VITUNGUU SWAUMU
Kitunguu swaumu chaweza kutibu magonjwa mengi ikiwa mgonjwa atafuata maelekezo vizuri . katakata kitunguu swaumu saizi ya vidonge kasha umeze kwa kutumia maziwa ya moto.
KITUNGUU SWAUMU HUTIBU MAGONJWA YAFUATAYO
BRONHITIS (MKAMBA):
Ugonjwa wa kifua au mkamba ni mwambukizo wa mifereji inayoingiza hewa mapafuni, hii husababisha kikohozi chenye sauti mara kwa mara ikiambatana na kutoa makohozi mazito.
DIARHOHEA (KUHARA):
Ugonjwa wa hatari wa kuharisha dalili zake ni kupata choo chenye maji maji zaidi ya mara 6 katika masaa 12
HARDENNING OF HARTERIES:
Tatizo katika mishipa ya damu inayochukua hewa safi, mishipa hiyo ambayo huwa miepesi na laini huwa migumu na kushindwa kufanya kazi yake na kuhatarisha maisha ya muhusika.
INTESTINAL PARASITE
Hawa ni wadudu wadogo wadogo ambao hujificha ndani ya utumbo mdogo tene ni wakubwa kuliko backteria.
HAEMORRHOIDS/ PILE (RUTUNI):
Nimishipa ya damu inayovimba na kukunjamana na kujitokeza katika njia ya haja kubwa, husababisha maumivu makali wengine huuitakutoka mgongo.
VARICOSIS / VARICOSE VEIN (MISHIPA YA DAMU ILIYOVIMBA)
Hii ni mishipa ya damu iliyovimba, hukunjana na kuuma sana. Mara nyingi huonakana katika miguu ya watu wa makamo na akina mama wajawazito na waliuokwasha zaa watoto wengi.
KIDNEY DISEASES (MAGONJWA YA FIGO):
Kuna matatizo mengi ya figo na njia ya mkojo, mara nyingi si rahisi kuyatofautisha. Dalii :- Maumivu katikati ya mgongo au kiuno, ambayo yanaenea mpaka sehemu ya juu ya tumbo na chini ya mbavu, Dalili nyingine ni damu kwenye mkojo na uvimbe utosini.
OBESITY (UNENE)
Ni unene unaopita kipimo, mara nyingi husababisha matatizo mengi kama vili ugonjwa wa moyo, ugonjwa wa figo na mshuko (stroke). Watu wanene ndio hasa wanaweza kuwa na blood pressure
PIMPLES (CHUNUSI)
Ni viuvimbe vidogo vidogo vilivyo na ncha nyeupe ya usaha, au ncha nyeupe ya uchafu. Mara nyingi vinaweza kuuma au kutanuka.
HYSTERIA:
Ugonjwa wa kuweweseka upweke, husababisha chembe Fulani ya ubongo kutodaka mambo kadhaa ya lazima kwake . ugonjwa huu huwapata wanawake na hasa wasichana katika shule zisizo za mchanganyiko.
SKIN DISEASES
Ni magonjwa mbalimbali ya ngozi kama vile:
-IMPERTIGO CONTAGIOSA (mzio wa ngozi)
-BAKAMBA SHINGLES / HERPES ZOSTER
CUSTO / FEAR (WOGA)
Mtu mwenye custo huwa na woga wasi wasi mwingi na ni mwoga, na mtu huyu anaweza kuanza kutetemeka, tabia isiyo ya kawaida, kukondeana na mwisho kufa.
RHEUMATIC (UGONJWA WA KUKAKAMAA SEHEMU MBALIMBALI ZA MWILI):
Kuna aina 3 za ugonjwa huu:-
1.Rheumatic ya mifupa
2. Rheumatic ya misuli
3. Rheumatic ya viungo
MUSCLES INFLAMATION:
Shida katika misuli.
CONSTIPATION (KUFUNGA CHOO):
Mtu ambaye hapati choo kwa muda wa siku 2 au zaidi. Anshauliwa kutumia kitunguu swaumu.
TYPHOID FEVER (HOMA YA MATUMBO)
Hii ni homa inayoambukiza utumbo na kusababisha maumivu makali mwili mzima. Dalili zake ni sawa na zile za malaria.
MATATIZO YA INI
Mtu hukosa kabisa hamu ya kula, hapendi kula, hutaka kutapika, macho na ngozi hubadilika rangi na kuwa ya njano, choo huwa cheupe.
HOARSE VOICE / LARYNGITIS:
Sauti kutotoka sawa sawa, au kutoa sauti ya mikwaruzo.
Kutokana au ugonjwa wa kifuko cha sauti
NEUROSIS
Shida katika mishipa ya fahamu
METABOLIC DISORDERS:
Kushindwa kuyeyusha chakula
GALLSTONE (UCHAFU ULIO NDANI YA KIFUKO CHA NYONGO)
Mara nyingi nyongo husaidia kuyeyusha vyakula vya mafuta , uchafu ulio ndani ya nyongo husababisha nyongo isifanye kazi vizuri , na wakati mwingine nyongo hudhurika.
EYE SIGHT DISEASES
Kupoteza uwezo wa kuona sawasawa.
ANOREXIA / LOSS OF APPETITE:
Kukosa hamu ya kula
COUGHS
Kukohoa au kikohozi
ASTHMA
Shida ya pumu, kubanwa katika mapafu na kushindwa kupumua ghafla..
UTAYARISHJI WA KITUNGUU SWAUMU SWAUMU KWA AJILI YA MATIBABU YA MARALIA
Chukua punje 6 mpaka 7 za vitunguu swaumu, menya kisha vikatekate saizi ya vidonge, vimeze kwa maziwa ya moto au maji/ mara 3 kwa siku kwa muda wa siku 14. kwa magonjwa mengine yaliyoandikwa humu vimeze kwa muda mrefu maana hutibu kama chakula.
KUUMWA NA NYOKA AU NGE
kwa kuumwa na nge, saga kitunguu swaumu kiasi fulani upake pale ulipoumwa na pia kwa kuumwa na nyoka fanya vile vile kama ulivyoumwa na nge, fanya hivyo mara 3 kwa siku kwa muda wa wiki 1
2 wafalme. 20:7 Mungu mungu alimwambia Hezekia kuwa angemwongeza miaka 15 katika maisha yake. Kwa nini hakumponya pale pale?
Ni kwa sababu matibabu hayo ya asili yalibarikiwa na mungu. Ndio maana aliwaambia wachukue mkate wa tini na wapake kwenye jipu lake.
Mungu wa viumbe vyote, alimwongoza mwanadamu atumie dawa za asili leo .
NYONYO
Majani ya nyonyo ni tiba ya kifua kikuu
Mizizi yake ni dawa ya mafindofindo, kuungua, macho yanjano, uvimbe, koo, kisonono, kaswende.
Kikonyo chake ni dawa ya kwikwi. Jaza maji kwenye kikonyo, mpe mgonjwa anywe kila baada ya dakika 3 mpaka kwikwi iishe.
Kumeza punje zake kwa maji bilauri moja kwa siku kwa muda wa siku 5 kunatibu kuungua.
Tumia majani kwa kufungia miguu inayouma.
Majani yake ukiyapasha moto yafaa kukanda mgongo unaotoka na kuurudisha
Mizizi yake ukiiponda na kuichemsha yafaa kwa kutibu kisonono na kaswende, mizizi yake pia ikitafunwa na mama mjamzito, yafaa kwa kutoa mfuko wa uzazi (kondo la nyuma) kwa urahisi na salama zaidi.
NDURA
Sugua matunda kichwani kwa kutibu minyoo (ring worms) kwa binadamu, weka mara 2 au 3 kwa siku 3, usile tunda lake ni sumu.
Mizizi yake ikipondwa na kuchemshwa, na kunywewa kama chai hutibu magonjwa ya tumbo, meno na tumbo la uzazi.
Maji yake unaweza kuoshea vidonda.
Mizizi ikipondwa na kuchemshwa ni dawa ya kikohozi , kifua. Kunywa kijiko kimoja cha chai kutwa mara 3, kwa siku 5.
Mazizi iliyopondwa kikombe kimoja cha maji yaliyochemka loweka kwa muda wa dakika 5, chuja, kisha kunywa vijiko 2 vikubwa kutwa mara 3 kwa siku 5.
UNGA WA MKAA
Unaweza kupata kutoka kwenye mti wa mkuyu, kifuu cha nazi, msonobari na mkaratusi (eucalyptus). Na unatibu magonjwa yafuatayo:-
Kuumwa na nyoka
Kiungulia
Kusaga chakula
Uvimbe
Kutapika
Kuhara damu, kuharisha
Vidonda vya tumbo
Macho
Kunywa sumu
Tindikali
MATAYARISHO
Choma kifuu cha nazi hadi kiwe mkaa, saga uwe unga. Kama ni mti, tumia magome yake. Chukua kijiko 1 kikubwa cha mkaa (unga) changanya na maji safi ya kunywa ya uvuguvugu uwe kama uji uji. Kunywa kikombe kimoja cha mchanganyiko huo kabla ya kula.
INATIBU MAGONJWA YAFUATAYO
KUUMWA NA NYOKA
Shona kifuko cha kitambaa cheupe, chota mkaa kijiko kikubwa, weka ndani ya kifuko na maji kidogo, funga sehemu iliyoumwa, kisha fungua baada ya saa1, fungia nyingine hadi ufikapo hospitalini.
Pia endelea kumpa ya dawa hiyo hiyo ya kunywa, iliyokorogwa na kuwa kama uji mzito baada ya saa1 ufikapo hospitalini sumu yaweza kuwa imekwisha .
Pia kwa mtu aliyekunywa sumu:- tumia njia hiyo ya kunywa. Inafaa kuwa na dawa hii nyumbani mwako kila wakati.
MACHO
Weka katika kifuko cha kitambaa kama hapo juu, fungia au weka kwenye jicho. Funga kwa siku 3 mfululizo wakati wa usiku.
GILIGILANI
Inatibu tumbo, moyo na kadhalika.
MATAYARISHO
Vijiko 2 vikubwa vya giligilani, maji lita 1, chemsha kwa dakika 10, kunywa nusu kikombe kutwa mara 3. kwa siku 5.
PAPAI
Tunda la papai lina vitamini A,B,C,D, na E
INATIBU MAGONJWA YAFUATAYO
Shida ya kusaga chakula tumboni
Udhaifu wa tumbo
Kisukari na asthma
Kikohozi kitokacho mapafuni
Kifua kikuu
Inaleta afya nzuri ukitumia kila siku
Maziwa yanayotoka katika jani lake huponya vidonda
Yanasaidia palipoungua moto
Yanatibu kiungulia
Ugonjwa wa colon (njia ya haja kubwa ndani)
Yanasaidia kutofunga choo
Maganda yake yanasaidia kuungua, vipele, cancer ya ngozi. Mbegu zake zinatibu ini zikitafunwa 10 – 12 kwa siku 5.
Majani yake yakaushie ndani, yanatibu pumu. Inapoanza kubana yachome majani yaliyokaushwa kisha jifukize, kule kubanwa kutakisha.
Majani yake yanasaidia shinikizo la damu.
Papai likimenywa na kupondwa linafaa Sana. Hutumika Kama vile unavyotumia lotion kulainisha uso.
Meza mbegu kijiko cha chakula mara 3 inaweza kutibu homa
Mbegu zilizokaushwa ndani kisha zikasagwa kuwa unga zinatibu malaria, tumia kijiko 1 cha chai changanya na uji, kunywa mara 3 kwa siku 5
Mgonjwa wa kifua kikuu akila matunda haya kwa muda mrefu atapona bila dawa nyingine.
Mizizi yake ikipondwa na kulowekwa katika maji yaliyochemshwa, lita 2 na nusu kwa dakika 15, yanatibu figo, bladder, yanazuia kutapika. Nusu kikombe cha chai kutwa mara 3 kwa siku 5.
KAROTI
Ina vitamini nyingi mbali mbali
INATIBU MAGONJWA YAFUATAYO
Inalainisha tumbo
Inapigana na upungufu wa damu
Saratani
Baridi yabisi
Kusafisha damu
Vidonda vya tumbo
Kutibu chunusi
Macho
Koo
Kibofu
MATAYARISHO
Chukua karoti kilo 1, ponda au twanga iwe laini, chemsha kwa dakika 15 ndani ya maji lita 1 na nusu au 2, chuja kunywa juisi yake kwa vidonda vya tumbo au saratani ya tumbo na matumbo au saratani ya kizazi, tumia nusu kikombe cha chai miezi 3 mpaka 6.
Kwa ajili ya kurembesha uso nawia juisiyakekila siku asubuhi mfululizo kwa siku 5.
VITUNGUU MAJI
HUTIBU MAGONJWA YAFUATAYO
Uvimbe
Kikohozi
Vidonda vya tumbo
Mifupa
Ngozi
Koo
Figo
Tumbo
mkojo
MATAYARISHO
Menya vitunguu 3 vikubwa, visage au vitwange ili upate maji yake, changanya na maji kidogo yaliyochemka. Chukua punje 3 za kitunguu swaumu, mwaga maji ya vitunguu maji juu yake acha mchanganyiko ukae ndani ya bilauri masaa 2, ongeza asali vijiko vikubwa 5. tumia kijiko kikubwa kimoja kutwa.
MALIMAO
Magonjwa yafuatayo yanatibiwa kwa kutumia malimao kama tiba na kinga:
Matatizo ya tumbo
Kusaga chakula
Tindikali
Kuumwa kichwa
Mafindofindo
Saratani ya damu
Mafua
Dosari ya figo
Kukosa hamu ya chakula
Baridi yabisi
Njia ya haja kubwa
Kupunguza unene uliozidi kipimo
Kikohozi
Kisukari
Neva
Ini
Uvimbe
Tauni
Kifua kikuu
Vidonda
Kunyonyoka nywele
Malengelenge
Malaria
Jipu
Kiungulia
Figo
Kuumwa na nyoka
Pumu
Mfuko wa uzazi
(a)Dose 1- watu wazima
(b)Dose 2- watu wazima
Siku ya
Idadi ya malimao
Siku ya
Idadi ya malimao
1
4
1
6
2
8
2
10
3
12
3
14
4
16
4
18
5
20
5
22
6
20
6
22
7
16
7
18
8
12
8
14
9
8
9
10
10
4
10
6
Jumla
120
jumla
140
MATAYARISHO
(c)Dose ya 3 – watu wazima
Siku ya
Idadi ya malimao
1
8
2
16
3
24
4
32
5
40
6
40
7
32
8
24
9
16
10
8
Jumla
240
ONYO:
Usinywe yote mara 1, tumia pole pole, toka saa 12 – asubuhi mpaka saa 12 – jioni
Usichanganye na kitu chochote
Kama unaweza weka kwenye friji
Ukisahau kutumia siku 1, umeharibu tiba, anza upya. Hii tiba ni ya siku 10, Kama huugui, tumia Kama kinga.
TIBA YA MALIMAO NA KINGA KWA WATOTO
Maji ya limao kijiko kikubwa
Limao
Limao
Limao
Limao
Mwaka 1 -2
Miaka 3 -4
Miaka 5 - 9
Miaka 10 - 15
Miaka 16 - 29
1
0.5
1
2
3
2
1
2
4
6
3
1.5
3
6
9
4
2
4
8
12
5
2.5
5
10
15
6
2.5
5
20
15
4
2
4
8
12
3
1.5
3
6
9
2
1
2
4
6
1
0.5
1
2
3
30
15
30
60
90
ONYO:
Usinywe yote mara 1, tumia pole pole, toka saa 12 – asubuhi mpaka saa 12 – jioni
Usichanganye na kitu chochote
Kama unaweza weka kwenye friji
Ukisahau kutumia siku 1, umeharibu tiba , anza upya. Hii tiba ni ya siku 10, kama huugui, tumia kama kinga.
MACHUNGWA
Magonjwa yafuatayo yanatibiwa kwa kutumia machungwa kama tiba na kinga:
Beriberi
Kupooza
Kuungua
Meno
Chuma
Kizazi
Kusafisha damu
Mishipa ya damu
Kukinga magonjwa
Inaongeza nguvu zakiume
Mirija ya uzazi Kusaga chakula
(a)Dose 1- watu wazima
(b)Dose 2- watu wazima
Idadi ya machungwa
Siku ya
Idadi ya machungwa
5
1
7
10
2
14
15
3
21
20
4
28
25
5
35
25
6
35
20
7
28
15
8
21
10
9
14
5
10
7
150
jumla
210
(c)Dose ya 3 – watu wazima
Siku ya
Idadi ya machungwa
1
8
2
16
3
24
4
32
5
40
6
40
7
32
8
24
9
16
10
8
Jumla
240
Kamua maji ya machungwa kila siku, tumia pole pole toka saa 12 – asubuhi hadi saa 12 – jioni, usichanganye na kitu chochote, usisaze kwa ajili ya kutumia kesho, usinywe kwa mkupuo, ukisahau siku 1, umeharibu dozi, anza upya. Tumia kwa siku 10.
MCHICHA
Hutibu yafuatayo
Kuumwa mgongo
Kusafisha njia ya mkojo
Kusafisha damu
Unatibu tigo
Unatibu minyoo
Unatibu damu
Baridi yabisi
Tezi la shingo
Homa
Kuongeza damu
Unatibu maumivu
Tonic ya nywele
Unasaidia kupata haja ndogo kwa wingi
MATAYARISHO
Chukua mchicha kilo 1 chemsha maji lita 2 na nusu.
Yakichemka loweka mchicha kwa dakika 15. Tumia kikombe. Ni bora utumie yote kwa siku . Dozi ni siku 5
KUTIBU MGONGO
Chukua mchicha ponda. Chua mara 3 kwa siku. Usiku unapasha moto mchicha kisha unufunga mahali panapouma. Lala nao wakati vuguvugu la joto lake lenye maji ndani (dawa) ikiingia ndani fanyahivyo kwa siku 5, ukibadilisha kila siku (fresh)
TIBA YA TEZI LA SHINGO
Chukua mchicha kiasi kidogo, ponda, fungia shingoni pale penye uvimbe wakati unapolala kwa kitambaa, kwa muda wa siku 5,
MCHAICHAI:
Unatibu magonjwa yafuatayo
Unatibu magonjwa yanayotokana na utumiaji wa masufuria ya aluminium
Shinikizo la damu
MATAYARISHO
Weka majani katika maji yaliyochemka, kwa dakika 15, kunywa nusu kikombe cha chai, mara 3 kwa siku 5.
MBUYU
Unatibu yafuatayo:
Homa
Malaria
Kifua kikuu
Kukohoa
Pumu
MATAYARISHO
Chukua magome yake, weka ndani ya maji safi baridi. Tumia nusu kikombe kutwa mara 3
BISI
Hupunguza sukari mwilini, inatibu kisukari na inasafisha damu
TANGAWIZI
Inatibu kuchelewa kupata siku kwa wasichana (hedhi)
Husaidia nguvu za kiume
Inasaidia ulimi
Mafua baridi
Matatizo ya tumbo
Goita
Uvimbe
Koo
Kuharisha
Tindikali
Kipindupindu
MATAYARISHO
Chemsha, kunywa ikiwa yamoto.
Unywe tangawizi mbichi iliyotwangwa kama chai bila sukari.
Kikombe kimoja kwa siku, kwa siku 5.
RADISHI
Dawa ya chunusi, twanga, paka kwenye chunusi.
SUN FLOWER (ALIZETI)
INATIBU
Kufunga choo
Afya ya nywele
Inaimarisha misuli hasa kwa wazee
Shinikizo la damu, la juu na chini
Saratani
Kifua (tafuna mbegu)
Kuumwa miguu (tumia mbegu)
Malaria – chuma majani kilo 1, maji lita 2 na nusu. Chemsha maji loweka majani kwa dakika 15, tumia nusu kikombe, kutwa mara 3, kwa siku 5.
NDEVU ZA MAHINDI
Zinatibu;
Figo
Kibofu cha mkojo
Inasaidia uvimbe wa miguu
Shida katika kukojoa hasa kwa wanaume wazee
Watoto wanaokojoa kitandani (wape wataacha)
MATAYARISHO
Chukua ndevu za mahindi za kutosha, chemsha katika maji ya lita mbili, loweka kwa dakika 15, chuja, kunywa bilauri 2 kila siku, kwa siku 5.
MPERA
Tunda lina vitamini B na C,
Inatibu :-
Kifua kikuu
Kuharisha
Kuhara
Beriberi inasaidia usivimbe mwili.
MATAYARISHO
Chemsha majani kilo 1 kwa dakika 10, katika maji lita 2 na nusu, mpe mgonjwa anayeharisha, kikombe 1 kutwa mara 3. anayeharisha damu mpe matunda ale
EGG PLANTS (BILINGANYA)
Tunda ukilipika kama mboga linatibu vidonda vya tumbo,
Linasaidia kupata usingizi
Uharakisha kupona magonjwa
Huleta afya nzuri ya mwili
Linatibu jipu (liponde na paka kwenye jipu)
Juisi yake huondoa sumu mwilini kwa njia ya mkojo.
KARANGA
Ina protini kwa wingi na calories.
Inakisiwa kuwa na pound moja ya karanga ina calories 3000. ina vitamini A,B na E, huwatia nguvu wale wanaojishughulisha na kazi za mikono na wale wafanyao kazi za ofisini ndiyo maana mafuta yake yamependekezwa kupikia.
TAHADHARI
Wale wanaougua gout au wenye matumbo dhaifu wanapaswa kuepuka karanga, kwa sababu zinapokaangwa hutoa “uric acid”ambayo inadhuru mwili
NAZI
Ina vitamini A,B na E
Nazi changa huwa na maziwa ambayo huleta afya mwilini, hasa kwa watoto na wazee.
Huleta afya ya damu
Huimarisha utumbo
Husaidia mapafu dhaifu
Husaidia magonjwa ya nerve
Huondoa uchovu mwilini
Hukomesha usahaulufu
Hufanya viungo viwe na nguvu
Husaidia homa ya nje na ndani
AVOCADO (PARACHICHI)
Lina vitamini A,B na C
Huleta yafuatayo mwilini:
Nguvu ya mwili na ubongo
Hujenga neva na fahamu
Hujenga mifupa na kuipa nguvu
Huleta kuona vizuri
Vita yake mwilini:
Hupiga vita ukosefu wa damu (anaemia)
Hufanya kazi kuondoa nywele zinazoanguka
Husaidia kukuza nywele zinazodumaa (dandruf)
Husaidia kutuliza maumivu (inapopakwa au kusuguliwa sehemu yenye maumivu)
Matibabu
Majani yake yakichemshwa kama chai na kunywewa husaidia kuondoa matatizo ya mwili;
Uchovu
Udhaifu
Kujisikia ovyo
Kuumwa kichwa
Koo (throat)
Tumbo
Mapafu
Uvimbe
Vidonda mdomoni (kwa kutafuna majani)
Kukwama kwa mkojo(kwa kutumia mbegu iliyosagwa na kukaangwa)
Koroga vijiko 2 vya unga huo katika maji ya moto kikombe kimoja.
Nyama hutia uric acid nyingi mwilini
Tunda hili hutoa uric acid
Nyama huleta yafuatayo mwailini
Udhaifu wa wa tumbo
Kufunga tumbo
Baridi yabisi
Magonjwa ya figo
Magonjwa ya ngozi
Gout
Magonjwa ya ini
Shida katika utumbo mwembamba
Arthritis
MAHARAGE YA SOYA
Soya ina vitamin A,B,C,D,E na K. hakuna chakula duniani chenye vitamini nyingi kama hiki, soya ina protini ya ajabu na mafuta pia ambayo huifanya kuwa chakula pekee na safi. Uboreshaji wake wa afya ulifanya watu wa zamani kuitambua kama chakula cha pekee kwao ikawa chakula kizuri cha mbadalaambacho walikitumia badala ya nyama, maziwa na mafuta (butter) pamoja na mayai.walitumia watu wa rika zote, na wagonjwa pia, ilitumiwa pia kulisha ndama, ng’ombe, na kwa kufanya hivyo 90% ya ugonjwa wa kifua kikuu ulipungua kwa ndama. Soya ina mambo mengi na misaada katika miili ya wanadamu.
KAZI YA SOYA MWILINI
Soya ina glycerine na fatty acid ambayo inasaidia kazi nzuri ya ufanyaji kazi wa ubongo na maini. Pia ina chakula kizuri kwa neva ya ufahamu iliyochoka maana ina licitini, hii huifanya kuwa chakula kizuri sana kwa wazee.
PROTINI YAKE
Kilogram 1 ni sawa na protein inayopatikana katika mayai sabini.
Kilogram 1 ni sawa na protein inayopatikana katika nyama kilo 3
Kilogram 1 ni sawa na protein inayopatikana katika maziwa lita 2.
MATUMIZI
Soya hutengenezwa karanga za kutafunwa
Soya hutengenezwa chakula cha nyama.
Soya hutengenezwa maziwa mazuri sana
Unga wa soya hutumiwa kwa:-
Kukaangia chakula
Kupikia ugali
Kupikia chapati na mikate.
MATAYARISHO
Weka maharage ya soya kwenye maji, kwa masaa 24. kisha yaanikwe na kusagwa ili kupata unga .
SOYA HUTIBU YAFUATAYO
Hutibu vidonda vya tumbo
Kisukari
Saratani
Tumbo
Figo
Ini n.k
MAELEZO ZAIDI KUHUSU MATAYARISHO NA MATUMIZI YA MAHARAGE YA SOYA
Ikumbukwe, kama tulivyoona hapo juu kwamba, maharage ya soya ni chanzo kizuri sana cha protein ifaayo kwa ukuzi na ustawi wa binadamu. Hata hivyo ni vyema izingatiwe kuwa, ndani ya maharage hayo vimo viini ambavyo visipodhibitiwa huudhuru mwili wa mlaji, viini hivyo vinajulikana kama “Anti Nutritional Factor” mojawapo na maarufu ni vile viitwavyo “Trypsin initiator” ambavyo vinapotumiwa huzuia protein isitumike mwilini mwa mlaji. Salama ni kuhakikisha kuwa hizo “Anti – Nutritional Factors” zimeangamizwa, nazo huweza kuangamizwa kwa njia ya joto kwa kuchemsha au kukaanga. Kwa matokeo mazuri, kabla ya kuchemshwa au kukaanga ni vyema kuyaloweka majini – kikombe kimoja cha soya katika vikombe 5 vya maji kwa muda wa masaa 6, kisha chemsha kwa dakika 30, yakaushe barabara ndipo yasagwe
ZINGATIA UWIANO UFUATAO
1:5 kwa kuyaloweka (soya : maji)
1:9 kwa ajili ya uji (unga wa soya : unga mwingine)
1:3 kwa wjili ya maziwa (unga wa soya : maziwa)
KWA MAZIWA
Baada ya kukoroga mchanganyiko huo, chujavyema na kitaambaa safi. Kimiminika kinachopatikana ndiyo maziwa ya soya. Ni vyema maji yatumiwe yaliyo salama baada ya kuchujakiasi.
Kukaanga maharageya soya yaliyolowekwa kwa masaa 6 hadi yanapo kuwa na rangi kama ya majani makavu (brown) kuangamiza trypsin initiators. Ikiwa maharage ya soya yasiyolowekwa yamekaangwa hadi kuwa na rangi kama ya majani makavu (brown) trypsin initiators huwa imeangamizwalakini protini huwa pia imedhurika. Hivyo salama na uloweke kwa masaa 6 kabla ya kukaanga, tumia moto kidogo ili usiyaunguze.
MUHIMU
Ili kuandaa unga wa soya wenye mwonjo wa lishe unaokubalika, tumia maharage ya soya mazima kabisa.
ASALI
Inafanya kazi ya kuponya maradhi yafuatayo:-
Hulainisha jipu na kuondoa usaha
Hutuliza tumbo
Husaidia uyeyushaji wa chakula tumboni
Husaidia kifua na mapafu
Hupakwa kwenye vidonda vya wazi, inalainisha na kutibu
It activates the internal glands
Huamarisha glands na tezi (hormones), hivyo iliwe kila mara.
Magonjwa mengine hujitokeza kama hakuna asali
Kipande cha mkate, maziwa na asali ni mlo kamili.
Ili tumbo lifanye kazi yake vizuru, jizoeze kul asali.
CUCUMBER (MATANGO)
Hutengenezwa kama juisi au kutafunwa bila kupikwa. Osha vizuri na kula na maganda, ukiondoa maganda siyo mbaya sana pia.
TIBA YAKE
Hutibu magonjwa ya saratani
Vidonda vya tumbo
Magonjwa ya ngozi
Majipu
Hutumiwa kwa urembo wa ngozi (sugua uso kwa kipande cha tango au osha uso kwa juisi yake)
Huondoa uric-acid katika mwili unapolia
Inasafisha na kutibu utumbo mwembamba
Inazuia na kutibu magonjwa ya ini na figo na figo.
Juisi yake inasaidia mwili kufanya vizuri.
NB: Vitamini na madini mengi, vipo kwenye maganda. Hivyo unapotumia, usitoe maganda ingawa mengine ni machungu kidogo.
Watu wenye mikono yenye michubuko, watumie matango kwa kupaka mikono na mwili wote .weka katika beseni , osha uso na mwili wote
NANASI
Nanasi ina vitamini A,B na C na pia ina madini ya chuma, calcium, copper na phosphorous. Tunda hili husaidia kutengeneza damu na kuimarisha mifupa , meno, neva na misuli (muscles).
TIBA YAKE
Hutibu matatizo ya tumbo
Bandama (spleen)
Ini
Utumbo mwembamba
Homa
Vidonda mdomoni
Magonjwa ya koo
Kupoteza kumbukumbu
Maradhi ya akili
Kukosa mori (low spirit)
Kikohozi
Kutetemeka
Woga
Matatizo ya wanawake (upungufu wa hormones au makosa fulani katika sehemu za siri )
Huondoa shida ya kufunga choo
Baridi yabisi
Upungufu wa danu
Inasaidia akina mama wanaonyonyesha (wenye maziwa machache)
NDIZI
Ina vitamini A,B na E pia ina madini ya iron, potassium, calcium, sodium, magnesium, silicon, phosphorous, surphur na chlorine.
Msaada wake mwilini
Hupigana na magonjwa ambayo huja na maji mwilini
Husaidia watu wadhaifu
Husaidia udhaifu wa tumbo au mwili
Inasaidia sana kuponya ugonjwa wa kifua kikuu
Pia huponya magonjwa kama:-
Rheumatism
Arthritis
Gout
Constipation
Diarrhoea
Gallstone
Chest
Kidney
Small intestine
Neva
Kuvimba miguu
Unene unaweza kuondoka kwa kuacha kula kila kitu isipokuwa ndizi
Tumia ndizi 10 hadi 15 mara 3 kutwa,
baada ya dozi hiyo, rudia kula ndizi 5 hadi 10 mara 3 kutwa,
baada ya dozi hiyo rudia kula ndizi 2 tu kwa kila mlo.
Matokeo yatakuwa wazi baada ya kumaliza dozi hiyo.
Tumia ndizi pia kusafisha damu, wengine damu huchafuka na acid na pia ulaji mbaya. Sasa dawa ya kusaidia ni ndizi. Maji ya mgomba wake hutumiwa kwa kuponyesha hermorrhoids (pile) kwa kupaka, na hata kwa kunywa ikiwa yamechanganywa kwa nephritis.
USHAURI
Ndizi isiliwe na mboga za majani (usababisha kiungulia)
Ndizi isitiwe mafuta mengi
Usile ndizi na pombe (usababisha kiungulia)
Ndizi isitumiwe mara 1 kwa wingi.
DAWA YA UVIMBE
Weka kipande cha limao
Kata kitunguu maji, chemsha weka kwenye uvimbe
Weka asali.
DAWA YA KIKOHOZI
Malimao 8, yakate vipande 2 bila kuyakamua, yachemshe kwa dakika 5 katika maji ya lita 2 na nusu.
Chukua punje 8 za vitunguu swaumu , chemsha kwa dakika 5
Chukua kitunguu maji nusu, na maji kidogo, chemsha.
Chukua tangawizi 3, menya, twanga, usichumshe
Changanya michanganyiko yote pamoja, viache kwa siku nzima, tumia nusu kikombe cha chai 1 mara 3 kutwa.
DAWA YA KIFUA
Chukua majani ya mkuyu kilo 1,yaponde, yaweke ndani ya maji lita 2 hadi 5, yachemshe kwa dakika 15, chuja ongeza maji ya limao 2 na asali kidogo. Kunywa vikombe 3 kwa siku
DAWA YA FANGASI
Maji ya malimao, paka. Ukiwashwa sehemu za siri, ni fangai, tumia kujisafisha na maji ya limao ukichanganya na maji safi. Na miguu pia, paka vidoleni pia.
SHINIKIZO LA DAMU
Tumia tiba ya malimao kwa siku 10, kulingana na umri
Karoti, zitwange karoti, zichemshe kwa dakika 5, ndani ya maji lita 2 hadi 5. kunywa kikombe kkubwa kwa siku mara 3
KIKOHOZI NA KUZIBA SAUTI
Chukua punje 10 za vitunguu swaumu, weka maziwa kiasi na asli. Kata vitunguu vipande vidogo vidogo, viache usiku kucha, kunywa kabla ya kula
DAWA YA KISUKARI
Star of Jerusalem – tafuna maua 3 kila siku
Tiba ya malimao a 120 kwa kulingana na umri
Tunda la parachichi
Maharaga ya soya
Tui la nazi
Epuks vyskuls vya sukari
Usile nyama
Punguza kula maziwa na mayai
Kunywa juisi ya karoti kila siku
Aloe vera
Chemsha mizizi ya star of Jerusalem, inywe kwa muda wa siku 10 kikombe kimoja mara 3.
TIBA ZA MAGONJWA YA NGOZI MAKALI
Tiba ya malimao a 120 kwa kulingana na umri
Mchicha kilo 1, loweka kwa dakika 15, katika maji ya lita 5 yaliyochemka. Tumia kama juisi, usichanganye na kitu kingine
Majani ya mwarobainia kilo 1, lita 5 za maji. Loweka majani katika maji ya moto kwa dakika 15. kunywa nusu kikombe cha chai kutwa mara 3.
Majani ya mkuyu, maji lita 5, lita 5 za maji. Chemshe kunywa, huongeza maziwa kwa akina mama wanyonyeshao.
STAR OF JERUSALEM
Hutibu
Kisukari - tafuna maua kila siku mara 3
Kisonono – ponda mizizi, chemsha, kunywa maji yake
Kaswende – ponda mizizi, kunywa maji yake (juisi)
Meno – ponda mizizi, tia kwenye jino linalouma
Malaria – chemsha maji kidogo, kamua malimao 2, weka maua machache,
itakuwa tayari baada ya dakika 5. tumia vijiko 2 vya chakula kwa siku
HOLYTHISTLE
Hutibu
Ugonjwa wa akili
Kupoteza fahamu
UANDAAJI
Chuma majani nusu kilo, chemsha maji lita 2 na nusu, loweka maji katika maji ya moto kwa dakika 5. tumia kikombe kikubwa cha nusu lita kutwa mara 3 kwa juma..
ULIMI WA MAMA MKWE –ALIBIZO (MTANGA)
Nzuri kwa masikio – kamua tone sikion
Juisi ya mizizi inafaa kwa haemolorrhages na minyoo ya tumboni (mizizi yaweza kuliwa mibichi au iliyochemshwa na maji au maziwa)
Husaidia ugonjwa wa meno – chemsha, sukutulia mara 3kwa siku 5 mfululizo
ALOEVERA
Usitumie ukiwa mjamzito au unanyonyesha
Hutibu :-
Malaria
Shinikizo la damu
Ukiumwa na mdudu
Mkanda wa jeshi
Ukiungua na jua
Husaidai wanawake wanaochelewa kupata hedhi
Baridi yabisi
Maumivu ya viungo
Husaidia myeyusho wa chakula tumboni
Husaidia wenye shida ya mkojo, mkojo unaotoka kwa shida
Saratani
Bawasiri
Kisukari
Nguvu za kiume
Inasaidia askari wa mwili
Huleta hamu ya kula
Huondoa homa ya matumbo
Vidonda vya tumbo
Hutibu kuvimba mwili
Huongeza siku kwa wagonjwa wa ukimwi.
MATAYARISHO
Kwa magonjwa yote yaliyoorodheshwa
Chukua vipande 3, osha vizuri kisha katakata vipande vidogovidogo, weka kwenye maji safi na salama yenye uvuguvugu kwa muda wa masaa 12, kisha tumia nusu kikombe cha chai kutwa mara 3, kwa siku 5 mfululizo. Rudia dawa hii mara kwa mara kwa kinga na tiba.
MGAGANI
Majani yake ni dawa ya sikio, hasa lenye usaha, safishia sikio kila jioni kwa siku 5.
UKWAJU
Chesha majani yake na magadi, paka mwili wa mgonjwa mwenye tetekuwanga
CASTOR TREE
Chemsha maji yake kwa kurudisha mgongo unaotoka nje (rectum)
Mizizi yake weka juu ya mkaa, ikishapata joto, mama mwenye mamba aitafune atazaa salama na mfuko utatoka bila matatizo
MATIBABU YA KIKOHOZI
Maji ya machungwa
Kitunguu swaumu
Tangawizi
VIFAA
Tangawizi
Machungwa 3
Kitunguu swaumu vikombe 2
NJIA
Nawa mikono yako kwa sabuni, kabla na baada ya matayarisho
Osha tangawizi, toa tope lote, toa ganda na utwangwe
Osha na machungwa ili utomvu wake usiingie katika mchanganyiko, kata na kamua maji na weka ndani ya maji ya machungwa
Tikisa mchanganyiko huo ndani ya maji ya chupa nyingine, ambayo ina kizibo imara.
Chuja mchanganyiko huo na chujio la chai
Unaweza kuweka sukari
Kunywa mchanganyiko huo bilauri 1, asubuhi na jioni. Angalia matokeo yake baada ya siku 3.
USHAURI KUHUSU ULAJI BORA
Magonjwa mengi yanayoonekana leo husababishwa na ulaji mbaya. Kwa kuzingatia mambo yafuatayo unaweza kuepuka magonjwa mengi.
Kula matunda kwa wingi na mboga za majani
Badilisha chakula chako mlo hadi mlo
Usitumie aina nyingi za vyakula kwenye mlo 1
Tumia nafaka zisizokobolewa (zilizokobolewa hazifai kwa afya)
Mchele usioshwe sana (kuosha sana mchele huondoa virutubisho)
Tumia sukari, chumvi na mafuta kwa kiasi kidogo
Epuka viungo vya kukolezwa chakula na dawa ya kuumulia
Kuwa na muda maalum wa mlo kila siku (kwa mmeng’enyo mzuri wa chakula)
Usile chohote katikati ya milo (uharibu uyeyushaji wa chakula tumboni)
Kula kiamsha kinywa kizuri na cha kutosha (huu unapaswa kuwa mlo mkubwa kuliko yote kwa siku)
Kula kiasi dogo cha chakula wakati wa jioni (masaa 2 au 3 kabla ya kulala)
Usile kupita kiasi (chakula kingi hupumbaza akili/ubongo, husababisha, uchovu, huongeza magonjwa, hufupisha maisha.)
Kula taratibu na kutafuna chakula vizuri huleta faida kwa mlaji.
Kunywa maji safi na salama yakutosha kila siku
Usinywe maji wakati wa mlo, kunywa mapema kabla au baada yam lo
Nb:- kufunga ni msaada katika kudhibiti tama ya chakula na zoezi la kuwa na kiasi maishani. Kufunga ni dawa bora kwa magonjwa mengi, hasa kwa watu wasiofanya kazi ngumu za mikono.
UMUHIMU WA CHAKULA KIZURI
Chakula ni uhai wa mtu, tena chakula ni uzima. Kile unachokula ndicho wewe. Chakula unachokula ndicho hukutengeneza wewe (mwanzo 1:29, eze 47:12)
Mungu huwaelekeza watu wake kutumia dawa nyepesi, kuna njia nyingi za uponyajilakini ipo moja tu ambayo imethibitishw na mbingu.
Dawa ya mungu ni rahisi na haidhoofishi mwili wa mtumiaji. Hewa safi, maji na chakula bora. Usafi wa maisha na imani imara juu ya mungu, ni dawa zinazotakiwa kwa maelfu ya wanaokufa, hata hivyo dawa hizo hazijaliwi kwa sababu matumizi yake yanahitaji uangalifu ambao watu wengi hawapendelei.
MAJI
Ni tiba ya magonjwa nje na ndani ya mwili
Maradhi ya muda mrefu na mfupi yanayosababisha kifo huweza kuponywa kwa urahisi sana kwa njia inayoiywa water therapy
Ikiwa njia hiyo itafuatwa huweza kutibu maradhi yafuatayo:-
Kuumwa na kichwa
Presha
Upungufu wa damu
Kupooza
Mapigo ya kasi ya moyo
Kuzimia
Kikohozi
Pumu
Kifua kikuu
Kiungulia
Kuharishadamu
Kisukari
Matatizo ya macho
Matatizo ya pua
Matatizo ya masikio
Matatizo ya koo
NAMNA YA KUTENGENEZA TIBA HII
Baada ya kuamka asubuhi na mapema, kabla ya kupiga mswaki na kunawa uso, kunywa bilauri 4 za maji. Usile wala kunywa chochote mpaka baada ya dakika 45. baada ya kunywa bilauri 4 za maji ndipo upige mswaki na kunawa uso
Kwa walio dhaifu wanashauriwa , waanze mpango huu kwa kunywa bilaui 1 mpaka 2, na pole pole waongeze idadi hata kufikia 4.
Water therapy pia ina msaada mkubwa kwa afya yako na huwasaidia wengi kujenga afya zao na kuwaponya kwa kipindi kifupi sana
Uchunguzi umebain kuwa, kwa tiba hii ya ajabu maradhi yafuatayo yanaweza kupona kwa kipindi kilichooneshwa.
Shinikizo la damu – mwezi 1
Matatizo ya gesi – siku 10
Kisukari – mwezi 1
Kufunga choo – miezi 6
Kana – miezi 6
Kifua kikuu – miezi 3
Wenye gesi na homa za mifupa (dozi ni mara 3, kwa siku 10.)
MDALASINI NA ASALI
Asali na mdalasini vyaweza kutibu magojwa yafuatayo
Ugonjwa wa viungo / maumivu na uvimbe
Tengeneza kikombe cha chai (vijiko 2 vya chakula vya asali na kijiko 1 cha chai cha mdalasini) kunywa asubuhi na jioni.
Chua sehemu yenye maumivu kwa kutumia mchangayiko wa asali,maji ya uvuguvugu na mdalasini
Kukatika nywele (hair loss)
Mchanganyiko wa asali, mdalasini na mafuta vuguvugu ya aloevera. Hutoa kichocheo maridhawa cha kuotesha nywele, kinachotumika katika dawa ya dork. Mchanganyiko huo vuguvugu unapakwa kwa kusugua kichwani na kuacha kwa dakika 15.
Ukungu wa miguuni (fungus)
Mchanganyiko wa asali kijiko cha mezani 1, mdalasini vijiko 2.
Paka semu zilizo athirika., kaa nayo kwa nusu saa, kisha nawa na sabuni.
Maambukizo kwenye kibofu cha mkojo (bladder infection)
Mchanganyiko wa asali kijiko 1, mdalasini vijiko 2 vya chai n maji ya uvuguvugu. Huondoa backteria kwenye kibofu,tumia kama juisi.
Maumivu ya jino (toothache)
Mchanganyiko wa asali kijiko 1 cha chakula, mdalasini kijiko 1 cha chakula. Koroga, iache siku 1 ndipo udondoshe kwenye jino 1, hasa lililochimbika. Fanya hivyo mara 2, kila siku kwa siku 5 mfululizo.
Vidonda vitokanavyo na kulala kwa muda mrefu (cancer sores / bed sores)
Mchanganyiko wa asali , mdalasini na saladi ya kupaka vidonda kwenye chai ya respebery ni dawa nzuri ya bed sores
Rehemu (chorestral)
Bilauri 1 yenye mchanganyiko wa mdalasini vijiko 2 vikubwa na maji ya moto.
Mafua (colds)
Kijiko 1 cha mezani, cha asali vuguvugu iliyochanganywa na kijiko cha chai cha mdalasini. Mchanganyiko huu huondoa chafya na kuvimba koo.
Ugumba
Asali huamsha ashiki kwa wapenzi wa aina zote 2. kunywa angalau vijiko 2 kwa siku, usiku kabla ya kulala. Familia 1 iliyokuwa haina watoto ilitumia mchanganyiko (mgando) huu wa asali na mdalasini na kufanikiwa kupata watoto mapacha wa kike, baada ya kushindwa kupata watoto kwa muda wa miaka 14.
Mdalasini umetumika kwa muda mrefu kama dawa ya kuongeza uwezo kwa akina mama wenye kuhitaji kuzaa. Kula kipande cha mkate, chenye virutibisho vingi, kilichopakwa kijiko 1 cha mezani cha mchanganyiko huo hapo juu kila siku. Hii hupunguza kuganda kwa mishipa ya damu.
Shinikizo la damu
Dozi za mara kwa mara za asali iliyochanganya na mdalasini
Kinga ya mwili (immune system)
Kinga yako ya mwili itaongezeka mara 3 zaidi, kama utatumia mara kwa mara asali na mdalasini
Mchafuko wa tumbo
Asali huondoa mchafuko wa tumbo pamoja na kichefuchefu, ongeza na kiasi kidogo cha mdalasini, utapunguza maumivu yaletwayo na vidonda vya tumbo.
Tindikali au gesi
Kula asali pamoja na mdalasini, huweza kuondoa mchafuko tumbo uletwao na gesi na acid
Ugonjwa wa moyo (heart diseases)
Unaweza kukinga ugonjwa wa moyo na kuzuia mkusanyiko wa mtando wa mafuta kwenye damu kwa kula asali na mdalasini mara kwa mara, au kwa kupaka kwenye mkate wakati wa kifungua kinywa.
Ukosefu wa nguvu za kiume / uhanisi (impotence)
Asali huamsha ashiki, ni dawa madhubuti ya kuponyesha uhanisi. Kutokana na uwezo wake ilipigwa marufuku kwa makasisi katika baadhi ya dini za mashariki
Kutomeng’enywa kwa chakula tumboni (indestion)
Kunywa vijiko 2 vya asali, vilivyonyunyiziwa mdalasini kabla yam lo. Huondoa kiungulia . asali pia husaidia kutolewa kwa juisi zinazotumika kumeng’enya chakula (enzymes) . na mdalasini unaongeza kasi ya kumeng’enya chakula
Flu (mafua makali)
Umri wa kuishi (longevity)
Pata kikombe baridi cha chai ya mdalasini na asali kila siku, unaweza kuishi hadi miaka 100, ukifurahia maisha
Weka vijiko 4 vikubwa vya mdalasini katika vikombe 3 vya maji, koroga kwa dakika 10. kunywa robo kikombe kutwa mara 3 au 4. kwa kufanya hivyo utakuwa na afya njema.
Chunusi (pimples)
Changanya vijiko 3 vya asali pamoja na kijiko 1 cha mdalasini. Kisha pakaa kwenye chunusi, unaweza kupaka sehemu iliumwa na wadudu washa washa wenye sumu pia, rudia mara 3 hadi viuvimbe viishe
Maradhi ya ngozi (skin infection)
Fanya kama alivyoelekezwa mwenye chunusi.
Kupungua uzito
Changanya asali vijiko 2 na mdalasini kijiko 1, katika maji ya uvuguvugu. Kunywa kila siku asubuhi na usiku kabla ya kulala.
Saratani (cancer)
Tumia dozi ya asali na mdalasini kila siku kwa mwezi 1. tumia kijiko cha asalina mdalasini kutwa mara 3.
Uchovu
Sukari asilia iliyoko kwenye asali huongeza nishati mwilini, sukari hii huwasaisia wazee wachovu. Changanya nusu kijiko cha asali katika bilauri yenye maji nusu, kunywa masaa 2 baada ya kuamka, rudia tena saa 9 alasiri. Fanya hivyo kila siku
Kuvimba nyayo (sore feet)
Chua kwa mchanganyiko vuguvugu wa asali na mdalasini. Kisha osha nyayo kwa maji baridi ndipo uvae viatu.
Harufu mbaya mdomoni
Kula kijiko 1 cha mdalasini na asali ili kuondoa harufu mbaya mdomoni, asali huua backteria na kupigana na harufu mbaya
Kupungua kwa usikivu (hearing loss)
Tumia asali na mdalasini kila siku.
MBAAZI
Majani yake ni dawa kwa sikio linalotoa usaha.
Chuma majani kidogo, twanga, loanisha kwa maji safi na salama halafu kamulia ndani ya sikio matone machache, weka kutwa mara 3 kwa siku 5.
Mizizi yake – hutibu tumbo linalouma kutokana na ugonjwa wa zinaa. Chukua mizizi kiasi, changanya na mizizi ya ndulele na mizizi ya mnyonyo na mizizi ya mgegele, itwange pamoja, ishemshe ndani ya maji lita 1 kwa nusu saa. Kunywa nusu kikombe kutwa mara 3 kwa siku 5
UGONJWA WA SARATANI
Unashauriwa, kula matunda kwa wingi
Usinywe kahawa , pombe, nyama na vyakula vilivyosindikwa viwandani (ni moja ya njia za kuepuka ugonjwa huo)
Saratani zote huanzia tumboni na baadae husambaa mwili mzima. Huweza kuonekana:-
Shavuni
Kwenye kizazi
Ini
Utumbo
Damu
Mifupa
Ngozi
Njia ya haja kubwa nk
DALILI ZA MAGONJWA
Kutoa mkojo mwingi mweupe
Kukojoa mara kwa mara
Kupata kiu kali, na kunywa maji mengi
Kuchoka sana
Kukonda
Kukosa hamu ya kula
Vidole kufa ganzi
Ugonjwa wa chembe ya moyo
Majipu
Kuto-ona vizuri
Figo kutofanya kazi vizuri
VYANZO VYA UGONJWA WA MOYO
Kuna mambo mengi yanayoweza kasababisha ugonjwa wa moyo, kila mwenye ugonjwa wa moyo, ana chanzo chake kilichomfanya augue, ambacho ni tofauti na mgonjwa mwingine.
Lakini mara nyingi, watu wanaougua ugonjwa huu, ni wale ambao ugonjwa wao unasababishwa na kuongezeka kwa nguvu ya damu (hypertansion) na chembe ya moyo (coronary heart disease) moyo ukilemewa na kazi ya kusukuma damu basi huo huitwa heart failure.
Baadhi ya vyanzo vyake ni:
Kuziba mishipa ya damu (atherosclerosis)
Unene
Chembe ya moyo (coronary heart disease)
Uvutaji wa sigara
Msongo / wasiwasi (anxiety)
Kimaumbile, mishipa ndio milango ya kupitisha damu. Moyo husukuma damu na mishipa ndo njia ya damu hiyo. Moyo ukielemewa mtu anaanza kupata shida. Watu ambao mishipa yao ya damu imeziba, wana mafuta /choresterol mengi mwilini, ambayo huziba mishipa mingi ya damu.
Kitambi nacho ni dalili ya kuwa na mafuta mengi mwilini. Na mishipa yake ikiubana moyo, moyo haupati damu na hivyo hudhoofika.
Cholesterol nyingi hutokana na kula vyakula vyenye mafuta mengi na hasa yale ambayo si ya mbegu. Mfano samli na ulaji wa nyama kwa wingi.
Pombe pia inadhaniwa kuongeza cholesterol, maana hutoa nguvu (calories) sawa na vyakula vya wanga. Kwa hiyo inasababisha unene.
Sigara nayo husababisha mishipa kusinyaa. Kahawa nayo huongeza mapigo ya moyo, kwa hiyo si kinywaji kizuri.
USHAURI
Punguza rehemu / cholesterol mwilini ambayo ni kichocheo chabp. kwa kutumia asali iliyochanganywa na unga wa mdalasini kama chai, kutwa mara 3 kila siku. Pia ufanye mazoezi ya viungo. Kufunga pia husaidia kupunguza rehemu mwilini.
Mgonjwa hatapona endapo hatabali tabia ya ulaji, hata kama atatumia dawa.
DALILI ZA UGONJWA
Kuumwa kichwa (kisichosikia dawa)
Kutoona vizuri
Akili kuchanganyikiwa
Moyo kwenda mbio
Kuziba pumzi na kuchoka haraka
Kuvimba miguu
HERPESZOSTER (MOTO WA MUNGU)
Ni ugonjwa wa mishipa ya fahamu, hutokea sehemu fulani ya mwili na kutoa malengelenge, na huweza kutawanyika katika sehemu mbali mbali za mwili.
Husababishwa na aina fulani ya virus (hersper virus), kwa sehemu kubwa ugonjwa huu huathiri zaidi watu wazima, mara nyingine ugonjwa unaweza kusababisha uti wa mgongo, kuvimba matezi, saratani ya damu. Pia ugonjwa huu hupunguza kinga ya mwili.
DALILI ZAKE
Maumivu makali ambayo hutofautiana kufuata matawanyiko ya mishipa ys fahamu.
Malengelenge na baadae homa
Muwasho mkali
Malengelenge yenye majimaji, na baadae husababisha mchubuko wa ngozi.
TIBA YAKE
Kitunguu swaumu – vikatekate na umeze kwa maziwa ya moto, mara 3 kwa siku, kwa siku 10
Aloevera lotion
Paka mchanganyiko wa kitunguu swaumu na asali wakati wa kulala kwa juma 1.
Kunywa juisi ya aloe vera nusu kikombe kutwa mara 3 kwa siku 10. katakata majani 2 hadi 3 ya aloevera , weka ndani ya maji ya uvuguvugu kwa masaa 12 ndio uanze kutumia.
UNGA WA MAJANI YA MLONGE (MORINGA LEAF POWDER)
Huimarisha msukumo wa damu,
Hudhibiti glucose kwa wenye sukari,
Huondoa mashaka na wasiwasi,
Huongeza kinga na nguvu mwilini,
Hutibu kuhara na kuhara damu,
Huondoa uvimbe kwenye utumbo mwembamba, na
Huondoa vimbe nyingine mwilini,
Huongeza kasi ya utoaji mkojo,
Huondoa matatizo mbalimbali ya moyo.
Hutibu homa na kikohoza
Unga wa mlonge hutengenezwa kutokana na majani bora ya mti wa mlonge, tumia kijiko cha chai 2 mara 3, kwa wiki 3.
MBEGU ZA MLONGE (MORINGA SEEDS)
Huondoa vipele kwenye ngozi
Huondoa shinikizo la damu
Huondoa saratani ya tumbo
Huondoa homa za mara kwa mara
Hutibu maralia
Hupunguza vitambi , kwa wanawake na wanaume
Huondoa mawe kwenye kibofu cha mkojo
Huongeza nguvu za kiume na za kike
Huongeza uwezo wa kumbukumbu
Hupunguza hasira
Hupunguza tatizo la mafua
Mbegu nazo huchumwa kutoka katika mti bora wa mloge
MAFUTA YA KUPAKAA YA MLONGE
Hulainisha ngozi
Huondoa uchovu
Hutumika kwa wanawake na wanaume kujipaka
Huondoa mabaka na mibabuko
Huondoa ukurutu na magamba mwilini
Huondoa harufu mbaya sehemu za siri
Hunawirisha mwili.
MIZIZI YA MLONGE
Chukua kilo 1 ya mizizi, chemsha ndani ya lita 2 za maji, chuja vizuri. Tumia glass 1 kutwa mara 3. kwa kuimarisha afya na kinga mwilini kwa siku 10.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni