoingia humo.... Ni
lazima sisi... tuepukane na kuingiza humo [moyoni] mashaka na kutokuamini. ----- Letter
104, 1894.
"Cho chote apandacho mtu, ndicho atakachovuna." Wagalatia 6:7. Mungu
hamwangamizi mtu ye yote. Kila mtu atakayeangamizwa atakuwa amejiangamiza
mwenyewe. Mtu anapoyazimisha maonyo ya dhamiri yake, anapanda mbegu za
kutokuamini, nazo hutoa mavuno ya hakika....
"Hawakukubali mashauri yangu, wakayadharau maonyo yangu yote. Kwa hiyo watakula
matunda ya njia yao wenyewe. Maana kurudi nyuma kwao wajinga kutawaua, na
kufanikiwa kwao wapumbavu kutawaangamiza. Bali kila anisikilizaye atakaa salama,
naye atatulia bila kuogopa mabaya." Mithali 1:30-33. ----- MS 56, 1898.TUMAINI KWA WASIO NA TUMAINI Januari 21
Mtu mbaya na aache njia yake, na mtu asiye na haki aache mawazo yake; Na amrudie
BWANA, Naye atamrehemu; Na arejee kwa Mungu wetu, Naye atamsamehe kabisa.
Maana mawazo yangu si mawazo yenu, wala njia zenu si njia zangu; asema BWANA.
Isaya 55:7,8.
Ni mawazo yako yasemayo kwamba makosa yako na maasi yako yamekuwa mengi mno
kiasi kwamba Bwana hawezi kuyastahi maombi yako, wala kukubariki na kukuokoa
wewe.... Kadiri unavyozidi kumkaribia Yesu, ndivyo kadiri utakavyojiona kuwa una
kasoro nyingi sana; maana kuona kwako kutakuwa safi zaidi, na upungufu wako
utaonekana kwa mapana yake na kwa dhahiri kuwa uko tofauti na tabia yake takatifu.
Lakini, basi, usikate tamaa. Huo ni ushahidi kwamba madanganyo ya Shetani
yamepoteza nguvu yake; kwamba mvuto ule unaohuisha wa Roho wa Mungu unakutia
nguvu, na kule kutojali kwako na kutojihusisha kunatoweka.
Upendo wenye kina kirefu wa Yesu hauwezi kukaa ndani ya moyo ambao hauoni wala
hautambui uovu wake. Moyo ule uliobadilishwa kwa neema utapendezwa na tabia Yake
ya Uungu; lakini endapo hatuoni ulemavu wetu wa kiroho, basi, ni ushahidi usiokosewa
unaoonyesha kwamba hatujauona uzuri wake Kristo usio na kiasi. Kadiri tusivyozidi
kuona cha kujisifia cho chote ndani yetu, ndivyo kadiri tutakavyoona kitu cha kusifu
katika utakatifu ule usio na kikomo na uzuri wa Mwokozi wetu. Kuona uovu wetu
wenyewe kunatufanya tukimbilie kwake Yeye awezaye kutusamehe.
Mungu hashughuliki nasi kama wanadamu wanaokufa wanavyoshughulikiana wao kwa
wao. Mawazo yake ni mawazo ya rehema, upendo, na huruma nyingi sana. "Naye
atamsamehe kabisa." Yeye asema hivi, "Nimeyafuta makosa yako kama wingu zito."...
Tazama juu, wewe unayepata maonjo hayo, unayejaribiwa, na kukata tamaa, tazama
juu.... Daima ni salama kutazama juu; ni kifo kutazama chini. Ukitazama chini, dunia
inalewa-lewa [kama mlevi] na kuwaya-waya [kama machela] chini yako; hakuna uhakika
wo wote. Lakini mbingu iliyo juu yako ni shwari na imara, na huko kuna msaada wa
Mungu kwa kila anayekwea. Mkono wa Mungu unanyoshwa kupitia katika buruji zile za
mbinguni ili kuushika mkono wako kwa nguvu. Msaidizi wako mwenye uweza yu karibu
kuwabariki, kuwainua juu, na kuwatia moyo wenye dhambi sugu, yaani, walio na dhambi
nyingi sana, iwapo watatazama juu kwake kwa imani. Lakini ni lazima kwa mwenye
dhambi kutazama juu. ----- RH, Feb.17,1885.HATUJASAHAULIWA KAMWE KATIKA MOYO WA MUNGU Januari 22
Huku mkimtwika yeye fadhaa zenu zote, kwa maana yeye hujishughulisha sana na
mambo yenu. l Petro 5:7.
Ili kuyapanua mawazo yetu juu ya fadhili zake Mungu, Kristo anatualika sisi tupate
kuziangalia kazi za mikono yake. "Waangalieni ndege wa angani," asema, "hawapandi,
wala hawavuni, wala hawakusanyi ghalani; na Baba yenu wa mbinguni huwalisha hao.
Ninyi je! si bora kupita hao?" Mathayo 6:26.
Ingawa wanaume na wanawake wametenda dhambi nyingi sana, hawaachwi. Mkono ule
unaoishikilia dunia hii, unamshikilia na kumtia nguvu mtoto wake aliye dhaifu kuliko
wote. Msanii yule Mkuu, ambaye ustadi wake umepita upeo wa ustadi wa mwanadamu
ye yote, ambaye analipa ua la kondeni rangi yake nzuri, anamjali hata shomoro. Hakuna
hata mmoja anayeanguka chini pasipo yeye kujua.
Iwapo ua linavikwa uzuri unaopita fahari yote ya Sulemani, je! ni thamani gani
anayoiweka juu ya urithi [watu] wake alioununua? Kristo anatuonyesha jinsi
anavyovishughulikia vitu vile vinavyonyauka kwa siku moja tu, ili kutuonyesha sisi jinsi
Mungu alivyo na upendo mwingi kwa viumbe vyake alivyoviumba kwa sura yake....
Anatufunulia mbele yetu gombo la fadhili za Mungu kwetu sisi, na kutuamuru kutazama
majina yetu yaliyoandikwa humo. Katika gombo hilo kila mwanadamu amepewa ukurasa
wake, juu yake yameandikwa matukio yote ya historia ya maisha yake. Na katika moyo
wake Mungu majina hayo hayasahauliki hata kwa dakika moja. Ni wa ajabu kweli
upendo wake Mungu na utunzaji wake kwa viumbe vyake alivyoviumba....
Ili apate kuziokoa roho za wanadamu wanaoangamia, alitayarisha kipawa cha hali ya juu
mno hata hapawezi kusemwa ya kwamba Mungu angekuwa amekifanya kipawa chake,
yaani, zawadi yake kwa familia hii ya kibinadamu, kuwa kikubwa zaidi [ya vile kilivyo].
Kipawa chake kinayapita mahesabu yote [ya kibinadamu]. Hayo yote Mungu alifanya ili
mwanadamu apate kujazwa kabisa na upendo na fadhili za Mungu. Kwa njia hiyo
angewathibitishia wenye dhambi kwamba dhambi za kiwango kikubwa mno zinaweza
kusamehewa iwapo yule mwenye dhambi anajitahidi kutafuta msamaha, akijisalimisha
mwenyewe, yaani, mwili wake, roho yake, na nafsi yake, ili apate kubadilishwa kwa
neema yake Mungu na kufananishwa naye.
Kwa ajili yake mwanadamu Mungu amemwaga chini hazina yote ya mbinguni, na
matarajio yake yeye ni kwamba anategemea na kutudai sisi tumpe mapenzi yetu yote. ----
- Letter 79, 1900.KUFANANA NA KRISTO Januari 23
Kwa maana mlikufa, na uhai wenu umefichwa pamoja na Kristo katika Mungu.
Wakolosai 3:3.
Yesu anataka wewe uwe na furaha, lakini huwezi kuwa na furaha kwa kufuata njia yako
mwenyewe wala kwa kufuata hisia za moyoni mwako.... Mawazo yetu, tabia zetu za
ajabu ajabu, vyote hivyo vina asili ya kibinadamu.kabisa, wala tusivibembeleze, wala
tusiviendekeze. Nafsi inapaswa kusulibishwa, sio mara kwa mara bali kila siku, na
mambo yale yanayohusu mwili, akili, na roho ni sharti yatawaliwe na mapenzi ya
Mungu. Utukufu wake Mungu, ukamilifu wa tabia ya Kikristo, linapaswa kuwa ndilo
lengo, yaani, kusudi, la maisha yetu. Wafuasi wake Kristo hawana budi kumwiga Kristo
katika tabia yake.... KUFANANA NA KRISTO hilo ndilo neno la kututia hamasa
[nguvu], sio kufanana na baba yako, wala mama yako, bali kufanana na Yesu Kristo -----
ufichwe ndani ya Kristo, uvikwe haki ya Kristo, na kujazwa na Roho wa Kristo. Tabia
zetu zote za ajabu tulizopewa kama urithi [kutoka kwa wazazi wetu] au zile tulizojizoeza
wenyewe kwa kujiendekeza au kwa njia ya elimu potofu, ni lazima tuzishinde zote kabisa
kabisa, na kuzipinga kwa vyo vyote vile. Kupenda kujitukuza na kuwa na kiburi katika
maoni yetu, vyote ni lazima vitolewe kafara [viachwe]....
Yesu ni msaidizi wetu; ndani yake na kupitia kwake inatupasa kushinda.... Neema yake
Kristo inakungojea wewe upate kuiomba. Atakupa neema na nguvu yake kwa kadiri ya
mahitaji yako kama utamwomba yeye.... Dini yake Kristo itaifunga na kuizuia kila tamaa
chafu, itatutia nguvu, itatuadibisha [ili tupate kujitawala], na kutupa bidii ya kufanya
kazi, hata katika mambo yale yahusuyo kazi za nyumbani, na kazi za maisha ya kawaida,
ikituongoza kujifunza matumizi mazuri ya vitu [kubana matumizi], busara, na kujikana
nafsi, na hata kuweza kustahimili ufukara pasipo manung'uniko yo yote. Roho wa Kristo
akiwa moyoni atajidhihirisha katika tabia, atakuza tabia zile zilizo nzuri pamoja na
kukuza uwezo. "Neema yangu yakutosha" (2 Kor. l2:9) asema Kristo. ----- Letter 25,
1882. Mungu amefanya mengi sana ili iwezekane kwetu kuwa huru ndani ya Kristo, huru
mbali na utumwa wa tabia zetu mbaya na mielekeo yetu mibaya. Enyi vijana wapendwa,
rafiki, je! hamwezi kujitahidi kuwa huru ndani ya Kristo? Mnasonda vidole vyenu kwa
huyu na kwa yule ambaye anajidai kuwa Mkristo, na kusema, Hatuna imani nao. Kama
maisha yao ni kielelezo cha Ukristo, basi, sisi hatutaki ukristo kama huo. Msiwaangalie
wale wanaowazunguka. Badala yake tazameni kielelezo kile kilicho kikamilifu, yaani,mwanadamu Kristo Yesu. Kumtazama, mtabadilishwa na kufanana naye. ----- YI, Agosti
21, 1902.
KAA KARIBU SANA NA YESU Januari 24
Walakini mimi ni pamoja nawe daima, Umenishika mkono wa kuume. Utaniongoza kwa
shauri lako, Na baadaye utanikaribisha kwa utukufu. Zaburi 73:23,24.
Kabla hujaanza kufanya kazi yo yote yenye maana, kumbuka kwamba Yesu ni mshauri
wako, na ya kwamba ni haki yako kumtwika mizigo yako yote.... Usimwache Yesu
nyuma yako na kutolitaja jina lake kamwe, bila hata kujaribu kuyageuza mawazo ya
rafiki zako kwake yeye aliye kando yako kama mshauri wako. Je, rafiki zako
wasingekuona wewe kuwa huna heshima kama wangekuwa kando yako, na wewe
usizungumze nao kabisa au kuongea juu yao?...
Wengi hulalamika kwamba Yesu anaonekana kana kwamba yuko mbali sana nao. Ni
nani aliyemweka mbali sana? Si njia zako za maisha zilizokutenga mbali na Yesu? Yeye
hajakuacha, bali ni wewe uliyemwacha na kuambatana na wapenzi wengine.... Ni wakati
ule unapotanga mbali naye, na kushawishika na sauti za yule mshawishi, na kuyakaza
mapenzi yako juu ya kitu fulani kidogo, unapokuwa katika hatari ya kupoteza amani na
matumaini na imani yako kwa Mungu.... Hapo ndipo Shetani anakuletea wazo la kusema
kwamba Yesu amekuacha; lakini, je! si wewe uliyemwacha Yesu?... Hatuthubutu kuacha
jina lake kufifia kinywani mwetu, wala upendo wake na kumbukumbu yake kuiacha ife
mioyoni mwetu. "Naam," yule mwalimu mshika kanuni asema kwa sauti yenye ubaridi,
"huko ni kumfanya Kristo kuwa kama mwanadamu kabisa jambo ambalo linavuka
mpaka"; lakini Neno la Mungu linaturuhusu kabisa kuwa na mawazo hayo. Ni ukosefu
wa kuwa na mawazo hayo ya busara na dhahiri juu ya Kristo, unaowazuia wengi
kutokuwa na maisha halisi katika kumjua Bwana na Mwokozi wetu Yesu Kristo. Hii
ndiyo sababu inayowafanya wengi kuogopa na kuwa na mashaka na kuomboleza.
Mawazo yao juu ya Kristo na mpango wake wa wokovu si dhahiri, yanaufanya moyo
kuwa mzito, tena yana utata. Endapo, kama Daudi, wangekuwa wamemweka Bwana
mbele yao daima,... miguu yao ingekuwa imejikita juu ya mwamba imara. Mtazame Yesu
aliyesulibiwa kwa ajili yako. Mtazame uone jinsi alivyohuzunishwa kwa dhambi zako; na
ukiwa katika maombi, tubu, na kwa dhati tamani kumwona Yeye kama Mkombozi wako
anayesamehe dhambi, aliye tayari kukubariki, na kukusikiliza unavyomkiri Yeye. Kaa
karibu sana kando yake. ----- YI, Julai 19, 1894. BIBLIA NI MWANGA WA NJIA YANGU Januari 25
Neno lako ni taa ya miguu yangu, Na mwanga wa njia yangu. Zaburi 119:105.
"Ni kitabu cha ajabu mno!
Mshumaa ung'arao wa Bwana! Nyota ya milele! nuru pekee
Ambayo kwayo jahazi la mwanadamu linaweza kuongozwa
Katika bahari ya maisha, na kufika pwani ile
Ya furaha kamili kwa salama."
Kwa nini kitabu hiki ----- hazina hii ya thamani ----- kisiinuliwe juu na kutukuzwa kama
rafiki anayethaminiwa? Hii ndiyo ramani yetu itakayotuwezesha kuivuka bahari ile ya
maisha iliyojaa tufani. Ni kitabu chetu cha mwongozo, kinachotuonyesha njia ile iendayo
kwenye makao yale ya milele, na tabia tunayopaswa kuwa nayo ili kuweza kuyakalia
makao yale. Hakuna kitabu kingine cho chote ambacho kikisomwa kwa makini kitaikuza
na kuitia nguvu akili kama kujifunza Biblia. Hapa akili itapata mambo makuu ya hali ya
juu kuweza kuzitumia nguvu zake zote. Hakuna kitu kingine cho chote ambacho kitazipa
nguvu akili zetu kama kuzileta ili zipate kugusana na kweli kuu mno za ufunuo. Juhudi
ya kuyashika na kuyapima mawazo haya makuu inaipanua akili yetu. Twaweza kuchimba
chini sana katika mgodi huu wa ile kweli, na kuzikusanya hazina za thamani ambazo
kwazo roho yetu inaweza kutajirishwa. Hapa tunaweza kujifunza njia ya kweli ya kuishi,
na njia salama ya kufa.
Kule kuyafahamu Maandiko kwa njia ya kawaida huzinoa nguvu zetu za utambuzi, na
kuijengea ngome roho yetu dhidi ya mashambulio ya Shetani. Biblia ni upanga wa Roho,
ambao hautashindwa kumshinda adui yetu. Ni kiongozi pekee cha kweli katika masuala
yote ya imani na maisha. Sababu ya kwa nini Shetani ametawala sana akili na mioyo ya
wanadamu ni kwamba hawajalifanya Neno la Mungu kuwa mshauri wao, na njia zao zote hazijapimwa kwa kipimo hicho cha kweli. Biblia itatuonyesha njia gani tuifuate ili kuwa
warithi wa utukufu. ----- RH, Jan.4, 1881.
Moyo unapofunguliwa na kuruhusu Neno kuingia ndani yake, hapo ndipo nuru kutoka
kwenye kiti cha enzi cha Mungu itakapoangaza moyoni. Neno hilo, likiwekwa moyoni,
litamzalia mwanafunzi huyo hazina ya maarifa isiyoweza kukadiriwa thamani yake.
Kanuni zake zinazoboresha maisha yetu zitaitia muhuri tabia yetu kwa kuiwekea
uaminifu na ukweli, kiasi na ukamilifu. ----- YI, Des.31, 1907.
KWELI NDANI YA MOYO Januari 26
Nimeichagua njia ya uaminifu, Na kuziweka hukumu zako mbele yangu. Zaburi 119:30.
Kazi ya Mungu inataka wanaume na wanawake watakaosimama juu ya jukwaa la ile
kweli bila kutetereka, na watakaoishikilia juu kwa nguvu bendera ya ile kweli, ili
asiwepo mtu awaye yote anayeweza kushindwa kuona ni upande gani wanasimama.
Mahali pao [wanaposimama] hapana budi kuonekana wazi. Mioyo yao haina budi kuwa
safi na mitakatifu, huru kutokana na unafiki au madanganyo. ----- Letter 44, 1903.
Kweli haina budi kupata mahali pake pa kukaa daima moyoni. Ndipo kwa uwezo wa
Roho Mtakatifu itatoa mvuto wake katika mambo yote unayofanya na kusema. Je!
tujaribu kuiweka kweli mahali isipoweza kuonekana? La, la, hata kidogo. Yatupasa kuipa
heshima ya utakatifu wake. Kanuni zake zitumike katika shughuli zako zote unazofanya.
Iwe mshauri wako katika matatizo yako yote, kiongozi katika uhusiano wako wote wa
maisha, msaada tele wakati wa kila shida. Hadharani, faraghani, yaani, mahali ambapo
jicho la mwanadamu haliwezi kuona, mahali ambapo sikio lo lote haliwezi kusikiliza,
isipokuwa lile la Mungu peke yake, hapo ndipo kweli itakapotuongoza sisi, ikiyaelekeza
mawazo yetu, na kutusukuma kusema maneno yetu na kutenda matendo yetu. ----- Letter
5b, 1891.
Unaweza kuuonyesha ulimwengu kwamba kweli unayoikiri inaitakasa na kuifanya tabia
yako kuwa bora zaidi na kukufanya uwe mchapa kazi mwenye bidii na mwangalifu
katika matumizi yako ya fedha na chakula, na kukufanya uepukane na uchoyo,
kuwaghilibu watu, na kila njia ya kukosa uaminifu. Katika maneno yako onyesha subira
na ustahimilivu, nawe unaweza kuhubiri kila siku hubiri juu ya uwezo wa ile kweli na
kufanya huduma inayofaa kwa kazi ya Mungu. Hebu na asiwepo mtu ye yote asemayekwamba ile kweli unayoikiri haileti tofauti yo yote [kati yako] na wapenda dunia....
Usitoe mwanya hata kidogo kwa ye yote kusema vibaya juu ya imani yako kwa sababu
ya wewe kutotakaswa na ile kweli. ----- Letter 30, 1878.
Kweli kama ilivyo katika Yesu inapozibadilisha tabia zetu, hapo ndipo itakapodhihirika
kuwa hiyo ndiyo kweli hasa. Inapotafakariwa na muumini wa kweli, itazidi kung'aa
katika uzuri wake wa awali. Tunapoitazama, itaongezeka thamani yake, na kuangaza
katika uzuri wake wa asili, ikiihuisha na kuitia nguvu akili yetu, na kuidhibiti tabia yetu
ya uchoyo, isiyokuwa ya Kikristo kwa kukosa adabu kwetu. Itaikuza hamu yetu ya
kupata mambo mema, na kutuwezesha sisi kukifikia kipimo kamili cha utakatifu. -----
MS 30, 1897.
KUIFURAHIA KWELI Januari 27
Ee BWANA, unifundishe njia yako, Nitakwenda katika kweli yako; Moyo wangu na
ufurahi kulicha jina lako. Zaburi 86:11.
Sema kwa moyo wako wote, "Nitakwenda katika kweli Yako." Kila azimio lililotamkwa
katika kicho cha Mungu litalitia nguvu kusudi lako na imani yako. Litakuwa na
mwelekeo wa kukuchochea na kukunyenyekeza, kukutia nguvu na kukuthibitisha.
"Nitakwenda katika kweli Yako." Hata hivyo, kweli inahitaji imani yetu kwa sababu
ulimwengu huu umegharikishwa na hadithi za uongo. Kwa sababu makosa na
udanganyifu vimeenea kote, huo ni ushahidi wa pekee wa ukweli kwamba ipo kweli,
yaani, kweli halisi, mahali fulani....
Haitoshi kwetu kuisikia tu ile kweli. Mungu anataka kwetu utii. "Heri walisikiao neno la
Mungu na kulishika." Luka 11:28. "Mkiyajua hayo, heri ninyi mkiyatenda." Yohana
13:17.
Twaweza kwenda kwa kuifurahia ile kweli. Kwetu haihitaji kuwa kongwa la utumwa,
bali faraja, kwetu ni ujumbe wa habari njema za furaha kuu, unaoichangamsha mioyo
yetu na kutufanya kuimba nyimbo kwa Mungu mioyoni mwetu. Kwa njia ya saburi na
faraja ya Maandiko tunalo tumaini. Tumaini la Kikristo sio la kununa, yaani, lisilokuwa
na faraja yo yote ndani yake. La, la. Halitufungii katika gereza la mashaka na hofu. Kweli
inawaweka huru wale waipendao na kutakaswa kwayo. Wanatembea katika uhuru wa
utukufu wa watoto wa Mungu. ----- Letter 8, 1873.Sisi tunaojidai kuiamini kweli yatupasa kuonyesha matunda yake katika maneno na tabia
yetu. Tunatakiwa kuwa mstari wa mbele katika ujuzi wetu wa kumjua Yesu Kristo,
katika kuupokea upendo wake kwa ajili ya Mungu na kwa ajili ya jirani yetu, ili tuwe nao
mwanga wa
mbinguni ukiangaza katika maisha yetu ya kila siku. Kweli haina budi kuingia mpaka
ndani kabisa ya moyo, na kukitakasa kila kitu kisichofanana na Roho wa Kristo, na nafasi
tupu inayoachwa [moyoni] kujazwa na tabia yake yule aliyekuwa safi na mtakatifu na
asiyeghoshiwa [Kristo asiyekuwa na uchafu wo wote], ili chemchemi zote za moyoni
ziwe kama maua, yanayonukia vizuri kwa manukato yake, yaani, harufu ile inayonukia
vizuri, harufu ya uzima iletayo uzima. ----- MS 109, 1897.
Ni kweli ile iliyohifadhiwa sana moyoni inayomfanya mtu kuwa mtu wa Mungu. -----
MS 1a, 1890.
KWELI NI HAZINA YA THAMANI Januari 28
Inunue kweli, wala usiiuze; Naam, hekima, na mafundisho, na ufahamu. Mithali 23:23.
Kweli ni ya thamani; imeleta mabadiliko ya maana katika maisha na tabia [ya mtu],
ikiwa na uwezo mkubwa sana wa kuyadhibiti maneno, mwenendo, mawazo, na maisha
[yake]. ----- Letter 14, 1885.
Dini ya Yesu Kristo haimdhalilishi kamwe yule anayeipokea. Endapo inawakuta
wanaume na wanawake wana maisha ya kidunia, ya kawaida, duni, wenye maneno
yasiyokuwa ya upole, wakali katika usemi wao, wachoyo na wanaojipenda wenyewe,
basi, kweli iliyopokewa moyoni mwao inaanza kazi yake ya kuwatakasa, yaani,
kuwasafisha. Matengenezo yanaonekana katika maneno yetu, mavazi yetu, tabia zetu, na
katika mambo yote yampendezayo Mungu. Basi ulimwengu wote waweza kuuona uwezo
wake [ile kweli] katika kazi yake ya kutubadilisha.
Kweli inazirekebisha tamaa zetu na kutakasa akili zetu za kutambua yaliyo mema.
Inatuinua na kututukuza, nayo hufanya kazi yake kama chachu kwa kimya na daima
mpaka mwili wote uwe umetakaswa na kufanywa chombo cha heshima chini ya uongoziwa Roho Mtakatifu, ili kumfanya mpokeaji wa kweli hiyo afae kuishi na jamii ya malaika
watakatifu, yaani, wasiokuwa na dhambi....
Wokovu ule ulionunuliwa kwa ajili ya wanadamu kwa gharama kubwa mno kama ile
unatakiwa kuwekwa na kila muumini katika chombo cha thamani. Kile ambacho kina
thamani kubwa mno kama hiyo daima kingefikiriwa sana na wale wanaoipokea kweli
hiyo, ambao bado wanaendelea kuwa na utovu wa adabu na kuwa wakali, wala
kisingerahisishwa na kufanywa kuwa cha kawaida. ----- MS 43, 1891
Kweli kama ilivyo ndani ya Yesu haina ubaridi wala hali ile ya kutovutia wala
uzoelefu.... Kweli hiyo imejaa ukunjufu, na ushuhuda wa kuwapo kwake Yesu.....
Tunao ujumbe wa kupeleka ulimwenguni. Unaambatana na msalaba. Kweli [za Biblia]
hazipendwi kwa sababu zinataka watu wajikane nafsi na kujitoa mhanga. Basi ni muhimu
jinsi gani kwamba wale wanaoichukua kweli, wanapoihubiri kweli hiyo kwa uaminifu,
waonyeshe kwa kila neno na tendo kwamba ni upendo wa Kristo unaowasukuma.
Kweli... daima ni nzuri, na wale wanaoishi sawasawa na kweli hiyo kama ilivyo katika
Yesu wanapaswa kujifunza jinsi ya kuifundisha kweli hiyo ili uzuri wake upate
kuonekana. ----- MS 62, 1886.
Itunze kweli kuliko kitu kingine cho chote; usiiuze kwa bei yo yote ile. ----- Letter 8,
1873.
BIBLIA HAINA MSHINDANI Januari 29
Maneno ya BWANA ni maneno safi, Ni fedha iliyojaribiwa kalibuni juu ya nchi;
Iliyosafishwa mara saba. Zaburi 12:6.
Biblia ni kitabu bora kuliko kitabu kingine cho chote; haina mshindani. Ujuzi na
kuyakubali mafundisho yake huleta nguvu na afya ya akili. Kuyafahamu mafundishoyake huhitaji mwanafunzi ayafahamu maarifa ya mapenzi ya Mungu yasiyokuwa na
kikomo. Neno la Mungu linawafundisha wanaume na wanawake namna ya kufanyika
wana na binti zake Mungu. Hakuna kitabu kingine, yaani, hakuna fundisho jingine,
kinachoweza kulingana na hicho; kanuni zake huingia taratibu, kama ulivyo uwezo na
tabia ya Mwasisi wake, tena zinapita uwezo wote. Kinaweza kutoa elimu ya juu sana,
ambayo akili ya kibinadamu inaweza kuifikia. ----- Letter 64, 1909.
Si salama kwetu kuyaacha Maandiko Matakatifu, na kuzisoma kurasa zake kwa nadra
tu.... Shika hatamu za akili yako na kuikabili kazi ya juu ambayo imewekwa mbele yake,
na kujifunza kwa ari thabiti, ili upate kuijua kweli hiyo ya mbinguni. Wale wanaofanya
hivyo, watashangaa kuona kile akili yao itakachoweza kukifikia. ----- YI, Juni 29, 1893.
Akili za wale wote wanaolifanya Neno la Mungu kuwa somo lao zitapanuka. Zaidi sana
kuliko somo jingine lo lote mvuto wake umekusudiwa kuzikuza nguvu za ufahamu na
kuipa akili uwezo mpya. Linaifanya akili igusane na kanuni zile pana, bora za ile kweli.
Linaileta mbingu yote kuungana kwa karibu sana na akili za wanadamu, ikiwapa hekima
na maarifa na ufahamu. Katika kushughulika na mambo ya kawaida yaliyotungwa na
wanadamu, na kujilisha maandiko ya watu wasiovuviwa, akili hudumaa na kuwa duni....
Ufahamu wake wa mambo yale ulioyazoea, na kwa njia ya kutafakari mambo yale
yasiyodumu, ufahamu huo hupungua, nguvu zake hupungua, na baada ya muda fulani
kupita [akili] haiwezi kupanuka....
Maarifa yote tunayopata katika maisha haya ya kipindi hiki cha majaribio, ambayo
yatatusaidia kujenga tabia itakayotufanya tufae kuwa wenzi wa watakatifu katika nuru,
hiyo ndiyo elimu ya kweli. Itatuletea mibaraka sisi wenyewe na kwa wengine katika
maisha haya, na siku za usoni itatupatia uzima wa milele ukiambatana na utajiri wake
usioharibika. ----- MS 67, 1898.
TIBA YA HAKIKA KWA MAGONJWA YA KIROHO Januari 30
Akusamehe maovu yako yote, Akuponya magonjwa yako yote. Zaburi 103:3.
Kristo ametupa sisi Neno lake, ili wanaume na wanawake waweze kupatiwa tiba kamili
kwa magonjwa yote ya kiroho. Neno hilo ndicho kipimo cha tabia ya wanadamu.
Linaonyesha ugonjwa, na kutoa ushauri wa dawa ya kuutibu. Katika neno hilo yamo
maagizo ya tiba ya kila ugonjwa wa kiroho. Amri dhahiri za Mungu zitaleta mvuto uletao
afya juu ya akili, na juu ya mwili wote. Zikipokewa kwa imani [amri hizo] na kuwekwa
katika matendo kwa uaminifu, dawa zake hazishindikani [ni za hakika kabisa]. -----
Letter 42, 1907.
Mbele ya walio wanyenyekevu sana zimefunguliwa ahadi za Neno la Mungu. Mungu
anatangaza hivi, "Lakini mtu wa kwenu akipungukiwa na hekima, na aombe dua kwa
Mungu, awapaye wote, kwa ukarimu...." Yakobo 1:5. Hataondoka mikono mitupu. Na
mtu yule anayeishi kwa kila neno la Mungu ataendelea kuwa na uwezo zaidi kiakili nakimaadili. Atakuwa na ufahamu mwingi zaidi kuliko ule aliouonyesha kabla hajafungua
moyo wake kuliruhusu neno la uzima kuingia humo. Nguvu za akili, zikiunganishwa kwa
imani na lile Chimbuko la hekima na maarifa, zitakua na kupanuka. Nguvu za akili
zilipokuwa zikiongozwa na Shetani, mtu mzima alikuwa amedumaa. Lakini uwezo wa ile
kweli inapoingia moyoni, unaubadilisha mwili wote. ----- MS 23, 1899.
Bwana amenena kwa sauti yake katika Neno lake Takatifu. Kurasa zile zenye mibaraka
zimejaa mafundisho na uzima, zinapatana kabisa na ile kweli. Hizo zina kanuni kamilifu
ya tabia. Mafundisho hutolewa, kanuni huwekwa, ambazo hutumika katika kila jambo la
maisha yetu, hata kama mtu fulani hajatajwa [kwa jina]. Hakuna kinachoachwa bila
kufunuliwa ambacho ni cha muhimu kwa mfumo kamili wa imani yetu na mwelekeo
sahihi wa matendo yetu. Kila wajibu ambao Mungu anatutaka kutekeleza umeelezwa kwa
wazi.... Hakuna watakaoweza kupotea kutoka katika njia ya kweli ambao kwa
unyenyekevu na unyofu wa moyo wanaikubali Biblia kama kiongozi wao, wakiifanya
kama mtu wao wa kuwashauri. ----- Letter 34, 1891.
Usiwe na shaka: Iwapo wewe unajifunza Neno la Mungu kwa hamu itokayo moyoni ili
kupata msaada, Bwana ataijaza roho yako na nuru. Kazi yako itakubalika mbele za
Mungu, na mvuto wako utakuwa harufu nzuri iletayo uzima. ----- AUCR, Okt. 1, 1903.
KUWEKA MOYONI AKIBA YA ILE KWELI Januari 31
Nisiyoyaona nifundishe Wewe; Kama nimefanya uovu sitafanya tena? Ayubu 34:32.
Chukua Biblia yako na kujiweka mwenyewe mbele za Baba yako aliye mbinguni,
ukisema, "Nielimishe; nifundishe kweli ni nini." Bwana ataifikiria sala yako, na Roho
Mtakatifu ataiweka kweli moyoni mwako. Katika kuyachunguza Maandiko kwa ajili
yako mwenyewe, utaimarishwa katika imani. Ni jambo la maana sana kwamba uendelee
daima kuyachunguza Maandiko, ukiweka moyoni akiba ya Neno la Mungu, maana
huenda ukatengwa mbali na marafiki zako Wakristo, na kuwa mahali ambapo hutaweza
kukutana na watoto wa Mungu. Unahitaji hazina za Neno la Mungu zilizofichwa moyoni
mwako, ili upinzani unapokujia, uweze kuleta kila kitu kwenye Maandiko hayo.
Tunaishi katika siku za mwisho, wakati kosa lile lililojaa udanganyifu mkuu
linakubaliwa na kusadikiwa, wakati kweli inatupiliwa mbali. Wengi wanaelekea katika
giza na ukafiri, wakitafuta makosa katika Biblia, wakileta mavumbuzi yao ya ushirikina,nadharia zao zisizoungwa mkono na Biblia, na mawazo yao yasiyofaa ya falsafa;
walakini ni wajibu wa kila mmoja kutafuta ujuzi kamili wa Maandiko. ----- ST, Feb.6,
1893.
Kweli inao uwezo pale tu inapotekelezwa kwa vitendo katika maisha yetu. Iwapo Neno
la Mungu linaikemea tabia fulani uliyoiendekeza, hisia fulani uliyoipenda sana, roho
fulani uliyoionyesha, usiliache Neno la Mungu, bali achana na maovu unayofanya, kisha
umruhusu Yesu ausafishe na kuutakasa moyo wako. Ungama makosa yako, na kuyaacha.
----- ST, Jan.30, 1893.
Usiikubali tu ile kweli, na kushindwa kuwa mtendaji wa maneno ya Kristo. Kweli ni
lazima itumiwe na mtu mwenyewe; sharti wanaume na wanawake wale wanaoipokea
iwalete kwake yule Mwamba, ili wapate kuanguka juu ya Mwamba huo na kuvunjika.
Hapo ndipo Yesu awezapo kuziumba upya na kuzibadilisha tabia zao zipate kufanana na
tabia yake takatifu. Kama tutapenda kuisikia sauti yake [katika Neno lake], basi, hatuna
budi kuiruhusu hali ya ukimya kutawala moyoni mwetu. Makelele ya nafsi yetu, unafiki
wake, tamaa zake, ni lazima zikemewe, tena yatupasa kulivaa vazi lile la unyenyekevu,
na kukaa mahali petu kama wanafunzi wanyenyekevu katika shule ya Kristo. ----- RH,
Okt. 31, 1893.
MWACHE YESU AKUONGOZE Februari 1
Yesu akamwambia, Mimi ndimi njia, na kweli, na uzima; mtu haji kwa Baba, ila kwa
njia ya Mimi. Yohana 14:6.
Laiti kama sisi ambao tu wasafiri na wageni katika nchi hii ya kigeni.... tungaliweza
kumfahamu Kristo, aliye njia, na kweli, na uzima. Yeye anasema hivi, "Mtu haji kwa
Baba, ila kwa njia ya Mimi." Njia aliyoiweka i wazi kabisa, tena i tofauti hata mwenye
dhambi kuliko wote, aliyelemewa na mzigo wa dhambi, hana haja ya kupotea katika njia
yake. Hakuna hata mtafutaji mmoja anayetetemeka awezaye kushindwa kuiona njia hiyo
ya kweli, na kwenda katika nuru ile safi na takatifu, kwa maana Yesu anaongoza njia.
Njia hiyo ni nyembamba sana, takatifu sana, kiasi kwamba dhambi yo yote haiwezi
kuvumiliwa ndani yake, bali nafasi ya kuingia katika njia hiyo imewekwa wazi kwa
wote, na hakuna hata mmoja anayekata tamaa, mwenye mashaka, atetemekaye
anayeweza kusema, "Mungu hanijali mimi kabisa." Kila mtu ni wa thamani machoni
pake.... Shetani alipokuwa anashangilia kama mfalme wa dunia hii, alipodai kwamba
dunia hii ilikuwa ufalme wake, sisi sote tulipokuwa tumeharibika vibaya na kuchafuliwa
na dhambi, Mungu alimtuma Mjumbe wake toka mbinguni, Mwanawe pekee,
kuwatangazia wakazi wote wa ulimwengu huu, akisema, "Nimeipata fidia. Nimefanyanjia ya kutokea kwa wote wanaoangamia. Ninazo hati za ukombozi wenu, zimetiwa
muhuri na Bwana wa mbingu na nchi."
Si kwa sababu kuna dosari yo yote katika hati ile ya kumiliki ambayo imenunuliwa kwa
ajili yenu hata hamtaki kuipokea. Si kwa sababu rehema, neema, yaani, upendo wa Baba
na Mwana hautoshi, wala haujatolewa bure, hata hamwufurahii upendo huo usameheo....
Mkipotea, itakuwa ni kwa sababu hamtaki kuja kwa Kristo ili mpate uzima.
Mungu anataka kuwapa, wale wote watakaouamini upendo wake, na kuupokea wokovu
wake, baraka ya msamaha wa dhambi zao, yaani, msamaha kwa ajili ya uovu wao, na
kipawa cha haki yake. Kristo yuko tayari kumwambia mwenye dhambi anayetubu,
"...Tazama, nimekuondolea uovu wako...." Zekaria 3:4-7. Kristo ndiye kiungo chetu kati
ya Mungu na mwanadamu. Damu ya Yesu Kristo ndilo ombi lenye ushawishi wenye
nguvu unaouamsha moyo [wa Mungu] na kuzungumza naye kwa niaba ya wenye
dhambi. ----- MS 32a, 1894.
MWANADAMU ANA THAMANI KULIKO DHAHABU Februari 2
Nitafanya wanadamu kuadimika [kuwa wa thamani] kuliko dhahabu safi, na watu kuliko
dhahabu ya Ofiri. Isaya 13:12.
Ni wachache mno wanaotambua thamani ya mwanadamu, na utukufu ambao angeweza
kumletea Mungu kama angekuza na kuhifadhi usafi, tabia nzuri, na ukamilifu wa tabia....
Kipindi kifupi cha wakati walichopewa wanadamu hapa ni cha thamani sana. Sasa,
wakati mlango wa rehema bado haujafungwa, Mungu anakusudia kuziunganisha nguvu
zake na udhaifu wa mwanadamu asiyedumu.... Wale wanaompenda Mungu kweli kweli
wanaweza kuwa mbaraka kwa wengine. Na hatimaye milango ya mbinguni itafunguliwa
wazi kuwaruhusu kuingia, na kutoka kinywani mwa Mfalme yule wa utukufu mibaraka
itaanguka masikioni mwao kama muziki mtamu sana, "Njoni, mliobarikiwa na Baba
yangu, urithini ufalme mliowekewa tayari tangu kuumbwa ulimwengu." Mathayo 25:34.
Hivyo ndivyo wale waliokombolewa watakavyokaribishwa kwenye makao yale ambayo
Yesu anayaandaa kwa ajili yao. Kule wenzi wao hawatakuwa waovu wale wa duniani ----
- waongo, waabudu sanamu, wasio safi, ama wale wasioamini; bali watashirikiana na
wale waliomshinda Shetani na hila zake, na kwa msaada wa Mungu wamekuza tabia
zilizo kamilifu. Kila mwelekeo wa dhambi, kila upungufu unaowaathiri hapa, vitakuwavimeondolewa kwa damu yake Kristo; na uzuri usio na kifani pamoja na mng'aro ule wa
jua katika utukufu wake
wakati wa adhuhuri, wanapewa wao. Na uzuri wa kimaadili, yaani, ukamilifu wa tabia
yake, huangaza kutoka ndani yao kwenda nje, ukiupita kwa thamani utukufu ule wa nje.
Wanakizunguka kiti kile cheupe cha enzi wakiwa hawana mawaa, wakishiriki heshima na
haki ya malaika.
"Jicho halikuyaona, wala sikio halikuyasikia, wala hayakuingia katika moyo wa
mwanadamu, mambo ambayo Mungu aliwaandalia wampendao." l Wakorintho 2:9. Kwa
kuzingatia urithi ule wa utukufu ambao unaweza kuwa wake, "mtu atatoa nini badala ya
nafsi yake?" Huenda akawa maskini [fukara]; lakini ndani yake anayo mali na cheo
ambacho ulimwengu huu usingeweza kumpa kamwe. Nafsi iliyokombolewa na
kutakaswa dhambi zake, pamoja na nguvu zake zote zilizotolewa wakf kwa Mungu, ni ya
thamani isiyokadirika. ----- ST, Aprili 3, 1884
MIMI SI MALI YANGU MWENYEWE Februari 3
Mlinunuliwa kwa thamani; Msiwe watumwa wa wanadamu. l Wakorintho 7:23.
Ni jambo la kawaida jinsi gani kwetu sisi kujifikiria kwamba tu mali yetu wenyewe
kabisa! Walakini Neno lile lililovuviwa linatangaza hivi, "Wala ninyi si mali yenu
wenyewe... Mlinunuliwa kwa thamani." l Wakorintho 6:19,20..... Katika uhusiano wetu
na wanadamu wenzetu sisi tunamiliki uwezo wa akili zetu na miili yetu tuliyokabidhiwa.
Katika uhusiano wetu na Mungu, sisi tu wapokeaji, yaani, mawakili wa neema Yake.
Wakati wetu hauna budi kutumiwa kwa akili, kwa bidii, na chini ya utakaso wa Roho
Mtakatifu. Yatupasa kuelewa kitu gani ni kizuri na kitu gani ni kibaya kufanya kuhusiana
na mali yetu na uwezo wetu wa akili na mwili. Mungu anao umilikaji halisi wa kila
nguvu inayotumika kwa ajili ya utukufu wa jina lake. Talanta ya usemi, ya kumbukumbu,
ya mali, zote zinapaswa kuongezeka kwa utukufu wa Mungu, kuendeleza ufalme wake.
Mungu ametukabidhi mali yake yeye akiwa hayupo. Kila wakili anayo kazi maalum ya
kufanya katika kuuendeleza ufalme wa Mungu. Hakuna aliye na udhuru. ----- Letter 44,
1900. Kristo aliufunika Uungu wake na ubinadamu na kulipa fidia kwa ajili ya mwanadamu,
naye anataka kwamba mwanadamu authamini uzima ule uliotolewa kwa ajili yake kwa
gharama kubwa mno isiyoweza kupimika ambayo ililipwa. ----- MS 23, 1899.
Ni haki yako kulitii Neno hai la Mungu kama mtu aliyeongoka kweli kweli na
kubadilika, kutoa huduma yako ya juu sana kama mtu huru, aliyezaliwa na mbingu, kutoa
ushuhuda wako kuwa wewe unastahili amana ile takatifu ambayo Mungu amekupa kwa
kumtuma Mwanawe pekee kufa kwa ajili yako. Iwapo wewe unamwamini Kristo kama
Mwokozi wako, basi, unapokea kila neema, kila kipawa cha kiroho, kilicho muhimu kwa
kuikamilisha tabia ya Kristo.
Onyesha kwamba unaithamini kafara ile iliyotolewa kwa ajili yako, nawe uione kuwa ni
kuu mno kiasi kwamba haiwezi kukuruhusu wewe kufanya dhihaka na imani yako ya
dini kwa njia ya tabia yako na mtindo wako wa maisha unaolingana na kipimo cha
kidunia. ----- MS 167, 1897.
MALI ILIYONUNULIWA KWA DAMU YAKE KRISTO Februari 4
Nanyi mfahamu kwamba mlikombolewa si kwa vitu viharibikavyo, kwa fedha au
dhahabu; mpate kutoka katika mwenendo wenu usiofaa mlioupokea kwa baba zenu; bali
kwa damu ya thamani, kama ya mwana-kondoo asiye na ila, asiye na waa, yaani, ya
Kristo. l Petro 1:18,19.
Yakupasa kuzingatia kwamba wewe huna uhuru wa kupanga kufanya kile
kitakachoifurahisha nafsi yako. Wewe u mali yake Bwana. Kristo amekununua wewe
kwa thamani ya damu yake mwenyewe. Mwili wako hauna budi kutakaswa kwa ajili
yake Bwana kama chombo chenye heshima. Huo ni mali yake Kristo aliyoinunua. Kwa
hiyo, tunza kila nguvu ya mwili wako, yaani, kila kiungo, kipate kuwa silaha ya haki.
Shetani anataka kuitawala nguvu yako ya ubongo [akili], na nia yako, lakini hivyo vyote
ni mali ya Yesu. Sikuzote tafakari hivi, "Mimi si mali yangu mwenyewe. Yanipasa
kuitunza kila sehemu ya mali hii iliyonunuliwa na Kristo kwa uangalifu na utakatifu."...
Shetani anaweza kujaribu kukufunga wewe kwenye gari lake uwe kama mtu asiye na
uwezo wo wote. Lakini, wewe piga kelele ya ushindi ukisema Kristo amekuweka wewe
kuwa mtu huru. Usimvunjie heshima Mungu kwa neno lako moja la kuelezea uzembe
wako na kutokuweza kwako kushinda kikamilifu, kabisa, na kwa utukufu kwa njia yaYesu Kristo, aliyekufia ili kukukomboa, na kukufanya wewe kuwa mtu aliye huru.
Shinda, naam, shinda. Weka nia yako kila dakika upande wa mapenzi ya Mungu.
Tafakari kwa matumaini na ujasiri. Kwa imani piga kelele dhidi ya Shetani, nawe ukiwa
unamtazama Yesu, mwenye kuanzisha na mwenye kutimiza imani [yako], mwambie hivi,
"Yesu, Mkombozi wangu, mimi ni dhaifu. Siwezi kufanya neno lo lote pasipo kupata
msaada wako wa pekee. Roho yangu isiyokuwa na uwezo wo wote naiweka mikononi
mwako." Kisha acha mawazo yako yaendelee kutafakari juu ya wazo la kwamba wewe u
mbele zake Yesu, unatembea na Mungu, uhai wako umefichwa pamoja na Kristo katika
Mungu.... Hapo ndipo hutaweza kumtukuza Shetani kwa kujifikiria wewe mwenyewe
kuwa u dhaifu na bila msaada wo wote. Wewe mwenyewe utajitia
moyo kwa kujiweka katika hali ya usafi na utakatifu. Utampokea Roho Mtakatifu kuwa
msaidizi [mfariji] wako, na mtakasaji wako.... Utakuwa na moyo wenye amani na
uliotulia katika Mungu. Utasema, "Yesu yu hai, na kwa sababu yu hai, na mimi nitakuwa
hai. Amemshinda Shetani kwa ajili yangu, na mimi sitaki kushindwa na mwovu hata kwa
mara moja tu. Sitaki kumwaibisha Bwana na Kiongozi wangu; lakini nitalishangilia jina
lake takatifu, na kuwa zaidi ya mshindi." ----- Lettr 31, 1893.
MUNGU ANAITAKA MALI YAKE Februari 5
Lakini sasa, BWANA aliyekuhuluku, Ee Yakobo, Yeye aliyekuumba, Ee Israeli, asema
hivi, Usiogope, maana nimekukomboa; nimekuita kwa jina lako, wewe u wangu. Isaya
43:1.
Kila mwanaume na mwanamke amelipiwa fedha yake ya fidia na Yesu Kristo. "Wala
ninyi si mali yenu wenyewe; maana mlinunuliwa kwa thamani" ----- damu ya thamani ya
Mwana wa Mungu. ----- MS 42, 1890.
Haileti tofauti yo yote iwapo sisi tunajitoa wenyewe kwa Bwana au la, sisi tu mali yake.
Ninyi si mali yenu wenyewe; Maana mlinunuliwa kwa thamani. Sisi tu mali yake Bwana
kwa uumbaji, na sisi pia tu wake kwa ukombozi, kwa sababu hiyo hatuna haki yo yote
kudhani ya kwamba tunaweza kufanya tupendavyo. Sisi hatuna haki yo yote kwa kitu cho
chote tulicho nacho, hata kwa uhai wetu wenyewe. Fedha yetu yote, wakati wetu na
talanta zetu ni mali ya Mungu, naye ametuazima ili tupate kuitekeleza kazi ile aliyotupaya kufanya. Ametuagiza, "Fanyeni biashara [tumieni] hata nitakapokuja." Luka 19:13. ---
-- Letter 97, 1898.
Msifanye biashara ya [msitumie kwa] kujinufaisha ninyi wenyewe na kupuuzia madai ya
Mungu aliyo nayo juu yenu. Ninyi ni mali yake.... Yesu amewanunua kwa thamani
isiyokadirika. Mawazo yenu sharti yawekwe katika hali safi; hayo nayo ni mali yake
Bwana. Mpeni Yeye. Hatustahili kupata kitu cho chote kutoka kwa Mungu. Hatuwezi
kumpa kitu cho chote ambacho si chake. Je! tutazuia kumpa Mungu kile ambacho ni
chake? Msimwibie Mungu na kutumia kwa manufaa yenu wakati wake, talanta zake, na
nguvu zake kwa kujifungamanisha wenyewe na ulimwengu huu. Anataka mapenzi yenu;
mpeni. Ni yake. Anataka wakati wetu, dakika kwa dakika; mpeni. Ni wake. Anataka akili
yenu; mpeni. Ni yake....
Bwana anaitaka mali yake. Tukiisha kumpa Mungu, roho, mwili na nafsi; tukiisha
idhibiti tamaa yetu ya chakula chini ya uongozi wa dhamiri iliyoongolewa, na kupigana
na kila tamaa mbaya ya mwili, tukionyesha ya kwamba sisi tunakihesabu kila kiungo cha
mwili wetu kuwa ni mali yake Mungu, kikiwa kimekusudiwa kwa kazi yake; mapenzi
yetu yote yanapopatana na mawazo yake Bwana, yakiwa yamefungamanishwa na mambo
yale "yaliyo juu, ambako Kristo ameketi mkono wa kuume wa Mungu" ----- hapo ndipo
tutakuwa tumempa Bwana mali yake. Ee Mungu "vitu vyote vyatoka kwako na katika
vitu vyako mwenyewe tumekutolea." 1 Mambo ya Nyakati 29:14. ----- Letter 23, 1873.
ITUNZENI MALI YAKE MUNGU Februari 6
Ambaye alijitoa nafsi yake kwa ajili ya dhambi zetu, ili atuokoe na dunia hii mbovu
iliyopo sasa, kama alivyopenda Mungu, Baba yetu. Gal.1:4.Gharama yenu ni kubwa sana. "Mtukuzeni Mungu katika miili yenu [na katika roho
zenu]." 1 Wakorintho 6:20 [KJV]. Kile mnachoweza kudhani kwamba ni chenu ni chake
Mungu. Itunzeni mali yake. Amewanunua kwa thamani isiyokadirika. Akili yenu ni yake.
Ana haki gani mtu kuutumia vibaya mwili ambao si mali yake mwenyewe, bali ni mali
yake Yesu Kristo? Ni raha gani anayoweza kupata mtu ye yote yule anayezipunguza
taratibu nguvu zake za mwili na akili kwa kutimiza tamaa zake za mwili kwa njia yo yote
ile?
Mungu amempa kila mwanadamu ubongo wake. Anataka utumike kwa utukufu wake.
Kwa huo, mtu anawezeshwa kushirikiana na Mungu katika juhudi za kuwaokoa
wanadamu wenzake wanaoangamia. Hatuna uwezo mkubwa mno wa ubongo wala uwezo
wa kufikiri. Yatupasa kuuelimisha na kuufanyia mazoezi kila uwezo wa akili na mwili
tuliopewa ----- mashine ya kibinadamu ambayo Kristo ameinunua ----- ili tuweze
kuiweka katika hali yake bora ya matumizi. Yatupasa kufanya yote tuwezayo
kuziimarisha nguvu hizo; maana Mungu anapendezwa kutuona sisi tukiwa watenda kazi
pamoja naye wenye mafanikio mengi na hata mengi zaidi....
Katika kitabu kile cha Kutoka twasoma kwamba wakati ule alipowaagiza Waisraeli
kumjengea patakatifu [hema] jangwani, aliwapa watu fulani uwezo wa pekee, talanta, na
ufundi wa kubuni vitu, kisha akawaweka kufanya kazi ile. Na sisi atatutendea vivyo
hivyo.... Na ijapokuwa tunaweza kulazimika kuanza kwa njia fulani ndogo sana,
atatubariki na kuzizidisha talanta zetu kama tunu [zawadi] ya uaminifu wetu. ----- MS 8,
1904.
Kristo amewafia ninyi, nanyi yawapasa kuishi kwa ajili ya Mungu. Hebu akili zenu
[mawazo yenu] na zisafishwe, ziwe safi kabisa, na takatifu, na zimwelekee Mungu.
Bwana anataka utakaso wa mwili mzima. Akili, pamoja na mwili wote, havina budi
kuadilishwa na kuwa bora zaidi. Mungu ana madai yake juu ya nafsi, roho, na mwili
wetu. ----- MS 167, 1897.
Haimo katika uwezo wa wale waliolitaja jina la Yesu kumpa zaidi ya kile kilicho chake.
Amemnunua kila mjumbe wake wa kibinadamu kwa thamani isiyokadirika, na sisi tu
mali yake kwa wakati huu wa sasa na hata milele. ----- Letter 51b, 1894.
MSHIRIKISHE MUNGU KATIKA MASHAURI YAKO Februari 7 Yeye mwenyewe alizichukua dhambi zetu katika mwili wake juu ya mti, tukiwa wafu
kwa mambo ya dhambi, tuwe hai kwa mambo ya haki; na kwa kupigwa kwake
mliponywa. 1 Petro 2:24.
Kristo alizichukua dhambi zetu katika mwili wake juu ya mti.... Dhambi inaweza kuwa
ni kitu gani, basi, iwapo hakuna mwanadamu ye yote ambaye angeweza kufanya
upatanisho? Laana yake inaweza kuwa ni kitu gani iwapo ni Mungu peke yake ambaye
angeweza kuikomesha? Msalaba wa Kristo unamshuhudia kila mtu kwamba mshahara
wa dhambi ni mauti.... Je! yamkini kuna nguvu fulani kama vile uchawi ambayo
inazipumbaza akili zetu za utambuzi, na kuzishupaza [kuzifanya ngumu kama chuma cha
pua] hata zisiweze kupokea mawazo ya Roho wa Mungu? Ninakusihi sana wewe, kama
mjumbe [balozi] wake Kristo,... uwe na bidii katika kujipatia neema ya Mungu.
Unaihitaji kila siku, ili usiweze kufanya kosa lo lote [kuanguka dhambini] katika maisha
yako....
Unaweza kujisikia kwamba unao uwezo wa kujiongoza wewe mwenyewe, kupanga
mipango yako na kuitekeleza kwa kutegemea akili zako mwenyewe. Hali hiyo si salama
kwako wala kwa ye yote. Nazungumza mambo yale ninayoyajua. Mshirikishe Mungu
katika mashauri yako. Mtafute kwa uongozi wake. Hutamtafuta bure.... Ninakusihi sana
usiache saa hizi za thamani za muda wako wa majaribio kupita bure pasipo kuwa na
maendeleo yo yote ya kiroho. Kwa vyo vyote vile usiache nguvu zako za maadili
kudumaa....
Mbingu na vivutio vyake i mbele yako, yaani, utukufu ule wa milele zote ambao
unaweza kuupoteza ama kuupata. Uchaguzi wako ni upi? Maisha yako na tabia yako
vitashuhudia uchaguzi wako ulioufanya. Ninaingiwa na wasiwasi mwingi sana kwa
sababu nawaona wengi sana hawayajali mambo haya yenye umuhimu wa milele.
Sikuzote wanajishughulisha sana hapa na pale na mambo madogo yasiyokuwa na maana
sana, na jambo lile kuu haliwekwi katika mawazo yao. Hawana muda wa kuomba,
hawana muda wa kukesha, hawana muda wa kuyachunguza Maandiko. Wanazo shughuli
nyingi mno kiasi cha kuwafanya washindwe kufanya maandalizi ya lazima kwa ajili ya
maisha yao ya baadaye. Hawawezi kutenga muda fulani kwa kusudi la kuzikamilisha
tabia zao za Kikristo na kutumia juhudi kubwa kujipatia haki ile ya kuingia mbinguni.
Kama unao uzima wa milele, basi, inakupasa kuwa na bidii na kufanya kazi kukifikia
kiwango kile.... Mtukuze Mungu kwa kuichagua njia yake, na mapenzi yake. Atakuwa
mshauri wako mwenye hekima na rafiki yako mwaminifu, asiyebadilika. ----- Letter 23,
1873.
KAMBA ILIYOTELEMSHWA KUTOKA MBINGUNI Februari 8 Tena, alipoonekana ana umbo kama mwanadamu, alijinyenyekeza akawa mtii hata
mauti, naam, mauti ya msalaba. Wafilipi 2:8.
Pimeni urefu wa kamba hiyo, kama mnaweza, ambayo imetelemshwa hapa chini kutoka
mbinguni ili kumwinua mwanadamu juu. Makadirio peke yake tunayoweza kuwapa
kuhusu urefu wa mnyororo huo ni kuwaonyesha kule Kalvari. ----- MS 6, 1893.
Wanadamu walioanguka wasingeweza kupata makao kule peponi [paradiso] kwa Mungu
pasipokuchinjwa yule Mwana-Kondoo tangu kuwekwa misingi ya dunia hii. Basi, je!
tusingeutukuza huo msalaba wa Kristo?...
Ukamilifu wa malaika ulishindwa kule mbinguni. Ukamilifu wa mwanadamu ulishindwa
kule Edeni, yaani, mahali pa raha kuu [peponi au paradiso]. Wote wanaotamani kuwa na
usalama hapa duniani na kule mbinguni hawana budi kumtazama Mwana-Kondoo wa
Mungu. Mpango wa wokovu, unaodhihirisha haki na upendo wa Mungu, hutupatia kinga
ya milele dhidi ya uasi kwa yale malimwengu yasiyoanguka [dhambini], na kwa wale
watakaokombolewa kwa damu ya Mwana-Kondoo. Tumaini letu la pekee ni kuiamini
kabisa damu ya yule awezaye kuwaokoa kabisa wale wote wamjiao Mungu kwa Yeye.
Kifo cha Kristo juu ya msalaba ule wa Kalvari ndilo tumaini letu la pekee katika
ulimwengu huu, na litakuwa ndilo wazo letu kuu katika ulimwengu ule ujao. Lo! hatujui
thamani ya upatanisho wetu! Kama tungejua, basi, tungeongea juu yake zaidi. Kipawa
cha Mungu katika Mwanawe Mpendwa kilikuwa ni udhihirisho wa upendo usioweza
kufahamika. Kiliwakilisha yale yote ambayo Mungu angeweza kufanya ili kuihifadhi
heshima ya sheria yake [Amri Kumi], na wakati uo huo kuweza kumwokoa mkosaji
[mvunjaji wa sheria] huyo. ----- 5BC 1132.
Yesu aliuweka msalaba wake katika mstari wa wima wa nuru ile iliyotoka mbinguni,
maana ni pale ambapo [nuru hiyo] itaweza kulifikia jicho la mwanadamu. Msalaba u
katika mstari ule wa moja kwa moja wa mng'ao wa sura ya Mungu, hata imekuwa
kwamba kwa kuutazama msalaba huo wanadamu wanaweza kumwona na kumjua Mungu
na Yesu Kristo, aliyemtuma. Kwa kumtazama Mungu tunamwona yule Mmoja
aliyeimwaga roho yake kwa kufa kwake. Kwa kuutazama msalaba mandhari inaelekezwa
kwa Mungu, na chuki ya Mungu dhidi ya dhambi, pia tunaona upendo wake kwa wenye
dhambi, ambao una nguvu kuliko mauti. Kwa ulimwengu msalaba ni hoja isiyokanushika
inayoonyesha kwamba Mungu ndiye ile kweli na nuru na upendo. ----- 5BC 1133.KITOVU CHA TUMAINI LANGU Februari 9
Lakini mimi, hasha, nisione fahari juu ya kitu cho chote ila msalaba wa Bwana wetu
Yesu Kristo, ambao kwa huo ulimwengu umesulibiwa kwangu, na mimi kwa ulimwengu.
Wagalatia 6:14.
Ukiuondoa msalaba kutoka kwa Kristo ni sawa na kuliondoa jua linalouangazia mchana,
na kuudondosha chini mwezi na nyota kutoka katika anga za mbingu wakati wa usiku.
Msalaba wa Kristo unatuleta karibu na Mungu, ukimpatanisha mwanadamu na Mungu,
kisha Mungu na mwanadamu. Baba anauangalia msalaba huo, anayaangalia mateso yale
aliyompa Mwanawe apate kuyastahimili ili kuliokoa taifa la wanadamu kutoka katika
huzuni isiyokuwa na matumaini na kuweza kumvuta mwanadamu kwake Mwenyewe.
Anauangalia kwa huruma za upendo wa Baba. Msalaba huo karibu umesahauliwa kabisa,
lakini bila msalaba hakuna uhusiano wo wote na Baba, hakuna umoja wo wote na
Mwana-Kondoo aliye katikati ya kile kiti cha enzi kule mbinguni, hakuna makaribisho ya
furaha kwa yule mpotevu ambaye angependa kurudi kwenye njia ile iliyoachwa ya haki
na kweli, hakuna tumaini lo lote kwa mwenye dhambi [mvunjaji wa sheria] katika siku
ile ya hukumu. Bila msalaba hakuna njia nyingine yo yote iliyotolewa ya kuushinda
uwezo ule wa adui yetu mwenye nguvu. Kila tumaini la wanadamu hutegemea msalaba
huo. ----- MS 58, 1900
Mwenye dhambi anapoufikia msalaba huo, na kutazama juu kumwangalia Yule
aliyekufa ili kumwokoa, anaweza kushangilia kwa furaha timilifu; kwa maana dhambi
zake zimesamehewa. Akiwa amepiga magoti yake chini ya msalaba, anakuwa amepafikia
mahali pa juu sana ambapo mwanadamu anaweza kupafikia. Nuru ya maarifa ya utukufu
wa Mungu inaonekana katika uso wake Kristo; na maneno yake ya msamaha
yanatamkwa: Mpate kuishi, enyi wenye dhambi mlio na hatia, mpate kuishi. Toba yenu
imekubaliwa; kwa maana nimeipata fidia.
Kwa njia ya msalaba huo tunajifunza kwamba Baba yetu aliye mbinguni anatupenda
kwa upendo usiokuwa na kikomo na upendo ule wa milele, na kutuvuta kwake kwa
huruma inayoipita ile ya mama akimwonea shauku nyingi sana mtoto wake mtundu. Je,
twaweza kustaajabu ya kwamba Paulo alisema kutoka moyoni mwake maneno haya,
"Lakini mimi, hasha, nisione fahari juu ya kitu cho chote ila msalaba wa Bwana wetu
Yesu Kristo"? Ni haki yetu pia kujisifia msalaba ule wa Kalvari, ni haki yetu kujitoa
kikamilifu kwake Yeye aliyejitoa kwa ajili yetu. Basi, pamoja na nuru ile inayong'aa
kutoka usoni pake kuja kwenye nyuso zetu, tutaweza kusonga mbele na kuiakisi kwa
wale walio gizani. ----- 5BC 1133UWEZO WA DAMU YA KRISTO Februari 10
Kwani ni hiyo damu ifanyayo upatanisho kwa sababu ya nafsi. Mambo ya Walawi
17:11.
Kristo alikuwa ndiye yule Mwana-Kondoo aliyechinjwa tangu kuwekwa misingi ya
dunia. Kwa wengi limekuwa fumbo kwa nini wanyama wengi wa kafara walitakiwa
katika kipindi kile cha Agano la Kale, na kwa nini wanyama wengi waliotokwa na damu
walipelekwa kwenye madhabahu ile. Lakini ukweli mkuu ambao ulitakiwa kuwekwa
mbele ya watu wale, na kupigwa picha katika akili zao na mioyo yao, ulikuwa ni huu:
"Pasipo kumwaga damu hakuna ondoleo." Waebrania 9:22. Katika kila kafara
kilionekana kivuli [mfano] cha "Mwana-Kondoo wa Mungu." Yohana 1:29.
Kristo Mwenyewe alikuwa ndiye Mwasisi wa Mfumo ule wa Kiyahudi wa ibada,
uliokuwa na mifano na ishara, ambao ulikuwa kivuli cha mambo ya kiroho na mambo
yale ya mbinguni.... Leo tunaishi wakati ambapo kivuli (type) kimekutana na asilia yake
(antitype) katika toleo lile la Kristo kwa ajili ya dhambi za ulimwengu; tunaishi katika
siku za ongezeko la nuru, na hata hivyo ni wachache jinsi gani wanaofaidika na kweli hii
kuu na ya maana sana isemayo kwamba Kristo ametoa toleo la kutosha kwa wote! Kile
ambacho haki ilidai, Kristo alikuwa ametekeleza kwa kujitoa kafara yeye mwenyewe,
basi "sisi je! tutapataje kupona, tusipojali wokovu mkuu namna hii?" Waebrania 2:3.
Wale wanaokikataa kipawa hiki cha uzima watakuwa hawana udhuru. ----- ST, Jan.2,
1893.
Mungu na ashukuriwe kwa maana yule aliyeimwaga damu yake kwa ajili yetu, yu hai
kuweza kuidai, yu hai kumwombea kila mtu anayempokea. "Tukiziungama dhambi zetu,
Yeye ni mwaminifu na wa haki hata atuondolee dhambi zetu, na kutusafisha na udhalimu
wote." 1 Yohana 1:9. Damu ya Yesu Kristo inatusafisha na dhambi zote. Inanena mema
kuliko ile ya Habili, kwa maana Kristo yu hai sikuzote ili atuombee. Daima yatupasa
kuweka mbele yetu uwezo wa damu ya Kristo. Damu itakasayo maisha yetu, damu
ihifadhiyo maisha yetu, ndilo tumaini letu. Yatupasa kukua katika ujuzi wa thamani yake
isiyo na kifani, kwa maana inanena tu kwa ajili yetu wakati tunapodai wema wake kwa
imani, tukiihifadhi dhamiri yetu katika usafi na amani na Mungu.
Hiyo inawakilishwa kama damu inayosamehe, haiwezi kutenganishwa na ufufuo na
maisha ya Mkombozi wetu, inaonyeshwa kwa kielelezo cha mto unaotiririka daima
kutoka kwenye kiti cha enzi cha Mungu, yaani, maji ya mto ule wa uzima. ----- 7BC
947,948.UBINADAMU WA KRISTO NI MNYORORO WA DHAHABU Februari 11
Kwa kuwa hamna kuhani mkuu asiyeweza kuchukuana nasi katika mambo yetu ya
udhaifu; bali yeye alijaribiwa sawasawa na sisi katika mambo yote, bila kufanya dhambi.
Waebrania 4:15.
Ushindi na utii wa Kristo ni ule wa mwanadamu halisi. Katika maamuzi yetu, tunafanya
makosa mengi kwa sababu ya misimamo yetu yenye makosa kuhusu ubinadamu wa
Bwana wetu. Tunapoupa ubinadamu wake nguvu ambayo haiwezekani kwa mwanadamu
kuwa nayo katika mapambano yake na Shetani, basi, tunaharibu utimilifu wa ubinadamu
wake. Neema yake pamoja na nguvu zake anawapa wale wote wanaompokea kwa imani.
Utii wa Kristo kwa Baba yake ulikuwa ni utii ule ule unaotakiwa kwa mwanadamu.
Mwanadamu hawezi kuyashinda majaribu yote ya Shetani pasipo kuwa na uweza wa
Mungu kuunganishwa na utendaji wake. Ndivyo ilivyokuwa kwa Yesu Kristo;
aliushikilia uweza ule wa Mungu. Hakuja katika dunia yetu kutoa utii wa Mungu
mwenye uwezo kidogo kwa yule mwenye uweza zaidi, bali kama mwanadamu kuitii
Sheria Takatifu ya Mungu [Amri Kumi], na kwa njia hiyo yeye ni Kielelezo chetu.
Bwana Yesu alikuja katika ulimwengu wetu, si kuja kuonyesha kile ambacho Mungu
angeweza kufanya, bali kile ambacho mwanadamu angeweza kufanya kwa njia ya imani
katika uweza wa Mungu kusaidia katika kila hatari. Kwa imani, mwanadamu anatakiwa
kuwa mshiriki wa tabia ya uungu, na kulishinda kila jaribu linalomkabili.
Bwana anadai sasa kwamba kila mwana na binti ya Adamu, kwa njia ya imani katika
Yesu Kristo, apate kumtumikia katika ubinadamu wake ambao tunao hivi sasa. BwanaYesu ameliziba lile shimo kubwa ambalo lilisababishwa na dhambi. Ameiunganisha
mbingu na dunia, wanadamu wasiodumu na Mungu wa milele. Yesu, Mkombozi wa
ulimwengu, aliweza kuzishika Amri [Kumi] za Mungu kwa njia ile ile ambayo
wanadamu wote wanaweza kuzishika. ----- 7BC 929.
Hatupaswi kumtumikia Mungu kana kwamba sisi hatukuwa binadamu, bali yatupasa
kumtumikia Yeye katika hali ya kibinadamu tuliyo nayo, ambayo imekombolewa na
Mwana wa Mungu; kwa njia ya haki ya Kristo tutasimama mbele zake Mungu tukiwa
tumesamehewa, na kuwa kana kwamba hatukufanya dhambi kamwe. ----- 5BC 1142.
Ubinadamu wa Mwana wa Mungu ni kila kitu kwetu. Ni mnyororo ule wa dhahabu
unaozifunga roho zetu kwa Kristo, na kwa njia yake Kristo [zinafungwa] kwa Mungu. ---
-- 1SM 244.
MWOMBEZI [MTETEZI] WETU KWA BABA Februari 12
Watoto wangu wadogo, nawaandikia haya ili kwamba msitende dhambi. Na kama mtu
akitenda dhambi tunaye Mwombezi [Mtetezi] kwa Baba, Yesu Kristo mwenye haki. l
Yohana 2:1.
Ni mwangalifu jinsi gani Bwana wetu Yesu Kristo kwamba hawezi kumpa mtu hata
mmoja nafasi ya kukata tamaa. Jinsi gani anavyomzungushia mtu huyo kinga dhidi ya
mashambulio makali ya Shetani. Kama kwa njia ya majaribu mengi tunachukuliwa kwa
mshangao au tunadanganywa kufanya dhambi yo yote, Yeye hageuki na kutuacha sisi ili
tuangamie. La, la, hivyo sivyo alivyo Mwokozi wetu.... Alijaribiwa katika mambo yote
kama sisi, naye akiisha kujaribiwa hivyo, anajua jinsi ya kuwasaidia wao wanaojaribiwa.
Bwana wetu aliyesulibiwa anatuombea sisi mbele za Baba yake kwenye kiti kile cha
neema. Kafara yake ya upatanisho tunaweza kuiomba kwa ajili ya msamaha wetu, yaani,
kuhesabiwa haki kwetu, na utakaso wetu. Mwana-Kondoo yule aliyechinjwa ndiye
tumaini letu la pekee. Imani yetu inamtazama Yeye, inamshika Yeye kama Mmoja
awezaye kutuokoa kabisa, na ile harufu nzuri ya toleo hili linalotosha kabisa hukubalika
kwa Baba. ----- 7BC 948.
Iwapo wewe unafanya makosa na kudanganywa katika dhambi, usijisikie wakati huo
kwamba huwezi kuomba... bali mtafute Bwana kwa bidii zaidi. ----- Letter 6, 1893.Damu ya Yesu inawaombea wale waliorudi nyuma kwa nguvu na uwezo, yaani, wale
walioasi, watendao dhambi dhidi ya nuru kuu na upendo. Shetani husimama mkono wetu
wa kuume kutushtaki, na Mwombezi [Mtetezi] wetu anasimama mkono wa kuume wa
Mungu kutuombea sisi. Hajapoteza kesi hata moja aliyokabidhiwa. Twaweza
kumtumainia Mwombezi wetu; kwa maana anaomba kwa kudai haki yake Mwenyewe
kwa ajili yetu.... Anawaombea wale walio wanyonge mno, waliokandamizwa mno na
kuteseka, na wale wanaopata maonjo mengi sana na majaribu. Kwa mikono iliyoinuliwa
juu anaomba hivi, "Tazama, nimekuchora katika vitanga vya mikono yangu." Isaya
49:16. ----- 7BC 948.
Kama ningeweza, ningependa kutoa sauti ya furaha kuifikia miisho yote ya dunia hii,
nikisema, "Kama mtu akitenda dhambi tunaye Mwombezi kwa Baba, Yesu Kristo
mwenye haki." Lo, huo ni ukombozi wa thamani! Ni upana ulioje wa ukweli huu mkuu --
--- kwamba Mungu kwa ajili ya Kristo Mpendwa wake, anatusamehe sisi dakika ile ile
tunapomwomba kwa imani iliyo hai, tukiamini kwamba Yeye anaweza kabisa kufanya
hivyo! ----- RH, Sept. 21, 1886.
KIUNGO KATI YA MUNGU NA MWANADAMU Februari 13
Naye, kwa sababu hii, aweza kuwaokoa kabisa wao wamjiao Mungu kwa yeye; maana
yu hai sikuzote ili awaombee. Waebrania 7:25.
Kristo ndiye kiungo kati ya Mungu na mwanadamu. Ameahidi kutuombea Yeye
mwenyewe kwa kutumia jina lake. Anauweka wema wake wote wa haki yake upande wa
mwombaji. Kristo anamwombea mwanadamu, na mwanadamu, anapohitaji msaada kwa
Mungu, anajiombea mwenyewe mbele za Mungu, akitumia uweza wa mvuto wa yule
Mmoja aliyejitoa nafsi yake kwa ajili ya ulimwengu. Tunapokiri mbele za Mungu
kwamba tunautambua wema wake Kristo, harufu nzuri inatolewa kuambatana na dua
zetu. Lo, ni nani awezaye kuthamini rehema hii kuu na upendo! Tunapomjia Mungu, kwa
kupitia katika wema wa Kristo, tunafunikwa na mavazi yake ya ukuhani. Anatuweka
karibu sana ubavuni pake, akitukumbatia kwa mkono wake wa kibinadamu, na wakati uo
huo kwa mkono wake wa uungu anakishikilia kiti cha enzi cha Mwenyezi. Anauweka
wema wake kama manukato mazuri, katika chetezo kilicho mkononi mwetu ili kuzitia
nguvu dua zetu. Anaahidi kusikiliza na kujibu maombi yetu. ----- 6BC 1078Kila mmoja atakayejinasua kutoka katika utumwa na utumishi wa Shetani, na kusimama
chini ya bendera yenye damu ya Mfalme Imanueli atalindwa kwa njia ya maombezi yake
Kristo. Kristo, kama Mpatanishi wetu, aliye mkono wa kuume wa Mungu, daima
anatukumbuka, maana ni muhimu kwake kwamba atulinde sisi kwa maombezi yake
kama vile ilivyokuwa muhimu kwake kutukomboa sisi kwa damu yake. Akiachilia
kutushika hata kwa dakika moja tu, Shetani yu tayari kutuangamiza. ----- 6BC 1078.
Maombi ya wale walio waaminifu na wenye toba yanapopanda mbinguni, Kristo
anamwambia Baba yake, "Nitazichukua dhambi zao. Waache wasimame mbele zako
wakiwa hawana hatia yo yote." Anapozichukua dhambi zao kutoka kwao, anaijaza mioyo
yao na nuru tukufu ya ile kweli na upendo wake. ----- 7BC 930.
Hitaji letu la maombezi yake Kristo ni la kudumu. Siku kwa siku, asubuhi na jioni, moyo
mnyenyekevu unahitaji kuomba maombi ambayo yataleta majibu ya kupewa neema na
amani na furaha. "Basi, kwa njia yake yeye, na tumpe Mungu dhabihu na sifa daima,
yaani, tunda la midomo iliungamayo jina lake." Waebrania 13:l5. ----- 6BC 1078.
BILA WAA KATIKA UKAMILIFU WAKE KRISTO Februari 14
Yeye asiyejua dhambi alimfanya kuwa dhambi kwa ajili yetu, ili sisi tupate haki ya
Mungu katika Yeye. 2 Wakorintho 5:21.
Msamaha na kuhesabiwa haki ni kitu kile kile kimoja. Kwa njia ya imani, muumini
anapita kutoka katika hali ya mwasi, yaani, mwana wa dhambi na Shetani, kwenda katika
hali ya raia mtiifu wa Kristo Yesu, si kwa sababu ya wema wo wote ulio ndani yake, bali
kwa sababu Kristo anampokea kama mwana wake wa kupanga [kuchaguliwa]. Mwenye
dhambi anapokea msamaha wa dhambi zake, kwa sababu dhambi hizo zinachukuliwa na
yule aliye Badala yake na Mdhamini wake. Bwana anamwambia Baba yake aliye
mbinguni, akisema hivi: "Huyu ni mwanangu. Namwachilia kwa muda kutokana na
hukumu ya kifo, nampa hati ya bima ya maisha yangu ----- yaani, uzima wa milele -----
kwa sababu nimekuwa badala yake na kuteseka kwa dhambi zake hizo. Hata amekuwa
mwanangu mpendwa." Kwa njia hiyo mwanadamu, akiwa amesamehewa, na kuvikwa
mavazi mazuri ya haki ya Kristo anasimama mbele zake Mungu bila waa.... Ni haki yake Baba kutusamehe sisi maasi yetu na dhambi, kwa sababu Kristo amebeba
hatia yetu yote na kutuachilia kwa kitambo, akituhesabia haki yake mwenyewe. Kafara
yake inayatosheleza kabisa madai ya sheria [haki]. ----- 6BC 1070.
Wengi hujisikia ya kwamba mawaa ya tabia zao yanafanya isiwezekane kwao kukifikia
kipimo kile alichokiweka Kristo; lakini yale yote ambayo watu kama hao wanapaswa
kufanya ni kujinyenyekeza wenyewe chini ya mkono wenye nguvu wa Mungu kwa kila
hatua wanayokwenda; Kristo haikadirii thamani ya mtu kwa kiasi cha kazi anayofanya,
bali kwa roho ambayo kwayo kazi hiyo inafanyika.
Anapowaona wanadamu wanainyanyua mizigo yao mizito [ya kazi], wakiwa wanajaribu
kuibeba kwa moyo wa unyenyekevu, pasipo kujitumainia nafsi zao wenyewe, huku
wakimtegemea Yeye, basi, yeye anaongezea juu ya kazi yao ukamilifu na utoshelevu
wake, na Baba yake anaikubali [kazi hiyo]. Sisi tunakubalika ndani ya mpendwa huyo.
Kasoro zote alizo nazo mwenye dhambi hufunikwa kwa ukamilifu na utimilifu wake
Bwana aliye haki yetu. Wale ambao kwa nia safi, kwa moyo wenye toba, wanajitahidi
kwa unyenyekevu kuishi kulingana na matakwa yake Mungu, wanaangaliwa na Baba
kwa huruma na upendo mwingi; Anawaona hao kama watoto wake watiifu, na haki ile ya
Kristo inahesabiwa juu yao. ----- Letter 4, 1889.
IMANI INAYOMHESABIA MTU HAKI Februari 15
Basi tukiisha kuhesabiwa haki itokayo katika imani, na tuwe na amani kwa Mungu, kwa
njia ya Bwana wetu Yesu Kristo. Warumi 5:1.
Kuhesabiwa haki ni fumbo [lisiloeleweka] kwa wengi. Mwenye dhambi anahesabiwa
haki na Mungu wakati ule ule anapotubu dhambi zake. Anamwona Yesu juu ya msalaba
ule wa Kalvari.... Anaitegemea kafara ile ya upatanisho kuwa ndilo tumaini lake la pekee,
kwa njia ya toba yake kwa Mungu ----- kwa sababu Sheria [Amri Kumi] za Serikali yake
zimevunjwa ----- pamoja na imani yake kwa Bwana wetu Yesu Kristo kama ndiye yule
Mmoja awezaye kumwokoa na kumtakasa mwenye dhambi kutokana na kila uasi
[uvunjaji wa Amri Kumi] wake aliofanya.
Kazi ya Kristo ya upatanisho ilianzia na mwanzo wa hatia ya wanadamu na mateso na
huzuni zao, yaani, mara tu mwanadamu alipogeuka na kuwa mwasi. Sheria [Amri Kumi]
haikufutwa ili kuweza kumkomboa mwanadamu na kumleta katika umoja na Mungu.Walakini Kristo alichukua kazi ya kuwa mdhamini na Mwokozi wake alipogeuka na
kuwa DHAMBI KWA AJILI YA MWANADAMU, ili mwanadamu apate kuwa haki ya
Mungu ndani yake na kupitia kwake yule aliyekuwa na umoja na Baba. Wenye dhambi
wanaweza kuhesabiwa haki na Mungu wakati ule tu anapowasamehe dhambi zao, yaani,
kuwaondolea adhabu ile wanayostahili, na kuwafanya kana kwamba walikuwa wenye
haki kweli kweli na walikuwa hawajapata kufanya dhambi, akiwapokea kwa fadhili zake
Mungu na kuwatendea kana kwamba wao walikuwa wenye haki. Wanahesabiwa haki
kwa njia ya haki ya Kristo peke yake ambayo huwekwa juu yao. Baba humkubali
Mwanawe, na kwa njia ya kafara ile ya upatanisho ya Mwanawe anamkubali mwenye
dhambi yule....
Kuna maelfu wanaoiamini injili na Yesu Kristo kama Mkombozi wa ulimwengu huu,
lakini hawaokolewi kwa imani ile.... Hawatubu na kuwa na imani inayomshika Kristo
kama Mwokozi wao anayesamehe dhambi; imani yao hiyo haileti toba....
Imani ile inayomhesabia mtu haki sikuzote inaleta kwanza toba ya kweli, kisha
yanafuata matendo mema, ambayo ni tunda la imani ile. Hakuna imani yo yote iokoayo
ambayo haizai matunda mazuri. Mungu alimtoa Kristo kwa ajili ya ulimwengu wetu ili
apate kuwa badala yake yule mwenye dhambi. Dakika ile ile inapotumika imani
inayotegemea wema wa kafara ile ya thamani ya upatanisho, ikimkiri Kristo kuwa ni
Mwokozi wake, ndiyo dakika ambayo mwenye dhambi huyo anahesabiwa haki mbele za
Mungu, kwa sababu amesamehewa [dhambi zake]. ----- MS 46, 1891.
AMETUKUBALI KATIKA HUYO MPENDWA Februari 16
Na usifiwe utukufu wa neema yake, ambayo ametuneemesha [ametukubali] katika huyo
Mpendwa. Waefeso 1:6 [KJV].
Baba alimpa heshima yote Mwana wake, akimketisha mkono wake wa kuume, juu ya
falme zote na mamlaka. Alionyesha furaha yake kuu na kupendezwa naye sana kwa
kumpokea yule Msulibiwa, na kumvika taji ya utukufu na heshima. Na upendeleo wote
aliouonyesha kwa Mwanawe kwa kuukubali upatanisho wake mkuu, anauonyesha pia
kwa watu wake. Wale walioyaunganisha mapenzi yao kwa kumpenda Kristo
wanakubalika katika huyo Mpendwa. Waliteswa pamoja na Kristo katika kudhalilishwa
mno kwake, na kutukuzwa kwake ndiyo shauku yao kubwa, kwa sababu wamekubalika
ndani yake. Mungu anawapenda wao kama vile alivyompenda Mwanawe. Kristo, yaani,Imanueli, anasimama kati ya Mungu na muumini, akiudhihirisha utukufu wa Mungu kwa
wateule wake, na kuzifunika kasoro [upungufu] zao zote pamoja na dhambi zao kwa
mavazi ya haki yake mwenyewe isiyokuwa na waa. ----- 6BC 1115.
"BWANA huwaridhia wao wamchao, na kuzitarajia fadhili zake." Zaburi 147:11. Lakini
ni kwa njia ile tu ya thamani ya kafara ile iliyotolewa kwa ajili yetu sisi tunaweza
kuonekana kuwa na thamani machoni pake Bwana. Ni kwa ajili ya haki ya Kristo
tunayopewa tunahesabiwa na Mungu kwamba sisi tu wa thamani. Kwa ajili yake Kristo
anawasamehe wale wote wamchao. Haoni ndani yao uovu wa yule mwenye dhambi.
Anaitambua ndani yao sura ya Mwanawe, ambaye wanamwamini. Kwa njia hiyo tu
Mungu anaweza kupendezwa na kila mmoja wetu. "Bali wote waliompokea aliwapa
uwezo wa kufanyika watoto wa Mungu, ndio wale waliaminio jina lake." Yohana 1:12.
Kadiri Bwana anavyoiona tabia ya Mwanawe Mpendwa ikifunuliwa ndani ya watu wake
kwa ukamilifu zaidi, ndivyo kuridhika kwake kunavyozidi kuongezeka na kupendezwa
nao sana. Mungu Mwenyewe na ulimwengu ule wa mbinguni wanawashangilia na
kuimba nyimbo kwa sababu Kristo hakuwafia bure [amejipatia matunda]. Mwenye
dhambi aaminiye anatangazwa kwamba hana hatia yo yote, wakati uovu wake unawekwa
juu ya Kristo. Haki ya Kristo inawekwa katika akaunti ya mdaiwa huyo, na mbele ya jina
lake katika mizania inaandikwa, Amesamehewa. Uzima wa milele. ----- MS 39, 1896.
MKOMBOZI WETU NI JIWE LILILOJARIBIWA Februari 17
Kwa ajili ya hayo Bwana, MUNGU, asema hivi, Tazama, naweka jiwe katika Sayuni,
liwe msingi, jiwe lililojaribiwa, jiwe la pembeni lenye thamani, msingi ulio imara; yeye
aaminiye hatafanya haraka. Isaya 28:16.
Mkombozi wetu ni "Jiwe Lililojaribiwa." Jaribio limefanywa, kipimo kikuu kimetumika,
na kuleta mafanikio kamili. Ndani yake kusudi lote la Mungu limetimizwa kwa wokovu
wa ulimwengu huu uliopotea. Kamwe hapajapata kutokea wakati ambapo msingi
ulipimwa kwa jaribio kali sana kama lilivyopimwa hilo "Jiwe Lililojaribiwa." Bwana
Yehova alijua kiasi gani jiwe hilo la msingi lingeweza kustahimili. Dhambi za
ulimwengu wote zingeweza kulundikwa juu yake. Wateule wa Bwana wangedhihirishwa,
na malango yale ya mbinguni yangefunguliwa na kuachwa wazi kwa ajili ya wote ambao
wangeweza kuamini; utukufu usioelezeka wangepewa washindi. "Jiwe Lililojaribiwa" ndiye Kristo, limejaribiwa kwa upotovu [ukaidi] wa mwanadamu.
Wewe, Ee Mwokozi wetu, umebeba mzigo wetu. Umeleta amani na pumziko;
Umejaribiwa, umeshuhudiwa na waumini waliokuletea maonjo yao kupata huruma zako,
huzuni zao kupata upendo wako, majeraha yao kupata uponyaji wako, udhaifu wao
kupata nguvu zako, utupu wao ili wewe upate kuwajaza kabisa; na kamwe, kamwe
hakuna hata mtu mmoja uliyemkatisha tamaa. Ee Yesu, Jiwe langu Lililojaribiwa, naja
kwako, dakika kwa dakika. Mbele zako nainuliwa juu ya maumivu yote. "Toka mwisho
wa nchi nitakulilia nikizimia moyo, Uniongoze juu ya mwamba nisioweza kuupanda."
Zaburi 62:2.
Ni haki yetu kufurahia ushirika mtamu na Mungu wetu. Ni ya thamani kwa muumini
damu yake ya upatanisho, ni ya thamani haki yake inayotuhesabia haki. Basi, [ni wa
thamani] heshima hii ni kwenu ninyi mnaoamini." 1 Petro 2:7 [KJV].
Mimi ninapotafakari juu ya chemchemi hiyo yenye nguvu ya uhai ambayo tunaweza
kuichota, nalia na kuomboleza kwa kuwa wengi mno wanaipoteza furaha hiyo ambayo
wangeweza kuwa nayo kwa kuzitafakari fadhili [wema] zake. Yatupasa sisi kuwa wana
na binti za Mungu tukiendelea kukua na kuwa hekalu takatifu katika Bwana. "Basi tangu
sasa ninyi si wageni wala wapitaji, bali ninyi ni wenyeji pamoja na watakatifu, watu wa
nyumbani mwake Mungu. Mmejengwa juu ya msingi wa mitume na manabii, naye Kristo
Yesu Mwenyewe ni jiwe kuu la pembeni." Waefeso 2:19,20. Hii ndiyo haki yetu. -----
RH, Machi 19, 1895.
YESU NI RAFIKI YETU MWEMA SANA Februari 18
Ajifanyiaye rafiki wengi ni kwa uangamivu wake [Mtu aliye na marafiki hana budi
kujionyesha mwenyewe kuwa rafiki - KJV]; Lakini yuko rafiki aambatanaye na mtu
kuliko ndugu. Mithali 18:24.
Ni wachache mno jinsi gani wanaomtazama daima Mgeni huyo asiyeonekana, na
kutambua kwamba yuko mkono wao wa kuume! Ni wangapi wasiojali kuwapo Kwake!
Tungewatendea wengine kama tunavyomtendea Yesu, ni utovu wa adabu ulioje
wangetufikiria kuwa tunao!
Tuseme rafiki yetu alikuwa pamoja nasi, kisha njiani tungekutana na mtu
tunayefahamiana naye sana, halafu tukayaelekeza mawazo yetu yote kwa rafiki huyompya tuliyekutana naye, na kupuuzia kuwapo kwa rafiki yetu [tuliyekuwa naye tangu
mwanzo], watu wangekuwa na maoni gani juu ya uaminifu wetu kwa yule rafiki yetu [wa
kwanza], na kiwango cha heshima yetu kwake? Na hivyo ndivyo tunavyomtendea Yesu.
Tunasahau kwamba yeye ni mwenzi wetu. Tunaingia katika maongezi yetu, jina lake
hatulitaji kamwe.... Tunaongea juu ya mambo ya biashara ya kidunia, na pale ambapo
maongezi yetu hayawezi kuijeruhi roho, ambapo ni ya muhimu kwetu, hapo hatumvunjii
Yesu heshima, lakini tunamvunjia heshima hapo tunaposhindwa kulitaja jina lake katika
mazungumzo yetu na rafiki zetu pamoja na wale tunaoshirikiana nao. Yeye ndiye rafiki
yetu mwema [bora] sana, nasi tungetafuta nafasi za kuongea juu yake.... Daima
tungemweka katika upeo wa macho yetu. Mazungumzo yetu yangekuwa ya tabia ile
ambayo isingeweza kumletea Mungu chukizo. ----- ST, Jan. 9, 1893. Najua kwamba
katika mioyo mingi swali hili linajitokeza, "Wapi nitamwona Yesu?" Kuna wengi
wanaotaka kuwapo kwake, yaani, wanaotaka upendo na nuru yake; lakini hawajui
wanaweza kumtafuta wapi yule ambaye mioyo yao inamtamani sana. Hata hivyo, Yesu
hajifichi mbali; hakuna anayehitaji kumtafuta bure [bila kumwona]. "Tazama," yeye
asema, "nasimama mlangoni, nabisha; mtu akiisikia sauti yangu, na kuufungua mlango,
nitaingia kwake, nami nitakula pamoja naye, na yeye pamoja nami." Ufunuo 3:20. Yesu
anatualika tukubali kuwapo kwake; yatupasa kuufungua mlango wa moyo wetu, na
kumkaribisha ndani. Lakini Yeye hataki kukaa katika moyo uliogawanyika. Iwapo [moyo
huo] umetolewa kwa utumishi wa mali, iwapo uchoyo na kiburi vimejaa katika vyumba
vyake, basi, hapatakuwa na nafasi kwa ajili ya Mgeni huyo wa mbinguni; Hatafanya
makao yake ndani yetu mpaka hapo hekalu hilo la moyo wetu litakapowekwa tupu na
kutakaswa. Lakini hakuna haja ya kushindwa katika maisha haya ya Kikristo. Yesu
anangojea kufanya kazi kubwa kwa ajili yetu, na mbingu yote ina hamu kubwa sana juu
ya wokovu wetu. ----- RH, Nov.24, l885.
YESU YU KARIBU NASI SIKUZOTE Februari 19
Mara Yesu alinena, akawaambia, Jipeni moyo ni Mimi; msiogope. Mathayo 14:27.
Nawaza juu ya wanafunzi wale katika tufani ile kali; chombo chao kilikabiliana na pepo
kali na dhoruba. Wameacha juhudi zao kama ni kazi bure, na wakati mawimbi yale yenye
njaa yanaongea na mauti, katikati ya dhoruba hiyo umbile linalong'aa linaonekana
likitembea juu ya mawimbi yale yanayotoa povu juu yake.... Sauti inasikika katikati ya
ngurumo za dhoruba ile, ikisema, "Jipeni moyo ni mimi; msiogope."Lo, ni wangapi katika wakati huu wa hatari, wanajitahidi kusonga mbele dhidi ya
mawimbi makubwa yaliyo mbele yao! Mwezi na nyota huonekana kana kwamba
zimefichwa na mawingu ya dhoruba, na katika hali ile ya kukata tamaa na kufa moyo,
wengi wetu husema, "Ni kazi bure; juhudi zetu ni sawa na bure. Tutaangamia.
Tumejitahidi sana kupiga makasia, lakini bila mafanikio yo yote."... Yesu yu karibu sana
nasi katikati ya mandhari [matukio] za dhoruba na maonjo kama vile alivyokuwa kwa
wafuasi wake waliotoswa huku na huku juu ya Bahari ile ya Galilaya. Yatupasa kutulia,
bila kusitasita, imara, pasipo kutikisika katika kumtegemea Mungu.... Hivi sasa yatupasa
kuwa na uzoefu kila mmoja wake peke yake katika kumshikilia Mungu sana. Kristo
yumo ndani ya chombo chetu. Sadikini ya kwamba Kristo ndiye Nahodha wetu, kwamba
atatulinda, sio sisi tu, bali na meli yetu....
Usiku ule katika mashua ile kwa wanafunzi wale ilikuwa ni shule ambayo kwayo
wangeweza kupata elimu yao kwa kazi yao kubwa ambayo ilipaswa kufanywa baadaye.
Saa zile za giza za maonjo [majaribu] zitamjia kila mmoja kama sehemu ya elimu yake
kwa kazi ile ya juu zaidi, kwa juhudi yake ya ziada na kujitoa wakf. Dhoruba haikuletwa
kwa wanafunzi wale kuwafanya wavunjikiwe na chombo chao, bali kuwapima na
kuwathibitisha, kila mmoja peke yake....
Wakati wa kuelimishwa kwetu karibu sana utakoma. Hatuna wakati wa kupoteza kwa
kutembea katika mawingu ya mashaka na kutokuwa na hakika yo yote.... Twaweza
kusimama karibu kando ya Yesu. Hebu na asiwepo hata mmoja... atakayekwepa fundisho
mojawapo gumu au kupoteza mbaraka kwa jambo moja gumu la kumwadibisha.
Haidhuru hali ya maisha yetu iweje, pamoja na biashara zetu, tunaye Kiongozi wa
kuaminika. Haidhuru hali yetu ya maisha iweje, Yeye ndiye Mshauri wetu. Haidhuru
tuwe wapweke kiasi gani, Yeye ndiye Rafiki yetu ambaye daima tunaweza kumtegemea.
----- Letter 13, 1892.
NDIYE KIELELEZO CHETU KIKUU Februari 20
Kwa hiyo, ndugu watakatifu, wenye kuushiriki mwito wa mbinguni, mtafakarini sana
Mtume na Kuhani Mkuu wa maungamo yetu, Yesu [Kristo]. Waebrania 3:1.Namweka mbele yenu yule aliye Kielelezo chenu Kikuu.... Alipambana hasa na
kuyapinga majaribu ya Shetani kama ilivyo kwa ye yote miongoni mwa wana wa
wanadamu. Kwa maana hii ya pekee angeweza kuwa kielelezo kamili kwa mwanadamu.
Alijinyenyekeza kuchukua ubinadamu na kuyapitia majaribu yote ambayo mwanadamu
anaweza kukabiliana nayo. Alichukua juu ya nafsi yake udhaifu wote na kujitwika huzuni
zote za wana wa Adamu.
Alipaswa "kufananishwa na ndugu zake." Waebrania 2:17. Alijisikia furaha na huzuni
kama vile wao wanavyojisikia. Mwili wake uliweza kuchoka kama wako. Mawazo yake,
kama yalivyo yako, yangeweza kusumbuliwa na kufadhaishwa. Kama wewe unazo shida,
basi, naye vivyo hivyo alikuwa nazo. Shetani aliweza kumjaribu. Maadui zake
walimwudhi. Mamlaka zilizokuwa zinatawala ziliweza kuutesa mwili wake; askari wale
waliweza kumsulibisha; nao hawawezi kufanya zaidi ya hayo kwetu. Yesu alikabiliwa na
shida nyingi, mapambano na majaribu, akiwa kama mwanadamu. Akawa Kiongozi Mkuu
[Kapteni] wa wokovu wetu kwa njia ya mateso. Aliweza kubeba mizigo yake vizuri
kuliko sisi, kwa vile aliibeba pasipo malalamiko, pasipo harara, pasipo kukosa imani,
pasipo kunung'unika; lakini huo sio ushahidi kwamba alipata mateso pungufu kuliko
mwana ye yote wa Adamu anayeteseka....
Kipindi cha utoto na ujana wake kilikuwa hakijulikani vizuri, lakini ni cha maana sana.
Katika kutokujulikana kwake alikuwa anajenga msingi mzuri wa afya yake ya mwili na
akili yenye nguvu. "Akakua, akaongezeka nguvu rohoni." Luka 1:80. Si kama mtu yule
aliyeinama
chini kwa mzigo wa uzee, Yesu anaonekana kwetu akitembea kupitia katika vilima vile
vya Yudea. Alikuwa katika nguvu zake za ujana. Yesu alisimama zamani akiwa na umri
kama ule ulio nao wewe.* Mambo yako, mawazo yako katika kipindi hiki cha maisha
yako, Yesu alikuwa nayo. Hawezi kukusahau wewe katika kipindi hiki cha hatari.
Anaziona hatari zako [zinazokujia]. Anayajua majaribu yako. Anakualika wewe ufuate
kielelezo chake. ----- Letter 17, 1878.
__________________________
* Dondoo hili limetoka katika barua aliyomwandikia mwanaume mmoja kijana.KUAKISI SURA YA KRISTO Februari 21
Lakini sisi sote, kwa uso usiotiwa utaji, tukiurudisha utukufu wa Bwana, kama vile
katika kioo, tunabadilishwa tufanane na mfano uo huo, toka utukufu hata utukufu, kama
vile kwa utukufu utokao kwa Bwana, aliye Roho. 2 Wakorintho 3:18.
Kumtazama Yesu, kuzungumza sana juu ya wema wake, fadhili zake, na utakatifu wake,
mambo hayo yatatia moyoni mwako chuki kubwa kwa kile ambacho ni dhambi, na kutia
shauku kuu na kiu ya haki ndani yake. Kadiri tunavyoendelea kumfahamu Yesu kwa
karibu sana, ndivyo kadiri tutakavyozidi kuziona kasoro [upungufu] katika tabia zetu:
hapo ndipo utapaswa kuyaungama mambo hayo kwa Yesu na kwa njia ya toba ya kweli
itokayo moyoni utashirikiana na uweza wa Mungu, Roho Mtakatifu, kuyaondolea mbali
mambo hayo [mabaya]. ----- Letter 10, 1893.
Ni Roho Mtakatifu, Mfariji [Msaidizi], ambaye Yesu alisema angemtuma ulimwenguni
humu, ambaye anazibadilisha tabia zetu zipate kufanana na sura ya Kristo; na jambo hilo
linapofanyika, sisi tunaakisi, kama vile katika kioo, utukufu wake Bwana. Yaani, tabia ya
yule anayemtazama hivyo Kristo hufanana sana na yake, hata mtu anayemtazama anaiona
tabia ya Kristo yenyewe ikiangaza nje kama vile katika kioo. Pasipo sisi wenyewe
kutambua tunabadilishwa siku kwa siku kutoka katika njia na nia zetu wenyewe kwenda
katika njia zake na nia ya Kristo, yaani, katika uzuri wa tabia yake. Kwa njia hiyo
tunakua katika Kristo, na bila kutambua tunaakisi sura yake. ----- 6BC 1097
Sio kwa kutazama mbali naye tunaweza kuiga maisha ya Yesu, bali ni kwa kuongea juu
yake, kwa kuzungumza sana juu ya ukamilifu wake, kwa kutafuta kuzitakasa tamaa zetu
za chakula na kuikuza tabia yetu, kwa kujitahidi, kwa njia ya imani na upendo, na kwa
juhudi ya dhati na ya kudumu, tukikichuchumilia kiolezo kile kikamilifu. Kwa kumjua
Kristo ----- maneno yake, mazoea yake, na mafundisho yake ----- tunaazima wema wa
tabia yake ambayo tumejifunza kwa karibu sana, na kujazwa na moyo ule ule
tulioutamani sana. Yesu kwetu anakuwa "mashuhuri miongoni mwa elfu kumi," na
Mmoja aliye "mzuri sana pia pia." ----- 6BC 1098,1099.
Moyo unapoletwa katika uhusiano wa karibu sana na yule Mwasisi Mkuu wa nuru na
kweli, picha inapigwa juu yake ikiudhihirisha uhusiano wake halisi mbele za Mungu.
Hapo ndipo nafsi itakufa, kiburi kitashushwa chini, na Kristo atachora sura yake kwa
mistari inayokwenda chini sana ndani ya moyo huo. ----- 6BC 1099.KUMPENDA KRISTO Februari 22
Maana ilitupasa sisi tuwe na kuhani mkuu wa namna hii aliye mtakatifu, asiyekuwa na
uovu, asiyekuwa na waa lo lote, aliyetengwa na wakosaji, aliyekuwa juu kuliko mbingu.
Waebrania 7:26.
Tabia ya Kristo ilikuwa moja yenye uzuri usiokuwa na kifani, ndani yake ikiwa na kila
kitu kilicho safi, cha kweli, kizuri, na chenye sifa njema. Hatujui habari yo yote kama
aliwahi kutembelea sherehe yo yote ya anasa au ukumbi wa dansi, na hata hivyo yeye
alikuwa ndiye utimilifu wa neema, tena alikuwa na umbile la kifalme. Kristo hakuwa
mwanafunzi [hakusoma shule]; alijulikana kwa kuwa na akili nyingi hata mapema katika
maisha yake. Ujana wake haukupotea bure kwa kuwa mvivu, wala haukupotea kwa
kujifurahisha kwa tamaa za mwili wake, wala kwa kujiendekeza kuuridhisha mwili wake
kwa kutumia vitu vinavyodhuru afya, au kupoteza wakati wake bure kwa mambo
yasiyokuwa na faida yo yote. Tangu utoto wake mpaka utu uzima hakuitumia vibaya saa
yake hata moja, wala hakuna saa zo zote alizozembea....
Yesu alikuwa hana dhambi wala hakuwa na hofu yo yote juu ya athari za dhambi. Hali
yake ilikuwa kama yako isipokuwa katika jambo hilo moja [la kutokuwa na dhambi].
Wewe huna shida hata moja ambayo haikumlemea Yeye, wala huna huzuni hata moja
ambayo moyo wake haujapata kuipitia. Hisia zake ziliweza kuumia, kwa urahisi kama
vile wewe unavyoumia, kwa kutojaliwa na watu, na kwa marafiki zake kutomtia
maanani. Je! njia yako ina miiba? Njia yake Kristo ilikuwa vivyo hivyo mara kumi zaidi.
Je! una dhiki? Ndivyo naye alivyokuwa nayo. Ni kwa uzuri jinsi gani Kristo aliandaliwa
kuwa Kielelezo chetu!...
Kumbukumbu ile Iliyovuviwa inasema hivi juu yake: "Naye Yesu akazidi kuendelea
katika hekima na kimo, akimpendeza Mungu na wanadamu." Luka 2:52. Alipoongezeka
umri wake, alizidi kuendelea katika ujuzi. Aliishi kwa kiasi; saa zake za thamani
hazikupotezwa katika anasa zile zinazouharibu mwili. Alikuwa na mwili wenye afya
kamili na nguvu halisi za akili. Nguvu zake za mwili na za akili zingeweza kuendelezwa
na kukuzwa kama zako au za kijana ye yote mwingine. Neno la Mungu lilikuwa ndilo
somo lake, kama linavyopasa kuwa lako.
Mchukue Yesu kuwa kipimo chako. Yaige maisha yake. Ipende tabia yake. Tembea
kama Kristo alivyotembea. Chimbuko jipya utapewa kwa akili zako, yaani, upeo mpanazaidi wa mawazo yako, unapozileta nguvu zako kugusana kwa nguvu na mambo yale ya
milele ambayo ndani yake ni makuu na ya kuridhisha. ----- Letter 17, 1878.
UTUKUFU NA UWE KWA MUNGU Februari 23
Simoni Petro, mtumwa na mtume wa Yesu Kristo, kwa wale waliopata imani moja na
sisi, yenye thamani, katika haki ya Mungu wetu, na Mwokozi Yesu Kristo. 2 Petro 1:1.
Ni neno kuu jinsi gani kwetu kulitafakari ----- haki ya Mungu na Mwokozi wetu Yesu
Kristo! Kumtafakari Kristo na haki yake hakuachi nafasi yo yote kwa haki yetu
wenyewe, yaani, kwa kuitukuza nafsi yetu. Katika sura hii hakuna kusimama mahali
pamoja. Kuna kusonga mbele daima kwa kila hatua katika kumjua Kristo....
Ndani ya Mungu twapaswa kujitukuza. Nabii anasema, "BWANA asema hivi, Mwenye
hekima ajisijifu kwa sababu ya hekima yake, wala mwenye nguvu asijisifu kwa sababu
ya nguvu zake, wala tajiri asijisifu kwa sababu ya utajiri wake; bali ajisifuye na ajisifu
kwa sababu hii, ya kwamba ananifahamu mimi, na kunijua, ya kuwa mimi ni BWANA,
nitendaye wema, na hukumu, na haki, katika nchi; maana mimi napendezwa na mambo
hayo, asema BWANA." Yeremia 9:23,24....
Tumeitwa ili tupate kumjua Kristo, na jambo hilo linamaanisha kwamba sisi tuwe na
maarifa ya utukufu na wema wake. Ni ujuzi wa tabia ile kamilifu ya Mungu,
iliyodhihirishwa kwetu ndani ya Yesu Kristo, ambayo inatufungulia sisi mlango wa
mawasiliano na Mungu....
Kwa shida mno akili ya kibinadamu inaweza kufahamu upana na kina na kimo cha
mafanikio ya kiroho yanayoweza kufikiwa kwa njia ya kuwa washirika wa tabia ile ya
Uungu. ----- YI, Okt.24, 1895.
Natamani kuzungumza na vijana wanaume na wanawake ambao wako tayari sana
kuvifikia viwango vile vilivyo duni tu. Laiti kama Bwana angaliiongoza mioyo yao kujua
maana ya ukamilifu wa tabia! Laiti kama wangaliijua imani ile itendayo kazi kwa
upendo, inayoutakasa moyo! Tunaishi katika siku za hatari kubwa. Ni Kristo peke yake
anayeweza kutusaidia na kutupatia ushindi. Kristo sharti awe vyote kwetu; hana budi
kukaa moyoni; maisha yake lazima yazunguke ndani yetu, kama vile damu
inavyozunguka katika mishipa ya damu. Roho wake sharti awe ndiye uwezo wetuunaotutia nguvu utakaotuwezesha kutoa mvuto wetu kwa wengine ili nao wawe kama
Kristo, yaani, wawe watakatifu. ----- YI, Okt.31, 1895.
Kama vijana wetu wangezizingatia sheria zilizowekwa katika sura hii, na kuziweka
katika vitendo, ni mvuto ulioje wangekuwa nao kwa upande wa haki! ----- YI, Okt.31,
1895.
ZOEZI LA KIWANGO CHA JUU SANA LA NGUVU ZETU Februari 24
Na uzima wa milele ndio huu, Wakujue wewe, Mungu wa pekee wa kweli, na Yesu
Kristo uliyemtuma. Yohana 17:3.
Kumjua na kumfurahia Mungu ni zoezi la kiwango cha juu sana la nguvu za
mwanadamu. Hilo linaweza kuzingatiwa tu kama mapenzi yetu yametakaswa na
kuboreshwa kwa neema yake Kristo.... Ndani ya Kristo ulikuwamo mng'ao wa utukufu
wa Baba yake, chapa ya nafsi yake. Alisema Mwokozi wetu, "Aliyeniona mimi
amemwona Baba." Yohana 14:9. Ndani yake Kristo umo uzima wa roho zetu. Mioyo
yetu inapomwelekea Yeye, katika shauku yetu kuu ya dhati na upendo katika kutaka
uzuri wake usio na kifani, katika kutafuta kwetu kwa bidii utukufu wake, tunapata uzima.
Tunapoyaacha mambo madogo madogo yasiyo na maana sana kujaza mawazo yetu, na
kumsahau Kristo, tukimpa kisogo na kukubali urafiki na mwingine, basi, tunaiweka
miguu yetu katika njia ile iendayo mbali na Mungu na mbali na mbinguni. Kristo hana
budi kuwa kitovu cha mapenzi yetu yote, hapo ndipo tutakapoishi ndani yake, ndipo
tutakapopata roho yake....
Ni kitu gani kinachoifanya mbingu kuwa na mng'ao wake? Furaha ya waliokombolewa
itakuwa katika kitu gani? Kristo ni vyote na ndani ya yote. Wataangaza macho yao kwa
furaha isiyoneneka kumtazama Mwana-Kondoo wa Mungu. Wataimba nyimbo zao za
shukrani na sifa na heshima kubwa kwa yule waliyempenda na kumwabudu hapa
[duniani]. Wimbo ule walijifunza na kuanza kuuimba walipokuwa hapa duniani.
Walijifunza kuliweka tumaini lao kwa Yesu wakati walipokuwa wanakuza tabia zile
zitakazofaa kuingia nazo mbinguni. Mioyo yao ilikuwa imepatana na mapenzi yake hapa.
Furaha yao ndani ya Kristo itakuwa katika kiwango kile kile cha upendo na tumaini
walilojifunza kwa kumwamini Yeye walipokuwa hapa. ----- RH, Mei 30, 1882. Ni lazima Mungu awe ndani ya mawazo yetu daima. Ni lazima tuzungumze naye
tunapotembea njiani, na wakati ule mikono yetu inaposhughulika kufanya kazi. Katika
makusudi yetu yote na mambo tunayoyatafuta katika maisha yetu inatupasa kujiuliza
swali hili, Hivi Bwana anataka mimi nifanye nini? Nitawezaje kumpendeza Yeye aliyetoa
maisha yake kuwa fidia kwa ajili yangu? Hivyo ndivyo tunavyoweza kutembea pamoja
na Mungu, kama alivyofanya yule Henoko wa zamani; na ushuhuda ule kwamba
alimpendeza Mungu unaweza kuwa wetu sisi. ----- RH, Mei 30, 1882.
TUKAENDELEE KUMJUA BWANA Februari 25
Nasi na tujue, naam, tukaendelee kumjua BWANA; kutokea kwake ni yakini kama
asubuhi; naye atatujilia kama mvua, kama mvua ya vuli iinyweshayo nchi. Hosea 6:3.
Twaweza kudhani ya kwamba tunajua kitu fulani juu ya kweli na Biblia, lakini ufunuo
wa ile kweli umepita upeo wa maono yetu mafupi yanavyoweza kufahamu. Kristo
anatuongoza sisi. Tutakaponyakuliwa kukutana naye angani, na kuingia katika mji ule wa
Mungu kupitia katika malango yale ya lulu, atatuongoza kando ya maji yale ya uzima, na
wakati wote atatufundisha na kuzungumza nasi juu ya mambo yale ambayo angekuwa
ametufunulia tupate kuyafahamu tulipokuwa duniani kama tungeweza kuyastahimili.
Lakini hatwendi kasi itakiwavyo. Tunarudi nyuma kwa hatua nyingi mno. Hatusongi
mbele kwenda mbinguni; kwa ajili hiyo, nuru ile ambayo ingetujia kwa mionzi ya
utukufu, haikuweza kutufikia kwa sababu sisi hatukuwa tayari kuipokea. Tunaenda hatua
moja nyuma ulimwenguni, kwenye anasa za dunia, ndipo tena tunachukua hatua moja
kwenda mbinguni, halafu tunachukua hatua moja kwenda nyuma, na kisha tunachukua
hatua moja kwenda mbinguni.
Iwapo mtaendelea kumjua Bwana, hapo ndipo mtakapojua kwamba kutokea kwake ni
yakini kama asubuhi. Mnaujua mwanga ule wa asubuhi ya kwamba unatokea kwetu
kwanza katika nuru iliyo na utusitusi, kisha inaongezeka na kuzidi kuongezeka katika
mng'ao wake mpaka hapo mfalme huyo wa mchana [jua] anapotembea mbinguni kwa
utukufu wake wote, yaani, kwa uzuri wake wote....
Sasa iwapo tutaendelea kumjua yeye, na iwapo hatutarudi nyuma hatua moja au mbili
mara kwa mara, na kulazimika kuzikusanya nguvu zetu tena na kusonga mbele ----- ni
bora kuzikusanya nguvu zetu kuliko kubaki katika hali ya kurudi nyuma na kuzidi kurudi
nyuma, lakini natamani kwamba tusingepoteza muda wetu mwingi sana na nguvu zetu
nyingi sana ----- basi, tutaweza kumjua Mungu zaidi na kujua habari zaidi za mbinguni,
na kuifahamu vizuri zaidi kweli ile yenye thamani na mibaraka tele aliyo nayo Mungukwa ajili yetu iwapo tu tutaweza kuijua. Ameandaa mambo ya ajabu sana kwa ajili yetu. -
---- MS 49, 1894.
MSHIPI [MKANDA] WA FURAHA Februari 26
Uligeuza matanga yangu kuwa machezo; Ulinivua gunia, ukanivika [mshipi wa] furaha.
Zaburi 30:11 [KJV].
Wengi wanaotafuta furaha watakatishwa tamaa katika matumaini yao, kwa sababu
wanakosea namna ya kuitafuta. Furaha ya kweli haipatikani katika kuifurahisha nafsi,
bali katika njia ile ya uwajibikaji. Mungu anataka mwanadamu awe na furaha, na kwa
ajili hiyo alimpa kanuni za Sheria yake [Amri Kumi], ili kwa kuzitii apate kuwa na furaha
nyumbani mwake na mbali. Anaposimama katika ukamilifu wake wa kimaadili, akiwa
mwaminifu kwa kanuni hizo, akizidhibiti nguvu zake zote, hawezi kusononeka. Vikonyo
vyake vikijinyonga kumzunguka Mungu, mtu huyo atasitawi katikati ya kutokuamini na
upotovu. Lakini wengi wanaotarajia kupata furaha wanashindwa kuipata, kwa sababu,
kwa kudharau wajibu wao ulio mdogo na kutozizingatia heshima ndogo ndogo za maisha
haya, wanazivunja kanuni ambazo furaha inazitegemea [imejengwa juu yake]. ----- RH,
Sept. 1, 1885.
Mikondo ya maisha ya kiroho haitakiwi kutuama. Maji yale ya chemchemi iliyo hai
hayana budi kuwa ndani yetu, yaani, kisima cha maji kinachobubujikia uzima wa milele,
na kuufagilia mbali uchoyo [kujipenda nafsi] ulio ndani ya moyo usioongoka.... Wengi
huweka vizuizi kati yao na Yesu hata upendo wake usipate nafasi ya kububujika mioyoni
mwao, na hapo ndipo wao hulalamika kwamba hawamwoni yule aliye Jua la Haki. Hebu
na waisahau nafsi yao na kuishi kwa ajili ya Yesu, ndipo nuru ile ya Mbinguni
itakapowaletea furaha mioyoni mwao....
Ukweli kwamba Yesu alikufa kwa ajili ya kuileta furaha na mbingu mahali tunapoweza
kuifikia ungekuwa neno letu kuu la kushukuru daima. Uzuri uliowekwa mbele yetu
katika viumbe alivyoviumba Mungu, ungeleta furaha mioyoni mwetu. Tunajifungulia
wenyewe milango ya mafuriko ya balaa au furaha. Iwapo tunayaruhusu mawazo yetu
kushughulika sana na taabu zetu na mambo madogo madogo ya ulimwengu huu, mioyo
yetu itajazwa na kutokuamini [mashaka], huzuni, na hisia za mambo mabaya
yanayotarajiwa [kutokea]. Iwapo tunayaweka mapenzi yetu katika mambo yale yaliyo
juu, sauti ya Yesu itatamka amani kwa mioyo yetu; manung'uniko yatakoma; mawazoyanayokera yatapotea katika sifa zitakazotolewa kwa Mkombozi wetu. Wale wanaoongea
sana juu ya fadhili kuu za Mungu, wala hawavidharau vipawa vyake vidogo, watajivika
mshipi wa furaha, na kuimba nyimbo mioyoni mwao kwa Bwana. ----- RH, Sept. 22,
1885.
MAISHA YENYE LENGO Februari 27
Heri ambaye Mungu wa Yakobo ni msaada wake, Na tumaini lake ni kwa BWANA,
Mungu wake. Zaburi 146:5.
Usalama wako wa pekee na furaha yako ni katika kumfanya Kristo kuwa Mshauri wako
wa kudumu. Unaweza kuwa na furaha ndani yake iwapo huna rafiki mwingine katika
dunia hii pana. Hisia zako za kukosa amani na shauku ya kukumbuka nyumbani kwenu,
au upweke huenda vikaja kwako kwa faida yako. Baba yako aliye mbinguni ana maana
ya kukufundisha wewe ili upate ndani yake urafiki na upendo na faraja kukidhi
matumaini yako ya dhati pamoja na tamaa zako....
Usiwe na wasiwasi kupita kiasi juu ya jambo lo lote. Nenda zako kwa utulivu kutekeleza
wajibu wako ambao siku hiyo inakuletea. Fanya kila unaloweza; mwombe Mungu awe
msaidizi wako.... Kila siku jisikie na kusema, "Mimi ninafanya kazi yangu kwa ajili yake
Mungu. Mimi siishi kwa ajili ya nafsi yangu mwenyewe, yaani, kujitukuza mwenyewe,
bali kumtukuza Mungu." Mtegemee Yesu, wala sio moyo wako mwenyewe! Umtwike
mzigo wako pamoja na wewe mwenyewe uwe juu yake. Endapo husikii furaha yo yote,
wala faraja yo yote, usikate tamaa. Tumaini tu na kusadiki. Unaweza kupata uzoefu wa
thamani katika mambo ya Mungu. Pambana na kukata tamaa kwako pamoja na mashaka
yako mpaka upate ushindi dhidi ya mambo hayo katika jina la Yesu. Usijiendekeze kuwa
na huzuni, kukata tamaa, na kuwa na mashaka.... Tulia katika ahadi za Mungu, pana na za
hakika. Pumzika katika ahadi hizo, pasipokuwa na shaka lo lote. ----- Letter 2b, 1874.
Nimeona kwamba wale wanaoishi kwa lengo, wakitafuta jinsi ya kuwanufaisha watu na
kuwaletea mibaraka wanadamu wenzao na kumheshimu na kumtukuza Mkombozi wao,
hao ndio walio na furaha ya kweli duniani, ambapo mtu yule asiyetulia, asiyeridhika, na
yule anayetafuta hiki na kukijaribu kile, akitumainia kupata furaha, analalamika sikuzote
kwa kukatishwa tamaa. Daima ni mhitaji, hatosheki kamwe, kwa sababu anaishi kwa ajili
ya nafsi yake peke yake. Hebu na liwe kusudi lako kutenda mema, kufanya sehemu yako
kwa uaminifu katika maisha haya. ----- Letter 17, 1872.Tafuta muda fulani wa kuweza kuufariji moyo wa mtu mwingine, kumbariki kwa neno
la upole, linalochangamsha moyo wa yule anayepambana na majaribu na pengine mateso.
Katika njia hiyo ya kumbariki mwingine kwa maneno ya kuchangamsha, yenye
matumaini, ukimwelekeza kwa yule aliye Mchukuzi wa Mizigo, unaweza kujipatia
amani, furaha, na faraja wewe mwenyewe bila kutazamia. ----- Letter 2b, 1874.
FURAHA ISIYONENEKA, YENYE UTUKUFU Februari 28
Naye mwampenda, ijapokuwa hamkumwona; ambaye ijapokuwa hamwoni sasa,
mnamwamini; na kufurahi sana, kwa furaha isiyoneneka, yenye utukufu. 1 Petro 1:8.
Kristo amesema, "Mtu akiona kiu, na aje kwangu anywe." Yohana 7:37. Je, umeimaliza
chemchemi hiyo? ----- La; kwa maana haiwezi kuisha kamwe. Mara tu unapojisikia kuwa
unalo hitaji, unaweza kunywa, na kunywa tena. Chemchemi hiyo sikuzote imejaa. Nawe
ukiisha kunywa mara moja kutoka katika chemchemi hiyo, hutatafuta kuizima kiu yako
katika visima vilivyokauka vya ulimwengu huu; hutajifunza namna ya kujipatia
mwenyewe anasa nyingi mno, burudani, michezo, na mizaha. La; kwa sababu umekuwa
ukinywa kutoka kwenye mto unaoufurahisha mji wa Mungu. Hapo ndipo furaha yako
itakuwa tele. ----- RH, Maachi 15, 1892.
Kwa nini dini ya Kristo isiwakilishwe kama ilivyo hasa, kama dini iliyojaa mvuto na
nguvu? Kwa nini sisi tusionyeshe mbele ya ulimwengu huu uzuri wake Kristo? Kwa nini
hatuonyeshi kwamba tunaye Mwokozi aliye hai, Mmoja awezaye kutembea nasi gizani
na katika nuru, na kwamba sisi tunaweza kumtegemea Yeye?...
Tumeyaona mawingu yanapoingia kati yetu na jua, lakini hatujaomboleza na kujivika
magunia kwa hofu kwamba tusingeweza kuliona jua tena. Hatukuonyesha wasiwasi wo
wote juu yake, bali kwa kuwa na uchangamfu mwingi kadiri ilivyowezekana tulingojea
mpaka wingu lile lilipopita na kulifunua jua. Hivyo ndivyo ilivyo katika maonjo na
majaribu yetu. Mawingu yanaweza kuonekana na kuifunika mionzi inayong'aa ya Jua lile
la Haki [Kristo]; lakini tunajua kwamba uso wa Mkombozi wetu haujafichwa milele.
Anatutazama kwa upendo na huruma nyingi. Hebu na tusiutupilie mbali ujasiri wetu,
ambao una thawabu kuu, walakini mawingu hayo yanapotanda juu ya moyo wetu, hebu
na tukaze macho yetu pale tuwezapo kumwona yule Jua la Haki, na kushangilia kwamba
tunaye Mwokozi aliye hai. Fikiria jinsi nuru ile tuliyoifurahia ilivyokuwa nzuri, kazamoyo wako juu ya Yesu, na nuru ile itaangaza tena juu yetu, na mawazo hayo ya huzuni
yatatoweka. Tutakuwa na furaha ndani ya Kristo, nasi tutakuwa tunaimba katika njia yetu
tukielekea kwenye Mlima Sayuni. ----- RH, Machi 15, 1892.
KRISTO, NGAZI ILE IFIKAYO MBINGUNI Machi 1
Akaota ndoto, na tazama, ngazi imesimamishwa juu ya nchi, na ncha yake yafika
mbinguni. Tena, tazama, malaika wa Mungu wanapanda, na kushuka juu yake. Mwanzo
28:12.
Hebu na tuitafakari ngazi hiyo iliyoonyeshwa kwa Yakobo.... Dhambi ya Adamu ilikata
mawasiliano yote kati ya mbingu na dunia. Mpaka dakika ile ya uasi wa mwanadamu
dhidi ya Sheria ya Mungu [Amri Kumi] palikuwa na mawasiliano huria kati ya dunia hii
na mbingu. Ziliunganishwa kwa njia ile aliyopitia Mungu. Lakini uasi wa Sheria ya
Mungu uliikata njia ile na mwanadamu akawa ametenganishwa na Mungu....
Kila kiungo kilichoifunga dunia hii kwa mbingu na mwanadamu kwa Mungu wa milele
kikaonekana kuwa kimevunjika. Mwanadamu angeweza kuitazama mbingu, lakini, je!
angewezaje kuipata? Lakini basi, furaha ni kwa ulimwengu huu! Mwana wa Mungu,
asiyekuwa na dhambi, aliye na utii mkamilifu, anakuwa njia ambayo kwayo mawasiliano
yale yaliyopotea yanarudishwa upya, njia ile ambayo kwayo paradiso [peponi] iliyopotea
inaweza kupatikana tena. Kwa njia ya Kristo, aliye Badala na Mdhamini wa
mwanadamu, mwanadamu anaweza kuzishika Amri [Kumi] za Mungu. Anaweza
kuurudia utii wake na Mungu atamkubali. Kristo ndiye ngazi ile. "Mtu akiingia kwa
mimi, ataokoka, ataingia na kutoka, naye atapata malisho." Yohana 10:9.
Ngazi hiyo ni ya mawasiliano kati ya Mungu na mwanadamu. Kwa njia ya ngazi hiyo ya
ajabu injili ilihubiriwa kwa Yakobo. Kama vile ngazi ilivyotoka duniani na kufika
kwenye mbingu zile za juu sana, na utukufu wa Mungu ulionekana juu ya ngazi ile, hivyo
ndivyo Kristo katika asili yake ya Uungu alivyoufikia ukuu mno na kuwa umoja na Baba
yake. Kama vile ngazi ile, ijapokuwa mwisho wake ulipenya na kuingia mbinguni,
ilivyokuwa na kitako chake duniani, hivyo ndivyo Kristo naye, japokuwa yeye ni Mungu,
alivyoufunika uungu wake kwa ubinadamu, naye akawa duniani humu akiwa "ana umbo
kama mwanadamu" (Wafilipi 2:8). Ngazi hiyo isingefaa kitu kama isingekaa juu ya dunia
hii au isingefika mbinguni.
Mungu alionekana katika utukufu wake juu ya ngazi ile, akiangalia chini kwa huruma
nyingi kumtazama yule Yakobo mwenye makosa na dhambi.... Ni kwa njia ya Kristo
Baba anamwangalia mwanadamu mwenye dhambi.... Viungo [vya ngazi] vilivyovunjika
vimetengenezwa tena. Njia kuu imewekwa iendayo juu ambamo wale waliochoka sana
na kulemewa na mizigo mizito wanaweza kupita. Wanaweza kuingia mbinguni na kupata
pumziko lao. ----- MS 13, 1884.
HAZINA YA THAMANI YA IMANI Machi 2Neema na iwe kwenu na amani iongezwe katika kumjua Mungu na Yesu Bwana wetu.
Kwa kuwa uweza wake wa Uungu umetukirimia vitu vyote vipasavyo uzima na utauwa,
kwa kumjua yeye aliyetuita kwa utukufu wake na wema wake mwenyewe. 2 Petro 1:2,3.
"Simoni Petro, mtumwa na mtume wa Yesu Kristo, kwa wale waliopata imani moja na
sisi, yenye thamani katika haki ya Mungu wetu, na Mwokozi Yesu Kristo.... Tena kwa
hayo ametukirimia ahadi kubwa mno, za thamani, ili kwamba kwa hizo mpate kuwa
washirika wa tabia ya Uungu, mkiokolewa na uharibifu uliomo duniani kwa sababu ya
tamaa." 2 Petro 1:1-4.
"Imani moja na sisi, yenye thamani"... ni imani ya kweli. Sio imani ile isiyozaa matunda.
Imani ya kweli iokoayo ndiyo hazina ya thamani kuu isiyopimika. Sio imani ya juu juu
tu. Mwenye haki huishi maisha halisi ya kiroho kama yale ya Kristo kwa imani. Ni kwa
njia ya imani hatua hizo huchukuliwa, hatua moja kwa wakati mmoja, kupanda juu ya
ngazi hiyo ya maendeleo. Imani hiyo haina budi kukuzwa. Inaiunganisha tabia ya
kibinadamu na ile ya uungu.
Maisha ya utii kwa Amri zote [Kumi] za Mungu ndiyo maisha ya maendeleo, yaani,
maisha ya kusonga mbele daima. Kadiri wateule, wale wa thamani, wanavyoongezewa
ufahamu wa kazi ya Yesu Kristo ya Upatanisho [Maombezi], ndivyo wanavyoziona na
kuzishikilia ahadi tele za thamani ambazo zinakuja kwa njia ya haki yake Kristo. Kadiri
wanavyozidi kupokea neema ya Mungu, ndivyo kadiri wanavyoufanyia kazi mpango ule
wa kuongeza.
"Neema na amani" vitazidishwa kwa njia ya "kumjua Mungu na Yesu Bwana wetu."
Hapa ndipo lilipo Chimbuko la nguvu zote za kiroho, na imani ni lazima itumike daima,
kwa maana maisha yote ya kiroho yanatoka kwa Kristo. Kumjua Mungu huamsha imani
katika Yeye kama ndiye njia ya pekee ya kuleta mibaraka ya mbinguni kwa mtu,
kumwinua juu, kumtukuza, kumtakasa mtu huyo, ----- kwa kumjua Mungu ----- hata
apate kuufikia utukufu wa juu na wema. "Kwa kuwa uweza wa Uungu umetukirimia vitu
vyote vipasavyo uzima na utauwa, kwa kumjua yeye aliyetuita kwa utukufu wake na
wema wake mwenyewe." ----- MS 13, 1884.
WEMA NA MAARIFA Machi 3Naam, na kwa sababu iyo hiyo mkijitahidi sana kwa upande wenu, katika imani yenu
tieni na wema, na katika wema wenu maarifa. 2 Petro 1:5.
"Katika imani yenu TIENI [ONGEZENI] wema." Hakuna ahadi yo yote iliyotolewa kwa
yule anayerudi nyuma. Katika ushuhuda wake, mtume analenga kuwaamsha waumini
kusonga mbele katika neema na utakatifu. Tayari wanakiri kwamba wanaishi kulingana
na hiyo kweli, wanao ujuzi [maarifa] wa kweli hiyo ya imani ya thamani, wamekuwa
washirika wa tabia ya uungu. Lakina kama watakomea hapo, basi, wataipoteza neema
ambayo wameipokea tayari...
Pasipo ku"jitahidi sana" kwenda kwa Mungu hatua kwa hatua juu ya ngazi hiyo, hakuna
kusonga mbele katika amani na neema na kazi ile ya utakatifu. "Jitahidini," akasema
Yesu, "kuingia katika mlango ulio mwembamba." Luka 13:24. Njia ya muumini
imewekwa na Mungu ambaye yuko juu ya ngazi hiyo. Juhudi zake zote zitakuwa ni bure
kabisa kama [muumini huyo] hana wema katika tabia yake, yaani, maarifa yale ya
kumjua Kristo kwa vitendo kwa njia ya utii wake kwa amri zake zote. Wale walio na
imani yawapasa kuwa waangalifu kuonyesha imani yao kwa matendo yao....
"Katika imani yenu tieni wema, na katika wema wenu maarifa" ----- maarifa [ujuzi] ya
ile kweli kama ilivyo katika Yesu, yaani, maarifa ya mpango ule mkuu wa wokovu.
Ujinga wa kutozijua Amri za Mungu na Sheria zake hautampa udhuru mtu ye yote.
Hataweza kuthubutu kusihi mbele ya kiti kile cha enzi cha Mungu, akisema, "Mimi
sikuijua kweli. Nilikuwa mjinga."
Bwana ametoa Neno lake kuwa kiongozi wetu, mwalimu wetu, nasi tukiwa na nuru hiyo
kutoka mbinguni hatuna sababu ya kutoa udhuru wo wote kwa ujinga wetu....
Kweli ni kanuni iliyo hai, inayotenda kazi, ikiubadilisha moyo na maisha ili daima
pawepo na maendeleo ya kupanda juu.... Katika kila hatua ya kupanda juu, nia inapata
nguvu mpya ya kutenda. Hali ya kimaadili inageuka na kufanana zaidi na nia na tabia
yake Kristo. Mkristo mwenye maendeleo ana neema na upendo unaopita ufahamu, kwa
maana utambuzi wa kiroho katika tabia ya Kristo unashikamana sana na mapenzi yake.
Utukufu wa Mungu uliofunuliwa juu ya ngazi ile unaweza tu kuthaminiwa na mpandaji
yule anayeendelea kupanda juu hatua kwa hatua, ambaye daima anavutwa juu zaidi na
zaidi, kwenda kwenye makusudi yale yaliyo bora ambayo Kristo anayafunua. Akili zake
zote pamoja na nguvu zake za mwili sharti zihusishwe zote. ----- MS 13, 1884."NA KATIKA MAARIFA YENU KIASI" Machi 4
Na katika maarifa yenu kiasi, na katika kiasi chenu saburi, na katika saburi yenu utauwa.
2 Petro 1:6.
Katika maarifa sharti kiongezwe kiasi. "Je! hamjui, ya kuwa wale washindanao kwa
kupiga mbio, hupiga mbio wote, lakini apokeaye tuzo ni mmoja? Pigeni mbio namna
hiyo, ili mpate. Na kila ashindanaye katika michezo hujizuia katika yote; basi hao
hufanya hivyo kusudi wapokee taji iharibikayo, bali sisi tupokee taji isiyoharibika. Hata
mimi napiga mbio vivyo hivyo, si kama asitaye; napigana ngumi vivyo hivyo, si kama
apigaye hewa, bali nautesa mwili wangu na kuutumikisha; isiwe, nikiisha kuwahubiri
wengine, mwenyewe niwe mtu wa kukataliwa." l Wakorintho 9:24-27.
Wapiga mbio wanatimiza masharti yote kwa furaha ili wapate kujizoeza kutumia nguvu
zao za mwili kwa kiwango cha juu sana. Hawaendekezi tamaa zao za kula na kunywa,
bali wanajizuia wenyewe daima, wakijiepusha na chakula kinachoweza kudhoofisha ama
kupunguza nguvu kamili za kiungo chao cho chote cha mwili. Lakini wao wanapigana
kama "apigaye hewa," ambapo Wakristo wako katika shindano la kweli kweli.
Washindanao katika michezo wanatafuta tu heshima ile inayoharibika. Wakristo mbele
yao wanayo taji ya utukufu isiyonyauka ya uzima wa milele. Na katika mbio hizo za
kwenda mbinguni kuna nafasi tele kwa wote kupokea thawabu. Hakuna hata mmoja
atakayeshindwa kama anakimbia vizuri, kama anafanya kulingana na nuru ile
inayomwangazia, akitumia uwezo wake wote ambao, kwa kadiri ajuavyo, ameutunza
katika hali nzuri ya afya....
Tabia au mazoea yo yote ambayo yatadhoofisha nguvu za neva na ubongo, au nguvu za
mwili, humfanya mtu huyo asifae kufanya zoezi la tabia inayofuata [katika ngazi]
ambayo inakuja baada ya kiasi ----- yaani, saburi [uvumilivu]....
Mtu asiyekuwa na kiasi, anayetumia vitu vile vinavyouchochea mwili wake ----- pombe,
mvinyo, vileo vikali, chai na kahawa, bangi [afyuni], tumbako, au kitu cho chote kati ya
hivyo ambacho kinaathiri afya yake ----- hawezi kuwa mtu mwenye saburi [mwenye
uvumilivu]. Basi kiasi ni hatua ya ngazi ambayo tunapaswa kukanyaga miguu yetu kabla
hatujaongeza juu yake tabia hiyo ya saburi. Katika chakula chetu, mavazi yetu, kazi zetu,
na saa zetu za kila siku, katika kufanya mazoezi yaletayo afya, tunapaswa kurekebishwa
kwa maarifa ambayo ni wajibu wetu kuyapata ili kwa juhudi ya dhati tupate kujiweka
katika uhusiano sahihi na uzima na afya. ----- MS 13, 1884"NA KATIKA MAARIFA YENU KIASI" Machi 4
Na katika maarifa yenu kiasi, na katika kiasi chenu saburi, na katika saburi yenu utauwa.
2 Petro 1:6.
Katika maarifa sharti kiongezwe kiasi. "Je! hamjui, ya kuwa wale washindanao kwa
kupiga mbio, hupiga mbio wote, lakini apokeaye tuzo ni mmoja? Pigeni mbio namna
hiyo, ili mpate. Na kila ashindanaye katika michezo hujizuia katika yote; basi hao
hufanya hivyo kusudi wapokee taji iharibikayo, bali sisi tupokee taji isiyoharibika. Hata
mimi napiga mbio vivyo hivyo, si kama asitaye; napigana ngumi vivyo hivyo, si kama
apigaye hewa, bali nautesa mwili wangu na kuutumikisha; isiwe, nikiisha kuwahubiri
wengine, mwenyewe niwe mtu wa kukataliwa." l Wakorintho 9:24-27.
Wapiga mbio wanatimiza masharti yote kwa furaha ili wapate kujizoeza kutumia nguvu
zao za mwili kwa kiwango cha juu sana. Hawaendekezi tamaa zao za kula na kunywa,
bali wanajizuia wenyewe daima, wakijiepusha na chakula kinachoweza kudhoofisha ama
kupunguza nguvu kamili za kiungo chao cho chote cha mwili. Lakini wao wanapigana
kama "apigaye hewa," ambapo Wakristo wako katika shindano la kweli kweli.
Washindanao katika michezo wanatafuta tu heshima ile inayoharibika. Wakristo mbele
yao wanayo taji ya utukufu isiyonyauka ya uzima wa milele. Na katika mbio hizo za
kwenda mbinguni kuna nafasi tele kwa wote kupokea thawabu. Hakuna hata mmoja
atakayeshindwa kama anakimbia vizuri, kama anafanya kulingana na nuru ile
inayomwangazia, akitumia uwezo wake wote ambao, kwa kadiri ajuavyo, ameutunza
katika hali nzuri ya afya....
Tabia au mazoea yo yote ambayo yatadhoofisha nguvu za neva na ubongo, au nguvu za
mwili, humfanya mtu huyo asifae kufanya zoezi la tabia inayofuata [katika ngazi]
ambayo inakuja baada ya kiasi ----- yaani, saburi [uvumilivu]....
Mtu asiyekuwa na kiasi, anayetumia vitu vile vinavyouchochea mwili wake ----- pombe,
mvinyo, vileo vikali, chai na kahawa, bangi [afyuni], tumbako, au kitu cho chote kati ya
hivyo ambacho kinaathiri afya yake ----- hawezi kuwa mtu mwenye saburi [mwenye
uvumilivu]. Basi kiasi ni hatua ya ngazi ambayo tunapaswa kukanyaga miguu yetu kabla
hatujaongeza juu yake tabia hiyo ya saburi. Katika chakula chetu, mavazi yetu, kazi zetu,
na saa zetu za kila siku, katika kufanya mazoezi yaletayo afya, tunapaswa kurekebishwa
kwa maarifa ambayo ni wajibu wetu kuyapata ili kwa juhudi ya dhati tupate kujiweka
katika uhusiano sahihi na uzima na afya. ----- MS 13, 1884KAZI KAMILIFU YA SABURI Machi 5
Mkifahamu ya kuwa kujaribiwa kwa imani yenu huleta saburi. Saburi na iwe na kazi
kamilifu, mpate kuwa wakamilifu na watimilifu bila kupungukiwa na neno. Yakobo
1:3,4.
Mtume huyo asema kwamba tunafanikiwa katika tabia hiyo ya kiasi ili tuweze kuongeza
saburi juu yake. Saburi chini ya maonjo itatuzuia kusema na kufanya mambo yale
ambayo yatazidhuru roho zetu wenyewe na kuwadhuru wale tunaoshirikiana nao.
Majaribu yako na yawe kama yalivyo, hakuna cho chote kinachoweza kukudhuru sana
wewe kama unajizoeza kuwa na saburi, kama umetulia na huna wasiwasi unapokuwa
katika hali za kujaribiwa....
Tunaweza kuiona hekima ya Petro katika kukiweka kiasi kuongezwa juu ya maarifa
kabla ya saburi. Hii ni sababu moja ya nguvu ya kuweza kuushinda uchu wa kula vitu
vyote vile vinavyouchochea mwili, kwa maana neva zinaposhtuliwa chini ya matumizi ya
vitu hivyo vinavyowasha, ni maovu mangapi na mazito yanayofanyika!...
Kuna umuhimu kwa Mkristo kuongeza saburi juu ya kiasi. Patakuwa na haja ya kuwa na
kanuni thabiti na kusudi imara ili tusikosee kwa neno, wala kwa tendo aidha kwa dhamiri
zetu wenyewe au kutokana na hisia za wengine. Yatupasa tusizifuate desturi za
ulimwengu huu ili tupate kustahimili aibu, kukata tamaa, hasara na misalaba pasipo
nung'uniko hata moja, bali kwa heshima isiyolalamika.... Mwanaume au mwanamke
mwenye chukichuki, yaani, mwenye hasira, kwa kweli hajui furaha ni kitu gani. Kila
kikombe anachokiweka kwenye midomo yake kinaonekana kuwa kichungu kama
pakanga na katika njia yake yamesambazwa mawe makali pamoja na mbigili na miiba;
lakini anapaswa kuongeza juu ya kiasi saburi na hapo ndipo hatajiona wala kujisikia
kuwa anadharauliwa.
Saburi inapaswa kuwa na kazi kamilifu, vinginevyo hatuwezi kuwa wakamilifu wala
kuwa wazima [kiroho], yaani, kutopungukiwa na kitu. Taabu na mateso yamechaguliwa
kwa ajili yetu, basi, je! tutavumilia vyote au tutafanya kila kitu kuwa kichungu kwa
malalamiko yetu? Dhahabu inawekwa katika tanuru ili uchafu upate kuondolewa. Je,
hatupaswi kuwa na saburi chini ya jicho lake atakasaye? Tunapaswa kukataa kuzama
katika hali ya huzuni isiyokuwa na faraja ya moyo, lakini tuonyeshe imani tulivu kwa
Mungu, tukihesabu kuwa ni furaha tupu tunaporuhusiwa kustahimili majaribu kwa ajili
yake Kristo. ----- MS 13, 1884.'NA KATIKA SABURI YENU UTAUWA" Machi 6
Kwa maana kujizoeza kupata nguvu za mwili kwafaa kidogo, lakini utauwa hufaa
mambo yote; yaani, unayo ahadi ya uzima wa sasa, na ya ule utakaokuwapo baadaye. l
Timotheo 4:8.
Baada ya kuongeza saburi kwa kiasi, inatupasa kupanda ngazi yetu ya maendeleo na
kuongeza juu ya saburi utauwa. Hayo ni matokeo halisi ya saburi. Mtume Paulo alisema,
"Tu[na]furahi katika dhiki pia; tukijua ya kuwa dhiki kazi yake ni kuleta saburi; na kazi
ya saburi ni uthabiti wa moyo; na kazi ya uthabiti wa moyo ni tumaini."... Warumi 5:3,4
[KJV].
Basi hapo yapo maendeleo katika tabia, yaani, utauwa, ambao maana yake ni kuwa na
roho na tabia inayofanana na ile ya Yesu Kristo. Kutuinua sisi kukifikia kipimo chake
cha Uungu ndilo lengo moja miongoni mwa mambo yote Mungu anayotutendea, na huo
ndio mpango mzima wa wokovu.... Uharibifu uliomo duniani unajaribu kutuibia akili
zetu, yaani, mivuto yote mibaya inayoonekana kila upande inafanya kazi kutushikilia sisi
katika hali duni ya kidunia ----- inatupofusha macho yetu ya kiroho, na kutushusha chini
katika tamaa mbaya, ikizidhoofisha dhamiri zetu na kuzilemaza akili zetu za mambo ya
dini kwa kutushawishi sisi ili tujiachilie katika tamaa mbaya za mwili....
Kutuvuta mbali na mambo hayo yote ndiyo kazi ya ngazi hiyo ya thamani. Jicho
linavutwa kumtazama Mungu juu ya ngazi hiyo. Mwito unakuja toka kwenye utukufu
ulio juu yake, Njoo huku juu zaidi. Moyo unavutwa. Hatua za kusonga mbele
zinachukuliwa, moja baada ya nyingine. Juu zaidi na zaidi tunaendelea kupanda. Kwa
kila hatua tunayochukua mvuto unazidi kuwa mkubwa zaidi. Tamaa ya kutaka mambo
yale ya juu zaidi yaliyo bora pamoja na utakatifu zaidi zinaijaza roho yetu. Hatia ya
maisha yetu yaliyopita imeachwa nyuma. Hatuthubutu kutazama chini ya ngazi hiyo
kuangalia mambo yale ambayo zamani yalizisumisha chemchemi za furaha yetu ya kweli
na kuamsha majuto, kuidhofisha na kuifanya nia yetu kuwa duni, na kuikandamiza kila
hamu iliyokuwa bora ndani yetu....
Lengo la Neno la Mungu ni kututia tumaini, kutuongoza sisi... kupanda hatua kwa hatua
kuelekea mbinguni, kwa nguvu inayoongezeka daima.... Tunapata tabia inayofanana na
Mungu kwa njia ya neema yake anayotupa.... Kama vile nta inavyochukua kifanani cha
muhuri, hivyo ndivyo roho inavyopokea na kuihifadhi sura ya Mungu kimaadili.Tunajazwa na kubadilishwa kwa mnga'o wake, kama vile wingu ----- lenyewe likiwa
jeusi ----- linapojazwa na mwanga linageuka na kuwa jeupe, safi. ----- MS 13, 1884.
MANUFAA YA UPENDANO WA NDUGU Machi 7
Na katika utauwa wenu upendano wa ndugu, na katika upendano wa ndugu, upendo.
2 Petro 1:7.
Neno la Mungu linamwagiza hivi kila mmoja wa watoto wake: "Mwe na nia moja,
wenye kuhurumiana, wenye kupendana kama ndugu, wasikitivu, wanyenyekevu." 1 Petro
3:8. Sasa kama utauwa usingeongezwa juu ya kiasi mwanadamu asingeweza kuonyesha
upendano ule wa ndugu. Katika utume wake kwa ulimwengu wetu, Kristo
amemwonyesha mwanadamu matunda ya Roho wa Mungu ambayo, kama akiyapokea,
yanamfanya na kumbadilisha mwanadamu mzima, nje na ndani, kwa kukishusha chini
kiburi chake na kumwongoza kutojihesabu yeye mwenyewe kuwa ni bora kuliko
wengine bali kumhesabu ndugu yake kuwa ni wa thamani machoni pake Mungu kwa
sababu Kristo alilipa bei isiyopimika kwa ajili ya roho yake. Mwanadamu
anapothaminiwa kama mali ya Mungu hapo ndipo tutakuwa wapole, marafiki, na
wanyenyekevu kwake.
Dini ya Kristo ni mfumo wa upole wa kweli wa mbinguni, nayo huwaongoza watu
kuonyesha kwa vitendo tabia ya daima yenye hisia ya kuumia kwa ajili ya wengine,
yaani, tabia ile ya
upole. Yule aliye na utauwa ataongeza pia tabia hiyo, akichukua hatua moja juu zaidi
katika ngazi hiyo. Kadiri anavyozidi kupanda juu, ndivyo kadiri neema zaidi ya Mungu
inavyodhihirishwa katika maisha yake, hisia zake za moyoni, na kanuni zake. Anaendelea
kujifunza, na kuzidi kujifunza masharti ya kukubalika kwake na Mungu, na njia ya pekee
ya kuupata urithi mbinguni ni kuwa kama Kristo katika tabia yake. Mpango mzima wa
rehema ni kulainisha ukali wake katika tabia yake, na kuifanya tabia yake yo yote
isiyokuwa ya upole kuwa ya kiungwana. Badiliko la ndani linajionyesha lenyewe katika
matendo yake ya nje. Matunda ya Roho wa Mungu yanafanya kazi yake ya kuibadilisha
tabia kwa uwezo uliojificha [usioonekana kwa macho]. Dini ya Kristo haitaonyesha
kamwe tendo moja la kisirani, lisilo na adabu, wala lisilo na heshima. Heshima ni tabia
njema ya Biblia. Manufaa ya tunda hili la upole wa ndugu yalikuwa tele katika maishayake Kristo. Kamwe palikuwa hapajapata kuonekana duniani heshima kama ile
aliyoionyesha Kristo, nasi hatuwezi kukadiria zaidi ya thamani yake ilivyo hasa....
Kukua katika neema ni kuwa na juhudi ya kufanya nje kile ambacho Mungu anafanya
ndani. Ni jitihada kwa ajili ya utukufu ule wa baadaye, yaani, utekelezaji hapa duniani wa
roho ile inayopendwa sana kule mbinguni. ----- MS 13, 1884.
UPENDO NI HATUA YA NGAZI YA MWISHO JUU Machi 8
Zaidi ya hayo yote jivikeni upendo, ndio kifungo cha ukamilifu. Wakolosai 3:14.
Hatua inayofuata katika ngazi hiyo ni upendo. Ongeza juu ya "upendano wa ndugu,
upendo."
Upendo kwa Mungu na upendo kwa jirani yetu hufanya wajibu wote wa mwanadamu.
Pasipo upendano wa ndugu hatuwezi kulionyesha tunda la upendo kwa Mungu wala kwa
wanadamu wenzetu.
Hatua hiyo ya mwisho katika ngazi hiyo huipa nia nguvu mpya ya kutenda. Kristo
anatoa upendo upitao ufahamu wetu. Upendo huo si kitu kinachowekwa mbali na maisha
yetu, bali unautawala mwili wote. Mbinguni anakopanda Mkristo kutafikiwa tu na wale
walio na tunda hili la kilele. Huo ndio upendo mpya unaoijaza roho. Ya kale yanaachwa
nyuma. Upendo ni nguvu kuu inayotuongoza. Upendo unapoongoza fahamu zote za akili
na roho hutumika. Upendo kwa Mungu na upendo kwa mwanadamu utatoa haki ile iliyo
safi ya kuingia mbinguni.
Hakuna anayeweza kumpenda Mungu kabisa na wakati uo huo kuivunja mojawapo ya
Amri zake [Kumi]. Moyo ule uliolainishwa na kuadibishwa kwa njia ya uzuri wa tabia
yake Kristo na kutiwa lijamu [kudhibitiwa] kwa kanuni zile safi na za juu alizotupa,
utayaweka katika matendo yale uliyojifunza juu ya upendo huo, nao utamfuata Yesu
mara moja kwa utii uliojaa unyenyekevu. Nguvu ya imani iliyo hai itajidhihirisha
yenyewe katika matendo yaliyojaa upendo.
Je, tunao ushahidi gani kama sisi tunao upendo huo ulio safi, usiochanganyika na
takataka zo zote? Mungu ameiinua juu kanuni yake ----- Amri zake [Kumi]. "Yeye aliye na amri zangu [kumi], na kuzishika, yeye ndiye anipendaye." Yohana 14:21. Maneno ya
Mungu ni lazima yapate nafasi katika mioyo yetu.
Yatupasa kuwapenda ndugu zetu kama vile Kristo alivyotupenda sisi. Yatupasa kuwa na
saburi na upole, na bado kuna kitu fulani kilichopungua ----- yatupasa kupenda. Kristo
anatuambia kwamba inatupasa kumsamehe yule anayetukosea hata sabini mara saba....
Kukiwa na mengi yaliyosamehewa, moyo huwa na upendo mwingi sana. Upendo ni
mmea mwororo sana. Unahitaji daima kupaliliwa au la utanyauka na kufa.
Matunda hayo yote hatuna budi kuwa nayo. Yatupasa kupanda juu urefu wote wa ngazi
hiyo. ----- MS 13, 1884.
FANYENI IMARA KUITWA KWENU NA UTEULE WENU Machi 9
Maana mambo hayo yakiwa kwenu na kujaa tele, yawafanya ninyi kuwa si wavivu wala
si watu wasio na matunda, kwa kumjua Bwana wetu Yesu Kristo. 2 Petro 1:8.
Usalama peke yake kwa Mkristo ni kutochoka katika juhudi zake za kuishi kulingana na
mpango huo wa kuongeza. Mtume anaonyesha manufaa yanayoweza kupatikana kwa
kufanya hivyo. Kwa wale wanaoongeza tunda juu ya tunda, Mungu atafanya kazi kwa
mpango wake wa kuzidisha, ili matunda hayo yapate kukaa ndani yao na kuzidi sana
katika maisha yao ya dini, nao wata"kuwa si wavivu wala si watu wasio na matunda...."
Wale waliojaa tele matunda hayo ya Kikristo watakuwa na bidii, watachangamka, na
kuwa na nguvu katika maisha yao yote ya Kikristo kwa vitendo, nao watajizoeza kuwa na
haki ----- kama vile tawi linalokaa katika mzabibu litakavyozaa tunda lile lile ambalo
mzabibu unazaa....
Yule asiyeipanda ngazi hiyo ya maendeleo na kuongeza tunda juu ya tunda "ni kipofu,
hawezi kuona vitu vilivyo mbali." Anashindwa kutambua kwamba bila kuchukua hatua
hizo zinazofuatana moja baada ya nyingine katika kupanda hatua kwa hatua, kwa kukua
katika neema na katika kumjua Bwana wetu Yesu Kristo, hajiweki mwenyewe mahali
pale nuru ya Mungu kutoka juu ya ngazi hiyo inapoweza kumwangazia juu yake. Kwa
vile yeye haongezi tunda juu ya tunda, basi, anakuwa amesahau madai ya Mungu juu
yake, ya kwamba alipaswa kuupokea msamaha wa dhambi zake kwa njia ya utii kwa
matakwa yake Mungu..."Kwa hiyo ndugu, jitahidini zaidi kufanya imara kuitwa kwenu na uteule wenu." 2 Petro
1:10. Hatuna haja ya kuwa na tumaini la kudhaniwa tu, bali kuwa na hakika. Kufanya
imara kuitwa kwetu na uteule wetu ni kufuata mpango wa Biblia kwa kujichunguza
wenyewe kwa karibu sana, kujihoji kwa ukali kama sisi tumeongoka kweli, kama mioyo
yetu inavutwa kweli kumwelekea Mungu na mambo yaliyoko mbinguni, kama nia zetu
zimefanywa upya kweli, na mioyo yetu kubadilishwa kabisa. Kufanya imara kuitwa
kwetu na uteule wetu huhitaji juhudi kubwa kuliko ile wengi wanayoitoa kwa jambo hilo
la maana. "Maana mkitenda hayo" ----- kama mkiishi kwa mpango huo wa kuongeza,
yaani, kama mkikua katika neema na kumjua Bwana wetu Yesu Kristo ----- basi,
mtapanda juu, hatua kwa hatua, juu ya ngazi ile aliyoiona Yakobo, nanyi "hamtajikwaa
kamwe." ----- MS 13,1884.
KUMSHIKA SANA KRISTO, ALIYE NGAZI Machi 10
Maana hivi mtaruzukiwa kwa ukarimu kuingia katika ufalme wa milele wa Bwana wetu,
Mwokozi wetu Yesu Kristo. 2 Petro 1:11.
Tunapanda kwenda mbinguni kwa kupanda ngazi hiyo ----- kimo chote cha kazi yake
Kristo ----- hatua kwa hatua. Lazima pawepo na kumshika sana Kristo, yaani, kupanda
juu kwa kutegemea wema wake Kristo. Kuachilia ni kukoma kupanda, ni kuanguka chini,
yaani, kuangamia. Yatupasa kupanda juu kwa njia ya Mpatanishi [Mwombezi] wetu na
wakati wote tuwe tumemshika sana Mpatanishi wetu, tukiwa tunapanda hatua
zinazofuatana moja baada ya nyingine, yaani, hatua kwa hatua kwenda juu, tukiunyosha
mkono wetu toka hatua moja kwenda hatua inayofuata juu yake.... Kuna hatari ya kutisha
kulegeza juhudi zetu katika juhudi yetu ya kiroho hata kwa dakika moja, kwa maana sisi,
kama ilivyo, tunaning'inia katikati ya mbingu na dunia.
Macho yetu hatuna budi kuyaelekeza juu kwa Mungu aliye juu ya ngazi hiyo. Swali kwa
wanaume na wanawake wanaoangaza macho yao juu mbinguni ni hili, Nawezaje mimi
kuyafikia makao yale ya waliobarikiwa? Ni kwa njia ya kuwa mshirika wa tabia ya
Uungu. Ni kwa njia ya ku"okolewa na uharibifu uliomo ulimwenguni kwa sababu ya
tamaa." Ni kwa kuingia patakatifu pa patakatifu kwa njia ya damu yake Yesu, tukilishika tumaini lile lililowekwa mbele yetu katika injili. Ni kwa kumshika sana Kristo na
kutumia kila uwezo tulio nao ili kuuacha ulimwengu huu nyuma yetu.... Ni kwa kukaa
ndani yake Kristo na kuongozwa naye; kwa kusadiki na kufanya kazi yake,... tukimshika
sana Kristo na kuendelea daima kupanda juu kuelekea kwa Mungu....
Tunawaelekeza kwenye makao yale ambayo Kristo anawaandalia wale wote
wampendao. Tunawaonyesha mji ule ulio na misingi, ambao mwenye kuubuni na
kuujenga ni Mungu. Tunawaonyesha kuta zake kubwa mno, na misingi ile kumi na
miwili, na kuwaambia kwamba kuta hizo ni lazima ziparamiwe hatua kwa hatua.
Mwaonekana kukatishwa tamaa mnapoiona kazi kubwa sana iliyo mbele yenu.
Tunawaelekeza kwenye ngazi hiyo iliyokitwa hapa duniani, inayofika kwenye mji ule wa
Mungu. Kanyageni miguu yenu juu ya ngazi hiyo. Achana na dhambi zenu. Pandeni
hatua kwa hatua, nanyi mtamfikia Mungu aliye juu ya ngazi hiyo, na Mji ule Mtakatifu
wa Mungu....
Hatua zinazofuatana zitakapokuwa zimepandwa zote, matunda yale yatakapokuwa
yameongezwa moja juu ya jingine, tunda la kilele likiwa ni ule upendo mkamilifu wa
Mungu ----- yaani, kumpenda Mungu upeo pamoja na wanadamu wenzetu. Hapo ndipo
mtaruzukiwa kwa ukarimu kuingia katika ufalme ule wa milele wa Mungu. ----- MS,
1884.
FAIDA YA KUWA NA HAKIKA Machi 11
Katika hili tutafahamu ya kwamba tu wa kweli, nasi tutaituliza mioyo yetu mbele zake.
l Yohana 3:19.
Ningependa kuwasisitizia vijana wa kiume na wa kike juu ya umuhimu wa kufanya
imara kuitwa kwao na uteule wao. Ningewasihi msifanye mambo yenu kiholela au kazi
yenu bila kuwa na hakika yo yote katika mambo yale yahusuyo umilele wenu. Mkifanya
hivyo mtapoteza furaha, amani, faraja, na tumaini katika maisha haya, nanyi mtapoteza
pia urithi wenu ule wa milele.
Enyi rafiki zangu, vijana, mnaelekea kwenye hukumu, na kwa neema yake Kristo
mnaweza kutoa utii wenu kwa zile Amri [Kumi] za Mungu, na kila siku kupata ushupavu
na nguvu katika tabia zenu, ili msishindwe wala msikate tamaa. Neema ya Munguimetolewa kwa wingi kwa kila mtu, ili kila mmoja aweze kuingia katika pambano hilo na
kuwa mshindi. Msiwe wavivu; msijitape wenyewe kwamba mnaweza kuokolewa wakati
mwenendo wenu unalingana na tabia zenu za asili [za kuzaliwa nazo] ----- huku mkiwa
mnachukuliwa na mkondo wa ulimwengu huu, na kuiendekeza na kuifurahisha nafsi
yenu, na baadaye kudhani mtaweza kuzipinga nguvu za uovu wakati ule wa dharura, na
kutoka mkiwa washindi pambano litakapopamba moto.... Kila siku inawapasa kujifunza
kuzitii amri zake yule Amiri [Kamanda] wa Jeshi la Bwana [Kristo].
Enyi rafiki zangu, vijana, je! mnaomba? Je! mnajizoeza wenyewe kutoa dua zenu ili
mpate kuwa na mawazo safi, hamu takatifu za kupata mambo fulani ya maisha haya,
moyo safi, na mikono safi? Je! mnaizoeza midomo yenu kuimba sifa kwa Mungu, na
kutafuta jinsi ya kuyafanya mapenzi ya Mungu? Hiyo ndiyo aina ya elimu itakayokuwa
ya thamani kubwa sana kwenu; kwa maana itawasaidieni kujenga tabia yenu kuwa kama
ile ya Kristo. ----- YI, Nov.7, 1895.
Msistarehe katika kiti cha raha cha Shetani, na kusema hakuna faida, hatuwezi kuacha
kutenda dhambi, na ya kwamba hamna nguvu ndani yenu ya kuzishinda [dhambi hizo].
Hakuna nguvu yo yote ndani yenu mbali na Yesu, lakini ni haki yenu kuwa naye Kristo,
akikaa ndani ya mioyo yenu kwa imani, Yeye anaweza kuzishinda dhambi ndani yenu,
mnaposhirikiana na juhudi zake.... Mwaweza kuwa barua zilizo hai, zinazojulikana na
kusomwa na watu wote. Haiwapasi ninyi kuwa barua mfu, bali ile iliyo hai, mkishuhudia
kwa ulimwengu huu kwamba Yesu anaweza kuokoa. ----- YI, Juni 29, 1893.
UMECHAGULIWA NA MUNGU Machi 12
Wewe niliyekushika toka miisho ya dunia, na kukuita toka pembe zake, nikikuambia,
Wewe u mtumishi wangu; nimekuchagua wala sikukutupa. Isaya 41:9.
Wengi wana mawazo yaliyochanganyikiwa kuhusu kile kinachofanyiza imani, nao
wanaishi chini kabisa ya haki zao. Wanachanganya hisia na imani, nao wanahuzunishwa
daima na kutatanishwa mioyoni mwao; maana Shetani anajitahidi kwa kadiri awezavyo
kuwadanganya kutokana na ujinga wao na kule kutokuwa na uzoefu kwao.... Yatupasa
kumpokea Kristo kama Mwokozi wetu kila mmoja binafsi, vinginevyo tutashindwa
katika jitihada yetu ya kuwa washindi. Hatutapata jibu [ufumbuzi] kwa kujitenga mbali
naye, na kusadiki ya kwamba rafiki yetu ama jirani yetu ndiye hasa awezaye kumpokea
kama Mwokozi wake binafsi, ila sisi tusiweze kuuonja upendo wake unaosamehe.Yatupasa kuamini kwamba sisi tumechaguliwa na Bwana, kuokolewa kwa imani, kwa
njia ya neema yake Kristo, pamoja na kazi yake Roho Mtakatifu; nasi yatupasa kumsifu
na kumtukuza Mungu kwa maonyesho hayo ya ajabu ya upendeleo wake tusioustahili. Ni
upendo wake Mungu unaomvuta mtu kwa Kristo, kupokelewa vizuri, na kutambulishwa
rasmi mbele zake Baba. Kwa njia ya kazi ya Roho uhusiano mtakatifu kati ya Mungu na
mwenye dhambi unafanywa upya. Baba anasema: "Mimi nitakuwa Mungu kwao, nao
watakuwa watu wangu. Nitatumia upendo wangu unaosamehe kwao, na kuwapa furaha
yangu. Kwangu watakuwa hazina ya pekee; kwa maana watu hawa niliojiumbia
mwenyewe watatangaza sifa zangu."
Baba anaweka upendo wake juu ya wateule wake wanaoishi miongoni mwa watu. Hao
ndio watu waliokombolewa na Kristo kwa thamani ya damu yake mwenyewe; na kwa
kuwa wanaitikia anapowavuta Kristo, kwa njia ya rehema kuu ya Mungu, wanateuliwa
kuokolewa kama watoto wake watiifu. Juu yao inadhihirishwa neema ya Mungu
inayotolewa bure, yaani, upendo ule ambao kwa huo amewapenda wao. Kila mmoja
atakayejinyenyekeza mwenyewe kama mtoto mdogo, atakayelipokea na kulitii neno la
Mungu kwa wepesi kama ule alio nao mtoto mdogo, atakuwa miongoni mwa wateule wa
Mungu. ----- ST, Jan.2, 1893.
Mnaweza kujithibitishia wenyewe kuwa mmeteuliwa na Kristo kwa kuwa waaminifu
kwake; mnaweza kujithibitishia wenyewe kuwa mmechaguliwa na Kristo kwa kuendelea
kukaa katika mzabibu huo. ----- 6BC 1079.
UTIMILIFU WA FIDIA YAKE KRISTO Machi 13
Kama vile alivyotuchagua katika yeye kabla ya kuwekwa misingi ya ulimwengu ili tuwe
watakatifu, watu wasio na hatia mbele zake katika pendo. Kwa kuwa alitangulia
kutuchagua, ili tufanywe wanawe kwa njia ya Yesu Kristo, sawasawa na uradhi wa
mapenzi yake. Waefeso 1:4,5.
Katika baraza lile la mbinguni, mpango ulifanywa kwamba, ijapokuwa wanadamu ni
waasi, wasiangamie katika uasi wao, bali, kwa njia ya imani katika Kristo kama mmoja
aliye Badala yao na Mdhamini wao, wapate kuwa wateule wa Mungu.... Mungu
anapenda kwamba watu wote waokolewe; kwa maana mpango wa kutosha umefanywa,
kwa kumtoa Mwanawe pekee ili kulipa fidia kwa ajili ya mwanadamu. Wale
wanaoangamia wataangamia kwa sababu wanakataa kufanywa watoto wa Mungu kwanjia ya Kristo Yesu. Kiburi cha mwanadamu kinamzuia kupokea mafao ya wokovu.
Lakini wema wa kibinadamu hautaweza kumwingiza mtu ye yote mbele za Mungu. Kile
kitakachomfanya mtu akubaliwe na Mungu ni ile neema ya Kristo anayopewa kwa imani
katika jina lake. Hakuna tegemeo linaloweza kuwekwa juu ya matendo au hisia za furaha
zinazopita kama ushahidi kwamba wanadamu wamechaguliwa na Mungu; kwa maana
wateule wanachaguliwa katika Kristo.
Yesu asema, "Wote anipao Baba watakuja kwangu; wala ye yote ajaye kwangu
sitamtupa nje kamwe." Yohana 6:37. Mwenye dhambi aliyetubu anapokuja kwa Kristo,
akiwa anayajua maovu yake na kutokufaa kwake, akitambua kwamba anastahili adhabu,
lakini akitegemea rehema na upendo wa Kristo, hatamtupa nje. Upendo wa Mungu
unaosamehe unatumika, na furaha iliyojaa shukrani inabubujika moyoni mwake kwa
sababu ya ile huruma ipitayo kipeo na upendo wa Mwokozi wake. Kwamba mpango huo
ulifanywa katika vikao vya mabaraza ya mbinguni kabla ya kuwekwa misingi ya
ulimwengu, kwamba Kristo angebeba adhabu ya dhambi za mwanadamu na kumpa haki
yake, ni jambo linalomshinda kabisa [kulielewa] na kumfanya abaki na mshangao. -----
ST, Jan. 2, 1893.
Baba aliziweka dhambi zetu mahali ambapo hakuna mtu ye yote ambaye angeweza
kuziona isipokuwa macho yake peke yake. Na kama vile alivyouficha uso wake ili
asiione hali ya Kristo ya kutokuwa na hatia, ndivyo atakavyouficha uso wake ili macho
yake yasiuangalie uovu wa mwenye dhambi anayeamini, kwa sababu ya haki ile
inayohesabiwa juu yake. Haki ya Kristo iliyowekwa juu yetu itatuletea mibaraka mingi
sana ya thamani katika maisha haya, na itatupa uzima wa milele katika ufalme wa
Mungu. ----- ST, Des. 8, 1898.
MUNGU ANADAI TUMPE MAPENZI YETU YOTE Machi 14
Hakuna mtu awezaye kutumikia mabwana wawili; kwa maana atamchukia huyu, na
kumpenda huyu; ama atashikamana na huyu, na kumdharau huyu. Hamwezi kumtumikia
Mungu na mali.Mathayo 6:24.
Wengi wamesimama kwenye eneo linalopendeza mno la yule adui. Mambo yale
yasiyokuwa na maana kabisa ----- sherehe za jumuia za kipuuzi, nyimbo za kipuuzi,
utani, na vichekesho ----- huijaza mioyo yao, wanamtumikia Mungu wakiwa na mioyoiliyogawanyika.... Tangazo la Kristo lisemalo, "Hakuna mtu awezaye kutumikia
mabwana wawili," halizingatiwi. -----
MS 38, 1890.
Mojawapo ya tabia dhahiri za wakazi wa dunia hii katika siku zile za Nuhu ilikuwa ni
kule kuipenda sana dunia hii. Walifanya mambo ya kula na kunywa, kununua na kuuza,
kuoa na kuolewa, kuwa ndilo lengu kuu mno la maisha yao. Si dhambi, bali ni kutimiza
wajibu, kula na kunywa, kama kile kilicho halali hakitumiwi kupita kiasi.... Mungu
mwenyewe ndiye aliyeianzisha ndoa alipompa Adamu Hawa. Sheria zote za Mungu kwa
ajabu zinapatana na asili [maumbile] ya mwanadamu. Dhambi ya watu wale walioishi
kabla ya Gharika ilikuwa ni ile ya kukitumia kwa upotofu kile ambacho chenyewe
kilikuwa ni halali. Waliviharibu vipawa vya Mungu kwa kuvitumia kukidhi tamaa zao za
uchoyo.... Kupenda kupita kiasi na kutumia muda mwingi sana kwa kitu kile ambacho
chenyewe ni halali, hushuhudia maangamizi ya maelfu kwa maelfu ya watu. Kwa mambo
yale yasiyokuwa na maana mara nyingi nguvu za akili hutumika ambazo zingetumika
zote kwa Mungu. Wengi, watu wengi hupotea kwa kujishughulisha na mambo yale
ambayo, kama yakidhibitiwa vizuri, hayana madhara yo yote, lakini ambayo,
yakipotolewa na kutumiwa vibaya, hugeuka na kuwa dhambi na kuiharibu tabia ya mtu. -
---- MS 24, 1891.
Iwapo tunafikiria daima na kujitahidi kuyapata mambo yale yanayohusu maisha haya,
basi, hatuwezi kukaza mawazo yetu juu kuyaangalia mambo yale ya mbinguni. Shetani
anatafuta kuyageuza mawazo yetu mbali na Mungu, na kuyaelekeza kwenye mitindo ya
kisasa, desturi [mila], na matakwa ya ulimwengu huu, ambavyo huleta magonjwa na
mauti....
Katika ulimwengu huu tunapaswa kujitayarisha ili tuweze kufaa kwa ulimwengu ule wa
juu. Mungu ametuachia sisi amana yake, naye anatutazamia kutumia akili zetu zote
kuwasaidia na kuwaletea mibaraka wanadamu wenzetu. Anadai tumpe mapenzi yetu
yote, nguvu zetu za juu sana. ----- MS 29, 1886.
NAHODHA YUPI? Machi 15
Kwa maana ndivyo alivyo MUNGU, Mungu wetu. Milele na milele Yeye ndiye
atakayetuongoza. Zaburi 48:14.Sisi sote tuko chini ya mmoja au mwingine wa manahodha wakuu wawili. Mmoja,
ambaye ni Muumbaji wa mbingu na nchi, ndiye mkuu kuliko wote. Wote wanatakiwa
kumpa utii wa mwili wao wote, kumpa mapenzi yao yote. Kama akili inakabidhiwa
kwake ili aitawale, na kama Mungu anahusika kuzibadilisha na kuzikuza nguvu za akili,
basi, nguvu mpya za maadili zitapokewa kila siku kutoka kwa huyo aliye Chimbuko la
hekima yote na nguvu zote. Mibaraka ya kimaadili na uzuri wa utakatifu utazawadiwa
kwa juhudi ya kila mmoja ambaye mawazo yake yameelekezwa mbinguni. Tunaweza
kuelewa mafunuo ----- uzuri wa mbinguni ----- ambao uko mbali kupita upeo mfupi wa
macho ya mtu aipendaye dunia hii, ambao unang'aa kupita mawazo ya wenye akili sana
yanavyoweza kumaizi [kutambua]....
Shetani ndiye nahodha [kiongozi] wa wale wanaoipenda dunia.... Lengo lake kubwa sana
ni kuwakusanya chini ya bendera yake umati mkubwa sana wa walimwengu, ili idadi
kubwa ipate kusimama dhidi ya nguvu ya haki na kweli ya milele. Talanta na nguvu
zilizotolewa na Mungu hutumika kwa kazi yake, yaani, huwekwa miguuni pa yule mwasi
mkuu wa serikali ya Mungu....
Wakati yule mwenye hekima mpenda ulimwengu huu anapita kwa juu juu tu, akiyashika
mambo ya kuona tu na kusikia, yule anayemcha na kumheshimu sana Mungu anaufikia
umilele, akipenya mahali pa ndani sana na kukusanya maarifa na utajiri ambavyo
hudumu milele. Haki, heshima, upendo, na kweli ndizo sifa za kiti cha enzi cha Mungu.
Hizo ndizo kanuni za serikali yake.... Hizo ndizo johari za kutafutwa na kutunzwa sana
kwa wakati huu na kwa milele...
Kutembea katika ulimwengu huu ukiwa mtu safi mwenye maadili yasiyokuwa na dosari,
ukichukua kanuni takatifu za ile kweli katika moyo wako, mvuto wake ukionekana katika
matendo ya maisha yako; ukiishi bila kupotolewa na uovu, uongo, na unafiki wa
ulimwengu huu ambao utatakaswa hivi karibuni kwa moto wa haki ya upatilizaji wa
Mungu kutokana na upotovu wake wa maadili, unatakiwa kuwa mtu ambaye
kumbukumbu zako zimewekwa katika kumbukumbu zile za milele kule mbinguni, ukiwa
unaheshimiwa miongoni mwa malaika watakatifu wanaopima na kutathmini kufaa kwa
maadili yako. Hiyo ndiyo maana ya kuwa mtu wa Mungu. ----- Letter 41, 1877.
SABABU YA MAJANGA YETU YOTE Machi 16
Lakini mwonyane kila siku, maadam iitwapo leo; ili mmoja wenu asifanywe mgumu
kwa udanganyifu wa dhambi. Waebrania 3:13.Zingatia sana maneno haya "udanganyifu wa dhambi." Shetani siku zote analeta
majaribu yake chini ya kificho cha mema. Jihadhari usianguke chini ya mtego huo.
Kukiuka mara moja tu ukweli ule ulio mnyofu hutayarisha njia kwa ukiukaji wa pili, na
makosa hayo hurudiwa tena, mpaka moyo wa kutokuamini unageuka na kuwa ngumu, na
dhamiri inapoteza ukali wake [wa kupambanua]. ----- MS 9, 1903.
Hebu na wasiwepo watu wanaojigamba kwamba dhambi za ujana wao zinaweza
kuachwa kwa urahisi baadaye. Hivyo sivyo mambo yalivyo. Kila dhambi inayopendwa
na kutunzwa moyoni inaidhoofisha tabia na kuiimarisha tabia hiyo mbaya; na uharibifu
wa mwili, akili, na maadili huwa ndiyo matokeo yake. Unaweza kuyatubia makosa
uliyokwisha kufanya, na kuiweka miguu yako katika njia ile ya haki; bali mwelekeo wa
mawazo yako na kule kuyazoea yale maovu kutafanya iwe vigumu kwako kutofautisha
kati ya jema na baya. Kwa njia ya mazoea mabaya uliyojizoeza Shetani atakushambulia
tena na tena. ----- MS 127, 1899.
Wengi... wanaiangalia dhambi kama kitu kidogo tu.... Wengi wanaongozwa na mashauri
ya matakwa yao na tamaa zao na kuifuata mielekeo yao na hatimaye wanaamua kuwa
dhambi sio ya kuchukiza sana, sio ya kutisha sana na kuogofya machoni pake Mungu.
Dhambi inayoweza kuonekana kuwa ni ndogo ambayo inaweza kutajwa kuwa ni ndogo
tu na dhamiri ile iliyopoteza makali yake [ya kubainisha], ni kitu cha kusikitisha sana
machoni pake Mungu kiasi kwamba hakuna kitu cho chote, isipokuwa damu ya Mwana
wa Mungu, kinachoweza kuiondoa. Ukweli huo unaweka makadirio halisi juu ya dhambi.
Mungu hatautia waa kamwe utukufu wake ujao kwa kufuata mawazo na maoni yetu.
Itatupasa sisi kufuata yake. Kwa kiwango kile kile cha uzuri wa Mungu usio na kifani,
ndivyo ulivyo ubaya wa kupindukia wa tabia hiyo ya dhambi....
Mungu anataka sisi tuwe na furaha ya kweli. Kama kitu cho chote kinazuia katika njia
ielekeayo kwenye furaha hiyo, basi, Yeye anahakikisha kinaondolewa kwanza.
Atayawekea vipingamizi makusudi yetu na kutukatisha tamaa katika matarajio yetu na
kupitia katika mambo hayo ya kukatisha tamaa na maonjo anatufunulia jinsi sisi
wenyewe tulivyo hasa.... Dhambi ni chimbuko la majanga yetu yote. Iwapo tunataka
kuwa na amani na furaha ya kweli moyoni mwetu, basi, dhambi haina budi kuondolewa.
----- Letter 29, 1879.
KWA KUTOJIAMINI WENYEWE TUNAMLILIA MUNGU Machi 17Nalikujulisha dhambi yangu, Wala sikuuficha upotovu wangu. Nalisema, Nitayakiri
maasi yangu kwa BWANA, Nawe ukanisamehe upotovu wa dhambi yangu. Zaburi 32:5.
Daudi mara nyingi alishangilia katika Mungu, alifikiri sana juu ya kutokufaa kwake na
dhambi zake. Dhamiri yake ilikuwa haijalala usingizi wala kufa. "Dhambi yangu," akalia,
"i mbele yangu daima." Zaburi 51:3. Hakujigamba mwenyewe kwamba dhambi ilikuwa
ni jambo ambalo hakuwa na la kufanya juu yake, wala kwamba lisingemhusu yeye.
Alipokiona kina cha udanganyifu ndani ya moyo wake, yeye ... aliomba kwamba Mungu
... angemtakasa na makosa yake ya siri.
Si salama kwetu kufumba macho yetu na kuzifanya dhamiri zetu kuwa ngumu, ili
tusione wala kutambua dhambi zetu. ----- 3BC 1147.
Mtu mwenye moyo mnyenyekevu hatafikiria kwamba maungamo yake yanamdhalilisha
yeye. Hataona kuwa ni aibu kuungama kama amemwumiza ndugu yake kwa njia yo yote,
hata kwa mawazo tu au kuizuia kazi ya Mungu kupitia kwake. ----- MS 23, 1899.
Dhambi zisizotubiwa ni dhambi zisizosamehewa. Wale wanaojifikiria wenyewe kuwa
wamesamehewa kwa dhambi zile ambazo hawajaona ubaya wake, wala hawajaona
kamwe toba moyoni mwao, hao wanajidanganya wenyewe tu.... Nguvu yetu i katika
kuutambua udhaifu wetu.... Kwa kutojiamini wenyewe tunamlilia Mungu apate
kutusaidia, nasi tunautimiza wokovu wetu wenyewe kwa kuogopa na kutetemeka.
Tukitupilia mbali kujiamini kwetu kote na kutegemea uwezo wetu, ndipo tunaweza
kumshikilia sana Yesu....
Mbingu haitafikiwa na watu wale wanaopenda mambo yaliyo rahisi, huku wakijidai tu
kuwa wao ni Wakristo. Mungu anataka kazi kamilifu kwa kila mmoja wa wafuasi
wake....
Kwa kujikana nafsi kabisa,
Kwa kukesha daima,
Kwa kuwa na bidii katika maombi,
Kwa juhudi katika kutumia kila njia ya neema,
Na kwa msaada wa Yesu Kristo Mkombozi wetu,
Tutakuwa washindi.Pumziko lile la mbinguni ni kwa waliochoka sana,
Taji ni kwa vipaji vya nyuso za wapiganaji.
----- Letter 24, 1888.
MPANGO KAMILI UMEFANYWA KWA MSAMAHA Machi 18
BWANA yu karibu nao waliovunjika moyo, Nao waliopondeka roho huwaokoa.
Zaburi 34:18.
Usidhani kwamba kwa sababu umefanya makosa, basi, siku zote utakuwa chini ya
hukumu, kwa kuwa si lazima kuwa hivyo....
Je! tutaziangalia dhambi zetu na kuanza kuomboleza, na kusema, Nimefanya makosa,
nami siwezi kuja kwa Mungu kwa ujasiri wo wote ule? Je! Biblia haisemi,
"Tukiziungama dhambi zetu, Yeye ni mwaminifu na wa haki hata atuondolee dhambi
zetu, na kutusafisha na udhalimu wote"? l Yohana 1:9. Ni jambo linalofaa kwetu
kutambua jinsi dhambi ilivyo na tabia ya kutisha. Ni dhambi iliyosababisha kifo kile cha
aibu cha Kristo pale Kalvari. Walakini, japo tunapaswa kutambua dhambi ilivyo ya
kutisha, hata hivyo isingetupasa kuisikiliza sauti ya adui yetu, isemayo, "Umetenda
dhambi, wala huna haki yo yote ya kudai ahadi za Mungu." Mnapaswa kusema hivi kwa
adui yule, "Imeandikwa, 'Kama mtu akitenda dhambi tunaye Mwombezi kwa Baba, Yesu
Kristo mwenye haki' (l Yohana 2:1)."...
Mtunga Zaburi anasema, "Nalikujulisha dhambi yangu, Wala sikuuficha upotovu wangu.
Nalisema, Nitayakiri maasi yangu kwa BWANA, Nawe ukanisamehe upotovu wa
dhambi yangu." Zaburi 32:5.... Huo ndio uzoefu tunaotakiwa kuwa nao. ----- Letter 97,
1895.
Daudi alisamehewa dhambi zake kwa sababu alijinyenyekeza moyo wake mbele za
Mungu kwa toba na majuto ya moyoni, na kusadiki kwamba ahadi ya Mungu ya
kusamehe ingetimizwa kwake. Aliungama dhambi yake, naye akaongolewa tena. Katika
furaha yake kuu ya kuwa na hakika ya msamaha, alishangilia, "Heri aliyesamehewa
dhambi, Na kusitiriwa makosa yake. Heri BWANA asiyemhesabia upotovu, Ambayerohoni mwake hamna hila." Zaburi 32:1,2. Baraka [furaha] huja kwa sababu ya msamaha;
msamaha huja kwa njia ya imani kwamba dhambi, ikiungamwa na kutubiwa,
inachukuliwa na Mchukuzi Mkuu wa Dhambi. Hivyo kutoka kwa Kristo huja mibaraka
yetu yote. Kifo chake ni kafara ya upatanisho kwa dhambi zetu. Yeye ndiye Mpatanishi
mkuu ambaye kwa njia yake tunapokea rehema na upendeleo wa Mungu. ----- 3BC 1146.
KUJENGA KWA AJILI YA UMILELE WAKO Machi 19
Basi kila asikiaye hayo maneno yangu, na kuyafanya, Atafananishwa na mtu mwenye
akili, aliyeijenga nyumba yake juu ya mwamba; mvua ikanyesha, mafuriko yakaja, pepo
zikavuma, zikaipiga nyumba ile, isianguke; kwa maana misingi yake imewekwa juu ya
mwamba.
Mathayo 7:24,25.
Ujenzi wa tabia yetu ni kazi ya maisha, na hiyo [tabia] ni kwa ajili ya umilele wetu.
Endapo wote wangetambua hivyo, endapo wangekuwa wamezinduka na kuwaza kwamba
kila mmoja wetu peke yake anaamua majaliwa yake ama kwa uzima ule wa milele ama
kwa maangamizi yale ya milele, basi, ni mabadiliko yalioje ambayo yangeonekana
[katika tabia yetu]! Kipindi hiki cha muda wetu wa majaribio kingetumika kwa tofauti
ilioje!...
Katika kujenga tabia yetu jambo la maana kuliko yote ni kwamba inatupasa kuchimba
chini sana, tukiondoa kila aina ya uchafu na kujenga juu ya mwamba ule usiotikisika,
mwamba imara, Kristo Yesu. Msingi ukiisha kuwekwa imara, basi, tunahitaji hekima ili
kujua namna tunavyotakiwa kujenga.... Katika Sheria yake [Amri Kumi] Mungu
ametupatia kiolezo, na ni kwa mfano wa kiolezo hicho tunapaswa kujenga. Sheria yake ni
kanuni kuu [kipimo kikuu] ya haki. Inaiwakilisha tabia ya Mungu, nayo ndiyo kipimo
cha utiifu wetu kwa serikali yake.
Ukamilifu ni wa lazima ili kuweza kufanikiwa katika ujenzi huo wa tabia yetu. Lazima
pawepo na ari ya kutekeleza mipango ya Mjenzi Mkuu [Kristo]. Mbao zilizotumika ni
lazima ziwe imara; kazi yo yote ya kizembe, isiyoaminika haiwezi kukubaliwa;
ingeliharibu jengo hilo. Nguvu zote za mwili sharti zitumike katika kazi hiyo. Inataka
nguvu na bidii; hakuna nguvu ya akiba yo yote itakayotumika kwa mambo yale
yasiyokuwa na umuhimu wo wote. Lazima pawepo na nia ya kutumia nguvu za
kibinadamu katika kazi hiyo, kwa kushirikiana na Mhudumu huyo wa Mbinguni [Kristo].
Lazima iwepo juhudi ya dhati, ya kudumu, ili kuweza kujinasua na desturi [mila] na semi
zake, pamoja na uhusiano wetu na ulimwengu huu. Fikira zenye kina, makusudi ya dhati, ukamilifu thabiti, ni muhimu. Haipasi kuwapo uzembe wo wote. Maisha ni amana
takatifu tuliyopewa; na kila dakika haina budi kutumika vizuri....
Kumbukeni ya kwamba mnajenga kwa ajili ya maisha yale ya milele. Hakikisheni
kwamba msingi wenu ni imara; kisha jengeni kwa imara, na kwa juhudi isiyojua kukata
tamaa, lakini kwa upole, unyenyekevu, na upendo. Hivyo ndivyo nyumba yenu
itakavyosimama pasipo kutikisika, sio tu dhoruba ya majaribu itakapokuja bali wakati ule
gharika iangamizayo ya ghadhabu ya Mungu itakapoifagia dunia yote. ----- YI, Feb. 19,
1903.
USIYAPE MAJARIBU NAFASI YO YOTE Machi 20
Kumcha BWANA ni tumaini imara; Watoto wake watakuwa na kimbilio. Mithali 14:26.
Mungu anataka kwamba sisi tuziungame dhambi zetu na kuinyenyekeza mioyo yetu
mbele zake; lakini kwa wakati uo huo yatupasa kuwa na tumaini kwake yeye kama Baba
yetu mpole, ambaye hatawaacha wale wanaomtumainia. Hatutambui jinsi wengi wetu
tunavyoenenda kwa kuona wala si kwa imani. Tunayaamini mambo yale yanayoonekana,
lakini hatuzithamini ahadi zake za thamani zilizotolewa kwetu katika Neno lake. Hata
hivyo, sisi hatuwezi kumvunjia Mungu heshima kwa dhahiri kabisa kama kwa kuonyesha
kwamba hatuyaamini yale asemayo. ----- RH, Aprili 8, l884.
Hata kwa dakika moja tu usiyakubali majaribu ya Shetani kwamba ati yanaafikiana na
moyo wako. Yape kisogo kama vile ambavyo ungefanya kama ungemwona adui huyo
mwenyewe. Kazi yake Shetani ni kumkatisha tamaa mtu. Kazi yake Kristo ni kuuchochea
moyo kwa kuupa imani na tumaini. Shetani anataka kutuvuruga ili tusiwe na imani.
Anatuambia kwamba matumaini yetu yamejengwa juu ya msingi wa uongo, wakati
yamejengwa juu ya neno lile lililo imara, lisilobadilika la Yeye asiyeweza kusema uongo.
----- MS 31, 1911.
Anapotushawishi [Shetani] kuwa na mashaka iwapo sisi kweli ni watu anaowaongoza
Mungu, ambao kwa kuwapima na kuwathibitisha anawatayarisha kusimama katika siku
ile kuu, sisi hatuna budi kuwa tayari kupambana na hila zake [Shetani] kwa kumpa
ushahidi ulio wazi kutoka katika Neno la Mungu lisemalo kwamba hao ndio watu wake
wa masalio wazishikao amri [kumi] za Mungu na imani ya Yesu. ----- RH, Aprili 8,
1884. Hebu na tuweke tumaini letu kwa Mungu wetu kwa ukamilifu, kwa unyenyekevu,
pasipokuwa na kujipenda nafsi ko kote. Sisi ni watoto wake wadogo, na hivyo ndivyo
yeye anavyotushughulikia. Tunapomkaribia yeye, anatulinda kwa rehema zake kutokana
na mashambulio yenye nguvu ya yule adui. Kamwe [Mungu] hatamsaliti yule
anayemtumainia kama vile mtoto mdogo anavyowatumainia wazazi wake. Anawaona
wale walio wanyenyekevu, yaani, wale wanaomtumainia wanapomkaribia, naye kwa
huruma na upendo anawakaribia, na kuinua juu kwa ajili yao bendera yake dhidi ya yule
adui. "Usiwaguse," Yeye asema, "maana hao ni wangu. Nimewachora juu ya vitanga vya
mikono yangu." Anawafundisha namna ya kuitumia imani yao bila kuwa na maswali yo
yote wanapoomba uweza wake upate kufanya kazi kwa ajili yao. Wakiwa wanayo hakika
wanasema, "Huku ndiko kushinda kuushindako ulimwengu, hiyo imani yetu." l Yohana
5:4. ----- Letter 5, 1903.
KUPENYA JUU YA UKUNGU WA MASHAKA Machi 21
Iweni hodari, mpige moyo konde [atawaimarisha mioyo yenu], Ninyi nyote mnaomngoja
BWANA. Zaburi 31:24 [KJV].
Hata Wakristo wenye uzoefu wa miaka mingi mara kwa mara wanashambuliwa na
mashaka ya kutisha mno pamoja na kutangatanga katika mawazo yao.... Haiwapasi
kufikiri kwamba kutokana na majaribu hayo mambo yenu hayana matumaini yo yote....
Mtumainini Mungu, Mtegemeeni Yeye na kutulia katika ahadi zake. ----- Letter 52, 1888.
Shetani anapokuja na kuleta mashaka yake na kutokuamini, funga mlango wa moyo
wako. Fumba macho yako ili usikiangalie kivuli chake cha kishetani. Yainue juu [macho
yako] ambako yanaweza kuyaona mambo yale ya milele, nawe utakuwa na nguvu kila
saa. Kupimwa kwa imani yako ni kwa thamani kuliko dhahabu.... Kunakufanya uwe
shujaa kuipiga vita ile ya Bwana....
Shetani anaungana na kila mmoja anayetaka kuungana naye. Kama atawapata wale
waliokwisha kupata uzoefu katika mambo ya dini, hao ndio vibaraka wake wanaofaa
sana kwake kuweza kuwafikia na kuzizungushia roho zao hali ile ya kutokuamini.
Huwezi kumudu kuruhusu mashaka yo yote kuingia moyoni mwako. Usimfurahishe
Shetani kiasi cha kumweleza mizigo mizito ya kutisha unayoibeba. Kila wakatiunapofanya hivyo, Shetani anacheka kwa vile roho yake inaweza kukutawala kiasi hicho
na kwamba wewe huwezi tena kumwona Yesu Kristo Mkombozi wako....
Inatupasa sisi kumtangaza yule aliyetuita kutoka gizani kuingia katika nuru yake ya
ajabu. Ni kwa njia ya imani iliyo hai sisi tunakaa katika nuru ile. Ni kwa njia ya imani
hiyo iliyo hai sisi tunaifurahia nuru ile kila siku. Hatupaswi kuongea juu ya mashaka na
maonjo yetu, maana yanazidi kuongezeka kila wakati tunapoongea juu yake. Kila wakati
tunapoongea juu ya hayo, Shetani anapata ushindi; lakini tunaposema, "Nitaweka
mikononi mwake [Mungu] utunzaji wa roho yangu, kama vile kwa shahidi yule aliye
mwaminifu," hapo ndipo tunapotoa ushuhuda kuonyesha kwamba tumejitoa wenyewe
kwa Yesu Kristo pasipo kuacha kitu, na hapo ndipo Mungu anatupa sisi nuru, nasi
tunafurahi ndani yake. ----- MS 17, 1894.
Moyo ule umpendao Mungu, unapenya juu ya ukungu wa mashaka; mtu huyo anapata
uzoefu wa maisha unaong'aa, mpana na wenye kina, naye anakuwa mpole na katika tabia
yake anafanana na Kristo. Moyo wake anampa Mungu, unafichwa pamoja na Kristo
ndani ya Mungu. ----- 7BC 907.
USHINDI JUU YA MAOVU UNAOENDELEA Machi 22
Heri mtu astahimiliye majaribu; kwa sababu akiisha kukubaliwa ataipokea taji ya uzima,
Bwana aliyowaahidia wampendao. Yakobo 1:12.
Sio utaratibu wala mapenzi ya Mungu kuwakinga watu wake wasipate majaribu.... Kweli
inapokaa moyoni, Mkristo huyo ataletwa katika mapambano.... Kuna upinzani ndani ya
nyumba yake mwenyewe, hata ndani ya moyo wake mwenyewe, na hakuna cho chote,
isipokuwa Roho wa Mungu aliye huru, kinachoweza kumhakikishia ushindi. ----- MS 59,
1900.
Mwanzo wa kuanguka katika majaribu ni katika dhambi ile ya kuuacha moyo wako
kuyumba, yaani, kutokuwa na tumaini thabiti kwa Mungu wako. Daima yule mwovu
anatafuta nafasi ya kumweleza Mungu vibaya, na kuuvuta moyo kwa kile
kilichokatazwa. Akiweza, ataukaza moyo huo juu ya mambo ya ulimwengu huu.
Atajaribu kuziamsha hisia za moyoni mwako, kuziamsha tamaa zako za mwili,
kuyafunga mapenzi yako juu ya kile ambacho si kwa manufaa yako; lakini ni wajibu
wako kuidhibiti kila hisia ya moyoni mwako na tamaa zako za mwili, ili kwa utulivuzipate kuitii akili yako na dhamiri yako inavyokuambia. Hapo ndipo Shetani hupoteza
nguvu yake ya kuutawala moyo wako. Kazi anayotuitia Kristo ni kazi ya kuendelea
kushinda maovu ya kiroho yaliyo katika tabia zetu. Mielekeo mibaya ya asili ni lazima
tuishinde.... Uchu mbaya wa chakula na tamaa ya mwili ni lazima tuvishinde, na nia yetu
haina budi kuwekwa upande wa Kristo kabisa. ----- RH, Juni 14, 1892.
Tunaomba kwa Baba yetu aliye mbinguni, tukisema, "Usitutie majaribuni," na kisha
mara nyingi sana, tunashindwa kuilinda miguu yetu isiingie majaribuni. Yatupasa kuwa
mbali na majaribu yale yanayotuangusha kwa urahisi. Mafanikio yetu hufanywa na sisi
wenyewe kwa njia ya neema yake Kristo. Yatupasa kulivingirishia mbali na njia yetu
jiwe lile linalotuangusha ambalo limetuletea sisi na wengine huzuni nyingi sana. ----- MS
124, 1902.
Majaribu na maonjo yatatujia sisi sote, lakini hatuna haja kamwe ya kufanywa na yule
adui kuwa wabaya kupindukia. Mwokozi wetu ameshinda kwa niaba yetu. Shetani sio
kwamba hashindikani.... Kristo alijaribiwa ili apate kujua jinsi ya kumsaidia kila mtu
ambaye hatimaye angeweza kujaribiwa. Kujaribiwa kwenyewe sio dhambi; dhambi i
katika kuanguka. Kwa mtu yule anayemtegemea Yesu, majaribu yanamaanisha ushindi
na nguvu nyingi zaidi. -----
MS 113, 1902.
JIHADHARINI NA HILA ZAKE SHETANI Machi 23
Shetani asije akapata kutushinda, kwa maana hatukosi kuzijua fikira [hila] zake.
2 Wakorintho 2:11.
Mipango na hila za Shetani hutushawishi kila upande. Daima yatupasa kukumbuka
kwamba anakuja kwetu kwa kujificha, akiyaficha makusudi yake na aina ya majaribu
yake. Anakuja katika mavazi ya nuru, bila shaka akiwa amevaa mavazi ya malaika wale
watakatifu, ili tusipate kutambua kwamba ndiye. Yatupasa kutumia uangalifu mkubwa
sana, kuchunguza kwa karibu sana hila zake, tusije tukadanganywa. ----- MS 34, 1897.
Shetani anao malaika zake waovu wanaotuzunguka kila upande, na ijapokuwa hawawezi
kuyasoma mawazo ya wanadamu, wanaangalia kwa karibu sana maneno yao pamoja namatendo yao. Shetani anatumia kwa manufaa yake udhaifu na kasoro za tabia
zinazodhihirishwa kwa njia hiyo, na kuleta majaribu yake mahali ambapo pana nguvu
kidogo mno ya kujizuia. Analeta vishawishi vyake viovu na kuyaamsha mawazo ya
kidunia, akijua fika kwamba kwa njia hiyo anaweza kuileta roho ya mtu huyo katika hatia
na utumwa. Kwa wale walio wachoyo [wanaojipendelea wenyewe], wapenda dunia,
wenye kupenda mno mali, wenye kiburi, wenye kutafuta makosa kwa wengine ----- kwa
wale wote wanaotunza makosa yao na kasoro zao za tabia ----- Shetani anawaonyesha
jinsi ya kujitosheleza nafsi zao, tena anamwongoza mtu huyo kwenda mbali katika njia
ambayo inashutumiwa na Biblia....
Kwa kila kundi la majaribu iko dawa yake. Hatuachwi peke yetu kupigana vita juu ya
nafsi na tabia zetu za dhambi kwa kutegemea nguvu zetu za kibinadamu. Yesu ndiye
msaada wetu wenye nguvu, msaada usiokosekana kamwe.... Hakuna wanaoweza
kushindwa au kukatishwa tamaa, wakati mpango wa kutosha umewekwa kwa ajili yetu.
Mawazo yetu ni lazima yazuiwe, wala yasiachwe kutangatanga ovyo. Yazoezwe
kutafakari sehemu fulani za Maandiko, hata sura nzima zinaweza kukaririwa, na
kusemwa tena wakati ule Shetani anapokuja na majaribu yake. Sura ile ya hamsini na
nane ya Isaya ni mojawapo iliyo na manufaa kwa kusudi hili. Ujengee ukuta moyo wako
kwa vizuio na mafundisho yaliyotolewa kwa uvuvio wa Roho wa Mungu. Shetani
anapotaka kuyageuza mawazo yetu kutafakari mambo ya kidunia na ya tamaa za mwili,
anaweza kupingwa kwa ufanisi kabisa kwa kusema, "Imeandikwa." ----- RH, Aprili 8,
1884.
JINSI NGUVU ZA SHETANI ZINAVYOVUNJWA Machi 24
Katika uungwana huo Kristo alituandika huru; kwa hiyo simameni, wala msinaswe tena
chini ya kongwa la utumwa. Wagalatia 5:1.
Toba ya mtu mmoja inasababisha furaha isiyoelezeka kwa yale majeshi yote ya
mbinguni. Nyimbo tamu za utukufu zinapigwa kutoka kwenye kila kinubi na kuimbwa na
kila sauti kwa sababu jina jingine limeandikwa katika kitabu kile cha uzima, nurunyingine imewashwa kuangaza katikati ya giza la kimaadili la ulimwengu huu
ulioharibika. Tukio lilo hilo linasababisha mshangao mkubwa sana miongoni mwa
malaika wale walioanguka, nalo linamdhalilisha sana kiongozi wao mkuu katika uasi ule
dhidi ya Sheria takatifu ya Mungu [Amri Kumi]. Mkuu huyo wa giza amwonapo mtu
yule aliyemhesabu kuwa ni mali yake akiponyoka chini ya madaraka yake kama vile
ndege anavyoponyoka katika mtego wa mwindaji, na kumfanya Kristo kuwa kimbilio
lake, basi, anafanya kazi yake ya kishetani kwa nguvu ili kumnasa tena yule
aliyemponyoka. ----- MS 46a, 1886.
Yatupasa sisi kufikiria zaidi juu ya matokeo ya uongofu ule wa kweli. Sio tu mwenye
dhambi anasamehewa anapotubu na kuungama uovu wake; bali anakuwa mtoto wa
Mungu,... Mrithi wa Mungu na mrithi pamoja na Kristo wa urithi ule wa milele.... Nguvu
za Shetani zinavunjwa. Mwanadamu huyo analetwa katika umoja mtakatifu na Kristo. ---
-- Letter 63, 1905.
Hakuna mtu ye yote anayeletwa kwa Kristo... pasipo kumshinda yule mjaribu, na
kukiponda kichwa cha yule nyoka. Jambo hilo litaamsha chuki ya yule adui kufanya
jitihada kubwa zaidi.... Akiwa amepigwa na butwaa kwa kumpoteza mateka wake,
Shetani atajaribu kumdanganya kwanza, kisha kumkandamiza na kumtesa. Wanadamu
waovu, waliokemewa na kanuni na kielelezo cha wale wanaokuja kwenye nuru ya kweli
ile ya Biblia, watakuwa vibaraka wa yule adui mkuu wa watu, nao hawataiacha njia hata
moja isiyojaribiwa ili kuwavuta mbali na utii wao kwa Mungu na kuwashawishi kuiacha
njia ile nyembamba ya utakatifu.
Lakini asiwepo hata mmoja atakayeingiwa na wasiwasi wala hofu. Neno la Mungu
limeahidi kwamba kama wao ni wakweli kwa kanuni, yaani, kama wanayaamini na
kuyatii matakwa yote ya Mungu, basi, wao ni watu wa nyumbani mwake Mungu, yaani,
wana wa Mfalme yule wa mbinguni. Wanayo hakika ya kupewa msaada kutoka upande
wa majeshi yao ya mbinguni na kuwa washindi kwa njia ya wema wake Kristo ----- zaidi
ya washindi kwa njia yake Yeye aliyewapenda. ----- MS 46a, 1886.
HATUOKOLEWI KWA KUWAKILISHWA NA MWINGINE Machi 25
Lakini kila mtu na aipime kazi yake mwenyewe, ndipo atakapokuwa na sababu ya
kujisifu ndani ya nafsi yake tu, wala si kwa mwenzake. Wagalatia 6:4Hakuna hata mmoja awezaye kumtumikia Mungu kwa kumtuma mtu wake wa
kumwakilisha. Kuna wengi sana wanaoonekana kufikiri kwamba kuna [mwanadamu]
mmoja ulimwenguni humu ambaye ana nguvu kuliko Kristo, ambaye wanaweza
kumtegemea. Na badala ya wao kuja moja kwa moja kwa Kristo, jinsi walivyo, na
kwenda kwake wenyewe bila kuacha kitu nyuma, wao wanaomba msaada kwa
mwanadamu. Mungu anataka sisi tuwe na uzoefu [maisha] kila mmoja wa kwake
mwenyewe.... Mimi siwezi kukujengea wewe tabia yako, wala wewe huwezi kunijengea
mimi tabia yangu. ----- GCB, Aprili 23, 1901.
Injili inashughulika na mtu mmoja mmoja. Kila mwanadamu anayo nafsi yake ya
kuiokoa au kuipoteza. Kila mmoja anao utu wake wa pekee ambao unatofautiana na ule
wa wengine wote. Kila mmoja anatakiwa kuamini yeye mwenyewe, kuongoka yeye
mwenyewe. Yampasa kuipokea kweli, kutubu, kuamini, na kutii yeye mwenyewe.
Yampasa kutumia nia yake kwa ajili yake mwenyewe.... Kila mmoja hana budi
kujisalimisha mwenyewe kwa Mungu kwa tendo lake mwenyewe. ----- MS 28, 1898.
Mungu hapendi utu wetu uharibiwe; si kusudi lake kwamba watu wawili wafanane
kabisa katika hisia zao na tabia zao. Wote wanazo tabia ambazo ni za pekee kwao
wenyewe, na hizo hazitakiwi kuharibiwa, bali kukuzwa, kubadilishwa, na kufananishwa
na mfano ule wa Kristo. Bwana anavigeuza vipawa vile vya kuzaliwa navyo pamoja na
uwezo tulio nao kuwa njia zenye manufaa. Katika kuziboresha akili zetu ambazo Mungu
ametupa, talanta na uwezo tulio nao vinakuzwa kama mjumbe huyo wa kibinadamu
atatambua ukweli kwamba nguvu zake zote amepewa na Mungu, zipate kutumika si kwa
kusudi la ubinafsi.... bali kwa utukufu wa Mungu na manufaa ya wanadamu wenzetu. ----
- Letter 20, 1894.
Kwa kila mtu Mungu ----- sio mwanadamu ----- amempa kazi yake. Hii ni kazi ya kila
mtu mmoja mmoja ----- kujenga tabia kwa mfano wa Mungu. Ua la kondeni halitakiwi
kujitahidi ili lifanane na ua waridi. Kuna tofauti katika mpangilio wa maua na matunda,
lakini vyote hupata tofauti zao za pekee kutoka kwa Mungu.... Kwa hiyo ni kusudi la
Mungu kwamba hata watu wale walio bora sana hawataweza kuwa na tabia ya aina moja.
Maisha yaliyotolewa wakf katika kumtumikia Mungu yatakuzwa na kufanywa kuwa
mazuri yakiwa katika utu wake wa pekee. ----- MS 116, 1898.
SEHEMU YA MUNGU NA YANGU Machi 26
Basi, wapendwa wangu, kama vile mlivyotii sikuzote, si wakati mimi nilipokuwapo tu,
bali sasa zaidi sana mimi nisipokuwapo, utimizeni wokovu wenu wenyewe kwa kuogopa na kutetemeka. Kwa maana ndiye Mungu atendaye kazi ndani yenu, kutaka kwenu na
kutenda kwenu, kwa kulitimiza kusudi lake jema. Wafilipi 2:12,l3.
"Utimizeni wokovu wenu wenyewe kwa kuogopa na kutetemeka." Maana yake nini?
Maana yake ni kwamba kila siku wewe inakupasa kutozitegemea juhudi zako za
kibinadamu na hekima yako. Inakupasa kuogopa kusema ovyo ovyo tu, kuogopa kufuata
hisia zako mwenyewe, kuogopa kwamba kiburi cha moyo wako na kuipenda kwako
dunia hii na tamaa za mwili wako vitakutenga na neema yake ya thamani ambayo Bwana
Yesu anatamani kukupa wewe. -----
MS 42, 1890.
Kutenda kazi kwa mwanadamu kulikoelezwa katika fungu hilo, si kazi ya kujitegemea
mwenyewe ambayo anaifanya pasipo Mungu. Tegemeo lake lote ni juu ya uwezo na
neema ya Mtendakazi yule wa Mbinguni. Wengi hapa ndipo wanapokosea lengo, nao
hudai kwamba mtu anapaswa kutenda kazi hiyo peke yake, bila kutegemea uweza wa
Mungu. [Wazo] hilo halilingani na fungu hilo. Mwingine anabisha akisema kwamba
mwanadamu yuko huru na uwajibikaji wote, ati kwa sababu Mungu anafanya yote, yaani,
KUTAKA pamoja na KUTENDA. Fungu hilo linamaanisha kwamba wokovu wa roho ya
mwanadamu unataka nguvu yake ya nia iwekwe chini ya nia ya Mungu.... Na hilo ndilo
pambano gumu kabisa, kali kabisa kwa mwanadamu ambalo huambatana na kusudi lile
na saa ile ya kukata shauri na kuamua kuweka mapenzi na njia yake chini ya mapenzi ya
Mungu na njia ya Mungu. ----- Letter 135, 1898.
Mwanadamu amepewa sehemu yake katika pambano hilo kuu la uzima wa milele;
inampasa kuitikia kwa utendaji ule wa Roho Mtakatifu. Itahitaji juhudi nyingi kuzivunja
nguvu zile za giza, bali Roho, anayetenda kazi ndani yake, anaweza na atalitimiza kusudi
hilo. Lakini mwanadamu si chombo kisichoweza kutenda jambo lo lote kinachookolewa
katika hali yake ya uvivu. Anatakiwa kutumia nguvu ya kila musuli wa mwili wake
katika kupigania uzima ule wa milele; hata hivyo, ni Mungu anayempa ufanisi. ----- ST,
Nov. 5, 1896.
Hizo ndizo kazi zake mwanadamu, na hizo ndizo kazi zake Mungu.... [Kazi] hizo mbili
zikiunganishwa pamoja, hapo ndipo mwanadamu atakuwa mshindi, na hatimaye
atapokea taji ya uzima.... Anatumia kila neva na musuli ili apate kuwa mshindi mwenye
mafanikio katika kazi hiyo, na ili apate mbaraka ule wa thamani wa uzima wa milele. ----
- MS 13, 1888.
PAMBANO TOKA KWA MAJESHI YASIYOONEKANA Machi 27 Kwa maana kushindana kwetu sisi si juu ya damu na nyama; bali ni juu ya falme na
mamlaka, juu ya wakuu wa giza hili, juu ya majeshi ya pepo wabaya katika ulimwengu
wa roho. Waefeso 6:12.
Bwana angependa kuiamsha mioyo yetu kuhusu mvuto wa malaika hao wabaya. Kristo
hatuambii juu ya hatari ile inayotutishia kutokana na mashambulio ya adui yule
aliyeanguka pasipo kutupa sisi uwezo wa kulipinga kila shambulio analofanya....
Wajumbe ambao ni malaika, wema au wabaya, wanajitahidi kututawala, na kila mvuto
ambao kwa sasa unatujia ni muhimu kuuchunguza kwa karibu sana. ----- MS 78, 1905.
Shetani daima yuko macho sana ili kutudanganya sisi na kutupotosha. Anatumia kila
aina ya anasa ili kutuvuta kuingia katika njia ile pana ya uasi. Anafanya kazi yake kwa
kuzichanganya hisia zetu pamoja na tamaa potofu, na kuziondoa alama za mipaka kwa
kuweka maandishi yake ya uongo juu ya vibao vya kuonyesha njia ambavyo Mungu
ameviweka ili kutuonyesha sisi njia ile ya kweli. Ni kwa sababu wajumbe hao wabaya
wanajitahidi kuzuia kila mwonzi wa nuru ili usipate kuingia moyoni ndio maana viumbe
wale wa mbinguni wamechaguliwa kufanya kazi yao ya utumishi, ili kuwaongoza,
kuwalinda, na kuwatawala wale ambao watakuwa warithi wa wokovu. Asiwepo mtu wa
kukata tamaa kwa sababu ya mielekeo mibaya ya tabia yake aliyorithi, lakini Roho wa
Mungu anapomhakikishia dhambi zake, basi, mwenye dhambi huyo hana budi kutubu na
kuungama na kuachana na uovu huo. Walinzi hao waaminifu wako katika ulinzi wao ili
kuwaongoza watu katika njia zile za kweli. ----- 6BC 1120.
Aidha malaika wale wabaya au malaika wa Mungu wanaitawala mioyo ya watu. Mioyo
yetu inatolewa kutawaliwa na Mungu, ama kutawaliwa na nguvu zile za giza; na litakuwa
jambo jema kwetu sisi kujiuliza kwamba tunasimama wapi leo hii ----- iwapo ni chini ya
bendera ile yenye damu ya Mfalme Imanueli, au chini ya bendera ile nyeusi ya nguvu zile
za giza. ----- 6BC 1120.
Kadiri watu wa Mungu wanavyohifadhi uaminifu wao kwake, kadiri wanavyomshikilia
Yesu kwa imani, ndivyo wanavyojiweka chini ya ulinzi wa malaika wale wa mbinguni,
na Shetani hataruhusiwa kutumia mbinu zake za kishetani juu yao ili kuwaangamiza. -----
RH, Nov. 19, 1908.
Ni furaha kuu mno ya malaika wale wa mbinguni kuweka ngao yao ya upendo juu ya
watu wale wanaomgeukia Mungu. ----- 7BC 922.KIELELEZO CHAKE KRISTO KATIKA KUSHINDA Machi 28
Umzuie mtumishi wako asitende mambo ya kiburi, yasinitawale mimi. Ndipo
nitakapokuwa kamili, Nami nitakuwa safi, sina kosa lililo kubwa. Zaburi 19:13.
Majaribu makuu ya kwanza ambayo mwanadamu angeweza kuzingirwa nayo na
kushambuliwa, alikutana nayo Kristo na kuyashinda katika nyika ile. Ushindi wake juu
ya uchu wa chakula, kiburi, na ulimwengu huonyesha jinsi sisi tunavyoweza kushinda.
Shetani amewashinda mamilioni kwa kuwajaribu kwa uchu wa chakula na kuwashawishi
watu kujitoa kufanya dhambi za kiburi [za makusudi]. Kuna wengi wanaojidai kwamba
wao ni wafuasi wake Kristo,... ambao, bila kufikiri hata kidogo, wanajitosa katika
mandhari za majaribu ambazo zingehitaji mwujiza kuwatoa humo bila ya wao kupata
mawaa. Tafakuri na maombi vingewahifadhi na kuwaongoza kuziepuka hali hizo za
hatari walimojitumbukiza wenyewe ambazo zinampa Shetani manufaa juu yao.
Ahadi za Mungu si kwa ajili yetu kuzidai bila kuwa na subira, ili zitulinde tunapokimbia
bila kujali na kujiingiza katika hatari, tunapozivunja sheria za maumbile yetu, au
kuipuuzia busara yetu na uwezo wetu wa kuamua aliotupa Mungu. Hiyo isingekuwa
imani ya kweli bali kiburi..... Shetani anakuja kwetu akituletea heshima ya kidunia, mali,
na anasa za maisha haya. Majaribu hayo yanawekwa tofauti tofauti kulingana na watu wa
kila cheo na kila daraja, ili kuwajaribu waende mbali na Mungu kujitumikia nafsi zao
wenyewe kuliko Muumbaji wao. "Haya yote nitakupa," alisema Shetani kwa Yesu. "Yote
haya nitakupa," asema Shetani kwa mwanadamu. "Fedha yote hii, nchi hii, mamlaka yote
haya, na heshima hii, na utajiri huu, nitakupa wewe"; na mwanadamu anashawishika,
anadanganyika, na kwa hila hiyo anavutwa kwenda kwenye maangamizi yake. Iwapo sisi
tunajitoa wenyewe kuwa na moyo wa kuipenda dunia hii na maisha yake, basi, Shetani
anaridhika.
Mwokozi alimshinda adui huyo mwerevu sana, akatuonyesha jinsi nasi tunavyoweza
kushinda. Ametuachia kielelezo chake, yaani, kumpinga Shetani kwa Maandiko.
Angeweza kutumia uweza wake mwenyewe kama Mungu,.... lakini kielelezo chake kama
hicho kisingekuwa na manufaa yo yote kwetu. Kristo alitumia Maandiko peke yake. Ni
jambo la maana jinsi gani, basi, kwamba Neno la Mungu lijifunzwe kwa ukamilifu na
kufuatwa, ili wakati ule wa hatari tuweze kuwa tu"mekamilishwa [tu]pate kutenda kila
tendo jema" na hasa tukiwa tumeimarishwa kukutana na adui huyo mwerevu sana. -----
Letter 1a, 1872.JINSI YA KUDUMISHA MSIMAMO WAKO! Machi 29
Vivyo hivyo ninyi nanyi jihesabuni kuwa wafu kwa dhambi na walio hai kwa Mungu
katika Kristo Yesu. Basi, dhambi isitawale ndani ya miili yenu ipatikanayo na mauti, hata
mkazitii tamaa zake. Warumi 6:11,12.
Wengine wanaifikiria dhambi kuwa ni kitu rahisi kabisa hata hawana kinga yo yote dhidi
ya kuitenda wala kukabiliana na athari zake....
Kama wewe unadhani kwamba kwa dakika moja tu Mungu ataweza kuihesabu dhambi
yako hiyo kuwa ni kitu rahisi tu, au kukuruhusu, au kukusamehe ili uendelee kuitenda,
wala nafsi yako isipate adhabu yo yote kwa kufanya hivyo, basi, wewe umedanganywa
vibaya sana na Shetani. Uvunjaji wo wote wa makusudi wa sheria ile [Amri Kumi] ya
haki ya Yehova unauacha moyo wako wazi kuweza kupata mashambulio yote ya Shetani.
Unapopoteza msimamo wako unaoujua kwa dhati, moyo wako unageuka na kuwa
uwanja wa mapambano ya Shetani; unayo mashaka na hofu ya kutosha kuzifisha ganzi
nguvu zako na kukufanya ukate tamaa....
Kumbuka kwamba kujaribiwa si dhambi. Kumbuka kwamba, haidhuru mazingira yawe
ya kumjaribu mtu kwa kiasi kikubwa jinsi gani, hakuna kitu cho chote kinachoweza
kuudhoofisha kweli moyo wake mradi tu asianguke majaribuni bali adumishe msimamo
wake. Mambo yale yaliyo ya maana sana kwenu kila mmoja peke yake yamo mikononi
mwenu wenyewe. Hakuna anayeweza kuyadhuru pasipo kibali chenu. Majeshi yote ya
Shetani hayawezi kukudhuru wewe isipokuwa kama wewe mwenyewe unaufungua moyo
wako kuruhusu hila zake na mishale ya Shetani kuingia humo. Maangamizi yako
hayawezi kutokea kamwe mpaka nia yako ikubali. Kama moyo wako haujachafuliwa
kwa njia yo yote ile, basi, uchafu wote unaokuzunguka wewe hauwezi kukutia waa, wala
kukuchafua.
Uzima wa milele ni wa thamani kuliko vyote kwetu au si kitu kwetu. Ni wale tu
wanaoweka juhudi yao ya kudumu pamoja na bidii isiyojua kuchoka, wakiwa wana
shauku kubwa kulingana na thamani ya kitu kile wanachokitafuta, hao ndio watakaopata
uzima huo ambao unakadiriwa kuwa uko sawa na uzima ule alio nao Mungu....
Tunacho kielelezo cha Adamu na Hawa mbele yetu, basi, matokeo ya kosa lao
yangeuongoza moyo wa kila mmoja wetu kuepukana na dhambi, yaani, kuichukia
dhambi kama kitu cha kuchukiza mno kama ilivyo hasa, na kwa kuzingatia mateso ya
hakika ambayo dhambi inaweza kuleta, tujisikie kwamba ni afadhali kupata hasara yamambo yote kuliko kukiuka amri yo yote ya Mungu iliyo ndogo sana. ----- YI, Juni 29,
1893.
MAFANIKIO KATIKA KUMPINGA Machi 30
Basi mtiini Mungu. Mpingeni Shetani, naye atawakimbia. l Yakobo 4:7.
Wako wale wanaojitia katika mandhari za hatari na maangamizi bila kujali, na kujiingiza
wenyewe katika majaribu, ambayo yangehitaji mwujiza ufanyike ili wapate kutoka ndani
yake bila kupata madhara wala mawaa. Matendo hayo ni kiburi [cha makusudi], ambacho
Mungu hapendezwi nacho. Jaribu lile la Shetani kwa Mwokozi wa ulimwengu huu
kumtaka ajitupe chini kutoka kwenye kinara cha hekalu, lilikabiliwa na kupingwa bila
kutetereka. Adui yule mkuu akadondoa ahadi ya Mungu kama dhamana yake [Yesu], ili
Kristo apate kufanya hivyo kwa salama akitegemea nguvu ya ahadi hiyo. Yesu alilikabili
jaribu hilo kwa Maandiko: "Imeandikwa, Usimjaribu Bwana Mungu wako." Kwa njia iyo
hiyo Shetani anawashurutisha wanadamu kuingia mahali ambapo Mungu hataki waende,
akiwaonyesha Maandiko kuhalalisha mashauri yake.
Ahadi za Mungu za thamani hazijatolewa kwa ajili ya kumwimarisha mwanadamu
katika njia yake ya kiburi au kwa ajili yake kuweza kuzitegemea anapokimbia kwa
haraka sana kuingia hatarini.... Sisi kama watoto wa Mungu tunatakiwa kuuhifadhi
unyofu wetu wa tabia ile ya Kikristo. Ingetupasa kutumia busara, hadhari, na
unyenyekevu, na kuenenda kwa uangalifu kwa wale walio nje. Hata hivyo, kwa vyo
vyote vile hatutakiwi kuziachilia mbali kanuni zetu.
Usalama wetu pekee ni kutokumpa nafasi yo yote yule mwovu; maana mashauri na
makusudi yake daima yanatudhuru sisi, na kutuzuia tusiweze kumtegemea Mungu. Yeye
mwenyewe [Shetani] anajigeuza awe kama malaika mtakatifu ili kwa njia ya majaribu
yake yanayozighilibu akili zetu apate kuziingiza hila zake kwa namna ambayo sisi
hatuwezi kuutambua ujanja wake. Kadiri tunavyojitoa kwake, ndivyo kadiri madanganyoyake yatakavyozidi kuwa na nguvu nyingi juu yetu. Si salama kupambana naye au
kufanya mashauri naye. Kwa maana kila nafasi tunayompa adui yetu huyo, atataka tumpe
nyingine zaidi. Usalama wetu pekee ni kulikataa katakata wazo la kiburi linapojipenyeza
ndani yetu kwa mara ile ya kwanza. Mungu ametupa neema yake ya kutosha kupitia kwa
wema wake Kristo ili kutuwezesha sisi kumpinga Shetani na kuwa zaidi ya washindi.
Kumpinga ni ushindi. "Mpingeni Shetani, naye atawakimbia." Kumpinga huko ni lazima
kuwe kwa moyo wa ushupavu na uthabiti. Tunapoteza yote tuliyopata iwapo tunampinga
leo na kesho tunasalimu amri kwake. ----- RH, Aprili, l880.
KARIBU ZAIDI, SALAMA ZAIDI Machi 31
Mkaribieni Mungu, naye atawakaribia ninyi. Itakaseni mikono yenu, enyi wenye
dhambi, na kuisafisha mioyo yenu, enyi wenye nia mbili. Yakobo 4:8.
"Mkaribieni Mungu." Kwa jinsi gani? Kwa kuuchunguza moyo wako kwa siri na kwa
bidii; kwa kumtegemea Mungu kwa dhati na kwa unyenyekevu kama mtoto mdogo,
ukimweleza Yesu udhaifu wako wote, na kwa njia ya kuziungama dhambi zako. -----
7BC 938.
Hatuwezi kumkaribia Mungu na kuuona uzuri wake na huruma zake bila kutambua
kasoro zetu na kujazwa na shauku ya kupanda juu zaidi. "Naye atawakaribia." Mungu
atamkaribia yule anayeungama kwa ndugu zake makosa aliyowatendea, na halafu
anakuja kwa Mungu kwa unyenyekevu na majuto yaletayo toba.
Yule anayejihisi mwenyewe kuwa yuko hatarini, hukesha asije akamhuzunisha Roho
Mtakatifu na kwenda mbali na Mungu kwa sababu anajua ya kwamba [Mungu]
hajapendezwa na matendo yake. Basi, ni vyema, tena ni salama zaidi jinsi gani
kumkaribia Mungu, ili nuru ile safi inayong'aa toka katika Neno lake ipate kuyaponya
majeraha ambayo dhambi imeujeruhi moyo. Kadiri tunavyomkaribia zaidi Mungu,
ndivyo kadiri tunavyokuwa salama, kwa maana Shetani anachukia na kuogopa kuwapo
kwake Mungu. ----- 7BC 937.Mkaribie kwa maombi, kwa kumtafakari, kwa kusoma Neno lake. Anapokukaribia,
anainua juu bendera yake kwa ajili yako dhidi ya yule adui. Hebu na tujipe moyo; kwa
maana adui yetu hawezi kuipita bendera hiyo. ----- 7BC 937,938.
Endapo tunamkaribia Mungu, kila mmoja peke yake, je! hamwoni jinsi matokeo
yatakavyokuwa? Hamwoni kwamba tutakaribiana sisi kwa sisi? Hatuwezi kumkaribia
Mungu, na kuuendea msalaba wake ule ule mmoja, bila mioyo yetu kuunganishwa vizuri
pamoja katika umoja kamili, tukiijibu sala ya Kristo kwamba wawe na umoja kama Yeye
alivyo umoja na Baba yake. Basi tungetafuta kwa moyo wetu, kwa ufahamu wetu, na
kwa imani yetu ili tupate kuwa na umoja, ili Mungu apate kutukuzwa ndani yetu kama
anavyotukuzwa ndani ya Mwana; ili Mungu apate kutupenda sisi kama anavyompenda
Mwanawe. ----- 7BC 937.
Mtu anayempenda Mungu, anapenda kuchota nguvu zake kutoka kwake kwa njia ya
kuhifadhi mawasiliano [maombi] kila wakati pamoja naye. Inapogeuka na kuwa tabia ya
mtu kuongea na Mungu, hapo ndipo nguvu ya yule mwovu inapovunjiliwa mbali; kwa
maana Shetani hawezi kukaa karibu na mtu yule anayemkaribia Mungu." ----- 7BC 937.
NJONI KWANGU Aprili 1
Njoni kwangu, ninyi nyote msumbukao na wenye kulemewa na mizigo, nami
nitawapumzisha. Mathayo 11:28.
Wengi wanaosikia mwito huu, wanatamani sana kupumzika, lakini wanazidi kusonga
mbele katika njia ile inayoparuza, wakiwa wameikumbatia mizigo yao karibu sana na
moyo wao. Yesu anawapenda, naye anatamani sana kuibeba mizigo yao pamoja na wao
wenyewe katika mikono yake yenye nguvu. Angependa kuziondoa hofu zao na mashaka
yao yanayowanyang'anya amani na pumziko; lakini hawana budi kwanza kuja kwake, na
kumweleza shida zao za siri zilizomo mioyoni mwao....
Wakati mwingine tunasimulia shida zetu zote masikioni mwa wanadamu, na kuwaeleza
wale wasioweza kutusaidia katika mateso yetu, na kuacha kumweleza Yesu siri zetu zote,
yeye awezaye kuigeuza njia ile inayotuletea majonzi na kutuingiza katika njia zake za
furaha na amani....
Anatushauri sisi ya kuwa yeye ndiye rafiki yetu, awezaye kutembea pamoja nasi katika
njia zetu zote za maisha zinazoparuza. Anatuambia, Mimi ni Bwana Mungu wako;
tembea nami, nami nitaijaza njia yako na nuru. Yesu, Mfalme Mtukufu wa Mbinguni,
anakusudia kuwainua katika hali ya kirafiki pamoja naye wale wote wanaokuja kwake
pamoja na mizigo yao, udhaifu wao, na matatizo yao... Mwaliko wake kwetu ni mwito kwetu tupate kuishi maisha safi, matakatifu, na ya furaha
----- maisha ya amani na raha, ya uhuru na upendo ----- na kupata urithi tele mwishoni,
yaani, ule uzima wa milele.... Ni haki yetu kila siku kuwa na matembezi ya amani, ya
karibu, na ya furaha pamoja na Yesu. ----- ST, Machi 17, 1887.
Pumziko [raha] linapatikana wakati kunapotupiliwa mbali kujihesabia haki kote, yaani,
hoja zote zitokanazo na msimamo wa ubinafsi. Kujisalimisha nafsi kabisa, kuzikubali
njia zake, hiyo ndiyo siri ya pumziko kamili katika pendo lake.... Fanya yale tu
aliyokuambia kufanya, nawe uwe na hakika kwamba Mungu atafanya yote aliyosema
atafanya.... Je, umekuja kwake, na kuyaacha mambo yako yote uliyoyaweka badala yake,
umeacha kutokuamini kwako kote, pamoja na kujihesabia haki wewe mwenyewe? Njoo
kwake jinsi ulivyo, dhaifu, usiyejiweza, na uliye tayari kufa.
Hivi "pumziko" lile lililoahidiwa ni pumziko gani? ----- Ni kule kujua ya kwamba
Mungu ni wa kweli, kwamba hamkatishi tamaa mtu ye yote anayekuja kwake. Msamaha
wake ni tele na wa bure, na kule kukubaliwa naye humaanisha pumziko [raha] moyoni
mwako, yaani, pumziko katika pendo lake. ----- RH, Aprili 25, 1899.
PUMZIKO KWA WALE WASIOTULIA Aprili 2
Kwa maana Bwana MUNGU, Mtakatifu wa Israeli, asema hivi, Kwa kurudi na kustarehe
mtaokolewa; nguvu zenu zitakuwa katika kutulia na kutumaini; lakini hamkukubali.
Isaya 30:15.
Yesu anakupenda wewe, naye anataka upendo wako. Angependa wewe ukumbuke
kwamba alikutolea maisha yake ya thamani ili usipotee [usiangamie]; na ya kwamba
kwako atakuwa msaada tele wakati wa shida. Wewe umwangalie tu Yesu na kumweleza
kila tatizo ulilo nalo pamoja na maonjo yako... Mwombe akusaidie na kukutia nguvu na
kukubariki, nawe amini kwamba anayasikia maombi yako....
Mbingu yote inakuangalia wewe kwa hamu kubwa. Mtu mmoja ambaye Kristo amemfia
ana thamani kuliko ulimwengu wote. Natamani kila kijana wa kiume na wa kike aweze
kutambua thamani ya roho ya mwanadamu. Iwapo wangejitoa wenyewe kwa Yesu jinsi
walivyo, ingawa ni wenye dhambi na wachafu, yeye atawakubali dakika ile ile
wanapojitoa wenyewe kwake, na Yesu atatia Roho wake ndani ya moyo wa yulemtafutaji mnyenyekevu. Ye yote ajaye kwake hatamtupa nje kamwe. Unaweza kumpenda
Yesu kwa moyo wako wote, naye hatakuangusha katika upendo wako huo na matumaini
yako. Maneno yake ni uzima, faraja, na tumaini. Shetani anajua kwamba yote
unayotakiwa kufanya ni kumtazama Yesu, Mwokozi wako aliyeinuliwa juu. Mtu yule
aliyejeruhiwa, aliyechubuliwa, na kupigwa atapata zeri [dawa ya kuponya] kwa majeraha
yake ndani ya Yesu....
Patakuwa na amani, yaani, amani ya kudumu, ikibubujika moyoni, maana pumziko hilo
linapatikana kwa kujinyenyekeza kabisa kwa Yesu Kristo. Utii kwa mapenzi ya Mungu
huleta pumziko hilo. Mwanafunzi yule anayekanyaga katika nyayo za Mkombozi wake
mpole na mnyenyekevu anapata pumziko [raha] ambalo ulimwengu huu hauwezi kumpa,
wala ulimwengu huu hauwezi kuliondoa. "Utamlinda yeye ambaye moyo wake
umekutegemea katika amani kamilifu, kwa kuwa anakutumaini." Isaya 26:3. ----- Letter
6, 1893.
Unyenyekevu na upole wa moyo, ambao daima ulikuwa ni tabia ya maisha matakatifu ya
Mwana wa Mungu, ukiwa ndani ya wafuasi wake wa kweli, huleta hali ya kuridhika,
amani, na furaha ambayo huwainua juu ya utumwa ule wa maisha ya unafiki. ----- HR,
Desemba, 1871.
"MJIFUNZE KWANGU" Aprili 3
Jitieni nira yangu, mjifunze kwangu; kwa kuwa mimi ni mpole na mnyenyekevu wa
moyo; nanyi mtapata raha nafsini mwenu. Mathayo 11:29.
"Mjifunze kwangu," alisema yule Mwalimu wa Mbinguni, "kwa kuwa mimi ni mpole na
mnyenyekevu wa moyo...." Yatupasa kujifunza kujikana nafsi, yatupasa kujifunza ujasiri,
saburi, ushupavu, na upendo unaosamehe.... Iwapo tunayo imani ndani ya Yesu kama
msaidizi wetu, iwapo macho yetu ya imani yanaelekezwa kwake kila wakati, basi,
tutakuwa kama Yesu katika tabia zetu. Atakaa ndani ya mioyo yetu, nasi tutakaa ndani
yake Kristo. Tukiwa tumevikwa haki ya Kristo, maisha yetu yanafichwa pamoja na
Kristo katika Mungu. Atakuwa mshauri wetu. Tukimwomba kwa imani, atatufungua
ufahamu wetu.... Mafundisho aliyotupa Kristo yatawekwa katika matendo. ----- MS 21,
1889.Kristo, Kielelezo Chetu, anapowekwa daima mbele ya macho ya akili zetu, hapo ndipo
tabia mpya zitaweza kukuzwa, mielekeo yetu mibaya yenye nguvu tuliyorithi pamoja na
ile tuliyojizoeza wenyewe itaweza kudhibitiwa na kushindwa, kujisifu kwetu kutatupwa
mavumbini, tabia mbaya za zamani za mawazo zitapingwa daima, kupenda kwetu makuu
kutajionyesha katika tabia yetu kwa dhahiri na kudharauliwa, nasi tutakushinda. ----- MS
6, 1892.
Kristo hana budi kuingia katika mawazo yetu yote, hisia zetu zote, na mapenzi yetu yote.
Anapaswa kutukuzwa katika mambo madogo sana ya utumishi wetu wa kila siku katika
kazi ile aliyotupa kufanya. Wakati tunapoketi miguuni pake Yesu, badala ya kutegemea
ufahamu wetu wa kibinadamu au kufuata maneno ya hekima ya ulimwengu huu,
tunapaswa kuyapokea maneno yake kwa shauku, tukijifunza kwake, na kusema, "Bwana,
wataka mimi nifanye nini?" hapo ndipo hali yetu ya asili ya kujitegemea wenyewe, yaani,
kujitumainia wenyewe, kufuata mapenzi yetu wenyewe, itabadilika, na mahali pake
itakuwapo roho ile ya kitoto, tiifu, inayokubali kufundishwa. Tunapokuwa na uhusiano
sahihi na Mungu wetu, tutaitambua mamlaka ya Yesu katika kutuongoza sisi, na madai
yake kwetu kwamba tumpe utii usiokuwa na maswali. ----- Letter 186, 1902.
Tutakuwa na mawazo ya hali ya juu kumhusu Yesu Kristo hata nafsi zetu zitajishusha
chini. Mapenzi yetu yatakuwa ndani ya Yesu, mawazo yetu yatavutwa kwa nguvu
kuelekea mbinguni. Kristo atakuwa hana budi kuzidi, wakati MIMI NINAPUNGUA....
Tutajizoeza kuwa na wema ule ulio ndani yake Kristo, ili sisi tupate kuakisi kwa wengine
mfano wa tabia yake. -----
MS 21, 1889.
KUJITIA NIRA YA KRISTO Aprili 4
Kwa maana nira yangu ni laini, na mzigo wangu ni mwepesi. Mathayo 11:30.
Kujitia nira ya Kristo, maana yake kufanya kazi kulingana na njia zake, kuwa mshirika
mwenzi pamoja naye katika mateso yake na taabu zake kwa ajili ya wanadamu
waliopotea. ----- 5BC 1092. Katika kuikubali nira yake Kristo ile ya kujizuia na utii, utaiona kwamba imekuwa
msaada mkubwa sana kwako. Kujitia nira hii kunakuweka wewe karibu na ubavu wake
Kristo, naye anachukua sehemu ile iliyo nzito kuliko zote ya mzigo huo. ----- 5BC 1090.
Nira na msalaba ni nembo zinazowakilisha jambo lile lile moja ----- kusalimisha
mapenzi [nia] yetu yote kwa Mungu. Kujitia nira kunamwunganisha mwanadamu katika
urafiki pamoja na yule mpendwa sana Mwana wa Mungu. Kuuinua msalaba juu
kunaiondoa nafsi moyoni, na kumweka mwanadamu mahali ambapo anajifunza kubeba
mizigo yake Kristo. Hatuwezi kumfuata Kristo bila kujitia nira yake, yaani, bila kuuinua
juu msalaba wetu, na kujitwika na kumfuata. Kama mapenzi yetu hayapatani na matakwa
yale ya mbinguni, basi, inatupasa sisi kuyakataa matakwa yetu, kuachana na tamaa zetu
tunazozipenda sana, na kukanyaga katika nyayo zake Kristo....
Wanadamu hujitengenezea nira ambazo huonekana kuwa ni nyepesi na za kupendeza
kuvaa kwa ajili ya shingo zao wenyewe, lakini matokeo yake ni kwamba zinachubua
vibaya mno. Kristo analiona jambo hilo, na kusema, "Jitie nira yangu. Nira ile unayoweza
kuitia shingoni mwako, ukidhani inakufaa sana, haitakufaa hata kidogo. Jitie nira yangu,
nawe ujifunze kwangu mafundisho ambayo ni ya muhimu kwako kujifunza." ----- 5BC
1090,1091.
Kazi yako sio kukusanya mizigo yako mwenyewe.... Mara nyingi sisi tunafikiri kwamba
tuna wakati mgumu katika kuibeba mizigo yetu, na mara nyingi mno mambo yanakuwa
hivyo, kwa sababu Mungu hajaweka mpango wo wote kwa ajili yetu kuibeba mizigo
hiyo; lakini tunapojitia nira yake na kuibeba mizigo yake, hapo ndipo tunaweza
kushuhudia kwamba nira ya Kristo ni laini na mizigo yake ni myepesi, kwa sababu yeye
ameweka mpango wa kuibeba hiyo [mizigo yake]. ----- 5BC 1091.
Hata hivyo, nira hiyo haitatupatia sisi maisha ya raha na uhuru na kujifurahisha nafsi
zetu. Maisha yake Kristo yalikuwa ni maisha ya kujitoa mhanga na kujikana nafsi kwa
kila hatua [aliyokwenda]; na kwa upendo unaodumu daima kama ule wa Kristo, mfuasi
wake wa kweli atatembea katika nyayo za Bwana wake; naye atakapokuwa anasonga
mbele katika maisha haya, atazidi kujazwa na roho ile ile na maisha yale yale ya Kriato. -
---- 5BC 1092.
KUJIFUNZA KATIKA SHULE YA KRISTO Aprili 5
Ni nani amchaye BWANA? Atamfundisha katika njia anayoichagua. Zaburi 25:12.Yesu amefungua shule kwa ajili ya kuwaelimisha na kuwapa mazoezi wateule wake, nao
wanapaswa kuendelea kujifunza daima kuyaweka katika matendo mafundisho yale
anayowapa, ili wapate kumjua kabisa.
Wale wanaofikiri kwamba wao ni wema kiasi cha kutosha, wala hawafanyi kazi kwa
bidii katika kuikamilisha tabia yao ya Kikristo, wataweka sanamu mioyoni mwao, nao
wataendelea kutenda dhambi katika maisha yao mpaka dhambi kwao itaonekana kuwa si
dhambi tena....
Yesu anajitoa nafsi yake kwa kila mtu aliye mgonjwa, kwa kila mtu anayejitahidi
kushinda. Roho Mtakatifu anamwombea kila mpiga mweleka mwaminifu, naye Kristo
atayafanya maneno yake kuwa roho na uzima, yaani, kuwa uweza wa Mungu uletao
wokovu kwa kila mtu aaminiye. Lakini wewe utashindwa kabisa utakapomruhusu yule
mwovu kuutawala moyo wako, yaani, kuyaongoza mawazo yako.... Mungu
hatadhihakiwa; hataukubali moyo uliogawanyika. Yeye anataka tumpe huduma yetu yote
kwa moyo wetu wote. Amelipa fedha ya fidia yetu kwa kujitoa nafsi yake mwenyewe
kwa ajili ya kila mwana na binti ya Adamu....
Kristo anayo madai juu ya kila mtu; lakini wengi huchagua maisha ya dhambi. Wengine
hawataki kuja kwa Yesu ili awape uzima. Wengine husema, "Naenda, Bwana," kwa
mwaliko wake, lakini hawaendi; hawajisalimishi nafsi zao kabisa ili kukaa ndani ya Yesu
peke yake, ambamo ni uzima na amani na furaha isiyoneneka, yenye utukufu.... Je!
hamtaamka na kuwa na hekima na kufanya kazi kwa bidii kwa ajili ya umilele? Itafuteni
neema yake Kristo kwa moyo wenu wote, kwa uwezo wenu wote, na kwa nguvu zenu
zote....
Mungu amewapa ninyi haki ya kumshikilia Yeye kwa njia ya maombi ya imani. Maombi
yaliyojaa imani ndicho kiini cha dini safi, ni nguvu ya siri aliyo nayo kila Mkristo....
Tafuta muda wa kuomba, kuyachunguza Maandiko, kuiweka nafsi yako chini ya
nidhamu ya Yesu Kristo. Uishi kwa kuwasiliana na Kristo aliye hai, na mara tu
unapofanya hivyo, atakuchukua na kukushika kwa mkono wake ulio imara ambao
hautakuachilia kamwe. ----- Letter 38, 1893.
KUJIANDAA KWA SHULE ILE YA JUU ZAIDI Aprili 6
Uniongoze katika kweli yako, Na kunifundisha. Maana wewe ndiwe Mungu wa wokovu
wangu, Nakungoja Wewe mchana kutwa. Zaburi 25:5.Wale ambao ni wana wa Mungu hapa duniani wanaketi pamoja na Yesu katika Shule ya
Maandalizi, wakijitayarisha kupokewa katika Shule ile ya Juu Zaidi. Siku kwa siku
tunatakiwa kila mmoja kufanya maandalizi yake mwenyewe; maana katika majumba yale
ya kifalme kule juu hakuna ye yote atakayewakilishwa na mtu mwingine. Kila mmoja
wetu anapaswa kuusikia yeye mwenyewe mwito ule usemao, "Njoni kwangu,... nami
nitawapumzisha...."
Bwana Yesu amekulipia ada ya mafundisho. Yote yakupasayo kufanya ni kujifunza
kwake. Upole kama ule wa Kristo utakaoonyeshwa kwa matendo katika Shule ile ya Juu
unatakiwa kuwekwa katika matendo na waumini wote, wazee kwa vijana, katika Shule
hii ya Chini. Wale wote wanaojifunza katika shule hii ya Kristo wako chini ya mafunzo
wakiongozwa na wajumbe wale wa mbinguni [malaika]; wala haiwapasi kamwe kusahau
ya kwamba wao ni tamasha kwa ulimwengu huu, kwa malaika, na kwa wanadamu.
Wanapaswa kumwakilisha Kristo. Wanatakiwa kusaidiana wenyewe ili waweze kufaa
kuingia katika Shule ile ya Juu zaidi. Wanapaswa kusaidiana kila mmoja na mwenzake ili
wapate kuwa watakatifu na wenye utukufu, na kulizingatia sana wazo lile la kweli
linaloonyesha maana ya kuwa mtoto wa Mungu. Wanapaswa kusema maneno ya kutia
moyo. Wanapaswa kuiinua juu mikono iliyo dhaifu na kuyafanya imara magoti
yaliyolegea. Juu ya kila moyo panatakiwa kuandikwa maneno haya, kana kwamba ni kwa
kalamu yenye ncha ya almasi, "Hakuna kitu cho chote ninachokiogopa, isipokuwa tu
kwamba mimi sitaujua wajibu wangu, au nitashindwa kuutekeleza."...
Moyo uliodhibitiwa, maneno ya upendo na upole, humletea heshima Mwokozi wetu.
Wale wasemao maneno ya upole, maneno ya upendo, maneno yaletayo amani,
watatunukiwa vizuri sana.... Tunapaswa kumruhusu Roho wake kuangaza katika maisha
yetu ya nje ule upole na unyenyekevu wa moyo tuliojifunza kwake. ----- Letter 257,
1903.
Yesu ndiye Mwalimu wetu Mkuu.... Anapenda sana, tena yu tayari sana kukuchukua
wewe katika ushirika wa karibu sana na Yeye mwenyewe. Yu tayari kukufundisha jinsi
ya kuomba kwa imani yenye matumaini na uhakika kama ile ya mtoto mdogo....
Jiandikishe upya jina lako kama mwanafunzi wa shule yake. Jifunze kuomba kwa imani.
Pokea maarifa yake Yesu.
Je! wewe huwezi kuketi miguuni pake Yesu na kujifunza kwake? ----- Letter 38, 1893.NGUVU HALISI YA NIA Aprili 7
Maana, kama nia ipo, hukubaliwa kwa kadiri ya alivyo navyo mtu, si kwa kadiri ya
asivyo navyo. 2 Wakorintho 8:12.
Dini iliyo safi inahusika na matumizi ya nia. Nia ni uwezo unaotawala katika maumbile
ya mwanadamu, ikiuleta uwezo mwingine wote uliomo mwilini chini ya mamlaka yake.
Nia si kuonja wala mwelekeo, bali ni uwezo wa kuamua la kufanya ambao unafanya kazi
yake ndani ya wana wa wanadamu ama ukiwaelekeza kwenye utii kwa Mungu, ama
kwenye uasi....
[Bila shaka] wewe unatamani kuyafanya maisha yako kuwa kama vile ambavyo
yangefaa kukuwezesha kuingia mbinguni hatimaye. Mara nyingi unakata tamaa
unapojiona mwenyewe kuwa u dhaifu katika uwezo wako wa kimaadili [tabia], unajikuta
u mtumwa wa mashaka, tena umetawaliwa na tabia na desturi za maisha yako ya zamani
ya dhambi.... Ahadi zako [maazimio yako] ni kama kamba zilizotengenezwa kwa
mchanga....
Daima utakuwa hatarini mpaka hapo utakapoielewa nguvu halisi ya nia yako. Unaweza
kuamini na kuahidi mambo yote, lakini ahadi zako au imani yako haina maana yo yote
mpaka hapo utakapoiweka nia yako nyuma ya imani yako na nyuma ya matendo yako.
Kama wewe unapiga vita ile ya imani kwa uwezo wako wote wa nia yako, utashinda.
Hisia zako, mvuto wako, mapenzi yako ya moyoni, mambo yote hayo hayaaminiki, kwa
sababu hayawezi kutegemewa....
Lakini wewe huna haja ya kukata tamaa.... Ni juu yako mwenyewe kuisalimisha nia
yako kwa nia ile ya Yesu Kristo; nawe unapofanya hivyo, Mungu atakushika mara moja
na kufanya kazi yake ndani yako ili upate kutaka na kutenda yale yampendezayo Yeye.
Mwili wako wote ndipo utakuwa chini ya utawala wa Roho wake Kristo, na hata mawazo
yako yatatawaliwa naye. Huwezi kuzitawala hisia zako, wala mapenzi yako ya moyoni,
kama unavyotaka mwenyewe; lakini unaweza kuitawala nia yako [maamuzi yako], nawe
[kwa njia hiyo] unaweza kufanya mabadiliko kamili katika maisha yako. Kwa
kuisalimisha nia [mapenzi] yako kwa Yesu, maisha yako yatafichwa pamoja na Kristo
katika Mungu na kuunganishwa na mamlaka ile ipitayo falme zote na mamlaka zote.
Utakuwa katika nguvu yake; na nuru mpya, yaani, nuru ile ya imani iliyo hai,
itawezekana kwako kuwa nayo. Lakini nia yako ni lazima ishirikiane na nia yake
Mungu....
Je! wewe hutasema, "Nitampa Yesu nia yangu, nami nitafanya hivyo sasa hivi," na
kuanzia dakika hii hutakuwa upande wake Bwana kabisa? ----- 5T 13, 514.NIA YANGU INAPOKUWA SALAMA Aprili 8
Lakini sasa mkiisha kuwekwa huru, na kuwa mbali na dhambi, na kufanywa watumwa
wa Mungu, mnayo faida yenu, ndiyo kutakaswa, na mwisho wake ni uzima wa milele.
Warumi 6:22.
Roho wa Mungu haumbi uwezo mpya wa nguvu za mwili ndani ya mtu yule
aliyeongoka, bali hufanya mabadiliko dhahiri kwa kutumia uwezo ule uliomo humo.
Akili na moyo na roho vinapobadilika, mwanadamu hapewi dhamiri mpya, bali nia yake
inanyenyekezwa chini ya dhamiri iliyofanywa upya, dhamiri ambayo fahamu zake
zilizolala usingizi zimeamshwa kwa utendaji wa Roho Mtakatifu. ----- Letter 44, 1899.
Kwa kuanguka kwake dhambini, mwanadamu aliiweka nia yake chini ya utawala wa
Shetani. Akawa mateka wake asiye na uwezo wo wote katika mamlaka ya yule mjaribu.
Mungu alimtuma Mwanawe katika ulimwengu wetu ili kuzivunja nguvu za Shetani, na
kuiweka huru nia ya mwanadamu. Alimtuma [Yesu] kuwatangazia mateka uhuru wao,
kuiondoa mizigo yao mizito, na kuwaacha huru wale waliosetwa. Kwa kumwaga hazina
yote ya mbinguni katika dunia hii, yaani, kwa kutupa sisi mbingu yote ndani ya Kristo,
Mungu ameinunua nia, mapenzi, akili, roho, ya kila mwanadamu. Mwanadamu
anapojiweka chini ya utawala wa Mungu, nia yake inakuwa imara na yenye nguvu
kuweza kufanya mema, moyo wake hutakaswa na uchoyo wake wote, na kujazwa na
upendo unaofanana na ule wa Kristo. Akili yake inasalimu amri kwa mamlaka ile ya
Sheria ya upendo, na kila wazo linatekwa nyara lipate kumtii Kristo. -----
MS 21, 1900.
Nia yetu inapowekwa upande wa Bwana, Roho Mtakatifu anaichukua nia hiyo na
kuifanya iwe katika umoja na nia ile ya Mungu.
Bwana anampenda mwanadamu. Ametoa ushahidi wa upendo wake kwa kumtoa
Mwanawe pekee kufa kwa ajili ya mwanadamu, ili kwa neema yake apate kumkomboa
kutoka katika uadui wake dhidi ya Mungu, na kumrejesha kwenye utii wake wa kwanza.
Kama mwanadamu atashirikiana na Mungu, basi, Bwana ataileta nia yake na
kuiunganisha na yake mwenyewe, naye ataitia nguvu kwa Roho wake mwenyewe.... Injili
haina budi kupokewa ili kuufanya upya moyo wake, na mapokezi ya ile kweliyatamaanisha kuisalimisha akili na nia yake kwa nia ile ya uwezo wa Mungu. ----- Letter
44, 1899.
Nia [mapenzi] ya mwanadamu ni salama pale tu inapounganishwa na nia [mapenzi] ya
Mungu. ----- Letter 22, 1896.
NIA INAYOTII Aprili 9
Mtu akipenda kuyatenda mapenzi [nia] Yake [Mungu], atajua habari za yale mafunzo,
kwamba yatoka kwa Mungu, au kwamba nanena kwa nafsi yangu tu. Yohana 7:17.
Wale walioyasalimisha mapenzi yao kwa Mungu wanapata mafunzo katika shule ya
Kristo....
Wanaadibishwa kuwa na tabia ya utii, ili wapate kufanya kazi kwa ajili yake Mungu. Sisi
si viumbe visivyokuwa na maadili yo yote katika tabia yetu. Injili haisemi na akili yetu
peke yake. Kama ingefanya hivyo, basi, tungeikabili kama vile tunavyolikabili somo la
kitabu kinachoshughulika na kanuni za hesabu [fomyula], ambalo linaihusu akili peke
yake. Lengo lake [injili] ni moyo. Inaiadibisha tabia yetu [maadili], na kuitawala nia yetu.
Inaangusha chini mawazo, na kila kitu kinachojiinua juu ya elimu ya Mungu; na kuteka
nyara kila fikira ipate kumtii Kristo.
Ni ukaidi wetu ulioziangusha chini nguvu zetu za kiroho. Wote wanaotaka kujifunza
sayansi ya wokovu wanatakiwa kuwa wanafunzi wanyenyekevu katika shule hiyo ya
Kristo, ili hekalu la mwili lipate kuwa makao yake yule Aliye juu. Kama tungetaka
kujifunza kwake Kristo, basi, ni lazima moyo wetu uweze kubaki tupu kwa kuviondoa
vitu vyake vyote unavyojivunia, ili Kristo apate kuweka chapa ya sura yake moyoni
mwetu.
Hapo ndipo tutakapokuwa na picha ya kafara ile ya milele aliyoitoa Kristo kwa ajili yetu
hata moyo wetu utalainika na kunyenyekezwa na kujazwa na shukrani kwa Mungu.
Shauku kubwa itazaliwa kwa uweza wa Roho Mtakatifu kutafuta nafasi inayofaa
kumshuhudia Kristo na kutoa shukrani na kicho kwake yeye aliyetukomboa. Utii na
upendo vitaonekana katika huduma yetu yote. Shauku ile inayowaka kama moto ya
kutaka kufanana na Kristo itaufanya moyo wetu kuwa mpole, na kuufanya uweze kutoa
shukrani bila woga, na machoni pa mbingu kumshukuru Mungu kwa fadhili zake, upendo wake, na huruma yake. Hao wanayo neema isiyoweza kunyamazishwa na kuwa kama ile
ya kila siku isiyobadilika ya kuikiri kweli wakati moyo hauguswi kabisa.
Ni salama jinsi gani kwetu kuweza kusumbuka kuingia katika mlango ule mwembamba!
Ni kwenye madhabahu ya Mungu pekee wanadamu wanaweza kuipata tochi ile ya
mbinguni [Roho Mtakatifu]. ----- Letter 5, 1898].
KUIPALILIA BUSTANI YA MUNGU Aprili 10
Wala msifuatishe namna ya dunia hii; bali mgeuzwe kwa kufanywa upya nia zenu,
mpate kujua hakika mapenzi ya Mungu yaliyo mema, ya kumpendeza, na ukamilifu.
Warumi 12:2.
Mwanadamu, yaani, mwanadamu aliyeanguka, anaweza kugeuzwa kwa kufanywa upya
nia yake, ili a"pate kujua hakika mapenzi ya Mungu yaliyo mema, ya kumpendeza, na
ukamilifu." Anayajuaje hayo? Kwa njia ya Roho Mtakatifu kama ameitawala nia yake,
roho yake, moyo wake, na tabia yake. ----- 6BC 1080.
Kanuni za kipuuzi zenye kuleta mashaka pamoja na desturi [mila] hazina budi
kufagiliwa mbali. Bwana anataka nia yetu ifanywe upya, na moyo upate kujazwa na
hazina za ile kweli.
MS 24, 1901.
Kweli inao uwezo wa kumwinua yule anayeipokea. Ina uwezo wa kutakasa moyo na
tabia.... Ni kwa kuiendeleza tu akili pamoja na nguvu za kimaadili, ndipo sisi tunaweza
kutumaini kutoa jibu kwa kusudi la Muumbaji wetu....
Mkristo anatakiwa kuwa na akili nyingi na utambuzi mkali kuliko mtu wa ulimwengu.
Kujifunza Neno la Mungu kunaendelea kuupanua ubongo wake na kuipa akili yake
nguvu. Hakuna kitu kinachoweza kuiadilisha na kuikuza tabia, na kuupa nguvu kila
uwezo uliomo mwilini, kama kuendelea kuitumia akili ili ipate kuyashika na kuyajua
mambo mazito na ya maana ya kweli hizo.
Ubongo wa mwanadamu unasinyaa na kudhoofika unaposhughulika na mambo ya
kawaida tu, usiweze kamwe kupanda juu ya usawa wa wakati uliopo na maoni ya
wanadamu wengi na kuweza kuzifahamu siri zile za mambo yale yasiyoonekana kwa
macho. Ufahamu unashuka taratibu kwenda chini mpaka kufika kwenye usawa wamambo yale ambayo unayafahamu sikuzote.... Mwanadamu hana haja ya kuacha kukua
kiakili na kiroho katika kipindi chote cha maisha yake. ----- MS 59, 1897.
Yatupasa kuzikuza talanta tulizopewa na Mungu. Ni vipawa vyake, na vinapaswa
kutumika kwa mpangilio wake mzuri kila kimoja kwa kingine, ili kufanya kitu kamili
kimoja. Mungu anatoa talanta, yaani, nguvu za akili; mwanadamu anajenga tabia yake.
Ubongo ni bustani ya Bwana, na mwanadamu hana budi kuipalilia kwa bidii ili kujenga
tabia inayofanana na ile ya Mungu. ----- Letter 73, 1899.
KATIKA HALI YA MWAFAKA NA MUNGU Aprili 11
Yesu akawaambia, Chakula changu ndicho hiki, niyatende mapenzi yake aliyenipeleka,
nikaimalize kazi yake. Yohana 4:34.
Yesu alitangaza, akisema, "Mimi sikushuka... ili niyafanye mapenzi yangu, bali mapenzi
yake aliyenipeleka." Yohana 6:37. Nia yake iliwekwa katika matumizi hai ya kuziokoa
roho za wanadamu. Nia yake ya kibinadamu ililishwa na nia ile ya uungu. Watumishi
wake leo wangefanya vizuri kujiuliza maswali haya wao wenyewe, "Ni aina gani ya nia
ninayoikuza mimi binafsi? Je, nimekuwa nikizitimiza tamaa zangu, na kujiimarisha
katika uchoyo wangu na kiburi?" Kama tunafanya hivyo, basi, tumo katika hatari kubwa,
maana sikuzote Shetani anaitawala nia ile ambayo haiko chini ya utawala wa Roho wa
Mungu. Tunapoiweka nia yetu katika hali ya mwafaka na nia ile ya Mungu, hapo ndipo
utaonekana katika maisha yetu utii ule mtakatifu uliodhihirishwa katika maisha yake
Kristo....
Paulo anatangaza hivi, "Nimesulibiwa pamoja na Kristo." Wagalatia 2:20. Hakuna kitu
kilicho kigumu sana kama kuisulibisha nia yetu. Kristo alijaribiwa katika mambo yote
kama sisi, lakini nia yake daima iliwekwa upande wa nia ya Mungu. Katika hali yake ya
kibinadamu alikuwa na nia ile ile iliyo huru kama aliyokuwa nayo Adamu kule Edeni.
Angeweza kuanguka majaribuni kama Adamu alivyoanguka. Naye Adamu, kwa
kumwamini Mungu na kuwa mtendaji wa neno lake, angeweza kuyapinga majaribu kama
Kristo alivyoyapinga. Kama Kristo angenuia, angeweza kuyaamuru mawe kuwa mikate.
Angeweza kujitupa mwenyewe chini kutoka kwenye kinara kile cha hekalu. Angeweza
kuanguka katika jaribu la Shetani na kuanguka chini na kumsujudia, yule tapeli wa
ulimwengu huu. Lakini katika kila jambo alipambana na mjaribu, akisema,"Imeandikwa." Nia yake ilitii kikamilifu mapenzi [nia] ya Mungu, na mapenzi ya Mungu
yalidhihirishwa katika maisha yake yote....
Utii wake Kristo kwa Amri [Kumi] za Baba yake ndicho kipimo cha utii wetu. Wale
wanaomfuata Kristo, kama wanataka kuwa wakamilifu ndani yake, ni lazima
wazisalimishe nia zao kwa nia [mapenzi] ile ya Mungu. Mpango kamili umefanywa ili
wale wanaomtafuta Mungu kwa moyo wote wapate ndani yake msaada tele kila wakati
taabu inapotokea. Msaada umewekwa juu ya Yule aliye na uweza. Kristo ameahidi,
Nitakuwa msaidizi wako. -----
MS 48, 1899.
"IWENI NA NIA IYO HIYO NDANI YENU" Aprili 12
Iweni na nia iyo hiyo ndani yenu ambayo ilikuwamo pia ndani ya Kristo Yesu. Wafilipi
2:5.
Sala ile aliyotupa Kristo, kwamba mapenzi ya Mungu yatimizwe hapa duniani kama kule
mbinguni, inapaswa kujibiwa. Hiyo ni sala ya ajabu, ambayo tunamtolea Mungu, na
kisha kuitimiza katika maisha yetu ya kila siku! Sayansi ya utakatifu, yaani, maadili
mema ambayo injili inayakazia, haikubaliani na kanuni yo yote isipokuwa ukamilifu wa
mawazo ya Mungu, yaani, mapenzi ya Mungu. Ni tabia na mawazo yake Kristo ambayo,
wakati wa kuongoka na kubadilika, wanadamu wanapaswa kupokea. Kwa njia ya
Mwanawe, Mungu ameufunua uzuri [wa tabia] ambao mwanadamu anaweza kuufikia.
Na mbele ya ulimwengu huu Mungu anatusitawisha sisi kuwa mashahidi wake walio hai
wa tabia ile ambayo mwanadamu anaweza kuwa nayo kwa njia ya neema yake Kristo.
Basi, kwa nini wengi sana wanausikitisha moyo wa upendo usio na mwisho wa
Mungu?...
Mungu anamruhusu kila mtu kuutumia utu wake wa pekee. Hakuna akili ya mwanadamu
ye yote inayopaswa kuzamishwa chini ya akili ya mwanadamu mwingine [kutegemea
mawazo ya mwingine]. Lakini mwaliko unasema hivi, "Iweni na NIA IYO HIYO ndani
yenu ambayo ilikuwamo pia ndani ya Kristo Yesu." Kila mtu anapaswa kusimama mbele
za Mungu akiwa na imani yake mwenyewe, uzoefu [maisha] wake mwenyewe, akijua
yeye mwenyewe ya kwamba Kristo ameumbika ndani yake, tumaini la utukufu. Kwetu
kuiga mfano wa mwanadamu ye yote ----- hata kama ni mtu yule ambaye katika maoniyetu ya kibinadamu tunaweza kumfikiria kuwa karibu amekamilika katika tabia yake -----
kungekuwa ni kuweka tumaini letu kwa mwanadamu asiyekuwa mkamilifu, yaani,
mwenye kasoro katika tabia yake, ambaye hana uwezo wo wote wa kumgawia
mwanadamu mwingine hata yodi moja au nukta moja ya ukamilifu alio nao.
Kama Kielelezo chetu yuko Mmoja ambaye ni yote katika yote, ni mashuhuri miongoni
mwa elfu kumi, Mmoja ambaye uzuri wake hauna kifani. Anasemaje, basi, Mwalimu
huyo wa Mbinguni? ----- "Basi ninyi mtakuwa wakamilifu, kama Baba yenu wa
mbinguni alivyo mkamilifu." Mathayo 5:48. Je! Kristo angeweza kututamanisha bure
kwa kututaka sisi kufanya kile kisichowezekana? ----- La, Hasha! Ni heshima ilioje
anayotutunukia sisi, anapotusisitizia kwamba tutakuwa wakamilifu katika mazingira yetu,
kama Baba alivyo mkamilifu katika mazingira yake! Na kwa njia ya uweza wake sisi
tunaweza kufanya hivyo; maana anatutangazia hivi, "Nimepewa mamlaka yote mbinguni
na duniani." Mathayo 28:18. Uwezo huo usio na mipaka ni haki yako wewe na haki
yangu mimi kuudai. ----- Letter 20, 1902.
USHAWISHI WA MOYO JUU YA MOYO MWINGINE Aprili 13
Maana Mungu hakutupa roho ya woga, bali ya nguvu na ya upendo na ya moyo wa kiasi.
2 Timotheo 1:7.
Ushawishi wa moyo juu ya moyo mwingine, ni uwezo wenye nguvu sana unapotakaswa,
pia ni uwezo wenye nguvu kuelekea maovuni ukiwa mikononi mwa wale wanaompinga
Mungu. Uwezo huo aliutumia Shetani katika kazi yake ya kuingiza polepole uovu ndani
ya mioyo ya malaika wale, naye alifanya ionekane kana kwamba alikuwa anatafuta faida
ya ulimwengu wote.... Akiwa ametupwa hapa chini kutoka mbinguni, Shetani alianzisha
ufalme wake ulimwenguni humu, na tangu wakati ule, bila kuchoka, amekuwa akijitahidi
kuwadanganya wanadamu wasiweze kutoa utii wao kwa Mungu. Anatumia uwezo ule ule
alioutumia mbinguni ----- ushawishi wa moyo juu ya moyo mwingine. Wanadamu
wanawaletea majaribu wanadamu wenzao. Hisia za Shetani zenye nguvu zinazoharibu
tabia zinatunzwa sana moyoni, nazo zina uwezo mkuu, unaovutia sana. ----- 7BC 973.
Macho safi ya kiroho yanatakiwa ili kutofautisha kati ya makapi na ngano, kati ya
sayansi ya Shetani [sayansi ya uongo] na sayansi ya Neno la kweli. Kristo, Tabibu Mkuu,
alikuja katika ulimwengu wetu ili kuwapa afya na amani na ukamilifu wa tabia wale wote watakaopenda kumpokea. Injili yake haihusiki na mbinu zile zinazoonekana kwa nje
pamoja na maigizo yatokanayo na sayansi ile ya uovu ambayo yanaweza kuletwa kama
mbaraka mkuu, lakini hatimaye kuonekana kwamba ni laana kubwa. Katika sura ile ya
pili ya Wafilipi unaonekana utauwa ule wa kweli. "Iweni na nia iyo hiyo ndani yenu
ambayo ilikuwamo pia ndani yaKristo Yesu." Wafilipi 2:5....
Kuitetea sayansi ya tiba ya akili [hiponozi] ni kufungua mlango ambao kwa huo Shetani
ataingia na kuitawala akili na moyo. Shetani anaidhibiti akili inayosalimishwa ili
kutawaliwa na akili ya mwingine, pamoja na akili ile inayotawala ya yule mwingine.
Mungu na atusaidie kuijua sayansi ya kweli inayojenga juu ya Kristo, Mwokozi na
Mkombozi wetu.
Kristo ni Tabibu Mkuu kuliko matabibu wote. Yeye ni Tabibu wa roho pamoja na mwili.
Kama asingalikuja humu duniani kutukomboa kutokana na uwezo wa kishetani wa yule
Ibilisi, basi, sisi tusingeweza kuwa na tumaini lo lote la kupata uzima ule wa milele....
Hebu na tusiwaelekeze watu kwa wanadamu wenye makosa. Hebu na tuseme, "Tazama,
Mwana-Kondoo wa Mungu, aichukuaye dhambi ya ulimwengu!" Yohana 1:29. -----
Letter 130, 1901.
MIOYO ILIYONASWA Aprili 14
Angalieni mtu asiwafanye mateka kwa elimu yake ya bure na madanganyo matupu, kwa
jinsi ya mapokeo ya wanadamu, kwa jinsi ya mafundisho ya awali ya ulimwengu, wala si
kwa jinsi ya Kristo. Wakolosai 2:8.
Mara nyingi Shetani humpata wakala wake mwenye nguvu ya uovu kupitia kwa moyo
mmoja ulio na uwezo wa kuathiri moyo mwingine. Uwezo huo una ushawishi mkubwa
sana kiasi kwamba yule mtu anayebadilishwa nao hawezi kuitambua nguvu yake. Mungu
ameniagiza mimi kutoa onyo dhidi ya uovu huo, ili watumishi wake wasiangukie chini ya
uwezo huo wa Shetani udanganyao. Adui wetu ni mtaalam, na endapo watu wa Mungu
hawaongozwi sikuzote na Roho wa Mungu, basi, watanaswa na kutekwa. Kwa maelfu ya
miaka Shetani amekuwa akifanya majaribio mbalimbali juu ya ubongo wa mwanadamu,
naye amejifunza na kuujua vizuri sana [unavyofanya kazi yake]. Kwa njia zake za siri
katika siku hizi za mwisho, anaiunganisha akili ya mwanadamu na yake, akiijaza mawazo
yake; anaifanya kazi hiyo kwa njia ya udanganyifu sana, kiasi kwamba wale wanaopokea
maongozi yake hawajui kwamba wanaongozwa na yeye kama anavyopenda yeye.Mlaghai huyo mkuu anatumainia kuwafanya wanaume na wanawake wachanganyikiwe
kimawazo, ili isisikike sauti nyingine yo yote ndani yao isipokuwa yake peke yake. -----
2SM 352,353.
Injili ya Kristo inatakiwa igusane na maisha yetu ya kila siku. Akili yetu inapaswa kuwa
katika hali iwezayo kuyatambua madai matakatifu ya injili. Haina budi kuzuiwa na
kuadibishwa kuwa na mazoea ya kujitawala na utii....
Mafundisho kutoka katika Maandiko yaliyo hai huangusha chini mawazo na kila kitu
kijiinuacho juu ya elimu ya Mungu; tukiteka nyara kila fikira ipate kumtii Kristo. Shetani
anao uwezo mkubwa juu ya moyo, huushusha chini mpaka kiwango cha chini. Wale
ambao kweli wanataka kujifunza kwa Kristo watalazimika kuuweka moyo wao katika
hali ya utupu kwa kuyaondoa moyoni mwao mawazo yote yaliyojaa kiburi, ili nafasi ya
kumtawaza Yeye [Kristo] iweze kupatikana humo. ----- RH, Des. 18, 1888.
Pambano kati ya Kristo na Shetani bado halijaisha. Huyo aliyetajwa mwisho anatafuta
daima kuimarisha nguvu zake na mamlaka yake mwenyewe. Kama anaweza
[kufanikiwa] kuinasa mioyo, basi, atafanya hivyo.... Madanganyo ya Shetani ni mengi,
bali Bwana atakuwa msaidizi wetu kama tukimtafuta kwa bidii. ----- RH, Des. 18, 1888.
KUUSHUGHULISHA MOYO Aprili 15
Mtu mwema katika hazina njema ya moyo wake hutoa yaliyo mema, na mtu mwovu
katika hazina mbovu ya moyo wake hutoa yaliyo maovu; kwa kuwa mtu, kinywa chake
hunena yale yaujazayo moyo wake. Luka 6:45.
Moyo [akili] umeumbwa kwa namna ambayo unapaswa kushughulishwa na mema au
maovu. Kwa kawaida unapokuwa katika usawa wake wa chini ni kwa sababu unaachiwa
kushughulika na mambo ya kawaida.... Mwanadamu anao uwezo wa kuratibu na
kutawala utendaji wa akili yake, na kutoa mwelekeo wa mtiririko wa mawazo yake.Lakini jambo hilo huhitaji juhudi kubwa kuliko ile tunayoweza kuitoa kwa kutegemea
nguvu zetu wenyewe. Ni lazima mioyo yetu imtegemee Mungu kama tukitaka mawazo
yetu yawe mema, na kutafakari mambo yale yanayofaa.
Ni wachache wanaotambua kwamba ni wajibu wao kuyatawala mawazo yao pamoja na
fikira zao. Ni vigumu kuuweka moyo ambao haujaadibishwa kutafakari mambo yale
yaliyo na manufaa. Lakini kama mawazo hayatumiki kama ipasavyo, basi, dini haiwezi
kusitawi moyoni. Moyo ni lazima ushughulishwe na mambo matakatifu na ya milele, la
sivyo, utapendelea mambo madogo madogo ya kipuuzi na mawazo yale ya juu juu tu.
Uwezo wote wa akili na maadili ni lazima uadibishwe, ndipo utapata nguvu na
kuongezeka kwa kuufanyisha mazoezi.
Kulielewa jambo hilo sawasawa, inatupasa kukumbuka ya kwamba mioyo yetu kwa asili
imekengeuka, na kwa nguvu zetu wenyewe hatuwezi kuifuata njia ile ya kweli. Ni kwa
neema ya Mungu tu, ikiungana na juhudi zetu zote kwa upande wetu, ndipo tunaweza
kupata ushindi.
Katika imani ya Kikristo yapo mafundisho ambayo kila mmoja wetu anapaswa kuuzoeza
moyo wake upate kuyatafakari. Upendo wa Yesu upitao ufahamu wote, mateso yake kwa
ajili ya wanadamu walioanguka, kazi yake ya upatanishi kwa ajili yetu, na utukufu wake
adhimu ----- hizo ndizo siri ambazo malaika walitamani kuzichunguza. Viumbe wale wa
mbinguni wanapata katika dhamira [mawazo makuu] hizo mambo ya kutosha kuyavuta
na kuyashughulisha mawazo yao yenye kina sana; na sisi tunaohusika kwa undani kabisa,
je! tuonyeshe shauku yetu kidogo kuliko ile ya malaika katika kuyachunguza maajabu
hayo ya upendo huo unaotukomboa?
Akili, pamoja na moyo, vyote viwili, havina budi kutolewa wakf kwa kazi yake Mungu.
Ana madai juu ya vyote tulivyo navyo katika mwili wetu. ----- RH, Jan. 4, 1881.
KUYAZOEZA MAWAZO Aprili 16
Kwa hiyo vifungeni viuno vya nia zenu, na kuwa na kiasi; mkiitumainia kwa utimilifu
ile neema mtakayoletewa katika ufunuo wake Yesu Kristo. 1 Petro 1:13.
Wengi wanahitaji kufanya mabadiliko dhahiri katika mfumo wa mawazo na matendo
yao, kama wanataka kumpendeza Yesu. ----- 3BC 1150Mawazo ni lazima yazoezwe. Vifungeni viuno vya nia zenu, ili zipate kufanya kazi
upande wa mema, kufuatana na mipango iliyoandaliwa vizuri; hapo ndipo kila hatua
itakuwa ni hatua moja mbele, na hakuna juhudi wala wakati unaopotezwa bure kwa
kuyafuata mawazo yasiyokuwa dhahiri na mipango ya ovyo ovyo. Yatupasa kulizingatia
kusudi na lengo letu la maisha, na daima kuweka makusudi yanayofaa mbele yetu. Kila
siku mawazo hayana budi kuzoezwa na kuwekwa kwenye jambo moja kama vile dira
inavyoelekea kaskazini. Kila mmoja angekuwa na malengo na makusudi yake
mwenyewe, kisha alifanye kila wazo na tendo kuwa la aina ile inayoweza kutimiza kile
alichokikusudia. Mawazo ni lazima yadhibitiwe. Ni lazima pawepo na uthabiti wa
makusudi ili kutekeleza kile unachotaka kufanya....
Hakuna mwingine, isipokuwa ni wewe mwenyewe, awezaye kuyatawala mawazo yako.
Katika jitihada ya kukifikia kiwango cha juu sana, ufanisi wake au kushindwa kwake,
kutategemea sana juu ya tabia na jinsi mawazo yako yalivyoadibishwa. Iwapo mawazo
yamefungwa vizuri, kama vile Mungu anavyoagiza kuwa yawe hivyo kila siku, basi,
yatakuwa juu ya mafundisho yale yatakayotusaidia kumcha Mungu zaidi. Iwapo mawazo
ni mema, basi, kama matokeo yake, maneno nayo yatakuwa mema; matendo yatakuwa ya
aina ile inayoleta furaha na faraja na raha kwa watu....
Wale wanaoenenda bila kufikiri kwa makini, huenenda pasipokuwa na busara.
Wanafanya jitihada yao kwa vipindi vinavyobadilikabadilika, wanapiga hapa kisha pale,
wanashika hili na kisha lile, lakini hakuna matokeo yo yote yanayoonekana. Wanafanana
na mzabibu; mizizi yake isiyoelekezwa kunakotakiwa na inayoachwa kujitahidi yenyewe,
itashika takataka zo zote inazoweza kuzifikia kila upande; lakini kabla mzabibu huo
haujaanza kuwa na manufaa yo yote, mizizi yake haina budi kutenganishwa na vitu vile
ilivyovizinga, kisha kuelekezwa kule inakoweza kujinyonga kwenye vitu vile
vinavyoifanya [mizizi hiyo] ionekane mizuri, na iliyoumbika vizuri. ----- Letter 33, 1886.
JINSI YA KUUADIBISHA MOYO Aprili 17
Maneno ya kinywa changu, Na mawazo ya moyo wangu, Yapate kibali mbele zako, Ee
BWANA, Mwamba wangu, na Mwokozi wangu. Zaburi 19:14.Mawazo yanapaswa kuwa safi, tafakuri za moyo zinapaswa kuwa stahifu, iwapo maneno
ya kinywa chako yanatakiwa kuwa maneno yanayopata kibali cha Mbingu, na kuwa
msaada kwa wenzi wako. ----- RH, Juni 12, 1888.
Moyo wa asili, uliojaa uchoyo, ukiachiwa kufuata tamaa zake mbaya, utafanya mambo
yake pasipokuwa na nia ya juu, pasipo kujali utukufu wa Mungu, wala manufaa kwa
wanadamu. Mawazo yatakuwa machafu, tena machafu tu, daima.... Roho wa Mungu
anatoa maisha mapya moyoni, na kuyaleta mawazo na tamaa chini ya utii kwa mapenzi
yake Kristo....
Vijana wangeanza mapema kujenga mazoea mazuri ya mawazo yao. Yatupasa
kuuadibisha moyo upate kufikiri kwa kufuata njia nzuri, wala tusiuruhusu kutafakari
mambo yaliyo maovu.... Mungu anapoendelea kutenda kazi yake moyoni kwa njia ya
Roho wake Mtakatifu, mwanadamu anapaswa kushirikiana naye....
Yatupasa kuyatafakari Maandiko, tukifikiri kwa makini na kuwa unyofu mambo yale
yanayohusu wokovu wetu wa milele. Rehema isiyokuwa na kikomo na upendo wake
Yesu, kafara ile iliyotolewa kwa ajili yetu, mambo hayo yote yanataka mawazo yetu
mazito na ya makini. Tungefikiria sana juu ya tabia ya Mkombozi na Mwombezi wetu
mpendwa. Tungetafuta kuelewa maana ya mpango ule wa wokovu. Tungetafakari juu ya
utume wake yule aliyekuja kuwaokoa watu wake kutoka katika dhambi zao. Kwa
kutafakari daima mambo makuu ya mbinguni, imani yetu na upendo vitazidi kuwa na
nguvu. Maombi yetu yatakubaliwa na Mungu zaidi na zaidi, kwa sababu yatakuwa
yamechanganyika zaidi na zaidi na imani na upendo. Yatakuwa yametolewa kwa akili
zaidi na kwa bidii. Daima patakuwa na kumtegemea Yesu zaidi, nawe utakuwa na uzoefu
ulio hai wa kila siku katika kujua kutaka kwake na uweza wake Kristo wa kuwaokoa
wote wamjiao Mungu kwa Yeye....
Patakuwa na njaa na kiu ya rohoni ya kutaka kuwa kama Yeye yule tunayemwabudu.
Kadiri mawazo yetu yanavyokazwa juu yake Kristo, ndivyo kadiri tutakavyozungumza
juu yake kwa wengine, na kumwakilisha Yeye kwa ulimwengu. ----- RH, Juni 12, 1888.
KIMO KINACHOFAA KWA MOYO WA MWANADAMU Aprili 18
Jidhilini mbele za Bwana, naye atawakuza. Yakobo 4:10. Ni jambo gani linaloupa moyo wa mwanadamu kimo chake kinachotakiwa? Ni ule
msalaba wa Kalvari. Kwa kumtazama Yesu, mwenye kuanzisha na mwenye kutimiza
imani yetu, hamu yote ya kujitukuza sisi wenyewe inatupwa chini mavumbini.
Tunapoelewa vizuri, hapo ndipo inakuja roho ile ya kujishusha hadhi yetu ambayo
inatuletea hali ile ya kujidhalilisha wenyewe na unyenyekevu wa moyo. Tunapoutafakari
msalaba, tunawezeshwa kuuona mpango ule wa ajabu ulioandaliwa kwa kila muumini.
Mungu ndani Kristo... tukimwona kama inavyostahili, ataweza kusawazisha kujikweza
na kiburi cha mwanadamu. Hapatakuwa na kujitukuza wenyewe, bali patakuwa na
unyenyekevu wa kweli. ----- Letter 20, 1897.
Nuru inayoangaza kutoka kwenye msalaba ule wa Kalvari italinyenyekeza kila wazo la
kutakabari lililomo ndani yetu. Wale wanaomtafuta Mungu kwa moyo wao wote, na
kuupokea wokovu mkuu waliopewa, wataufungua mlango wa moyo wao kwa Yesu.
Wataacha kujihesabu kuwa wanao utukufu wao wenyewe. Hawatajivunia mafanikio yao
wenyewe, wala kujitwalia sifa wao wenyewe kwa uwezo walio nao, bali wataziona
talanta zao zote kuwa ni vipawa vyake Mungu, kutumika kwa utukufu wake. Kila uwezo
wa akili walio nao watauona kuwa ni wa thamani pale tu utakapotumika katika kazi yake
Kristo. ----- YI, Des. 6, 1900.
Unyenyekevu wake Kristo wakati ule alipouvika uungu wake na ubinadamu unastahili
kutafakariwa. Fundisho hilo lingekuwa limejifunzwa kwa makini kama vile ambavyo
lingestahili, pangesikika "Mimi" chache sana na zaidi sana angesikika Kristo. Ni kule
kujitukuza kwetu sisi wenyewe kunakosimama kati ya mjumbe wa kibinadamu na
Mungu na kuzuia mkondo unaotititika kutoka kwa Kristo ambao unaweza kumtajirisha
kila mwanadamu. Tunapomfuata Yesu katika njia ile ya kujikana nafsi na ya msalaba,
tutagundua kwamba hatuhitaji kujitahidi sana kuwa wanyenyekevu. Tunapotembea
katika nyayo za Kristo, tutajifunza upole na unyenyekevu wake wa moyo. Mawazo
machache mno yangetolewa kuifikiria nafsi yetu; kwa kuwa sisi hatuwezi kamwe
kujifanya watu wakubwa. Ni ule upole wake Kristo unaotufanya sisi kuwa wakubwa. ----
- Letter 100, 1895
Watu wa Mungu waaminifu, wanyenyekevu, wanaomwamini yeye wataivunjilia mbali
ibada ya nafsi zao kutoka katika mioyo yao, na Kristo atakuwa yote na katika yote. -----
MS 29, 1900.
SOMO ZURI SANA KWA MAWAZO YETU Aprili 19
Kutafakari kwangu na kuwe kutamu kwake; Mimi nitamfurahia BWANA. Zaburi
104:34.Mbona mawazo yenu hamyakazi juu ya utajiri wa Kristo usiopimika, ili mpate
kuwagawia wengine johari za ile kweli? Katika Neno la Mungu kuna migodi iliyojaa
utajiri wa ile kweli hata tunaweza kutumia maisha yetu yote kuutafuta, na bado tutajikuta
ndio kwanza tunaanza tu kuziona hazina zake za thamani. Chimbeni shimo liende chini
sana, na kuzileta juu hazina zake. Lakini ni vigumu kufanya hivyo kama tunayo roho ya
uvivu, isiyotulia mahali pamoja, inayotafuta daima kitu kile tu kitakachozifurahisha
fahamu za mwili, yaani, kitu cha kuchekesha, na kutuletea kicheko cha kipumbavu....
Mioyo ambayo inajishughulisha sana kusoma mambo ya kipuuzi, yaliyojaa hadithi za
kusisimua, au inayotafuta burudani, haiwezi kutafakari juu ya Kristo, wala haiwezi
kuufurahia utimilifu wa pendo lake. Moyo ule unaopata furaha yake katika mawazo ya
kipumbavu na maongezi ya ovyo, umepungukiwa na furaha ya Kristo kama vile Milima
ile ya Gilboa ilivyokosa umande au mvua.
Je! uzoefu [maisha] wenu wenyewe hauwashuhudii hayo? Mnakuwa na amani moyoni
mwenu ya kiasi gani mwisho wa siku iliyotumika kwa mambo ya kipuuzi, yaani, katika
mazungumzo ya kawaida yasiyokuwa na maana? Je! mnaweza kwenda kulala usiku,
mkisema, "Salama, ni salama rohoni mwangu?"... Wewe unapokuja katika nyumba ya
Mungu, yaani, katika mkutano wa ibada, ni mara ngapi mawazo yako yanageuka na
kulitafakari neno lile la kipuuzi ambalo mtu fulani amelisema, au hadithi ile ya kipuuzi
au jambo lile la kuchekesha ulilolisoma au uliloliona. Na wazo hilo litakuja tu wakati ule
ili kuuzuia mwonzi unaong'aa wa utukufu wake Kristo usiingie ndani ya moyo wako,
nawe unapoteza manufaa ya nuru ile iliyotumwa kwako kutoka mbinguni ambayo
ungestahili kuipokea....
Tuna haja ya kuujaza moyo wetu na Kristo daima, na kuuondoa uchoyo [kujipenda
nafsi] wote uliomo humo pamoja na dhambi zote.... Kwa hakika ile ile unavyouacha
moyo wako kuwa tupu kabisa kwa kuondoa kujisifu na upuuzi , ndivyo nafasi tupu
iliyobaki humo itakavyojazwa na kile ambacho Mungu anangojea kukupa ----- yaani,
Roho wake Mtakatifu. Hapo ndipo katika hazina njema ya moyo wako utatoa yaliyo
mema, yaani, johari nyingi za mawazo mema, na wengine watayashika maneno yako
utakayowaambia.... Mawazo yako na mapenzi yako yatakuwa juu ya Kristo, nawe
utaakisi kwa wengine kile ambacho kimekuangazia juu yako kutoka kwa Jua lile la Haki.
----- RH, Machi l5, 1892.
MUDA WA KUTAFAKARI MAMBO YA MUNGU Aprili 20 Bali Sheria ya BWANA ndiyo impendezayo, Na Sheria yake huitafakari mchana na
usiku. Zaburi 1:2.
Wazo lako la mwisho usiku, wazo lako la kwanza asubuhi, lingekuwa juu yake Yeye
ambaye ndani yake tumaini lako la uzima wa milele limewekwa. ----- Letter 19, 1895.
Wengi wanaonekana kuwa na chuki kwa ajili ya muda unaotumika kwa kutafakari
mambo ya Mungu, na kuyachunguza Maandiko, pamoja na maombi, kana kwamba muda
huo uliotumika hivyo umepotea bure. Natamani kwamba ninyi nyote mngeweza
kuyaangalia mambo hayo katika nuru ile ile ambayo Mungu angetaka mfanye hivyo; kwa
maana hapo ndipo mngeweza kuufanya ufalme wa mbinguni kuchukua umuhimu wa
kwanza kwenu.... Kama vile mazoezi ya mwili yanavyoongeza hamu ya kula chakula, na
kuupa mwili nguvu na afya, hivyo ndivyo mazoezi ya ibada yanavyoongeza neema na
nguvu ya kiroho.
Mapenzi yako uyaelekeze kwake Mungu. Tafakari ukuu wake, rehema zake, na utukufu
wake. Hebu moyo wako na upendezwe na fadhili zake na upendo wake na utimilifu wa
tabia yake. Zungumza juu ya uzuri wa kuvutia sana ulioko mbinguni, na makao yale ya
mbinguni anayowaandalia wale walio waaminifu. Mtu yule ambaye maongezi yake yako
mbinguni, ni Mkristo mwenye manufaa sana kwa wote wanaomzunguka. Maneno yake
yana manufaa na yanaburudisha. Yana uwezo unaowabadilisha maisha yao wale
wanaoyasikia. ----- 3BC 1157.
Kuna hitaji la kudumu la kuwa na maombi ya faragha [ya mtu mmoja mmoja peke yake]
pamoja na Mungu. Yatupasa kuwa na roho ile ile ya Kristo kama tunataka kuwagawia
hiyo wengine. Hatuwezi kupambana na wajumbe wa kishetani na kibinadamu
walioungana pamoja isipokuwa tu kama tunatumia muda mwingi kuongea na yule aliye
Chimbuko la nguvu zote. Kuna nyakati fulani ambapo tutatakiwa kwenda mbali na kelele
za shughuli za kidunia na sauti za wanadamu, yaani, kwenda mahali pa kimya kuisikiliza
sauti ya Yesu. Kwa njia hiyo tunaweza kuuonja upendo wake na kuinywa roho yake.
Kwa njia hiyo tutajifunza kuisulibisha nafsi yetu. Njia hiyo ya utendaji huenda ikaweza
kuonekana kwa moyo wa kibinadamu kuwa haiwezekani. "Sina muda," wewe waweza
kusema. Lakini unapolitafakari sana jambo hilo kama vile lilivyo hasa, utaona kwamba
hupotezi muda wo wote; maana unapojipatia uweza na neema vitokavyo kwa Mungu
peke yake, basi, WEWE siwe unayeikamilisha kazi hiyo. Ni Yesu ambaye ndiye mtendaji
hasa. "Pasipo mimi" asema Kristo, "ninyi hamwezi kufanya neno lo lote." Yohana 15:5....
Kutafakari pamoja na maombi yale ya dhati kutaamsha juhudi yetu takatifu. ----- MS 25a,
1891.IMANI NI KITU GANI? Aprili 21
Basi imani ni kuwa na hakika ya mambo yatarajiwayo, ni bayana ya mambo
yasiyoonekana. Waebrania 11:1.
Imani ndani ya Kristo si kazi ya maumbile yetu, bali ni kazi ya Mungu ndani ya mioyo
ya wanadamu; ambayo inafanywa mioyoni mwetu hasa na Roho Mtakatifu, anayemfunua
Kristo kwetu, kama vile Kristo alivyomfunua Baba kwetu. Imani ni kuwa na hakika ya
mambo yatarajiwayo, ni bayana ya mambo yasiyoonekana. Pamoja na uweza wake
unaotuhesabia haki, yaani, unaotutakasa; [imani hiyo] iko juu ya kile wanadamu
wanachokiita sayansi. Ni sayansi ya mambo yale ya hakika ya milele. Sayansi ya
kibinadamu mara nyingi inatuhadaa na kutupotosha, lakini sayansi hiyo ya mbinguni
haitupotoshi kamwe. Ni rahisi mno hata mtoto mdogo anaweza kuielewa, hata hivyo
wasomi sana [wataalam] hawawezi kuifafanua. Haielezeki wala haipimiki, inapita upeo
wa maneno yote ya kibinadamu. ----- MS 44, 1904.
Kuukubali upatanisho wake Kristo ndio msingi wa imani hiyo ya kweli.... Wale
watakaojiangalia kwa muda mrefu wa kutosha katika kioo cha Mungu [Amri Kumi]
wataziona na kuzidharau dhambi zao, wataona jinsi wasivyofanana na Yesu mpole na
mnyenyekevu wa moyo, hapo ndipo watapata nguvu za kushinda. Wale wote
wanaoamini kweli kweli wataungama dhambi zao na kuziacha. Watashirikiana na Kristo
katika kazi ya kuileta chini ya utawala wa mapenzi yake Mungu mielekeo yao yote
mibaya [ya dhambi] waliyoirithi [kwa wazazi wao] na ile waliyojifunza wenyewe kwa
kujizoeza, ili dhambi isipate kuwatawala. Wakimtazama Yesu, mwenye kuanzisha na
mwenye kutimiza imani yao, watabadilishwa wapate kufanana naye. Watakua [kiroho] na
kukifikia cheo cha wanaume na wanawake cha kimo kile cha utimilifu wake Kristo
Yesu.... Wale wanaoamini kweli kweli, yaani, wanaoungama na kuziacha dhambi zao,
wataendelea zaidi na zaidi kufanana na Kristo, mpaka hapo itakaposemwa juu yao kule
mbinguni, "Ninyi mmetimilika katika Yeye." Wakolosai 2:10. ----- Letter 21, 1901.
"Ombeni, nanyi mtapewa" (Mathayo 7:7) ni ahadi tuliyopewa. Sehemu yetu ni
kulitegemea Neno kama lisemavyo kwa imani isiyotikisika, tukiamini kwamba Mungu
atafanya kulingana na ahadi yake. Iache imani ipasue njia yake na kupenya katikati ya
kivuli cha yule adui. Linapotokea [moyoni mwako] shaka lo lote linalouliza swali, nenda
kwa Kristo na kuuacha moyo wako kutiwa nguvu kwa kuzungumza naye. Ukombozi ule
alioununua kwa ajili yetu ni kamili. Toleo lile alilolitoa lilitosha na halina mipaka.
Mbingu ina msaada tele usiokwisha kamwe kwa wote wanaouhitaji. ----- Letter 42, 1900.MMEOKOLEWA KWA NEEMA YA MUNGU Aprili 22
Kwa maana mmeokolewa kwa neema, kwa njia ya imani; ambayo hiyo, haikutokana na
nafsi zenu, ni kipawa cha Mungu; wala si kwa matendo, mtu awaye yote asije akajisifu.
Waefeso 2:8,9.
Upendeleo wa Mungu, yaani, neema ya Mungu aliyotupa sisi kwa njia ya Yesu Kristo, ni
wa thamani mno kuweza kubadilishana na matendo yanayodhaniwa kuwa ni ya haki, kwa
upande wa mwanadamu anayekufa, mwenye dhambi, ambayo ameyatenda. Mwanadamu
hana cho chote ndani yake mwenyewe. Talanta ile inayotukuzwa mno haitokani na
mwanadamu, bali ni kipawa cha Muumbaji wake, wala haiwezi kununua kitu cho chote
kutoka kwa Mungu. Dhahabu wala fedha haviwezi kununua upendeleo huo wa Mungu;
kwa maana utajiri wa ulimwengu huu ni talanta ya Mungu aliyotukabidhi. Hebu na
asiwepo mtu ye yote anayefikiri kwamba matoleo yake ya thamani kubwa kwa mashirika
ya ufadhili yatamwinua mbele za macho ya Mungu, au kumnunulia upendeleo wa
Mbingu, au kumpatia nafasi katika makao yale Yesu aliyokwenda kuwaandalia wale
wampendao. Damu ya thamani ya Kristo inatosha kabisa....
Ufufuo wa Kristo kutoka kwa wafu ulikuwa ndio muhuri wa Baba yake wa kuukubali
utume wake Kristo. Lilikuwa ni tangazo la hadhara la kuridhika kwake kabisa na kazi ile
ya upatanisho. Aliikubali kafara ile Yesu aliyoitoa kwa ajili yetu. Ilikuwa ni kila kitu
alichotaka Mungu, timilifu na kamilifu. Hakuna mwanadamu awaye yote ambaye kwa
matendo yake mwenyewe angeweza kuikamilisha kazi ile aliyoifanya Kristo. Akiwa pale
msalabani Yesu alilia kwa sauti kuu, akisema, "Imekwisha!" utukufu na shangwe
viliitikisa Mbingu, na mfadhaiko mkubwa ukauangukia ule muungano wa nguvu za uovu.
Baada ya kilio kile cha ushindi mkuu, Mkombozi wa ulimwengu akainamisha kichwa
chake na kufa,... lakini kwa kifo chake akawa mshindi, naye amefungua malango yale ya
utukufu wa milele ili kwamba wale wote wanaomwamini wasipotee [wasiangamie], bali
wawe na uzima wa milele.
Tumaini pekee la mwenye dhambi ni kumtegemea kabisa Yesu Kristo.... Kukubalika
kwetu na Mungu ni kwa hakika tu kupitia kwa Mwanawe mpendwa, na matendo mema
ni matokeo tu ya utendaji wa upendo wake unaosamehe dhambi. Hatuna sifa yo yote sisi
katika hayo [matendo mema], wala hatupewi kitu cho chote kwa matendo yetu mema
ambacho tunaweza kukitumia kudai kwamba tulikuwa na sehemu katika wokovu wa roho
zetu. Wokovu ni kipawa kinachotolewa bure kwa muumini, anapewa kwa ajili ya Kristo peke yake. Moyo unaosumbuka unaweza kupata amani kwa njia ya Imani katika Kristo....
[Mwanadamu] hawezi kuonyesha matendo yake mema kama sababu ya wokovu wa roho
yake. ----- RH, Jan. 29, 1895.
HISIA SI KIONGOZI SALAMA Aprili 23
Mwenye haki ataishi kwa imani yake. Habakuki 2:4.
Wengi wanapitisha miaka mingi wakiwa gizani na mashakani kwa sababu hawajisikii
ndani yao kama vile wanavyotaka wenyewe. Lakini hisia [kujisikia] haina uhusiano wo
wote na imani. Imani ile itendayo kazi kwa upendo na kuitakasa roho si suala la kujisikia.
Inakwenda kwa ujasiri kwenye ahadi za Mungu, ikiamini kwa uthabiti kwamba kile
alichosema [Mungu], anaweza pia kukitenda. Mioyo yetu inaweza kufunzwa kusadiki,
yaani, kufundishwa kulitegemea Neno la Mungu. Ni Neno lile lile linalotangaza kwamba
"Mwenye haki ataishi kwa imani" (Warumi 1:17), sio kwa hisia [kujisikia]. ----- YI, Julai
8, 1897.
Hebu na tuweke mbali kila kitu, kama vile, kuwa na mashaka na utovu wa imani katika
Yesu. Hebu na tuanze kuishi maisha ya kawaida, yaani, kumtegemea Mungu kama mtoto
mdogo, pasipo kuzitegemea hisia zetu, bali kwa kutegemea imani. Usimwaibishe Kristo
kwa kuona mashaka juu ya ahadi zake. Anataka sisi tumwamini Yeye kwa imani ile
isiyotikisika.
Kuna kundi fulani la watu wasemao, "Naamini, Naamini," na kuzidai ahadi zote za
Mungu ambazo zimetolewa kwa sharti la utii; lakini wao hawataki kutenda kazi zake
Kristo. Mungu haheshimiwi kwa imani kama hiyo. Ni ya unafiki mtupu. Kundi jingine
nalo linajaribu kuzishika Amri zote [Kumi] za Mungu, bali wengi wao hawaifikii haki
yao tukufu kwa kuwa hawazidai ahadi zile zilizotolewa kwa ajili yao. Ahadi za Mungu ni
kwa wale wazishikao Amri zake [Kumi], yaani, wale wafanyao yale yanayopendeza
machoni pake.
Najikuta kwamba mimi napaswa kupiga vita vile vizuri vya imani kila siku. Yanipasa
kutumia imani yangu yote, na sio kutegemea hisia zangu [ninavyojisikia ndani yangu];
yanipasa kutenda kana kwamba nilijua ya kwamba Bwana alikuwa amenisikia, na
kwamba angenijibu mimi na kunibariki. Imani sio hisia ya furaha inayopita upesi moyoni; ni kumwamini Mungu kama asemavyo katika Neno lake ----- kusadiki kwamba
atazitimiza ahadi zake kwa sababu alisema angefanya hivyo. ----- Letter 49, 1888.
Umtumainie Mungu, umtegemee yeye, na kutulia katika ahadi zake, si kitu kama
unajisikia kwamba unayo furaha au la. Hisia nzuri [kujisikia vizuri] moyoni sio ushahidi
wa kukuthibitishia wewe kwamba wewe u mwana wa Mungu, wala hisia zile
zilizovurugika, yaani, zilizojaa wasiwasi, hofu, na kuchanganyikiwa sio zinazokupa
wewe ushahidi kwamba wewe sio mwana wa Mungu. Njoo kwenye Maandiko na kwa
kutumia akili yako mwamini Mungu kama anavyosema katika Neno lake. Tekeleza
masharti yaliyowekwa na kusadiki kwamba atakupokea wewe kama mwana wake [kwa
kuwa Neno lake linasema hivyo]. Usiwe mtu asiyeamini, bali aaminiye. ----- Letter 52,
1888.
HISIA NA IMANI NI VITU VIWILI TOFAUTI KABISA Aprili 24
Maana twaenenda kwa imani, si kwa kuona [kujisikia moyoni]. 2 Wakorintho 5:7.
Tunapotekeleza matakwa ya Neno lile Lililoandikwa hapo ndipo tunapokwenda kwa
imani. Tunamwaibisha Mungu tunaposhindwa kumtegemea baada ya Yeye kutupatia
ushahidi wa ajabu kama huo wa upendo wake uliojaa huruma nyingi katika kipawa cha
Mwanawe. Yatupasa kuendelea kumtazama Yesu, kutoa maombi yetu kuelekea juu kwa
imani, yaani, kuishikilia nguvu yake. Iwapo tutazungumza zaidi juu ya imani, yaani,
kufurahia zaidi mibaraka tunayojua kwamba tunayo, basi, kila siku tungekuwa na
uchangamfu mkubwa na nguvu nyingi.
Hisia [kuona au kujisikia moyoni] na imani ni vitu viwili tofauti kabisa, kila kimoja kwa
chenzake, kama vile mashariki ilivyo mbali na magharibi. Imani haitegemei hisia. Kila
siku yatupasa kujitoa wakf wenyewe kwa Mungu, na kuamini kwamba Kristo anaijua na
kuikubali kafara yetu hiyo tuliyoitoa, pasipo sisi wenyewe kuanza kujichunguza
wenyewe kuona kama tuna kiasi fulani cha hisia ndani yetu ambacho tunadhani
kingelingana na imani yetu [ili tuwe na hakika]. Je! sisi hatunao ushahidi kwamba Baba
yetu aliye mbinguni atazidi sana kuwapa Roho wake Mtakatifu hao wamwombao kwa
imani kuliko vile wazazi wawezavyo kuwapa watoto wao vipawa vyema? Yatupasa
kusonga mbele kana kwamba kila ombi tunalolipeleka kwenye kiti kile cha enzi cha
Mungu tulikuwa tumesikia jibu kutoka kwake Yule ambaye ahadi zake hazikosi kamwe
kutimizwa. Hata kama tumevunjwa moyo kwa huzuni ni haki yetu kumwimbia Mungunyimbo tamu mioyoni mwetu. Tunapofanya hivyo ukungu na mawingu vitakunjuliwa na
kuondolewa kwetu, nasi tutapita kutoka kwenye kivuli na giza na kuingia katika
mwangaza safi wa kuwapo Kwake.
Kama tungeizoeza mioyo yetu kuwa na imani zaidi, upendo mwingi zaidi, uvumilivu
mwingi zaidi, tegemeo letu timilifu kwa Baba yetu aliye Mbinguni, basi, tungekuwa na
amani nyingi zaidi na furaha tunapopita katika mapambano ya maisha haya. Bwana
hapendezwi kutuona sisi tukiwa na wasiwasi na masumbuko na kujiondoa sisi wenyewe
kutoka mikononi mwake Yesu. Yeye peke yake ndiye Chimbuko la kila neema [kila
tendo jema], utimilifu wa kila ahadi, na upatikanaji wa kila baraka.... Safari yetu
ingekuwa ya upweke kweli kama asingekuwapo Yesu. "Sitawaacha ninyi yatima [bila
faraja ya Roho Mtakatifu]," (Yohana 14:18) asema kwetu sisi. Hebu na tuyahifadhi kwa
upendo mkubwa maneno yake, tuziamini ahadi zake, tuzikariri tena na tena wakati wa
mchana na kuzitafakari wakati wa usiku, kisha na tufurahi. ----- MS 75, 1893.
IMANI ITENDAYO KAZI NA KUTUTAKASA Aprili 25
Ambaye alijitoa nafsi yake kwa ajili yetu, ili atukomboe na maasi yote, na kujisafishia
watu wawe milki yake mwenyewe, wale walio na juhudi katika matendo mema. Tito
2:14.
Unapotazama kule Kalvari si kwa kusudi la kuunyamazisha moyo wako katika utendaji
wake wa majukumu uliyopewa, si kwa kusudi la kujilaza usingizi wewe mwenyewe, bali
ni kwa sababu ya kuwa na imani ndani ya Yesu, imani itakayotenda kazi, ikiutakasa
moyo wako na unafiki wako unaoletwa na choyo yako. Tunapomshika Kristo kwa imani,
kazi yetu ndipo tu inapoanza. Kila mtu ana mazoea machafu na ya dhambi ambayo
inampasa kuyashinda kwa kupigana vita kwa nguvu. Iwapo mmoja ni mfuasi wake
Kristo, basi, hawezi kuwa mdanganyifu katika biashara yake, hawezi kutumia lugha
chafu katika maongezi yake. Hawezi kuwa na makuu mengi na kujitukuza mwenyewe.
Hawezi kuwa jeuri, wala hawezi kutumia maneno makali, na kukaripia na kushutumu
watu. Kazi ya upendo hutokana na kazi ya imani. Dini ya Biblia inamaanisha kufanya kazi
daima.... Yatupasa kuwa na juhudi katika matendo mema; kuwa waangalifu kuendelea
kuwa na matendo mema. Na yule Shahidi wa Kweli asema, "Nayajua matendo yako."
Ingawa ni kweli kwamba shughuli [kazi] zetu zote tunazofanya kwa bidii haziwezi
zenyewe kutuhakikishia wokovu wetu, lakini ni kweli pia kwamba imani ile
inayotuunganisha sisi na Kristo itaichochea mioyo yetu kufanya juhudi hiyo. ----- 6BC
1111.
Mkristo wa kweli amejaa matendo mema; anazaa matunda mengi sana. Anawalisha
wenye njaa, anawavika nguo walio uchi, anawatembelea wagonjwa, na kuwahudumia
wale wanaoteswa. Wakristo wanapendezwa kwa moyo wao wote na watoto
wanaowazunguka, ambao, kwa njia ya majaribu ya yule adui ambayo ni vigumu
kuyatambua, wako tayari kuangamia. Akina baba na mama, kama ninyi mmewalinda
watoto wenu wenyewe kutokana na hila za yule adui, basi, waangalieni wale
wanaowazunguka ninyi ili kuziokoa roho za watoto ambao hawana ulinzi kama huo....
Kuna vijana wanaotuzunguka pande zote ambao washiriki wa kanisa wanawajibika
kwao; kwa maana Kristo amewafia nao.... Wana thamani machoni pake Mungu, naye
anataka nao wapate furaha yao ya milele.... Kristo anatoa mwito wa ushirikiano wa hiari
kutoka upande ule wa wajumbe wake katika kuifanya kazi hiyo kwa bidii na kwa
uaminifu kwa ajili yawokovu wa roho za watu. ----- RH, Jan. 29, 1895.
Dini inayong'aa kwa matendo mema inatoa mwanga safi, wa hakika, na ulio salama. -----
Letter 38, 1890.
MAHALI PAKE HAYO MATENDO MEMA Aprili 26
Maana tu kazi yake, tuliumbwa [upya] katika Kristo Yesu, tutende matendo mema,
ambayo tokea awali Mungu aliyatengeneza ili tuenende nayo. Waefeso 2:10.
Hebu na asiwepo mtu ye yote anayechukua msimamo uliowekewa mipaka, yaani, ulio
mfinyu, kwamba matendo yo yote ya mwanadamu yanaweza kusaidia kuchangia hata
kwa kiasi kidogo sana kulipa deni la dhambi zake. Hilo ni kosa la kufisha. Kama ninyi
mnataka kulielewa jambo hilo, basi, hamna budi... kwa mioyo yenu minyenyekevu
kuuchunguza upatanisho wake. Jambo hilo linaeleweka kwa utusitusi mno kiasi kwamba
maelfu kwa maelfu wanaodai kuwa ni wana wa Mungu [kwa kweli] ni wana wa yule
mwovu, kwa sababu wanategemea matendo yao wenyewe [kuwaokoa]. Sikuzote Mungualidai matendo mema, Sheria yake [Amri Kumi] inayadai, lakini kwa kuwa mwanadamu
alijiweka mwenyewe dhambini mahali ambapo matendo yake mema hayakuwa na
thamani yo yote, basi, ni haki ya Yesu peke yake inayoweza kufaa. ----- 6BC 1071.
Lakini, je! matendo mema hayana thamani yo yote halisi? Je! mwenye dhambi yule
anayetenda dhambi kila siku bila kuwa na hofu ya kuadhibiwa, anaangaliwa na Mungu
kwa upendeleo ule ule kama yule ambaye kwa njia ya imani katika Kristo anajitahidi
kutenda mema katika uadilifu wake? Maandiko yanajibu hivi, "Tu kazi yake, tuliumbwa
[upya] katika Kristo Yesu, tutende matendo mema, ambayo toka awali Mungu
aliyatengeneza ili tuenende nayo." Katika mpango wake mtakatifu kwa njia ya upendeleo
wake tusiostahili [tusioufanyia kazi], Bwana ameagiza kwamba matendo mema yatapata
thawabu yake. Tunakubalika kwa njia ya wema wake Kristo peke yake; na matendo yale
ya rehema, yaani, matendo yale ya upendo tunayotenda, ni matunda [matokeo] ya imani;
nayo yanakuwa mbaraka kwetu sisi; kwa maana wanadamu watalipwa kwa kadiri ya
matendo yao. Ni manukato ya wema wake Kristo yanayoyafanya matendo yetu mema
kukubalika kwa Mungu, tena ni ile neema inayotuwezesha kutenda matendo hayo
ambayo kwayo atatulipa ujira wetu. Matendo yetu yenyewe kama yalivyo hayana sifa yo
yote.... Hatustahili kupewa shukrani zo zote kutoka kwa Mungu [kwa matendo hayo].
Tumefanya tu yale tuliyopaswa kutenda, wala matendo yetu hayo yasingeweza kutendwa
kwa nguvu zetu wenyewe zitokanazo na miili yetu ya dhambi. ----- RH, Jan. 29, 1895.
Kristo anaweza kuokoa kabisa.... Yote yale mwanadamu anayotakiwa kufanya kwa ajili
ya wokovu wake mwenyewe ni kuukubali mwaliko ule usemao, "Na yeye atakaye, na
ayatwae maji ya uzima bure." Hakuna dhambi yo yote iwezayo kutendwa na mwanadamu
ambayo utoshelevu wake haujatimizwa pale Kalvari. ----- 6BC 107l.
USIWE MNAFIKI Aprili 27
Amin, amin, nawaambieni, Yeye aniaminiye mimi, kazi nizifanyazo mimi, yeye naye
atazifanya; naam, na kubwa kuliko hizo atafanya, kwa kuwa mimi naenda kwa Baba.
Yohana 14:12.
Kwa kweli Wakristo wanapaswa kuwa wawakilishi wake Yesu Kristo; hawapaswi kuwa
wanafiki. Je! ulimwengu utakuwa na dhana gani juu ya Mungu kwa kuuangalia
mwenendo wa wale wanaolichukua bure jina lake Kristo, wala hawafanya kazi zake? Je! wale wanaojidai kuwa ni waumini, lakini ambao si waumini ndani ya mioyo yao, ambao
wanazisaliti amana takatifu walizopewa, na kufanya kazi za yule adui, hawatasondwa
kidole [na walimwengu], wakisema, "Lo! hao ndio Wakristo, nao wanadanganya na
kusema uongo, wala hawawezi kuaminika?" Hao, kusema kweli, sio wale
wanaomwakilisha Mungu. Lakini Mungu hatawaacha walimwengu kudanganyika.
Mungu anao watu wake wa pekee hapa duniani, wala haoni haya kuwaita ndugu zake;
kwa maana wanafanya kazi zake Kristo. Wanadhihirisha kwamba wanampenda Mungu,
kwa sababu wanazishika Amri zake [Kumi]. Wanachukua sura ya Mungu. Wao ni
tamasha kwa ulimwengu, kwa malaika, na kwa wanadamu. -----
RH, Jan. 29, 1895.
Thawabu, yaani, utukufu ule wa mbinguni, watakayopewa washindi italingana na
kiwango kile kile walichoiwakilisha tabia yake Kristo kwa ulimwengu huu. "Apandaye
haba atavuna haba." 2 Wakorintho 9:6. Mungu na ashukuriwe kwamba ni haki yetu
kupanda duniani mbegu zitakazovunwa katika ule umilele. Taji ya uzima itang'aa sana,
au itafifia, itang'aa ikiwa na nyota nyingi juu yake, ama itaangazwa na johari chache tu,
kulingana na matendo yetu wenyewe. Siku kwa siku tunaweza kujiwekea msingi mwema
kwa wakati ule ujao. Kwa kujikana nafsi, kwa kuwa na roho ya umishonari, kwa
kuyaweka matendo yote mema katika maisha yetu kwa kadiri iwezekanavyo, kwa
kutafuta kumwakilisha Kristo kwa tabia zetu ili tupate kuwaleta wengi kwenye kweli,
tutaheshimiwa kwa kupewa ile thawabu.
Ni juu yetu sisi kwenda katika nuru, kuitumia vizuri sana kila nafasi na haki
tunayopewa, kukua katika neema na katika kumjua Bwana wetu Yesu Kristo, na kwa njia
hiyo tutaweza kufanya kazi zake Kristo, na kujiwekea hazina yetu kule mbinguni kwa
salama. ----- 6BC 1105.
SHIKILIA NAFASI YAKO SAA KWA SAA Aprili 28
Na tulishike sana ungamo la tumaini letu, lisigeuke; maana yeye aliyeahidi ni
mwaminifu.
Waebrania 10:23. Ni haki yetu, sisi kama watoto wa Mungu, kulishika sana ungamo la tumaini letu,
lisigeuke. Wakati fulani uwezo mkuu wa majaribu unaonekana kuichosha kabisa nia
yetu, na kule kuitumia imani yetu huonekana kwamba ni kinyume kabisa na ushahidi
wote wa fahamu au hisia zetu; walakini nia yetu ni lazima tuiweke upande wa Mungu.
Yatupasa kuamini kwamba ndani yake Kristo zimo nguvu za milele na ufanisi.... Saa kwa
saa yatupasa kuishikilia nafasi yetu na kushangilia ushindi wetu ndani yake Mungu,
tukiwa imara katika nguvu zake....
Yote yawezekana kwao waaminio. Kwa vile Mungu anafanya kazi yake ndani yenu,
basi, kwa salama kabisa mnaweza kuukaza uso wenu kama gumegume na kufanya
mapenzi yake, nanyi mnaweza kumtumainia Bwana kabisa.
Kila siku unapaswa kujitoa wakf wewe mwenyewe kwa Mungu. Kila siku inakupasa
kulifanya upya agano lako kuwa wake kabisa kuanzia siku hiyo na hata milele. Usiweke
tumaini lo lote juu ya hisia zako zinazobadilikabadilika, bali ikite miguu yako juu ya
jukwaa lililo imara la ahadi za Mungu, ukimwaambia hivi: Wewe umesema; Mimi
naiamini ahadi yako hiyo. Hiyo ndiyo imani iliyojaa hekima.
Hisia zako zitakusumbua utakapowaona baadhi yao wakifuata njia ile iliyo kinyume na
kanuni zake Kristo; maonjo na kupimwa kwa imani yako vitakujia; walakini mimi
ninakusihi sana kwamba umtazame Yesu peke yake, nawe usiruhusu hata mojawapo ya
mambo hayo kuufanya moyo wako kuwa mgumu, wala kukuletea giza, wala mashaka.
Usiruhusu kitu cho chote kuifanya imani yako kushindwa. Uishi kama uko machoni pake
Mungu. Zungumza na Yesu kama vile ambavyo wewe ungeweza kuongea na rafiki yako.
Yeye yuko tayari kukusaidia katika maonjo yako yaliyo makali mno; yu pamoja nawe
katika mashaka yako mazito mno....
Hisia ile inayokufanya wewe kuwa na hakika usiidharau; tunapaswa kumsifu Mungu
kwa njia hiyo; lakini hisia zako zinaposhuka chini kutokana na majonzi uliyo nayo,
usifikiri ya kwamba Mungu amebadilika kwako. Msifu Yeye vivyo hivyo, kwa sababu
unalitumainia neno lake, na sio hisia zako. Umefanya agano naye kwenda kwa imani,
kutotawaliwa na hisia zako. Hisia zinabadilika kulingana na hali ya mambo ilivyo....
Nenda mbele zake Mungu kwa imani, nawe tulia kabisa katika ahadi zake. Yesu asema,
"Na tazama, mimi nipo pamoja nanyi siku zote, hata ukamilifu wa dahari [mwisho wa
ulimwengu]." Mathayo 28:20. ----- Letter 42, 1890.
NGUVU KWA SIKU YA LEO Aprili 29Na kadiri ya siku zako ndivyo zitakavyokuwa nguvu zako. Kumbukumbu la Torati
33:25.
Namshukuru Mungu kwa ahadi ya neema yake, ambayo ni kwa watu wake sasa, siku ya
leo.... Ahadi hii sio kwamba tutakuwa na nguvu kwa siku ya leo kwa ajili ya dharura ya
siku zijazo, sio kwamba shida inayotarajiwa kutokea mbele itafanyiwa maandalizi yake
kabla haijatokea, yaani, kabla haijatufikia. Sisi, tukienda kwa imani, tunaweza kutazamia
kupewa nguvu hiyo na msaada huo kwa haraka kama vile mambo yetu yanavyohitaji.
Tunaishi kwa imani, sio kwa kuona [kuhisi]. Mpango wa Bwana ni kwamba sisi
tumwombe yeye mambo yale yale tunayoyahitaji [kwa wakati huo]. Neema ya kesho
haitolewi leo. Shida za wanadamu ni nafasi ya Mungu kutenda kazi yake.... Neema ya
Mungu haitolewi kamwe ili kutapanywa ovyo, kutumiwa vibaya, ama kupotolewa, ama
kuachwa inapata kutu kwa kukosa kutumika....
Wakati mnapobeba majukumu yenu ya kila siku kwa upendo na kicho chake Mungu,
kama watoto watiifu wanaotembea katika unyenyekevu wote wa moyo, hapo ndipo
nguvu na hekima itokayo kwa Mungu itakapotolewa kwenu ili mpate kukabiliana na kila
jambo linalochosha.
Hatutaweza kukabiliana na maonjo ya wakati huu bila kuwa na Mungu. Hatupaswi kuwa
na ushujaa na ushupavu waliokuwa nao wale wafia dini wa zamani mpaka hapo
tutakapoingizwa katika hali waliyokuwa nayo.... Yatupasa kupokea kila siku akiba ya
neema kwa kila dharura ya siku hiyo. Hivyo ndivyo tunavyokua katika neema na katika
kumjua Bwana wetu Yesu Kristo, na kama mateso yanatujia, kama tunapaswa kufungwa
ndani ya kuta za magereza kwa ajili ya imani ya Yesu na kuitunza Sheria takatifu [Amri
Kumi] ya Mungu, basi, "Kadiri ya siku zako ndivyo zitakavyokuwa nguvu zako." Kama
mateso yatarudiwa tena, basi, neema itatolewa ili kuichochea kila nguvu ya mioyo yetu
ipate kuonyesha ushujaa halisi.
Yatupasa kuwa karibu sana na Chimbuko la nguvu zetu siku kwa siku, na adui
atakapotujia kama gharika, Roho wa Mungu atainua juu bendera kwa ajili yetu dhidi ya
adui huyo. Ahadi ya Mungu ni ya hakika, kwamba nguvu zitatolewa kwetu kulingana na
siku zetu [kipindi tunachoishi]. Tunaweza tu kuwa na ujasiri wa kuzikabili nyakati zijazo
kwa nguvu ile inayotolewa kwetu kwa ajili ya shida zilizopo sasa. Uzoefu wetu ndani ya
Mungu kila siku unazidi kuwa wa thamani sana.... Usiuazime [leo] wasiwasi wa siku zile
za baadaye. Ni siku ya leo ambapo sisi tunayo mahitaji yetu.... Bwana ni msaada wetu,
Mungu wetu, na nguvu zetu kwa kila wakati wa shida. ----- MS 22, 1889.USHINDI JUU YA USHINDI Aprili 30
Kwa maana kila kitu kilichozaliwa na Mungu huushinda ulimwengu; na huku ndiko
kushinda kuushindako ulimwengu, hiyo imani yetu. 1 Yohana 5:4.
Mawingu yanapokuja kati ya roho yako na Mungu wako, na mambo yote
yanayokuzunguka yanapogeuka na kuwa giza linaloogofya, adui anaposimama tayari
kuirubuni roho yako kutokana na uaminifu wake kwa Mungu na kwa ile kweli, na
makosa yanapojitokeza na kuonekana kuwa yanakubalika na yanapendeza, huo ndio
wakati wa kuomba na kuitumia imani yako kwa Mungu wako.... Kuihifadhi imani yako,
moyo wako unawezeshwa kupaa juu kupita upeo wake wenyewe, na kupenya kivuli kile
cha kishetani ambacho yule adui anakitupa katika njia ya kila mtu anayejitajidi kuipata
taji ile isiyonyauka....
Yesu alisema, "Kesheni mwombe, msije mkaingia majaribuni." Marko 14:38. Yatupasa
kukesha na kuomba kwa kadiri Shetani anavyozidi tu kutuletea mawingu ya mashaka,
yaliyojaa kila aina ya uovu anaoweza kutunga ili kuushawishi moyo wa mwanadamu
kuanguka majaribuni. Lakini wingu hilo linalokuwa kati ya Mungu na mjumbe wake wa
kibinadamu haliwezi kumfunika mwanadamu huyo na kupenya ndani ya moyo wake
isipokuwa kama anafungua akili yake na moyo wake kuipokea mionzi yake ya giza.
Malaika wa Mungu watamlinda kutokana na malaria yenye sumu ya majaribu ya yule
mwovu kila mtu atakayepaa juu kuliko nafsi yake na mambo yale yanayomzunguka
pamoja na mazingira yake, akimtazama Yesu kupitia katika kila umande na ukungu na
wingu, na kuyapenya kwa imani majaribu hayo ya giza nene mno....
Wewe ukiunganishwa na Kristo, basi, nguvu zote unazotaka utapewa. Ukikaa ndani
yake, unaweza kupigana kiume kwa kadiri unavyozidi kumwamini na kumtegemea
Bwana Yesu kama vile mtoto mdogo afanyavyo, hivyo ndivyo uwezo wako wa kuamini
utakavyozidi kuwa mkubwa. Kwa imani unasimama. Ni kwa kutumia imani tu unaweza
kuishinda nafsi yako.... Nafsi ni uwanja ambapo Shetani sikuzote anapambana nao na
kuwadhibiti wale wote anaotaka kuwadanganya na kuwashinda. Lakini kama haki ya
Kristo imefunuliwa ndani yako, basi, wewe unakuwa na nguvu. Ukiangalia mbali na
wewe mwenyewe kwa Mwokozi yule aliyesulibiwa, Bwana yule aliyefufuka na kupaa
mbinguni, ambaye, kama Mwombezi [Mtetezi] wako, anakuombea wewe, ukizishikilia
nguvu zake Kristo na ufanisi wake, hapo ndipo wewe unapoweza kushinda. ----- Letter
30, 1896.Hakuna ushindi wo wote uliopata kutokea [miongoni mwa mataifa ya dunia hii] ambao
kwa njia yo yote ile unaweza kulinganishwa na ushindi huo wa imani. Usiiachilie kamwe
imani yako. Inaweza kushinda hata ukiwa katikati ya mambo yanayokukatisha tamaa,
itakupatia ushindi juu ya ushindi. ----- Letter 111, 1902.
MAOMBI, NJIA YA KUPATIA MIBARAKA YOTE Mei 1
Na yo yote mtakayoyaomba katika sala mkiamini, mtapokea. Mathayo 21:22.
Maombi ni pumzi ya mtu, ni njia ya kupatia mibaraka yote. Pamoja na kuyatambua
mahitaji ya wanadamu na kuwa na hisia ya kujichukia mwenyewe, mtu yule anayetubu
anaomba sala zake, Mungu anaona jitihada yake, anayaona mapambano yake, na
kuangalia kwa makini unyofu wake. Kidole chake [Mungu] kinagusa mapigo yake, na
kuangalia kwa makini kila pigo la moyo wake. Hakuna hisia yo yote inayousisimua moyo
wake [mtu huyo], hakuna hisia yo yote inayoufadhaisha moyo wake, hakuna huzuni yo
yote inayoutia kivuli, hakuna dhambi yo yote inayoutia waa, hakuna wazo lo lote wala
kusudi lo lote linalougusa [moyo wake] ambalo Yeye [Mungu] halijui. Mtu huyo
alinunuliwa kwa gharama isiyopimika, naye anapendwa [na Mungu] kwa mapenzi
yasiyoneneka....
Kristo Mwokozi wetu.... alikuwa na mahitaji ya kimwili yaliyohitaji kutoshelezwa,
uchovu wa mwili uliohitaji kuburudishwa. Ilikuwa ni kwa njia ya maombi kwa Baba
yake aliweza kutiwa nguvu kufanya kazi yake na kuyakabili maonjo. Siku kwa siku
alizunguka huku na huku kufanya kazi yake, akitafuta kuziokoa roho za watu. Moyowake uliwahurumia waliochoka na kulemewa na mizigo mizito. Naye alitumia usiku
kucha [mara nyingi] katika maombi kwa ajili ya wale wanaojaribiwa....
Mkristo amepewa mwaliko kupeleka mizigo yake kwa Mungu kwa njia ya maombi, na
kujishikamanisha kwa karibu sana na Kristo kwa kamba zile za imani iliyo hai. Bwana
anatuamuru, akitutangazia kwamba atayasikia maombi ya wale wanaoitegemea nguvu
yake isiyo na kikomo. Ataheshimiwa na wale wanaomkaribia yeye, wanaofanya kazi
yake kwa uaminifu. "Utamlinda yeye ambaye moyo wake umekutegemea katika amani
kamilifu, kwa kuwa anakutumaini." Isaya 26:3. Mkono wa Mungu Mwenye nguvu zote
umenyoshwa kutushauri sisi na kutuongoza mbele na mbele zaidi. Endelea mbele, Bwana
asema; Nalijua shauri lako, nami nitakupa msaada wangu. Endelea kuomba. Uwe na
imani nami. Ni kwa utukufu wa jina langu wewe unaomba, nawe utapokea.
Nitaheshimiwa mbele zao wale wanaokuangalia kwa madhumuni ya kukukosoa kwa
sababu ya kushindwa kwako. Wataiona ile kweli na kushangilia kwa utukufu. "Na yo
yote mtakayoyaomba katika sala mkiamini, mtapokea."...
Imani ya kweli, maombi ya kweli ----- yana nguvu jinsi gani! ----- RH, Okt.30, 1900.
MLANGO WAZI KWENDA KWENYE KITI CHA ENZI CHA MUNGU Mei 2
Tazama, nimekupa mlango uliofunguliwa mbele yako, ambao hapana awezaye
kuufunga.
Ufunuo 3:8.
Shahidi wa Kweli anatangaza hivi: "Tazama, nimekupa mlango uliofunguliwa mbele
yako." Hebu na tumshukuru Mungu kwa moyo wetu na kwa roho zetu na kwa sauti zetu;
hebu na tujifunze namna ya kumkaribia yeye kwa kupitia kwenye mlango huo
uliofunguliwa, tukisadiki kwamba tunaweza kumwendea kwa uhuru pamoja na dua zetu,
na ya kwamba atatusikia. Ni kwa njia ya imani iliyo hai katika uwezo wake wa
kutusaidia, ndipo tutapata nguvu za kupiga vita yake Bwana kwa imani kwamba
tutakuwa na hakika ya kupata ushindi. ----- 7BC 960,961. Wale wanaojaribu kuwa
waaminifu kwa Mungu wanaweza kunyimwa haki nyingi za ulimwengu huu; njia yao
inaweza kuwekewa vipingamizi na kazi yao kuzuiwa na maadui wa ile kweli, lakini
hakuna uwezo wo wote unaoweza kufunga mlango huo wa mawasiliano kati ya Mungu
na roho zao. Mkristo mwenyewe anaweza kufunga mlango huo kwa kujifurahisha katikadhambi, au kwa kuikataa nuru ile ya mbinguni. Anaweza kukataa kuusikia ujumbe wa ile
kweli, na kwa njia hiyo kukata kiungo kati ya Mungu na roho yake.... Kila siku tunayo
haki ya thamani ya kujiunganisha wenyewe na Kristo, ambaye ameweka mbele yetu
mlango huo ulio wazi. Mbingu yote iko chini ya amri yetu. Kama sisi tu watoto wa
Mungu watiifu, basi, kila siku tunaweza kuchota akiba hiyo ya neema. Haidhuru ni
majaribu, maonjo, au mateso ya aina gani yanaweza kuja juu yetu, hatuna haja ya kukata
tamaa. Si mwanadamu wala Shetani awezaye kuufunga mlango huo ambao Kristo
ametufungulia.
Wakati wo wote tunapojaribiwa, tunao mlango huo ulio wazi, kuutazama. Hakuna
mamlaka yo yote iwezayo kuificha kwetu nuru ile ya utukufu ambayo inaangaza kutoka
kwenye lango lile la mbinguni kwa urefu wake wote wa ngazi hiyo ambayo tunapaswa
kuipanda; kwa maana Bwana ametugawia nguvu zetu kutoka katika nguvu zake, ujasiri
wetu kutoka katika ujasiri wake, nuru yetu kutoka katika nuru yake. Nguvu za giza
zinaposhindwa, nuru ya utukufu inapoigharikisha dunia yote, hapo ndipo sisi tutakapoona
na kuelewa kwa wazi zaidi kuliko tunavyofanya sasa. Laiti kama tungalitambua kwamba
utukufu wa Mungu umetuzunguka, kwamba mbingu i karibu zaidi na dunia hii kuliko
tunavyodhani, basi, tungejitahidi kuwa na mbingu nyumbani mwetu wakati tunajiandaa
kwa mbingu ile iliyo juu. ----- 7BC 961.
MIBARAKA KWA WALE WAIOMBAO Mei 3
Wala hamna kitu kwa kuwa hamwombi! Yakobo 4:2.
Hatuwezi kuishi bila kuwa na neema yake Kristo. Yatupasa kupata msaada kutoka juu
endapo tutaweza kuyapinga majaribu mengi ya Shetani, na kuzikwepa hila zake. Katikati
ya giza lililopo, yatupasa kuwa na nuru toka kwa Mungu kutuonyesha hila na mitego ya
makosa inayofyatuka yenyewe, vinginevyo tutanaswa. Yatupasa kuitumia vizuri nafasi
ya maombi, kwa faragha na kwenye madhabahu ya familia. Wengi wanahitaji kujifunza
jinsi ya kuomba.... Kama kwa unyenyekevu tunamwambia Bwana haja zetu, basi, Roho
mwenyewe anatuombea; hisia zetu za mahitaji zinatufanya kuufunua wazi moyo wetu
mbele ya jicho lile linalochunguza yote la Mwenyezi, maombi yetu yanayotolewa kwa
bidii huingia ndani ya lile pazia, imani yetu huzidai ahadi zake Mungu, na msaada huja
kwetu....Maombi ni wajibu tena ni haki. Yatupasa kuupata msaada ambao ni Mungu peke yake
awezaye kutupa, na msaada huo hauwezi kuja kwetu pasipo sisi kuuomba. Kama sisi
tunajivuna sana kwamba tuna haki yetu wenyewe kiasi cha kutoweza kuisikia haja yetu
ya kupata msaada toka kwa Mungu, basi, hatutapata msaada wake wakati ule
tutakapouhitaji sana. Kama tunajitegemea sana na kujitosheleza wenyewe kiasi cha
kutojitupa chini wenyewe na kuomba kwa bidii kila siku juu ya wema wake Mwokozi
yule aliyesulibiwa na kupaa juu, basi, tutaachwa kupatwa mara kwa mara na majaribu ya
Shetani.... Maombi... ya bidii, ya kweli... yangeweza kutuletea nguvu na neema kuweza
kuzipinga nguvu za giza. Mungu anataka kutubariki. Yu tayari sana kuwapa Roho wake
Mtakatifu wale wamwombao kuliko wazazi walivyo tayari kuwapa vipawa vyema watoto
wao. Lakini wengi hawaioni haja yao. Hawatambui kwamba hawawezi kufanya lo lote
pasipokuwa na msaada huo wa Yesu....
Nimeonyeshwa ya kwamba malaika wa Mungu wote wako tayari kuwagawia neema na
nguvu wale wanaojisikia kuwa wanayo haja ya kupata nguvu ya Mungu. Lakini wajumbe
hao wa mbinguni hawatatoa mibaraka hiyo isipokuwa kama wameombwa. Wamengojea
kilio kutoka kwa watu wale wenye njaa na kiu ya kupata mbaraka wa Mungu; mara
nyingi wamengojea bure. Naam, palikuwa na maombi ya kawaida tu, bali si dua zile
zilizotolewa kwa bidii kutoka katika mioyo minyenyekevu, iliyotubu....
Wale ambao wangetaka kuupokea mbaraka wa Bwana, hawana budi wao wenyewe
kutayarisha njia, kwa maungamo ya dhambi, kwa kujinyenyekeza mbele zake Mungu,
kwa toba ya kweli, na kwa imani katika wema wa damu yake Kristo. ----- RH, Machi 26,
1889.
JIFUNZE JINSI YA KUOMBA Mei 4
Bwana, tufundishe sisi kusali. Luka 11:1.
Kristo hakuitoa sala hiyo [Sala ya Bwana, Luka 11:2-4] ili wanadamu wapate kuikariri
kama mtindo fulani wa ibada. Aliitoa kama kielelezo cha jinsi sala zetu zinavyopaswa
kuwa ----- rahisi, za dhati, na zenye kuwa na mambo yote [tunayohitaji] ndani yake. -----
MS 23, 1899.
Sala nyingi zinatolewa pasipokuwa na imani. Mtindo fulani wa maneno unatumika,
lakini hali halisi ya kuomba kwa kumsihi sana [Mungu] huwa haipo. Sala hizo ni zamashaka, zinasitasita; haziwaletei msaada wo wote wale wanaozitoa, wala haziwaletei
wengine faraja yo yote, wala tumaini lo lote. Mtindo ule ule wa sala unatumika, lakini
moyo haumo ndani yake, ikionyesha kwamba yule mwenye kutoa dua hiyo haioni haja
yake aliyo nayo....
Jifunze kuomba kwa kifupi na kwa kuigusia haja ile ile uliyo nayo, ukiomba kitu kile tu
unachokihitaji. Jifunze kuomba kwa sauti kubwa mahali pale ambapo Mungu anaweza
kukusikia. Usitoe maombi ya kinafiki, bali dua zako uzitoe kwa bidii, kwa kujisikia,
ukionyesha njaa yako ya kiroho kwa ajili ya Mkate wa Uzima. Kama tungeomba zaidi
katika faragha [peke yetu], tungeweza kuomba kwa akili zaidi hadharani. Maombi
yaliyojaa mashaka, maombi ya kusitasita, yangekoma. Na wakati ule ambapo sisi
tungeshirikiana na ndugu zetu katika ibada, tungeweza kuongeza furaha ya mkutano huo;
maana tungeweza kuleta pamoja nasi baadhi ya mvuto ule wa mbinguni, na ibada yetu
ingekuwa ya kweli, na sio ya mtindo tu.... Kama moyo hauvutwi kuomba katika chumba
chako cha siri na wakati ule unapofanya kazi yako ya kila siku, basi, hali hiyo
itajidhihirisha katika mkutano wa maombi....
Uhai wa kiroho unategemea mazoea ya kuzungumza na Mungu. Haja zake zinajulikana,
na moyo unakuwa wazi kupokea mibaraka mipya. Shukrani inatoka katika midomo ya
kweli; na nyakati za kuburudishwa [Roho Mtakatifu] zinazopokewa kutoka kwa Yesu
zinadhihirishwa katika maneno, katika matendo ya ukarimu halisi, na katika ibada ya
pamoja. Upendo kwa Yesu unakuwamo moyoni; na mahali ulipo upendo huo, hauwezi
kuzuiwa, bali utajidhihirisha wenyewe. Maombi ya siri [faragha] yataimarisha maisha ya
ndani. Moyo unaompenda Mungu utatamani kuongea naye, nao utamtegemea kwa
tumaini takatifu.
Hebu na tujifunze kuomba kwa akili, tukitaja dua zetu kwa wazi na usahihi. Hebu na ...
tuombe kana kwamba tuna maana hasa na kile tunachokiomba. "Kuomba kwake mwenye
haki kwafaa sana, akiomba kwa badii." Yakobo 5:16. ----- RH, Aprili 22, 1884.
MTAFUTE MUNGU KWA MOYO WOTE Mei 5
Irudieni ngome, enyi wafungwa wa tumaini; hata hivi leo nasema ya kwamba
nitakurudishia maradufu. Zekaria 9:12.Tunahitaji kuufunza moyo wetu kuzishika, na kuzishikilia sana ahadi nyingi za Kristo.
Bwana Yesu anajua kwamba haiwezekani kwetu sisi kuyapinga majaribu mengi ya
Shetani, ni pale tu tutakapokuwa na uwezo tutakaopewa na Mungu ndipo tutakapoweza.
Anajua vizuri kwamba kwa nguvu zetu wenyewe za kibinadamu tungeweza kushindwa
kabisa. Kwa hiyo amefanya maandalizi yote ili katika kila wakati wa hatari na maonjo
tupate kukimbilia kwenye Ngome yetu.... Tunalo neno la ahadi litokalo katika midomo
ile isiyoweza kusema uongo.... Tunapaswa kila mmoja wetu kuihifadhi imani ile
inayosadiki kwamba tunapokea kwake mambo yale aliyoahidi.
Kwetu Mungu atakuwa kila kitu sawasawa na vile sisi tutakavyomruhusu kuwa. Sala
zetu dhaifu, zisizotolewa kwa moyo wote hazitatuletea sisi matokeo yo yote kutoka
mbinguni. Oo! tunahitaji kuzitilia mkazo sana dua zetu! Omba kwa imani, pokea kwa
imani, furahi katika tumaini hilo, maana kila atafutaye ataona. Uwe na bidii katika jambo
hili. Mtafute Mungu kwa moyo wote. Watu huweka moyo wao wote pamoja na juhudi
yao katika kila kitu wanachofanya katika mambo ya ulimwengu huu, mpaka juhudi zao
zitunukiwe na mafanikio. Kwa juhudi kubwa jifunze mbinu ya kuitafuta mibaraka tele
aliyoiahidi Mungu, na kwa kustahimili na kuwa na juhudi thabiti utapata nuru yake na
kweli yake na neema yake nyingi. ----- MS 39, 1893.
Kwa unyofu wa moyo, ukiwa na njaa yako ya kiroho, mlilie sana Bwana. Pigana
mweleka na wajumbe wale wa mbinguni mpaka umepata ushindi. Weka mwili wako
wote mikononi mwake Bwana, yaani, roho yako, mwili wako, na nafsi yako, na kuazimia
ya kwamba utakuwa mjumbe wake mwenye upendo, aliyejitoa wakf, ukiongozwa na
mapenzi yake, ukitawaliwa na nia yake, na kujazwa na Roho wake. ----- SD 105.
Mweleze Yesu mahitaji yako kwa unyofu wa moyo. Hutakiwi kuwa na mabishano
marefu na Mungu au kutoa hotuba kwake, bali kwa moyo wenye huzuni kwa ajili ya
dhambi zako, sema, "Niokoe, Bwana, la sivyo, naangamia." Liko tumaini kwa mioyo
kama hiyo. Watamtafuta, watamwomba, watabisha, nao watapata. Yesu anapouondoa
mzigo wa dhambi unaoukandamiza moyo wako, utajisikia furaha inayotokana na amani
yake Kristo. ----- MS 29, 1896.
USHINDI KWA NJIA YA KUKESHA Mei 6
Kesheni mwombe, msije mkaingia majaribuni. Marko 14:38.
Majaribu yanaweza kukuzunguka kila upande, lakini wewe u salama kwa kadiri
usivyojiingiza katika hayo. Wengi wetu tunashindwa na Shetani kwa sababu tunajiingiza
ndani ya majaribu hayo.... Ni kazi yako kujitenga na kila mmoja na kila kitu chenye
mwelekeo wa kukuongoza mbali na wajibu wako na kuugeuza moyo wako kutoka kwa
Mungu.... Ukilazimika kuwa katika jamii ya wale walio waovu, hushurutishwi kuingia au
kushiriki katika maovu yao. Kwa kuomba na kukesha, unaweza kubaki bila kutiwa waa
kutokana na maovu yanayoonekana yanayokuzunguka wewe. ----- Letter 16, 1867.
"Kesheni mwombe" ni agizo linalorudiwa mara nyingi katika Maandiko. Katika maisha
ya wale wanaolitii agizo hilo patakuwa na mkondo usioonekana wa furaha ambao
utawabariki wote wanaokutana nao. Wale ambao ni wachungu na wakali katika tabia zao
watageuka na kuwa wazuri na wapole; wale ambao wana kiburi watakuwa wapole na
wanyenyekevu wa moyo. ----- MS 42, 1904.
Mtu hawezi kuwa Mkristo mwenye furaha isipokuwa kama ni Mkristo anayekesha. Yule
ashindaye hana budi kukesha; maana kwa njia ya kujifungamanisha na mambo ya dunia
hii, makosa yake, na ushirikina wake, Shetani anajitahidi kuwashawishi wafuasi wa
Kristo kutoka kwake, na kuiweka mioyo yao iwe inashughulika na hila zake. Haitoshi
kwamba tuziepuke hatari za waziwazi na hatua zile zinazoweza kuleta maangamizi
ambazo hazifuati utaratibu. Yatupasa kuwa karibu sana upande wake Kristo, tukitembea
katika njia ile ya kujikana nafsi na kujitoa mhanga. Hatupaswi kuacha fahamu zetu za
kiroho kupofushwa, kama mara nyingi zinavyokuwa, tuwe na nia yenye nguvu, yaani, nia
iliyo thabiti. Na ili kugundua hila za Shetani na kupinga mashambulio yake
yasiyotarajiwa, yatupasa kuwa na neema yake Kristo na kupewa Roho wake....
Neno la Mungu linatuonya sisi kwamba tunao maadui wengi, sio wale wa wazi, wala
wale wanaojitangaza wenyewe hadharani, bali ni maadui wale wanaotujia wakiwa na
maneno laini na hotuba nzuri, na wale ambao wangeweza kuwadanganya yamkini hata
walio wateule. Hivyo ndivyo Shetani anavyokuja kwetu. Na tena, inapofaa kwa kusudi
lake, anazunguka-zunguka huku na huko kama simba angurumaye, akitafuta mtu wa
kummeza. Mapenzi ya mwanadamu, isipokuwa kama yamewekwa chini ya mapenzi ya
Mungu, mara kwa mara yako upande wa yule adui kama vile yanavyoweza kuwa upande
wake Bwana. Kwa hiyo Kesheni mwombe; kesheni na kuomba sikuzote. ----- Letter 5,
1903.MAOMBI YA UNYENYEKEVU BILA KUKOMA Mei 7
Elia alikuwa mwanadamu mwenye tabia moja na sisi, akaomba kwa bidii mvua
isinyeshe, na mvua haikunyesha juu ya nchi muda wa miaka mitatu na miezi sita.
Akaomba tena, mbingu zikatoa mvua, nayo nchi ikazaa matunda yake. Yakobo 5:17,18.
Mafundisho muhimu yameletwa kwetu katika uzoefu wa Eliya. Alipokuwa juu ya mlima
ule wa Karmeli aliomba kwa ajili ya mvua [ipate kunyesha], imani yake ilijaribiwa, lakini
aliendelea kumjulisha Mungu juu ya ombi lake. ----- 2BC 1034.
Mtumishi alienda kuangalia wakati Eliya alipoendelea kuomba. Mara sita alirudi kutoka
mahali pake pa kuangalia, akisema, Hakuna kitu cho chote, wala wingu, wala dalili ya
mvua.... Lakini nabii yule hakuacha kuomba kwa kukatishwa tamaa. Aliendelea
kuyachunguza maisha yake kuona ni wapi alikuwa ameshindwa kumheshimu Mungu....
Alipouchunguza moyo wake, alionekana kuwa anapungua na kupungua, katika maoni
yake mwenyewe na machoni pake Mungu. Kwake ilionekana ya kwamba yeye alikuwa si
kitu, na ya kwamba Mungu ni kila kitu; naye alipofikia mahali pa kuikana nafsi yake,
huku akiwa amemshikilia Mwokozi wake kama ndiye pekee nguvu na haki yake, hapo
ndipo jibu likaja. Mtumishi akaja, na kusema, "Tazama, wingu linatoka katika bahari,
nalo ni dogo kama mkono wa mtu." 1 Wafalme 18:44. -----
2BC 1035.
Tunaye Mungu ambaye sikio lake halijazibwa hata asiweze kuzisikia dua zetu; na kama
tutalijaribu neno lake, ataiheshimu imani yetu. Anataka mambo yetu yote tuyapendayo
yaunganishwe na mambo ayapendaye yeye, hapo ndipo anaweza kutubariki kwa
usalama; maana hapo hatutajichukulia utukufu sisi wenyewe mbaraka huo utakapokuwa
wetu, bali tutampa sifa zote Mungu. Mungu hajibu maombi yetu siku zote mara ile ya
kwanza tunapomwita; maana kama angefanya hivyo, basi, sisi tungeyachukulia mambo
kijuu juu tu na kudhani tulikuwa na haki ya kupewa mibaraka yote hiyo pamoja na
upendeleo wake ambao ametupa sisi. Badala ya kujichunguza mioyo yetu kuona kama
uovu wo wote tulikuwa tumeutunza moyoni, yaani, kama tulikuwa tumetenda dhambi yo
yote, sisi tungekuwa wazembe, na kushindwa kutambua tegemeo letu juu yake....
Eliya alijinyenyekeza mwenyewe mpaka akafikia hali ambayo asingeweza kujichukulia
utukufu yeye mwenyewe. Hii ndiyo hali ambayo kwayo Bwana anasikia maombi yetu,
maana hapo ndipo tunaweza kumpa yeye sifa.... Ni Mungu peke yake anayestahili
kutukuzwa. -----
2BC 1034. NGOJEA JIBU LA MUNGU Mei 8
Ni vema mtu autarajie wokovu wa BWANA Na kumngojea kwa utulivu.
Maombolezo 3:26.
Kuna ahadi za thamani katika Maandiko kwa wale wanaomngojea Bwana. Sisi sote
tunatamani kupata jibu la papo hapo kwa maombi yetu, nasi tunajaribiwa kukata tamaa
kama maombi yetu hayajibiwi mara moja. Sasa uzoefu wangu umenifundisha kwamba
hilo ni kosa kubwa. Kuchelewesha majibu ni kwa faida yetu maalum. Imani yetu inapewa
nafasi ya kujaribiwa kuona kama ni ya kweli, nyofu, au haibadilikibadiliki kama
mawimbi ya bahari. Yatupasa kujifunga sisi wenyewe juu ya madhabahu kwa kamba
zenye nguvu za imani na upendo, na kuiacha saburi yetu iwe na kazi yake kamilifu.
Imani inapata nguvu kwa kuitumia daima. ----- Letter 37, 1892.
Yatupasa kuomba zaidi na kwa imani. Hatupaswi kuomba na halafu kukimbia kwenda
mbali kana kwamba tulikuwa tunaogopa kupata jibu. Mungu hatatudhihaki sisi. Atatujibu
kama tunakesha na kuomba, kama tunaamini kwamba tunapokea vitu vile
tulivyomwomba, na kuendelea kuamini na kutopoteza saburi yetu katika kuamini. Huko
ndiko kukesha na kuomba. Tunayalinda maombi yetu ya imani kwa kuwa na matarajio na
matumaini. Yatupasa kuyazungushia ukuta kwa njia ya kuwa na hakika, wala tusiwe
watu wasio na imani, bali tuwe watu wanaoamini. Maombi ya bidii ya mwenye haki
hayapotei kamwe. Huenda jibu lisije kama tulivyotarajia, lakini litakuja, kwa sababu
neno la Mungu limeahidi hivyo. ----- Letter 26, 1880.
Tunahitaji utulivu wa kumngojea Bwana. Hitaji la hali hiyo ni sharti mojawapo. Si
makelele wala kushughulika sana duniani humu kunakothibitisha kufaa kwetu. Angalia
jinsi Mungu anavyofanya kazi yake kwa kimya!... Wale wanaotaka kutenda kazi pamoja
na Mungu wana haja ya kuwa na Roho wake kila siku; wanahitaji kuenenda na kufanya
kazi kwa upole na unyenyekevu wa moyo, bila kutafuta kufanya mambo ya ajabu,
wakiridhika kufanya kazi iliyo mbele yao na kuifanya kwa uaminifu. Watu huenda
wasiweze kuziona wala kuzithamini juhudi zao, lakini majina ya watoto hao wa Mungu
walio waaminifu yanaandikwa mbinguni miongoni mwa watenda kazi wake walio bora
sana, kama wapandaji wa mbegu kwa matazamio ya mavuno yale yenye utukufu. -----
4BC 1144.Mngojee Bwana, si kwa kusumbuka kunakoletwa na wasiwasi, bali kwa imani isiyojua
hofu, na tumaini lisilotikisika. ----- Letter 66, 1901.
MAKUMBUSHO NDANI YA KUMBI ZA KUMBUKUMBU Mei 9
Ndipo Samweli akatwaa jiwe, na kulisimamisha kati ya Mispa na Sheni, akaliita jina
lake
Eben-ezeri, akisema, Hata sasa BWANA ametusaidia. 1 Samweli 7:12.
Kwetu kuna kutiwa moyo sana katika mbaraka ulio mdogo kabisa tunaoupokea sisi
wenyewe kuliko katika kusoma vitabu vya historia ya maisha ya watu wengine kuhusu
imani na uzoefu wa watu maarufu wa Mungu. Mambo yale ambayo sisi wenyewe
tumeyapitia kuhusu mibaraka ya Mungu kwa njia ya ahadi zake nyingi tunaweza
kuyatundika ndani ya kumbi za kumbukumbu zetu, haidhuru tuwe matajiri au maskini,
wasomi au wasiojua kusoma na kuandika, tunaweza kuziangalia na kuzitafakari ishara
hizo za upendo wa Mungu kwetu. Kila ishara ya utunzaji wa Mungu na fadhili zake
pamoja na rehema zake, mambo hayo yangetundikwa ndani ya kumbi za kumbukumbu
zetu kama makumbusho yasiyoweza kuharibika. Mungu angependa upendo wake, na
ahadi zake, viandikwe katika vibao vya mioyo yetu. Hifadhi mafunuo ya thamani ya
Mungu ili hata herufi moja isipate kufutika, wala kufifia.
Israeli walipopata ushindi maalum baada ya kutoka Misri, kumbukumbu ziliwekwa za
ushindi huo. Musa na Yoshua waliagizwa na Mungu kufanya hivyo, kujenga ukumbusho.
Waisraeli walipopata ushindi maalum juu ya Wafilisti, Samweli aliweka jiwe la
ukumbusho na kuliita Eben-ezeri, akisema, "Hata sasa BWANA ametusaidia."...
Tunapoyaangalia yaliyopita, je! hatuwezi kuyaangalia maonjo mapya na matatizo
yanayozidi kuongezeka ----- hata mateso, ufukara, na misiba ----- bila kuvunjika moyo,
na kutazama wakati uliopita, na kusema, "'Hata sasa BWANA ametusaidia.' Nitakabidhi
utunzaji wa nafsi yangu kwake Yeye kama Muumbaji mwaminifu. Atakilinda kile
nilichokiweka amana kwake hadi siku ile."----- MS 22, 1889.
Hebu na tuziangalie nguzo za ukumbusho, zinazotukumbusha kile Bwana alichotufanyia
sisi ili kutufariji na kutuokoa kutoka mkononi mwa yule mharabu [mwangamizaji]. Hebuna tuzikumbuke upya katika kumbukumbu zetu fadhili zake Mungu alizotuonyesha -----
machozi yetu aliyoyafuta, maumivu yetu aliyoyatuliza, wasiwasi wetu aliotuondolea,
hofu zetu alizozifukuzilia mbali, mahitaji yetu aliyotupatia, mibaraka yake aliyotupa -----
kwa njia hiyo tunaweza kujitia nguvu sisi wenyewe kuweza kuyakabili yale yote yaliyo
mbele yetu katika safari yetu yote iliyobaki. ----- SC 125.
MLIMANI MBELE ZA BWANA Mei 10
Akasema, Toka, usimame mlimani mbele za BWANA. 1 Wafalme 19:11.
Amri hiyo huja kwa kila mmoja wetu anayekuangalia kukata tamaa kwake na
kuomboleza juu ya udhaifu wake na [kwa njia hiyo] kuupa ulimwengu kielelezo cha
kutomtumainia Mungu, yaani, kukataa kutazama na kuishi.... Unamfurahisha yule adui
wa Mungu na wa mwanadamu kwa kuishi katika pango lako lenye giza ambamo hakuna
hata mwonzi mmoja wa Nuru ile ya uzima....
Nataka kupaza sauti yangu kwa niaba ya Yesu na kusema, Ye yote amwaminiye
hatapotea [hataangamia], bali atakuwa na uzima wa milele. Toka nje ya pango hilo kwa
imani. Mtazame Yesu, msaidizi wako. Mtazame Mwana-Kondoo wa Mungu, achukuaye
dhambi ya ulimwengu! Mtazame yeye aliye Kafara yako ya upatanisho akiwa
ameinuliwa juu ya msalaba, Asiye na dhambi akiwafia wenye dhambi.....
Toleo lake mwenyewe lilikuwa kamilifu na la kutosha. Hakuna kilichopungua. Kwa
kweli ule ulikuwa ni upatanisho kamili na wa kutosha uliofanywa pale [Kalvari]. Basi,
kwa nini... wewe uonyeshe kwa maneno yako na mfano wako ya kuwa Kristo alikufa
bure kwa ajili yako? Baada ya yeye kuudhihirisha upendo wake kwako ambao haukuwa
na mfano, wewe kwa maneno yako yaliyojaa mashaka na kukata tamaa kunakosikitisha
sana, unasema, "Hanipendi mimi. Hatanisamehe mimi. Dhambi zangu ni za aina ile iliyo
ngumu mno kuweza kutibiwa kwa damu ya Yesu. Toleo lile halina thamani ya kutosha
kulilipa deni lile ninalodaiwa kwa ajili ya kuiokoa nafsi yangu."
Laiti kama wanaume na wanawake wangeweza kuona tu na kutambua jinsi kutokuamini
kwao na manung'uniko yao yaliyojaa maombolezo yanavyomtukuza na kumpa heshima
Shetani, na wakati uo huo yakiwa yanamnyang'anya Kristo utukufu wake katika kazi
yake ya kuwaokoa wao, kabisa kabisa, na kwa ukamilifu kutoka katika dhambi zao
zote!... Hebu na tutoke nje katika pango letu lenye giza. Hebu na tuzifunze akili zetukupambanua kile ambacho Yesu amekuwa kwetu sisi. Hebu na tuifundishe mioyo yetu
kusimama mlimani mbele za Mungu kwa imani, tukiwa na nguvu katika Mungu chini ya
kila namna ya majaribu....
Mlimani tutamwona vizuri Yesu. Shetani hatakuwa na uwezo wa kututupia kivuli chake
cha kishetani kuingia kati ya roho zetu na Yesu, na kutuzuia tusimwone Yesu, na
kumfanya aonekane kwetu kama mwongo, na kuitia nguvu mioyo yetu kuwa na mashaka
ya kikatili sana juu ya fadhili zake, rehema zake, na upendo wake [Yesu] ambao kwa huo
yeye ametupenda sisi. ----- MS 42, 1890.
SHERIA YA MUNGU NI UKUTA UNAOTULINDA Mei 11
Heri walio kamili njia zao, Waendao katika sheria ya BWANA. Zaburi 119:1.
Mungu, mtawala mkuu wa ulimwengu, amekiweka kila kitu chini ya sheria. Ua dogo
sana na mwaloni mrefu sana, punje ya mchanga na bahari kuu, mwangaza wa jua na
manyunyu, upepo na mvua, vyote hivyo hutii sheria za maumbile yao. Lakini
mwanadamu amewekwa chini ya Sheria ya juu zaidi. Amepewa akili kuyaona, na
dhamiri ya kuhisi, madai yale yenye nguvu ya Sheria kuu ya Mungu [Amri Kumi] ya
Maadili, yaani, sura ya kile anachotaka watoto wake
kuwa.
Mungu ametujulisha mapenzi yake kwa wazi sana hata hawezi kuwako mtu wa kukosea.
Anataka wote waijue vizuri sana Sheria yake, wausikie uwezo wa kanuni zake [maishani
mwao]; kwa maana mambo yao ya milele yanahusika hapo. Yule aliye na ufahamu wa
madai mapana mno ya Sheria ya Mungu anaweza kujua kitu fulani kuhusu dhambi ilivyo
ya kuchukiza mno. Na kadiri mawazo yake yanavyokuwa ya juu zaidi kuhusu matakwa
hayo ya Mungu, ndivyo kadiri shukrani zake kwa msamaha aliopewa zitakavyozidi....
Kwa nguvu zake mwenyewe mwenye dhambi hawezi kutimiza madai yote ya Mungu.
Yampasa kwenda kuomba msaada kwa yule Mmoja aliyelipa fidia kwa ajili yake....
Kristo ndiye tumaini letu. Wale wanaomtumainia wanatakaswa. Neema yake Kristo
[kwa njia ya injili] na serikali yake Mungu [kwa njia ya Amri Kumi] hwenda bega kwa
bega kwa mwafaka ulio mkamilifu. Yesu alipokuwa Badala yake mwanadamu, rehema
na kweli vilikutana, na haki na amani vikabusiana [pale msalabani]. Msalaba wa Kalvari
unashuhudia madai ya hali ya juu ya Sheria ya Mungu. ----- ST, Julai 31, 1901.Sheria ya Amri Kumi isiangaliwe zaidi kwa upande wake wa kukataza, bali iangaliwe
zaidi kwa upande wake wa rehema. Makatazo yake ni uthibitisho wa hakika [kwa
mwanadamu] wa furaha inayopatikana kwa utii. Ikipokewa ndani yake Kristo, inafanya
ndani yetu utakatifu wa tabia yetu ambao utatuletea sisi furaha kwa milele zote. Kwa
watiifu ni ukuta unaowalinda. Tunaona wema wa Mungu ndani yake, ambaye kwa
kuwaonyesha wanadamu kanuni hizo za haki zisizobadilika kamwe, anajaribu kuwalinda
kutoka katika maovu yanayotokana na ukiukaji wake [uvunjaji wa sheria hiyo]. ----- 1SM
235.
KANUNI KAMILIFU YA MAISHA Mei 12
Kisha Hekalu la Mungu lililoko mbinguni likafunguliwa, na sanduku la agano lake
likaonekana ndani ya hekalu lake. Ufunuo 11:19.
Mkombozi wetu anatushuhudia hivi: "Tazama, nimekupa mlango uliofunguliwa mbele
yako, ambao hapana awezaye kuufunga." Ufunuo 3:8. Kupitia katika mlango huo na
kuingia ndani ya hekalu la Mungu, tunaiona Sheria ile ya kifalme, imewekwa ndani ya
sanduku lile la agano. Kupitia katika mlango huo ulio wazi, nuru inaangaza kutoka katika
Sheria ile takatifu, ya haki na njema, ikiweka mbele ya mwanadamu kanuni ya kweli, ya
haki, ili asifanye makosa katika kujenga tabia yake ambayo itatimiza matakwa ya Mungu.
Dhambi inahukumiwa kwa Sheria ile; hatuna budi kuiweka [dhambi] mbali nasi. Kiburi
na uchoyo [kujipenda nafsi] haviwezi kupata nafasi katika tabia yetu bila kumfukuza nje
yule aliyekuwa mpole na mnyenyekevu wa moyo [Kristo].
Sheria ya Mungu ni kanuni ambayo kwayo tabia inapaswa kupimwa; kama tunajenga
kwa kufuata kanuni inayotufaa sisi wenyewe, na kujaribu kufuata kielelezo
tulichojiwekea wenyewe, basi, mwisho wake tutashindwa kabisa kuipata mbingu....
Moyo wetu unapaswa kuitii Sheria hiyo ya Kifalme ya Uhuru, Sheria ambayo Roho wa
Mungu anaiandika moyoni mwetu, na kuifanya ieleweke wazi kwa ufahamu wetu.
Kuifukuza dhambi ni lazima iwe kazi ya mtu mwenyewe, kwa kuzitumia nguvu zake
bora. Uhuru pekee wa nia ya mwanadamu anaoweza kuufurahia, unapatikana kwa
kuafikiana na mapenzi ya Mungu, yaani, kutimiza masharti yanayomfanya mtu kuwa
mshirika wa tabia ile ya uungu. -----
RH, Nov. 24, 1885.Sheria ya Mungu iliyotolewa pale Sinai [Amri Kumi] ni nakala ya mapenzi na nia ya
Mungu wa milele. Inaheshimiwa kwa utakatifu wake na malaika wale watakatifu. Utii
kwa matakwa yake, utaikamilisha tabia ya Kikristo, na kumwezesha mwanadamu, kwa
njia yake Kristo, kuirudia hali yake aliyokuwa nayo kabla ya Anguko lile. Dhambi
zilizokatazwa katika Sheria hiyo zisingeweza kupata nafasi ya kuingia mbinguni.
Ulikuwa ni upendo wake Mungu kwa mwanadamu uliomsukuma kuonyesha mapenzi
yake katika Amri zile Kumi za Sheria yake [Amri Kumi Asilia zimo katika sanduku la
agano mbinguni].... Mungu amempa mwanadamu kanuni kamilifu ya maisha katika
Sheria yake. Ikitiiwa, ataishi kwayo, kwa njia ya wema wake Kristo. Ikivunjwa, inao
uwezo wa kumhukumu mtu. Sheria hiyo inawatuma watu kwa Kristo [anayewatakasa
dhambi zao zilizotokana na kuivunja Sheria hiyo], naye Kristo anawarudisha tena
kwenye Sheria hiyo [ili waendelee kuishi kwayo kwa neema ya Yesu]. ----- RH, Sept. 27,
1881.
KUPIMWA KATIKA MIZANI KWA AJILI YA MBINGU Mei 13
Na nipimwe katika mizani iliyo sawasawa, Ili Mungu aujue uelekevu [unyofu wa moyo]
wangu. Ayubu 31:6.
Kipimo cha kweli hupima yote. [Kipimo hicho] ni Sheria [Amri Kumi] ya Mungu hasa.
Anaiweka Sheria yake katika matendo madogo sana na mambo yote wanayotendeana
wanadamu, ili wakijifunza na kuishi kwa hiyo wapate kutukuzwa, na kuadibishwa, na
kutakaswa moyoni na katika mapenzi yao ----- wakiwa waaminifu katika mambo yaliyo
madogo sana. ----- MS 62, 1896.
Mungu anapima nia, makusudi, na tabia. Wanadamu wote wanapimwa katika mizani ile
ya patakatifu [mbinguni], na Mungu angependa wote wautambue ukweli huu. Hana
alisema, "Kwa kuwa BWANA ni Mungu wa maarifa, Na matendo hupimwa na yeye kwa
mizani." 1 Samweli 2:3. Daudi amesema, "Hakika binadamu ni ubatili, Na wenye cheo ni
uongo, katika mizani huinuka; Wote pamoja ni hafifu kuliko ubatili." Zaburi 62:9. Isaya
asema, "Wewe uliye mnyofu wainyosha [waipima kwa mizani - KJV] njia ya mwenye
haki." Isaya 26:7....Mungu wa mbinguni ni wa kweli. Hakuna nia yo yote iliyojificha ndani kabisa ya moyo
wetu, wala siri yo yote ndani yetu, wala mpango wo wote ambao Mungu haujui kwa
ukamilifu. Lakini, je! kanuni hiyo ya haki ni ipi? Ni ile Sheria ya Mungu [Amri Kumi].
Sheria ya Mungu huwekwa upande mmoja wa mizani, yaani, Sheria yake isiyobadilika
kamwe ambayo madai yake yameelezwa wazi, ikizijumuisha Amri zake nne za kwanza,
yaani, upendo mkuu kwa Mungu, na zile sita za mwisho, yaani, upendo kwa jirani
yetu[Kutoka 20:3-17]. "Mpende Bwana Mungu wako kwa moyo wako wote,... na jirani
yako kama nafsi yako." Luka 10:27. Katika kanuni hiyo hatuwezi kuondoa hata chembe
moja ndogo mno. Mungu anataka moyo wote, akili yote, roho yote, na nguvu zote, tena
anataka u"mpende jirani yako kama nafsi yako." Mambo hayo yanawekwa katika mizani
upande mmoja, ambapo tabia ya kila mtu mmoja mmoja haina budi kufaulu mtihani wa
kupimwa katika mizani upande wake wa pili. Na kwa kuilinganisha kwa haki, umilele wa
kila mwanadamu unafungwa pasipo kubadilika tena....
Je! itaandikwa kule [mbele ya jina lako], "Umepimwa katika mizani nawe umeonekana
kuwa umepunguka"? Kama utaonekana kuwa umepunguka katika siku ile ya Mungu
litakuwa ni jambo la kuogofya sana kwako, kwa hiyo tunatakiwa kuzichunguza kwa
karibu sana nia zetu pamoja na matendo yetu kwa kutumia Sheria ya Mungu [kama kioo -
Yak.1:21-25], kulitubia kila tendo la uasi, na sisi kama wenye dhambi kuushikilia sana
wema wake Kristo ili upate kutujazia upungufu wetu. Damu yake Kristo peke yake
itafanya kazi hiyo. ----- MS 65, 1886.
UTII UTOKAO MOYONI Mei 14
Wala si kwa utumwa wa macho tu kama wajipendekezao kwa wanadamu bali kama
watumwa wa Kristo, mkitenda yampendezayo Mungu kwa moyo. Waefeso 6:6.
Sheria yake Yehova ni pana mno. Yesu... alitangaza wazi kwa wanafunzi wake kwamba
Sheria hiyo takatifu ya Mungu [Amri Kumi] inaweza kuvunjwa hata kwa mawazo na
hisia na tamaa, kama vile inavyoweza kuvunjwa kwa neno na tendo. Moyo ule
unaompenda Mungu kabisa kwa vyo vyote vile hautaweza kuyapunguza kwa kiwango
cha chini kabisa madai ya amri zake, bali mtu yule aliye mtiifu, mtu mwaminifu, atatoa
utii wake wa kiroho ulio mkamilifu kwa moyo wa uchangamfu wakati Sheria hiyo
atakapoiona katika uwezo wake wa kiroho. Ndipo amri hizo zitaingia nyumbani mwake
katika moyo wake kwa nguvu yao halisi. Dhambi itaonekana kuwa ni dhambi kabisa....Hakuna tena haki yake mwenyewe, wala kujisifu, wala kujitafutia heshima yeye
mwenyewe. Kule kujiona yeye mwenyewe kuwa yuko salama kumetoweka. Kujisikia
anayo hatia ya dhambi moyoni mwake na kujichukia nafsi hayo ndiyo matokeo yake, na
mtu huyo anapohisi kwamba yu katika hali ya hatari anaishikilia sana damu ya MwanaKondoo wa Mungu kuwa ndiyo dawa yake ya pekee....
Siku hizi wengi wanajidanganya wenyewe. Wanayawekea mipaka maagizo [amri] ya
Mungu kwamba yanayahukumu matendo ya nje tu, wala hawafikiri kwamba ni dhambi
inayomwaibisha Mungu kuwa na mawazo na mapenzi machafu ndani ya mioyo yao.
Wanajigamba wenyewe ya kwamba wao wanaishika Sheria ya Yehova wakati maisha
yao na tabia yao vimepigwa picha [kama zile za mkanda wa video] katika vitabu vile vya
mbinguni mbavyo vinawaonyesha wakiwa na moyo wa ujasiri kuona kama wanaweza
kwenda mbali kiasi gani upande wa matendo mabaya pasipo kutiwa alama ya aibu kama
wavunjaji wa Sheria ya Mungu....
Kila mtu anayetaka kuachana na maovu yote... atajitahidi daima kuwa upande waBwana
kwa mawazo, maneno, na tabia yake, akiyatii matakwa yake yote. Badala ya kutafuta
nafasi ya kuikwepa Sheria ya Mungu, atakuwa anazifafanua amri zake zilizo pana sana,
naye atajitahidi kwa bidii yake yote kuzitukuza kanuni kuu za amri zake [Mungu]
takatifu.... Kazi hiyo haina budi kuanza moyoni mwake.... Moyo ukiwa sawa na Mungu,
basi, maisha yote yatakuwa safi, yataadibishwa, yatatukuzwa, na kutakaswa. Jicho
[dhamiri] likiwa safi, basi, mwili wote utajazwa na nuru. Dini si jambo la nje tu.... Dini ni
jambo la moyoni. ----- Letter 51, 1888.
KUCHANGANYA PAMOJA SHERIA NA INJILI Mei 15
Basi, je! twaibatilisha sheria kwa imani hiyo? Hasha! kinyume cha hayo twaithibitisha
sheria. Warumi 3:31.
Tunawasikia wengi waliodanganywa na yule adui wakijidai daima, wakisema,
"Nimeokoka";
lakini... wanaonyesha dharau kubwa kwa kanuni ya Mungu ya haki [Amri Kumi] kiasi
kwamba sisi tunatambua kwamba wao.... hawajui kitu kuhusu neema ile iokoayo. Moyo
wao haupatani na Sheria ya Mungu [Amri Kumi], bali una uadui na Sheria hiyo. Hivyo
ndivyo yule mwasi mkuu [Shetani] alivyokuwa kule mbinguni. Je! Mungu atawachukuawanaume na wanawake kwenda nao mbinguni ambao hawaiheshimu kabisa Sheria ya
malimwengu yake?...
Ni kitu gani kinachoweza kumfanya mwenye dhambi kuzitambua dhambi zake kama sio
kujua dhambi ni kitu gani? Tafsiri sahihi ya dhambi katika Neno la Mungu imetolewa
katika
l Yohana 3:4 (AJKK): "Dhambi ni uvunjaji wa Sheria." Mwenye dhambi sharti ajisikie
kuwa ni mvunjaji wa Sheria [Amri Kumi]. Kristo aliyekufa juu ya msalaba ule wa
Kalvari anayavuta kwake mawazo yake [yule mwenye dhambi]. Hivi kwa nini Kristo
alikufa? Kwa sababu ilikuwa ni njia peke yake kwa mwanadamu ya kuweza
kuokolewa.... Alibeba dhambi zetu zote ili apate kuwahesabia haki yake wale wote
wanaomwamini yeye.... Wema na upendo wake Mungu unamwongoza mwenye dhambi
kuwa na toba kwa Mungu na imani kwa Bwana wetu Yesu Kristo. Mwenye dhambi
aliyezinduka.... anaonyeshwa Sheria ile aliyoivunja. [Sheria hiyo] inamwita apate kutubu,
ila hakuna uwezo wa kuokoa ndani ya Sheria hiyo ili kuweza kusamehe uvunjaji huo wa
Sheria, na shauri lake [mwenye dhambi huyo] huonekana kuwa halina matumaini yo
yote. Lakini Sheria inamvuta na kumpeleka kwa Kristo. Haidhuru dhambi zake ziwe na
kina kirefu jinsi gani, damu ya Yesu Kristo inaweza kumsafisha na udhalimu huo wote....
Sheria na Injili vinakwenda bega kwa bega. Moja inaikamilisha ile nyingine. Sheria
pasipo imani katika injili yake Kristo haiwezi kumwokoa mvunjaji wa Sheria hiyo. Injili
pasipo Sheria haifai kitu wala haina uwezo wo wote. Sheria na injili ni kitu kizima
kimoja kilicho kikamilifu. Bwana Yesu aliweka msingi wa jengo, naye analiweka lile
"Jiwe la kuwekwa juu kabisa pamoja na vigelegele vya, Neema, neema, ilikalie." Zekaria
4:7. Yeye ndiye mwenye kuanzisha na mwenye kutimiza imani yetu, Alfa na Omega,
Mwanzo na Mwisho, Wa Kwanza na Wa Mwisho. Hivyo viwili vikichanganywa pamoja
----- injili ya Kristo na Sheria ya Mungu ----- hutoa upendo na imani isiyo na mipaka. ----
- MS 53, 1890.
NJIA IENDAYO KWENYE UTAKATIFU Mei 16
Na kila mwenye matumaini haya katika yeye hujitakasa, kama yeye alivyo mtakatifu.
1 Yohana 3:3. Je, fungu hili lina maana kwamba mwanadamu anaweza kuliondoa waa moja la dhambi
toka moyoni mwake? La. Basi, kujitakasa mwenyewe maana yake nini? Kuna maana ya
kuiangalia ile kanuni kuu ya maadili ya haki yake Bwana, yaani, ile Sheria takatifu ya
Mungu, na kujiona mwenyewe ya kuwa u mwenye dhambi kwa nuru ile inayotoka katika
Sheria hiyo. "Kila mtu atendaye dhambi anavunja Sheria ya Mungu [Amri Kumi], maana
dhambi ni uvunjaji wa Sheria. Nanyi mnajua ya kuwa yeye alidhihirishwa ili aziondoe
dhambi; na dhambi haimo ndani yake." 1 Yohana 3:4,5 [AJKK]. Ni kwa njia ya imani
katika Yesu Kristo.... mwanadamu anatakaswa na kusafishwa.... "Kila akaaye ndani yake
hatendi dhambi; kila atendaye dhambi hakumwona yeye, wala hakumtambua." Fungu la
6. Mungu anao uwezo wa kumlinda mtu aliye ndani ya Kristo.... Kukiri kwa mdomo tu
kwamba mtu ni mtauwa ni bure kabisa. Ni yule akaaye ndani ya Kristo aliye Mkristo....
Katika hali ya hewa ya kila nchi, katika kila taifa, vijana wetu wangeshirikiana na
Mungu. Njia pekee ya mtu kuwa mtakatifu ni kuwa na nia ile ile aliyo nayo Mungu.
Twawezaje kumjua Mungu? Kwa kujifunza Neno lake....
Nia ya Mungu isipokuwa ndiyo nia ya mwanadamu, basi, kila juhudi ya kujitakasa
mwenyewe itakuwa ni bure; maana haiwezekani kabisa kumwinua mwanadamu
[aliyeanguka] isipokuwa kwa njia ya kumjua Mungu. Mng'ao wa nje unaweza kuvaliwa,
na watu wanaweza kuwa kama vile walivyokuwa wale Mafarisayo ambao Yesu
anawaeleza kuwa ni "makaburi yaliyopakwa chokaa," yaliyojaa uchafu na mifupa ya
watu waliokufa. Lakini ulemavu wote wa moyo u wazi kwake anayehukumu kwa haki,
na kweli isipopandwa moyoni, haiwezi kuyatawala maisha [ya mtu]. Kusafisha kikombe
kwa nje hakutakifanya chombo hicho kuwa safi ndani. Kuikubali kweli kwa juu juu tu ni
kuzuri kama kulivyo, na uwezo wa kutoa sababu kwa imani yetu ni mafanikio mema,
lakini kweli isipokwenda chini zaidi ya hapo, moyo huo hautaokolewa kamwe. Moyo
hauna budi kutakaswa na uchafu wote wa kimaadili. "Nami najua, Mungu wangu; ya
kuwa wewe wawajaribu moyo, nawe wapendezwa na unyofu." 1 Mambo ya Nyakati
29:17. "Ee Mungu, unichunguze, uujue moyo wangu, Unijaribu, uyajue mawazo yangu;
Uone kama iko njia iletayo majuto ndani yangu, Ukaniongoze katika njia ya milele."
Zaburi 139:23,24. ----- Letter 13, 1893.
DHAMIRI ILIYOONGOKA Mei 17
Nami ninajizoeza katika neno hili niwe na dhamiri isiyo na hatia mbele za Mungu na
mbele ya watu siku zote. Matendo ya Mitume 24:16.Katika Neno la Mungu twasoma ya kwamba kuna dhamiri njema na dhamiri mbaya....
Ichukue dhamiri yako na kwenda nayo kwenye Neno la Mungu, na kuona kama maisha
na tabia yako vinapatana na ile kanuni ya haki ambayo Mungu ameifunua humo. Kisha
unaweza kuamua kama unayo imani yenye busara au la, na dhamiri ya aina gani unayo.
Dhamiri ya mwanadamu haiwezi kutegemewa isipokuwa kama iko chini ya uongozi wa
neema ya Mungu. Shetani anaidanganya dhamiri ambayo haijaongoka na kwa njia hiyo
anawaongoza wanadamu katika kila aina ya madanganyo yake. ----- RH, Sept. 3, 1901.
Haitoshi kwa mtu kufikiri mwenyewe kwamba yuko salama katika kuyafuata maongozi
ya dhamiri yake.... Swali la kutatua ni hili, Je! dhamiri hii inapatana na Neno la Mungu?
Kama sivyo, haiwezi kufuatwa kwa usalama, maana itakudanganya. Dhamiri yako
inapaswa kuongolewa na Mungu. Muda unatakiwa uweze kutengwa kwa ajili ya
kujifunza Maandiko na kuomba. Hivyo moyo wako utaimarishwa, utatiwa nguvu, na
kutulia. ----- Letter 21, 1901.
Ni haki ya kila mmoja wetu kuishi kwa namna ambayo Mungu atamkubali na kumbariki.
Waweza kuwa na mawasiliano na Mbingu kila saa; si mapenzi ya Baba yako aliye
mbinguni kwamba daima uwe chini ya hukumu ya adhabu na giza. Haipendezi kwa
Mungu kwamba ujiumbue wewe mwenyewe. Yakupasa kujiheshimu mwenyewe kwa
kuishi kwa namna ambayo dhamiri yako itakubaliana nawe, utakubalika mbele ya
wanadamu na malaika.... Ni haki yako kwenda kwa Yesu na kutakaswa, na kusimama
mbele ya Sheria bila kuwa na aibu, wala masikitiko. "Sasa, basi, hakuna hukumu ya
adhabu juu yao walio katika Kristo Yesu [wasioenenda kwa kufuata mambo ya mwili,
bali mambo ya roho]." Warumi 8:1 [KJV]. Wakati hatupaswi kujifikiria wenyewe kuliko
vile tunavyostahili, Neno la Mungu halilaumu kujiheshimu wenyewe kama inavyostahili.
Kama wana na binti zake Mungu, tungekuwa na utambuzi moyoni mwetu wa tabia yenye
kuheshimika tunayopaswa kuwa nayo, ambayo haina kiburi wala kujiona ndani yake. ----
- RH, Machi 27, 1888.
Dhamiri isiyo na hatia mbele za Mungu na mbele ya watu ni kitu kizuri sana kuwa
nacho.
----- MS 126, 1897.
MATAWI YANAYOZAA MATUNDA Mei 18 Mimi ni mzabibu wa kweli, na Baba yangu ndiye mkulima. Kila tawi ndani yangu
lisilozaa huliondoa; na kila tawi lizaalo hulisafisha, ili lizidi kuzaa. Yohana 15;1,2.
Mwokozi... anaisonda kidole ishara yake inayotufanya sisi kuwa wanafunzi wake:
"Hivyo hutukuzwa Baba yangu, kwa vile mzaavyo sana; nanyi mtakuwa wanafunzi
wangu." Kwa imani tunapaswa kumshika Mungu aliye hai na kuwa na uzoefu wa maisha
utakaopumua upendo, utakaoumia kwa ajili ya wengine, uliojaa upole, huruma, na
shauku. Sifa hizo za tabia ndiyo matunda ambayo Bwana Yesu anatamani sisi tuzae, na
kuyadhihirisha mbele ya ulimwengu kama ushuhuda kwamba sisi tunaye Mwokozi
awezaye kutuinua juu, tena awezaye kututosheleza.... Hatuna haja ya kuwa upande ule
unaoshindwa, maana katika kila jambo yeye ndiye utoshelevu wetu.
Tunachohitaji ni kuwapo kwake Kristo. Tunataka kweli yake iangaze mioyoni mwetu,
ikienea katika matendo yetu yote ya maisha. Hiyo itaamua kama sisi ni matawi ya
Mzabibu wa Kweli au la. Kama sisi ni matawi yanayozaa matunda, basi, tunaweza
kutazamia kwamba Mkulima yule Mkuu atatusafisha, ili tupate kuzidi kuzaa matunda.
Yote yale yasiyokuwa na faida yo yote, yote yale ambayo yangeweza kuzuia kukua
kwetu katika maisha ya Kikristo, hayana budi kuondolewa. ----- MS 37, 1908.
Kusafishwa kunapokuja, mara kwa mara tunajisikia kwamba Bwana yu kinyume nasi.
Badala ya kuwa na hisia hiyo tungepaswa kujichunguza wenyewe na kuona kama kuna
kitu cho chote ambacho tumeacha kukifanya au kitu fulani tunachohitaji kukiondoa
katika maisha yetu kabla hatujasimama katika uhusiano wetu mzuri na Mungu....
Yatupasa kuwa matawi yaliyo hai ya Mzabibu wa Kweli, kila siku tukimshika
Mkombozi wetu ili tupate kuzaa matunda ya tabia ya Kikristo.... Tunapokuwa tayari
kujizoeza kujikana nafsi na kujitoa mhanga, kama Kristo alivyofanya katika maisha yake,
hapo ndipo tutakapozaa matunda kwa ajili ya utukufu wa Mungu. ----- MS 19, 1909.
Ni furaha ya Mwokozi wetu kuwaona wafuasi wake wakiwa watenda kazi pamoja na
Mungu, wakipokea kwa wingi uwezo wote utakaowawezesha kuzaa matunda, na kutoa
kwa ukarimu, kama watenda kazi chini yake. Kristo alimtukuza Baba yake kwa matunda
aliyozaa, na maisha ya wafuasi wake wa kweli yatakuwa na matokeo yayo hayo. Kwa
kupokea na kutoa, watenda kazi wake watazaa sana matunda. ----- Letter 42, 1900.KUKAA NDANI YA KRISTO Mei 19
Kaeni ndani yangu, nami ndani yenu. Kama vile tawi lisivyoweza kuzaa peke yake,
lisipokaa ndani ya mzabibu; kadhalika nanyi, msipokaa ndani yangu. Yohana 15:4.
Tawi lililokatwa, lisilokuwa na majani, na linaloonekana kana kwamba halina uhai wo
wote, linapopandikizwa katika mzabibu ulio hai, na kuunganishwa nao nyuzi kwa nyuzi,
na mshipa kwa mshipa, linakunywa uhai na nguvu ya Mzabibu mpaka linaanza kuchipua
na kutoa maua na kuzaa matunda, hivyo ndivyo yule mwenye dhambi, kwa toba na
imani, awezavyo kuwa mshirika wa tabia ya uungu, na kuzaa matunda ya maisha yaliyo
matakatifu kwa njia ya maneno na matendo yake.
Yesu "anao uzima ndani yake mwenyewe," na uzima huo anajitolea kuwapa bure wale
waliokufa katika makosa na dhambi. Naam, anashiriki pamoja nao utakatifu wake,
heshima yake, na furaha yake.... Tawi linalonyauka, likipandikizwa katika mzabibu ulio
hai, huwa sehemu ya mzabibu huo. Linaishi likiwa limeunganishwa na mzabibu huo.
Kwa hiyo Mkristo anaishi kwa sababu ya muungano wake na Kristo. Sehemu yenye
dhambi ya kibinadamu inaunganishwa na sehemu takatifu ya Mungu. Mtu yule aaminiye
hukaa ndani ya Kristo, na kuwa umoja pamoja naye. Watu wanapounganishwa kwa
karibu sana katika uhusiano wao wa maisha haya, hisia zao hufanana, wanayapenda
mambo yale yale. Hivyo ndivyo wale wanaokaa ndani ya Kristo watakavyopenda mambo
yale yale anayoyapenda yeye. Kwa kicho watazitunza na kuzitii Amri zake [Kumi]....
Tawi la mzabibu, likipata lishe yake kutoka kwa mzabibu, husitawi na kuzaa. Vichala
vyake vilivyojaa na vinavyotoa harufu nzuri hushuhudia muungano wake na mzabibu
ulio hai. Hivyo ndivyo Mkristo, anayekaa ndani ya Yesu, atakavyozaa matunda. Katika
tabia na maisha yake yataonekana, kama vichala vilivyojaa tele vya mzabibu, matunda
mazuri ya Roho, ----- upendo, furaha, amani, uvumilivu, utu wema, fadhili, uaminifu,
upole, kiasi....
Amueni ya kwamba ninyi mtakuwa matawi yanayozaa matunda ya Mzabibu huo ulio
hai. Kishina cha tawi kinaweza kusitawi tu kadiri kinavyoendelea kupokea uhai na nguvu
kutoka kwa mzabibu mama. Basi, tumieni vizuri kila nafasi inayopatikana kujiunganisha
wenyewe kwa karibu sana na Kristo. Ni kwa njia ya kumwamini, kumpenda, kumwiga,
na kumtegemea kabisa, ndipo mnaweza kuwa na umoja naye; na kupitia kwenu uzima
wake na tabia yake vitadhihirishwa kwa ulimwengu. ----- RH, Sept. 11, 1883.CHIMBUKO LA NGUVU ZANGU Mei 20
Mimi ni mzabibu; ninyi ni matawi, akaaye ndani yangu nami ndani yake, huyo huzaa
sana; maana pasipo mimi ninyi hamwezi kufanya neno lo lote. Yohana 15:5.
Sisi ni wanadamu, lakini mpango wa ajabu umeandaliwa ili tupate kuwa na uhusiano wa
karibu na Mungu.... Wanadamu kwa juhudi yao yote wanaweza kufanya kidogo mno,
lakini Kristo akitenda kazi yake kupitia kwa binadamu matokeo ya ajabu yanaweza
kupatikana.
Ni wazo linalonitia uchungu sana kwamba mimi naweza kufanya kidogo mno.Upeo
mdogo wa uwezo wa kibinadamu unanifanya mimi kuyasikia mpaka ndani ya moyoni
wangu maneno haya ya Kristo, "Pasipo MIMI ninyi hamwezi kufanya NENO LO
LOTE." Wengi wamekirimiwa talanta zilizo bora wala hawazitumii, kwa sababu hawana
uhusiano hai na Mungu.... Ujuzi wangu wa juu juu na juhudi zangu dhaifu hunisukuma
kwenda kwa Yesu, na lugha ya moyo wangu ni hii, "Ee Mungu, mimi siwezi kufanya
neno lo lote. Naiweka roho yangu isiyokuwa na msaada juu yako, Yesu Kristo Mwokozi
wangu. Weka neema yako moyoni mwangu. Moyo wangu upate kuuvuta kutoka katika
udhaifu wake kwenda kwenye nguvu zako, kutoka kwenye ujinga wangu kwenda kwenye
hekima yako ya milele, kutoka kwenye udhaifu wangu wa mwili kwenda kwenye uweza
wako udumuo. Nipe mawazo sahihi juu ya mpango ule wa wokovu. Niwezeshe kuona na
kuelewa jinsi Kristo alivyo kwangu mimi, na ya kwamba moyo wangu, roho yangu, nafsi
yangu, na nguvu zangu vimenunuliwa kwa thamani. Kristo amenipa mimi ili na mimi
niweze kuwapa wengine. Naomba roho yangu uiinue juu; nitie nguvu na kuielimisha akili
yangu ili niweze kufahamu kwa wazi zaidi tabia ya Mungu kama ilivyofunuliwa ndani ya
Yesu Kristo, ili mimi nijue ya kwamba ni haki yangu kuwa mshirika wa tabia ile ya
uungu."
Uweza mkuu na wa milele wa Mungu unaujaza moyo wangu kwa kicho, na wakati
mwingine hofu.... Naam, hebu na nimwangalie Yesu, aliyejaa fadhili na huruma na
upendo, na kumtazama Bwana Mungu, na kumwita kwa jina lake lile linalopendwa sana
la Baba.
Mapambano makali yaliyo ndani ya moyo wangu dhidi ya majaribu, na shauku kuu ya
akili na moyo wangu ya kutaka kumjua Mungu na Yesu Kristo kama Mwokozi wangu
hasa, na kuwa na imani, amani, na raha katika upendo wao, hunifanya mimi kutamani
kila siku kuwa mahali pale ambapo mionzi ya Jua la Haki inaweza kuniangazia juu
yangu. ----- MS 41, 1890.KUZIFURAHIA AHADI ZAKE Mei 21
Ninyi mkikaa ndani yangu, na maneno yangu yakikaa ndani yenu, ombeni mtakalo lote
nanyi mtatendewa. Yohana 15:7.
Ni za thamani haki alizopewa yule anayekaa ndani ya Kristo.... Nia ya Kristo hukaa
ndani ya wafuasi wake waaminifu; tamaa zao zinapatana na mapenzi yake; dua zao
zinaongozwa na Roho wake. Wanapata majibu kwa maombi yao; kwa kuwa wanaomba
mibaraka ile tu anayopenda kutoa.
Lakini kuna maelfu ya maombi yanayotolewa kila siku ambayo Mungu hayajibu. Yapo
maombi yanayotolewa pasipokuwa na imani. "Mtu amwendeaye Mungu lazima aamini
kwamba yeye yuko, na kwamba huwapa thawabu wale wamtafutao." Waebrania 11:6.
Yapo maombi ya uchoyo, yatokayo katika moyo unaotunza sanamu ndani yake.... Kuna
maombi yasiyokuwa na uvumilivu ndani yake, yaliyojaa wasiwasi, yakinung'unika kwa
sababu ya mizigo mizito na masumbufu ya maisha haya, badala ya kutafuta neema kwa
moyo wa unyenyekevu ili kuweza kuifanya [mizigo hiyo] iwe myepesi. Wale
wanaoomba dua kama hizo hawakai ndani ya Kristo. Hawatimizi sharti la ahadi ile, na,
kwa hiyo, haitimizwi kwao.
Wale wanaokaa ndani ya Yesu wanayo hakika kwamba Mungu atawasikia, kwa sababu
wanapenda kufanya mapenzi yake. Hawaombi sala yo yote, yenye maneno mengi, kwa
kufuata mtindo, bali wanamwendea Mungu kwa imani ya dhati, yenye unyenyekevu
ndani yake kama ile ya mtoto mdogo kwa baba yake mwema, na kumweleza kisa cha
majonzi yao na hofu zao pamoja na dhambi zao, na katika jina la Yesu wanamkabidhi
shida zao; wanaondoka mbele zake wakifurahia uhakika wa kupewa upendo wake
unaosamehe na neema yake inayowatunza. ----- RH, Sept. 11, 1883.Ukiwa na hisia kwamba Yesu yuko kando yako, basi, wewe utakuwa na uchangamfu,
matumaini, ujasiri, na furaha.... Kamwe, kamwe usijitenge mbali na Yesu. Yeye hajitengi
mbali nasi kamwe. Kwa njia ya msalaba ule wa Kalvari ametoa ushahidi kwetu wa
upendo wake ulio mwingi kwa ajili yetu. Hatuachi kupigana vita kwa nguvu zetu
wenyewe za kibinadamu. Yeye anasema, "Sitakupungukia kabisa, wala sitakuacha
[sitakutelekeza] kabisa." Waebrania 13:5.... Yesu hatutupi, hata pale tunapomhuzunisha;
bado anaendelea kutushikilia sisi. Hebu moyo wako na usisimke kwa upendo wake Yesu
na kuwa motomoto kutenda kazi yake kwa ajili ya utukufu wake. ----- Letter 5b, 1891.
WATU WENYE FURAHA KULIKO WOTE DUNIANI Mei 22
Hayo nimewaamia, ili furaha yangu iwe ndani yenu, na furaha yenu itimizwe. Yohana
15:11.
Sisi, kama Wakristo, hatutakiwi kwenda huku na huko tukiwa na nyuso ndefu [zenye
huzuni], tukishusha pumzi yetu kana kwamba hatukuwa na Mwokozi wala tumaini lo
lote. Jambo hilo halitamtukuza Mungu. Anatamani kutuona sisi tukiwa wachangamfu.
Anatamani sisi tujazwe na sifa kwa ajili ya jina lake. Anatamani sisi tuichukue nuru
katika nyuso zetu, na furaha mioyoni mwetu. Tunalo tumaini lililo juu sana kuliko anasa
zo zote ambazo ulimwengu huu unaweza kutoa, na ukweli huu hauna budi kudhihirishwa
[katika maisha yetu].
Kwa nini furaha yetu isitimizwe ----- yaani, isiwe timilifu, isiyopungua kitu? Tunayo
ahadi kwamba Yesu ni Mwokozi wetu, na ya kwamba tunaweza kuchota kwake bure.
Tunaweza kula bure vinono alivyotuandalia sisi katika Neno lake. Tunaweza kumwamini
asemavyo, yaani, kumwamini yeye, na kujua kwamba atatupa neema na uwezo wa
kufanya kama vile anavyotuagiza.... Daima tunaweza kutafuta furaha ya kuwapo kwake.
Si lazima kila wakati tuwe tumepiga magoti katika sala zetu, bali daima tunaweza
kuomba neema yake, hata wakati tunapotembea mitaani, au tunapofanya kazi zetu za
kawaida za kila siku. Daima tunaweza kuyafanya mawazo yetu yawe yanapaa juu kwa
Kristo, naye atatupa bure neema yake....
Furaha ya Kristo ni safi, yaani, inao uchangamfu usiochanganyika na kitu kingine cho
chote. Sio uchangamfu ule usio wa kiungwana, ambao unaelekea kwenye maneno ya
ovyo au tabia iliyo hafifu. La, yatupasa sisi kuwa na furaha YAKE, na furaha yake kuu
mno ilikuwa ni kuona wanadamu wanaitii kweli yake.... Umsihi Mungu wako, ukisema,"Mimi najisalimisha kwako kabisa.... Najitoa mwenyewe kwako kabisa." Kisha uwe na
furaha. Neno li ndani yako, litakutakasa na kukusafisha tabia yako. Mungu hataki watoto
wake kwenda huku na huko wakiwa na wasiwasi na huzuni katika nyuso zao. Anataka
ionekane sura yake iliyojaa upendo ndani ya kila mmoja wetu sisi tunaoishiriki tabia yake
ya uungu; kwa kuwa tunao uwezo wa kuokolewa na uharibifu uliomo duniani....
Sisi hatujaachwa kama kundi la yatima kutokana na kufa kwake Kristo.... Kwetu upo
uwezekano wa kupata ushindi juu ya ushindi, na kuwa watu wenye furaha kuliko wote
katika uso wa dunia hii. ----- MS 37, 1908.
URAFIKI NA YESU Mei 23
Ninyi mmekuwa rafiki zangu, mkitenda niwaamuruyo. Yohana 15:14.
Tabia na mwenendo wa Mkristo ni tofauti kabisa na ule wa walimwengu. Mkristo
hawezi kupata furaha yake katika burudani na mandhari mbalimbali za shamrashamra
[tafrija] za ulimwengu huu. Mapenzi yao yanavutwa na mambo yale ya hali ya juu na
matakatifu zaidi. Wakristo watadhihirishwa kwamba wao ni rafiki zake Mungu kwa utii
wao. "Ninyi mmekuwa rafiki zangu," asema Kristo, "mkitenda niwaamuruyo.... Kama
mngekuwa wa ulimwengu, ulimwengu ungewapenda walio wake; lakini kwa kuwa ninyi
si wa ulimwengu, bali mimi naliwachagua katika ulimwengu, kwa sababu hiyo
ulimwengu huwachukia."
Kristo ni mwamba wako na ngome yako. Wenye haki hulikimbilia jina lake na kuwa
salama.... Haki na ukuu wa matakwa yake hautambuliwi na ulimwengu, ambao huiona
dini ya Kristo kama kongwa la utumwa, yaani, kama ni kusalimisha uhuru wao. Kila
moja ya matakwa yake Mungu ni agizo kwetu kuweza kuwa na hekima, matajiri, na
waungwana kwa njia ya kuiunganisha nguvu yetu dhaifu na uweza wa Mungu
Mwenyezi. Tunapozifuata nyayo zake Kristo hatuna haja ya kutahayari, maana dhamiri
yetu haitatushutumu kamwe. Kazi yake sikuzote ni ya maana. Kazi yake sikuzote ni ya
heshima na tukufu. Rafiki zetu wanaotutaka sisi kuchagua anasa za ulimwengu huu,
wanaotuona sisi kama wakaidi, hawawezi kuwa na madai yo yote juu yetu ambayo
yanaweza kustahili kulinganishwa na madai yale ya Kristo....
Thamani ya mwanadamu kama Mungu anavyomkisia inapatikana kwa njia ya muungano
wake na Kristo; kwa maana Mungu ndiye peke yake awezaye kumwinua juumwanadamu katika mizani ile inayopima thamani ya maadili kwa njia ya haki yake
Kristo. Heshima ya ulimwengu na ukuu wa kilimwengu hukisiwa kuwa vina thamani ile
tu anayoiweka Muumbaji wa mwanadamu juu yake. Hekima yao ni upumbavu, nguvu
zao ni udhaifu.
Hebu na tukithamini kile ambacho Mungu anakiheshimu. Ukuu wa kweli wa tabia
unapatikana peke yake kwa njia ya Kristo. Mwokozi wetu humhesabia haki yake mtu
yule anayeyasalimisha kwake mapenzi yake yaliyo bora na matakatifu sana ya moyo
wake! Thamani yetu inawiana na muungano wetu na Mungu. ----- Letter 9, 1873.
KIPAWA CHA KRISTO KIPITACHO VYOTE Mei 24
Lakini mimi nawaambia iliyo kweli; yawafaa ninyi mimi niondoke, kwa maana mimi
nisipoondoka, huyo Msaidizi hatakuja kwenu; bali mimi nikienda zangu, nitampeleka
kwenu. Yohana 16:7.
Kristo alinena kwa nguvu ya kwamba baada ya kupaa kwake angetuma kwa Kanisa lake,
kipawa kipitacho vyote, yaani, yule Msaidizi, ambaye angechukua mahali pake. Msaidizi
huyo ni Roho Mtakatifu ----- nafsi ya uhai wake, ufanisi wa kanisa lake, nuru ya na
uzima wa ulimwengu....
Katika kipawa chake hicho cha Roho Mtakatifu, Yesu alimpa mwanadamu fadhili kuu
sana ambazo mbingu ingeweza kutoa.... Ni Roho anayekamilisha kile kilichofanywa na
Mkombozi wa ulimwengu. Ni kwa njia ya Roho moyo hutakaswa. Kwa njia hiyo ya
Roho muumini anakuwa mshirika wa tabia ya uungu. Kristo amemtoa Roho wake kama
uweza wa Mungu wa kushindia mielekeo yetu yote mibaya tuliyorithi kwa wazazi wetu
na ile tuliyojifunza wenyewe kwa kuifanyia mazoezi, na kuipiga chapa tabia yake
mwenyewe juu ya kanisa lake.... Ni haki ya kila mwana na binti ya Mungu kuwa na Roho
akikaa ndani yake. ----- RH, Mei 19, 1904.
Hebu kila mshiriki wa kanisa na apige magoti mbele za Mungu, na kuomba kwa bidii ili
apewe Roho. Mlilie sana, ukisema, "Bwana, niongeze imani yangu. Uniwezeshe
kulielewa Neno lako; maana kulifafanua neno lako kwatia nuru. Uniburudishe kwa
kuwako kwako. Unijaze moyo wangu na Roho wako."...Mtu anapojazwa na Roho, kadiri anavyopimwa na kupata maonjo mengi, ndivyo kadiri
anavyothibitisha wazi kwamba yeye ni mwakilishi wa Kristo. Amani inayokaa ndani ya
moyo wake inaonekana usoni pake. Maneno na matendo yake huonyesha upendo wa
Mwokozi wake.... Nafsi inakanwa. Jina la Yesu huandikwa juu ya yote yanayosemwa na
kufanywa.
Twaweza kuongelea juu ya mibaraka ya Roho Mtakatifu, lakini tusipojiandaa sisi
wenyewe kumpokea, matendo yetu yatakuwa na faida gani? Je! tujitahidi kwa uwezo
wetu wote kukifikia cheo cha wanaume na wanawake cha kimo cha utimilifu wa Kristo?
Je! tunautafuta utimilifu wake wote, daima tukiwa tunasonga mbele kwenda kwenye
alama ile iliyowekwa mbele yetu ----- yaani, ule utimilifu wa tabia yake? Watu wa
Mungu watakapoifikia alama hiyo, ndipo watakapotiwa muhuri juu ya vipaji vya nyuso
zao. Wakiwa wamejazwa na Roho, watatimilika katika Kristo, na malaika yule anayetia
alama atatangaza, akisema, "Imekwisha." -----
RH, Juni 10, 1902.
ROHO ANATOLEWA KWA MASHARTI Mei 25
Basi, ikiwa ninyi mlio waovu mnajua kuwapa watoto wenu vipawa vyema, je! Baba
aliye mbinguni hatazidi sana kuwapa Roho Mtakatifu hao wamwombao? Luka 11:13.
Kristo ameahidi kipawa cha Roho wake kwa kanisa lake, na ahadi hiyo ni yetu sisi
sawasawa na vile ilivyokuwa kwa wanafunzi wale wa kwanza. Lakini kama ilivyo ahadi
nyingine yo yote, anatolewa kwa masharti. Wako wengi wanaoamini, na kukiri kwamba
wanaidai ahadi hiyo ya Bwana, lakini hawapokei manufaa yo yote. Hao huwa
hawasalimishi moyo wao kuongozwa na kutawaliwa na wajumbe wale wa mbinguni. Sisi
hatuwezi kumtumia Roho Mtakatifu. Roho ndiye anayetakiwa kututumia sisi. Kwa njia
ya Roho, Mungu anatenda kazi ndani ya watu wake "kutaka [kwao] na kutenda [kwao],
kwa kulitimiza kusudi lake jema." Wafilipi 2:13. Lakini wengi hawakubali kutumiwa
hivyo [na Roho]. Wanataka kujiongoza wenyewe. Hii ndiyo maana hawapokei kipawa
hicho cha mbinguni. Ni kwa wale tu wanaomngojea Bwana kwa unyenyekevu,
wanaotazamia uongozi wake na neema yake, Roho huyo anatolewa....
Hakuna mpaka wa kuwa na manufaa kwa yule ambaye, nafsi yake akiiweka kando,
anaweka nafasi kwa Roho Mtakatifu kufanya kazi moyoni mwake, na kuishi maisha
yaliyowekwa wakf kabisa kwa Mungu.... Endapo watu wake wataviondoa vizuizi, basi,yeye atawamwagia maji ya wokovu kwa wingi kupitia katika vijito kwa njia mbalimbali
za kibinadamu....
Roho anatoa nguvu inayowaimarisha watu wale wanaojitahidi na kupigana mieleka
katika kila hali ya hatari inayowajia, katikati ya uadui wa ndugu zao, chuki ya
ulimwengu, na kuwawezesha kutambua upungufu wao wenyewe pamoja na makosa yao.
Muungano wa juhudi ya Mungu na ya kibinadamu, yaani, muungano wa karibu sana na
Mungu, ambaye ni Chimbuko la nguvu zote, mwanzoni, mwishoni, na daima ----- ni
jambo la muhimu kabisa. -----
RH, Mei 19, 1904.
Roho alitolewa bila kipimo kwa Yesu, aliyejitoa nafsi yake kabisa kwa ajili ya wokovu
wa wanadamu waliopotea. Hivyo ndivyo atakavyotolewa kwa kila mfuasi wa Kristo
wakati moyo wake wote utakapokuwa umejisalimisha ili [Roho] apate kukaa ndani yake.
Bwana wetu mwenyewe ametoa agizo hili, "Mjazwe Roho," na agizo hilo pia ni ahadi
kwetu ya kutimizwa kwake. Yalikuwa ni mapenzi yake Baba kwamba ndani ya Kristo
ukae "utimilifu wote" wa Mungu; na "ninyi mmetimilika katika yeye" (Wakolosai
2:9,10). ----- RH, Nov. 5, 1908.
ALIYE BADALA YA KRISTO Mei 26
Naye akiisha kuja, huyo atauhakikisha ulimwengu kwa habari ya dhambi, na haki, na
hukumu. Yohana 16:8.
Msaidizi huyo atakapokuja, na kukuhakikisha wewe kwa habari ya dhambi, haki, na
hukumu, jihadhari sana usije ukampinga Roho wa Mungu.... Uwe tayari kupambanua kile
atakachokufunulia. Achilia mbali mapenzi yako mwenyewe, yaani, tabia zako
ulizoziabudu kwa muda mrefu ambazo ni za kwako wewe peke yako, ili upate kuzipokea
kanuni za ile kweli. -----
RH, Aprili 12, 1892.Kwa gharama kubwa isiyokadirika ya kujitoa mhanga na kuteseka, Kristo ametuandalia
sisi kila kitu kilicho cha muhimu kwa ufanisi wetu katika vita hii ya Kikristo. Roho
Mtakatifu huleta nguvu ambayo inamwezesha mwanadamu kushinda. Ni kwa njia ya
huduma ya Roho huyo serikali ya Shetani itashindwa. Ni Roho anayetuhakikisha kwa
habari ya dhambi, na, kwa kibali cha mwanadamu, anaifukuza dhambi kutoka moyoni
mwake. Kisha moyo wake unawekwa chini ya Sheria mpya ----- Sheria ya Kifalme ya
Uhuru [Amri Kumi]. -----
RH, Mei 19, 1904.
Bwana Yesu anatenda kazi yake kwa njia ya Roho Mtakatifu; maana huyo ndiye aliye
Badala yake. Kupitia kwake anatia uzima wa kiroho moyoni, akiziamsha nguvu zake ili
zipate kutenda mema, anautakasa na uchafu wote wa kimaadili, na kuupa hadhi inayofaa
kwa ufalme wake. Yesu anayo mibaraka mingi sana ya kugawa, yaani, vipawa vingi vya
kuwagawia wanadamu. Yeye ndiye Mshauri wa Ajabu, mwenye hekima na nguvu isiyo
na kifani; na kama sisi tutaipokea nguvu ya Roho wake, na kunyenyekea ili tupate
kubadilishwa naye, basi, sisi tutatimilika katika yeye. Ni wazo lililoje hilo! Katika Kristo
"unakaa utimilifu wote wa Mungu, kwa jinsi ya kimwili. Na ninyi mmetimilika katika
yeye." Wakolosai 2:9,10.
Kamwe hautaijua furaha moyo wa mwanadamu mpaka hapo utakapojinyenyekeza na
kukubali kubadilishwa na Roho wa Mungu. Roho anaigeuza nia iliyofanywa upya ipate
kufanana na mfano ule halisi, yaani, Yesu Kristo. Kwa njia ya uweza wake [Roho], uadui
dhidi ya Mungu unageuzwa na kuwa imani na upendo, na kiburi kinakuwa unyenyekevu.
Moyo huo unatambua uzuri wa ile kweli, naye Kristo anaheshimiwa kwa njia ya uzuri
usio na kifani na utimilifu wa tabia yake. Mabadiliko hayo yanapotokea, malaika huimba
wimbo kwa shangwe kuu, naye Mungu pamoja na Kristo wanashangilia juu ya watu wale
waliofanywa wapate kufanana na mfano wa [tabia ya] Mungu. ----- RH, Agosti 25, 1896.
KUKUBALI KUONGOZWA NA ROHO Mei 27
Kwa maana kama mkiishi kwa kufuata mambo ya mwili, mwataka kufa; bali mkiyafisha
matendo ya mwili kwa Roho, mtaishi. Kwa kuwa wote wanaoongozwa na Roho wa
Mungu, hao ndio wana wa Mungu. Warumi 8:13,14. Nia ya mwanadamu ni jeuri, nayo inajitahidi daima kuyakunja mambo yote kuelekea
kwenye makusudi yake. Kama inawekwa upande wake Mungu, na haki, basi, matunda ya
Roho yataonekana katika maisha hayo; naye Mungu amemchagulia utukufu, heshima, na
amani kila mtu anayetenda mema.
Shetani akiruhusiwa kuibadilisha nia yetu, basi, yeye anaitumia kutimiza makusudi
yake.... Anaichochea mielekeo ile mibaya ya moyo, anaamsha tamaa mbaya za mwili na
moyo ule wa kutaka makuu. Anasema, "Mamlaka hiyo yote, heshima hizo, na utajiri huo,
na anasa hizo za dhambi, nitakupa wewe"; lakini masharti yake ni kwamba uaminifu
utaachwa, na dhamiri itakuwa haina makali yake [ya kupambanua mema na mabaya].
Hivyo ndivyo anavyozidhalilisha nguvu za akili ya kibinadamu, na kuwaleta katika
utumwa wa dhambi. ----- RH, Agosti 25, 1896.
Lakini Mungu anajaribu daima kuigusa mioyo yetu kwa Roho wake Mtakatifu, ili tupate
kuhakikishwa kwa habari ya dhambi, haki, na hukumu ijayo. Tunaweza kuiweka nia yetu
upande wa nia yake Mungu, na kwa nguvu zake na neema yake kuweza kuyapinga
majaribu ya yule adui. Tunapojitoa kuongozwa na Roho wa Mungu, dhamiri yetu
inakuwa nyororo na nyepesi kupambanua [mema na mabaya], na dhambi ile tuliyoipita
bila kuifikiria sana, inageuka na kuwa dhambi kubwa mno. ----- ST, Sept. 4, 1893.
Mungu anawaagiza watu kuzipinga nguvu zile za uovu. Anasema: "Basi, dhambi
isitawale ndani ya miili yenu ipatikanayo na mauti, hata mkazitii tamaa zake; wala
msiendelee kuvitoa viungo vyenu kuwa silaha za dhuluma kwa dhambi; bali jitoeni
wenyewe kwa Mungu kuwa silaha za haki." Warumi 6:12,13....
Katika pambano hilo la haki dhidi ya dhuluma, tunaweza kuwa washindi tu kwa msaada
wa Mungu. Nia yetu ya kibinadamu lazima iletwe mahali ambapo itaweza kunyenyekea
chini ya mapenzi yake Mwenyezi; nia ya kibinadamu ni lazima iunganishwe vizuri na ile
ya Mungu. Jambo hilo litamfanya Roho Mtakatifu kuja kutusaidia; na kila ushindi
utaelekea kukifanya kile kilichopotea ambacho Mungu alikinunua kuweza kupatikana
tena, yaani, kuirejesha tena sura yake [Mungu] moyoni. ----- RH, Agosti, 1896.
AIFUNUAYE NEEMA YA KRISTO Mei 28
Lakini yeye atakapokuja, huyo Roho wa kweli, atawaongoza awatie kwenye kweli yote;
kwa maana hatanena kwa shauri lake mwenyewe, lakini yote atakayoyasikia atayanena,
na mambo yajayo atawapasha habari yake. Yohana 16:13 Kuhusu habari zake huyo Msaidizi imeandikwa hivi, " Atawaongoza awatie kwenye
kweli yote...." Kwa njia ya Roho Mtakatifu, Kristo atawafunulia kwa wazi zaidi wale
wanaomwamini kile alichokuwa amewavuvia watu wale watakatifu kuandika juu ya ile
kweli. -----
RH, Aprili 12, 1892.
Kristo alisema hivi juu yake Roho, "Yeye atanitukuza mimi." Yohana 16:14. Kama vile
Kristo alivyomtukuza Baba kwa kuudhihirisha upendo wake, hivyo ndivyo Roho
alivyotakiwa kumtukuza Kristo kwa kuufunulia ulimwengu utajiri wa neema yake. Sura
ile ile ya Mungu inapaswa kuonekana ndani ya wanadamu. Heshima ya Mungu, heshima
ya Kristo, inahusika katika utimilifu wa tabia ya watu wake....
Roho anafanya kazi yake ndani yetu kwa kutukumbusha, kwa wazi na mara kwa mara,
kweli zile za thamani kuhusu mpango wa ukombozi. Tungezisahau kweli zile, na kwetu
ahadi za Mungu zingepoteza ufanisi wake, kama isingalikuwa ni yule Roho,
anayeyachukua mambo ya Mungu, na kutuonyesha sisi.... Roho anatuangazia giza letu,
anatupasha habari za mambo yale tusiyoyajua, na kutusaidia katika shida zetu nyingi.
Lakini moyo hauna budi kumwendea Mungu daima. Kama kuipenda dunia kunaruhusiwa
kuingia ndani yetu, kama hatuna hamu ya kuomba, yaani, bila hamu ya kuzungumza na
yule ambaye ni Chimbuko la nguvu na hekima yetu, basi, Roho hataweza kukaa ndani
yetu. Wale wasiokuwa na imani hawapokei neema nyingi ambayo ingewafanya kuwa na
hekima hata kupata wokovu, na kuwa na saburi, uvumilivu, na wepesi wa kuzifahamu na
kuzithamini huduma zile zinazotoka mbinguni, kuwa wepesi kupambanua hila zake
Shetani, na wenye nguvu kuipinga dhambi. ----- RH, Mei 19, 1904.
Dini ya Kristo ina maana zaidi ya ule msamaha wa dhambi; inamaanisha kwamba
dhambi imeondolewa, na mahali pake palipoachwa tupu pamejazwa na Roho.
Inamaanisha kwamba nia imepata nuru ya mbinguni, na kwamba moyo umeachwa tupu
baada ya kuiondoa nafsi [uchoyo], na kujazwa na kuwako kwake Kristo. Kazi hiyo
inapofanyika kwa washiriki wa kanisa, kanisa hilo litakuwa ni kanisa lililo hai, yaani,
kanisa linalofanya kazi. ----- RH, Juni 10, 1902.
KIPINDI CHA UWEZA WA ROHO Mei 29Lakini mtapokea nguvu, akiisha kuwajilia juu yenu Roho Mtakatifu; nanyi mtakuwa
mashahidi wangu katika Yerusalemu, na katika Uyahudi wote, na Samaria, na hata
mwisho wa nchi. Matendo ya Mitume 1:8.
Tungeomba kwa bidii kwa ajili ya kutushukia Roho Mtakatifu kama vile walivyoomba
wanafunzi wake siku ile ya Pentekoste. Iwapo wao walimhitaji wakati ule, basi, nasi
tunamhitaji zaidi leo. Kila aina ya mafundisho ya uongo, uzushi, na madanganyo
huipotosha mioyo ya watu; na pasipo msaada wa Roho, juhudi zetu za kuihubiri kweli ile
ya mbinguni zitashindwa.
Tunaishi katika kipindi cha uweza wa Roho Mtakatifu. Anataka kujichanganya pamoja
na wanadamu, na kwa njia hiyo kuongeza uweza wake ulimwenguni. Mtu awaye yote
atakayekunywa maji yale ya uzima, yatakuwa ndani yake "chemchemi ya maji,
yakibubujikia uzima wa milele" (Yohana 4:14); na mbaraka huo hautakomea kwake tu,
bali wengine wataweza kuushiriki [pia]....
Pambano kati ya wema na uovu halijapungua ukali wake kuliko vile lilivyokuwa katika
siku zake Mwokozi. Njia ya kwenda mbinguni si laini sasa kuliko vile ilivyokuwa wakati
ule. Dhambi zetu zote ni lazima tuzitupilie mbali. Kila zoea baya tunalolipenda sana
ambalo linazuia maisha yetu ya Kikristo ni lazima likatiliwe mbali. Jicho la kuume au
mkono wa kuume ni lazima ukatwe, kama unatukosesha. Je! tuko tayari kuikataa hekima
yetu wenyewe, na kuupokea ufalme wa mbinguni kama mtoto mdogo? Je! tuko tayari
kuachana na haki yetu wenyewe? Je! tuko tayari kuacha kusifiwa na wanadamu? Tunu ya
uzima wa milele ni ya thamani kubwa isiyopimika. Hivi tuko tayari kuukaribisha msaada
wa Roho Mtakatifu, na kushirikiana naye, tukijitahidi na kujitoa mhanga kulingana na
thamani ya kile tunachotaka kukipata? ----- RH, Agosti 25, 1896.
Moyo wa mwanadamu unaweza kuwa makao ya Roho Mtakatifu. Amani yake Kristo,
ipitayo ufahamu wote, inaweza kukaa moyoni mwako; na uwezo ule ubadilishao wa
neema yake unaweza kufanya kazi maishani mwako, na kukutayarisha upate kufaa kuishi
katika majumba yale ya kifalme yenye utukufu [kule mbinguni]. ----- CS 217.
AHADI YA KUKUBALIKA KWETU Mei 30
Naye Yesu alipokwisha kubatizwa mara akapanda kutoka majini; na tazama, mbingu
zikamfunukia, akamwona Roho wa Mungu akishuka kama hua, akija juu yake; natazama, sauti kutoka mbinguni ikisema, Huyu ni Mwanangu, mpendwa wangu,
ninayependezwa naye. Mathayo 3:16,17.
Mandhari hii ina maana gani kwetu? Ni kwa jinsi gani tumekisoma kisa hicho cha
ubatizo wa Bwana wetu bila kuwa na fikira zo zote, bila kutambua kwamba umuhimu
wake ulikuwa na maana kubwa sana kwetu, na kwamba Kristo alikubaliwa na Baba yake
kwa niaba ya mwanadamu. Yesu alipoinamisha kichwa chake kwenye kingo zile za
Yordani na kutoa dua yake, ubinadamu ulikabidhiwa kwa Baba na yule aliyekuwa
ameuvika uungu wake kwa ubinadamu. Yesu alijikabidhi mwenyewe kwa Baba kwa
niaba ya mwanadamu, ili wale waliokuwa wametengwa mbali na Mungu kwa ajili ya
dhambi zao wapate kurejeshwa kwa Mungu kwa njia ya wema wa Mtoa-Dua yule wa
mbinguni....
Sala ya Kristo kwa niaba ya wanadamu waliopotea ilikipenya kila kivuli alichokiweka
Shetani kati ya mwanadamu na Mungu, na kuacha njia wazi ya mawasiliano mpaka kule
kwenyewe kwenye kiti kile cha enzi cha utukufu....
Sauti ya Mungu ilisikika ikijibu ombi lake Kristo, na jambo hilo linamwambia mwenye
dhambi kwamba sala yake itapata nafasi ya kupokewa kule kwenye kiti cha enzi cha
Baba. Mbingu i wazi kupokea dua zetu, nasi tunaalikwa kukikaribia kile "kiti cha neema
kwa ujasiri, ili tupewe rehema, na kupata neema ya kutusaidia wakati wa mahitaji."
Waebrania 4:16. -----
5BC 1078.
Pamoja na dhambi zetu zote tulizo nazo na udhaifu wetu wote, hatutupwi kando kama
watu wasiofaa kitu. "Ametuneemesha [ametukubali - KJV] katika huyo Mpendwa."
Waefeso 1:6. Utukufu uliokuwa juu yake Kristo ni ahadi ya upendo wa Mungu kwetu.
Unatusimulia habari ya uwezo wa maombi ----- jinsi sauti ya mwanadamu inavyoweza
kulifikia sikio lake Mungu, na dua zetu kupata kibali katika majumba yale ya kifalme
kule mbinguni. Nuru ile iliyoshuka juu ya kichwa cha Mwokozi wetu kutoka katika
malango yale juu, itatushukia nasi tunapoomba msaada ili kuyapinga majaribu
yanayotukabili. Sauti ile iliyosema na Yesu inasema na kila mtu aaminiye, "Huyu ni
mwanangu, mpendwa wangu, ninayependezwa naye." ----- 5BC 1079.
WASAIDIZI WENYE NGUVU WATATU Mei 31Basi tulizikwa pamoja naye kwa njia ya ubatizo katika mauti yake, kusudi kama Kristo
alivyofufuka katika wafu kwa njia ya utukufu wa Baba, vivyo hivyo na sisi tuenende
katika upya wa uzima. Warumi 6:4.
Yesu alikuwa kielelezo chetu katika mambo yote yahusuyo uzima na utauwa. Alibatizwa
katika Yordani, kama vile wale wote wanaomjia inavyowapasa kubatizwa. ----- 5BC
1077.
Kristo aliufanya ubatizo kuwa kiingilio katika ufalme wake wa kiroho.... Wale
wanaopokea ukumbusho huo wa ubatizo papo hapo wanatoa tangazo la kwamba
wameukataa ulimwengu huu, nao wamekuwa watu wa familia ile ya kifalme.... Wale
wafanyao hivyo wanapaswa kuyaweka mambo yote [mazuri] ya dunia kuwa na umuhimu
wa pili kwa uhusiano wao huo mpya. Hadharani wanatangaza kwamba hawataendelea
tena kuishi maisha yale ya kiburi na kujifurahisha nafsi zao.... Wamefungwa na agano
hilo zito ili kuishi kwa ajili ya Bwana tu. Kwa ajili yake wanalazimika kutumia uwezo
wao wote waliopewa kama amana. ----- 6BC 1075.
Tunapoikubali kawaida hiyo ya dini ya ubatizo, tunashuhudia mbele ya malaika na
wanadamu ya kwamba tumesafishwa dhambi zetu za zamani, na ya kwamba kuanzia
sasa, sisi tukiwa tumeufia ulimwengu, tuta"tafut[a] mambo yaliyo juu...." (Wakolosai
3:1). Na tusisahau kiapo chetu cha ubatizo. Mbele za mamlaka zile tatu zenye nguvu
zilizo juu sana kule mbinguni ----- Baba, Mwana, na Roho Mtakatifu ----- tumeahidi
wenyewe kufanya mapenzi yake yeye ambaye... alitangaza hivi, "Mimi ndimi huo
ufufuo, na uzima." Yohana 11:25. Kristo anamsamehe kila mwenye dhambi anayetubu,
na yule aliyesamehewa wakati wa ubatizo wake, anapopanda kutoka katika kaburi lile la
maji, anatangazwa kuwa yeye ni kiumbe kipya, ambaye uzima wake umefichwa pamoja
na Kristo katika Mungu. Hebu na tukumbuke daima ya kwamba ni haki yetu kuu
kutakaswa dhambi zetu za zamani. ----- RH, Mei 26, 1904.
Mkristo anapokula kiapo chake cha ubatizo, msaada wa Mungu unaahidiwa kwake.
Baba, Mwana, na Roho Mtakatifu wanasimama na kuwa tayari kufanya kazi kwa ajili
yake. Mungu anaweka msaada wote wa mbinguni mikononi mwake [yule aliyebatizwa],
ili apate kuwa mshindi. Nguvu zake mwenyewe ni ndogo; bali Mungu ana uweza wote,
na Mungu ndiye msaidizi wake. Kila siku inampasa kujulisha mahitaji yake kwenye kiti
kile cha neema. Kwa imani na tumaini, kwa kuutumia msaada wote aliopewa, anaweza
kuwa zaidi ya mshindi. -----
RH, Feb. 18, 1904.WAKATI WA KIANGAZI PAMOJA NA MUNGU Juni 1
Maana tazama, kaskazi imepita, Masika imekwisha, imekwenda zake; Maua yatokea
katika nchi, Wakati wa kupelea umefika, Na sauti ya mwigo husikiwa kwetu.
Wimbo Ulio Bora 2:11,12.
Asubuhi hii nzuri viumbe vyote vinaonekana kuwa ni vipya na vizuri. Dunia imevaa
mavazi yake ya kiangazi ya kijani na inachekelea katika uzuri wake unaokaribiana sana
na ule wa Edeni.
Nadhani furaha yetu ya majira haya ya kiangazi inakuwa kubwa zaidi kwa kuwa na
kumbukumbu ya miezi mirefu ya majira yale ya baridi; na kwa upande mwingine, tarajio
la kiangazi hutusaidia kustahimili kwa uchangamfu mwingi zaidi kipindi hiki
kinachotawaliwa na majira ya baridi. Endapo tungeiruhusu mioyo yetu kutafakari utupu
na ukiwa unaotuzunguka ulioletwa na mfalme huyo aitwaye barafu, basi, huenda
tungalikuwa hatuna furaha kabisa; lakini, tukiwa na hekima zaidi ya mambo hayo,
tunatazama mbele kwa matarajio ya kuja majira yale ya kuchipua, ambayo yatawaleta
tena ndege, yatayaamsha maua yanayolala usingizi, na kuivika dunia mavazi yake ya
kijani, na kuijaza anga na nuru pamoja na manukato na wimbo.
Kukaa hapa duniani kwa Mkristo kunaweza kulinganishwa vizuri na kipindi kirefu cha
baridi katika majira yale ya baridi. Hapa tunakabiliana na maonjo, huzuni, na kukata
tamaa; lakini tusingeiruhusu mioyo yetu kuyatafakari mambo hayo. Ni afadhali kutazama
mbele kwa matumaini na imani kuja kwa kile kiangazi tutakapokaribishwa nyumbani
kwetu Edeni, ambako vyote ni nuru na furaha, ambako vyote ni amani na upendo.
Mkristo asingekuwa amepambana na dhoruba za mateso ulimwenguni humu, moyo
wake usingekuwa umepata kukatishwa tamaa kamwe au kukandamizwa kwa hofu, basi,
kwa shida sana angejua jinsi ya kuifurahia mbingu. Hatutakata tamaa, japo mara nyingi
tunachoka sana, tunahuzunika, na kuumwa moyo kwa kusononeka; majira haya ya baridi
hayatadumu siku zote. Kiangazi cha amani, furaha, na raha ya milele kinakuja haraka.
Hapo ndipo Kristo atakapokaa pamoja nasi na kutuongoza kwenye chemchemi za maji ya
uzima, naye atayafuta machozi yote katika macho yetu. ----- Letter 13, 1875.
Basi usiruhusu kitu cho chote... kukuzuia wewe kufanya kazi timilifu [ya kujenga tabia
yako] kwa ajili ya umilele wako.... Hazitakuwako pepo zenye baridi kali kule, wala
mafua ya majira ya baridi, bali kiangazi kile cha milele na milele. Kuna nuru kwa ajili ya
kuilisha akili yako, na upendo udumuo wa kweli. Kutakuwa na siha [afya] na uzima wa milele, nguvu kwa kila kiungo. Kila huzuni na kila sikitiko vitakuwa vimefungiwa nje
milele. ----- Letter 4, 1885.
ISHARA YA MOYO MPYA Juni 2
Nami nitawapa ninyi moyo mpya, nami nitatia roho mpya ndani yenu, nami nitatoa
moyo wa jiwe uliomo ndani ya mwili wenu, nami nitawapa moyo wa nyama. Ezekieli
36:26.
Mojawapo ya sala za dhati iliyoandikwa katika Neno la Mungu ni ile ya Daudi aliposihi,
akisema, "Ee Mungu, uniumbie moyo safi, Uifanye upya roho iliyotulia ndani yangu."
Zaburi 51:10. Jibu la Mungu kwa sala kama hiyo ni hili: Nami nitawapa ninyi moyo
mpya. Hiyo ndiyo kazi ambayo hakuna mwanadamu ye yote awezaye kuifanya.
Wanaume kwa wanawake wanapaswa kuanza toka mwanzo, kumtafuta Mungu kwa bidii
sana ili wapate uzoefu wa kweli wa Kikristo. Wanapaswa kuusikia [ndani yao] uwezo ule
wa uumbaji wa Roho Mtakatifu. Wanapaswa kupokea moyo mpya, uliolainishwa na
kufanywa mwororo kwa neema ile itokayo mbinguni. Roho ile ya uchoyo [kujipenda
nafsi] inapaswa kusafishwa ili ipate kutoka moyoni. Wanapaswa kutenda kazi kwa bidii
na kwa unyenyekevu wa moyo, kila mmoja wao akimtazama Yesu kwa uongozi na
kutiwa moyo. Hapo ndipo jengo lote, linaunganishwa pamoja, na kukua hata liwe hekalu
takatifu katika Bwana. ----- 4BC 1165.
Hasa vijana ndio wanaojikwaa sana juu ya neno hili, "moyo mpya." Hawajui lina maana
gani. Wanatazamia kuona badiliko maalum likitokea katika hisia zao. Hali hiyo wanaiita
kuongoka. Juu ya kosa hilo maelfu wamejikwaa na kuangamia, wasiweze kuelewa maana
ya usemi huu, "Hamna budi [lazima] kuzaliwa mara ya pili." Yohana 3:7.
Shetani anawaongoza watu kufikiri kwamba kwa sababu wamejisikia wanayo furaha
nyingi sana moyoni mwao, basi, wameongoka. Lakini maisha yao hayabadiliki. Matendo
yao ni yale yale waliyokuwa nayo kabla ya wakati huo. Maisha yao hayaonyeshi tunda lo
lote lililo jema. Wanaomba mara kwa mara na kwa muda mrefu, nao wanataja kila mara
hisia zao walizokuwa nazo wakati fulani uliopita. Lakini hawaishi maisha mapya.
Wamedanganyika. Maisha yao hayaendi chini zaidi ya hisia walizo nazo. Wanajenga juu
ya mchanga, na pepo zile za mbisho zinapokuja, nyumba yao inafagiliwa mbali.... Yesu anapozungumza juu ya moyo mpya, anamaanisha nia, maisha, mtu mzima. Kuwa
na badiliko la moyo ni kuyatoa mapenzi yetu yote kutoka katika mambo ya ulimwengu
huu, na kuyakaza kwa Yesu. Kuwa na moyo mpya ni kuwa na nia mpya, makusudi
mapya, sababu mpya za kufanya mambo yetu. Ishara ya moyo mpya ni nini? ----- Ni
maisha yaliyobadilika. -----
4BC 1164,1165.
JIHADHARI USIWE NA MOYO MGUMU Juni 3
Kwa maana ndiye Mungu wetu, Na sisi tu watu wa malisho yake, Na kondoo za mkono
wake. Ingekuwa heri leo msikie sauti yake! Msifanye migumu mioyo yenu; kama vile
kule Meriba, kama siku ya Masa [majaribu] jangwani. Zaburi 95:7,8.
Hakuna mtu ye yote anayeweza kuzitumia nguvu zake alizopewa na Mungu kuitumikia
dunia hii au kiburi bila kujiweka mwenyewe upande wa yule adui.... Kila dhambi
inayorudiwa tena na tena huzidhoofisha nguvu zake za kuipinga, hupofusha macho yake,
na kuizima dhamiri yake inayomshuhudia....
Bwana anatupelekea maonyo, mashauri, na makaripio, ili tupate wasaa wa
kuyarekebisha makosa yetu kabla hayajageuka na kuwa tabia yetu ya pili. Lakini
tukikataa kukosolewa, basi, Mungu haingilii kati ili kuipinga mielekeo yetu mibaya ya
mwenendo tuliyoichagua. Hafanyi mwujiza wo wote ili mbegu ile iliyopandwa isiweze
kuota na kuzaa matunda. Mtu yule anayeonyesha moyo mgumu wa ukafiri au aliye na
hisia zisizoonekana kwa urahisi za kutoijali kweli ya Mungu, anavuna tu mazao yale
aliyopanda yeye mwenyewe. Huo umekuwa ni uzoefu wa watu wengi. Wanasikiliza kwa
moyo wa ukakamavu usiojali kweli zile ambazo zamani ziliisisimua sana mioyo yao.
Walipanda mbegu za kuipuuzia, kutoijali, na kuipinga kweli; na hayo ndiyo mavuno
wanayovuna. Ubaridi kama barafu, ugumu kama chuma, tabia ya mwamba usiopenyeka,
usioweza kugandamizwa ----- yote hayo hupata sehemu yake inayofanana na tabia ya
wengi wanaojiita Wakristo. Ilikuwa ni kwa njia hiyo Bwana aliufanya moyo wa Farao
kuwa mgumu. Mungu alisema na mfalme yule wa Misri kwa kinywa cha Musa akitoa
ushahidi ulio dhahiri mno wa uweza wake kama Mungu; lakini mfalme yule kwa
ushupavu wa moyo aliikataa nuru ile ambayo ingemfikisha kwenye toba! Munguhakupeleka nguvu fulani ya kimwujiza kuufanya moyo wa mfalme huyo mwasi kuwa
mgumu, bali Farao kadiri alivyozidi kuipinga kweli, ndivyo kadiri Roho Mtakatifu
alivyozidi kuondolewa kwake, naye alibaki katika giza na mashaka aliyokuwa
amejichagulia mwenyewe. Kwa kuendelea daima kuukataa uongozi wa Roho, wanadamu
wanajitenga wenyewe mbali na Mungu. Katika akiba yake hana njia nyingine zaidi yenye
nguvu ya kuwaelimisha watu. Hakuna ufunuo wa mapenzi yake unaoweza kuwafikia
katika hali yao ya kutokuamini. ----- RH, Juni 20, 1882.
Kanuni ile isiyoweza kukunjwa itaonyesha kwa dhahiri njia ya wale wanaoketi miguuni
pake Yesu na kujifunza kwake. ----- RH, Juni 20, l882.
KAZI YA KUULINDA MOYO Juni 4
Linda moyo wako kuliko yote uyalindayo; Maana ndiko zitokako chemchemi za uzima.
Mithali 4:23.
Kuulinda moyo kwa bidii ni muhimu ili kukua vizuri katika neema. Moyo katika hali
yake ya asili ni makao ya mawazo machafu na tamaa mbaya za mwili. Unapoletwa chini
ya utawala wa Kristo, hauna budi kutakaswa na Roho kutokana na uchafu wake wote.
Jambo hilo haliwezi kufanyika bila kibali cha mtu mwenyewe.
Moyo unapokuwa umekwisha takaswa, ni wajibu wa Mkristo huyo kuulinda
usichafuliwe. Wengi wanaonekana kufikiri ya kwamba dini ya Kristo haiwataki watu
kuachana na dhambi zao za kila siku, kuzivunja tabia zao ambazo zimeushikilia moyo
katika hali ya utumwa. Wanakataa baadhi ya vitu vinavyolaumiwa na dhamiri, lakini
wanashindwa kumwakilisha Kristo katika maisha yao ya kila siku. Hawaileti tabia
inayofanana na ile ya Kristo nyumbani mwao. Hawaonyeshi uangalifu wa makini katika
kuchagua maneno yao. Mara nyingi sana, maneno ya wasiwasi, ya harara yanasemwa,
maneno yanayochochea hasira kali za moyo wa kibinadamu. Watu kama hao wanahitaji
kuwako kwake Kristo kunakodumu ndani ya mioyo yao. Ni katika nguvu zake tu
wanaweza kuweka ulinzi juu ya maneno na matendo yao.
Katika kazi hii ya kuulinda moyo tunapaswa kudumu katika maombi, tusichoke kutoa
dua zetu kwenye kiti kile cha neema kuomba msaada. Wale wanaolichukua jina la
Mkristo wangepaswa kumwendea Mungu kwa bidii na unyenyekevu wakimsihi sanaawasaidie.... Mkristo hawezi kuwa mahali pake pa sala sikuzote, lakini mawazo na
shauku yake vinaweza kuelekezwa juu sikuzote. ----- 3BC 1157.
Kuuweka moyo wako mbinguni kutayatia nguvu matendo yako yote na kuzifufua kazi
zako zote. Juhudi zetu ni dhaifu, nasi tunapiga mbio katika mbio zile za Kikristo
polepole, na kuonyesha uzembe na uvivu, kwa sababu tunaithamini kidogo sana thawabu
ile ya mbinguni. Sisi tumedumaa katika mambo ya kiroho. Ni haki na wajibu wa Mkristo
kuzidi kukua katika kumjua Mwana wa Mungu, "hata kuwa mtu mkamilifu." ----- 3BC
1157.
NI NANI ANAYEYAONGOZA MAISHA YANGU? Juni 5
Ee Mungu, unichunguze moyo wangu, unijaribu, uyajue mawazo yangu; Uone kama iko
njia iletayo majuto ndani yangu, Ukaniongoze katika njia ya milele. Zaburi 139:23,24.
Mungu anawaongoza watu wake, hatua kwa hatua. Anawaleta mahali mbalimbali
palipokusudiwa kuyafunua makusudi yaliyo moyoni mwao. Wengine hustahimili mahali
pamoja, bali huanguka panapofuata. Kwa kila hatua ya kusonga mbele moyo unapimwa,
na kujaribiwa kwa karibu zaidi. Iwapo watu wo wote wale wanaona mioyo yao
inapingana na kazi hii nyofu ya Mungu, basi, iwahakikishie kwamba wanayo kazi ya
kufanya katika kupata ushindi, vinginevyo, hatimaye watakataliwa na Bwana.
Dunia hii ni mahali pa kujiweka tayari ili kuonekana mbele zake Mungu. Watu mmoja
mmoja watadhihirisha hapo kwamba ni nguvu gani inayoigusa mioyo yao, na
kuyaongoza matendo yao.... Kama wanakithamini kitu kingine cho chote kuliko ile kweli,
basi, mioyo yao haiko tayari kumpokea Yesu, na matokeo yake anafungiwa nje. Iwapo
watu mmoja mmoja wanapopimwa, wanakataa kuachana na sanamu zao,.... Roho wa
Mungu atawaacha pamoja na tabia zao za dhambi bila kudhibitiwa, wapate kutawaliwa
na malaika wale waovu.
Wengi wanaojidai kuwa wafuasi wa Kristo hawako tayari kuichunguza mioyo yao kwa
karibu zaidi, ili kuona kama wamepita kutoka mautini kuingia uzimani. Wengine
wanategemea uzoefu wao wa zamani, wakionekana kana kwamba wanafikiri ya kuwakule kuikiri tu ile kweli kutaweza kuwaokoa, lakini Neno la Mungu linafunua ukweli wa
kuogofya kwamba hao wote wanalishikilia tumaini la uongo....
Vijana kwa wazee, Mungu anawapima sasa. Ni sasa mnakata shauri juu ya umilele wenu
ninyi wenyewe. Kiburi, mitindo ya kisasa, maongezi yasiyokuwa na maana, na uchoyo
[kujipenda nafsi] ni maovu ambayo yakitunzwa, yatazidi kuongezeka, na kuisonga ile
mbegu njema iliyopandwa mioyoni mwenu [isipate kuzaa matunda]. ----- RH, Aprili 8,
1880.
Hebu, sisi kama wafuasi wake Kristo, na tuichunguze mioyo yetu kama kwa mshumaa
uliowashwa ili kuona sisi ni watu wa roho [tabia] gani. Kwa faida yetu ya sasa na ile ya
milele, hebu na tuyakosoe matendo yetu, kuona yanasimamaje katika nuru ya Sheria ya
Mungu [Amri Kumi]. ----- 7BC 986.
Tunawahitaji wale watakaomfuata Kristo kabisa, ambao vichwa vyao, mikono yao,
masikio yao, na kila kiungo chao na uwezo walio nao vinatolewa wakf kwa Yesu. Si
uwezo wa pesa mfukoni, wala uwezo wa akili, bali ni uwezo wa moyo ambao sisi
tunauhitaji. ----- Letter 26, 1880.
ASKARI KATIKA UWANJA WA MAPAMBANO WA MAISHA Juni 6
Piga vita vile vizuri vya imani; shika uzima ule wa milele ulioitiwa, ukaungama
maungamo mazuri mbele ya mashahidi wengi. 1 Timotheo 6:12.
Watu wanapoongoka, wokovu wao bado haujakamilika. Kuanzia hapo hawana budi
kupiga mbio; pambano lile linalohitaji nguvu zao li mbele yao ili wapate ku"piga vita vile
vizuri vya imani."... Pambano hilo ni la maisha yote, nalo halina budi kuendelezwa mbele
kwa juhudi thabiti kulingana na thamani ya lengo unalotaka kulifikia, ambalo ni uzima
wa milele....
Daima Shetani anatafuta kutuangamiza; anakitupa kivuli chake cha kishetani katikati ya
roho zetu na nuru ile ya Jua la Haki. Unapoongea juu ya mashaka yako, na kutoutegemea
upendo wa Baba yako aliye mbinguni, basi, Shetani anaingia na kuiimarisha hisia hiyo
ndani ya moyo wako, na kile alichokiweka kama kivuli hugeuka na kuwa giza nene la
kukata tamaa. Sasa, tumaini lako la pekee ni kuacha kuongea juu ya mambo yale
yanayokuletea giza. Unapoongea sana juu ya upande ule wa giza, unautupilia mbaliujasiri wako kwa Mungu, na jambo hilo ndilo hasa analolitaka Shetani kwamba ulifanye.
Anataka kukupepeta kama ngano; lakini Yesu anakuombea; upendo wake ni mpana, tena
una kina kirefu. Pengine wewe utasema hivi, "Unajuaje kuwa ananipenda mimi?" Mimi
natazama kule unakoweza kutazama wewe, yaani, kwenye msalaba ule wa Kalvari.
Damu ile iliyomwagika msalabani inasafisha dhambi zote....
Kila siku tunafanya kazi kwa ajili ya maisha yetu ya baadaye. Tunayo taji ile ya uzima
wa milele kuipata, na jehanum kuikwepa. Ni kweli hatuwezi kujiokoa wenyewe, na
tunajua kwamba Kristo anataka sisi tuokolewe. Alijitoa nafsi yake mwenyewe ili alipe
fidia kwa ajili ya roho zetu. Anapotoa kafara hiyo isiyo na kifani, yeye hatuangalii sisi
kama mtu asiyetujali....
Sisi tunataka kuing'ang'ania ile Njia, Kweli, na Uzima.... Tunaye Mwokozi aliye hai,
Mwombezi wetu aliye hai, Mmoja atakayetusaidia kila wakati tutakapokuwa na shida.
Unapojaribiwa kuingia katika pango lile lenye giza la mashaka na kukata tamaa, imba
hivi:
"Amka, roho yangu, amka!
Tupilia mbali hofu zako zilizojaa hatia;
Mbele ya kiti kile cha enzi
Mdhamini wangu anasimama;
Jina langu limeandikwa
Katika vitanga vya mikono yake."
----- Letter 9a, 1891.
JUMBA LA KIFALME LA MAISHA MATAKATIFU Juni 7
Bali ninyi ni mzao mteule, ukuhani wa kifalme, taifa takatifu, watu wa milki ya Mungu
[watu wa pekee - KJV], mpate kuzitangaza fadhili zake yeye aliyewaita mtoke gizani,
mkaingie katika nuru yake ya ajabu. 1 Petro 2:9.Kanisa la Kristo hapa duniani li katikati ya giza la kimaadili la ulimwengu huu usiotii,
ambao unaikanyaga chini ya miguu yao Sheria ya Yehova [Amri Kumi]. Lakini
Mkombozi wao, ambaye amewanunua kwa kulipa fidia ya damu yake ya thamani,
amefanya maandalizi yote ili kanisa lake liwe mwili wake uliobadilika, ulioangazwa kwa
Nuru ile ya Ulimwengu, ukiwa na utukufu ule wa Imanueli. Mionzi ing'aayo ya Jua la
Haki, ing'aayo kupitia kwa Kanisa lake, itamkusanya katika zizi lake kila kondoo
aliyepotea, anayetangatanga, ambaye atakuja kwake na kupata kimbilio ndani yake.
Watapata amani na nuru na furaha ndani yake yule ambaye ndiye Amani na Haki milele.
----- 7BC 968.
Washiriki wa kanisa hilo kila mmoja angeiruhusu nuru ya upendo wa Mungu kung'aa
vizuri moyoni mwake, ili ipate kuwaangazia na wengine pia. Tunakabiliwa na hatari
kubwa sana tunapouruhusu uchovu wa kiroho kuja juu yetu. Hebu na tujihadhari
tusiikaribishe roho ile ya kutopendelea ibada zetu za kidini na majukumu yetu ya kidini.
Hebu na tupige vita kwa ushupavu mkubwa dhidi ya ulegevu wa roho zetu ambao ni wa
kufisha kuhusiana na ukuaji [wetu wa kiroho] au hata maisha yetu ya Kikristo. Kanisa
lile litakuwa na afya na mafanikio ambalo washiriki wake wanafanya juhudi yao
wenyewe kwa vitendo kuwatendea mema wengine, kuziokoa roho. Hilo litakuwa
kichocheo cha kudumu kwa kila kazi njema. Wakristo kama hao watafanya kazi kwa
bidii zaidi kujipatia wokovu wao wenyewe. Nguvu zao ambazo hazitumiki zitaamshwa
na kutiwa nguvu, moyo wote utavuviwa na kuwa na ari isiyoshindikana ili wajipatie
hongera kutoka kwa Mwokozi, atakayesema, "Vyema," na ili wapate kuivaa ile taji ya
mshindi. ----- ST, Jan. 12, 1882.
Kristo analifanya kanisa lake kuwa hekalu zuri kwa ajili ya Mungu. "Kwa kuwa walipo
wawili watatu wamekusanyika kwa jina langu," akasema, "nami nipo papo hapo katikati
yao." Mathayo 18:20. Kanisa lake ni Jumba la Kifalme la Maisha Matakatifu, limejazwa
na vipawa mbalimbali, na kupewa kipawa cha Roho Mtakatifu. Majukumu yanayopasa
amepewa na Mbingu kila mshiriki wa kanisa hilo duniani humu, na wote hawana budi
kupata furaha yao katika furaha ya wale wanaowasaidia na kuwaletea mibaraka. ----- ST,
Machi 1, 1910.
NDANI YA KARAKANA YAKE MUNGU Juni 8
Ninyi nanyi, kama mawe yaliyo hai, mmejengwa mwe nyumba ya Roho, ukuhani
mtakatifu, mtoe dhabihu za roho, zinazokubaliwa na Mungu, kwa njia ya Yesu Kristo. 1
Petro 2:5.Hekalu lile la Kiyahudi lilijengwa kwa mawe yaliyochongwa kutoka milimani; na kila
jiwe lilitayarishwa kukaa mahali pake katika Hekalu lile, likiwa limechongwa, na
kulainishwa, na kupimwa, kabla ya kulileta Yerusalemu. Na wakati ule yalipoletwa yote
kwenye eneo lile, jengo lilipanda juu bila kusikika sauti ya shoka wala nyundo. Jengo lile
linaliwakilisha Hekalu la Mungu la Kiroho, ambalo limejengwa kutokana na vifaa
vilivyokusanywa kutoka katika kila taifa, na lugha, na watu, wa kila daraja, yaani, wa
daraja la juu na wa lile la chini, matajiri kwa maskini, wasomi kwa wasiojua kusoma.
Hao sio vifaa vilivyokufa, vinavyopaswa kutayarishwa kwa nyundo na patasi. Wao ni
mawe yaliyo hai, wamechimbuliwa kutoka ulimwenguni kwa njia ya ile kweli; na Mjenzi
Mkuu, Bwana wa Hekalu, sasa anawachonga na kuwalainisha, akiwatayarisha kila
mmoja kwa mahali pake katika hekalu lile la kiroho. Likiwa tayari, hekalu hilo litakuwa
kamili katika sehemu zake zote, litapendwa na malaika pamoja na wanadamu; kwa
maana Mjenzi na Mtengenezaji wake ni Mungu. ----- 2BC 1029.
Uangalifu ulioonyeshwa katika kulijenga hekalu lile ni fundisho kwetu kuhusu uangalifu
tunaopaswa kuuonyesha katika ujenzi wa tabia zetu. Vifaa duni vyo vyote havikutakiwa
kutumika. Kazi ya ovyo ovyo yo yote haikutakiwa kufanyika wakati wa kuunganisha
sawasawa sehemu zake mbalimbali. Kipande kimoja sharti kiungane sawasawa na
kipande kingine kwa ukamilifu. Kama vile lilivyokuwa hekalu lile la Mungu, ndivyo
linavyopaswa kuwa kanisa lake. Katika ujenzi wao wa tabia watu wake hawatakiwi
kuleta mbao zo zote zisizofaa, wala kazi yo yote ya kizembe, iliyofanyika pasipo kujali. -
---- 2BC 1030.
Hivi sasa tumo ndani ya karakana yake Mungu, na kazi inaendelea mbele katika saa hizi
za kipindi hiki cha majaribio ili kututayarisha sisi kwa ajili ya hekalu lile tukufu. Hivi
sasa hatuwezi kuwa kama watu wasiojali, wala wanaopuuzia mambo, wala wazembe,
wala kukataa kuachana na dhambi,... na wakati uo huo kutazamia kwamba sisi tutakuwa
na tabia ile inayofanana na Jumba hilo la Kifalme.... Sasa ndio wakati wa kujiweka
tayari; sasa ni wakati tunapoweza kuondolewa kasoro zetu. ----- Letter 60, 1886.
Jiwe lisilong'aa halifai kitu. Kile ambacho kinayafanya makanisa yetu kuwa na thamani
sio mawe yale yaliyokufa, yasiyong'aa, bali ni mawe yale yaliyo hai, mawe ambayo
yanaweza kuipokea mionzi inayong'aa kutoka kwa lile Jiwe Kuu la Pembeni, yaani, yule
Jua la Haki [Kristo]. ----- 6BC 1116.
MIBARAKA YA USHIRIKA WA KIKRISTO Juni 9 Wala tusiache kukusanyika pamoja, kama ilivyo desturi ya wengine; bali tuonyane; na
kuzidi kufanya hivyo, kwa kadiri mwonavyo siku ile kuwa inakaribia. Webrania 10:25.
Wale walio wa nyumba ya imani wasipuuzie kamwe kukusanyika pamoja; maana hiyo
ndiyo njia aliyoichagua Mungu ya kuwaongoza watoto wake katika umoja, ili kwa njia ya
upendo na ushirika wa Kikristo wapate kusaidiana, kuimarishana, na kutiana moyo wao
kwa wao....
Sisi kama ndugu za Bwana wetu, tumeitwa kwa mwito mtakatifu kuishi maisha
matakatifu, ya furaha. Tukiisha ingia katika njia ile nyembamba ya utii, hebu na
tujiburudishe mioyo yetu kwa kuongea sisi kwa sisi na pamoja na Mungu wetu. Kadiri
tunavyoiona siku ya Bwana kuwa inakaribia, hebu na tukusanyike mara kwa mara
kujifunza Neno lake na kuonyana ili tupate kuwa waaminifu mpaka mwisho.
Mikusanyiko hii ya hapa duniani ni njia aliyoichagua Mungu ambayo kwayo tunapata
fursa ya kuzungumza sisi kwa sisi na kupata msaada wote unaowezekana ili kujiandaa,
kwa njia iliyo sahihi, kupokea kutoka katika mikusanyiko ile ya mbinguni utimilizo wa
ahadi zile za urithi wetu.
Kumbuka kwamba katika kila kusanyiko unakutana naye Kristo, Bwana wa
mikusanyiko. Tianeni moyo ili kila mmoja apate kuyaangalia mambo ya wengine; kwa
maana haitoshi kuwafahamu watu kwa juu juu tu. Yatupasa kuwafahamu watu KATIKA
KRISTO YESU. Tunaagizwa ku"angaliana sisi kwa sisi." Hiki ndicho kitovu cha injili.
Kitovu cha ulimwengu huu ni nafsi. ----- Letter 98, 1902.
Ningependa kuwatia moyo wale wanaokusanyika katika makundi madogo madogo ili
kumwabudu Mungu. Ndugu na dada, msikatishwe tamaa kwa vile ninyi ni wachache kwa
idadi. Mti unaosimama peke yake kwenye uwanda, unaizamisha mizizi yake chini sana
ya ardhi, unatandaza matawi yake mbali kila upande, na kukua ukiwa na nguvu na
ulinganifu mzuri wakati unaendelea peke yake kupigana mieleka na dhoruba au
unafurahia mwangaza wa jua. Hivyo ndivyo Mkristo, akiwa ametengwa mbali ili asipate
kuutegemea ulimwengu huu, hapo ndipo anaweza kujifunza kumtegemea Mungu kabisa,
naye anaweza kupata nguvu na ujasiri kutokana na kila pambano [analokutana nalo].
Bwana na awabariki hao waliotawanyika na kukaa katika hali ya upweke, na kuwafanya
watenda kazi wake wanaofaa. ----- ST, Jan. 12, 1882.NI MOJA NA KANISA LILILOKO JUU Juni 10
Kwa hiyo nampigia Baba magoti, ambaye kwa jina lake ubaba wote wa [familia yote ya
- KJV] mbinguni na wa [ya] duniani unaitwa. Waefeso 3:14,15.
Kanisa la Mungu hapa duniani ni moja na kanisa la Mungu lililoko juu. Waumini hapa
duniani, na wale ambao hawajawahi kuanguka dhambini walioko mbinguni, ni kanisa
moja. Kila mwenye hekima wa mbinguni anapendezwa na mikusanyiko ya watakatifu,
ambao hapa duniani wanakutana kumwabudu Mungu katika roho na kweli, na katika
uzuri wa utakatifu. Ndani ya Majumba yale ya Kifalme kule mbinguni wanasikiliza
ushuhuda unaotolewa na mashahidi wake Kristo walioko katika ua wa nje ulio hapa
duniani, na sifa na shukrani zitokazo katika kanisa la chini, huchukuliwa juu katika
wimbo wa kumsifu Mungu, na sifa na shangwe huvuma katika Majumba yote ya Kifalme
yaliyoko kule mbinguni kwa sababu Kristo hakufa kifo cha bure [kisichokuwa na faida
yo yote] kwa ajili ya wana wa Adamu walioanguka. Malaika wanapokunywa maji yale
kutoka kwenye Chimbuko [Mwanzo] la chemchemi ile, watakatifu walioko duniani
hunywa maji yao kutoka katika vijito safi vinavyotiririka kutoka kwenye kiti cha enzi cha
Mungu, vikiufurahisha mji wa Mungu.... [Ufunuo 22:1,2; Zaburi 46:4].
Katika kila kusanyiko la watakatifu hapa chini, malaika wa Mungu wanasikiliza
shukrani, sifa, dua za watu wa Mungu zinazotolewa kwa njia ya ushuhuda wao, nyimbo
zao, na maombi yao. Hebu na wakumbuke ya kwamba sifa zao zinaungwa mkono na
kwaya za majeshi yale ya malaika kule juu...
Kundi la waumini huenda likawa na idadi ndogo sana ya watu [wanaokusanyika pale],
lakini hao wametwaliwa na yule Mpasuaji-Mawe wa ile Kweli kama mawe yanayoparuza
kutoka kwenye machimbo ya ulimwengu huu... kutayarishwa kwa kupimwa na maonjo ili
kupewa nafasi yao katika hekalu la Mungu lililoko mbinguni, nao ni wa thamani sana
machoni pake Bwana.... Hata katika hali yao ya kuparuza wana thamani machoni pake
Mungu. Shoka na nyundo na patasi ya maonjo na kupimwa kwao viko mkononi mwa
yule Mmoja aliye Bingwa, na vinatumika si kwa kusudi la kuangamiza, wala si kufanya
pasiwe na kitu cho chote cha kufaa, bali kutenda kazi kwa ajili ya utimilifu wa
[kumkamilisha] kila mtu....
Bwana hataweza kumtupilia mbali muumini ye yote katika Kristo aliye mnyenyekevu na
duni kabisa kama vile asivyoweza kukivunjilia mbali kiti chake cha enzi. Sisi
tunakubalika katika yule Mpendwa wetu [Kristo]. Sisi ni jamii ya familia ile ya kifalme,
watoto wa Mfalme yule wa mbinguni, warithi wa Mungu, na warithi-wenzi pamoja na
Yesu Kristo. ----- MS 32a, 1894MKUTANO WA THAMANI KULIKO YOTE Juni 11
Ndipo wale waliomcha BWANA waliposemezana wao kwa wao. Naye BWANA
akasikiliza, akasikia; na kitabu cha ukumbusho kikaandikwa mbele zake, kwa ajili ya hao
waliomcha BWANA, na kulitafakari jina lake. Malaki 3:16.
Hii ni picha inayotia matumaini ilioje, inayomwonyesha Bwana akiinama chini na
kusikiliza ushuhuda unaotolewa na mashahidi wake!...
Maneno ambayo Mungu na malaika huyasikiliza kwa furaha ni maneno yale ya
kukithamini kipawa kile kikuu ambacho kimetolewa kwa ulimwengu huu katika
Mwanawe wa pekee. Kila neno la sifa kwa mbaraka ule wa nuru ya kweli yake...
limeandikwa katika kumbukumbu zile za mbinguni. Kila neno linalokiri rehema za pendo
lake Baba yetu aliye mbinguni kwa kutupa Yesu ili kuziondoa dhambi zetu, na
kutuhesabia haki yake, limeandikwa katika kitabu chake cha ukumbusho. Shuhuda kama
hizo "[hu]zitangaza fadhili zake yeye aliyewaita mtoke gizani mkaingie katika nuru yake
ya ajabu." 1 Petro 2:9....
Muda wenyewe [uliowekwa] na majira yake ni vya thamani sana. Waumini
waliokusanyika pamoja wamo katika Chumba cha Kusikilizia Mambo cha ulimwengu ule
wa mbinguni. Wanapaswa kutoa ushuhuda wao kwa ajili ya Mungu na Bwana Yesu
Kristo aliyejitoa nafsi yake kwa ajili ya ulimwengu huu.... Ni umuhimu wa kina na uzito
ulioje anaouambatanisha na mikusanyiko hiyo midogo! Yesu Kristo amekwisha lipa
fedha ya fidia kwa njia ya damu yake mwenyewe kwa ajili ya roho zao, naye yu katikati
yao wanapokutana kumwabudu Mungu. Mfalme huyo Mtukufu wa mbinguni
anayafunganisha mambo yake na mambo ya waumini wale [wanaokusanyaka pamoja]
haidhuru mazingira yao duni yaweje. Na po pote wanapobahatika kukutana pamoja,
yafaa kwamba wasemezane mara kwa mara wao kwa wao, wakitoa shukrani na upendo
wao kutokana na kulitafakari kwao jina lake Bwana. Hivyo ndivyo Mungu
atakavyotukuzwa anaposikiliza na kusikia, na mkutano huo wa ushuhuda utaangaliwa
kama ni wa thamani kuliko mikutano yote....
Hebu na tukumbuke kwamba... malaika wanaandika katika Kitabu kile cha Ukumbusho
kila neno linalothibitisha tabia na utume wa Kristo. Kwa habari ya wale wanaotoa
ushuhuda wao juu ya upendo wa Mungu, Bwana asema, "Nao watakuwa wangu,... katika
siku ile niifanyayo; naam, watakuwa hazina yangu hasa." Malaki 3:17. ----- MS 32, 1894.UMOJA KWA KUTOFAUTIANA Juni 12
Mwili [Kanisa] mmoja, na Roho mmoja, kama na mlivyoitwa katika tumaini moja la
wito wenu mlioitiwa;... Mungu mmoja, naye ni Baba wa wote, aliye juu ya yote na katika
yote na ndani ya yote. Lakini kila mmoja wenu alipewa neema kwa kadiri ya kipimo cha
kipawa chake Kristo. Waefeso 4:4-7.
Umoja kwa kutofautiana ndio mpango wake Mungu. Miongoni mwa wafuasi wake
Kristo panatakiwa kuwapo mchanganyiko mzuri wa watu wanaohitilafiana, mmoja
akipatana na mwingine, na kila mmoja akifanya kazi yake maalum kwa ajili yake Mungu.
Kila mtu anapo mahali pake katika kujaza mpango huo mkuu ulio na muhuri wa sura
yake Kristo.... Mmoja anatayarishwa kufanya kazi fulani, mwingine ana kazi iliyo tofauti
ambayo ameandaliwa kuifanya, mwingine ana mkondo wa kazi ulio tofauti; lakini kila
mmoja anatakiwa aikamilishe kazi ya wale wengine.... Roho wa Mungu, akifanya kazi
yake ndani ya na kupitia kwa watu mbalimbali, ataleta umoja katika utendaji....
Panatakiwa kuwapo roho moja tu inayoongoza ----- Roho wake yule aliye na hekima
isiyo na kifani, na ambaye ndani yake vitu vyote mbalimbali hukutana katika umoja
unaopendeza, usio na kifani....
Tofauti katika tabia zipo kwa asili, bali umoja wetu hutegemea kiwango tunachojitoa
wenyewe ili kuongozwa na Roho wa Mungu. Kwa njia ya neema yake Kristo, watu
wengine wana tabia za thamani, yaani, upole na uungwana; makaripio yao yamejawa na
upendo, kwa kuwa Roho wake Kristo anaonekana wazi ndani yao.... Uweza wa neema
yake utaiumba upya na kuibadilisha tabia kulingana na Kielelezo kile cha Mbinguni
[Kristo], ukiifanya iwe mpya katika ulaini na uzuri wake, ipate kufanana na sura yake
mwenyewe iliyo takatifu....
Ni tofauti kuu ilioje inayoonekana katika ulimwengu wa asili! Kila kitu kina mazingira
yake ya pekee ya utendaji; lakini vyote vinaonekana kuwa vimeunganishwa pamoja na
kuwa kitu kikubwa, kizima kimoja. Kristo Yesu ana umoja na Baba yake, na kutoka
katika kitovu hicho kikuu umoja huu wa ajabu unatakiwa kuenea... katika talanta za aina
yote pamoja na tofauti zake. Sisi sote hatuna budi kuziheshimu talanta za kila mmoja
wetu; tunatakiwa kuafikiana katika wema, mawazo na matendo yetu yasiyokuwa na
uchoyo [ubinafsi] ndani yake, kwa kuwa Roho wake Kristo, kama mjumbe aliye hai,
hutenda kazi yake, akizunguka kupitia katika mwili [kanisa] wote.... Si matendo yaleyanayovutia macho sana ambayo yanaleta umoja; ni ule uumbaji wa Roho Mtakatifu juu
ya tabia yetu. ----- Letter 78, 1894.
KUUNGANA KATIKA KRISTO Juni 13
Wote na wawe na umoja; kama Wewe, Baba, ulivyo ndani yangu, nami ndani yako; hao
nao wawe ndani yetu; ili ulimwengu upate kusadiki ya kwamba wewe ndiwe
uliyenituma.
Yohana 17:21.
Sala ile nzito, ya dhati aliyotoa Kristo... inatufikia hadi siku zetu. Hicho ni cheo kilioje
kwa mwanadamu aliyeanguka kuweza kukifikia kwa njia ya utii ----- umoja na Mungu
kwa njia ya Yesu Kristo! Ni kimo kilichoje tunachoruhusiwa kukifikia kama
tutaiheshimu ile fidia itakayotupatia malipo ya thawabu ile kuu! Yatupasa kupokea nguvu
kutoka kwa Mungu ili tabia hii ya kibinadamu, chini ya utendaji wake Mungu, isiendelee
kubaki potovu sikuzote, wala isiwe chini ya mvuto ule mwovu, na mchafu wa dhambi.
Tabia ya kibinadamu, kwa njia ya Yesu Kristo, inaweza kupatana na ile ya malaika -----
naam, hata na ile ya Mungu Mkuu. -----
MS 43, 1891.
Wale waliounganishwa na Mungu kweli kweli hawatahitilafiana wao kwa wao.... Roho
wake akitawala mioyoni mwao ataleta amani, upendo, na umoja. Kinyume cha hayo
kinatenda kazi ndani ya watoto wa Shetani; kwao kuna kupingana kunakoendelea daima.
Ugomvi na husuda na wivu ni tabia zinazotawala. Tabia ya Mkristo ni upole ule wa
Kristo. Ukarimu, upole, rehema, na upendo hutoka kwa yule Mwenye Hekima isiyokuwa
na kifani, ambapo kinyume chake ni tunda lile la dhambi la moyo ambao haupatani na
Yesu Kristo.... Katika umoja kuna nguvu. Kutengana kunaleta udhaifu na kushindwa. ----
- MS 2, 1881.
Hoja inayowashawishi sana watu ambayo tunaweza kuitoa kwa ulimwengu kwa habari
ya utume wake Kristo inapatikana katika umoja ulio mkamilifu.... Kwa kiwango cha
umoja wetu pamoja na Kristo ndivyo itakavyokuwa nguvu yetu ya kuziokoa roho. -----
MS 88, 1905.Iwapo tunaweza kukifikia kiwango hicho cha ukamilifu, basi, tabia zetu za ajabu tulizo
nazo hazina budi kufanywa upya kufananishwa na mapenzi yake Kristo. Hapo ndipo sisi
tutakapoketi pamoja katika ulimwengu wa roho ndani ya Kristo. Ndugu watafanya kazi
pamoja, pasipokuwa na wazo lo lote la kugongana. Tofauti ndogo, zikiongelewa sana,
huwafanya watu kutenda matendo yanayoharibu ushirika wa Kikristo.... Hebu na tuzidi
kumkaribia Mungu zaidi, naye atatukaribia. Hapo ndipo, sisi kama mtu mmoja, tutapanda
juu kwenda kwake. Makanisa yatakuwa kama bustani za Mungu [Edeni], chini ya
utunzaji wake. Watu wa Mungu watakuwa miti ya haki, iliyopandwa na Bwana, na
kumwagiliwa kwa maji yale ya mto ule wa uzima. ----- Letter 141, 1902.
UNDUGU MMOJA MKUBWA Juni 14
Basi ndugu, nawasihi, kwa jina la Bwana wetu Yesu Kristo, kwamba nyote mnene
mamoja; wala pasiwe kwenu faraka, bali mhitimu katika nia moja na shauri moja. 1
Wakorintho 1:10.
Tunaye Bwana mmoja, imani moja, ubatizo mmoja. Injili yake Kristo inapaswa
kuwafikiria watu wa tabaka zote, mataifa yote, lugha zote na watu wote. Mvuto wa injili
unatakiwa kuwaunganisha wote katika undugu mmoja mkubwa. Tuna mmoja tu aliye
Kielelezo chetu ambaye tunapaswa kumwiga katika kujenga tabia zetu, na hapo sisi sote
tutafanana na Kristo; tutakuwa na umoja mtimilifu; mataifa yatachanganyika vizuri
katika Kristo Yesu, wakiwa na nia ile ile, na shauri lile lile, wakinena mamoja, na kwa
kinywa kimoja wakimtukuza Mungu. Hii ndiyo kazi ambayo Mkombozi wa ulimwengu
atatufanyia sisi. Iwapo tunaipokea kweli kama ilivyo katika Yesu, basi, kiburi cha kitaifa
na wivu wake vitavunjwa-vunjwa, na yule Roho wa kweli ataiunganisha mioyo kuwa
mmoja. Tutapendana kama ndugu; tutawahesabu wengine kuwa ni bora kuliko sisi
wenyewe; tutakuwa wakarimu na wenye adabu, wapole na wanyenyekevu wa moyo,
wepesi kusihiwa; waliojaa huruma na matunda mema....
Mungu anajua jinsi ya kushughulika na tabia za ajabu za mataifa mbalimbali.... Ujumbe
wa malaika wa tatu... utawaunganisha watu kufanya kazi maalum, kuwaandaa wawe na
tabia kamilifu ili kujiunga katika familia moja kubwa katika makao yale ambayo Kristo
amekwenda kuandaa kwa ajili ya wale wampendao....Kweli yake ina nguvu na inafika mbali sana. Itayaunganisha mataifa katika undugu
mmoja mkubwa.... Kristo ndani ya wanadamu anawaunganisha katika jukwaa moja
kubwa, akifanya maandalizi ya kuwaunganisha katika familia moja mbinguni. Ni ile
kweli inayowafanya wanadamu kuwa umoja na kuondoa kiburi cha kitaifa....
Kweli itakuwa na uwezo ule ule wa kuiumba upya mioyo ya watu haidhuru wawe wa
mataifa gani. Kila moyo wa kibinadamu unaoipokea kweli utasujudu chini ya utukufu wa
mvuto wake, na Kristo anapokaa moyoni mwao kwa imani watakuwa na nia moja, maana
Kristo hajagawanyika. Watakuwa na nguvu katika nguvu zake, wenye furaha na
walioungana katika amani yake. Kweli ni ile ile katika uwezo wake uadibishao juu ya
mioyo yote. Itautakasa na kuufanya mwema zaidi moyo wa yule anayeipokea. ----- MS
12, 1886.
USHINDI DHIDI YA KILA ADUI Juni 15
Katika neno la kweli, katika nguvu ya Mungu; kwa silaha za haki za mkono wa kuume
na za mkono wa kushoto. 2 Wakorintho 6:7.
Kupitia katika vizazi vile vya giza la kimaadili, katika karne zile za migongano na
mateso, Kanisa la Kristo limekuwa kama mji uliojengwa juu ya kilima. Toka kizazi hadi
kizazi, kupitia katika vizazi vilivyofuatana mpaka wakati huu wa sasa, mafundisho safi
ya Biblia yamekuwa yakifunuliwa ndani ya mipaka yake. Kanisa la Kristo, japokuwa
linaweza kuonekana kana kwamba limedhoofika na kuwa na dosari, ni kitu kimoja hapa
duniani ambacho kwa maana ile ya pekee [Mungu] anaweka juu yake upendo wake na
kukistahi. Kanisa ni Jumba la Upasuaji la [Thieta ya] neema yake, ambamo anapendezwa
kufanya majaribio ya rehema yake juu ya mioyo ya wanadamu.
Kanisa ni ngome ya Mungu, yaani, Mji wake wa makimbilio, ambayo anaishikilia katika
ulimwengu huu ulioasi. Usaliti wo wote wa amana zake takatifu ni uhaini kwake yeye
aliyelinunua kwa damu ya thamani ya Mwanawe pekee. Katika historia ya ulimwengu
huu toka mwanzo mpaka sasa, watu walio waaminifu wamekuwa sehemu ya kanisa hilo
hapa duniani....
Leo hii, kama zamani, mbingu yote inaangalia ili kuliona kanisa hilo likikua katika
sayansi ya kweli ya wokovu.... Kisto anatuita tupate kuingia katika njia ile nyembamba,
ambamo kila hatua inamaanisha kujikana nafsi. Anatuita kusimama juu ya jukwaa lakweli ile ya milele, na kuishindania, naam, kuishindania kwa bidii imani ile
waliyokabidhiwa watakatifu mara moja tu....
Tunapoukaribia wakati ule... uwezo wa madanganyo wa Shetani utakapokuwa mkubwa
sana hata, yamkini, angeweza kuwadanganya wale walio wateule, uwezo wetu wa
kupambanua mambo hauna budi kuwa mkali kwa njia ya nuru ile itokayo kwa Mungu, ili
tusikose kuzijua hila zake Shetani. Hazina yote ya mbinguni inangoja amri yetu katika
kazi hii ya kutengeneza njia ya Bwana. ----- ST, Machi 1, 19l0.
Ni mpango wa Mungu kwamba kanisa lake daima lisonge mbele katika utakatifu na
maarifa, toka nuru hata nuru, toka utukufu hata utukufu. ----- RH, Des. 4, 1900.
Tumaini letu si kwa mwanadamu, bali ni kwa Mungu wetu aliye hai. Kwa hakika
timilifu ya imani, tunaweza kutazamia kwamba Yeye ataunganisha uweza wake usio na
kikomo na juhudi za vyombo vyake vya kibinadamu, kwa ajili ya utukufu wa jina lake.
Tukiwa tumevikwa silaha ya haki yake, tunaweza kupata ushindi dhidi ya kila adui. -----
PK 111.
MNYORORO WA DHAHABU WA UPENDO Juni 16
Amri mpya nawapa, Mpendane. Kama vile lnilivyowapenda ninyi, nanyi mpendane
vivyo hivyo. Hivyo watu wote watatambua ya kuwa ninyi mmekuwa wanafunzi wangu,
mkiwa na upendo ninyi kwa ninyi. Yohana 13:34,35.
Upendo wa Kristo ni mnyororo wa dhahabu unaowafunga kwa Mungu wa milele
wanadamu wasiodumu milele, ambao wanamwamini Yesu Kristo. Upendo alio nao
Bwana kwa watoto wake unapita ufahamu wetu. Hakuna sayansi yo yote inayoweza
kuufafanua wala kutoa sababu yake. Hakuna hekima yo yote ya kibinadamu inayoweza
kuupima kina chake. ----- 5BC 1141.
Uchoyo [kujipenda nafsi] na kiburi huzuia upendo huo safi unaotuunganisha kiroho na
Yesu [usiweze kufanya kazi]. Iwapo upendo huo utakuzwa kweli, basi, mwanadamu
ataunganishwa vizuri na mwanadamu mwenzake, na wote kitovu chao kitakuwa ndani ya
Mungu yule wa milele. Ubinadamu utaunganika na ubinadamu, na wote
watafungamanishwa pamoja na moyo ule wa Mungu aliye upendo. Upendo uliotakasika,
kila mmoja kwa mwenzake, ni wa kuheshimiwa sana. Katika kazi hii kuu upendo waKikristo, kila mmoja kwa mwenzake, ----- ni wa juu zaidi, unadumu zaidi, ni wa heshima
zaidi, hauna uchoyo, kuliko wo wote ule uliopata kuonekana ----- unatunza kanuni za
huruma ya Kikristo, ukarimu wa Kikristo, na upole, na kuukumbatia undugu wa
kibinadamu katika mikono ya Mungu, ukionyesha hadhi ambayo Mungu amezizingira
haki za mwanadamu. ----- 5BC 1140.
Mnyororo huo wa dhahabu wa upendo, ukiifunga mioyo ya waumini katika umoja,
katika vifungo vya ushirikiano na upendo, na katika umoja wao pamoja na Kristo na
Baba, hukifanya kiungo hicho kuwa kikamilifu na hutoa ushuhuda kwa ulimwengu juu
ya nguvu ya Ukristo ambayo haiwezi kupingwa.... Hapo ndipo uchoyo utakapong'olewa
na kutokuwa waaminifu hakutakuwapo. Hapatakuwa na magomvi wala mafarakano.
Hapatakuwa na ukaidi ndani ya mtu awaye yote ambaye amefungamanishwa na Kristo.
Hakuna hata mmoja wao atakayeonyesha kwa matendo yake hali yake ya ushupavu ya
kujitegemea mwenyewe, kama ile aliyo nayo mtoto mtukutu, mwenye harara, ambaye
anauachilia mkono ule unaomwongoza na kuchagua kutembea kwa kujikwaa akiwa peke
yake na kutembea katika njia zake mwenyewe. ----- Letter 110, 1893.
Upendo ni mmea mwororo sana, unapaswa kukuzwa na kutunzwa, na mizizi ile
inayoleta uchungu ni lazima ing'olewe yote kuuzunguka mmea huo ili upate nafasi ya
kuzunguka huku na huko, hapo ndipo utaleta chini ya mvuto wake nguvu zote za akili,
moyo wote, hata tutaweza kumpenda Mungu kwa moyo wote, na jirani yetu kama nafsi
zetu wenyewe. ----- MS 50, 1894.
CHINI YA NIRA YAKE KRISTO Juni 17
Yeye ampendaye ndugu yake, akaa katika nuru, wala ndani yake hamna kikwazo. 1
Yohana 2:10.
Shetani, kwa njia ya majaribu yake, anatafuta kuwadanganya watu. Usiruhusu jambo lo
lote unaloweza kufanya au kusema limletee mtu mwingine awaye yote majaribu au
kukatishwa tamaa. Kumbuka kwamba yeye amenunuliwa kwa damu yake Kristo. Kila
mtu ni wa thamani. Ni wakati ule tu unapoutazama msalaba wa Kalvari unapoweza
kukadiria kwa usahihi thamani ya mtu mmoja. Lingekuwa ni jambo la kusikitisha jinsi
gani kumfanya mtu ayumbe na kwenda katika njia mbaya kutokana na kile ufanyacho au
usemacho. Umefungwa kwa Mungu na kwa mwanadamu mwenzako kwa kamba zauwajibikaji; huwezi kuzikata kamba hizo na kujiweka huru mbali na uwajibikaji huo. ----
- Letter 13a, 1879.
Usisumbuke kufikiria yale watu wengine wanayofikiri au kusema, ... bali wewe
umng'ang'anie Bwana; hatakuangusha kamwe.... Daima tunapaswa kukumbuka kwamba
Shetani anafanya kazi yake kwa bidii kutaka kumnasa kila mtu. Sisi hatuna budi kufanya
kazi yetu tukiwa upande wa Bwana, tusimpe nafasi hata kidogo mtu ye yote
kutudanganya.... Kama maneno yanasemwa na shutuma zinatolewa ili kukuchokoza
wewe, basi, kemeo kali sana unaloweza kutoa ni kunyamaza kimya, kana kwamba
hujasikia.... Sisi sote yatupasa kukumbuka kwamba tuko chini ya nira yake Kristo, nasi
hatupaswi kumwaibisha Mwokozi wetu au kuitweza nira yake aliyotualika kuivaa. Kama
vile tunavyoivaa nira yake, hivyo ndivyo tutakavyoitawala mioyo yetu. ----- Letter 117,
1899.
Yale wawezayo kufanya wengine, yale wawezayo kusema wengine, yale wawezayo
kukufikiria wengine, hayataweza kuyageuza mawazo ya Mungu aliyo nayo kwako.
Atendaye haki yuna haki, wala maoni ya mwanadamu [mwingine ye yote] hayataweza
kuibadilisha tabia yake.... Yesu anakupenda; wala yeye hachukui tathmini ya tabia yako
iliyofanywa na mwanadamu ye yote. Wewe huna budi kumtazama Yesu na kuakisi sura
yake. Utafakari upendo wake katika mawazo yako. Mkaribishe Mgeni huyo wa mbinguni
apate kukaa pamoja nawe....
Moyo wenu na utakaswe kutokana na uchafu wote wa kidunia, mawazo yote machafu,
yasiyokuwa na wema wo wote ndani yake. Maneno yenu na yawe safi, yaani, matakatifu,
yawe ya kuwatia nguvu na kuwaburudisha wote mnaoshirikiana nao. Msiwe wepesi wa
kukasirika. Acheni sifa ya Mungu iwe moyoni mwenu na kinywani mwenu, ili jambo lo
lote ovu kwa ukweli lisiweze kusemwa juu yenu. ----- Letter 102, 1899.
MBUBUJIKO WA UPENDO Juni 18
Wapenzi na tupendane; kwa kuwa pendo latoka kwa Mungu, na kila apendaye
amezaliwa na Mungu, naye anamjua Mungu. 1 Yohana 4:7.
Kanuni ya mbinguni ya upendo wa milele inapoujaza moyo, itabubujika na kwenda kwa
wengine, sio tu kwa sababu tumepokea upendeleo fulani kutoka kwao, bali kwa sababu
upendo ndiyo kanuni ya utendaji, nao unaifanya tabia kuwa nzuri zaidi, unatawala hisiaza moyoni, unatawala tamaa za mwili, unaudhibiti uadui, na kuyakuza mapenzi yetu.
Upendo huu haujapunguka, yaani, kiasi cha kunihusisha "mimi na vyangu" tu, bali ni
mpana kama ulimwengu huu ulivyo, nao unakwenda juu kama mbingu ilivyo. Unapatana
na ule wa malaika watendao kazi. Upendo huu, ukihifadhiwa moyoni, unayafanya maisha
yetu yote kuwa matamu, na kutoa mvuto utakasao kwa wote wanaotuzunguka. Tukiwa
nao, hatuwezi kukosa kuwa na furaha, hata kama bahati itatuchekelea ama itatukunjia
uso. Na iwapo tunampenda Mungu kwa moyo wetu wote, basi, yatupasa kuwapenda
watoto wake pia. Upendo huu ni roho ya Mungu. Ni pambo la mbinguni ambalo
linatupatia ukuu na heshima ya kweli moyoni mwetu. -----
YI, Des. 23, 1897.
Moyo uliojazwa na upendo wa Yesu unatoa mchango mwema kwa maneno, tabia,
mwonekano, tumaini, ujasiri, na utulivu.... Unaamsha shauku ya kutaka maisha yaliyo
bora; roho zilizo tayari kuzimia zinatiwa nguu; wale wanaopambana na majaribu
wataimarishwa na kufarijika. Maneno, usemi, tabia, hutupa nje mwonzi unaong'aa wa
mwanga wa jua, na kuacha nyuma yao njia inayoonekana wazi ya kwenda mbinguni....
Kila mmoja wetu anazo nafasi nyingi za kuwasaidia wengine. Daima tunaacha picha
inayowaathiri vijana wanaotuzunguka. Mwonekano wa uso wetu wenyewe ni kioo cha
maisha yaliyo ndani yetu. Yesu anatamani kwamba sisi tuwe kama alivyo yeye
mwenyewe, tukiwa tumejazwa na huruma nyingi, tukiwa tunatoa huduma yetu ya upendo
katika kazi zetu ndogo ndogo za maisha haya....
Wajibu wetu ni kuishi katika mazingira ya upendo wake Kristo, kuvuta hewa nyingi sana
ya upendo wake, na kuakisi joto lake kutuzunguka. Lo, ni upeo mpana ulioje wa mvuto
wetu ulio wazi mbele yetu! Ni kwa uangalifu jinsi gani tungeipalilia bustani ya roho zetu,
ili kwamba ipate kuzaa maua ya aina ile tu iliyo safi, ya kupendeza, yenye harufu nzuri!
Maneno ya upendo, upole, na fadhili huutakasa mvuto wetu kwa wengine. ----- MS 24,
1887.
KAMBA LAINI INAYOIFUNGA MIOYO PAMOJA Juni 19
Tumikianeni kwa upendo. Wagalatia 5:13.
Upendo ndiyo kamba ile laini inayoifunga mioyo pamoja. Haitupasi kujisikia kwamba
tunalazimika kujiweka wenyewe kama kiolezo [mfano]. Kadiri sisi tunavyozidikujifikiria wenyewe na kile tunachostahili kupata kutoka kwa wengine, ndivyo
itakavyokuwa vigumu sana kwetu kuweza kufanya kazi yetu ya kuziokoa roho za watu.
Yesu anapoitawala kabisa mioyo yetu hatutaweza kuendelea tena kujiwekea mduara
finyu wa nafsi zetu kuwa ndicho kitovu cha mawazo yetu na usikivu wetu.
Ni heshima ya ajabu ilioje aliyoionyesha Yesu kwa maisha ya kibinadamu katika utume
wa maisha yake. Hakusimama kama mfalme miongoni mwa watu, akidai watu
wamwangalie yeye, wamche yeye, wamtumikie yeye, bali kama mmoja aliyekuwa na
shauku ya kutumika, na kuwainua wanadamu. Alisema kwamba hakuja kutumikiwa bali
kutumika.... Po pote pale Kristo alipomwona mwanadamu, alimwona mtu aliyehitaji
huruma kutoka kwa wanadamu wenzake. Wengi wetu tuko tayari kuwatumikia watu
fulani maalum ----- wale tunaowaheshimu ----- lakini wale hasa ambao Kristo angetutaka
sisi kuwa mbaraka kwao kama tusingekuwa na mioyo baridi, wakali, na wachoyo, sisi
tunawapita na kuwaona kama watu wasiostahili kuangaliwa na sisi....
Fundisho kuu la msamaha linapaswa kujifunzwa kwa ukamilifu zaidi na sisi sote.... Kosa
kubwa sana tunaloweza kuwatendea wengine ni lile la kutowasamehe kama tunafikiri
kwamba wametudhuru kwa njia yo yote ile. Huo ni msimamo wa hatari mno kwa yule
anayejiita Mkristo, kwa sababu kwa jinsi ile ile anavyowatendea ndugu zake, ndivyo
naye Bwana atakavyomtendea.
Tunahitaji kuwa na mawazo ya juu zaidi na yaliyo dhahiri zaidi kuhusu tabia yake
Kristo. Haitupasi kumfikiria Mungu kama hakimu tu na kumsahau kwamba yeye ni Baba
yetu atupendaye. Hakuna kitakachozidhuru roho zetu sana kuliko hicho, maana maisha
yetu yote ya kiroho yanaumbwa upya kutokana na dhana [fikira] zetu juu ya tabia yake
Mungu. Tunayo mafundisho ya kujifunza kwa habari ya upendo wake Kristo. ----- MS
35, 1886.
"Hivyo mfuateni Mungu, kama watoto wanaopendwa; mkaenende katika upendo, kama
Kristo naye alivyowapenda ninyi tena akajitoa kwa ajili yetu, sadaka na dhabihu kwa
Mungu, kuwa harufu ya manukato." Waefeso 5:1,2. Hicho ndicho kimo cha upendo
tunachotakiwa kukifikia. Asili ya upendo huo haijatiwa waa lo lote la uchoyo [haina
ubinafsi wo wote]. ----- MS 1, 1899.MSAADA KWA YULE ANAYEPOTEA Juni 20
Ndugu zangu, mtu akighafilika katika kosa lo lote, ninyi mlio wa Roho mrejezeni upya
mtu kama huyo kwa roho ya upole, ukijiangalia nafsi yako usije ukajaribiwa wewe
mwenyewe.
Wagalatia 6:1.
Hapa kuna agizo maalum la kuwashughulikia kwa upole wale walioghafilika katika
kosa. "Akighafilika" lazima liwe na maana yake kamili.... Kuingizwa katika dhambi
pasipo kujua ----- sio kukusudia kutenda dhambi, bali kutenda dhambi kwa kukosa
kukesha na maombi, pasipo kulitambua jaribu la Shetani na kwa sababu hiyo kuanguka
katika mtego wake ----- jambo hilo ni tofauti kabisa na yule anayepanga na kwa
makusudi kabisa anajiingiza katika majaribu na kupanga njia ya kuitenda dhambi hiyo....
Hatua za kufaa zaidi zinahitajika ili kuizuia dhambi ya makusudi, lakini mtume anaagiza
jinsi ya kuwashughulikia wale wanaoghafilika au wanaoshtuliwa au wanaoangushwa kwa
majaribu.... Mrejezeni upya kwa upole, "ukijiangalia nafsi yako usije ukajaribiwa wewe
mwenyewe." Imani na makaripio vitahitajika, na mashauri ya upole na dua kwa Mungu,
ili kuwafanya wajitambue wenyewe kwa kuwaonyesha hatari na dhambi yao. Neno la
asili ni 'rudisha kiungo mahali pake,' kama mfupa ulioteguka; kwa hiyo, juhudi na
zifanywe kuwarudisha mahali pao, na kuwafanya wajitambue kwa kuwahakikishia
dhambi yao na kosa lao.... Pasiwepo na kushangilia ko kote katika anguko la ndugu ye
yote. Bali kwa roho ya upole, kwa kumcha Mungu, kwa upendo kwa ajili ya roho zao,
tafuta jinsi ya kuwaokoa kutoka dhambini. ----- Letter 11, 1887.
Watu wanapolazimika kuogelea kinyume na mkondo wa maji ya mto, kuna uzito wa
mawimbi unaowarudisha nyuma. Hebu mkono na unyoshwe, kama ulivyonyoshwa
mkono wa Kaka yetu yule Mkubwa kwa Petro aliyekuwa anazama.... Hebu yule
anayedhaniwa kuwa ameenenda vibaya asipewe nafasi yo yote na ndugu yake ya kukata
tamaa, bali mwache ausikie mkono wa huruma ukimshika kwa nguvu; mwache asikie
mnong'ono usemao, "Na tuombe." Roho Mtakatifu atawapa uzoefu mkubwa sana wote
wawili. Ni maombi yanayoiunganisha mioyo. Ni maombi kwa yule Tabibu Mkuu ili
apate kuiponya roho ambayo yatamletea [mwenye dhambi huyo] mbaraka wa Mungu.
Maombi yanamleta Yesu kando yetu, na kumpa nguvu na neema mpya yule anayezimia,
mwenye mashaka, ili apate kuushinda ulimwengu, mwili, na mwovu. Maombi
yanayageuzia kando mashambulio ya Shetani. ----- Letter 50, 1897.KOSA MOJA KWA YAKE MIA MOJA Juni 21
Kisha Petro akamwendea akamwambia, Bwana, ndugu yangu anikose mara ngapi nami
nimsamehe? hata mara saba? Yesu akamwambia, Sikuambii hata mara saba, bali hata
saba mara sabini. Mathayo 18:21,22.
Kazi kubwa i mbele yetu. Kuna wanaume na wanawake wanaotangatanga mbali na zizi
la Kristo, nao wanapokuwa baridi na kutojali, na kupoteza ari yote ya kurudi,
hawatakukimbilia. Yakupasa kuwachukua pale pale walipo.... Ukimpata kondoo
aliyepotea, mwite aje zizini; nawe usimwache mpaka umwone salama salimini
amefungiwa mle.... Nenda nje ukawatafute kondoo wale waliopotea wa nyumba ya
Israeli.
Kama liko jambo moja ambalo kwalo wewe umefanya kosa moja, basi, liondoe kosa lile
ulilofanya katika njia yako na kufungua njia kwake ili apate kurudi tena. Huenda ndilo
lililokuwa kitu chenyewe [kipingimizi] kilichomzuia mtu huyo. Katika unyenyekevu
wako, ungama kosa lako hilo moja, pengine linaweza kumgusa na kumwongoza akiwa
analia na kuungama makosa yake mia moja, na kuyaondoa njiani. Hivyo roho ile aliyoifia
Kisto itakuwa imeokolewa....
Waweza kusema, Nimejaribu kumwokoa huyu hapa na yule kule, nao wamenijeruhi tu,
nami sitaki kujaribu tena kuwasaidia. Lakini usikate tamaa kama hawarudi zizini MARA
MOJA. Zidi kutoka na kuwaendea wanadamu wenzako wanaokuzunguka. Utavuna
usipozimia. ----- Undated MS 141.
Iweni na mshikamano. Msiweke tofauti zenu ndogo ndogo za maoni kuwa kabari
zinazowatenganisha, na kuzipigilia sana ili kuutenganisha moyo na moyo, bali angalieni
jinsi mnavyoweza kupendana ninyi kwa ninyi kama vile Kristo alivyowapenda.
Angalieni jinsi mnavyoweza kuwasamehe wale wanaowakosea, kama vile mnavyotaka
Baba yenu aliye mbinguni awasamehe makosa yenu. Hapo ndipo mnapoweza kuwa na
maombi ya hakika; mnaweza kuwa na ujasiri ndani yake Kristo; kwa kuwa Kristo
anayawakilisha maombi yenu kwa Mungu yakiwa na vitambulisho vile vya mbinguni
ambavyo ni haki yake mwenyewe, nanyi mnaweza kusadiki kwamba Kristo anasikia,
kusadiki kwamba anawabariki, na kusema, "Mimi ni wake, na yeye ni wangu." ----- MS
12, 1891. HESHIMA YOTE NI KWA WAPATANISHI! Juni 22
Heri wapatanishi; maana hao wataitwa wana wa Mungu. Mathayo 5:19.
Wapatanishi! Ni hazina ilioje mpatanishi akiwamo katika familia; ni mbaraka ulioje
ndani ya kanisa! Wapatanishi wanaweza kujaribiwa, bali maisha yao yamefichwa pamoja
na Kristo katika Mungu. Wanamtazama Yesu, na kuiga mfano wake... Wanapokea amani
anayowapa Kristo...
Hali halisi ya dini yetu haipatikani katika cheo tunachokalia, bali katika roho ile ya
uungwana, upole, amani, ambayo sisi tunaionyesha. Dini yetu inadhihirika nyumbani
mwetu kwa hali ile inayomzunguka mtu yule anayeleta furaha kwa familia....
Wakristo wa kweli... hawatasema kwa njia ya kujidhalilisha wala kwa wasiwasi. Katika
mazingira ya kawaida ya nyumbani watatoa huduma za upendo na heshima ya Kikristo.
Huduma hizi zinaweza kuonekana kama za kawaida sana, bali ulimwengu ule wa
mbinguni utapendezwa kuona mwenendo mnyofu wa wale wanaotaka kuwanufaisha
wengine....
Si haki yetu tu bali ni wajibu wetu kukuza tabia ya upole, kuwa na amani ya Kristo
moyoni, na kama wapatanishi na wafuasi wake Kristo, kupanda mbegu za thamani
zitakazotoa mavuno kuelekea kwenye uzima ule wa milele. Wanaojiita wafuasi wake
Kristo wanaweza kuwa na sifa nyingi nzuri na zenye manufaa; lakini tabia zao
zinaharibiwa sana na ukali, kuwa na wasiwasi, kuwatafuta makosa wengine, na
kuwahukumu wengine kwa ukali. Mume au mke anayekuwa na shuku na mashaka
analeta faraka na ugomvi nyumbani. Wote wawili wasingesema maneno ya upole na
kutabasamu kwa wageni tu, wala wasingeonyesha harara nyumbani mwao, kwa njia hiyo
kuweza kuifukuzilia nje amani na ridhaa....
Ni kule kufanana na Kristo peke yake kunakoweza kumfanya mtu kuwa mpatanishi
nyumbani, kanisani, katika ujirani, na ulimwenguni. Dini ya nyumbani ni utakaso kwa
njia ya matendo.... Hali halisi ya dini hupimwa kwa namna ambavyo kila mshiriki katika
familia anavyofanya wajibu wake kwa wenzake.... Jifunzeni fundisho hili la thamani la
kuwa wapatanishi katika maisha yenu ya nyumbani. ----- Letter 34, 1894.HAKUNA TABAKA KWA MUNGU Juni 23
Ndugu zangu, imani ya Bwana wetu Yesu Kristo, Bwana wa utukufu, msiwe nayo kwa
kupendelea watu. Yakobo 2:1.
Maovu yanayopatikana katika jamii ya ulimwengu huu kamwe, kamwe yasipate kibali
miongoni mwa Wakristo.... Mungu anataka wewe uukunjue mkono wako kwa wahitaji
[maskini], na kuwa na huruma nyingi sana kwa wale wanaoteswa, au wanaoteseka kwa
njaa....
Kama ninyi mnayo roho yake Kristo, basi, mtapendana kama ndugu; mtamheshimu
mfuasi aliye duni katika nyumba yake ya kimaskini, kwa kuwa Mungu anampenda yeye
sawasawa na vile anavyowapenda ninyi, na huenda akawa anampenda zaidi. Haitambui
tabaka yo yote ya watu. Anaweka muhuri wake juu ya wanadamu, si kwa kufuata vyeo
vyao, si kwa mali waliyo nayo, si kwa akili nyingi sana walizo nazo, bali ni kwa umoja
wao na Yesu. Ni usafi ule wa moyo, yaani, unyofu wa makusudi yao, unaowafanya
wanadamu kuwa na thamani ya kweli kwake.... Wote wanaoishi kwa njia ya kuwa na
mawasiliano ya kila siku na Kristo, watawathamini wanadamu kama vile
anavyowathamini Yeye. Watawaheshimu wale walio wema na safi, japokuwa hao wawe
maskini wa mali ya dunia hii.... Kupenda sana mali, kujipenda nafsi, na uchoyo ni ibada
ya sanamu, na mambo hayo yanamvunjia heshima Mungu.... Upole, huruma, na ukarimu
ni maagizo waliyopewa Wakristo.---- RH, Okt. 6, 1891.
Tungejifunza kukiiga Kiolezo [Mfano wetu], ili Roho yule aliyekaa ndani yake Kristo
apate kukaa ndani yetu. Mwokozi hakuonekana miongoni mwa wenye vyeo na
waheshimiwa wa ulimwengu huu. Hakutumia wakati wake miongoni mwa wale
waliotafuta raha na anasa. Alienda huku na huko akitenda mema. Kazi yake ilikuwa ni
kuwasaidia wale waliohitaji msaada, kuwaokoa wale waliopotea na wanaoangamia,
kuwainua waliokandamizwa, kuivunja nira ya ukandamizaji kwa wale waliokuwa
kifungoni, kuwaponya wagonjwa, na kusema maneno ya huruma na faraja kwa waliokata
tamaa na wenye huzuni. Sisi tunatakiwa kukiiga Kiolezo hicho. Hebu na tuamke na
kuanza kufanya kazi, tukitafuta kuwabariki wahitaji na kuwafariji wale waliokata tamaa.
Kadiri tunavyoshiriki roho ile ya Kristo, ndivyo tutakavyoona mambo ya kufanya kwa
ajili ya wanadamu wenzetu. Tutajazwa na upendo kwa roho zile zinazoangamia, nasi
tutaipata furaha yetu kwa kufuata nyayo zake Mfalme yule Mtukufu wa mbinguni. -----
MS 1, 1869.NG'OA MIMEA YENYE SUMU Juni 24
Zaidi ya yote iweni na juhudi katika kupendana; kwa sababu upendano husitiri wingi wa
dhambi. 1 Petro 4:18.
Kifungo kile kinachotufunga sisi kingetubana kwa karibu sana na kwa ulaini jinsi gani!
Tungekuwa waangalifu jinsi gani ili maneno na matendo yetu yaweze kupatana na kweli
zile takatifu ambazo Mungu ametukabidhi!...
Mazungumzo yenu na yawe ya aina ile ambayo hamtakuwa na haya kuyajutia.... Kama
neno limetolewa ambalo linaathiri tabia ya rafiki au ndugu, usiuendeleze usengenyaji
huo; maana hiyo ndiyo kazi ya yule adui. Mkumbushe msemaji kwamba Neno la Mungu
linakataza maongezi kama hayo.... Mkombozi wetu ametuambia sisi namna tunavyoweza
kumdhihirisha kwa ulimwengu huu. Tukiwa na roho yake, tukionyesha kwa wengine
upendo wake, tukilinda mambo ya kila mmoja wetu, tukiwa wapole, wavumilivu,
wastahimilivu, basi, matunda tunayozaa yataupa ulimwengu ushahidi kwamba sisi tu
watoto wa Mungu.... Kujengana sisi kwa sisi katika imani hii takatifu sana ni kazi yenye
baraka; kuraruana ni kazi iliyojaa uchungu na huzuni....
Tungetafuta kuufanya mzigo wa kila mmoja wetu kuwa mwepesi kwa kuonyesha
upendo wa Yesu kwa wale wanaotuzunguka. Iwapo maongezi yetu yangekuwa juu ya
mbingu na mambo ya mbinguni, basi, masengenyo yangekoma upesi kuwa na mvuto wo
wote kwetu. Basi tusingekuwa tunaiweka miguu yetu juu ya eneo la hatari; wala
tusingejiingiza majaribuni, tukianguka chini ya nguvu za yule mwovu.
Badala ya kutafuta makosa ya wengine, hebu na tujikosoe wenyewe. Kila mmoja
angejiuliza mwenyewe, Hivi moyo wangu uko sawa mbele zake Mungu? Je, hivi
ninamtukuza Baba yangu aliye mbinguni? Kama umekuwa na roho mbaya, iondoe
moyoni mwako. Futa moyoni mwako kila kitu kilicho kichafu. Ng'oa kila mzizi wa
uchungu, ili wengine wasije wakaathirika kwa mvuto wako mbaya. Usiache mmea hata
mmoja wenye sumu kubaki katika udongo wa moyo wako. Ung'oe saa hii hii, na mahali
pake otesha mmea ule wa upendo. Hebu Kristo na atawazwe katika hekalu la moyo
wako.... "Tukipendana Mungu hukaa ndani yetu, na pendo lake limekamilika ndani yetu."
1 Yohana 4:12. ---- RH, Feb. 25, 1904.KUSAIDIANA SISI KWA SISI Juni 25
Kwa hiyo kadiri tupatavyo nafasi na tuwatendee watu wote mema; na hasa jamaa ya
waaminio. Wagalatia 6:10.
Katika mpango wake Bwana wanadamu wamefanywa kuwa wa maana kila mmoja kwa
mwenzake. Iwapo wote wangefanya kila wanaloweza kuwasaidia wale wanaohitaji
msaada wao, kwa kuonyesha huruma na upendo wao usio na uchoyo [ubinafsi], ni kazi
ya mibaraka ilioje ambayo ingeweza kufanyika. Kwa kila mmoja Mungu amemkabidhi
talanta. Talanta hizo tunapaswa kuzitumia kusaidiana sisi kwa sisi ili tupate kutembea
katika njia ile nyembamba. Katika kazi hiyo kila mmoja ameunganishwa kwa mwingine,
na wote wameunganishwa na Kristo. Ni kwa njia ya huduma hiyo isiyo na uchoyo sisi
tunaweza kuziendeleza na kuziongeza talanta zetu.
Washiriki wa kanisa la Mungu humu duniani ni kama sehemu mbalimbali za mashine,
zote zina uhusiano wa karibu sana kila moja kwa nyingine, na zote zikiwa zina uhusiano
wa karibu sana zinakitegemea kitovu kikuu kimoja. Panatakiwa kuwapo na umoja katika
kutofautiana. Hakuna mshiriki wa shirika lake Bwana anayeweza kufanya kazi yake kwa
ufanisi akiwa anajitegemea mwenyewe, yaani, akijitenga mbali na wengine.... Wote
wanatakiwa kuutumia uwezo wao waliokabidhiwa katika kazi yake, ili kila mmoja apate
kutumika kwa ajili ya utimilifu wa wote. Kila mmoja anatakiwa kufanya kazi yake chini
ya usimamizi wa Mungu.
Kwa njia ya muungano wa ajabu wa uungu na ubinadamu wa Kristo, tunahakikishiwa ya
kwamba hata katika dunia hii sisi tunaweza kuwa washirika wa tabia ya uungu.... Kristo
ameahidi yeye mwenyewe kutufundisha kuwa watenda kazi pamoja naye. Atatusaidia sisi
kufuata mfano wake, tukitenda mema na kukataa kutenda mabaya. Sisi tunatakiwa kuwa
vyombo vilivyowekwa wakf ambavyo kwa hivyo upendo wa Kristo unatiririka kwenda
kwa wale wanaohitaji msaada....
Kristo anaituma nuru yake kwa wale wanaoacha wazi madirisha ya roho zao kuelekea
mbinguni. Chini ya uongozi wa Roho Mtakatifu, wanafanya kazi zake Mungu. Yule
anayekaribia sana kwenye utii wa Sheria ya Mungu [Amri Kumi] atamtumikia Mungu
vizuri sana. Anayemfuata Kristo, akinyosha mkono wake kupokea wema wake, huruma
zake, upendo wake kwa familia ya kibinadamu, atakubaliwa na Mungu kama mtenda kazi
pamoja naye. Mtu kama huyo hataridhika kubaki katika daraja la chini la maisha ya
kiroho. Daima atazidi kupanda juu zaidi na zaidi. ----- Letter 115, 1903NEEMA YA KUWA NA HURUMA Juni 26
Basi imetupasa sisi tulio na nguvu kuuchukua udhaifu wao wasio na nguvu, wala
haitupasi kujipendeza wenyewe. Warumi 15:1.
Tunachohitaji sisi sote ni moyo wa huruma ulio safi zaidi, unaofanana na ule wa Kristo;
si huruma kwa wale walio wakamilifu ----- hao hawaihitaji ----- bali huruma kwa
maskini, kwa wale wanaoteseka, kwa wanaojitahidi ambao mara nyingi wanaghafilika
katika makosa, wakitenda dhambi na kutubu, wakijaribiwa na kukatishwa tamaa. Kazi ya
neema ni kuulainisha na kuudhibiti moyo. Hapo ndipo ubaridi huo wote unaozuia watu
kukaribiana unapoyeyuka, yaani, [moyo] unalainishwa, na Kristo anaonekana.
Upendo wa Mungu peke yake unaweza kuufungua na kuupanua moyo, na kuupatia
upendo na huruma upana wake na kimo chake pasipo kipimo. Wale wanaompenda Yesu
watawapenda watoto wote wa Mungu. Kutambua udhaifu na upungufu wa mtu
mwenyewe kutamwongoza mjumbe huyo wa kibinadamu kutazama mbali na nafsi yake
mwenyewe kwa Kristo; na upendo wa Mwokozi utakivunjilia mbali kila kizuizi cha
ubaridi, yaani, cha Kifarisayo, utaufukuzilia mbali ukali wote na uchoyo [ubinafsi], na
kutakuwa na kuungana kwa moyo na moyo, hata pamoja na wale walio tofauti katika
tabia yao.
Wema na uvumilivu wake Mungu, upendo wake wa kujitoa mhanga kwa wanadamu
wenye dhambi, hauna budi kuwaongoza wote wanaoitambua neema yake kuonyesha
tabia zizo hizo, kuonyesha huruma kwa wingi kwa wengine. Kielelezo cha ajabu cha
maisha yake Kristo, upole usio na kifani uliomwezesha kuingia katika hisia za
waliosetwa rohoni mwao, kulia pamoja na wale waliolia; kufurahi pamoja na wale wote
waliofurahia upendo wake, kinaweza kuwa na mvuto wenye kina juu ya tabia ya wote
wampendao Mungu na kuzishika amri zake.
Wataonyesha huruma yao, sio kwa shingo upande, bali kwa wingi; kwa maneno na
matendo ya upole watajaribu kuifanya njia kuwa rahisi kwa miguu ile iliyochoka kama
wanavyotaka njia iwe kwa miguu yao. Tunapopokea kila siku na kila saa mibaraka ya
Mungu, hatuwezi kufanya chini ya hapo kuonyesha shukrani zetu kuliko kuwa na upole,
na shauku kwa ajili ya wengine aliowafia Kristo. Je, tunayo mibaraka? Ndio, tunayo.
Vema, Kristo asema, Ipitisheni kwa wengine, sio kwa wachache tunaowapendelea, bali
kwa wote tunaokutana nao. Yatupasa kutoa neema kwa neema. ----- Letter 78, 1894."JIRANI YANGU NI NANI?' Juni 27
Kwa pendo la udugu, mpendane ninyi kwa ninyi; kwa heshima mkiwatanguliza
wenzenu.
Warumi 12:10.
Maisha ya Kikristo yanadhihirishwa kwa kuwa na mawazo ya Kikristo, maneno ya
Kikristo, na mavazi ya Kikristo. Ndani ya Kristo umo utimilifu wa tabia ya Mungu.
Ndani ya Kristo sisi tutatenda kazi zake Kristo. Ndani ya Kristo tutakitambua kifungo
chetu, yaani, wajibu mpana sana kwa Mungu na kwa mwanadamu mwenzetu.... Kuna
kamba nyingi zinazotuunganisha sisi kwa wanadamu wenzetu, yaani, kwa binadamu, na
kwa Mungu, na uhusiano huo ni wa maana pamoja na uzito wa majukumu yake. -----
Letter 13a, 1879.
Kadiri tunavyokaa duniani humu, hatuna budi kuunganishwa kila mmoja kwa
mwenzake. Sisi kama Wakristo tu viungo kila mmoja kwa mwenzake.... Mungu
ametuweka sisi kuwa wana na binti zake, ambao anawaita rafiki zake, ili tupate
kusaidiana sisi kwa sisi. Hii inatakiwa kuwa sehemu ya kazi yetu ya Kikristo kwa
matendo.
"Jirani yangu ni nani?"... Huyo ndiye hasa anayehitaji msaada wako kuliko wote. Ndugu
yako, mgonjwa kiroho, anakuhitaji wewe kama nawe ulivyomhitaji. Anahitaji uzoefu wa
yule ambaye amekuwa dhaifu kama yeye mwenyewe, anayeweza kumhurumia na
kumsaidia. Kule kuujua udhaifu wake mwenyewe humsaidia yule mwingine ili naye
amsaidie mwingine katika udhaifu wake.
Hebu na isitokee kwetu kwamba kamba zile za huruma, ambazo zingekuwa nyepesi
kutetemeka zikiguswa kidogo tu, ziwe baridi kama chuma cha pua, kana kwamba
zimeganda kwa baridi, nazo zisiweze kusaidia pale ambapo msaada unahitajika. -----
Letter 117, 1899.
Tafuta jinsi ya kuwasaidia, kuwatia nguvu, kuwabariki wale unaoshirikiana nao. Mungu
atakuwa na rehema kwa wale walio na rehema. Bwana atakuwa mpole na mwenye
kuwasikitikia wale wanaojizoeza upole na huruma na kuwasikitikia wengine. Yatupasakutambua kwamba sisi tumo katika shule yake Kristo, si kujifunza namna ya kujitukuza
wenyewe, yaani, jinsi ya kuenenda sisi wenyewe ili kupokea heshima ya wanadamu, bali
jinsi ya kuhifadhi unyenyekevu wake Kristo. Nafsi na kujipenda nafsi daima vitajitahidi
kututawala. Ni vita tunayolazimika kuwa nayo sisi wenyewe, ili nafsi yetu isitushinde.
Kwa njia ya Kristo tunaweza kushangilia ushindi; kwa njia ya Kristo tunaweza kushinda.
----- Letter 13a, 1879.
KATIKA NYAYO ZA YESU Juni 28
Kwa hiyo inyosheni mikono iliyolegea na magoti yaliyopooza, mkaifanyie miguu yenu
njia za kunyoka, ili kitu kilicho kiwete kisipotoshwe, bali afadhali kiponywe. Waebrania
12:12,13.
Ufanisi wa ufalme wa Shetani hupatikana katika kuziunganisha vizuri nguvu zote za
kishetani ili kueneza uambukizaji wa maovu; walakini Bwana Yesu amebuni mpango
ambao kwa huo anaweza kufanya kazi kuipinga kazi hiyo ya Shetani. Amekusudia
kuwajaza wajumbe wake wa kibinadamu, yaani, raia wa ufalme wake, na kanuni zile za
upendo na umoja. Kwa moyo uliotakasika wanatakiwa kujengana na kukiimarisha na
kukieneza kile kilicho chema. Wakiurudisha upendo wake Kristo, wanapaswa
kushughulika na mali ya mbinguni. Kanisa lake halina budi kuchukua Maandiko yake, na
kwa njia hiyo kuweza kushuhudia kwa ulimwengu ya kwamba Mungu alimtuma
Mwanawe kuwa Mwokozi wa ulimwengu huu.... Upendo unatakiwa kusukwa pamoja
kama nyuzi za dhahabu katika matendo yao yote.
Kila Mkristo anayemfurahia Bwana atafanya kazi yake kwa bidii, kuleta furaha ile ile
katika moyo na maisha ya yule aliye mhitaji na mtesekaji. Wafuasi wa Kristo wataifanya
furaha yao wenyewe iingie katika mioyo ya wengine kwa kufanya kazi kama zile za
Kristo. Wataueneza mvuto ulio safi, wa amani, na unaofanana na ule wa Kristo.
Watatenda kulingana na tabia zile za mbinguni, na kuzaa matunda yanayofanana na yale
ya mbinguni na ya aina ile ile. Kile wanachopanda watakivuna pia.
Ni jambo la maana kwamba kila mtu anayelitaja jina la Kristo aifanyie miguu yake njia
za kunyoka. Kwa nini? Ili viwete wasije wakapotoshwa. Ni jambo la kutisha , la kutisha
sana kuweza kumwonyesha mtu mfano mbaya, na kumwongoza katika njia potofu, kwa
jinsi wewe unavyoweza kuenenda.... Yo yote yale unayoyaona yanatendwa na wengine
ambayo akili yako inakuhakikishia kuwa hayafai kwa Mkristo, hakikisha kwamba wewe
hutendi kamwe mambo yanayofanana na yale.... Kadiri utakavyofuata nyayo za Yesu tu,
ndivyo wewe utakavyotembea salama salimini....Tunapaswa kuyaangalia makosa ya wengine si kwa kuwalaumu, bali kwa kuwarejesha
na kuwaponya. Kesheni katika sala, songeni mbele na kwenda juu, mkizidi kuwa na roho
ya Yesu zaidi na zaidi, na kuipandikiza roho iyo hiyo kando ya maji mengi. ----- Letter
89, 1894.
FURAHA KATIKA KUFANYA KAZI DUNI Juni 29
Lakini simama, uingie mjini, nawe utaambiwa yakupasayo kutenda. Matendo ya Mitume
9:6.
Si kitu hali yetu iweje au uwezo wetu uwe mdogo jinsi gani, tunayo kazi ya kufanya kwa
ajili ya Bwana wetu. Matendo yetu yanakuzwa na kukomazwa kwa kuyafanyia mazoezi.
Kweli ya Mungu inapowaka moyoni mwetu, hatuwezi kuwa wavivu. Furaha
tutakayoionja kwa kufanya kazi hata katika maisha haya itafidia kila juhudi yetu
tunayofanya. Ni wale tu walioionja furaha ile inayotokana na juhudi ya kujikana nafsi
katika kazi yake Kristo wawezao kusema juu ya jambo hili kwa ufahamu. Kwa kweli ni
furaha safi, yenye kina, ambayo lugha haiwezi kuieleza.
"... Kupitia katika siku ya maisha haya inayopita
Kuna kazi maalum iliyowekwa kwa ajili yako;
Huenda ikawa ya daraja la chini sana,
Huenda ikahitaji nguvu za hali ya juu sana kuifanya.
Bali hakuna mwingine zaidi ya wewe awezaye kuifanya kazi yako.
'Wataka nikufanyie kazi gani?' Ukiwa na jicho lako safi Kwa ajili ya utukufu wa
Mkombozi wako, Mfanyie kazi;
Ukiangazwa na nuru toka juu kwa kila dakika uliyo nayo,Jitahidi katika kila tendo lako kumtukuza Mungu,
Wala usiache wazo hata moja la ubinafsi
Kuipunguza nuru ya maisha yako."...
Tunaweza kuwa na Kristo pamoja nasi tunapofanya kazi zetu za ziada kila siku. Po pote
tulipo, katika shughuli yo yote ile tunayofanya, twaweza kuinuliwa juu kweli kweli kwa
kuwa sisi tumeunganishwa na Kristo. Tunaweza kuzifanya kazi zetu za maisha zilizo
duni mno kuwa bora sana na kutakaswa kwa njia ya ahadi ya upendo wa Mungu.
Ukifanya kazi kwa kufuata kanuni zinazotakiwa hata katika kazi iliyo duni sana
unaifanya iwe ya heshima. Kule kujua kwamba sisi ni watumishi wake Kristo kwa kweli
kutazipa kazi zetu za kila siku hadhi bora ----- daima tutakuwa wachangamfu,
wavumilivu, wastahimilivu, na wapole....
Wakikuona wewe kuwa unasimama imara juu ya kanuni, bila hofu katika kufanya kazi
yako, mwenye bidii katika kumtukuza Kristo katika kazi yako ya kila siku, ila ukiwa
mpole, mnyenyekevu na mwenye huruma, mvumilivu na mwenye kusamehe, ukiwa
tayari kuteswa na kusamehe majeraha [uliyoyapata kwa wengine], basi, hapo ndipo
utakapokuwa barua iliyo hai, ijulikanayo na kusomwa na watu wote. ----- Letter 9, 1873.
HAZINA YA THAMANI YA WAKATI Juni 30
Usiku umeendelea sana, mchana umekaribia, basi na tuyavue matendo ya giza, na
kuzivaa silaha za nuru. Warumi 13:12.
Kama sisi tutataka kuishiriki thawabu ile ya wenye haki mwishoni, basi, kwa hekima ni
lazima tuutumie vizuri wakati wetu huu wa majaribio [wa kupimwa]. Dakika hizi ni za
thamani kuliko dhahabu....
Kuja kwake Bwana kunakaribia. Tunao wakati mchache tu wa kujiweka tayari. Kama
nafasi hizi za thamani zinadharauliwa, basi, matokeo yake kwetu ni hasara ya milele.Tunahitaji kuwa na uhusiano wa karibu sana na Mungu wetu. Hatuko salama hata kwa
dakika moja isipokuwa kama tunaongozwa na kutawaliwa na Roho Mtakatifu....
Miezi ... inapita upesi. Hivi punde mwaka huu, pamoja na mizigo ya kumbukumbu zake,
utahesabiwa pamoja na wakati ule uliopita. Hebu na itumike miezi hii ya thamani
iliyobaki kwa kazi ya dhati na kwa juhudi kwa ajili yake Bwana wetu. Laiti kama
tungaliweza kuiona kumbukumbu iliyoandikwa kwa uaminifu kuhusu tulivyoitumia
tayari miezi iliyopita, je! kuiona [kumbukumbu hiyo] kungeturidhisha? Ondoa kila tendo
ambalo halikumfaidia mtu ye yote, ... ni kidogo jinsi gani inabaki kazi ile ya hiari,
iliyofanyika kwa utukufu wake Mungu! Je! kumbukumbu hiyo haitutii wasiwasi? Ni saa
ngapi za thamani zimetumika vibaya kwa kujifurahisha nafsi zetu! Mara ngapi, kwa
kujifurahisha wenyewe, tumeziachilia nafasi za kumtumikia Kristo!...
Maisha, pamoja na haki zake na nafasi zake za ajabu, yatakoma mara moja. Wakati wa
kufanya mambo yetu vizuri zaidi utakuwa umepita. Dhambi zetu zisizotubiwa sasa, na
kufutwa kwa damu ya Mwana-Kondoo, zitabaki katika leja ile ya mbinguni kutukabili
sisi katika siku ile inayokuja....
Maisha yetu ni mafupi. Vitu vya dunia hii vinachakaa kwa kuvitumia. Hebu na tuwe na
hekima, na kujenga kwa ajili ya umilele wetu. Hatuwezi kumudu kuzipoteza bure saa
zetu za thamani, wala kujiingiza katika shughuli nyingi ambazo hazitatuletea matunda yo
yote kwa ajili ya umilele wetu. Hebu wakati wetu tunaoutumia kwa kukaa kivivu, kwa
mambo yale yasiyokuwa na maana, kwa kuipenda dunia hii, na utumike kwa kujipatia
maarifa ya kuyajua Maandiko, kuboresha maisha yetu, na kuyabariki na kuyafanya kuwa
bora maisha na tabia ya watu wengine. Kazi hii itapata kibali cha Mungu, na kutupatia
mbaraka wa mwisho mbinguni wa "Vyema." ----- RH, Juni 15, 1886
ZAIDI, ZAIDI, ZAIDI! Julai 1
Utajiri na heshima ziko kwangu,
Naam, utajiri udumuo, na haki pia.
Matunda yangu hupita dhahabu,
naam, dhahabu safi, Na faida yangu
hupita fedha iliyo teule. Mithali 8:18,
19.
Mtu aliye mchoyo anazidi kuwa
mchoyo kadiri anavyoikaribia siku
yake ya kufa. Mtu yule ambaye
katika maisha yake yote analundika
hazina ya ulimwengu huu, hawezi
kujitoa kwa urahisi katika shughuli
zake alizozoea kuzitafuta. Je! yule
anayeitafuta hazina ile ya mbinguni
asiweze kuwa na bidii zaidi, kuwa motomoto zaidi, na kuvutwazaidi
kuitafuta hazina ile iliyoko huko juu?
Je! hataona wivu kukipata kitu kile
kilicho bora sana na kinachodumu
sana? Je! hataitafuta ile taji ya
utukufu ambayo hainyauki, utajiri ule
ambao nondo wala kutu haviwezi
kuuharibu, wala wevi hawawezi
kuvunja nakuiba? Kadiri tumaini
lake linavyokuwa la motomoto
zaidi, ndivyo juhudi zake zitakavyohitaji nguvu zaidi itumike na
ndivyo atakavyokazana zaidi ili
asikose hazina ile ya milele.... Kazi
yake hapa duniani ni kujipatia utajiri
ule wa milele. Hawezi walahataweza kukubali, baada ya
kuvionja vipawa vile vya Mungu
vya mbinguni, kubaki akiwa
ombaomba [mkata], akiachwa katika
ufukara milele zote. Shauku ya
moyoni mwake ni zaidi, zaidi. Hilo
ndilo hitaji halisi la moyo. Tunataka
neema zaidi ya Mungu,nuru zaidi, na
imani zaidi....
Laiti kama nguvu zote zilitotumika
vibaya zingalitumika kulifikia lengo
hilo moja kuu ---- utajiri unaotokana
na neema ya Mungu katika maisha
haya ----- ni hati za sifa zilioje
tungezitundika katika ukumbi wa
kumbukumbu zetu, tukisimulia tena fadhili naupendeleo wa Mungu
kwetu!... Ndipo tabia hiyo ingebaki
nasi kama kanuni ya kudumu ya
kulundikahazina za kiroho kwa bidii
na kwa uvumilivu kama vile wale
wanaoipendasana dunia hii
wanavyofanya kazi kwa ajili ya
mambo ya kidunia yadumuyo kwa
muda mfupi. Yawezekana wewe
umetosheka sana na ruzuku
unazopata sasa wakati Bwana anayo
mbingu yote ya mibaraka na hazina
ya vitu vyema na vizuri vya kukidhi
mahitajiya roho yako. Leo tunataka
neema zaidi, leo tunataka upendo wa
Mungu utolewe upya kwetu pamoja na ishara za fadhili zake, naye
hatamnyima mema hayo yule aliye
mtafutaji mwaminifu wa hazina hizo za
mbinguni....
Wale wanaoyaona mahitaji yao ya
kiroho wataonyesha shauku ya mioyo
yao, ari zao za motomoto, ambazo
zinaelekea juu na kuzidi kwenda juu
kupita kila kivutio cha kidunia, yaani,
cha maisha haya, hadi kwenye [kivutio]
kile cha milele. ----- MS 22, 1889.
HATARI KUBWA YA MALI Julai 2
Mali izidipo msiiangalie sana moyoni.
Zaburi 62:10.
Miongoni mwa hatari kubwa sana
zinazolitishia kanisa ni kule kuipenda dunia. Kutokana na jambo
hilo huja dhambi za kujipenda nafsi
na uchoyo. Kwa wanadamu, kadiri
wanavyopata zaidi hazina ya dunia
hii, ndivyo kadiri wanavyoweka
mapenzi yaojuu yake, na bado
wanazidi kutaka zaidi....
Shetani anatumia kila njia
anayoweza kuibuni ili kuwaangusha
wafuasi wake Kristo. Kwa ustadi wa
ajabu na hila anayabadilisha majaribu
yake kulingana na tabia ya pekee ya
kila mmoja wetu. Wale ambao kwa
asili wanajipenda wenyewe, tena ni
wachoyo, maranyingi anawajaribu
kwa kuwatupia utajiri njiani mwao. Anajua kwamba wasipoishinda tabia yao hiyo ya asili, basi, huko
kupenda mali kwao kutawafanya
wajikwae na kuanguka. Lengo lake
mara nyingi linatimizwa. Wanapopewa
utajiri wa dunia hii, wengiwao kwa
hamu kubwa huikamata hazina hiyo,
na kudhani ya kwamba
wamefanikiwa ajabu. Upendo wao
wenye nguvu kwa ulimwengu huu
mara huumeza upendo wa ile kweli....
Kama wale waliofanikiwa kwa njia
hiyo wangeweka vyote walivyo
navyo juu yamadhabahu ya Mungu,
wangeweza kuishinda ile roho ya
kujipenda nafsi zao na uchoyo, na hivyo kuuzuia mpango wa Shetani.
Mali ya dunia hii inaweza kuwa
mbaraka, ikitumika vizuri. Wote
walio nayo wangepaswa kutambua
kwamba wameazimwa naMungu, ili
kutumika katika kazi yake. Kwa
kutoa kwa wingi ili kuendeleza kazi
ya ile kweli na kuwapunguzia shida
maskini, wanaweza kuwa njia ya
kuwaokoa wengine, nakwa njia hiyo
kuweza kujiletea wenyewe mibaraka
hapa, na mbinguni kujiwekea hazina
ambayo itakuwa yao baadaye....
Wengi bado wanajua kwa shida mno
maana ya kujikana nafsi, au maana
halisi ya kutoa kwa ajili ya ile kweli. Lakini hakuna atakayeingia mbinguni
ila kwa njia ile ile aliyoipitia Mwokozi
ya unyenyekevu, kujitoa mhanga, na
kujitwika msalaba. Ni wale tu walio
tayari kutoa vyote kwa ajili ya uzima
ule wa milele ambao wataupata,
lakini itafaa kuteseka kwa ajili yake,
yaani, itafaa kujisulibisha nafsi na
kuacha kila sanamu kwa ajili yake.
Utukufu wenye uzito [maana] upitao
wote na udumuo milele utaizidi kila
hazina ya dunia hii na kukifunika kila
kivutio [kishawishi] cha dunia hii. -----
RH, Sept. 4, 1883.
WAJUMBE WAKE WA
KUPUNGUZA DHIKI Julai 3Na Mfalme atajibu, akiwaambia,
Amin, nawaambia, kadiri
mlivyomtendea mmojawapo wa hao
ndugu zangu walio wadogo, mlinitendea
mimi. Mathayo 25:40.
Ingekuwaje iwapo wale wanaojiita
kuwa ni wafuasi wa Yesu
wangeweza kuyaangalia mavazi yao ya
gharama na kuyaona maneno haya
yameandikwa juu yake kwa kidole cha
Mungu, "Wavike nguo walio uchi."
Ingekuwaje, basi, kama wangeyaona
maandishi haya juu ya mapambo yao
ya gharama yaliyo ndani ya nyumba
zao, juu ya picha zao, na juu ya samani
[fanicha] zao, "Walete maskini waliotupwa nje nyumbani mwako"!
Katikachumba kile cha kulia
chakula, ambamo meza yako imejaa
chakula kingi, kidole cha Mungu
kimeandika, "Je! sio kuwagawia
wenye njaa chakula chako...?" Hebu
wote,wazee kwa vijana, watafakari
ya kwamba si jambo rahisi kuwa
wakili wa Bwana....Maskini, pamoja na wale
waliosetwa wameachwa wakiwa
wahitaji, wakati fedha ya Bwana
inatumika vibaya kwa kujifurahisha
nafsi, ikitapanywa ovyo kwa njia
yaubadhirifu na anasa. Laiti kama
wote wangalikumbuka ya kwamba Mungu hapendelei mtu ye yote! Ni
jambo kubwa kuwa wakili mwaminifu
na wa kweli, mbele za Mungu
mwenye haki, asiyependelea mtu....
Sheria ya Mungu [Amri Kumi]
inamshikilia kila mwanadamu kuwa
anawajibika kutoahesabu kwa
matumizi ya kila dola [shilingi]
inayokuja mikononi mwake; kwa
maana Bwana amewaweka wanadamu
kuwa wajumbe wake wa kupunguza
dhiki iliyomo humu duniani. Iwapo
mwanadamu atahodhi au kutumia kwa
faida yake binafsi mali ya Bwana
aliyokabidhiwa, basi, itakuwa kwa
maangamizi ya roho yake mwenyewe; maana atakuwa anajiheshimu, anajisifu,
na kujitukuza yeye mwenyewe....
Katika dunia yetu hii wakowale
ambao, japokuwa ni wateule hasa wa
Mungu, sikuzote wanapita kando na
kuwaacha maskini [bila kuwasaidia].
Yesu analiona jambo hilo; Yesu
analiweka katika kumbukumbu zake;
yeye hatapita kando na kuliachilia
jambo hilo. Yesu alisisitizakwamba
alikuja kuhubiri injili kwa maskini.
Ametugawia mali zake, ili upendo
na ukarimu udumishwe, ukiendelea
daima kuwa na nguvu zaidi mioyoni mwa
watu wake....
Mgawanyo wa thawabu siku ile ya mwisho utategemea hoja hii ya
ukarimu wetu kwa matendo; "Kadiri
mlivyomtendea mmojawapo wa hao
ndugu zangu walio wadogo,
mlinitendea mimi." Kristo anajiweka
mwenyewe mahali pa mtu aliye
maskini, yaani, anayafananisha mambo
yake na yale ya maskini....
Anamtaka kila mfuasi wake kwa
shukrani kugawa kwa ukarimu
vipawa alivyokabidhiwa, kana
kwamba alikuwa anamgawia vipawa
hivyo Mkombozi wake. ----- MS 11,
1892.
HAKUNA CHA THAMANI MNO
USICHOWEZA KUMPA MUNGU Julai 4
Kwa imani Ibrahimu alipojaribiwa,
akamtoa Isaka awe dhabihu; na
yeye aliyezipokea hizo ahadi alikuwa
akimtoa mwanawe, mzaliwa pekee.
Waebrania 11:17.
Jaribio la Ibrahimu lilikuwa kali mno
ambalo lilipata kumjia mwanadamu.
Angeshindwa chini ya jaribio hilo,
asingeweza kuandikwa kamwe kama
baba wa wenye imani....Fundisho
hilo lilitolewa lipate kuangaza katika
vizazi vyote, ili sisi tupate kujifunza
ya kwamba hakuna kitu cho chote
cha thamani mno ambacho hatuwezi
kumpa Mungu. Ni wakati ule tunapokiangalia kila kipawa kama
chake Bwana ili kipate kutumika
katikakazi yake, hapo ndipo
tunapojipatia ule mbaraka wa
mbinguni. Mrudishie Mungu mali yako uliyokabidhiwa, ndipo
utakapokabidhiwa mengi zaidi. Tunza
mali yako kwa ajili yako mwenyewe,
nawe hutaweza kupokea thawabu
yo yote katika maishahaya, tena
utapoteza thawabu yako katika maisha
yale yajayo....
Wako wengi ambao hawajapata
kamwe kujisalimisha kabisa kwa
Mungu. Hawana wazo sahihi juu ya
kafara ile isiyokuwa na kifani ambayo ilitolewa na Mungu
kuuokoa ulimwengu huu ulioharibika.
Endapo Mungu angesema nao kama
vile alivyosema naIbrahimu,
wasingeweza kuifahamu sauti yake
kiasi cha kutosha kujua kwamba
alikuwa anawataka wamtolee sadaka, ili
kukipima kina cha upendo wao na
unyofu wa imani yao.
Baa la kujipenda nafsi [uchoyo]
huambukiza kama vile ukoma. Wale
watakaoingia katika majumba yale ya
kifalme ya mbinguni hawana budi
kutakaswa kutokana na kilasazo la
baa hilo....
Bwana anayo kazi kubwa kwa ajili yetu ili tupate kuifanya, naye
anatuita tumtazameYeye, tumtegemee
Yeye, tutembee naye, na kuzungumza
naye. Anatualika tuvisalimishe kabisa
vyote tulivyo navyo pamoja na sisi
wenyewe jinsi tulivyo, ili
atakapotutaka sisikumtolea sadaka,
tuwe tayari na tumtii kwa hiari.
Tutafurahia utimilifu wa neema yake
pale tu tutakapompa vyote Kristo.
Tutajua tu maana ya furaha ya
kweli hapo tutakapoendelea
kuuchochea moto unaowaka juu ya
madhabahu ya kafara. Mungu
atawapa urithi mwingi sana baadaye
wale waliofanya mengi sana wakati huu wa sasa.... Kila siku, chini ya
mazingira tofauti, anatupima; nakatika
kila juhudi ya kweli itokayomoyoni
anawachagua watenda kazi wake, si
kwa sababu wao ni wakamilifu, bali
kwa sababu wako tayari kufanya
kazi bila kuwa na ubinafsi kwa ajili
yake, naye anaona kwamba kwa njia
ya kuunganishwa naye wanaweza kupata
ukamilifu huo. -----
YI, Juni 6, 1901.
AKAUNTI YAKO IKOJE? Julai 5
Hapo tena inayohitajiwa katika mawakili,
ndiyo mtu aonekane kuwa mwaminifu.
l Wakorintho 4:2.
Je! unamkiri Kristo katika matumizi yako ya mali yake aliyokukabidhi?...
Endapo Kristo angepata kile kilicho
chake kwa zaka na sadaka,
hakuna kiasi kikubwa ambacho kingeachwa kwa matumizi yako ya
binafsi kununua vikorokoro na
kujionyesha. Kiasi kidogo kingetumika
kwa mavazi, kwa safari za anasa,
kwa tafrija, ama kwa kujionyesha kwa
kuweka vyakula vingi mezani.
Tunaweza kumkiri Kristo kwa njia
ya kutofanya maandalizi makubwa
sana kwa ajili ya wageni wetu;
tunaweza kumkana kwa kufanya
maandalizi makubwa kuliko kawaida,
yanayochukua muda mwingi kutayarisha, mudaambao kwa haki
ni wake Bwana.... Kabla ya
kujiingiza katika burudani kwa ajili
ya kujifurahisha nafsi yako jiulize
mwenyewe swali hili, Je! huu si
wakati wake na fedhayake
ninavyotumia mimi isivyolazimu?
Fungua kitabu chako cha Akaunti, na
kuiangalia jinsi Akaunti yako hiyo ilivyo
kwa Mungu, kwa nyumba yako, na kwa
ulimwengu.
Je, umemkiri Kristo kwa kutoa
kwa uaminifu zaka za mnanaa,
bizari, na jira? Tunapompa Bwana
zaka, tunampa tu kile kilicho chake,
kuzuia ni wizi na unyang'anyi....Je, kitabu chako cha Akaunti
kinaonyesha kwamba umekuwa
mwaminifu kwa Bwana wako? Je,
wewe ni maskini? Basi toa kidogo
ulicho nacho. Je, umebarikiwa kwa
kupata vingi? Basi hakikisha unaweka
kando kile ambacho Bwana
anakiandika kuwa ni chake.... Kupuuzia
kumkiri Kristo katika kitabu chako
cha Akaunti [ya Benki] hukutenga
wewe mbali na haki kuu ya
kuandikwa jina lako katika kitabu
kile cha uzima cha MwanaKondoo. --
--- MS 13, 1896.
Baba yetu aliye mbinguni
anatufundisha kwa mfano wa ukarimuwake. Mungu anatupasisi kila siku,
bure na kwa wingi. Kila mbaraka
wa kidunia unatoka mkononi mwake.
Ingekuwaje, basi, kama Bwana
angeacha kugawa vipawa vyake
kwetu? Ni kilio cha jinsigani cha
umaskini, mateso, na dhiki ambacho
kingepanda juu kutoka duniani! Kila
siku tunahitaji mkondo wa Mungu wa
upendo wake na fadhili zake. ----- MS
153, 1903.
HASARA INAPOKUWA FAIDA Julai
6
Akawaambia, Angalieni, jilindeni na
choyo, maana uzima wa mtu haumo
katika wingi wa vitu vyake alivyo navyo.Luka 12:15.
Jambo moja muhimu linaloonekana
wazi katika mafundisho ya Kristo ni
kwamba marakwa mara na kwa
bidii aliikemea dhambi ya uchoyo na
kuonyesha hatari ya kujipatiamali ya
dunia hii na kuwa na tamaa
isiyozuilika ya kujipatia faida....
Kichwa na mikono vinaposhughulishwa
daima katika kupanga na kufanya kazi
kwa muda mrefu kwa ajili ya
kujilimbikizia mali, madai ya Mungu na hazina ya thamani, kama ikitumika
kwa uangalifu, kwa hekima na
pasipo kutumika vibaya.... Kwa
kuwawanadamu wanaokufa wana
miili na vichwa na mioyo ya kulisha,
basi, sehemu fulani kwa ajili ya
mwili haina budi kuwekwa kando
ili uweze kuwa na mahali pake
ulimwenguni humu. Si kwa ajili ya
kutimiza viwango vilivyowekwa na
ulimwengu huu---- la, la, kabisa; bali ni
kwa ajili ya kuwa na mvuto mzuri katika
ulimwengu huu....
Dhiki na umaskini ni maovu ya
kuogopwa sana; lakini njaa na uchi,
kukosa makao, huruma, au jina, na
binadamu husahauliwa. ----- RH, Okt.
17, 1882. Mali ni ya thamani na ya
kutamanika. Ni mbaraka, yaani, hata kufa kwa njaa, ni afadhali
kuliko kuiacha kanuni moja ya ile
kweli. Kweli ya milele na itunzwe,
maana inadumu milele. Tukiifanya iwe
sehemu yetu,bila shaka tutaipata taji ile
isiyonyauka na utajiri ule wa milele....
Kama Mungu hajakupa wewe nguvu
ya kupata mali kwa unyofu hasa na
uaminifu, basi, hakukusudia kwamba
wewe uwe nayo, na ni bora kwako
kunyenyekea chini ya mapenzi ya
Mungu.... Muumbaji Mungu ndiye
mwenye vitu vyote. Hasara yo yote
unayowezakupata kwa kumtii yeye
ni faida isiyopimika katika maisha
yale ya milele ya baadaye, iwapo haitapatikana kikamilifu katika maisha
haya....
Tazama utukufu wa anga. Angalia
juu kuziona johari zile za nuru ambazo
kama dhahabu ya thamani zinaipamba
mbingu.... Je! yule aliyeitandaza juu
yetu anga hiyo tukufu,ambaye,
kama jua, mwezi, na nyota
vingeweza kufagiliwa mbali, angeweza
kuvitia tena viwepo mahali pake kwa
dakika moja, hawezi kuwalipa
waaminifu wake, watumishiwake
watiifu ambao wangependa kumtii
yeye hata kama wangepoteza mali,
heshima, auhata ufalme [wa duniani]
kwa ajili yake? ----- Letter 41, 1877. NI LAANA AU MBARAKA? Julai 7
Msijiwekee hazina duniani, nondo na
kutu viharibupo, na wevi huvunja na
kuiba.
Mathayo 6:19.
Hazina ni vitu vile vinavyoujaza sana
moyo, na kuchota mawazo yote, na
kumwacha nje Mungu na ile kweli.
... Mwokozi wetu alitoa onyo
dhahiri dhidi ya kuhodhi
[kujilimbikizia] hazina za ulimweingu huu. Matawi yote ya biashara, kazi za
aina zote, ziko chini ya uangalizi wa
jicho la Mungu; na kila Mkristo
amepewa uwezo wa kufanya kitu
fulani katika kazi yake Bwana. Si kitukama mtu anafanya shughuli zake za
kazi shambani, katika bohari, au katika
chumba cha mahesabu, watu
watawajibika kwa Mungu kwa
matumizi ya busara na uaminifu ya
talanta zao. Wanawajibika sawasawa
kwa kazi YAO, kama vile mchungaji
anayehudumukwa neno na mafundisho
awajibikavyo kwa kazi yake....
Mali inayowekwa katika hazina
hapa duniani itakuwa ni laana
tupu, lakini kama ikitumika katika
kuijenga kazi ya ile kweli, ili Mungu
apate kuheshimiwa, na roho zipate
kuokolewa, basi, hapo haitakuwa muhimu katikakuiendeleza kila kazi
iliyo nzuri; na kama vile watu
wengine walivyopewa uwezo zaidi wa
kupata mali kuliko wengine, basi,
wangezitoa talanta zao kwa hao
watoao riba, iliBwana apate iliyo yake,
pamoja na faida, hapo atakapokuja....
Wale waliotayari na wanaotaka
kuweka mali yao katika kazi ya
Mungu, watabarikiwakatika juhudi
zao za kupata fedha. Mungu
aliumba chimbuko hilo la utajiri.
Alitupa mwanga wa jua, na
umande, na mvua, na kuifanya
mimea kusitawi. Aliwabariki
wanadamu kwa kuwapa nguvu za akili na mwili, na kuwawezesha
kujipatia mali, ili kazi yake ipate
kuendelezwa na wale wanaojiita
kuwa ni watoto wake. Maskini
wametuzunguka kila upande, na
Mungu anatukuzwa, maskini na
wanaotesekawanaposaidiwa na
kufarijiwa. Si dhambi kupata na
kumiliki mali kama mawakili wake
Mungu, tukiishikilia tu mpaka pale
atakapoitaka kwa mahitaji ya kazi
yake.----- RH,Sept. 18, 1888.
Yatupasa kukumbuka daima kwamba
sisi tumeingia ubia pamoja na Mungu.
Kazi yakena kusudi lake hudai
kupewa kipaumbele katika fikira zetu. ---
laana, bali mbaraka. Mali ni ya
-- MS 13, 1896.
BENKI ISIYOFILISIKA Julai 8
Bali jiwekeeni hazina mbinguni,
kusikoharibika kitu wala nondo wala
kutu, wala wevi hawavunji wala
hawaibi; kwa kuwa hazina yako
ilipo, ndipo utakapokuwapo na moyo
wako.
Mathayo 6:20,21. Hapa imefafanuliwa thamani ya
utajiri ule wa milele, kwa
kuutofautisha na ule wa duniani.
Iwapo kusudi na lengo la maisha
yako ni kujiwekea hazina mbinguni,
basi,utainuliwa juu ya mvuto ule
mbaya, dhalili, unaoharibu tabia ambao unatokana na tamaa isiyozuilika
ya kupata mali katika maisha haya.
Kujiwekea hazina mbinguni
kutaifanya tabia yako kuwa nzuri sana;
kutaimarisha ukarimu wako; kutakutia
moyo upate kuwa na rehema;
kutaikuza huruma yako, upendano wa
ndugu, na upendo. Kutaiunganisha
roho ya mwanadamu na ile ya Kristo
kwa viungo visivyoweza kuvunjika
[kukatika] kamwe.Mnaweza kujiwekea
hazina yenu mbinguni kwa kuwa
matajiri wa matendo mema ----
matajiri katika vitu vile visivyoharibika na
vya kiroho.
Agizo ni hili, "JIwekeeni [WENYEWE] hazina mbinguni." Ni
kwa faida yetu wenyewekwamba
tujipatie utajiri ule wa mbinguni.
Mungu hafaidiki kitu kwa ukarimu
wetu.Ng'ombe juu ya milima elfu ni
zake. "Nchi na vyote viijazavyo ni
mali ya BWANA, Dunia na wote
wakaao ndani yake." Zaburi 24:1.
Lakini katika kutumia kwa ajili ya
wokovu wa roho za watu vipawa
vile alivyotukabidhi mikononi mwetu
ili tumtunzie,tunahamishia mali yetu
katika hazina ile ya mbinguni [kwa
njia hiyo]. Tunapotafuta kumpa
Mungu utukufu, na kuiharakisha
siku ile ya Mungu, tunakuwa watenda kaziwenzi na Kristo, na
furaha yetu inakuwa si hisia zilizojaa
uovu zipitazo, bali ni furaha hasa ya
Bwana wetu. Tunainuliwa juu ya
masumbufu yanayotula na kutujaza
wasiwasi ya ulimwengu huu mbovu,
unaobadilikabadilika tu.
Wakati bado tungali katika
ulimwengu huu, tutakabiliwa na
hasara na kukata tamaa.Wevi
huvunja na kuiba; nondo na kutu
huharibu; moto na dhoruba hufagilia
mbali mali zetu.... Ni wangapi ambao
waliyatoa maisha yao yote kuchuma
mali, ambao hawakuwa matajiri kwa
Mungu; na ambao, maafa yalipokuja juu yao, na mali yao kufagiliwa mbali,
hawakuwa na kitu walichojiwekea
mbinguni. Walikuwa wamepoteza
vyote ----- mali ya duniani na ile ya
milele....
Kila kitu kilichowekwa katika hazina
ya hapa duniani kinaweza kufagiliwa
mbali kwa dakika moja; lakini
hakuna cho chote kinachoweza
kuivuruga hazina iliyowekwa
mbinguni. ----- RH, Sept. 18, 1888.
TABASAMU YAKE MUNGU Julai 9
Baraka ya BWANA hutajirisha, Wala
hachanganyi huzuni nayo. Mithali 10:22. Hakuna kitu cho chote
kinachoweza kutuletea sisi mema pasipo baraka ya Mungu.
Anachokibariki Mungu kinabarikiwa.
Kwa hiyo, "Kidogo alicho nacho
mwenye haki ni bora kuliko wingi
wa mali wa wasio haki wengi."
Zaburi 37:16. Kidogo pamoja na
baraka ya Mungu kina manufaa
zaidi, na kitakwenda mbali zaidi.
Neema ya Mungu itafanya kilicho
kidogo kwenda mbali sana kwa
njia nyingi. Tunapojitoa wenyewe
kushughulika na mambo ya ufalme
wa Mungu, atayajali mambo yetu. ---
-- Letter 8,1873.
Bwana ametupa sisi mibaraka ya
thamani katika maua ya kawaida ya makondeni, katika manukato yake
yaliyo matamu sana kwa fahamu
zetu. Amelipamba kila ua kwa rangi
nzuri; maana yeye ni Bingwa
Mkuu Msanii. Yeye aliyeviumba
vitu vizuri katika maumbile atafanya
mambo makubwa zaidi kwa roho
zetu. Mungu ni mpenzi wa uzuri,
naye angependa kuzipamba tabia
zetu kwa matendo yake mema
sana. Angependamaneno yetu yawe
na harufu nzuri kama maua ya
kondeni. Ametupa sisi mibaraka kwa
kutupa riziki yetu ya kila siku ili
kukidhi mahitaji ya miili yetu. Mkate
[chakula] ule uletunaokula juu yake una picha na maandishi ya msalaba. -----
Letter 97, 1895.
Wamebarikiwa kweli kweli wale tu
ambao shughuli yao kuu ni kujipatia
mibaraka ileitakayoilisha roho yao
na itakayodumu hata milele.
Mwokozi wetu ametuambia, "Bali
tafuteni kwanza ufalmewake, na haki
yake; na hayo yote mtazidishiwa."
Mathayo 6:33.Mungu
anatushughulikia sisi, hata
kutumwagia mibaraka yake ya
kidunia juu yetu. Mema yetu ya
hapa duniani sio kwamba hayaoni
Baba yetu aliye mbinguni. Anajua
kwamba tunahitaji hayo yote.... Mungu anapotabasamu kuziona juhudi
zetu ni jambo lathamani kuliko kipato
cho chote cha duniani. "Faraja za kila
siku zinakuwa tamu jinsi gani
Zinapotiwa kiungo kile cha pendo lake."
----- Letter 8, 1873.
Kila kuokolewa hatarini, kila
mbaraka, ambao Mungu zamani
aliwapa watu wake, vingetunzwa
upya katika ukumbi wa kumbukumbu
zetu kama ahadi yake ya hakika ya
mibaraka zaidi, na mingi zaidi,
yaani, mibaraka inayozidi
kuongezeka atakayoweza kutugawia sisi.
----4BC 1183.
Hakuna mwisho wa mibaraka ambayo ni haki yetu kuipokea. ----- 7BC 906. ZAWADI ANAYOIKUBALI MUNGU
Julai 10
Wapeni watu vitu, nanyi mtapewa;
kipimo cha kujaa na kushindiliwa,
na kusukwasukwa hata kumwagika,
ndicho watu watakachowapa vifuani
mwenu. Kwa kuwa kipimo kile kile
mpimacho ndicho mtakachopimiwa.
Luka 6:38.
Hebu na tuache kulalamika kwa
sababu mara kwa mara tunaombwa
kutoa kwa ajili ya kuiendeleza kazi ya
Mungu. Ni jambo gani linalofanya
mwito huu wa mara kwa marauwe
wa muhimu hivyo? Je, si ongezeko la miradi ya
kimishonari? Je, sisitutaichelewesha
miradi hiyo isiweze kukua kwa kukataa
kutoa?...
Wale wote walio na Roho wake
Kristo watakuwa na moyo laini,
wenye huruma, na wenye mkono
uliofumbuliwa, yaani, mkono wa
ukarimu.... Kwetu imekabidhiwa kazi
yakuutangaza ujumbe wa mwisho
wa rehema ambao unapaswa
kutolewa kwa ulimwengu huu -----
ujumbe huo ambao umekusudiwa
kuwatayarisha watu kusimama katika
siku ile ya Mungu. Je, tunautambua
uwajibikaji wetu? Je, tunafanya sehemu yetu katika kuutangaza
ujumbe huo? Kipindi hiki cha sasa
kimebeba mzigo mzito wa mambo yale
ya milele. Tunalazimika kuitweka
bendera ya ile kweli mbele ya
ulimwengu unaoangamiakwa makosa
[mafundisho potofu]. ----- RH, Aprili 18,
1912.
Kadiri tunavyozidi kuleta katika
hazina yake Mungu, ndivyo kadiri
tutakavyozidi kuleta; maana
atatufungulia njia nyingi mbele yetu,
akiongeza mali yetu. Mimi
nimeshuhudia hilo kuwa ni jambo la
kweli katika maisha yangu
mwenyewe. Mungu anapozidishaMKONO WA MUNGU WENYE REHEMA USAIDIAO Julai 11
Heri wenye rehema; Maana hao watapata rehema. Mathayo 5:7.
Iweni wenye rehema, kama Baba yenu wa mbinguni alivyo na rehema. Kitafakarini
kipawa kile kikuu ambacho Mungu ametoa kwa ajili yenu.... Mungu amewapa uthibitisho
wa upendo wake ambao unayashinda mahesabu yote [ya kibinadamu]. Hakuna kamba ya
kuupima, wala kanuni ambayo tunaweza kuilinganisha nao. Mungu anawaita ili shukrani
zenu mziache ziwe zikibubujika kwa njia ya vipawa na sadaka zenu. Anawaita mwe
mkono wake wa rehema usaidiao. Je, mwaweza kukataa ombi la yule Mmoja
aliyewatendea mambo mengi sana?
Kristo alilia alipoziona shida walizokuwa nazo watu. Hebu huruma zake na ziingie
mioyoni mwenu. Jizoezeni kujikana nafsi ili mpate kuwa na kitu cha kusaidia kupunguza
mateso ya watoto hao wa Mungu. ----- RH, Aprili 18, 1912.
Mungu aliona kwamba ni muhimu kwetu kuzungukwa na maskini, ambao katika
kutojiweza kwao na mahitaji yao wanadai kupata huduma kwetu. Wangekuwa msaada
kwetu katika ukamilishaji wa tabia yetu ya Kikristo; maana kwa kuwapa chakula cha
kuweka mezani pao na mavazi kwa ajili ya miili yao tungeweza kukuza sifa za tabia yake
Kristo. Kama tusingalikuwa na maskini miongoni mwetu, tungepoteza mengi; kwa
maana ili kuweza kuikamilisha tabia ya Kikristo, inatupasa kuikana nafsi yetu. ----- RH,
Okt. 15, 1895.
Kristo mwenyewe, Bwana wa utukufu, alikuwa hapa duniani kama Mtu wa huzuni
nyingi, ajuaye sikitiko. Alijua maana ya dhiki na ufukara. Katika utoto wake, akiwa
amekandamizwa na umaskini, alijizoeza kanuni zile za kujikana nafsi. Alikuja ...
kuwasaidia wanadamu walioanguka, walio maskini. Naye anawatazamia wafuasi wake,aliowakabidhi mali yake, kujizuia katika mahitaji yao wanayodhania kuwa wanayo, na
kuwa wakarimu katika kusaidia kupunguza shida za wengine. ----- MS 101, 1906.
Mnapotumia fedha zenu, fikirieni kile ambacho Yesu angeweza kufanya kama angekuwa
mahali penu. Anawataka wafuasi wake kukanyaga katika nyayo zake za kujikana nafsi na
kujitoa mhanga. Tabia ya Mkristo inatakiwa kuwa picha halisi [chapa] ya tabia yake
Kristo. Upendo ule ule, neema ile ile, ukarimu ule ule usiojipendelea nafsi, ulioonekana
katika maisha yake, unapaswa kuonekana katika maisha ya wafuasi wake. ----- RH,
Aprili 18, 1912.
UTAMU WA KUJINAKA NAFSI Julai 12
Mheshimu BWANA kwa mali yako, Na kwa malimbuko ya mazao yako yote. Ndipo
ghala zako zitakapojazwa kwa wingi, Na mashinikizo yako yatafurika divai mpya.
Mithali 3:9,10.
Madai ya Mungu ni msingi wa madai mengine yote. Anaweka mkono wake juu ya yote
ambayo kutokana na utimilifu na ukarimu wake, amemkabidhi mwanadamu na kusema,
"Mimi ndimi mmilikaji wa halali wa ulimwengu, na vitu hivi ni mali yangu. Vitumie
kuiendeleza kazi yangu, yaani, kuujenga ufalme wangu, na mbaraka wangu utakuwa juu
yako." ----- RH, Okt.6, l891.
Baadhi ya watu hutoa katika wingi wa vitu walivyo navyo, lakini hawajisikii
kupungukiwa. Hawajizoezi kujikana nafsi kwa ajili ya kazi yake Kristo. Wanatoa kwa
ukarimu na kwa moyo wa furaha, lakini bado wanajikuta wanavyo vyote ambavyo moyo
wao unaweza kutamani. Mungu anaangalia kitendo hicho. Kitendo hicho na nia iliyo
nyuma yake huangaliwa sana naye, na hao hawatakosa thawabu yao. Walakini wale
walio na mali kidogo hawawezi kutoa udhuru [kuwa hawawezi kutoa] kwa sababu
hawawezi kutoa kiasi kile kile kama wale wengine. Fanya lile unaloweza. Jikane nafsi
kwa kitu fulani unachoweza kuishi bila kuwa nacho, nawe kitoe kiwe sadaka kwa ajili ya
kazi ya Mungu. Kama yule mjane maskini, toa visenti vyako viwili. Kwa kweli utakuwa
umetoa zaidi kuliko wale wote wanaotoa katika wingi wa vitu walivyo navyo; nawe
utajua jinsi utamu ulivyo wa kujikana nafsi yako, kwa kuwapa maskini, kutoa kwa ajili
ya kuiendeleza kweli, na hivyo kujiwekea hazina yako mbinguni.
Vijana... wanaoikiri kweli hii, bado wanalo fundisho la kujikana nafsi ambalo
wanapaswa kujifunza. Kama hao wangetoa zaidi kwa ajili ya ile kweli, basi, wangeweza
kuiheshimu kwa hali ya juu zaidi. Nayo ingeibadilisha mioyo yao, na kuyatakasa maisha yao. Mara nyingi mno vijana hawabebi mzigo wa kazi ya Mungu, au kujisikia ya kuwa
wanao wajibu wo wote kuhusiana nayo. Je! ni kwa sababu Mungu amewaachia huru? La;
wanatoa udhuru wao wenyewe. Hawatambui kwamba wao si mali yao wenyewe. Nguvu
zao, wakati wao, si vyao wenyewe. Wamenunuliwa kwa thamani; na wasipokuwa na
roho ile ya kujikana nafsi na kujitoa mhanga, hawawezi kamwe kupata urithi ule wa
milele. ----- RH, Sept.16, 1884.
Toa uwezacho kutoa sasa, nawe unapoendelea kushirikiana na Kristo, mkono wako
utakunjuliwa ili upate kutoa zaidi. Naye Mungu ataujaza mkono wako, ili hazina ya ile
kweli ipate kupelekwa kwa roho nyingi. Atakupa wewe ili nawe upate kuwapa wengine. -
---- CS 50.
KIPIMO CHA TABIA Julai 13
Lakini hao watakao kuwa na mali huanguka katika majaribu na tanzi, na tamaa nyingi
zisizo na maana, zenye kudhuru, ziwatosazo wanadamu katika upotevu na uharibifu.
Maana shina moja la mabaya ya kila namna ni kupenda fedha; ambayo wengine hali
wakiitamani hiyo wamefarakana na imani, na kujichoma kwa maumivu mengi. 1
Timotheo 6:9,10.
Shetani ana nyavu na mitego, kama mitego ile ya mwindaji ndege, yote hiyo
imeandaliwa kuzitega roho zetu. Ni kusudi lake lililodhamiriwa kwamba wanadamu
wazitumie nguvu zao walizopewa na Mungu kwa makusudi ya kibinafsi kuliko kuzitoa
kwa ajili ya kumtukuza Mungu. Mungu angependa wanadamu waingie katika kazi ile
itakayowaletea amani na furaha, na itakayowaletea faida ya milele; bali Shetani anatutaka
sisi kukusanya juhudi zetu zote na kuzitumia kwa kile kisicho na faida yo yote, yaani,
kwa vitu vile vinavyoharibika vikitumiwa. ----- RH, Sept.1, 1910.
Utukufu wa ulimwengu ule ujao unafunikwa na vitu vile vinavyoharibika vya
ulimwengu huu. "Kwa kuwa hazina yako ilipo, ndipo utakapokuwapo na moyo wako."
Mathayo 6:21. Mawazo yako, mipango yako, nia yako, vyote vitakuwa na mfumo wa
kidunia, na nafsi yako itanajisiwa kwa uchoyo na kujipenda nafsi. "Kwa kuwa itamfaidia
mtu nini kuupata ulimwengu wote, akipata hasara ya nafsi yake? Marko 8:36. Siku yaja
ambayo sanamu za fedha na dhahabu zitatupiliwa mbali kwa fuko na popo, na watu walio
matajiri watalia na kupiga yowe kwa sababu ya mashaka yao yatakayowajia....Iwapo mawazo yako, mipango yako, makusudi yako, vyote vimeelekezwa katika
kujilimbikizia vitu vya ulimwengu huu, basi, mashaka yako, mafunzo yako, mambo
uyapendayo, yatakazwa juu ya ulimwengu huu. Mambo ya mbinguni yanayopendeza
sana yatapoteza uzuri wake kwako.... Moyo wako utakuwa pamoja na hazina yako....
Hutakuwa na muda wa kuutenga kando kwa ajili ya kujifunza Maandiko wala kuwa na
maombi ya dhati ili upate kuokoka katika mitego ya Shetani....
Laiti kama mambo yale ya kuvutia sana ya ulimwengu ule ujao yangethaminiwa! Kwa
nini wanadamu hawajihusishi sana na wokovu wa roho zao wakati zilinunuliwa kwa
gharama kama hiyo na Mwana wa Mungu? ----- RH, Sept.1, 1910.
Kwa kudra yake Mungu, baadhi ya watu wanaweza kuchuma mali nyingi kuliko
wengine kwa ustadi wao wa kimwili au kwa maarifa yao ya ubunifu. Mungu anawabariki
kwa kuwapa mali, busara, na ustadi ili wapate kupokea mali yake na kuwagawia wengine
ambao huenda hawajapata mibaraka hiyo. Kule kuwa na mali kunakuwa ndicho kipimo
cha tabia. -----
MS 101, 1906.
JE! HIVI NI KWELI TUNAJITOLEA MHANGA? Julai 14
Washangilie, wakufurahie, Wote wakutafutao. Waupendao wokovu wako waseme
daima, Atukuzwe BWANA. Zaburi 40:16.
Wengi wanasema juu ya maisha ya Mkristo kuwa yanatuondolea anasa na raha za dunia.
Mimi nasema hayaondoi kitu cho chote kinachofaa kukitunza. Je, kuna mashaka,
umaskini, na dhiki anayopata Mkristo? Ndiyo, jambo hilo linatazamiwa katika maisha
haya. Lakini mwenye dhambi tunayesema anafurahia anasa za ulimwengu huu, je! yu
huru mbali na mabaya hayo yanayopatikana katika maisha haya? Je! hatuwaoni mara kwa
mara wakiwa katika mashaka makubwa na taabu?...
Wakati mwingine Wakristo wanadhani ya kwamba wanao wakati mgumu na ya kwamba
ni kujidhalilisha wenyewe kuishikilia kweli hii isiyopendwa na watu wengi na kukiri
kuwa wao ni wafuasi wake Kristo, kwamba kwao njia huonekana kuwa ngumu na
kwamba wanayo mambo mengi yanayowataka kujitolea mhanga, ambapo ukweli ni
kwamba hawajitoi mhanga hata kidogo. Iwapo wao wameingizwa kweli katika familia ya Mungu, je! wametoa kafara gani? Kumfuata kwao Kristo kunaweza kuwa kumevunja
urafiki fulani pamoja na ndugu zao waipendao dunia hii, lakini, basi, angalia
walichobadilishana ----- majina yao yameandikwa katika kitabu kile cha uzima cha
Mwana-Kondoo, wametukuzwa, naam, wametukuzwa sana, yaani, kuwa washirika wa
wokovu, warithi wa Mungu na warithi-wenzi pamoja na Yesu Kristo katika urithi ule
usionyauka milele. Je! huko tutakuita kuwa ni kujitoa mhanga kwa upande wetu
tunapoachana na makosa na kuipokea kweli, tunapoachana na giza kwa ajili ya kuipokea
nuru, tunapoachana na dhambi kwa ajili ya kuipokea haki, tunapoachana na jina
lisilodumu na urithi wa hapa duniani kwa ajili ya heshima zile za milele na milele,
pamoja na hazina ile isiyo na waa lo lote ambayo hainyauki kamwe?
Hata katika maisha haya, Mkristo anaye Mmoja ambaye anaweza kumtegemea kwa
msaada, ambaye atamsaidia kustahimili maonjo yake yote. Lakini yule mwenye dhambi
analazimika kustahimili maonjo yake akiwa peke yake. Anaingia kaburini kwenye giza
akiwa na majuto makali, akiwa mfungwa wa Shetani, maana yeye ni mateka wake
halali....
Kama kuna mtu ye yote ambaye angekuwa na shukrani daima, basi, mtu huyo ni yule
mfuasi wa Kristo. Kama kuna mmoja anayefurahia raha ya kweli, hata katika maisha
haya, basi, ni Mkristo yule aliye mwaminifu.... Kama sisi tukiuthamini au kuwa na
fahamu yo yote ya kujua jinsi wokovu wetu ulivyonunuliwa kwa gharama kubwa mno,
basi, cho chote tunachoweza kukiita kujitolea mhanga kitazama chini kisiweze
kuonekana kama kitu chenye maana yo yote ile. ----- Letter 18, 1859.
KWELI NI DAWA YA KUUA DHAMBI Julai 15
Na maneno haya ninayokuamuru leo, yatakuwa katika moyo wako; nawe uwafundishe
watoto wako kwa bidii, na kuyanena uketipo katika nyumba yako, na utembeapo njiani,
na ulalapo, na uondokapo. Kumbukumbu la Torati 6:6,7.
Kufanana kwa shamba lisilolimwa na moyo usiofunzwa kunashangaza sana. Watoto na
vijana katika nia zao na mioyo yao tayari wanazo mbegu mbaya, zikiwa ziko tayari
kuchipuka na kuzaa mazao yake mapotovu; uangalifu mkubwa sana na tahadharivinahitajika katika kukuza na kuhifadhi moyoni mwao mbegu za thamani za ukweli wa
Biblia....
Moyo unapojazwa na ukweli wa Biblia, kanuni zake huotesha mizizi mirefu moyoni, na
mambo yale unayopendelea zaidi na hisia zake huoanishwa na ile kweli, wala hakuna
hamu ya kusoma maandiko yaliyo machafu, yanayosisimua, ambayo huzidhoofisha
nguvu za maadili, na kuharibu fahamu zile alizoziweka Mungu kwa matumizi yanayofaa.
Maarifa ya Biblia yatathibitika kuwa ndiyo dawa ya kuondoa nguvu ya sumu
iliyojipenyeza na kupokewa kwa njia ya kusoma bila kuwa na hadhari [ya kile
usomacho]....
Wazazi wanaweza kuchagua, kama wakitaka, iwapo kumbukumbu za watoto wao
zitajazwa na mawazo safi na matakatifu pamoja na hisia zao au la; lakini mambo yale
wayapendayo hayana budi kuwekwa chini ya nidhamu na kufunzwa kwa uangalifu
mkubwa sana. Wanapaswa kuanza mapema kuwafunulia Maandiko kulingana na akili
zao zinazokua, ili tabia sahihi na mambo mema wanayoyapenda vipate kujengwa....
Misingi ya dhambi haiwezi kuangamizwa kabisa isipokuwa kwa kuingiza chakula humo
kwa ajili ya mawazo safi, yaliyo thabiti....
Nawasihi watoto na vijana kuiacha tupu mioyo yao kwa kuondoa upumbavu wa kujisifu,
na kumfanya Kristo kuwa rafiki yao wa kudumu. Hakikisheni ya kwamba mnalo tumaini
lenye msingi.... Ni wazimu kuwa kimya na kukaa raha mustarehe kama walivyo wengi
kwa wakati kama huu, bila kuwa na hakika yo yote kwamba wao kweli ni wana na binti
za Mungu. Mambo yale ya milele yako hatarini. Wekeni mbali hadithi ile, pigeni magoti
na kuomba ili mpate kuyashinda majaribu, na wakati wenu utumieni kwa kuzichunguza
Biblia zenu.... Hamna haja ya kuachwa mashakani; nuru ya kweli huangaza toka katika
Neno la Mungu katika mioyo yote iliyofunguliwa wazi kuipokea mionzi yake ya
thamani; tena ni haki yenu kusema, "Mimi najua ya kuwa Mteteaji wangu yu hai." Ayubu
19:25. ----- RH, Nov.9, 1886.
KWA MACHO YA IMANI Julai 16
Macho ya mioyo yenu yatiwe nuru, mjue tumaini la mwito wake jinsi lilivyo; na utajiri
wa utukufu wa urithi wake katika watakatifu ulivyo. Waefeso 1:18.
Sifa ya hali ya juu sana ya akili haitaweza kuchukua mahali pa unyoofu wa kweli na
utauwa halisi. Biblia yaweza kujifunzwa kama fani mojawapo ya sayansi ya kibinadamu;
ila uzuri wake, ushahidi wa uwezo wake wa kuiponya roho inayoamini, ni fundishoambalo halijifunzwi kamwe kwa njia kama hiyo. Kama mazoezi ya lile neno hayaletwi
katika maisha, basi, Roho kwa upande wake atakuwa hajaujeruhi moyo ule wa asili.
Litakuwa limefichwa katika nadharia ya ushairi tu. Hisia zitakuwa zimelifunga hata
moyo utakuwa haujasikia ukali wa ncha yake [upanga huo wa Roho], ikichoma na
kuzikatilia mbali madhabahu zake za dhambi mahali ambapo juu yake nafsi huabudiwa....
Macho ya mioyo ni lazima yatiwe nuru, na moyo na nia vipate kuletwa katika umoja na
Mungu, aliye Kweli. Yule anayemtazama yesu kwa jicho la imani haoni utukufu wo wote
ndani yake mwenyewe, maana utukufu wa Mkombozi unaakisiwa [unaangaza] kupitia
katika nia na moyo wake. Upatanisho wa damu yake unatambuliwa, na kuondolewa kwa
dhambi kunauchochea moyo kutoa shukrani.
Akiisha kuhesabiwa haki na Kristo, yule anayeipokea kweli anabidishwa kujisalimisha
kabisa kwa Mungu, naye anaingizwa katika shule ya Kristo, ili apate kujifunza kwake
yeye aliye mpole na mnyenyekevu wa moyo. Ujuzi wa upendo wa Mungu unamiminwa
moyoni mwake. Anashangilia, Lo! ni upendo ulioje! Ni kujishusha hadhi kulikoje!
Akiwa anazishikilia ahadi nyingi kwa imani, anakuwa mshiriki wa tabia ya uungu. Moyo
wake ukiisha kufanywa tupu kwa kuiondoa nafsi, ndipo maji yale ya uzima hububujika
ndani yake; utukufu wa Mungu huangaza nje. Kwa kumtazama Yesu daima, ubinadamu
unafanana na uungu. Muumini anabadilishwa na kufanana naye.... Tabia ya kibinadamu
inabadilishwa na kuwa kama ile ya Mungu. ----- Undated MS 12.
Kristo anawaona watu wake katika usafi na ukamilifu wao kama tunu ya mateso yake
yote, kudhalilishwa kwake, na upendo wake, na ongezeko la utukufu wake ----- Kristo
ndiye kitovu kile kikuu, ambacho kwacho unaangaza utukufu wake wote. ----- 4BC 1180.
KUCHIMBA MIGODI YA ILE KWELI Julai 17
Kufafanusha maneno yako kwatia nuru, Na kumfahamisha mjinga. Zaburi 119:130.
Najisikia ya kwamba nina shauku ya pekee kwa ajili ya vijana wetu wanaoipenda
kweli.... Nina dukuduku kwamba ingewapasa kusonga mbele na kupanda juu ili mpate
kukifikia kimo cha tabia ya Kikristo ambacho kimefunuliwa katika Neno la Mungu.
Hebu Neno la Mungu na liwe kiongozi wenu, ili katika kila jambo mpate kuumbwa upya
katika mwenendo na tabia yenu kulingana na matakwa yake.... Njia pekee ambayo kwayo Mkristo atajifunza na kuwa bila waa kutokana na mvuto wa
ulimwengu huu itakuwa kwa kuyachunguza Maandiko na kwa kulitii Neno la Mungu
kabisa. Shetani anacheza mchezo wa maisha kwa kila mtu, lakini hakuna anayehitaji
kushindwa kutokana na sababu zake za udanganyifu. Ni wale tu wanaokubali
madanganyo yake ambayo wataweza kudanganyika kwa mashauri yake. Lakini kama
kweli ya Mungu inayaongoza maisha, basi, ni lazima ipandikizwe moyoni. Kweli hiyo
itazaa uzuri wa kweli moyoni ambao utaonekana katika tabia. Lakini matokeo haya kama
yanapatikana, basi, itakuwa ni kwa sababu ile kweli inapaliliwa na kupendwa moyoni. ---
-- Letter 51, 1894.
Biblia haina budi kuwa kanuni yako; Maandiko hai ya Yehova yanapaswa kuwa
kiongozi wako. Yakupasa kuichimba kweli kama hazina zilizositirika: yakupasa kuipata
hazina pale pale ilipo, kisha yakupasa kulima kila inchi ya shamba lile ili kuzipata johari
zile. Yakupasa kuchimba migodi ya ile kweli kwa ajili ya johari mpya, kwa ajili ya vito
vipya, kwa ajili ya almasi mpya, nawe utazipata. ----- MS 1, 1889.
Mtafutaji kweli mwaminifu anapolisoma Neno, na kuufungua moyo wake kulipokea
Neno hilo anatamani kuipata kweli kwa moyo wake wote. Upendo, huruma, kuumia kwa
ajili ya watu wengine, heshima, upole wa Kikristo, ambazo zitakuwa ndizo sifa za lazima
na za maana katika makao yale ya mbinguni ambayo Kristo amekwenda kuwaandalia
wale wampendao, hizo zitatawala moyoni mwake. ----- 6BC 1104.
Hebu vijana na wafundishwe kupenda kujifunza Biblia. Hebu nafasi ya kwanza katika
mawazo na mapenzi yetu itolewe kwa kile Kitabu cha vitabu, kwa vile kina maarifa
tunayoyahitaji juu ya mengineyo yote. ----- CG 513.
JINSI YA KUJIFUNZA BIBLIA Julai 18
Mwayachunguza [Chunguzeni] Maandiko, kwa sababu mnadhani kwamba ninyi mna
uzima wa milele ndani yake; na hayo ndiyo yanayonishuhudia. Yohana 5:39 [KJV].
Kitabu cha vitabu vyote kina madai ya juu sana kwetu kuweza kukisikiliza kwa kicho.
Tusiridhike na maarifa ya juu juu tu, bali tunapaswa kutafuta jinsi ya kujifunza maana
kamili ya maneno ya kweli hiyo, na kunywa kwa kina roho ya Maandiko hayo
Matakatifu. Kusoma idadi fulani ya sura kila siku, au kukariri kiasi kilichowekwa [cha
mafungu] bila kutafakari kwa makini maana ya fungu hilo takatifu, ni kazi isiyokuwa na
faida sana.... Mafungu fulani ya Maandiko, kwa kweli, yako wazi mno kuweza kukosa
kuyaelewa; lakini yako mengine ambayo maana yake haipatikani juu juu, yaani, haiwezikuonekana kwa kutazama mara moja tu. Maandiko ni lazima yalinganishwe na Maandiko
[mengine]; ni lazima utafiti wa makini uwepo pamoja na tafakuri stahimilivu. Na
kujifunza kama huko kutalipwa vizuri sana. Kama vile mchimba mgodi anavyogundua
tabaka za madini ya thamani zilizofichwa chini ya uso wa ardhi, hivyo ndivyo
itakavyokuwa kwa yule anayestahimili kulichunguza Neno la Mungu kana kwamba ni
hazina iliyositirika, yaani, atakavyopata thamani kubwa mno, ambayo imefichwa kwa
macho ya mtafutaji mzembe.
Isiachwe kufanywa juhudi yo yote ya kuimarisha mazoea sahihi ya kujifunza. Kama
moyo unatangatanga, urudishe. Kama mtazamo wako kiakili na kimaadili umepotolewa
kwa hadithi za kubuni zilizotiwa chumvi mno na zinazosisimua, ... basi, wewe unayo vita
ya kupigana na nafsi yako wenyewe ili kuishinda tabia hiyo potofu.... Tumezungukwa na
kutokuamini. Hewa yenyewe inayotuzunguka inaonekana kujaa na hali hiyo. Ni kwa
juhudi inayoendelea tu tunaweza kuishinda nguvu yake.... Nawasihi vijana kwa wazee:
Lifanyeni Neno la Mungu kuwa kitabu chenu cha mafundisho. Humo mtapata kanuni ya
kweli ya tabia....
Katika shamba lote la mafunuo hayo zimetawanyika chemchemi za kweli ile ya
mbinguni, na amani, na furaha. Zinaweza kufikiwa na kila mtafutaji. Maneno hayo
yaliyovuviwa, yakitafakariwa moyoni, yatakuwa kama vijito vinavyotiririka kutoka
katika ule mto wa maji ya uzima. Mwokozi wetu aliomba kwamba akili za wanafunzi
wake zipate kuzinduliwa ili wapate kuyaelewa Maandiko. Na po pote pale tunapojifunza
Biblia kwa moyo wa maombi, Roho Mtakatifu yu karibu kutufunulia sisi maana ya
maneno yale tunayoyasoma. -----
RH, Okt.9, 1883.
BIBLIA YASEMA NAMI Julai 19
BWANA asema hivi, Simameni katika njia kuu, mkaone, mkaulize habari za mapito ya
zamani, I wapi njia iliyo njema? mkaenende katika njia hiyo, nanyi mtajipatia raha katika
nafsi zenu. Yeremia 6:16. emia 6:16. Yule aliye Mtakatifu ametoa kanuni kwa ajili ya kumwongoza kila mtu ili asiwepo awaye yote anayehitaji kupotea katika njia yake. Maagizo hayo yana maana sana kwetu; maana yanaweka kanuni ambayo kwayo kila mwana na binti ya Adamu anapaswa kufuata. Hatuwezi kugeuka kando mbali na kanuni hizi za mbinguni, bila kupatikana na hatia. Tunatakiwa kuyapa mapenzi ya Mungu kipaumbele katika maisha yetu, na kuwa na imani ile inayofanya kazi kwa upendo na kuitakasa nafsi. Ningependa kuwaonya ninyi kujitenga na uwanja ule wa hatari ambao miguu yenu kwa kawaida ingeelekea kutangatanga huko.... Lichukue Neno la Mungu, piga magoti mbele zake Mungu, uliza, Mungu ameniambia nini toka katika Neno lake? Ngojea mbele za Bwana ili kujifunza njia unayopaswa kuenenda kwayo.... Unaweza kujifunza kwa Mwalimu huyo wa Mbinguni upole na unyenyekevu wake wa moyo. Katika nguvu zake uwe imara, nawe simama na kupinga yote yale yasiyompendeza Mungu, na kuyaendeleza yote yaliyo ya haki, na yaliyo safi, na yaliyo ya kweli. Uishi maisha yale ambayo Yesu, Baba yako wa Mbinguni, na jeshi la malaika wanaweza kuyaangalia na kuyakubali.... Bwana atakuwa msaidizi wako, nawe kama ukimtegemea yeye, atakupandisha upate kukifikia kimo kilicho bora na kitukufu, naye ataiweka miguu yako juu ya jukwaa la kweli ile ya milele. Kwa njia ya neema yake Kristo, unaweza kuutumia vizuri uwezo uliokabidhiwa, na kuwa mjumbe wake daima katika kuziongoa roho kwa Kristo. Kila talanta uliyo nayo ingepaswa kutumika upande wa haki. Wale walio vijana Wanaozivaa silaha zote za Mungu, Watakaoutenga muda fulani kila siku kujichunguza wenyewe, Watakaomtafuta Bwana kwa bidii katika maombi yao, na Watakaojifunza Maandiko kwa bidii, Watapewa msaada wa malaika zake Mungu, Nao watajenga tabia zitakazowafanya wafae Kukaa na jamii ya waliokombolewa katika ufalme ule wa utukufu. ----- Letter 57, 1894. Kila andiko, lenye pumzi ya Mungu, lafaa kwa mafundisho, na kwa kuwaonya watu makosa yao, na kwa kuwaongoza, na kwa kuwaadibisha katika haki; ili mtu wa Mungu awe kamili, amekamilishwa apate kutenda kila tendo jema. 2 Timotheo 3:16,17. Hebu mtafutaji wa ile kweli anayeikubali Biblia kama Neno la Mungu lililovuviwa, aweke kando kila wazo analolithamini, na kulichukua Neno katika urahisi wake. Angepaswa kukataa katakata kila zoea la dhambi, na kuingia Patakatifu pa Patakatifu kwa moyo uliolainika na kutulizwa, tayari kusikia kile asemacho Mungu. Usiiendee Biblia ukiwa na imani ya kanisa lako (Creed), na kuyasoma Maandiko yake kwa nuru ya imani hiyo. Ukigundua kwamba maoni yako yanapingana na maneno yaliyo wazi ya "Hivi ndivyo asemavyo Bwana," au yanapingana na amri yo yote au makatazo aliyotoa, basi, wewe unapaswa kulisikiliza Neno la Mungu kuliko maneno wanayosema watu. Hebu mabishano yote au majadiliano yasuluhishwe kwa "Imeandikwa"... Hebu moyo wako na ulainishwe na kutulizwa kwa roho ya maombi kabla Biblia haijasomwa. Kweli itashinda wakati Roho wa kweli anaposhirikiana na mwanafunzi wa Biblia mnyenyekevu. Ni wazo la thamani jinsi gani ya kwamba Mwasisi wa ile kweli yu hai naye anatawala. Mwombeni aiandike mioyoni mwenu kweli yake. Kuchunguza kwenu Maandiko ndipo kutakuwa na manufaa. Kristo ndiye Mwalimu Mkuu wa wafuasi wake, naye hatawaacheni ninyi kwenda gizani. Biblia inajitafsiri yenyewe. Kwa urahisi unaopendeza sehemu moja inaungana na sehemu nyingine, mpaka Biblia yote imeunganishwa vizuri katika sehemu kuu moja inayopatana. Nuru inamulika toka katika fungu moja na kuliangazia fungu jingine katika Neno lile lililoonekana kuwa halieleweki vizuri sana. ----- RH, agosti 13, 1859. Mafundisho yake Kristo yatastahili kufanyiwa utafiti wa karibu sana. Kweli moja ikifahamika katika urahisi wake itaonekana ya kuwa ni ufunguo wa hazina zote za nyumba ya ile kweli, ambazo zinahitaji busara, mbinu, na utafiti wenye kina unaotaka bidii katika kuziokota na kuziunganisha pamoja katika mnyororo wa ile kweli. Neno ndilo nyumba ya hazina ile ya kweli. Linaweka mikononi mwetu mambo yote muhimu kwa maandalizi yetu ya kuingia katika mji ule wa Mungu. ----- MS 8, 1898. MAJANI YA MTI ULE WA UZIMA Julai 21 Yesu akawaambia, Mimi ndimi chakula cha uzima; yeye ajaye kwangu hataona njaa kabisa, naye aniaminiye hataona kiu kamwe." Yohana 6:35. Ulimwengu unaangamia kwa kuikosa kweli, kweli ile safi, isiyoghoshiwa. Kristo ndiye ile kweli. Maneno yake ndiyo kweli. ----- MS 130, 1897. Muumini, akiwa katika ushirika wa Roho, anapoishika kweli yenyewe hasa, na kuitumia, anakula mkate [chakula] ule ushukao chini kutoka mbinguni. Anaingia katika maisha yake Kristo, na kuithamini kafara ile kuu iliyotolewa kwa ajili ya wanadamu wenye dhambi. Maarifa yatokayo kwa Mungu ndiyo ule Mkate [chakula] wa uzima. Hayo ndiyo majani ya mti ule wa uzima ambayo ni kwa kuwaponya mataifa. Mkondo ule wa maisha ya kiroho huifurahisha nafsi wakati maneno yake Kristo yanaposadikiwa na kuwekwa katika matendo. Hivyo ndivyo tunavyofanywa kuwa umoja na Kristo. Uzoefu wa maisha uliokuwa dhaifu na mnyonge unageuka na kuwa na nguvu. Ni uzima wa milele kwetu iwapo tunashikamana sana na mwanzo wa ujasiri wetu mpaka mwisho. Kweli yote haina budi kupokewa kama maisha yake Yesu. Kweli inatutakasa sisi na uchafu wote, na kuutayarisha moyo kwa ajili ya kuwamo kwake Kristo. Kristo anaumbika ndani, tumaini la utukufu. ----- MS 103, 1902. Kweli inapaswa kuliwa kila siku. Hivyo tunayala maneno yake Kristo, anayoyatangaza kuwa ni roho, tena ni uzima. Kule kuipokea kweli kutamfanya kila mpokeaji kuwa mtoto wa Mungu, yaani, mrithi wa mbinguni. Kweli iliyomo moyoni si andiko baridi, yaani, lililokufa.... Kuna furaha kamili ndani ya kweli hiyo. Kuna utukufu katika maisha ya mjumbe yule wa kibinadamu anayeishi na kufanya kazi chini ya mvuto uhuishao wa ile kweli. Kweli ni takatifu na tukufu. Ina nguvu na uwezo kuliko kitu kingine cho chote katika kujenga tabia inayofanana na ile ya Kristo. Ukihifadhiwa moyoni, upendo wake Kristo ni bora kuliko upendo wa mwanadamu ye yote. Huo ndio Ukristo hasa. Hivyo kweli hiyo ----- kweli iliyo safi, yaani, isiyoghoshiwa ----- hukaa katika ngome ya mwili wa mwanadamu. Huo ndio uzima wa Mungu ulio moyoni. "Nami nitawapa ninyi moyo mpya, nami nitatia roho mpya ndani yenu." Ezekieli 36:26. ----- MS 130, 1897. MKATE [CHAKULA] UNAOSHIBISHA Julai 22 Mimi ndimi chakula [mkate] chenye uzima kilichoshuka kutoka mbinguni; mtu akila chakula hiki, ataishi milele. Na chakula nitakachotoa mimi ni mwili wangu, kwa ajili ya uzima wa ulimwengu.... Kwa maana mwili wangu ni chakula cha kweli, na damu yangu ni kinywaji cha kweli. Yohana 6:51-55. Maneno haya, "Utupe leo riziki yetu [mkate wetu wa kila siku]," yanamaanisha si chakula tu cha kimwili bali chakula cha kiroho kinachotupatia uzima wa milele kwa yule anayekipokea. Tunaposadiki na kulipokea Neno la Kristo, tunakula mwili wake na kunywa damu yake.... Kama vile kula chakula cha kimwili kunavyoufanya mfumo wa mwili kupata nguvu, hivyo ndivyo kula mwili na kunywa damu ya Mwana wa Mungu, kunavyoiimarisha tabia ya kiroho. Neno la Mungu ni roho, tena ni uzima kwa kila mmoja anayelitumia. Anayekula mwili na kunywa damu yake Kristo anakuwa mshiriki wa tabia yake ya uungu.... Mkondo wenye nguvu, uletao uzima hutiririka kutoka kwa Mwokozi kwenda kwake. ----- MS 48, 1895. Hakuna ye yote awezaye kula mwili na kunywa damu hiyo kwa niaba ya mtu mwingine. Kila mmoja sharti aje kwake Kristo akiwa na roho yake yenye njaa, yaani, kila mmoja ni lazima asadiki yeye mwenyewe, ajisikie kuwa anayo haja ya rohoni mwake mwenyewe. - ---- MS 29, 1896. Tukijazwa na Mkate huo wa Uzima, hatuwezi kuwa na njaa ya vishawishi vya ulimwengu huu, wala misisimko ya ulimwengu huu, wala utukufu uliomo ulimwenguni humu. Uzoefu wetu wa kidini utakuwa wa aina ile ile kama chakula kile tulacho. ----- MS 50, 1895. Chakula tunachokula katika mlo mmoja hakitutoshelezi [hakikidhi njaa yetu] milele. Kila siku ni lazima tule chakula hicho. Kwa hiyo, kila siku yatupasa kula Neno la Mungu ili uzima nafsini mwetu upate kufanywa mpya. Ndani ya wale wanaokula kila siku Neno hilo, Kristo anaumbika, tumaini la utukufu. Kupuuzia kusoma na kujifunza Biblia huleta njaa ya kiroho.... Kristo ndiye uzima wetu. Moyo ule anamokaa utatimiza matakwa ya kanuni zake kwa kumcha yeye kabisa na kujitoa wakf kwa Mungu. Kristo anapougusa moyo anaujenga, UKUTA WA MOTO DHIDI YA MAJARIBU Julai 23 Moyoni mwangu nimeliweka neno lako, Nisije nikakutenda dhambi. Zaburi 119:11. Shetani anatafuta daima kuishawishi mioyo ya wanadamu kwa hila zake. Yeye ndiye mwanzilishi mwamba; alipewa uwezo huo na Mungu, lakini akauharibu uwezo wake wote mtukufu kwa kuyapinga na kuyafanya mashauri yake yule Aliye juu sana yasiwe na maana yo yote.... Tunaweza tu kushinda kwa kulisadiki kila neno litokalo katika kinywa chake Mungu. Yatupasa kujua kile kilichoandikwa ili tusishindwe na madanganyo na uchawi wake Shetani.... Iwapo tumenaswa kwa uwezo wake ulio kama uchawi, basi, hebu katika jina lake Yesu na tuukemee uwezo wake, na kujitenga na Shetani pasipo kuchelewa.... Wale wanaomlilia Mungu ili awaokoe kutokana na uchawi wa kutisha ambao Shetani anataka kuwatupia, itawapasa kuyathamini sana Maandiko. Usalama wetu pekee ni katika kuipokea Biblia nzima, si kwa kuchukua mafungu yale tu yaliyojitenga, bali kwa kuiamini kweli yote. Miguu yako iko juu ya mchanga unaonyiririka kama wewe unalihafifisha neno moja lililoandikwa. Biblia ni mawasiliano yatokayo mbinguni, tena ni ujumbe hai kwa ajili ya roho zetu kana kwamba sauti kutoka mbinguni ilikuwa imesikika ikisema nasi. Kwa kicho gani na heshima na unyenyekevu tungekuja kuyachunguza Maandiko, ili tupate kujifunza mambo yale ya milele.... Hebu kila mmoja na ajifunze Biblia yake, akijua kwamba Neno la Mungu linadumu milele kama kilivyo kiti chake cha enzi ambacho ni cha milele. Kama ukija kujifunza Maandiko kwa unyenyekevu, kwa maombi ya dhati ukitaka uongozi wake, basi, malaika wake Mungu watakufunulia mambo yake yaliyo hai; na kama unazihifadhi kweli hizo, basi, zitakuwa kwako kama ukuta wa moto dhidi ya majaribu, madanganyo, na uchawi wa Shetani.... Neno la Mungu linaweza kuziokoa roho zenu, yaani, kuwafanya mwe na hekima hata kupata wokovu. Mtunga Zaburi asema hivi, "Moyoni mwangu nimeliweka neno lako, nisije nikakutenda dhambi." Basi na tulifiche Neno la Mungu mioyoni mwetu, ili tu"pate kuweza kushindana siku ya uovu, na [tu]kiisha kuyatimiza yote, kusimama." Waefeso 6:13. ---- ST, Sept. 18, 1893. KWELI INAENDELEA KUFUNULIWA Julai 24 Hata bado nikali ninayo mengi ya kuwaambia, lakini hamwezi kuyastahimili hivi sasa. Yohana 16:12. Ufahamu mfinyu na wenye mwelekeo wa kidunia waliokuwa nao wanafunzi wake juu ya mafundisho ya Kristo ulifanya iwe vigumu kwa Mwalimu Mkuu kuiongoza mioyo yao kuyafahamu mambo ya mbinguni, na uliweka kiwango cha mawasiliano yake ya Uungu.... Kazi yake hasa ilikuwa kudhihirisha tabia bora ya kimaadili ambayo Bwana anataka. ----- MS 23, 1889. Kristo hakutoa maoni yake kamili au hotuba zilizounganishwa juu ya mafundisho ya dini, lakini mara nyingi alisema kwa sentensi fupi fupi, kama mmoja ambaye alipanda mbegu za mbinguni za mafundisho ya dini mfano wa lulu zinazohitaji kukusanywa na mtenda-kazi mwenye utambuzi.... Wanafunzi wa kweli, wakiketi chini ya miguu yake Kristo, wanavumbua johari hizo za thamani za ile kweli ambazo zilinenwa na Mwokozi wetu, nao wanatambua umuhimu wake na kuzithamini sana. Zaidi na zaidi, kadiri wanavyokuwa wanyenyekevu na kuwa tayari kufundishwa, ndivyo kadiri ufahamu wao unavyozinduliwa ili wapate kugundua mambo ya ajabu katika Sheria yake.... Kweli itaendelea kufunuliwa daima, ikipanuka, na kukua, kwa maana ni takatifu, kama alivyo Mwasisi wake. ----- MS 23, 1889. ukua, kwa maana ni takatifu, kama alivyo Mwasisi wake. ----- MS 23, 1889. Yesu asema, "Hata bado nikali ninayo mengi ya kuwaambia, lakini hamwezi kuyastahimili hivi sasa." Yohana 16:12. " 'Hamwezi kuyastahimili hivi sasa,' Ni huruma ilioje inayoonekana katika lugha hii! Inaeleza vizuri kanuni Yako ya kufundisha. 'Huku kidogo na huku kidogo,' Huo ndio mpango ambao Wewe unaufuata; Ukingojea mpaka macho yetu dhaifu yanapoweza kustahimili Kweli zile ambazo upendo wako unazifunua mbele ya macho yetu. Huo ni upole wake Kristo! Bwana, je! sisi katika kuwafundisha wengine tusijitahidi kufanya kama Wewe! Mvumilivu, usiye na haraka, kwa wale wanaojifunza Lakini polepole katika shule Yako; wale wanaoonekana kuhitaji Mstari juu ya mstari kabla hawajaweza kutambua Mafundisho matakatifu tunayoyasoma kwa wazi sana." ----- Letter 9, 1873. UWEZO UTAKASAO WA ILE KWELI Julai 25 Uwatakase kwa ile kweli; neno lako ndiyo kweli. Yohana 17:17. Utakaso ni nini? Ni kujitoa nafsi yako kabisa na bila kubakiza kitu ---- roho, mwili, na nafsi ----- kwa Mungu; kutenda haki; kupenda rehema, na kwenda kwa unyenyekevu na Mungu wako; kuyajua na kuyatenda mapenzi ya Mungu bila kujali nafsi yako wala mambo yako uyapendayo; kuwa na nia inayowaza mambo ya mbinguni, yaliyo safi, yaani, isiyo na uchoyo, takatifu, na isiyo na doa wala waa. ----- Letter 9, 1893. Ni kwa njia ya ile kweli, kwa uweza wa Roho Mtakatifu, tunapaswa kutakaswa ----- yaani, kubadilishwa katika mfano wake Kristo. Ili badiliko hilo lipate kutokea ndani yetu, ni lazima pawepo na ukubali usiokuwa na masharti yo yote, wa moyo wote kwa ile kweli, kujisalimisha roho yetu bila kubakiza kitu kwa nguvu yake [ile kweli] itakasayo. Tabia zetu kwa asili zimepotoka na kuharibika. Kwa kukosa kukuzwa ipasavyo zina upungufu katika mlingano wake. Tabia zetu bora zimeunganishwa na tabia za kuchukiza, na kwa mazoea ya muda mrefu mielekeo hiyo mibaya huwa sehemu ya tabia, na watu wengi huzing'ang'ania sana tabia zao za ajabu. Hata baada ya kukiri kuipokea kweli, yaani, kujitoa wenyewe kwa Kristo, tabia zile zile za zamani zinaendekezwa, kujisifu wenyewe kule kule hudhihirishwa, maoni yale yale ya uongo hukaribishwa. Japokuwa watu kama hao hudai kwamba wameongoka, ni dhahiri kwamba hawajajitoa wenyewe kubadilishwa na uweza ule wa ile kweli.... Iwapo yule anayemwakilisha vibaya Kristo kwa jinsi hiyo angejua madhara yaliyoletwa na kasoro zake alizo nazo katika tabia yake ambazo amezitolea udhuru na kuzipenda, basi, angejazwa na hofu.... Hebu na asiwepo mtu awaye yote anayejisikia kwamba hana haja ya kubadili njia yake.... Hakuna awezaye kwenda salama isipokuwa akiacha kujitumainia nafsi yake, na kulitegemea Neno la Mungu daima, akijifunza hilo kwa hiari ili kuyaona makosa yake, na kujifunza mapenzi yake Kristo, na kuomba ya kwamba yatimizwe ndani yake na kwa njia yake na kupitia kwake. Wataonyesha ya kwamba tumaini lao si katika nafsi zao, bali katika Kristo. Wataishika kweli kama hazina takatifu, iwezayo kuwatakasa na kuwaadilisha, nao watatafuta daima kuyaleta maneno yao na njia zao katika mwafaka na kanuni zake [hiyo kweli]. ----- RH, Aprili 12, 1892. "IWENI WATAKATIFU ZAIDI, NAAM, ZAIDI SANA" Julai 26 Maana haya ndiyo mapenzi ya Mungu, kutakaswa kwenu, mwepukane na uasherati.yo mapenzi ya Mungu, kutakaswa kwenu, mwepukane na uasherati. l Wathesalonike 4:3. Utakaso wetu ndilo lengo lake Mungu katika kushughulika kwake na sisi. Ametuchagua tangu milele ili tuwe watakatifu. Kristo alijitoa nafsi yake kwa ajili ya ukombozi wetu, ili kwa njia ya imani katika uweza wake wa kutuokoa toka dhambini, tupate kutimilika ndani yake.... Sisi kama Wakristo tumeahidi wenyewe kutimiza wajibu wote unaotukalia, na kuuonyesha ulimwengu ya kuwa sisi tuna uhusiano wa karibu sana na Mungu. Hivyo, kwa njia ya matendo mema na kazi za wanafunzi wake, Kristo hana budi kuwakilishwa na kuheshimiwa. Mungu anatutazamia sisi kuwa na utii mkamilifu kwa Sheria yake. Sheria hiyo ni mwangwi wa sauti yake, ikisema kwetu, Iweni watakatifu zaidi, naam, zaidi sana. Takeni utimilifu wa neema yake Kristo, naam, takeni sana ----- iweni na njaa na kiu ----- ya haki. Ahadi ni hii, "[M]TAshibishwa." Mioyo yenu na ijazwe na tamaa ya kuipata haki hiyo.... Mungu amenena wazi ya kwamba anatutazamia sisi kuwa wakamilifu, na kwa vile anatazamia hivyo, ameweka msaada kwa ajili yetu ili tupate kuwa washirika wa tabia yake ya uungu. Ni kwa njia hiyo tu tunaweza kupata ushindi katika jitihada yetu ya kupata uzima wa milele. Uwezo huo unatolewa na Kristo. "Bali wote waliompokea aliwapa uwezo wa kufanyika watoto wa Mungu, ndio wale waliaminio jina lake." Yohana 1:12. Watu wa Mungu wanatakiwa kuakisi [kuangaza] ulimwenguni mionzi inayong'aa ya utukufu wake. Lakini ili wao waweze kufanya hivyo, wanapaswa kusimama mahali mionzi hiyo inapoweza kuwaangukia juu yao. Ni lazima washirikiane na Mungu. Moyo sharti utakaswe kwa kuyaondoa mambo yote yanayouelekeza kwenye dhambi. Neno la Mungu linapaswa kusomwa na kujifunzwa kwa hamu ya dhati ili kupata nguvu ya kiroho kutokana nalo. Mkate huo wa mbinguni ni sharti uliwe na kuingia mwilini na kuwa sehemu ya maisha yetu. Hivyo ndivyo tunavyopata uzima wa milele. Hivyo ndivyo sala ya Kristo inavyojibiwa, aliyosema, "Uwatakase kwa ile kweli, neno lako ndiyo kweli." Yohana 17:17. "Haya ndiyo mapenzi ya Mungu, kutakaswa kwenu." Je, ni mapenzi YAKO kwamba tamaa zako pamoja na mielekeo yako ipatane na mapenzi hayo ya Mungu? ----- RH, Jan. 28, 1904.SIRI YA UTAKATIFU Julai 27 Mkavae utu mpya, ulioumbwa kwa namna ya Mungu katika haki na utakaktifu wa kweli. Waefeso 4:24. Hakuna mtu awaye yote anayeupokea utakatifu kama haki yake ya kuzaliwa nayo, au kama zawadi kutoka kwa mwanadamu mwingine awaye yote. Utakatifu ni kipawa cha Mungu kwa njia ya Kristo. Wale wanaompokea Mwokozi wanakuwa wana wa Mungu. Ni watoto wake wa kiroho, waliozaliwa mara ya pili, waliofanywa upya katika haki na utakatifu wa kweli. Mapenzi yao yamegeuzwa. Wakiwa wanaona vizuri zaidi wanayatazama mambo yale ya milele. Wameingizwa katika familia yake Mungu, nao wanafananishwa na mfano wake, wakibadilishwa na Roho wake toka utukufu hata utukufu. Kutoka katika hali yao ya kuipenda mno nafsi yao, wanabadilishwa na kumpenda sana Mungu na Kristo.... Kumpokea Kristo kama Mwokozi wako binafsi, na kufuata kielelezo chake cha kujikana nafsi ----- hiyo ndiyo siri ya utakatifu. ----- 6BC 1117. Utakatifu sio kuwa na furaha nyingi sana; ni matokeo ya kutoa yote kwa Mungu; ni kuishi kwa kila neno litokalo katika kinywa chake Mungu; ni kufanya mapenzi ya Baba yetu aliye mbinguni, ni kumtegemea Mungu katika maonjo, kuamini ahadi yake katika giza kama vile katika nuru. Dini ni kwenda kwa imani, pamoja na kwenda kwa kuona, kumtegemea Mungu kwa imani yote, na kukaa katika pendo lake. ----- YI, Feb. 17, 1898. Utakaso ni hali ya utakatifu, nje na ndani, kuwa mtakatifu na kuwa wake Bwana bila kubakiza kitu, si kwa mtindo tu, bali katika kweli. Kila uchafu wa mawazo, kila tamaa mbaya ya mwili, huitenga roho mbali na Mungu; kwa maana Kristo kamwe hawezi kuliweka vazi lake la haki juu ya mwenye dhambi, yaani, kuufunika ulemavu wake.... Lazima iwepo kazi inayoendelea ya kupata ushindi juu ya uovu, ya kushirikiana na mema, yaani, kuiakisi [kuiangaza] tabia ya Yesu. Yatupasa kwenda katika nuru, ambayo itaongezeka na kung'aa zaidi mpaka siku ile kamilifu. Huku ni kukua hasa na kuwa imara, ambako hatimaye kutawafikisha wanaume na wanawake kwenye cheo cha kimo cha utimilifu wake Yesu Kristo.... Kufananishwa na mfano wa tabia yake Kristo, kushinda dhambi zote na majaribu, kwenda kwa kicho chake Mungu, kumweka Bwana mbele yetu daima, kutaleta amani na furaha duniani, na kutuhakikishia furaha takatifu kule mbinguni. ----- Letter 12, 1890. UZOEFU WA KILA SIKU WA KUONGOKA Julai 28 Kwa hiyo hatulegei; bali ijapokuwa utu wetu wa nje unachakaa, lakini utu wetu wa ndani unafanywa upya siku kwa siku. 2 Wakorintho 4:16. Kuongoka kweli kweli kunahitajika, si mara moja kwa miaka, bali kila siku. Kuongoka huku humleta mwanadamu katika uhusiano mpya na Mungu. Mambo ya kale, tamaa zake mbaya za asili na mielekeo yake mibaya ya kurithi na kujizoeza mwenyewe, hupita, naye hufanywa upya na kutakaswa. Lakini kazi hiyo ni lazima iwe ya kudumu; kwa maana kadiri Shetani anavyozidi kuwako, ndivyo atakavyozidi kufanya juhudi ya kuiendeleza kazi yake hiyo. Yule anayejitajidi kumtumikia Mungu atapambana na mkondo wa chini wenye nguvu unaotaka kumwelekeza kwenye uovu. Moyo wake unahitaji kuzungushiwa boma kwa njia ya kukesha na kuomba daima, la sivyo, boma hilo litabomoka; na kama vile mto ule unaoendesha kinu, mkondo wa chini wa uovu utaifagilia mbali kinga hiyo. Hakuna moyo wo wote uliofanywa upya unaoweza kuwekwa katika hali ya utamu pasipo matumizi ya kila siku ya chumvi ya lile Neno. Neema ya Mungu ni lazima ipokewe kila siku, la sivyo, hakuna mtu awaye yote atakayeendelea kuwa katika hali ya kuongoka.... Majaribu na maonjo yatamjia kila mtu ampendaye Mungu. Bwana hafanyi mwujiza wo wote kuzuia majaribu hayo makali, yaani, kuwakinga watu wake kutokana na majaribu ya yule adui.... Tabia zile zinapaswa kukuzwa zitakazoamua kufaa kwa familia ya kibinadamu kukaa katika makao yale ya mbinguni ----- tabia zile zitakazostahimili msongo wa mambo yasiyofaa katika maisha ya faragha kwa neema yake Mungu zitakuwa za kishujaa na za kweli, zitakuwa imara kama mwamba katika kuzitetea kanuni, nazo zitatoka katika majaribu hayo ya moto zikiwa na thamani kubwa kuliko dhahabu ya Ofiri yenye umbo la kabari. Mungu ataidhinisha kwa maandishi yake mwenyewe ya kuwa hao ni wateule wake, yaani, wale walio na tabia kama hizo.... Bwana haikubali kazi inayofanywa nusu nusu. Anamtaka mtu mzima. Dini inatakiwa kuletwa katika sehemu zote za maisha, kuingizwa katika kazi za kila namna. Mwili wote unatakiwa kuwa chini ya utawala wa Mungu. Hatupaswi kufikiri kwamba tunaweza kuyachunga mawazo yetu wenyewe. Hayana budi kutekwa nyara na Kristo. Nafsi haiwezi kuiongoza nafsi; haitoshi kwa kazi hiyo.... Ni Mungu peke yake awezaye kutufanya na kutulinda sisi kuwa watiifu kwake. ----- RH, Sept. 14, 1897. KATIKA MWANGA WA JUA LA KRISTO Julai 29 Kwa hiyo hatulegei; bali ijapokuwa utu wetu wa nje unachakaa, lakini utu wetu wa ndani unafanywa upya siku kwa siku. 2 Wakorintho 4:16. Kuongoka kweli kweli kunahitajika, si mara moja kwa miaka, bali kila siku. Kuongoka huku humleta mwanadamu katika uhusiano mpya na Mungu. Mambo ya kale, tamaa zake mbaya za asili na mielekeo yake mibaya ya kurithi na kujizoeza mwenyewe, hupita, naye hufanywa upya na kutakaswa. Lakini kazi hiyo ni lazima iwe ya kudumu; kwa maana kadiri Shetani anavyozidi kuwako, ndivyo atakavyozidi kufanya juhudi ya kuiendeleza kazi yake hiyo. Yule anayejitajidi kumtumikia Mungu atapambana na mkondo wa chini wenye nguvu unaotaka kumwelekeza kwenye uovu. Moyo wake unahitaji kuzungushiwa boma kwa njia ya kukesha na kuomba daima, la sivyo, boma hilo litabomoka; na kama vile mto ule unaoendesha kinu, mkondo wa chini wa uovu utaifagilia mbali kinga hiyo. Hakuna moyo wo wote uliofanywa upya unaoweza kuwekwa katika hali ya utamu pasipo matumizi ya kila siku ya chumvi ya lile Neno. Neema ya Mungu ni lazima ipokewe kila siku, la sivyo, hakuna mtu awaye yote atakayeendelea kuwa katika hali ya kuongoka.... Majaribu na maonjo yatamjia kila mtu ampendaye Mungu. Bwana hafanyi mwujiza wo wote kuzuia majaribu hayo makali, yaani, kuwakinga watu wake kutokana na majaribu ya yule adui.... Tabia zile zinapaswa kukuzwa zitakazoamua kufaa kwa familia ya kibinadamu kukaa katika makao yale ya mbinguni ----- tabia zile zitakazostahimili msongo wa mambo yasiyofaa katika maisha ya faragha kwa neema yake Mungu zitakuwa za kishujaa na za kweli, zitakuwa imara kama mwamba katika kuzitetea kanuni, nazo zitatoka katika majaribu hayo ya moto zikiwa na thamani kubwa kuliko dhahabu ya Ofiri yenye umbo la kabari. Mungu ataidhinisha kwa maandishi yake mwenyewe ya kuwa hao ni wateule wake, yaani, wale walio na tabia kama hizo.... Bwana haikubali kazi inayofanywa nusu nusu. Anamtaka mtu mzima. Dini inatakiwa kuletwa katika sehemu zote za maisha, kuingizwa katika kazi za kila namna. Mwili wote unatakiwa kuwa chini ya utawala wa Mungu. Hatupaswi kufikiri kwamba tunaweza kuyachunga mawazo yetu wenyewe. Hayana budi kutekwa nyara na Kristo. Nafsi haiwezi kuiongoza nafsi; haitoshi kwa kazi hiyo.... Ni Mungu peke yake awezaye kutufanya na kutulinda sisi kuwa watiifu kwake. ----- RH, Sept. 14, 1897. KATIKA MWANGA WA JUA LA KRISTO Julai 29 Ili tusiwe tena watoto wachanga, tukitupwa huku na huku, na kuchukuliwa na kila upepo wa elimu, kwa hila ya watu, kwa ujanja, tukizifuata njia za udanganyifu. Lakini tuishike kweli katika upendo na kukua hata tumfikie yeye katika yote, yeye aliye kichwa, Kristo. Waefeso 4:14,15. "Kesh[a] [u]ombe," nawe utazidi kukua katika neema na katika kumjua Kristo. Uzoefu wako hautakuwa wa upande mmoja, uliodumaa, bali wenye afya, wenye ulinganifu. Bila kujitambua mwenyewe, utakuwa umekua kama mwerezi unaotandaza matawi yake mbali, na wengi watafaidika kwa ushauri wako; ushirikiano wako pamoja nao utakuwa na manukato ya mbinguni. Kuna wengi wanaokiri ya kwamba wao ni wanadini ambao hawajakua hata inchi moja kwa miaka mingi. Takataka za ulimwengu, uchoyo, na uzembe, vimewatenga na huruma zao na kazi zao mbali na Kristo.... Kama wewe unaishi katika mwanga wa jua la Kristo, basi, utatawanya nuru kwa watu wale walio maskini ambao wamedumaa katika maisha yao ya kidini. Ukiwa umefunikwa na haki ya Kristo, ni kitu gani usichoweza kufanya kuwabariki wengine!... Ushirika wako ni pamoja na Baba na Mwana, nawe unakua kwa kuujua utimilifu wa uungu. Unakua katika kicho chako kwake, unapata ujasiri wa kuzungumza na Mungu. Ukimtazama Yesu bila kusita, unakua katika imani, nawe unapojifunza kutojitumainia nafsi yako, hapo ndipo utayathamini maneno yake Kristo, aliyosema, "Pasipo mimi ninyi hamwezi kufanya neno lo lote." Yohana 15:5.... Unaweza kuwa na nia ya dhati, moyo wako wote ukiwaka moto kwa upendo wa Yesu. Kaa ndani yake Kristo kama vile tawi linavyokaa katika mzabibu; likipata lishe yake kutoka katika mzabibu huo, wewe utakuwa tawi linalositawi, nawe utazaa matunda mengi kwa ajili ya utukufu wake Mungu. Oo! unahitaji sana kukaza macho yako kwa Yesu! Endelea kuutazama uzuri wake. Ukitazama utauona ukizidi kung'aa na kuongezeka mpaka hapo utakapokuwa umejazwa na utimilifu wote wa Mungu na kuzaa sana matunda kwa ajili ya utukufu wake. Tawi linaunganishwa na mmea mzazi na kuwa imara sana kiasi cha kutoweza kusukwasukwa huku na huku na kila upepo ulio mwanana. Nguvu na ukuaji wako wa haraka unauambia ulimwengu kwamba mzizi wako u ndani ya Kristo, yaani, kwamba msingi wako ni imara. ----- Letter 5b, 1891.JINSI YA KUKUA KATIKA NEEMA Julai 30 Lakini, kueni katika neema, na katika kumjua Bwana wetu na Mwokozi Yesu Kristo. Utukufu una yeye sasa na hata milele. 2 Petro 3:18. Hivi yawezekanaje kwetu sisi kwamba tuweze kukua katika neema? Yawezekana kwetu sisi wakati ule tu tunapoiacha tupu mioyo yetu kwa kuiondoa nafsi yetu humo, kisha kuikabidhi [mioyo yetu] kwa Mungu, ipate kuumbwa upya kwa mfano wake Mungu. Tunaweza kuunganishwa na ile njia hai ya nuru; tunaweza kuburudishwa kwa umande ule wa mbinguni, na kupata manyunyu ya mbinguni juu yetu. Tunapoutumia mbaraka huo wa Mungu, tutaweza kupokea vipimo vikubwa zaidi vya neema yake. ----- 7BC 947. Sisi, kama watoto wadogo, tunapaswa kukaa miguuni pake Kristo, tukijifunza kwake.... Tusingeruhusu siku hata moja kupita bila kupata ongezeko la maarifa katika mambo ya kidunia na ya kiroho. Tusizipige mambo zo zote ambazo hatuwezi kuzing'oa na kuzipiga mbele zaidi, karibu na miinuko tunayotumainia kuipanda. Elimu ya juu kuliko zote hupatikana kwa kuzielimisha akili zetu kusonga mbele siku kwa siku. Mwisho wa kila siku ungetukuta tukiwa tumesafiri mwendo wa siku moja karibu zaidi na thawabu ile ya mshindi. Siku kwa siku ufahamu wetu unatakiwa kupevuka. Siku kwa siku tunapaswa kutoa maamuzi yetu yatakayotuletea thawabu nyingi katika maisha haya na katika maisha yale yajayo. Tukimtazama Yesu daima, badala ya kutazama kile tulichokwisha kufanya tayari, tutapiga hatua zinazoonekana katika maendeleo yetu katika mambo yale yanayohusu maisha haya pamoja na yale yanayohusu maarifa ya kiroho. Mwisho wa mambo yote umekaribia. Kile tulichokwisha kukifanya kisiwe kizuizi kwa kazi ya Mungu. Mkuu wa wokovu wetu asema, "Songeni mbele. Usiku waja asipoweza mtu kufanya kazi." Daima yatupasa kuzidi kuwa watu wenye manufaa [kwa wengine]. Maisha yetu sikuzote yanapaswa kuwa chini ya uweza wake Kristo. Taa zetu zinapaswa kuendelea kuwaka sana.... Yule anayejiweka mahali ambapo Mungu anaweza kumwelimisha, husonga mbele, kama ilivyo, kutoka katika hali ile ya utusitusi ya mapambazukoni kwenda kwenye nuru kamili ya adhuhuri. ----- ML 109. Kila musuli wetu na neva ya kiroho ni lazima tuvitumie kwa ukamilifu kabisa.... Mungu... hapendi wewe ubaki katika hali ya kuwa mwanafunzi. Anataka wewe upate kuifikia hatua ya juu kabisa ya ngazi ile, na kutoka kwayo [hiyo ngazi] upate kupiga hatua na kuingia katika ufalme wa Bwana wetu na Mwokozi Yesu Kristo. ----- MS 8, 1899. "KARIBU SANA KUUFIKIA UTUKUFU WALIO NAO MALAIKA" Julai 31 Lakini mwenye haki ataishika njia yake, Na mwenye mikono safi atazidi kupata nguvu. Ayubu 17:9. Mungu amemkabidhi kila mtu talanta zinazopaswa kukuzwa kwa busara. Endapo zikitumika vizuri, talanta hizo zitaakisi [zitaangaza kwa] utukufu wa Mpaji. Lakini zawadi za thamani sana kutoka kwa Mungu zinaweza kutumika vibaya, na hivyo kugeuka na kuwa laana badala ya baraka.... Bwana amempa mwanadamu uwezo wa kuendelea mbele daima, naye amempa kila msaada unaowezekana katika kazi hiyo. Kwa msaada wa neema ya Mungu, tunaweza kuufikia utukufu walio nao malaika. Itasemwa nini juu ya wale ambao, baada ya kupata uzoefu wa miaka mingi katika kweli, pamoja na manufaa mengi ya kukua katika neema, wao bado mwelekeo wao ni katika ulimwengu huu, nao hupendezwa sana na burudani zake pamoja na maonyesho yake? Badala ya wao kwenda mbele toka nguvu hata nguvu, kidogo kidogo wanajitenga mbali na Mungu, na kupoteza maisha yao ya kiroho.... Talanta kamwe haiwezi kuwa badala ya kumcha Mungu, wala sifa za wanadamu haziwezi kutupatia sisi upendeleo wa kukubaliwa na Mungu. Wengi wa wale wanaojidai kuwa Wakristo wanachohitaji hasa ni kuongoka kabisa. Iwapo moyo ni mwema, basi, matendo yatakuwa mema. Mvuto wa kidunia unaodhalilisha huonekana katika tabia na maisha ya wale ambao mioyo yao haiwaki kwa moto wa wema ule wa kweli. Wengi mno wanaojidai kwamba wanamfuata Kristo, hujisikia kuwa wako huru kufuata maoni yao wenyewe, na kujifurahisha wenyewe katika tamaa za mioyo yao. Yule anayetaka kusonga mbele katika maisha haya ya Kikristo ni lazima atumie mikono yake mwenyewe na moyo wake katika kazi hii. Marafiki wanaweza kumwonya na kumshauri, yaani, kumshurutisha asonge mbele na kupanda juu; Mbingu inaweza kuimwaga mibaraka yake iliyochaguliwa vizuri sana juu yake; anaweza kupewa kila msaada unaowezekana toka upande wa kuume na toka upande wa kushoto, walakini yote hayo yatakuwa ni bure kabisa, isipokuwa kama yeye atatumia juhudi yake kwa dhati kujisaidia mwenyewe. Ni yeye mwenyewe anayelazimika kuingia katika pambano hili dhidi ya dhambi na Shetani, ama sivyo, ataukosa uzima ule wa milele. ----- RH, Juni 20, 1882. Dini safi daima humwongoza juu yule aliye nayo, humchochea apate kuwa na makusudi yaliyo bora, humfundisha kuvaa mavazi yenye heshima, na kulipa kila tendo analotenda heshima yake linayostahili. ----- RH, Juni 20, 1882.UMUHIMU WA KUIDHIBITI NAFSI Agosti 1 Mkumbuke Muumba wako siku za ujana wako, Kabla hazijaja siku zilizo mbaya, Wala haijakaribia miaka utakaposema, Mimi sina furaha katika hiyo. Mhubiri 12:1. Nawezaje kuweka mbele ya vijana umuhimu wa kuidhibiti nafsi, hili ndilo swali ninalojiuliza daima. Ningewasisitizia vijana kuiona kila dakika ya muda walio nao kama dhahabu. Msizipoteze kwa kukaa kivivu; msizitumie katika mambo yenu ya kipumbavu; bali zishikilieni kwa nguvu hazina zile zilizoko juu. Yadhibitini mawazo yetu na kuupanua moyo wenu kwa kuvifunga viuno vya nia zenu, msiziruhusu zijazwe na mambo yasiyo na maana yo yote. Jipatieni kila faida iliyo katika uwezo wenu kwa kuziimarisha akili zenu. Msitosheke na kiwango cha chini mlichokifikia. Msikae raha mustarehe mpaka kwa juhudi yenu ya uaminifu, kukesha, na bidii katika maombi, mwe mmejipatia hekima ile itokayo juu. Kwamba mpate kukua katika tabia zenu, na kuwa na mvuto juu ya mioyo ya wengine, mkiwezeshwa kuwaelekeza katika njia ile ya unyofu na utakatifu. Hii ndiyo faida yenu kubwa. Hifadhi kila mwonzi wa nuru unayoweza kuipata kwa kulichunguza Neno la Mungu. Fanya kazi ile aliyokupa Mungu leo hii, nawe angalia ni wema kiasi gani unaoweza kuutenda kwa nguvu zake Kristo. Mfanye Mungu kuwa mshauri wako. Udhibiti na kuuongoza uwezo wa akili yako. Kujitawala nafsi ni uwezo ambao wote wanaweza kuwa nao. Unapatikana kwa njia ya kuyaweka kabisa mapenzi yako upande wa Mungu, ukiyachukua mapenzi ya Mungu badala ya mapenzi yako. Kristo anaweza na ataweza kuvijaza na Roho wake Mtakatifu vyumba vya moyo wetu pamoja na nafasi za nafsi zetu zilizojificha ndani sana kama tunajinyenyekeza kwake. Hapo ndipo mapenzi yetu yatakapopatana kabisa na mapenzi ya Mungu. Roho zetu zitafanana na Roho wake na mapenzi yake, na hata katika mawazo na makusudi yetu tutakuwa kitu kimoja naye. Hapo ndipo Shetani hataweza kututawala sisi tena. Kristo ni Kiongozi wetu, na wafuasi wake hupenda kwenda hatua kwa hatua pamoja naye. Anasema, na wao wanaitii sauti yake kwa nia moja na roho moja. ----- MS 128, 1898. Mpendwa kijana, jambo bora kupita yote unaloweza kufanya ni kujiandikisha kwa hiari yako na kwa vyo vyote vile katika jeshi lake Bwana. Jisalimishe mwenyewe mikononi mwake Mungu, ili mapenzi na nia yako vipate kuongozwa na Yule ambaye hakosei katika hekima yake, naye anazo fadhili zake zisizokoma.... Hebu jina lako na liandikwe katika kumbukumbu zile za mbinguni kama mmojawapo wa waliochaguliwa na wateule wake Mungu. ----- YI, Aprili 26, 1894. KUCHAGUA KAZI YANGU YA MAISHA Agosti 2 Maana siku ile itadhihirisha, kwa kuwa yafunuliwa katika moto; na ule moto wenyewe utaijaribu kazi ya kila mtu, ni ya namna gani. l Wakorintho 3:13. Tungepaswa kuyapima kwa makini sana mambo yale yanayohusiana na kazi tunayochagua. Je, kazi hii itakuwa mbaraka kwa roho za watu? Mungu hajatupa sisi kazi kwa ajili tu ya kutushughulisha, bali kwa ajili ya utukufu wake. Wengi wanashughulika sana kukusanya miti, majani makavu, na mabua. Lakini vyote hivyo vitateketezwa.... Kwa uteuzi wake Mungu kila mtu ana mahali pake pa kazi. Hoja ambayo inatakiwa kufanyika kwa uangalifu na maombi ni hii, Ni majukumu gani kila mmoja wetu amepewa, kama wanaume na wanawake wanaowajibika kwa Mungu? Na iwapo kazi yetu yote inahusu mambo yale ya kiroho tu, ama iwapo imechanganyika na mambo ya maisha haya ya kawaida na mambo ya kiroho, basi, sisi tunatakiwa kutekeleza kazi yetu kwa uaminifu. Mambo ya kidunia na mambo ya kiroho hayana budi kuchanganywa pamoja, ila mambo ya kiroho hayatakiwi kufunikwa na mambo ya kidunia. Kristo anataka huduma toka kwa mtu mzima, yaani, kwa kutumia nguvu zake za kimwili, kiakili, na kimaadili zikiwa zimechanganywa pamoja. Hizo zinatakiwa kutumika katika kazi ya Mungu. Mwanadamu anapaswa kukumbuka ya kwamba ni Mungu anayemiliki vyote, na ya kwamba mambo yale anayoyatafuta hayana budi kuvikwa na utakatifu ambao hayakuwa nao zamani kabla ya yeye kujiunga katika jeshi hilo la Bwana. Kila tendo halina budi kuwa tendo la kujitoa wakf, maana linachukua talanta ya Mungu ya wakati ambayo tumekabidhiwa. Utakatifu kwa Bwana huandikwa juu ya matendo yote ya mtu kama huyo, kwa sababu mwili wake wote unaletwa chini ya utawala wa Mungu. Shughuli yo yote ile isifanywe, hata katika maisha haya ya kawaida, kama mvuto wake unaleta ubaya katika fahamu zako. Tu katika shule ya mafunzo ya Bwana, naye ana njia zake alizoziteua mwenyewe ambazo kwazo tunaweza kuingizwa katika kazi yake.... Wengi wanasumbuka kwa sababu hawafanya kazi moja kwa moja kwa ajili ya kuuendeleza ufalme wa Mungu. Lakini kazi iliyo duni kupita zote isidharauliwe. Kama inafanyika kwa unyofu wa moyo, inageuka na kuwa mbaraka, nayo inaweza kumwongoza mtu kwenye sehemu za juu za kazi yake hiyo. ----- 6BC 1087. Si kitu kwetu kama tunao mwaka mmoja mbele yetu, au mitano, au kumi, tunapaswa kuwa waaminifu kwa amana yetu leo hii. Yatupasa kufanya kazi za kila siku kwa uaminifu kana kwamba siku hiyo ingekuwa ndiyo siku yetu ya mwisho. ----- RH, Okt. 25, 1881. KUTAFAKARI PAMOJA NA BIDII YA KAZI Agosti 3 Kwa bidii, si walegevu; mkiwa na juhudi katika roho zenu; mkimtumikia Bwana. Warumi 12:11. Kuna wengi waliozama katika shughuli za ulimwengu huu, wala hawampi Bwana kicho ambacho ni cha muhimu kwa maendeleo yao ya kiroho. Wanauchosha kabisa ubongo, mfupa, na musuli, na kujikusanyia mizigo inayowafanya wamsahau Mungu. Nguvu zao za kiroho hazifanyiwi mazoezi kama zinavyofanyiwa nguvu zao za kimwili, na kila siku wako upande wa hasara, wakizidi kuwa maskini zaidi na zaidi katika mali ile ya mbinguni. Lipo kundi jingine la wale ambao wanapata hasara kwa sababu wao ni wavivu, nao hutumia nguvu zao kwa kujifurahisha wenyewe, kwa kuzitumia ndimi zao, na kuiacha misuli yao kupata kutu kwa kutotumika. Wanapoteza nafasi zao nzuri kwa kukaa bila kufanya kazi yo yote, hao hawamtukuzi Mungu.... Kuna kazi fulani ya kufanya kwa kila mmoja wetu katika dunia yetu hii. Bwana anakuja, na kungoja kwetu si kipindi cha kutazamia huku tukiwa tumekaa kivivu, bali ni kipindi cha kukesha kwa kufanya kazi. Hatutakiwi kuutumia muda wetu wote katika kutafakari na maombi, wala hatutakiwi kujilazimisha kufanya kwa haraka na kufanya kazi kana kwamba hilo ndilo lililokuwa limetakiwa kwetu ili kuipata mbingu, huku tukiwa tumeacha kuutumia muda tulio nao kwa kukuza utauwa wetu kila mmoja peke yake. Ni lazima pawepo na mchanganyiko wa kutafakari na bidii ya kazi. Kama Mungu alivyoeleza katika Neno lake, tunapaswa kuwa na "bidii, si walegevu; [tu]kiwa na juhudi katika roho ze[tu]; [tu]kimtumikia Bwana." Shughuli zetu za kidunia zisiizuie kazi ya Bwana. Moyo unahitaji utajiri wa neema yake Bwana, na mwili unataka mazoezi ya viungo ili upate kutekeleza kazi ile ipaswayo kufanywa kwa kuitangaza injili yake Kristo.... Wazazi wangewafundisha watoto wao ya kwamba Bwana anataka wawe watenda kazi wenye bidii, si wavivu katika shamba lake la mizabibu.... Kila mmoja hana budi kufanya sehemu yake katika kazi ile kuu kwa ajili ya wanadamu.... Kwa njia hiyo, taa ya rohoni haitasahauliwa, kama muda utatengwa kwa ajili ya kuomba na kuyachunguza Maandiko. Kazi tuliyogawiwa inaweza kufanywa, na taa ya rohoni kutengenezwa vizuri na kuachwa ikiwa inawaka. ----- Letter 62, 1894. HATARI KUBWA YA "KUTOKUWA NA KAZI YO YOTE YA KUFANYA" Agosti 4 Njia ya mtu mvivu ni kama boma la miiba; Bali mapito yao wenye unyofu hufanyika njia kuu. Mithali 15:19. Bidii ya kazi ni mbaraka kwa vijana. Maisha ya uvivu yanapaswa kuepukwa na kijana kama ufisadi. Haidhuru kazi yake iwe duni jinsi gani, kama ni ya heshima, na kama kazi hizo duni zinafanywa kwa uaminifu, basi, hatapoteza thawabu yake. Bidii ya kazi ni ya muhimu kwa afya njema. Kama mazoea ya kufanya kazi kwa bidii yangesisitizwa, basi, mlango ungefungwa dhidi ya majaribu elfu moja. Wale wanaopoteza siku zao kwa kukaa kivivu, pasipokuwa na lengo lo lote wala kusudi lo lote katika maisha yao, wanasumbuliwa na kuvunjika moyo na kujaribiwa kutafuta furaha katika tamaa mbaya za mwili zilizokatazwa ambazo huudhoofisha mfumo wa mwili na kuzichosha sana nguvu za mwili mara kumi kuliko kazi ile inayochosha mno. Uvivu unaua kuliko kazi ngumu. Wengi hufa kwa sababu hawana uwezo wala mwelekeo wa kujilazimisha kufanya kazi. "Kutokuwa na kazi yo yote ya kufanya" kumeua maelfu yake. Kama vijana wangetunza tabia ya kufanya mema na usafi hasahasa, na kuzitimiza sheria zile alizoziweka Mungu katika maumbile yao, wangeweza kuyahifadhi maisha yao ijapokuwa wanaweza kutakiwa kufanya kazi nzito sana katika kipindi cha maisha yao. Maisha marefu ni urithi unaotokana na jitihada. Baadhi ya wanaume vijana hudhani kwamba kama wangetumia maisha yao bila kufanya kazi yo yote, basi, wangekuwa na furaha nyingi sana. Wanakuza chuki yao dhidi ya kufanya kazi ile inayoleta faida kwao. Wanawaonea wivu wana wa anasa wanaoyatoa maisha yao kwa ajili ya burudani pamoja na shamrashamra.... Kukosa furaha na kuumwa na kichwa ndiyo matokeo ya mawazo kama hayo na tabia kama hiyo. Kutokuwa na kazi yo yote ya kufanya kumewazamisha wanaume vijana wengi katika upotovu. Kazi iliyopangwa vizuri ni ya muhimu kwa mafanikio ya kila kijana. Mungu asingeweza kuwapiga wanaume na wanawake kwa laana kubwa sana kama ile ya kuwaacha waishi maisha ya kutofanya kazi yo yote. Uvivu utaiangamiza roho na mwili. Moyo, tabia ya kimaadili, na nguvu za mwili hudhoofishwa. Akili huathirika, na moyo nao huachwa wazi kukabiliwa na majaribu kama vile barabara ile isiyokuwa na kizuizi cho chote ilivyo, nao huingia katika kila aina ya uovu. Mtu mvivu anamjaribu Shetani ili aje kumjaribu.... Dini itathibitika kwako kuwa ni nanga. Kuzungumza na Mungu kutaipa kila hisia takatifu nguvu yake itakayozifanya kazi za maisha haya kuwa furaha. ----- MS 2, 1871. MBARAKA WA KUFANYA KAZI Agosti 5 Ewe mvivu, mwendee chungu, Zitafakari njia zake ukapate hekima. Mithali 6:6. Mungu aliwaweka wazazi wetu wa kwanza katika Paradiso [Peponi], akawazungushia yote yale yaliyokuwa na manufaa kwao na ya kupendeza. Katika nyumba yao ya Edeni hapakukosekana kitu cho chote ambacho kingeweza kutumika kwa faraja na furaha yao. Naye Adamu akapewa kazi ya kuitunza ile Bustani. Muumbaji alijua ya kwamba Adamu asingeweza kuwa na furaha bila kufanya kazi. Uzuri wa Bustani ile ulimpendeza, lakini huo haukutosha. Ni lazima apate kazi ya kufanya ili kuvizoeza viungo vya ajabu vya mwili wake. Kama furaha ingetokana na kutofanya kazi yo yote, basi, mwanadamu, katika hali yake ya utakatifu usiokuwa na waa lo lote, angeachwa bila kupewa kazi ya kufanya. Lakini yule aliyemuumba akampa kazi yake aliyomchagulia. Ahadi ya utukufu ule wa baadaye, na agizo kwamba mwanadamu sharti afanye kazi kwa jasho lake ili kujipatia chakula chake cha kila siku, vyote viwili vilitoka kwenye kiti kile kile cha enzi.... Mwili usipofanya kazi, damu huzunguka mwilini kwa polepole, na misuli hupungua unene wake na nguvu yake.... Mazoezi ya viungo vya mwili, na kutumia kwa wingi hewa nyingi ya nje pamoja na mwanga wa jua ----- mibaraka ambayo mbingu imewapa wote kwa wingi ----- ingewapa uzima na nguvu wagonjwa wengi waliokonda sana.... Kazi ni mbaraka, sio laana. Kufanya kazi kwa bidii huwazuia wengi, vijana kwa wazee, wasiweze kunaswa na mitego yake yule "ambaye bado anaitafutia mikono mivivu utundu fulani wa kufanya." Hebu na asiwepo mtu ye yote anayeona aibu kufanya kazi, maana kazi ya uaminifu inamfanya mtu kuwa na hadhi yake. Mikono inapojishughulisha katika kufanya kazi za kawaida sana; moyo unaweza kujazwa na mawazo ya hali ya juu na matakatifu. Kusinzia na uvivu huua utauwa, na kumhuzunisha sana Roho Mtakatifu. Dimbwi lenye maji yaliyosimama huchukiza; bali mto safi unaotiririka husambaza afya na furaha juu ya nchi. Hakuna mwanaume au mwanamke ye yote aliyeongoka ambaye anaweza kuwa kitu cho chote isipokuwa mtenda kazi. Kwa hakika iko na daima itakuwako kazi kule mbinguni. Waliokombolewa hawataishi katika hali ya uvivu ya kuota ndoto za mchana. Inasalia raha kwa watu wa Mungu ----- raha watakayoipata kwa kumtumikia Yeye ambaye kwake wanawiwa vyote walivyo navyo na wao wenyewe walivyo. ----- YI, Feb. 27, 1902. JUHUDI INAYOENDELEA KINYUME NA ILE YA KUSHTUKIA TU Agosti 6 Mawazo ya wenye bidii huuelekea utajiri tu; Bali kila mwenye pupa huuelekea uhitaji. Mithali 21:5. Ni vijana wangapi wangeweza kuwa watu wa manufaa na mamlaka ambao wameshindwa kwa sababu mapema katika maisha yao waliambukizwa tabia ya kutoweza kukata shauri ambayo iliwafuata katika maisha yao yote na kuzidhoofisha kabisa juhudi zao zote. Mara kwa mara wanajazwa na juhudi ya ghafula ya kufanya kitu fulani kikubwa, lakini wanaiacha kazi yao hiyo ikiwa imefanywa nusu tu, basi, inakuwa sawa na si kitu. Uvumilivu wa kuendelea kufanya mema ni wa lazima kwa mafanikio yo yote yale.... Kazi inayofanywa kwa kiasi, kwa uvumilivu, na bila kubadilika italeta mafanikio kuliko ile iliyofanywa kwa juhudi ya kushtukia tu.... Kazi iliteuliwa kwa ajili ya mwanadamu na Muumbaji wake. Mungu aliwapa kazi wazazi wetu wa kwanza katika Edeni takatifu. Na tangu Anguko lao, mwanadamu amefanya kazi ngumu kwa jasho lake, akila chakula chake kwa jasho la uso wake. Kila mfupa wa mwili wake, kila mwonekano wa uso wake, kila musuli wa viungo vyake, hushuhudia ukweli kwamba aliumbwa kwa ajili ya kufanya kazi ----- si kwa ajili ya kukaa kivivu. Tabia ya kuwa na bidii ya kazi ingepaswa kujengwa wakati wa ujana.... Kufanya kazi za maisha kwa uaminifu, haidhuru uwe na cheo gani, huhitaji ukuzaji wa talanta zote na uwezo wote aliokupa Mungu kwa kutumia busara. Jihadhari sikuzote usiwe na haraka, hata usiweze kuzalisha cho chote kinachoistahili juhudi yako hiyo. Juhudi hizo ambazo hazina matunda yo yote mara nyingi husababishwa na kushindwa kuifanya kazi hiyo kwa wakati wake unaofaa. Cho chote kile kinachoachwa kufanywa kwa wakati ule kinapotakiwa kufanywa, kama ni katika mambo ya kilimwengu au ya kidini, kwa shida mno kinaweza kufanyika vizuri. Wengi wanaonekana kufanya kazi kwa bidii kila saa ya siku hiyo, lakini matokeo ya kazi zao hayalingani na juhudi zao.... Jihadhari usipoteze wakati wako kwa mambo madogo sana, na kisha kushindwa kufanya mambo yako ambayo ni ya maana sana.... Kuling'ang'ania kusudi lako bila kugeuka ni muhimu ili kufikia mwisho wake. Mtu mmoja mashuhuri aliulizwa zamani kwa jinsi gani aliweza kufanya biashara kubwa sana kama ile. Jibu lake lilikuwa hivi, "Nafanya jambo moja kwa wakati mmoja."... Yesu alikuwa mtenda kazi mwenye bidii, na wale wanaofuata kielelezo chake watakuwa na uzoefu wa kujikana nafsi, kufanya kazi kwa bidii, na kujitolea mhanga. ----- Letter 3, 1877. MUNGU ANAHUSIKA NA KILA TENDO LA BIASHARA Agosti 7 Mizani ya hadaa ni chukizo kwa BWANA; Bali vipimo vilivyo sawasawa humpendeza. Mithali 11:1. Mizani ya hadaa ni ishara ya biashara ya dhuluma, yaani, kila chombo kinachotumika ili kuficha uchoyo na dhuluma chini ya mwonekano wa haki na usawa. Mungu hatayakubali matendo kama hayo hata kwa kiwango kidogo mno. Anaichukia kila njia iliyopotoka. anachukia sana kujipenda nafsi kote pamoja na uchoyo. Kutendeana bila huruma hataweza kukuvumilia, bali atalipiza kisasi. Mungu anaweza kuwapa utajiri wale wanaofanya kazi ambao mali yao wanaipata kwa uaminifu. Lakini laana yake inakaa juu ya vyote vilivyopatikana kwa matendo yenye uchoyo ndani yake. Mmoja anapoendekeza uchoyo wake au kudanganya katika biashara yake, anaonyesha kwamba hamwogopi Bwana wala kulicha jina lake. Wale wanaohusiana na Mungu hawataepuka dhuluma yote tu, bali watadhihirisha rehema na fadhili zake kwa wote watakaoshughulika nao. Bwana hatakubali kumpendelea mtu ye yote; lakini hataiunga mkono njia ya wale wasioweka tofauti yo yote katika kuwafanyia wema wale walio maskini, wajane, na yatima. ----- 3BC 1158, 1159. Imani yako ya dini inapasa ikuinue wewe juu ya kila hila mbaya. Bidii ya kazi, uaminifu, msimamo thabiti upande wa haki, na kumtegemea Mungu vitakuhakikishia ushindi. Nenda polepole, kwa unyofu, kwa kufuata kabisa kanuni za Biblia, vinginevyo, acha kufanya biashara yako. Hakuna mapatano yo yote yanayofanywa, hakuna deni lo lote linalolipwa, ambalo Mungu hahusiki nalo. Yeye ni mwenye hekima yote, mlinzi wa haki wa milele. Huwezi kumwacha Mungu nje ya jambo lo lote linalohusu haki za watu wake. Mkono wa Mungu umenyoshwa kama ngao juu ya viumbe vyake vyote. Hakuna mtu ye yote anayeweza kuzijeruhi haki zako bila kuupiga mkono ule; huwezi kuzijeruhi haki za mtu ye yote bila kuupiga ule. Mkono ule unashika upanga wa haki. Jihadhari unavyowatendea watu.... Kama nuru yako inawaka katika maisha yako ya biashara, ikionyesha wazi nguvu ya utauwa wako kwa matendo, basi, ina thamani kubwa sana kwa wote unaokutana nao kuliko mahubiri au imani za kidini (Creeds). Ulimwengu utakutazama kwa makini sana na kukukosoa kwa ukali na kukujua, wakati wewe u katikati ya shughuli zako za kidunia. Lile unalosema kanisani halina hata nusu ya matokeo kama yale unayofanya katika biashara yako ya kila siku. ----- Letter 5, 1879. KUZA TABIA YA UAMINIFU Agosti 8 Msimlipe mtu ovu kwa ovu. Angalieni yaliyo mema machoni pa watu wote. Warumi 12:17. Dini ya Kristo inawaagiza watu kuzitumia kanuni safi za ile kweli katika maisha yao ya kila siku, katika kununua na kuuza kwao, katika kila tendo lao la biashara zote, kuwa na hisia halisi ya wajibu wao wa kidini kama ule wanaokuwa nao wanapotoa dua zao kwa Mungu. Unapaswa kuwa ni mfano wako katika kuudhihirishia ulimwengu kwamba kweli ya Mungu inamtakasa yule anayeipokea na kuzaa [ndani yake] bidii ya kazi, hali ya kubana matumizi, na uvumilivu, na wakati uo huo ikikomesha kabisa uchoyo, kurubuni watu, na kila aina ya udanganyifu.... Hakuna kitu cho chote kilicho cha thamani sana kwa mwanaume kijana ambaye ndiyo tu anaanza maisha yake kama ile sifa ya kuwa na msimamo usiopindika. ----- Letter 5, 1879. Kila tendo la biashara linatakiwa liwe la namna ile inayoweza kuungwa mkono na Mbingu, vinginevyo, litakuwa ni harufu mbaya ya mvuto wake Shetani iletayo mauti. Kila tendo linapaswa kuiwakilisha ile sayansi ya kanuni zile za Mbinguni. ----- MS 113, 1903. Ukweli na kusema kweli bila kuficha ungehifadhiwa na wale wote wanaojidai kuwa wafuasi wake Kristo. Mungu na haki yake yangekuwa ndiyo maneno yetu makuu. Tenda kwa uaminifu na kwa haki katika ulimwengu mwovu wa sasa. Wengine watakuwa waaminifu wanapoona ya kwamba uaminifu hautahatarisha biashara zao za kidunia; lakini wote wanaotenda kwa kufuata kanuni hiyo [ya kutozihatarisha biashara zao] majina yao yatafutwa kutoka katika kitabu kile cha uzima. Uaminifu kamili hauna budi kukuzwa. Tunaweza kupita katika ulimwengu huu mara moja tu; hatuwezi kurudi kusahihisha makosa yo yote tuliyofanya; kwa hiyo, kila hatua tunayochukua ingekuwa kwa kicho kwa Mungu wetu na kwa kuifikiria kwa makini. Uaminifu na ujanja haviwezi kupatana; ama ujanja utadhibitiwa, na kuiachia kweli na uaminifu kushika hatamu zake za uongozi, ama ujanja utazishika hatamu hizo, na uaminifu utakoma kuongoza. Vyote viwili haviwezi kufanya kazi pamoja, haviwezi kupatana kamwe. Mungu atakapozikusanya johari zake, wale walio wa kweli, wasioficha kitu, waaminifu, watakuwa ndio wateule wake, yaani, hazina zake. Malaika wanawaandalia taji watu kama hao, na nuru kutoka kwenye kile kiti cha enzi cha Mungu itaakisi kwa utukufu wake kutoka kwenye taji hizo za kifalme zilizojaa vito vyenye nyota. ----- 6BC 1081. WAKUU MACHONI PAKE MUNGU Agosti 9 Aliye mwaminifu katika lililo dogo sana, huwa mwaminifu katika lililo kubwa pia; na aliye dhalimu katika lililo dogo, huwa dhalimu katika lililo kubwa pia. Luka 16:10. Maisha hayajajengwa juu ya mambo makuu peke yake; ni mambo yale yaliyo madogo yaletayo jumla ya furaha au taabu katika maisha yetu. Ni mambo madogo katika maisha yanayoidhihirisha tabia halisi ya mtu. Laiti kama vijana wote na wale wenye umri mkubwa wangeweza kuona kama mimi nilivyokwisha kuona katika kioo cha maisha ya watu kilicholetwa mbele yangu, ndipo wangeziangalia kwa uzito zaidi hata kazi zile za maisha zinazoonekana kuwa ndogo. Kila kosa, yaani, kila upotofu, haidhuru lifikiriwe kuwa halina maana yo yote, linaacha kovu katika maisha haya na doa katika kumbukumbu zile zilizoko mbinguni. Maisha yamejaa kazi ambazo hazipendezi, lakini kazi hizo zote zisizopendeza zitafanywa ziweze kupendeza kwa kuzifanya kwa moyo mchangamfu kwa sababu ni sawa kufanya hivyo. Kuzipenda kazi zile ambazo mtu fulani anapaswa kuzifanya, na kujitahidi kuzifanya kwa moyo, kutazifanya zipendeze kazi zile zisizopendeza kabisa. ---- - Letter 41a, 1874. Wako wengi wanaodharau matukio madogo madogo ya maisha, yaani, matendo madogo yanayopaswa kufanywa siku kwa siku; lakini hayo yasikadiriwe kuwa ni madogo, kwa maana kila tendo ama linaleta baraka ama linaleta madhara kwa mtu fulani. Kila tendo husimulia kisa chake lenyewe, huchukua historia yake lenyewe kwenda kwenye kiti cha enzi cha Mungu. Hujulikana iwapo liko upande wa wema au upande wa uovu. Ni kwa kutenda kulingana na kanuni za Neno la Mungu katika mambo madogo ya maisha haya, sisi tunajiweka upande wa haki. Tunajaribiwa na kupimwa kwa matukio hayo madogo madogo, na tabia yetu itatathminiwa kulingana na kazi yetu itakavyokuwa. ----- RH, Okt. 15, 1895. Ni kwa kuzingatia kwa makini kile ambacho ulimwengu huu unakiita mambo madogo kunakoleta uzuri mwingi na ufanisi katika maisha yetu. Matendo madogo ya upendo, Maneno madogo ya upole, Matendo madogo ya kujikana nafsi, Kuzitumia vizuri sana kwa busara nafasi zinazojitokeza, Kuziendeleza kwa bidii talanta zile zilizo ndogo, Huwafanya watu wawe wakuu machoni pake Mungu. ----- MS 59, 1897. MANUFAA YA KUFUATA UTARATIBU NA MPANGILIO Agosti 10 Namshukuru Mungu sikuzote kwa ajili yenu, kwa sababu ya neema ya Mungu mliyopewa katika Kristo Yesu; kwa kuwa katika kila jambo mlitajirika katika yeye, katika maneno yote, na maarifa yote. 1 Wakorintho 1:4,5. Ipo haja ya kukuza kila neema ambayo Yesu... ameileta karibu nasi; maana ni neema peke yake iwezayo kuuponya upungufu wetu; ni Kristo peke yake awezaye kuzibadilisha tabia zetu. Na Mungu angependa sisi tupate kuidhihirisha neema hiyo, ambayo imetolewa kwa wingi sana, katika mambo madogo na makubwa ya maisha yetu.... Mungu wetu ni Mungu wa utaratibu, naye anataka kwamba watoto wake waNIE kujiweka wenyewe kuwa watu wanaofuata utaratibu, wakiwa chini ya uongozi wake.... Iwapo vijana wangejenga tabia ya kufuata utaratibu na mpangilio, basi, wangekua kiafya, kiroho, katika uwezo wao wa kukumbuka mambo, na katika mwelekeo mzuri wa tabia zao. Ni wajibu wa watu wote kuzizingatia kanuni hizi kwa ukali katika mazoea yao ya maisha. Hiyo ni kwa faida yenu, wapendwa vijana, kimwili na kimaadili. Unapoamka asubuhi, kwa kadiri iwezekanavyo fikiria kazi ile unayotaka kuikamilisha kwa siku hiyo. Kama ni lazima, uwe na kitabu kidogo ambamo utaandika mambo yanayohitajika kufanywa, kisha tenga muda wako fulani wa kuifanya kazi hiyo.... Tabia ya kufanya kazi polepole, yaani, kwa ugoigoi, huifanya kazi ionekane kuwa ni nyingi wakati ambapo ni ndogo sana. Lakini, kama unataka, unaweza kuishinda tabia hiyo ya kufanya kazi kwa madoido mengi mno na kukawia-kawia. Kutumia utashi wako kutaifanya mikono yako iende kwa ustadi.... Mambo hayo yameangaliwa kama ni mambo madogo, na karibu yasiyostahili kuangaliwa. Lakini wengi wamedanganyika kuhusu umuhimu wa mambo hayo madogo. Yana uzito mkubwa sana juu ya mambo yote. Mungu haliangalii jambo lo lote lihusulo usitawi wa familia hii ya kibinadamu kuwa halina maana. Alimtoa Mwanawe pekee kwa manufaa ya mwili wetu pamoja na roho zetu, na hivyo vyote vinatakiwa kutolewa wakf kwake..... Kweli zile kuu zinaweza kuletwa katika mambo hayo madogo; dini ya matendo inapaswa kuingizwa hata katika kazi duni za maisha yetu ya kila siku. Na katika utendaji wa kazi hizo, mnajenga tabia zile zitakazoshinda katika kipimo kile cha Hukumu. Basi, haidhuru ziwe kazi gani unazofanya, zifanye vizuri na kwa uaminifu, ukitambua ya kwamba Mbingu yote inaiangalia kazi yako. ----- YI, Jan. 28, 1897. MAMBO MADOGO YALIYO MAKUBWA Agosti 11 Tukamatie mbweha, Wale mbweha wadogo, Waiharibuo mizabibu, Maana mizabibu yetu yachanua. Wimbo Ulio Bora 2:15. Mungu anatutaka sisi kufanya haki katika mambo ya maana, na wakati uo huo anatuambia kwamba kuwa waaminifu katika mambo madogo hututayarisha tuweze kufaa kwa nafasi za juu zaidi za madaraka.... Tabia nzuri walizo nazo wengi hufichwa, badala ya kuwavuta watu kwa Kristo wanawafukuza. Kama watu hao wangeweza kuona mvuto wa njia zao hizo zilizo na utovu wa adabu pamoja na maneno yao makali dhidi ya wale wasioamini, na jinsi ilivyo ya kuchukiza tabia kama hiyo machoni pake Mungu, basi, wangeweza kuzirekebisha tabia zao, kwa maana utovu wa adabu ni mojawapo ya vikwazo vikuu sana kwa wenye dhambi. Wakristo wachoyo [wajipendao wenyewe], walalamikaji, waliojaa uchungu, wanazuia njia, kiasi kwamba wenye dhambi hawajali kuja kwake Kristo. Kama tungeweza kuona chini ya mambo yanayoonekana juu, tungegundua kwamba nusu ya taabu za maisha haya husababishwa na maneno yanayosemwa kwa ukali na kukunja nyuso, ambayo yangeweza kuzuiwa ama kutozuiwa. Wengi wanajifanyia jehanum yao wenyewe hapa duniani na pia kwa wale ambao wangeweza kuwafariji na kuwaletea mibaraka. Hao hawastahili kuitwa Wakristo.... Watu wengine husema kwa ukali, bila heshima, kiasi cha kuiumiza mioyo ya wengine, kisha wanajihesabia haki wenyewe wakisema, "Hiyo ndiyo njia yangu, Siku zote nasema kile ninachofikiri"; nao huitukuza tabia hiyo mbaya kuwa huo ndio wema hasa. Tabia yao hiyo yenye utovu wa adabu ingepaswa kukemewa kwa nguvu. ----- RH, Sept. 1, 1885. Neno lile kali lingeachwa bila kulisema, kule kutojali furaha ya wengine kungeondolewa ili ipatikane nafasi ya moyo ule wa huruma na wa kuwafikiria wengine. Heshima ya kweli, ikichanganyika na kweli na haki, itayafanya maisha sio tu kuwa ya manufaa, bali kuwa na harufu nzuri.... Uadilifu, haki, na upole wa Kikristo, vikichanganywa pamoja, hufanya mchanganyiko mzuri. Heshima [adabu/uungwana] ni mojawapo ya matunda ya Roho. Hiyo ndiyo tabia ya mbinguni. Kamwe malaika hawakasiriki ghafula, kamwe hawana wivu, wala uchoyo, wala kijicho. Hakuna maneno machungu huko, wala maneno makali yanayotoka katika vinywa vyao. Kama sisi tunataka kuwa wenzi wa malaika hao, basi, yatupasa kuwa waungwana na wenye adabu pia. ----- RH, Sept. 1, 1885. MPANGILIO NA USAFI Agosti 12 Basi, wapenzi wangu, kwa kuwa tuna ahadi hizo, na tujitakase nafsi zetu na uchafu wote wa mwili na roho, huku tukitimiza utakatifu katika kumcha Mungu. 2 Wakorintho 7:1. Ni jambo la maana sana kwamba Wasabato wanapaswa kuishi kulingana na imani yao kwa kila hali. Yawapasa kuwa wepesi kutenda kazi zao na kuwa nadhifu, tena kuyanyosha mambo yao yote ya biashara.... Hakuna wanaopaswa kuogopa sana kufanana na ulimwengu huu, kiasi cha kuwafanya wasiwe waangalifu katika utunzaji wa nyumba zao, wakiwa wanaviacha vitu vyao vimezagaa ovyo ovyo na katika hali ya uchafu. Si kiburi kuwa nadhifu katika mavazi, kuwa safi kimwili, kuwa na utaratibu na mpangilio mzuri katika kuvipanga vitu vya nyumbani mwao.... Mwonekano huo wa nje huonyesha tabia ya shughuli zao hao wanaoishi ndani ya nyumba hiyo, tena, si hivyo tu, bali huonyesha na tabia ya kidini ya wakazi wa nyumba hiyo. Haiwezekani kwa mtu aliye mzembe, yaani, yule asiyekuwa na utaratibu wo wote, kuwa Mkristo mwema. Maisha yao, katika mambo ya kidunia na ya kidini, ni ya ovyo kama vile yalivyo na mavazi yao, nyumba zao, utu wao, na mazingira yao. Kuna utaratibu kule mbinguni. Kuna sheria na taratibu zinazoliongoza jeshi lote la mbinguni. Wote huenda kwa utaratibu. Vyote vilivyoko kule ni safi, vyote vinaishi kwa amani. Na kila mmoja atakayehesabiwa kuwa anastahili kuingia mbinguni atakuwa mwungwana kabisa, tena atakuwa bila waa, wala kunyanzi, wala kitu cho chote kama hicho. Wale wasiokuwa na malezi mazuri wana mawaa na makunyanzi juu yao hivi sasa. Heri wasingepoteza wakati wo wote na kuanza kazi ya kujitakasa wenyewe kutokana na uchafu wote wa mwili na roho, huku wakitimiza utakatifu katika kumcha Mungu. Mungu anataka usafi, unadhifu, mpangilio mzuri, na utakatifu. Mungu anawataka watu wake wote wanaopungukiwa na sifa hizo kuzitafuta na kutotulia kamwe mpaka wazipate. Yawapasa kuanza kazi ya matengenezo na kuyainua juu maisha yao, ili kwamba kwa njia ya mwenendo wao na mavazi yao, sifa za kudumu za imani yao zipate kuonekana katika matendo yao na maisha yao, hapo ndipo watakuwa na uwezo ule unaoongoa na kuwavutia sana wale wasioamini ili walazimike kukiri ya kwamba nao ni watoto wa Mungu. ----- MS 3, 1861. Kweli kama ilivyo ndani ya Yesu haitamdhalilisha bali itamwinua juu yule anayeipokea, yaani, itayatakasa maisha yake, itayarekebisha mapenzi yake, na kuutakasa uamuzi wake. ----- Letter 2, 1861. HARUFU NZURI YA UPENDO HUENEA MBALI Agosti 13 Bwana na awaongeze na kuwazidisha katika upendo, ninyi kwa ninyi, na kwa watu wote, kama vile sisi nasi tulivyo kwenu. l Wathesalonike 3:12. Mungu angependa watoto wake watambue kwamba ili kumtukuza yeye, upendo wao hauna budi kutolewa kwa wale wanaouhitaji sana.... Hakuna kujipenda nafsi ko kote kama ni kwa njia ya mtazamo wa macho, kwa neno, au kwa tendo, kunakotakiwa kuonekana tunaposhughulika na wale wenye imani ya thamani kama yetu,... wawe na vyeo au wawe wanyonge, wawe matajiri au wawe maskini. Upendo ule unaotoa maneno ya upole kwa wachache tu, wakati wengine wanatendewa kwa ubaridi na pasipo kuwajali, sio upendo, bali ni kujipenda nafsi. Kwa vyo vyote vile hautaleta manufaa yo yote kwa watu, wala utukufu kwa Mungu. Upendo wetu... usitiwe muhuri na kuwekwa kwa ajili ya watu maalum tu, na kuwaacha wengine. Ivunje chupa yako [ya upendo], kisha harufu nzuri itaijaza nyumba yote. Wale wanaokusanya mwanga wa jua la haki yake Kristo, wala hawauruhusu kuangaza katika maisha ya wengine, punde watapoteza mionzi mizuri inayong'aa ya neema ile ya mbinguni, waliyoiweka akiba kwa uchoyo ili ipate kuwaangazia wachache tu. Wale walio na upendo mwingi wanawajibika kwa Mungu kuugawa upendo huo... kwa wote wanaohitaji msaada wao.... Kupenda kama vile Kristo alivyopenda humaanisha kuonyesha roho ile isiyokuwa na uchoyo wakati wote na mahali pote, kwa maneno ya upole na mtazamo wa macho unaopendeza. Mambo hayo hayawagharimu cho chote wale wanaoyatoa, lakini yanaacha nyuma yake harufu nzuri inayoizunguka roho ya mtu. Matokeo yake kamwe hayawezi kukisiwa. Sio tu yanakuwa mbaraka kwa mpokeaji, bali kwa mtoaji pia; maana yanamrudia mwenyewe. Upendo wa kweli ni tabia ya thamani itokayo mbinguni, ambao huo unaongezeka utamu wa harufu yake kulingana na jinsi unavyogawiwa kwa wengine.... Mioyo ya wale wanaompenda Yesu itazungukwa na hali ya hewa iliyo safi, yenye harufu nzuri. Kuna wale wanaoificha njaa yao ya rohoni. Hao watasaidiwa sana kwa njia ya neno la upole au kwa wema wa kuwakumbuka. Vipawa hivyo vya mbinguni, vimetolewa bure na kwa wingi na Mungu, vinatakiwa vitolewe nasi bure kwa wale wote wanaokuja katika eneo la mvuto wetu. Hivyo ndivyo tunavyoufunua upendo ule uliotoka mbinguni, ambao utazidi kuongezeka kadiri unavyotolewa bure na kutumika kwa ajili ya kuwaletea mibaraka wengine. Kwa njia hiyo tunamtukuza Mungu. ----- MS 17, 1899. MBONA UNAZITAFUTA KASORO ZA MWENZIO? Agosti 14 Msitende neno lo lote kwa kushindana wala kwa majivuno; bali kwa unyenyekevu, kila mtu na amhesabu mwenziwe kuwa bora kuliko nafsi yake. Wafilipi 2:3. Lo! ni magumu jinsi gani wengi huyafanya maisha ya Kikristo! Wanapanda miinuko mikali, wanapita katika njia zenye miiba, wakipepesuka chini ya mizigo mizito waliyojitwika wenyewe, kana kwamba wanapaswa kuzipiga tabia za wengine kama bati.... Hawapati uzoefu wa amani tamu ya Kristo. Hawaushiki msaada ule anaowapa Yesu, lakini wanasononeka daima kwa mabaya ya wengine wanayoyadhania tu, na kutotilia maanani dalili za kuchangamsha na baraka ya mema katika njia yao yote. Mara tu mmoja anapotambua kwa dhahiri na kwa kina sana uwajibikaji wake alio nao kwa Mungu na jukumu lake kwa wanadamu wenzake, na kuhisi kwamba mvuto wake unafika mbali sana, ukifika hadi umilele, hataridhika kufikia kiwango cha chini, hatatafuta makosa na kuwakosoa wengine. Atayafanya maisha yake mwenyewe kuwa kama vile anavyotaka maisha ya wengine kuwa. Ataishi tu ndani ya Kristo, akimtegemea kabisa na kwa ukamilifu kwa kila urembo na uzuri wa tabia yake. ----- Letter 42a, 1878. Tungekuwa tunayang'oa magugu yote ya kulalamika na kutafuta makosa kwa wengine kutoka katika mawazo yetu. Hebu na tusiendelee kuziangalia kasoro zo zote tunazoweza kuziona.... Kama tungeweza kumshika Mungu vizuri, basi, tungepaswa kuendelea kuyatazama mambo yale makuu ya thamani ----- utakatifu, utukufu, uwezo, upole, mapenzi, upendo, ambayo Mungu anatugawia. Na kwa kutazama hivyo, mawazo yetu yatakazwa sana juu ya mambo hayo yenye manufaa ya milele kwetu hata hatutakuwa na hamu yo yote ya kuzitafuta kasoro za wengine. ----- MS 153, 1907. Mtafakarini Bwana Yesu, pamoja na wema na upendo wake, ila msizitafute kasoro na kuzungumza sana juu ya makosa ambayo wengine wamefanya. Myakumbuke mambo yale yanayofaa kwenu ili mpate kuyatambua nayo yawapatie sifa yenu; na kama ninyi mna akili kali ya kutambua makosa ndani ya wengine, basi, iweni na akili kali zaidi kutambua yale yaliyo mema na kuyasifu yale yaliyo mazuri. Ninyi, kama mkijikosoa wenyewe, mnaweza kuona mambo fulani ndani yenu ambayo hayapendezi ambayo ni sawa na yale mnayoyaona ndani ya wengine. Basi, tufanye kazi daima kwa kutiana nguvu katika imani yetu iliyo takatifu sana. ----- MS 151, 1898. KUKOSOA SIO KAZI YETU Agosti 15 Msihukumu, msije mkahukumiwa ninyi. Kwa kuwa hukumu ile mhukumuyo, ndiyo mtakayohukumiwa; na kipimo kile mpimacho, ndicho mtakachopimiwa. Mathayo 7:1,2. Miili yetu inajengwa kutokana na kile tunachokula na kunywa; na tabia ya uzoefu wetu wa kiroho hutegemea juu ya kile akili zetu zinacholishwa na kukifanya kiwe sehemu yake. Kwa kuongea daima juu ya makosa na kasoro za wengine, wengi wanageuka na kuwa wagonjwa wa kiroho, nao wanashindwa kukiyeyusha chakula kile wanachokula.... Wale ambao wanajishughulisha sana kukata-kata maneno na matendo ya wengine, yaani, kugundua kile kisichopendeza, wanashindwa kutambua mambo yale yaliyo mema na mazuri. Hawali chakula kinachofaa kukuza nguvu yao ya kiroho na kukua kiafya. ----- MS 4a, 1893. Mungu hapendezwi na watu wake wanapoacha kujikosoa nafsi zao wenyewe, na badala yake huwakosoa wengine. Hii ni kazi ya Shetani. Unapoifanya kazi hiyo, kumbuka kwamba adui anakutumia kama njia ya kuwajaribu wengine, ili wale ambao wangeungana pamoja katika umoja na furaha, wakiwa wanajengana wao kwa wao katika imani ile takatifu sana, wawe wanapigana na kunung'unikiana kwa sababu mtu fulani mwingine anatenda dhambi. Kristo hajakuweka wewe kuwa mchukuzi wa dhambi za watu. Huwezi kuzichukua hata dhambi zako mwenyewe. Kwa hiyo uwe mwangalifu sana usitoe lawama yo yote dhidi ya jirani yako. Mungu anataka watu wake wawe huru.... Je, hatuwezi kukumbuka ya kwamba kwa maneno yetu tunayosema ama tunaweza kuwajeruhi watu ama kuwaponya? Je, hatuwezi kukumbuka ya kwamba kwa kadiri tunavyowahukumu wengine, ndivyo tutakavyohukumiwa, sisi ambao huenda tumepewa nafasi nyingi nzuri sana kuliko wale tunaowahukumu? Mioyo yetu haina budi kuyeyuka na kuwa myororo na kuwa na upendo kwa kila mmoja. Tunaweza kujikosoa wenyewe kwa ukali ule ule kama tupendavyo. Mmoja anayemkosoa mwingine anatoa ushahidi kwamba yeye ndiye hasa anayehitaji kujikosoa mwenyewe. Mwombeni Mungu awaonyeshe mnachopaswa kukiondoa ndani yenu wenyewe ili mpate kuuona ufalme wa Mungu.... Kuna taji kwa kila mshindi. Je, unaitaka? Je, unataka kupiga mbio kwa saburi? Basi usitafute kupata kitu fulani cha kushutumu ndani ya jirani yako bali mtazame Yesu Kristo moja kwa moja. Tazama utakatifu wake, nawe utapendezwa sana na utaweza kuiakisi sura yake. ----- GCB, Aprili 23, 1901. KUSHINDA WIVU NA KIJICHO Agosti 16 Tusijisifu bure, tukichokozana na kuhusudiana. Wagalatia 5:26. Wivu na kijicho ni magonjwa yanayouathiri uwezo wa mwili wa kufanya tendo lo lote. Vilianzishwa na Shetani kule Paradiso.... Wale wanaoisikiliza sauti yake [Shetani] watawatoa dosari wengine, na kusema vibaya na kuwasemea uongo ili wapate kujijenga wenyewe. Lakini hakuna cho chote kilicho kinyonge kitakachoingia mbinguni, na wale wanaoitunza roho hiyo wasipobadilika, hawawezi kamwe kuingia kule, maana wangeendelea kuwakosoa malaika. Wangeona wivu kwa taji ya kila mmoja. Wasingejua waongee juu ya mambo gani zaidi ya kutaja mapungufu na makosa ya wengine. Laiti kama hao wangebadilika kwa kumtazama Kristo! Laiti kama wangekuwa wapole na wanyenyekevu wa moyo kwa kujifunza kwake! Hapo ndipo wangesonga mbele, sio kama wamishonari wa Shetani, waletao mtengano na faraka, wanaoichubua na kuiharibu tabia, bali kama wamishonari wa Kristo, ambao ni wapatanishi na waponyaji. Umruhusu Roho Mtakatifu kuingia ndani yako na kuifukuzilia mbali tamaa hiyo chafu, ambayo haiwezi kuishi mbinguni. Iache ife; iache isulibiwe. Fungua moyo wako kupokea tabia ya Kristo, aliyekuwa mtakatifu, mpole na safi.... Neno la Mungu linatusihi, likisema, "Wenye kupendana [Pendaneni] kama ndugu, [iweni] wasikitivu, [iweni] wanyenyekevu," 1 Petro 3:8 [KJV]. Thamani ya kweli ya maadili haitafuti nafasi yake yenyewe kwa kufikiri na kusema maovu, kwa kuwadhalilisha wengine. Wivu wote, kijicho chote, masengenyo yote, mashaka yote, ni lazima viondolewe mbali na watoto wa Mungu. ----- RH, Sept. l4, 1897. Biblia imejaa mafundisho yanayotuagiza kuonyesha upendo, uvumilivu, na heshima katika usemi wetu na kutendeana sisi kwa sisi. Upendo wa Yesu moyoni haumwongozi mtu kuwa na kijicho wala wivu. Mmea mwororo wa upendo wa Kikristo unatakiwa kutunzwa kwa uangalifu sana. Hautakua usipopaliliwa. Mbingu humwangalia yule anayezungukwa na hali ya amani na upendo kila aendako. Mtu kama huyo atapokea thawabu yake. Atasimama katika siku ile kuu ya Bwana. ----- MS 26, 1886. NAMNA YA KUISHUGHULIKIA HASIRA Agosti 17 Asiye mwepesi wa hasira ni mwema kuliko shujaa; Na mtu aitawalaye roho yake kuliko mtu atekaye mji. Mithali 16:32. Shetani anashangilia jinsi gani anapowezeshwa kumfanya mtu awake moto kwa hasira! Mtazamo wake wa macho, ishara zake za mikono, na sauti yake inavyosikika, huweza kunaswa na kutumiwa kama mshale wa Shetani ili kuujeruhi na kuusumisha moyo uliofunguka kuupokea [mshale huo]. ----- 2BC 1020. Mmoja anapoachia tu nafasi na kuwa na roho iliyojaa hasira anakuwa amelewa sawasawa tu na mtu aliyekunywa gilasi moja ya kileo. ----- MS 6, 1893. Kristo anaihesabu hasira kuwa ni sawa na kuua.... Maneno ya harara ni harufu ya mauti iletayo mauti. Yule anayeyatamka hashirikiani na Mungu kumwokoa mwanadamu mwenzake. Kule mbinguni ukosoaji huo mbaya unawekwa katika orodha ile ile kama kuapa kule kwa kawaida. Chuki inapotunzwa moyoni hakuna hata chembe ya upendo wa Mungu mle. ----- Letter 102, 1901. Unaposikia roho ya hasira inainuka ndani yako, mshike sana Yesu Kristo kwa imani. Usiseme neno lo lote. Hatari iko katika kunena neno moja unapokuwa umekasirika, kwa maana mfululizo wa maneno ya harara utafuatia.... Mtu yule anayejiachilia na kuwa mpumbavu kwa kusema maneno ya harara, anatoa ushuhuda wa uongo; maana hana haki kamwe. Anatia chumvi kila dosari anayodhani anaiona; anakuwa kipofu mno na kuzidi hata asiweze kushawishika juu ya wazimu wake. Anazivunja amri za Mungu, na mawazo yake yanapotolewa kwa uvuvio wa Shetani. Hajui alitendalo. Ni kipofu na kiziwi, anamruhusu Shetani kushika hatamu na kumwongoza ko kote apendako [Shetani]. Mlango unafunguliwa wazi kwa kijicho, kwa wivu, na kwa kuwafikiria wengine vibaya, na maskini huyo mhanga anasombwa [na Shetani] akiwa hana uwezo wo wote.... Lakini tumaini lipo kwa kadiri saa za muda ule wa majaribio zinavyozidi kukawia, kwa njia ya neema yake Bwana wetu Yesu Kristo.... "Fanyeni bidii ili mwonekane katika amani kuwa hamna mawaa wala aibu mbele yake." 2 Petro 3:14. Hicho ndicho kipimo ambacho kila Mkristo anapaswa kujitahidi kukifikia, sio kwa uwezo wake wa kuzaliwa nao, bali kwa njia ya neema ile anayopewa na Yesu Kristo. Hebu na tupigane mieleka ili kupata ushindi juu ya kila dhambi, na kuweza kulizuia kila neno linaloamsha harara, yaani, linaloleta kiherehere. ----- Letter 38, 1893. MGUSO WENYE HARUFU NZURI WA UNYENYEKEVU Agosti 18 Neno la mwisho ni hili; mwe na nia moja, wenye kuhurumiana, wenye kupendana kama ndugu, wasikitikivu, wanyenyekevu. 1 Petro 3:8. Katika kushughulika na wanadamu wenzetu sisi sote tunapaswa kuwafikiria kuwa nao wana asili moja na sisi, hujisikia udhaifu ule ule tulio nao sisi na kusumbuliwa na majaribu yale yale. Wao, pamoja na sisi, wanalo pambano maishani mwao wanapotaka kuudumisha uaminifu wao.... Unyenyekevu wa kweli wa Kikristo unaunganisha na kukamilisha haki na upole, na rehema na upendo hujazia nafasi iliyobaki, vyote hivyo hukamilisha kabisa na kuongeza mvuto mzuri kabisa katika sifa za kitabia.... Ibrahimu alikuwa mwungwana kweli. Katika maisha yake tunacho kielelezo kizuri sana cha uwezo wa unyenyekevu wa kweli. Angalia mwenendo wake na Lutu.... Kwa heshima ilioje anawakaribisha wale wageni, yaani, wajumbe wale wa Mungu, katika hema yake, na kuwakirimu! Aliinama mbele ya wana wa Hethi aliponunua kutoka kwao pango alimomzika mpenzi wake Sara.... Ibrahimu alijua vizuri deni alilowiwa mwanadamu kwa mwanadamu mwenzake. Paulo, ingawa alikuwa imara kama mwamba juu ya kanuni, lakini daima alitunza heshima yake. Alikuwa na bidii katika mambo yale makuu, wala hakupuuzia matendo mema na upole katika maisha yake ya kijamii. Mtu huyo wa Mungu hakummeza mtu yule wa kibinadamu [yaani, uungu wa Paulo haukuumeza ubinadamu wa Paulo]. Walakini, tunamleta kwenu yule aliye Mkuu kuliko Ibrahimu na Paulo ----- yaani, yule Mwokozi wa ulimwengu. Maisha yake yalikuwa kielelezo cha ajabu cha uungwana halisi. Haiwezekani kuorodhesha mifano yote ya upole wake, uungwana wake, na huruma yake ya kuwasikitikia wengine pamoja na upendo wake. Ni mionzi iliyofifia na mizuri ilioje iliyoangaza katika maisha yake yote kwa kujishusha hadhi yake kwa namna ya kushangaza! Aliwaangalia watu kwa upole na kuwa na neno la kutia moyo kwa wote waliokuwa wamechoka na kudhoofika kwa kazi. Alikuwa tayari kuwasaidia wale waliokuwa hawajiwezi kabisa. ----- Letter 25, 1870. Upendo, heshima, urafiki ----- mambo hayo hayapotei kamwe. Wanadamu watakapobadilishwa katika hali yao ya kufa na kwenda katika hali ya kutokufa, hapo ndipo matendo yote matakatifu yaliyotendwa nao yatakapodhihirishwa. Matendo hayo yatahifadhiwa milele hata milele. Hakuna hata moja, haidhuru liwe dogo kiasi gani au la kawaida jinsi gani, litakalopotea. Kwa njia ya wema wa haki yake Kristo anayotuhesabia bure [matendo hayo] yanaihifadhi harufu yake nzuri. ----- Letter 21, 1897. "MFUMO WA UPOLE HALISI" Agosti 19 Tena iweni wafadhili ninyi kwa ninyi, wenye huruma, mkasameheane kama Mungu katika Kristo alivyowasamehe ninyi. Waefeso 4:32. Yatupasa kutumia maneno yaliyo bora kuelezea mwenendo wa wengine.... Iwapo tunashuku daima mambo yaliyo maovu, basi, tuko katika hatari ya kufanya kile tunachokishuku kipate kutokea.... Hatuwezi kupita [duniani] bila kuumizwa mioyo yetu na hasira yetu kujaribiwa, lakini sisi kama Wakristo tunapaswa kuwa wavumilivu tu, yaani, wastahimilivu, wanyenyekevu, na wapole kama vile tunavyotaka wengine kuwa hivyo kwetu. Ni maelfu mangapi ya matendo mema na matendo ya fadhili tunayopokea... ambayo yanapitiliza mpaka mioyoni mwetu na kutoweka kama umande wakati wa jua, ambapo madhara tunayoyawazia tu au ya kweli yanaacha alama ambayo haiwezekani kabisa kuifuta! Mfano ulio rahisi kabisa wa kuwapa wengine ni ule wa sisi wenyewe kutenda mema kwao, na kisha kuacha sifa yetu mikononi mwa Mungu pasipo kuonyesha wasiwasi mwingi wa kutaka kuisahihisha mivuto mibaya inayotuzunguka na kuliweka shauri letu [mbele ya watu] katika nuru iliyo nzuri.... Kupuuzia kuikuza roho ile ya kufikiriana sisi kwa sisi kwa huruma na ustahimilivu kumeleta mafarakano, kutoaminiana, kutafutana makosa, na kutokuwa na umoja kwa jumla. Mungu... anatuagiza kuiweka mbali dhambi hiyo kubwa na kujitahidi kuijibu sala ya Kristo aliyoomba kwamba wafuasi wake wawe na umoja kama yeye alivyo na umoja na Baba yake.... Ni kazi maalum ya Shetani kuleta faraka,... ili ulimwengu ukose kupata ushuhuda wenye nguvu sana unaoweza kutolewa na Wakristo kwamba Mungu amemtuma Mwanawe kuipatanisha mioyo iliyojaa fujo, kiburi, wivu, kijicho, na ushupavu wa dini.... Kweli ya Mungu haikuwekwa kwa ajili ya kushughulika na makosa na maovu tu.... Kweli hiyo imewekwa kwa ajili ya kumtakasa mpokeaji, kumgeuza na kumuumba upya mwanadamu, kwa nje na kwa ndani, kwa kukishusha chini kiburi chake na mipango ya moyo wake ili awe mpole na mpenda urafiki na mwenye kujidhalilisha. Naam, dini ya Kristo ni mfumo wa upole halisi, na ushindi wake ni kamili wakati ulimwengu unapowaangalia watu wanaokiri kuwa ni wacha Mungu wakiwa wameungana katika umoja, yaani, waumini wale waonyeshao tabia zile za huruma na upole katika mwenendo wao na kujali kwa dhati kutunza sifa ya kila mmoja wao. ----- Letter 25, 1870. MVUTO USIOWEZA KUZUILIKA Agosti 20 Basi, kwa kuwa mmekuwa wateule wa Mungu, watakatifu wapendwao, jivikeni moyo wa rehema, utu wema, unyenyekevu, upole, uvumilivu. Wakolosai 3:12. Maneno ya upole, mtazamo mzuri wa macho, uso mchangamfu, huitupa nguvu ya mvuto mzuri kumzunguka Mkristo, ambayo inaufanya mvuto wake uwe karibu hauzuiliki. Hiyo ndiyo njia ya kujipatia heshima, na kupanua eneo la kuweza kutumika kwa manufaa, jambo ambalo hugharimu kidogo tu. Hiyo ndiyo dini ya Kristo moyoni ambayo inayafanya maneno yanayotoka humo kuwa ya kiungwana na mwenendo kuwa wa kujishusha hadhi, hata kwa wale walio katika hali duni sana ya maisha. Mtu anayefoka, anayetafuta makosa kwa wengine, anayewalazimisha wengine sio Mkristo; kwa maana kuwa Mkristo ni kufanana na Kristo.... Anayekunywa roho ya Kristo ataiacha ibubujike kwa njia ya maneno ya upole, na kuionyesha katika mwenendo wake wa heshima. Mpango wa wokovu umekusudiwa kukilainisha kitu cho chote kinachoparuza au kikali katika mwenendo wa mtu. Badiliko la nje litashuhudia badiliko la ndani. Kweli ndiyo inayotakasa, yaani, inayomfanya mtu kuwa mwungwana. Ikipokewa moyoni, inafanya kazi kwa uwezo uliojificha, ikimbadilisha mpokeaji. Lakini wale wanaoikiri kweli na wakati uo huo wanakuwa wakorofi, na wachungu, yaani, wale wanaokuwa na maneno makali na mwenendo usioonyesha huruma, hao hawajajifunza kitu kwa Yesu; mwonekano wote huo hudhihirisha kwamba hao ni watumwa wa yule mwovu. Hakuna mtu ye yote anayeweza kuwa Mkristo pasipo kuwa na roho ya Kristo, yaani, pasipo kuonyesha upole, uungwana, na matendo mazuri katika mwenendo wake.... Wakristo wanaopendeza, wapole, na waliolelewa vizuri watakuwa na mvuto kwa ajili yake Mungu na kweli yake; haiwezekani kwao kuwa kinyume na hayo.... Nuru ile iliyoazimwa kutoka Mbinguni itatawanya mionzi yake mikali kupitia kwao na kwenda katika njia ya wengine.... Maneno tusemayo, yaani, mwenendo wetu wa kila siku, ni tunda linalokua juu ya mti huo. Kama tunda hilo ni chungu na ladha yake sio nzuri, basi, mizizi midogo sana ya mti huo haipati chakula chake kutoka kwenye chanzo safi. Iwapo mapenzi yetu yanapatana na yale ya Mwokozi, iwapo tabia zetu ni za upole na unyenyekevu wa moyo, basi, tunatoa ushahidi kwamba uhai wetu umefichwa pamoja na Kristo katika Mungu; na nyuma yetu tutaacha njia inayong'aa.... Watazamaji watatambua kwamba tumekuwa pamoja na Kristo na kwamba tumejifunza kwake. ----- RH, Sept. 1, 1885. KUIHIFADHI ROHO YA YESU Agosti 21 Mkichukuliana, na kusameheana, mtu akiwa na sababu ya kumlaumu mwenzake; kama alivyowasamehe ninyi, vivyo na ninyi. Wakolosai 3:13. Tumo ulimwenguni humu kukutana na watu walio na mawazo ya aina mbalimbali na wenye tabia zinazohitilafiana, nanyi yawapasa kuwafikiria hao kuwa hawatofautiani sana nanyi kama vile ninyi nanyi msivyotofautiana sana nao.... Yatupasa kujizoeza kuwa na moyo wa kuchukuliana [kuvumiliana], ustahimilivu, upole, utu wema, na upendo, kisha tupate kufungwa pamoja nao kwa vifungo vya undugu wa kibinadamu. Hebu yule Mwokozi wetu mpendwa na awe mgeni anayekaribishwa moyoni mwenu. Kama Kristo anakaa moyoni mwenu, basi, mtamdhihirisha Kristo kwa maneno yenu, sheria ya upole itakuwa katika ulimi wenu, nanyi mtakuwa na amani mioyoni mwenu. Hapo ndipo mambo yote ya nje yatakapokuwa amani, nanyi mtamwimbia Mungu nyimbo mioyoni mwenu. ----- Letter 64, 1888. Baraka inawakalia wapatanishi.... Laiti kama Bwana angenijaza Roho wake Mtakatifu, ili daima nipate kuwa kile Kristo anachokiita mpatanishi! Mimi sipendi kuwa katika mazingira ya ugomvi na malumbano. Nataka niweze kusema Sala ya Bwana, "Utusamehe deni zetu, kama sisi nasi tuwasamehevyo wadeni wetu." Je! twawezaje kuisema sala hiyo na wakati uo huo tusiwe na roho ya kusamehe?... Kuwahukumu ndugu zetu, kuruhusu hisia zetu mbaya kutunzwa dhidi yao, hata kama sisi twajisikia kwamba hawajatutendea haki kabisa; hakutaleta baraka yo yote mioyoni mwetu, wala hakutasaidia hata kidogo katika shauri hilo. Mimi sithubutu kuziruhusu hisia zangu kukimbia katika njia ile ya kuwinda [kutafuta-tafuta] manung'uniko yangu yote na kuyasimulia tena na tena, na kukaa katika mazingira yale ya kuwa na mashaka, uadui, na mfarakano.... Kuna nuru katika kumfuata Yesu, kuzungumza na Yesu, kumpenda Yesu, nami sitauruhusu moyo wangu kutafakari au kunena vibaya juu ya ndugu zangu. Kristo alisema, "Kadiri mlivyomtendea mmojawapo wa hao ndugu zangu walio wadogo, mlinitendea mimi." Mathayo 25:40. Nisingependa kukosa kuwa na huruma kwa mtu ye yote au kumchukia. Nisingependa kuwa mshtaki wa ndugu zangu. Shetani atajaribu kuuchochea moyo wangu kufanya hivyo, lakini mimi siwezi [kukubali] kufanya hivyo. Nitaihifadhi roho ya Yesu ya kusamehe. ----- Letter 74, 1888. "HAUONI UCHUNGU" Agosti 22 Upendo huvumilia, hufadhili; upendo hauhusudu; upendo hautakabari; haujivuni; haukosi kuwa na adabu; hautafuti mambo yake; hauoni uchungu; hauhesabu mabaya. 1 Wakorintho 13:4,5. Wengi wanazo hisia kali zilizo dhahiri, ambazo hazijatakaswa, zinazowafanya wawe macho sana kulidaka neno fulani, kuangalia mtazamo fulani wa macho, au kuliona tendo fulani ambalo wanaweza kulitafsiri kuwa ni utovu wa adabu na kutomthamini mtu mwingine. Yote hayo ni lazima tuyashinde. Kila mmoja hana budi kusonga mbele katika kicho chake Mungu, akifanya vizuri kwa kila awezalo pasipo kusumbuliwa na sifa anazopewa na watu, wala kuchukizwa kwa lawama zile zinazotolewa na watu juu yake, akiwa anamtumikia Mungu kwa bidii, na kujifunza kuweka tafsiri nzuri sana juu ya yote yale yanayoweza kuonekana kuwa ni ya kuchukiza ndani ya wengine. ----- MS 24, 1887. Tunaweza kutazamia ya kwamba taarifa za uongo juu yetu zitazunguka huku na huku; lakini kama sisi tunaifuata njia ile iliyonyoka, kama sisi hatujali mambo kama hayo, basi, wengine nao hawatajali pia. Hebu na tumwachie Mungu ulinzi wa sifa zetu.... Kashfa inaweza kupuuzwa na kusahaulika kwa namna tunavyoishi sisi; haisahauliki kwa kusema maneno machungu. Hebu wasiwasi wetu mkuu na uwe katika kutenda kwa kicho cha Mungu, na kuonyesha kwa mwenendo wetu kwamba taarifa hizo ni za uongo. Hakuna mtu ye yote awezaye kuiharibu tabia yetu kuliko vile sisi wenyewe tuwezavyo. Ni miti ile iliyo dhaifu na nyumba zile zinazoyumbayumba ambazo daima huhitaji kuinuliwa kwa nguzo. Tunapojionyesha sisi wenyewe kuwa tuna wasiwasi sana wa kuilinda sifa yetu dhidi ya mashambulio kutoka nje, hapo ndipo tunapotoa picha inayoonyesha kwamba sifa hiyo ina dosari mbele zake Mungu, na kwamba, kwa ajili hiyo, inahitaji kutetewa daima. ----- 3BC 1160. Wale ambao Yesu anawavumilia katika mengi sana, kutokana na kushindwa kwao na upotovu wao, hawapaswi kukumbuka daima dharau pamoja na makosa halisi au ya kuwazia tu waliyotendewa na watu.... Moyo ule uliojazwa na upendo ule usiohesabu mabaya hautakesha na kuangalia utovu wa adabu na manung'uniko ambayo huenda yakawa yamelengwa kwake. Mapenzi ya Mungu ni kwamba upendo wake [Mungu] utayafunga macho, masikio pamoja na moyo ili visiathiriwe na chokochoko hizo zote pamoja na mashauri yote ambayo Shetani angeyajaza humo. Kuna utukufu wa kifalme katika kunyamaza kimya kwa yule aliyekabiliwa na kufikiriwa vibaya au kutendewa vibaya. Kuitawala roho yako ni kuwa na nguvu kuliko wafalme au washindi. ----- 3BC 1160. JE, DINI IMEKUFANYA WEWE KUWA BORA ZAIDI? Agosti 23 Lakini hao kama wanyama wasio na akili, ambao walizaliwa kama wanyama tu wa kukamatwa na kupotezwa, wakikufuru katika mambo wasiyoyajua, wataangamizwa katika siku ya maangamizo yao. 2 Petro 2:12. Kwa namna yo yote ile tulivyo mioyoni mwetu ndivyo itakavyodhihirishwa katika tabia yetu, ambayo itakuwa na mvuto wa aina yake juu ya wale wote tutakaoshirikiana nao. Maneno yetu, na matendo yetu, ni harufu ya uzima iletayo uzima ama mauti iletayo mauti. Na katika hukumu ile tutaletwa ana kwa ana kukutana na wale ambao tungekuwa tumewasaidia kwenda katika njia za haki, zilizo salama kwa maneno yetu yaliyochaguliwa vizuri, kwa kuwapa mashauri, kama sisi tungekuwa tuna uhusiano mzuri wa kila siku na Mungu wetu na shauku hai ya kudumu ya kuziokoa roho zao. ----- Undated MS 73. Mkristo asiridhike tu kuwa mtu mwenye bidii katika biashara yake. Asingejiingiza mno katika mambo ya dunia hii kiasi cha kukosa hata muda mchache alioutenga kwa ajili ya faida ya wengine, kwa ajili ya kujiendeleza akili zake, au kwa ajili ya usitawi wa roho yake, au kuwa na wazo la kujiburudisha, au kufanya urafiki. Nguvu na bidii katika biashara [kazi] vina sifa yake, lakini hivyo visingetufanya sisi kuupuuzia upendo wetu kwa Mungu na kwa mwanadamu ambao Biblia inatuagiza kuuonyesha.... Kusema kweli, katika mambo ya maisha yetu ya kidunia, mwenendo wetu sisi kwa sisi, unaongelewa kwa makini sana na kwa ukali. Tusemayo kanisani hayana matokeo makubwa sana kama ulivyo mwenendo wetu kwa wale wanaotuzunguka nyumbani mwetu na miongoni mwa majirani zetu. Neno lile la upole, tendo lile la kuwafikiria wengine, upole wa kweli pamoja na ukarimu, daima vitakuwa na mvuto wenye nguvu kuweza kuifanya dini ya Kikristo ipendwe na watu. Hebu ushuhuda wa aina hii usitolewe kwa ye yote miongoni mwetu. "Dini haijawafanya kuwa bora zaidi. Wanajifurahisha nafsi zao, wanaipenda dunia, ni wadanganyifu katika biashara zao, hakuna tofauti na vile walivyokuwa zamani." Wale wote wanaozaa matunda kama hayo wanawatawanya watu mbali na Kristo, badala ya kuwakusanya pamoja naye. Wanaweka vipingamizi katika njia ya wale ambao kwa njia yao ya unyofu wangeweza kuwaleta kwa Yesu. Sisi kama Wakristo ni wajibu wetu kuupa ulimwengu ushahidi usioweza kukosewa kwamba sisi tunaitii amri ile kuu, isemayo, "Mpende jirani yako kama nafsi yako," ambayo inafanana kabisa na Sheria ya Dhahabu ya Mwokozi wetu, isemayo, "Basi yo yote myatakayo mtendewe na watu, nanyi watendeeni vivyo hivyo." ----- ST, Jan. 12, 1882. SIRI YA KURIDHIKA Agosti 24 Walakini utauwa pamoja na kuridhika ni faida kubwa. 1 Timotheo 6:6. Dini iliyo safi huleta amani, furaha, kuridhika; utauwa una faida katika maisha haya na maisha yale yajayo. ----- Letter 1b, 1873. Hali ile ya kutotulia na kutoridhika inayoishia katika wasiwasi na kulalamika ni dhambi; ila hali ile ya kutoridhika na nafsi yako, ambayo inakusukuma wewe kutumia juhudi nyingi zaidi kwa maendeleo makubwa zaidi kiakili kwa ajili ya kuwa na upeo mpana wa kutumika inastahili kupongezwa. Kutoridhika kama huko hakuishii katika kukata tamaa bali katika kuzikusanya nguvu ili kuufikia upeo wa juu ulio mpana wa kutumika. Ila tu inakupasa daima kuweka uwiano kwa kuishikilia kanuni imara ya dini na kuwa na dhamiri kali, ukiweka kicho cha Mungu mbele yako daima, ndipo utafanikiwa kwa hakika kuwa katika hali ya maisha inayofaa kwa kutumika. ----- Letter 16, 1872. Ingetupasa sisi kuishi kwa ajili ya ulimwengu ule ujao. Ni jambo baya mno kuishi maisha ya ovyo, yasiyokuwa na lengo lo lote. Tunataka kuwa na lengo katika maisha haya ----- kuishi kwa kusudi fulani. Mungu atusaidie sisi sote kuwa watu wanaojitolea mhanga, wasiojifikiria wenyewe sana, wanaojisahau nafsi zao pamoja na mambo yao wayapendayo; na kufanya mema, si kwa heshima tunayotazamia kuipokea hapa, bali kwa sababu hilo ndilo kusudi la maisha yetu na litakuwa ndilo jibu la kuwako kwetu hapa. Hebu maombi yetu ya kila siku na yapande juu kwa Mungu ili atuvue uchoyo wetu.... Nimeona ya kwamba wale wanaoishi kwa kusudi fulani, wakiwa wanatafuta kuwanufaisha na kuwaletea mibaraka wanadamu wenzao na kumheshimu na kumtukuza Mkombozi wao, hao ndio wenye furaha ya kweli hapa duniani, ambapo mtu yule asiyetulia, asiyeridhika, na yule atafutaye hiki au kukijaribu kile, akitumainia kupata furaha, daima huwa analalamika juu ya kukatishwa tamaa. Daima yeye ni mhitaji, hatosheki kamwe, kwa sababu anaishi kwa ajili ya nafsi yake peke yake. Hebu na liwe ndilo lengo lako kutenda mema, kufanya sehemu yako katika maisha haya kwa uaminifu. ----- Letter 17, 1872. Uwe na wasiwasi pamoja na bidii kukua katika neema, ukitafuta ufahamu ulio wazi zaidi na wa busara ili kuyajua mapenzi ya Mungu kwako wewe, ukijitahidi kwa bidii kuifikia mede ya thawabu iliyo mbele yako. Utimilifu wa Kikristo peke yake ndio utakaokupatia vazi lile la tabia lisilokuwa na waa, ambalo litakupatia haki ya kusimama mbele ya kiti kile cha enzi cha Mungu miongoni mwa kundi lile kubwa lililofua mavazi yao katika damu ya Mwana-Kondoo, ukishika tawi la mtende la ushindi wa milele na shangwe ya milele. ----- Letter 16, 1872. CHUNGA HATUA YAKO! Agosti 25 Ulisawazishe pito la mguu wako, Na njia zako zote zithibitike. Mithali 4:26. "Mkaifanyie miguu yenu njia za kunyoka," asema mtume, "ili kitu kilicho kiwete kisipotoshwe." Waebrania 12:13. Njia ile inayokwenda mbali na Mungu, yaani, mbali na kanuni yake ya haki, takatifu, na kamilifu [Amri Kumi], sikuzote imepotoka na ni ya hatari. Hata hivyo... wengi wamekuwa wakienda katika njia hiyo ya uasi. Katika mifano mingi [inayofahamika], hawakuanza vizuri katika utoto na ujana wao, nao wamezifuata njia hizo potofu katika safari yao yote. Sio tu kwamba wao wenyewe wamekosa kwa kuiacha njia ile ya kweli, bali kwa mvuto wa mfano wao wengine vile vile wamepotoshwa kutoka katika njia ile dhahiri iliyonyoka, nao wamefanya makosa ya kufisha.... Sikuzote huwa hatuitambui nguvu ya kielelezo. Tunakutana na wengine. Tunakutana na watu wanaotenda makosa, yaani, wanaotenda dhambi kwa njia mbalimbali; huenda wakawa ni watu wasiokubalika, wepesi kutenda, wenye harara na watumiaji wa mabavu. Tunaposhughulika na watu kama hao yatupasa kuwa wavumilivu, wastahimilivu, wapole, na waungwana. Shetani anafanya kazi yake kupitia kwao kuleta chokochoko kwetu na kutuhangaisha, ili tusipate nafasi ya kuonyesha tabia nzuri ya kupendeza. Kuna maonjo na matatizo kwa ajili yetu tunayopaswa kupambana nayo; kwa maana sisi tumo katika ulimwengu wa masumbufu, wasiwasi, na kukata tamaa. Lakini maudhi hayo yanayoendelea daima hayana budi kushughulikiwa katika roho ya Kristo. Kwa njia ya neema yake tunaweza kuinuka na kuwa washindi wa mazingira yetu, na kuzihifadhi roho zetu katika hali ya ukimya na utulivu katikati ya mahangaiko na masumbufu ya maisha ya kila siku. Kwa njia hiyo, sisi tutaweza kumwakilisha Kristo kwa ulimwengu.... Kujitoa wakf kwa Mungu ni lazima liwe jambo lililo hai, linalofanywa kwa vitendo; sio nadharia tu ya kuzungumza habari zake, bali kanuni iliyosukwa pamoja na maisha yetu. Tungeiacha nuru yetu iangaze mbele ya wengine ili, wanapoyaona matendo yetu mema, wapate kumtukuza Baba yetu aliye Mbinguni. Yatupasa kuzitangaza sifa zake yeye aliyetuita tutoke gizani tukaingie katika nuru yake ya ajabu. Iwapo nuru ya mbinguni imo ndani ya moyo wetu, basi, itaakisiwa kwa wote wanaotuzunguka. Natamani wote wangeweza kuliona somo hili la maana katika nuru yake halisi. Hapo ndipo pasingalikuwapo na hali hii ya kutojali kutumia maneno na kutenda matendo yasiyofaa, wala kuishi maisha haya ya ovyo, ya kizembe, yasiyokuwa ya dini. ----- ST, Jan. 1, 1885. KUJENGA MAZOEA NA TABIA Agosti 26 Usiingie katika njia ya waovu, wala usitembee katika njia ya wabaya. Mithali 4:14. Ni wachache sana wanaotambua nguvu ya mazoea. Maandiko haya yaliyovuviwa huuliza swali hili, "Je! Mkushi aweza kuibadili ngozi yake, au chui madoa-doa yake?" Kisha yanaongeza maneno haya, "Ndipo na ninyi mnaweza kutenda mema, ninyi mliozoea kutenda mabaya." Yeremia 13:23. Hilo ni dai zito.... Lakini faraja iko na ujasiri katika kulitafakari wazo hili, kwamba iwapo mazoea mabaya hupata nguvu kama hiyo ambayo inaonekana kuwa karibu sana huwa haiwezekani kugeukia katika njia ile ya haki, basi, vivyo hivyo uwezo wa mazoea mazuri una nguvu iyo hiyo. Matokeo ya kazi ya kila siku, yaani, mwelekeo wake kama ni wa kutuinua juu katika mizani ya thamani ya maadili au kama ni wa kutushusha chini kwenda kwenye maangamizi, hutegemea yaliyofanyika katika siku zile zilizotangulia. Kushindwa leo huandaa njia ya kushindwa zaidi kesho; ushindi leo unahakikisha ushindi rahisi kesho. Basi, ni kwa jinsi gani tunapaswa kuwa waangalifu kuona kwamba mazoea na tabia tunazojenga ni sahihi na njema!... Enyi rafiki zangu vijana, izuieni miguu yenu isiende katika njia zote zilizo mbaya.... Wanadamu wanaweza kujidhibiti wenyewe na kufanya mema. Kama Danieli wanaweza kuwa na kusudi lililoanzishwa mbinguni mioyoni mwao hata wasiweze kuzinajisi nafsi zao au miili yao, licha ya kushuka chini kwa maadili na ufisadi wa kizazi hicho. Mungu alimpa Danieli "maarifa na ujuzi katika elimu na hekima." Danieli 1:17. Baraka yake iliambatana na mtu yule aliyetumia juhudi yake ya kibinadamu kulingana na mapenzi ya Mungu. Msaada uo huo bado utaendelea kutolewa kwa wale wote wanaofuata njia inayofanana na hiyo, nao wakiuweka utukufu wa Mungu mbele yao hujizoeza kutokunywa vileo kabisa na kujitawala nafsi zao. Tofauti ile ile itaonekana kati yao na wale wasiojizuia kama ile iliyokuwapo kati ya Danieli na wenzake na wale vijana wengine katika jumba lile la mfalme. Jicho litakuwa safi pamoja na rangi ya ngozi, hatua zitakuwa zenye nguvu, akili itakuwa na nguvu na wepesi, utambuzi mkali wa ile kweli utakuwamo moyoni. ----- ST, Jan. 1, 1885. Hebu na tukumbuke ya kwamba tabia haitokei kwa bahati, bali siku kwa siku inajengwa kwa wema au kwa ubaya. Umuhimu mkuu unaambatana na kazi hii ya kujenga tabia; kwa kuwa matokeo yake yanafika mbali sana. Sisi tu wajenzi kwa wakati huu wa sasa na kwa umilele. ----- ST, Jan. 1, 1885. MIBARAKA INATAWANYIKA KAMA MWANGA WA JUA Agosti 27 Ili mpate kuwa wana wa Baba yenu aliye mbinguni; maana yeye huwaangazia jua lake waovu na wema, huwanyeshea mvua wenye haki na wasio haki. Mathayo 5:45. Nayaona maongozi ya Mungu katika kazi zake zote.... Mawingu na mvua, pamoja na mwangaza wa jua unaong'aa, hivyo vyote vina utume wao katika kumpelekea mwanadamu mibaraka. Mungu wa maumbile anajua kile tunachohitaji hasa, naye husonga mbele kufuata mstari ule ulionyoka, akipeleka mibaraka yake juu ya wenye haki na wasio haki. Mimi nashukuru sana kwamba mawazo ya wanadamu hayawezi kupanga mambo kwa utaratibu mzuri kama huo. Makusudi yanayopingana yangedhihirika! ----- MS 54, 1886. Kuna ufinyu katika ufahamu wa kibinadamu ambao unamvunjia Mungu heshima. Hebu yule anayekiri kwamba Kristo ni Mwokozi wake asilikaribishe wazo la kwamba fadhili za Mungu zimewekwa kwa ajili yake na kwa wachache sana anaowapenda. Upendo na fadhili zake Mungu ni kwa kila mmoja. Hebu na tuzikusanye ishara za upendeleo wake, na kurudisha sifa na shukrani kwake kwa fadhili zake, ambazo ametugawia sisi, si kwa ajili ya kuzihodhi, bali kuzipitisha kwa wengine.... Mungu anamtazamia kila mmoja anayeifurahia neema yake kuisambaza neema hiyo kwa wingi kama Kristo anavyogawa fadhili zake. Kama vile jua linavyoangaza juu ya wenye haki na wasio haki, hivyo ndivyo Jua la Haki linavyoiakisi nuru yake kwa ulimwengu mzima. ----- MS 31, 1911. Mibaraka ya Mungu, mwanga wa jua na manyunyu, joto na baridi, na kila mbaraka wa asili, imetolewa kwa ulimwengu huu. Kujitenga kusidumishwe na watu wo wote wale. "Mimi ndimi nuru ya ulimwengu" (Yohana 8:12), Kristo alisema. Nuru ni mbaraka, mbaraka kwa ulimwengu wote, ambayo inamwaga hazina zake juu ya ulimwengu huu usiokuwa na shukrani, mwovu, na wenye kuharibika katika maadili yake. Bwana Yesu alikuja kuvunjilia mbali kila ukuta uliowatenganisha watu, kuubomoa kila ukuta uliomo hekaluni ambamo Mungu anakaa, ili kila sikio lipate kusikia, kila jicho lipate kuona, kwamba kila mtu aliye na kiu anywe maji ya uzima bure. ----- MS 168, 1898. Mungu anaitawanya mibaraka yake katika njia yetu yote.... Tunaweza kulia na kuguna na kuomboleza na kujikwaa kwa kila hatua moja tunayokwenda kama tutachagua kufanya hivyo, ama tunaweza kukusanya maua ya thamani yenye harufu nzuri na kufurahi katika Bwana kwa fadhili zake katika kuifanya njia yetu ya kwenda mbinguni kuwa ya kupendeza sana. ----- Letter 17, 1886. KUJIFUNZA TABIA YA KRISTO Agosti 28 Ndipo mimi sitaaibika, Nikiyaangalia maagizo yako yote. Zaburi 119:6. Katika ulimwengu huu tunaweza kuchanganyikiwa vibaya sana, kama vile yule mwovu anavyotaka sisi tuwe, iwapo tutaendelea kuyaangalia mambo yale yanayotutatiza; maana kwa kuyafikiria sana, na kuzungumza juu yake, sisi tunakata tamaa. Katika kuwakosoa wengine kwa sababu wanashindwa kuonyesha upendo kwetu, tutauua ule mmea wa upendo katika mioyo yetu wenyewe. Je, sisi, kila mmoja peke yake, tumeona thamani yake na kulisikia joto la upendo ule ambao Kristo aliuwakilisha katika maisha yake? Basi ni wajibu wetu kuudhihirisha upendo huo kwa ulimwengu. Hebu na tuogope kufikiria sana, kutazama na kuzungumza juu ya makosa makubwa ambayo wengine wanafanya.... Mnaweza kujenga ulimwengu wa kufikirika katika mawazo yenu ninyi wenyewe na kuiona picha ya kanisa kamilifu, ambalo ndani yake majaribu ya Shetani hayawachochei tena watu kufanya maovu; lakini ukamilifu huo umo tu katika mawazo yenu. Ulimwengu huu ni ulimwengu ulioanguka, na kanisa nalo ni mahali panapowakilishwa na shamba ambamo hukua magugu na ngano. Vinapaswa kukua pamoja mpaka wakati wa mavuno. Si kazi yetu kuyang'oa magugu, kwa kufuata hekima yetu ya kibinadamu, chini ya ushauri wake Shetani, tusije tukaing'oa ngano.... Hakuna haja kwa watu wo wote kupoteza dakika zao za thamani za historia ya maisha yao mafupi kwa kujaribu kuyapima mapungufu waliyo nayo wale wanaojiita Wakristo. Hakuna hata mmoja wetu aliye na wasaa wa kufanya kazi hiyo. Kama tunaiona kwa dhahiri tabia ambayo Wakristo wangepaswa kuikuza, kisha tukaweza kuona ndani ya wengine kile kisichokwenda sawasawa na tabia hiyo, basi, hebu na tudhamirie kwamba sisi tutampinga kwa nguvu yule adui katika majaribu yake ya kutufanya sisi kutenda kwa njia isiyokuwa na uwiano wo wote na hali halisi ya mambo, kisha tutasema, "Sitamwaibisha Kristo. Nitajifunza kwa makini sana tabia ya Kristo ambaye ndani yake haikuonekana hitilafu yo yote, wala uchoyo, wala waa, wala kipaku cha uovu, yeye ambaye aliishi si kwa kujipendeza wala kujitukuza mwenyewe, bali kumtukuza Mungu, na kuwaokoa wanadamu walioanguka. Sitaziiga tabia zenye dosari za Wakristo hao wasiokuwa na msimamo mzuri, wala makosa yao waliyoyafanya hayatanifanya nifanane nao. Mimi nitamgeukia Mwokozi wangu wa thamani ili nipate kufanana naye." ----- Letter 63, 1893. NGOME IMARA YA ILE KWELI Agosti 29 Ambao Mungu alipenda kuwajulisha jinsi ulivyo utajiri wa utukufu wa siri hii katika Mataifa, nao ni Kristo ndani yenu, tumaini la utukufu. Wakolosai 1:27. Ninazidi kutamani sana ili Kristo apate kuumbika ndani yangu, tumaini la utukufu. Natamani kupambwa vizuri kila siku kwa unyenyekevu na upole wake Kristo, yaani, kukua katika neema na katika kumjua Yesu Kristo hata kukifikia kimo kile cha utimilifu wa wanaume na wanawake katika Kristo Yesu. Yanipasa mimi, kama mtu peke yangu, kwa njia ya neema niliyopewa na Yesu Kristo, kuiweka roho yangu katika hali ya afya na kuitunza kama njia ya Mungu ambayo kwayo neema yake, upendo wake, uvumilivu wake, na upole wake vitabubujika na kwenda ulimwenguni. Huo ndio wajibu wangu, nao hauko chini ya wajibu ule umpasao kila mshiriki wa kanisa anayedai kuwa yeye ni mwana au binti ya Mungu. Bwana Yesu ameliweka kanisa lake kuwa ghala [bohari] ya kweli yake takatifu. Ameliachia kazi ya kutekeleza makusudi yake pamoja na mipango yake ya kuziokoa roho alizozionyesha upendeleo wake, yaani, upendo kama huo usio na kifani. Kama vile lilivyo jua kuhusiana na dunia yetu, ndivyo naye anavyopanda juu katikati ya giza hili la kimaadili ----- Jua lile la Haki. Alisema hivi juu ya habari zake mwenyewe, "Mimi ndimi nuru ya ulimwengu." Yohana 8:12. Aliwaambia wafuasi wake, "Ninyi ni nuru ya ulimwengu." Mathayo 5:14.... Kwa njia ya kuakisi sura ya Yesu Kristo, kwa uzuri na utakatifu wa tabia zao, kwa kujikana nafsi zao daima na kujitenga mbali na sanamu zote, kubwa ama ndogo, wanaonyesha ya kwamba wamejifunza katika shule yake Kristo. Daima wanaishika roho yake ya upendo na uvumilivu, unyenyekevu, na upole, nao husimama kama wawakilishi wake Kristo, yaani, tamasha kwa ulimwengu, kwa malaika na kwa wanadamu.... Kwa kutembea na kufanya kazi duniani humu, bila kuwa wa ulimwengu huu, wanaijibu sala hii ya Kristo kwa tabia zao: "Mimi siombi kwamba uwatoe katika ulimwengu; bali uwalinde na yule mwovu." Yohana 17:15. Wanatakiwa kusimama kama ngome imara ya ile kweli, nuru yao ikiangaza mbali katika giza la kimaadili la ulimwengu huu. Bwana anao ujumbe wa kupeleka kwa walinzi juu ya kuta za Sayuni. Tarumbeta haina budi kutoa sauti yake inayoeleweka wazi. ----- MS 53, 1890. NJIA NZURI YA KUYAANGALIA MAMBO Agosti 30 Hatimaye, ndugu zangu, mambo yo yote yaliyo ya kweli, yo yote yaliyo ya staha, yo yote yaliyo ya haki, yo yote yaliyo safi, yo yote yenye kupendeza, yo yote yenye sifa njema; ukiwapo wema wo wote, ikiwapo sifa nzuri yo yote, yatafakarini hayo. Wafilipi 4:8. Kadiri Shetani anavyoendelea kuwa na uwezo wa kufanya kazi yake katika mioyo ya wanadamu ambayo haina kizuizi cha Roho Mtakatifu, ndivyo kadiri kutakavyokuwako na pambano kali na lenye nguvu kati ya wema na uovu, na uovu utadhihirishwa, hata miongoni mwa wale wanaojidai kuwa ni watoto wa Mungu.... Hakuna sababu yo yote kwetu sisi kukaza macho yetu juu ya makosa, kusikitika na kulalamika, na kupoteza muda wetu wa thamani na nafasi zetu nzuri kuomboleza kwa ajili ya makosa ya wengine.... Je! isingependeza zaidi kwa Mungu kama sisi tungekuwa na mtazamo usiopendelea upande wo wote, na [badala yake] kuona ni watu wangapi wanaomtumikia Mungu, ambao wanayapinga majaribu, na kumtukuza na kumheshimu yeye kwa talanta zao za mali na akili? Je! isingekuwa bora kwetu kuutafakari uwezo wa ajabu wa Mungu, ufanyao miujiza katika kuwabadilisha maskini wenye dhambi, waliodhalilishwa, ambao wamejaa uchafu wa kimaadili, ambao wanabadilika sana kiasi kwamba wanafanana na Kristo katika tabia zao?... Hebu na tuyageuze macho yetu tusiangalie mapungufu ya wale waliomo kanisani, lakini ambao hawafanani na Kristo. Sisi hatutawajibika kwa sababu ya madai makubwa ya wale wasiokuwa na tabia njema zinazolingana na madai yao. Hebu na tumshukuru Mungu kwamba ni nafasi yetu nzuri kuyageuza macho yetu mbali na Wakristo hao walio na kasoro katika tabia zao, na kuwatazama wale waliojitoa wakf kweli kweli, ambao ni watendaji wa lile Neno, na ambao katika maisha yao na tabia zao wanachukua chapa ya sura ya Mungu. Na juu ya hayo yote, unapaswa kumshukuru Mungu kwamba ni nafasi yako nzuri kumtazama Kristo, aliye kielelezo chetu kamili.... Kila kitu kinachotufanya sisi kuuona udhaifu wetu wa kibinadamu kimo katika kusudi lake Bwana kwa ajili ya kutusaidia sisi kumtazama yeye, na kwa vyo vyote vile tusiweke tegemeo letu kwa mwanadamu, wala kumfanya mwanadamu kinga yetu.... Tunabadilishwa kufanana na sura ya kile tunachokitafakari sana. Basi ni muhimu jinsi gani kwetu kuifungua mioyo yetu kwa mambo yale tu yaliyo ya kweli, yenye kupendeza na yenye sifa njema. ----- Letter 63, 1893. INUENI JUU BENDERA Agosti 31 Piteni, piteni, katika malango; Itengenezeni njia ya watu; Tutieni, tutieni barabara; toeni mawe yake; Twekeni bendera kwa ajili ya kabila za watu. Isaya 62:10. Neno la Mungu linatangaza sio tu kanuni kuu za ile kweli ambazo zingeyatawala maisha yetu pamoja na wajibu wake, bali linaonyesha pia, kwa kututia sisi moyo, historia ya wengi ambao wamezionyesha kanuni hizo katika maisha yao.... Ukiondoa Kiolezo kile kikamilifu [Kristo], hakuna mtu hata mmoja aliyeelezwa katika Kurasa zake Takatifu [Biblia] anayefaa zaidi kuigwa tabia yake kama nabii Danieli. Akiwa ameachwa bila kinga katika ujana wake alikabiliwa na vishawishi vyote vya jumba lile la kifalme, akawa mtu mwenye msimamo usiopindika na mwenye bidii katika kumcha Mungu. Mara kwa mara alipatwa na majaribu makali ya Shetani, lakini bado tabia yake haikuyumba, wala njia yake kugeukageuka. Alikuwa imara mahali ambapo wengi wangeshindwa; alikuwa mkweli mahali ambapo wangekuwa waongo; alikuwa na nguvu mahali ambapo wangekuwa dhaifu. Danieli alikuwa ule mwerezi mrefu wa Lebanoni.... Laiti kama imani ile, msimamo ule, na kumcha Mungu kule alikokuwa nako Danieli kungalikuwa ndani ya mioyo ya watu wa Mungu leo! Sifa hizo nzuri za tabia hazijapata kuhitajika kamwe ulimwenguni kama ilivyo leo.... Katika kumbukumbu za wale waliotenda kazi na kuteswa kwa ajili ya jina la Yesu, hakuna jina linalong'aa kwa mng'ao au lililo na fahari isiyo na waa kama jina la Paulo, mtume kwa Mataifa. Upendo wake Yesu, uliokuwa unawaka moyoni mwake, ulimfanya ajisahau nafsi yake, yaani, ajikane nafsi yake. Alikuwa amemwona Kristo yule aliyepaa juu, na sura ile ya Mwokozi wake ilipigwa chapa moyoni mwake, na kuangaza nje katika maisha yake. Kwa imani, ujasiri, na ushupavu wake, ambao haukuweza kutishwa na hatari wala kucheleweshwa kwa vizuizi, alisonga mbele katika safari yake toka nchi hata nchi kueneza maarifa ya msalaba.... Je, hivi wale wanaojidai kuwa ni wafuasi wake Kristo wanazionyesha kwa mfano [wa maisha yao] kanuni hizo za imani yao? Uko wapi uzoefu wenye kina, ulio hai, na mtakatifu, ambao watu wa Mungu hawakukosa kusimulia habari zake? Je, kiwango cha Ukristo kimeshushwa chini?... Hapana; kiwango kile kimebaki pale pale tu alipokiweka Mungu. Watu wake walio watakatifu wa vizazi vilivyopita walitakiwa kuviacha vyote kwa ajili ya Kristo, kuwa na roho kama yake, na kukiiga kielelezo chake. Hakuna kitu pungufu kuliko hicho atakachokikubali hivi sasa.... Tukiitwa kuviacha vyote kwa ajili ya Kristo, ni nani atakayesimama imara katika jaribio hilo? ----- RH, Nov. 7, 1882. KUMBUKUMBU ZA MAKAO YETU MBINGUNI Septemba 1 Wewe ndiwe BWANA, wewe peke yako; wewe ulifanya mbingu, mbingu za mbingu, pamoja na jeshi lake lote, dunia na vyote vilivyomo, nawe unavihifadhi vitu hivi vyote; na jeshi la mbinguni lakusujudu wewe. Nehemia 9:6. Kuna uzuri wa aina yake katika utukufu wa kuogofya wa bonde, wa miamba mizito, mikubwa sana, iliyopasuka; kuna fahari katika milima mirefu kama mnara inayoonekana kana kwamba inazigusa mbingu. Kuna miti mirefu sana yenye majani yaliyotengenezwa kwa namna ya kupendeza sana; minara ya majani iliyochongoka kwenda juu, jicho la ua linalofunguka na ua linalochanua, miti ya porini, na kila kitu kilicho na uhai. Vyote hivyo huyaelekeza mawazo yetu kwa Mungu mkuu, yule aliye hai. Kila uwezo tulio nao mwilini mwetu hushuhudia ya kwamba yuko Mungu aliye hai, nasi tunaweza kujifunza kutoka katika kitabu hicho kilicho wazi cha viumbe vya asili mafundisho ya thamani mno kumhusu Bwana yule wa mbinguni. Katika kujifunza kama huko mawazo yetu hupanuka, na kuinuliwa juu na kutiwa nguvu, tena yanakuwa na njaa ya kutaka kujua zaidi juu ya Mungu na ukuu wake. Tumeamsha mioyoni mwetu hisia sio tu zile za kumheshimu na kumcha, bali za upendo, za imani, za kumtumainia na kumtegemea kabisa yule ambaye ni Mpaji wa mema yote. Na kadiri mimi ninavyoziangalia kazi zake za ajabu na kuona ushahidi wa uweza wake, kimoyomoyo najiuliza hivi: "Mtu ni kitu gani hata umkumbuke, Na binadamu hata umwangalie?" Zaburi 8:4. Ukuu na utukufu wote wa vitu hivi vya ajabu katika nyumba ya Mungu unaweza kuthaminiwa tu tunapovitafakari katika mawazo yetu kuhusiana na Mungu na makao yetu yale ya baadaye yenye raha kuu ambayo anawaandalia wale wampendao.... Wakati sisi tunazungumza sana habari za nchi zingine, mbona tunakaa kimya kuhusu nchi ile ya mbinguni, na nyumba ile ya milele isiyojengwa kwa mikono, iliyo katika mbingu zile? Nchi hiyo ya mbinguni ina matokeo makubwa kwetu kuliko mji mwingine wo wote au nchi yo yote duniani humu, basi, tungetafakari na kuzungumza zaidi juu ya nchi hiyo nzuri sana ----- yaani, ile ya mbinguni. Tena, ni kwa nini hatuzungumzi kwa dhati zaidi, na kwa roho ile ya mbinguni, kuhusu vipawa vya Mungu tunavyoviona katika ulimwengu wetu? Ameviumba vitu vyote hivyo, naye anakusudia kwamba sisi tutaweza kumwona Mungu katika kazi zake hizo alizoziumba. Vitu hivyo vinapaswa kumweka Mungu katika kumbukumbu zetu na kuiinua juu mioyo yetu mbali na mambo ya anasa na kuifunga katika vifungo vya upendo na shukrani kwa Muumbaji wetu. ----- MS 62, 1886. VIUMBE VYA ASILI HUMTANGAZA MUNGU Septemba 2 Nimezikumbuka siku za kale, Nimeyatafakari matendo yako yote, Naziwaza kazi za mikono yako. Nakunyoshea mikono yangu; Nafsi yangu inakuonea kiu kama nchi kame. Zaburi 143:5,6. Tumeiangalia milima mirefu sana yenye matuta ya mkingamo katika uzuri wake mkuu, pamoja na buruji zake za miamba zinazofanana na nyumba kubwa za zamani zenye boma [ngome]. Milima hiyo hututangazia sisi ghadhabu ya Mungu iangamizayo ili apate kuithibitisha sheria yake iliyovunjwa; kwa maana [milima hiyo] iliinuliwa juu kwa tetemeko lililoitikisa sana nchi wakati ule wa Gharika. Ni kama mawimbi yenye nguvu nyingi sana yaliyosimama wakati yaliposikia sauti ya Mungu ----- mawimbi yaliyogandishwa, yaliyozuiwa katika kiburi chake kikubwa sana na kuwa mawimbi makubwa. Milima hiyo mirefu sana ni yake Mungu; anakaa juu ya ngome za miamba yake iliyo imara. Utajiri unaotokana na migodi yake ni wake pia, na hivyo ndivyo vilivyo mali yake vilindi vile virefu vya nchi. Ukitaka kuona ushahidi kwamba Mungu yuko, angalia pande zote po pote bahati yako inapoweza kukuangukia. Anazungumza na fahamu zako na kuugusa moyo wako kwa njia ya kazi zake alizoziumba. Hebu moyo wako na uzipokee picha hizo, ndipo viumbe vya asili vitakuwa kitabu kilichofunguliwa kwako, na vitakufundisha kweli ya Mungu kwa njia ya vitu vya kawaida unavyovifahamu. Miti mirefu sana haitaangaliwa kwa moyo usiojali. Kila ua linalochipua, kila jani lenye mishipa yake myororo, litashuhudia ustadi usio na kifani wa yule Msanii Mkuu sana. Miamba mikubwa sana na milima mirefu sana inayoinuka kule mbali si matokeo ya nasibu. Inatangaza kwa lugha ya kimya inayoshawishi habari za yule Mmoja anayekaa juu ya kiti cha enzi cha malimwengu, yule aliye juu na mwenye kutukuzwa. "Kazi zake zote zajulikana kwa Mungu tangu mwanzo wa ulimwengu." Mipango yake yote ni mikamilifu. Ni kicho na heshima ilioje jina lake lingeweza kuamsha ndani yetu!... Mungu mwenyewe ndiye Mwamba wetu wa Kale, kimbilio la watu wake, kificho mbali na dhoruba, kivuli jua kali linapounguza. Ametupatia ahadi zake, ambazo ni imara zaidi na madhubuti kuliko miinuko hiyo ya miamba, ni milima ile ya milele. Milima itatoweka, na vilima vitaondolewa; bali fadhili zake hazitaondoshwa, wala agano lake la amani halitaondolewa kwa wale ambao kwa imani wanamfanya yeye kuwa tegemeo lao. Iwapo tungeweza kumtazamia Mungu kutupa msaada wake kwa uthabiti kama ule wa milima hiyo kame yenye miamba, inayozielekea mbingu zilizo juu yake, basi, tusingeweza kuondolewa kamwe katika imani yetu kwake wala katika utii wetu kwa sheria yake takatifu. ----- RH, Feb. 24, 1885. SHULE YA AKILI NA MAADILI Septemba 3 Nao wauimba wimbo wa Musa, mtumwa wa Mungu, na wimbo wa Mwana-Kondoo, wakisema, Ni makuu, na ya ajabu, matendo yako, Ee Bwana Mungu Mwenyezi; Ni za haki, na za kweli, njia zako, Ee Mfalme wa mataifa. Ufunuo 15:3. Mwasisi Mkuu ameumba na kuzitengeneza mandhari mbalimbali katika maumbile [ulimwengu huu] ili zipate kuwa na maana kubwa katika tabia ya mwanadamu kiakili na kimaadili. Hizo zinatakiwa ziwe shule ya Mungu ya kuikuza akili na maadili. Hapo ndipo akili inaweza kuwa na nyanja pana sana ya utafiti katika maonyesho hayo ya matendo makuu ya Mungu wa milele. Miamba ni miongoni mwa vitu vya thamani ulimwenguni, ikiwa na hazina za hekima na maarifa. Katika miamba na milima hiyo umeandikwa ukweli kwamba hakika Mungu aliwaangamiza kwa Gharika wale waovu juu ya uso wa nchi hii. ----- MS 73, 1886. Watu wale walijifikiria wenyewe kwamba walikuwa na hekima kuliko Mungu, na hekima ya kupindukia hata wasitake kutii... sheria na amri zake Yehova. Utajiri wa dunia hii aliowapa Mungu haukuwafanya kutii, bali kuasi, kwa sababu walivitumia vibaya vipawa vizuri vilivyotoka mbinguni, na kuifanya mibaraka ile waliyopewa na Mungu kuwa vitu vya kuwatenga mbali na Mungu. Na kwa kuwa walikuwa na tabia kama ile ya Shetani, badala ya ile ya Mungu, Bwana alituma maji ya Gharika juu ya ulimwengu ule wa zamani. ----- MS 62, 1886. Mungu amejaa upendo, naye ni mwingi wa rehema; lakini kwa vyo vyote vile hataweza kuwaachilia [pasipo kuwapa adhabu] wale wasioujali wokovu wake mkuu aliowapa. Wakazi wale walioishi kwa miaka mingi sana kabla ya Gharika wakafagiliwa mbali kutoka juu ya uso wa nchi hii kwa sababu waliitangua sheria ya Mungu. Mungu hataleta tena maji kutoka katika mbingu za juu na chini ya nchi hii kama silaha zake za kutumia katika maangamizi ya ulimwengu huu; bali kisasi kinachokuja kitakapomwagwa juu ya wale wanaoyadharau mamlaka yake, [waovu] wataangamizwa kwa moto uliofichwa chini kabisa ya dunia hii, utakaochochewa sana na kufanya kazi yake kwa mioto ile itakayotoka mbinguni juu. Baada ya tukio hilo ndipo kutoka katika nchi hii iliyotakaswa utaimbwa wimbo huu wa sifa: "Baraka na heshima na utukufu na uweza una yeye aketiye juu ya kiti cha enzi, na yeye Mwana-Kondoo, hata milele na milele." Ufunuo 5:13. "Ni makuu, na ya ajabu, matendo yako, Ee Bwana Mungu Mwenyezi; Ni za haki na za kweli, njia zako, Ee Mfalme wa mataifa [watakatifu]." Na kila mmoja aliyeifanya hazina ile ya mbinguni kuchukua nafasi ya kwanza katika mawazo yake, ... atajiunga kuimba wimbo huo mkuu wa ushindi. ----- RH, Feb. 24, 1885. MABWAWA MAKUBWA YA MUNGU Septemba 4 Kabla haijazaliwa milima, wala hujaiumba dunia, Na tangu milele hata milele ndiwe Mungu. Zaburi 90:2. Baba yetu wa Mbinguni ametupatia ishara nyingi zinazoonyesha ukuu wake na utukufu wake. Jambo hilo ni hivyo hasa kwa kiwango cha kustaajabisha katika sehemu hizi za milima....* Mandhari mbalimbali katika milima hii mirefu sana na miinuko yake yenye miamba, makorongo ya milima hii yenye kina kirefu pamoja na vijito vyake vya maji vinavyokwenda kasi na kupiga kelele toka juu ya milima hii, ... maji yake yakipasuka yanapogonga miamba, na kutawanyika katika rasharasha kama mtandio, huifanya mandhari hiyo kuwa nzuri kupita kiasi na yenye utukufu ajabu.... Milima ina hazina zenye mibaraka ambayo Muumbaji amewapa wakazi wa dunia hii. Ni tofauti inayoonekana juu ya uso wa nchi, milimani, katika nyanda tambarare, na mabondeni, ambayo inafunua hekima na uweza wa huyo Mtendakazi Bingwa Mkuu. Na wale ambao wangetaka kuiondolea mbali kutoka katika dunia hii miamba hiyo na milima, makorongo yasiyokaliwa na watu pamoja na vijito vinavyopiga kelele viendavyo kasi, na magenge marefu ----- hao akili zao ... ni finyu mno kuweza kufahamu utukufu wa Mungu ulivyo. Mungu, Mjenzi Mkuu, ameijenga milima hii mirefu sana, ambayo mvuto wake juu ya hali ya hewa ni mbaraka kwa ulimwengu wetu. Inavuta kutoka mawinguni unyevu mwingi unaourutubisha udongo. Safu za milima ni mabwawa makubwa ya Mungu, yanayoipatia bahari maji yake. Hizo ndizo vyanzo vya chemchemi, vijito, na mito midogo ya maji baridi, pamoja na mito mikubwa. Zinapokea, kwa njia ya mvua na theluji, mvuke uliojaa hewani, na kuusafirisha kwenda chini kwenye nyanda kame, tambarare. Tungeiangalia milima hiyo isiyokuwa na umbo linganifu kama chemchemi za Mungu zenye mibaraka ambazo kutoka kwazo hububujika maji ya kukidhi mahitaji ya viumbe vyote vilivyo hai. Kila wakati ninapoitazama milima hiyo najisikia moyoni mwangu kujawa na shukrani kwa Mungu.... Kila kitu kinachotuzunguka hutufundisha sisi siku kwa siku mafundisho ya upendo wa Baba yetu na ya uweza wake, na ya Sheria zake zinazotawala viumbe vyake vya asili, ambazo ndizo msingi wa serikali zote mbinguni na duniani. ----- MS 62, 1886. _____________ * Iliandikwa Ulaya. HARUFU NZURI KATIKA KAZI YETU YA MAISHA Septemba 5 Na mavazi, ya nini kuyasumbukia? Fikirini maua ya mashamba, jinsi yameavyo; hayafanyi kazi, wala hayasokoti, nami nawaambia, ya kwamba hata Sulemani katika fahari yake yote hakuvikwa vizuri kama mojawapo la hayo. Mathayo 6:28,29. Msanii wetu Mkuu anayageuza mawazo yetu kuelekea kwenye maua ya mashamba yasiyokuwa na roho, akituonyesha rangi zake nzuri na aina mbalimbali za rangi ambazo ua moja linaweza kuwa nazo. Kwa njia hiyo, Mungu ametufunulia ustadi na utunzaji wake. Hivyo ndivyo ambavyo angelionyesha pendo lake alilo nalo kwa kila mwanadamu. ----- 5BC 1086. Bwana Muumbaji wetu anatumia uangalifu mkubwa, hekima, na muda wake juu ya ua dogo sana kama vile anavyotumia juu ya mambo yale makuu anayoyaumba. Katika maua yaliyo madogo sana huonekana uzuri na ukamilifu ambao hakuna sanaa ya kibinadamu yo yote iwezayo kuufuatisha. Pambo lile lenye mistari-mistari inayovutia sana la ua waridi ambalo limetiwa rangi, na nyota zile zilizoko mbinguni, huionyesha ile kalamu iliyochora ya Msanii huyo Mkuu. Maua mazuri sana... huonyesha faida ya kukua na kupevuka kwa akili na mwili wa kibinadamu kutokana na mafunzo au uzoefu wa kutenda kazi. Yanatufundisha kwamba ni haki yetu kujiendeleza. Mungu anatutaka sisi kuleta harufu nzuri katika kazi yetu ya maisha. Tunatakiwa kuwa mimea yake Bwana, kumtumikia kwa njia yo yote anayopenda yeye. Hebu na tufanye kila linalowezekana kuzifanya tabia zetu ziweze kupendeza.... Uangalifu mkuu unapaswa kutolewa kwa mimea hiyo myororo. Chipukizi ambazo hazina faida lazima ziondolewe. Sehemu zilizochubuliwa sharti zifungwe kwa uangalifu. Kwa hiyo wale walio dhaifu katika imani wanapaswa kuwa na matunzo ya kuwalea. Yatupasa kuwashirikisha wale walio dhaifu katika makusudi yetu yenye nguvu katika bustani ya Bwana, tukiwapa msaada unaohitajika. ----- MS 47, 1898. Kutokana na aina mbalimbali za mimea ambazo hazina mwisho, tunaweza kujifunza fundisho la maana. Chipukizi zote za maua hazifanani kwa umbo wala kwa rangi. Nyingine zina nguvu za kuponya magonjwa. Nyingine zinatoa harufu nzuri sikuzote. Kuna wale wanaojiita Wakristo ambao hudhani kwamba ni jukumu lao kumfanya kila Mkristo kuwa kama wao wenyewe walivyo. Huo ni mpango wa mwanadamu, sio mpango wa Mungu. Katika kanisa la Mungu kuna nafasi kwa tabia mbalimbali kama vile maua yalivyo katika bustani. Katika bustani yake ya kiroho kuna maua mengi ya aina mbalimbali. ----- Letter 95, 1902. Bwana ndiye anayeyatunza maua. Anayapa uzuri wake na harufu nzuri. Je! hatazidi sana kutupa sisi harufu nzuri ya tabia iliyo changamfu? ----- Letter 153, 1902. HEWA SAFI YA MAADILI Septemba 6 Ili upate kwenda katika njia ya watu wema, Na kuyashika mapito ya wenye haki. Mithali 2:20. Ili kuwa na mwili wenye afya, ni lazima damu izungukayo katika mishipa iwe safi; ili ipate kuwa safi ni lazima ipate hewa safi na chakula safi. Matumizi ya chakula kisichofaa na uvutaji wa hewa chafu huleta ugonjwa ambao hujitokeza katika hali mbalimbali. Usafi na ukamilifu wa maisha yetu ya kidini hutegemea sio tu juu ya kweli ile tunayoipokea, bali juu ya kundi lile tunaloongea nalo, na hewa ya maadili tunayoivuta. Imani, mabadiliko ya mwili na nguvu yake, kuwa na matumaini, kuwa na furaha, kuwa na mashaka na hofu, uvivu, upumbavu, wivu, kijicho, shuku, uchoyo, utukutu na kurudi nyuma, ni matokeo ya ushirikiano wa kirafiki tunaokuwa nao, kundi tunalotembea nalo, na hewa tunayovuta. Kushiriki katika urafiki mbaya kutakuwa na matokeo yake maovu.... Biblia inaweza kusomwa na maombi kutolewa, bila kuwa na ongezeko lo lote la afya ya kiroho, wala kukua kiroho, kwa kadiri ilivyo mbaya hewa ile tunayovuta.... Uangalifu mkubwa sana ungetumika na waumini kujiweka wenyewe katika uhusiano wa karibu sana na Mungu, tena pamoja na wale waliofunzwa na Mungu. Ni jambo linaloumiza sana kuwaona wale waliouamini ukweli wa leo wakiingia katika wavu wa Shetani.... Tunapaza sauti zetu na kupiga kelele kwa kila muumini wetu aliye katika ukweli wa leo: Ukitaka kuwa na afya ya kiroho, angalia mapafu yako. Angalia chakula chako cha kiroho unachokula. Kuza upendo wako kwa jamii ya wale walio safi na wema, kama unataka kuwa na Kristo aliyeumbika ndani yako kama uzima wa roho yako. Afya ya roho yako hutegemea kuvuta hewa ile nzuri ya maadili. ----- Letter 1, 1882. Kristo, Tabibu Mkuu, ameandika dawa ya kutumia kwa kila muumini. Yampasa kula chakula kile kitakachotolewa katika Neno la Mungu. Na imani ile itendayo kazi kwa upendo hutegemea sio tu juu ya chakula tulacho bali juu ya hewa tuvutayo. Tukifanya urafiki na wale walio waovu, tunavuta hewa iliyochafuliwa na malaria ya dhambi. Hakikisha kwamba kwa kufanya urafiki wako na wafuasi wa Yesu walio wapole na wanyenyekevu wa moyo, unavuta hewa safi, takatifu. ----- MS 60, 190l. UWE NA UWEZO WA KUCHAGUA! Septemba 7 Wala msishirikiane na matendo yasioyozaa ya giza, bali myakemee. Waefeso 5:11. Mkristo anapaswa kujitenga mbali na kundi la wale ambao ni kama mtego kwa roho yake. Unapokutana na wale usioweza kuwainua katika hali ile ya hewa iliyo safi na takatifu kwa sababu mwelekeo wao wa kimaadili umepotoka, itakupasa kuwaepuka usishirikiane nao. Watu wa tabaka hiyo kwa kawaida wana utashi wenye nguvu na tabia inayovutia, na yule adui wa Mungu anapowashughulikia, wanakuwa mawakala wake wanaofanikiwa sana katika kuziongoza roho za watu mbali na njia ile ya haki na kwenda katika njia zile za udanganyifu na za hatari. Hali ya hewa ya kimaadili inayowazunguka watu hao imetiwa waa la dhambi, nayo inaleta kwa wengine shinikizo la mvuto unaonajisi. ----- YI, Sept. 29, 1892. Marafiki zako unaoshirikiana nao hawawezi kutazamiwa kuwa huru mbali na upungufu mwingi katika tabia zao au dhambi. Lakini katika kuchagua marafiki zako, ungeweka kipimo chako juu sana kadiri unavyoweza. Namna ya maadili yako yalivyo hupimwa kwa aina ya marafiki unaowachagua. Epukana na kufanya urafiki wa karibu sana na wale ambao mfano wao usingechagua kuuiga.... Chagua kuwa marafiki zako wale ambao wanaiheshimu sana dini na kuyaweka katika matendo yao maongozi yake. Daima weka mbele yako maisha yale ya baadaye. Marafiki zako wasiondoe mawazo hayo moyoni mwako. Hakuna kitu kitakachofukuzilia mbali mawazo hayo ya maana kama kuongea na watu wa ovyo, yaani, wale wasioijali, wala kuipenda dini. Haidhuru wawe wamefikia kisomo cha juu jinsi gani, kama hawaiheshimu dini, au hawaijali, basi, hao wasingekuwa marafiki zako wateule. Kadiri tabia zao zinavyovutia kwa njia zingine, ndivyo kadiri ungeweza kuuogopa mvuto wao kama wenzi wako, kwa sababu wangekuzungushia mvuto wao usiokuwa wa kidini, wa kikafiri, yaani, usioheshimu mambo matakatifu, na hata hivyo wanaweza kuuchanganya na mambo yao mengi ya kuvutia kiasi kwamba itakuwa ni hatari kweli kwa maadili yako. --- -- Letter 17, 1878. Uwe shujaa kama Danieli. Uwe shujaa kusimama peke yako.... Ukimya unaoletwa na woga mbele ya marafiki zako waovu, wakati wewe unasikiliza hila zao, hukufanya wewe kuwa mmoja wao.... Uwe na ujasiri kutenda mema. ----- 3BC 1155. CHUNGA MAPENZI YAKO. Septemba 8 Msifungiwe nira pamoja na wasioamini, kwa jinsi isivyo sawasawa; kwa maana pana urafiki gani kati ya haki na uasi? Tena pana shirika gani kati ya nuru na giza? 2 Wakorintho 6:14. Ningependa kukuonya* ujilinde kuhusu ni wapi unayaweka mapenzi yako.... Kumbuka kwamba maisha yako ni mali yake Yesu, na ya kwamba haikupasi kuishi kwa ajili ya nafsi yako tu. Haikupasi kuingia katika uhusiano wa ndoa na mtu asiyekuwa muumini, maana kwa kufanya hivyo, unafanya kinyume kabisa na kile alichoagiza Yesu. Waepuke wale wasioyaheshimu mambo ya dini. Mwepuke yule apendaye kukaa kivivu; mwepuke yule anayeyadhihaki mambo matakatifu. Epuka kushirikiana na yule anayetumia lugha chafu, au mwenye mazoea ya kutumia hata gilasi moja tu ya kileo kikali. Usisikilize posa ya mtu ambaye hautambui wajibu wake kwa Mungu. Kweli safi, inayoitakasa nafsi, itakupa ujasiri wa kuzikata kamba zinazokufunga kwa mwenzi wako anayekupendeza sana ambaye unamjua kuwa hampendi wala hamchi Mungu, wala hajui cho chote juu ya kanuni za haki ile ya kweli. Sikuzote tunaweza kuvumilia udhaifu wa rafiki yetu na ujinga wake, bali maovu yake kamwe. Usiolewe kamwe na mtu asiyeamini. Mimi nanena kwako Neno la Mungu tu, maana yeye anasema kwa nguvu ya kwamba muungano kama huo utakuwa na matokeo ya kuuvuta moyo wako mbali hata usiweze kumpenda na kumtumikia [Mungu].... Wewe kama mtoto wa Mungu, unaruhusiwa kufanya mkataba wa ndoa katika Bwana tu.... Endapo utakubali kuunganisha maisha yako na ya yule asiyeamini, basi, utakuwa unalidharau neno la Mungu na kuihatarisha roho yako.... Maisha yako ni kitu cha thamani mno kuweza kuyafanya kana kwamba yana thamani kidogo sana. Kalvari inakushuhudia wewe juu ya thamani ya roho yako. ----- Letter 51, 1894. Hebu kila hatua unayochukua kuelekea kwenye muungano wa ndoa yako iwe ya staha, isiwe ya anasa, isiwe ya kujipamba kwa nje, iwe nyofu, kisha iwe na kusudi la dhati ili kumpendeza na kumheshimu Mungu. Ndoa inaathiri maisha ya baadaye katika ulimwengu huu na katika ulimwengu ule ujao. Mkristo mwaminifu hatafanya mipango yo yote ambayo Mungu hawezi kuikubali.... Mfanye Kristo kuwa mshauri wako. Jifunze neno lake kwa maombi. ----- MH 359. ----------------------- * Mashauri kwa mwanamke kijana. YAKUPASA KUCHAGUA KUNDI LAKO Septemba 9 Kwa hiyo, Tokeni kati yao, Mkatengwe nao, asema Bwana, Msiguse kitu kilicho kichafu, Nami nitawakaribisha. 2 Wakorintho 6:17. Mkristo wa kweli hatachagua kundi la wale ambao hawajaongoka. Iwapo Kristo ameumbika ndani, tumaini la utukufu, hatuwezi kufurahia hali ya hewa yenye malaria ya kiroho ambayo inazizunguka roho za wale wanaoipinga dini.... Marafiki zako wanaochukia kabisa mambo ya kiroho hawajatakaswa, hawajaadilishwa, wala hawajatukuzwa kwa kuiweka ile kweli katika vitendo. Hao hawako chini ya uongozi wake Kristo, bali chini ya bendera nyeusi ya mkuu yule wa giza. Kushirikiana na wale wasiomcha Mungu, wala kumpenda, isipokuwa kama unashirikiana nao kwa kusudi la kuwaongoa kwa Yesu, kutakuwa na matokeo mabaya kwa maisha yako ya kiroho. Kama huwezi kuwainua juu, basi, mvuto wao utaonekana juu yako kwa kuiharibu na kuitia waa imani yako. Ni vema kwako kuwatendea kwa upole; ila si vyema kwako kulipenda na kulichagua kundi lao, maana ukichagua hewa ile inayozizunguka roho zao, utapoteza urafiki wako na Yesu. Kwa njia zote zilizo katika uwezo wako jitahidi kuikomesha dhambi; walakini usiiruhusu dhambi hata kwa dakika moja kwa matendo yako, maneno yako, kimya chako, au kuwapo kwako. Kila wakati dhambi inaporuhusiwa na yule anayejidai kuwa ni mfuasi wake Kristo, utambuzi wake wa dhambi unadhoofika, na uamuzi wake kwa njia hiyo hupotolewa.... Bwana Yesu hawezi kumlinda mtu ye yote anayejiweka kwenye uwanja wa adui na kujizungushia marafiki wanaopendelea maongezi na tabia kama hiyo ambayo ni chukizo kwa Mungu anayemheshimu na kumpenda.... Ambatana kwa karibu sana na wale walio na mvuto unaoelekea kukuinua juu, ambao roho zao zimezungukwa na hali ya hewa iliyo safi na takatifu.... Mungu atakuwa karibu sana na moyo wako, zaidi hasa katika mawazo yako, kwa sababu umejitenga mbali na ulimwengu na mbali na mivuto ambayo ingekupeleka mbali na ile kweli, nawe hutaweza kuzingirwa sana na mitego ya Shetani. ----- Letter 51, 1894. RAFIKI KWA WALE WASIOKUWA NA RAFIKI Septemba 10 Marhamu na manukato huufurahisha moyo; Kadhalika utamu wa rafiki ya mtu utokao katika kusudi la moyo wake. Mithali 27:9. Ingetupasa sisi kuwa na upendo wa Kristo moyoni mwetu kwa kiwango kile ambacho kuwapenda wengine kutakuwa kwa haki na unyofu. Mapenzi yetu yangekuwa na upeo mpana, wala yasingewekwa tu kwa wachache wanaojipendekeza kwetu kwa kutuambia siri zao muhimu. Mwelekeo wa urafiki kama huo ni kutufanya tuwasahau wale walio na hitaji kubwa la kupendwa kuliko wale ambao mawazo yetu yanaelekea kwao. Tusingeifanya duara ya marafiki zetu kuwa ndogo kwa kuwaingiza wale walio wachache sana tunaowapenda sana kwa sababu wanatubembeleza na kujipendekeza kwetu kwa madai yao ya kutupenda. Kuwapendelea hao wachache kwa kuwapa na kupokea usikivu, hakuleti manufaa ya hali ile ya juu kwa wale ambao wangependa kumtumikia Mungu. Mmoja anapata nguvu yake kutoka kwa mwingine, kisha sifa, kujipendekeza na upendo anapokea kwa mwingine, mambo hayo huchukua nafasi ile ambayo ingejazwa na neema ya Mungu, na kwa njia hiyo marafiki wa kibinadamu huyaondoa mapenzi yetu kutoka kwa Kristo.... Wasiri wa kibinadamu, marafiki wa kibinadamu, huchukua upendo wote na matumaini yote ambayo angestahili kupewa Mungu peke yake.... Badala ya wewe mwenyewe kutaka upendwe sana, au kujipendekeza kwa mtu mmoja ambaye huenda anaheshimiwa sana, angalia iwapo hakuna mtoto maskini ye yote ambaye hapendwi, ambaye hakuna wema wo wote maalum unaoonyeshwa kwake, nawe mfanye huyo kuwa lengo la usikivu wako usio na ubinafsi. Wale ambao wanavutia hasa hawatakosa marafiki; ambapo wale ambao hawapendezi kabisa kwa mwonekano wao, ambao ni waoga na wagumu kufanya urafiki nao, wanaweza kuwa na sifa nzuri za tabia, hao nao wamenunuliwa kwa damu yake Kristo. ----- YI, Mei 25, 1893. Hisia zako za kuwa na wasiwasi, kutamani kurudi nyumbani, au upweke huenda zikawa kwa faida yako. Baba yako aliye mbinguni ana maana ya kukufundisha wewe ili uweze kupata ndani yake urafiki na upendo na faraja ambayo itakidhi matumaini na tamaa zako za dhati.... Usalama na furaha yako ya pekee ni katika kumfanya Kristo kuwa mshauri wako wa kudumu. Unaweza kuwa na furaha ndani yake kama hujawahi kuwa na rafiki mwingine ye yote katika ulimwengu huu mpana. ----- Letter 2b, 1874. MATENDO MEMA HUONGEZEKA KWA KUYAFANYIA MAZOEZI Septemba 11 Katika mambo yote ukijionyesha wewe mwenyewe kuwa kielelezo cha matendo mema, na katika mafundisho yako ukionyesha usahihi na ustahivu, na maneno yenye uzima yasiyoweza kuhukumiwa makosa, ili yule mwenye kupinga atahayarike, kwa kuwa hana neno baya la kunena juu yetu. Tito 2:7,8. Mkristo mwenye afya, anayeendelea kukua hatakuwa mpokeaji anayekaa tu bila kutenda lo lote akiwa miongoni mwa wenzake. Yampasa kutoa na vile vile kupokea. Matendo yetu mema huongezeka kwa kuyafanyia mazoezi. Jamii ya Kikristo itatupatia hewa safi ya kuvuta, na katika kuivuta kwetu hatuna budi kuwa na juhudi. Kazi ya Kikristo ifanyike, huruma zetu, kuwatia moyo wengine, na mafundisho vitolewe nasi kwa wale wanaohitaji, kujizuia, upendo, uvumilivu, na ustahimilivu ambavyo huhitajika, vikitumika katika kazi hii ya Kikristo, vitajenga ndani yetu wenyewe imani, utii, tumaini, na upendo kwa Mungu wetu.... Ni jambo la maana ili kuwa na musuli wa kiroho na nguvu kwamba roho iwe na mazoezi. Kazi inapaswa kufanywa kwa utendaji wa kiroho tukizitumia vizuri nafasi za kufanya mema.... Kadiri mtu anavyozidi kuwa mwaminifu katika kufanya kazi zake za Kikristo, ndivyo atakavyozidi kuwa mkamilifu.... Udhaifu na kutokuwa na msimamo wo wote havitatupatia kamwe heshima yo yote katika imani yetu ya Kikristo. Haiwezekani kuwafikia watu kule waliko na kuwainua juu isipokuwa kama tumaini fulani limeamshwa ndani yao kwa njia ya uaminifu na utauwa wako. Huwezi kamwe kuwafikia kwa kushuka chini ya jukwaa hilo la kweli na matengenezo, isipokuwa kwa kuwaleta wengine juu ya jukwaa hilo ambalo Neno la Mungu limekuandalia wewe. Iwapo watu wale wanaoipinga imani yetu wanaona kwamba ninyi mnaoikiri hamna utani, yaani, mko imara, wala hamna tabia mbaya kwa nyakati zote na chini ya hali zote, na ya kwamba mnakaa ndani ya Kristo, Mzabibu hai, na ya kwamba ninyi ni wafuasi wa ile kweli na wafanya matengenezo msioyumba, hapo ndipo mtakapoakisi roho na tabia ile ya Kristo. Katika biashara zenu, katika ushirikiano wenu na waumini pamoja na wale wasio waumini, katika patakatifu [kanisani], nyumbani mwenu, na kila mahali, hapo ndipo mtakapoonyesha mvuto wa upendo wake Mwokozi, ambao utawatawala waumini. Kipaji, talanta, na fedha sio vya muhimu ili kuweza kuwa na mvuto huo; lakini jambo la maana ni kwamba wewe ukae ndani yake Kristo, maana kwa njia hiyo matunda yako yatakuwa ya haki. ----- Letter 1, 1882. JIPATIENI UMASHUHURI WENU ULIMWENGUNI Septemba 12 Mtu awaye yote asiudharau ujana wako, bali uwe kielelezo kwao waaminio, katika usemi na mwenendo; na katika upendo na imani na usafi. 1 Timotheo 4:12. Katika kipindi kile cha utoto na ujana ----- ni mambo mangapi yamefungwa [yamesitirika] katika miaka hiyo ya majaribio! Mungu anawataka kukitumia vizuri kipindi hicho, enyi wapendwa vijana, kwa kujipatia siha ya kufanya kazi. Iwapo mnahitaji elimu, basi, fanyeni kazi ninyi wenyewe na kudhamiria kuipata. Msingoje nafasi ijitokeze yenyewe; tafuteni nafasi kwa ajili yenu wenyewe. Ishikilieni nafasi yo yote iliyo ndogo ambayo inajitokeza mbele yenu. Iweni wakamilifu na waaminifu katika jambo lo lote mnalolishika, haidhuru liwe dogo sana jinsi gani. Baadhi ya vijana wetu hawana msimamo kiasi cha wao wenyewe kuweza kushindwa kufanikiwa katika jambo lo lote lile wanalofanya; kipindi cha maisha yao mara nyingi huwa kimetumika nusu yake kabla hawajakata shauri lo lote kuwa watafanya kazi gani, ama watakuwa nani. Wanazifukia talanta zao chini ya takataka nyingi. Kwa hao mimi ningesema hivi, Jizoezeni kutumia vizuri fedha na vitu mlivyo navyo. Msitumie mapato yenu kwa kujiendekeza katika tamaa ya chakula na vinywaji, wala kwa kutafuta anasa zenu. Jipatieni umashuhuri ulimwenguni. Mbele yenu wekeni lengo la kuwa watu wenye manufaa na watenda kazi hodari kama vile Mungu anavyowaitia. Mtakapozidi kujiendeleza katika maarifa mnayopata, mtaweza kupata maarifa mengi zaidi. Kujishughulisha kusoma vitabu vyenu na kufanya kazi za mikono zinazofaa, pamoja na kujitoa wakf kwa moyo na utiifu wenu kwa Mungu, mambo hayo yatawafanya ninyi kuwa wanaume na wanawake kwa maana ile ya juu sana. Kujitoa wakf kwa Mungu kweli kweli, pamoja na kujifunza sayansi mbalimbali, kutawapa vijana elimu ile itakayowafanya kuwa waungwana, wanaompenda Mungu kwa unyenyekevu, waliojaa fadhili nyingi na matunda mazuri, pasipokuwa na upendeleo, wala pasipokuwa na unafiki. Watu kama hao, watoao harufu nzuri ya upendo wao kwa Mungu na kwa wanadamu wenzao, wanaweza kutumiwa na Mungu kama vyombo vyake vya heshima. -- --- YI, Juni 24, 1897. Wapendwa vijana, Yesu alikufa sio kwa ajili ya kuwaokoa ninyi pamoja na dhambi zenu, bali kutoka katika dhambi zenu. Anawataka ninyi kukifuata kielelezo alichokiweka mbele yenu ----- kujikana nafsi, kujitwika msalaba wenu kila siku, na kumfuata. Anawadai mpate kumpa huduma yenu, mapenzi ya mioyo yenu yaliyo bora na matakatifu sana. Kama mtakwenda katika njia ile ya utii kwa mapenzi yake, mkijifunza kwa uchangamfu na kwa bidii mafundisho ya maongozi ya Mungu, basi, baada ya kupita siku nyingi ataweza kuwaambia, "Mwanangu, panda juu zaidi kuja huku kwenye makao haya ya mbinguni ambayo nimekuandalia wewe." ----- YI, Julai 15, 1897. UWANJA WA MAFUNZO WA NYUMBANI Septemba 13 Uniendeshe katika mapito ya maagizo yako [amri zako], Kwa maana nimependezwa nayo. Zaburi 119:35. Wanadamu wamefundisha kwamba sheria ya Mungu imefutiliwa mbali. Kama hivyo ndivyo mambo yangekuwa, basi, tusingekuwa na kipimo cha tabia, wala tusingekuwa na kitu cho chote cha kutuonyesha madai ya Mungu ya haki juu yetu. Tungekuwa tunaelea juu ya bahari kubwa ya mashaka, na kukosa mwongozo katika kuyashughulikia majukumu mazito ya uhusiano wetu wa kifamilia. Lakini ni katika uhusiano wetu huo wa kifamilia ambamo tunapata mafunzo ya kutusaidia kuweza kushughulika na wanadamu wenzetu kwa jumla. Endapo Mungu asingekuwa na sheria yo yote ambayo kwayo angeweza kuwatawala wanadamu wenye akili, basi, asingekuwa na cho chote ambacho kingeonyeshwa kama kielelezo cha tabia yake ambacho wanadamu wangeweza kukifuatisha katika kuzijenga tabia zao, je! watoto wetu wangepata picha gani ya kuwaonyesha kile kinachoyafanya maisha yetu kuwa maadilifu [manyofu] na kuonyesha ulivyo ukamilifu wa tabia?... Amri ya tano inawaagiza watoto kuwatii wazazi wao, na wazazi wanatakiwa kuwasaidia watoto wao kuishika amri hii kwa kufanya sehemu yao wakishirikiana na Mungu kwa kuwataka wawe na utii tangu utoto wao mpaka ujana wao. Wazazi wenyewe wanapaswa kuwa chini ya utawala wa Mungu. Inawapasa kuonyesha sifa za tabia zile za thamani, wakitoa kielelezo mbele ya watoto wao, wakionyesha uvumilivu na ustahimilivu na kuzichanganya tabia hizo na msimamo wao thabiti, na kwa njia hiyo kuwafundisha watoto wao kumtii Baba yao aliye mbinguni.... Shetani anafurahi kuona familia zisizokuwa na utaratibu na familia zinazotawaliwa vibaya, maana mafanikio yake yanategemea sana udhibiti wake juu ya familia za ulimwengu huu.... Amedhamiria kwamba kanuni ile ya haki [Amri Kumi] haitakuwa sheria ya kufuatwa katika kuzijenga tabia zao.... Amri Kumi zinatoka kwa Mungu wa mbinguni, ambaye moyo wake umejaa upendo, ambaye hekima yake haina kikomo, ambaye kamwe hafanyi makosa. Ana hekima nyingi mno kiasi kwamba hawezi kufanya makosa, ni mwema mno hata hawezi kumdhuru mtu awaye yote ambaye atayatii matakwa yake. Baraka itaambatana na wale wanaotii na wale wanaoisimamia [wanaoitetea] sheria ya Yehova.... Furaha na amani ya wazazi na watoto katika maisha haya, na manufaa yao makubwa, yatapatikana kwa kwenda katika njia ya amri zake, maana kwa kufanya hivyo watakuwa na amani na Mungu yule wa mbinguni. - ---- Letter 34, 1894. WAFUNDISHENI CHIMBUKO LA FURAHA YA KWELI Septemba 14 Mlee mtoto katika njia impasayo, Naye hataiacha, hata atakapokuwa mzee. Mithali 22:6. Wazazi wengi kwa kuacha kwao kujizoeza kujitawala wenyewe kama inavyostahili, wanawakosesha furaha watoto wao sana. Vijana wale wanaoachiliwa huru kutafuta anasa zao daima katika burudani au kwa kujifurahisha nafsi zao wenyewe hawana furaha kamwe wanapoendelea kuifuata njia hiyo. Akina baba na akina mama, wafundisheni watoto wenu ya kwamba njia pekee ya kuwa na furaha ya kweli kweli ni kumpenda na kumcha Mungu; nanyi imarisheni fundisho hilo kwa kuonyesha mfano wenu wenyewe. Hebu na waone kwamba amani ya Kristo inatawala mioyoni mwenu, na ya kwamba upendo wake umejaa katika maisha yenu. ----- ST, Jan. 7, 1889. Je, ninyi wenyewe mtaitoa wakf kwa Mungu mioyo yenu, ili mpate kuwa na mvuto wenye nguvu, utakasao, juu ya watoto wenu? Je, mtawatenga mbali na dhambi na mbali na wenye dhambi, na kwa imani iliyo hai kuwaunganisha na Mungu? Ingekuwa kazi ya kila mzazi kuendeleza yale yote yaliyo mema, na ya kweli, na yaliyo bora ndani ya watoto wake. Ni jukumu lake kuyasahihisha makosa yao, yaani, kuwazuia wasiwe watukutu.... Lifanye Neno la Mungu kuwa mwongozo wako katika elimu ya watoto wako, daima ukiwa unafikiria mambo gani yatakayokuwa na manufaa kwao kwa baadaye.... Mama anaweza kuwapa binti zake elimu itakayokuwa ya thamani, kwa kuwafundisha kufanya sehemu yao katika kubeba mizigo ya familia. Baba anaweza kuwapa wanawe raslimali iliyo ya thamani kuliko dhahabu au mashamba, kwa kuwafundisha kupenda kufanya kazi zenye manufaa, badala ya wao kutafuta furaha yao katika burudani zao za kivivu au katika ubadhirifu. Enyi wazazi, sasa ndio wakati wa kujenga mazoea ya kuwa na bidii ya kazi, kujitegemea, na kujitawala ndani ya watoto wenu; kujizoeza kutumia vitu kwa uangalifu [kubana matumizi] na kutumia busara katika kuendesha vizuri biashara. Sasa ndio wakati wa kuwafundisha kuwa na adabu na ukarimu kwa wanadamu wenzao, na kumheshimu na kumpenda Mungu.... Nyumbani pangekuwa ni mahali palipo na uchangamfu mwingi sana pamoja na mvuto katika dunia hii; napo panaweza kufanywa kuwa hivyo kwa kutumia maneno mazuri na matendo mema, na, chini ya yote hayo, unyofu katika kuyashikilia mambo yaliyo mema.... Hebu na tusikizuie kitu cho chote kwake Yeye aliyetoa uzima wake wa thamani kwa ajili yetu. Akina baba na mama, waleteni kwake watoto wenu, katika ubichi na kuchanua kwa ujana wao, na kuwatoa wakf kwa kazi yake. ----- ST, Jan. 7, 1889. UTII N I SIFA YA LAZIMA NA MUHIMU YA UKUU Septemba 15 Enyi watoto, watiini wazazi wenu katika Bwana, maana hii ndiyo haki. Waefeso 6:1. Yesu ametupa kielelezo kamili kwa hali ile ya utoto na ujana. Jifunzeni Kielelezo chetu hicho, yaani, Kristo Yesu, na kukiiga kama mnataka kufanana naye ----- kuwa safi, watakatifu, bila dhambi, na pasipo uchafu wo wote. Jifunzeni maisha ya utoto wake Kristo. Yeye alikuwa Mwana wa Mungu, hata hivyo kumbukumbu ya Biblia inatueleza kwamba alirudi nyumbani kwao kutoka Yerusalemu, naye akawatii wazazi wake.... Yesu, Mkombozi wa ulimwengu, alifanya kama alivyoambiwa hata kama kazi ile ilikuwa haipendezi kulingana na hisia zake. Utii ni sifa ya ukuu wa kweli. Hakuna mtu ye yote awezaye kuwa mwema na mkuu ambaye hajajifunza kuwa mwepesi wa kutii.... Unapojaribiwa kufuata njia yako mwenyewe na kupingana na matakwa ya wazazi wako, sema, "Hapana; Yesu alikuwa mtiifu kwa wazazi wake." Omba msaada kwa Yesu, ajuaye majaribu yanayomjia kila mtoto, kila kijana, kwa maana yeye mwenyewe amejaribiwa. naye anaujua udhaifu wako wote, naye atakusaidia upate kuushinda.... Jitahidi kuwaletea manufaa wengine, kuwasaidia wazazi wako, kuwa mwangalifu na mwenye kuwafikiria wengine. Unaweza kuwasaidia kwa njia mbalimbali kadhaa.... Kufanya lile unalopaswa kufanya kwa moyo wa uchangamfu, kwa hatua ya haraka, uso wako ukiwa unang'aa kwa furaha kwa kuwa unaweza kufanya kitu fulani kwa ajili ya wazazi wako ili kuwapunguzia mzigo wao, kutakufanya wewe kuwa mbaraka nyumbani mwenu.... Kazi ndogo hizo zote zikifanywa kwa uaminifu huingizwa katika leja ile ya mbinguni.... Mungu hatafanya kosa lo lote; ataingiza kitabuni kwa usahihi kazi zako zote za maisha yako zilizofanywa kwa ajili ya utukufu wake. Kwa hiyo, usikunje uso wako [unapozifanya], bali uwe na uso mchangamfu sikuzote, wenye furaha, uwe mwepesi wa kusaidia, sikio lako liwe jepesi kusikiliza matakwa ya watu, na moyo wako uwe tayari kutii, na kuwa mwepesi kuona huruma kwa wale wanaohitaji msaada wako.... Kumbukeni kwamba tabia zenu bado hazijakamilika; mnajenga tabia zenu kwa kupanda juu siku kwa siku. Fumeni katika tabia zenu upole wote, utii, kuwafikiria wengine, kufanya kazi kwa bidii, pamoja na upendo kwa kadiri mwezavyo. Zifanyeni [tabia zenu] kuwa kama kilivyo kielelezo cha tabia ya Mungu. Jifunzeni ninyi wenyewe ya kwamba mnaweza kuwa na pambo lile la roho ya upole na utulivu, ambalo lina thamani kuu mbele za Mungu. Mnaweza kuifanya dunia yenu kuwa nzuri zaidi kwa kuishi kwenu ndani yake endapo ninyi mtafanya tu kila mnaloweza. ----- Letter 17, 1883. HEKALU TAKATIFU LA MWILI Septemba 16 Au hamjui ya kuwa mwili wenu ni hekalu la Roho Mtakatifu aliye ndani yenu, mliyepewa na Mungu? Wala ninyi si mali yenu wenyewe; maana mlinunuliwa kwa thamani. Sasa basi, mtukuzeni Mungu katika miili yenu, [na katika roho zenu, ambavyo ni vya Mungu]. 1 Wakorintho 6:19,20 [KJV]. Tabia takatifu anayoitaka Bwana ni ile ya kumtayarisha mtu mzima kuwa hekalu la kukaa Roho Mtakatifu ndani yake. Mungu hatakubali huduma yo yote iliyo pungufu ambayo haimhusishi mwanadamu mzima. Haitoshi kuzitumia sehemu fulani fulani tu za mashine yetu hii [mwili] iliyo hai. Sehemu zote ni lazima zifanye kazi yake kwa kupatana kikamilifu, la sivyo, huduma yake itakuwa na upungufu. Ni kwa njia hiyo mwanadamu anapata sifa za kushirikiana na Mungu katika kumwakilisha Kristo kwa ulimwengu. Hivyo Mungu anataka kuwatayarisha watu kusimama mbele zake wakiwa safi na watakatifu, ili apate kuwaingiza katika jamii ile ya malaika wa mbinguni. ----- RH, Nov. 12, 1901. Tumepewa amana ya ujumbe mzito mno ambao haujapata kutolewa katika ulimwengu wetu, na lengo linalopaswa kuwekwa wazi na kubainishwa mioyoni mwetu ni ule utukufu wa Mungu. Hebu na tujihadhari tusifanye kitu cho chote kitakachodhoofisha afya yetu ya mwili, akili, au roho, kwa maana Mungu hatakubali kafara yo yote iliyooza, yenye magonjwa, na iliyo najisi. Uangalifu ni lazima utumike katika kula, kunywa, kuvaa mavazi, na kufanya kazi, tusije tukakengeuka na kutoka katika utendaji wetu bora na kushindwa kufanya kazi yetu tukufu sana kwa njia iliyo bora kabisa, ili matokeo ya kazi yetu yapate kudumu milele. Ni wajibu wetu kuufunza na kuudhibiti mwili wetu ili tupate kumfanyia Bwana wetu kazi ya hali ya juu sana kwa kadiri iwezekanavyo. Matakwa yetu yasitutawale sisi. Hatupaswi kuubembeleza uchu wetu mbaya wa chakula, wala kujiendekeza kutumia kile kisichokuwa kwa manufaa yetu, ati kwa kuwa kinakidhi tu ladha yetu; wala hatutakiwi kujaribu kuishi kwa mpango ule wa kushinda na njaa, tukiwa na wazo kwamba tutakuwa na mwelekeo mzuri wa kiroho, na kwamba Mungu atatukuzwa. Yatupasa kutumia akili aliyotupa Mungu ili tupate kuwa wakamilifu katika mwili, roho, na nafsi, ili tuwe na tabia yenye ulinganifu, akili safi, tena tupate kufanya kazi kamilifu kwa ajili yake Bwana. ----- MS 60, 1894. Hekalu takatifu la mwili sharti litunzwe katika hali ya usafi, bila kuwa na uchafu wo wote, ili Roho Mtakatifu apate kukaa humo. ----- Letter 103, 1897. ADHABU YA HAKIKA INAYOLETWA NA ULAFI Septemba 17 Kama mtu akiliharibu hekalu la Mungu, Mungu atamharibu mtu huyo. Kwa maana hekalu la Mungu ni takatifu, ambalo ndilo ninyi. 1 Wakorintho 3:17. Ukamilifu wa tabia hauwezi kufikiwa kama sheria za maumbile yetu zinapuuzwa; kwa maana tendo hilo ni kuivunja Sheria ya Mungu. Sheria yake imeandikwa kwa kidole chake mwenyewe juu ya kila neva, kila musuli, kila nyama ya mwili wetu, na juu ya kila uwezo aliokabidhiwa mwanadamu ambao umo mwilini mwake. Vipawa hivi vimetolewa, si kwa ajili ya kuvitumia vibaya, wala kuviharibu, bali ili vipate kutumika kwa ajili ya heshima na utukufu wake katika kuwainua wanadamu.... Uhusiano uliopo kati ya akili na mwili ni wa karibu sana: kimoja kikiathirika, basi, takriban sikuzote kile kingine kinaathirika pia. Ni vigumu kabisa kwa wanadamu, walio chini ya uwezo wa dhambi, na mazoea yale yanayoharibu afya ya mwili, kuweza kuzithamini zile kweli takatifu. Akili inapotiwa giza, nguvu za kimaadili hudhoofika, na dhambi haionekani kuwa ni dhambi. Mafundisho adhimu, na makuu ya Neno la Mungu yanayomfanya mtu kuwa mwungwana yanaonekana kana kwamba ni hadithi za uongo. Hapo ndipo Shetani anaweza kuidaka kwa urahisi ile mbegu njema iliyopandwa moyoni; kwa kuwa moyo wake haumo katika hali ya kuweza kuifahamu na kuijua thamani yake halisi. Hivyo ndivyo mazoea yale ya kujifurahisha nafsi, yanayoathiri afya, yanavyopingana na mvuto wa ujumbe ule uliokusudiwa kuwatayarisha watu kwa siku ile kuu ya Mungu. Tunaishi katika saa ya kutisha sana inayoambatana na mambo ya ibada ya dini katika historia ya ulimwengu huu. Hakuna hata mtu mmoja ambaye maisha yake ni ya kujidhalilisha ovyo kwa njia ya kuzivunja sheria zile za maumbile yake, ambaye ataweza kusimama katika siku ya kujaribiwa ambayo i karibu sana kutujilia mbele yetu. Kuna hesabu ya kutisha inayotakiwa kutolewa kwa Mungu na wale ambao hawaujali sana mwili wao wa kibinadamu, yaani, wale wanaoutendea kwa ukatili.... Dini ya kweli na Sheria za Afya huenda bega kwa bega. ----- RH, Nov. 12, 1901. Kuacha kidogo tu kuwa na msimamo mkali sana chini ya hali yo yote ile kwa sababu tu ni usumbufu kwetu, kutaifanya dhamiri yetu kuwa ngumu na kutayarisha njia kwa uvunjaji wa majukumu ya kimaadili kwa njia nyinginezo. Kama tunaishughulikia afya ya mwili wetu, ambayo ndiyo shauku yetu kuu, pasipo kufikiria ipasavyo, basi, tunajiandalia njia kwa majaribu na kuvunja madai [ya Mungu] ya juu zaidi. ----- Letter 29a, 1875. NURU YA MATENGENEZO YA AFYA Septemba 18 Mpenzi naomba ufanikiwe katika mambo yote na kuwa na afya yako, kama vile roho yako ifanikiwavyo. 3 Yohana 2. Nuru aliyotoa Mungu juu ya Matengenezo ya Afya ni kwa wokovu wetu na wokovu wa ulimwengu. Wanaume na wanawake wangejulishwa juu ya makao haya ya kibinadamu [mwili wetu], yaliyojengwa na Muumbaji wetu kama maskani yake, ambayo anatutaka sisi kuwa mawakili wake waaminifu.... Miili yetu imeumbwa kwa ajabu, na Mungu anatutaka sisi tuitunze vizuri. Wote wanawajibika kwake kulitunza jengo hili la kibinadamu katika hali nzuri ya afya na siha, ili kila musuli, kila kiungo, kipate kutumika katika kazi ya Mungu.... Mungu, aliyeliumba jengo hilo la ajabu la mwili, atalitunza kwa uangalifu wa pekee ili liwe katika hali yake nzuri, kama wanadamu watashirikiana naye, badala ya kupingana na makusudi yake. Kweli hizi kuu ni lazima zitolewe kwa ulimwengu. Yatupasa kuwafikia watu pale pale walipo, na kwa mfano wa maadili yetu kuwaongoza kuuona uzuri wa njia hii bora. Ulimwengu una haja ya kusikitisha ya kukosa kupata mafundisho katika mambo haya. Wakati umewadia ambapo kila mtu anapaswa kuwa imara na mkweli katika kila mwonzi wa nuru ambayo Mungu ametoa, na kuanza kwa dhati kufundisha injili hii ya afya kwa watu. Tutakuwa na nguvu na uwezo wa kufanya hivyo iwapo sisi wenyewe tunajizoeza kuishi kulingana na kweli hizo katika maisha yetu.... Wale wanaoifurahia mibaraka ya thamani inayowajia kwa njia ya kuutii ujumbe huu wa rehema watafanya yote yaliyo katika uwezo wao ili wengine nao wapate kushiriki mibaraka iyo hiyo. Lakini tukae tukiwa na hakika kwamba Shetani atafanya yote yaliyo katika uwezo wake kuzuia kitu cho chote kinachofanana na ujumbe huo wa matengenezo ili usipate kutolewa kwa ulimwengu kwa wakati huu. Je! watu wa Mungu wataonekana upande wa yule adui, kwa kushindwa kuutii wao wenyewe, ama kwa kupuuzia kuutoa kwa wengine? "Mtu asiye pamoja nami yu kinyume changu; na mtu asiyekusanya pamoja nami hutapanya." Mathayo 12:30. Iwapo tungetaka kuwa salama, basi, hatupaswi kushindwa kujua tunasimama upande wa nani. ----- RH, Nov. 12, 190l. Mungu anawataka wachukuzi wake wa nuru kuweka mbele yao daima kanuni hiyo ya juu. Kwa njia ya maadili yao na mfano wao wanapaswa kuishikilia juu kanuni hiyo kamilifu kuliko kanuni ile ya uongo ya Shetani. ----- RH, Nov. 12, 190l. WATU WALIOFANYWA KUWA WAKAMILIFU Septemba 19 Basi, mlapo, au mnywapo, au mtendapo neno lo lote, fanyeni yote kwa utukufu wa Mungu. 1 Wakorintho 10:31. Tukiwa na jicho safi kwa ajili ya utukufu wa Mungu, tungefikiria kwa uangalifu suala hili la kula na kunywa kwetu. Tunahitaji uongozi wake Mungu, hata katika tabia zetu za kawaida sana za maisha yetu ya kila siku, ili pasiwe na uvujaji wo wote mdogo ambao utakula mapato yetu isivyopasa, ati kwa ajili tu ya kukidhi uchu wetu wa chakula uliopotoka. Katika Agano Jipya hakuna hata moja katika matakwa ya Mungu ambalo limepoteza nguvu yake ya kuwafunga watu, wala kulegeza hata kidogo utekelezaji wa wajibu wake.... Badala ya matakwa ya Mungu kulegezwa katika Agano Jipya, msimamo unakazwa kwa karibu zaidi. Mtume anasema, "Mtendapo neno lo lote," hata katika suala hili la kula na kunywa, "fanyeni yote kwa utukufu wa Mungu." Swali linaweza kuulizwa, "Je, siwezi kufanya ninalotaka na mwili wangu? Je, mwili wangu sio mali yangu?" Unaweza kufuata njia yako mwenyewe, bali itakuwa kwa hasara ya roho yako, au unaweza kufuata njia ya Mungu na kuishi kwa kusudi maalum katika ulimwengu huu, na katika ulimwengu ule ujao kupata uzima wa milele. ----- MS 60, 1894. Wale waliokwisha kupokea mafundisho haya kuhusu ubaya wa kutumia nyama, chai, na kahawa, pamoja na maandalizi ya chakula kilichokolezwa sana [kwa viungo], ambayo hayafai kiafya, ambao wamedhamiria kufanya agano na Mungu wao kwa kujitoa mhanga wao wenyewe, hawataendelea kujifurahisha katika uchu wao wa chakula kwa kula chakula kile wakijuacho kuwa hakifai kwa afya. Mungu anataka kwamba uchu wetu wa chakula upate kutakaswa, na kwamba kujikana nafsi kwetu katika vitu vile visivyokuwa vizuri kuonekane katika matendo yetu. Hii ni kazi ipaswayo kufanywa kabla watu wake hawajaweza kusimama mbele zake wakiwa ni watu waliofanywa kuwa wakamilifu.... Wale wanaodai kwamba wanayaamini mafundisho haya ya matengenezo ya afya, lakini bado wanakwenda kinyume na kanuni zake katika mazoea yao ya kila siku, wanajidhuru nafsi zao wenyewe na kuacha nyuma yao mvuto mbaya juu ya mioyo ya waumini na wale wasiokuwa waumini. ----- 9T 153,l54. Usitumie vibaya au kuharibu sehemu yo yote ya nguvu zile ulizopewa na Mungu, ziwe za kimwili, kiakili, au kimaadili. Mazoea yako yote yanapaswa kuwekwa chini ya utawala wa akili yako ambayo yenyewe iko chini ya utawala wa Mungu. ----- Letter 103, 1897. THAWABU YA MAZOEA YA KUWA NA KIASI Septemba 20 Lakini Danieli aliazimu moyoni mwake ya kuwa hatajitia unajisi kwa chakula cha mfalme, wala kwa divai aliyokunywa; basi akamwomba yule mkuu wa matowashi ampe ruhusa asijitie unajisi. Danieli 1:8. Maandiko haya yaliyovuviwa yameandika historia ya Danieli na rafiki zake kama kielelezo kinachong'aa kwa ajili ya vijana wa vizazi vyote vilivyofuata.... Wale wanaotaka kuzihifadhi nguvu zao bila kuziharibu kwa ajili ya kazi ya Mungu ni lazima wazingatie sana kuwa na kiasi katika kutumia mibaraka yake yote, pamoja na kujizuia kabisa kukidhi tamaa yo yote iletayo madhara au tamaa mbaya ya mwili inayomvunjia mtu hadhi yake. Vijana wanazungukwa na vishawishi vingi vilivyolengwa kwenye uchu wao wa chakula.... Wale ambao, kama Danieli, wanakataa kujinajisi wenyewe, watavuna thawabu ya mazoea yao ya kuwa na kiasi. Wakiwa wanazo nguvu zao nyingi sana za ushupavu wa mwili na ongezeko la nguvu za kustahimili, watakuwa na akiba yao [ya nguvu] katika benki ambayo wanaweza kuichota wakati wa shida. Mazoea sahihi ya mwili hukuza sana ubora wa akili. Nguvu za akili, nguvu za mwili, na maisha marefu, hutegemea sheria hizo zisizobadilika. Katika jambo hili afya haiwezi kutokea vivi hivi tu, wala kwa nasibu. Nguvu zile za juu zaidi [Mbingu] hazitaingilia kati ili kuwalinda wanadamu wasipatwe na matokeo ya kuzivunja Sheria za maumbile yao. --- -- ST, Machi 2, 1882. Swali kwa kila kijana... lingekuwa hili, Je, nifuate matakwa yangu, na kujiendekeza katika uchu wangu wa chakula, au, je, nifuate msukumo wa dhamiri yangu, na kukiweka kichwa changu safi na kuhifadhi nguvu zangu za mwili kwa kujinyima kila zoea ambalo lingeniletea udhaifu? Je, niwe mateka wa desturi za ulimwengu huu,... au je, nijitenge na kila desturi inayonishusha hadhi yangu kutokana na athari zake? Je, nisimheshimu Mungu kuliko kuupendeza ulimwengu?... Danieli na wenzake walitambua kwamba kanuni ile ilikuwa katika hatari ya kuvunjwa, na kwamba wasingeweza kumudu kufanya mapatano na yule mjaribu. Nuru na kweli zilizoangaza kutoka kwenye kiti kile cha enzi cha Mungu zilikuwa za thamani sana kwao kuliko heshima yo yote ambayo watu wangeweza kuwapa. Ni nafasi nzuri kwa vijana wa leo kuwa imara na wakweli, kuwa wanyenyekevu na kufanikiwa, kama vile walivyofanikiwa wale vijana wa Kiyahudi katika ufalme ule wa Babeli.... Mungu alimheshimu Danieli, naye atamheshimu kila kijana anayefuata njia ile aliyokwenda Danieli kwa kumheshimu Mungu. YI, Okt. 25, 1894. AKILI TIMAMU KATIKA MWILI WENYE AFYA Septemba 21 Bali nautesa mwili wangu na kuutumikisha; isiwe, nikiisha kuwahubiri wengine, mwenyewe niwe mtu wa kukataliwa. 1 Wakorintho 9:27. Kitu cho chote kinachopunguza nguvu za mwili huidhoofisha nguvu ya akili. Kwa hiyo, kila zoea linaloathiri afya ya mwili lingeepukwa kabisa.... Hatuwezi kudumisha kujitoa kwetu wakf kwa Mungu, na wakati uo huo kuendelea kuiathiri afya yetu kwa kuwa na mazoea mabaya. Kujikana nafsi ni mojawapo ya masharti, sio tu ya kuingilia katika kazi ya Kristo, bali kuweza kudumu katika hiyo. Lakini ni wangapi wanaojidai kuwa Wakristo ambao hawako tayari kujizoeza kujikana nafsi zao, hata kama ni kwa ajili yake Kristo. Ni mara ngapi upendo wao kwa anasa fulani yenye kuleta madhara mwilini mwao una nguvu nyingi kuliko tamaa yao ya kuwa na akili timamu katika mwili wenye afya! Saa za thamani za muda wao wa majaribio zinatumika [vibaya], mali waliyopewa na Mungu inatapanywa ovyo ili kulifurahisha jicho lao au kukidhi uchu wao wa chakula.... Hakuna aliye na haja ya kushindwa katika ulimwengu huu wa kujikana nafsi. Mungu atampa msaada kila mtafutaji mwenye bidii.... Iwapo kwa unyofu wa moyo tunautafuta uso wake, basi, maisha yetu yatalingana na imani yetu tunayoikiri.... Yeye anajua kama mioyo yetu imetolewa wakf kabisa katika kazi yake, au imetolewa kwa mambo ya ulimwengu huu. Tunaweza kukiri cho chote tuwezacho, lakini maisha yetu yasipolingana na imani yetu, basi, imani yetu imekufa. Kanuni iliyotolewa na mtume Paulo ndiyo njia ya pekee iliyo salama ya kutuongoza katika mambo yote ya maisha yetu. "Basi, mlapo, au mnywapo, au mtendapo neno lo lote, fanyeni yote kwa utukufu wa Mungu." 1 Wakorintho 10:31. Katika kuchagua chakula chetu, tusingetafuta tu kuifurahisha ladha yetu; bali tungechagua kile ambacho hutuletea afya nyingi sana mwilini. Kwa upande wa mavazi, tungetafuta yale yasiyokuwa na mapambo, yenye kuleta raha yanapovaliwa, yanayokaa vizuri mwilini, na yale yanayofaa. ----- RH, Juni 15, 1886. Yule atakayefuata hali ya kawaida katika mazoea yake yote, akijizuia katika uchu wake wa chakula na kuzidhibiti tamaa zake za mwili, anaweza kuuhifadhi uwezo wake wa akili upate kuwa na nguvu yake, wepesi wake wa kutenda, siha yake, na wepesi wake wa kupambanua kila kitu kinachohitaji kufikiriwa au kutendwa, utambuzi wake mkali kubainisha kile kilicho kitakatifu na kile kisicho kitakatifu, naye atakuwa tayari kuingia katika shughuli zo zote za biashara kwa utukufu wa Mungu na kwa manufaa ya mwanadamu. ----- 2BC 1006. TOFAUTI KATIKA MAVAZI Septemba 22 Vivyo hivyo wanawake na wajipambe kwa mavazi ya kujisitiri, pamoja na adabu nzuri, na moyo wa kiasi; si kwa kusuka nywele, wala kwa dhahabu na lulu, wala kwa nguo za thamani; bali kwa matendo mema, kama iwapasavyo wanawake wanaoukiri uchaji wa Mungu. 1 Timotheo 2:9,10. Wana wa Israeli... waliagizwa kuweka utepe wa kibuluu usiokuwa na mapambo katika upindo wa mavazi yao ili kuwatofautisha na mataifa yaliyowazunguka, na kuwa ishara ya kuonyesha kwamba wao walikuwa watu wa Mungu wa pekee. [Angalia Hesabu 15:38,39.] Watu wa Mungu wa siku hizi hawatakiwi kuwa na alama maalum ya kuwekwa juu ya mavazi yao. Bali katika agano Jipya mara kwa mara tunarudishwa nyuma kwa Israeli ya kale kuwa ndicho kielelezo chetu. Iwapo Mungu aliwapa maagizo dhahiri kama hayo watu wake wale wa kale kuhusu mavazi yao, je! mavazi ya watu wake wa kizazi hiki hataweza kuyaangalia? Je! isingekuwapo tofauti yo yote katika mavazi yao na yale ya walimwengu? Je! watu wa Mungu ambao ni hazina yake ya pekee, wasitafute kumtukuza Mungu hata kwa mavazi yao? Nao, je! wasingekuwa kielelezo katika suala hili la mavazi, na kwa njia ya mtindo wao ulio rahisi kuweza kukemea kiburi, ubatili, na ubadhirifu wa wale wanaokiri kuzipenda anasa za ulimwengu huu? Mungu anawataka watu wake kufanya hivyo. Kiburi kinakemewa katika Neno lake. ----- 1BC 1114. Yatupasa kumjua Yesu na upendo wake kuliko mitindo ya ulimwengu huu. Katika jina la Bwana wangu, nawasihi vijana wapate kujifunza kwa kufuata kielelezo cha Kristo. Mnapotaka kutengeneza kitu cho chote, mnaangalia kiolezo chake kwa makini, ili mpate kutoa kitu kama kile kile kwa kadiri iwezekanavyo. Anzeni sasa kufanya kazi kwa kumwiga yule aliye Kielelezo cha Mbinguni.... Hamwezi kufanana na Yesu, na wakati uo huo kuwa na kiburi mioyoni mwenu.... Dhahabu au lulu au mavazi ya thamani, hivyo vyote vina thamani ndogo sana ukivilinganisha na upole na uzuri wake Kristo. Uzuri wa kuzaliwa nao una ulinganifu wake, au uwiano mzuri wa sehemu zake za mwili, kila moja kwa nyingine; lakini uzuri ule wa kiroho una mlandano wa umoja au kufanana kwa roho zetu na Yesu. Jambo hilo litamfanya yule aliye nao kuwa wa thamani sana kuliko dhahabu safi, au hata kuliko ile kabari ya dhahabu ya Ofiri. Neema yake Kristo kwa kweli ni pambo la thamani mno. Inamwinua juu na kumfanya mwungwana yule aliye nayo, na kuiakisi miali ile ya utukufu juu ya wengine, na kuwavuta nao pia kwa yule aliye Chimbuko la nuru na baraka. ----- RH, Des. 6, 1881. UZURI UNAOVUTIA WA KUTOKUWA NA MAPAMBO Septemba 23 Maana kila kilichomo duniani, yaani, tamaa ya mwili, na tamaa ya macho, na kiburi cha uzima, havitokani na Baba, bali vyatokana na dunia. 1 Yohana 2:16. Kiburi cha mavazi si jambo dogo, bali ni uovu mkuu. Kinasababisha muda, mawazo, na fedha kutumika kwa kuupamba mwili, na muda wa kuyakuza matendo yale ya mbinguni yaliyo mema unapuuzwa. Saa za thamani ambazo Mwokozi wetu ametuonya tuzitumie kwa maombi na kujifunza Maandiko hutolewa kwa maandalizi ya mavazi yasiyokuwa ya lazima kwa ajili ya maonyesho ya nje. ----- RH, Machi 20, 1958. Shetani anasimama nyuma yao, akiendelea kubuni mitindo inayowaongoza watu kwenye ubadhirifu katika matumizi ya mapato yao. Katika kutengeneza mitindo ya kisasa, ana kusudi lake maalum. Anajua ya kwamba muda na fedha itakayotumika kukidhi matakwa ya mtindo huo haitatumika kwa makusudi yale ya juu zaidi, yaani, matakatifu zaidi. Muda wa thamani unapotezwa ili kwenda na wakati na mitindo ile inayobadilikabadilika daima na isiyoweza kukidhi haja kabisa. Mara tu mtindo mmoja unapoingizwa, mitindo mingine mipya hubuniwa, na tena, ili watu hao wa mitindo ya kisasa wapate kuendelea kubaki katika mitindo hiyo, mavazi yao hayana budi kutengenezwa upya kulingana na mitindo hiyo mipya. Hivyo ndivyo wale wanaojidai kuwa Wakristo, yaani, wenye mioyo iliyogawanyika, wanavyoutumia vibaya muda wao, wakiupa ulimwengu karibu nguvu zao zote.... Uchaguzi sahihi wa mavazi usidharauliwe wala usilaumiwe.... Hakuna faida yo yote kujaribu kuokoa fedha kwa kununua vitambaa vya nguo vilivyo duni. Hebu nguo na ziwe pasipo mapambo na ziwe nadhifu, bila kuwa na ubadhirifu wo wote, wala kujionyesha. Mabibi vijana wanaojinasua kutoka katika utumwa wa mitindo hiyo watakuwa mapambo wao wenyewe katika jamii yao. Yule ambaye anavaa mavazi yasiyokuwa na mapambo, wala hajidai kwa mavazi yake, wala kwa mwenendo wake, anaonyesha ya kwamba anajua ya kuwa bibi wa kweli thamani yake inajulikana kwa maadili yake mema. Inapendeza jinsi gani, inavutia jinsi gani kuyaona mavazi yale yasiyokuwa na mapambo, ambayo kwa uzuri wake yanafananishwa na maua yale ya kondeni!... Wale wanaojizoeza kuvaa mavazi yasiyokuwa na mapambo wanao muda wa kuwatembelea wagonjwa, tena wanakuwa wamejiandaa vizuri sana kuweza kuomba pamoja nao na kuwaombea. Juu ya kila Mkristo mwanaume na mwanamke linakaa jukumu zito la kurekebisha na kubana matumizi yake binafsi, ili kwa kufanya hivyo waweze kuwasaidia maskini, kuwalisha wenye njaa, na kuwavika nguo walio uchi. ----- RH, Machi 20, 1958. DALILI YA KUWA MWANAMKE WA HESHIMA Septemba 24 Kujipamba kwenu, kusiwe kujipamba kwa nje, yaani, kusuka nywele; na kujitia dhahabu, na kuvalia mavazi; bali kuwe utu wa moyoni usioonekana, katika mapambo yasiyoharibika; yaani, roho ya upole na utulivu, iliyo ya thamani kuu mbele za Mungu. 1 Petro 3:3,4. Wanaopenda mitindo wanaweza kujidai kwamba wao ni wafuasi wake Kristo, lakini mavazi yao na mazungumzo yao huonyesha kile kiujazacho moyo wao na kuyashika mapenzi yao. Mwonekano wa nje ni kielezo cha moyo ulivyo ndani. Uungwana wa kweli hautoshelezwi kwa kuupamba mwili kwa ajili ya kujionyesha. Mwanamke wa heshima, anayemcha Mungu, atavaa mavazi ya kujisitiri. Mavazi yasiyokuwa na mapambo yanamfanya mwanamke mwenye akili kuonekana vizuri sana. Moyo ule uliostaarabika na kuelimika, utajidhihirisha katika uchaguzi wa mavazi yasiyokuwa na mapambo na yale yanayofaa. Katika moyo ule uliotakaswa hakuna nafasi kwa mawazo ya mapambo yasiyohitajika. ----- CTBH 93. Kuna pambo moja ambalo halitatoweka kamwe, ambalo litakuza furaha ya wote watuzungukao katika maisha haya, na litakalong'aa kwa mng'ao usio na utusitusi katika umilele ule ujao. Ni pambo hilo la roho ya upole na unyenyekevu. Mungu ametuagiza sisi kulivaa vazi hilo la thamani kuu rohoni mwetu. ----- 4T 643. Pambo hilo la ndani la roho ya upole na utulivu lina thamani kuu mno. Katika maisha ya Mkristo wa kweli pambo lake la nje sikuzote hupatana na amani na utakatifu uliomo ndani [ya moyo wake].... Kujikana nafsi na kujitoa mhanga vitakuwa ndiyo ishara ya maisha ya Mkristo. Ushahidi unaodhihirisha kwamba uchaguzi umeongoka utaonekana katika mavazi ya wote wanaopita katika njia ile inayokwenda juu kwa ajili ya waliokombolewa na Bwana. Ni sawa kupenda uzuri na kuutamani; bali Mungu anapenda sisi tupende na kutafuta kwanza uzuri ule wa juu mno, yaani, ule usioharibika kamwe. Hakuna pambo lo lote la nje litakalolingana kwa thamani na uzuri wake kama ile "roho ya upole na utulivu," ile "kitani nzuri, nyeupe na safi" (Ufunuo 19:14), ambayo watakatifu wote wa duniani wataivaa. Vazi hilo litawafanya wawe wazuri na wanaopendwa sana hapa, na baadaye itakuwa kitambulisho chao cha kuingilia katika jumba lile la Mfalme. Ahadi yake ni hii, "Nao watakwenda pamoja nami hali wamevaa mavazi meupe, kwa kuwa wamestahili." Ufunuo 3:4. ----- AA 523, 524. UZURI WA KUFANANA NA KRISTO Septemba 25 Bali wauonyeshe uaminifu mwema wote, wayapambe mafundisho ya Mwokozi wetu Mungu katika mambo yote. Tito 2:10. Kila mmoja anayelitaja jina la Kristo anatakiwa kuyapamba mafundisho ya Kristo Mwokozi wetu kwa maisha mazuri na mwenendo wake wa utauwa, hata kwa roho ile ya upole na utulivu.... Ukiwa nayo utapendwa na Mungu na wanadamu. Maneno yale yaliyosemwa kwa harara yanaziumiza na kuzijeruhi roho za watu, na jeraha lenye kina kirefu sana huonekana ndani ya moyo wa msemaji. Kipawa cha Kristo, yaani, pambo lile la roho ya upole na utulivu, hutangazwa kwa mamlaka na yule asiyeweza kufanya kosa kwamba ni cha thamani kuu. Kila mmoja wetu anatakiwa kuiona thamani yake yeye mwenyewe kwa kukitafuta kutoka kwa Mungu. Si kitu kama watu watatutathmini kwa njia gani, kama sisi tutalivaa pambo hilo, tutakuwa tumechukua alama ya uanafunzi wetu pamoja na Kristo. Tunapewa heshima na yule Aliye juu; kwa maana pambo lile tunalolivaa machoni pake ni la thamani kuu. Kito hicho cha thamani ni lazima kukitafuta.... Kwa kila mtu yatakuja mambo ya kukasirisha, ya kuchochea hasira, na endapo wewe huko chini ya uongozi kamili wa Mungu, basi, utakasirika mambo hayo yatakapokujia. Lakini upole ule wa Kristo unatuliza roho ile iliyochafuka, unautawala ulimi, na kuuleta mwili wote chini ya mamlaka ya Mungu. Hivyo ndivyo tunavyojifunza kustahimili lawama zinazotoka kwa wengine. Tutaeleweka vibaya, bali pambo hilo la thamani la roho ya upole na utulivu linatufundisha sisi namna ya kustahimili, namna ya kuwasikitikia wale wanaotamka maneno kwa harara, bila kutumia busara. Roho yo yote mbaya inayoonyeshwa ni hakika itamwamsha Shetani wa hasira kali katika mioyo ile isiyolindwa. Hasira isiyokuwa takatifu haina haja ya kuimarishwa, bali kudhibitiwa. Ni cheche itakayoiwasha moto tabia ile ya asili ya kinyama. Epuka kusema maneno yatakayochochea ugomvi. Afadhali uteseke vibaya kuliko kufanya vibaya. Mungu anataka kila mmoja wa wafuasi wake, kwa kadiri inavyowezekana, apate kuishi kwa amani na watu wote.... Yatupasa kufanana na Kristo. Hebu na tujitahidi kuyafanya maisha yetu kuwa kama vile Kristo anavyokusudia yawe, yakiwa yamejaa harufu nzuri ya upendo kwa Mungu na upendo kwa wanadamu wenzetu, yakiwa yamejaa Roho Mtakatifu wa Kristo, yakiwa yamejaa shauku ya kupata ule utakatifu toka kwa Mungu, yakiwa yamejaa utajiri wa uzuri kwa kufanana na Kristo. ----- Letter 117, 1899. MACHO YALIYOWEKWA WAKF Septemba 26 Moyo wa mwenye ufahamu hutafuta maarifa; Bali kinywa cha wapumbavu hula upumbavu. Mithali 15:14. Wengi hawatafuti kwa bidii kuyajua mafundisho yanayopatikana katika Neno la Mungu. Wanaiweka kando Biblia, na kuiacha mioyo yao kujishughulisha sana na usomaji duni unaopatikana katika vitabu vya hadithi za uongo [novels], magazeti, na magazeti ya kila mwezi. ----- MS 146, 1903. Mazoea mabaya ya kusoma hadithi hizo ni mojawapo ya njia zinazotumiwa na Shetani kuziangamiza roho nyingi za watu. Moyo unaojishughulisha na hadithi hizo zinazosisimua hupoteza utamu wote wa kusoma mambo magumu.... Ninafahamu mifano mingi ya kusikitisha ya matokeo mabaya ya mazoea haya maovu.... Kadiri walivyokuwa na hamu ya kuonja aina hii ya chakula cha kiakili, ndivyo kadiri walivyozidi kutaka. Fikra zao daima zinatamani sana kichocheo kile zilichokizoea, kama vile mlevi anavyotamani sana mvinyo wake au tumbako yake. Nguvu zao za akili na maadili hudhoofika na kupotolewa. Walipoteza hamu yao katika Maandiko na utamu wa maombi; nao kwa kweli walikuwa wameangamizwa kiakili na kiroho, kama vile alivyo mnywaji wa kileo au yule aliyebobea katika kuvuta tumbako. Wasomaji wa riwaya [hadithi za kubuni zinazosisimua] ni walevi wa kiakili; nao wanahitaji kutia sahihi zao katika ahadi ya kujizuia kabisa kusoma [mambo kama hayo] kama vile alivyo yule mhanga wa aina nyingine yo yote wa utovu wa kiasi. ----- ST, Mei 19, 1887. Mungu amewapa watu wake mambo mazuri sana ya kusoma. Hebu Neno la Mungu na lipate nafasi katika kila chumba ndani ya nyumba zetu. Iweke Biblia, mkate wa uzima, mahali pa wazi inapoweza kuonekana.... Daima tunza vitabu vilivyochaguliwa vizuri, yaani, vile vyenye kuwainua kiroho, mbele ya watu wa familia yako. ----- ML 89. Usomaji wa Neno la Mungu hauzisisimui fikra zetu, wala kuzichochea tamaa zetu za mwili, kama zilivyo hadithi zile za kubuni za uongo katika kitabu kile cha hadithi [novel], bali unaulainisha na kuutuliza moyo wetu, na kuyaadilisha na kuyatakasa mapenzi yetu. ----- Undated MS 93. Ni haki yao vijana kuweza kusema, "Bwana amenipa macho na masikio kwa ajili ya utukufu wake. Nitayaziba masikio yangu kwa mambo yale ya kipumbavu na ya ovyo. Nitasoma Neno lile litakaloweza kunitayarisha kuwa na mahali pangu katika makao yale anayoyaandaa Kristo kwa ajili ya wale walioitakasa mioyo yao kwa kuitii ile kweli. Sauti yangu itatangaza utukufu wa Mungu; kila nguvu ya mwili wangu itatolewa wakf kwa Mungu. ----- Letter 288, 1908. JIHADHARINI NA KILE MSOMACHO Septemba 27 Kwa kuwa BWANA huwapa watu hekima; Kinywani mwake hutoka maarifa na ufahamu; Huwawekea wanyofu akiba ya hekima kamili; Yeye ni ngao kwao waendao kwa ukamilifu. Mithali 2:6,7. Kizazi baada ya kizazi udadisi wa wanadamu umewaongoza kuutafuta mti ule wa maarifa; na mara nyingi wanadhani kwamba wanachuma tunda la maana sana, ambapo, kama Sulemani katika utafiti wake, wanaliona kuwa ni ubatili mtupu na si kitu ukilinganisha na ile sayansi ya utakatifu wa kweli. ----- YI, Okt. 27, 1898. Vitabu vile vilivyoandikwa kwa kalamu za makafiri visingepata nafasi yo yote ya kuwekwa katika maktaba za wale wanaopenda kumtumikia Mungu. Vitafaa sana kuwa vitu vya kuwashia moto kwenye jiko lako kuliko kuwa chakula cha akili yako. Vitabu hivyo vya makafiri vimekuwa chanzo cha maangamizi kwa roho nyingi. Watu wamejifunza vitabu hivyo vilivyovuviwa na Shetani, nao wamechanganyikiwa kabisa kuhusu kweli ni nini. Shetani anasimama kando ya yule anayekifungua kitabu hicho cha kikafiri, naye ataufunza moyo ule unaosoma kwa makini maandiko kama hayo, na kuiduwaza roho yake hata iwe karibu sana kutoweza kuvunjilia mbali kupumbazwa kwake huko. Hebu muumini ye yote asijitape mwenyewe kuwa mlima wake uko imara, na ya kwamba hataweza kuondoshwa kamwe kutoka katika mahali pake aliposimama katika imani yake. ----- YI, Nov. 23, 1893. Tumezungukwa na hali ya kutoamini. Hewa yenyewe hasa inaonekana kujazwa na hali hiyo; na ni kwa juhudi ya kudumu tu tunaweza kuipinga nguvu yake. Wale wanaouthamini wokovu wa roho zao wangeyaepuka maandiko hayo ya makafiri kama vile wanavyouepuka ukoma. Kwa vijana mimi ningesema hivi, Jihadharini na kile msomacho. Kwa kadiri mawazo yenu yanavyoelekezwa katika njia ile mbaya ya usomaji ule usiofaa, haitawezekana kwenu kuifanya kweli ya Mungu kuwa somo lenu la kudumu la kutafakari. Kama palipata kuwapo na wakati ambapo ujuzi wa Maandiko ulikuwa na maana kuliko wakati mwingine wo wote ni sasa. Nawasihi wazee kwa vijana, Ifanyeni Biblia kuwa kitabu chenu cha mafundisho. Humo mtakipata kipimo sahihi cha tabia. ----- ST, Mei 19, 1887. Msitumie talanta yenu ya thamani ya kuona kwa kusoma kile ambacho... hakitawaletea ninyi faida yo yote.... Nguvu zenu za akili na roho na mwili zinapaswa kutakaswa kwa ajili ya Bwana Yesu, ambaye amewanunua kwa damu yake. ----- Letter 339, 1905. JE! NI MAKAPI AU NGANO? Septemba 28 Mwanangu, sikiliza maneno yangu; Tega sikio lako, uzisikie kauli zangu. Zisiondoke machoni pako; Uzihifadhi ndani ya moyo wako. Maana ni uhai kwa wale wazipatao, Na afya ya mwili wao wote. Mithali 4:20-22. Nuru na kweli vinaweza kupatikana kwa wote,... bali wasipoiweka mioyo yao katika kulichunguza Neno la Mungu, basi, Shetani atawajaza mioyo yao na makapi, asiache nafasi yo yote kwa ile mbegu ya kweli kuweza kukua.... Tumezungukwa na majaribu yaliyojificha kiasi kwamba yanatushawishi na wakati uo huo yanautia uchafu na kuuharibu moyo wetu. ----- RH, Nov. 9, 1886. Vijana wa miji yetu wanaivuta hewa yenye uvundo, chafu, ya uhalifu.... Wanafunzwa uhalifu kwa kusoma hadithi zinazojaa katika vitabu vile vinavyopendwa na watu wengi siku hizi. Wakiwa hawajali mema kwa kuwa ni mema, wanapozisoma hadithi za wizi, mauaji, na kila aina ya uhalifu, wanaongozwa kubuni mipango ambayo kwayo wanaweza kuzikuza zaidi mbinu hizo za wahalifu, na kukwepa kugunduliwa. Kwa njia hiyo vitabu hivyo vichafu husaidia katika kuyakamilisha mafunzo ya vijana katika njia ile inayokwenda kwenye uharibifu. ----- MS 13, 1895. Ni dhambi kubwa kuyaleta magazeti hayo yaliyojaa upuuzi katika familia zetu, na hata hivyo wazazi wengi wamelala usingizi wasiweze kuiona hatari hiyo kubwa. Hawajui ni chakula gani kinatolewa kwa fikra za watoto wao. Chakula kile kinachotolewa kwa fikra zao kinatakiwa kiwe safi na kiweze kuleta afya. Mungu anawaagiza watu wake kugeuka na kuiacha mito ile ya bondeni yenye maji ya chumvi-chumvi, na kunywa maji kutoka katika mito safi ya Lebanoni. Kujifunza Neno la Mungu, ambalo ni uzima wa milele kwa yule anayelipokea, kungezitia nguvu na kuziimarisha akili zake; lakini mara nyingi mno neema ya Kristo hukuta njia ile njema imezuiwa na lundo kubwa la takataka ambalo limeachwa kulundikana moyoni. Moyo hauwekwi katika hali ya kuona njaa ya Neno takatifu la Mungu, ambalo halina budi kuliwa ili mawazo yapate kuwa safi na matakatifu.... Kwa wale wanaojaribiwa sana kujifurahisha katika kusoma maandiko yale ya kipuuzi ningewaambia hivi, Someni Biblia zenu. "Mwayachunguza [Chunguzeni] Maandiko," Kristo aliagiza; "kwa sababu mnadhani kwamba ninyi mna uzima wa milele ndani yake; na hayo ndiyo yanayonishuhudia mimi." Yohana 5:39. Utii kwa Neno la Mungu ndio usalama wetu wa pekee. ----- MS 53, 1911. KUTEMBEA NA YESU KATIKA ULIMWENGU ULIOHARIBIKA Septemba 29 Henoko akaenda pamoja na Mungu, naye akatoweka, maana Mungu alimtwaa. Mwanzo 5:24. Maisha na tabia ya Henoko, ambayo ilikuwa takatifu sana kiasi kwamba alinyakuliwa kwenda mbinguni pasipo kuonja mauti, huwakilisha maisha na tabia za wote zinavyotakiwa kuwa, iwapo, kama Henoko, wanapaswa kunyakuliwa na Kristo hapo atakapokuja. Maisha yake yalikuwa ni maisha ambayo kila mmoja wetu angeweza kuishi iwapo anajiunganisha kwa karibu sana na Mungu. Ingetupasa kukumbuka kwamba Henoko alizungukwa na mivuto iliyopotoka mno hata Mungu akalazimika kuleta gharika ya maji juu ya uso wa dunia na kuwaangamiza wakazi wake kwa ufisadi wao.... Kristo atakapokuja, miili yetu hii ya dhambi itabidilishwa, na kufanana na mwili wake wa utukufu; lakini tabia ya dhambi [ambayo watu wengi wanayo] haitafanywa kuwa takatifu wakati ule. Mabadiliko katika tabia zetu ni lazima yatokee kabla ya kuja kwake. Tabia zetu hazina budi kuwa safi na takatifu; yatupasa kuwa na nia ya Kristo, ili kwa furaha apate kuiona sura yake ikiakisiwa rohoni mwetu.... Yusufu alitunza unyofu wake alipozungukwa na waabudu sanamu katika nchi ile ya Misri, katikati ya dhambi na makufuru na mivuto mibaya inayoharibu tabia. Alipojaribiwa kuiacha njia ile njema, jibu lake likawa hivi, "Nifanyeje ubaya huu mkubwa nikamkose Mungu?" Mwanzo 39:9. Henoko, Yusufu, na Danieli waliitegemea nguvu ile iliyotoka kwa Mungu. Hii ndiyo njia peke yake iliyo salama kwa Wakristo kuifuata katika siku hizi zetu. Maisha ya watu hao mashuhuri yalifichwa pamoja na Kristo katika Mungu. Walikuwa watiifu kwa Mungu katikati ya ukafiri, walikuwa safi katikati ya upotovu, wacha Mungu wenye bidii, walipokutana na ukafiri na ibada ya sanamu. Kwa imani walijipatia sifa zile tu za tabia zinazofaa kwa ajili ya kukuza tabia zile zilizo safi na takatifu. Hivyo ndivyo inavyoweza kuwa kwetu sisi; haidhuru tuwe na cheo gani, haidhuru mazingira yetu yawe ya kuchukiza au kuvutia jinsi gani, imani yetu inaweza kupanda juu ya yote hayo na kumpata Roho Mtakatifu. Roho ile ile waliyokuwa nayo wakina Henoko, Yusufu, na Danieli, tunaweza kuwa nayo. Tunaweza kupata nguvu zetu kutoka kwenye chimbuko lile lile moja, na kupokea uwezo ule ule wa kujitawala nafsi zetu; na matendo yale yale yanaweza kuangaza katika maisha yetu. ----- RH, Sept. 1, 1885. VIJANA WANAPASWA KUMTETEA KRISTO Septemba 30 Kwa sababu kila atakayenionea haya mimi na maneno yangu, Mwana wa Adamu atamwonea haya mtu huyo atakapokuja katika utukufu wake na wa Baba na wa malaika watakatifu. Luka 9:26. Sikuzote umtetee Kristo. Kwa maneno, kwa roho, na kwa matendo yako, uwe shahidi wake. Anakupenda, naye anataka kukupa wewe neema yake nyingi, ili nawe upate kuwapa wengine.... Kristo amekununua kwa damu yake mwenyewe. Basi kila mahali, nyakati zote na chini ya hali zote, umtetee Yesu. Kumbuka kwamba kwa njia hiyo utakuwa na mvuto wenye nguvu nyingi sana juu ya wote unaoshirikiana nao.... Ni haki yako kukua katika neema daima, ukizidi sana katika kumjua na kumpenda Mungu, endapo wewe utahifadhi umoja wako na Kristo, basi, hapo itakuwa ni haki yako kuifurahia. Kwa imani ya kawaida inayonyenyekea mwombe Bwana aufungue ufahamu wako, ili upate kutambua na kuyathamini mambo yale ya thamani yaliyo katika Neno lake. Hivyo unaweza kukua katika neema, kukua ukiwa na imani ya kawaida, inayomtumainia yeye. Ndipo nuru yako itakapoangaza kwa wote unaoshirikiana nao. Moyo wako uukaze umwelekee Mwokozi.... Uwe na hakika kwamba maisha yako ya kiroho hayawi duni, dhaifu, yasiyo na ufanisi wo wote. Wako wengi wanaohitaji maneno na kielelezo cha Mkristo. Udhaifu na kusitasita huchokoza mashambulio ya yule adui, na ye yote yule anayeshindwa kukua kiroho, katika ujuzi wa ile kweli na haki, mara kwa mara atashindwa na yule adui. ----- Letter 36, 190l. Uso wako na uakisi tabia ya Bwana. Zungumza juu ya fadhili zake na simulia juu ya uweza wake. Hapo ndipo nuru yako itakapozidi kuangaza kwa wazi zaidi na zaidi. Juu ya maonjo yako na kukata tamaa kwako yataonekana maisha yako ya kidini yaliyo safi na yenye afya. ----- Letter 121, 1904. Hakuna kikomo cha mvuto wa mjumbe yule wa kibinadamu anayeivaa nira ile pamoja na Kristo. Kila siku anajifunza maisha ya Kristo na kuyafananisha maisha yake kulingana na kielelezo hicho cha mbinguni.... Ni kwa kuonekana roho ile ya Kristo katika maneno na matendo yetu ulimwengu unajua ya kuwa sisi tumekuwa pamoja na Yesu, ya kuwa sisi tu watoto wa Mungu. Tabia halisi ya dini yetu inapatikana... katika roho ya tulivu, ya upole, na amani tunayoionyesha. ----- Letter 34, 1894.USIIACHE ROHO YAKO IFE KWA NJAA! Oktoba 1 Na shughuli za dunia, na udanganyifu wa mali, na tamaa za mambo mengine zikiingia, hulisonga lile neno, likawa halizai. Marko 4:19. Yatupasa kuwa macho tusije tukalemewa na mizigo mizito hata kama inaonekana kuwa ni ile ya masumbufu muhimu ya maisha, kiasi cha kutufanya sisi tusiweze kufanya kazi ile iliyo ya maana sana.... Sehemu kubwa ya mawazo yetu na shughuli nyingi zinazotumia mikono na mioyo yetu, huwa juu ya mambo yetu ya uchoyo, ubinafsi, na ulimwengu huu. Mambo hayo hutuvutia mno kiasi cha kuyafanya mawazo yetu yasiyaangalie mambo yale ya milele. Roho inaachwa ife kwa njaa kwa kukosa lishe. Ubongo na mwili huchakaa kwa kutumia saa nyingi sana katika mambo ya ulimwengu huu. Hivyo ndivyo hasa Shetani alivyokusudia mambo yawe. Afya na nguvu yote ya ubongo, mawazo yote makali [mepesi kuelewa], hutolewa kwa shughuli za ulimwengu huu, na Mungu hupewa mawazo duni, yaliyotawanyika, hayo ndiyo matokeo ya ubongo uliochoka na kusumbuka. Mambo yale yaliyo na matokeo makubwa sana, yahusuyo amani ile ya milele yanagandamizwa chini ya mambo yale ya kawaida ya maisha haya, na Mungu ananyang'anywa kila siku huduma ile ambayo ingeweza kuyaimarisha maisha yetu ya kiroho, na kuyainua mawazo yetu juu mbinguni, na kumleta mtu katika umoja na Mungu pamoja na malaika wale watakatifu. ----- Letter 23a, 1892. Hatutakiwi kuyaruhusu mambo ya ulimwengu huu kuyachota mawazo yetu yote kiasi cha kuushughulisha sana ubongo na mwili wetu. Kwa ajili hiyo, wale wanaotuzunguka hunyimwa kusikia maneno yetu ya upole na matendo yetu mema ambayo yangewasaidia katika njia ile iendayo juu. Njia ya kupitishia nuru hiyo huzibwa na mambo ya ulimwengu huu. Neema ambayo Kristo anatamani kutupa, hawezi kutupa. Kwa wengi nguvu ile ambayo wangeweza kuwapa wengine huzidi kupungua, kwa sababu hawapokei uwezo wao kutoka kwenye Chimbuko lile la uwezo wote. Mungu anawasihi hao kujitenga mbali na mambo yale yanayokula nguvu ya ubongo wao na kuyaharibu maisha yao ya kidini. ----- Letter 181, 1904. Wote wanasongwa na masumbufu ya maisha haya ambayo yanahitaji ufumbuzi wa haraka, pamoja na mizigo, na majukumu mbalimbali; lakini kadiri shinikizo linavyozidi kuwa kubwa juu yako, ndivyo mizigo yako inavyozidi kuwa mizito ambayo unalazimika kuibeba, na haja yako ndivyo kadiri inavyozidi kuwa kubwa hata kukufanya utake msaada wake Mungu. Yesu atakuwa msaidizi wako. Daima unahitaji nuru ile ya uzima ili ipate kukuangazia katika njia yako, hapo ndipo mionzi yake ya kimbingu itakapowaangazia wengine. ----- MS 59, 1897. FUNGU LILILO JEMA Oktoba 2 Bwana akajibu akamwambia, Martha, Martha, unasumbuka na kufadhaika kwa ajili ya vitu vingi; lakini kinatakiwa kitu kimoja tu; na Mariamu amelichagua fungu lililo jema, ambalo hataondolewa. Luka 10:41,42. Onyo hilo la Kristo linakuja kwa akina Martha wengi wa siku zetu. Wanapoteza maarifa mengi ya kiroho pamoja na utakatifu, mambo ambayo yangewafanya kupata hekima ile itakayowapatia wokovu, kwa njia ya pilikapilika zao wakitaka kufanya mambo mengi sana katika kushughulikia mambo ya ulimwengu huu, kwa madhumuni ya kuwamiminia fadhili zao wale wawapendao. Iwapo wangehifadhi hali ile ya kawaida katika maandalizi yao yote, na kuzitumia vizuri nafasi zao za thamani ili kujipatia maarifa bora yatakayowawezesha kuyajua mapenzi yake Mungu na kuwa watendaji wa maneno yake, basi, wangejiepusha na harara, nao wangekunywa maji ya Chemchemi ile ya uzima idumuyo milele.... Martha... alihangaika sana kumpa Kristo heshima yote aliyostahili kwa kushughulika sana na maandalizi ya chakula, kiasi kwamba alipoteza saa za thamani zinazofaa sana kusikiliza mafundisho yale yaliyotoka katika kinywa chake kitukufu. Mariamu aliketi miguuni pake kulidaka kila neno. Aliona jambo hilo kuwa ni la maana sana. Kitendo hicho kikamchukiza Martha, naye akamwuliza Bwana Yesu iwapo yeye hakuona vibaya kwamba awe anatumika peke yake, wakati Mariamu alikuwa anakwepa majukumu hayo. Yesu akamwambia Martha, Mariamu amelichagua fungu lililo jema, ambalo hataondolewa. Fungu hilo jema lilikuwa ni kitu gani? Ni kujifunza kwa Yesu, yaani, kuyathamini maneno yake. Kule kuyasikiliza maneno yale yaliyotoka kinywani mwake, alikuwa anaonyesha upendo wake kwa Mwokozi wake.... Kila neno lililotoka kinywani mwake Yesu lilikuwa la thamani kwake. Ilikuwa ni furaha kwake kumwona Mariamu akipendezwa na mafundisho yake. Kadiri maneno ya Kristo yanavyoendelea kusikilizwa mara kwa mara ndivyo yanavyozidi kuuvuta moyo sana, ndivyo yanavyozidi kueleweka sana, na ndivyo yanavyozidi kuwa rahisi kuyatii kikamilifu. Roho hii ambayo daima iko tayari kujionyesha sana kwa marafiki zetu ni mbinu ya yule adui.... Yeye [Kristo] anawataka wafuasi wake ----- mali iliyonunuliwa kwa damu yake ----- kuachana na upumbavu wote pamoja na majivuno yote na uozo wote unaotokana na uharibifu uliomo duniani katika maisha yao.... Hebu wazo lisemalo, "Tazama, Mungu yupo hapa," na liufanye kila moyo kumkumbuka Mungu na kuifurahisha kila roho. ----- MS 42, 1890. NGUVU YA UJANA NA UJASIRI VYAHITAJIKA Oktoba 3 Nimewaandikia ninyi, vijana, kwa sababu mna nguvu, na neno la Mungu linakaa ndani yenu, nanyi mmemshinda yule mwovu. 1 Yohana 2:14. Kazi ya Mungu inahitaji ari, nguvu, na ujasiri wa ujana. Nguvu za kiakili na kimwili ni muhimu katika kuiendeleza kazi ya Mungu. Kufanya mipango kwa akili safi na kutekeleza kwa ujasiri hutaka nguvu mpya isiyopunguzwa. Ili kazi ipate kwenda mbele katika matawi yake yote, Mungu anataka nguvu ya ujana. Wanaume vijana na wanawake vijana wanaitwa kumpa nguvu za ujana wao, ili kwa kutumia nguvu zao walizopewa na Mungu, kwa njia ya mawazo mazuri na matendo ya kutumia nguvu, wapate kumletea Mungu utukufu na wokovu kwa wanadamu. Mungu anawasihi ninyi, enyi vijana wanaume, kutumia uwezo wenu wote aliowakabidhi. Jizoezeni kuwa na tabia ya kufanya kila mnaloweza katika kila jambo mfanyalo. Mungu ndiye Bwana wenu, na ninyi ni watumishi wake mlioajiriwa.... Mnatakiwa kuendelea kujifunza daima katika shule ya Kristo; mnatakiwa kutumia kazini mwenu nguvu za kimwili na kiakili alizowakabidhi.... Juhudi ya kutumia akili itakuwa rahisi na ya kuridhisha zaidi mnapojiweka wenyewe kufanya kazi ya kuyaelewa mambo ya Mungu yenye kina.... Mnaweza kuzikusanya tena nguvu zenu bora za akili, nanyi mkiwa mnatambua uwajibikaji wenu kwa Mungu, mnaweza kufanya kila mnaloweza, wala hamtaacha kuendelea mbele, na kuyashinda matatizo yenu. Msikae chini kwa raha inayoletwa na uvivu, bila kufanya juhudi yo yote kutimiza kazi yenu. Chagueni sehemu fulani katika shamba kubwa la Bwana, na kufanya kazi ile ambayo itataka kutumia busara na talanta zenu. ----- RH, Mei 20, 1890. Natoa ombi kwa wafuasi vijana wa Kristo waamke, wasiendelee tena kujifurahisha katika kutafuta anasa, kujipenda wenyewe na kupenda raha; wasiendelee tena kutawaliwa na matakwa yao, wala kwa tamaa zao mbaya zinazotokana na moyo wao usioongoka.... Ombi langu kwa Mungu ni kwamba uweza wake uongoao wa Roho wake Mtakatifu upate kuja juu ya vijana wetu, ili wapate kuwa wajumbe wake wanaotenda kazi ya kuwaongoa kwa Kristo makumi kwa makumi ya vijana, ili wapate kuwa miongoni mwa kundi lile litakalohesabiwa kuwa lina busara, ambalo lita"ng'aa kama mwangaza wa anga," tena "kama nyota milele na milele." Danieli 12:3. ----- YI, Juni 29, 1893. JE, SISI TUNA HATIA? Oktoba 4 Msiipende dunia, wala mambo yaliyomo katika dunia. Mtu akiipenda dunia, kumpenda Baba hakumo ndani yake. 1 Yohana 2:15. Ni ukweli unaoshtua ya kwamba kuipenda dunia kumeitawala kabisa mioyo ya vijana wetu. Kwa vyo vyote vile wanaipenda dunia, na kwa sababu iyo hiyo kumpenda Mungu hakuna nafasi ndani ya mioyo yao. Starehe zao hupatikana duniani, na katika mambo ya dunia hii, na wao ni wageni kwa Baba [hawamjui], tena ni wageni kwa yale matunda ya Roho wake. Upuuzi na mitindo ya kisasa, na maongezi matupu, yaani, yasiyo na maana, pamoja na vicheko, huashiria maisha ya vijana wetu kwa jumla, na Mungu anavunjiwa heshima yake.... Shetani anaridhika anapoyafanya mawazo ya vijana kuvutwa na kitu cho chote kinachoikengeusha mioyo yao mbali na Mungu.... Hawatambui ya kwamba Msanii yule wa Mbinguni anaona kila tendo, kila neno,... na ya kwamba hata mawazo na makusudi ya moyo yanafafanuliwa naye kwa uaminifu.... Maneno yale matupu, ya upuuzi yote huandikwa kitabuni. Maneno yale ya uongo huandikwa. Matendo yale ya udanganyifu, pamoja na makusudi yake yaliyojificha kwa macho ya kibinadamu, lakini ambayo huonekana kwa jicho la Yehova linaloona yote, huandikwa kwa herufi hai. Kila tendo la uchoyo hufichuliwa. Vijana kwa kawaida huenenda kana kwamba saa za thamani za muda wao wa majaribio zilikuwa ni siku kuu ya mapumziko wakati rehema bado inangoja, na ya kwamba wamewekwa humu duniani kwa ajili ya burudani yao tu. ----- RH, Machi 30, 1886. Maneno na matendo hushuhudia wazi kile kilichomo moyoni. Endapo upuuzi na kiburi, kujipenda nafsi na kupenda mavazi, huujaza moyo, basi, maongezi yatakuwa juu ya mitindo ya kisasa, mavazi, na mwonekano wa nje, bali sio juu ya Kristo, wala juu ya ufalme ule wa mbinguni. Kama hisia za wivu zimo moyoni, basi, zizo hizo zitajionyesha katika maneno na matendo.... Wengine huongea sana juu ya kile watakachokula na kunywa na kile watakachovaa. Mioyo yao inajazwa na mawazo hayo, nayo yanatoka nje kutoka katika wingi uliomo moyoni mwao, kana kwamba mambo hayo ndilo lengo lao kuu katika maisha haya, yaani, mafanikio yao ya juu sana. Wanasahau maneno ya Kristo, yasemayo, "Bali utafuteni kwanza ufalme wake, na haki yake; na hayo yote mtazidishiwa." Mathayo 6:33. ----- RH, Machi 30, 1886. BURUDANI PEKEE ZILIZO SALAMA Oktoba 5 Watashibishwa kwa unono wa nyumba yako, Nawe utawanywesha mto wa furaha zako. Zaburi 36:8. Adui anatafuta kwa njia nyingi kuivuta mioyo yetu mbali na Neno ili tusipate kujifunza. Wengi anawaongoza kupata furaha yao katika michezo na anasa, mambo ambayo huonekana kuwa ni ya kupendeza kwa mtu yule ambaye hajaongoka. Lakini watoto wa kweli wa Mungu hawatafuti furaha yao katika ulimwengu huu; wanatafuta furaha zile zinazodumu za makao yale katika jiji lile la milele, ambako Kristo anakaa, na ambako wale waliokombolewa watapokea thawabu zao kutokana na utii wao kwa matakwa ya Mungu. Hao hawazitamani furaha zile za upuuzi zinazopita za maisha haya, bali [wanatamani] furaha ile kamili inayodumu milele kule mbinguni. Mungu amewakabidhi wanaume na wanawake uwezo mkubwa ----- uwezo ambao angetaka utumike katika kazi yake; na nuru ile ni ya thamani ambayo humjia kila mmoja ambaye anazitumia talanta zake kwa uaminifu kwa utukufu wa Mungu. Tungejitahidi kuiweka mioyo yetu katika hali ile itakayotuwezesha kupokea muhuri wa Roho Mtakatifu. Walakini hawawezi kupokea nuru zaidi wale wanaoyaacha mawazo yao kukimbilia kila wakati kwenye mambo yale ya kipuuzi. Moyo ungejazwa na hazina ya mbinguni, na chakula kile kitakachotuwezesha sisi kukua kiroho, na hivyo kutuandaa kwa ajili ya mbingu ile takatifu.... Kuna njia nyingi ambazo kwazo tunaweza kuwasaidia wale wanaoshirikiana nasi, iwapo moyo wetu tutauelekeza huko. Lakini inanisikitisha sana ninapoona mipango inaandaliwa kwa ajili ya burudani na kujifurahisha nafsi. Mambo hayo yanapoujaza moyo, hakuna nafasi inayopatikana kwa ile kweli ya thamani ya Mungu kuweza kuitawala nafsi. Ninapowaona wale ambao mapenzi yao yameelekezwa kwenye anasa za ulimwengu huu, natamani jinsi gani kwamba wangeweza kuongolewa. Wangepata wasaa wa kusema maneno ambayo yangekuwa ya kutia moyo, na yangeleta nuru na furaha kwa watu wanaohitaji msaada kama huo. ----- MS 51, 1912. Burudani pekee zilizo salama ni zile zisizoweza kuyafukuzilia mbali mawazo yale ya kweli na ya kidini; mahali salama pekee pa kwenda ni pale tunapoweza kwenda pamoja na Yesu. ----- RH, Nov. 6, 1883. KUYAVUNJILIA MBALI MALIWAZO YA ULIMWENGU HUU Oktoba 6 Na dunia inapita, pamoja na tamaa zake, bali yeye afanyaye mapenzi ya Mungu adumu hata milele. 1 Yohana 2:17. Mafundisho ya Kristo ni ya namna ile inayoonyesha uhusiano muhimu uliopo kati ya mbingu na dunia. Anaweka picha mbele ya macho yetu inayoonyesha kwamba madai ya mbinguni yanapata umuhimu wa kwanza. Madai ya Mungu ni makubwa kabisa. Anatudai sisi tumpe moyo wetu wote, akili yetu yote, uwezo wetu wote, na nguvu zetu zote. Mambo ya duniani anayaweka mahali pake, ili yapate kudhibitiwa na mambo yale ya milele. Majaribu ya Shetani huyaonyesha mambo ya ulimwengu huu na kuyafanya yachukue mawazo yetu yote na kutuvutia, ili mambo halisi ya mbinguni yapate kufunikwa, ndipo kule kufungamana na ulimwengu huu kupate kupewa nafasi ya kwanza; na uwezo huo umekuwa mkubwa mno kiasi kwamba ni Mungu peke yake mwenye uwezo wote awezaye kuuondolea mbali [kwa nguvu zake]. Kazi ya Shetani ni kuzifunga fahamu zetu ili zielekee kwenye mambo ya ulimwengu huu. Kristo alikuja ili kuzivunjilia mbali nguvu hizo za Shetani, kuipinga kazi ya Shetani, na kuuvuta moyo wetu kutoka katika mambo ya ulimwengu huu kwenda kwa yale ya mbinguni. Yeye peke yake ndiye awezaye kuuvunjilia mbali mvuto huo.... Bado miaka michache tu dunia hii na utukufu wake wote, ambayo kwa nguvu ya uchawi wake yule Mlaghai Mkuu imekuwa lengo la ibada yake, itachomwa moto, pamoja na mapambo yote ya sanaa za mwanadamu. Ni kitu gani, basi, kitakachopatikana ili kufidia hasara ya [kuipoteza] nafsi ya mwanadamu? Yule Mkuu wa uzima anayaelekeza mawazo yetu kwenye ulimwengu ule wa milele.... Angependa utukufu ule wa milele utakaokuja baadaye upate kuivutia sana mioyo ya wanadamu, na ulimwengu huu wa sasa uchukue mahali pake pa chini katika mapenzi yao. Anayarekebisha mambo yale aliyoyageuza Shetani. Akiisha kuushusha chini ulimwengu huu kutoka kwenye kiti chake cha enzi ambako umegeuka na kuwa mamlaka inayotawala na kuabudiwa kama Mungu, anauweka mahali pake panapoustahili.... Mambo yale ya milele yakiwa yanaonekana hivyo mbele yetu, itatubidi sisi tujizoeze kuyakuza mawazo yetu ili yapate kutambua kuwako kwake Mungu pamoja nasi. Jambo hilo litakuwa ndiyo ngao yetu dhidi ya adui yule anayetaka kuingia ndani yetu; litatupa nguvu na imani, na kuiinua mioyo yetu juu mbali na hofu. Tukiwa tunaendelea kuivuta hewa ile ya mbinguni, hatutaendelea kuivuta hewa ile iliyojaa malaria ya ulimwengu huu. Hatutabaki katika chumba cha giza cha chini ya ardhi, bali tutapanda juu katika vyumba vile vya juu, ambako kila dirisha liko wazi kuelekea mbinguni, tena linaingiza miali ile inayong'aa toka kwa Jua lile la Haki [Kristo]. ----- MS 42, 1890. MAMBO YA KWANZA NI YA KWANZA Oktoba 7 Msisumbuke, basi, mkisema, Tule nini? au Tunywe nini? au Tuvae nini? Mathayo 6:31. Mungu asingependa kumwona mtu ye yote kati yetu aliye na kiburi kile cha makusudi, asiyejali afya yake, wala asiye na mpango wo wote wa kujipatia riziki yake; walakini, Yeye anapoona ulimwengu ukiyachukua mawazo yetu yote na kuchota mapenzi yetu yote, basi, anaona kwamba mambo yale ya milele hatuyaangalii kabisa. Angependa kuusahihisha uovu huo, ambao ni kazi yake Shetani. Moyo, ambao ungefunzwa kutafakari mambo yale ya milele yaliyo juu, na yaliyo bora, unageuka na kuwa wa vivi hivi tu, yaani, unachukua sura ya ulimwengu huu. Yesu anakuja kutuonyesha faida na uzuri wa mandhari ile ya mbinguni, ili mivuto ile ya mbinguni tupate kuizoea katika mawazo yetu, na ukumbi wetu wa kumbukumbu utundikwe picha zinazoonyesha uzuri ule wa mbinguni, yaani, ule wa milele. Anaviona vyumba vya mioyo yao vimejazwa na mambo yale yaliyo machafu. Anamweka Mungu mbele yao kama ndiye kitovu chao.... Anapita sokoni, ambako kila kitu kiko katika shughuli yake na pilikapilika, na sauti za wafanya biashara zinasikika. Mafundisho anayotoa katika halaiki ile kubwa inayokusanyika pale kusikiliza maneno yake ni onyo kutoka mbinguni linalolia kama parapanda ya Mungu ili kuweza kuvunjilia mbali uchawi ule tuliotupiwa [na Shetani] wa kupenda mno mambo ya dunia hii. "Kwa kuwa itamfaidia mtu nini kuupata ulimwengu wote, akipata hasara ya nafsi yake? Ama mtu atoe nini badala ya nafsi yake?" Marko 8:36,37. Mwalimu Mkuu huyo anamwonyesha mwanadamu picha ya ulimwengu ule ujao. Anauleta, pamoja na mambo yake yote yanayopendeza sana, katika upeo wa macho yake.... Anaonyesha madai halisi ya Mungu na Mbingu. Kama anaweza kuufunga moyo ili upate kuelekea kwa maisha yale ya baadaye na mibaraka yake, ukiyalinganisha na mambo ya muda ya ulimwengu huu, basi, tofauti inayoonekana dhahiri itapigwa picha moyoni humo, ikiujaza moyo na roho na mwili wote. Kwa njia hiyo anaviondoa vitu vile vya muda na vile vinavyoweza kufahamika kutoka katika mapenzi yetu ambamo vilishika hatamu, na kuviweka mahali pake vikiwa chini ya mamlaka ile ya juu na mambo yale ya milele. Anawapa watu majukumu ya juu kabisa. Anamwonyesha mwanadamu kwamba anapaswa kuishi akiwa na kusudi fulani, akijitenga mbali na ubatili wote wa maisha. ----- MS 42, 1890. KUUTII MWITO WA MUNGU Oktoba 8 Akawaambia wote, Mtu ye yote akitaka kunifuata, na ajikane mwenyewe, ajitwike msalaba wake kila siku, anifuate. Luka 9:23. Kujikana nafsi kutawekwa katika matendo na wale wote wanaomfuata Kristo. Yuda alijitolea kumfuata Yesu, na wakati ule ule kutekeleza mipango yake ya ubinafsi, yaani, ya uchoyo. Alikuwa na haki zile zile walizokuwa nazo wanafunzi wale wengine. Alikuwa na nafasi ile ile ya kusikiliza mafundisho ya Kristo, ambayo yaliweka wazi utauwa kwa vitendo; lakini yeye sikuzote hakupendezwa na ukweli ule ulio wazi. Ulimchoma, na badala ya kujifanyia kazi yeye mwenyewe kama Yuda Iskariote, akawa akiyakosoa maneno na matendo ya Kristo, na kuyashutumu mafundisho yake yaliyo wazi. Badala ya kubadilika katika tabia yake, akawa anaendelea kukuza tabia ya kujipenda mwenyewe, kujisifu, na kupenda fedha. ----- RH, Agosti 21, 1894. Kuishi kwa ajili ya nafsi ni kuangamia. Uchoyo, yaani, tamaa ile ya kupata faida kwa ajili ya nafsi, huitenga nafsi mbali na uzima. Ni roho ya Shetani kupata, yaani, kuvisogeza vitu vyote kwa nafsi. Ni roho ya Kristo kutoa, kuitoa nafsi mhanga kwa ajili ya manufaa ya wengine. ----- MS 107, 1908. Hapawezi kuwapo na roho ya kutafuta mambo yake mwenyewe katika maisha ya yule anayemfuata Mwokozi. Mkristo wa kweli anaondolea mbali uchoyo wote toka moyoni mwake. Anawezaje kuishi kwa ajili ya nafsi yake anapowaza juu ya Kristo anayening'inia msalabani, akitoa uhai wake kwa ajili ya uzima wa ulimwengu? Kwa niaba yako Yesu alikufa kifo kile cha aibu! Je, uko tayari kujitoa wakf mwenyewe katika kazi yake? Kuwa tayari kufanywa au kufanya kitu cho chote anachoweza kutaka? Je, u tayari kuiweka kando nafsi yako, na kusema neno moja la onyo kwa mwenzako unayemwona anaanguka chini ya majaribu ya Shetani? Je, uko tayari kuiacha baadhi ya mipango yako kwa ajili ya kujaribu kumwongoza katika njia zilizo salama? Vijana wengi wako hatarini ambao wangeweza kuokolewa endapo Wakristo wangewaonyesha moyo wa upendo usiokuwa na ubinafsi.... Mkristo wa kweli anafanya kazi yake bila kuwa na ubinafsi, wala uchovu kwa ajili ya Bwana wake. Hatafuti raha, wala kujifurahisha nafsi yake, bali anayaweka mambo yote, hata uhai wake wenyewe, chini ya mamlaka ya mwito wa Mungu. Na maneno haya yanasemwa kwake, "Mwenye kuipoteza roho yake kwa ajili yangu ataiona." Mathayo 10:39. ----- YI, Juni 12, 1902. MBINGU NI RAHISI KWA GHARAMA YO YOTE Oktoba 9 Mtu ye yote asiyeuchukua msalaba wake na kuja nyuma yangu, hawezi kuwa mwanafunzi wangu. Luka 14:27. Ni jambo la kweli kabisa kwamba umati mkubwa ulio na uwezo na talanta hauchagui kusafiri katika njia ile ya Kikristo. Je, talanta zao na uwezo wao ni vya thamani sana hata hawawezi kuvitoa kwa Mpaji wao, Bwana wa mbingu na dunia?... Wengi wangependa kuwa wafuasi wa Kristo kama angeshuka chini kutoka msalabani na kuja kwao kwa njia ile wanayotaka wao. Endapo angekuja na utajiri na anasa, wengi wangempokea kwa furaha na kufanya haraka kumvika taji kama Bwana wa wote. Endapo angeweka kando kudhalilishwa kwake na mateso yake na kupiga kelele, akisema, "Mtu awaye yote akitaka kunifuata, na ajifurahishe mwenyewe na kuifurahia dunia hii, naye atakuwa mwanafunzi wangu," hapo ndipo makundi kwa makundi wangemwamini. Lakini Yesu, yule mbarikiwa, atakuja kwetu kwa tabia ambayo si nyingine bali ni ile ile ya yule Msulibiwa, aliye mpole na mnyenyekevu wa moyo. Ni lazima tushiriki kujikana nafsi kwake pamoja na mateso yake tukiwa tungali hapa kama tunataka kuivaa taji ile baadaye.... Neno la Mungu halijaipanua njia ile nyembamba, na kama wengi wameipata njia nyingine wanamoweza kuvaa mfano wa utauwa, halafu wasiweze kujitwika msalaba, wala kupata dhiki, basi, hao wameipata njia ambayo Mwokozi wetu hakutembea humo, nao wanafuata kielelezo kingine kuliko kile alichokiweka Kristo mbele yetu. Je, haitoshi kwamba Yesu aliacha furaha kuu na utukufu wa mbinguni, akastahimili maisha ya kimaskini na mateso makubwa, na kufa kifo cha kikatili, cha aibu, ili kutupatia sisi furaha ya utakatifu na mbingu juu? Tena, yawezekanaje kwamba sisi, watu tusiostahili kujidhili kwake kukuu na upendo wake, kujitafutia fungu lililo bora katika maisha haya kuliko lile alilopewa Mkombozi wetu? ----- Letter 2, 1861. Ingekuwa rahisi jinsi gani njia ile ya kwenda mbinguni kama pasingalikuwapo na kujikana nafsi, wala msalaba! Wapenda anasa wangekimbia kwa kasi jinsi gani kuingia katika njia hiyo, na wanafiki wengi sana wangesafiri humo! Na tumshukuru Mungu kwa ajili ya msalaba, yaani, kujikana nafsi. Utwezo na aibu yake Mwokozi wetu aliyostahimili kwa ajili yetu haidhalilishi sana kwa wale waliookolewa na kununuliwa kwa damu yake. Mbingu kwa kweli itakuwa rahisi ya kutosha. ----- Letter 9, 1873. TALANTA KWA KILA MMOJA Oktoba 10 Maana [ufalme wa mbinguni] ni mfano wa mtu atakaye kusafiri, aliwaita watumwa wake, akaweka kwao mali zake. Akampa mmoja talanta moja; kila mtu kwa kadiri ya uwezo wake; akasafiri. Mathayo 25:14,15 [KJV]. Mungu hajawapa talanta zake wateule wake wachache tu, bali amempa kila mmoja. Amempa kipawa kimoja cha pekee ili kukitumia katika kazi yake. Wengi ambao Bwana amewapa talanta za thamani wamekataa kuzitumia kwa ajili ya kuuendeleza ufalme wa Mungu; hata hivyo, wanawajibika kwa Mungu kwa matumizi ya vipawa vyake. Kila mmoja, haidhuru kama anamtumikia Mungu au anajifurahisha mwenyewe, amekabidhiwa amana fulani, ambayo ikitumika vizuri itamletea Mungu utukufu na ambayo ikitumika vibaya itamnyang'anya Mpaji [utukufu wake].... Jamii ya kibinadamu imejengwa na watu wenye kuwajibika kimaadili, kuanzia wale wa juu kabisa wenye vipawa vingi mpaka wale wa chini kabisa ambao hawajulikani kabisa, wote hao wamepewa bidhaa zile za mbinguni. Wakati ni kipawa tulichopewa na Mungu, nao unapaswa kutumika katika kazi ya Kristo. Mvuto ni kipawa cha Mungu, nao hauna budi kutumika kwa kuyasukuma mbele makusudi yale ya juu kabisa, yaani, yaliyo bora sana.... Akili ni talanta tuliyokabidhiwa. Huruma na upendo ni talanta ambazo hazina budi kulindwa kwa bidii na kukuzwa, ili tupate kumtumikia yeye aliyetununua sisi kuwa mali yake. Vyote vile tulivyo [kimaumbile] au tunavyoweza kuwa sisi ni mali yake Mungu. Elimu, nidhamu, na ustadi katika kila kazi vinapaswa kutumika kwa ajili yake. Mtaji ni wake yeye, na kuuendeleza ndio ushuru ambao ni mali yake Bwana kihalali. Haidhuru kama kiasi kile tulichokabidhiwa ni kikubwa au kidogo, Bwana anawataka wale wanaoisimamia nyumba yake kufanya kila wanaloweza. Si kiasi kile kilichokabidhiwa, wala kule kukiendeleza kutakakofanyika ambako kutawaletea wanadamu sifa za Mbingu, bali ni ule uaminifu, utiifu kwa Mungu, yaani, kazi ile iliyofanywa kwa moyo wa upendo, ambayo inaleta mbaraka ule wa mwisho kutoka mbinguni, atakaposema, "Vema, mtumwa mwema na mwaminifu; ulikuwa mwaminifu kwa machache, nitakuweka juu ya mengi; ingia katika furaha ya Bwana wako." Fungu la 23. Thawabu hiyo ya furaha haingoji mpaka hapo tutakapoingia katika mji ule wa Mungu, bali mtumishi mwaminifu anaionja hata katika maisha haya. ----- ST, Jan. 23, 1893. UNAZITUMIAJE TALANTA ZAKO? Oktoba 11 Mara yule aliyepokea talanta tano akaenda, akafanya biashara nazo, akachuma faida talanta nyingine tano. Vile vile na yule mwenye mbili, naye akachuma nyingine mbili faida. Lakini yule aliyepokea moja alikwenda akafukua chini, akaificha fedha ya Bwana wake. Mathayo 25:16-18. Ujuzi wa ile kweli ni wa thamani kabisa hata hauwezi kuhodhiwa [kuwekwa kama akiba], na kufungiwa, na kufichwa ardhini. Hata ile talanta moja aliyokupa Bwana inapaswa kutumika kwa uaminifu.... Mungu anatoa baraka yake juu ya juhudi isiyo na ubinafsi ndani yake, isiyochoka; na ijapokuwa sisi tunaweza kuwa na talanta moja tu, na kutumia nguvu kidogo tu, hata hivyo Mungu ataifanya juhudi hiyo kuzaa matunda kama matokeo yake. Mtu anayefanya kazi yake kwa imani atagundua kwamba akili yake, mapenzi yake, uwezo wake wote, ni mali ya Mungu, naye atajitahidi kutumia nguvu zake kwa bidii, na kuukuza uwezo wake pamoja na talanta zake. Lakini basi, badala ya kutambua kwamba uwezo wetu wote ni mali ya Mungu, ni wangapi wasiojali, wasiofikiri kwamba mvuto wao, maneno yao ya ovyo na ya kipuuzi, yanazibadilisha tabia za wale wanaoshirikiana nao, na kuyashusha mawazo yao kwenye kiwango cha chini!... Mazingira yale yanayomzunguka mtu hujaa mvuto wa mema au mabaya.... Yanaweza kujaa sumu na malaria, au harufu nzuri na safi na ya aina ile inayoleta afya. Mvuto huo wa kimaadili utalingana na uhusiano wetu na Kristo au mtengano wetu naye, yeye ambaye ni nuru na uzima wetu. Wale waliounganishwa na Kristo watatambua ya kwamba amewakabidhi amana nyingi kulingana na uwezo wa kila mmoja; na bila kujali mazingira yao, watazifikiria kuwa zinafaa sana kwa kukuzia tabia zao za kimaadili. Yatupasa kufanya kila tuwezalo kwa kutumia kila mafao tuliyo nayo na nafasi nzuri zinazojitokeza.... Yatupasa kuukuza na kuuendeleza uwezo wetu ili tusije tukamsikitisha Bwana wetu, bali tupate kukifikia kiwango kile cha juu kabisa kinachowezekana, na kwa njia hiyo kuwavuta wengine kufuata katika nyayo za Kielelezo chetu. Twaweza kusema, "Si jamii, wala marafiki zangu wa karibu sana wanaopaswa kuwa na mawazo ya tabia ya Kikristo yaliyohafifishwa kutokana na mwenendo wangu."... Unafanya nini na talanta zako? Je, unaziweka kwa wale watoao riba? ----- ST, Jan. 23, 1893. UWEZO WA KUSEMA NI TALANTA YA THAMANI Oktoba 12 Kwa kuwa kwa maneno yako utahesabiwa haki, na kwa maneno yako utahukumiwa. Mathayo 12:37. Mungu amempa kila kijana uwezo wa kusema ili upate kukuzwa kwa ajili yake. Hii ni amana ya maana sana.... Maneno yako na yawe ni yale yanayoleta uzima, yakiwaelekeza wale wakuzungukao kwa Mwokozi. Hebu yalete mwanga wa jua badala ya giza, amani badala ya uadui. Usiseme neno lo lote ambalo usingekuwa tayari kusema mbele zake Yesu na mbele ya malaika. Usitamke neno lo lote litakalochochea ugomvi ndani ya moyo wa mtu mwingine. Haidhuru uwe umechokozwa kiasi gani, zuia neno lile la harara [lisitoke kinywani mwako]. Iwapo wewe unafanana na Kristo katika usemi wako na matendo yako, basi, wale wanaoshirikiana nawe watabarikiwa kwa ushirikiano huo. Maneno na matendo yako ya haki yana mvuto wenye nguvu kuwaelekeza watu kwenye mema kuliko mahubiri yote yanayoweza kutolewa. ----- YI, Jan. 1, 1903. Hebu na tujihadhari kusema maneno ya kukatisha tamaa. Hebu na tuazimie kutosema mabaya, wala kusengenya hata kidogo. Hebu na tukatae kumtumikia Shetani kwa kupandikiza mbegu za mashaka. Hebu na tujihadhari tusiwe na moyo usioamini, wala tusiuonyeshe kwa wengine. Mara nyingi sana nimetamani kwamba kingezungushwa kiapo [maalum] kilicho na ahadi nzito ya kusema maneno yale tu yanayopendeza kwa Mungu. Ipo haja kubwa kwa kiapo kama hicho kuwapo, kama ilivyo kwa kile cha kukataa kutumia vileo vikali. Hebu na tuanze kuufuga ulimi wetu, tukikumbuka daima kwamba tunaweza kufanya hivyo tu kwa kuudhibiti moyo wetu, maana "kinywa cha mtu huyanena yaujazao moyo wake." Mathayo 12:34. Kwa msaada anaoweza kutupa Kristo, sisi tutaweza kujifunza kuuzuia ulimi wetu. Kama vile yeye alivyojaribiwa mno juu ya jambo hilo la kusema kwa harara na hasira, hata mara moja yeye hakupata kutenda dhambi kamwe kwa kinywa chake. Kwa ukimya wake wenye ustahimilivu alipambana na kicheko cha dharau, dhihaka, na kebehi, kutoka kwa watenda kazi wenzake kwenye benchi lile la seremala. Badala ya kujibu kwa hasira, yeye alianza kuimba mojawapo ya Zaburi nzuri za Daudi; na wenzi wake, kabla hawajatambua walichokuwa wakifanya, walijiunga naye kuimba wimbo huo wa kumsifu Mungu. Ni badiliko lililoje lingeweza kutokea ulimwenguni humu kama wanaume na wanawake wa siku hizi wangeuiga mfano huo wa Kristo katika kutumia maneno yao! ----- RH, Mei 26, 1904. KIELEZO CHA TABIA Oktoba 13 Wala aibu wala maneno ya upuuzi wala ubishi, hayo hayapendezi; bali afadhali kushukuru. Waefeso 5:4. Tabia ya mtu inaweza kutathminiwa kwa usahihi kabisa kwa kufuata tabia ya maongezi yake.... Wale wanaofanya utani na mzaha na mazungumzo ya kipuuzi wanajiweka mahali ambapo Shetani anaweza kuwaingia.... Mnaposhirikiana pamoja, mnaweza kuwa msaada na mbaraka ninyi kwa ninyi kama mnajizungushia mvuto wa kimbingu. Lakini wapo wale walio na kasoro kubwa ambazo zimewashikilia sana na ambazo iwapo hawatazishinda zitamfukuzilia mbali Roho wa Mungu kutoka moyoni mwao.... Utani na mzaha huenda vikaifurahisha mioyo duni, hata hivyo mvuto wa tabia kama hiyo huyaangamiza maisha ya kiroho. Nazungumza nanyi kama kundi na pia kama mtu mmoja mmoja: Chunga sana maneno yako. Hebu utulivu na busara viwe ndiyo tabia ya maongezi yenu. Msifanye mchezo na usafi na ubora wa roho zenu kwa kujishusha hadhi zenu na kujifurahisha kwa mizaha ya ovyo, na kwa kujenga mazoea ya kuwa na maongezi ya kipuuzi. Matakwa ya Mungu ni wazi kuhusu mambo hayo, nayo yanaweka mbele yenu wajibu unaowakalia ninyi kama wana wa Mungu. Neno la Mungu lasema hivi, "Na kila mfanyalo, kwa neno au kwa tendo, fanyeni yote katika jina la Bwana, mkimshukuru Mungu Baba kwa yeye." Wakolosai 3:17. ----- Letter 2, 1895. Laiti kama kila mmoja wa vijana wetu angetambua ubaya wa maongezi ya kipumbavu, na kusahihisha tabia yake ya kusema maneno yasiyokuwa na maana! Hebu kila mmoja aliyeitenda dhambi hii na aitubie, aiungame mbele zake Mungu, na kuiweka mbali naye. Katika kusema maneno ya kipumbavu, umeliaibisha jina lake Kristo; kwa maana umemwakilisha vibaya kwa tabia yako hiyo. Neno lo lote lililo ovu halikuonekana katika kinywa chake, wala neno lo lote la kukwepa kusema ukweli wote, wala lile la uongo. Watu wale wanaoelezwa kuwa wanafanya idadi ile ya mia moja na arobaini na nne elfu, wana jina la Baba limeandikwa katika vipaji vya nyuso zao, na juu yao inasemwa hivi: "Na katika vinywa vyao haukuonekana uongo. Maana hawana mawaa." Ufunuo 14:5. ---- - YI, Juni 27, 1895. UNYAMAVU UNAPOKUWA UNENAJI UNAOKOLEA Oktoba 14 Afunikaye kosa hutafuta kupendwa; Bali yeye akashifuye neno hutenga rafiki. Mithali 17:9. Mtunga Zaburi anauliza, "BWANA, ni nani atakayekaa katika hema yako? Ni nani atakayefanya maskani yake katika kilima chako kitakatifu? Ni mtu aendaye kwa ukamilifu, na kutenda haki. Asemaye kweli kwa moyo wake, Asiyesingizia kwa ulimi wake. Wala hakumtenda mwenziwe mabaya, Wala hakumsengenya jirani yake" [Zaburi 15:1-3]. Wakati mtu ye yote anapokuja kwako na kisa cho chote juu ya jirani yako, ingekupasa kukataa kukisikiliza. Ungemwambia hivi, "Je! umezungumza jambo hilo na mtu huyo anayehusika?... Mwambie kwamba anapaswa kuitii kanuni ile ya Biblia, na kumwendea ndugu yake kwanza, na kumweleza kosa lake faraghani, na kwa upendo. Kama maagizo ya Mungu yangetekelezwa, basi, milango ya kufungulia maji ya umbea [uongo] ingekuwa imefungwa. Ndugu zako na majirani zako wanapokuja kwako kukuona, ongea nao juu ya upendo wa Yesu wa ajabu. Furahia maombezi yake anayofanya kwa ajili ya mwanadamu aliyepotea. Waambie rafiki zako juu ya upendo ulio nao kwa roho zao, kwa sababu nao wamenunuliwa kwa damu yake Kristo. Mungu na apishe mbali ili sisi tusiifanye njia ya wasafiri wengine waliochoka sana kuwa ngumu kwa kuyakuza makosa yao, na kwa kuwahukumu matendo yao. Mungu na atusaidie ili tupate kuzungumza maneno ya faraja na tumaini na imani ili kuyachangamsha maisha ya wale walio wapweke, na waliokata tamaa, na wale wanaofanya makosa. ----- YI, Juni 27, 1895. Unapojaribiwa kutaka kusema maneno yasiyokuwa ya busara, jihadhari. Kama mtu mwingine ye yote anakuja kwako akiwa na maneno ya kumkosoa mmojawapo wa watoto wa Mungu, geuza sikio lako kama kiziwi usisikilize neno lo lote kama hilo. Kama wakikusemea kwa ukali, usilipize kisasi hata kidogo. Usitamke neno lo lote. Unapochokozwa, kumbuka kwamba "Unyamavu ni unenaji unaokolea." Unyamavu ni kemeo kubwa mno unaloweza kumpa yule anayekutafuta makosa au yule ambaye hasira yake imelipuka. ----- MS 95, 1906. Lingekuwa lengo letu kuleta uzuri wote unaowezekana katika maisha yetu, na kufanya wema wote unaowezekana kwa wale wanaotuzunguka. Maneno ya upole hayapotei kamwe. Mungu anayaweka katika kumbukumbu zake kana kwamba yamesemwa kwake mwenyewe. Pandeni mbegu za wema, upendo, na upole, nazo zitachipua na kuzaa matunda. ----- 6BC 1118. MANENO YALETAYO MWANGA WA JUA NA FURAHA Oktoba 15 Maneno yenu yawe na neema siku zote, yakikolea munyu, mpate kujua jinsi iwapasavyo kumjibu kila mtu. Wakolosai 4:6. Talanta ya usemi ilitolewa kutumika kwa faida ya wote. Maneno matamu, yenye kuchangamsha watu hayana gharama kama yalivyo maneno yale ya kuchukiza, ya kuvunja moyo. Maneno makali yanajeruhi na kuumiza moyo. Katika maisha haya kila mmoja anayo matatizo anayotakiwa kupambana nayo. Kila mmoja anakabiliwa na manung'uniko na kukata tamaa. Je! tusilete mwanga wa jua badala ya giza katika maisha ya wale tunaokutana nao? Je! hatuwezi kuzungumza maneno yatakayowasaidia watu na kuwaletea furaha? Maneno kama hayo yatakuwa mbaraka kweli kweli kwetu sisi kama vile yatakavyokuwa kwa wale ambao yatasemwa kwao. Enyi wazazi, msiruhusu kuwemo nyumbani mwenu kutafutana makosa. Wafundisheni watoto wenu kusema maneno matamu, maneno yatakayoleta mwanga wa jua na furaha. Malaika hawavutiwi [hawapendezwi] kwenda kwenye nyumba ambayo imetawaliwa na mafarakano. Leteni dini ya matendo nyumbani mwenu. Jiwekeni tayari pamoja na watoto wenu kuingia katika mji ule wa Mungu. Malaika watakuwa wasaidizi wenu. Shetani atawajaribu, lakini msikubali. Msiseme neno moja ambalo yule adui atalitumia kwa manufaa yake. ----- RH, Jan. 28, 1904. Siku kwa siku tunapanda mbegu kwa mavuno ya baadaye. Hatuwezi kuwa waangalifu mno juu ya mbegu tunayopanda kwa njia ya maneno yetu. Mara kwa mara maneno yanasemwa bila kujali na kusahaulika, lakini maneno hayo, kwa mema au kwa mabaya, yatatoa mavuno yake. Panda neno moja lisilo jema, neno kali, na mbegu hiyo, ikipata udongo mzuri katika mioyo ya wasikilizaji, itaota na kuzaa matunda ya aina yake. Panda mbegu moja kwa kutumia maneno ya upendo, upole, maneno yanayofanana na yale ya Kristo, nayo itakuletea mavuno mengi. Hebu na tujihadhari, tusije tukasema maneno ambayo hayaleti baraka, bali laana. Tukipanda ngano tutavuna ngano; tukipanda magugu tutavuna magugu; na mavuno hayo, kama ni ya ngano, ama ni ya magugu, yatakuwa ya hakika na mengi. "Msidanganyike, Mungu hadhihakiwi; kwa kuwa cho chote apandacho mtu, ndicho atakachovuna." Wagalatia 6:7. Mavuno ni ya hakika. Hakuna umande ulioganda kwa baridi unaoweza kuyaharibu, wala mdudu wa mchikichi atakayeyaharibu. Mungu anawaagiza watoto wake kuyachunga sana maneno yao. ----- MS 99, 1902. MANENO NI KAMA MATOFAA YA DHAHABU Oktoba 16 Neno linenwalo wakati wa kufaa, Ni kama machungwa [matofaa ya dhahabu] katika vyano vya fedha. Mithali 25:11 [KJV]. Wengine wanapotoka kwenye mazungumzo yao ya kila siku na Mungu huonekana kuwa wamevikwa na upole ule wa Kristo. Maneno yao... yanatoka vinywani mwao yakiwa matamu. Wanatawanya mbegu za upendo na upole katika njia yao yote,... kwa kuwa Kristo anaishi mioyoni mwao. ----- 3BC 1159. Ulimi unahitaji kuelimishwa na kudhibitiwa na kufunzwa ili upate kuongea habari za utukufu ule wa mbinguni, na kuzungumza juu ya upendo wa Yesu usiokuwa na kifani. --- -- 3BC 1146. Kuna watu wanaofanya makosa, na kuiona aibu yao na upumbavu wao. Hao wana njaa ya kusikia maneno ya kuwatia moyo. Wanayaangalia makosa yao na dhambi zao mpaka wanakaribia kukata tamaa kabisa. Badala ya... kuwakaripia na kuwahukumu na kuwaondolea mwonzi wa mwisho wa tumaini lao, ambao yule aliye Jua la Haki anawaangazia mioyoni mwao, hebu maneno yako na yapate kuanguka masikioni mwa mtu huyo aliyejeruhiwa kama zeri [dawa iponyayo]. Usiwe kama mvua ile ya mawe iharibuyo ambayo inapiga na kuliharibu tumaini lile hafifu linaloanza kuchipuka mioyoni mwao. Usimwache mtu mwenye njaa aangamie, yaani, yule anayekufa kwa njaa, katika hali yake ya kutojiweza kwa sababu wewe unashindwa kumwambia maneno ya upole na ya kutia moyo. ----- RH, Agosti 20, 1895. Usemaji unaokolea sana ni lile neno linalosemwa kwa moyo wa upendo na huruma. Maneno kama hayo yataleta nuru kwa wale waliochanganyikiwa na tumaini kwa wale waliokata tamaa, na kuweka mbele yao mandhari [picha] inayong'aa. Kipindi hiki tunachoishi kinahitaji sisi tuwe na nguvu iliyotakaswa; juhudi, moyo, na huruma nyingi sana pamoja na upendo; na maneno ambayo hayawezi kuzidisha maumivu, bali kuamsha imani na tumaini. Tunasafiri kwenda nyumbani, tukiwa tunaitafuta nchi ile iliyo bora, yaani, ya mbinguni. Badala ya kusema maneno ambayo yatatia uchungu vifuani mwa wale wanaoyasikia, je! haitupasi kusema juu ya upendo ambao kwa huo Mungu alitupenda sisi? Je! tusijaribu kuifanya mioyo ya wale wanaotuzunguka kuwa myepesi kwa maneno yaliyojaa huruma kama yale ya Kristo? ----- RH, Feb. 16, 1897. Wale wanaompenda Yesu Kristo wataitafakari tabia yake, watayatafakari maneno yake, wataziweka katika matendo amri zake, na kuwa wamishonari walio hai. Maneno yale wasemayo yatakuwa kama machungwa [matofaa ya dhahabu] katika vyano vya fedha. --- -- Letter 2, 1895. WAKRISTO NI KAMA MWANGA WA JUA Oktoba 17 Ondoka uangaze; kwa kuwa nuru yako imekuja, Na utukufu wa BWANA umekuzukia. Isaya 60:1. Ni haki yake Mkristo kujiunganisha na Chimbuko la nuru [Kristo], na kwa muungano huo ulio hai kuwa nuru ya ulimwengu. Wafuasi wa Kristo wa kweli wataenda nuruni kama yeye alivyo nuruni, na kwa hiyo hawatasafiri katika njia isiyojulikana, wakiwa wanajikwaa kwa sababu wanaenda gizani. Mwalimu huyo Mkuu anawapa picha wasikilizaji wake jinsi wanavyoweza kuwa mbaraka kwa ulimwengu huu, wanawakilishwa kama jua linalochomoza mashariki, likifukuzilia mbali umande na vivuli vya giza. Macheo hugeuka na kuwa mchana. Jua, likitia rangi yake ya dhahabu, na rangi yake ya kivulivuli, na halafu likizitukuza mbingu hizo kwa nuru yake yenye ndimi za moto ni mfano wa maisha ya Kikristo. Kama mwanga wa jua ulivyo nuru na uzima na mbaraka kwa vitu vyote vilivyo na uhai, ndivyo Wakristo nao walivyo, kwa njia ya matendo yao mema, kwa uchangamfu na ujasiri wao, wanapaswa kuwa nuru ya ulimwengu. Kama mwanga wa jua unavyovifukuzilia mbali vivuli vya usiku na kumwaga utukufu wake mabondeni na vilimani, hivyo ndivyo Mkristo naye atakavyoliakisi [atakavyourudisha mwanga wa] Jua lile la Haki linalomwangazia juu yake. Mbele ya maisha manyofu ya wafuasi wa kweli wa Kristo, ujinga, ushirikina, na giza vitatoweka, kama vile jua linavyolifukuza giza la usiku. Kwa njia kama hiyo wafuasi wa Yesu watakwenda katika sehemu zenye giza ulimwenguni humu, wakitawanya nuru ya ile kweli mpaka hapo njia ya wale walio gizani itakapoangazwa kwa nuru ya ile kweli. Ni kinyume kilichoje kwa maisha ya yule anayejidai kuwa ni mwana wa Mungu ambaye amekuwa kama chumvi iliyopoteza ladha yake.... Hao wanaojigamba, ambao hawana mwanga huo wa jua, ni vivuli vya giza.... Wote wanaweza kuwa njia za kupitishia nuru hiyo iwapo watajiunganisha na yule aliye Chimbuko la nuru. Wanaweza kupeleka mionzi inayong'aa katika ulimwengu huu. Hakuna aliye na haja ya kuimarisha mashaka yake kwa kuzungumza [habari za] giza. Kila neno lenye mashaka huimarisha kutoamini. Kila wazo na neno lenye matumaini, imani, nuru, na upendo huimarisha imani na kujenga ngome moyoni itakayoweza kulipinga giza hilo la kimaadili ambalo limo ulimwenguni humu. ----- Letter 16, 1880. Wakristo wa kweli ni harufu ya uzima iletayo uzima, kwa sababu Kristo anakaa mioyoni mwao. Wanaiakisi [Wanarudisha mwanga wa] sura yake, yaani, wanakuwa watoto wa nuru. ----- MS 33, 1892. NURU YENU NA IANGAZE Oktoba 18 Vivyo hivyo nuru yenu na iangaze mbele ya watu, wapate kuyaona matendo yenu mema, wamtukuze Baba yenu aliye mbinguni. Mathayo 5:16. Kwa kila mtu anayezaliwa katika ufalme wa Kristo agizo zito limetolewa: Nuru yako na iangaze mbele ya watu, wapate kuyaona matendo yako mema, wamtukuze Baba yako aliye mbinguni. Wamwagie majirani zako miali mingi ya nuru uliyoipokea kutoka kwa Jua lile la Haki [Kristo]; wamulikie rafiki zako walio ulimwenguni kwa johari zile za nuru zinazong'aa pamoja na ile kweli uliyopewa kwa wingi kutoka kwenye kiti kile cha enzi. Hiyo ndiyo maana ya kufanya biashara kwa kutumia talanta zile ulizopewa. Endelea mbele toka kwenye nuru ndogo kwenda kwenye nuru kubwa, ukizidi kuinasa mionzi ile myeupe inayong'aa itokayo kwa yule aliye Jua la Haki, nawe uzidi kung'aa zaidi na zaidi mpaka siku ile kamilifu. ----- MS 41, 1890. Yesu hamwagizi Mkristo kujitahidi kuangaza, bali kuiacha tu nuru yake ipate kuuangazia ulimwengu kwa mionzi yake miangavu, inayoonekana wazi. Usiifunike nuru yako kwa blanketi. Usiizuie nuru yako kwa kutenda dhambi. Usiruhusu umande na ukungu na malaria ya ulimwengu huu kuizima nuru yako. Usiifiche chini ya kitanda au chini ya pishi, bali uiweke juu ya kiango, ili ipate kuwaangazia wote waliomo nyumbani.... Mungu anakuagiza uangaze, na kulipenya giza hilo la kimaadili la ulimwengu huu. ----- MS 40, 1890. Wengi hawajui jambo gani linalowasibu [linalowapata]. Wanataka nuru, wala hawaoni mwonzi wo wote wa nuru hiyo. Wanaomba msaada, wala hawasikii jibu lo lote. Je! mashaka na kutoamini kwangu vizidi kuendelea ati kwa sababu mimi sikusanyi mionzi yo yote ya nuru kutoka mbinguni kwa Yesu Kristo na kuiacha iangaze kwa wengine?... Mapambano ni makubwa sana niliyo nayo ndani ya moyo wangu mimi mwenyewe dhidi ya majaribu mengi yanayonikabili, shauku yangu niliyo nayo katika mawazo yangu na moyo wangu ya kutaka kumjua Mungu na Yesu Kristo kama Mwokozi wangu, na kuwa na hakika, amani, na kupumzika katika pendo lao [Baba, Mwana, na Roho], hunifanya mimi kuzidi kutamani kila siku kuwa mahali pale inapoweza kuniangazia mionzi ile ya Jua la Haki. Pasipo mimi kuwa na uzoefu huo, kwa kweli nitapata hasara kubwa, halafu wale wote ninaoshirikiana nao wataathirika kwa kukosa nuru ile ambayo ningestahili kuipokea kutoka kwa yule aliye Chimbuko la nuru na faraja yote, na kuweza kuwamulikia katika njia yao. Je! kweli mimi nitakuwa nuru kwa ulimwengu huu, ama kivuli cha giza? ----- MS 41, 1890. UWE MWAMINIFU PALE PALE ULIPO Oktoba 19 Akawaambia, Enendeni ulimwenguni mwote, mkaihubiri Injili kwa kila kiumbe. Marko 16:15. Kuhubiri Injili ni zaidi ya kuhutubu [kutoa hotuba]; na kazi hiyo sio ya wachungaji peke yao. Maelfu wanakaa bila kazi ambao wangekuwa wanafanya kazi kwa njia mbalimbali kwa ajili ya wokovu wa roho za watu. ----- YI, Juni 17, 1897. Wengi wanajisikia kuchochewa na ari ya kufanya makuu kwa kutoa huduma kwa wengine. Hebu hao na wajifunze kwenda kwa unyenyekevu na Mungu wao, kuwa watendaji wa Neno lake pale pale walipo. Hebu na wajifunze kutii, na kutumika katika nafasi yo yote wanayoweza kuipata. Hebu na wajifunze kufanya kazi zile zilizo duni sana, na kutambua kwamba wanamtumikia Kristo katika mazingira yo yote wanayoweza kuwekwa. Kwa kufanya kazi ya mikono iliyo duni unaweza kudhihirisha ukweli kwamba Mungu yu pamoja nawe, na ya kwamba unafanya biashara na talanta zile alizokukabidhi. Pale pale ulipo, nafasi nzuri na manufaa mengi yatajitokeza kwako, na iwapo wewe unajitahidi kumtumikia Kristo, basi, utaziona na kuzitumia vizuri. Katika mazingira duni kabisa utapata nafasi za kuonyesha msimamo wako thabiti na uaminifu wako; na iwapo wewe u mwaminifu katika kumtumikia Mungu kwa cheo kile cha chini kabisa, basi, utadhaminiwa kupewa madaraka ya juu zaidi. Kama wewe u mwaminifu katika mambo machache, basi, uaminifu wako utakushuhudia ya kwamba wewe u mwanafunzi katika shule ya Kristo, na ya kwamba unaukuza uwezo wako wa kumtumikia katika maeneo makubwa zaidi. ----- YI, Nov. 7, 1895. Tunaukaribia mwisho ule wa kufungwa kwa historia ya ulimwengu huu; karibu sana tutasimama mbele za kiti kile cha enzi, kikubwa, cheupe. Nafasi zako nzuri za kufanya kazi zitakuwa zimepita. Kwa hiyo, fanya kazi wakati inapoitwa leo. Kwa msaada wa Mungu, kila muumini wa kweli anaweza kuona mahali ilipo kazi ya kufanya. Mapenzi ya mwanadamu yanaposhirikiana na mapenzi ya Mungu, yanakuwa na uwezo mkuu mno, na mtenda kazi anaweza kufungua nafasi nyingi zilizo nzuri. Kesha kwa ajili ya watu wale unaokutana nao. Tafuta nafasi nzuri za kuwaambia neno linalofaa kwao. Usingoje kutambulishwa kwao, au mpaka uwe umefanya urafiki nao kabla hujajitahidi kuwaokoa watu hao wanaoangamia ambao wanakuzunguka. Iwapo utakwenda kufanya kazi hiyo kwa bidii, basi, njia zitafunguliwa mbele yako za kukuwezesha kuitimiza kazi hiyo. Tegemea mkono wa Mungu kwa hekima, nguvu, na ustadi wa kufanya kazi ile ambayo Mungu amekupa wewe kufanya. ----- YI, Juni 24, 1897. TABIA YA WAJUMBE WA KRISTO Oktoba 20 Basi tu wajumbe [mabalozi] kwa ajili ya Kristo, kana kwamba Mungu anasihi kwa vinywa vyetu; twawaomba ninyi kwa ajili ya Kristo mpatanishwe na Mungu. 2 Wakorintho 5:20. Kila Mkristo wa kweli atajisikia kuwa anacho kitu fulani cha kufanya kwa ajili ya wokovu wa roho za watu. ----- RH, Mei 29, 1900. Unapomkaribia mgeni ye yote, unaposimama ana kwa ana na yule asiyetaka kutubu, yule anayeteswa, na mwenye njaa ya rohoni, [kumbuka kwamba] Bwana yu kando yako kama wewe mwenyewe umejitoa kweli kwake. Anaugusa moyo wako. Lakini huenda wewe unaweza kuwa chombo chake kwa kazi yake ile ya neema.... Wale wanaoitangaza kweli wanapaswa kujificha ndani ya Yesu; yeye ndiye umashuhuri wao, uwezo wao, na ufanisi wao. Yawapasa kuzipenda roho za watu kama yeye alivyozipenda, kutii kama yeye alivyofanya, kuwa na heshima, na kujawa na huruma nyingi. Yawapasa kupambana kwa nguvu zao zote dhidi ya kasoro ndogo ndogo sana za tabia ambazo wanazo ndani yao wenyewe. Yawapasa kumwakilisha Yesu. Katika kila tendo anatakiwa aonekane yeye. ----- RH, Aprili 12, 1892. Yule awezaye kusoma mioyo ya wanadamu... anajua hali inayoizunguka kila roho. Anajua ni mapambano mangapi na makali kiasi gani ambayo roho ya mwanadamu inafanya ili kuishinda mielekeo mibaya aliyorithi kwa njia ya kuzaliwa kwake pamoja na dhambi zile zilizogeuka na kuwa mazoea yake kwa kuzitenda tena na tena.... Maelfu... wanakabiliwa na majaribu yaliyoandaliwa na Shetani kwa werevu sana, tena hawamjui Mungu, wala Yesu Kristo aliyemtuma ulimwenguni kuwaokoa wenye dhambi wakuu kupindukia. Lo! mbona hatutambui sehemu yetu ya kazi tunayotakiwa kufanya katika mpango huo mkuu wa ukombozi?... Ndani ya kila moyo ulioongoka itakuwamo huruma ya kweli, iliyotakaswa, kuhusiana na mateso yale aliyopata Kristo, yaani, yale aliyostahimili ili kuwaokoa wenye dhambi. Kama wao ni watenda kazi pamoja na Kristo, basi, wataushinda moyo ule wa kupenda starehe, kujifurahisha nafsi, kujiachilia katika tamaa za mwili, kisha watakua katika nyama na musuli wao wa kiroho kwa kuzitumia nguvu walizopewa na Mungu katika kuziongoa roho za watu kwa Yesu Kristo. Kazi hiyo iliyoteuliwa na Mbingu imekusudiwa kutupatia uzoefu na tabia ya Kikristo yenye upana na kina na utengemano [uthabiti], na kuwaunganisha watenda kazi pamoja na Mungu katika mazingira yale ya juu, yaliyo safi, ambako upendo wao kwa Kristo utakuwa unazidi kuongezeka daima na upendo wao kwa wanadamu wenzao utazidi kuongezeka zaidi na zaidi. ----- MS 41, 1890. JE, NINAMWAKILISHA BWANA WANGU IPASAVYO? Oktoba 21 Ninyi ni mashahidi wangu, asema BWANA, na mtumishi niliyemchagua. Isaya 43:10. Iwapo waumini wanafanya urafiki na wale wasioamini kwa kusudi la kuwaleta kwa Kristo, basi, watakuwa mashahidi wake Kristo, na baada ya kutekeleza utume wao huo, watajitenga ili kuvuta hewa safi na takatifu. Wataweza kumkaribia Mungu, na kupeleka dua zao juu kwa Kristo kwa niaba ya rafiki zao na wale wanaoshirikiana nao, wakijua kwamba anaweza kuwaokoa kabisa wale wote wamjiao Mungu kwa yeye. Unapokuwa katika jamii ya wasioamini, kumbuka daima kwamba kwa tabia yako wewe u mwakilishi wake Yesu Kristo, usiruhusu maneno ya kipuuzi, na yale yasiyo na maana, yaani, maongezi ya kipuuzi, kutoka kinywani mwako. Zingatia thamani ya roho ya mtu, nawe kumbuka kwamba ni haki yako na wajibu wako kwa kila njia inayowezekana kuwa mtenda kazi pamoja na Mungu. Usijishushe hadhi yako ili upate kuwa sawa na wale wasioamini, na kucheka na kusema maneno yasiyo na maana kama wao wanavyofanya. Kwa kufanya hivyo... unajiweka katika hali moja na mwenye dhambi yule. Mwenendo kama huo utakufanya uwe kikwazo katika njia ya wenye dhambi.... Roho Mtakatifu anapougusa moyo wetu, ingetupasa kushirikiana na mvuto wake unaozibadilisha tabia zetu, nasi tutakuwa na hamu ya kupata mambo yale yaliyo bora, ufahamu safi wa ile kweli, upole, kuwa wepesi kufundishwa, tena tutaweza kuitekeleza kazi yetu kwa unyenyekevu. Hiyo ndiyo njia ambayo kwayo wewe utaweza kumjua vema Mungu, na kumjua Mungu ni haki ya Mkristo. Hapo ndipo unaweza kufanya kazi kwa ajili ya wale wasioongoka, na jamii ya wasioamini haitakuletea madhara yo yote, kwa kuwa maisha yako yatakuwa yamefichwa pamoja na Kristo katika Mungu, nawe utatafuta urafiki kwa wale walio nje ya Kristo kwa madhumuni ya kuwaongoa wapate kumtumikia yeye. Umoja wako na Mungu hukufanya uwe na nguvu kiroho, ili upate kustahimili mivuto yo yote mibaya inayoweza kutoka kwao.... Hakikisha kwamba wewe mwenyewe unajiweka katika njia ile ya nuru, na kwa matendo yako unakuwa mfuasi wake yeye aliyekwenda huku na huku "akitenda mema." ----- Letter 51, 1894. KUPANDA MBEGU ZA ILE KWELI Oktoba 22 Asubuhi panda mbegu zako, Wala jioni usiuzuie mkono wako. Kwa maana wewe hujui ni zipi zitakazofanikiwa, kama ni hii au hii, au kama zote zitafaa sawasawa. Mhubiri 11:6. Sisi tunaokiri kuwa watoto wa Mungu, tuko chini ya jukumu zito sana la kuwatafuta na kuwaokoa wale waliopotea.... Mungu anakutaka wewe kushirikiana na waumini pamoja na wale wasioamini, ili upate kuwasaidia wote kuifahamu kweli kwa ukamilifu zaidi. Fahamiana na wale unaodhani kwamba unaweza kuwasaidia; kisha unapoanza kuongea nao usiongee maneno yasiyo na maana, wala upumbavu, bali waambie mambo yale ya thamani yatokayo kwa Mungu.... Malaika wa Mungu wataigusa mioyo yao, iwapo katika roho ya Kristo wewe utajitahidi kuwafikia na kuwasaidia watu hao. ----- MS 81, 1909. Po pote pale ulipo, nuru yako na iangaze. Wagawie magazeti na vijizuu wale unaoshirikiana nao, wakati unaposafiri kwa magari, unapowatembelea watu, unapoongea na majirani zako; nawe uitumie vizuri kila nafasi kwa kusema neno linalofaa kwa wakati huo.... Tungeikuza tabia ile ya upole na heshima katika uhusiano wetu na wale tunaokutana nao. Hebu... na tujitahidi kuifundisha kweli kwa njia rahisi. Kweli hiyo inamaanisha uzima, yaani, uzima wa milele kwa yule anayeipokea. Jifunze, basi, kupita kwa urahisi na kwa heshima kutoka kwenye masomo ya kidunia kwenda kwenye masomo ya kiroho na ya milele.... Unapotembea njiani, au kuketi kando ya njia, unaweza kuweka ndani ya moyo fulani mbegu ya ile kweli. ----- CH 435. Ipo kazi ya kufanya kwa ajili ya Bwana wetu. Kuna watu wanaoweza kuletwa kwa Kristo kutokana na mvuto wetu. Ni nani aliye tayari kuingia katika kazi hiyo kwa moyo wake wote?... "Wako ni wakati wa kupanda mbegu; Ni Mungu peke yake aonaye kile kilichopandwa; Kupita upeo wetu, wenye upungufu na usioona vizuri, Wakati wa mavuno umefichwa huko kwake; Lakini haijasahauliwa mahali ilipo, Ile mbegu ya kujitoa mhanga kwa ukarimu wako, Japo ionekane kana kwamba imetupwa jangwani, Itachipuka na kuchanua na matunda yatatokea hatimaye. ----- ST, Jan. 19, 1882. KESHA, OMBA, FANYA KAZI Oktoba 23 Imetupasa kuzifanya kazi zake yeye aliyenipeleka maadamu ni mchana, usiku waja asipoweza mtu kufanya kazi. Yohana 9:4. Laiti kama Leja ile ya Mbinguni ingaliweza kufunguliwa mbele yetu, tungeshangaa sana kuona sehemu kubwa ya wale wanaojidai kuwa Wakristo ambao hawachangii cho chote katika kuujenga ufalme wa Kristo, ambao hawafanyi juhudi yo yote kwa ajili ya wokovu wa roho za watu. Hao ni watumwa [watumishi] walegevu. Wengi wanaoridhika kutofanya mema mengi, hujigamba kwamba hawafanyi ubaya wo wote kwa kadiri wao wasivyowapinga watenda kazi wenye bidii wanaofanya kazi. Lakini kundi hilo linafanya madhara makubwa kwa mfano wao.... Mtumwa yule mlegevu [mvivu] hakulaumiwa kwa kile alichofanya, bali kwa kile ambacho hakufanya. Hakuna adui aliye wa hatari sana kwa kazi ya Mungu kama Mkristo mvivu. Anayekufuru waziwazi anafanya madhara kidogo tu, maana hawezi kumdanganya mtu ye yote; anaonekana kama alivyo hasa, yaani, yeye ni mchongoma, mwiba. Wale wasiofanya kitu cho chote hao ndio kipingamizi kikubwa sana. Wale wasiotaka kubeba mizigo yo yote, wanaokwepa kazi zote zile zisizopendeza, ndio wa kwanza kunaswa na mtego wa Shetani, yaani, ndio wa kwanza kuutumia mvuto wao kwa njia mbaya. Kesha, Omba, Fanya Kazi ----- hayo ndiyo maneno ya kumlinda Mkisto. Wasiwepo wale wanaotoa udhuru wao ili wasifanye kazi ya kuziokoa roho za watu. Wasiwepo wanaojidanganya wenyewe kwa kuamini kwamba hakuna kitu cho chote kinachotakiwa kutoka kwao. Hakuna kitu pungufu kinachotakiwa kwa ye yote kuliko kile kilichotazamiwa kwa mtu yule mwenye talanta moja. ----- RH, Mei 1, 1883. Kuna kazi ya kufanya kwa ajili ya Kristo katika familia zetu, katika ujirani wetu, na kila mahali. Kwa kuwatendea mema maskini, wagonjwa, au wafiwa, tunaweza kuwa na mvuto juu yao, ili kweli ile ya mbinguni ipate nafasi ya kuingia mioyoni mwao. Nafasi nzuri za kutumika ziko kila upande. Wote waliojazwa na roho ya Kristo watajionyesha wenyewe kuwa ni matawi yanayozaa matunda ya Mzabibu ule ulio hai.... Ni juu yetu kujiwekea kumbukumbu tunayotaka kukutana nayo baadaye. Je, tungependa kurasa zake zijazwe na historia inayoonyesha bidii yetu katika kazi ya Mungu na wanadamu? Basi, na tufuate katika nyayo zake yule aliyesema, "Imetupasa [Imenipasa] kuzifanya kazi zake yeye aliyenipeleka maadamu ni mchana, usiku waja asipoweza mtu kufanya kazi." Yohana 9:4 [KJV]. ----- RH, Mei 1, 1883. "KILA MTU KAZI YAKE" Oktoba 24 Mfano wake ni kama mtu mwenye kusafiri, ameiacha nyumba yake, amewapa watumwa wake amri, na kila mtu kazi yake, naye amemwamuru bawabu akeshe. Marko 13:34. Tuna kazi kila mtu yake, yaani, uwajibikaji wa mtu mmoja mmoja, taarifa inayotakiwa kutolewa na kila mtu, tena ni wokovu wetu wenyewe tunaopaswa kujipatia, maana ni suala linalomhusu mtu mmoja mmoja.... Utauwa [uchaji Mungu] na utii wa watu wengine hautatuokoa sisi, wala hawatafanya kazi yetu. Juhudi zao hazitaandikwa kamwe kama zetu mbele ya majina yetu.... Mungu ameacha kwa kila mmoja wetu kazi yake ----- sio kazi ile ya kawaida ya maisha, kama vile kupanda miche, kupanda mbegu, na kukusanya mavuno, bali ni ile ya kuujenga ufalme wake, yaani, kuwajulisha watu maarifa ya ile kweli, na kuiona hiyo kuwa ndiyo kazi yetu ya kwanza na ya juu kuliko zote. Mungu ana madai juu yetu. Ametupa uwezo na kutupa nafasi, iwapo sisi tutaweza kuziona na kuzitumia vizuri. Majukumu hayo kwa Mungu hakuna mwingine awezaye kuyatekeleza isipokuwa ni sisi wenyewe, mmoja mmoja. Uhalifu [makosa] wa wengine... hautakuwa udhuru kwa ye yote kuiga mfano wao, kwa sababu Kristo ameinuliwa juu kama Kielelezo chetu cha pekee ----- hana waa, ni mtakatifu, hajatiwa unajisi [uchafu] wo wote.... Kuna wale wanaoshirikiana pamoja kufanya maovu, nao huonekana kufikiri kwamba katika jambo hilo wanapoteza uwajibikaji wao wa mtu mmoja mmoja. Lakini Mungu anawashikilia kuwa wanahusika kwa kila tendo lililofanyika ambalo lina mwelekeo wa kuipinga kazi ya Kristo hata kwa kiwango kidogo sana; si kitu kama wamejiunga na watu wengi, ama na watu wachache sana, dhambi ni ile ile moja. Tunawajibika kila mtu peke yake. Tungekuwa na wasiwasi juu yetu wenyewe. Je, tunaujenga ufalme wa Kristo kwa maneno na matendo yetu yote, au tunaubomoa? Yesu asema kwa kila mmoja wetu, "Nifuate." Basi, na tuonekane kwamba sisi tu wafuasi wa Yesu Kristo. ----- MS 15, 1885. Sasa ndio wakati wa kufanya kazi. Sasa ndio wakati wetu wa kujenga tabia kwa mfano wa yule wa Mbinguni [Kristo].... Kama sisi tunamjua Kristo, basi, tutamdhihirisha kwa wengine. "Kama vile ulivyonituma mimi ulimwenguni, nami vivyo hivyo naliwatuma hao ulimwenguni." Yohana 17:18. Alikuja duniani humu kumwakilisha Baba yake, na kazi ile aliyotupa sisi ni ya kuiwakilisha tabia yake [katika maisha yetu]. Hatuwezi kusamehewa ili tusiweze kuifanya kazi hiyo. ----- Letter 42, 1890. KANISA DOGO NYUMBANI Oktoba 25 Lakini hakumruhusu, bali alimwambia, Enenda zako nyumbani kwako, kwa watu wa kwenu, kawahubiri ni mambo gani makuu aliyokutendea Bwana, na jinsi alivyokurehemu. Marko 5:19. Katika kujenga uhusiano wake na Kristo, mtu yule aliyefanywa upya ni kwamba anarudia tu uhusiano ule uliowekwa kati yake na Mungu. Yeye anakuwa mwakilishi wa Kristo.... Majukumu yake yako kila upande, hapa karibu na kule mbali. Jukumu lake la kwanza ni kwa watoto wake na ndugu zake wa karibu sana. Hakuna kitakachompa udhuru wa kuacha kuwahudumia wale wanaomzunguka huko nje. Katika siku ile ya mwisho ya kutoa hesabu akina baba na akina mama watapaswa kujibu hoja ya watoto wao. Wazazi wataulizwa walifanya nini na kusema nini ili kuwapatia wokovu watu wale ambao ni wao wenyewe waliojitwika jukumu la kuwaleta duniani.... Enyi akina baba na mama, je! mnawaruhusu watoto wenu kukua katika uchafu na dhambi? Wema mwingi uliofanywa kwa ajili ya wengine hautalifuta deni mnalowiwa na Mungu katika kuwalea watoto wenu. Usitawi wa kiroho wa familia yenu unakuja kwanza. Wachukueni pamoja nanyi kwenda nao kwenye msalaba ule wa Kalvari, mkijitahidi kwa ajili yao kama watu watakaotoa hesabu. Wazazi wangejitahidi kupata ushirikiano wa watoto wao. Hivyo watoto wao wanaweza kuwa watenda kazi pamoja na Mungu. Baadhi ya nyumba zina kanisa dogo nyumbani mwao. Upendo kati yao unaufunga moyo huu kwa moyo ule mwingine, na umoja unaokuwamo miongoni mwa watu waliomo katika familia hiyo unahubiri hubiri moja lenye nguvu sana ambalo lingeweza kuhubiriwa juu ya utauwa kwa matendo. Wazazi wanapofanya kazi yao kwa uaminifu, wakiwazuia, wakiwakosoa, wakiwaonya, wakiwashauri, wakiwaongoza, baba akiwa kama kuhani wa nyumba hiyo, mama akiwa kama mmishonari wa nyumbani humo, basi, hapo ndipo watakuwa wanalijaza eneo [la mamlaka] ambalo Mungu angetaka walijaze. Kwa kufanya kazi yao kwa uaminifu nyumbani mwao, wanaongeza njia za kufanya mema huko nje ya nyumba hiyo. Wanakuwa katika hali bora inayofaa kufanya kazi ndani ya kanisa. Kwa kulilea kundi lao dogo kwa akili, wakiwafunga watoto wao kwao wenyewe na kwa Mungu, akina baba na mama wanakuwa watenda kazi pamoja na Mungu.... Watu waliomo ndani ya familia hiyo huwa watu wa familia ile ya kifalme huko juu, watoto wa Mfalme yule wa mbinguni. ---- - MS 56, 1899. HAKUNA KUSIMAMA KATIKATI KATIKA KAZI YA MUNGU Oktoba 26 Mtu asiye pamoja nami yu kinyume changu; na mtu asiyekusanya pamoja nami hutapanya. Mathayo 12:30. Ee ndugu zangu Wakristo, tuko mbali na kukifikia kipimo kile kitakatifu. Matendo yetu hayalingani na haki ile aliyotupa pamoja na wasaa huu tuliopewa.... Katika kazi ya Bwana hakuna kusimama katikati [kutojihusisha upande huu au ule].... Hebu na asiwepo mtu ye yote anayetazamia kupatana na ulimwengu huu, kisha kuweza kuifurahia baraka ya Bwana. Hebu watu wa Mungu na watoke katika ulimwengu huu, na kujitenga nao. Na tujaribu kwa bidii zaidi kuyajua na kuyafanya mapenzi ya Baba yetu aliye mbinguni. Nuru ya ile kweli ambayo imetuangazia sisi na ipokewe kwa njia ambayo mionzi yake inayong'aa inaweza kuangaza kutoka kwetu kwenda kwa ulimwengu. Wale wasioamini na waone ya kwamba imani tuliyo nayo inatufanya sisi kuwa wanaume na wanawake wema zaidi; ya kwamba hiyo ndiyo kweli hai, inayoitakasa tabia yetu, na kuyabadilisha maisha yetu.... Maongezi yetu na yawe juu ya mambo yale ya mbinguni. Hebu na tujizungushie mazingira ya uchangamfu wa Kikristo. Hebu na tuonyeshe kwamba dini yetu inaweza kustahimili mtihani wa maonjo. Kwa upole, ustahimilivu, na upendo wetu hebu na tuuhakikishie ulimwengu juu ya uwezo wa imani yetu. Wengi wanaoianza vizuri safari ya maisha yao ya Kikristo huendelea kupoteza nguvu yao ya kiroho, na kujiweka wenyewe katika uwezo wa yule adui, kwa kujiachilia kuwa na maongezi yasiyo na maana na ya kipuuzi. Hawawezi kumtazama Mungu juu kwa ujasiri ulio mtakatifu na kuomba nguvu wanayoihitaji. Kwa mwenendo wao huo usiokuwa wa kidini wanazuia njia kwa watu hao ambao wangeweza kuja kwa Kristo. Hebu hao wasiojali kuongea mambo ya kipuuzi na wakumbuke kwamba kila neno na tendo [linanaswa na] linapigwa picha [kama kanda ya video] katika vitabu vile vya mbinguni. Hakuna mkono wa mwanadamu ye yote uwezao kufuta doa moja la aibu humo.... Tunapokutana kila siku na wale ambao hawamjui Kristo na kweli yake, je! tuongee tu juu ya mashamba yetu, biashara zetu, faida na hasara zetu; au tuongee habari za mambo yale yanayohusu maisha yetu ya baadaye? Ni aibu ilioje inayobaki imeandikwa humo dhidi ya wale wanaojidai kuwa ni wafuasi wake Kristo kwa kuacha kufanya wajibu wao! Hebu na tujichunguze kwa undani sana kwa nuru ile inayotoka katika Neno la Mungu, tujaribu kugundua kila kasoro tuliyo nayo katika tabia zetu, ili tupate kuyafua mavazi yetu na kuyafanya meupe katika damu ya Mwana-Kondoo. ----- RH, Juni 15, 1886. UJIRA WA KUFANYA KAZI Oktoba 27 Ni vema mwanadamu aichukue nira wakati wa ujana wake. Maombolezo 3:27. Mungu anawaita vijana wanaume kwa wanawake kuingia katika kazi yake. Vijana ni wepesi kupokea [mafundisho], wana nguvu, wana hamasa [wako motomoto], na matumaini. Wakionja mara moja roho ile ya kujitolea, basi, hawataridhika wasipojifunza daima kwa Mwalimu yule Mkuu.... Tunapofanya kazi tukiwa tumeungana na Mwalimu huyo Mkuu, uzoefu wetu utazidi kuongezeka. Uwezo wa akili utapanuka. Dhamiri itakuwa chini ya uongozi wa Mungu. Kristo atautawala mwili wote. Tu salama pale tu tunapomruhuru kufanya hivyo kwetu; kwa maana kuna [mjamaa] mwingine aliye karibu nasi, anayetafuta nafasi ya kuingia ndani yetu na kuanza kazi yake ya uharibifu, yaani, ya kutunasa. Basi, tunapoingia katika kazi ya Mungu, hebu na tumruhusu kuutwaa mwili wetu wote, yaani, mwili, roho, pamoja na nafsi.... Hakuna awezaye kuunganishwa na Kristo kweli kweli, yaani, yule anayejizoeza kuyatenda mafundisho yake, akiwa ananyenyekea na kuivaa nira yake inayomdhibiti, ambaye hawezi kutambua kile ambacho yeye hawezi kamwe kukieleza kwa maneno. Mawazo mapya, bora, humjia. Akili yake hupewa nuru, mapenzi yake hupewa mwelekeo thabiti, dhamiri yake huwa nyororo, mawazo yake huwa safi. ----- MS 18, 1901. Vijana wanaume kwa wanawake walioongoka kweli kweli watajitenga na maovu yote.... Endapo wataona jinsi dhambi inavyochukiza, kisha wataichukia kuwa ni kitu kibaya kama vile ilivyo hasa, na kuja kwa Yesu kwa moyo wa toba, wakijitakasa nafsi zao kwa kuitii kweli, hapo ndipo wanaweza kudhaminiwa kupewa sehemu fulani ya kazi ili wapate kuifanya.... Mungu anausoma moyo, anaipima tabia katika mizani, naye anaijua kazi ya kila mtu. Anatoa Roho wake kwa kipimo kinacholingana na kujitoa wakf na kujitoa mhanga kwa wale wanaoonyesha tabia hizo ambao wanaingia katika kazi yake. ----- RH, Mei 20, 1890. Vijana wana nguvu. Hawalemewi na mzigo wa miaka mingi [uzee], pamoja na masumbufu yake. Mapenzi yao yako motomoto, na kama hayo yataondolewa yasishughulike na mambo ya ulimwengu huu, na kuwekwa juu ya Kristo na mbingu, wakiwa wanafanya mapenzi ya Mungu, basi, hapo watakuwa na tumaini la maisha bora ya kudumu, tena wataishi milele, wakivikwa utukufu, heshima, kutokufa, na uzima wa milele. ----- RH, Machi 30, 1886. JIHADHARI NA KUJIAMINI MWENYEWE Oktoba 28 Petro akamwambia, Bwana, kwa nini mimi nisiweze kukufuata sasa? Mimi nitautoa uhai wangu kwa ajili yako. Yesu akamjibu, Je! wewe utautoa uhai wako kwa ajili yangu? Amin, amin, nakuambia, Jimbi [Jogoo] hatawika hata wewe utakapokuwa umenikana mara tatu. Yohana 14:37,38. Muda mfupi tu kabla ya anguko lake Petro, Kristo alimwambia, "Simoni, Simoni, tazama, Shetani amewataka ninyi apate kuwapepeta kama vile ngano." Luka 22:31. Ni urafiki wa kweli ulioje aliokuwa nao Mwokozi kwa Petro! Onyo lake limejaa huruma jinsi gani! Lakini basi, onyo lile lilichukiwa. Kwa kujitosheleza mwenyewe Petro alitangaza kwa imani kwamba asingeweza kamwe kufanya kile alichomwonya Kristo kuwa atafanya, ""Bwana," akasema, "niwapo pamoja na wewe, mimi ni tayari kwenda gerezani au hata kifoni." Kule kujiamini mwenyewe kulithibitisha kuangamia kwake. Alimjaribu Shetani ili naye apate kumjaribu, akaanguka chini ya hila za yule adui mwerevu sana. Kristo alipomhitaji sana, akawa amesimama upande wa yule adui, na kwa waziwazi akamkana Bwana wake.... Wengi leo husimama mahali pale pale aliposimama Petro alipotangaza kwa kujiamini ya kwamba hangeweza kumkana Bwana wake. Na kwa sababu ya kujitegemea kwao, wanatekwa kwa urahisi na mbinu za Shetani. Wale wanaoutambua udhaifu wao hutegemea nguvu iliyo juu kuliko nafsi zao. Na kwa wale wanaomtegemea Mungu, Shetani hana nguvu dhidi yao. Lakini wale wanaojiamini wenyewe wanashindwa kwa urahisi. Hebu na tukumbuke kwamba kama hatujali maonyo ya hatari anayotupa Mungu, basi, anguko li mbele yetu. Kristo hatamwokoa asipate majeraha yule anayejiweka mwenyewe kwenye uwanja wa yule adui bila kualikwa. Anamwacha yule anayejitegemea, yaani, yule anayejifanya kana kwamba anajua mengi kuliko Bwana wake, ili aendelee mbele katika nguvu zake mwenyewe anazodhani kwamba anazo. Ndipo maumivu humjia pamoja na maisha yaliyopungua nguvu zake au pengine hushindwa na kufa. Katika pambano hili adui anatumia kwa manufaa yake ule udhaifu walio nao wale anaowashambulia kama kinga yake. Hapo [penye udhaifu] anafanya mashambulio yake makali sana. Mkristo asiwe na udhaifu wo wote [kitabia] katika kujihami kwake. Angejiwekea kizuizi [ngome] cha Maandiko yanayompa msaada yule afanyaye mapenzi ya Mungu. Yule anayejaribiwa atapata ushindi akifuata kielelezo cha yule aliyepambana na mjaribu akitumia neno hili, "Imeandikwa." Anaweza kusimama imara katika ulinzi wa maneno haya yasemayo, "Hivi ndivyo asemavyo Bwana." ----- MS 115, 1902. NGUVU KATIKA MBIO ZA KIKRISTO Oktoba 29 Je! hamjui, ya kuwa wale washindanao kwa kupiga mbio, hupiga mbio wote, lakini apokeaye tuzo ni mmoja? Pigeni mbio namna hiyo, ili mpate. Na kila ashindanaye katika michezo hujizuia katika yote; basi hao hufanya hivyo kusudi wapokee taji iharibikayo; bali sisi tupokee taji isiyoharibika. 1 Wakorintho 9:24,25. Ili kumtolea Mungu huduma yetu iliyo kamilifu, inatupasa kuwa na dhana [fikra] zilizo dhahiri kuhusu mapenzi yake. Jambo hilo litatutaka sisi kutumia chakula kile tu kinacholeta afya mwilini, kilichotengenezwa kwa njia ya kawaida, ili neva ndogo za ubongo zisidhurike, na kufanya iwe vigumu kwetu kutambua thamani ya upatanisho, na thamani isiyokadirika ya damu ya Kristo itakasayo.... Iwapo, kwa lengo lile lisilokuwa la juu kuliko lile la kupata shada la maua au taji iharibikayo kama thawabu ya shauku yao kuu, wanadamu walijiweka chini ya sharti la kuwa na kiasi katika mambo yote, je! si zaidi sana kwa wale wanaokiri kutafuta, sio tu taji ile isiyonyauka ya utukufu wa milele, bali maisha yale ambayo yatadumu kadiri kiti cha enzi cha Yehova kitakavyoendelea kuwako, na utajiri ule wa milele, yaani, heshima zile zisizoweza kuharibika, na utukufu ule wa milele uzidio kuwa mwingi sana. Je! motisha [vivutio] zilizowekwa mbele ya wale wanaopiga mbio katika mashindano ya mbio zile za Kikristo hazitawafanya wajizoeze kujikana nafsi na kuwa na kiasi katika mambo yote?... Kwa shauku ya dhati, yenye nguvu, katika kufanya mapenzi ya Mungu, tungekuwa na ari kubwa sana kuipita ile waliyo nayo wale wanaoshughulika katika shughuli mbalimbali za kibiashara, kwa kiwango kikubwa zaidi kama vile ilivyo thamani ya kitu kile tunachotafuta kukipata. Hazina ile ambayo sisi tunajitahidi kuipata haiharibiki, ni ya milele, tena inao utukufu kabisa; ambapo ile anayoitafuta mtu wa ulimwengu huu inadumu kwa siku moja tu.... Na usiwe ndio wasiwasi wetu mkuu kutaka kufanikiwa katika ulimwengu huu; bali mzigo wa nafsi zetu na uwe hivi, Nitawezaje kuipata dunia ile iliyo bora zaidi? Je, nifanye nini nipate kuokoka?... Mahali ambapo wote wanapaswa kupafikia ni kuuthamini wokovu kuliko faida ya ulimwengu huu, wakihesabu kila kitu kuwa hasara ili wampate Kristo. Kujitoa wakf lazima kuwe kamili kabisa. Mungu hatakubali kuzuia kitu cho chote, wala kafara iliyogawanyika, wala sanamu. Wote ni lazima waifie nafsi yao pamoja na ulimwengu huu. Basi, kila mmoja wetu na ajitoe wakf kila siku kwa Mungu. Uzima wa milele unastahili kuupa juhudi yote ya maisha yetu, ustahimilivu wetu, tena pasipo kuchoka. ----- RH, Machi 18, 1880. "JITUNZE NAFSI YAKO" Oktoba 30 Jitunze nafsi yako, na mafundisho yako. Dumu katika mambo hayo; maana kwa kufanya hivyo utajiokoa nafsi yako na wale wakusikiao pia. 1 Timotheo 4:16. Agizo hilo lililotolewa kwa Timotheo linapaswa kuzingatiwa katika kila nyumba, na kuwa ndiyo mamlaka ya kufundishia katika kila familia na kila shule.... Lengo kuu kuliko yote la vijana wetu lisingekuwa kujitahidi sana kupata kitu fulani kipya. Hapakuwa na kitu kama hicho katika fikra na kazi ya Timotheo. Yawapasa kukumbuka kwamba, mikononi mwa yule adui wa mema yote, maarifa peke yake yanaweza kuwa uwezo wa kuwaangamiza wenyewe. Alikuwa ni yule kiumbe mwenye akili nyingi sana, yule aliyekalia cheo cha juu miongoni mwa halaiki ile ya malaika, ambaye mwishowe aligeuka na kuwa mwasi; na wengi wa wale walio na mafanikio makubwa kiakili sasa wanatekwa kwa uwezo wake [Shetani]. Vijana wangejiweka wenyewe chini ya mafundisho ya Maandiko Matakatifu, na kuyaweka kila siku katika mawazo na maisha yao kwa matendo. Hapo ndipo watakuwa nazo sifa za tabia zinazowekwa katika daraja la juu kabisa katika majumba yale ya kifalme kule mbinguni. Watajificha wenyewe ndani ya Mungu, na maisha yao yatashuhudia utukufu wake. ----- YI, Mei 5, 1898. "Jitunze nafsi yako, na mafundisho yako." Wewe mwenyewe unahitaji kuangaliwa kwanza. Jitoe kwanza wewe mwenyewe kwa Bwana ili upate kutakaswa kwa ajili ya kazi yake. Kielelezo chako cha utauwa kitakuwa na nguvu kwa ajili ya ile kweli kuliko ufasaha mkuu sana usioambatana na maisha mazuri. Tengeneza taa ya roho yako, na kuijaza mafuta ya Roho. Tafuta kwake Kristo neema, yaani, ufahamu ulio wazi kama ule, ambayo itakuwezesha kufanya kazi kwa mafanikio. Jifunze kwake maana ya kuwashughulikia wale aliotoa uzima wake kwa ajili yao. Mtenda kazi mwenye talanta nyingi anaweza kufanya kazi kidogo tu, isipokuwa kama Kristo ameumbika ndani yake, tumaini na nguvu ya uzima. ----- 7BC 916. Utu uzima ulio mkamilifu na wenye tabia nzuri hauji kwa nasibu. Ni matokeo ya kujenga tabia katika miaka ile ya mwanzo ya ujana, ni kujizoeza [kuitii] sheria ya Mungu nyumbani. ----- YI, Mei 5, 1898. Mungu anangoja kuwatia nguvu [kuwavuvia] vijana kwa uweza ule unaotoka juu, ili wale wote wanaosimama chini ya bendera ile ya Yesu Kristo yenye alama ya damu wapate kufanya kazi ile ya kuwaita, kuwaonya, na kuwaongoza watu katika njia zile zilizo salama, na kuikita miguu ya wengi juu ya ule Mwamba wa Kale. ----- Letter 66, 1894. "WAFANYA KAZI PAMOJA NA MUNGU" Oktoba 31 Maana sisi tu wafanya kazi pamoja na Mungu; ninyi ni shamba la Mungu, ni jengo la Mungu. 1 Wakorintho 3:9. Mwanadamu hawezi kuvutwa kwa kamba kwenda mbinguni; hawezi kwenda huko kama msafiri anayekaa chini bila kufanya kitu cho chote. Yeye mwenyewe ni lazima ayatumie makasia, na kufanya kazi kama mfanya [mtenda] kazi pamoja na Mungu. ----- Letter 135, 1897. Kama unadhani kwamba unaweza kuacha kupiga makasia, na bado ukaweza kwenda upande wa juu wa mto, basi, umekosea. Ni kwa juhudi ya dhati tu, yaani, kwa kuyatumia makasia hayo kwa nguvu zako zote, ndipo unaweza kwenda juu na kuupinga mkondo huo wa maji. Ni wangapi walio dhaifu kama maji, wakati wanaye yule aliye Chimbuko la nguvu lisiloweza kushindwa kamwe! Mbingu i tayari kutugawia ili tupate kuwa na nguvu katika Mungu wetu, na kukua kukifikia kimo cha wanaume na wanawake cha cheo cha utimilifu wake Kristo Yesu. Lakini ni akina nani kati yenu waliokuwa wakifanya maendeleo katika njia ile ya utakatifu katika mwaka huo uliopita?... Ni akina nani waliowezeshwa kupata ushindi wa thamani mmoja baada ya mwingine, mpaka wivu, kiburi, nia ya kudhuru wengine, kijicho, na kila aina ya waa la dhambi vimefagiliwa mbali nao, na matunda ya Roho peke yake yamebaki?... Mungu atatusaidia kama tutaushikilia msaada wake aliotupa. "Au azishike nguvu zangu, Afanye amani nami; Naam, afanye amani nami." Isaya 27:5. Hiyo ndiyo ahadi yenye mibaraka. Mara nyingi mimi ninapokuwa nimekata tamaa na kuwa karibu sana na kufa moyo kabisa, nimeweza kumjia Bwana na ahadi hiyo.... Na ninapozishika nguvu za Mungu, napata amani ipitayo ufahamu wote. ----- MS 1, 1869. Kuna nguvu kuu mbili zinazofanya kazi katika wokovu wa roho ya mwanadamu. Unahitajika ushirikiano wa mwanadamu na nguvu zile za mbinguni ----- yaani, mivuto ile ya mbinguni pamoja na imani [ya mwanadamu] yenye nguvu, iliyo hai, itendayo kazi. Ni kwa njia hiyo peke yake mjumbe wa kibinadamu anaweza kuwa mfanya kazi pamoja na Mungu. Bwana haungi mkono imani ile iliyopofuka, ya kijinga iliyomo ndani ya ye yote kati yetu. Yeye haudharau ufahamu wa kibinadamu, lakini mbali na huo, anataka mapenzi ya kibinadamu yaletwe katika uhusiano mzuri na mapenzi ya Mungu. Anataka ubunifu wa akili ya kibinadamu, busara yake, ustadi wake, vitumike kwa nguvu nyingi katika kuichunguza kweli yake KAMA ILIVYO NDANI YA YESU.... Ninyi ni wafanya kazi pamoja na Mungu. ----- Letter 109, 1893. JE! UMEIHESABU GHARAMA YAKE? Novemba 1 Ulimwenguni mnayo dhiki; lakini jipeni moyo; mimi nimeushinda ulimwengu. Yohana 16:33. Mkombozi wa ulimwengu huu anaweka mbele ya wafuasi wake mpango wa mapambano ambayo anawaita kujiunga nayo, tena anawaagiza kuihesabu gharama yake. Anawahakikishia ya kwamba malaika walio na nguvu isiyo na kifani watakuwa katika jeshi lake, nao watawawezesha wale wanaomtumainia kupigana vita kwa ujasiri. Mmoja atawafukuza elfu moja, na wawili watawakimbiza elfu kumi ----- si kwa nguvu zao wenyewe, bali kwa nguvu za Mungu mwenye uweza wote.... Amiri [Kamanda] wa Jeshi la Bwana yu pamoja nao, akiyaongoza majeshi yake, na kuwapatia ushindi. Kutokana na udhaifu wao wa kibinadamu, yaani, kutokana na dhambi zao, wanaweza kuogopa na kutetemeka wanapoyaona majeshi makubwa sana ya mamlaka zile za giza; lakini wanaweza kushangilia wanapowategemea malaika wa Mungu walio tayari kuwahudumia wale watakaourithi wokovu. Wanaweza kushangilia wanapotambua ya kwamba yule ambaye ni Amiri [Kamanda] wa Jeshi la Bwana ndiye atakayewaongoza wanaposonga mbele katika kila pambano dhidi ya maadui wa kawaida pamoja na wale wasioonekana kwa macho [malaika waovu].... Kiongozi wenu ni Mshindi. Songeni mbele kwenye ushindi.... Ahadi hizo ni za thamani jinsi gani kwamba sisi hatutaachwa kamwe kuchukua hatua moja kwa kutegemea nguvu zetu wenyewe za kibinadamu, kwa maana yeye alisema, "Sitakupungukia kabisa, wala sitakuacha kabisa." Waebrania 13:5. Tunapigana vita huku yakiwapo majeshi yale yasiyoonekana kwa macho. Viumbe wale wenye hekima wasioonekana huvikagua vikosi vyote vya uovu vilivyojipanga tayari kwa vita, na msaada wetu upo karibu. Hatutapewa kile kilicho cha lazima tu, bali tutawekwa kwenye uwanja wa manufaa kwetu.... Neno lile lililosemwa kwa Petro linakuja kwa kila Mkristo, likisema, "Shetani amewataka ninyi apate kuwapepeta kama vile ngano; lakini nimekuombea wewe ili imani yako isitindike." Luka 22:31,32. Mungu na ashukuriwe, hatujaachwa peke yetu. Huu ndio usalama wetu. Shetani hawezi kumgusa na kumletea maangamizi yale ya milele yule ambaye Kristo amemwandaa kwa majaribu kwa njia ya maombezi yake ya nyuma; kwa maana neema hutolewa ndani ya Kristo kwa kila mtu, na njia ya kutokea imewekwa, ili asiwepo ye yote wa kuanguka chini ya uwezo wa yule adui. ----- YI, Des.20, 1894. JE! UTAUVUMILIA MOTO WA MTU ASAFISHAYE FEDHA? Novemba 2 Ili kwamba kujaribiwa kwa imani yenu, ambayo ina thamani kuu kuliko dhahabu ipoteayo, ijapokuwa hiyo hujaribiwa kwa moto, kuonekane kuwa kwenye sifa na utukufu na heshima, katika kufunuliwa kwake Yesu Kristo. 1 Petro 1:7. Dhahabu husafishwa kwa moto, ili isafishwe na uchafu wote; bali imani iliyosafishwa kwa majaribu, ni ya thamani kuliko dhahabu safi. Basi, na tuyaangalie majaribu kwa njia ya busara. Tusipite ndani yake huku tukiwa tunanung'unika na kuona chuki. Hebu na tusifanye makosa ya kujitoa ndani yake [majaribu]. Katika nyakati za kujaribiwa yatupasa kumshikilia sana Mungu na ahadi zake. Wengine wameniambia hivi, "Je! wakati mwingine wewe hukati tamaa unapokuwa chini ya majaribu?" Nami nimewajibu hivi, "Ndiyo, kama kwa kukata tamaa mnamaanisha kuhuzunika au kushushwa moyo." "Je! hukuongea na ye yote juu ya hisia zako?" "La; kuna wakati wa kunyamaza, yaani, wakati wa kuuzuia ulimi kama kwa lijamu, nami niliamua kutosema neno lo lote lenye kuleta mashaka au giza, yaani, kutoleta kivuli cho chote chenye utusitusi kwa wale nilioshirikiana nao. Nimejiambia mwenyewe hivi, Nitavumilia moto wa mtu yule asafishaye fedha; Sitateketezwa kabisa. Nisemapo, basi, itakuwa juu ya nuru; itakuwa juu ya imani na tumaini kwa Mungu; itakuwa juu ya haki, juu ya utu wema, juu ya upendo wa Kristo Mwokozi wangu; itakuwa juu ya kuyaongoza mawazo ya wengine kuelekea mbinguni na juu ya mambo yale ya mbinguni, juu ya kazi yake Kristo anayofanya huko mbinguni kwa ajili yetu, na juu ya kazi yetu tunayofanya hapa duniani kwa ajili yake. ----- RH, Feb. 11, 1890. Tanuru lile la moto usafishao linaondoa uchafu tu. Yule Asafishaye [Kristo] anapoiona sura yake ikiakisiwa [ikiangaza] kikamilifu ndani yako, atakuondoa katika tanuru hilo. Hutaachwa kuteketezwa wala kuvumilia mateso ya moto huo kwa muda mrefu kuliko ilivyo lazima kwa utakaso wako. Lakini ni jambo la maana kwako kujiweka chini ya njia ile anayokuchagulia yule Asafishaye [Malaki 3:1-3], ili upate kuakisi sura ya Mungu, yaani, ili upate kusafishwa, kutakaswa, na kila waa na doa kuondolewa kwako ----- lisibakie hata kunyanzi moja katika tabia yako ya Kikristo. Bwana na akusaidie... kuchagua mapenzi na kazi ya Mungu ipate kutimilika ndani yako.... Tazama juu! Yesu wako yu hai. Yesu anakupenda. Yesu anakuhurumia, naye atakupokea pamoja na mzigo wako wa masumbufu na shida kama wewe utakuja kwake na kumtwika mzigo wako. Yeye ameahidi kwamba hatawapungukia kabisa, wala hatawaacha kabisa wale wanaoliweka tumaini lao kwake. ----- Letter 2, 1870. FURAHA KWA NJIA YA KUTESWA PAMOJA NA KRISTO Novemba 3 Wapenzi, msione kuwa ni ajabu ule msiba ulio kati yenu, unaowapata kama moto ili kuwajaribu, kana kwamba ni kitu kigeni kiwapatacho. Lakini kama mnavyoyashiriki mateso ya Kristo ni heri yenu; kwa kuwa Roho wa utukufu na wa Mungu anawakalia. 1 Petro 4:12,13. Sikuzote sisi hatufikiri kwamba utakaso ule tunaoutamani sana na ambao kwa ajili yake tunaomba kwa bidii sana unaletwa kwa njia ya ile kweli na, kwa mpango wa Mungu, unakuja kwa njia ambayo hatukuitazamia hata kidogo. Tunapotazamia furaha, tazama ipo huzuni. Tunapotazamia amani, mara kwa mara tunakuwa na shuku na mashaka kwa sababu tunajikuta tumetumbukizwa katika majaribu ambayo hatuwezi kuyakwepa. Katika majaribu hayo tunapokea majibu kwa maombi yetu. Ili sisi tupate kutakaswa, moto wa mateso ni lazima uwake juu yetu, na mapenzi yetu hayana budi kufanana na mapenzi ya Mungu.... Mungu anaona ni vyema sana kutuwekwa sisi chini ya mafunzo ya nidhamu ambayo ni ya muhimu kwetu kabla hatujahesabiwa kuwa raia wanaofaa kupewa baraka ile tunayoitamani sana. Tusingekuwa tunakatishwa tamaa na kuruhusu mashaka kutujia, na kudhani kwamba maombi yetu hayatambuliwi [hayawekwi maanani]. Tungemtegemea Kristo kwa salama zaidi na kuyaacha mambo yetu mikononi mwake Mungu ili apate kujibu maombi yetu kwa njia ile anayotaka mwenyewe. Mungu hatajatuahidi kutupa mibaraka yake kupitia katika njia zile tulizozitia alama zetu.... Sikuzote mipango ya Mungu kwetu ni mizuri kabisa, ingawa sikuzote hatuwezi kuitambua hivyo. Kukamilisha tabia ya Kikristo kunaweza kupatikana tu kwa kazi ngumu, mapambano, na kujikana nafsi. Hatutegemei sikuzote kuyapata mambo hayo, wala hatudhani kwamba ni ya lazima kwetu njia ile inayotuletea maumivu mengi na mara nyingi hatua ile ya kututakasa inayoendelea kwa muda mrefu ili tupate kufanana na sura yake Kristo. Mara kwa mara Mungu anajibu maombi yetu kwa njia ile tusiyoitazamia hata kidogo. Anatuleta mahali pale ambapo pana majaribu mengi sana, ili kufunua kile kilichomo mioyoni mwetu. Ili kuendeleza ukuaji wa matunda yale ya Kikristo, atatuweka katika mazingira yatakayohitaji jitihada zaidi kwa upande wetu kuilinda imani yetu kwa kufanya mazoezi yaliyo hai. Hebu na tukumbuke jinsi thamani ya vipawa vya Mungu ilivyo kubwa mno ----- yaani, yale matunda ya Roho wake ----- basi, hatutajikunyata tutakapopitishwa katika njia hiyo inayotujaribu na kutupima, hata kama iwe ya kutuletea maumivu makali sana ama ya kutudhalilisha. ----- Letter 9, 1873. ISHARA YA AGANO LA MILELE Novemba 4 Basi huo upinde utakuwa winguni; nami nitauangalia nipate kulikumbuka agano la milele lililoko kati ya Mungu na kila kiumbe hai katika wote wenye mwili kilichoko katika nchi. Mwanzo 9:16. Wakati fulani uliopita, tulipata fursa ya kuuona upinde uliokuwa na utukufu mwingi sana ambao tulikuwa hatujapata kuuona. Mara nyingi tumetembelea nyumba za sanaa, na kupendezwa sana na ustadi ulioonyeshwa katika picha za rangi zilizochorwa zinazoonyesha upinde mkuu wa Mungu wa ahadi. Lakini hapa tuliziona rangi mbalimbali ----- nyekundu iliyoiva, zambarau, buluu, chanikiwiti, fedha, na dhahabu, zote zikiwa zimechanganywa vizuri pamoja na yule Msanii Mkuu [Kristo]. Tulivutiwa sana tulipoiangalia picha hiyo tukufu mbinguni. Tunapouangalia upinde huo, yaani, muhuri wa ishara ya ahadi ile ya Mungu kwa mwanadamu, kwamba ghadhabu ya hasira yake haitaiangamiza tena nchi yetu kwa maji ya gharika, basi, sisi tunadhani kwamba macho ya wanadamu wengine nayo yanaiangalia mandhari [picha] hiyo tukufu. Malaika wanashangilia wanapoangaza macho yao juu ya ishara hiyo ya thamani inayoonyesha upendo wa Mungu kwa mwanadamu. Mkombozi huyo wa ulimwengu anaiangalia; maana ni kwa njia yake yeye upinde huo uliumbwa ili uonekane mbinguni kama ishara au agano la ahadi yake kwa mwanadamu. Mungu mwenyewe anauangalia upinde huo mawinguni, na kukumbuka agano lake la milele kati yake na mwanadamu.... Upinde huo unauwakilisha upendo wa Kristo unaoizunguka dunia, na kufika kwenye mbingu zile za juu kabisa, ukiwaunganisha wanadamu na Mungu, na kuiunganisha nchi na mbingu. Tunapoangaza macho yetu juu kuiangalia mandhari hiyo nzuri, tunaweza kufurahi katika Bwana, tukithibitishiwa kwamba hata yeye mwenyewe anaiangalia ishara hiyo ya agano lake, na ya kwamba anapoiangalia anawakumbuka watoto wake waliomo duniani, ambao kwa ajili yao ulitolewa. Mateso yao, hatari zao, na maonjo yao hayajafichwa kwake. Tunaweza kufurahi tukiwa na tumaini kwa vile upinde wa agano la Mungu u juu yetu. Hatawasahau kamwe watoto wake anaowatunza. Ni vigumu jinsi gani kwa moyo wa mwanadamu kuupokea upendo huu wa pekee na huruma ya Mungu, na kujidhili kwake kusikokuwa na kifani pale aliposema, "Nami nitauangalia winguni, na kuwakumbuka ninyi." Ni vyepesi jinsi gani kwetu kumsahau Mungu, ambapo yeye hatusahau sisi kamwe; anatupa rehema zake kila saa. ----- RH, Mei 20, 1880. MUNGU HUZUNGUMZA KUPITIA KATIKA UKIMYA Novemba 5 Mimi Yohana, ndugu yenu na mwenye kushiriki pamoja nanyi katika mateso na ufalme na subira ya Yesu Kristo, nalikuwa katika kisiwa kiitwacho Patmo, kwa ajili ya Neno la Mungu, na ushuhuda wa Yesu. Ufunuo 1:9. Kwa kumruhusu Yohana kufukuzwa nchini na kutupwa kisiwani Patmo, Kristo alimweka mwanafunzi wake mahali ambapo angeweza kuipokea ile kweli ya thamani mno kwa ajili ya kuyaelimisha makanisa. Alimweka katika hali ya upweke, ili sikio lake na moyo wake vipate kutakaswa na kuipokea kweli hiyo.... Mateso ya Yohana yaliyoletwa na adui zake yakageuka na kuwa njia ya neema kwake. Patmo ilifanywa nzuri kwa utukufu wa Mwokozi aliyefufuka.... Ni sabato nzuri ilioje kwa mkimbizi yule mpweke!... Kamwe alikuwa hajapata kujifunza mengi sana juu ya Yesu kama wakati huo. Kamwe alikuwa hajapata kuisikia kweli iliyotukuzwa kama hiyo. Mtenda kazi wa Mungu mara nyingi anazifikiria shughuli za maisha yake kama ni za maana katika kuiendeleza kazi yake. Ubinafsi wake unachanganyika na yote yale anayosema na kutenda.... Mtenda kazi huyo anajiona kama ni wa muhimu. Mungu husema hivi, "Maskini huyo hanioni Mimi wala utoshelevu wangu. Yanipasa kuitupa nuru yangu na uweza wangu utiao nguvu ndani ya moyo wake. Yanipasa kumwandaa kuipokea kweli yangu kwa kumpaka mafuta kwa njia ya dawa ile ya macho ya mbinguni. Anaviona vitu vingi mno. Jicho lake halijakazwa kwangu...." Wakati mwingine Bwana anafungua njia yake kuingia katika moyo wa mtu kwa njia ambayo inaleta uchungu kwa binadamu. Analazimika kuuimarisha moyo wake [mtu huyo] dhidi ya kujisifu mwenyewe na kujitegemea, ili mtenda kazi huyo asipate kufikiri kwamba kushindwa kwake na udhaifu wake unaotokana na tabia yake ya dhambi kuwa huo ndio wema, na hivyo kuangamizwa kwa njia ya kujikweza mwenyewe. Iwapo wale wanaojidai kuziamini kweli zile kuu za leo wangejiandaa wenyewe kuyachunguza Maandiko, na kuwa na bidii katika maombi, na kwa kuitumia imani yao, wangekuwa wamejiweka mahali ambapo wangeweza kuipokea nuru ile wanayoitamani sana.... Ukimya unenao kwa ufasaha mara nyingi ni wa muhimu mbele za Mungu. Kama mawazo yanaendelea kuchochewa wakati wote, badala ya kutulia, basi, sikio huzuiwa lisiweze kuisikia kweli ile ambayo Mungu angetaka kuwaambia wale walio wake ambao wanamwamini. Kristo anawaondoa watoto wake kutoka katika kile kinachoyashika mawazo yao ili wapate kuutazama utukufu wake. ----- MS 94, 1897. MAFUNZO YA LAZIMA KWENDA MBINGUNI Novemba 6 Lakini yeye ajua njia niendeayo; Akisha kunijaribu, nitatoka kama dhahabu. Ayubu 23:10. Mungu atawafanyia kazi wale wanaoliweka tumaini lao kwake. Ushindi wa thamani utapatikana kwa wale walio waaminifu. Mafundisho ya thamani yatajifunzwa. Uzoefu wa thamani utapatikana ambao utakuwa na manufaa makubwa sana wakati wa maonjo na majaribu. Wale watakaompa Mungu utukufu wote, pasipo kujichukulia sifa wao wenyewe, watadhaminiwa na kupewa mibaraka mingi zaidi na zaidi. Bwana atatukuzwa na wale wanaomheshimu katikati ya wanadamu. Maonjo yaliyovumiliwa, mtihani walioshinda kwa uaminifu, vitawathibitisha kuwa wanastahili kupewa madaraka, naye Mungu atawafanya kuwa wajumbe wake wa kutekeleza mapenzi yake.... Kwa mpango wake Mungu, mapambano tuliyo nayo duniani humu hutupatia mafunzo yale yale hasa yanayohitajika katika kuzikuza tabia zetu ili zipate kufaa kwa ajili ya kuishi katika majumba yale ya kifalme yaliyoko mbinguni. Sisi tunapaswa kuwa watu wa familia ile ya kifalme, yaani, wana wa Mungu, na "mambo yote hufanya kazi katika kuwapatia mema" wale wampendao Mungu, na kujinyenyekeza wenyewe chini ya mapenzi yake. Mungu wetu ni msaada tele kwetu utakaoonekana kila wakati tunapokuwa na shida. Anayaelewa kabisa mawazo yetu ya siri sana yaliyo ndani ya mioyo yetu, pamoja na shauku na makusudi ya mioyo yetu. Tunapopata matatizo hata kabla hatujamfunulia shida yetu, yeye anafanya mipango kutuokoa. Huzuni yetu sio kwamba haioni. Sikuzote yeye anayajua vizuri sana kuliko vile sisi tunavyojua, mambo yale yaliyo ya muhimu kwa ajili ya manufaa ya watoto wake, naye anatuongoza kama vile ambavyo sisi tungependa kuongozwa kama tungeweza kuifahamu mioyo yetu na kuona mahitaji yetu muhimu na hatari zake, kama vile Mungu aonavyo. Lakini wanadamu wasiokuwa na maisha ya kudumu kwa shida sana wanajijua wenyewe. Hawaujui udhaifu wao.... Mungu anawajua vizuri sana kuliko wanavyojijua wenyewe, naye anajua jinsi ya kuwaongoza.... Iwapo sisi tutamtegemea yeye, na kumkabidhi njia zetu, basi, yeye atayanyosha mapito yetu ili tupate kwenda katika njia ile ile itakayoleta matokeo ya kutupatia sisi ushindi juu ya kila tamaa mbaya ya mwili, na kila sifa ya tabia yetu ambayo haifanani na Kiolezo chetu kile cha mbinguni [Kristo]. ----- ST, Mei 25, 1888. MUNGU AJUA KILICHO BORA KWETU Novemba 7 Kila adhabu wakati wake haionekani kuwa kitu cha furaha, bali cha huzuni; lakini baadaye huwaletea wao waliozoezwa nayo matunda ya haki yenye amani. Waebrania 12:11. Mungu ajua kilicho bora kwetu. Nidhamu ya aina yake ambayo tunawekwa chini yake ni nidhamu ile itakayozidhihirisha sifa za tabia, sio zile zilizo mbaya sana, wala zile zisizopendeza, bali zile za upole na wema wake Kristo, na kukuza matunda ya Kristo ya thamani. Mnahitaji kujifunza katika Shule ya Kristo ili mpate kufanana na Kristo. Mungu anaitumia neema yake kulingana na mahitaji ya pekee ya kila mmoja wetu. "Neema yangu yakutosha." 2 Wakorintho 12:9. Mzigo wako unavyozidi kuwa mzito, tazama juu, na kwa imani shikilia kwa nguvu sana mkono ule wa Yesu, msaidizi wako mwenye nguvu nyingi. Shida zinapozidi kuongezeka na kuwazunguka watu wake katikati ya hatari kubwa za siku hizi za mwisho, yeye anawatuma malaika zake ili wapate kutembea nasi njia yote wakiwa kando yetu, wakituvuta karibu na karibu zaidi kwenda kwenye ubavu ule wa Yesu unaotoka damu. Na maonjo makubwa yanapokuja, maonjo madogo sana husahauliwa.... Yakupasa kuendelea kuwa safi na mkweli na imara, ukikumbuka kwamba tabia yako inapigwa picha [kama mkanda wa video] katika vitabu vile vya mbinguni.... Hakuna jambo lo lote au mahali po pote au shida yo yote au dhiki yo yote, ambayo inaweza kutufanya tushindwe kuishi maisha yale mazuri yaliyo sahihi ya Kikristo na kuwa na mwenendo ule unaokubalika.... Ushindi haupatikani kwa kuyakwepa maonjo ----- yaani, kuyaondoa ----- bali kwa kupambana nayo kishujaa, na kuyastahimili kwa saburi. ----- Letter 29, 1884. Kila mmoja atakutana na maonjo.... Ukimtazama Yesu, ukimwamini kama Mwokozi wako wewe binafsi, utapitishwa katika kila onjo, na kuyastahimili maonjo hayo kwa saburi, utakuwa na nguvu nyingi zaidi za kustahimili mtihani unaofuata, yaani, onjo linalofuata ----- Letter 6, 1893. Ni ufinyu tu wa mtazamo wetu unaotuzuia kuzitambua fadhili zake Mungu katika nidhamu ambayo kanisa lake analiweka chini yake, pamoja na mibaraka yake mikubwa anayolipa. Katika nyakati zote za dhiki na machafuko, Mungu ni kimbilio lililo salama kwa watu wake. Katika kivuli cha ulinzi wake wanaweza kuitunza njia yake kwa salama. Katika mateso yale yaliyokusudiwa kuwatakasa, nguvu ya injili inapaswa kuwa ndiyo faraja yao. Katika neno lake thabiti wanayo ngome yao. ----- Letter 54, 1908. MAMBO YOTE HUFANYA KAZI PAMOJA Novemba 8 Nasi twajua ya kuwa mambo yote hufanya kazi pamoja kwa manufaa ya wale wampendao Mungu, yaani, wale walioitwa kwa kusudi lake. Warumi 8:28 [Tafsiri ya KJV]. Moyo ule uliojisalimisha chini ya nidhamu ya Mungu yenye hekima utatumainia kila utendaji wa mapenzi yake.... Endapo Mungu angemwacha kila mtu kufanya apendavyo, basi makuu na kiburi vingeweza kuimarishwa, na neema ile ya unyenyekevu isingependwa sana moyoni. Kukomaa [kupevuka] kwa akili na mwili kwa kweli kunawezekana tu kwa wale walio wanyenyekevu kweli kweli. Mambo yale tunayoweza kutamani sana kufanya yanaweza kufanyika kweli baada ya Mungu kututhibitisha katika shule yake ya uzoefu wa maisha, na miongoni mwa mibaraka yetu mikuu kabisa linaweza kuhesabiwa jambo lile ambalo hatukupewa fursa ya kulifanya, ambalo lingekuwa limezuia njia ya kufanya mambo yale hasa yaliyokusudiwa kabisa kututayarisha sisi kwa kazi ile ya juu zaidi. Majukumu yale ya kawaida, yaliyofanywa kwa makini katika maisha yetu halisi yalikuwa ya muhimu ili kuzuia jitihada ile isiyozaa matunda kwa kufanya mambo yale ambayo sisi hatukustahili kuyafanya. Mipango yetu tuliyobuni mara nyingi inashindwa ili mipango ya Mungu kwa ajili yetu ipate kuwa na ufanisi kamili. O! ni katika maisha yale ya baadaye tutakapoweza kuona zikifafanuliwa zile vurugu tulizokabiliana nazo hapa na mafumbo yale yasiyoelezeka ya maisha yetu, ambayo yametuudhi sana na kutuvunja moyo katika matumainio yetu. Ndipo tutakapoona ya kwamba maombi na matumaini yetu kwa mambo fulani fulani tuliyotaka ambayo yalizuiliwa yamekuwa miongoni mwa mibaraka yetu mikubwa kabisa. ----- Letter 2, 1889. Tusitazamie kupata mwanga wa jua tu katika ulimwengu huu. Mawingu na dhoruba vitajikusanya na kutuzunguka, nasi tunapaswa kuwa tayari kuyaelekeza macho yetu mahali pale tulipoiona nuru kwa mara ya mwisho. Mionzi yake huenda ikawa imefichwa, lakini bado ipo, na bado inaangaza nyuma ya wingu hilo. Ni jukumu letu kungoja, kukesha, kuomba, na kuamini. Tutaithamini zaidi sana nuru ya jua baada ya mawingu hayo kutoweka. Tutauona wokovu wa Mungu iwapo tutamtegemea Mungu katika giza sawa kama katika nuru. ----- Letter 23, 1870. Maonjo yote, mateso yote, amani yote, usalama wote, afya, tumaini, uzima, na mafanikio yako mikononi mwake Mungu, naye anaweza kuyadhibiti mambo yote hayo kwa manufaa ya watoto wake. Ni fursa yetu kuwa waombaji, kuomba cho chote na kila kitu kutoka kwa Mungu, tukitoa dua zetu kwa unyenyekevu chini ya makusudi yake yenye hekima na chini ya mapenzi yake ya milele. ----- MS 1 1867. KUVIANGALIA VISIVYOONEKANA Novemba 9 Maana dhiki yetu nyepesi, iliyo ya muda wa kitambo tu, yatufanyia utukufu wa milele uzidio kuwa mwingi sana; tusiviangalie vinavyoonekana, bali visivyoonekana. Kwa maana vinavyoonekana ni vya muda tu; bali visivyoonekana ni vya milele. 2 Wakorintho 4:17,18. Kama mawazo yetu yamekazwa juu ya vitu vile vya milele, wala sio juu ya vitu vya ulimwengu huu, tutaweza kuushika mkono ule wa uweza wa Mungu, basi, ni kitu gani kitakachoweza kutuhuzunisha sisi?... Hatuna haja yo yote ya kuachwa tukiwa mateka wa uwezo wake Shetani.... Watoto wa Mungu hawapaswi kumruhusu Shetani kujiingiza kati yao na Mungu wao. Ukimruhusu kufanya hivyo, atakuambia kwamba taabu zako ni nzito mno, tena ni chungu mno ambazo hajapata kukutana nazo mwanadamu ye yote mwenye maisha mafupi. Ataweka miwani yake inayokuza mambo mbele ya macho yako, na kukuonyesha kila kitu katika hali yake iliyokuzwa mno ili kukufanya wewe ushindwe na kufa moyo.... Lichukue Neno la Mungu kama mshauri wako, na kuunyenyekeza moyo wako ulio na mashaka mbele zake Mungu, na kwa moyo wa toba kusema, "Mzigo wangu nautua hapa chini. Siwezi kuubeba. Ni mzito mno kwangu. Nauweka chini miguuni pa Mkombozi wangu mwenye huruma nyingi."... Shetani anapokujaribu, usitoe neno hata moja linaloonyesha mashaka yako au giza. Unaweza kuwa na uchaguzi wako kuhusu yule atakayeutawala moyo wako na kuyadhibiti mawazo yako. Ukichagua kuufungua mlango na kuyakaribisha mashauri ya yule mwovu, basi, moyo wako utajazwa na mashaka na maswali ya uasi. Unaweza kusema hisia zako, lakini kila shaka unalotamka ni mbegu itakayoota na kuzaa matunda yake katika maisha ya mtu mwingine na itakuwa haiwezekani kuupinga mvuto huo wa maneno yako. Unaweza kupona kutoka katika kipindi chako cha majaribu, na kutoka katika mtego wa Shetani, lakini wale wengine huenda wasiweze kuokoka kutokana na mashaka yale uliyoyatamka. Ni jambo la maana jinsi gani kwamba inatupasa kuwaambia wale wanaotuzunguka mambo yale tu yatakayowatia nguvu ya kiroho na ufahamu! Hebu na tujaribu kuwainua watu juu kwa Yesu, ambaye, ijapokuwa hatujamwona, tunaweza kumpenda, na kujazwa na furaha isiyoneneka, yenye utukufu. ----- RH, Feb. 11, 1890. HAKUNA MAMLAKA YO YOTE ITAKAYOTUTENGA NA KRISTO Novemba 10 Ni nani atakayetutenga na upendo wa Kristo? Je! ni dhiki au shida, au adha, au njaa, au uchi, au hatari, au upanga? Warumi 8:35. Wakati wa shida ni ahadi ya thamani ilioje kwetu sisi kuunganishwa na Yesu!... Twaweza kusema, "Ni nani atakayetutenga na upendo wa Kristo? Je! ni dhiki? ----- La, maana hiyo inatufanya sisi kujisikia kwamba ni Kristo peke yake aliye kimbilio letu, nasi tunamkimbilia ili kupata kinga yetu. "Au shida?" La, maana yeye ndiye faraja yetu. "Na ahimidiwe Mungu, Baba wa Bwana wetu Yesu Kristo, Baba wa rehema, Mungu wa faraja yote; atufarijiye katika dhiki zetu zote...." 2 Wakorintho 1:3,4. "Au adha?" ----- La; "Heri wenye kuudhiwa kwa ajili ya haki; Maana ufalme wa mbinguni ni wao." Mathayo 5:10.... "Au njaa?" ----- La, kwa maana tunayo ahadi ya Mungu, isemayo,... "Wakati wa njaa atakukomboa na mauti." Ayubu 5:20. "... Na siku za njaa watashiba." Zaburi 37:19. Kwa kumkimbilia Yesu tutashiba kabisa. "Au uchi?" ---- Sikiliza sauti ya Yesu ikisema, "Ununue kwangu dhahabu iliyosafishwa kwa moto, upate kuwa tajiri, na mavazi meupe upate kuvaa, aibu ya uchi wako isionekane." Ufunuo 3:18.... "Yeye ashindaye atavikwa hivyo mavazi meupe." Ufunuo 3:5. "Au hatari?" ----- La; kwa uzoefu wake, Paulo alijua maana ya kuwa katika hatari.... "hatari za mito; hatari za wanyang'anyi [majambazi]; hatari kwa taifa langu; hatari kwa mataifa mengine; hatari za mjini; hatari za jangwani; hatari za baharini; hatari kwa ndugu za uongo." 2 Wakorintho 11:26. "Naye akaniambia, Neema yangu yakutosha." 2 Wakorintho 12:9.... "Au upanga?"... Upanga hauwezi kuiua roho, maana uzima wetu umefichwa pamoja na Kristo katika Mungu. Basi, twaweza kuuliza swali hili pamoja na Paulo, "Ni nani atakayetutenga na upendo wa Kristo?" Kisha tutajibu hivi, "Kwa maana nimekwisha kujua hakika ya kwamba, wala mauti, wala uzima, wala malaika, wala wenye mamlaka, wala yaliyopo, wala yatakayokuwapo, wala wenye uwezo, wala yaliyo juu, wala yaliyo chini, wala kiumbe kingine cho chote hakitaweza kututenga na upendo wa Mungu ulio katika Kristo Yesu Bwana wetu." Warumi 8:38,39. ----- Letter 25, 1892. CHUNGU CHA MAJARIBU MAKALI YATAKAYOLETA TAABU Novemba 11 Ole! maana siku ile ni kuu, hata hapana inayofanana nayo, maana ni wakati wa taabu yake Yakobo; lakini ataokolewa nayo. Yeremia 30:7. Njia inayoleta uhuru kutoka dhambini ni ile ya kuisulibisha nafsi, na kupambana na nguvu zile za giza. Na asiwepo mtu ye yote wa kukatishwa tamaa kwa sababu ya maonjo makali watakayokutana nayo katika kipindi kile cha wakati wa taabu ya Yakobo ambacho kiko mbele yao. Wanapaswa kufanya kazi kwa bidii, kwa wasiwasi, si kwa ajili ya wakati ule, bali kwa leo hii. Tunachotaka ni kupata maarifa ya ile kweli kama ilivyo katika Kristo hivi sasa, na kuwa na uzoefu sasa kila mmoja wa kwake [wa maisha yale ya ushindi dhidi ya kila dhambi]. Katika saa hizi za thamani za kufungia mlango wa rehema, tunapaswa kuwa na uzoefu huo wenye kina na ulio hai. Kwa njia hiyo, tutajenga tabia zile zitakazotuhakikishia kuokolewa kwetu katika wakati ule wa taabu. Wakati wa taabu ni chungu cha majaribu makali ambacho kitazidhihirisha [ndani ya watu wake] tabia zile zinazofanana na ile ya Kristo. Kimekusudiwa kuwaongoza watu wa Mungu wafikie mahali pa kumkataa Shetani na majaribu yake. Pambano lile la mwisho litamfunua kwao Shetani kwa tabia yake halisi, yaani, ile ya mtawala katili anayetumia mabavu, nalo litawafanyia mambo yale ambayo hakuna kitu kingine cho chote ambacho kingeweza kuyafanya, yaani, kumng'oa kabisa [Shetani] kutoka katika mapenzi yao. Kwa maana kuipenda na kuihifadhi dhambi, ni kumpenda na kumhifadhi mwasisi wake, yaani, adui yule wa hatari mno wa Kristo. Wanapotoa udhuru kwa ajili ya dhambi zao na kung'ang'ania tabia ile iliyopotoka, wanampa Shetani nafasi katika mapenzi yao, na kumsujudu. ----- RH, Agosti 12, 1884. Mbingu yote inampenda mwanadamu na kutaka apate wokovu. Hilo ndilo kusudi kuu katika shughuli yote ya Mungu kwa mtu mmoja mmoja.... Ni jambo linalolishangaza mno jeshi lile la mbinguni kuona kwamba ni wachache mno wanaojali kuwekwa huru kutoka katika utumwa wa mivuto mibaya ya dhambi, wachache sana walio tayari kutumia nguvu zao zote kwa kuafikiana na Kristo katika kazi yake kuu ya ukombozi wao. Kama watu wangeonyeshwa mbele yao picha ya kazi zile anazozifanya yule mlaghai mkuu kwa kuwashikilia wanadamu katika uchungu mkali sana kama ule wa nyongo na kuwaweka katika utumwa ule wa dhambi, ni kwa bidii ilioje wangeyakataa kabisa matendo yale ya giza, ni kwa jinsi gani wangejilinda ili wasianguke majaribuni, wangekuwa waangalifu jinsi gani kuiona na kuiondoa kila kasoro inayoharibu sura ya Mungu ndani yao; kwa jinsi gani wangekaribia sana kando ya Yesu, na kwa jinsi gani dua zao za dhati zingepanda mbinguni ili wapate kutembea kwa amani, karibu zaidi, na kwa furaha na Mungu wao. ----- RH, Agosti 12, 1884. JE! HIYO NI JOHARI AU NI CHANGARAWE? Novemba 12 Katika siku ile, asema BWANA wa majeshi, nitakutwaa wewe, Ee Zerubabeli, mtumishi wangu, mwana wa Shealtieli, asema BWANA, nami nitakufanya kuwa kama pete yenye muhuri; kwa kuwa nimekuchagua, asema BWANA wa majeshi. Hagai 2:23. Wakristo ni johari zake Kristo. Wanatakiwa kung'aa sana kwa ajili yake, wakiwa wanatoa mwanga wa uzuri wake. Mng'ao wao unategemea kung'arishwa wanakofanyiwa. Wanaweza kuchagua kung'arishwa au kubaki bila kung'arishwa. Lakini kila mmoja anayetangazwa kuwa anastahili kuwa na mahali pake katika hekalu lake Bwana ni lazima akubali hatua hiyo ya kung'arishwa. Bila kung'arishwa ambako Bwana anafanya hawawezi kuakisi nuru [kuangaza] zaidi ya ile ya changarawe ya kawaida. Kristo anamwambia mwanadamu, "Wewe u wangu. Mimi nimekununua wewe. Wewe ni jiwe linaloparuza tu, lakini kama utajiweka mikononi mwangu, nitakung'arisha, na mng'ao ambao kwa huo utaweza kung'aa utaleta utukufu kwa jina langu. Hakuna mtu ye yote atakayekupokonya toka mkononi mwangu. Nitakufanya uwe hazina yangu ya pekee. Siku ya kutawazwa kwangu, utakuwa johari katika taji yangu ya furaha." Mtenda kazi huyo wa mbinguni anatumia wakati mchache tu juu ya vitu vile visivyofaa. Ni zile johari za thamani tu anazozing'arisha kwa kuzifananisha na mfano wa jumba lile la kifalme, akizikatilia mbali pembe zake zote zinazoparuza. Hatua hiyo ni kali, nayo huleta usumbufu; inakiumiza kiburi cha mwanadamu. Kristo anachoma mpaka ndani ya uzoefu ule wa mwanadamu wa kujitosheleza kwake ambao yeye [mwanadamu] alifikiri kwamba umekamilika, naye hukuondolea mbali kujiinua nafsi kote kutoka katika tabia yake. Anaikatilia mbali sehemu ya juu iliyozidi, na kuliweka jiwe hilo kwenye gurudumu linalolilainisha, analigandamiza kwa karibu zaidi ili kuparuza kote kupate kuondolewa mbali. Ndipo anapoishikilia johari hiyo na kuielekeza kwenye mwanga, Bwana anaona ndani yake sura yake mwenyewe ikiakisiwa [ikirudishwa], naye anaitangaza kuwa inafaa kuwa na mahali katika kikasha chake. "Katika siku ile, asema BWANA wa majeshi, nitakutwaa wewe,... nami nitakufanya kuwa pete yangu yenye muhuri; kwa kuwa nimekuchagua, asema BWANA wa majeshi." Heri uzoefu ule wa maisha, haidhuru upitie mateso makali yaliyoje, ambao hulipatia jiwe thamani yake mpya na kulifanya ling'ae kwa mng'ao ulio hai. ----- 4BC 1177. Mungu hatastahimili kumwacha peke yake mmojawapo wa watenda kazi wake walio na moyo mnyofu kupigana peke yake na mambo yale yasiyokuwa ya kawaida na kushindwa. Anamlinda kama johari ya thamani kila mmoja ambaye uhai wake umefichwa pamoja na Kristo katika Mungu. ----- 7T 67. MUNGU ANALIPIMA KILA JARIBU Novemba 13 Jaribu halikuwapata ninyi, isipokuwa lililo la kawaida ya wanadamu; ila Mungu ni mwaminifu; ambaye hatawaacha mjaribiwe kupita mwezavyo; lakini pamoja na lile jaribu atafanya na mlango wa kutokea, ili mweze kustahimili. 1 Wakorintho 10:13. Kila mmoja anayo mapambano yake ya kupambana nayo, na uzoefu wake wa [maisha yake ya] Kikristo anaotakiwa kuupata kwa njia fulani akiwa anajitegemea mbali na mtu mwingine ye yote; na Mungu anayo mafunzo kwa kila mmoja ili ayapate yeye mwenyewe ambayo mwingine awaye yote hawezi kumpatia.... Baba yetu aliye mbinguni analipima na kuona uzito wake kila jaribu kabla hajaliruhusu kumjia muumini huyo. Anayafikiria mazingira yake na nguvu za yule atakayesimama chini ya kupimwa na kujaribiwa na Mungu, naye haruhusu kabisa majaribu yale yanayozidi uwezo wake wa kuyapinga. Iwapo mtu huyo ustahimilivu wake umezidiwa nguvu; na mtu huyo anashindwa kabisa, basi, jambo hilo haliwezi kamwe kumfanya Mungu ashutumiwe;... ila yule aliyejaribiwa hakuwa anakesha na kuomba, wala hakuutumia kwa imani msaada ule ambao Mungu anao tele kwa ajili yake. Kristo alikuwa hajamwacha kamwe muumini huyo katika saa yake [Kristo] ya mapambano. Muumini anapaswa kudai ahadi na kupambana na adui yule katika jina la Bwana.... Lo! kuna kazi kubwa inayotakiwa kufanywa kwa ajili ya watu wa Mungu kabla hawajawa tayari kubadilishwa na kunyakuliwa kwenda mbinguni! Joto la tanuru kwa wengine halina budi kuwa kali sana ili lipate kuzifunua takataka zilizo ndani yao. Nafsi itapaswa kusulibiwa. Iwapo kila muumini, kwa kiwango cha ufahamu wake wote, anamtii Bwana, na wakati uo huo anajitahidi kutowapa nafasi yo yote inayostahili wanadamu wenzake kuweza kumwonea, basi, hapo asingeogopa matokeo, hata kama atakabiliwa na kifungo na mauti.... Moyo wa Mungu wenye huruma nyingi uko kwa watu wake. Imani, imani ya ajabu ----- inawaongoza watu wa Mungu katika njia zile zilizosonga. Pasipo kuwa na imani hiyo, kwa hakika tutayaelewa vibaya maongozi yake kwetu, nasi tutakuwa na mashaka na upendo na uaminifu wake. Haidhuru majaribu na mateso yaweje,... pasiwe na woga wo wote, wala kuguna kunakokera sana , wala kunung'unika.... Mwonzi mmoja tu wa ushahidi wa fadhili zake Mungu ambazo hatustahili kupewa ukiangaza mioyoni mwetu utalizidi kwa uzito kila jaribu la aina yo yote ile, haidhuru liwe kali kiasi gani.----- MS 6, 1889. IMANI NI LAZIMA ILIPENYE GIZA HILO Novemba 14 Tazama, ataniua; sina tumaini [ajaponiua, nitamngojea vivyo]; Ila hata hivyo nitaithibitisha njia yangu mbele yake. Hili nalo litakuwa ni wokovu wangu; Kwani asiyemcha Mungu hatanikaribia mbele yake. Ayubu 13:15,16 [KJV]. Mkristo wa kweli hana wazo lo lote la kuliruhusu jambo lo lote la kidunia kuingilia kati ya roho yake na Mungu wake.... Majonzi yo yote yanapokaa moyoni mwako, jambo hilo halimaanishi kwamba Mungu amebadilika kwako. Yeye ni yeye yule, jana na leo na hata milele." Waebrania 13:8. Unayo hakika ya kupata upendeleo wa Mungu unapoitambua miali ya lile Jua la Haki; lakini kama mawingu yanapita juu ya roho yako, hupaswi kujisikia ya kwamba umeachwa. Imani yako ni lazima ilipenye giza hilo. Jicho lako halina budi kuwa safi, hapo ndipo na mwili wako wote utakuwa na nuru. Utajiri wa neema ya Kristo unapaswa kuwekwa mbele ya mawazo yako. Uyahifadhi mafunzo unayopewa kwa njia ya upendo wake. Imani yako na iwe kama ile ya Ayubu, hata upate kutangaza hivi, "ajaponiua, nitamngojea vivyo."... Maonjo mazito mno katika uzoefu wa maisha ya Mkristo yanaweza kuwa ni mbaraka mkubwa mno kwake. Msaada wa pekee uliowekwa kwa saa zile za giza unaweza kumtia nguvu mtu huyo kuweza kukabiliana na mashambulio ya Shetani ya baadaye, na kumvika silaha mtumishi huyo wa Mungu kuweza kusimama katika maonjo yaliyo makali kama moto. Kujaribiwa kwa imani yako ni kwa thamani kuliko dhahabu. Unapaswa kuwa na imani ya kumtegemea Mungu ambayo haiwezi kuathiriwa na majaribu, wala na hoja za yule mlaghai [Shetani]. Mwamini Bwana kama Neno lake lisemavyo. Yakupasa kujifunza ahadi zake, na kuzitumia unapokuwa na haja, "Basi imani, chanzo chake ni kusikia; na kusikia huja kwa neno la Kristo." Warumi 10:17.... Ni imani inayouzoeza moyo kuwa na dhana ya kuwako na kuwapo kwake Mungu; na sisi tunapoishi tukiwa na jicho safi linalouangalia utukufu wake, tunautambua zaidi na zaidi uzuri wa tabia yake. Roho zetu zinapata nguvu ya kiroho, kwa kuwa tunavuta hewa ile ya mbinguni, na, tukitambua kwamba Mungu yuko mkono wetu wa kuume, hatutaondoshwa.... Tungeishi kana kwamba tuko mbele zake Yule aliye wa milele.... Hekima ya Mungu itaziongoza hatua za wale wanaomtumainia Bwana, nao watatambua kuwapo kwake yule Mfariji, yaani, Roho Mtakatifu. ----- RH, Sept. 8, 1910. "NILIZIONJA FADHILI ZAKE BWANA" Novemba 15 Ikiwa mmeonja ya kwamba Bwana ni mwenye fadhili. 1 Petro 2:3. Je, umepata kuonja ya kwamba Bwana ni mwenye fadhili kwako? Je, njaa yako ya kiroho inakutuma kutamani sana kuongea na Bwana wako? Unaweza kugundua kwamba Bwana ni mwenye fadhili [mwema] kwako, si kwa kupata vyote unavyotamani, bali kwa kuipitia shule ile ya mateso. Mapema sana katika utoto wangu sikupata kitu kingine cho chote cha thamani kwangu isipokuwa maneno ya thamani ya Yesu. Tangu nilipolionja Neno la Mungu katika utamu wake wote, sijapoteza hamu yangu ya kuzidi kulionja. Baada ya kwenda Australia niliugua ugonjwa wa baridi yabisi na malaria. Kwa kipindi cha miezi kumi na moja sikuweza kuwa na uhuru wa kuitumia mikono yangu. Baada ya juma la kwanza la kupigwa na mshangao kutokana na mambo hayo yote yaliyonisibu kuwa yalikuwa na maana gani kwangu, niliamua kwamba ingekuwa vyema sana kwangu kuacha kushangaa, na kujikabidhi mwenyewe mikononi mwake Bwana. Nilionja fadhili zake na kuona kwamba Bwana ni mwenye fadhili [mwema] kwangu. Kitambo kidogo tu wakati wa usiku niliweza kusahau maumivu yangu kiasi cha kuweza kulala usingizi. Hata hivyo, mimi nilionja fadhili zake Bwana. Hisia za kuwapo kwake zikanifungia mbali na ulimwengu huu, hata ikaonekana kana kwamba ningeweza kusema naye ana kwa ana, kama vile Musa alivyofanya. Katika kipindi chote cha maumivu na mateso yangu, nilijisikia ya kuwa nilikuwa na Mwenzi wangu yule wa mbinguni.... Kristo asema hivi, Mimi niko mkono wako wa kuume kukusaidia. Katika udhaifu wetu tungetamani kitu gani zaidi kuliko hicho? Je, kila mmoja wetu amwendee mwenzake na shida zake zote, akiwaeleza wanadamu majaribu tuliyo nayo na jinsi sisi tulivyo dhaifu? Mwokozi anasimama mkono wetu wa kuume, akijitolea kutuinua juu ili tupate "[kuketishwa] pamoja naye katika ulimwengu wa roho, katika Kristo Yesu." Waefeso 2:6. Lakini mara nyingi sana tunageuka na kumpa kisogo yeye na ahadi zake na kuwaeleza shida zetu wale ambao kama sisi, ni wanadamu tu, wenye shida nyingi ambazo ni Kristo tu awezaye kuzichukua.... Hebu tusiendelee kumwaibisha Mungu kwa kugeuka na kumpa kisogo ili kuwaendea wanadamu wasiokuwa na mafanikio yo yote.... Nenda na shida zako kwa Bwana. Mwambie yeye, ukisema, "Mimi niko hapa, Bwana. Wewe unajua mambo yangu yote, nawe ndiwe unayeweza kunisaidia. Nitazifuata nyayo zako na kufanya mapenzi yako." Unapojitoa kabisa kwa Bwana, uwe na hakika kwamba katika nyakati zote za mateso yako utapewa msaada ule ule hasa unaouhitaji. ----- MS 91, 1901. FURAHINI! Novemba 16 Furahini katika Bwana siku zote; tena nasema, Furahini.... Msijisumbue kwa neno lo lote; bali katika kila neno kwa kusali na kuomba, pamoja na kushukuru, haja zenu na zijulikane na Mungu. Wafilipi 4:4-6. Linaweza kuonekana kuwa ni jambo gumu kufurahi katika Bwana unapokabiliwa na shida, lakini tunapoteza mengi sana kwa kujiachia kuwa na roho ya kulalamika. Ni haki yetu kuwa na amani ya Kristo wakati wote mioyoni mwetu. Tusingejiachilia kirahisi kuweza kuvurugwa akili zetu. Ni kwa madhumuni ya kutupima sisi ndiyo maana Mungu anatupitisha katika maonjo na matatizo mbalimbali, na iwapo sisi tutakuwa wastahimilivu na wenye matumaini chini ya kupimwa naye, basi, yeye atatusafisha na uchafu wote, na hatimaye atatutoa tukiwa tunashangilia na kufurahi sana. Mibaraka mingi imewekwa kwa wale wanaonyenyekea pasipo kulalamika wakiwa chini ya nira ambayo Mungu anawataka waivae.... Nuru ya kweli ile uliyo nayo na iangaze katika maisha yako. Je, wewe wasema, Nitaiachaje iangaze? Iwapo kabla hujaipokea kweli hiyo, ulikuwa huna uvumilivu, na tena ulikuwa mwenye kunung'unika, basi, acha maisha yako ya sasa yawaonyeshe wale wanaokuzunguka ya kuwa kweli ile uliyo nayo imekuwa na mvuto wake wa utakaso juu ya moyo wako na juu ya tabia yako, na badala ya wewe kuwa mtu mwenye manung'uniko, asiye na uvumilivu, sasa wewe uwe mchangamfu na uwe mtu usiye na manung'uniko. Kwa njia hiyo unamfunua Kristo kwa ulimwengu.... "Shukuruni kwa kila jambo" (1 Wathesalonike 5:18) kwa ajili ya uweza wa Mungu unaotulinda kwa njia ya Yesu Kristo.... Wakati ule unapotoa sala yako ili kuomba msaada huenda usiweze kujisikia furaha na kupata mibaraka yote ambayo ungependa kujisikia kuwa unayo, lakini kama wewe unasadiki kwamba Kristo atakusaidia na kukujibu dua yako, basi, amani ya Kristo itakujia.... Ukiishika nguvu ya Msaidizi huyo mwenye nguvu, pasipo kuhojiana na adui yako na pasipo kumnung'unikia Mungu, basi, ahadi zake zitathibitika kwako. Uzoefu utakaoupata leo kwa kumtumainia yeye utakusaidia wewe kukabiliana na matatizo ya kesho. Kila siku unatakiwa kuja karibu zaidi na Yesu na Mbingu, ukimtegemea yeye kama vile mtoto mdogo afanyavyo [kwa wazazi wake]. Unapokabiliana na majaribu ya kila siku pamoja na matatizo yake, kama wewe unamtegemea Mungu pasipo kutetereka, hapo ndipo utakapozihakikisha tena na tena ahadi zile za Mbinguni, na kila wakati utajifunza fundisho la imani. Hivyo utapata nguvu ya kuyapinga majaribu, na wakati ule yatakapokujia maonjo makali zaidi, utaweza kuyastahimili. ----- MS 8, 1885. AMANI KATIKA MATESO Novemba 17 Na amani ya Mungu, ipitayo akili zote, itawahifadhi mioyo yenu na nia zenu katika Kristo Yesu. Wafilipi 4:7. Yesu alikuja ulimwenguni si kuwa Mkombozi wa mwanadamu tu, bali kuwa Kielelezo chake kikuu. Maisha yake yalikuwa makamilifu, yaani, maisha yake ya upole, unyenyekevu wa moyo, utakatifu, na imani isiyo na kikomo kwa Mungu.... Kwa matendo alitufundisha sisi fundisho kuu la kuwa na imani tulivu, idumuyo, isiyoyumba kwa Baba yetu wa mbinguni. Anayaruhusu majaribu, maonjo, na mateso kuwajia wapendwa wake. Hayo ni njia zake za kusaidia, mapatilizo yake ya rehema ili kuwarejesha wanapotanga mbali toka ubavuni pake, na kuwa pa hisia yenye kina zaidi ya kuwapo kwake na ulinzi wake unaofaa. Amani ile ipitayo ufahamu si kwa wale wanaojikunyata wanapokabiliwa na maonjo, mapambano, na kujikana nafsi.... Jicho la Yesu li juu yetu kila dakika. Mawingu yanayoingia kati ya roho zetu na Jua lile la Haki yameruhusiwa kutokea katika mpango wake Mungu ili imani yetu ipate kuimarishwa na kuyashikilia matumainio yale makuu, ahadi zake za hakika, ambazo zinang'aa bila utusitusi wo wote katika giza la kila dhoruba. Imani ni lazima ikue kwa njia ya mapambano na mateso. Kila mmoja wetu ni lazima ajifunze kuteseka na kuwa na nguvu, na bila kuzama chini ya udhaifu wetu.... Ni fadhili kuu kwa upande wa Baba yetu aliye mbinguni anapoturuhusu kuwekwa chini ya mazingira yale yanayopunguza mivuto ya ulimwengu huu kwetu, na kutufanya tuweke mapenzi yetu katika mambo yale yaliyoko juu. Mara kwa mara kuipoteza mibaraka ya duniani humu hutufundisha mengi sana kuliko tunapokuwa nayo. Tupitapo katika maonjo na mateso hayo, si ushahidi kwamba Yesu hatupendi sisi, wala kwamba hatupi mibaraka yake. Mwana-Kondoo wa Mungu anayetuhurumia huyafunganisha mapenzi yake pamoja na yale ya watu wake wanaoteseka. Anawalinda kila dakika. Anaijua kila huzuni waliyo nayo; analijua kila shauri analowapa Shetani, na kila shaka linalouumiza moyo.... Anawaombea wale wanaojaribiwa, wanaopotea, na wasiokuwa na imani. Anajitahidi kuwainua ili wapate kushirikiana pamoja naye katika urafiki wake. Ni kazi yake kuwatakasa watu wake, kuwaosha, kuwaadibisha, na kuwasafisha, na kuwajaza mioyo yao na amani yake. Hivyo ndivyo anavyowatayarisha kwa ajili ya utukufu, heshima, na uzima wa milele; kwa ajili ya urithi ule ulio mwingi sana na wa kudumu kuliko ule alio nao mwana wa mfalme ye yote ulimwenguni humu. ----- RH, Agosti 12, 1884. URITHI WA AMANI KUTOKA KWA KRISTO Novemba 18 Amani nawaachieni; amani yangu nawapa; niwapavyo mimi sivyo kama ulimwengu utoavyo. Msifadhaike mioyoni mwenu, wala msiwe na woga. Yohana 14:22. Muda mfupi tu kabla ya kusulibiwa kwake Kristo aliwarithisha wanafunzi wake urithi wa amani.... Amani hii si amani inayokuja kwa kuishi kwa kufanana na ulimwengu huu. Ni amani ya ndani badala ya ile ya nje. Huko nje kutakuwa na vita na mapigano, kutokana na upinzani wa maadui wale wanaojitangaza hivyo wenyewe, na kutokana na ubaridi na shuku ya wale wanaojidai kuwa ni marafiki zetu. Amani yake Kristo haiyaondoi mafarakano. Ijapokuwa yeye alichukua cheo cha Mfalme wa Amani, Kristo alisema maneno haya juu yake mwenyewe, "Msidhani ya kuwa nimekuja kuleta amani duniani; la! sikuja kuleta amani, bali upanga." Mathayo 10:34.... Mfalme wa Amani, hata hivyo, alikuwa ndiye chanzo cha mafarakano hayo. ----- RH, Jan. 16, 1900. Familia ni lazima zifarakane ili wale wote wanaoliitia jina la Bwana wapate kuokolewa. Wale wote wanaoukataa upendo wake wa milele watauona Ukristo kuwa ni upanga, yaani, kuwa kitu kinachovuruga amani yao.... Haiwezekani kwa mtu ye yote kuwa mfuasi wa kweli wa Yesu Kristo bila kujionyesha kuwa yuko tofauti na umati mkubwa wa ulimwengu huu wa wale wasioamini. Kama ulimwengu ungemkubali Yesu, basi, pasingekuwa na upanga wa mafarakano; maana ulimwengu wote ungekuwa wanafunzi wake Kristo, tena wangeshirikiana wao kwa wao, na umoja wao usingevunjika. Lakini hivyo sivyo mambo yalivyo. Hapa na pale mmoja katika familia ni mwaminifu kwa imani ya dhamiri yake, naye hulazimika kusimama peke yake.... Mstari huo wa mpaka unakuwa dhahiri.... Amani ambayo Kristo aliwapa wanafunzi wake, na ambayo sisi tunaomba, ni amani inayozaliwa kutokana na ile kweli, amani ambayo haiwezi kuzimwa kwa sababu ya mafarakano yaliyotokea. Huko nje huenda kukawa na vita na mapigano, kijicho, wivu, chuki, na ugomvi; lakini amani yake Kristo sio ile ambayo ulimwengu huu unatoa au kuondoa. ----- RH, Julai 24, 1894. MSINGI WA AMANI YOTE YA KWELI Novemba 19 Hayo nimewaambieni mpate kuwa na amani ndani yangu. Yohana 16:33. "Mpate kuwa na amani ndani yangu" ----- amani ndani ya Kristo, yaani, amani kwa njia ya Roho wake wa Kweli kwa sababu kuna faraja na tumaini na amani katika kweli. Uongo [mafundisho potofu] hauwezi kutoa amani ya kweli; hiyo inaweza kupokewa tu kwa njia ya ile kweli.... Yesu aliomba kwamba wafuasi wake wawe na umoja; lakini haitupasi sisi kuiacha kweli ili kuupata umoja huo, kwa maana tunapaswa kutakaswa katika hiyo kweli. Hapa ndipo ulipo msingi wa amani yote ya kweli. Hekima ya mwanadamu ingeyageuza [ingeyapindua] yote hayo, na kutamka ya kuwa msingi huo ni mfinyu mno. Wanadamu wangejaribu kuleta umoja kwa njia ya kukubaliana na maoni yale yanayopendwa sana na watu wengi, kwa kukubaliana na ulimwengu, yaani, kuachilia mbali utauwa ulio hai. Lakini kweli ndiyo msingi wa Mungu wa umoja kwa watu wake. Utakaso, umoja, na amani ----- vyote vinaweza kuwa vyetu kwa njia ya hiyo kweli. Kule kuiamini kweli hakuwafanyi watu kununa na kukosa raha. Kama wewe unayo amani ndani yake Kristo, basi, damu yake ya thamani inaitangazia nafsi yako msamaha na tumaini. Naam, zaidi ya hayo, unayo furaha ndani ya Roho Mtakatifu, kwa njia ya kuzipokea ahadi zake za thamani. Yesu asema, "Ulimwenguni mnayo dhiki; lakini jipeni moyo; Mimi nimeushinda ulimwengu." Yohana 16:33. Kwa hiyo, ulimwengu huu hautakushinda wewe ukiniamini Mimi. Ni ulimwengu ambao Mimi nimeushinda. Kwa kuwa mimi nimeshinda, ukiniamini Mimi, nawe utashinda.... Yote yale aliyoyaahidi Yesu, atayatimiza; na ni jambo la kumwaibisha sana kwetu sisi kuwa na mashaka naye. Maneno yake yote ni roho, tena ni uzima. Yakipokewa na kutiiwa, yataleta amani na furaha na imani milele.... Kristo anatangaza kwamba ametupa amani yake; ni yetu sisi. Naye amenena mambo hayo, ili ndani yake tuweze kupata kile ambacho kwa kujitoa kwake mhanga kwa gharama isiyo na kifani alitununulia sisi ----- anachokishikilia kama chetu. Amani hiyo hatuna haja ya kuitafuta ulimwenguni humu, kwa maana ulimwengu hauwezi kuitoa. Imo ndani ya Kristo. Ataitoa yeye, bila kuujali ulimwengu, licha ya vitisho vyake na amri zake, na vishawishi vyake, na ahadi zake zidanganyazo. RH, Aprili 12, l892. UZOEFU WA JUU JUU HAUTOSHI Novemba 20 Mpate kuwa wana wa Mungu wasio na lawama, wala udanganyifu, wasio na ila kati ya kizazi chenye ukaidi, kilichopotoka; ambao kati ya hao mnaonekana kuwa kama mianga katika ulimwengu. Wafilipi 2:15. Sikuzote kuna hatari ya kuridhika na kazi ya juu juu tu; sikuzote ipo hatari kwamba watu hawatatia nanga zao ndani yake Mungu, bali watatosheka na kuchukuliwa na mkondo huku na huko, yaani, kuwa wa kuchezewa na majaribu ya Shetani.... Kazi ya Roho wa Mungu moyoni mwao itakuza toba ya kweli, ambayo haitakomea tu na maungamo, bali itafanya kazi na kuleta matengenezo yaliyo dhahiri katika maisha yao ya kila siku. Itaonekana bidii, uvumilivu, na azma ambayo inaweza kuwakilishwa vizuri kwa kusumbuka sana.... Ukweli kwamba dhambi inazidi, kwamba tumezungukwa na makafiri na wenye mashaka, au wale wanaojidai kuwa ni Wakristo ambao wana jina la kuwa hai, nao wamekufa, hauwezi kuwa sababu ya kumfanya mmoja wetu afagiliwe mbali na mkondo huo kwenda kwenye maangamizi. Kwa kuwa karibu ulimwengu wote umemwacha Mungu, pana haja kubwa zaidi kwamba tusimame tukiwa imara na watiifu.... Yatupasa kukusanya mionzi ile ya mbinguni kutoka kwa yule aliye Jua la haki, na kuiakisi [kuiangaza] ulimwenguni. Kati ya kizazi hiki kikaidi, kilichopotoka, yatupasa kutangaza sifa zake yeye aliyetuita tutoke gizani tuingie katika nuru yake ya ajabu. Hakuna kitu cho chote ambacho kitatuwezesha sisi kufaulu mtihani ule wa maonjo na majaribu, ambayo tutakutana nayo katika vita yetu ya Kikristo, isipokuwa kwa njia ya uzoefu wenye kina wa mtu mmoja mmoja. Mara nyingi sana tunajisikia vizuri wakati kila kitu kinapokwenda vizuri; lakini mashaka yanapoushambulia moyo, na Shetani anaponong'ona mashauri yake humo, hapo ndipo ngome yetu inatoweka, nasi tunaanguka kwa urahisi katika hila za yule mwovu, bila kuwa na juhudi hata kidogo ya kumpinga na kumfukuza. Haitoshi kuwa na hisia nzuri. Moyo hauna budi kuzungushiwa ngome kwa njia ya maombi na kujifunza Neno la Mungu. Akiwa amejihami kwa silaha hizo, Yesu alipambana na adui yake mwerevu sana kwenye uwanja ule wa mapambano, na kumshinda. Sisi sote tunaweza kushinda kwa nguvu zake; ila halitakuwa jibu kwetu kudhani kwamba tunaweza kuondokana na msaada wake. Yeye asema, "Maana pasipo mimi ninyi hamwezi kufanya neno lo lote." Yohana 15:5. Walakini hakuna mtu ye yote aliye mnyenyekevu kweli kweli ambaye anakwenda nuruni kama vile Kristo alivyo nuruni, atakayenaswa kwa hila hizo zidanganyazo za Shetani. ----- ST, Okt. 16, 1904. ANA MIZIZI NDANI YA KRISTO Novemba 21 Mwenye haki atasitawi kama mtende, Atakua kama mwerezi wa Lebanoni. Zaburi 92:12. Mkristo anafananishwa na mwerezi wa Lebanoni. Nimesoma kwamba mti huu unafanya kazi zaidi ya ile ya kuipeleka chini mizizi yake michache iliyo mifupi katika udongo tifutifu wenye rutuba. Unaipeleka mizizi yake yenye nguvu chini sana ardhini, na kuizamisha chini zaidi na zaidi kutafuta mahali pa kujishikilia kwa nguvu zaidi. Na katika tufani kali inayopiga kwa nguvu, unasimama imara, ukiwa umeshikiliwa chini na mtandao wa mizizi yake kana kwamba kwa kamba nene za waya. Hivyo ndivyo Mkristo anavyoizamisha mizizi yake chini ndani ya Kristo. Ana imani kwa Mkombozi wake. Anamjua amwaminiye. Ameamini kabisa ya kwamba Yesu ni Mwana wa Mungu na Mwokozi wa wenye dhambi.... Mizizi ya imani yake inazama chini sana. Wakristo wa kweli, kama mwerezi wa Lebanoni, hawakui katika udongo tifutifu ulio juu ya ardhi, bali wana mizizi ndani yake Mungu, wakiwa wamepigwa ribiti katika nyufa za miamba ya mlima. ----- Letter 95, 1902. Iwapo Mkristo huyo anasitawi na kuendelea mbele, basi, yampasa kufanya hivyo akiwa kati ya watu walio wageni kwa [wasiomjua] Mungu, kati ya kejeli, yaani, kufanyiwa dhihaka mara kwa mara. Yampasa kusimama wima kama mtende jangwani. Mbingu zinaweza kuwa kama shaba nyeupe [hazina mvua], mchanga wa jangwani unaweza kuipiga mizizi ya mtende huku na huku, na kujilundika wenyewe katika malundo kulizunguka shina lake. Hata hivyo mti huo unaendelea kuishi ukiwa na majani mwaka mzima, ukiwa mbichi na wenye nguvu katikati ya mchanga wa jangwani unaounguza. Ondoa mchanga mpaka uifikie mizizi yake midogo ya mtende, nawe utagundua siri ya maisha yake; unazamisha mizizi yake chini sana ya uso wa ardhi, hadi kwenye maji ya siri yaliyofichwa chini ya ardhi. ----- 3BC 1151. Kama vile mtende unaopata lishe yake kutoka katika chemchemi za maji yaliyo hai, unavyokuwa na rangi ya chanikiwiti na kusitawi katikati ya jangwa, hivyo ndivyo Mkristo anavyoweza kupata neema nyingi kutoka kwenye chemchemi ya upendo wa Mungu, naye anaweza kuwaongoza watu waliochoka, wasiotulia kabisa na walio tayari kufa katika jangwa la dhambi, hadi kwenye maji yale wanayoweza kunywa, na kuishi. Daima Mkristo anawaelekeza wanadamu wenzake kwa Yesu, anayeita, akisema, "Mtu akiona kiu, na aje kwangu anywe." Yohana 7:37. Chemchemi hiyo haikauki; tunaweza kuchota, na kuchota tena. ----- 3BC 1151. JE, HUNA MZIZI ULE MKUU? Novemba 22 Basi, ndugu zangu wapendwa, mwimarike, msitikisike, mkazidi sana kutenda kazi ya Bwana sikuzote, kwa kuwa mwajua ya kwamba taabu yenu siyo bure katika Bwana. 1 Wakorintho 15:58. Ili kuweza kutia nanga iliyo imara, ni lazima pawe na kitu kilicho imara ambacho kinatushikilia; na hakuna kitu cho chote kitakachofaa mpaka hapo Kristo atakapoutwaa moyo wetu.... Wengi ambao sasa wanaonekana kuwa wana nguvu, na ambao huzungumza juu ya kuitetea kweli, hawana mizizi wala msingi. Hawana ule mzizi mkuu; na dhoruba za upinzani na mateso zitakapokuja, hao wanafanana na mti uliong'olewa na mizizi yake na upepo mkali. ----- RH, Aprili 29, 1884. Tutashambuliwa kwa kila pointi; tutajaribiwa upeo. Hatutaki kuishika imani yetu ati kwa sababu tu ilikabidhiwa kwetu na mababa zetu. Imani kama hiyo haitasimama wakati wa jaribio la kutisha lililo mbele yetu. Twataka kujua kwa nini sisi ni Waadventista Wasabato ----- sababu gani hasa tunayo kwa kujitenga na ulimwengu kama watu wa pekee na walio tofauti.... Watu wanapotaka kuwa wasomi kuhusiana na kazi ya Mungu kwa sababu wameweka imani na mali yao katika kazi hiyo, Mungu atawasaidia kupata ujuzi nao watakuwa imara katika imani hiyo; ila wanapokuwa na nadharia yake tu, yaani, imani ile isiyo na kina ambayo hawawezi kuifafanua, basi, jaribu la ghafula litawafanya wachukuliwe mbali na mkondo kuelekea ulimwenguni.... Mioyo yetu ni lazima itayarishwe kusimama imara chini ya kila jaribio, na kulipinga kila jaribu, liwe linatoka nje ama ndani. Yatupasa kujua kwa nini tunaamini kama tunavyoamini, kwa nini sisi tuko upande wake Bwana. Kweli hiyo yapasa kutulinda mioyoni mwetu, ikiwa tayari kutoa ilani na kutuita kuchukua hatua dhidi ya kila adui. Nguvu za giza zitapiga mizinga yake juu yetu; na wale wote wasiojali na wazembe, ambao wameyaweka mapenzi yao juu ya hazina iliyomo duniani, na ambao hawakujali kuyajua matendo yake Mungu kwa watu wake, watakuwa wahanga tayari. Hakuna nguvu yo yote ila ujuzi wa ile kweli kama ilivyo katika Yesu, utakaotufanya sisi kuwa imara; lakini tukiwa na ujuzi huo, mtu mmoja atafukuza watu elfu, na wawili watawakimbiza elfu kumi. ----- RH, Aprili, 29, 1884. USHUPAVU UTOKANAO NA DINI ILIYO SAFI Novemba 23 Nami nitakwenda panapo nafasi, Kwa kuwa nimejifunza mausia yako. Zaburi 119:45. Kuna watu wengine wanaozungumza kwa njia inayoonyesha majuto makubwa kuhusu vizuio [mipaka] ambavyo dini ya Biblia inaviweka juu ya wale wanaoyafuata mafundisho yake. Wanaonekana kuwaza ya kwamba kizuio kinaleta hasara kubwa, lakini tunayo sababu ya kumshukuru Mungu kwa moyo wetu wote kwa kukiweka kizuizi cha mbinguni kati yetu na uwanja wa yule adui. Kuna mielekeo fulani ya tabia yetu ya asili [kuzaliwa nayo] ambayo wengi wanafikiri kwamba inapaswa kufuatwa ili maendeleo mazuri sana ya mtu huyo yaweze kupatikana, lakini kile ambacho mwanadamu anafikiri ni cha maana Mungu anakiona kuwa kisingekuwa mbaraka kama ule watu wanaoufikiria kwamba ungefaa kwa wanadamu; kwa sababu kukuza sifa za tabia kama hizo kungewafanya wasiweze kufaa kukaa katika makao yale yaliyoko juu. Mungu anawaweka watu chini ya jaribio na maonjo ili uchafu upate kutenganishwa na dhahabu; ila hamlazimishi mtu ye yote. Hamfungi kwa pingu wala kwa kamba, wala kwa vizuizi; kwa kuwa hivyo vinaongeza chuki kuliko kuipunguza.... Dini ya kweli haina mvuto mfinyu; ni ukosefu wa dini unaouviza uwezo wetu na kuyafanya mawazo yetu kuwa mafinyu. ----- MS 3, 1892. Dini ni kanuni iliyo hai, itendayo kazi, na kutupatia ushupavu wa kutosha kukabiliana na mambo magumu ya maisha haya.... Daima dini inatoa uwezo kwa yule aliye nayo ili kumzuia, kumdhibiti, na kuweka ulinganifu kati ya tabia na akili na mapenzi yake. Ina nguvu ya kushawishi, kusihi, na kuuamuru uwezo wote na mapenzi yote tuliyo nayo kwa kutumia mamlaka ile ya mbinguni. Dini ----- O! natamani sisi sote tungejua inavyofanya kazi yake! Inatuweka sisi chini ya majukumu mazito mno. Tunapojiunganisha na Kristo tunatoa ahadi nzito ya kuenenda kama Kristo alivyoenenda. ----- Letter 25, l882. Ni haki yetu kuzitangaza sifa zake yeye aliyetuita tutoke gizani tuingie katika nuru yake ya ajabu.... Njia ya Bwana ni lazima itunzwe, na njia yake hiyo imetukuzwa katika haki. Wakristo, kwa mwenendo wao na maneno na tabia yao, wanapaswa kuidhihirisha ile asili yao ya mbinguni. Hatupaswi kamwe kuomba radhi kwa ulimwengu kwa sababu sisi tu Wakristo na tunathubutu kufanya haki. ----- Letter 31a, 1894. Dini iliyo safi huleta amani, furaha, kutosheka; utauwa una faida kwa maisha haya na kwa maisha yale yajayo. ----- Letter 1b, 1873. WAKATI UNAOFAA KUWA KIPOFU NA KIZIWI Novemba 24 Ni nani aliye kipofu, ila mtumishi wangu? au aliye kiziwi, kama mjumbe wangu nimtumaye? Ni nani aliye kipofu, kama yeye aliye na amani [mkamilifu]? naam, kipofu kama mtumishi wa BWANA? Unaona mambo mengi, lakini huyatii moyoni; masikio yake ya wazi, lakini hasikii. Isaya 42:19,20 [KJV]. Ni upofu gani huu? Ni upofu ambao hautayaruhusu macho yetu kutazama sana maovu. Hautayaruhusu macho yetu kutulia juu ya maovu. Hautayashika mambo yale yanayoonekana na kuupoteza umilele katika kumbukumbu zake.... Tunataka kuona ipasavyo, tunataka kuona kama vile aonavyo Mungu; maana Shetani anajaribu daima kuyageuza mambo yale ambayo macho yetu yanayaangalia sana ili tupate kuyaona kwa njia yake aliyoichagua.... Mtumishi wa Mungu aliye hai anaona akiwa na kusudi fulani. Macho hutakaswa na masikio nayo hutakaswa, na wale watakaofumba macho na masikio yao wasiyaangalie maovu watabadilika. Lakini endapo watawasikiliza wale wanaozungumza nao na wanaojaribu kuyaongoza mawazo yao mbali na Mungu na mbali na mambo yao yale ya milele, basi, hapo ndipo fahamu zao zote zitapotolewa kutokana na kile macho yao yanachokiangalia sana. Yesu asema, "Basi... jicho lako likiwa safi, mwili wako wote utakuwa na nuru. Lakini jicho lako likiwa bovu, mwili wako wote utakuwa na giza." Mathayo 6:22,23. Inaleta tofauti kubwa juu ya kile tunachoilisha mioyo yetu na roho zetu. Tunaweza kuiacha mioyo yetu kutafakari sana hadithi zile za mahaba na ndoto zisizowezekana, je! hayo yatatufanyia nini sisi? Yatatuangamiza, mwili na roho.... Twataka kuwa na nguvu ile itakayotuwezesha kuyafumba macho yetu kwa mandhari [picha] zile zisizokuwa nzuri; zisizotuadilisha tabia zetu, zile ambazo hazitatutakasa na kutufanya kuwa waungwana; na kuziba masikio yetu kwa kila kitu kilichokatazwa katika Neno la Mungu. Anatukataza kuwaza maovu, kusema maovu, na hata kutafakari maovu.... Ndani ya Yesu mimi naona kila kitu kilicho chema, kila kitu kilicho kitakatifu, kila kitu kinachotia moyo na kilicho safi. Basi, kwa nini mimi nipende kuyafumbua macho yangu sana ili kuangalia kila kitu kinachochukiza? Kwa kutazama tunabadilishwa. Na tumtazame Yesu na kuutafakari uzuri wa tabia yake, na kwa kutazama tutabadilishwa tupate kufanana na sura yake. ----- MS 17, 1894. ACHA MKONO WA MUNGU UFINYANGE UDONGO Novemba 25 Lakini sasa, Ee BWANA, wewe u baba yetu; Sisi tu udongo, nawe u mfinyanzi wetu; Sisi sote tu watu wako. Isaya 64:8. Hatujui Mungu atakachotutendea sisi kama tutakubaliana naye. Mungu anaona anavyoweza kumfinyanga mwanadamu. Kuna uwezekano mwingi sana ambao imani yetu hafifu haiwezi kuutambua. "Ninyi ni shamba la Mungu, ni jengo la Mungu." 1 Wakorintho 3:9. Anaziona tabia zote za uadui zilizo ndani ya mwanadamu sasa, naye anajua kwamba kama wanadamu watajifunza upole na unyenyekevu wa moyo alio nao Kristo, basi, yeye anaweza kuifinyanga na kuitengeneza tabia ile ya ugomvi, yaani, tabia ya uadui, na kuileta kila nguvu ya mwili katika hali nzuri ya utendaji ili kuuendeleza ufalme wake. Anatamani sana kuyatakasa, kuyainua juu, na kuyaboresha maisha yake yote.... Kwa uwezo wa Roho Mtakatifu anaweza kuwatumia watu wale wale walio na tabia mbaya kupindukia, na kuwafanya wawe wanaume na wanawake wenye nafasi nzuri. Heri mtu yule ambaye kwa imani anaweza kuiona angalau kidogo tu imani aliyo nayo Kristo.... Hapo ndipo uwezekano unakuwapo wa kufanana na Kristo kitabia.... Nuru kuu humjia mwanadamu anapoziona haki zile ambazo ni zake. Anaiona mipango ya Mungu kwa ajili yake, naye anaifia nafsi yake.... Anakubali kufanyiwa kazi.... Anapokubali kuwa kama udongo mikononi mwa mfinyanzi, hapo ndipo Mungu anamfinyanga mtu huyo kuwa chombo chake cha heshima. ----- Letter 63, 1898. Udongo mikononi mwa mfinyanzi... unageuzwa tena na tena mpaka mapenzi ya mfinyanzi yanapotimilika kwa chombo hicho. Neema na kweli huikamilisha kazi hiyo ya kuufinyanga udongo huo wa kibinadamu, ili utukufu wa Mfinyanzi Mkuu uonekane katika kukitengeneza chombo chenye umbo zuri, kilichofinyangwa na kulainishwa tayari kwa kazi yake. ----- Letter 48, 1888. Mfinyanzi hawezi kukifinyanga na kukitengeneza kuwa chombo cha heshima kile ambacho kamwe hakijawekwa mikononi mwake. Maisha ya Kikristo ni ya kujisalimisha kila siku, kutii, na kuendelea kupata ushindi. Kila siku ushindi mpya utapatikana. Nafsi inatakiwa isionekane kabisa, na upendo wa Mungu unatakiwa kukuzwa daima. Hivyo ndivyo tunavyokua katika Kristo. Hivyo ndivyo maisha yanavyotengenezwa kulingana na Kielelezo kile cha mbinguni [Kristo]. ----- 4BC 1154. Acha mkono wa Mungu ufinyange udongo kwa ajili ya kazi yake. Anajua ni chombo cha aina gani hasa anachotaka. ----- Letter 63, 1898. JIJARIBUNI WENYEWE Novemba 26 Jijaribuni wenyewe kwamba mmekuwa katika imani; jithibitisheni wenyewe. Au hamjijui wenyewe, kwamba Yesu Kristo yu ndani yenu? isipokuwa mmekataliwa. 2 Wakorintho 13:5. "Jijaribuni wenyewe kwamba mmekuwa katika imani." Wengi... wanaweza kujibu mara moja, wakisema, "Naam; mimi nimo katika imani, ninaliamini kila neno la ile kweli." Lakini, je! mnatenda kile mnachokiamini? Mnayo amani na Mungu pamoja na ndugu zenu? Mnaweza kuomba kwa moyo mnyofu, mkisema, "Utusamehe deni zetu, kama sisi nasi tuwasamehevyo wadeni wetu"?... Je! hamna uchungu wo wote mioyoni mwenu, wala wivu, wala kijicho, wala kuwafikiria wengine vibaya?... Je! hakuna husuda, wala tamaa ya kupata upendeleo na heshima fulani, wala kutaka makuu?... Twafanya vema kujijaribu wenyewe kuona ni roho gani tuliyo nayo ndani yetu. Hebu na tujifunze kusema kwa upole, kwa kimya,hata chini ya mazingira yanayoleta usumbufu mwingi kwetu. Hebu na tujizuie si katika maneno yetu tu, bali katika mawazo yetu na dhana zetu. Hebu na tuwe wapole, wenye heshima. ----- RH, Aprili 29, 1884. Wengi wanautambua upungufu mkubwa walio nao, nao husoma, huomba, na kuweka maazimio, lakini hawana maendeleo yo yote. Wanaonekana kama hawana nguvu kabisa ya kuyapinga majaribu yao. Sababu yenyewe ni kwamba, hawaendi chini zaidi ya kutosha. Hawajitahidi kuongoka kabisa katika moyo wao, ili vijito vinavyotoka humo viwe safi, na mwenendo wao upate kushuhudia ya kwamba Kristo anatawala ndani yao. Kasoro zote za tabia huanzia moyoni. Kiburi, ubatili, hasira mbaya, na uchoyo hutoka ndani ya moyo wa asili ambao haujafanywa kuwa mpya kwa neema yake Kristo. Iwapo moyo umesafishwa, umelainishwa, na kuadilishwa, basi, maneno na matendo yatashuhudia ukweli wa jambo hilo. Moyo unapokuwa umesalimishwa kabisa kwa Mungu, patakuwa na tegemeo lililo imara juu ya ahadi zake, tena patakuwa maombi ya bidii na juhudi dhahiri katika kutaka kuyadhibiti maneno na matendo yao. ----- RH, Sept. 1, 1885. Imani tunayoitangaza ni kuu na takatifu; na tabia zetu nazo zinapaswa kulingana na imani hiyo, pamoja na kanuni ile kuu ya Mungu ya Maadili [Amri Kumi].... Hebu na tujijaribu mioyo yetu katika nuru ya kanuni ile kuu ya Sheria ya Mungu kama ilivyofafanuliwa na Kristo: "Mpende Bwana Mungu wako kwa moyo wako wote,... na kwa akili zako zote; na jirani yako kama nafsi yako." Luka 10:27. ----- RH, Aprili 29, 1884. UJILINDE NAFSI YAKO UWE SAFI Novemba 27 Heri wenye moyo safi; maana hao watamwona Mungu. Mathayo 5:8. Kujua kile kinacholeta usafi wa nafsi, roho, na mwili ni elimu ya daraja la juu kabisa. Mtume Paulo anatoa muhtasari katika waraka wake kwa Timotheo kuhusu mafanikio yanayowezekana kwake, akisema, "Ujilinde nafsi yako uwe safi." ----- Letter 145, 1897. Ni kazi maalum ya Shetani katika siku hizi za mwisho kuitawala mioyo ya vijana, kuyachafua mawazo yao, na kuziwasha tamaa zao za mwili. Wote ni mawakala huru [wana uhuru wa kuchagua watakalofanya] kimaadili, na mambo yakiwa hivyo, basi, inawapasa kuyaongoza mawazo yao kwenda katika njia ile ya uadilifu.... Shetani akijaribu kuugeuza moyo wako kuelekea kwenye mambo yale yaliyo duni na yanayohusu tamaa mbaya za mwili, urudishe tena mahali pake, na kuuelekeza kwenye mambo yale ya milele; na Bwana anapoiona juhudi yako dhahiri katika kuyatunza mawazo yale yaliyo safi tu, basi, atauvuta moyo wako kwake, kama vile sumaku ifanyavyo, na kuyasafisha mawazo yako.... Kazi ya kwanza kwa wale ambao wangependa kufanya matengenezo ni kuyatakasa mawazo yao. Kama mawazo yako yanaelekea upande ule wa mabaya, basi, ni lazima yazuiwe ili yapate kutafakari tu juu ya mambo yale yaliyo safi na yale yaliyo mema. Unapojaribiwa kuyaachia mawazo machafu kuendelea kukutawala, hapo ndipo inakupasa wewe kukimbilia kwenye kiti kile cha neema, na kuomba nguvu kutoka mbinguni. Katika nguvu zake Mungu mawazo yako yanaweza kudhibitiwa ili yadumu katika kutafakari mambo yale yaliyo safi na yale ya mbinguni.... Wale ambao wangependa kuwa na hekima ile itokayo kwa Mungu, hawana budi kuwa wapumbavu katika maarifa ya dhambi ya kizazi hiki, ili wapate kuwa na hekima. Wangeyafumba macho yao, ili wasione na kujifunza maovu. Wangeyaziba masikio yao, wasije wakasikia yale yaliyo maovu, na kujipatia maarifa yale ambayo yangetia doa katika usafi wa mawazo na matendo yao. Nao wangepaswa kuzichunga ndimi zao, wasije wakatamka maneno machafu, na hila ikaonekana vinywani mwao. Wote watatoa hesabu kwa matendo yao katika kipindi chao cha majaribio humu duniani. Wote wanao uwezo wa kuyatawala matendo yao. Kama wao wana udhaifu kwa upande wa kutenda mema na katika kuyatakasa mawazo na matendo yao, basi, wanaweza kupata msaada kutoka kwa Rafiki wa wale wasiokuwa na msaada. Yesu anaujua udhaifu wote wa tabia ya asili ya kibinadamu, na iwapo ataombwa sana, atatoa nguvu ya kuweza kuyashinda majaribu yenye nguvu nyingi kabisa. Wote wanaweza kupata nguvu kama wakiitafuta kwa moyo wa unyenyekevu. ----- Undated MS 93. "HATA KUWA MTU MKAMILIFU" Novemba 28 Hata na sisi sote tutakaopoufikia umoja wa imani na kumfahamu sana Mwana wa Mungu, hata kuwa mtu mkamilifu, hata kufika kwenye cheo cha kimo cha utimilifu wa Kristo. Waefeso 4:13. Ni kazi kubwa, nzito, kujipatia uadilifu [mwenendo mwema] unaofaa utakaotuwezesha kukaa pamoja na jamii ile ya watakatifu na ya wale waliobarikiwa.... Ni kwa kulifuata Neno la Mungu peke yake sisi tunaweza kutumainia kufika "kwenye cheo cha kimo cha utimilifu wa Kristo." Lakini ni lazima sisi tufanye hivyo, vinginevyo, hatutaingia kamwe mbinguni. Pasipokuwa na usafi na utakatifu wa moyo, hatuwezi kupata ile taji ya utukufu wa milele. ----- RH, Mei 30, 1882. Maisha ya kiroho hayawezi kudumishwa, isipokuwa kwa kuyatumia ipasavyo mapenzi yetu na kuyaelekeza mbinguni, kuyaelekeza kwa Kristo, kuyaelekeza kwa Mungu. Toba na imani katika Kristo kwa ajili ya msamaha wa dhambi zetu ni muhimu kwetu, lakini sio vyote hivyo vinavyotakiwa.... Maisha ya Mkristo sasa ndipo yanaanza tu. Anapaswa "kuendelea hata kuwa mtu mkamilifu," kama alivyoshauri mtume huyo. Anapaswa kuliteka kila wazo ili lipate kumtii Kristo. Iwapo sisi tunamwanini Yesu, basi, tutapenda kumtafakari yeye, kuzungumza habari zake, kupeleka maombi yetu kwake. Yeye anapewa kipaumbele katika mapenzi yetu. Tunakipenda kile anachokipenda Kristo, na kukichukia kile anachokichukia Kristo.... Maisha ya Kikristo hayasimami pale pale kamwe. Yanasonga mbele, na ni lazima yasonge mbele. Upendo wetu kwa Kristo ungezidi kuwa na nguvu zaidi na zaidi.... Ee ndugu yangu, ee dada yangu, je! moyo wako u katika pendo lake Mungu? Wengi wenu mna nuru iliyo na utusitusi [giza-giza] katika kuufahamu ukuu alio nao Kristo ambao unapita upeo, na moyo wenu husisimka kwa furaha. Mnatamani sana kuwa na ufahamu wa upendo wake Mwokozi ulio kamili zaidi, yaani, wenye kina zaidi. Mnatamani sana kuyafunga mapenzi yenu karibu sana na Mwokozi. Hamjatosheka. Lakini msikate tamaa. Mpeni Yesu mapenzi yenu yote, yaliyo matakatifu sana, ya moyo wenu. Uhifadhini kila mwonzi wa nuru mnayopokea. Itunzeni kila tamaa ya moyo wenu ipate kumwelekea Mungu. Jizoezeni kuyakuza mawazo yenu ya kiroho na kuwa na maongezi matakatifu.... Harakisheni kukomaa [kupevuka] kwenu kwa ajili ya Mbingu.... Itatugharimu kitu fulani kujipatia uzoefu wa maisha ya Kikristo na kukuza tabia ile iliyo nyofu na nzuri.... Lakini ule mkutano mkubwa sana wa waliokombolewa uliovaa mavazi yale meupe, unatokana na wale walioyafua mavazi yao, na kuyafanya meupe katika damu ya Mwana-Kondoo. ----- RH, Mei 30, 1882. KUMWONA YEYE ASIYEONEKANA Novemba 29 Kwa imani Musa alipokuwa mtu mzima, akakataa kuitwa mwana wa binti Farao.... Kwa imani akatoka Misri, asiogope ghadhabu ya mfalme; maana alistahimili kama amwonaye yeye asiyeonekana. Waebrania 11:24-27. Musa... aliishi kama amwonaye yeye asiyeonekana, na kwa sababu hiyo aliweza kuhesabu ya kuwa kushutumiwa kwake Kristo ni utajiri mkuu kuliko hazina za Misri. Iwapo watu wangeishi hivyo, basi, tungeweza kuziona nyuso zao zikiwaka kwa utukufu wa yule aliye wa milele, na kwa kutazama, wangeweza kubadilishwa katika sura yake Kristo. ----- ST, Jan. 9, 1893. Mioyo yetu huchukua usawa ule ule wa mambo yale mawazo yetu yanayoyatafakari sana, na kama tunatafakari sana mambo ya ulimwengu huu, basi, tutashindwa kuichukua picha ya mambo yale ya mbinguni mioyoni mwetu. Tungenufaika sana kwa kutafakari juu ya rehema, fadhili, na upendo wa Mungu; lakini tunapata hasara kubwa kwa kuyatafakari mambo yale ya kidunia na yale yanayohusu maisha yetu ya kila siku. Tunakaribisha huzuni na masumbufu na matatizo ili vipate kuivuta mioyo yetu kuelekea duniani, tena, tunakikuza kichuguu kionekane kama mlima mrefu.... Mambo ya maisha yetu ya kila siku hayapaswi... kuishughulisha sana mioyo yetu mpaka mawazo yetu yawe kabisa ya ulimwengu huu na ya kidunia. Tunatakiwa kuufunza, kuuadilisha, na kuuelimisha moyo wetu kiasi cha kuweza kufikiri kwa njia ile ya mbinguni, ili tupate kuyatafakari mambo yale yasiyoonekana na ya milele, ambayo yatatambulikana kwa macho ya kiroho. Ni kwa kumwona yeye asiyeonekana ndipo sisi tunaweza kupata nguvu yetu ya kiakili na nguvu yetu ya kiroho.... Po pote pale majaliwa ya Mungu yanapotuita kwenda, tunaweza, kwa imani, kutazamia kwamba Mungu atakuwa ndiye msaidizi wetu. Hatupaswi kuchezewa kama mwanaserere na mambo yale yanayotuzunguka, bali tunapaswa kuishi juu ya mambo hayo.... Tunapowekwa mahali penye majaribu makali, na kuona mambo yanayotuzunguka tusiyoyataka yakitujaribu uvumilivu wetu, na kutupima imani yetu, basi, hapo hatupaswi kufa moyo, bali kumshikilia Mungu kwa nguvu zaidi, na kuonyesha ya kwamba sisi hatuyaweki mapenzi yetu katika mambo ya ulimwengu huu, bali katika mambo yale yaliyo juu; kwamba sisi tunamtazama Yesu, mwenye kuanzisha na mwenye kutimiza imani yetu. Ni lazima Yesu awe ndiye mwanzo na mwisho, wa kwanza na wa mwisho. Yeye ndiye anayepaswa kuwa nguvu yetu katika wakati wote wa kujaribiwa. ----- ST, Jan. 9, 1893. KUVUTWA KWA UZURI WA UPENDO WAKE KRISTO Novemba 30 Basi mkiwa mmefufuliwa pamoja na Kristo, yatafuteni yaliyo juu Kristo aliko, ameketi mkono wa kuume wa Mungu. Yafikirini yaliyo juu, siyo yaliyo katika nchi. Wakolosai 3:1,2. Tunapojaribiwa kuyaweka mapenzi yetu juu ya kitu cho chote cha kidunia ambacho kina mwelekeo wa kuyachota mapenzi yetu yote, basi, hatuna budi kuitafuta neema ya kutuwezesha kukipa kisogo kitu hicho, wala tusikiruhusu kuingia kati yetu na Mungu wetu. Tunataka kuweka mbele ya jicho la moyo wetu makao yale ambayo Yesu amekwenda kutuandalia. Tusiruhusu nyumba zetu na mashamba yetu, shughuli zetu za kibiashara na shughuli za uchumi wa ulimwengu huu kuingia kati yetu na Mungu wetu. Mbele yetu ingetupasa kuziweka ahadi zile za thamani ambazo ametuachia katika kumbukumbu zake. Tungejifunza njia zile kuu zinazoonyesha nyakati tunazoishi.... Sasa ingetupasa sisi kuomba kwa bidii sana ili tupate kuwa tayari kwa mapambano ya siku ile kuu ya maandalizi ya Mungu. Tungefurahia matumaini yetu ya kuwa pamoja na Yesu upesi katika makao yale aliyokwenda kutuandalia.... Yesu anaweza kukidhi kila hitaji ulilo nalo.... Unapomtazama yeye utavutwa kwa utajiri wa utukufu wa upendo wa Mungu. Upendo wa kuviabudu vitu vile vinavyoonekana utamezwa na upendo ule wa hali ya juu, ulio bora sana wa vitu vile visivyoharibika na vya thamani. Unaweza kutafakari utajiri ule wa milele mpaka mapenzi yako yafungwe pamoja na mambo yale yaliyo juu, na wewe unaweza kuwa chombo cha kuwaongoza wengine ili wayaweke mapenzi yao juu ya hazina zile za mbinguni.... Wale wanaoithamini fedha kama ipasavyo ni wale wanauona upatikanaji wake kuwa ni kwa kusudi la kuipeleka kweli mbele ya wale ambao hawajapata kuisikia kamwe, na kwa njia hiyo kuwaokoa kutoka katika uwezo wa yule adui. Kama mtu mmoja anaipokea kweli, basi, upendo wake kwa mambo ya dunia utang'olewa. Atauona uzuri ule usiokuwa na kifani wa utukufu wa mambo yale ya mbinguni, atautambua ukuu wa mambo yale yanayohusu uzima wa milele. Atavutiwa sana na mambo yale yasiyoonekana, yaani, ya milele. Atalegeza kuvishikilia sana vitu vya ulimwengu huu. Atakaza macho yake kwa mshangao kuuangalia utukufu ule usioshindikana wa ulimwengu ule mwingine. Atatambua kwamba maonjo yake yanafanya kazi kumletea utukufu wa milele uzidio kuwa mwingi sana, na kwa kulinganisha na utajiri ule ambao ni wake kuufurahia, anahesabu dhiki yake kuwa ni nyepesi, iliyo ya muda wa kitambo tu. ----- Letter 97, 1895. ONYESHA TABIA YAKO ILIVYO HASA! Desemba 1 Macho yako yatazame mbele, Na kope zako zitazame mbele yako sawasawa. Mithali 4:25. Katika kitabu cha Safari ya Msafiri (Pilgrim's Progress) kuna mhusika mmoja aitwaye Mwelekevu [Mwenye kushawishika kwa urahisi]. Enyi vijana, iepukeni tabia hiyo. Wale wanaowakilishwa kwa tabia hiyo ni wepesi kubadilishwa msimamo wao, lakini ni kama tete linalotikiswa na upepo. Hawana uthabiti wa moyo wala nia thabiti. Kila kijana anahitaji kujizoeza kukata shauri. Hali ya mgawanyiko wa nia ni mtego, na itakuwa maangamizi ya vijana wengi. Uwe shupavu, vinginevyo utaachwa na nyumba yako, yaani, tabia yako, ikiwa imejengwa juu ya msingi wa mchanga.... Onyesha msimamo wako kwa gharama iwayo yote.... Wale ambao wangeweza kwenda katika njia ile iendayo juu iliyowekwa kwa ajili ya wateule wa Bwana, hawapaswi kuyumbishwa katika mambo yale yanayohusu dhamiri na watu wale walio na bidii ya kutenda maovu. Yawapasa kuonyesha uhuru wa kimaadili walio nao, tena wanapaswa kutoogopa kusimama peke yao.... Wengi wanageuzwa huku na huku na kila mkondo unaopita. Wanangoja kusikiliza kile anachofikiri mtu mwingine, na wazo lake linakubalika kama ni la kweli kabisa. Endapo wangeegamia kabisa kwa Mungu, wangekuwa na nguvu katika nguvu zake; walakini wao hawasemi hivi kwa Bwana, Mimi siwezi kukata shauri lo lote mpaka [kwanza] niyajue mapenzi yake. Mwelekeo wao wa asili ni kumruhusu mtu mwingine kuwa dhamiri kwa ajili yao; nao wanasema baada ya yeye kumaliza kusema, wakisema yale yale asemayo, na kutenda kama anavyotenda. Watu hao wakiwekwa katika mazingira ambayo yatawalazimisha kufikiri na kutenda wao wenyewe, hawatathubutu kutamka wazo lo lote lililo dhahiri. Hata hivyo, mara nyingi, kama vile Haruni, wanao uwezo mwingi. Mungu na awahurumie watu dhaifu kama hao.... Yatupasa kujiweka huru mbali na mila na utumwa wa jamii [tunamoishi], ili kwamba kanuni za imani yetu zinapokuwa hatarini, tusisite kuonyesha tabia yetu, hata kama tutaitwa kuwa ni wa wa pekee kwa kufanya hivyo. Dhamiri yako na iwe nyororo, ili upate kusikia mnong'ono wa chini kabisa wa sauti ile iliyosema asivyopata kusema mtu mwingine ye yote. Hebu wale wote ambao wangependa kujitia nira yake Kristo waonyeshe kusudi lao thabiti kwa kutenda haki kwa sababu ni haki. Kaza macho yako juu kwa Yesu, ukijiuliza kwa kila hatua unayochukua, Je! hivi hii ndiyo njia ya Bwana? Bwana hatamwacha ye yote anayefanya hivyo kuwa uwanja wa Shetani wa majaribu yake.... Msiwaige watu. Jifunzeni Biblia zenu, na kumwiga Kristo. ----- RH, Mei 9, 1899. HAKUNA DINI YA VIRAKARAKA! Desemba 2 Lakini mwenye kuvumilia hata mwisho, ndiye atakayeokoka. Mathayo 24:13. Dini iliyojengwa juu ya nafsi haifai kitu; maana Mungu hafanyi mapatano yo yote na uchoyo.... Dini ya Kristo ni kitambaa imara, kilichotengenezwa kwa busara na ustadi. Ni kwa hekima ya Mungu peke yake anayotupa, tunaweza kukifuma kitambaa hicho. Tunapojitumainia sisi wenyewe, tunaweka ndani yake nyuzi za ubinafsi, na kiolezo hicho kinaharibika. Kuna aina nyingi za vitambaa ambavyo mwanzoni huonekana kuwa vina mwonekano mzuri, lakini havistahimili jaribio. Rangi zake sio za kudumu. Zinachujuka. Wakati wa jua lile la kiangazi zinachujuka na kutoweka. Kitambaa kama hicho hakiwezi kustahimili kushikwa ovyo ovyo, tena thamani yake ni ndogo sana. Hivyo ndivyo ilivyo dini. Wakati nyuzi za kufumia kitambaa cha dini zinaposhindwa kustahimili jaribio la maonjo, aina ya kitambaa kile kilichofumwa na nyuzi hizo huwa hakifai kabisa. Na juhudi ya kuweka kiraka katika kitambaa kile cha zamani haifanyi hali ya mambo kuwa bora; maana kitambaa hicho kichakavu, hafifu, huchanika kutoka kwenye kitambaa kile kipya, na kuacha sehemu iliyapasuka kuwa kubwa kuliko ilivyokuwa mwanzoni. Kushona viraka hakutasaidia kitu. Njia pekee ni kulitupa vazi lile la zamani na kununua jipya. Dini iliyojengwa juu ya nafsi, iliyo na nyuzi zinazochujuka na kuchanika chini ya msongo wa majaribu, ni lazima itupwe kando, mahali pake iwekwe dini ile iliyofumwa na yule ambaye katika maisha yake yote hakuwa na uchoyo wo wote. Mpango wa Kristo ndio ulio salama peke yake. Anatangaza, akisema, "Tazama, nayafanya yote kuwa mapya." Ufunuo 21:5. "Mtu akiwa ndani ya Kristo amekuwa kiumbe kipya." 2 Wakorintho 5:17. Mwokozi hamtii moyo mtu ye yote kudhani ya kwamba ataikubali dini yo yote ya virakaraka. Dini kama hiyo haina thamani yo yote machoni pake. Mwanzoni inaweza kuonekana kuwa ina sehemu fulani ya nafsi na sehemu fulani ya Kristo; lakini punde huonekana kwamba hakuna sehemu yo yote ya Kristo ndani yake. Viraka vya uchoyo huongezeka mpaka vazi lote limefunikwa navyo.... Dini iliyojengwa kwa mfano wa Kiolezo kile cha mbinguni [Kristo] ndiyo peke yake itakayodumu. Ni kwa kujitahidi kuishi maisha yale ya Kristo hapa ndipo tunaweza kujiandaa kuishi pamoja naye milele zote. ----- ST, Jan. 8, 1902. ISHARA YA PEKEE YA MUNGU Desemba 3 Mimi ni BWANA, Mungu wenu; endeni katika amri zangu, mkazishike hukumu zangu, na kuzitenda; zitakaseni sabato zangu; zitakuwa ishara kati ya mimi na ninyi, mpate kujua ya kuwa mimi ndimi BWANA, Mungu wenu. Ezekieli 20:19,20. Sabato ilitolewa kwa wanadamu wote kusherehekea kazi ya Uumbaji. Yehova mkuu, alipokwisha kuiweka misingi ya nchi hii, alipoivika dunia nzima kwa vazi lake zuri, na kuyaumba maajabu yote juu ya nchi na baharini, aliiweka siku ya Sabato na kuitakasa. Nyota za asubuhi zilipoimba pamoja na wana wote wa Mungu walipopiga kelele kwa furaha, Sabato ilitengwa na kuwa kumbukumbu ya Mungu. Mungu aliitakasa na kuibariki siku hiyo aliyokuwa amepumzika kwa kuacha kufanya kazi yake yote ya ajabu.... Kama vile mti ule wa ujuzi wa mema na mabaya ulivyowekwa katikati ya Bustani ile ya Edeni, ndivyo amri ile ya Sabato ilivyowekwa katikati ya Sheria ile ya Amri Kumi. Kuhusu matunda ya mti wa ujuzi wa mema na mabaya, kizuizi kiliwekwa, "Msiyale... msije mkafa." Mwanzo 3:3. Kwa habari ya Sabato, Mungu alisema, Hamtainajisi, bali mtaitakasa. "Ikumbuke siku ya Sabato uitakase." Kutoka 20:8. Kama vile mti ule wa ujuzi wa mema na mabaya ulivyokuwa jaribio la utii kwake Adamu, ndivyo amri hiyo ya nne ni jaribio alilotoa kuupima utii wa watu wake wote. ----- RH, Agosti 30, 1898. Sabato ni ishara kati ya Mungu na watu wake. Ni siku takatifu iliyotolewa na Muumbaji kwa mwanadamu kama siku ya kupumzika, na kutafakari juu ya mambo matakatifu. Mungu aliiweka ili itunzwe katika kila kizazi kama agano la milele. Ilitakiwa iangaliwe kama hazina ya pekee, amana ya kutunzwa kwa uangalifu. Tunapoitunza Sabato hebu na tukumbuke ya kwamba ni ishara ambayo mbingu imempa mwanadamu kuonyesha kwamba anakubalika katika yule Mpendwa; kwamba akitii anaweza kuingia katika mji ule wa Mungu, na kula matunda ya mti wa uzima. Tunapoacha kufanya kazi siku ile ya saba, tunashuhudia kwa ulimwengu huu kwamba sisi tu upande wa Mungu, nasi tunajitahidi kuishi kwa kupatana kabisa na amri zake [kumi]. Kwa njia hiyo tunamtambua Mungu kama Mfalme wetu aliyeiumba nchi katika siku sita na kupumzika siku ya saba. Sabato ni kifungo kinachowaunganisha Mungu na watu wake. ----- RH, Okt. 28, 1902. KATIKA WAKATI ULE WA KUJARIBIWA Desemba 4 Basi jueni ya kuwa BWANA, Mungu wenu, ndiye Mungu; Mungu mwaminifu, ashikaye agano lake na rehema zake kwao wampendao, na kushika amri zake, hata vizazi elfu. Kumbukumbu la Torati 7:9. Tutakuwa wapi kabla ya vizazi hivyo elfu vilivyotajwa katika andiko hilo kufikia mwisho wake? Mwisho wetu utakuwa umeamuliwa kwa milele zote. Ama tutakuwa tumetangazwa kuwa tunastahili kuwa na makao katika ufalme wa Mungu ule wa milele, ama tutakuwa tumepokea hukumu ya mauti ya milele. ----- RH, agosti 4, 1904. Mungu anawapima watu wake, kuona ni akina nani watakaokuwa watiifu kwa kanuni za kweli yake. Kazi yetu ni kuutangazia ulimwengu ujumbe wa malaika wa kwanza, wa pili, na wa tatu. Katika kutekeleza majukumu yetu hatupaswi kuwadharau wala kuwaogopa adui zetu.... Sabato ya kweli inapaswa kuwa ishara inayowatofautisha wale wanaomtumikia Mungu na wale wasiomtumikia. Hebu wale wanaosinzia na wale wasiojali waamke. Tunaitwa kuwa watakatifu, na kwa uangalifu tungejiepusha tusionyeshe picha kwamba ni jambo lisilo na matokeo makubwa sana kama tunahifadhi au hatuhifadhi sehemu muhimu za imani yetu hii ya pekee. Wajibu mzito unatukalia sisi ili tupate kuchukua msimamo thabiti zaidi kwa ajili ya kweli na haki kuliko tulivyofanya wakati uliopita. Mstari unaogawa kati ya wale wanaozishika amri [kumi] za Mungu na wale wasiozishika unapaswa kuonyeshwa wazi bila kukosea. Kwa dhati tunatakiwa kumheshimu Mungu, kwa bidii tukitumia kila njia kutunza uhusiano wetu wa agano pamoja naye, ili tupate kuipokea mibaraka yake ----- mibaraka muhimu sana kwa watu ambao wanatazamia kujaribiwa vikali sana. Kutoa picha inayoonyesha kwamba imani yetu, yaani, dini yetu, sio uwezo unaotutawala maishani mwetu ni kumfedhehesha Mungu sana. ----- RH, Agosti 4, 1904. Tukiwa tumeliweka tumaini letu kwa Mungu, inatupasa kusonga mbele kwa taratibu, tukifanya kazi yake pasipo kuwa na ubinafsi, tukimtegemea kwa moyo wa unyenyekevu, tukijikabidhi sisi wenyewe na mambo yetu ya sasa na yale ya baadaye katika uongozi wake wenye hekima, tukishimanana sana na mwanzo wa ujasiri wetu mpaka mwisho, tukikumbuka kwamba si kwa sababu ya kufaa kwetu tunapokea mibaraka hiyo ya mbinguni, bali ni kwa sababu ya kufaa kwake Kristo, na ukubali wetu kwa njia ya imani katika yeye wa neema ya Mungu nyingi sana. ----- RH, Agosti 4, 1904. WATU TULIO TOFAUTI NA WA PEKEE Desemba 5 Hapa ndipo penye subira ya watakatifu, hao wazishikao amri [kumi] za Mungu, na imani ya Yesu. Ufunuo 14:12. Watu wa Mungu wanapaswa kutambulikana kama watu wanaomtumikia yeye kikamilifu, kwa moyo wote, pasipo kujichukulia heshima wao wenyewe, na kukumbuka ya kwamba kwa agano zito mno wamejifunga wenyewe kumtumikia Bwana, na yeye peke yake.... Wana wa Israeli walitakiwa kuitunza Sabato katika vizazi vyao vyote "kuwa ni agano la milele." Kutoka 31:16. Sabato haijapoteza maana yake hata moja. Ingali bado ni ishara kati ya Mungu na watu wake, na itakuwa hivyo milele. Sasa na daima yatupasa kusimama kama watu tulio tofauti na wa pekee tusiofungwa na maongozi ya ulimwengu huu, tusioona aibu kujizuia kuungana kwa mikataba na wale wasiokuwa na hekima ya kutosha kuweza kuyatambua madai ya Mungu, ambayo yamewekwa wazi katika sheria yake [Amri Kumi]. Yatupasa kujionyesha kwamba sisi tunajitahidi kufanya kazi kwa kushirikiana vizuri na mbingu ili kuitengeneza njia ya Bwana. Yatupasa kutoa ushuhuda wetu kwa mataifa yote, kwa kila kabila na kila lugha, ya kwamba sisi ni watu tunaompenda na kumcha Mungu, watu tunaotunza Sabato ya siku ya saba, nasi yatupasa kuonyesha waziwazi kwamba tunayo imani kamili ya kwamba Bwana anakuja upesi juu ya mawingu ya mbinguni.... "Wala hapatakuwa na laana yo yote tena. Na kiti cha enzi cha Mungu na cha MwanaKondoo kitakuwamo ndani yake. Na watumwa wake watamtumikia; nao watamwona uso wake, na jina lake litakuwa katika vipaji vya nyuso zao." Ufunuo 22:3,4. Hao ni akina nani? ----- Ni watu wa Mungu walioitwa kwa jina lake ----- wale ambao duniani hapa wameshuhudia kwa utii wao. Hao ni nani? ----- Ni wale waliozishika amri [kumi] za Mungu na imani ya Yesu; wale ambao wamemkubali yule Msulibiwa kama Mwokozi wao. "Wala hapatakuwa na usiku tena; wala hawana haja ya taa wala ya nuru ya jua; kwa kuwa Bwana Mungu huwatia nuru, nao watatawala hata milele na milele. Fungu la 5. "Heri wale wazishikao amri zake, wawe na haki kuuendea huo mti wa uzima, na kuingia mjini kwa milango yake." Fungu la 14 [Tafsiri ya Toleo la King James]. ----- RH, Agosti 4, 1904. SAA YA KUAMKA IMEKWISHA KUWADIA Desemba 6 Naam, tukiujua wakati, kwamba saa ya kuamka katika usingizi imekwisha kuwadia; kwa maana sasa wokovu wetu u karibu nasi kuliko tulipoanza kuamini. Warumi 13:11. Pambano kuu linakaribia mwisho wake. Kila taarifa ya maafa baharini au katika nchi kavu ni ushuhuda wa ukweli kwamba mwisho wa mambo yote umekaribia. Vita na tetesi za vita huitangaza habari hiyo. Je, yupo Mkristo ambaye moyo wake haudundi kwa kasi anapotazamia kuyaona matukio makuu yanayoonekana mbele yetu? Bwana anakuja. Tunasikia hatua za Mungu anayekuja. ----- Ev 219. Ujuzi huo wa ukaribu wa marejeo yake Kristo usiachwe kupoteza nguvu zake, na sisi tukawa wazembe na wasio na usikivu, na kulala usingizi ----- katika hali ya kupoteza fahamu zote na kutojali ukweli wa mambo ulivyo. Usingizini tunakuwa katika ulimwengu wa kufikirika, wala hatuyatambui mambo yanayotokea kutuzunguka.... Wako wale walio na nuru ya ile kweli ambayo inawaka sana ikiwa inawaangazia pande zote kuwazunguka, na hata hivyo, wao hawaitambui. Wamelogwa na yule adui, na kuduwaa chini ya uwezo wake wa uchawi. Hawajiweki tayari kwa siku ile kuu ambayo inaharakisha kuujia ulimwengu huu. Wanaonekana hawana fahamu zo zote kabisa kwa kweli ile ya kidini. Hivi hakuna baadhi ya vijana walioamka? Wale wanaouona usiku kwamba unakuja, na mchana pia, wangefanya kazi kwa nguvu bila kuchoka kwa kuwaamsha wenzi wao wanaolala usingizi. Je, hawawezi kuhisi hatari yao [wenzi wao], kuwaombea, na kuwaonyesha kwa njia ya maisha na tabia yao kwamba wao wenyewe wanasadiki kwamba Kristo anakuja upesi?... Wakati unaokwisha upesi sana kati yetu na ule umilele ungetugusa sana mioyo yetu. Kila siku ipitayo hupunguza siku moja katika zile tulizobakiwa nazo ili kukamilisha kazi yetu ya kuifanya tabia yetu kuwa kamilifu.... Kadiri wanavyokuwapo wengi wanaolala usingizi, wengi wanaozichezea saa hizi za thamani kwa uzembe usiojali kitu, kama ilivyo, wakiwa ukingoni kabisa mwa ulimwengu ule wa milele, ndivyo wale waaminio wanavyopaswa kuwa na busara, kuamka, kuwa na bidii na kuwa waangalifu, na kukesha katika sala.... Je! wapendwa vijana, mmezitengeneza taa zenu na zinawaka? ----- YI, Agosti 25, 1886. UASI UNAKOANZIA Desemba 7 Basi, wapenzi mkitangulia kujua hayo, jilindeni nafsi zenu, msije mkachukuliwa na kosa la hao wahalifu mkaanguka na kuuacha uthibitifu wenu. 2 Petro 3:17. Katika siku hizi za mwisho, maovu yanapozidi kuongezeka, na upendo wa wengi unavyozidi kupoa, Mungu atakuwa na watu wake watakaolitukuza jina lake, na kusimama kama wakaripiaji wa dhambi. Wanatakiwa kuwa "watu wa pekee," ambao watakuwa waaminifu kwa sheria ya Mungu [Amri Kumi], wakati ulimwengu utakapojaribu kuzitangua amri zake; na wakati uweza wa Mungu unaoongoa utakapofanya kazi ndani ya watumishi wake, majeshi yale ya giza yatajipanga na kutoa upinzani mkali sana, uliodhamiriwa. Shetani atafanya kazi yake kwa "uwezo wote, na ishara na ajabu za uongo, na katika madanganyo yote ya udhalimu kwa hao wanaopotea." Atatumia kila mbinu ya udanganyifu kuishawishi mioyo ya wanadamu.... Kazi hiyo ya uasi huanzia katika maasi fulani ya kisirisiri ndani ya moyo wa mtu dhidi ya matakwa ya Sheria ya Mungu. Tamaa chafu, tamaa isiyo halali ya kupenda makuu, hutunzwa na kuendekezwa moyoni, na mashaka na giza humtenga mtu huyo mbali na Mungu. Tusipoyashinda maovu hayo, yatatushinda. Watu ambao kwa muda mrefu wamekuwa wakisonga mbele katika njia ile ya kweli, watajaribiwa kwa maonjo na majaribu. Wale wanaosikiliza mashauri ya Shetani, na kukengeuka kutoka katika unyofu wao, wataanza kwenda katika njia ile inayoshuka chini, na jaribu fulani lililoandaliwa [na Shetani] kwa werevu sana litawaharakisha kwenda kwenye njia ile ya uasi, mpaka kushuka kwao kutaonekana dhahiri na kunakuwa kwa kasi sana. Dhambi zile zilizokuwa za kuchukiza mno kwao hapo kwanza, [sasa] zinakuwa za kuvutia sana, nazo hukaribishwa na kutendwa na wale waliotupilia mbali kicho chao kwa Mungu pamoja na utiifu wao kwa sheria yake. Lakini furaha yao nyingi sana mwanzoni mwa uasi wao, itaishia katika majonzi, kujivunjia heshima [aibu], na maangamizi. Tunahitaji kuwa macho daima, kukesha na kuomba ili tusije tukaingia majaribuni. Kujiendekeza kuwa na kiburi cha kiroho, tamaa mbaya, mawazo machafu, na cho chote kile kinachotutenga mbali na ushirika wetu wa karibu sana, ulio mtakatifu, pamoja na Yesu, huziweka roho zetu katika hatari kubwa. Yatupasa kuwa na imani iliyo hai kwa Mungu.... Kama wazo hilo la uasi linawasikitisha ninyi, nanyi hamtaki kuwa maadui wa ile kweli,... basi, "lichukieni lililo ovu, mkiambatana na lililo jema." Warumi 12:9. ----- RH, Mei 8, 1888. HIVI MIMI NI MLAODIKIA? Desemba 8 Nayajua matendo yako, ya kuwa hu baridi wala hu moto; ingekuwa heri kama ungekuwa baridi au moto. Basi, kwa sababu una uvuguvugu, wala hu baridi wala moto, nitakutapika utoke katika kinywa changu. Ufunuo 3:15,16. Hali ya wengi wanaojidai kuwa ni watoto wa Mungu imewakilishwa vizuri kabisa na ujumbe huo kwa Kanisa la Laodikia [Kanisa la Waadventista Wasabato]. Mbele ya wale wanaomtumikia Mungu zimefunuliwa kweli ambazo thamani yake haikadiriki, ambazo, kama zikiwekwa katika maisha yetu kwa matendo, zitaonyesha tofauti kati ya wale wanaomtumikia Mungu na wale wasiomtumikia.... Biblia ni ghala ya utajiri wa Mungu usiopimika. Lakini wale wanaoijua ile kweli hawaijui kwa ukamilifu kama vile ambavyo wangeweza [kuijua]. Hawauweki upendo wa Kristo mioyoni mwao wala katika maisha yao. Mwanafunzi wa lile Neno anajikuta akiinama juu ya chemchemi ya maji hayo yaliyo hai. Kanisa linahitaji kunywa kwa kina, hali ya kiroho ya Neno hilo. Huduma yao kwa Mungu inahitaji kuwa tofauti sana na uzoefu wao wa kidini uliopoa, usiovutia, ulio baridi ambao unawafanya waumini wengi kuwa na tofauti ndogo tu na wale wasioamini. ----- 7BC 963, 964. Wakristo nusu-nusu ni wabaya mno kuliko makafiri; maana maneno yao yadanganyayo na msimamo wao usioelekea upande wo wote huwafanya wengi kupotea. Kafiri anaonyesha msimamo wake. Mkristo aliye na uvuguvugu anayadanganya makundi yote mawili. Yeye si mlimwengu mzuri, wala yeye si Mkristo mzuri. Shetani anamtumia kufanya kazi ile asiyoweza kufanya mtu mwingine ye yote. ----- 7BC 963. Kujipenda nafsi [uchoyo] huufukuzilia mbali upendo wa Kristo. Wale wanaoishi kwa kujifurahisha wenyewe wameorodheshwa chini ya kichwa cha Kanisa la Laodikia upande wa wale walio na uvuguvugu, si moto wala si baridi. Ari ile ya upendo wao wa kwanza imeishia katika ushupavu wa kujipenda nafsi [wenyewe]. Upendo wa Kristo moyoni huonyeshwa kwa matendo. Kama upendo wao kwa Kristo umepoa, basi, upendo kwa wale aliowafia Kristo utapungua sana. Yaweza kuonekana juhudi ya ajabu pamoja na matendo maalum ya dini [ibada], lakini hayo ni matokeo ya dini yao iliyovimbishwa kwa kiburi cha ubinafsi wao. Kristo anawasema kwamba wanamletea kichefuchefu kinywani mwake. ----- 7BC 962. Na tumshukuru Mungu kwamba wakati kundi hilo lina watu wengi sana, bado upo wakati kwao wa kutubu. ----- 7BC 963. HAKI YETU WENYEWE NI NGUO ILIYOTIWA UNAJISI. Desemba 9 Kwa kuwa wasema, Mimi ni tajiri, nimejitajirisha, wala sina haja ya kitu; nawe hujui ya kuwa wewe u mnyonge, na mwenye mashaka, na maskini, na kipofu, na uchi. Ufunuo 3:17. Ni kwa wazi ulioje imeonyeshwa picha ya wale wanaodhani kwamba wanayo kweli yote, wanaojivunia ujuzi wao wa Neno la Mungu, wakati uwezo wake utakasao hauonekani katika maisha yao. Moto wa upendo wa Mungu haumo mioyoni mwao. ----- 7BC 961. Wengi ni Walaodikia, wakiishi kwa kujidanganya wenyewe kiroho. Wanajivika mavazi ya haki yao wenyewe, wakiwaza ya kwamba wao ni matajiri, nao wamejitajirisha, wala hawana haja ya kitu cho chote, ambapo wanahitaji kujifunza kwa Yesu kila siku, upole wake na unyenyekevu wake wa moyo. ----- 7BC 962. Ni kitu gani kinachowafanya kuwa wanyonge na uchi watu hao wanaojiona kuwa ni matajiri na waliojitajirisha? Ni ukosefu wa [kutokuwa na] haki ile ya Kristo. Katika haki yao wenyewe wanaonekana kuwa wamevikwa nguo iliyotiwa unajisi, na, hata hivyo, wanapokuwa katika hali hiyo wao hujitapa kwamba wamevikwa haki ya Kristo.... Wanaweza kuwa wanapiga mekelele, wakisema, "Hekalu [Kanisa] la BWANA, Hekalu [Kanisa] la BWANA ndio sisi," wakati mioyo yao imejaa biashara ya magendo na dhuluma. Nyua za hekalu la moyo wao zinaweza kuwa ni maskani ya wivu, kiburi, tamaa mbaya, kuwafikiria wengine vibaya, uchungu, na ibada ya bure. Kristo kwa masikitiko makubwa anawaangalia wale wanaojiita kuwa ni watu wake ambao hujisikia kwamba wao ni matajiri na ya kuwa wamejitajirisha katika ujuzi wa ile kweli, na ambao, hata hivyo, ni maskini wa [hawana] kweli hiyo katika maisha na tabia yao. ----- RH, Agosti 7, 1894. Yesu asema, "Mimi, Mkombozi wako, nayajua matendo yako. Naijua nia inayokusukuma kusema kwa majivuno kuhusu hali yako ya kiroho, ukisema, 'Mimi ni tajiri, nimejitajirisha, wala sina haja ya kitu.' Wewe 'hujui ya kuwa u mnyonge, na mwenye mashaka, na maskini, na kipofu, na uchi.'"... Ni hali [ya kusikitisha] ilioje kuwa ndani yake! Wanasimama katika nuru yao wenyewe. Lakini licha ya ujinga wao wenyewe, hawaachwi na Bwana pasipo onyo la ziada na shauri lake. ----- 7BC 963. VAZI LISILO NA WAA LA HAKI YA KRISTO Desemba 10 Nakupa shauri, ununue kwangu dhahabu iliyosafishwa kwa moto, upate kuwa tajiri, na mavazi meupe upate kuvaa, aibu ya uchi wako isionekane, na dawa ya macho ya kujipaka macho yako upate kuona. Ufunuo 3:18. Mkombozi wetu mkuu anajisema mwenyewe ya kuwa yeye ni mfanya biashara wa mbinguni, mwenye utajiri mwingi, anayetembea nyumba kwa nyumba, akizionyesha bidhaa zake za thamani isiyopimika. ----- 7BC 965. Ni lazima tuwafukuze wanunuzi na wauzaji kutoka katika hekalu la moyo wetu, ili Yesu apate kukaa mahali pake ndani yetu. Hivi sasa anasimama mlangoni pa moyo kama mfanya biashara atokaye mbinguni; Anasema hivi,... "Nifungulie; ununue kwangu dhahabu iliyosafishwa kwa moto." Nunua kwake imani na upendo, sifa za thamani na nzuri za tabia yake Mkombozi wetu.... Anatuita tununue kwake mavazi meupe, ambayo ni haki yake mwenyewe iliyo tukufu; na dawa ya macho, ili tupate kubainisha mambo ya kiroho. Je! hatutaufungua mlango wa moyo wetu kwa mgeni huyo aliyetoka mbinguni? -- --- 7BC 964. Hatuwezi kujipatia vazi la haki sisi wenyewe, maana nabii anasema hivi, "Kwa maana sisi sote tumekuwa kama mtu aliye mchafu, na matendo yetu yote ya haki yamekuwa kama nguo iliyotiwa unajisi." Isaya 64:6. Ndani yetu hakuna kitu cho chote ambacho kwacho tunaweza kuivika roho yetu ili uchi wake usionekane. Yatupasa kulipokea vazi lile la haki lililofumwa mbinguni, yaani, vazi lile jeupe la haki ya Kristo. ----- RH, Julai 19, 1892. Jicho ni dhamiri yetu kali, yaani, nuru ile ya ndani ya moyo. Afya ya kiroho ya moyo wote na mwili mzima hutegemea linavyoyaona vizuri mambo. Dawa ya macho, yaani, Neno la Mungu, huifanya dhamiri kuuma [kuchomwa] chini ya matumizi yake, kwa vile inaihakikisha dhambi. Lakini kuuma huko ni kwa lazima ili uponyaji ufuatie, na jicho liwe safi kwa utukufu wa Mungu.... Asema Kristo, kwa kuachilia utoshelevu wako, na kuyaacha mambo yako yote, haidhuru uyapende kiasi gani, unaweza kununua dhahabu, mavazi, na dawa ya macho upate kuona. ----- 7BC 965. Mwokozi wetu anakuja na johari zake za thamani kubwa mno za ile kweli ambazo ni tofauti kabisa na zile zote za bandia, yaani, zile zote za uongo. Anakuja nazo kwa kila nyumba, kwa kila mlango; Anabisha, akiwa amezileta hazina zake za thamani mno, akitubembeleza, na kusema, "Ununue kwangu." ----- 7BC 964. NI UJUMBE UNAOTIA MOYO SANA Desemba 11 Wote niwapendao mimi nawakemea, na kuwarudi; basi uwe na bidii, ukatubu. Ufunuo 3:19. Shauri la Shahidi huyo wa Kweli halionyeshi kwamba wale walio na uvuguvugu wako katika hali mbaya isiyokuwa na matumaini. Bado ipo nafasi kwao ya kuisahihisha hali yao, na ujumbe huo wa Laodikia unatia moyo sana.... Usafi wa moyo, usafi wa nia, bado unaweza kuwa tabia ya wale walio nusu-nusu, ambao wanajitahidi kumtumikia Mungu na mali [ya ulimwengu huu]. Bado wanaweza kuyafua mavazi ya tabia zao na kuyafanya meupe katika damu ya Mwana-Kondoo. ----- 7BC 966. Dhahabu ile ya imani na upendo, mavazi yale meupe ya tabia ile isiyokuwa na waa, na dawa ile ya macho, au uwezo ule wa kupambanua kati ya mema na mabaya ----- vyote hivyo hatuna budi kuvipata kabla hatujaweza kuanza kuwa na tumaini la kuingia katika ufalme wa Mungu. Lakini hazina hizo za thamani hazitadondoka juu yetu pasipo sisi kuwa na juhudi kiasi fulani kwa upande wetu. Yatupasa kununua ----- lazima sisi "[tu]we na bidii, [t]ukatubu" kwa sababu ya hali yetu hiyo ya uvuguvugu. Yatupasa kuamka na kuyaona makosa yetu, kuzichunguza dhambi zetu, na kuziondolea mbali nasi.... Ni ustahili wake Kristo ambao hauna budi kutuokoa sisi, yaani, damu yake ambayo ni lazima itutakase sisi. Walakini tunazo juhudi za kufanya. Yatupasa kufanya tuwezavyo ili tuwe na bidii na tutubu, kisha tuamini kwamba Mungu anatukubali.... Mbingu yote inapendezwa kuona wokovu wetu; basi, sisi, je! tuwe watu wasiojali? Je, tuwe wazembe, kana kwamba ni jambo dogo iwapo tutaokolewa au tutapotea? Je! tuidharau ile kafara iliyotolewa kwa ajili yetu?... Katika kipindi kile cha hatari kilicho mbele yetu wale wanaokiri kumfuata Kristo watajaribiwa. Hakuna hata mmoja atakayeweza kusimama isipokuwa wale waliokwisha kupata uzoefu wenye kina, ulio hai, katika mambo ya Mungu. Hapo ndipo kazi ya wote itakapopimwa; kama ni dhahabu, au fedha, au mawe ya thamani, hao watalindwa kwa salama, kama vile katika mahali pa siri pa sitara yake Bwana.... Ni wale tu walio tayari kuviacha vyote kwa ajili ya uzima ule wa milele watakaoupata; lakini itafaa kuteseka kwa ajili yake, itafaa kuisulibisha nafsi na kuachana na kila kinyago. Utukufu upitao wote, uzidio kuwa mwingi sana utaipita kila hazina iliyomo humu duniani na kukifunika kila kishawishi [kivutio] cha duniani humu. ----- RH, Sept. 4, 1883. JE! UTAUFUNGUA MLANGO? Desemba 12 Tazama, nasimama mlangoni, nabisha; mtu akiisikia sauti yangu, na kuufungua mlango nitaingia kwake, nami nitakula pamoja naye, na yeye pamoja nami. Ufunuo 3:20. Yesu asema, "Tazama, nasimama mlangoni, nabisha." Je! tutamfungulia? Yeye asingependa kutuona sisi tukisimama wakati huu, katikati ya hatari kubwa za siku za mwisho, kwa nguvu zetu wenyewe za kibinadamu.... Ni haki yetu kutembea katika mwanga wa jua wa kuwapo kwake, na kufuma katika tabia zetu tunazozijenga kamba zile za dhahabu za uchangamfu, shukrani, uvumilivu, na upendo. Kwa njia hiyo tunaweza kuonyesha uwezo wa neema ya Mungu, na kuakisi [kuiangaza] nuru ile itokayo mbinguni katikati ya wasiwasi na maudhi yanayotujia siku kwa siku.... Basi, mbona tunatembea kwa kujikwaa katika njia yetu bila kuwa na nuru hiyo? ----- RH, Novemba 24, 1884. Kila onyo, kila karipio, na kila ombi katika Neno la Mungu, au kupitia kwa wajumbe wake aliowatuma, ni kubisha [kugonga] mlangoni pa moyo wako; ni sauti yake Yesu, ikiomba kuingia ndani yako. Kila bisho [kugonga] unalolidharau, huifanya azma yako ya kutaka kufungua kufifia zaidi na zaidi. Kama sauti hiyo ya Yesu haisikilizwi mara moja, basi, itachanganyika pamoja na sauti zingine nyingi katika moyo wako, yaani, masumbufu ya dunia na shughuli zake, mambo hayo yatachota mawazo yako yote, na hisia hiyo [ya kusikia sauti ya Yesu] itatoweka [moyoni mwako]. Moyo wako utaguswa kidogo tu, na kuishia katika hali ile ya hatari ya kupoteza uwezo wake wa kutambua hata usiweze kujua ufupi wa wakati ulio nao, na umilele ulioko ng'ambo ile ya pili. ----- 7BC 966,967. Wengi wanazo takataka nyingi sana walizozilundika mlangoni pa moyo wao hata hawawezi kumruhusu Yesu kuingia ndani. Wengine wana matatizo kati yao na ndugu zao ambayo hayana budi kuondolewa [kusuluhishwa], wengine wana hasira mbaya, kiburi, uchoyo; kwa wengine ni kule kuipenda dunia kunakoweka kizuizi mlangoni pao. Vyote hivyo ni lazima viondolewe, kabla hawajaweza kufungua mlango na kumkaribisha ndani Mwokozi wao. Ni ya thamani jinsi gani ahadi hii, "nitaingia kwake, nami nitakula pamoja naye, na yeye pamoja nami." Lo! ni pendo lililoje, pendo la ajabu la Mungu kwetu sisi! Baada ya sisi kuwa na uvuguvugu wote huu na dhambi tulizo nazo, yeye anatuambia, Nirudieni, nami itawarudieni, nami nitawaponya na kurudi nyuma kwenu kote. ----- RH, Sept. 4, 1883. Kazi yetu sisi ni kuufungua mlango wa moyo wetu na kumkaribisha Yesu ndani. Anabisha [Anagonga] akitaka kuingia ndani yako.... Je! utaufungua mlango? Yesu anasimama nje ya mlango wa moyo wako. Mkaribishe ndani, Mgeni wako huyo wa mbinguni. ----- Letter 110, 1893. USHINDI NI WA HAKIKA Desemba 13 Yeye ashindaye, nitampa kuketi pamoja nami katika kiti changu cha enzi, kama mimi nilivyoshinda nikaketi pamoja na Baba yangu katika kiti chake cha enzi. Ufunuo 3:21. Shahidi huyo wa kweli anawatia moyo wale wote wanaojaribu kutembea katika njia ile ya moyo wa unyenyekevu wenye utii, kwa njia ya imani katika jina lake. Anatangaza hivi, "Yeye ashindaye, nitampa kuketi pamoja nami katika kiti changu cha enzi, kama mimi nilivyoshinda nikaketi pamoja na Baba yangu katika kiti chake cha enzi." Hayo ni maneno ya yule aliye Badala yetu na Mdhamini wetu. Yeye ambaye ni Kichwa cha Mungu cha Kanisa, mwenye nguvu kuliko washindi wote, angependa kuwaonyesha wafuasi wake maisha yake, taabu zake, kujikana nafsi kwake, mapambano yake, na mateso yake, kwa njia ya kudharauliwa, kwa njia ya kukataliwa, kudhihakiwa, kubezwa, kutukanwa, kuchekwa, kusemewa uongo, akiipanda njia ile ya kwenda Kalvari kwenye tukio lile la kusulibiwa kwake, ili wapate kutiwa moyo na kusonga mbele kuifikia tunu na thawabu ile ya mshindi. Ushindi ni wa hakika kwa njia ya imani na utii. Hebu na tuyatumie maneno yake Kristo katika mambo yetu wenyewe. Je, sisi ni maskini, na vipofu, na wanyonge, na wenye mashaka? Basi, na tutafute dhahabu na mavazi yale meupe anayotupa. Kazi hii ya kushinda haijawekewa mipaka kwa kizazi kile cha wafia dini [Ufunuo 6:9-11]. Pambano ni letu katika siku hizi za majaribu yaliyoandaliwa kwa werevu sana ili kutufanya tuipende dunia, tujitafutie usalama wetu wenyewe, tujiendekeze kwa kuwa na kiburi, uchoyo, mafundisho ya uongo, na maisha ya uasherati [ufisadi]. ----- 7BC 966. Tunaweza kushinda. Naam; kwa ukamilifu, yaani, kabisa. Yesu alikufa kwa madhumuni ya kutupatia njia ya kuokoka, ili tupate kushinda kila kosa [dhambi], kupinga kila jaribu, na hatimaye kuketi pamoja naye katika kiti chake cha enzi. ----- RH, Sept. 4, 1883. Hatuna ujumbe wo wote wa kukatisha tamaa kwa ajili ya kanisa hili. Ingawa makaripio na maonyo na masahihisho yamekwisha kutolewa, hata hivyo, kanisa hili [la Waadventista Wasabato] limesimama kama chombo cha Mungu cha kusambaza nuru yake. Watu wa Mungu wazishikao amri zake [kumi] wamekwisha toa onyo kwa ulimwengu huu [Ufunuo 14:6-12].... Kanisa hili la Mungu ni shahidi aliye hai, ushuhuda wake unaendelea daima ili kuwashawishi wanadamu endapo watakubali [kuupokea ujumbe huo], kuwahukumu endapo wataupinga na kuukataa. ----- 7BC 967. Kanisa hili ni lazima liangaze na litaangaza "kama mwezi, safi kama jua, [l]akutisha kama wenye bendera [jeshi la vita]." Wimbo Ulio Bora 6:10. ----- 7BC 966. HAWATAONDOSHWA KATIKA ULIMWENGU ULIOTIKISWA Desemba 14 Nimemweka BWANA mbele yangu daima, Kwa kuwa yuko kuumeni kwangu, sitaondoshwa. Zaburi 16:8. Tunaishi katika kizazi cha hatari, wakati ambapo uovu ni jambo la kawaida. Hata wale wanaokiri ya kuwa wao ni Wakristo hawaziamini Biblia zao. Ukweli wa Neno la Mungu uko wazi mno na umeelekezwa kwao.... Mawazo ya Mpinga Kristo, desturi, na mazoea huendelea kuwako, na hata mambo hayo hufikiriwa kuwa ni ya Kikristo; lakini kile kilicho cha thamani mno, kile ambacho Mungu anakitukuza kuliko vyote, kinaangaliwa kwa dharau. Anayemcha Mungu anaweza kuuliza, Mwisho wa mambo haya utakuwaje? Upendo kwa Kristo na upendo wetu sisi kwa sisi unakufa haraka kutoka katika mioyo ya wanadamu.... Maovu yameenea kila upande; kwa maana Shetani ameshuka chini akiwa na ghadhabu nyingi, akijua ya kuwa ana wakati mchache. Ni mtenda kazi mstahimilivu, mwenye bidii, asiyechoka, na kama ulikuwapo wakati ambapo wanadamu walihitaji kuwako kwake Kristo mkono wao wa kuume, ni SASA.... Tunamhitaji daima Kapteni wa Wokovu Wetu awe kando yetu. Ipo, na itaendelea kuwapo, misukosuko kila upande kutuzunguka; maana falme za ulimwengu huu hazitakuwa katika hali ya utulivu. Kamwe hapajapata kuwa na wakati ambapo majaribu ya kumkana Kristo kiroho na kitabia, yalikuwa na nguvu zaidi [kama sasa], na majaribu hayo yatazidi kuongezeka kwa nguvu kadiri tunavyokaribia mwisho. Majaribu yenye nguvu na yanayowashinda wanadamu yatawajia. Mafundisho ya uongo na hadithi za uongo zitafundishwa kama ndiyo kweli yenyewe ya Biblia, ili watu wapate kuyapokea; na kama ingewezekana, basi, wangeweza kuwadanganya, yamkini hata walio wateule. Lakini, je! huu ndio wakati kwa upendo wetu kupoa, wakati maovu yanapozidi kuongezeka? Je! huu ndio wakati wa kukaa raha mustarehe? Je! huu ndio wakati wa kujitenga mbali na Mungu, Mshauri wetu? Mwisho wa mambo yote umekaribia. Siku ya Mungu inaharakisha sana. Ulimwengu umejaa uhalifu na utungu na huzuni. Kuna maafa katika nchi kavu na baharini. Dhoruba na tufani hufanya isiwe salama kwetu kujitenga na Mungu hata kwa dakika moja tu. Ni wale tu wanaoishi kwa imani katika maisha haya ya kipindi hiki cha majaribio ambao wataweza kusimama katika siku ile ya kujaribiwa, wakati mambo yote yanayoweza kutetemeshwa [kutikiswa] yatakapotetemeshwa [yatakapotikiswa], bali wao watakaa salama wala hawataondoshwa. ----- YI, Julai 19, 1894. HATARI KUBWA MBELE YETU Desemba 15 Nanyi mtachukuliwa mbele ya maliwali na wafalme kwa ajili yangu, kuwa ushuhuda kwao na kwa mataifa. Mathayo 10:18. Wakati hauko mbali watu wa Mungu watakapoitwa kutoa ushahidi wao mbele ya watawala wa dunia hii. Hakuna mtu hata mmoja katika watu ishirini anayetambua ni hatua za haraka jinsi gani tunazotembea kwenda kwenye hatari kubwa sana katika historia yetu.... Hakuna muda wa kufanya mambo ya ubatili, mambo madogodogo, na kushughulika na mawazo yasiyo na maana. ----- RH, Aprili 26, 1892. Wafalme, maliwali, na wakuu watawasikiliza ninyi kupitia kwa watu wale walio na uadui dhidi yenu, na imani yenu pamoja na tabia yenu, mambo ambayo watayaeleza vibaya mbele yao. Lakini wale wanaoshtakiwa kwa uongo watapewa nafasi ya kuonekana mbele ya washtaki wao ili wapate kujitetea wenyewe. Watakuwa na nafasi nzuri ya kuileta nuru mbele ya wale wanaoitwa wakuu wa dunia hii, na kama ninyi mmejifunza Biblia, kama ninyi mko tayari kutoa jibu kwa upole na hofu kwa kila mtu awaulizaye juu ya tumaini lile lililo ndani yenu, basi, adui zenu hawataweza kuipinga hekima yenu. Hivi sasa mnayo nafasi ya kuufikia uwezo wa juu sana kiakili kwa njia ya kujifunza Neno la Mungu. Ila kama ninyi ni wavivu, na mnashindwa kuchimba chini katika machimbo hayo ya hiyo kweli, basi, hamtaweza kuwa tayari kwa hatari kubwa ambayo itatujia karibuni sana. Laiti kama mngetambua ya kwamba kila dakika ni ya thamani sana. Iwapo mnaishi kwa kila neno litokalo katika kinywa cha Mungu, basi, hamtakutwa katika hali ya kutokuwa tayari. ----- RH, Aprili 26, 1892. Hamjui ni mahali gani mtakakotakiwa kutoa ushuhuda wenu kwa ajili ya ile kweli. Wengi watatakiwa kusimama mbele ya wafalme [Ma-Rais] na mbele ya wasomi wa ulimwengu huu, kujitetea kwa ajili ya imani yao. Wale walio na ujuzi wa juu juu tu wa ile kweli hawataweza kuyafafanua Maandiko kwa wazi, na kutoa sababu za wazi kuunga mkono imani yao. Watakuwa wamechanganyikiwa, nao hawatakuwa watenda kazi ambao hawawezi kutahayari. Hebu na asiwepo ye yote anayedhani kwamba hana haja ya kujifunza [Neno la Mungu], ati kwa sababu hawezi kutakiwa kuhubiri mimbarani. Hamjui kile ambacho Mungu anaweza kutaka kutoka kwenu. ----- FE 217. JE, UKO TAYARI KUPIMWA IMANI YAKO? Desemba 16 Lakini hapo watakapowapeleka, msifikiri-fikiri jinsi mtakavyosema; maana mtapewa saa ile mtakayosema. Mathayo 10:19. Watumishi wake Kristo wasiandae hotuba yo yote maalum ya kutoa watakapohukumiwa kwa ajili ya imani yao. Maandalizi yao yanatakiwa kufanywa siku kwa siku, kwa kuhifadhi mioyoni mwao kweli zile za thamani za Neno la Mungu, kwa kujilisha mafundisho ya Kristo, na kwa njia ya maombi yao kuiimarisha imani yao; ndipo watakapopelekwa hukumuni, Roho Mtakatifu atawakumbusha kweli zile zile ambazo zitaiokoa mioyo ya wale watakaokuja kusikiliza. Mungu atayapitisha ghafula katika kumbukumbu zao maarifa yale yaliyopatikana kwa kuyachunguza Maandiko kwa bidii wakati ule ule yatakapohitajika. ----- CSW 40,41. Wewe unatakiwa kujiandaa sasa kwa ajili ya wakati ule utakapohukumiwa. Hivi sasa yakupasa kujua iwapo miguu yako imesimama juu ya ule Mwamba wa Milele. Unatakiwa kuwa na uzoefu wako peke yako, wala usiwategemee wengine kwa nuru yako. Hapo utakapoletwa kupimwa imani yako, utajuaje wewe kama hutakuwa peke yako, bila kuwa na rafiki wa kidunia kando yako? Je, utaweza kuikumbuka ahadi hii, "Na tazama, mimi nipo pamoja na [we] siku zote, hata ukamilifu wa dahari"? Kila upande kukuzunguka watakuwapo wale wasioonekana [malaika za Shetani] wenye nia ya kukuangamiza. Shetani na mawakala wake watatafuta kila njia kukufanya wewe uyumbe katika msimamo wako kwa Mungu na kweli yake. Lakini kama wewe una jicho safi kwa utukufu wake, huna haja ya kufikiri-fikiri jinsi utakavyotoa ushuhuda wako kwa ajili ya kweli yake. ----- RH, Aprili 26, 1892. Enyi vijana, wanaume kwa wanawake, hivi mnaendelea kukua ili kuweza kukifikia cheo cha kimo cha wanaume na wanawake cha utimilifu wa Kristo ili hatari ile kubwa itakapokuja msitengwe mbali na yule aliye Chimbuko la nguvu zenu? Iwapo tutasimama wakati ule wa kupimwa imani yetu, basi, ni lazima sasa, wakati huu wa amani, tuwe tunajipatia uzoefu hai katika mambo ya Mungu. Hivi sasa tunapaswa kujifunza na kuelewa maongozi yenye kina ya Roho wa Mungu ndani yetu. Kristo kwetu anapaswa kuwa yote na ndani ya yote, Alfa na Omega, Wa Kwanza na Wa Mwisho, Mwanzo na Mwisho. ------ RH, Mei 3, 1892. TOKA KINYWANI MWA SIMBA Desemba 17 Msiwaogope wauuao mwili, wasiweze kuiua na roho; afadhali mwogopeni yule awezaye kuangamiza mwili na roho pia katika jehanum. Mathayo 10:28. Danieli ni kielelezo kwa waumini kuonyesha maana ya kumkiri Kristo. Alikuwa na cheo chenye madaraka makubwa cha Waziri Mkuu katika Ufalme ule wa Babeli, na palikuwa na wale waliomwonea wivu Danieli miongoni mwa wakuu wa jumba lile la Mfalme, nao walitaka kupata kitu fulani dhidi yake ili wapate kumshtaki kwa mfalme. Lakini yeye alikuwa mtawala mwaminifu, nao hawakuweza kuliona kosa lo lote katika tabia au maisha yake.... Basi, wakapatana kumwomba mfalme kutoa amri ili asiwepo mtu ye yote atakayeomba dua kwa Mungu wala kwa mwanadamu awaye yote kwa muda wa siku thelathini isipokuwa kwa mfalme, na ya kwamba endapo mtu ye yote hakuitii amri hiyo, basi, ajipaswa kutupwa katika tundu lile la simba. Lakini, je! Danieli aliacha kuomba kwa sababu amri hiyo ilikuwa inaanza kutumika? La, huo ulikuwa ndio wakati hasa alipohitaji kuomba.... Danieli hakujaribu kuficha utiifu wake kwa Mungu. Hakuomba moyoni mwake, bali kwa sauti, kwa nguvu, dirisha lake likiwa limefunguliwa kuelekea Yerusalemu. Hapo ndipo maadui zake walipopeleka malalamiko yao kwa mfalme, na Danieli akatupwa katika tundu la simba. Lakini Mwana wa Mungu [Kristo] alikuwa mle.... Mfalme alipokuja asubuhi, na kuita, "Ee Danieli, mtumishi wa Mungu aliye hai, je! Mungu wako unayemtumikia daima, aweza kukuponya na simba hawa? Ndipo Danieli akamwambia mfalme, Ee mfalme, uishi milele. Mungu wangu amemtuma malaika wake, naye ameyafumba makanwa ya simba, nao hawakunidhuru." Danieli 6:20-22. Tunaweza kujua ya kwamba kama maisha yetu yamefichwa pamoja na Kristo katika Mungu, basi, hapo tutakapofikishwa hukumuni kwa sababu ya imani yetu, Yesu atakuwa pamoja nasi. Tutakapopelekwa mbele ya watawala na wakuu wa nchi kujitetea kwa ajili ya imani yetu, Roho wa Bwana atatueleza katika fahamu zetu, nasi tutaweza kutoa ushuhuda kwa utukufu wa Mungu. Na iwapo tutalazimika kuteswa kwa ajili yake Kristo, basi, tutaweza kwenda gerezani tukimtumainia yeye kama vile mtoto mdogo anavyowatumainia wazazi wake. Sasa ndio wakati wa kujenga imani yetu kwa Mungu. -- --- RH, Mei, 1892. KATIKATI YA MOTO Desemba 18 Basi, kila mtu atakayenikiri mbele ya watu, nami nitamkiri mbele za Baba yangu aliye mbinguni. Mathayo 10:32. Kumkiri Kristo maana yake ni zaidi ya kutoa ushuhuda katika mkutano wa maombi. ----- RH, Mei 3, 1892. Tuna ushuhuda tofauti wa kutoa kuliko ule tuliokwisha kutoa; nasi tutalazimika kuutoa chini ya mazingira yanayotofautiana. Waebrania wale watatu walishurutishwa kumkiri Kristo mbele ya tanuru linalowaka moto mkali. Walikuwa wameamriwa na mfalme kuanguka chini na kuisujudu sanamu ile ya dhahabu aliyokuwa ameisimamisha, na kutishia kwamba kama wasingetaka kufanya hivyo, basi, wangetupwa wakiwa wangali hai katika tanuru lile la moto, lakini wao wakajibu, "Hatuna haja ya kujibu katika neno hili. Kama ni hivyo, Mungu wetu tunayemtumikia aweza kutuokoa na tanuru ile iwakayo moto; naye atatuokoa na mkono wako, Ee Mfalme. Basi kama si hivyo, ujue, Ee Mfalme, ya kuwa sisi hatukubali kuitumikia miungu yako, wala kuisujudia hiyo sanamu ya dhahabu uliyoisimamisha." Danieli 3:16-18. Iliwagharimu kitu fulani kumkiri Kristo, kwa maana maisha yao yalikuwa hatarini. Ndipo mfalme akaamuru tanuru litiwe moto mara saba kuliko desturi yake ya kutiwa moto, na watoto wale wa Mungu, waaminifu, walitupwa katika tanuru lile. "Ndipo Nebukadreza akastaajabu, akainuka kwa haraka; akanena, akawaambia mawaziri wake, Je! hatukutupa watu watatu, hali wamefungwa, katikati ya moto ? Wakajibu wakamwambia mfalme, Kweli, Ee mfalme. Akajibu, akasema, Tazama, mimi naona watu wanne, nao wamefunguliwa, wanatembea katikati ya moto hali hawana dhara; na sura yake yule wa nne ni mfano wa wana wa miungu." Fungu la 24,25.... Ndipo Nebukadreza akawaita watumishi wa Mungu watoke nje, nao hawakuwa na harufu ya moto hata kidogo juu yao. Endapo utaitwa kupita katika tanuru la moto kwa ajili ya Kristo, basi, Yesu atakuwa kando yako. "Upitapo katika maji mengi nitakuwa pamoja nawe; na katika mito, haitakugharikisha; uendapo katika moto, hutateketea; wala mwali wa moto hautakuunguza." Isaya 43:2. ----- RH, Mei 3, 1892. PAMBANO DHIDI YA UPEPO NA MAJI KUPWA NA KUJAA Desemba 19 Heri ninyi watakapowashutumu na kuwaudhi [kuwatesa] na kuwanenea kila neno baya kwa uongo, kwa ajili yangu. Furahini, na kushangilia; kwa kuwa thawabu yenu ni kubwa mbinguni; kwa maana ndivyo walivyowaudhi [walivyowatesa] manabii waliokuwa kabla yenu. Mathayo 5:11,12. Mkombozi wetu mwenye rehema aliangalia upande wa chini wa mto huu wa wakati na kuziona hatari kubwa ambazo katika siku hizi za mwisho zitawazunguka wateule wake.... Endapo washiriki wa kanisa wanafanya kazi yao kwa uaminifu katika kuijenga kazi ya ile kweli, basi, hawatakwepa udaku, uongo, na masengenyo. "Naam, na wote wapendao kuishi maisha ya utauwa katika Kristo wataudhiwa [watateswa]." 2 Timotheo 3:12. Njia yao thabiti, isiyoyumba ni karipio la kudumu juu ya kutokuamini, kiburi, na uchoyo wa yule mnafiki anayejidai [kuwa Mkristo]. Maombi na maonyo yao huyavuruga malengo yake ya kidunia, naye atajitahidi kuwashutumu wafuasi waaminifu wa Yesu. Atayachanganya mawazo yao, atazipotosha habari zao, na kueleza vibaya mambo yao yaliyo ya kweli, kwa roho ile ile iliyowasukuma Mafarisayo katika upinzani wao dhidi ya Kristo. Yesu hawasahau watu wake walio na mambo mengi sana ya kuwakatisha tamaa ambayo wanatakiwa kupambana nayo. Inahitaji juhudi kidogo tu kuogelea kule unakoelekea mkondo wa maji unaopendwa na watu wengi, lakini wale ambao wangependa kufika kwenye pwani zile za milele hawana budi kupambana na upepo na maji ya kupwa na kujaa. Kuna mfumo fulani wa Ukristo ----- mfumo wa bandia ----- ambao hauna nguvu ya kumbadilisha mtu [tabia yake]. Walio nao huo wanafurahia kupinga na kushutumu imani ya wengine. Dini yao haionekani sokoni, wala katika familia, wala katika karakana. Uzoefu wao wa kidini unakwenda katika njia ile mbaya ya ulimwengu huu. Mfuasi mwaminifu wa Kristo asingevunjika moyo kupokea shutuma kutoka kwa kundi hilo. Mtume yule aliyependwa sana, alisema, "Ndugu zangu, msistaajabu, ulimwengu ukiwachukia." l Yohana 3:13. Naye Mwokozi wetu anawakumbusha wanafunzi wake, akisema, "Iwapo ulimwengu ukiwachukia, mwajua ya kuwa umenichukia mimi kabla ya kuwachukia ninyi." Yohana 15:18. Wale walio waaminifu kwa Mungu hawatapata madhara yo yote kutokana na shutuma hizo au upinzani huo. La, zaidi sana, wema wao utakuzwa ambao hautaweza kusitawi katika mwanga wa jua wa mafanikio. Imani, uvumilivu, upole, na upendo vitachipuka na kutoa maua katikati ya mawingu na giza. ---- - ST, Jan. 12, 1882. ADUI WA HATARI MNO Desemba 20 Basi, Roho anena waziwazi ya kwamba nyakati za mwisho wengine watajitenga na imani, wakisikiliza roho zidanganyazo, na mafundisho ya mashetani. 1 Timotheo 4:1. Adui wa roho zetu anajaribu daima kuipotosha mioyo yetu kwa kutuletea mambo madogo yasiyo na maana. Tusidanganyike. Waache maadui wako walitumie jina lako na langu kama wapendavyo. Hebu wayapotoshe, yaani, wayaeleze vibaya maneno na matendo yetu. Hatuwezi kumudu kuiacha mioyo yetu kupotoshwa [kugeuziwa kando] kutoka kwa Yesu na kutoka kwenye maandalizi yetu ya moyo ambayo ni lazima tuwe nayo ili kuweza kukutana naye kwa amani.... Kwa niaba yake Kristo, nawasihi sana mpate kuomba msivyopata kuomba siku za nyuma, kujitahidi kutafuta kwa bidii ili mpate kuwa na imani na upendo, mambo hayo ambayo huonekana ya kwamba yameondolewa kabisa duniani. Yawapasa kuishi kila siku kana kwamba mko mbele zake Mungu.... Hebu waalimu wale wa uongo wasiwachanganye mawazo yenu na kuiyumbisha imani yenu kwa kuwashutumu wale ambao Mungu amewatuma kwenu wakiwa na ujumbe wa maonyo na mafundisho kwenu. Kumbukeni ya kwamba si wanadamu tu ambao mnapaswa kupambana nao, bali ni "juu ya falme na mamlaka, juu ya wakuu wa giza hili, juu ya majeshi ya pepo wabaya katika ulimwengu wa roho." Sasa ndio wakati hasa ambapo Shetani anatenda kazi yake kwa madanganyo yote ya udhalimu. Kwa kweli, ni wengi wanaopiga vita vyake [Shetani] wakati wao wanajidai kutumika chini ya bendera ya Kristo. Wasaliti hao waliomo kambini [kanisani] huenda tusiweze kuwashuku, lakini wanafanya kazi yao kwa kuleta mashaka, machafuko, na ugomvi. Hao ndio adui wa hatari mno. Wakati wanajiingiza wenyewe kutaka tuwapendelee, na kutufanya sisi tuwaamini na kuwahurumia, wanajishughulisha kwa kutoa mashauri yao yaletayo mashaka na kuanzisha tuhuma. Wanafanya kwa njia ile ile kama Shetani alivyofanya kule mbinguni alipowadanganya malaika kwa maelezo yake ya hila, akiweka giza badala ya nuru, tena akiufanya uvumilivu na rehema zake Mungu kuonekana kama ni ukatili na ukali. Kama alivyofanya hapo mwanzo, ndivyo anavyofanya wakati huu wa mwisho, ila tu anajificha kabisa ili asionekane [kama ndiye].... Haitoshi kwetu kuwa na nadharia tu ya ile kweli; kanuni zake ni lazima zikae ndani ya moyo wetu, na kuonyeshwa katika maisha yetu, la sivyo, tutakuwa mateka wa madanganyo hayo yaliyoandaliwa kwa siku hizi za mwisho. ----- RH, Agosti 28, 1883. MSALABA KABLA YA TAJI Desemba 21 Naam, na wote wapendao kuishi maisha ya utauwa katika Kristo Yesu wataudhiwa [watateswa]. 2 Timotheo 3:12. Tunaweza kuimarisha imani yetu na kuamsha upendo wetu kwa kwenda mara kwa mara chini ya msalaba, na tukiwa pale yatupasa kutafakari kujidhili kwake. Mtazame, Mfalme wa mbinguni akiteswa kama mwenye dhambi! Usafi usiokuwa na waa, haki isiyo na doa, havikuweza kumkinga kutokana na uongo na shutuma za watu. Kwa unyenyekevu alivumilia ukinzani wa wenye dhambi dhidi yake yeye mwenyewe, na kutoa uhai wake, ili sisi tupate kusamehewa na kuishi milele. Je, sisi tuko tayari kuzifuata nyayo zake? Sababu ya pekee kwa nini hatupati mateso makubwa zaidi ni kwamba katika maisha yetu hatuonyeshi kwa mfano maisha yale ya Kristo. Enyi ndugu na dada zangu, iwapo mnaenenda kama alivyoenenda, nawahakikishia ya kwamba mtajua jinsi kuteswa na kushutumiwa kwa ajili yake kulivyo hasa. Tukitumainia kuivaa ile taji, basi, yatupasa kubeba msalaba wetu. Maonjo yetu makubwa mno yatatoka kwa wale wanaojidai kuwa ni wacha Mungu. Ilikuwa hivyo kwa Mkombozi wa ulimwengu huu, itakuwa hivyo kwa wafuasi wake.... Wale wanaojitaidi sana kuipata taji ile ya uzima wa milele wasishangae wala wasivunjike moyo kwa vile wanavyokutana na vipingamizi na kukabiliwa na maonjo kwa kila hatua wanayokwenda kuelekea Kanaani ile ya mbinguni.... Mwokozi anajua kilicho bora sana kwetu. Imani hukua kwa kupambana na mashaka na shida na maonjo. Wema unapata nguvu zake kwa kupingana na majaribu. Maisha ya askari mwaminifu ni mapambano na kusonga mbele. Hakuna kupumzika, msafiri mwenzangu, tukiwa upande huu wa Kanaani ile ya mbinguni... Lakini Yohana katika maono yake matakatifu, anawaona wale walio waaminifu watokao katika dhiki ile kuu, wakikizunguka kiti kile cha enzi cha Mungu, wakiwa wamevaa mavazi meupe, na kuvikwa taji ya utukufu wa milele. Ni nini, basi, kama wamehesabiwa kuwa ni takataka za dunia hii? Katika Hukumu ya Upelelezi maisha yao na tabia zao huchunguzwa mbele zake Mungu, na mahakama hiyo yenye taadhima huyageuza maamuzi [huyabatilisha] yale ya adui zao. Uaminifu wao kwa Mungu na kwa Neno lake hudhihirika, na heshima za juu za kule Mbinguni hutolewa kwao kama washindi katika pambano lao dhidi ya dhambi na Shetani. ----- RH, Agosti 28, 1883. KUKESHA KILA WAKATI Desemba 22 Lakini watu wabaya na wadanganyaji wataendelea, na kuzidi kuwa waovu, wakidanganya na kudanganyika. 2 Timotheo 3:13. Kwa kila mbinu anayoweza kutunga adui huyo anajaribu kutufanya sisi tusiweza kukesha. Kwanza, anaweza kutudanganya kwa maneno yake laini na kuzipenyeza hila zake ndani yetu, [mbinu] hizo zikishindwa, anaendelea kutumia mabavu waziwazi. Ana mitego mingi aliyoitega chini kabisa kwa ajili ya miguu ile inayotangatanga, na wale wanaonaswa mara moja wanaona ni vigumu kabisa kujinasua. Wakati wengine anawasifu, anawabembeleza, na kuwatukuza, wengine anawatupia mishale yake ya moto. Tunapaswa kukesha kila dakika. Siku za maonjo ya ajabu, dhiki, na hatari zi mbele yetu.... Yatupasa kuamua ya kwamba badala ya kutazamia mambo kugeuka na kuwa mazuri zaidi kwetu, watu wabaya, waalimu wapotofu, wataendelea na kuzidi kuwa waovu, wakijidanganya wenyewe na kuwadanganya wengine. Tunaweza kutazamia upinzani mkubwa kuliko ule tuliopata kuuona.... Sasa tunapaswa kumfanya Kristo kuwa kimbilio letu, vinginevyo, katika siku za usoni roho zetu zitagubikwa na giza pamoja na kukata tamaa. Kiko kikomo ambacho msaada wa kibinadamu hauwezi kufaa kitu kwetu. Kila mmoja ni lazima aishi kwa imani anapolazimishwa kuingia katika pambano lililo karibu sana na la kufisha dhidi ya nguvu zile za giza. Kila mmoja ni lazima asimame au aanguke mwenyewe. Mishale ya yule mharabu karibu sana itatupwa dhidi ya wale walio waaminifu, na hakuna mamlaka yo yote ya kidunia itakayougeuzia kando mshale huo. Lakini kama macho yetu yangefumbuliwa tungeweza kuwaona malaika wa Mungu wakiwazingira wenye haki, ili madhara yo yote yasipate kuja juu yao.... Yatupasa kumtazama Yesu, kujifunza maneno yake, kumwomba Roho wake. Tungetumia muda mwingi faraghani pamoja na Mungu katika tafakuri na maombi. Hebu na tuombe zaidi na kuzungumza kidogo. Hatuwezi kuitumainia hekima yetu wenyewe, uzoefu wetu wenyewe, na ujuzi wetu wenyewe wa ile kweli; kila siku ni lazima tujifunze, tukimwangalia Mwalimu wetu wa mbinguni kwa ajili ya kutupatia mafundisho, kisha, bila kujali starehe zetu, anasa zetu, wala hali zile zinazotufaa sisi, yatupasa kusonga mbele, tukijua ya kwamba yeye aliyetuita ni mwaminifu.... Ijapokuwa tunautambua udhaifu wetu, hebu na tuzitegemee nguvu zake, na kushinda kwa njia ya neema yake anayotupa. ----- RH, Agosti 28, 1883. TAJI KWA WALIO WAAMINIFU Desemba 23 Baada ya hayo nimewekewa taji ya haki, ambayo Bwana, mhukumu mwenye haki, atanipa siku ile; wala si mimi tu, bali na watu wote pia waliopenda kufunuliwa kwake. 1 Timotheo 4:8. Je, yule mtume mkuu kwa Mataifa ni kweli alijitolea mhanga alipobadili Ufarisayo wake na kuipokea injili ile ya Kristo? Twajibu Hapana! Kwa kusudi lake thabiti aliacha utajiri, marafiki na heshima zake katika jamii, heshima za watawala, na ndugu zake aliowapenda sana kwa moyo wake wote. Alichagua kuliunganisha jina lake na maisha yake ya baadaye pamoja na yale ya watu wale aliowaona kuwa ni duni na takataka miongoni mwa watu wote; lakini kwa ajili yake Kristo alipata hasara ya mambo yote. Kazi zake zilikuwa nyingi sana kuliko zile za wanafunzi [wake Kristo], kupigwa kwake kulipita kiasi. Alipigwa kwa viboko, alipigwa kwa mawe, alivunjikiwa meli, na katika mauti mara nyingi. Alikuwa hatarini katika nchi kavu na baharini, mjini na jangwani, kutoka kwa wanyang'anyi [majambazi] na kutoka kwa watu wa nchi yake. Alitekeleza utume wake chini ya udhaifu daima, katika maumivu makali, katika uchovu, katika kukesha mara nyingi, katika baridi kali, katika uchi.... Alipomjibu Nero aliyekuwa na kiu ya kumwaga damu, hakuna mtu aliyesimama pamoja naye.... Lakini, je! Paulo aliutumia muda wake mwingi wa thamani kusimulia jinsi alivyotendewa vibaya? La, aliyageuza mawazo ya watu kutoka kwake kuelekea kwa Yesu. Hakuishi kwa ajili ya furaha yake mwenyewe, hata hivyo alikuwa na furaha.... "Katika dhiki yetu yote nimejaa furaha ya kupita kiasi." 2 Wakorintho 7:4. Na katika siku zile za mwisho wa maisha yake, akiwa anakiona kifo cha mfia dini mbele yake, anashangilia akiwa ameridhika, "Nimevipiga vita vilivyo vizuri, mwendo nimeumaliza, Imani nimeilinda." 2 Timotheo 4:7. Akiyakaza macho yake juu ya umilele ule ujao, ambao ulikuwa ndio nia yake kuu iliyomtia nguvu katika kazi yake yote, anaongezea na kusema hivi, akiwa na imani iliyo na hakika, "Baada ya hayo nimewekewa taji ya haki, ambayo Bwana, mhukumu mwenye haki, atanipa siku ile" ----- Kisha mtu huyo aliyeishi kwa ajili ya wengine anajisahau mwenyewe ----- "wala si mimi tu, bali na watu wote pia waliopenda kufunuliwa kwake." Lo! ni mwanaume mwungwana alioje huyo! ----- Letter 1, 1883. Paulo alikuwa kielelezo hai cha vile kila Mkristo wa kweli anavyopaswa kuwa. Aliishi kwa ajili ya utukufu wa Mungu.... "Kwa maana kwangu mimi kuishi ni Kristo." Wafilipi 1:21. ----- 6BC 1112. LENGA JUU! Desemba 24 Maana katika yeye unakaa utimilifu wote wa Mungu, kwa jinsi ya kimwili. Na ninyi mmetimilika katika yeye aliye kichwa cha enzi yote na mamlaka. Wakolosai 2:9,10. Tunalenga chini mno. Alama ya kulenga iko juu zaidi. Mawazo yetu yanahitaji kupanuka ili tupate kujua umuhimu wa mpango wa Mungu. Tunatakiwa kuziakisi [kuzionyesha maishani mwetu] sifa za juu sana za tabia ya Mungu.... Sheria ya Mungu [Amri Kumi] ndicho kipimo cha juu ambacho inatupasa kukifikia kwa njia ya haki ile ya Kristo anayotuhesabia sisi ----- RH, Julai 12, 1892. Ni kwa njia ile tu ya kuelewa vizuri utume wake Kristo na kazi yake ndipo uwezekano wa kutimilika katika yeye, yaani, kukubalika katika yule Mpendwa, unaweza kufikiwa.... Sayansi ya kibinadamu sio taaluma ya mbinguni. Sayansi ya Mungu ni maonyesho ya Roho wa Mungu, akiamsha imani thabiti kwake. Watu wa ulimwengu huu wanaifikiria imani hiyo kuwa ni ya chini mno kuweza kuzingatiwa na mawazo yao makuu na akili zao nyingi, kuwa ni kitu kilicho duni mno kukiangalia; lakini hapo ndipo wanapokosea. Ni ya juu kabisa kuliko upeo wa akili zao za kibinadamu. Ujumbe wa injili haupingani na elimu ya kweli pamoja na mafanikio yale ya kiakili. Huo [Ujumbe] wenyewe ndio sayansi ya kweli, yaani, maarifa ya kweli ya kiakili. Hekima ya kweli inapita kabisa ufahamu wa wenye hekima wa ulimwengu huu. Hekima ile iliyositirika, ambayo ni Kristo kuumbika ndani, tumaini la utukufu, ndiyo hekima iendayo juu kama vile mbingu zilivyo juu. Kanuni zile zenye kina za kumcha Mungu ni za hali ya juu sana na za milele. Uzoefu wa maisha ya Kikristo peke yake unaweza kutusaidia kulielewa tatizo hili, na kujipatia hazina za maarifa ambazo zimesitirika katika mashauri yake Mungu, lakini ambazo sasa zinajulikana na wote walio na muungano hai na Kristo. ----- 6BC 1113,1114. Katika Kristo ulikaa utimilifu wote wa Mungu, kwa jinsi ya kimwili. Hii ndiyo maana, ijapokuwa alijaribiwa katika mambo yote kama sisi, alisimama mbele ya ulimwengu huu, tangu alipoingia humu kwa mara yake ya kwanza, akiwa hana waa lo lote la uovu, japo alikuwa amezungukwa nao [huo uovu]. Je, sisi pia hatupaswi kuwa washirika wa ule utimilifu, na je! si kwa njia hiyo, na hiyo tu, sisi tunaweza kushinda kama alivyoshinda? - ---- 7BC 907. Kwa njia ya kafara yake, wanadamu wanaweza kukifikia kipimo cha juu kilichowekwa mbele yao, na hatimaye kusikia maneno yasemayo, "Na ninyi mmetimilika katika yeye." ----- 7BC 909. UTAJIRI WAKE KRISTO USIOPIMIKA Desemba 25 Awajalieni, kwa kadiri ya utajiri wa utukufu wake, kufanywa imara kwa nguvu, kwa kazi ya Roho wake katika utu wa ndani. Waefeso 3:16. Mawazo makuu juu ya ukombozi ni mawazo makuu, ya maana sana, tena ni wale tu walio na mwelekeo wa kiroho wanaoweza kufahamu kina chake na umuhimu wake. Ni usalama wetu, furaha yetu, kuzungumza sana juu ya kweli zile za mpango wake wa wokovu. Imani na maombi ni muhimu kwetu ili tupate kuyaangalia mambo yale ya Mungu yenye kina. Mawazo yetu yamefungwa sana na mawazo finyu tuliyo nayo kiasi kwamba tunapata kwa kidogo tu picha ile ya uzoefu [wa maisha ya Kikristo] ambao ni haki yetu kuwa nao.... Kwa nini wengi wanaokiri kuwa na imani katika Kristo hawana nguvu zo zote za kuweza kuyapinga majaribu ya yule adui? ----- Ni kwa sababu hawatiwi nguvu kwa uwezo wa Roho wake katika utii wao wa ndani. Mtume anaomba hivi: "Mkiwa na shina na msingi katika upendo; mpate kufahamu pamoja na watakatifu wote jinsi ulivyo upana, na urefu, na kimo, na kina; na kuujua upendo wake Kristo, upitao ufahamu kwa jinsi ulivyo mwingi, mpate kutimilika katika utimilifu wote wa Mungu." Waefeso 3:17-19. Endapo tungekuwa na uzoefu huo, tungejua kitu fulani juu ya msalaba ule wa Kalvari. Tungejua maana ya kuwa washirika wa Kristo katika mateso yake. Upendo wa Kristo ungetubidisha, na ijapokuwa tusingeweza kueleza jinsi upendo wa Kristo ulivyoisisimua mioyo yetu, tungeuonyesha upendo wake kwa kujitoa wakf kwa bidii katika kazi yake. Kwa lugha ile inayojumuisha mambo mengi sana, Paulo anafunua mbele ya kanisa lile la Waefeso uwezo wa ajabu na maarifa wanayoweza kuwa nayo kama wana na binti zake yule Aliye Juu sana. Ilikuwa ni haki yao "kufanywa imara kwa nguvu...," kuwa na "shina na msingi katika upendo,... kuujua upendo wake Kristo, upitao ufahamu."... Yehova Imanueli [Kristo] ----- Yeye ambaye ndani yake hazina zote za hekima na maarifa zimesitirika ----- kuletwa katika ushirikiano naye, kuwa naye, kadiri moyo unavyozidi kupokea sifa za tabia yake zaidi na zaidi: kuujua upendo na uweza wake, kuwa na utajiri wake Kristo usiopimika... huo ndio urithi wa watumishi wa Bwana, na "haki yao inayotoka kwangu mimi, asema BWANA." Isaya 54:17. ----- RH, Nov. 5, 1908. MPATE KUTIMILIKA KWA UTIMILIFU WOTE WA MUNGU Desemba 26 Na kuujua upendo wake Kristo, upitao ufahamu kwa jinsi ulivyo mwingi, mpate kutimilika kwa utimilifu wote wa Mungu. Waefeso 3:19. Hapa vinafunuliwa vimo vya kuvifikia ambavyo twaweza kuvifikia kwa njia ya imani katika ahadi za Baba yetu aliye mbinguni, tunapotimiza matakwa yake. Kwa njia ya wema wake Kristo, tunaweza kukiendea kiti cha enzi cha uweza ule usio na kikomo. "Yeye asiyemwachilia Mwana wake mwenyewe, bali alimtoa kwa ajili yetu sisi sote, atakosaje kutukirimia na mambo yote pamoja naye?" Warumi 8:32.... Moyo ule uliopata kuonja mara moja upendo wake Kristo, unapiga kelele daima ili upate kunywa kwa kina zaidi; na kwa kuugawa, mtapokea kwa wingi zaidi na kwa kipimo kilichoshindiliwa. Kila ufunuo wa Mungu kwa roho ya mtu huongeza uwezo wake wa kujua na kupenda. Kilio cha daima cha moyo ni hiki, Niwe nawe zaidi, na dama jibu la Roho ni hili, Bado utakuwa nami zaidi... Maisha yake Kristo yalikuwa ni maisha yaliyojaa ujumbe wa upendo wake Mungu, naye alitamani sana sana kuugawa upendo huo kwa wingi kwa wengine. Huruma yake iliangaza toka katika uso wake, na mwenendo wake ulidhihirishwa kwa neema na unyenyekevu wake, upendo na kweli yake. Kila mshiriki wa kanisa lake lililo katika mapambano hana budi kuzidhihirisha sifa zizo hizo kama anataka kujiunga na kanisa lile litakaloshinda. Upendo wake Kristo ni mpana sana, umejaa utukufu mwingi sana, kiasi kwamba kwa kuulinganisha, kila kitu ambacho mwanadamu anakichukulia kuwa ni cha maana sana hufifia na kupoteza maana yake. Tunapouona ulivyo, tunashangilia, na kusema, Jinsi kilivyo kilindi kile kikuu cha utajiri wa upendo ambao Mungu amewapa wanadamu katika kipawa cha Mwanawe wa pekee!... Ni siri ya Mungu katika mwili, Mungu ndani ya Kristo, uungu ndani ya ubinadamu. Kristo aliinama chini kwa unyenyekevu usio na kifani, ili kwa kutukuzwa kwake katika kiti kile cha enzi cha Mungu apate kuwatukuza pia wale wamwaminio na kuwaketisha pamoja naye juu ya kiti chake cha enzi.... "Yeye awezaye kufanya mambo ya ajabu mno kuliko yote tuyaombayo au tuyawazayo," atatupa sisi "roho ya hekima na ya ufunuo katika kumjua yeye" (Waefeso 1:17), ili sisi tupate "kufahamu pamoja na watakatifu wote jinsi ulivyo upana, na urefu, na kimo, na kina; na kuujua upendo wake Kristo, upitao ufahamu," ili tupate "kutimilika kwa utimilifu wote wa Mungu." ----- RH, Nov. 5, 1908. WAKO KARIBU SANA KUFIKA NYUMBANI! Desemba 27 Basi mimi nikienda na kuwaandalia mahali, nitakuja tena niwakaribishe kwangu; ili nilipo mimi, nanyi mwepo. Yohana 14:3. Zaidi ya miaka elfu moja na mia nane imepita tangu Mwokozi alipoitoa ahadi hiyo ya kuja kwake. Kupitia katika karne hizo zote maneno yake hayo yameijaza ujasiri mioyo ya watu wake walio waaminifu. Ahadi hiyo bado haijatimizwa;... lakini, hata hivyo, ni neno la hakika ambalo limenenwa naye. ----- RH, Nov. 13, 19l3. Kristo atakuja katika utukufu wake, katika utukufu wa Baba yake, na katika utukufu wa malaika zake watakatifu. Elfu kumi mara elfu kumi na maelfu kwa maelfu ya malaika wale wazuri, wana wa Mungu washindi, walio na uzuri na utukufu usio na kifani, wataandamana pamoja naye katika safari yake. Mahali pa taji ya miiba, atavaa taji ile ya utukufu ----- taji ndani ya taji. Mahali pa mavazi yake ya zambarau, atavikwa mavazi meupe mno, "jinsi asivyoweza dobi duniani kuyafanya meupe." (Marko 9:3). Na juu ya mavazi yake na juu ya paja lake jina litaandikwa, "Mfalme wa wafalme, na Bwana wa mabwana." Ufunuo 19:16.... Kwa wafuasi wake waaminifu Kristo amekuwa mwenzi wao wa kila siku, rafiki anayejulikana. Wameishi pamoja na Mungu katika ushirikiano wa karibu sana na wa kudumu. Juu yao utukufu wake Bwana umewazukia. Ndani yao nuru ya elimu ya utukufu wa Mungu katika uso wa Yesu Kristo imeangaza. Kwa sasa wanaifurahia mionzi inayoonekana wazi ya mng'ao na utukufu wake Mfalme yule katika Utukufu Wake. Wamejiweka tayari kwa ushirikiano ule wa mbinguni, kwa vile wanayo mbingu mioyoni mwao. Wakiwa wameviinua vichwa vyao juu, miali inayong'aa ya Jua lile la Haki ikiwa inawaangazia juu yao, wakiwa wanashangilia kwa kuwa ukombozi wao umekaribia, wanatoka na kwenda kumlaki Bwana Arusi, wakisema, "Tazama, huyu ndiye Mungu wetu, ndiye tuliyemngoja atusaidie."... Wakati wa kungoja karibu sana umekwisha. Wasafiri na wageni ambao kwa muda mrefu sana wamekuwa wakiitafuta nchi ile iliyo bora wako karibu sana kufika nyumbani. Najisikia kana kwamba inanibidi kupiga kelele, nikisema, Twaenda nyumbani!... "Kwa hiyo, wapenzi, kwa kuwa mnatazamia mambo hayo, fanyeni bidii ili mwonekane katika amani kuwa hamna mawaa wala aibu mbele yake." 2 Petro 3:14. ----- RH, Nov. 13, 1913. KATIKA DUARA YA NDANI Desemba 28 Yeye ashindaye atavikwa hivyo mavazi meupe, wala sitalifuta kamwe jina lake katika kitabu cha uzima, nami nitalikiri jina lake mbele za Baba yangu, na mbele ya malaika zake. Ufunuo 3:5. Mpendwa kijana, je! unaweza kutazama mbele kwa furaha iliyojaa matumaini na matarajio hadi wakati ule Bwana, Hakimu wako mwenye haki, atakapolikiri jina lako mbele za Baba yake na mbele ya malaika zake watakatifu? Maandalizi bora unayoweza kufanya kwa ajili ya marejeo yake Kristo ni kukaa kwa imani thabiti katika wokovu ule mkuu aliotuletea alipokuja mara yake ya kwanza. Yakupasa kumwamini Kristo kama Mwokozi wako binafsi. ----- YI, Jan. 28, 1897. Wengi wetu hawatambui uhusiano wa agano tulio nao mbele zake Mungu kama watu wake. Tuko chini ya majukumu mazito kuweza kumwakilisha Mungu pamoja na Kristo. Yatupasa kujizuia tusimwaibishe Mungu kwa kujidai kwetu kwamba sisi ni watu wake, halafu kwenda kinyume na mapenzi yake. Tunajitayarisha kuhama. Basi na tutende kana kwamba tumefanya hivyo. Hebu na tujiweke tayari kwa ajili ya makao yale Kristo aliyokwenda kuwaandalia wale wampendao. ----- GCB, Aprili 1, 1903. Wale wanaojidai kuuamini ukweli wa wakati huu wasiponyenyekea chini ya malezi ya Mungu hapa duniani kwa ajili ya maisha yao ya baadaye, hawatamwona kamwe yule Mfalme katika uzuri wake.... Hawana budi wao kwa wao kukuza uvumilivu, utu wema, upole, fadhili, huruma, na usikitikivu. Mwelekeo wao wote wa kuwa na fujo, utovu wa adabu, na tabia isiyofanana na ile ya Kristo ni lazima uondolewe, kwa maana hakuna mojawapo ya tabia hizo za ukali inayotokana na Kristo, bali inafanana na ile ya Shetani. Tabia safi za mbinguni zinapokewa na kusitawi mawazoni, yaani, moyoni, na katika tabia pale tu mtu anapokuwa mshirika wa tabia ile ya uungu.... Mbingu haina budi kuanza papa hapa duniani kwa kila mtu atakayeingia katika makao yale juu mbinguni. ----- MS 29, 1892. Mbingu yote inayathamini sana mapambano ya wale wanaopiga vita kwa ajili ya taji ile ya uzima wa milele, ili wapate kushiriki pamoja na Kristo katika mji ule wa Mungu.... Mungu anawataka waweko kule, Kristo anawataka waweko kule, na majeshi ya mbinguni yanawataka waweko kule. Malaika wako radhi kusimama katika duara ya nje, na kuwapisha wale waliokwisha kukombolewa kwa damu yake Yesu ili wapate kusimama katika duara ya ndani.... Taji ya utukufu inawangojea wale wote wanaopiga vita vile vizuri vya imani. ----- MS 21, 1895. HEBU NA TUORODHESHE TULIYOFANYA NA KUYAKAGUA Desemba 29 BWANA, unijulishe mwisho wangu, Na kiasi cha siku zangu ni kiasi gani; Nijue jinsi nilivyo dhaifu. Zaburi 39:4. Mwaka mwingine karibu umepita milele.... Hebu na tuzipitie kumbukumbu zetu za mwaka huu ambao kwa haraka sana utakuwa umepita. Ni maendeleo gani tuliyofanya katika maisha yetu ya Kikristo? Kazi yetu ----- je! tumeifanya kiasi cha kustahimili kukaguliwa na Bwana, ambaye amempa kila mtu kazi yake kulingana na uwezo wake? Je! itateketea kama majani makavu, miti, au mabua hata isiweze kuhifadhiwa? au itastahimili kupimwa kwa moto?... Mpango wote umekwisha kufanywa ili sisi tupate kukifikia kimo cha cheo cha utimilifu wake Kristo Yesu ambacho kitatimiza kipimo kile cha mbinguni. Mungu hapendezwi na wawakilishi wake walioridhika na hali yao ya kudumaa wakati ambapo wangeweza kukua na kukifikia kimo cha cheo cha wanaume na wanawake cha utimilifu wake Kristo. Anawataka ninyi kuwa na kimo na upana katika uzoefu wenu wa Kikristo. Anataka ninyi mwe na mawazo makuu, azma bora, ufahamu ulio wazi wa kweli yake, na makusudi ya juu ya utekelezaji. Kila mwaka unaopita ungeongeza shauku ya mtu ili apate kutamani sana usafi na ukamilifu wa tabia yake ya Kikristo. Na iwapo ujuzi huo utaongezeka siku kwa siku, mwezi kwa mwezi, mwaka kwa mwaka, basi, haitakuwa kazi ambayo itateketezwa kama majani makavu, miti, na mabua; bali itakuwa ni ile ya kujenga juu ya msingi wa mawe, [kwa kuweka juu yake] dhahabu, fedha, na mawe ya thamani ----- kazi ambazo haziwezi kuteketea, bali zitaistahimili mioto ya siku ile ya mwisho. Je, kazi yetu ya kidunia, yaani, ya maisha haya tuliyo nayo, inafanywa kwa ukamilifu, uaminifu, kiasi kwamba itastahimili kuchunguzwa sana? Je, wapo wale tuliowakosea ambao watatoa ushuhuda wao dhidi yetu katika siku ile ya Mungu? Kama ndivyo ilivyo, basi, kumbukumbu hiyo imekwenda mbinguni, nasi tutakutana nayo tena. Tuko kazini kwa ajili ya [kuchunguzwa na] jicho lake yule Mkuu wa Kazi, haidhuru kama juhudi zetu nyingi zinaonwa na kuthaminiwa na watu au la. Hakuna mwanaume, mwanamke, wala mtoto awaye yote awezaye kumtumikia Mungu inavyokubalika kama anafanya kazi yake kwa uzembe, ovyo ovyo tu, kwa unafiki, iwe ni kazi ya kidunia au ya kidini. Mkristo wa kweli atakuwa na jicho safi kwa utukufu wa Mungu katika mambo yote, akijitia moyo katika makusudi yake na kujiimarisha katika kanuni zake, akiwa na wazo hili, "Nafanya hili kwa ajili yake Kristo." ----- RH, Des.16, 1884. SAHAU UCHUNGU WOTE Desemba 30 Siku zangu hupita upesi kuliko chombo cha kufumia. Ayubu 7:6. Kama sisi tuna wakati mchache tu, hebu basi, na tuutumie vizuri wakati huo mchache kwa bidii. Biblia inatuhakikishia kwamba sisi tu katika siku ile kuu ya upatanisho. Siku hii ya kivuli ya upatanisho ilikuwa ni siku ambayo Waisraeli wote walijitesa nafsi zao mbele zake Mungu, wakiziungama dhambi zao, na kuja mbele zake Bwana kwa toba mioyoni mwao, yaani, kwa majuto kwa ajili ya dhambi zao, toba ya kweli, na imani iliyo hai katika kafara [sadaka] ile ya upatanisho. Kama pamekuwa na matatizo,... yaani, kama mambo haya yamekuwapo, wivu, kijicho, uchungu, kuwawazia wengine vibaya, basi, ungama dhambi hizo, sio kwa njia ya kawaida bali waendee wewe mwenyewe ndugu na dada zako. Uwe wazi. Kama wewe umetenda kosa moja na wao ishirini, ungama hilo moja [la kwako] kana kwamba wewe ulikuwa mhalifu mkuu. Washike mkono, acha moyo wako ulainike chini ya uongozi wa Roho wa Mungu, kisha waambie hivi, "Je, mtanisamehe? Sijisikii ya kuwa nimetenda haki kwenu. Nataka kusahihisha kila kosa nililowatendea, ili kitu cho chote kisibaki kimeandikwa dhidi yangu katika vitabu vile vya mbinguni. Yanipasa kuwa na kumbukumbu safi kule." Unadhani ni nani angepinga hatua kama hiyo uliyochukua? Kuna hali ya ubaridi mno na kutojali ----- yaani, roho ile ya kusema, "Mimi sijali" imeenea sana ----- inayonekana miongoni mwa wafuasi wake Kristo. Wote wangejisikia ya kuwa wanajali, kila mmoja amjali mwenzake, wakiyatunza kwa kijicho mambo ya kila mmoja wao. "Pendaneni ninyi kwa ninyi." Basi tungeweza kuusimamisha ukuta wenye nguvu dhidi ya hila zake Shetani. Katikati ya upinzani na mateso tusingejiunga na wale wanaotaka kulipiza kisasi, tusingejiunga na wafuasi wa yule mwasi mkuu, ambaye kazi yake maalum ni kuwashtaki ndugu, kuwaumbua na kuwatia mawaa juu ya tabia zao. Hebu sehemu iliyobaki ya mwaka huu na itumike vizuri kwa kuharibu kila mzizi wa uchungu, na kuuzika kaburini [kuusahau] pamoja na mwaka huu mkongwe. Anzeni mwaka mpya kwa kujali sana, mkiwa na upendo wenye kina zaidi kwa kila mshiriki wa familia yake Bwana. Songeni mbele kwa pamoja. "Tukiungana, tunasimama; tukigawanyika, tunaanguka." Iweni na msimamo wa hali ya juu, ulio bora kuliko mliopata kuwa nao huko nyuma. ----- RH, Des. 16, 1884. THAWABU YA MWITO MKUU WA MUNGU Desemba 31 Ndugu, sijidhanii nafsi yangu kwamba nimekwisha kushika; ila natenda neno moja tu; nikiyasahau yaliyo nyuma, nikiyachuchumilia yaliyo mbele; nakaza mwendo, niifikilie mede ya thawabu ya mwito mkuu wa Mungu katika Kristo Yesu. Wafilipi 3:13,14. Yule ambaye angetaka kujenga tabia yenye nguvu, linganifu, yule ambaye angetaka kuwa Mkristo mwenye busara, hana budi kutoa yote na kufanya yote kwa ajili yake Kristo.... Paulo alifanya mambo mengi. Tangu wakati ule alipojitoa kumtii Kristo, maisha yake yalijazwa na huduma isiyojua kuchoka. Toka mji hata mji, toka nchi hata nchi, alisafiri, akisimulia kisa cha msalaba, akiongoa watu kwa injili yake, na kuanzisha makanisa.... Wakati fulani alifanya kazi yake mwenyewe ili kujipatia chakula chake cha kila siku. Lakini katika shughuli zake zote za maisha yake, Paulo hakulisahau kamwe kusudi lile moja kubwa ----- kukaza mwendo na kuifikilia thawabu ya mwito mkuu wa Mungu. Kusudi moja tu aliliweka mbele yake daima ----- kuwa mwaminifu kwake yeye ambaye katika lango lile la Dameski alijifunua kwake. Kutokana na kusudi hilo hakuna cho chote kilichokuwa na uwezo wa kumkengeusha.... Kusudi kubwa lililomsukuma Paulo kukaza mwendo wake licha ya shida na dhiki zilizomkabili lingemfanya kila mtenda kazi Mkristo kujitoa wakf mwenyewe kikamilifu kwa kazi ya Mungu. Vishawishi vya ulimwengu huu vitaletwa ili kuyavuta mawazo yake mbali na Mwokozi wake, lakini anapaswa kukaza mwendo kulifikia lengo lile, akionyesha kwa ulimwengu, kwa malaika, na kwa wanadamu ya kwamba tumaini lake la kuuona uso wa Mungu linastahili kupewa juhudi yake yote pamoja na kujitolea mhanga ili kutekeleza matakwa ya tumaini hilo. ----- AA 483,484. Mfuasi wa Kristo aliye duni [mnyonge] kuliko wote anaweza kuwa mwenyeji wa mbinguni, mrithi wa Mungu kwa urithi ule usioharibika, na usionyauka. Laiti kama kila mmoja angekichagua kipawa hicho cha mbinguni, kuwa mrithi wa Mungu kwa urithi ule ambao hati yake ya kuumiliki ni salama mbali na mharabu awaye yote, yaani, ulimwengu ule usio na mwisho! Songa mbele, kaza mwendo wako kuifikilia mede ya thawabu ya mwito wako mkuu katika Kristo Yesu. ----- FE 235. Hivi karibuni tutashuhudia kutawazwa kwa Mfalme wetu. Wale ambao maisha yao yamefichwa pamoja na Kristo, yaani, wale ambao katika dunia hii wamevipiga vita vizuri vya imani, watang'aa kwa utukufu wa Mkombozi wao katika ufalme wa Mungu. ----- 9T 287.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni