Jumamosi, 15 Desemba 2018

SEMINA YA UONGOZI

UONGOZI NA
UTUMISHI BORA
NDANI YA KANISA
Semina ya watenda kazi wa
kanisa la Mungu ulimwenguni.

            Ijue ofisi yako Namna ya kumtumikia
 Mungu kwa Ufanisi wa hali ya juu na Mafanikio!





Imesanifiwa, Kukusanywa, Kuandaliwa na
IDARA YA HUDUMA ZA WACHUNGAJI                                                    
SOUTHERN HIGHLANDS CONFERENCE






UTANGULIZI:
          Kanisa waadvetista wasabato ni kanisa ambalo limejengwa kwa mfumo wa ajabu ambao unashagaza makanisa mbalimbali namna ya utendaji wake. Kanisa hii lenye mfumo wa uwakilishi (Representatives) limejenga katika mfumo wa ktoka chini kwenda juu. Ninaposema chinimaana yake ni kanisa mahalia ambalo limeundwa na waumini waliobatizwa kuanzia 25 na kuendelea.hatimaye linafuata ngazi ya field au konferensi aambapo ni muuganiko wa makanisa yote yaliyojengwa katika eneo lililiamuliwa kuunda jimbo lao. Hatimaye linakwenda katika ngazi ya union ambayo ni muunganiko wa fild au konferensi zote zilizo katika eneo moja la nchi au kazi. Hatimaye ndipo linakwenda katika ngazi ya ulimwengu mzima general konferensi.
          Tunapotoa semina kwa watenda kazi katika kanisa mahalia zinazowahusu waumini wale ambao hawajapata mafunzo ya kichungaji. Waumini hawa wanafanya kazi ya kujitolea ndani ya kanisa kama watenda kazi wa kujitolea. Ni watu wenye shughuli za binafsi wakiwasaidi wachungaji katika kuendesha huduma za kiroho kanisani kupitia idara mbalimbali. Wachungaji wao wanafanya kazi muda wote (fulltime) na washiriki hawa wanafanya kaza kwa muda mfupi (part time). Viongozi wa kanisa mahalia(hii linajumuisha wachungaji, wazee wa kanisa, mashemasi,wahazini makarani, wakuu wa idara wote,kila mtendakazi yeyote na waumini wote kwa ujumla wasio na nyadhifa za madaraka kanisani)-hawa wote wanawajibu wa kufanya kwa ajili ya kirsto. Ndio maana tunapokotoa semina hizi tunashirikisha kanisa lote bila kuja una kazi ya uongozi ama la. Viongozi na waumini wanapoamka na kufanya wajibu wao wa kazi ndani ya kanisa na nje ya kanisa inapunguza kwa kiasi kikubwa hali ya kupoa na kurudi nyuma kwa waumini wengi.
          Ni kusundi la semina hizi kutoa kwa washiriki ujuzi na ufahamuutakaowasidia kutambua na kuzingatia kanuni za msingi zitakazosaidia wachungaji.wazee wa kanisa, mashemasi na wawakuu wa idara wote waliopewa dhamana ya uongozi wa kuleta na kulea roho hizi za thamani.pia watambue namna ya kuwaongoza katika mwelekeo sahihi na uzima wa milele.upande mmoja tunapaswa kuelewa kuwa wajibu wa kuleta na kuzuia uasi wa imani kwa waumini ama hali yao ya kuppoa SIO KWA VIONGOZI WA kanisa TU NI KWA WAUMINI WOTE. Neno linalotumika la kigiriki’laos’ ambalo tunalitumia kama “laity” yaani walei haimanishi kundi la pili la watubali linamaanisha watu wote (crowdsor or all people) likijumuisha na mchungaji. Hivyo tunaposema ‘loas’ maana yake watu wote na mchungaji akiwemo naye ni mlei.katika kitabu cha minister manual (1997), uk.121 ikisema;
          “Neno hilo tunalitumia vibaya kabisa wakati tunapolitumia kuelezea kama wasaidizi au wanaosaidia huduma. Tunalitumia kwa usahihi wakati tunapomanisha watendakazi wenza katika huduma(associatedin ministery). Mama white anasema hivi: “wajibu wa kupeleka ujumbe mbele kwa ajlili ya kukamilisha utume huu hawakuwekewatu kwa wachungaji waliowekewa mikono. Kila mmoja ambaye amempokea kristo anaitwa kufanya kazi kwa ajili ya wokovu wa wanadau wenzao.”- Acts of APpostles, uk.110.
          Hivyo ni kusundi la semina hizi kuamsha roho ya utendaji waidara zote ndani ya kanisa kutekeleza utume mkuu wa kanisala waadventista wasabato la UFUNUO 14:6- 12; MATHAYO 28:19, 20. Kila idara iliyopo kanisani ipo kwa kusudi moja tu kutekeleza utume wetu ndani ya kanisa. Hivyo wakuu wetu wa idara wanaweza wakashidwa kutekeleza utume wao kwa kushib\ndwa kuelewa majukumu yao wakarithi mazoezi kutoka kwa viongozi waliopokea kazi ambao nao hawakupata semina hizi. Ni makusudi ya kitabu hiki kitumiwe kwenye mikutano mbalimbali ya kanisa katika kutoa semina ili kuwasaidia wachungaji ambao wanawajibu mzito wa kuangalia shughuli zote ndani ya kanisa. Wazee wa kanisa au wainjilisti walioteuliwa watakuwa na uwezo wa kuelimisha waumini wa kushiriki katika huduma za kanisa katika idara mbalimbali. Uongozi wa kanisa mahalia unapolenga shughuli zake katika mabo mengine yasiyohusu uinjilisiti kanisa hilo linahesabika limekufa (mfu). Ni wajibu wa kila kiongozi kuliingiza kanisani kazini. Mwongozo wa mzee unasema,
          “madhehebu yote yanaukubali kwa kiasi Fulani wajibu huu. lakini waadvetista waasabato wanasimama peke yao katika kusikia kuwajibikia kupeleka ujumbe wa malaika watatu. “kwa kila taifa, kabila, lugha na jamaa” (ufunuo)  14:6)….. kanisa mahalia lolote lile linalolenga katika shughuli mahalia tu litapoteza njozi ya pekee ya kanisa  la waadvetista wasabato kiulimwengu.”
          Hapa chini ninaanza na semina ya uongozi ambayo ilitolewa kwa ajili ya idara ya vijana. Kitini hiki mtuzi wake sikumbuki ni nani aliyekiandaa lakini kinafaa kwa ajili ya kupata mambo ambayo yatakusaidia katika uongoziwako. Kimetumika kwa idara ya vijana lakini ukweli usiopigika kiongozi bora ni Yule aliye na uwezo kuongoza vijana na kukubalika ili kuwa watu wakiroho. Ikiwa uongozi wako utafanikiwa kuwapata vijana ndani ya kanisa wakatulia na kumtumikia kuwa kiongozi kwa asilimia 90 ya uongozi wako basi umefanikiwa kuwa kiongozi bora wakuliongoza kanisa la Mungu katika ushidi wa milezi ya kiroho. Kwani kanisa hili linaundwa na vijana kwa takirabani asililimia 80 ni vijana wa rika mbalimbali kitini hiki kimekinakili kama kilivyo nikaanza vipengele vichache na kuerebisha mambo machache sana lakini ni kwa makusundi mema ya kuwapa semina fupi viongozi na washiriki wapate kuelewa pointi za misingi katika swala la uongozi wa kanisa la ungu.
          Kitabu hiki hakijamaliza idara zote ndani ya kanisa. Nimeacha kukamilisha wakati wakati wa toleo la pili litajumuisha idara mbalimbali kama vile usikivu,uchapaji na kadhalika. Pia ntafanya marekebisho zaidi kwa ajili ya mabadiliko yanayotokea kutokana na semina zinazokuja kutoka ngazi za juu. Ni muhimu kwenda na wakati na mabadiliko yanpotokea.                                                                                            


1.    UONGOZI3

 

         Wale wanaochanguliwa kuwa viongozi wa vijana, au viongozi wa aina yeyote ile, wanatakiwa kujifunza uongozi ili wawaongoze vizuri wale wanaowaongoza. Bila kujifuza uongozi, haiwezekani kuongoza watu vizuri. Mbinu za uongozi hubadilika mara kwa mara kutokana na jamii kubadilika mara kwa mara. Jamii hubandilika kutokana na kuongezeka kwa maarifa katika jamii. Kubadilika kwa mtazamo wa jamii. Yale ambayo jamii iliyafikilia kuwa ni adili, inaweza kugeuka na kuyaona kuwa si adili. Mfano, Ukomunisti ulifikiliwa kuwa ni mfumo bora sana, lakini sasa, mtazamo huo umebadilika.  Elimu na mtazamo inapobadilika, uongozi nao lazima ubadilishe namna ya kuongoza jamii hiyo.

          Wale waliokuwa viongozi wazuri sana miaka 40 iliyopita, wakiongoza leo kwa kutumia mbinu za enzi zao, watajikuta wameshindwa kufanikisha kitu chochote kile. Hivyo mbinu za uongozi zinabadilika badilika mara kwa mara.

Umuhimu wa somo la uongozi kwa viongozi wa vijana.
          Somo la uongozi ni la muhimu sana kwa vijana kwani vijna, wanatakiwa waelekezwe juu ya mambo mengi maana hawana uzoefu unaotokana na kuishi siku nyingi na kuona mambo mengi. Vijana maelekezo juu ya:
                     
1.    Urafiki ulio mzuri na aina ya marafiki wazuri.
2.    Masomo ya kuchukua yatakayomsaidia katika maisha yake.
3.    Maisha ya ujana na ndoa
4.    Mwonekano bora
5.    Maburudisho yanayofaa
6.    Namna ya kudumisha Kristo
7.    Namna ya kumtumikia Mungu
8.    Mmambo mengine mengi ya maisha
Vijana wanahitaji kuelekezwa kwanini hawajawa na mda mrefu hapa duniania, hivyo wanahitaji kujua maana ya mambo mengi iliwasifanye uchanguzi mbaya wa mambo Fulani Fulani na kujiletea hasara kubwa katika maisha haya yajayo. Vijana wanaweza kufanya utafiti  juu ya mambo.
Unknown; Kitini cha Uongozi kwa ajili ya Idara ya Vijana. Semina kwa ajili ya idara ya vijana uk. 1-19.
Fulani Fulani ili kuja ubora wake. Kufanya utafiti ni jambo zuri sana, lakini kufanya utafiti kwa jambo ambalo limeshafanyiwa utafiti na matokeo yake yakapatikana ni kupoteza muda. Ni vema kupata matokeo ya utafiti uliopita ili ufanye uchanguzi mwema kuliko kupoteza mda kufanya utafiti wa jambo ambalo lina majibu yake. Hivyo, kusikiliza kutokana kwa walio na uzoefu wa mambo ni muhimu sana kwa vijana. Lazima wajulishwe umuhimu wa kutafuta kujua maana ya mambo toka kwa wenye uzoefu.

          Jambo la pili la muhimu kuzingatia ni kuwa, yawapasa viongozi wawe na majibu ya maswali ya vijana wanaowaongoza, kwani wasipokuwa na majibu ya maswali ya vijana wanaowaongoza, kwani wasipokuwa na majibu ya kuwapa, wanaweza kutafuta majibu kwenye vyazo vingine vinavyopoteza. Viongozi wasiowapatia vijana maeleakezo katika maisha yao, wanaweza kutafuta majibu kutoka kwenye vyanzo vifuatavy:-

1.    Marafiki zao –wasio kama wao.
2.    Redio
3.    Television
4.    Magazeti na vitabu
5.    Mtandao  (Internet)
6.    Kompyuta na vyanzo vingine visivyo na maadili mazuri.
                Kiongozi wa vijana lazima ajisikie kuwa amepewa dhamana ya kuwaadhibisha vijana katika mambo mema ili wawe watu wazuri, wasipotee. Hivyo kazi ya kuongoza vijana ni kubwa sana kuliko wengi wanavyodhani, maana, ni kazi ya kumjenga kijana tabia yake atakayoishi nayo maisha yake yote na kumwezesha kuingia mbinguni.

                     Msingi wa uongozi bora.
            Msingi wa uongozi bora ni Tabia bora ya kiongozi.Kiongozi huwavuta watu wamfuate kwa upendo na hiari yao wenyewe kama kiongozi huyo ana tabia inayokubalika na anaowaongoza. Kama tabia yako haikubaliki, huwezi kuwaongoza watu, hata kama unawaambia maneno ya msingi kiasi gani,. Unapochanguliwa kushika nafasi Fulani Kanisani, au mahali popote pale, unapewa madaraka (authority). Madaraka hayatoshi kukufanya uongoze watu usiokuwa MVUTO wao unowafanya wakufuate (power) na mvuto huo, unategemea tabia yako.

          Uongozi ni nini? Jibu la swali hilo ni kuwa, uongozi ni Mvuto. Kiongozi anakuwa na mvuto kama ana tabia inayokubalika na anawaongoza. Mtu mwenye tabia mbaya anaweza kuwaongoza watu wakafanya mambo mabaya kama atawashawishi waipende tabia yake hiyo mbaya, kutengemea msingi w tab walio nao. Wasipoipenda tabia yake, watamkimbia.

          Swali kubwa na la pekee kwa viongozi kujiuliza ni kuwa: Je! “TABIA yangu inakubalika na inawaongoza” Kanisa linatakiwa kuchangua viongozi wenye tabia nzuri ili wawaongoze vijana na watu wengine katika mambo mazuri yanayowajenga  katika mambo ya hapa duniania na ya Mbinguni. Na ikubukwe kuwa, kiongozi asiye na tabia nzuri, anaweza kufanya anaowaongoza waipende tabia yake mbaya, hiyo wao nao kuharibika katika maisha yao ya kuwa watu wenye tabia hiyo mbaya.  

          Ni rahisi sana kupima  tabia ya kiongozi. Haihitaji mtu kwenda shule au kuwa na umri mkubwa ili aweze kupima tabia ya kiongozi. Wasomi wasio wasomi , watoto na watu wazima, wanaweza kupima tabia ya kiongozi na kuielewa bayana tena kwa muda mfupi.

          Maneno machache anayoyasema mtu kwa mda mfupi yanaonyesha tabia yake kama ni njema ( nzuri) au la. Tabia ya mtu si ile ambayo watu huisema akiwepo bali ni ile wanayoisema wakati mhusika hayupo. Kufaa kwa uongozi wako si kule kunakosemwa wakati ukiwepo bali ni kule kunakosemwa wakati haupo. Haihitaji kupewa elimu ya shule kupima tabia ya mtu, tunapima tabia ya mtu kwa kutumia utambuzi wa asili ( common sense) ambapo upo kwa kila mtu mkubwa na mdogo.

          Kiongozi anatakiwa awe na tabia njema inayokubalika na Mungu anawaongoza.Yesu alimpendeza “Mungu na wanadamu” (Luka 2:52). Usiseme kuwa wewe hutajali chochote mradi unasema ukweli hata kama watu watachukia. Unaweza ukasema ukweli lakini ukasema kwa namna ya kuwatweza, kuwafedhehesha au kuwadharau wale unaowaeleza ukweli huo, hivyo ukweli wako ukakataliwa na watu.

              Upendo kwa unaowaongoza.
Ø Kiongozi anatakiwa kuwapenda wote anaowaongoza ndipo atakapofanya kazi yake kwa mafanikio makubwa. Upendo ni kichocheo cha kufanyakazi kubwa. Kiongozi aonyeshe upendo kwa wote.
Ø Kutompenda kijana hata mmoja aliye mdogo, kutaleta madhara kwa kundi zima.Hali ya kutopendwa ya mtoto mdogo itakuwa moto utakaoenea kwenye kundi lote.
Ø Fungu linaloeleweka sana duniani linasema: “Kwa maana jinsi hii Mungu aliupenda ulimwengu, hata akamtoa mwana wake wa pekee,ili kila mtu amwaminiye asipotee, bali awe na uzima wa milele” (Yoh. 3:16.  Ili kumkomboa mwenye dhabi, Mungu alianza na kumpenda upeo (yoh. 13:1). Akafa kwa ajili ya kumkomboa.
Ø Ili kuwaongoza vijana, inatupasa kuwapenda sana.Vijana wasipoona upendo wowote ndani yetu, hatuwezi kuwaongoza. Watakuwa wanafiki kwetu. Upendo wa kiongozi kwa anaowaongoza, unamfanya anayeongozwa ajitoe zaidi kwa kiongozi  wake.Kadri kiongozi anavyowapenda anaowaongoza, ndivyo inavyokuwa rahisi kwake kuwaongoza. Hivyo, UPENDO KWA UNAOWAONGOZA UNARAHISISHA UONGOZI. Wanaoongozwa wanajitoa kufanya lolote lile kama wanaojua kuwa kiongozi wao anawapenda.
Ø Kinachotangulia ni kiongozi kuwapenda anaowaongoza ndipo wao nao watampenda na kufanya yote anayowaeleza hata kiasi cha kufa naye Mbeba silaha wa mfalme sauli alipomwona amejiua, alijiua pia, maana alimpenda sana. Viongozi wanaopendwa sana wanapokufa, baadhi ya wanaowaongoza hufa pia kwa kukata tama. Tunatakiwa kuwapenda sana wavumbuzi, Watafuta njia, Mbolezi, Wanafunzi  vijana wakubwa, nao watatupenda na itakuwa rahisi kuwaongoza.
Ø Ukiwapenda unaowaongoza: Unawagusa mioyo yao kabla hujawaomba uwanguse mikono. (Touch the heart before you ask for a hand). Kila kiongozi anatakiwa kujifunza uongozi kabla hajaanza kuongoza vijana, ili asifanye makosa katika uongozi wake, na kuwafanya viongozi wachukue vyama vyetu. Anatakiwa aendelee  kujifunza uongozi  siku baada ya siku, kwani jamiii inabadilika, hivyo mbinu zinabadilika pia. Kiongozi ajaribu kuhusianisha mambo anayojifunza na kundi la watu anaowafundisha. Kiongozi anatakiwa kujifunza aina za watu anaowaongoza vizuri.

AINA ZA WATU
Zifatazo ni aina za watu:-
1.    Blockers (Wapingaji)Wanaopiga kila kitu. Wanasaidia viongozi kujua mahali wanapohitaji kurekebisha. Hawa ni wapizani kutokana na malezi walivyoyapata awali, wakisaidiwa watageuka na kuwa wazuri.
2.    Recognition seeker [ wanaotafuta kutambulika] – Wale wanaotafuta kufahamika kwa wengine, wataongea ili wafahamike. Ubinafsi ndio unaowavuta kutaka kufahamika. Wakisaidiwa wataacha ubinafsi katika maisha yao.
3.    Non participants [Bora Twende au wasiojihusisha]- Wale wasiotaka kujihusisha na mambo ya kikundi. Hawa mzingo wa mafanikio ya kikundi chao au ni waoga kwani hawakufundishwa kuwa jasiri.Wasaidiwe waondoe woga wao kwa kuobwa kutoa jibu fupi la “ndio” au “la” kwanza baadaye wazoeshwe kutoa majibu mafupi. Watakuwa jasiri baada ya muda mfupi.
4.    Fighters [ washambuliaji} – Wale wanaoshambulia viongozi. Hawa wanaweza kuwa wameingia hali ya kushambuliana toka kwa wazazi wao. Zaidi ya hayo, wivu unaweza kuwasukuma kuwashambulia viongozi wao au wenzao. Hulaumu kila kitu bila ya kuwa na jia nzuri ya kufanyawasaindiwe kujua malengo ya chama kuwa ni kujenga wale si kulaumu.
5.    Dorminators[ wanaohodhi] –wale wanaotafuta kutawala kikundi katika maongezi au utoaji maamuzi. Hujaribu kuwasaidia viongozi hujionyesha kuwa ni watu wa hali ya juu kuliko wengine Wasaidiwe kuheshimu mawazo ya watu wengine na waondoe ubinafsi.
6.    Gossipers [Wasengenyaji] – Wasengenyaji huongea juu ya watu wakati hawapo. Waweka sumu kwenye kundi na kuharibu. Huondoa upendo na amani kati ya watu. Wasaidiwe waache kusema watu. Wafundishwe kuwa, kama una neno na mtu, ni vyema kwenda kumwona kuliko kumsengenya, Mungu anatutaka tuwapende wenzentu kama nafsi zetu.
7.    Humble and supportive [wanyenyekevu na Mtegemezaji [watia shime] Wale walio wa kweli na wanaojitahidi kuona kuwa kundi lao linaendelea. Hawa walipata msingi bora wa malezi toka kwa wazazi au wazi wao. Wasaidiwe ili kuiga tabia tabia mbaya ya kundi.

Aina za uongozi
1.    Authoritative [wenye mamlaka] – Uongozi unaokuwa na mamlaka kamili.
A.   Uongozi huu unasikiliza watu wake wanayosema lakini, unasimamia utekelezaji wa mambo karibu yote yaliyopendekezwa na watu.
B.   Uongozi huu una njozi na kutoa mwelekeo nini kinchotakiwa kifanyike.
C.   Uongozi huu unafanya maamuzi wenyewe kwa kupata mashauri ya watu wachache tu au bila kupata kitu chochote  kutoka mahali popote au kutoshirikisha kundi lote.
D.   Uongozi huu unapenda kunukuu mambo ya viongozi wa kale katika kuongoza.
E.    Uongozi huu unaweka tofauti ya uongozi na wafuasi wao. Kiongozi anajulika.
F.    Uongozi huu unaamini kuwa wafuasi wao au kunndi analoliongoza linahitaji  usimamizi wa moja kwa moja.
G.   Uongonzi huu unaonekana ni mgumu sana kukubali kuhama kutoka kwenye mamlaka yake kwenda kwenye demokrasia. Kwani ni rahisi demokrasia kuhamia kwenye aina hii ya uongozi wa wenye mamlaka.
H.   Uongozi huu unabeba madaraka yote na kuwachukua kundi sehemu kidogo tu.

2.    Democratic – [ Demokrasia] Uongozi wa kidemokrasia ni uongozi wa kufanya maamuzi wote kwaajili ya wote. Katika uongozi wa aina hii.
A.   Maamuzi hufanya na watu wote.
B.   Utekelezaji wa mambo huwa mzur maana mapendekezo yanakubalika na wote.
C.   Uamuzi hufikiwa baada ya muda mrefe kwa kusubili kuafikiana, hivyo kuna upotezaji wa muda katika ufikia maamuzi.
D.   Utekelezaji  huwa wa mambo ambayo wote wanayakubali na kuyapenda.

3.    Laizzer faire [ holela au bora Twende] – Uongozi usio na msimamo sera maalumu katika utendaji wake wa kazi. Katika uongozi wa aina hii:-
A.   Uongozi haufanyi chochote.
B.   Watu hufanya wanayotaka wao wenyewe.
C.   Hakuna maendeleo ya jamii iliyo na uongozi wa aina hii.
D.   Uongozi hauna dira au hauna mwelekeo wowote ule.

4.    Domineering- [ukandamizaji] uongozi unaoshughulikia vitu vyote wenyewe, katika aina hii ya uongozi, uongozi unajua yote, unatoa sera na maelekezo yote.

Uongozi wa aina hii:-
A.   Unawanyika watu nafasi ya kutoa mawazo kuhusu mambo ya kufanya.
B.   Unafanya utekelezaji wa mambo ufanyike haraka maana hausubiri ukubali wa kila mmoja au wawakilishi wa watu.
C.   Kama uongozi ameamua kufanya mambo mazuri, kikundi kitanufaika  maana utekelezaji wa maamuzi ya uongozi huu hufanywa haraka.
D.   Kama uamuzi wa uongozi ni wa makosa, kikundi kitapata hasara kwa kufanya mambo yasiyokisaindia.
E.    Aina hii ya uongozi ni nzur wakati wa hadharu tu. Kama jingo moto, haihitjia  kukakaa kikao ili muamue kukodi kampuni ipi ya zima moto maana kusubili make kikao kunazidi kufanya madhara yaongezeke.
Hakuna aina ya uongozi ulio bora. Kiongozi mzuri ni Yule anayetumia aina zote za uongozi kwa wakati unotakiwa.

                             Uongozi mashuleni
                             Uongozi una changamoto kubwa mashuleni kwani:

1.    Unaogoza watu wa rika tofauti – wanafunzi wa miaka kumi na, hadi ishirini, walimu pamoja na wafanyakazi wazoefu na wachanga.
2.    Lazima namna ya kuongoza marika yote – wanafunzi wa miaka kumi na; hai ishirini na, walimu na wafanyakazi wazoefu na wachanga.
3.    Elewa mabadiliko ya vijana na mahitaji ya kila rika.
4.    Elewa wanapenda na kutopenda nini.
5.    Elewa namna wanavyojifunza ili utumie mbinu hizo kuwafundishia.
6.     Elewa mtazamo wao kuhusu watu wazima wanawafundisha wanatabia gani.
7.    Elewa vitu vinavyowaangusha.
8.    Waelewe watu wazima wanaowafundisha wanatabia gani.
9.    Elewa namna ya kuwasaidia wanaowafundisha ili wasiwaadhiri vijana.
10.Elewa nafsi iliyo kati ya vijana na walimu wao; ili uwlete karibu.
11. Elewa namna ya kupatanisha watu.
12.Elewa umuhimu wa kutunza siri za vijana ili wakueleza shida zao uwasaidie.
13.Elewa namna ya kuwasaidia waelewe malengo makuu katika maisha yao.
14.Elewa namna ya kushughulika na “mob psychology”
15.Elewa namna ya kuhusiana na viongozi wengine.
Hivyo, kiongozi wa shuleni anatakiwa awe na uzoefu mkubwa  na kiongozi wa kiroho shuleni anahitaji elimu zaidi ya uchungaji.Si kila mchungaji anaweza kuwa chaplain maana kazi ya chaplain inahitaji elimu ya ziada

Mahusiano:
Hapo awli tulisema kuwa, MVUTO ni kitu cha muhimu sana kwa kiongozi na kiongozi yapasa awe na tabia inayokubalika na kuwaongoza. Mema na anawaomgoza. Hivyo uongozi unahusisha mahusiano na wala huwezi kuutenga uongozi na mahusiano.

Viongozi wanajihusisha na matatizo ya watu, wanakubalika sana na watu wanawaongoza,kwani kujihusha na matatizo ya watu kunaonyesha  UPENDO.wako kwa watu.
1.    Kiongozi anaweza kuwavutia [ impress}watu akiwa mbali, yaani akiwa hahusiani nao kwa karibu. Kiongozi anatakiwa kuwa karibu na watu anaowaongoza.
2.    Kiongozi anaweza kuwashawishi [influency] watu akiwa karibu kidogo nao. Kiongozi hatakiwi kuwa karibu kidogo na watu, awe karibu nao zaidi. Uongozi usikufanye ujitenge na watu. Kiongozi anayekaa mbali na watu hufanya hivyo kwa kudhani kuwa yeye ni wa maana zaidi ya watu wanaowaongoza. Kuwa kiongozi hakumanishi kuwa wewe ni wa maana kuliko unaowaongoza. Inabidi mmoja wawe kiongozi na si wote.
Yesu alichangamana na watu wa aina zote, matajiri [zakayo] kwa masikini [ Martha, mariamu na zakayo]. Yesu alichangamana na wenye dhambi [watoza ushuru]. Kiongozi hakuitwa kuhudumia watu  wachache bali wote, hivyo anatakiwa kuchangamana na wote. Kiongozi lazima aelewe mahitaji ya wale anaowaongozi.

Umoja katika kazi (team work)
Umoja ni wa muhimu sana katika jamii yeyote ile. Bila umoja hakuna kitu chema kinachoweza kufanywa na jamii. Pakiwepo na umoja, mafanikio makubwa yatapatikana kwa jamii. Hata wenye nguvu, huogopa watu dhaifu wakiwa na umoja

Unawezaje  kulifanya kundi lisilo na umoja likawa timu yenye umoja?jiulize maswali yafuatayo:
1.    Je, ninawajenga watu au ninajenga himaya yangu kwa kutumia watu?
2.    Je, ninajali kutoa changamoto kwa watu kama patakuwa na tofauti baada ya kuwapa changamoto hiyo?
3.    Je, ninawasikiliza ninawaongoza zaidi ya kuwasikiliza kwa masikio [kuwasikiliza kwa masikio matatu,  yaani masikio mwili na moyo pia]. Ukiwasikiliza, unaweza kupata majibu ya matatizo yanayoondoa umoja kazini.
4.    Je, ninauliza maswali sahihi ili kujenga uhusiano sahihi?
5.    Je, ni mambo yapi ya msingi aliyonayo kila kila mmoja wa wanakikundi?.
6.    Je, kazi zao ninazipa uzito unaostahili?
7.    Je, nimewaonyesha thawabu watakayoipa kutokana na kazi zao/ watu wanaweza kuvumilia yote ya sas, kama kuna matazamio ya kupata mema baadaye.
8.    Malengo yao yanapatana na yangu? Watu husema: “UMOJANI NGUVU” Shetani hataki kuona kuna umoja katika vikundi vya vijana. Tujitahidi tumshinde Kwa kuwa na umoja.

Kiongozi na njozi
Kila kiongozi anatakiwa kuwa na njozi, la sivyo, hatafanya kitu chochote kwenye uongozi wake. Wengi wanaongoza bila ya kuwa na lengo la kufikisha kundi analoliongoza mahali Fulani bora zaidi . baada ya uongozi wao, hawaachi kitu chochote kinachokumbukwa, [legacy]. Katika njozi ya kiongozi:
1.    Anatakiwa kuhakikisha kuwa njozi yake inatimia, [asikatishwe tama na chochote].
2.    Kiongozi anatakiwa kuieleza njozi yake ili watu waijue, waiepende , waiunge mkono.
3.    Kitu kikubwa kwa kiongozi mwenye njozi ni mawasiliano awasiliane vizuri ili aeleweke. Hivyo, kiongozi awasiliane, na kuwasiliana.

A.   Mifano ya viongozi wenye njozi katika jamii

Wafuatao hapa chini ni viongozi wenye na watu aliokuwa na njozi na watafanikiwa kufikia njozi walizojiwekea.

1.    Abraham Linchon
Mmarekani mweupe. Alizaliwa marekani 1809 na kufa 1865. Alikuwa rais wa marekani mwaka 1861. Alipigania kukomeshwa kwa watumwa.aliandikia waraka wa kuachiria huru watumwa 3,120,000 huko marekani, ila alipingwa sana. Alifanikiwa kuondoa utumwa kabisa mwaka 1865.

Aliuawa na john wilkes  april 14,1865, kutokana na sera yake ya kuheshimu binadamu wote. Mara nyingi, viongozi wazuri wamekuwa wakiuawa na maadui wasiopenda haki. Wengi wa viongozi wazuri hawakutawala muda mrefu, wala hawakuishi maisha marefu. Shetani hapendi wenye haki watawale maana watawasaindia binadamu nay eye anataka watu wawe na shida na taabu daima.
Kama utaongonza kwa kufuata haki yote na kuona kunapta upinzani,usife moyo. Nyuma ya upinzani huo kuna shetani anayeuongoza, lakini mbele yako, kuna yesu anaye kutangulia. Usihofu kwa lolote litakalo kupata. Tazama huyo ibilisi atawatupa gerezani, nanyi mtakuwa na dhiki siku chache, msife moyo. Omba sana uhakikishe unaongoza vizuri na matokeo umwachie Mungu.

               2. Martin luther king. Jr.

Alizaliwa marekani jan,151929, na kufariki april 4, 1968. Alikuwa president wa jimbo la kanisa la Baptist. Alikuwa mmarekani mweusi aliyekuwa na njozi ya kuondoa ubaguzi wa rangi kwa amani nchini marekani. Hotuba yake mashuhuri sana  na ila yeye maneno: “I have a dream”. Aliyoitoa Washington D.C August 1963 baada ya maandamano ya watu 3000,000/= ya kupinga ubaguzi wa rangi.
          Japo utumwaulitoweshwa na Araham Lincoln, lakini ubaguzi wa rangi ulikuwa bado unaendelea kwa kiwango kikubwa. Watu weusi walikuwa wakibaguliwa hivyo:
a)    Hawakutakiwa kusoma pamoja na wazungu, na shule zao zilikuwa duni, za wazungu zilikuwa nzuri sana.
b)    Hawakutakiwa kusafiri kwenye gari moja pamoja na wazungu.
c)    Hawakutakiwa kusubili basi kwenye chumba kimoja cha kusubiria basi na wazungu.
d)    Hawakutakiwa kuingia kwenye hoteli ya wazungu
e)    Hawakupewa kazi kubwa serikali, na mambo mengine mengi.
f)     Vuguvugu la kuondoa ubaguzi lilifanikiwa kwani serikali ilipitisha sheri ya kutowabagua watu weusi, hata hivyo, si wote walioifurahia sheria hiyo.
Martin luther king. Jr. aliuwa na mzungu ambaye hakufurahishwa na vuguvugu lake la kupigania haki. Kabla ya kuuwawa kwake, palikuwepo na jaribio jingine la kumuua, alichomwa kisu ila hakufa. Alitambua wazi kuwa kuna siku aliuawa. Aliandaa hotuba na kuirekodi kwenye kanda, itakayotolewa kwenye ibada ya mazishi yake, hotuba iliyosikitisha watu wengi.
    Hali njema ya kutobaguliwa iliyoko leo marekani, inatokana na vuguvugu lililoendeshwa na martin  luther king, jr. ambaye aliuawa wala hakuishi aone hali njema waliyoipata watu weusi.

3. Nelson Rolihlahla Mandela
    Alizaliwa 1918, afrika ya kusini. Alisoma shahada ya kwanza kwenye chuo kikuu kimoja lakini hakumaliza, alifukuzwa kwa kujihusishwa na vuguvugu la kisiasa. Alimaliza shahada ya kwanza kwenye chuo kikuu kimoja lakini hakumaliza, alifukuzwa kwa kujihusisha na vuguvugu la kisiasa. Alimaliza shahada yake  nyumbani. Alichukua shahaha ya pili ya sheria. Alijihusisha na chama cha African national congress na 1962 alifungwa kwa kujihusisha na upingaji ubaguzi na kutoka nje ya nchini bila  ruhusu maalum.
    Mwaka 1964 kifung chake kilibadilishwa na kuwa cha maisha. Akiwa gerezani, mkewake Winnie mandele alijihusisha kama kiongozi wa chama na kuendeleza upigaji ubaguzi. Alipata tuzo ya amani ya Nobel 1993. Mwaka 1990, F. W. de Clrk, kiongozi wa wakati huo waafrika kusini, alimtoa gerezani maana, vuguvugu la kupiga ubaguzi liliendelea sana.
    Wazungu walipaga kumununua Mandela kwa kumpanyumba nzuri iliyojengwa mahali walioishi wazungu na gari la thamani kubwa na kuombwa aache mambo  ya siasa afurahie maisha maisha kwa kuhudumiwa na serikali ya wazungu. Baada ya kukabidhiwa vyote hivyo, aliviacha vyote na kuondoka kwenda Soweto kwa miguu. Akaenda kuishhi na wafrika maskini kule Soweto.
          Alikuwa rais wa kwanza mweusi wa afrika kusini mwaka 1994 hadi 1999, ubaguzi wa rangi ukaisha afrika ya kusini. Hakupenda 
kung’ang’ania madaraka bali alistafu baada ya kufanya kazi miaka mitano tu. Ni kiongozi anayeheshimiwa Sana duniani.

4. Julius kambrage Nyerere [1992- 1998]
Njozi yake ilikuwa kuleta maisha sawa kwa wote na kukomboa nchi zote za kiafrika toka ukoloni na kuleta mwungano wan chi za kiafrika alifanikisha kusaidia kuleta ukombozi kwa nchi za mozambiki, nambia, zimbambwe na nchi zingine za kiafrika. Alishiriki kuanzisha umoja wan chi za afrika ya mashariki. Alisaidia kuleta muungano wa Tanganyika na   zanzibri.
          Aliwaunganisha watanzania na kuwa wamoja asiobaguana  wakati kuna mabila 120 hivi.
          
            5. mahatma Gandhi.
Jina halisi ni mohandua karamchand Gandhi. Alizaliwa oktoba 2, 1869 na aliuawa January 30, 1947, njozi yake ilikuwa  uondoa ubaguzi na kuleta uhuru. Aliendesha vuguvugu la amani kama la luther. Alisomea sheria huko londn.
          Alifanya kazi kama mwanasheria wa kampuni huko afrika ya kusini kwa miaka 20. Alifungwa mara kadhaa huko afrika kusini kwa kupiga ubaguzi wa rangi, wahindi walibanguliwa pia huko afrika kusini.
          Alirudi india na kujiunga na vuguvugu la kudai uhuru toka kwa waingereza.india ilikuwa na vyama viwili vilivyokuwa vikidai uhuru,cha waislamu na cha wahindu. Chake kilikuwa cha wahindu. Alipigania muungano wa india na uhuru ukapatikana 1946. Makundi ya wahindu na waislamu hayakuridhika sana. Alifanya sala za kufunga ili umoja upatikane. Aliuwa na nathuram godse, mhindu mwenye siasa kali January 30, 1947, mwaka mmoja tu baada ya kuleta uhuru wa india.

                 6. Mama Teresa
          Alizaliwa huko Albania 1910 na kufariki 1997. Alijiunga kazi ya usister ya kanisa la roman catholic akiwa na miaka 18. Alipokuwa Calcutta, kama mkuu wa shule, aliguswa sana na wagonjwa na watu waliokuwa wakifa mitaani. Njozi yake ikawa kusaidia wagonjwa na maskini.
          Aliomba kuacha kazi ya ukuu wa ssshule na kuazisha shirika la kusaidia wagonjwa na maskini huko Calcutta. Kazi yake iliendelea vizuri, akafungua vituo vingine duniani. Mwaka 1979 alipewa tuzo ya nobel kwa kazi zake za kusaidia watu. Alifarikia mwaka 1997.

              7. kwame Nkrumah
Alizaliwa Ghana 1909 na kufariki 1972. Alikuwa mwafrika wa kwanza kuleta uhuru kwenye nchi ya kiafrika, dhana , mwaka 1957, na kuwa waziri mkuu 1957 -1960, na rais 1960- 1966 aliponduliwa. Aliishi uhamishoni guinea na kufanywa rais mwenza wa rais wa nchi hiyo sekou toure. Ni umoja na upendo kiasi waliokuwa nao watu hawa.
          Aliugua saratani ya koo na kufia hospitalini  Rumania mwaka 1972 na kurudishwa na kuzikwa kijijini kwake nchini Ghana. Alisimamia uazishwaji wa OAU, maana yake ilikuwa kuifanya afrika iwe taifa moja.

                  8. John Fitzgerald kennedy

          Alizaliwa 1917 na kufariki 1963. Alikuwa rais wa marekani mwaka 1960-1963. Njozi yake ilikuwa kutetea watu wa hali ya chini, aliongeza kima cha chini cha mishahara.
          Alianzisha shirika la kusaidia nchi zinazoendelea kwa upande wa elimu, kilimo na afya, ili kujenga urafiki wa nchi hizo. Alipata upinzani mkubwa alipotumia nguvu zake zote kukataza kiwanda cha chuma kisipandishe bei ya bidhaa zake. Alitetea usawa kati aya wamarekani weupe na weusi.
                    13. kati ya hotuba zake zinazokumbukwa sana ni ile aliposema:
usiulize kuwa nchi yako itakufanyia nini, lakini jiulize kuwa utaifanyia nini nchi yako”. Aliuawa na oswald 1963.

A.   Mifano ya viongozi wa kiroho wenye njozi:
1.    Musa –alifanya kazi kubwa ya kuwakomboa wana wa Israeli toka utumwa wa misri na kuwaongoza kwenda kaanani.
2.    Martin luther- aliongoza matengenzo ya kurudisha kanisa kwenye neno la mungu wakati wa zama za giza.
3.    Elleni G. White – alisaidia uazishwaji wa misheni mbalimbali duniani.
4.    Fares muganda- alisaidia uimarishaji wa unjilisti  katika Tanzania.
5.    Harry fenner na luther warren- walisaidia uazishwaji wa vyma vya vijana.
  Viongozi wote wa vijana wanatakiwa kuwa na njozi na wafurahie kuona  wanaacha vitu Fulani walivyoviazisha vikendelea kusaidia watu kwa muda mrefu. Kiongozi anatakiwa kujali matokeo mema ya kikundi anachokiongoza [result oriented]. Kiongozi lazima ajitahidi kuleta mabadiliko mema katika kikundi chake [ change oriented].
Usikubali kuongoza kikundi na kukiacha palepale ulikokikuta; utakuwa ‘mlinzi’. Na si kiongozi – kama aliyepewa talanta moja.

          Kutayarisha viongozi
Swala la kiongozi kutayarisha viongozi watakaoongoza pamoja au baada yake kuondoka kwenya uongozi ni wa  muhimu sana. Kiongozi anayetayarisha viongozi ni wa muhimu sana kuliko anayeongoza vizuri. Anayetayarisha viongozi, anazalisha viongozi, si mchoyo, anatakiwa awe nyota yeye pekee yake, ana ubinafsi.
Kuna tofauti kati ya kiongozi, anayejikusanyia wafuasi, na kiongozi, anayeandaa viongozi:
1.    Anayekusanya wafuasi, na kiongozi, anayeandaa viongozi, anahitajika [yaani kuogoza] warithi wake.
2.    Anayekusanya wafuasi, huagalia zaidi udhaifu wao [weaknesses].wakati anayeandaa viongozi, huangalia zaidi nguvu ( strength) zao, ili awanoe wawe viongozi wazuri kama au kuliko yeye.
3.    Anayekusanya wafuasi, hawatendea wote sawa, wakati anayeandaa viongozi, humtendea kila mmoja kuligana na alivyo, hakuna watu wawili walio sawa, kila mtu ana mahitaji yake,.
4.    Anayekusanya wafuasi, anautimia muda wake (uses), wakati anayendaa viongozi, anawekeza (invests) kwenye muda anaoutumia.
5.    Anayekusanya wafuasi, huwataka wajitoe kidogo, wakati anayendaa viongozi, anawataka wajitoe sana.
6.    Anayekusanya wafuasi, anahudumia kizazi hiki, wanayeandaa viongozi, anahudumia vizazi vijavyo pia.
7.    Anayekusanya wafuasi, hulenga mafanikio kidogo wakati, anayeandaa viongozi, hulenga mafanikio makubwa.
Ni jambo la muhimu sana kuandaa viongozi katikavyama vyetu vya vijana na hata katika mashuleni yetu na mahali popote mtu anapoongoza kwa sababu;
1.    Hakuna kiongozi atakayeongoza wakati wote, utafika utaacha uongozi. Kama anaipenda kazi yake, na si mtu wa kutafuta faida yake mwenyewe, atahakikisha ameacha mtu atakayeendeleza kazi aliyekuwa akiifanya izidi kufanikiwa.
2.    Kanisa na vyama vyetu  vinakua, hivyo vinahitaji viongozi wengi zaidi wa kuviongoza.
3.    Viongozi wakiwa wengi, makundi  ya kuongoza yatakuwa madogo madogo, mzigo wao huwa mdogo. Kiongozi asifurahie kuona anaongoza  kundi kubwa la watu, kwani anapoongoza kundi dogo, anawasaidia vizuri watu anaowaongoza kuliko Yule anayeongoza watu wengi

Uadilifu kwa kiongozi
Kiongozi anatakiwa kuwa mwadilifu ili awavute wale anaowaongoza kumfuata na wao pia kuiga uadilifu wawke. Ni vema kukataa kuchukua nafasi ya uongozi kama wewe si mwadilifu, maana wasio waadilifu huharibu kazi wanayoifan ya kama viongozi. Uadilifu unaleta nini?
1.    Uadilifu huleta kuaminika na kuaminika hujenga mahusiano.
2.    Uadilifu hufanya kazi ifanyike vizuri na kwa haraka
.
Gharama ya uongozi

Huwezi kuwa kiongozi na kuepuka kukosolewa katika utendaji wako. Gharama ya uongozi ni kukosolewa; hata hivyo kiongozi hawezi kuepuka kukosolewa. Aristote anasema:  “kukosolewa ni kitu rahisi kuepukwa kwa kutosema lo lote; kutofanya lo lote na kutokuwa cho chote”
Kuna ukosoaji wa aina mbili:
1.    Ukosoaji unaojenga (constructive criticism). Mkosoaji anatoa njia ya kuboresha jambo analolikosoa.
2.    Ukosoaji unaobomoa (Distructive criticism). Mkosoaji hatoi njia ya kuboresha jambo wala hajui namana ya kuboresha jambo analolikosoa.

Usiumizwe na wakosoaji bali pokea yote kwa upole; pima wasemavyo na urekebishe unapoona kama nuru katika yale waliyokuambia. Kamwe usibishane na mtu hadharani kwani hili linakufedhehesha na kukuharibia uongozi wako wala usimshambulie akukukosoaye hadharani kwani  itakuwa vigumu kumwongoza.

Kukabili matatizo
Kiongozi hawezi kuepuka kukabli tatizo ( confront a problem) maana, matatizo hayawezi kukosekana katika uongozi kwani bado tupo kwenye dunia uliyo na shetani na malaika wake wafuasi wake waliovaa mavazi ya mbwa mwitu, yani wanaojulikana kuwa ni madui wa kazi ya mungu

Unapokabili tatizo zingatia
1.    Angalia kinachokusukuma (motive) kukabiri tatizo, kiwe kujenga na si kuaibisha.
2.    Hakikisha kuwa tatizo linastahili kukabiliwa (worth of confrontation), kuna yanayothaniwa kuwa ni matatizo na hali si matatizo, usipoteze muda kuyakabiri
3.    Shughulika na tatizo lenyewe tu usishughulike na vitu vingine ( be specific).
4.    Usimpuuze mtu anayeleta matatizo wala kujiamini kwake; mdhamini (don’t- estimate).
5.    Uwe mboreshaji jambo si mkosoaji tu.
6.    Usimshambulie mtu.
7.    Usiahirishe kushughulikia tatizo, litakuwa na kuleta madhara makubwa au litafikia hali ambayo haiwezekani tena kulitatua kwa amani.
8.    Jitazame uone unavyowatazama watu, unaweza ukawa unawaona kwa mtazamo tofauti na walivyo na kuwalaumu wakati hawana tatizo.
9.    Maliza kukabiri tatizo kwa mtazamo chanya. (end withi a positive tone). Tathmini uongozi wako kwa kuangalia mambo mliyoyafanya na chama au kikundi chako uone kama uongozi hauleti matatizo yeyote kwenye kikundi chenu. Lenga kufanya makubwa.

Uongozi na mipango ya maendeleo            
Hakuna sehemu inayoweza kuwa na maendeleo makubwa bila ya kuwa na malengo ya mambo ya kufanya. Kutokuwa na malengo kumesababisha kutokuwepo na maendeleo katika sehemu nyingine sana duniani. Usipojua unachokihitaji kukipata, unakohitaji kufika, hutafanya juhudi zozote maana huna malengo. Muda wa kuongoza bila malengo umepita. Hata katika  familia zetu, tunatakiwa kuwa na malengo.
Kuna malengo ya aina mbili a) malengo ya muda mrefu b) malengo ya muda mfupi. Panga malengo aina zote mbili na panga mikakati ya kufikia malengo yako uliyojiwekea . unapotaka kupanga malengo, fanya utafiti juu ya mambo yafuatayo;-
                        i./          Kuna kitu kipi mnachokifanya vizuri zaidi katika kikundi chenu? (strength). Mambo hayo mnayofanya vizuri lazima yapangiwe mikakati ya kuendelezwa ili yaendelee kufanyika vizuri na pengine vizuri zaidi.
                      ii./          Kuna mambo gani mnayafanya kwa hali dhaifu katika kikundi chenu (weaknesse ), ambayo yanasababisha kikundi chenu kisipata faida ya kutosha. Haya yanahitajika kuimarishwa ili kuleta mafanikia katika kikundi.
                    iii./          Kuna mambo gani ambayo mna nafasi nzuri ya kufanyika lakini hamtumii nafasi hiyo ili kuyafanya (opportunities), lakini mkiyafanya, yanaleta mafanikio. Mambo hayo yakiorodheshwa na kuanza kufanyika yanaleta mafanikio mfano, mnaweza kuwa mahali palipo na soko zuri la mbga mboga na kuna maji tele na ardhi tele na watu wanaagiza mboga mboga  toka mbali.
                    iv./          Kuna mambo gani ambayo ni tishio (threats) kwa shughuli zenu, mfano,niyi mnafanya biashara ya kuuza nyama za kuku na hivi karibuni, pamefunguliwa kiwanda cha nyama za kuku na kinauwa kwa bei ya chini kuliko yenu. Msipoangalia mambo kama hayo yote, mtajikuta mmefunga biashara yenu.
Baada ya kuangalia mambo hayo yote, mnahitajika kupanga malmengo mnayotaka kuyafikia na namna ya kuyafikia na namna ya kufikia malengo hayo ili kuleta maendeleo katika kikundi chenu. Katika kupanga malengo mambo yafuatayo yanahitajika kuzingatiwa:
          Panga lengo na mikakati, wahusika wa kutekeleza mikakati hiyo, muda wa utekelezaji wa mikakati hiyo na gharama za kutekeleza  mikakati hiyo,. Angalia mfano ulio hapa chini:

Mkakati: kila mwanachama wa PF ana sare kamili ya chama.

No
Hatua za kuchukua
(action steps)
Mhusika
(responsible)
Gharama
(cost)
Muda
(time frame)
1.
Kutafuta gharama za kushona sare kamili ya  PF
Mkurugenzi wa PF
Tshs 5000/=
January 30, 2008
2.
Kuhamasisha umuhimu wa kuwa na sare ya chama
Mkurugenzi wa PF wa kanisa
Hakuna
January 30,2008
3.
Kuhamasisha wazazi wajue umuhimu wa kununulia watoto wao sare za vyama
Mkurugenzi wa PF wa kanisa
Hakuna
Februari 28, 2008.
4.
Kukusanya fedha za sare toka kwa wazazi
Karani mtunza hazina wa PF
Hakuna
Aprili 31,2008
5.
Kushonesha sare
Karani mtunza hazina wa PF
TSHS 10,000/=
June 30,2008
6.
Kutoa taarifa ya ushonaji wa sare na kulionyesha kanisa sare hizo
Mkurugenzi wa PF wa kanisa
Hakuna
July 31, 2008

          Japo kazi ya kutengeneza malengo  na kuweka mikakati  ni kazi ngumu, kila kiongozi anatakiwa kuifanya kazi hiyo wala asiwe mvivu wa kuifanya maana hakuna maendeleo bila ya kupanga kuwa na maendeleo hayo.
          Tafuta lengo moja na kulipangia mkakati na hatua za kuchukua kama zoezi litakalokupa uzoefu wa namna  ya kupanga malengo.

Vichocheo.
          Ili mtu afanye kazi kwa juhudi zake zote na kwa akili zake zote, yapasa pawe na kichocheo, yaani pawepo kitu anachotarajia kupata baada ya kufnya kitu Fulani. Ili kuwafanya vijana hasa wavumbuzi na watafuta njia wajifuze kwa bidii, kuna pin tuzo na nishani wanazopewa baada ya kujifunza. Vitu hivi vinapokosekana, vijana hawapati kichocheo cha kujifunza yale wanayotakiwa kujifunza, hivyo, wanaweza kuacha kujifunza na kujitoa kwenye madarasa yao.
          Hivyo viongozi wa vyama vya vijana wanatakiwa kuhakiksha kuwa wanawapatia pin, tuzo na nishani wote wanohitimu masomo yao. Utaratibu maalumu ufanywe ili kuwapatia vitu hivyo na siku ya kuwapatia hasa watoto wadogo walioshiriki katika kujifunza na kufanikiwa wapatiwe wote. Asiache kumpa yeyote  Yule, yaani mpango afanywe kupata tuzo zao zote au pin zao zote bila ya kupeleza yeyote aliyeshinda.
          Vijana wadodgo hutaka kufanana  na wenzao katika kila kitu, ndio maana ni vizuri wawe na sare ili pasiwepo na yeyote anayepungukiwa na kitu walicho nacho wanzake, asije akajisikia vibaya na kukata tama.
          Mwanzoni mwa mwaka, viongozi wa vyma wapange tuzo, nishani na fani za kufundisha na mipango ya kupata tuzo, nishani na vyeti ifanywe mapema ili pasiwe na upungufu wa kitu chochote  siku ya mahafari yao.
          Kwa upande wa washiriki wa kawaida, kichocheo cha kuwa mkristo ni kurithi uzima wa milele. Hata hivyo, mtu anaweza kukata tama kama patatokea  chochote kinachoweza kumsonga wakati huu wa kupoteza njozi yake ya kuusubili uzima wa milele. Migogoro yoyote ile inaweza kumfanya mtu asahau kikuu cha kupata uzima wa milele.
          Kanisa lenye migogoro, linasababisha watu wasione thamani ya kichocheo kikuu wanaweza kupoa na hata kuasi. Mtu anaweza kuona ugumu wa kukaribiana na shida ya sas, akasahau faida ya baadaye, kilakiongozi ashugulike kwa juhudi zake zote kuzuia kuwepo kwa migogora katika kundi la watu analoliongoza, maana mogogora huondoa kabisa maendeleo. Mungu si mungu wa machafuko bali wa utaratibu na amani. Palipo na machafuko au migogoro mungu hayupo.

Mambo ya kuzingatia kwa kiongozi wa kikristo
          Kiongozi wa kikristo anatakiwa kuzingatia kuwa:
1.    Nguvu halisi za uongozi wetu zinatokana muunganiko wetu na mbigu,
2.    Imani kwa mungu ni mfereji wa kutupatia maisha ya kiroho ya kiongozi.
3.    Ahakikisha kuwa kamanda yesu yu mbele ya kundi analoliongoza daima.
4.    Anayefuata mtindo wa uongozi wa yesu. Azingatie kuwa yesu alikuwa mkweli na alitoa huduma    za kweli, hakuna mnafiki katika huduma zake. Mawasiliano yake yalikuwa ya kweli. Mahusiano yake yalikuwa           ya kweli.
5.    Aelewe umuhimu wa kutumikia watu.
6.    Uongozi ni kutoa mfano way ale unayotaka unawaongoza wayafuate. Uwe kielelezo chema kwa unaowaongoza.
Shetani hutaka zaidi kuangusha viongozi ili iwe rahisi kwake kuangusha wale anawaongoza. Hivyo, kiongozi anatakiwa kuomba sana maana anawindwa zaidi na shetani. Palikuwepo wazinzi wengi sana katika Israeli wakati wa mfalme daudi, lakini uzinzi wa daudi alisababisha jina la Mungu likatukanwa kwa sababu daudi alikuwa kiongozi mkuu sana katika Israeli, na hata dhambi yake ikaandikwa katika Biblia. Hivyo kosa lilidhaniwa kuwa ni dogo kwa watu wengine, kwa kiongozi ni kubwa sana maana linatumiwa na sheteni kudhoofisha mioyo ya watu wengine wanaogozwa watenda dhambi maana hata viongozi wameshindwa kuishi sawasawa na yale wanayotaka yafuatwe na wale wanaoongoza. Watu wengi huangalia viongozi kuliko kumwangalia yesu.
Ni kiongozi yupi katika biblia ambaye anakuvutia na unataka kuingia mbinu zake za uongozi? Mtaje na orodhesha aina yake ya uongozi.

Kumaliza uongoza vizuri
Kiongozi anatakiwa kujua umuhimu wa kuongoza vizuri na kumalizia uongozi wake vizuri. Kama kiongozi atamalizia uongozi wake vibaya, atakuwa ameyafuta, mawazoni mwa watu ambao alikuwa akiwaongoza, maelekezo yote mazuri aliyowapatia katika uongozi wake. Mwisho wa uongozi wa kiongozi ni wa muhimu zaidi kuliko mwanzo wake. Yale unayoyafanya mwishoni yanabakia mawazoni mwa unaowaogoza, kama picha yako halisi. Mwombe sana mungu umalize kazi yako ya uongozi vizuri.
          Unapomaliza kazi yako, uangalie kuwa huneni lolote kudhoofisha uongozi baada yako. Wapo viongozi wanaotaka uongozi unafuata baada ya uongozi wazuri. Hata wanapotakiwa kutoa  mawazo  yeyote yale kwa uongozi mpaya ili kuukwamua kutoka katika hali inayokabili uongozi hu, huwa hawataki kusaindia kabisa. Kikundi ulichokuwa ukikuongoza si chako binafsi. Kama ulikuwa kiongozi usiyetafuta faida yako mwenyewe, utatafuta mazuri kwa kikundi ulichokuwa ukikiongoza.
          Hautakiwi kuingia kikundi ulichokuwa ukikiongoza, lakini, ukitakiwa kutoa mawazo ya kukisaidia, yatoe wala usiwe na wivu, ukidai kuwa kama kiongozi ulimwachia kazi akifanikiwa, siafa zitakwenda kwake.hautakiwi kufanya kazi kwa  kutafuta sifa. Sifa zote zimwendee yesu na si mtu yeyeote Yule.
          Kiongozi mzuri, atatamani kikundi alichokuwa akikiongoza kinafanikiwa zaidi ya wakati alipokuwa akikiongoza kwa sababu kuna mbinu mpya na na dhana za kufanyia kazi bora zaidi  kuliko wakati uliopita. Maana kadri siku zinavyooendelea mambo huboleka zaidi katika nyanza zote kuliko wakati uliopita, hivyo utendaji ukawa mkubwa zaidi hali kadhalika matokeo ya utendaji. Tuombee kazi ya mungu ifanikiwe zaidi kuliko wakati wa zamani tulipokuwa  kiongozi na tukiona inarudi nyuma, tuombe sana mungu afanikishe kazi yake.
          Yesu aliomba kuwa wale watakaokuja baada yake kama viongozi wa kanisa wafanye makubwa kuliko anayoyafanya    yeye. Tuwaombee viongozi watakaotufuata wafanye makubwa zaidi ya tuliyoyafanya sisi.

                    2. MAOFISA WA KANISA.
Maofisa ni viongozi wa mstari wa mbele ndani ya kanisa mahali wanaoshirikiana na wakuu wa idara mbalimbali katika malezi ya kiroho ya waumini na hatimaye kuliongoza kanisa katika kutekeleza utume mkuu wa kanisa la waadventista wasabato ulimwenguni. Tunapo zungumzia maofisa wa kanisani ni kama ifuatavyo: mashemasi,mhazini,karani na mzee wa kanisa. Mchungaji wa kanisa au mtaa anaingia kila mahali maana yeye ndiye kiongozi mkuu wa kanisa aliyekabidhiwa wajibu huo na conference katika eneo lake. Hivyo yeye naye ni mmojawapo wa maofisa wa kanisa mahalia akishirikiana kwa karibu sana na mzee wa kanisa maana ni ofisi moja  na mzee wa kanisa katika etendaji wa kazi.

A.   KARANI WA KANISA.
v Hii ni ofisi muhimu kwa sababu inashughulika na mambo nyeti ya kanisa. Karani wa kanisa ndiye mtunzaji wa kumbukumbu za kanisa.
v Hivyo anapaswa awe ni mtu makini maana yeye ni mkumbushaji wa kanisa kwa taarifa yeyote inayohitajika ama kuuliziwa.
v Kanuni ya kanisa la waadventista wasabato inaeleza bayana kuwa karani wa kanisa   ni ofisi muhimu sana. Mara kadhaa imeshauriliwa kuwa karania wa  karani achanguliwe mtu ambaye anayeweza kutobadilishwa kazi yake mara  kwa mara. Ingefaa ashike nafasi hiyo walai miaka miwili mfululizo ili kutunza vyema kumbukumbu za kanisa mahalia.
“karani wa kanisa anashika mojawapo ya nyadhifa muhimu sana za kanisa, ambao ufanisi thabiti wa shughuli za kanisa hutengemea umakini wa utendaji kazi wa karani wa kanisa. Kama walivyo maofisa wengine wote ndani ya kanisa, karani wa kanisa huchanguliwa kwa muhula wa mwaka mmoja au miwili kadri inavyoamuriwa na kanisa la pale pale;lakini kwa sababu ya umuhimu na umalumu wa shughuli za wadhifu huu ni busara kumchangua mtu ambaye ataweza kuchanguliwa tena kwa mihula ya kujirudiarudia  ili kuleta mfululizo wa uzoefu katika  utunzaji wa kumbukumbu na utoaji wa taarifa”.
v Karani anapaswa kuwepo kila baraza la kanisa na mashauri ya kanisa. Asipokuwepo ahakikishe amewasiliana na msaidizi wake ili ahudhurie kikao hicho.

Majukumu ya karani wa kanisa:-
1.    Kupokea ajenda zote kutoka kwenye barza la huduma au wakuu wa maidara, kisha kujadiliana na mchungaji au wazee kuapnga ajenda zotepamoja ili karani aziorodheshe taayari kwa mjadala wa baraza la kanisa.
2.    Kupokea barua zote za kanisa na kuzitendea kazi;maana yake ndiye katbu au msomaji wa barua zote zinazohusu kanisa.
3.    Mwandishi wa barua zote za kanisa na msomaji wa barua zote za kanisa
a)    Kuandika barua zote zinazohushu mawasiliano na kanisa linguine au field /conference / taasisi yeyote kwa idhini ya mashauri ya kanisa.
b)    Pia kuandika baruza za mawasiliano na washiriki wanaohitaji  kufanya ushirika au kuhamia kanisa linguine
c)    Kuandika barua za safari za washiriki na barua za mialiko za maidara yote kwa niaba ya kania. Mf: kualika kwaya , PF, wahubiri na n.k
4.    Karani aorodheshe mali zote za kanisa n a kuhifadhi nyaraka zote muhimu katika file kwa ajili ya utunzaji wa kumbukumbu za kanisa mf: hati za viwanja, mikataba mbalimbali n.k.
5.    Atatunza kumbukumbu mbalimbali za washiriki tangu kanisa lilipotengwa jinsi walivyotoka kwa kuasi au kuhama au kifo.
6.    Atatoa taarifa ya washiriki mbele ya mkutano wa halmashuri ya kanisa kila robo
7.    Atatuma taarifa hiyo kila robo kwenda conference ikionesha ni washiriki wangapi walioingia na kutoka kwa robo hiyo.
8.    Atahusika sana wakati wa ubatizo na kuchukua taarifa ya watu waliobatizwa na kuwaingiza katika kitabu cha ushirika
9.    Utuzanji wa vitabu vya kanisa; hili ni pamoja na siri za kanisa yaani washiriki, na vikao vya baraza. Vitabu vyenye majina ya washiriki na mafiles. Kitabu hiki kitahidhi mambo mengi, mf, wanaoshiriki meza ya bwana,majina ya washiriki,taarifa ya mabara ya kanisa, taarifa ya mapokeo na marudio n.k
10.Karani ndiye mtoaji wa taarifa ya maamuzi ya baraza la kanisa na mashauri ya kanisa.
11.Karani aandike taarifa ya sababu ya kuondoa jina la mshiriki kwa uasi au kifo, tarehe iliyokubalika kupokea jina, n.k namna ya kuondoa jina ni kama ifuatavyo;  kifo pigia mstari mwekundu chini ya jina; uasi – pigia mistari miwili ya bluu au mweusi; uhamisho pigia mstari mmoja wa bluu; na kisha toa taarifa ya tukio.
12.Tawanya ajenda mapema kwa wajumbe ili watambue nini wanachokwenda kujadili. Hii itasaidia wakuu wa maidara wajue juu ya mipango yao ipo kuliko kupata ajenda ukiwa mezani.
13.Atatoa taarifa za vikao kwa wahusika kwa njia ya barua wale ambao mambo yao yamejandiliwa katika baraza la kanisa au halmashauri ya kanisa.
14.Karani kabla ya baraza na mashauri ya kanisa atakaa chini na mwenyekiti wa mabaraza hayo kupaga ajenda na pia kukusanya ajenda kutoka kwa wakuu wa idara kisha kujandiliana na mwenyekiti wa baraza la kanisa kabla ya kikao.

Utunzaji wa kumbukumbu za washiriki na matumizi ya kitabu cha karani wa kanisa6
          Yapo makosa mengi sana ambayo yameonekana katika utunzaji wa kumbukumbu za washiriki.
1.    Wengine huandika majina kwa kuyarundia kila mwaka. Hilo ni kosa. Majina yanaandikwa mara moja tu wakati tu mtu anapoingia katika ushirika wa kanisa kwa njia ya ubatizo, barua au kwa mikono.
Ø Kwa kufanya hivyo namba za ushirika zitakuwa zinabadilika badilika kila wakati, lakini namba za ushirika ya mshiriki hubalia ileile muda wote.
Ø Ni rahisi kupoteza majina kwa kuyaruka wakati wa kuyarudia kuyaandika.
Ø Hata kama mtu ameasi au amefariki au amehama, jina lake haliondolewi katika kitabu isipokuwa maelezo yatawekwa kwenye upande wa ma-ondoleo kuwa ametoka kwa njia ipi.
1.    Wengine hutenganisha orodha ya wale wa kiume na wale wa kike. Hilo ni kosa si utaratibu ila waweza kuweka kilelezo mbele ya jina la mshiriki kuonesha kama ni kiume au wa kike. Mfano:-
·       John mfumaji (ME) kuonesha kuwa huyu ni wakiume.
·       Fausta msomali (KE) kuonesha kuwa huyu ni wakike.
Washiriki wote huingia kitabu cha ushirika kulingana na tarehe aliyoingia mtu siyo kwa kunakili kila mwaka wala kutenganisha jinsia.
2.    Wengine huandika kufuata alfabeti. Hilo ni kosa. Orodha ya majina iende katika mtiririko wa tarehe jinsi mtu alivyoingia. Zingatia –orodha ya majina haibadilishwi, bali hudumu vilevile tangu kanisa lilipotengwa, hata kama majina yatafika watu 1000 na wanosali pale na walio katika ushirika halisi 300 hizo kumbukumbu zinabaki hivyo hivyo na hazibadiliki.
Hata kama mtu akifutwa ushirika au alihama na namba yake ushirika ilikuwa 73 na aliporudi tena kanisa akakuta idadi ya washiriki imekuwa 400, basi yeye atakuwa na namba yake  ya ushiriki 401. Jina lake litaonekana mara mbili, namaba yake ya kwanza ya ushiriki wa kanisa hilo, ile ya 401 itaonesha namna alivyoingia tena. Angalia kielelezo “B”
          Karatasi y MAPOKEO na MAONDOLEO ni vizuri zikiwa zmefuatana, yaani upande mmoja mshiriki alivyoingia na ng’ambo yake mshiriki alivyotoka. Lakini wakati Fulani kwa kuwa karatasi zilizochapishwa basi inakuwa sehehu ya juu ni mapokeo na sehemu ya nyuma ya karatasi hiyo ni maondoleo. Mstari uleule ambao una jina la mshiriki alivyoingia, mstari uleule  utaonesha mshiriki alivyotoka.

          Nasisitiza:
1.    Hata kama mtu anaodolewa kushirika kwa kuasi, kwa mauti, kwa barua jina lake halitaondolewa, bali litaendele kuonekana ila kwenye upande wa maondoleo itaelezwa ameondolewaje.
2.    Kamwe majina yasinakiliwe kila mwaka makarani wamekuwa wakiandika upya majina ya washiri. Hilo jambo lisiendelee, kwani namba za usjhirika zitabadilika kila mwaka wakati zinatakiwa zidumu vilevile.
·       Majina ya wale waliohama, kufariki au kuasi huachwa kabisa, na huo  si utaratibu.
·       Upo uwezekano mkubwa kusahau au kuruka jina Fulani bila kuliandika na hasa yale makanisa yenye washiriki zaidi ya 200.
3.       Hakikisha baada ya ubatizo wale waliobatizwa wanaingia kwenye orodha ya kitabu cha ushirika siku hiyohiyo. Uzembe mdogo tu waweza kusababisha majina ya watu kutoingia kwenye kitabu cha ushirika. Na kwa sababu viongozi wanabadilika mara kwa mara si rahisi baadaye kukumbuka kuwa hawa walibatizwa lini watakuwa wamebatizwa bila kuingia kwenye kirabu.
4.    Hakikisha jina la mshiriki anayehama kutoka kanisa lenu anaondolewa kwene kitabu cha ushirika baada ya kupata barua ya kukiri kuwa amepokelewa kule alikohamia. Na ile tarehe waliyompokea kule ndiyowatakayoindika kwenye nafasi ya upande wa MAONDOLEO.
5.    Hakikisha baada ya kumpokea msshiriki aliyehamia katika kanisa lenu kwa njia ya barua wakati kanisa lililopo nyoosha mikono kukubali kumpokea jina lake liingie moja kwa moja kitabuni. Kisha wajulishe kule alikotoka kuwa tayari mmekwisha mpokea mshiriki Yule ili na wao waweze kuondoa jina kwa kuandika tarehe aliyopokelewa katika kanisa lile jipya.
6.    Yule mshirika ambaye amefariki haondolewi ushiriki kwa maamuzi ya baraza au halmashauri ya kanisa, yeye baada tu ya kufariki jina lake litaondolewa na karania moja kwa moja kwa kuingiza tarehe ambayo amefariki.
7.    Washiriki wasiojulikana mahali walipo.
·       Mzee wa kanisa aitishe mkutano wa washiriki wote na majina yale yasomwe mbele yao ili kulishirikisha kanisa mahali walipo.
·       Wakishajulikan mahali walipo basi mawasiliano yafanywe ili kuwashuri wahamishe ushirika wao.
·       Wale ambao hawajulikani  mahali walipo watafutwe kwanza ndani ya mtaa wa kanisa lao  na wasipopatika leteni majina yao ili tuwatafute katika coferensi yote na nje ya conferensi.
·       Wasipopatikana kwa jitihada hizo zote, basi tutatoa muda wa miaka miwili kisha waweza kuondolewa katika ushirika/
Namna ya kuendesha baraza:-
ü Mambo ya muhimu sana karani anapaswa kuzingatia kwenye vikao vya makanisa kama ifuatavyo
o   Tarehe ya kikao cha mkutano
o   Mahali pa kikao
o   Mwenyekiti wa kiako (jina)
o   Majina ya wajumbe wote waliohudhuria na wasiohudhuria siku hiyo.
o   Jina la aliye toa ombi la kufungua na kufunga kikao
o   Muhtasari uwe wa taarifa sahihi za maamuzi yaliyofanyika kwa kupiga kura.
o   Atatunza hizo muhtasari au “minutes” kwenye karatasi maalumu zilizokusudiwa
ü Karani anataka kujua baraza linaaza saa ngapi. Zingatia muda wa kuanza na kumaliza kwa makubaliano wa baraza kuligana na ajenda kisha kumsaidia mwenyekiti kutawala kikao. Rudisha kikao wanapotoka nje ya mada.
ü Mambo ya kuandika :- orodha ya ajenda, idadi ya wajumbe waliofika kwa kuandika majina yao na vyeo na sahihi zao. Hii utaepusha usaliti kwa mambo yanayoharibika kwa madai ya kutokuwepo kwenye kikao.Pia pata taarifa kwa wajumbe ambao hawakuhudhuria kwa taarifa na wale wasio hudhuria bila taarifa onyesha kwa maelezo. Mwenyekiti ameanza saa  ngapi na somo kutoka wapi; nani alitetoa ombi’wimbo ulioibwa.
ü Hesabu idadi ya wajumbe kama inaruhusu mwenyekiti kuanza kikao ikiwa idadi iliyokusudiwa (colum) inatimia. Baraza la dharura halina idadi kamili (colum) bali inashauriwa isiwe wachache sana zaidi ya robo angalau ivuke robo ya wajumbe.
ü Ajenda za baraza dharura zisiwe nzito ambazo zina mvutano au zinazohitajika maamuzi ya wengi. Baraza hilo lisijadili ajenda za kuondoa majina, kupitisha bajeti, kuingia mikataba yeyote, au kufanya maamuzi makubwa ambayo yanaweza kuliadhiri kanisa, n.k.
ü Zingatia mabaraza ya kanisa yote yanapokuwa na  ajenda nzito kama vile kuhusu kuuza mali ya kanisa kama vile viwanja au jingo au gari, kufuta washiriki wengi kwa wakati mmoja ni muhimu sana kuwasiliana na uongozi wa field/ coferensi kabla ya kufanya maamuzi. Hili linahusu hata ujenzi wa njego la kanisa linalozidi dola miliono 25 na zaidi. Pia kuingia mikataba yoyote ya kisheria na pia ufungaji wa kesi yeyote mahakamani. Haya nia maamuzi ambayo konferensi lazima ishirikishwe kwani kumbuka kanisa hilo na mali ya konferensi.
ü Kisha soma ajenda zote na mwenyekiti aziingize kwa mjadala. Halafu ndipo uandike miniti (minute). Minit ni sauti ya mwisho inayokubaliwa kwa kura au sauti kubwa. Usiandike hoja bali maamuzi ya kikao tu. Ikiwa watu wanajdili hoja na mwenyekiti anaonekana hajapigisha kura basi kumbusha kikao kuwa hatujamaliza hoja niandike nini, hapo unahitaji kura.
ü Mwisho wa kikao kama kuna mengineo yajadiliwe sio ajenda mpya. Kisha kikao kifungwe kwa kuwasomea maamuzi yote uliyoyaandika kama kuna marekebisho yafanyike kabla hujazihamisha katika kitabu cha kudumu.
ü Taratibu za uendeshaji wa baraza la mashauri ziko sawa na zile za baraza la kanisa. Tofauti yake ni kuwa agenda zake zinatokana na mapendekezo ya baraza la kanisa wakati zile za baraza zinaazia kwa watu binafsi, idara au mwenyekiti wa kikao. Washiriki wanaweza kuleta ajenda kwa baraza iliyo na manufaa ya kanisa ili ijadiliwe kwa maendeleo ya kanisa husika.
ü Baraza la mashauri unposoma ajenda zake usome kama mapendekezo kutoka kwa baraza la kanisa na sio maamuzi ya kanisa. Hizi za kutoka kwa baraza zinawapa picha na dira washiriki kutokutafuna jambo kwa muda mrefu na kuangalia maamuzi ya baraza yalikuwa  sahihi au sio sahihi. Ikiwa kuna marekebisho baraza lising’ang’anie maamuzi yake kuwa ya mwisho. Lisikilize washiriki ndio sauti ya mwisho.
ü Karani anapaswa kuandika  maamuzi ya kanisa kwa kufuata jinsi mashauri itakayoamua. Hivyo siku zote ndio sauti ya kanisa nzima na wala sio baraza la kanisa.

Mambo ambayo karani hapaswi kufanya:-
Ø Usiandike barua yeyote ambayo inahusu kanisa kwa maamuzi ya baraza la kanisaau mzee wa kanisa tu bali mpaka maamuzi ya mashauri ya kanisa.
Ø Karani usiondoe au kuongeza jina la mshiriki kitabuni binafsi au kwa idhini ya baraza la kanisa tu bila idhini ya washauri ya kanisa. Karani anruhusiwa kuondoa jina la mtu aliyekufatu.
Ø Usiwe mwandishi wa baraza la kanisa amblo halikutangazwa kihalali siku ya sabato ili kuwezesha wajumbe kuhudhuria labda tu liwe la dharura.
Ø Karani asitumie muhuri wa kanisa kwa matumizi ambayo hayakuhalalishwa na kanisa au kutumia  kwa kikundi ambacho sio mali ya kanisa husika.
Ø Karani hapaswi kutoa siri za baraza. Atunze siri za  kanisa kwa uangalifu mkubwa hata kutokuziweka mahali ambapo zitaonekana na watu wengine kama vile wanafamilia yake au wauminnnnnni wasio wajumbe wa baraza la kanisa.
A.   MASHEMASI WA KANISA.
Shemasi ni cheo cha juu baada ya mzee wa kanisa katika malezi ya kiroho.majukumu ya mzee wa kanisa, mchungaji na shemasi ni sawa katika malezi ya kiroho. Tofauti ni katika ngazi ya uongozi. Wazee na mchungaji ni viongozi na watalawa wakati mashemasi ni viongozi sio watawala. Lakiniwote ni wazi wa washiriki. Ndio maana ofisi hizi zinawekewa mikono kwa makusudi haya ya malezi ya washiriki. Kitabu SDA Bible Commetary kinaonyesha usawa kwa kusema “katika nyakati za zamani wazee waliitwa waangalizi (overseers) au maakofu (bishops) na wachungaji (ministers) au mashemasi (deacons) wa kikristo, na wangalizi, wazee”( first homily on  epistle to the Corinthians I, in mign, patrologia craeca, vol, 62,col.183)
Biblia imeweka wazi swala la ushemaji na sifa zake.imetamkwa wazi ni kuwa nia daraja nzuri- kusema daraja nzuri daraja la kupandia cheo cha uzee wa kanisa kama wengine wanavyofundisha. Bali ni daraja nzuri la kiroho la mtu kama mtenda kazi wa kirsto kuokolewa binafsi. Hivyo sifa za shemasi zinafanana kabisa kwa sehemu kubwa na mzee wa kanisa. Hebu angalia Paulo anaposema hivi;
“Vivyo hivyo mashemasi na wawe wastahivu;si mwenye kauli mbili, si watu wa kutumia mvinyo sana, si watu wanaotamani fedha ya aibu; wakiishika siri ya ianikatika dhamiri safi. Hawa pia na ajaribiwe kwanza;baadae waetende kazi ya shemas. Wakiishi kuonekana kuwa hawana, hatia. Vivyo vivyo wake zao za wawe wastahivu; si wasingiziaji; watu wa kiasi waaminifu katika mambo yote. Mashemasi na wawe waume wa mke mmoja, wakiwasimamia watoto wao vizuri, na nyumba zao. Kwa maana watendao kazi ya shemasi hujipatia daraja nzuri, na ujasiri mwingi katika imani iliyo katika kristo yesu”.- 1 timetheo 3;8-13
Shemasi ni neno linalotokana na neno la kigiriki ‘diakonos’ yaani ‘deacon’ kwa kiingereza. Kwa Kiswahili ni mhudumu, mchungaji, mwangalizi, mtumishi, n.k

Sifa za mashemasi wa kanisa.
v Mashemasi wawe ni watu wa kiroho tena maombi waliojitoa kufanya kazi  ya mungu hasa uhamasishaji wa injili maana ndio njia pekee inayoweza kuwajenga washiriki.
v Mashemasi wanapaswa kuwa watu wenye kauli moja sio wazushi au wenye kuwasingizia     watu wa kutumia mvinyo kabisa. Neno kabisa n asana lina maana ileile katika lugha ya kigiriki.

Majukumu na wajibu wa mashemasi ndani ya kanisa
          Tena wawe waangalizi wa wenye shida, maskini,na wajane na yatima. Hizo ndizo kazi na kusudi la kuchangua mashemasi 7 wa kwanza. Matendo 6:1-7
          Kanisa linapaswa kuwa na bodi au baraza la mashemasi ambalo litashughulukia hali ya kiroho. Jambo lolote hairuhusiwi kuingia kwenye baraza la kanisa kabla ya kupitia kwenye bodi na baraza la mashemasi.
*    Shemasi mkuu wa kike na wa kiume ni wajumbe wa baraza la kanisa ambao hupeleka ajenda juu ya maisha ya kiroho ya washiriki.
*    Mwenyekiti wa baraza la mashemasi ni shemasi mkuu wa kiume na katbu wake ni shemasi mkuu wa kike.
*    Mashemasi wawe ni watu wa kiroho tena wa maombi waliojitoa kufanya kazi ya mungu hasa uhamasishaiji wa injili maana ndio njia pekee inayoweza kuwanjenga washiriki.
*    Hivyo kama mchungaji katika eneo lake na mwangalizi wa mambo ya kiroho ( yaani mpelelezi wa kanisa kujua hali ya hewa –atmosphere of the church) yapo mambo yakufanya:-
*    Kazi kuu ya shemasi ni kutembelea washiriki na kuwatia nguvu waaminifu na wale wasio waaminifu. Na pia kuzuia uasi kanisani.
*    Awe msikivu kujua hali ya kiroho ya washiriki. Watu wanasemaje juu ya mwenendo wa kikristo kwa jamii ya kanisa.
*    Shemasi ni mtunzi wa mali zote za kanisa kwa kuorodhesha mali hizo katika ledger. Kuhakiki usalama wa mali za kanisa.
*    Mashemasi wa kiume ni waangalizi na wakarabati wa majengo ya kanisa na pia usafi wa kiwanja cha kanisa.
*    Mashemasi wa kiume wanawekewa mikono. Ndani ya kanisa la waadventista wasabato ni nyadhifa tatu tu ambazo zinawekewa mikono. Mzee wa kanisa ,mchungaji na shemasi. Ijapokuwa mashemasi wa kike hawawekewi mikono bali huweka wakfu.

Kazi ya mashemasi wa kike.
          Shemasi wa kike ni cheo kinachopatikana pia ndani ya biblia. Soma warumi 16:1-2. Fibi kama mhudumu ni neno ambalo limetafsiriwa kutokana na neneo hilohilo linatafsiriwa katika timotheo  yaan ‘diakonos’
*    Shemasi wa kike anapaswa kuwatunza wagonjwa.
*    Kutengeneza meza ya bwana wakishirikiana na wakiume katika maadalizi.
*    Pia kutembelea washiriki pamoja na wajane na kujua hali zao za kiroho.
*    Usafi wa kanisa na ukusanyaji wa sandaka kanisani.
*    Kujali utulivu wakati wa ibada kwa kusimamia nidhamu ya kanisa. Hii inahusu ukaribishaji wa wageni na kuwaonyesha mahali pa kuketi. Mf roman katholic wanavyopita kwa utulivu na pia waumini wanvyoketi kimya.
*    Utunzaji wa siri za washiriki. Hii ni pamoja na kuunda bodi ya mashemasi ya wakike. Kazi ya bodi ni kujadili mambo yawahusuyo wanawake.

Swala la huduma ya meza ya bwana na ubatizo:-
§  Mashemasi wahakikishe wawe na muda mrefu wa kuandaa washiriki  kushiriki meza ya bwana hata wiki mbili au tatu kabla kwa njia ya matangazo na kuwatembelea washiriki.
§  Kusiwepo na uchelewaji katika meza ya bwana kwa kuandaa vifaa kwa wakati.
§  Vifaa vya meza ya bwana haviruhusiwi kutumiwa kwa matumizi mengine ya kanisa. Ni kazi ya mashemasi kuvitunza kwa uangalifu.
§  Wakati wa upishi wa meza ya bwana iandaliwe kwa kicho na heshima  mbele za mungu kwa kuanza na ombi na kumaliza kwa ombi. Mara Baada ya ombi la mwisho shemasi haruhusiwi kuonja kitu chochote. Hii inamanisha vitu hivyo vimewekwa wakfu kwa matumizi matakatifu.
§  Mashemasi wanatakiwa kuwa na taarifa za watu ambao hawawezi kuhudhuria meza ya bwana ili waweze kupelekewa.
§  Zingatia meza ya bwana inaandaliwa na mashemasi tu na pia wakati wa kugawa ni mashemasi wakiume watakaopita kuhudumu.
§  Mashemasi wanapaswa kuandaa kisima cha ubatizo au sehemu hiyo. Pia vifaa vya ubatizo kam mablacketi au shuka na vitambaa, pamoja vyumba vya kubadilishia nguo.
§  Hakikisha shemasi unatangulia ndani ya maji kabla ya mchungaji kwa ajili kumwelekeza mahali pa kusimama maana yeye ndiye uliyeandaa eneo la ubatizo; hivyo unalifahamu vyema

Namna mashemasi wanavyozuia uasi kanisa
ü Wapokea washiriki na wageni kwa uso wa babasamu. Kuwakarimu wageni.
ü Kutembelea waongofu wapya waliobatizwa hivi karibuni.
ü Kufundisha nyumba kwa nyumba misingi ya kanisa kwa waumini wapya pia kuwaelekeza namna ya kuwa na utaratibu wa usomaji wa neno la mungu na maombi ya familia kila siku.
ü Kuwafundisha waumini wapya kuzifahamu taratibu za ibada za kanisa na maelekezo yote muhimu namna ya kushiriki huduma za kanisa.
ü Kuwatembelea washiriki wote kuhudhuria meza ya bwana  wiki mbili kabla ya kuwatia moyo waliohudhuria na kuwasaidia wasiohudhuria waweze kujua umuhimu wa meza ya bwana.
ü Kwa kutembelea na kusisitiza washiriki kuhudhuria ibada zote za kanisa, usomaji wa lesoni, Biblia na roho wa unabii majumbani, utoaji wa zaka na sandaka kwa mpango, na mahudhurio ya meza ya bwana, n.k.


A.   MZEE WA KANISA.
Mzee wa kanisa ni nafasi ya juu katika kanisa akiwa chini ya mchungaji wa kanisa au mtaa. Cheo hiki ni nafasi ambayo mzee anawekewa mikononi. Hili kuonyesha kuwa anatengwa kwa matumizi matakatifu na jukumu nzito.
Katika biblia cheo hiki kintambuliwa kama mwangalizi au askofu. Ni mtu anayeshughulika na mambo ya ndani ya kanisa. Ni neno linalotumika hapa la kigiriki ‘presbuteroi’ unaweza kutamka puresibuteroi. Maana yake ni mtu mzee wa umri (older men). Kitabu cha SDA Bible commentary kinaeleza kuwa,
“neno mzee”, kwa kwa mtizamo mpana zaidi katika ofisi ndani ya kanisa ambayo imechukuliwa, kuwa historia kwa wote wapangani na maisha ya wayahudi. Maadishi kutoka misri (papyri) yanaonesha kwamba “wazee” walikuwa wajibu wa muhimu sana katika maisha ya uchumi wa wanakijiji…..kuhusiana na ukodishaji wa ardhi na malipo ya kodi…………. Kwa maisha ya wayahudi “mzee (prebuteros) alikuwa akitumika kwa ajili ya wanachama wa baraza la sanhedrini.”
Hivyo majukumu na heshima ambayo mzee alipewa kwa jamii, kanisa la awali lilichukua wajibu ule ule na kuingia katika matumizi yam zee.
“katika kanisa la awali mzee alikuwa akijulikana vile vile kama episkoros (episkopos) ikimaanisha “mwagalizi” (overseer), neno ambalo lilikuja katika lugha ya kiingereza kama” asofu (bishop), igawa kihistoria. Angalau katika karne ya 3B.K neno presbyter” (mzee) na “bishop” (askofu)yamewakilisha maofisa wawili tofauti wa kanisa, ushahidi wa agano jipya unaonyesha wazi kuwa katika kipindi cha mitume maneno haya mawili yalimaanisha maofisa walewale (the same official) (linganisha)1 timotheo 3:2-7 na Tito 1:5-9; angalia matendo ya mitume 20:28; liganisha Wafilip 1:1).

Sifa za mzee wa kanisa
Biblia inataja sifa kadhaa ambazo ni sifa za maadili na mwenendo wa  maisha ya mkristo. Kwa sifa hizi zinazoorozeshwa hapa kwenye mafungu ya biblia (Timotheo 3:1-7, Tito 1:5-9) tunapata sifa nyingi zinazojitosheleza katika mktadha wa biblia namna ya kupata mtu anayefaa kuwa mzee wa kanisa mahalia.
v Mzee wa kanisa ni mtu ambaye ni kielelezo kwa kanisa na  pia mfano bora wa jamii.
v Ni pamoja kuw na uhusiano bora wa familia yake.
v Asiye mtu anayelaumiwa jambo lolote.
v Asiwe msengenyaji wala asiyetunza siri za watu.
v Asiwe mgomvi
v Awe ni mucha Mungu na mtulivu asiyependa marumbano.
v Awe muombaji ili asitumie nguvu zaidi kwa kuwaswaga kondoo badala ya kuwaongoza.
v Awe ni mtu mwenye nguvu ya kirohokwa kusoma neno, maombi na kazi.
v Awe mfano katika utoaji wa zaka na sadaka na michango mingine kanisani
v Anapaswa kuchanguliwa mtu mwenye kupenda ushirikiano na tena umoja.


Majukumu na wajibu wa mzee wa kanisa
*    Mzee wa kanisa anapaswa kutambua kuwa ana familia mbili ya kanisani nay ya nyumbani.
*    Mzee wa kanisa ni cheo cha juu ndani ya kanisa mara baada ya mchungaji. Ni ofisi moja na mchungaji. Awe na umoja na mchungaji.
*    Mzee wa kanisa awe ni mtu mwenye uwezo wa kufundisha kuhubiri 1. Timotheo 5:17-22.
*    Mwenye kuelewa misingi ya kanisa na mafundisho makuu ya kanisa.
*    Unga mkono mafundisho ya kanisa. Kamwe usitangaza mashaka yako kwani utadhoofisha imani ya washiriki. Tito 2:1
*    Awe ni mtu anayebeba mizigo yaw engine yaani kuwa tayari wakati wowote ufaao na usiofaa.
*    Awe ni mtu anayetia moyo na motisha maafisa wa kanisa wengine katika kuendesha huduma za kanisa katika Nyanja mbalimbali za kanisa.
*    Mzee aepuke ukabila na njisia. Apende watu wote na kufanya kazi na watu wote.
*    Ni mwenyekiti wa baraza la kanisa wakati ambapo mchungaji hayupo. Bali ataitisha kikao halali kwa idhini ya mchungaji wa kanisa au mtaa.
*    Awatembelee washiriki nyumba kwa nyumba na kuomba nao na kujua shida zao za kiroho na kimwili. Maana mzee ni mlezi wa washiriki.
“kutokana na waraka wa yakobo mojawapo ya mzee ni kutembelea wagonjwa, kuomba kwa bwana kwaajili ya urejeshwaji wa afya zao, na kuwapaka mafuta kwaajili ya uponyaji (YAKOBO 5:14)”. Na kusaidia kufuga “malango wa nyuma” wa kanisa yaani kuzuia uasi kanisani utokaji wa washiriki kanisani.
*    Mzee anapaswa kudumisha mahusiano na familia yake. Tumia masaa mawili au manne kwa juma ukifanya kazi ya uzee na pia tumia muda na familia yako.
“kazi ya mzee, kama iliyokazi ya mchungaji kamwe haiishi. Kamwe hatatimiza yote unayoyapenda kutenda kwa ajili ya kanisa. Huna budi kutoruhusu kazi ya kanisa kukusababisha usahau familia yako na majukumu mengine. Kwa upande mwingine, usipoweza kutumia angalau masaa mawili hadi manne kwa juma ukifanya kazi ya uzee wa kanisa, yamkini unapaswa kukataa cheo hicho”.
*    Mzee wa kanisa anapaswa kujua udhaifu wake na kukubali makosa unapokosolewa maana hakuna mwanadamu asiye na udhaifu.
*    Kutoa mashuri na kusikiliza hoja za watu na shida zao. Kufanya upatanisho wa ndugu na ndugu katika kristo.
*    Kuheshimu taratibu na kusimamia na kitunza kanuni ya kanisa na taratibu zake zote. Awe ni mtu anayefuata kanuni zote za kanisa .
“kuhakikisha mambo yanakwenda kulingana na kanuni za kanisa siyo tu kwamba jukumu lako kama mzee, ila pia ni kwa manufaa yako kiutendaji. Iwapo utaiunga mkono kanuni hata maneno ambayo binafsi ungalitamani yabadilishwe, bali utaitengemea kanuni hiyo kusimama  imara pale wengine anapokushawishi kwenda kinyume na kanuni. Kwa maneno mengine, iwapo utapuunzia sera hizi za kanisa ulimwengu, washiriki wakko watajifunza kuhafifisha sera zilizopitishwa katika kanisa lako mahali”.
*    Anapaswa kuwa na wivu na mimbari kwa kutoruhusu watu wasiofaa kutumia ya malumbano au mabishano.
kanisa la waadventista wasabato katika ngazi ya conferensi/fild huliheshimu kanisa lenu mahalia kwa kuwapatia mchungaji. Pia hutoa vitambulisho vya kazi ya injili. Hii husaidia kanisa mahalia lisidanganywe na mtu Fulani ambaye hakuidhinishwa na kanisa. Wakati mnapotoa mialiko kutaka mtu kuhubiri kanisani mwenu, lazima ulilirinde kanisa lako kwa kutoruhusu mimbarani mtu anayedai ni mchungaji kumbe cheti chake muda wake umepita au kimebadilishwa. Watu ambao wamefutwa uchungaji, ama wamefutwa ushiriki wa kanisa Fulani, ama watu wa kujifanya ambao hawana kibali chochote toka kanisani,usiruhusiwe,naam, ukawaruhusu kwenda kutubu mimbarani. Uangalifu mkuu ufanyike kuzuia jambo hii”.
*    Mzee wa kanisa ndiye kiongozi wa ibada zote kanisani na pia mkuu wa maidara yote. Ajitahidi kuhudhuria vikao mbalimbali vya idara zote. Asipendelee idara yoyote.
*    Kanisa lenye idadi kubwa ya wazee wa kanisa akiwapo zaidi ya mzee mmoja yapaswa achanguliwe mzee wa kanisa wa kwanza au kiongozi. Huyo kazi  yake ni kupaga safu ya wazee wanzake.
*    Mzee kiongozi ni msaidizi maalumu wa mchungaji. Anawapatia wazee wazee wenzake kazi zao maalumu. Ikiwa mchungaji hayupo, na kuna hitaji la mwenyekiti wa baraza ya mashauri ya kanisa, kwa kawaida ni mzee wa kanisa kwanza anakuwa mwenyekiti. Somo mwongozo wa wazee uk.44(Kiswahili toleo la 2007).
*    Kila mzee apangiwe kikundi au idara kadhaa atakazosimamia kila mhula wa uongozi wake.
*    Kazi kubwa na ya pekee ambao wengi wameshindwa kuitambua na kuifanya ni kuwachukua wachungaji wao na familia za kichungaji kiroho. Ni kazi ya mzee wa kanisa kutembelea familia za mchungaji na mchungaji mwenyewe maana yeye ni binadamu anahitaji kutiwa nguvu na pia maombi. Soma wagalatia 6:2. Mchungaji anachunga kondoo lakini pia naye ni kondoo.

Mambo ambayo wazee wa kanisa wanapaswa kujiepusha nayo:-
§  Usitembelee nyumba kwa nyumba pekee yako. Kama ni mzee mmoja tembea na mke wako au shemasi wa jinsia yako.
§  Usiende kuwafarija wale ambao ni wajane, au walioachwa na waume zao peke yao – waliotelekezwa, nyumba ambazo waume nip ambo, waume zao wamesafiri mbali kimasomo au kikazi, n.k jiepushe badala yake ukawa wewe ndiye mfariji badala ya yesu kuwa mfariji.
§  Jiepushe kuchukua fedha ya kanisa kwa idhini yako mwenyewe bila taarifa ya kanisa au mwenzako kujua
§  Usiwe na vikundi vya watu Fulani unaowapendelea kwa sababu ya uwezo wao au cheo au hadhi zao. Watu wote wawe na hadhi sawa bila kujali kitajiri au kisomo.
§  Jiepushe kusema nimesema; kumbuka kanisa hili ni la demokrasia.
§  Usidharau wazo la mtu yeyote hata kama ni la kijinga jinsi gani. pongeza kila mtu kwa mchango wake. Pia sikiliza kila mtu bila kumdharau.


4. MHAZINI WA KANISA.
          Mhazini wa kanisa anafanya kazi ngumu sana kuliko zote kwani ni eneo ambalo linahitaji umakini sana. Tena kunakukata tama kwingi kwan mahali Fulani wahazini wanapokea mashutumu na hisia mbaya wanapofanikiwa katika maisha yao kuwa wameiba fedha za kanisa.
          Mhazini ni mtu wa kuombewa sana kwani anasimamia malia zote za kanisa kwa ushirikiano na idara za mashemasi. Mhazini anjulikana kama  ‘custodian’ (mwangalizi, mlizi, msimamizi, mtunzaji wa mali) wa kanisa lote.
          Mhazini ni cheo kitakatifu maana anagusavitu vilivyo vitakatifu ambayo haviliki. Kanuni ya kanisa inasema mhazini ni cheo kitakatifu lakini karani ni cheo muhimu.

Majukumu na wajibu wa mhazini wa kanisa.
o   Mhazini ni mtu anyeshikilia hazina ya bwana. Hivyo mhazini ndiye mmiliki wa mali zote za kanisa.
o   Mhazini anapaswa kutunza fedha zote za idara zote za kanisa.
o   Wakuu wote wa idara wanpaswa kutambua kuwa kila senti ya kanisa inaingia kwa mhazini wa kanisa kwanza kabla ya matumizi yoyote. Hivyo hakuna mkuu wa idara anyeruhusu kukaa na fedha za idara au chama mkononi isipokuwa mhazini.
o   Kanisa linapswa kuwa na akaunti yake.
o   Matumizi yote ya kanisa lazima yaidhinishwe na mashauri ya kanisa. Hii itawezekana tu ikiwa wakuu wa maidara wataleta budget zao na kupitishwa na washiriki. Hivyo mhazini atagawa atagawa kulingana na budgeti hiyo.
o   Mahali ambapo pana huduma za kibenki inashauriwa kanisa kufungua akaunti ili kuleta usalama kwa mhazini na pia maisha yake ya fedha ya kanisa kuwa salama.

Mambo ambayo mhazini anapaswa kufanya:-
Ø Haruhusiwikutumia fedha za trust fund – yaani za field/conference. Usikope kwa matumizi yoyote ya kanisa.
Ø Haruhusiwi kutumia fedha za maidara au chama chochote zilizowekwa katika mfuko wa kanisa bila idhini ya idara au chama husika.
Ø Mhazini haruhusiwi kumonyesha mtu yeyote ambaye sio mhusika kitabu cha zka na sadaka. Hili ni utunzaji wa wa siri za watu; na pia itaepusha janga lolote litakaloletwa na kukosa huko uaminifu. Wanaopaswa kukiona kitabu hicho ni mhazini, mzee wa kanisa, katibu wa uwakili,na mchungaji.
Ø Wakati wa kuhesabu sadaka , mhazini haruhusiwi kuhesabu peke yake.
Ø Usibandilishe lengo la mtoaji; bali katia lisiti kutokana na hitaji la mtoaji sio la kanisa. Kama huma tatizo ni bora kumwona kwanza kabla ya kaukatia risiti.
Ø Usikopeshe fedha ya kanisa kwa mtu yeyote hata kama jambo ni nzito kiasi ngani. Ni bora kanisa liketi na kumsaidia mhusika moja kwa moja.

3.    IDARA MBALIMBALI  NDANI YA KANISA
Idara hizi wakati mwingine zimeitwa vyama saidizi ndani ya kanisa . vinaitwa hivyo kwa sababu ni mgawanyo unaowasaidia maofisa wa kanisa katika kuliongoza kanisa . wakuu wa idara ni sehemu ya uongozi wa kanisa kwani ni wajumbe wa baraza la kanisa linaloongaoza kanisa nzima kwa kushirikiana na washiriki wa kanisa mahalia. Hivyo hawa maofisa wanapswa kuwatambua wakuu wa maidara kama watu wenye mchango wa lazima katika kutekeleza mipango endelevu na madhubuti ya kanisa katika ufanisi wake. Mara nyingi kanisa linapodorora inawezekana walipewa dhamamna ya ofisi ya uongozi kama wazee wa kanisa na karani, mhazini wameshindwa kutoa ushirikiano wa kutosha ama kutowatumia vyema wakuu wa idara kama invyostahili.
          Hebu maofisa wa wakuu wa maidara wafanye kazi kama viungo katika mwili wa kristo. Kwani kiongozi ni vichwa basi watambue kuwa kuwa kichwa hakiwezi kufanya  kazi vyema ikiwa mkono hajaobeba tonge na mdomo kupeleka tumboni. Hatimaye ndipo miguu ipate nguvu ya kutembe ili kusonga mbele na safari. Macho yanapokuwa na njaa hayawezi kuonga na Yule anayeona watu kama miti. Ni vyema viongozi wa kanisa wa wakuu wa idara kuona kuwa aliyebora kuliko mwingine kwani kila kiungo na thamani. Hebu chukulia kidole cha mwisho cha mguu kile kidogo kinapokatika  hakika mwili wote unapotembea utakuwa uwiano lazima utakwenda upande. Paulo anasema wazi katika 1 wakorintho 12:14-27 kuwa :
          “kwa maana mwili si kiungo kimoja, bali ni vingi. Mguu ukisema, kwa kuwa mimi si mkono, mimi si wa mwili;je! Si mwili  kwa sababu hiyo?.....Bali Mungu amevitia viungo kila kimoja katika mwili kama alivyotaka. Lakini kma vyote vigekuwa kiungo kimoja,mwili ugekuwa wapi? Lakini sasa viungo ni vingi ila mwili ni mmoja. Na jicho haliwezi kuuambia mkono, sina haja na wewe; wala tena kichwa hakiwezi kuiambia miguu, sina haja na ninyi. Bali zaidi sana vile viungo vya mwili vidhaniwavyo kuwa havina heshima, viungo vile twavipa heshima zaidi; na viungo vyetetuvilivyo na uzuri havina uhitaji; bali Mungu ameeunganisha ,na kukipa heshima zaidi kile kiungo kilichopungukiwa; ilikusiwe na furaha katika mwili, bali viungo vituzane kila kingo na mweziwe. Na kiungo kimoja kikiumia, viungo vyote huumia nacho, na kiungo kimoja kikitukuzwa, viungo vyote hufurahi pamoja nacho. Basi ninyi mmekuwa mwili wa kristo, na viungo kila kimoja peke yake.”

          Hivyo ni wazi kuwa majukumu na kazi za vyama na idra mbalimbali ndani  ya kanisa ni kuokoa na kutunza roho za watu. Idara inafananishwa na mifupa iliyoungana kufanya mwili wote. Hakuna mfupa wowote   utakaosema wenyewe una umuhimu zaidi kuliko mifupa mingine. Sote tumefungwa katika mnyororo mmoja wa kanisa la waadventista wasabato. Sasa tuangalie kila mtu binafsi jinsi aivutayo hiyo kamba. Idra zote ni nyet ndani ya kanisa. Kwahhiyo, na nia ya kila idra ni kupeleka injili. Hivyo idara zote zinafanya kazi kwa kutengemeana. Ushirikiano kati ya idara unafananishwa na mwili unavyofanyakazi yake.

Nani mwenye mamlaka ya kuazisha idara au chama?
          Hakuna kiongozi ambaye anaweza kuazisha chama au idra ndani ya kanisa. Bali mtu yeyote anaweza kutoa mapendekezo tu kwa jambo husika yaani halmashauri kuu ya kanisa ulimwenguni (general conference in session). Idara zinaundwa kupitia halmashauri kuu ya kanisa. Ambacho ndicho chombo cha juu cha kanisa la waadventista wasabato duniani. Hiki ni chombo pekee kinachopitisha na kuunda idara mbalimbali, na maamuzi yanaingizwa katika kile kinachoitwa kanuni za kanisa. Hatimaye utendaji na usimamizi wa kazi unaachwa mikononi mwa kamati kuu ya halmashauriya kanisa ulimwenguni [ general conference executive committee]. Kamati hii kuu imepewa dhana ya kusimamia maamuzi na kuendesha kazi kwa muda wa miaka mitano.
          Hivyo, kamati hii kuuinafanya kazi kwa maelekezo na maamuzi yanayofanywa na mkutano mkuu wa kanisa unaofanyika mara moja kwa miaka mitano. Mkutano huu unajumisha wajumbe kutoka mahali pote duniani {unaojulikana kama ‘general conference in session’}. Hili hili ndilo ambalo maamuzi yake mama white amezungumza kuwa ni sauti ya mungu. Ndio mkutano pekee unaoweza kubadili kanuni, kurekebisha, kuongeza na kufanya masahihisho ya lazima inapolazima. Hakuna kingine kinachoweza kutangua maamuzi yake baada ya kumaliza isipokuwa mkutano huo huo unapoitwa tena. Mkutano huu ndio unaoweka watendakazi wa kazi ulimwengu katika ngazi ya juu ya general conference na divisheni zake zote.
          Katika hali hiyo ni wajibu wa kila kanisa kuheshimu na kupokea maamuzi mbalimbali kutoka kwenye chombo hiki cha juu kabisa hapa duniani. Soma kile Ellen G. white asemacho juu yake;

          “Mungu ameamuru kuwa wawakilishi wa kanisa lake kutoka sehemu zote za dunia, wanapokuwa wamekusanyika katika general conference  watakuwa na mamlaka. Mungu amelipa kanisa lake mamlaka maalumu na uwezo, ambao hakuna yeyote awezaye kuhesabiwa kuwa hana hatia kama hatajali na kuuza na kudharau kwa maana yeyote anyefanya hivyo huidharau sauti ya Mungu. (wakati ambapo halmashauri kuu inapokutania toka kila mahali  duniani, hiyo ni sauti ya mungu duniani….).

Majukumu na wajibu wa idara na vyama ndani ya kanisa.
Ø Idara zote na vyama vyake vipo kwa ajili ya kuleta washiriki kiroho, kiakili, kimwili, na kijamii. Hivyo kila moja ni ya muhimu sana katika kanisa.
Ø Kazi kubwa ya idara ni kupanga mikutano ya utume ya kanisa. Kila idara inayoazishwa ndani ya kanisa ina wajibu/ majukumu yafuatayo:
1.    Kuhubiri injili [mathayo 28:19 -20]
2.    Kuangalia kuwa hali ya kirsto ya wale walio mkubali mwokozi inaendeleaje?
Kupitia baraza la kule yerusalem kazi ya injili ilifanyika pamoja na malezi yz kiroho. Walichanguliwa kama watenda kazi pamoja na mitume. Soma matendo ya mitume 6:1-7
Pia kanisa lilichangua wazee waangalizi wa makanisa na kuwawekea mikono matendo 20;17, 15:2, 4:6. Hivyo kanisa la waadventista waasabato linalo baraza lake kuu ambalo makao makuu yapo Maryland,washgton, D.Cmarekani. ndilo lililopewa mamlaka ya kusimamia taratibu za kazi na maaswala yote ya uongozi. Hiyo baraza la yerusalem ilikuwa linafanana utendaji wake na baraza kuu la kanisa yaani kamati kuu ya general conference.

A.   IDARA YA HUDUMA ZA WASHIRIKI.
Idara hii inafanya kazi kanisani kwa kuliongoza kanisanikaziya utume wa kanisa. Hutoa zana na kuwafunza washiriki wa kanisa amna ya kuwa watendakazi pamoja na bwana wao. Lengo kuu la idara hii ni kuwaadikisha washiriki wote katika utendaji wa dhati wa huduma ya uongozi war oho za watu.
v Idara hii ina vyama saidizi katika utume wa kanisa kwa njia ya huduma kwa jamii. Navyo ni AMO (ADVESTIST MEN ORGANIZATION) na DORKASI. Haya ni makundi saidizi ndani ya idara ya huduma za washiriki.
v Idara hii iliazishwa mahsusi katika kuelekeza utume wa kanisa na kuliingiza kanisa katika kazi hiyo ya kuokoa. Hii ni pamoja na kumwandikisha kila mshiriki katika kazi hii ya utume baada ya kuwafundisha na kutambua vipawa vyao.
v Idara hii inaleta watu kanisani kwa njia ya injilisti kwa njia mbalimbali; ugawaji wa vitabu, vijizuu, magazeti,n.k mahubiri ya hadhara, nyuba kwa nyumba, magerezani,hospital, n.k.
v Baraza la huduma linapaswa kukutana kila mwezi mara moja ili kujadili mambo mbalimbali ambayo yatapelekwa katika baraza la kanisa kwa ajili ya kazi ya mungu. Ikiwa baraza hili litafanya kazi vizuri basi kanisa lote litaamka kwa uinjilisti na mipango madhubuti kulirahisishia baraza la kanisa kutokuwa na vikao virefu vya kuchosha.
v Idara hii inaweza kupungua uasi kanisani kwa kiwango kikubwa kanisani kwa kuwaingiza washiriki kazini na waongofu wapya kwa kuwapa majukumu katika kamati za effort.
v Kupanga maeneo ya kazi kwa washiriki kwa lengo la uongoaji roho.
v Kuendesha semina za walei kanisani namna ya ushuhudiaji na kuhubiri.
v Kutoa hamasa kwa washiriki kufanya kazi ya mungu, kiongozi atumie vyema sabato ya kwanza ya kila mwezi huo.
v Ni kazi ya idara kutoa mafunzo ya kupata wainjilisti wengi ndani ya kanisa kama wamisionari wa maeneo mapya ya kanisa kwa ufunguzi wa kazi ya mungu.
v Idara hii inapaswa kuratibu effort zote za kanisa kwa mwaka kwa kushirikiana na maidara mengine kupitia baraza lake la huduma. Kisha kanisa liwe na mwelekeo.
v Idara hii inapaswa kupaga mipango yake kwaajili ya huduma za jamii kama vile kugawa misaada, faraja na kwa njia tiba kupitia vyama vyake vya AMO na Dorkasi.


Mkuu wa huduma na majukumu yake:
ü Kiongozi wa huduma za washiriki ni mtu maalumu katika utendaji wa kazi ya kusimamia uinjilist wa kanisa mahalia.
ü Anafanya kazi karibu sana na mzee wa kanisa na mchungaji na baraza lote la kanisa katika kutekeleza utume wa kanisa hili.
ü Ndiye mwenyekiti wa baraza la huduma za washiriki. Ambalo mara nyingi  linahusika wakuu wa idara kanisa kasoro karani wa kanisa.
ü Kiongozi  wa huduma hutoa semina kwa washiriki kutambua vipawa vyao na kuviingiza kazini. Kila mshiriki ameitwa kwa utume Fulani ndani ya kanisa hili.
ü Kiongozi wa idara ya huduma anatazamiwa kutoa hamasa kwa washiriki kazi ya mungu kila juma kupitia dakika 10 kabla ya matangazo ya kanisa. Kanuni za kanisa imewekwa bayana kuwa “ili kuimarisha na kuhamasisha moyo wa umisionary miongoni mwa washiriki, mikutano ya ziada ya huduma binafsi inaweza kufanywa katika njia moja au zaidi ya hizi zifuatazo: mkutano wa dakika kumi wa huduma binafsi unaofanyika kila sabato, kawaida mara baada ya kufunga shule ya sabato na kabla ya huduma ya mhubiri.”
ü Kiongozi wa huduma hutoa semina kwa washiriki namna ya kwenda nyumba kwa nyumba, kugawa vitabu, vijizuu na machapisho yetu, na pia kuendesha mikutano ya hadhara na kuhamasisha uinjilisti wa aina zote.
ü Kiongozi wa huduma anapaswa kutambua mipaka yake ya kanisa na kupanga maeneo ya kazi kwa malengo ya kufikia kazi katika eneo jipya la kanisa lao.
ü Mkuu wa huduma ni mjumbe wa baraza la kanisa kwa cheo chake. Anatazamiwa kushirikiana na katibu wa huduma katika kusimamia ya mikakati ya uinjilisiti inatekelezwa na baraza la kanisa kama ilivyobainishwa kwenye kanuni ya kanisa kuwa ajenda ya kwanza baraza la kanisa ni Uinjilisti.

Katibu wa huduma na majukumu yake:
Ø Katibu wa huduma ni karani wa baraza la huduma za washiriki. Ataandika ajenda na miniti zote na kuzipeleka kwa karani wa kanisa kwa ajili baraza la kanisa.
Ø Katibu wa idara atume taarifa ya utendaji wa washiriki field / conference kwa wakati.
Ø Katibu ahakikishe kila mwezi anapata taarifa kutoka kwa mhazini juu ya fedha za utume kufanikisha malengo yaliyokusudiwa na sadaka hizo.
Ø Atahifadhi kumbukumbu za utendaji kazi na uinjilist za kila mshiriki kwa kuandaa katoa taarifa ya utendaji wa idara wakati wa mashauri ya kanisa.
Ø Atatunza vifaa vya uinjilist kama vile vijizuu, vitabu, magazeti, vyombo na kadhalika kwa kuorodhesha kwenye daftari maalum kwa kumbukumbu za idara.
Ø Atachora ramani ya kanisa yaani jiografia ya kanisa lake kwa mipango ya uinjilist kwa kushirikiana na uongozi wa kanisa  ili kujua maeneno yanayopewa kipaumbele katika ngazi ya uinjilist.
Ø Katibu wa huduma ni mjumbe wa baraza la kanisa kwa cheo chake. Anategemewa kushirikiana na mkuu wa huduma kuwasilisha mipango ya uinjilist wa waumini wote na kanisa kwa ujumla.
Ø Katibu wa huduma atakuwa anasoma riport ya utendaji kazi za uinjilisti kutoka kwa vikosi vya ushuhudiaji ndani ya kanisa ya utume. Kila siku kuna dakika 10 za idara ya huduma kutoa taarifa hizo na shuhuda mbalimbali.
Zingatia: dakika hizi kumi zinaweza kutumiwa pia na idara nyingine kuhamisha mambo ya uinjilisiti kama inavyoelekezwa kwenye kanuni ya kanisa pia. Kanuni za kanisa zinaonyesha kuwa idara hizo kutekeleza utume wa kanisa “katibu-mhazini ataandika kumbukumbu za shughuli za chama cha vijana, kutoa taarifa kila mwezi katika form zitolewazo na mkurugenzi wa konferensi, na kuwahimiza vijana kutoa taarifa za shughuli zao za ushuhudiaji katika kipindi cha dakika kumi cha huduma mahususi.”

Makanisa ambayo yanakituo cha kuendesha huduma kwa jamii basi kwa hakika majukumu ya vyama ya AMO na DRKASI yamekuwa yamemezwa kwa namna moja katika kituo hiki za huduma za jamii. Mfano mzuri ni ngazi ya konferensi mpaka general coference kanisa lina kituo cha huduma au shirika la huduma kwa ajili ambalo linajulika kama ADRA ( ADVENTIST DEVELOPMENT RELIEF AGENCY). hivyo hatuna vyama au kwa kuonekana kama ilivyo makanisa kwa idara nyingine.
          Vyma hivi vinafanya kazi kwa kushirikiana sana tena kwa ukaribu. Maana majukumu yao yamefanana kabisa isipokuwa mambo machache yanayotofautishwa kwa jinsia zao. Hivyo chama hivi tofauti yao kubwa kuwepo kanisani ni jinsia ya kiume au kike. Idara ya huduma za washiriki inapopeleka ujumbe wa malaika watatu kwa njia ya kulihubiri neno, basi vyma hivi kama kiganja na mkono vinahubiri ujumbe huohuo kwa kutoa misaada kwa jamii yaani huduma za matendo kutekeleza ujumbe wa yakobo.
YAKOBO 1:27; YAKOBO 2:14-22.
          Nitaanza kwa na AMO: ni chama cha wadvetista  wanaume wote ndani ya kanisa. hili linamaanisha kuwa kuitwa chama ni ili kujua idadi ya wanachama wake na pia kufanya tathimini ya wale ambao wako hai wanaopenda kushiriki huduma za jamii. lakini haimaanishi kuwa kutokuwa mwanachama wa AMO uko sahihi bali UMEKOSEA LENGO! Kumbuka na kuzingatia vizuri MATHAYO 25:31-45. Hivyo kusema umekosea lengo maana yake ni kuwa umefanya uchanguzi mbaya ya kuwa katika kundi la mbuzi wakati wewe ni kondoo wa Mungu pale tu ulipochangua kuwa Mkristo!

Chama cha AMO kina mjukumu yake ya msingi kama ifuatavyo:-
1.    Kila mwanume aliye ndani ya kanisa aandikishwe kuwa mwanachama wake.
2.    Kuendesha program kuu ya utume ya kanisa la waadventista wasabato (umishonari) zinazotekelezwa na kundi hili la wanaumeni kama ifuatavyo:-
a)    Kufanya mahubiri ya walei –wasiriki wa kanisa.
b)    Kufanya huduma ya magereza:- kuwaona wafungwa, kuwafundisha na kuendesha ibada magerezani, kugawa vitu kama sabuni, miswaki, nguo, Biblia, vitabu n.k
c)    Kufanya huduma za jamii kama vile kuwaona vikongwe, kujengea nyumba vikongwe au wasiojiweza, maskini, vilema, n.k. kutoa misaada mbalimbali ya nguo, fedha, chakula , fanichs, n.k.
3.    Kutembeleana wanaume kwa wanaume ndani ya kanisa na kuhamasisha katika ukuaji wa kiroho. Kiuchumi, na pia kubadilishana mbinu mbalimbali za kiuchumi kwa njia ya kuwakwamua wanaume ambao uchumi umewabana kiasi cha kushindwa kuwa n amwenedo mzuri wa mikutano ya kanisa. Kutiana shime katika safari yetu ya ukristo.
4.    Kutoa ushauri kwa vijana wa kiume na pia kuendesha shughuli za usafi kwa jamii.
Tunapozingatia fungu la mathayo 25 juu ya swala la huduma kwa jamii katika biblia inatufundisha jambo hili litakuwa kikuu kitakachotumika wakati wa huduma pia. Hivyo kama wewe  ni mwanaume au mwanaume haupo katika vyama hivi umesahau kidogo wajibu wako jambo ambalo utachelewa sana kulikumbuka kama wale mbuzi waliosema ni lini bwana tulikuona una njaa? Uchi? Gerezani? Huna nguo? Hili jambo mama Ellen white amelizungumza vizuri kwa upendo wetu wa mungu unapimwa vipi? Ni namna tunavyowahudumia wengine. Soma
DORKASI: Ni chama cha wanawake kanisani ambao wameamua kutii sauti ya yesu inayoangiza,”Enendeni ulimwenguni kote…….” Chama hiki ni chama kinachotenda kazi kwa uhusiano wa karibu sana na mashemasi wa kike na kiume ndani ya kanisa.
Huduma hizi mbili za mashemasi na vyama hivi ni kama pete na kidole. Makusudi ya mashemasi kuwepo na Dorkasi mambo yao ni mamoja kusaidia wenye shida kwa hali na mali. Soma MATENDO 6:1-2, 3-5:9:39. Kuhudumia wajane,maskini, wasiojiweza, na wenye shida.
Ili kuelewa vizuri chama cha DORKASI ni muhimu kuelewa chanzo nz maana ya jina hili kuwa limetoka wapi! Seventh- day Adventist Bible commentary inasema,
“jina TABITHA ni jina la kiaramaiki ‘Tabyetha’ likuwa sawiana na jina kiebrania’zibiah’ katika agano agano la kale(2waflme 12:1;2 nyakati 24:1), au zibia (1nyakazi 8:9), “swala (gazelle)” lugha ya kigiriki nni dorkasi, ikiwa na maana ‘paa (wild shegoat)’ au swala (gazelle).”
Unaposoma kitabu cha matendo kinasema alikuwa amejaa matendo mema. Hivyo kwa baadhi wanamwona Dorkasi kama mtu aliyeishi katika kipindi cha filipo mmoja aliyeshi na mashemasi saba wa kwanza wa kanisa. Na pia ipo dhana ya kuwa yawezekane dorkasi alikuwa shemasi wa kike                                                                                                                                                                        kwani alifanya huduma zile zile za mashemasi walizochanguliwa kwazo.
Kitabu hiki cha wachambuzi wa Biblia kinaonyesha kuwa yawezekana kabisa kuwa alikuwa shemasi aliyefanya kazi kwa bidii. Tena Biblia inasema mwanafunzi mmoja akiwa sawa na mwanafunzi wa Yesu kigiriki ni mathetria- mwanafunzi wa kike. Wakiume ni mathetes. Soma SDA Bible commentary gombo la 6,
“kwa baadhi, dorkasi aliliganishwa kama shemasi wa kike katika kanisa huku yafa (joppa). Ikiwa hili ni kweli, inaweza kutuonyesha mvuto wa filipo. Alikuwa mmoja wa wale mashemasi saba (angalia matendo 6:3,39). Na inawezekana kwamba  alichukua utawala wa kanisa katika  huenda alikuwa na uangalizi malumu wa wajane wa kanisa (liganisha  6:1; 9;39).

MATENDO YA DORKAS : MATENDO  9:37-42.
1.    Tabitha alikuwa mkarimu mwenye kusaidia watu yaani mtoaji wa misaada.
2.    Dorksi alitoka alitoa huduma yake kwa matendo mema hili likimaanisha utoaji wa misaada. ‘almsdeeds’.
3.    Hakutoa mali zake kwa  kutuma watu bali alioa mali zake mwenyewe nay eye alijitoa na mali zake pia.( she was not content to be  haritable by proxy, but give gave herself as her possessions.)
4.    Wajane wa kanisa waliangana kwa umuhimu. Matendo 6:1 kifungu hiki kinashauri kwamba kanisa katika yafa (joppa). Lilikuwa kama shiriki la hisani (the church at joppa also was organized  for charty).
5.    Dorkasi alitengeneza au alishona nguo kwa makusudi ya kutoa msaada (charitable purposes). Fungu la 36.
6.    Dorkasi alitengeneza au alishona nguo kwa makusudi ya kutoa msaada (charible purposes). Fungu la 36.

Waliamini hata baada ya kufufuka kwake. Fungu. La 42. Alikufa lakini bado angali akinena kama sadaka ya habili mwenye haki. hivyo kwa kuyaelewa  matendo haya ya dorkasi ni jambo linalokuonyesha kama njinsia ya kike unapaswa kufanya nini katika kutenda mema kwa jamii inayolizunguka kanisa lako mahalia. Kumbuka kipimo cha hukumu bali tunafanya mema kama matokeo ya kuzaa matunda mema  ya yesu akaaye ndaniyetu. Yesu anasema  katika YOHANA 15: 1-55; GALATIA 5:22-23. Haya ndio matunda ya roho…. Upendo…. Utu wema, fadhila- ni tafsiri ya kuwa ukiwa umemvua bwana yesu hutuweza kuwa nje ya vyama hivi.
Kumbuka dorkasi alijitoa yeye mwenyewe na mali zake pia. Ni wito wangu kuwa usitoe tu vitu bali pia tuhusike namna ya kupanga katika utumiaji na ugawaji wa vitu hivo. Kujihusisha katika kazi hii ya upendo kwa vitendo ni jambo linaloambukiza. Kumbuka yohana anasema huwezi kwenda kwa mtu ukaomba naye tu lakini usifanye kitu kwa ajili yake. YAKOBO 2:14-22.


kazi za chama cha dorkasi kanisani ni zipi?
1.    Kuandaa mavazi, vyakula, na mahitaji ya misingi kwani ya maskini, wahitaji, na wenye shida. Kumbuka kapu la dorkasi lirudishwe  kanisani haraka!
2.    Kutoka elimu wazima: kuwatembelea –kuzuru, kusaidia shughuli za nyumbani kwa watu mbalimbali kama vile wale walioadhirika na magonjwa ya muda mrefu.
3.    Kutoa tiba ya nyumbani, ushauri nasaha na huduma nyinginezo-tuna madaktari kati yetu, watalamu wa mambo ya uchumi, nk.
4.    Kuendesha mahuburi mbalimbali ya walei kwa kushirikiana idara mbalimbali ndani ya kanisa.
5.    Kutembelea magereza ya wanawake na kutoa msaada ya fedha ya fedha, sabuni, dawa za meno, miswaki, nguo, na kutoa neno kwa wafungwa wa kike, nk.

Chama cha Dorkasi
          Dorkasi ni chama kisaidizi katika ngazi mbalimbali. Ni chama ninachokuwa  chini ya mwavuli wa idara ya hudumu za washiriki. Chama hili hufanya kazi za kwenda nje ya kupitia huduma za jamii ambapo hufanya kazi kwa njia zifuatazo:

1.    Kutayarisha nguo ili ziwe kwenye hali nzuri na kupeleka kwa wahitaji, au kushona nguo mablimbali wao wenyewe.
2.    Kuwatembelea watu majumbani na kuwafundisha watu juu ya elimu ya afya na malezi nyumbani, pamoja na neno la Mungu.
3.    Uanachama wa dorkasi ni wanawake ambao wako kanisani na wenye utayari wa kufanya kazi kupitia huduma za kijamii nje ya kanisa.
4.    Uongozi wake huchanguliwa na baraza la kanisa kila mwisho mwa mwaka.
5.    Dorkasi hufanya kazi zake chini ya idara ya huduma kanisani .
6.    Kiongozi wa chama cha dorkasi ni mjumbe wa baraza la kanisa.
7.    Viongozi wengine ni
·       Msaidizi wa kiongozi wa dorkas(ikiwa anahitajika katika kanisa kubwa)
·       Katibu wa chama cha dorkasi

Chama cha Amo –(Adventist Men Organization)
v Ni  chama ambacho nacho kipo chini ya idara ya huduma za washiriki.wanachama wake ni wanaume ndani ya kanisa. Kinashughulika sana na huduma za jamii. Vyama hivi katika makanisa yanatenda huduma za uinjilisti kwa njia ya matendo. Mathayo 25:34-42.
v Kazi za msingi  ambazo kiongozi wa chama na wanachama wanapaswa kuzitenda ni:-
                                                                                    i./          Kusaidia wazee vikongwe walio nje ya kanisa au hata ndani kukarabati nyumba zao.
                                                                                  ii./          Kutoa misaada ya nguo, chakula, fedha n.k. kwa wajane na maskini na wenye shida.
                                                                                iii./          Kutembelea magerezani na kugawa misaada ya vitu mbalimbali pamoja na injili.
                                                                                iv./          Kufanya uinjilisiti wa hadhara na rafiki wa nyumba kwa nyumba kuendesha mahubiri.
                                                                                  v./          Kutoa ushauri kwa vijana wa kiume na pia kuendesha shughuli za usafi kwa jamii



B.   IDARA YA HUDUMA YA WANAWAKE
Biblia inatambua huduma za wanawake kwa vizazi vyote. Kuazisha idara ya huduma za wanawake ilikuwa kuwawekea mfumo rasmi ambao utakuwa unatambulika  kwa maana ya idara. Lakini sio kusema wanawake wamekuwa hawafanyi kazi. Ni kweli idara hii imekuja pia kwa makusudi ya kuwainua wanawake    wanaojisilia duni katika kazi ya Mungu nao wapate hamasa ya kuamka na kufanya kazi ya mungu.biblia katika ZABURI 68:11, 12: YOELI 12:28- 32 imenukuliwa hivi
“Bwana analitoa neno lake; wanawake watangazao habari ni jeshi kubwa; wafalme wa majeshi wanakimbia, na mwanamke akaaye nyumbani agawa nyara.” Yoeli inasema. “hata itakuwa, baada ya hayo, ya kwamba  nitamimina roho yangu juu ya wote wenye mwili: na vijana wenu wataona maono; tena juu ya watumishi wenu, wanaume kwa wanawake katika siku zile, nitamimina  roho  yangu…..”
·       Idara hii imeazishwa mahsusi kuwawezesha wanawake walioko ndani ya kanisa kujua utume wao na kungudua vipawa walivyo navyo katika ngazi ya Mungu. Hili ni pamoja na kuwafanya waweze kutumika kikamilifu katika kazi ya Mungu badala ya kufikiria kazi ya kuokoa ni wanaume tu kama wengi wanavyokudhani
Kazi ya idara ya wanawake ni:
          a. kueneza injili.
          b. kuleta washiriki.
·       Kazi ya kuleta washiriki wanawake wote walio ndani ya kanisa, ndilo jukumu kuu la idara hii. Ilivyo idara nyingine yeyote ndani ya kanisa, ndivyo ilivyona idara hii pia. Idara imepewa dhamana ya kuwalea wanawake vijana na wazee ndani ya kanisa kwa kuelewa magumu sita ambayo wanawake wanapitia katika maisha haya. Nayo ni unyanyasaji wa kinjisia. Kutokujua kusoma, ukatili kwa wanawake na watoto wao, umaskini, ubakaji, na nk.
·       Kazi ya kuleta washiriki wanawake wengi wamefikiri kuwa imeachwa kwa wanaume peke yao; na hata wanawake wengi wameona kuwa kuna karama ambazo sio zao wakati biblia inasema kila aliyeokolewa amepewa kipawa kwa ajili ya kujenga ufalme wa Mungu. soma Efeso 4:8-13: Paulo anasema yesu ametenda mateka wanadamu sio waume na amewapatia silaha, katika kueneza ufalme wa Mungu wa kuvunja ufalme wa giza. Elewa maana ya neno ‘adamar’ yaani adamu au udongo sio mwanaume tu bali jinsia zote.

Viongozi wa idara na namna wanavyochanguliwa.
1.    Afisa wa idara wa kanisa, ambaye huchanguliwa na kibaraza cha uchanguzi.
·       Kiongozi wa idara yuko chini ya mchungaji wa mtaa
·       Kiogozi wa idara ni mjumbe katika baraza la kanisa
2.    Katibu wa idara.
3.    Kamati ya ushauri ya idara
·       Mke wa mchungaji (shepherdess), yeye atashiriki kamati ya kanisa pale alipo mtaani.
·       Katika makanisa mengine mtaani, mke wa mzee wa kanisa husika atakuwa mjumbe wa kamati hiyo.
·       Wajumbe wengine ni.
ü Mkuu wa usomaji biblia
ü Mkuu wa kutia moyo wanawake
ü Mkuu wa uinjilisti
ü Mkuu wa huduma za jamii
ü Mkuu wa elimu ya umishonari.
4.    Idadi ya ukubwa wa kamati utategemea ukubwa wa kanisa; katika kanisa kubwa watu 5-8; kanisa dogo wajumbe 3-5.

MUUNDO WA IDARA YA WANAWAKE WAADVENTIST






KATIBU/ MTUNZA HAZINA WA IDARA
 

MCHUNGAJI WA KANISA
 
                             

KIONGOZI WA IDARAKANISANI
 
 

         
·        

KAMATI YA USHAURI (WAJUMBE WATANO)WASAIDIZI
 
                                       
 















·        
·        
1)     

5.  wasaidizi, ambao ni wakuu wa vitengo; wanapaswa kuandika taarifa mbalimbali kwa yale walioyafanya kwa kila mwezi.
·       Kazi ya Mungu haifanywi kwa uwezo wa mtu. Mungu ndiye anayeweza kumtumia yeyote ikiwa ikiwa tu yupo tayari kutumika. Angalia kisa cha williamu foe, hazzen foss na Ellen white kwenye ASD BC Vol.8-10.
·       Kamati hufanya kazi kazi kwa mwezi mmoja , baadaye hubadilishwa. Hii ni kulinda idara ya watu wanaokatisha tama wale walio tayari kufanya kazi kwa juhudi.(mathayo 18:15-18)
6.  idara inapotakiwa kutoka nje kwa huduma za kanisa, hufanya hivyo kama sehemu ya uinjilisti.
          Kumbuka idara hi ni kamili. Idara hii haipo chini ya idara nyingine knisani, bali hushirikiana na idara hii haipo katika kufanya kazi. Ni tofauti na dorkasi ambayo ni chama ambacho kipo chini ya idara ya huduma za washiriki.

          Mbinu za utendaji wa uinjilisti:
a)    Anza ndani, kwa mtu mmoja, katika nyumba za washiriki, na watoto wetu.
b)    Uinjilisti wa kikundi; kujiunga pamoja kwa kazi ya Mungu
c)    Uinjilisti kwa njia ya semina- wanasemina, baada ya mafunzo hutoka kwenda kuleta wengine..
d)    Uinjilisti kwa njia ya familia.( zaidi ya moja)
e)    Uinjilisti kwa majirani zetu.
f)     Uinjilisti wa kikundi kwa njia ya:
o   Mapishi
o   Ushonaji n.k.
g)    Uinjilisiti wa “Effort,” mahubiri ya hadhara.
h)    Unjilisti wa kuleta watu wanje walioingia ndani ya kanisa.
o   Kuwalea kimwili- huduma ya kimwili, apate chakula
-mwongozo mpya anapaswa kupewa chakula “neno”
o   Kuwalea kiakili
-        Mama yeyote huwa anatamani mtoto awe na akili njema
-        Mlee mtoto iliakue kwa kujitegemea.
-        Waongofu mpya wafundishwe vizuri ili wakue kiakili
o   Kulea kiroho
-        Wamjue Mungu katika maisha yao (kumb 6:6-7)
-        Wafundishwe kwa bidii katika malezi ya kiroho.
o   Kuwalea kijamii:
-mtot aweze kutambua mazingira yanayomzunguka
Watoto wajifunze kupenda watu wanoishi kuwazunguka.
o   Kuwalea kihisia.
-        Onyesha upendo na kuwafanyia vitu ambavyovitamfanya ajisikie vizuri.
Wajibu wa idara
1.    kuwalea wanawake vijana na wazee walio ndani ya kanisa
2.    kuwaandaa kwa kazi mbalimbali za kueneza injili.
3.    Kuwawezesha kufanya uinjilist katika mafanikio
4.    Kuwapatia changamoto mbalimbali zinazotokana na njisia yao na jinsi ya kukubaliana nazo.(kupata ufumbuzi) ili kuwezesha majukumu hayo kupata nafasi, idara ya wanawake, kuhimiza yafuatayo kufanyika kwa wanawake:
·       Kusoma Biblia na Roho  ya unabii, ili kukubaliana na changamoto ya kusema”siwezi’ (Fil 4:13)
·       Kuwasomesha watoto kwa njia ya kuwafundisha, maadili yote ya kiroho, kijamii, kiakili, na kimwili.
·       Kutoa hudumu ndani ya kanisa kuona kwamba wanawake wanapata fursa ya kushiriki katika huduma za kanisa kupata au kuligana na talanta na vipawa wallizonazo. Pia kuwawezesha kugundua karama zao.
-idara  hii intenda kazi zake kupitia kwenye bajeti ya kanisa.


Kazi au wajibu wa viongozi wa idara
Kiongozi wa idara:
1.    kiongozi wa idara ya wanawake, aunde kamati ya ushauri, na hatimaye baraza litachangua wanaofaa kushauri na kuendesha mipango ifayo.
2.    Afanye utafiti ndani ya kanisa, kuafahamu idadi ya wanawake waliopo:
·       wasichana wangapi?
·       walioachika wako wangapi?
·       Walioolewa  na wasioamini wangapi?
·       Wajane ni wangapi?
·       Wenye shida ni wangapi?
·       Walio-olewa (wenye ndoa ni wangapi?
3.    Atayarishe programme kwa ushirikiano na kamati yake ya mambo ya kufanya katika kanisa lake:
·       Program ziwe na makusudi ya kiuinjilisti
a)    Mambo ya afya
b)    Kuwa na ushirikiano na wasichana katika hali ya moyo mmoja.
c)    Kutoa masomo maalumu kwa mama wajane na kuwatia moyo.
d)    Kuendsha masomo ya mapishi ya aina mbalimbali kupatana  na mashauri ya roho ya unabii. (mafundisho yetu).
e)    Kuwa mbunifu kwa kuwashirikisha wanawake wenzake.

            4. Kiongozi ni mwenyekiti wa  shughuli zote za wanawake  ndani ya kanisa.
·       Anapoitisha watu awe ameandaa taratibu zote katika “ note book”/ daftari ya kumbukumbu;ili kuepuka kusahau yaliyo mhimu.
·       Toa taarifa kwa katibu mhazini au msaidizi wako kama yupo.
·       Kiongozi uwe mfumo kwa utunzaji muda, fika na kumaliza kwa wakati.
5. Kiongozi ni mjumbe wa Baraza la Kanisa.Hivyo hakikisha unahudhuria                                                 katika mabaraza yote, ya kanisa na mashauri ya washiriki.

6. Uwe na kalenda ya mambo ya kufanya katika idara yako kwa wiki,mwezi,robo na mwaka.
·       Lijulishe kanisa kama yanayofanyika ndani ya idara kupitia mashauri ya Kanisa na vikao halali.
·       Unapotayarisha kalenda yako ya idara husisha matukio ya kalenda ya GC; yenye Sabato maalumu ya za idara ya wanawake.
a)    Sabato ya maombi ambayo hufanyika ,kila mwezi wa tatu Sabato ya 1.
b)    Sabato ya 2 ya mwezi juni ni mkazo kwaajili ya huduma ya wanawake.
c)    Juma au wiki ya mwisho mwezi Agosti ni mkazo kuzuia aina zote za ukandamizaji, Unyanyapaa, na ukatili kwa wanawake.
d)    Kaika Sabato hizo kuna masomo maalumu yanayoandaliwa kutoka Makao makuu ya Kanisa GC.
7. Ni wajibu wa kiongozi kuandaa na kutuma taarifa ya shughuli za idara kila mwezi.

KAZI ZA KATIBU
    i./          Ni msaidizi wa kiongozi wa idara; asipokuwepo, yeye ndiye anapaswa kufanya kazi zote kwa niaba ya kiongozi.
  ii./          Ni mwadishi wa taarifa na kumbukumbu zote za idara za kila siku,mwezi, robo, na mwaka.
iii./          Anapokea fedha za idara, kutoka katika miradi na michango mbalimbali; na kuziwakilisha kwa mhazini wa kanisa. Huku yeye akizitunza kumbukumbu za fedha hiyo.
iv./          Kila zinapotoka/ kuingia fedha ni vyema kuhakikisha kuwa, taarifa yake inatunzwa vizuri. Na kuwa tayari kueleza/kusoma mbele ya wana idara,kanisa n.k
  v./          Yenye ndiye mtunzaji wa mihutasari (miniti) za vikao mbalimbali katika idara.
vi./          Si mjumbe wa baraza la kanisa, kwa nafasi yake.

Mambo ya kuzingatia katika kuongoza wanawake:

a.     watie moyo wale unaowaongoza katika kila jambo, kupitia biblia, Roho ya unabii (mamlaka ya neno la BWANA).
b.    Omba kwa pamoja na wana idara mara kwa mara (mara nyingi kadri iwezekanavyo).
c.     Ongea maneno ya faaraja, shukrani onyesha, onyesha furaha wakati wote, mtie moyo kila mmoja, hata kwa njia ya kuandika ujumbe.
d.    Ukisikia kitu kibaya juu ya mtu/wanaidara, usikiongelee, usikiongezee chochote; thibiti, kisha mwone mhusika.
e.     Mpelekee kila mtu chochote kilicho bora, pongeza, zawadi inapo wezekana.
f.      Jitahidi kuimba nyimbo za pamoja au nyimbo maalum.
g.    Kusiwe na matabaka yeyote katika kutoa huduma za misaada, kiroho na kijamii miongoni wa washiriki na wanaidara.

A.   IDARA YA SHULE SABATO.
Shule ya sabato ni nini? Ni mahari ambapo waadvestista wasabato hukaa chini ya madarasa ya kujifunza ukweli wa neno la Mungu na kumwimbia Mungu nyimbo za sifa na kumtolea bwana sadaka na kuzungumza naye kwa sala. Kauli mbiu ya shule ya sabato kwa miaka mingi imekuwa ni ‘Moyo wa kanisa’ kama kielelezo kuwa uhai wa kanisa unategemea uhai wa shule ya sabato moto moto katika kutekeleza utume wake Biblia inaonyesha wazi kuwa: “Moyo ulio mzima ni uhai wa mwaili;…..” MITHALI 14:30.
Shule ya sabato ni kituo cha kuelimisha kanisa ili kujua wajibu wao mkuu wa kumtumikia Bwana. Ni mahali ambapo karama mbalimbali zimepewa mafunzo kwa ajili ya utumishi. Kituo cha kuandaa waumini ndani ya kanisa kwenda kujenga mwili wa kirsto wa kutumia talanta mbalimbali walizonazo.
Shule ya sabato ni mahali mahususi ambapo malezi kamili ya kiroho hutolewa kwa waumini wa kanisa. Muumini hulishwa kiroho kila siku kwa usomaji wa mwongozo wa kujifunzia Biblia (maarufu kama lesson)’ kufahamiana kwa ukaribu kunawepo hii ikijumisha ushirika wa pamoja(fellowship) katika madarasa madogo ya watu 6-8; ni mahali ambapo matendo mema huhubiriwa pale watu waliofanya kazi wanapoleta taarifa zao kwa yesu juu ya utendaji wa kazi ya Bwana; ni mahali ambapo waumini wanachota tena chaji (nguvu) kwa ajili ya juma linguine katika safari yao ya kiroho na utumishi. Ni mahalia ambapo wenye uzoefu wanapotoa uzoefu kwa wasio na uzoefu katika kujjifunza mapenzi ya mungu kwa njia ya shuhuda mbalimbali.
Shule sabato ni kipimo ambacho waadvetista wasabato wanapopata elimu ya kweli kuliko huduma zote ndani ya kanisa jambo ambalo linawafanya kuonekana kuwa ni wasomi wa Biblia na wajuzi wa maadiko kwa ufasaha kuliko madhehebu mengine mtu alisema kuwa ukisoma mwongozo wa Biblia (lesson) kwa miaka minne mfululizo utakuwa umehitimu ya  digri yako ya mambo ya dini(BA in region lakin  sio watu waliobobea katika maadiko matakatifu tena wengine ni wakufunzi wa vyuo vya kitheolojia katika vyuo vikuu maarufu duniani kama vile Newbold, Adrews, Lomalinda, na kadhalika. Hivyo inaweza ikawa kweli ya asilimia 93.
Shule ya sabato ni mahalia ambapo watu hufundishwa mambo mbalimbali, hasa yale yanayohusu maisha ya mwanadamu na uhusiano wake wa Mungu/Muumba wake. Shule ya sabato ni shule ya kujifunza Biblia. Katika Biblia mna mambo mengi ambayo ni budi  tuyajue. Ni barua ya Mungu kwa mwanadamu. Katika shule hii kila mmoja hutoa shuhuda mbalimbali zinazohusiana na utume wa Bwana. Yeyote anayehitimu shule hii ndiyo elimu ya kweli. Mathayo 13:51-52; yohana 17” 17; 7:14-15.

Shule ya sabato ilivyo.
Ni kama ilivyo shule nyingine, shule ya sabato nayo ina viongozi wake ambao ni kama  inavyoonyeshwa   hapa chini:-
a)    Mkuu wa shule sabato
b)    Mkuu msaidizi kwa ajili ya washiriki.
c)    Mkuu msaidizi kwa ajili ya uinjilisti.
d)    Mkuu msaidizi kwa ajili ya divisheni-watoto.
e)    Karani wa shule ya sabato.
f)     Karani wa sadaka ya kupata faida.
g)    Karani wa shule ya sabatoutandaaji.
h)    Mwimbishaji  nyimbo za SS.
i)      Mkurugenzi wa shule ya Biblia wakati wa likizo.
Wote Hawa Wanachanguliwa Wakati Wa Baraza La Uchanguzi Wa Watenda Kazi wa kanisa.

Makusudi ya shule ya sabato
a)    Kufundisha ukweli wa neno la Mungu.
b)    Kuokoa roho zilizopotea na kuzileta kwenye lengo la ukweli.
c)    Kuwahusianisha watu wazima watoto karibu na muumba wao lia juma.
d)    Ni shule ya kuwashirikisha washiriki, kujifunza neno la Mungu pamoja na kumtukuza.
e)    Mungu kwa nyimbo na kumuomba pamoja na kumshukuru kwa sala na sadaka pamoja.
f)     Kuimarisha na kuwakamilisha   watakatifu.

Historia ya shule ya sabato kwa ufupi.
Ø Tunamsemo usemao ‘shule ya sabato ni moyo’ hapa kila mshiriki amekariri maana si wote wanaoelewa maana gani halisi. Yawezekana wa slogan (mbiu) hiyo kuwa alikuwa na maana gani halisi. Yawezekana wengine wakamaanisha moyo kama upendo, au uhai wa kanisa kama kiungo cha moyo kilivyo muhimili wa uhawetu. Au ikawa na naama kwa inasukuma idara nyingine zote kama vile moyo unavyosukuma damu katika eneo lote la mwili.
Ø Yote katika yote lazima Biblia itupe wazi wazo mtunzi. Mithali 14:30 “….Moyo ni uhai wa mwili….” Hivyo maana halisi ya shule ya sabato ni uhai wa kanisa. Ikiwa kanisa kanisa lina shule ya sabato iliyo uha(active) hakika kanisa hilo litakuwa hai.
Ø Shule ya sabato iliazishwa rasmi mwaka wa 1853 kwa wazo la waasisi wa kanisa ambao wengi wao walitoka katika makansia ya kujumapili wakiwa na zile ‘sunday shool’. Ilianza huko Ronchester, New York; baadaye mwaka 1854 huko Bucks Bridge New  York. Ndipo mwaka 1870 shule za sabato zikawa na mpango namna ya uendashaji na kuwa na viongozi wake.
Ø Historia ya masomo ya robo yaani ‘Lesson’ yalianza mwaka 1852; yaliandaliwa na james White kwa ajili ya vijana. Na 1869 G.H. Bell alitayarisha masomo ya ambayo yalikuwa katika kitabu cha mwaka mzima. Hatimaye mwaka 1888 Lesson za watu zilitolewa kwa mara  ya kwanza.
Ø Ilipofika maka 1876 iliitwa ‘international Sabbath school association’ na 1901 ikawa idara ya shule ya sabato.
Ø Lakini ilipofika mwaka 1886 iliboreshwa zaidi katika conference ya IOWA huko marekani. Mwanamke mmoja aitwaye Florence Plummer Lorena aliweza kuwa ndiye mkurugenzi wa kwanza katika conference. Alifanya mambo mazuri ambayo yaliwavutia viongozi wa kanisa wa General conference hatimaye 1901 akachanguliwa kuwa mkurugenzi wa kwanza duniani wa shule sabato katika General conference. Aliongoza idara hiyo kwa muda mrefu kuliko wengine wote waliofata. Aliongoza kuanza 190111 hadi 1936 alipostaafu.
Ø Hivyo misingi mingi ya shule sabato aliasisiwa na yeye katika tunzi za miongozo yake aliyoandika kama:- A soul winningi Teacher, soul winning Sabbath school; na pia historia ya shule sabato.
Ø Kutokana na miongozo yake ilifanya shule ya sabato iwe ni kitovu cha uinjilisti. Mpaka leo makusundi ya shule ya sabato ni kuongoa roho. Hii ni shule inayopelekea wanafunzi wa aina zote. Wale ambao hawajabatizwa ni washiriki wa shule ya sabato pamoja na wale ambao wamebatizwa.

Historia ya sadaka za shule sabato:-
·       Mwaka 1885 Oakland Clifornia walitoa sadaka yao  ya roho ya kwanza kwa ajili ya kazi ya Uastrali. Ilipofika mwaka 1909 mpango wa kutoa sadaka ya shule ya sabato kila juma ulianza rasmi kwa mpango maalum.
·       Na mwaka 1912 sadaka ya 13 ya mazidio ilianzishwa kwa mpango maalumu.
·       Na mwaka 1919 sadaka ya shukrani ilianzishwa; na hatimaye 1925 sadaka ya kupata faida nayo ikaazishwa.
Makusundi ya msingi kuazisha shule ya sabato ni kusaidia kazi ya mungu kusonga mbele kwa kuzingatia mambo haya manne yafuatayo:-
i)      Kuwa na ushirikiano wa pamoja (fellowship)
ii)    Kuleta washiriki walio ndani ya kanisa (nurturing)
iii)  Kushuhudia walioko nje ya kanisa. (witnessing or ortreach)
iv)  Kufanya uinjilisti wa ndani ya kanisa (worship or inreach)
Shule ya sabato ni darasa kamili.wengi wamesema yeyote anayehudhuria shule ya sabot kwa uaminifu na kusoma lesson zote kila siku kama utaratibu ulivyo, na kuhudhuria prodramer zke zote kama ilivyo bila kukosa; baada ya miaka mine atakuwa amehitimu digrii yake ya mabo ya dini yaani Batchelor of Art in Religion studies.
Hivyo kiongozi wa shule sabato ni mtu mwenye uwezo wa kubuni mambo tena mhamasishaji katika kujifunza lesson.
Awe mjuzi wa maadiko yaani msomaji hodari wa Biblia . ndio maana wengine wanasema kiongozi wa shule ya sabato ni mzee wa kanisa kubwa ndani ya kanisa dogo; yaani kanisa hili lenye idadi kujumisha idadi kubwa ya waumini ndani ya kanisa husika lenye idadi ndogo ya washiriki kitabuniwashiriki wake ni kila aiingiaye ndani ya kanisa ni mshiriki wake. Kwanini? Kiongozi wa shule ya sabato ni mtu anayeongoza waumini na wasio waumini – wenye ushirika na wasio na ushirika; na darasa la ubatizo na wale watoto wote ana mamlka nao. Wakati mzee wa kanisa  ni mzee anayewaongoza wale tu waliobatizwa ndio alio na mamlaka nao. Hivyo shule ya sabat ni kitengo nyeti maana ndio uhai wa kanisa. Kumbuka ni kuwa bado mzee wa kanisa  ni mkuu wa idara zote ndani ya kanisa. Hivyo kufanya kazi bega kwa bega  kati ya kiongozi wa shule ya sabato ni mzee wa kanisa kunaleta ufanisi wa kazi ya Mungu. 
Kiongozi wa shule ya sabato anapaswa kufanya yafuatayo:-
·       Awe ni mbunifu na mtu mwenye njozi ili aweze kuleta mvuto wa shule sabato.
·       Aongoze timu ya wasaidizi wake kuelewa majukumu yao. Itamuwia rahisi kuongoza kwa ufanisi na mafanikio.
·       Ahakikishe kanisa limegawanywa katika madarasa ya watu 6-8. Mpango huu utasaidia yafuatayo:- washiriki wawe watendaji sio watazamaji; wawe washuhudiaji; wasaidiane katika shida mbalimbali; wapendane na kufahamiana zaidi; na kupunguza uasi kwa wanaorudi nyuma kufahmika kwa haraka na utembeleaji wa waumini wapya mara kwa mara. Na kuhakikisha kila mshriki ana lesoni yaani kuhamasisha utoaji wa fedha ya lesson kila robo.
·           Kuhamasisha sadaka za kanisa kila sabato; sabato ya kwanza mni uinjilisti; ya pili ni sadaka ya kupata faida; ya tatu ni washiriki; nay a nne ni shukrani ya kuzaliwa .
·       Kusimamia darasa la walimu au kupanga  mtu wa kusimamia na kupanga walimu kwa kushirikiana na baraza la shule ya sabato.
·       Kuwa mwenyekiti wa baraza la shule yaaaa sabato linalolatibu mipango yote ya SS.
·       Atastawisha na kuboresha mambo yote ya SS pamoja na sadaka zote za shule ya sabato. Siku yake ya kusimamia shule  ya sabato; ni sabato ya nne kila mwezi.

Viongozi wa wasaidizi wa shule     ya sabato na kazi zao:-
Ø Mkurugenzi wa SS- washiriki (watu wazima)
o   Huyu anashughulika katika kumsaidia mkurugenzi wa SS katika kuendesha program zote za SSS watu wazima. Hawa ni miaka 19+++
o   Kupanga wa hudumu na kuona program zilivyoendeshwa kwa utaratibu. Pia kumsaidia mkurugenzi kuhamasisha ununuzi wa lesson za watu wazima.
o   Kuona watu wameketi katika madarasa ya watu 6-8 na utaratibu wake wa muda umefuatwa.
o   Kubuni namna ya kuendesha shule ya sabato yenye kuvutia. Hii itawezekana kwa kusimamia waendeshaji wa prodram kanisani wanapata mbinu mbalimbali kwa kujifunza kwa maknisasa mengine.
o   Kuona kuwa kila msiriki, ameandikwa kwenye makadi ya shule ya sabato. Kuhakikisha wote wanahudhuria katikaa shule ya sabato.
o   Kuhakikisha kuwa wagojwa wasiojiweza- wadhaifu wanaoorodheshwa majina yao. Kumpata mkuu wa SS utaandaji majina ya wagonjwa na wadhaifu.
o   Kuhakikisha kwamba kila mshiriki anayo lesson  yake na kwamba anaisoma kila.

Kuorodhesha majina katika makundi matatu:-
·       Ashirki wa ss ambao ni pia ni washiriki wa kanisa.
·       Washiriki wa ss ambao hawajabatizwa.
·       Majina ya washiriki waliorudi nyuma, na majina ya wale wanotazamiwa kubatizwa.

Ø Mkurugenzi wa shule ya sabato –uinjilisiti
·       Anamsaidia mkurugenzi kuhamasisha swala la uinjilisti wa vikosi ndani ya madarasa ya SS. Hii ni pamoja kugawa vijuzuu na masomo ya uguduzi/VOP/Biblia  yasema.
·       Kupanga sabato za wangeni kupitia baraza la shule ya sabato. Kusimamia mipango yote ya maadalizi ya sabato ya wageni na michango ya ufanikishaji.
·       Kuhakikisha kila sabot taarifa ya  ushuhudiaji imetolewa kwa kila darasa kwa kutembelea madarasa hayo na kutumia wahamasishaji wa kila darasa kuhamasisha uinjilisti wa nyumba kwa nyumba. 
·       Kubuni mikakati ya  ufunguaji wa matawi ya shule ya sabato mapya.

Mkurugenzi wa shule sabato – utendaji
ü Kumsaidia mkurugenzi kuwatia moyo wale ambao hawahudhurii shule sabato.
ü Pia wale ambao wanafika wakiwa wamechelewakuwatia nguvu kuwahi.
ü Kuwasaidia wale ambao hawanunui lesson waweze kununua.
ü Akisaidiana na wanadarasa wakongwe, wagonjwa, na wenye shida ambao hawahudhuria SS. Atawapelekea lesson zao, ikiwa walikwisha toa fedha, na kuchukua sadaka ya SS.
ü Wale wasiofika kwa ajili shida mbalimbali anaweza pia kuwasiliana nao kwa njia ya simu, kadi maalum(get wellsoon n.k);wale ambao hawa kufika kanisani siku hiyo.

Mkurugenzi wa shule ya sabato- watoto (divisheni)
ü Anamsaidia mkurugenzi katika usimamizi wa kugawanya kanisa katika divisheni ndogondogo kutokana na umri wao.
ü Yeye anasimamia watoto katika shule ya sabatowa umri kuanzai: 0-3 (crale); 4-6 (kindergarten); 7-9 (primary); 10-12 (teenage); 13-15 (Adolescent of eary teen); 16 -18 (late teen or youth).
ü Achukue idadi ya watoto walioko kanisani.
ü Atakuwa msimamizi wa shule sabato ya watoto
ü Pia atahamasisha wazazi kununua lesson za watoto.
ü Kutafuta walimu watakaoweza kufundisha watoto katika mgawayo huo. Pia kutafuta masomo ya hizo divisheni.

Mwimbishaji wa nyimbo za vitambuni wa shule ya sabato:-
ü Ni mtu muhimu katika shule ya sabato. Kipindi chake huanza saa 3:00 kila siku ya sabato asubuhi.
ü Aachanguliwe mtu wenye uwezo wa kujua nyimbo za vitambuni angalau robo tatu awe anazifahamu ikiwezekana na noteni afahamu.
ü Nyimbo zile zisizofahamika ndizo hutiliwa maanani kufundishwa.
ü Ataongoza pia nyimbo zote wakati wa vipindi vya SS.
ü Daima aonekane katika mavazi mazuri/ nadhifu na safi.
ü Atahimiza watu waimbao kwa furaha na akili wakimsifu Mungu.

Karani wa shule sabato
ü Karani wa SS ni katibu wa baraza la shule ya sabato.
ü Ndiye mkusanyaji taarifa ya utendaji mzima ya mambo ya SS kanisani.
ü Anapaswa kuwahi mapema zaidi pamoja na darasa la walimu kuchukua taarifa ya darasa hilo na mahudhurio ya walimu.
ü Anapaswa kuanda taarifa ya kusomwa kila sabato kwenye shule ya sabato.
ü Anapaswa kusirikiana na karani wa huduma kupata taarifa ya huduma yangu kwa yesu.
ü Atatunza makadi na kuwapa walimu kila juma.
ü Ataandika kumbukumbu mbalimbali katika vikao vya baraza la SS.
ü Atatuma taarifa ya kila robo kwa mchungaji wa mtaa.
ü Ataandika majina ya madarasa yaliyopangwa 6-8, i- mtaa.
ü Atatunza kumbukumbu muhimu za kila darasa.
ü Hesabu ya waliotembelewa, hudumiwa n.k.
ü Mahudhurio ya wanadarasa kila mwezi.
ü Idadi ya misaa iliyotolewa na wana darasa.

Karani wa sadaka ya kupata faida
ü Atafundisha watu namna ya kupata/ kutoa sadaka hiyo k.m kwa njia ya kuuza magazeti, matunda, karanga, kuku,au kutenga mshahara wa siku moja.

Kiongozi wa upokeaji – Bawabu.
ü Wawe wachangamfu wajue lugha vizuri. Awe na uso wa machungwa sio malimao. Wageni wakaribishwe vizuri.
ü Bawabu asichanguliwe aliye na kasoro ya viungo, kiziwi, killema au bubu.
ü Wahamasishe washiriki kuwakaribisha wageni nyumbani, tufahamiane zaidi nao na kula nao.
ü Karibisha watu wote kwa furaha wenyeji na wangeni bila kuwabangua kuwa huyu ni mgeni wa kumkaribisha mwenyeji hapana.
Kiongozi wa vbs – (vocational bible school)
Ni kitengo ndani ya idara ya shule sabato. Ni shule ya Biblia wakati wa likizo. Shule hii imekusudiwa kuwasaidia wanafunzi wakati wakiwa wapo likizo ili kuweza kujishughulisha na mambo ya kiroho ili kuepuka mambo maovu na anasa.

Kitengo hiki ni sehemu ya uinjilisti kanisani kwa kuwa watoto hao wanaalika watoto ambao sio wa imani yetu ili kujifunza mambo mazuri.
Mambo ambayo yanapaswa kutendwa wakati huo wa likizo na watoto chini ya usimamizi wa kiongozi wa VBS na walimu wao ni kama ifuatavyo:=
·       Utaratibu wa program unaanza kwa kupandisha bebdera ya Taifa kisha wimbo wa Taifa unaimbwa
·       Nyimbo na mafungu ya biblia
·       Watoto wanajifunza yafuatayo:-
i)      Mashujaa wa Biblia
ii)    Kisa au hadithi.
·       Walimu kuita ya wanafunzi na kurundisha bahasha kwa wanafunzi.
·       Kucheza michezo mbalimbali kati ya walimu pamoja na watoto.
·       Kujinfuza juu ya maisha :- a.  wanyama – nature b. afya ya mwili.
·       Kupaka rangi picha zilizochorwa tayari.
·       Kurudisha vifaa- bahasha ya rangi.
·       Kuimba na kuomba kisha kutawanyika – kwaheri.

Waalimu wa shule ya sabato
Ø Wameitwa kwa ajili ya kazi kubwa ya kulea kiroho washiriki wa SS
Ø Daima wanatakiwa kuwa mfano mzuri katika hali ya kiroho kwa wale wanao waongoza.
Ø Waweze wao wenyewe kuwa wanafunzi wazuri wa Biblia.
Ø Wawe wasomaji wa lesson zao kila siku; na kuadaa hadidu za kurejea fupi/ ktk mada ya kufundishwa juma husika.
Ø Waweze kufahamu wanafunzi wao; kitabia/ mwenendo, uwezo wa uelewa, wanakoishi (mtaani).
Ø Waendeshe darasa  la lesson kama wahubiri.
Ø Wajue kuhusianisha somo la juma hudika na maisha ya wakati wanaoishi washiriki.
Ø Waweze kuonyesha namna ya ibada ya majadiliano yenye kicho, katika darasa.

Kazi za walimu wa shule ya sabato
Ø Kazi yao ni kuleta ushirikiano kiroho
Ø Kuhimiza washiriki kutoka katika ulegevu/uvivu wa mambo ya kiroho.
Ø Mwalimu asiwe mwimbaji bali mwibishaji yaani awe mwenyekiti wa mjadala sio mhubiri.
Ø Kuhakikisha kwamba kila mwanadarasa anacho kitabu cha masomo ya kasha la asubuhi, na kwamba anakisoma.
Ø Kuona kwamba wanadarasa wanatembeleana  angalau mara moja kwa juma; ili kupanga mipango ya kushuhudia majirani zao.
Ø Kuhakikisha kuwa kila mwana darasa anaelewa wajibu wake wa kuleta uhai wa darasa.
Ø Mwalimu n mwenyekiti wa darasa hivyo awe na katibu watakaye saidiana kuratibu uboreshaji wa mipango. Kutembleana wana darasa.

Darasa la walimu
Ø Darasa la walimu huanza saa 2:00 asubuhi. Kama ilivyodesturi ya nchi yetu ya Tanzania. Linashuriliwa kuwa lifanyike kabla ya sabato ili kwamba lisihalakishwe siku ya sabato asubuhi wanapokutana walimu kukamilisha mambo machache.
Ø Kadhalika kuligana na kanuni ya kanisa, sura ya 9, uk 14 toleo la 17 mwaka 2005; inashauriliwa kukutana katikati ya juma ili kujifunza/kujadili lesson na kuweka hadidu za rejea  za somo la juma hilo.
Ø Darasa la walimu linapangwa ili kuhudumia vizuri, matakwa ya kiini cha somo la juma husika.
Ø Waalimu wana takiwa kujifunza lesson kwa jinsi ya kufaidika na muktadha  somo.
Ø Wanatakiwa  wachangue maswali angalau matatu au manne, yaliyo kiini cha lesson amabyo yatapelekwa kwenye mjadala wa madarasani.
Ø Kiongozi wa SS anasimamia mjadala au kupanga mtu mwingine aendeshe darasa.
Ø Mzee wa kanisa anapaswa kuhudhuria ili kusaidia mahali penye utata juu ya mafundisho yetu makuu.

Vipengele 7 vya funguo za mafanikio ya vikosi vya shule ya sabato.
i)      Namna ya uendeshaji wa darasa.
ii)    Kujali washiriki wa darasa wanaokosekana
iii)  Mratibu wa kutunza muda.
·       Kupeana uzoefu wa kufundishana
·       Kuomba, kuhamasisha, na kutembeleana.
iv)  Matumizi ya lesson maishani
v)    Tathimini/ mashuri ya kiongozi
vi)  Ushirikiano wa karibu (corporate sharing)
vii) Mahusiano ya nyumbani/ tathmini.
Uendeshaji wa darasa.
i)      Kiongozi wa mjalada. (anatumia dk 5)
·       Kuangalia wale ambao wanakikosi ambao wamekosekana.
ii)    Mratibu wa uinjilisti (Dk.  Care coordinator)
·       Kutoa uzoefu unaohusiana na mpango wa darasa.
·       Kutoa mafunzo kulingana na uzoefu uliotolewa.
·       Kupanga mipango ya utembeleaji
·       Kuhamasisha mipngo ya darasa
·       Kuendesha huduma ya maombi kwa kikosi.
iii)  Msimamizi wa mjadala – kiongozi wa kwaya na sio solo(Dk. 35)
·       Kupitia mada za muhimu sana ndani ya lesson
·       Uliza maswali 3 au 4.
·       Hakikisha kila mtu anashiriki kutoa mchango.
·       Litumie somo katika maisha ya juma hili.
Mahitaji ya darasa
i)      Ukubwa wa darasa la watu 6-8
ii)    Kiongozi wa ushuhudiaji.
iii)  Mipango ya ushuhudiaji
iv)  Muda (dakika 25)
Makusudi ya shule ya sabato yazingatiwe:
i)      Malezi ya kiroho.
ii)    Usirikiano (mahusiano)
iii)  Ushuhudiaji kwa jamii
iv)  Utume ulimwenguni.

A.   IDARA YA VIJANA (ADVENTIST YOUTH – AY)
Idara hii ilianzishwa mahsusi kwa ajili ya kutumia nguvu ya  vijana iliyopo kanisani, kwa ajili ya wokovu wa wengine. Inaunganishwa vijana wote wenye umri wa miaka 6 mpaka 35 ndani ya kanisa. Nabii wa Mungu alionyesha kuwa kazi ya injili itafungwa kwa nguvu ya vijana watakapoungana na wazee katika  kutekeleza utume wa kanisa. Biblia inaeleza katika YOELI 2:28- 32. “Hata itakuwa, baada ya hayo, ya kwamba alitaminiwa robo yangu juu ya wote wenye mwili; na wana wenu wataona maono; tena juu ya watumishi wenu wanaume kwa wanawake, katika siku zile, nitaminiwa roho yangu…….”
 Vijana wanapaswa kujitambua kuwa wao wapo kanisani kwa ajili ya kutumika na kuokoa. Hili litawasaidia kujua baada ya wao kuokolewa basi wanajkukumu la kuongoa vijana wezao walio ndani ya kanisa   na walio nje ya kanisa.

Chimbuko la idara ya vijana
 Mapema katika historia ya waadvetista wasabto idra ya shuleeeee ya sabato ndiyo iliyoanza mapema mwaka 1852. Makusudi yake yalikuwa kutunza maisha ya kiroho ya watoto na vijana. Somo kuhusu vijana liliandaliwa na ndugu james white na kuchapwa mwaka huo 1852.
Wito ulikuwa mara kwa mara ka nia ya maadishi ya Ellen G. white ya kutaka kuwaunganisha vijana wote katika jeshi kusaidia kumaliza kazi kubwa ya kuchukua ujumbe wa marejeo ulimwenguni. “Nabii alitangaza kwamba kila kijana kila mtoto, ana kazi ya kufanya kwa ajili ya utukufu wa mungu.”  (Ed. Uk. 58)
Mwaka 1879 Harry Ferner (miaka 16) na Luther warren (miaka 14) walipata wazo la kuona kuwa vijana angekuwa na umoja Fulani ambao ugewaunganisha vijana na kuleta ufanisi wa kazi ya mungu katika kanisa. Vijana hawa waliishi USA, michigani  kitongoji cha Hazzeeton. Siku moja waliandaa mkutano kwa ajili  ya wavulana tu katika chumba kidogo cha luther katika nyumba ya wazazi wake. Lengo lake ilikuwa kuhamasisha kazi ya umishenari na vitabu na baadae mambo ya afya ya wazi.baadae wasichana walikaribishwa kujiunga. Baadae mkutano uliendelea kupanuka ukawa mkubwa sana hata wazima katika familia ile wakahudhuria.
Agenda ya namna ya kuwasaidia vijana ililetwa kanisani kupitia wazazi wa wale vijana. Ferner na  wenzake waliombwa  kuendele kuwatia moyo vijana wenzao wavulana na wasichana. Kadri mpango huu ulivyoendelea kuimarika hatimaye ulikubarika  na general conference. 1889 G.C ikaita umoja huu kwa jina la “Christan Volunteers.”
Mwaka 1901 idara ya shule ya sabato iliunganishwa na idara ya vijana ili kuendesha shughuli zao vizuri. Mwaka 1907 idara hizi mbili zikatenganishwa mwaka 1907 idara ya vijana ilipewa jina lililokubarika katika general conference nalo ni missionary volunteers (M.V) yaani wafanya kazi ya umisheonari kwa kujitolea. Mkurugenzi alikuwa mchungaji M.E Kern. Vita ya kwanza ya dunia iliathiri sana shughuli za idara hii ya vijana. Lakini mambo kama hiking, michezo, kusimulia hadith, sanaa, ufundi, na kambi za moto ili kukithi mahitaji ya vijana yaliendelea kufanyika. Baadaye chama kiliendelea kuimarika. Mwaka 1926 kambi la kwanza la vijana lilifanyika huko Michigan, USA, ilikuwa lenye mvuto mkubwa sana kwa vijana.

Historia ya AJY (Advenist junior youth) vijana wadogo.
          Mwaka 1919 ndugu A. W spalding alianzisha chama cha skauti cha kimishenari cha vijana wadogo huko madson, Tannessee, chama hiki kilikuwa cha vijana wadogo wa kime na vijana wa rafiki za vijana hao. Mambo yaliyosisitizwa yalikuwa ufundi wa kazi ya uselemala na ukabikaji. Walijiwekea sheria, ahadi na kusudi ambayo baadaye wana M.V walifuatisha.
          Mwaka 1920 baraza la general conference lilikutana na kupitisha ndugu hot kuwa katika idara ya vijana kama msaidizi wa katibu wa M. V ili yeye ahamishe watoto ambao walijulikana katika mwaka huo kuwa J.M.V (junior missionary volunteer) vijana wadogo wa kimishenari wa kujitolea.
          Mwaka huo huo 1920 madarasa ya vijana wadogo yalianzishwa. Mwaka  1928 mafunzo ya uongozi  yalianzishwa  kufundisha viongozi waliojulikana kama master comrades (baadaye waliitwa master Guides).
Mwaka 1946 chama cha watafuta njia kiliazishw ahuko California ya kusini na ndugu juhn Hancock. Tangu mwaka 1947 – 1940 program za watafuta nija ziliendelea kukua. Ilipofika mwaka 1950 baraza la general conference lilianzisha chama cha watafuta njia.
          Mwaka 1978 jina lilibadisha kutoka M.V (missionary volunteer) na kuwa A.Y( Adventist youth) yaani kijana wa kiadvetista.
          Kwa kuzingatia vipawa mbalimbali walivyonavyo vijana, viongozi waliazisha  shughuli za madarasa mbalimbali yakiwepo yale ya kujifunza Biblia, viumbe vya asili, ujuzi wa nyumbani, shughuli za kambi, huduma ya kwanza, afya ya nyumbani, mazoezi ya viungo, huduma za jamii na shughuli   nyingine za kushuhudia.
          Mwaka 1927 Baraza la General conference liliazisha madarasa mabalimbali ya mafunzo yaliyoitwa  rafiki, mwenzi, na comrade kwa ajili ya vijana wadogo  na daras moja la watu wazima.
          Mwaka 1928 nishani mbalimbali ziliznazishwa na darasa la master comrade liliendelea kuimarishwa, ambalo baadae liliitwa master Guide. Wahitimu wa kwanza wa master guide walivikwa pini za o mwaka 1931.
          Madarasa ya MV na JMV ambayo baadaye yameitwa AY yamebuniwa ili kuwasaidia vijana kukua kimwili, kiakili, kiroho na kijamii.yamethibitishwa kuwa yanafaa kujenga tabia, na yamekuwa mbaraka kwa maisha ya maelfu ya vijana.
          Chama cha wafumbuzi (Advenist Adventurer club) kiliazishwa na general conference maka 1979.

A.   Ufafanuzi wa vyama vya idara ya vijana.

      I.          A. Y Advetista Youth ( vijana wa kiadventista) miaka 6-35. Hii ni idara inayounganisha vijana  wote wa vyama vitatu vinavyounda idara ya vijana navyo ni:-
1. Adventist Adventurer club (chama cha wafumbuzi) kinchochukua watoto wote wa miaka 6- 9 (A.C)
2. Advetist pathfinder club ( chama cha watafuta njia ) kinachukua  watoto wote wa   miaka  6-9 ( A.C)
3. Advestist senior Youth ( chama cha watafuta njia ). Kinachukua watoto wote wa miaka  16-35 (A.Y )kiufupi chake kinafanana na kile cha Advest youth ( jina la idara).
   II.          A.J.Y – Adventist junior youth (vijana wadogo wa kiadvetista.)
(miaka 6-15). AJY ina unganisha vyama viwili A.C na P.F.C .
i)      A.C – chama hiki kina madarasa manne kuligana na umri wao.
Miaka 6 darasa la nyuki wa shughuli {busy bee)
Miaka 7 darasa la mwali wa jua (sun beam)
Miaka 8 darasa la mjenzi (Builder )
Miaka 9 darasa la mkono wa msaada (helping hand)
ii)    PFC Chama  hiki kina madarasa sita kuligana na umri wao
Miaka kumi darasa la rafiki (friend)
Miaka 11 darasa la mwezi (companion)
Miaka 12 darasa la mgunduzi (Explorer)
Miaka 13 darasa la msimamizi (ranger)
Miaka 14 darasa la msafiri (voyager)
Miaka 15 darasa la kiongozi (guide)
III.          A.Y.S (Advetist youth services) hawa ni vijana ambao wameamua kufanya huduma mbalimbali za kanisa kwa njia ya kujitolea na kwa gharama zao. Mpaka sasa kuna wanachama  4,000 tu duniani. Tanzania hatujapata ata mmoja .

B.   Adventist senior Youth (A. Y) Chama cha vijana wakubwa.
Madhumuni:-
          Katika roho ya unabii kumeelezwa madhumuni ya chama cha vijana wakubwa kama ifuatavyo:-
i)      Kuwaelimisha vijana kufanya kazi kwa ajili ya vijana wenzao.
ii)    Kuwaandaa vijana kusaidia kanisa lao na wale watunzao sabato.
iii)  Kufanya kazi kwa ajili ya wale wasio na imani yetu (sign of the times, may 29, 1893).

Katika kutimiza madhumuni haya vijana
·       Wataomba pamoja
·       Watajifunza neno la mungu pamoja
·       Watashirikiana pamoja katika maburudid\sho ya kikrsto.
·       Kushuhudia pamoja katika vikundi vidogo vidogo.
·       Kukuza mbinu, ujuzi na talanta katika huduma ya bwana wetu.
·       Kutia ndugu kila mmoja kila mmoja wetu katika kukua  kiroho.
Kanisa linfanya kazi zake mbalimbali kupitia chama hiki cha vijana wakubwa wa kiadvetista. Katika mipango yote ya kanisa program  za Vijana zisitengwe na shughuli nyingi za kanisa vijana  wahusishwe katika majukumu ya kanisa  ya uongozi na program zote za kanisa zima.kunapaswa kuwe na wazee wa kanisa vijana, mashemasi vijana wa kike na wa kiume, n.k huku  wakifanya kazi na maofisa wenye  uzoefu katika kona zote za kanisani. Vijana wanapaswa kuwa moto.

Madondoo ya Roho ya unabii:
Chama cha vijana ndicho pekee kinachoweza kuwafanya vijana wajisikie kuwa na furaha wanaposhiriki shughuli za kanisa kwa pamoja. Umuhimu wake umeridhika baada ya kuchunguza madhumuni yake ambayo ni:-
·       Kutunza changamoto ya kusundi, moto na ahadi mbele ya chama,
·       Kumfanya kila mmoja awe na moyo wake ujitoao ndani ya chama.
·       Kuhamasisha sura ya chama cha AY na shughuli za kivikosi katika kufikiri na maisha ya chama.
·       Kuwaunganisha vijana na kanisa na wana AY wote ulimwenguni
·       Kumpa kila mwanachama  uzoefu wa kuzungumza mbele ya watu,kufanya kazi pamoja, kuomba pamoja, kujifunza pamoja na kupanga pamoja.
·       Kuwafundisha vijana kanuni ya maisha ya kikristo na kuwasaidia vijana kupata suluhisho la matatizo yao.
·       Kujifunza mbinu mbalimbali zilizo bora za huduma za kikristo na vijana kuwa na vikosi vya kushuhudia.
·       Kutoa mvuto bora wa kushiriki wa kikiristo kwa vijana wa kanisa .

C.   Kijana mwadvetista afanye vipi.
Mawazo ya kijana mwadvetista yameelezwa katika KUSUDI, MOTTO, AHADI  na SHERIA.
i)      Mdhumuni ya mwana A.Y
“Kutoka dhabini na kuwaogoza katika utumishi.” Kupata wokovu katika maisha ya vijana ni muhimu sana. Wafundishwe mamfundisho ya imani yetu na waweza  kujitoa kwa kristo. Kisha washirikishwe katika shughuli za kanisa. Kwa kuwa shughulika tunawaandaa kuwa watumishi bora na kwa njia hiyo wanalindwa na uovu.
·       Vijana wenzao (MYP. UK 208,204,207)
·       Kanisa lao (Ed. Uk 269, MYP uk. 220, FCE. Uk. 488)
Madhumuni hayo matatu ndiyo ambayo Mungu ametupa katika kuifanya kazi yake.
ii)    Kusudi la mwana A.Y
“Ujumbe wa mrejesho katika ulimwengu wote wa kikazi hiki.” Ujumbe injili ambayo vijana wataibeba ulimwenguni mwote – maneno mbalimbali ambayo vijana watapeleka ujumbe huu katika kizazi hiki. Vijana hapaswi kujua ujumbe tu wa kiadvetista, bali kwamba yesu atarudi upesi na maisha yao yaonyeshe kwamba kwa katika wanaamini hivyo.
iii)   Moto wa chama cha AY
“upendo wa kikristo watubidisha” 11 kor. 5:14 bila upendo wa kikristo kutakuwa na kushindwa njiani, kwa upendo wa yesu mafanikio ni ya hakika.
iv)  Ahadi ya chama cha AY
“nikimpenda bwana Yesu, naahidi kuchukua sehemu ya juhudi yangu katika kazi za chama cha vijana waliojitolea kumtumikia kristo, kufanya yote niwezayo kuwasaidia wengine na kuimaliza kazi ya injili kwa ulimwengu wote.”
Vijana wa kiadvetista wanaweza kufanya mambo manne ili kumaliza kazi:-
·       Kuishi maisha ya kujitolea.
·       Kuwafanya wapatikane katika kila nafasi ya kuokoa.
·       Kuombea kazi ya Mungu kanisani na ulimwenguni.
·       Kujitolea kwa hali na mali katika kuendekeza na kumaliza kazi ya injili. Kwa kufanya hivyo watakuwa wameingia katika uwakili wakatoa muda wao, vipawa vyao, fedha zao, na wao wenyewe.

D.   Maofisa wa chama cha AY
i)      Maofisa wanaochanguliwa na kibaraza cha uchanguzi wa kanisa
o   Kongozi
o   Kiongozi msaidizi
o   Katibu/mhazini
o   Katibu /mhazini msaidizi
o   Mshauri

ii)    Wengine wanachanguliwa na wanachama wenyewe wa A.Y
o   Kiongozi wa nyimbo
o   Kiongozi wa mawasiliano
o   Kiongozi wa nidhamu
o   Kiongozi wa elimu
o   Kiongozi wa mambo ya ushirika (fellowship)
o   Viongozi wa vikosi;-kikundi cha maombi na kazi za binafsi
·       Kikundi cha kusaidia cha kikristo (washiriki)
·       Kikundi cha uinjilisti
·       Kikundi cha uimbaji n.k
·       Vikundi hivi vikishaundwa  vitadumu kwa miezi mitatu au miezi sita ili kutoa uzoefu kwa vijana wote kushiriki kwenye vyote

Wanaounda baraza la chama cha A.Y
·       Kiongozi                                                        - mwenyekiti
·       Kiongozi msaidizi                                          -mjumbe
·       Katibu mhazini                                              -mwandishi wa baraza
·       Katibu mhazini                                              mjumbe
·       Mshauri                                                         -mjumbe
·       Kiongozi wa mawasiliano                              mjumbe
·       Kiongozi wa nyimbo                                     -mjumbe
·       Mkuu wa nidhamu                                         -mjumbe
·       Kiongozi wa elimu(mkutubi)                         -mjumbe
·       Kiongozi wa ushirika                                     -mjumbe
·       Viongozi wa vikosi                                        -wajumbe
·       Mkurungezi wa (PF)                                      -mjumbe, mwalikwa
·       Kurugenzi wa huduma za kanisa                   -mjumbe,mwalikwa
·       Mzee wa kanisa au mchungaji aua wote         -wajumbe, mwalikwa.
Maofisa wote ni wajumbe wa baraza.
Vikao vya mwezi: kutakuwa na vikao vya kila mwezi (angalau kila mwezi) ili kujifunza na kupanga pamoja.
Vikao vya juma: kuwe na vikao vya muda mfupi kila jumakwaajili ya kuomba pamoja na kushauriana kuhusiana na yaliyopo pamoja na kujadili mambo ya dharura yanayojitokeza.

E.   Wajibu wa wana baraza wa A.Y
1.    Wataomba pamoja kama tmu ya maofisa
·       Watachukua mizigo war oho za vijana wote kanisani.
·       Watakuwa na orodha ya vijana wote (miaka 16-35)
·       Wawaone vijana waliokata tama na wengine wasioogoka.
·       Wawatie moyo kuhudhuria kanisani na kufanya shughuli za kanisa.
2.    Wawe wajuzi wa mafundisho yote ya AY
·       Wajifunze kitabu cha “messages to young people .” Youth Ministry, Training Course na maarifa mengine ya vijana kwa kadri yanavyowez kupatikana.
3.    Kupanga mikutano ya A.Y “Yule anayeshindwa kuanzaa, anajiandaa kushindwa.
4.    Kutathimimi taarifa za chama
5.    Kuchunguza kumbukumbu za chama kila mwisho wa mwezi na kwamba taarifa zitumwe field/conference kila roho.
6.    Kuchunguza mahitaji ya pesa na matumizi yake.
7.    Kupanga shughuli 1 za maburudisho yale ya kikristo na shughuli za ushirika.
8.    Kupanga mipango ya juma la maombi la vijana.
9.    Kuhamasisha haja ya elimu ya kikristo.
10.Kudhamini master Guide club na A.Y club.
11.Kukuza moyo wa utii kwa vijana utakao waongoza.
12.Kushiriki huduma za kiroho za kila juma.
13.Kurudisha kwa uaminifu zaka na sadaka.
14.Kusisitiza majuma ya maombi na maombi kwa ujumla.
15.Kujaza nafasi za uongozi pale ambapo pana pengo la viongozi.
16. Kuendelea kupokea wanachama wapya.

F.   Kazi za kila ofisi wa AY
     I.          Kiongozi wa AY
·       Aelewe vizuri mipango ya chama
·       Awe karibu na mkurugenzi wa field
·       Kupanga ratiba ya baraza  la A.Y
·       Atakuwa karibu na mshauri wa vijana
·       Atawapa madaraka viongozi wengine kwa kadri uwezavyo.
·       Mwenyekiti wa baraza la A.Y
  II.          Kiongozi msaidizi wa A.Y (Kazi zake)
·       Atafanya shughuli za kiongozi wa AY (watasaidiana)
·       Atasaidiana na kiongozi kujulisha baraza la kanisa mahitaji ya vijana kwa ujumla.
III.          Kazi za mshauri au mdhamini wa vijana
·       Mjumbe wa baraza la chama na baraza la kanisa
·       Ayajue madhumuni ya chama na njia za kuendesha program
·       Yeye ni mshauri na kiongozi wa kiongozi wa chama na maofisa wake
·       Ni mshauri wa matatiz ya vijana binfsi.
·       Atasaidiana na kiongozi kuwasilisha mahitaji ya vijana kwenye baraza la kanisa
IV.          Katibu mtunza hazina (kazi zake)
·       Mjumbe wa baraza la vijana na mwadishi wa miniti na mtunza warekodi za yale yaliyoamuriwa na baraza.
·       Kutunza majina ya wanachama wote na anuani zao katika kitabu
·       Atatoa taarifa za maendeleo ya chama.
·       Atawaelimisha vijana taarifa za kazi zao kila robo
·       Atatunza majina na anuani za viongozi wa chama
·       Atatunza orodha ya wale wanaochukua kozi ya uongozi wa watafuta njia ( master Guide) na wale wanaochukua kozi ya kiongozi mwadvestista.
·       Atapeleka taarifa za kuhitimukwao kwa mkurugenzi wa vijana wa fied, pini zitolewazo na vyeti
·       Atapokea fedha na kuzitunza hazina kwa mtunza hazina wa kanisa akiambatanisha risiti yake
·       Atatoa taarifa ya fedha kila mwezi kuonyesha mapato na matumizi yake
·       Ataangiza vifaa vya chama kutoka ofisini ya field kwa kadri atakavyo ruhusiwa na baraza la chama.
   V.          Kazi za katibu mhazini msaidizi
·       Mjumbe wa baraza la chama cha AY
·       Atafanya majukumu yote ya katibu mhazini wa chama.
VI.          Kazi za kiongozi wa nyimbo wa wa nyimbo wa chama
·       Mjumbe wa baraza la chama
·       Atawajibika na shughuli zote za nyimbo za chama
·       Atashauriana na viongozi ili ili nyimbo ziende sambamba na mtoa mada kuhamasisha uimbaji bora kwa vijana
VII.          Kazi za kiongozi wa mambo ya kiroho
·       Mjumbe wa baraza la AY
·       Atashauriana na wanabaraza kuunda vikosi vya maombi
·       Atawashauri wanachama kujenga moyo wa kujitoa wakfu katika mikutano ya chama na shughuli za kanisa
·       Program za maombi kwenyekwenye vikosi zifanyike
·       Atakuwa mwanafunzi wa Biblia na kupata orodha ya wale wote wanaosoma Biblia kwa mwaka na kasha la asubuh
·       Atawaelimisha vijana namna ya kutunza Biblia na kila mmoja kwa nayo ya kwake na kuja nazo kanisani
·       Kutoa taarifa kwa katibu wa chama juu ya wale walihitimu usomaji wa biblia kwa mpango na kutumwa kwa mkurugenzi wa field/ conference
·       Atasimamia masomo ya juma la maombi la vijana na kupanga ratiba ya wahudumu.
·       Atawatia moyo vijana kusoma vitabu vya robo ya unabii.
VIII.          Kazi ya kiongozi wa elimu- mkutubi
·       Mjumbe wa baraza la AY
·       Atakuwa na orodha ya majina ya wanachama
·       Atakuwa na orodha ya wale wanaosoma vitabu vilivyopangwa
·       Kila mwezi atapeleka majina ya wale waliohitimu kusoma vitabu vilivyopangwa kwa katibu ili majina hayo yatumwe kwa mkuruugenzi wa field/conference
·       Atawahamasisha vijana kuanzisha maktaba zao
·       Atawahamasisha vijana kusoma vitabu mabalmbali
  
IX.          Kazi za kiongozi wa mawasiliano
·       Mjumbe wa baraza la chama
·       Afahamu mipango ya chama ili aandae matangazo, mada zitakazofundishwa na matukio maalumu kwa mujibu wa kalenda ya chama
·       Kupeleka matangazo ya chama kwa uongozi wa kanisa ili yatangazwe
·       Anaweza kuwa na kamera kwa ajili ya kumbukumbu za matukio ya matendo ya vijana na kuyabandika kwenye ubao wa matangazo
   X.          Kazi ya kiongozi wa maburudisho
a.     Mjumbe wa baraza la chama
b.    Atahusiana na wanabaraza juu ya maburudisho yafuatayo kwa mujibu wa roho ya unabii na Biblia
Ataongoza katika kupanga shughuli za ushirika
a.     Atawakaribisha wageni wote wanohudhria mikutano ya chama
   II.          Kazi za kiongozi wa kikosi
a.     Mjumbe wa baraza la chama
b.    Atawajibika katika shughuli za kushuhudia  za kikosi
c.     Atakuwa na karani wa kikosi ambaye atatunza yafuatayo
                                                   i.     Nini kifanyike
                                                 ii.     Wapi kifanyike
                                               iii.     Nani ameshiriki katika kazi
                                               iv.     Atatoa taarifa ya kikosi
III.          Kazi za mabawabu
a.     Watahakikisha kuwa viti vya mbele vipo sawa
b.    Watafunga madirisha au kuwasha taa na feni
c.     Watahakikisha chumba kimepangwa vizuri kabla ya mkutano kuanza
d.    Watachukua sakaka na kumkabidhi katibu mhazini

IV.          Uanachama
Vijana wa miaka 16 – 35 wanapojiunga na chama wanapaswa kukubali ahadi hii,  “yesu, naahidi kuchukua sehemu ya juhudi yangu katika kazi za vijana wajitoleao kumtumikia kristo na kufanya yote niwezayo kuwasaidia wengine, na kuimaliza kazi y ainjili katika ulimwengu wote.

Kuna aina tatu za uanachama
1.    Wanachama wa kawaida  -(miaka 16-35) ambao ni waadvetista wasabato wanaopenda kumtumikia bwana wao
2.    Wanachama wachagamana – hawa ni vijana ambao hawajaamua kuwa waadvetista wasabato lakini wanapenda program zetu.
3.    Wanachama wa heshima- hawa ni watu wazima walio pita umri  wa miaka 35 lakini wao wanapenda kuendelea kushiriki za vijana.
·       NB: kijana anayekubari ahadi, moto na kusudi na kuwa mwanachama pia anakubali changamoto kuwa na sehemu ya kumaliza kazi ya injili.
   V.          SARE ZA AY
Sare ni sehemu ya utambulisho wetu. Kwa mjibu wa idara ya vijana kanda ya mashariki mwa Africa ilipitishwa kuwa sare AY itakuwa kama ifuatavyo:-
·       Sketi/suruali           -kijivu
·       Shati/blouse           -light blue au nyeupe
·       Tai                         -damu ya mzee
·       Kiatu                      -nyeusi
·       Koti                       - Nevy blue
Kadri ambavyo mmeamua kuchangua aina Fulani ya kijivu katika kanisa lenu kila mmoja ajitahidi ya aina hiyo. Kwani kijivu kimegawanyika katika aina mbalimbali.
          Sare ya AY imeandaliwa au kubuniwa rasmi kwa huduma za ibada na mafundisho mbalimbali ndaniya kanisa.

Sare ivaliwe wakati wa matukio ya program za wana A.Y.
          Ikubukwe kuwa namna ya kuwa mwanachama wa chama hiki ni kwa hiari ya kila kijana. Na kipimo cha kijana hai AY ni kujiandikisha kila mwaka na kuwa na pia kutoa michango ya chama au ada, na pia kushiriki katika shughuli mbalimbali za chama.

Majukumu mengine ya idara ya vijana wakubwa
          Kiongozi wa AY anapaswa kufanya mambo yafatayo:-
Ø Kiongozi  wa AY anapaswa awe ni mtu aliyepitia kozi ya kiongozi mkuu yaani ‘masterguide’.
Ø Kuongoza vijana kuunda vikundi vidogo vidogo vya kushuhudia na kujifunza pamoja neno la mungu.
Ø Vijana waweza kuomba pamoja na kutembeleana kwa ajili ya kutiana moyo.
Ø Kushirikiana pamoja katika maburudisho mbalimbali kama vile Bible conference, picknick, na kutazama viumbe vya asili, n.k
Ø Kupanga na kuhamasisha vijana kuhudhuria makambi mbalimbali.
Ø Kufundisha miongozo mbalimbali na mafunzo yahusuyo vijana na pia kutafuta wakufunzi waliofaulu katika mambo ya vijana.
Ø Kuendeleza talanta na vipawa walivyonavyo vijana kwa kushirikisha vijana katika program mbalimbali.
Ø Kuongoza vijana wajue namna ya kushuhudia kwa ajili ya vijana wasio wa imani yetu na pia kuamsha vijana ambao wamepoa ndani ya kanisa.
Ø Kuhakikisha kanisa linatumia vijana ambao wamepoa ndani ya kanisa.uongozi kanisani. Hii ni katika kuwapangia kazi za kufanya ili wawe sehemu ya kanisa. Kwani kanisa lolote linajengwa na asilimia 80 litazuia kwa kiasi kikubwa uasi kanisani. Kisa cha malangali: kanisa lote ni vijana chini ya miaka 35 kasoro watu wawili tu.
Ø Kuandaa mataala wa kozi ya kiongozi mkuu ili kijana ajifunze kozi hiyo. Hili litawandaa vijana kuwa viongozi bora kwa kupitia kozi hii.

HUDUMA ZA CHAMA CHA MABALOZI






Nembo ya kwanza ina jina la Ambassadors. Wengine wanatumia hii isiyo na maandishi. Hivyo chama hiki kina nembo yake ambayo ni rasmi kwa kanisa la ulimwengu. Hiki ni chama kipya ndani ya kanisa ambacho kimeanza mwaka 2009. Chama hiki ni cha vijana wenye umri ambao ni wa miaka 16-21 wanaojulikana kama ‘late adolesencent’ (rika la vijana wakubwa waliobalehe)
          Tangu huduma za idara ya vijana zilipoanzishwa kanisa la waadvetista  wasabato, idara ya vijana katika divisheni mbalimbali likagudua kwamba vijana wanaomaliza matakwa wa chama cha watafuta njia wanaachwa bila kuwa na program zinzokidhi  mahitaji yao. wanatamani kuendelea katika chama cha watafuta njia, na wakati huohuo wanajikuta kwamba hawako tayari kujiunga na chama cha vijana wakubwa katika kikao cha mwaka 2001 na uongozi wa vijana ulimwenguni kilichofanyika huko Brazil, kilichukua azimio muhimu kwa kuita idara ya vitini kwa ajili ya kundi la vijana wa miaka 16-21, ili kukidhi mahitaji yao ndani ya kanisa     la waadvetista wasabato. Mtaala wa mabalozi ni matokeo ya mazimiano hayo.
          Kumbuka kwamba, chama cha mabalozi sio mbadala wa chama cha vijana wakubwa, baada yake kitawaimarisha vijana hawa wakubwa wa miaka 16-21 katika kanisa letu. Hatua hii mpya imekusudiwa kutengeneza muundo na kuandaa njia ambazo vijana hawa wa miaka 16-21 watakuwa hai katika kulitumikia kanisa, kanisa mahalia na ulimwengu kwa ujumla.

Tamko la utume.
Chama cha wavumbuzi ni chama katika kanisa la waadvetista wasabato kilichowekwa wakfu kukidhi mahitaji ya kiroho, kijamii, na mtindo wa maisha kwa vijana wa umri wa miaka 16-21 kwa kuwaptia changamoto ya uzoefu, na kuwashirikisha wengine juu ya uhusiano binafsi na yesu kristo, kukuza mtindo wa maisha utakaokidhi mahitaji ya imani yao, na matamanio yao, na  kuwapatia fursa bora za ukuaji wa ujumla wa urafiki unaodumu.



Kusudi.
          Ujumbe wa marejeo katika ulimwengu wote wa kizazi chnagu. Uhusiano wangu na yesu kikristo wa asili ya moyoni, na ndio unaonisukuma kumshirikisha yeyote aliyetayari kuupokea, injili- bahari njema za kuja kwa yesu upesi.

Motto
Upendo wa kirsto wanibidisha. Nimesongezwa kwake kwa mfano wa maisha  yake, kwa tukio la kusulubiwa kwake, ushindi wake, na kwa ahadi yake ya kuifanya dunia upya katika muktadha wa jinsi ilivyokuwa wakatia wa uumbaji. Kwa kadri ninavyokuwa karibu naye, ndivyo ninavyojisikia kuwa karibu na mahitaji ya binadamu wezangu.

Chama cha watafuta njia-(pathfinder club).
          Chama hiki kinawaandaa watoto kutafuata njia ya kuelekea  ukubwani kwa kuachana na mivuto mibaya ya dunia. EFESO 6:1-4.
          wanachama wake ni umri kuanzia miaka 10 had 15. na pia wanachama wake ni watoto wa washiriki, washiriki wenyewe {waliobatizwa), na wale ambao watoto au wazazi wao sio wa imani yetu.
Kanisa liandae masomo yao au mitaala yao kwa kumsaidia mwalimu.sehmu kubwa wao wawe ni wale ambao nia masterguide mafunzoni kama sehemu ya kukamilisha matakwa ya kozi yao ya masterguide.
Ni kipindi kibaya cha umri maana wengi wao ni umri wa kubalehe. Hivyo inahitajika umakini zaidi katika kuwafundisha .
Nembo ya chama ina pembe tatu.
Kiongozi wa PF anapaswa kufanya mambo yafuatayo:-
Ø Kiongozi ahakikishe watoto hawa wafundishwe katika makundi mawili;wale wa umri miaka 10-12 na wale wa miaka 13-15 wasichanganywe mara kwa mara katika mafundisho yao.
Ø Kiongozi anapaswa kuandaa camporee yao kila mwaka ambapo watajifunza mambo mbalimbali.
Ø Wafundishwe namna ya kuwaogoa watoto wenzao kwa uundaji wa vikosi vya kushuhudia na ugawaji wa vijizuu na mialiko kwa watotowenzao kanisani.
Ø Kuwafundisha masomo ya ufudi wa kazi ya mikono.
Ø Kujifunza Biblia hasa mafundisho makuu ya kanisa. Kukariri kusiwe sehemu kubwa tena. Bali wajue namna ya kufundiasha Biblia.
Ø Kuwe na matembezi mashambani ili wajifunze viumbe vya asili kwa vitendo na matembezi ya kuapnda milima.
Ø Wafundishwe namna ya kutunza uniform zao. Wajue wakati gani wa kuvaa na usio wa kuvaa uniform.
Ø Wafundishwe namna ya kutengeneza mahema yao na namna ya kukambika kwa kuweka kambi mbali na nyumbani.
Ø Kuhamasisha wazazi kununua uniforma zao.  Uniform ni uinjilisiti tosha kwa chama

Chama cha wavumbuzi –(Adveturer Club).
 Chama ambacho kimeazishwa mahsusi kwa watoto wadogo. Hasa kwa kusaidia watoto wale ambao wako kanisani lakini hawasomi katika shule zetu za ki-advetista. Hivyo ikiwa kanisa linaprogram madhubuti katika chama hiki, basi ni hakika watoto wetu wataokolewa kutoka katika maagamizi ya mafundisho yaliyopo katika dunia hasa katika mashule yasiyo ya kanisa.
Watoto wanaitwa wavumbuzi maana umri wao upo katika shule za msingi hivyo ni wadadisi kwa mambo mengi. Ni watoto ambao sehemu ya ubogo haijajaa bado inahitaji kunasa mambo mengi. Ubongo unanasa kila kitu chema au kibaya.
Wanachama wake ni wa umri kuanzia miaka 6 hadi 9. Chama hiki kinajumuisha wanachama wale ambao ni watoto wa washiriki na pia ambao wazazi wao washiriki.
Walimu wanapaswa kuwa wavumilivu maana umri huu ni wasumbufu kwa kuchokozana, kucheza kwingi, kudeka, na ujeuri.
Kanisa linapaswa kuhakikisha kuwa chama kinakuwa na miogoni yao ambayo inapatikana kwenye ofisi ya idara ya vijana field au konferensi.

Kazi ya kiongozi wa chama hiki ni kufanya haya:
§  Kiongozi anapaswa kutumia mitaala yetu kwa ajili kuwaandaa watoto hawa kujiunga na mafunzo mengine baadaye katika chama cha watafuta njia- P.F.
§  Kuwatafuta walimu wenye wito kwa watoto na wenye kupenda watoto na aliueogoka kwelikweli kisha wapitishwe kwenye baraza la kanisa.
§  Kufundisha watoto mafundisho yanayohusiana na kanisa letu kwa kujenga msingi uliobora kwa ajili ya maisha ya ukubwani.
§  Kuhakikisha watoto wanapitia madarasa yao kama ifuatavyo:- Rafiki,mwenzi, mvumbuzi, na msimamizi
§  Kiongozi awafundishe usanii,ustadi wa magari, namna ya utengenezaji wa mahema, na viumbe vya asili.
§  Kufundishwe kukariri mafungu ya Biblia kwa kuanza na mafungu mafupi mafupi ili wazoee kuhariri na pia wajifunze kwa njia ya picha wataelewa zaidi.
§  Kiongozi ahakikishe wanachama wawe na uniform. Hata wale wazazi sio waadvetista au ni maskini basi kanisa liandae urtaratibu wa kuwashonea maana si vyema wengine wawe nazo na wengine wasiwe nazo. Jambo hili linawaumiza watoto kisaikolojia.

A.    KWAYA YA KANISA NA VIKUNDI VYA UIMBAJI
      Zamani na kwa miaka mingi ilijulikana kuwa kwaya ni kitengo ndani ya idara ya vijana. Kumbe sivyo ilivyo. Kwaya ni kitengo ambacho ni mali ya kanisa lote. Ipo chini ya mchungaji na wazee wa kanisa. Ipo chini ya utawala wa kanisa. Kumbuka idara ya vijana inaweza kwa na kwaya yake na itaitwa kwaya ya kanisa ya idara ya vijana.
Kwaya ya kanisa ni chombo kinachotumika kutoa muziki wa kikristo. Kwa sababu muziki unamvuto mkubwa katika mema na mabaya, basi uchanguzi wa makini utumike katika kupata waimbaji bora. Ijulikane kuwa kwaya ina kiongozi wa kwaya na sio mwenyekiti wa kwaya. Mwenyekiti wa kwaya ni mchungaji au mzee wa kanisa.
Ø Kanisa lapaswa kuwa makini kupata viongozi bora kwaya. Hili litaepusha migogoro inayoletwa na viongozi ambao wanatumia kikundi cha kwaya kwa manufaa yao kwa kuanzisha malumbano ndani ya kanisa.
Ø Viongozi wa kwaya watende kazi kwa ushirikiano wa karibu na mchungaji na wazee wa kanisa. Hili litawezesha malezi ya kiroho kwa waimbaji na wanakwaya kwa ujumla kufanikiwa.
Ø Kanisa lapaswakusajili vkundi vyote vya uimbaji kwa majina yao na wanachama  wao ili kuthibiti mwenendo na maadili mabaya yasipitie katika vikundi hivyo vya uimbaji.
Ø Viongozi wa vikundi vya uimbaji wanapochanguliwa basi wajulikane   kwa kanisa kwa mawasiliano ya karibu na kupata maelekezo mbalimbali au kutumika ndani ya kanisa.

Sifa za kiongozi wa kwaya na waimbaji wa kwaya
Ø Kiongozi wa kwaya kuwa mshiriki wa kanisa mwenye msimamo mzuri.
Ø Kiogozi wa kwaya awe ni mtu aliyeongoka vyema kani anaweza kuleta uasi kwa sababu ni kikundi chenye mvuto sana ndani ya kanisa.
Ø Kiongozi wa kwaya anapaswa asimamie na kuzielewa taratibu na kanuni za kanisa vyema. Hivyo aongoze kwaya chini ya taratibu hizo.
Ø Waimbaji wa kwaya wawe ni waumini wenye msimamo mzuri ndani ya kanisa.
Ø Waimbaji wa kwaya wawe ni washiriki wa kanisa au wa shule ya sabato au wanachama wa idara ya vijana.
Ø Muimbaji au waimbaji wasiwe ni watu waliochukuliwa hatua za kinidhamu za kanisa kama vile kalipio aua kuondolewa ushirika.hawaruhusiwe kuimba wanapokuwa katika kipindi hicho cha hatua za kinidhamu.
Ø Tabia zao ziendane na zipatane na mwenedo wa mkristo katika mavazi na muonekano wan je na ndani.

Sifa za kwaya za kanisa.
            Kwaya ya kanisa ni watu wanaofuatana utaratibu wa kaisa la waadvetista wasabato. Kanisa linaweza kuwa na kwaya zaidi ya moja. “Makanisa yanaweza kuwa na kwaya zaidi ya moja. Kwaya ya watoto ni njia ya malezi ya kiroho, ikiwafungamanisha familia ya kanisa na uinjilisti.”
            Kwaya hizi zinweza kutokana na idara mbalimbali tulizonazo ndani ya kanisa. Kama vile idara ya vijana, chama cha dorkasi, idara ya wanawake,chama cha watafuta njia, chama cha mambolezi, na kadhalika. Lakini kwaya zote hizi zinawajibika moja kwa moja kwa kanisa sio mali ya mtu Fulani au kikundi cha watu Fulani. Maadili yake ni yale yale yameorodheshwa kwa kanisa lenye kwaya moja au zaidi. Kiongozi wa kwaya husika atafanya kazi kwa karibu zaidi na mchungaji au mzee wa kanisa husika.
Mjukumu ya kwaya ya kanisa na uongozi wake
Ø Wana kwaya wanapaswa kuelewa kuwa mziki ni ibada kamili yaani neno, kusifu na maombi yapo ndani ya uimbaji. Hebu sauti ziinuliwe vyema katika nyimbo za kusifu na ibada.
Ø Wanakwaya wanapaswa kutoa huduma za uimbaji katika ibada zote za kanisa- ibada kanisani, mazishi, ndoa, na kadhalika, mikutano ya kanisa.
Ø Uimbaji sio sifa pekee ya kuwa mwanakwaya bali sifa nyingine ni tabia ya uimbaji anayefaa na pia kumpitisha katika kujiunga na kwaya sio kwaya au mzee wa kanisa.
Viongozi wa kwaya na waimbaji wanapaswa kujua:
Ø Kiongozi wa kwaya ya kanisa sio kiongozi wa vikundi vyote vya uimbaji au kwaya za makundi za kansia. Yeye ni kiongozi wa kwaya moja tu ya kanisa.
Ø Hatuna kiongozi wa kwaya zote isipokuwa mchungaji wa kanisa/ mtaa au wazee wa kanisa kwa kuwa ni wasaidizi wa wachungaji.
Ø Kiongozi au waimbaji wanapaswa kujua wao ni kwaya ya kanisa moja na sio makanisa mengi. Hivyo waheshimu taratibu iwe ni kwa ruhusa kwenda kanisa lingine inyofuata utaratibu wa kanisa kwenda kuhudumu eneo jingine.
Mambo ambayo kwaya hairushusiwi kutenda bila idhini;
Ø Kanuni zote zinazohusu masharti ya kujiunga na kwaya lazima yapitishwe na kanisa. Sio kwaya peke yao tu, bali wao kama timu wanaweza kuunda katiba yao na kupeleka mapendekezo kwa baraza la kanisa kisha mashauri ya kanisa.
Ø Wanaweza kukaa kama kikundi na kupanga muda wao wa mazoezi na taratibu zao kisha kuleta mapendekezo kwa baraza la kanisa ili yapate kupitishwa kwa kuchunguzwa vyema. (kisa cha kutaka waimbaji wote wanyoe nywele size moja).
Ø Unoforma zao lazima zipitishwe na washiriki maana ni mali ya kanisa. Hairuhusiwi waimbaji kushona uniform yeyote bila makubaliano ya kanisa maana uniform ina mvuto mkubwa kwa wema na uovu kwa njisi ishonwavyo K.K uk 1995.
Ø Waimbaji hawaruhusiwi kufanya reconding yeyote kabla ya nyimbo hizo kupitishwa na washiriki wa kanisa kuwa zinakubaliana na msingi ya mafundisho yetu makuu au la. Ikiwa itangudulika kukiuka taratibu hizo kanisa litawajibika viongozi na wanakwaya wote kwa ukaidi na kisha kuharibu hiyo master record.
Ø Kwaya hairuhusiwi kusafiri safari yeyote bila idhini ya kanisa.
Ø Kwaya hairuhusiwi kufanya changizo lolote kwa kusudi lolote bila uongozi wa kanisa kuridhia michango hiyo. Iwe ni ndani ya kwaya au nje ya kwaya. Hili litasaidia usimamizi wa matumizi ya fedha za kwaya na pia kuepuka ubadhirifu kwa kutumia jina la kwaya la kwaya ya kanisa.
Ø Fedha zote za kwaya hazifunguliwiakaunti yake bali zitatuzwa na mhazini wakanisa hilo kama fedha za amana za idara nyingine. Zitakuwa risiti kilakinachoingia kwenye mapato yake.

F. MUZIKI WA KIKRISTO
            Leo kanisa limeona umuhimu mkubwa wa kuwa na mtu ambaye anahusika na usimamizi wa mziki kanisani ili kudumisha usafi na utaratibu mzuri wa usimamizi wa muziki wa kikristo. Kiongozi wa muziki kanisani anajulikana kama mratibu wa muziki (music coordinator) . hivyo kazi yake kuu ni kuratibu muziki wa kikristo kuwa uibwe na kuchanguliwa muziki unaoendana na maadili ya kanisa na kufuata msimamo wa mafundisho makuu ya kanisa la waadvetista wasabato.

Sifa na kazi kiongozi au viongozi (waratibu)wa muziki kanisani.
            Kiongozi huyu anapaswa awe ni mtu anayeuelewa vyema muziki wa kikristo.
1.    Mratibu awe ni mtu alijitoa maisha yake kwa yesu ili kulipatia kanisa muziki ambao unaenda sambasamba na maadili ya kikristo.
2.    Mratibu atafanya kazi kwa karibu na mchungaji au wazee wa kanisa ili uchanguzi wa muziki uende sambamba na mada na hubiri.
3.    Mratibu atafanya kazi chini ya uongozi wa mchungaji au wazee wa kanisa na sio kama apendavyo.
4.    Kiongozi huyu atashirikiana na uongozi wa kanisa (mchungaji wa wazee) katika swala la uchanguzi wa waimbaji na wapiga muziki kanisani.
5.    Mratibu wa muziki anapaswa kuwa mtu makini kutoruhusu muziki  wa kidunia au ule uletao mashaka kwa namna ulivyo kuingizwa katika ibada zetu ndani ya kanisa au matukio yote mikutano ya kanisa.
6.    Mratibu wa muziki anaweza kuwa mshauri wa mtunzi wa nyimbo na aina ya upigaji  wa muziki kwa waimbaji na kwaya zetu bila kuwaamulia aina gani   ya utunzi ama upigaji. Atawaongoza kujiepusha na upigaji wa kidunia wenye mvuto mbaya.
G. IDARA YA ELIMU:
            Kanisa la Waadvetista Wasabto linawajali binadamu wote katika malezi ya kiroho, kiakili, kimwili na hata kijamii . hivyo linashirikiana na serikali za dunia katika kuelimisha jamii kupitia taasis zote yaani shule ya awali mpaka chuo kikuu. Kanisa huendesha utaratibu wa shule ili kuhakikisha kwamba vijana wake wanapokea elimu yenye uwiano wa Nyanja nne nilizotaja hapo juu .
Sifa za kiongozi au katibu wa elimu.
1.    Kiongozi au katibu wa elimu ni mtu anayepaswa kuwa na mipango kwa ajili ya kuendekeza elimu ya kikristo.
2.    Elimu ya kikristo ni elimu itolewayo kwa ajili ya kumwinua mwanadamu katika hali yake ya maisha ya kiroho, kiakili, na kimwili.
3.    Awe ni mtu mwenye elimu pana juu ya maadili ya kanisa na mipango yake katika kumwedeleza binadamu.
4.    Awe ni mtu mwenye mwamko wa elimu binafsi na ambye ataweza kuhamasisha wazazi kuwa na mwamko wa elimu pia.
Wajibu na mjukumu ya kiongozi wa elimu.
Ø Kutia mkazo juu ya swala la Elimu ya kikristo.
Ø Kuhamasisha wazazi kupeleka watot katika shule zetu za kiadvetista – msingi, sekondari, na vyuo. Pia kuwatia nguvu wazazi kuelewa namna ya kupata ya fedha za masomo.
Ø Mahali ambapo hatuna shule zetu basi kiongozi wa elimu ahamasishe kanisa litoe elimu yetu katika eneo hilo. Mf.Kupitia vipindi vya dini katika shule za binafsi na serikali
Ø Kuhakikisha anakuwa na mawasiliano ya karibu na wanafunzi /watoto wetu ambao wanasoma katika shule zilizo karibu na zilizo mbali.
Ø Kuhamasisha wazazi ambao watot wao bado si wa umri wa kwenda shule waweze kutiwa moyo kusaidia wanafunzi waadvetista wenye shida za kusindwa kulipa ada.
Ø Kudumisha hesabu sahihi za watoto wote na  vijana walio n aumri wa kwenda shule.
Ø Kuweka mipango kwa kanisa lake kuazisha shule za chekechea, msingi na hatimaye sekondari.

H. IDARA YA HUDUMA ZA AFYA.
            Idara hii iliazishwa mahususi katika kutoa ufahamu wa mwanadamu katika kufahamu mwili wake na mazingira yanayomzukuka kisha ufahamu mpango na makusudi ya mungu kwa ajili ya afya zetu. Biblia inaeleza makusudi hayo katika e yohana  1:2  Mpenzi naomba ufanikiwe katika mambo yote na kuwa na afya yako, kama vile roho ifanikiwavyo.”
            Hii ni idara nyeti sana maana afya ya kanisa kimwili, kiakili  na kiroho inategemea sana jinsi kiongozi alivyojitoa wakfu kwa kufanya kazi yake na majukumu ya idara hii. Washiriki wanapokuwa wangojwa katika nyaja mojawapo ya afya yaani kimili, kiroho, na kiakili- moja kwa moja ibada za kanisa lazima zitaadhirika kwa kiwango cha juu sana. Soma Mithali 14:30.
·       KIROHO: Usomaji hakuna, kazi ya Mungu haifanyiki, uchelewaji wa saa za ibada kwa kiwango cha juu, kupoa kiroho, n.k
·       KIAKILI:-Hakuna utambuzi wa mambo matakatifu, ugomvi ndani ya kanisa na familia na kaya, mabaraza ya kanisa kuwa na maamuzi yasiyo ya busara, n.k.
·       KIMWILI:- Kanisa kuwa na wagonjwa wengi, umaskini, uzembe, na afya mabya, n.k
Wajibu   na majukumu ya kiongozi wa idara hii.
Ø Ili kutatua matatizo yote haya, kiongozi wa afya na kiasi anapaswa awe na baraza madhubuti ambalo litawahudumia washirikikwa kusaidia wale ambao ni wangonjwa kimwili na kiakili, na  pia mutoa elimu madhubuti ya maswala ya afya. Ellen White anasema.. “siku zote aliye mgonjwa kimwili atakuwa atakuwa mgonjwa kiroho, na aliye mgonjwa kiroho atakuwa mgonjwa kimwili”.
Ø Hivyo kiongozi anapaswa kufanya mambo yafuatayo kulisaidia kanisa kukua katika afya kisha wawe na kiasi katika mambo yote ni haya yafuatayo:
1.    Kiongozi apange  program za mwaka mzima akishauriana na mchungaji na mzee wa kanisa ambazo zitasisitiza afya na kiasi kwa kanisa na jamii.
2.    Kutoa elimu juu ya vitu vinavyodhuru mwili na akili na mambo ya kiroho kama tumbaku, pombe chai, kahawa, madawa ya kulevya,kazi nyingi, kutokupata pumziko, n.k hata kama huna utalaamu huo haikisha unapatamtu mwenye huruma juu ya mambo hayo kisha apewe nafasi ya kufundisha kwa idhini ya mchungaji wa kanisa.
3.    Kukuza mahusiano ya karibu sana na mashirika ya afya kisha tuwatumie kwa zile mada ngumu kama vile magonjwa ya kutisha,vifo visivyo vya lazima, uchafunzi wa mazingira n.k
4.    Kiongozi anapaswa awe mwanfunzi hodari wa Biblia na Roho ya unabii juu ya mafundisho ya afya.
5.    Kiongozi lazima apange ratiba ambazo ainangusa maisha ya jamii kwa ujumla sio kwa mtizamomtu wa kiadvetista. Nina maana usije ukaacha kufundisha swala la tumbaku au pombe ukidhani kuwa walevi au wavutaji hawapo ndani ya kanisa. Tambua wapo wanfanya kwa siri au watakaojaribiwa na dhambai kama hizo.
6.    Unapoandaa semina kama hizo, ratiba yako ijumuishe mambo yafuatayo:-
a)    Namna ya kuacha uvutaji wa tumbaku au pombe –kisha toa matangazo kwa njia ya radio au mabango juu ya mada za uvutaji wa tumbaku au ulevi-mf semina ya namna kuacha ulevi wa tumbaku; kisha tafuta wakufunzi ndani ya kanisa au nje ya kanisa . zaidi ya yote tafuta ndani ya kanisa watu watakaotoa ushuhuda wake njisi alivyoshida mazoezi mabaya.
b)    Onyesha juu ya mafunzo ya mapishi- familia nyingi hawajui namna namna ya upangaji wa ratiba ya chakula mfano maembe + mchicha= kimoja. Nyama +maharange = protini.
c)     Program za kuthibiti misongo ya mawazo- wapo wanaokuja kanisani lakini ana msongo wa mawazo.
d)    Madarasa ya afya – namna ya kuzuia magonjwa ya luambukiza, usafi wa mazingira, dawa na miti shamba, kutambua ‘first  aid’ – huduma ya kwanza.
e)    Kuonyesha jinsi mtu anavyoweza kuwa na kiasi katika upangaji wa kazi na majukumu mengine na muda wa kupumzika.
f)      Namna ya kulea watoto wakiwa na afya bora. Hili litahusu kufundisha uandaaji wa chakula bora cha watoto wadogo.
g)    Kufundisha namna ya kuhifadhi chakula katika mazingira safi na pia swala la ujenzi bora kwa afya bora. Siyo nyumba za madirisha ya kuziba na nguo, isiyoingiza hewa ya kutosha.
I. IDARA YA HUDUMA ZA FAMILIA
            Kanisa la waadvetista wasabato linajali msingi wa kwanza wa kanisa ni yesu Kirsto. Kwa kanisa ni mwili wa kirsto. Basi kanisa halizuki angani bila kuwa mawe yanayoweza  kulijenga kanisa.familia imejulikana kuwa ni jiwe la pembeni katika kujenga jingo imara la kanisa. Kuwa na familia.idara ya huduma za familia inajumuisha kwa kuanza na mtu mmoja, mume na mke, mzazi mmoja, wazazi n awatoto. Ndio maana Paulo anasema hivi katika EFESO 6:1-4 KUWA;
            Enyi watoto watiini wazazi wenu katika Bwana, maana hii ndiyo haki. Waheshimu baba yako na mama  yako; amri hii ndiyo amri ya kwanza yenye ahadi, apate heri ukae siku nyingi katika dunia. Nayi akina Baba, msiwachoke watoto wenu; bali waleeni katika adabu na maonyo ya Bwana.”
Kanuni za kanisa zinaonyesha wazi kuwa kaya ni jiwe la pembeni  la kanisa maana kristo ndiye mwasisi wa familia zote duniani. Kanisa lililo bora linaazishwa na familia bora. Kanisa bovu linaazishwa na familia mbovu. Ni muhimu sana kanisa lolote kuimarisha familia zetu ili tuwe na kanisa imara lenye msingi imara kutoka kwa Yesu Kirsto. Hivyo ni wajibu wa kiongozi wa idara kukanzia maombia ya familia na ibada ili familia hizi zifunikwe na mapenzi ya Mungu.” Hebu angalia kanuni za kanisa, sura 13, uk.4
            “kaya ni  jiwe la pembeni la kanisa, na kaya ya kikristo ni nyumba ya sala.”Baba na mama” inasema Roho ya unabii. “ijapokuwa shughuli zenu ziwe nyingi kiasi gani, msishindwe kukusanya familia yenu kuizunguka madhahabu ya Mungi…. Wale wanaoishi maisha ya uvumilivu, upendo na furaha, hawana budi kuomb.” Ministry of Healing uk. 393.
Utendaji wa idara ya huduma za familia kanisani mahalia
Ø Idara hii ipo kanisani katika kufundisha kanisa kuwa linapaswa kuwa na familia ambazo ni mbigu ndogo katika familia kubwa ya kanisa.
Ø Kanisa kama familia kubwa ulimwenguni inapaswa kujengwa na familia ambazo zimemtambua Yesu kama kichwa cha familia kubwa- kanisa na hivyo kumwiga Kirsto.
Ø Idara hii husaidia kanisa kuelewa unyonge unaopitiwa na watu binfsi na familia katika ulimwengu ulioanguka na kuwezesha familia kupiga hatua kuelekea malengo ya kimbigu.
Ø Idara hii hulenga watu wenye uhusiano kwa kuhusika na mahitaji ya waliooa, wazazi na watoto, mahitaji ya kifamilia kwa waseja na pia kwa wazazi wa upande mmoja (single parents).
Ø Pia idara hii hueneza tumaini na kutoa msaada wa hali zote kwa wale ambao wamejeruhiwa na kuumizwa na dhuluma, mmonyoko wa familia, kuvujika kwa mahusiano, n.k.
Ø Pia kwa upande mwingine hutoa ushauri wa kukuza mahusiano na kutoa elimu ya kunufaisha maisha ya familia-katika kujikwamua kimaisha.
Ø Ni kazi ya idara kufanya tathimini kujua familia zenye mahitaji maalum ili idara iweze kuwakwamua, mf, kushindwa kusomesha mtoto aliyefaulu kwa ajili ya uwezo mdogo, au mmoja wa wanafamilia kuugua kwa muda mrefu na hivyo familia kuadhirika kiuchumi,n.k

Majukumu na wajibu wa kiongozi wa familia
·       Ni jukumu la kiongozi huyu kuona familia zinaishi kwa amani na upendo hasa kwa kujenga familia zenye maadili ya Kirstin a yenye kuishi kwa kufuata haki za msingi za mwandamu. Mfano/; watoto waende shule, wawe na afya bora, kupiga ukadamizaji, n.k
·       Kiongozi ni muhimu kutambua kaya ngapi ambazo wazazi waliopo ndani ya kanisa wamefunga ndoa na pia kuhamasisha wale wasio  na ndoa kutengeneza ndoa zao.
·       Kiongozi anaweza kuanda sabato maalum kwa ajili ya kuendesha huduma za kaya na familia hata kwa kualika familia ambzao sia za kiadvetista. Ni jambo la msingi kuwepo na sabato za wangeni ambazo zitaendeshwa na idara hii kwa kuandaa mkufunzi mzuri wa mambo ya kaya na familia.
kama kiongozi uapnge mambo yafuatayo:-
·       Kiongozi uwe na kamati madhubuti ya kaya na familia itakayoratibu mahitaji makuu ya familai. Kamati hiyo ijumuishe waseja, wanadoa, mzazi mmoja zu zaidi, na mwakilishi anayejumuisha makundi ya rika mbalimbali kanisani.
·       Andaa semina kwa kutumia miongozo kwa wenzi kabla ya ndoa ili kusaidia na kujenga ndoa imara.
·       Andaa semina zinazoimarisha ndoa change na za muda mrefu ambazo zinakabiliana na wawimbi ya maisha.
·       Toa mafuzo kwa wazazi namna ya uleaji wa familia zao kwa mahusiano yenye mvuto wa kikristo.
·       Toa mbinu mbalimbali namna mzazi mmoja anavyoweza kukabiliana na changamoto za maisha na upweke na pia wale ambao wanaishia na watoto wa kambo namna ya kuwatunza katika upendo wa  kweli.
·       Toa mafunzo kwa familia zetu kufanya uinjilisti wa familia kwa familia. Mf. Chakula cha pamoja siku ya sabato au ijumaa jioni. N.k
·       Hakikisha nakusanya takwimu sahihi za idadi ya familia ndani ya kanisa na pia jamii inayolizunguka kanisa ambao ni walengwa wetu wa injili.
·       Kukuza hali ya joto la ushirikiano, ili kuleta maana ya “ufamilia” kanisani mwetu na robo ya ukombozi na wale wanaohitaji msaada.
·       Kuweka mikakati ya kuwa na vipindi vya mchana au sabato maalumu ya kaya na familia ambayo itakuwa na shuhuda za baadhi ya familia namna walivyopita maisha yao ili kuwatia nguvu ndoa changa kuwa ndoa sio lelemama; hivyo wakaze mwendo.
J. IDARA YA UWAKILI NA MAENDELEO.
            Idara ya uwakili  ilianzishwa kuwasaidia washiriki wawewe kuwa mawakili dhabiti na kusaidia katika utekelezaji wa mpango wa Mungu wa mfumo wa ukarimu wa kanisa lote. Jambo hili linajumuisha usimamizi sahihi wa maisha yote, dhana za uwakili kuhimiza ungalizi na matumizi sahihi wa hekalu la mwili, wakati, uwezo na mali. Hapo mwanzo idara idara hii ilijulikana kama uwakili na maendeleo. Lakini kanuni za kanisa za mwaka 2005 na 2010 kipengele hicho kimeondolewa. Hivyo inajulikana kama idara ya uwakili.
Swala la uwakili ni jambo nyeti na pan asana katika Nyanja zote za maisha ya mwanadamu. Uwakili unahusu ujumla wa binadamu kwa maisha yake yote (wholesome or whole being). Biblia inasema tuwe mawakili waamiinifu. Unaweza kuwa wakili lakini siyo wakili mwaminifu.
Uwakili katika tafsiri ya maisha ya mkristo ninajaribu kuigawa katika vipengele vikuu vinne. Vipengele hivyo vitatu vinajulikana sana na kukubalika na wakristo wengi lakini kimoja wapo baadhi wanakubali na wengine hawakubalikipengele hiki cha mwili kuwa hekalu la mwili. Ijapokuwa kanuni za kanisa kinatambua kipengele hiki cha hekalu la mwili. Kuwa na mojawapo ya swala la uwakili wa mwanadamu kwa mungu wake. Vipengele hivyo ni kama ifuatavyo;-
1.    Uwakili wa muda(wakati)
2.    Uwakili wa mwili(miili)
3.    Uwakili wa talanta(vipawa/karama au uwezo wetu)
4.    Uwakili wa mali(amana au vyote tunavyovimiliki).
Biblia inasema kuwa tunaweza kujiita mawakili, lakini wale watakaookolewa ni wale ambao wamekuwa mawakili waaminifu wa kweli.paulo anasema hivi katika 1wakorintho 4:1,2 “mtu na na atuhesabu hivi, kuwa tu watumishi wa kirsto, na mawakili wa siri za Mungu. Hapa tena inahitajiwa katika mawakili, ndiyo mtu aonekane kuwa mwaninifu.”
Sifa za kiongozi wa uwakili
·       Kingozi wa uwakili awe ni mtu ambaye ni mfano bora kwa kanisa.
·       Kiongozi wa kiroho
·       Kiongozi anayetekeleza kanuni za uwakili wa kikristo.
·       Kiongozi anayepaswa awe na ufahamu wa kiroho wa program za uwakili na za uwakili wa kifedha.
·       Kiongozi awe tayari kutoa muda unaohitajika kupanga, akuasisi, na kuongoza katika maeneo yaliyotengwa ya majukumu kwa ushirikiano na mkurugenzi wa conference au fild.
Wajibu na majukumu ya kiongozi au taratibu wa uwakili
·       Katibu afundishe kanisani namna ya kuwa mawakili kwa mali zao na namna ya kupanga bajeti zao kwa maendeleo ya familia za.
·       Kiongozi aelewe program za fedha zote yaani sadaka zote namna zinavyotumika kisha wafundishe washiriki umuhimu wa utoaji wa sadaka hizo.
·       Kiongozi atumie dakiki zake 10 kwa siku za sabato kuhamasisha swala la utoaji zaka na sadaka. Pia uwakili wa washiriki katika kila jambo.
·       Kujaza taarifa yake kila mwezi ili itumwe kwa mkurugenzi wa uwakili field sambamba na taarifa ya mhazini.
·       Kusimamia na kuendesha prgramu zote za uwakili na uendeshaji wa majuma ya uamsho na semina mbalimbali juu ya uwakili mf. Kualika ata wahubiri wazuri kwa maswala ya uwakili ili kuliamsha kanisa katika uwakili.
Kamati ya uwakili ina wajumbe wafuatao:-
1.    Mwenyekiti
2.    Katibu wa uwakili
3.    Mhazini wa kanisa
4.    Mzee wa kanisa
5.    Shemasi mkuu wa kike na kiume
6.    Karani wakanisa
7.    Wajumbe wawili wa kuteuliwa- kutoka kwa washiriki wa kanisa wa kawaida.
# idadi inaweza kuongezeka bali itatengemea ukubwa wa kanisa.
Majukumu ya kamati ya uwakili ni haya:
1.    Upangaji wa budget za kanisa.
2.    Usimamizi wa bajeti ya knaisa kwa maidara yote.
3.    Uelimishaji wa maendeleo ya kanisa katika Nyanja zote za maisha; hili ni pamoja na kutoa eleimu ya kujitegemea kwa kuinua kipato cha washiriki na pia utambuaji wa karama.
4.    Usimamizi wa uendeshaji wa taratibu za vikao na shughuli za kanisa kuona kuwa unafuatwa kama ipasavyo; na kurekebisha kama kuna kasoro yoyote kwa kingozi yoyote.
5.    Kamati hii inapaswa kukutana kila mwezi au muda watakaokubaliwa kulingana uzito wa majukumu ili kufanya tathimini ya maendeleo ya kanisa lao.
K: IDARA YA MAMBO YA UMMA NA UHURU WA DINI.
      Kanisa linatambua mamlaka zilizowekwa na wanadamu zote zimepita kibali kutoka kwa Mungu. Paulo anasema katika WARUMI 13:1 wazi kuwa “kila mtu na aiitii mamlaka iliyo kuu; kwa maana hakuna mamlaka isiyoyopo imeamriwa na Mungu.”lakini upande wa pili wa shilingi ni kuwa dunia hii imejaa uovu wa kila namna .Uongozi wa dunia unaweza kupingana na mungu ,hapo ndipo kama Kanisa tunapaswa kusimama chini ya bendera ya kristo na kusema kuwa”Petro na mitume wakajibu, wakisema,Imetupasa kumtii Mungu kuliko wanadamu.”MATENDO 5:29.
Wajibu na majukumu ya idara hii.
·       Kanisa la Mungu lingali bado duniani;mahali ambapo dhuluma na ufisadi vinatawala.Hakuna hofu ya mambo ya Mungu.Hivyo idara hii iko kanisani kwa lengo maalumu kutetea haki na maslahi ya washiriki na Kanisa kwa ujumla.
·       Hili linagusa swala la uhuru wa dini kwa mkazo juu ya uhuru wa dhamili ya mtu binafsi. Uhuru wa dini hujumuisha uhuru wake wa kuabudu,au kuchagua dini au kuchagua dini aipendayo;kubadili imani yake pia kudhihirisha dini yake binafsi au katika jamii pamoja na waumini wenzake katika ibada,kuadhimisha mambo ya dini,desturi,ushuhuda, na mafundisho kulingana na heshima yake kwa haki za watu wengine.
·       Idara hii katika swala la mambo ya kuadhimisha inatetea haki ya siku ya kuabudu kwa waumini wake kama msingi wa Biblia.Pia husimamia katika ufafanuzi wa matukio ya duniani ambayo yanaweza kudhihirisha mambo ya unabii.Mf, Jumapili ni alama ya mnyama,papa ndiye mnyama wa ufunuo 13 au pembe ndogo ya Danieli 7,n.k.
·       Idara hii inasimamia haki za dini na kutangaza imani yake na mafundisho yake wazi wazi pasipo kuingiliwa na serikali kwa shinikizo la kundi la watu fulani ya watu wa imani nyingine.
·       Ili kupata nguvu idara hii inashirikiana na chama cha kimataifa cha kutetea Uhuru wa Dini na vyama shiriki ulimwenguni kote.
zingatia hili lifuatalo:-Kila kanisa linachukuliwa kama chama cha kutetea Uhuru wa Dini kisicho rasmi. Na kwa sababu hiyo kila mshiriki ni mwanachama wa chama hicho.
o   Hivyo mchungajiau mzee wa kanisa ni mwenyekiti wa chama katika kila kanisa
o   Kanisa linaweza pia kuchangua mtu mwingine badala ya nafasi hizo hapo juu kutokana na majukumu.lakini anapaswa awe ni mtu wenye mvuto na mwenye kufanya kazi karibu sana na mchungaji. Anajulikana kwa jina la kiongozi wa chama cha kutetea uhuru wa dini kanisani.
o   Kiongozi huyu anapaswa awe na uhusiano na umma na mwenye kufahamu taratibu za nchi au umma; na pia mwenye kudumisha uhuru wa watu wa Mungu ili waweze kutekeleza kazi ya Mungu
Kazi na majukumu muhimu ya kiongozi huyu:-
·       Kukuza usambazaji wa magazeti yanayotetea uhuru na makala mengine yanayotolewa au kukubaliana na kanisa katika ulimwengu.
·       Kutoa semina  juu ya uhuru wa dini kwa washiriki. Hili ni pamoja program, mikutano au makongamano yanayozungumzia uhuru wa dini.
·       Kutetea wanafunzi wetu katika shule ya vyuo wanapolazimishwa kufanya kinyume na uhuru wao wa kuabudi. K.m kufanya mitihani au kusoma siku za sabato, au kutopewa ruhusa ya kuadhimisha desturi zao kama vile makambi, n.k
·       Kuliwezesha kanisa kufahamu taratibu za nchi yao na haki zao za uraia kwa kufundisha katiba ya nchi, au kujua maswala ya mirathi, uadikaji wa wosia, na mambo mbalimbali kama taratibu za kisheria, n.k.
·       Kiongozi huyu anatoa ushirikiano wa karibu pale kanisa linapodhulumiwa mali zao au linapohitaji kuingia mikataba ya kisheria kwa kutafuta vyombo husika katika ushughulikiaji  mfano kupata mwanasheria mzuri.
L: IDARA YA MAWASILIANO.
      Idara hii ni mpya katika makanisa mengi lakini ipo siku nyingi bila kueleweka vyema. Na kama makanisa yagelifahamu kwa hakika, basi waadvetista wasabato tugekuwa na mtandao wa mawasiliano ambao ungetufanya tuwe watu wanaokwenda na wakati siku zote(upto date) kanisa ligefahamika vyema kwa waulimwengu kwa njia ya matangazo. Ukuaji wa kanisa kwa nyakati hizi inatengemea sana idra ya mawasiliano namna inavyotenda kazi yake ndani ya kanisa.
Wengine kwa kushindwa kuelewa idara hii wamelaumu kanisa kwa kutumia mamilioni ya fedha kwa usambazaji wa injili kwa mahubiri ya satellite. Nadhani watu hawa hawajawahi kusoma roho ya unabii tunapaswa kutumia kila njia halali ili kufikisha nuru mbele za watu….. hebu uchapishaji utumiwe na kila wakala wa utangazaji ambao watatangaza kazi za injili utumiwe.”- 6 Tuk. 36. “njia za kuwezesha kufikia mioyo ya watu zibuniwe. Baadhi ya mbinu zinazotumika katika kazi hii zitakuwa tofauti na mbinu zilizotumiwa kazini katika siku za nyuma……….” Evangelism, uk.105.
Ø Idara hii inahusika katika kuhamasisha kanisa kutumia Nyanja zote za mawasiliano katika kupashia habari kwa kutangaza injili.
Ø Ni kazi ya idara hii kutoa habari za program kwa jamii kwa njia ya matangazo yaliyoandaliwa vyema na kupimwa na kamati ya mawasiliano ili kanisa lijulikane kwa jamii yote. Tangaza mambo yanayotedwa na kanisa kwa njia ya mabango, redio, televisheni, magari, sticker, vipeperushi, n.k mfano sabato za wageni, efoti, siku maalimu za vijana, watafuta njia, n.k.
Ø Hivyo ili kila kanisa kutimiza agizo la mbingu la utangazaji injili milele kwa njia ya kisasa, inapasa kila kanisa kuchangua katibu wa mawasiliano na ikiwezekana na kamati ya mawasiliano.
Kamati ya mawasiliano ina wajumbe wafuatao :-katibu wa mawasiliano kama mwenyekiti wake, na wajumbe ambao wana ujuzi katika Nyanja za mawasiliano kama magazet, radio, televisheni  , huduma ya masomo kwa njia ya posta na pia vyombo vya mawasiliano  ndani ya kanisa. Mnaweza kumwalika mmoja wa wafanyakazi wa chombo kilicho karibu cha mawasiliano cha kanisa kuwa pia mjumbe wa kamati.
Kazi ya katibu wa mawasiliano.
Ø Anahusika katika ukusanyaji na usambazaji wa habari.
Ø Anapaswa kuwa karibu na wanahabari ili kutoa habari sahihi za utendaji wa kanisa. Kwa kutoa mtangazo ya kanisa kwa njia ya redio au magazeti kama vile mikutano, effort, kongamano, n.k pia upokeaji wa habari sahihi.
Ø Anapaswa kuanzisha huduma za masomo ya Biblia kwa njia ya posta.
Ø Anapaswa kuhimiza sadaka ya radio na televisheni; na piakushiriki kugawa vijizuu vya redio na televisheni kwa na masomo ya Biblia kwa njia ya posta.
Ø Utoaj wa taarifa za mipango ya field/conference katika mikutano wa mashuri katika kanisa lake na namna ya kutekeleza mipango hiyo.
Ø Kuhakikisha kanisa lake limeweka kibao kinchotambulisha uwepo wa kanisa mahali hapo (sign board).
Ø Kuchukua matukio  muhimu ya mikutano na shuhuda mbalimbali kwa kuhifadhi kumbukumbu kwa njia ya kamera, maadishi kurekodi,n.k
·       Upangaji wa matukio yanayoangukia kalenda ya kanisa ulimwenguni kwa kumpatia taarifa kiongozi wa idara husika juu ya tukio lake linalotokea
·       Kupeleka katika maktaba na vituo vingine vya habari, habari zinazohusu kanisa la waadventista wasabato mf. Magazeti yetu, shughuli zetu, n.k
·       Kuhamasisha washiriki katika swalla la uandishi wa habari kwa kutuma katika magazeti yetu kama maranatha, outlook, n.k.
·       Kuratibu program zote za mahubiri ya satellite kwa kutoa parameters na pia kutuma shuhuda mbalimbali kwa kiongozi wa mawasiliano field.
·       Utengenezaji wa mabango mbalimbali yanayoeleza mada mbalimbali wakati wa semina maalumu za kanisa au effort au mahubiri ya satellite na miamsho

M. IDARA YA HUDUMA ZA WATOTO
Kanisa la waadventista wasabato linathamini sana watoto na vijana kwani ndio nguzo ya kanisa. Watoto wanapolelewa vema tunakuwa na kanisa bora la baadaye na umilele wake. Idara ya huduma za watoto ipo ili kukuza Imani ya watoto toka kuzaliwa hadi umri wa miaka kumi na nne

UTUME: utume wa idara ya huduma za watoto ni kuwalea watoto katika uhusiano wa upendo na utumishi pamoja na yesu.

Wajibu na majukumu ya idara ya huduma za watoto
·       Idara hii ilianzishwa kanisani kwa makusudi ya kusaidia malezi ya watoto na pia kusaidia kanisa kujua mahitaji ya msingi ya watoto kwa swala zima la ibada kanisani
·       Idara inakusudia kuanzisha huduma nyingi zitakazowavuta watoto kwa yesu na kuwafanya kuwa wanafunzi wake katika kazi zao za kila siku.
·       Idara hii inakuza Imani ya watoto wadogo kuanzia umri wa kuzaliwa mpaka anapofikia umri wa miaka kumi na nne au na tano ili hatimaye aweze kujiunga katika kanisa la Mungu.
·       Idara hii inafanya kazi kwa karibu sana na idara ya shule ya sabato kitengo cha watoto na pia idara nyingine kama vile vijana, kaya na familia, wanawake, na vyama mbalimbali kama watafuta njia, wavumbuzi, n.k.
·       Idara inapaswa kufanya kazi kama kitengo cha wainjilisti kwa kuwatumia watoto kufikisha ujumbe kwa watoto wenzao na hatimaye kwa wazazi ambao si waumini wetu na kupewa mafunzo mbalimbali wakati wa likizo

Wajibu na majukumu ya kiongozi wa idara ya watoto
·       Kiongozi wa idara hii anapaswa kuhakikisha watoto wanapewa haki zao za kiibada badala ya kuwaacha wakiwa wamezagaa huko nje wakati ibada ikiendelea kwa watu wazima. Kiongozi anapaswa kwa kushirikiana na mashemasi kuona utulivu waibada kanisani
·       Kiongozi awasiliane na mchungaji au mzee waw kanisa kuona ibada ya watoto inafanyika kila siku kwa kupewa wahudumu: kwa makanisa yasiyo  na jengo basi muhubiri akumbushwe kona ya watoto
·       Kila kanisa ambalo halina jengo yawapaswa kupanga wahubiri wawili kila juma. Wa kwanza ataanza na watoto kwa dakika 7 hadi 10 kisha muhubiri mwingine atamalizia muda uliosalia
·       Kama kiongozi weka mikakati kwa kushirikiana na mkuu wa majengo kupata jengo la kuabudia watoto – kwa uendeshaji wa shule ya sabato ya watoto na ibada yao kuu.
·       Kama kiongozi washirikishe watoto kwwa kushirikiana na wazee wa kanisa kuona vipawa vya watoto mapema na kuwapa majukumu yakanisa mapema ili waanze kulipenda kanisa tangu utotoni. Mfano kuendesha shule ya sabato, kuhubiri siku zao maalumu, program za mchana za watoto, n.k
·       Kiongozi afanye jitihada ya kuwaingiza watoto katika uinjilisti wangali bado wadogo. Kuandaliwa efoti za wiki moja au sikua nane ambazo zitaendeshwa na watoto. Mahubiri yao maalumu na miongozo ya kufundisha vipindi vya afya. Imegudulika program hizi zimeleta wengi kanisani wakubwa kwa wadogo katika maeneo zilipofanyika.

IDARA YA MAJENGO YA KANISA
Hiki ni kitengo kilichomo ndani ya kanisa ambacho kinahusika na ujenzi wa majengo ya kanisa. Kitengo hiki viongozi wake mara nyingi wanatumika pale wanapohitajika  hususani kanisa linapokuwa na jengo tayari. Hivyo inaonekana umuhimu wake haupo.
      -kiongozi au mkuu wa majengo ya kanisa anachaguliwa wakati baraza la uchaguzi au wakati wa baraza jipya la kanisa baada ya uchaguzi. Hili litatokana  na umuhimu wa kiongozi huyu kwa kipindi hicho.

·       Kiongozi huyu ataratibu  mambo ya ujenzi wa majengo ya kanisa akishirikiana na kamati yake ya ujenzi pamoja na baraza la kanisa.
·       Atawajibika kusimamia ujenzi wa kanisa au majengo yote ya kanisa kama vile choo, ofisi na kadhalika.
·       Kiongozi wa majengo atakuwa ni mtu ambaye anashauriana na kanisa kutafuata ramani inayofaa nay a kupendeza kwa ujenzi wa majengo ya kanisa
·       Kiongozi huyu atashirikiana nakamati ya ujenzi kuhakikisha kuwa majengo yetu yanajengwa katika viwango vinavyokubalika na kumtukuza Mungu
·       Kiongozi wa idara ya majengo atakuwa ni mwenyekiti wa kamati ya majengo ya kanisa
·       Kiongozi huyu ataleta bajeti ya jingo lolote kwa baraza la kanisa hatimaye kwa mkutano wa kanisa
·       Kongozi wa majengo atahusika pia kutafuta viwanja vya kanisa na kuhakikishwa kuwa vimepimwa na mamlaka husika ya kiserikali
·       Kiongozi ataratibu mipango ya upatikanaji wa fedha kwa ajili ya ujenzi au ununuzi wa viwanja akishirikiana na idara nyingine katika swala la kupata ardhi kwa matumizi ya kanisa.
·       Wajumbe wa kamati ya majengo mara nyingi inaundwa kulingana na busara ya kanisa mahalia. Makanisa mengine yanakuwa na kamati kama ifuatavyo
a.     Mkuu wa majengo – mwenyekiti
b.    Msaidizi mkuu wa majengo – karani
c.     Mchungaji wa mtaa – mjumbe
d.    Mzee wa kanisa - mjumbe
e.     Karani wa kanisa – mjumbe
f.      Mhazini wa kanisa -  mjumbe
g.    Mashemasi wakuu [kiume na kike]
h.    Kiongozi wa uwakili – mjumbe
i.      Washiriki wa uwakili – wajumbe
j.      Wengineo kwa busara za baraza la kanisa.
IDARA YA UKAGUZI [AUDITOR]
Kitengo cha ukaguzi makanisa mengi sana wamepuuza kumchagua kiongozi wake kwani anaonekana  kana kwamba sio mtu wa muhimu sana. Lakini kama kuna kitengo cha muhimu sana na ambacho kinaweza kuwa na lawama nyingi sana wakati anapowajibika kwa usahihi ni Mkaguzi wa kanisa
Mkaguzi anapochaguiwa ni mtu aliyesaidia kanisa kutembea katika barabara iliyonyooka wakati wote. Mkaguzi wa kanisa anapokuwepo ni jicho la kanisa kutazama utendaji bora wa kanisa. Kwani kila mmoja anawajibika  kwa uaminifu kuwa siku moja atakaguliwa na taarifa yake itasomwa kwa wote waliomchagua
Sifa za mkaguzi wa kanisa
Awe ni mtu anayejua kutunza siri za watu hasa anapokagua vitabu vya zaka na sadaka. Awe ni mtu mvumilivu na pia asiwe na hasira kwani hatapendwa anapokagua na kutoa taarifa ya ukweli. Anaweza kuchukiwa bila sababu ya kweli.
Asiwe mwepesi wa kuropoka ripoti yeyote anayegunduakutoleta hali ya kukosa Imani kwa mhazini au kiongozi husika kwa washiriki
Awe anajua kuandika na mahesabu vizuri ili kupitia vitabu vya zaka na sadaka kwa usahihi Zaidi
Asiwe ni mjumbe wa baraza la kanisa ili awe nauwezo wa kulikagua kwa uhuru
Awe ni mtu mwaminifu katika utendaji wake wa kazi. Aliywe na hofu ya Mungu
Awe ni mtu asiye na chuki au kisasi kwa ajili ya kutenda haki kwa wote.
Anapaswa awe na hekima na pia mwenye kushaurika na mtu aliye mwanana na mplle (utii)
Anapaswa kutambua kuwa kitengo hiki cha muhimu kwani kinalinda mali ya Bwana kwa wivu wa Bwana. Hivyo awe ni mzalendo kwa mali za Mungu. Asiye muonea mungu haya yeyote yule
Asiwe ni mtu anayeridhiamaovu pia mwenye kuchukia mapato ya udhalimu na aibu. Awe tayari kukemea maovu na roho ya kurekebisha maovu
Majukumu na wajibu wa mkaguzi wa kanisa
Kuhakiki na kukagua taarifa zote zinazohitajika kutolewa kwa washiriki
Kusimamia na kudhibiti mali za Mungu zinazomilikiwa na Kanisa mahalia ziweze kutumika vyema kama ilivyopitishwa na halmashauri ya kanisa hilo
Kukagua fedha na matumizi yake kuendana na jinsi ilivyopitishwa kwenye bajeti ya kanisa hilo
Kulijulisha kanisa usafi wa matumizi ya kanisa na michango  mbalimbali inayotolewa na washiriki wa kanisa hilio ili kujenga Imani kwa watoaji.
Kulisaidia baraza la kanisa kuona kuwa linaongoza kanisa kulingana na mujibu  wa kanuni na taratibu za kanuni za kanisa hili. Ina maana mkaguzi anatakiwa kuangalia miniti za vikao kuwa vinazingatia utaratibu wa kanisa
Kukagua mali za kanisa kama vile majengo, viti, vitabu, vyombo vya meza ya bwana na ubatizo, vifaa vya mahubiri na kwaya, na mali zote zinazomilikiwa na kanisa hilo kuwa vipo katika idadi ile ile kila mwaka au kuna upotevu.
Mkaguzi atatoa ripoti yake kwa mchungaji ili irekebishwe kabla ya kwenda kwa baraza  la kanisa kujadiliwa hatimaye ifae kwenda kusomwa kwa mashauri ya kanisa.
Kumsaidia mhazini wa kanisa kuona kuwa mapato ya kanisa kutoka makundini na matawini yanamfikia sawa. Na pia kumkumbusha namna anavyogawa matumizi ya kanisa bila kuendelea kitengo chochote ama kuonea kitengo mojawapo bila kujali bajeti ya kanisa.

HUDUMA ZA MAZISHI

Huduma ya Mazishi  (Mchungaji, mzee wa kanisa, au shemasi anaweza kufanya huduma hii). Ushauri umetolewa kwamba, kadiri inavyowezekana, maz...