Jumamosi, 1 Aprili 2017

MASOMO


  1. Biblia
    2Pet1:21Wanadamu walinena yaliyotoka kwa Mungu wakiongozwa na Roho Mtakatifu 2Tim.3:16 kila andiko lenyepumzi ya Mungu Zab.119:160 Neno la Mungu la kweli Zab.119:105 Neno taa Zab.12:6-7 Mungu amelihifadhi Neno kwa karne zote Mt.24:35 Neno la Mungu litadumu milele Rum.15:4 Makusudi ya Neno kutupa tumaini 2Tim.3:15 Neno linatuhekimisha nakutupa wokovu Yoh.5:39 Neno linaonyesha Yesu kama Mwokozi 2Tim.2:15 Tunapojifunza inatupasa kulitumia Yoh.16:13 Roho hutuongaza kutulia 1Kor.2:13 Mungu atatuongoza Isa.28:9-10 Kulinganisha andiko na andiko Yoh.17:17 Ukweli umo katika Neno la Mungu Yoh.7:17 Tunapoliendea Neno la Mungu kwa moto ulio tayari kulipokea atatuongoza (Ufu.hatatuacha Biblia ina vitabu 66 vilivyoandikwa na waandishi 44. USHAHIDI WA KUVUVIWA KWA BIBLIA NI PAMOJA NA: UBII-SOMA MAFUNGU HAYA: Babeli(Isa.13:19-22), Tiro (Eze.26:3-5), Sidoni (Eze.28:21-23), Koreshi (Isa.44:28;45:1) Umedi, Uajemi na Uyunani (Dan.8:20-21), na mahali alipozaliwa Yesu (Mika.5:2).
  2. UKWELI KUHUSU BIBLIA
    Biblia ina vitabu 66 iliandikwa na waandishi  44. Iliandikwa kwa kipindi cha zaidi miaka 1500. Ushahidi wa kuvuviwa kwa Biblia ni pamoja na: Unabii-Soma mafungu haya:Babeli (Is. 13:19-22), Tiro (Ez. 26:3-5), Sidoni(Ez.28:21-23), Koreshi(Isa.44:28;45:1). Umedi na Uajemi na Uyunani (Dan. 8:20-21 ), na mahali alipozaliwa Yesu(Mika 5:2). ELIMU YA KALE -Jiwe la Moabu liligunduliwa mwaka 1868 kule Dibon, Yordani,linahibitisha mashambulio ya Moabu na Israeli kama ilivyoandikwa katika 2Fal.2na3. Barua za Lakishi ziligunduliwa mwaka 1932-1938, maili 24 kaskazini ya Beersheba, zinaelezea shambulio la Nebukadreza dhidi ya Yerusalemu mwaka 586K.K. magombo ya Bahari ya chumvi yaligunduliwa mwaka wa 1948. Yanaonyesha yaliandikwa mwaka 170-150K.K., nayo yana vitabu vyote vya Agano la Kale au sehemu zake, isipokuwa kitabu cha Esta. Yanathibitisha usahihi wa Biblia. Jiwe la Rosetta liligunduliwa mwaka 1799 kule Misri na wanasayansi wa Napoleon, liliandikwa kwa lugha tatu -maandishi ya kale ya Misri (yaliyo tumia michoro ), lugha ya Misri wa kawaida na Kiyunani. Jiwe hilo lilisaidia kuyaelewa maandishi ya picha. Kuyaelewa hayo, kunasaidia kuthibitisha ukweli wa Biblia. INAVYO AFIKIANA YOTE -Ushahidi wa kuvuviwa kwa Biblia ni pamoja vile inavyo afikiana kama kitu kimoja. Kuna sehemu zaidi ya 3000 ambapo Biblia inajieleza kuwa Biblia imevuviwa(2Pet.1.21). Hakuna inapopingana. Ama imevuviwa na Mungu au udanganyifu. KRISTO AFUNULIWA-Ushahidi mkubwa kuliko wote wa kuvuviwa kwa Biblia, unaonekana ndani ya Kristo ambaye inamfunua na katika mabadiliko ya maisha yanayo tokea kwa wale wanaoisoma(Yn.5:39;Mdo.4:12,Mt.1:26-28).
  3. SOMO: MUNGU (MWENYE TABIA YA UPENDO)

     hofu zetu. Isa.41:10 AnaahidZab:90:3 Tangu milele hata milele Dan.2:20 Anao uwezo na hekima yote Dan.2:21 HuuzuluHuuzulu na kumilikisha ufalme Isa.46:10 Huyatangaza mambo ya baadaye tangu mwanzo Isa.45:21 Ni yeye peke yake aliye na uwezo wa kuonyesha mambo ya siku za usoni. Za.33:6-9;Mwa.1:1 Ni Muumbaji mwenye uwezo wote. Kut.34:6-7 Ni mvumilivu, mwenye fadhili na mwingi wa rehema. Yer.31:3 Anatuvuta kwa wema uliojaa upendo. Zab.24 Ni mmiliki wa ulimwengu wote. Zab.19:1 Mbingu za hubiri utukufu wake. Zab.34:1-4 Anatualika tumsifu yeye naye atatuponya
  4. SOMO: CHANZO CHA  UOVU


    1Yoh. 4:8 Mungu  ni pendo. Mat. 13:24-28 Adui Mungu na mwanadamu hupanda magugu. Ez. 28:12-17 Zamani Lusifa alikuwa malaika mzuri aliyeumbwa na Mungu akiwa na uhuru wa kuchagua .Isa. 14:12-14Lusifa alitamani kukiinua kiti chake kuliko cha  Mungu. Ufu. 12:7-9 Vita ikaanza kule mbinguni. Luka. 10:18 Shetani  atupwa chini. Mwa. 1:27-31Mungu alimuumba mwanadamu akamweka kwenye bustanini. Mwa. 3:1-7 Shetani aliwafanya Adamu na Hawa wasimwamini Mungu. Isa. 59:1-2 Dhambi  hututenga na Mungu. Rum. 6:23 Hatima ya uasi ni mauti. Yer. 17:9 Hali ya mwanadamu kubadilika. Rum. 5:12; 6:16 Jamaa yote wanadamu ikatumbukia katika hatia, uasi na dhambi. Ebr. 2:14-17;Ebr. 4:15 Yesu alitwaa asili ya ubinadamu aliyakabili majaribu ya mwanadamu naye akashinda. Rum. 5:17-19 Yesu alilipa fidia kwaajili  ya kosa la adamu. Rum. 3:24-25 Kupitia kwa Yesu tunapata wokovu kama zawadi. Isa. 41:13 Yesu yu pamoja nasi katika shida zetu. Eze. 28:17-18 Hatimaye Shetani ataangamizwa kabisa. Ufu. 21:1- 5 Mungu wetu atafanya mbingu mpya na nchi mpya. Nah. 1:9 Kamwe dhambi haitainua tena kichwa chake kibaya kwa mara nyingine. 
  5. SOMO:  UNABII JUU  YA MASIHI
    Mika. 5:2 Mahali alipozaliwa -Bethlemu(Luk. 2:1-7). Isa. 7:14 Kuzaliwa na Bikira (Mat. 1:23). Mwa. 49:8-10 Kuzaliwa katika kabila la Yuda (Lk. 1:30-32). Yes. 24:17 Nyota itatokea katika Yakobo (Mt. 2:1-2). Isa. 61:1-3 Huduma ya Masihi ilitabiriwa kabla (Lk. 4:16-21). Zab. 52:12-13 Alisalitiwa na rafiki yake (Mt.26:47-50). Zek.11:12-13 Alisalitiwa kwa vipande 30. Fedha iliyonunua konde la mfinyanzi (Mt. 27:3-9). Isa. 53:4-7 Aliongozwa kwenda machinjioni. (Yoh. 1:29; Mdo. 8:32-35). Zab. 22:16 Mikono na miguu ya Yesu ilitobolewa, hakupigwa kwa mawe (Lk. 23:33; 24:39). Zab. 22:18 Mavazi kupigiwa kura (Mt. 27:35). Zab. 22:1 Maneno ya mwisho ya Yesu (Mt. 27:46). Zab. 34:20 Mifupa haikuvunjwa (Yoh. 19:36). Isa. 53:9 Alizikwa katika kaburi la tairi (Mt. 27:57-60). Zab. 16:10 Alifufuliwa kutoka kwa wafu (Mt. 28:2-7).
  6. UUNGU WA KRISTO
    Mat. 1:23 "Emanuel Mungu pamoja nasi" Yoh. 1:1-14 Neno alikuwa Mungu. Yoh. 17:5-24 Yesu alikuwako pamoja na Baba. Yoh. 8:58 Alijieleza hana mwanzo na mwisho. Kuto. 3:14 MIMI NIKO NI JINA LA MUNGU. Luk. 5:20-24 Yesu alisamehe dhambi ni Mungu pekee anaweza fanya hivyo. Yoh. 20:28 Tomaso alishudia Yesu kuwa Bwana na Mungu. Ebr. 1:5-9 Baba alimwita Mwana kuwa ni Mungu. Isa.9:6 Yesu ni wa milele. Mik. 5:2 Matokeo ya Yesu yamekuwa tangu milele. 1Tim. 6:15-16 Yesu hapatikani na mauti. Ufu. 1:18 Yesu ni wa kwanza na mwisho, Yesu anafunguo za kuzimu na mauti. Flip. 2:5-12 Yesu aliacha Uungu kwa hiari ili awe Mwokozi.
  7. SWALI LINALOULIZWA MARA KWA MARA JUU YA UUNGU WA KRISTO 

    Je, Biblia haifundishi kwamba Yesu ni mzaliwa wa kwanza wa viumbe vyote, na kwahiyo, yeye ni kiumbe kilicho umbwa wala hakuwa na Baba yake tangu milele? Fungu linalo zungumziwa ni Lol. 1:15 ambalo humwita Yesu kuwa mzaliwa wa kwanza wa viumbe vyote. Neno la Kiyunani linalotumika hapa prototokos ambalo humaanisha mwenye cheo cha juu kupita wengine wote -yaani yule ambaye anabaki zote na heshima ya Mungu Yesu ni mzaliwa wa kwanza si kwa wakati, bali kwa maana ya heshima. Haki zote za mzaliwa wa kwanza ni zake. Daudi mwana wa nane kwa Yese, lakini aliitwa mzaliwa kwanza. Yesu alisema mimi ndiyo yule "Mimi niko"(Yoh. 8:58), akimaanisha asiye na mwanzo wala mwisho. Alisema, "Yeye Ibrahim asijakuwako Mimi niko".Isaya, nabii, anamwita Baba wa milele (Isa. 9:6). Mika anasema kuwa mwanzo wake tangu milele (Mika 5:2). Yohana anasisitiza, "Hapo mwanzo kulikuwa na Neno naye Neno alikuwako kwa Mungu, naye Neno  alikuwa Mungu. (Yohana 1:1)Yesu alikuwa na haki na heshima ya Mungu. Hakuona kule kuwa sawa na Mungu lilikuwa jambo la kung'angani wakati Ulimwengu huu umepotea, kwahiyo kwa hiari yake aliondoka mbinguni na kuja hapa kwa wanadamu. Aliishi katika mwili wa kibinadamu, alipambana na vita vya majaribu kama sisi tunavyo pambana navyo na alishinda kwa niaba yetu (Flp. 2:5-11,Ebr.2:14-17).
  8. WOKOVU



    1Yoh. 4:8-9 Upendo Mungu ulimfanya atukombowe. Mwa. 12:7-31Mungu aliwaumba watu kwa mfano wake. Mwa. 3:8 Dhambi huharibu uhusiano wetu na Mungu na kutufanya tumkimbie (Isa. 59:1-2). Rum. 6:23 Tunapo kuwa tumetengwa na Mungu tunasitahili kufa milele. Rum. 3:23 Wote wamefanya dhambi, nao wako chini ya adhabu ya mauti. Rum. 5:18-19 Adamu alileta mauti Yesu ameleta uzima. Gal. 3:13 Yesu alichukua laana yetu. Ebr. 2:8-9 Yesu alionja mauti badala yetu. 2Kor. 5:21 Yesu alifanywa kuwa dhambi. Mdo. 3:19 Tunapotubu anatuwia radhi. 1Yoh. 1:9 Tunapo ungama anatusamehe. Rum. 8:1Tunapompokea Yesu, hakuna hukumu tena juu yetu. Efe. 2:8 Tunaokolewa kwa neema kwa njia ya imani. Yoh. 1:12Tunapomwamini, tunakuwa watoto wa Mungu. 1Yoh. 5:11-13 Tunapomwamini tunapokea karama ya uzima wa milele. Yoh. 3:16 Wokovu ni uzoefu wa wakati huu na ni kipawa cha Mungu kwa wamwaminio.
  9. SWALI LINALOULIZWA MARA KWA MARA JUU YA WOKOVU 

    Je, Biblia haifundishi kuwa mara unapo kuja kwa Yesu huwezi kupoteza tena wokovu wako? Yoh. 10:28 husema hivi, "Nami nawapa uzima wa milele ;wala hawatapoteza kamwe; wala hakuna mtu atakaye wapokonya mikononi mwangu." Tunapokuja kwa Yesu tunapokea msamaha wake kwa imani, tukiipokea neema yake, tunapokea kipawa cha uzima wa milele(Ef.2:8,Rum.3:22-25). Wokovu ni kipawa cha bure. Si kitu kinachostahili kutokana na utii wetu. Wokovu ni kwa neema kwa njia ya imani. Yule mlinzi wa gereza alipouliza, "Bwana zangu nifanye nini nipate kuokoka? "Paulo alijibu, akasema, "Mwamini Bwana Yesu" (Mdo. 16:30-31). Imani ni matokeo ya utashi wa mtu. Moyo ule ule unaochagua kuamini unaweza kuchagua kutokuamini na kutokuamini husababisha mauti ya kiroho(Ebr.3:12-14). Tusipo shikilia sana uthabiti wetu kwa Mungu mpaka mwisho, tutakuwa tunajenga moyo wa kutoamini. "Mwenye kuvumilia hata mwisho ndiye atakayeokoka."(Mt. 24:13). Tunaokolewa tu pale tunapoendea kukumbuka yale yaliyohubiriwa na kuishi maisha ya Imani (1Kor. 15:1-2). Siku zote kunauwezekano wa kuyatumia maisha ya zamani ya dhambi, na majina yetu kufutwa kwenye vitabu vya uzima na kupotea milele(2Pet.2:19-22,Uf.3:5,1kor.9:27). Neno "kukataliwa" analolitumia Paulo katika 1Kor.9:27 ni neno lile lile ambalo linatumika katika Yer.6:30 Kuhusu wale watakaoteketezwa na hatimaye kupotea. Katika Ya. 10:28, tunapokuja kwa Yesu tunapokea uzima wa milele. Kama vile kuingia kwake mioyoni mwetu kwa njia ya imani kunavyo leta uzima, ndivyo kutokuamini kwetu kunavyo leta mauti ya kiroho. Hatuwezi kutangua kuzaliwa kwetu, tunaweza kufa. Hakuna chochote kinachoweza kutupokonya mikononi mwake isipokuwa uamuzi wetu wenyewe. 
  10. MAMBO YA BAADAYE KUHUSU ULAYA YAFUNULIWA 
    Dan. 2:1 Nebukadreza aliota ndoto ambayo hakuikumbuka. Dan. 2:2-1 Wenye hekima wa mfalme hawakuweza kuijua wala kuifasiri ndoto. Dan. 2:16 Danieli alisihi apewe muda ili apate kuomba. Dan. 2:21-23 Mungu alimwonyesha Danieli ile ndoto. Dan. 2:28 Yuko Mungu mbinguni afunuaye siri. Dan. 2:29-30 Ndoto hii ilionyesha mambo yatakayotokea  baadaye. Ndoto yafunuliwa:Dan.2:31 Sanamu kubwa. Dan. 2:32-36 kichwa cha dhahabu na mikono ya fedha, tumbo na viuno vyake ni vya shaba, miguu ya chuma, nyayo za chuma na udongo. Jiwe linavunja ile sanamu vipande vipande. Ndoto ya fasiriwa :Dan. 2:36 "Nasi" (Mungu na Danieli ) tutaihubiri fasiri yake. Dan. 2:38 Ee Nebukadreza "Wewe ukichwa kile cha dhahabu."ufalme wa Babeli ulitawala dunia toka mwaka wa 605K.K.-539K.K. Dan. 2:39 Ufalme mwingine mdogo kuliko wewe. Dan. 5:28-31 Wamedi na Waajemi waliwashinda Wababeli. Isa. 44:27-28; 45:1 Unabii wa kushangaza kwa Koreshi, jemadari wa Wamedi na Waajemi, angeshambulia na kuiangusha Babeli na kuwaachilia huru watu wa Mungu. 

  11. UNGAMO NA MSAMAHA

    Mik. 7:18-19 Mungu husamehe kwa hiari yake. Ebr. 8:12 Mungu husamehe hakumbuki tena dhambi. Mdo. 3:19 Anayafuta makosa yetu. 1Yoh. 1:9 Anasamehe bila kushinikizwa. Isa.44:22 Anazifuta dhambi zetu kama wingu Zito. Isa. 43:25 Mungu hazikumbuki dhambi zetu tena. Zab. 32:1 Msamaha huleta furaha. Isa.55:7 Mungu husamehe kabisa. Neh. 9:17 Hata katika uasi wetu, Mungu yuko tayari kutusamehe. Kol. 1:14 Kusamehe ni sehemu ya tabia ya Mungu. Zab. 103:3 Msamaha wa Mungu ni kamili. Luk. 7:47 Anatusamehe dhambi zetu zilizo nyingi. Ef. 4:32 Tunasameheana sisi kwa sisi kwakuwa Yeye alitusamehe. 2Kor. 2:7-9 Kufanana na Kristo ni kusamehe.
  12. JINSI YESU ATAKAVYOKUJA MARA YA PILI
    Yoh. 14:1-3 Yesu aliahidi kwamba atarudi. Mdo. 1:9-11 Malaika walithibitisha ahadi yake. Yud. 14. Henoko mtu wa saba alitabiri kurudi kwa Yesu. Zab. 50:3 Daudi alisema Mungu wetu atakuja. Ufu.1:7 Yesu atakuja kila jicho litamwona. Mt. 24:27. Kuja kwake kutakuwa kama umeme. 1The. 4:16-17 Litakuwa ni tukio linalosikika. Wafu wenye haki watafufuliwa na watanyakuliwa na walio hai wenye haki pamoja kwenda mbinguni. 1Kor. 15:51-54 Mungu atawavika watu wake kutokufa. Mt.16:27 Kurudi kwake litakuwa tukio lenye utukufu. Anakuja na ujira. Ufu. 6:14-17 Waovu wataogopa. Mt. 13:37-43 Waovu wataunguzwa kwa moto. Isa. 25:9 Wenye haki watafurahi kumwona akija. Ufu. 19:11-16 Atakuja kama Bwana aliye shinda na Mfalme. Tit. 2:13 Kuja kwake kutaitwa tumaini lenye baraka. Ufu. 21:11-20 Mwito wa Mwisho kutoka kwa Yesu ni kujiandaa kwaajili ya ujio wake .
  13. DALILI ZA KUJA KWA YESU




     Mt. 24:3 Wanafunzi walimuuliza Yesu nini dalili ya kuja kwako? Mt. 24:1-24 Walimu Wa Dini wa uongo. Mat. 24:6-7 Vita na tetesi za vita. Ufu. Mataifa yatakapo kasiriaka. Luk. 21:26 Watu wakivunjika mioyo kwa hofu. 1The. 5:2-3 Mazungumzo ya amani. Mat. 24:7 Maafa ya asili. Mat. 24:12 Kuongezeka kwa uhalifu, ukatili na uovu . 2Tim. 3:1-4 Nyakati za hatari, Mmomonyoko maadili. Mt. 24:37-39 Ulafi, ufisadi. Yak. 5:1-5 Matatizo ya kiuchumi. Luk. 21:34 Kulemewa na masumbufu ya maisha haya. Mat. 24:14 Injili kuhubiriwa ulimwenguni kote (ufu. 14:6-7). 2Pet. 3:8-10 Mungu amechagua kuwaokoa wote. Mat. 24:48 Mtumwa mbaya anasema, "Bwawa wangu amekawia". Mat. 24:42-44 Ushauri wa Mungu, "Jiwekeni tayari ".
  14. HUKUMU
    Ufu. 14:6-7 Ujumbe wa mwisho unazungumzia hukumu. Ufu. 22:12 Yesu anakuja kulipa ujira kama niwema au ubaya. Mat. 12:36 Yesu alieleza hukumu kama tukio litakalo tokea baadaye. Mdo. 24:25 Paul anahojiana na Feliki juu ya hukumu itakayokuja. Dan. 7:9-10 Daniel aliona kikao cha mahakama kuu. Mhu. 12:13-14 Mungu ataleta hukumuni kila neno. Ebr. 4:13 Mambo yote yako wazi mbele za Mungu. 2Kor. 5:10 Sisi Sote imetupasa kusimama mbele ya kiti cha hukumu cha Kristo. Rum. 14:12 Kila mtu atatoa habari zake mbele za Mungu. Zab. 87:6 Katika hukumu, Bwawa ataangalia mahali tulipozaliwa. Yer. 2:22 Uovu wetu wote umeandikwa mbele za Mungu. Mal. 3:16 Matendo yetu yote ya haki yanaandikwa mbele za Mungu. Ufu. 20:12 Hukumu itategemea habari za maisha yetu. Mdo. 3:19 Tukitubu na kuziacha dhambi zetu, Bwana atazifuta. Ufu. 3:5 Tukiendelea na dhambi, majina yetu yanafutwa kwenye kitabu cha uzima. Rum. 8:1 Njia pekee ya kushinda laana ya hukumu ni kupitia Yesu. Ebr. 7:24-25 Kuhani wetu Mkuu (Yesu ) anaweza kuwaoka wote wanaoingia. Yoh. 14:26 Roho Mtakatifu Ni mwalimu aliye tumwa na Mungu. Mat. 12:31-32 Kukataa uwezo wa Roho Mtakatifu unaotuongoza, kushawishi na kutufundisha ni kutenda dhambi isiyo sameheka.
  15. AMRI ZA MUNGU 

    Zab. 111:7-8 Amri za Mungu ni kanuni ya milele ya tabia ya mbinguni ambayo inasimama milele. Rum. 3:20 Sheria ya Mungu inatufanya tuone hatia yetu na kutuelekeza kwa Yesu. Zab. 19:7 Sheria ya Mungu ni njia ya kutuongoza ili tufikie wongofu. Zab. 19:11 Katika kuzishika Amri zake kuna thawabu kubwa. Rum. 6:14 Hatuko chini ya Sheria kama njia ya kujipatia wokovu. Siku zote wokovu huja kwa neema (Waefeso 2:8). Rum. 6:15 Ingawa hatuko chini ya sheria, haina maana kwamba tuko huru kuvunja sheria ya Mungu. 1Yoh. 3:4 Dhambi ni uvunjaji wa sheria ya Mungu. Isa. 59:1-2 Dhambi au uvunjaji wa sheria hutufanya tutengwe na Mungu na kutuletea mauti ya milele (Rum. 6:23). Rum. 3:28-31 Tunapokuwa tumeokolewa kwa imani, tunakuwa na shauku ya kuishika sheria ya Mungu (Ebr. 10:7;Yoh.8:29). Yoh. 14:15 Mkinipenda mtazishika Amri zangu, upendo daima huleta utii. 1Yoh.2:4-5 Asiye zishika amri zangu ni mwongo, wala kweli haimo ndani yake. Ebr. 8:10 Katika agano jipya, Yesu huiandika sheria yake moyoni. Zab. 40:8 Anatia ndani yetu shauku ya kuyafanya mapenzi yake. Uf. 14:12 Watu wa Mungu wa siku za mwisho watakuwa wanazishika amri za Mungu kwa njia ya imani. Uf. 12:17 Watu walio salia, sawa na waaminifu wa vizazi vilivyopita, watakuwa wanashika sheria yake
  16. SABATO 
Uf. 14:6-7 Ujumbe wa mwisho wa Mungu kwa wanadamu ni wito wa kumsujudia Muumba. Uf.14:11 Msingi wa kumwabudu Mungu ni ule ukweli kwamba alituumba. Ef. 3:9 Kwakuwa Yesu ndiye aliyekuwa mtendaji katika uumbaji, wito wa mwisho katika ufunuo wa kumsujudia Muumbaji ni wito wa kumheshimu Yesu. Kut.20:8-11 Tumwabudu yeye kama Muumbaji kwa kuishika Sabato yake. Mwa.2:1-3 Sabato iliwekwa wakfu wakati ule wa uumbaji. Mungu alipumzika katika siku ya saba, akaibariki na kuitakasa. Mark.2:27-28 Sabato ilitolewa kwa wanadamu wote yapata miaka 2300 kabla ya kuwepo Wayahudi ili kuwa ukumbusho kwa wanadamu wote. Ez.20:12-20 Sabato ilianzishwa kwaajili ya wanadamu wote kama ishara katika ya Mungu na watu wake. Luk. 4:16 Yesu alikuwa mshika Sabato mwaminifu. Mat.24:20 Yesu alitabiri kwamba Sabato ingekuwa bado inashikwa katika mwaka 70B.K. Wakati wa kuangamizwa kwa Yerusalemu, yaani,zaidi ya miaka 35 baada ya kifo chake. Mdo. 13:42-44 Paulo alikuwa akishika Sabato, tena alikutana na mji mzima, wakiwemo Wayahudi na watu Wamataifa  ili kumwabudu Mungu. Mdo. 16:13 Kule Filipi, Paulo alikutana na kundi la waumini nje ya mji kwa vile kulikuwa hakujawa na Kanisa la Kikristo. Uf. 1:10 Bwana bado alikuwa na siku maalumu mwishoni mwa karne ya kwanza. Uf. 1:10 Haisemi wazi wazi siku ya Bwana ni ipi lakini Mat. 12:8, Mark. 2:27-28,na Luk. 6:5 Zinasema wazi. Mat. 12:8 Mwana wa Adamu ndiye Bwana wa Sabato. Kama Mwana wa Adamu ndiye Bwana wa Sabato, basi, Sabato ni lazima iwe ndiyo siku ya Bwana. Luk. 23:54-56,24:1 Mafungu haya yanaorodhesha siku tatu zinazofuatana moja baada ya nyingine. Siku aliyo kufa Kristo - maandalio - Ijumaa. Siku ambayo Yesu alipumzika kaburini - Sabato - Jumamosi. Siku aliyo fufuka Yesu - Siku ya kwanza ya Juma - Jumapili. Ni kwamba Sabato ni Jumamosi, yaani, siku ya saba ya juma. Ebr. 13:8 Yesu ni yeye yule jana, leo na hata milele. Isa. 66:22-23 Katika mbingu mpya na nchi mpya tutaishika Sabato kila Juma. 

MAFUNGU YANAYOHUSU SIKU YA KWANZA YA JUMA 
KUT. 31:17-18 Sabato ni ishara kati ya Mungu na watu wake milele. Ez. 20:12 Sabato ni ishara ya utakaso. Ebr. 4:4-9 Sabato ni ishara ya pumziko letu ndani ya Yesu tukimtumaini yeye kwaajili ya wokovu wetu. Luk.23:56 Wafuasi waminifu wa Yesu hawakupaka mafuta mwili wa Yesu siku ya sabato. Hakika sabato ilikuwa haijagongomelewa msalabani, kwa maana wanafunzi wake waliishika baada ya kifo chake. Lk. 24:1 Wanafunzi walikwenda kuupaka mafuta mwili wa Yesu siku ya kwanza ya Juma. Mt. 28:1 Wanawake walikwenda kaburini siku ya kwanza ya Juma. Mk.16:2 Wanawake walikwenda kaburini siku ya kwanza ya Juma. Mk.16:9 Yesu alifufuka siku ya kwanza ya Juma. Yoh. 20:1 Mariamu alikwenda kaburini  alfajiri kungali giza bado . (Zingatia- mafungu yaliyo tajwa hapo juu hayawezi kuwa yanaonyesha utakatifu wowote ambao jumapili ilipewa na waumini wa mwanzo, kwa vile mpaka wakati huo walikuwa hawajajuwa kuwa Yesu amefufuka.) Rum. 6:3-5 Ishara ya ufufuo ni ubatizo wa kuzamishwa majini, sio ibada ya jumapili. Mdo. 20:7 Katika mkutano ule ulio fanyika jumamosi usiku ambao ni usiku wa kuamkia siku ya kwanza ya Juma, Paulo alihubiri mpaka usiku wa manane. Siku iliyofuata yaani jumapili, alisafiri kwa miguu kwenda Troa, akapanda merikebu. Hakika, Paulo hakuwa mtu anayetakasa jumapili. Yoh.20:19 Wanafunzi wake walikusanyika siku ya kwanza ya Juma, si kwa madhumuni ya kufanya ibada, bali kwa sababu ya hofu Wayahudi. 1Kor. 16:2 "Kwake" inamaanisha yeye mwenyewe nyumbani kwake. Lugha ya asili inazungumzia kufunga mahesabu. Sabato imekwishapita . Ni siku ya kwanza ya Juma - ni wakati mzuri kule nyumbani wa kutenga fedha za kulipia madeni, kufunga mahesabu na kutenga sadaka kwaajili ya kazi ya Bwana. Mwanzo 2:1-3 Mungu aliibarikia siku ya Saba yaani Sabato katika siku ya uumbaji. Rum. 13:10 Upendo wetu kwa Mungu unatufanya sisi kama watumishi waminifu kutimiza au kushika sheria. Mt. 5:17 Yesu hakuja kutangua, bali kuitimiza torati. Rum. 8:4 Tunapomwendea ,anatuwezesha kwa njia ya Roho wake kuishika sheria. 

JARIBIO LA KUBADILI SHERIA YA MUNGU 

Yoh. 17:17 Neno lako ndilo kweli. Mit. 23:23 Inunue kweli, wala usiiuze. Ebr. 13:8 Yesu ni yeye yule, jana ,leo na hata milele. Zab. 89:34 Mimi sitalihalifu agano langu (sheria). Kut.31:18 Amri kumi ziliandikwa kwa chanda cha Mungu . Mat.5:17-18 Yesu alikuja kutimiza na sio kubadili sheria ya Mungu. Mwa. 2:1-3 Sabato iliwekwa wakfu , ikatakaswa na kubarikiwa katika Edeni. Lk 4:16 Yesu alishika sabato. Mdo. 13:42-44 Paulo alishika sabato. Mdo. 20:28-31 Ilitabiriwa uasi ungeingia kanisani wakati wa Ukristo wa mwanzo. Dan. 8:12 Kweli iliangushwa chini. Dan. 7:25 Jaribio la kubadili sheria ya Mungu. Isa. 8:16 Ukaitie mhuri sheria. Kut. 20:8-11 Sabato inayo mambo matatu yanayohitajika katika muhuri rasmi wa Kifalme wa mbinguni :Jina la Mungu, cheo chake, na himaya anayotawala. Ufu. 7:1-3 Watu wa Mungu watapokea muhuri wa sabato kabla ya ule wa mwisho. Ufu. 14:7-12 Ujumbe wa mwisho toka kwa Mungu unatutaka tumwabudu Muumbaji na kuzishika amri zake. 

UTUNZAJI WA SABATO
Isa. 56:2 Mungu anatoa baraka za pekee kwa wale wanaotunza sabato. Kum. 28:1-15 Mungu anatoa baraka kwa wale wanaotunza amri zake. Kut.20:8-11 Sabato ni siku "iliyotakaswa "iliyotengwa na zingine zote. Law. 23:3 Sabato inaitwa "kusanyiko takatifu "au kusanyiko la watu wa Mungu. Ni siku pekee iliyoteuliwa kwaajili ya Ibada. Lk. 4:16 Kila sabato Yesu alikwenda kuabudu. Kama vile Paulo alivyofanya (Mdo. 18:4). Law. 23:32 Sabato huanza machweo ya Ijumaa na kumalizika machweo ya Jumamosi (Mk. 1:32). Kut. 20:8-10 Sabato si siku ya kufanya kazi za kidunia. Isa. 58:13-14 Sabato ni siku ya kujifurahisha katika Bwana. Sio siku ya kufanya anasa zetu wenyewe. Mambo kama riadha, michezo au burudani za kidunia ,ambazo hazipatani na utakatifu wa sabato. Neh. 13:15-22 Sabato inaweza kunajisiwa kwa kununua, kuuza na kuihafifisha kwa kufanya kazi za kawaida za kidunia. Mt. 12:11-13 Katika maisha ya Yesu mwenyewe alitoa kielelezo cha furaha inayotokana na kutenda mema siku ya sabato. Mk. 2:23-28 Yesu aliwapa wanafunzi mahitaji yao ya kimwili  katika siku ya sabato. Sabato ni kielelezo cha Mungu anayekidhi mahitaji yetu. Kut. 16:28-30 Wakati baadhi ya Waisraeli walipofanya kazi siku ya sabato wakijaribu kuokota na kutayarisha mana, wakiwa wamepuuza mpango wa Mungu wa siku ya maandalizi, yaani, Ijumaa, Mungu aliwakemea wazi wazi. Mt. 11:28-30 Wito wa Mungu ni kwenda kupata pumziko ndani ya Kristo. Kila sabato inatupatia nafasi ya kufanya upya kujitoa kwetu kwa Bwana. 

IMANI 
Ebr. 11:6 Pasipo imani haiwezekani kumpendeza Mungu. Rum. 12:3 Mungu amempa kila mtu kiasi fulani cha imani. Mk. 11:22-24 Tukiitumia imani tuliyo nayo, milima ya matatizo yetu itaondolewa. Rum. 10:17 Imani yetu huongezeka tunapo ya sikia maneno ya Mungu. Ebr. 11:1 Imani ndio msingi unaotegemeza uzoefu wetu wote wa Kikristo. Ebr. 4:2 Tunanufaika kwa neno la Mungu tunapolitumia katika maisha yetu. 1Yoh. 5:14 Imani ni kutumainia Mungu, hali inayotuwezesha kufanya mapenzi yake. La. 5:20 Imani inaweza kuonekana. Inadhihirishwa katika matendo. Mt. 17:20 Imani ndogo kama mbegu ya haradali, inaweza kukua. Efe. 2:8 Tunaokolewa kwa neema kwa njia ya imani. Rum. 1:5 Neema inaleta utii utokanao na imani. Gal. 2:20 Mkristo huishi kwa imani. Ebr. 10:38 Mwenye haki ataishi kwa imani. Ebr. 6:12 Kwa njia ya imani tunarithi ahadi za Mungu. Yak.2:17 Imani pasipo matendo imekufa. 1Yoh.5:4 Tunaushinda ulimwengu kwa njia ya imani. 

AFYA 
3Yoh.1:2 Mungu anapenda tufanikiwe na kuwa na afya 1The.5:23 Utakaso unajumuisha mwili, akili, na hisia pamoja na uwezo wa kiroho. Rum. 12:1-2 Itoweni miili yenu iwe dhabihu iliyohai takatifu kwa Bwana 1Kor. 6:19-20 Mwili wenu ni hekalu la Mungu. 1Kor.10:31 Chochote mnachokula au kunywa, fanyeni yote kwa utukufu wa Mungu. Mit. 20:1 Mvinyo hudhihaki, kileo huleta ugomvi. Mit. 23:29-32 Usinywe divai iliyochachuka. Inaleta huzuni, misiba na ugomvi. Hudanganya na kupotosha hukumu. Isa. 5:11 Ole wao wanaolewa kwa mvinyo. Mit. 4:17 Ulevi kupindukia huleta ukatili. Mit. 31:4-5 Mvinyo haifai kwa Wafalme au Wakuu kwakuwa inapotosha hukumu ambayo ingekuwa ya busara. Ufu. 5:10 Kwakuwa sisi ni wafalme na makuhani kwa Mungu, tunahitajika kuwa na akili safi. Mwa. 1:29 chakula cha awali alichotupa Mungu ilikuwa mimea. Mwa. 7:2 Nuhu alifahamu tofauti kati ya wanyama safi na walio najisi. Kwakuwa tangu wakati wa gharika, Mungu aliruhusu kula nyama, wanyama walio safi walingizwa saba saba. Wale najisi walao mizoga waliingizwa wawili wawili. Law. 11:1-12 Utofauti kati ya wanyama najisi na wasio najisi. Isa. 66:15-17 Wale wanaoasi kanuni za chakula alizoziweka Mungu hawataurithi ufalme wa Mungu. Isa. 65:1-5 Mungu anauweka ulaji wa vyakula najisi kundi moja na ibada ya sanamu. Mdo. 10:9-16 Nguo iliyomshukia Petro ilijaa wanyama najisi wa kila namna. Mungu akamwambia Petro inuka uchinje ule. Petro akaogopa! Mungu ana maana gani? Fungu la 17 linaonyesha kuwa Petro aliona mashaka. Mdo 10:28 Petro alieleza kwamba maono hayo hayakuhusu chakula, bali yalihusu kuwaita watu wa mataifa najisi. Katika maono haya, Mungu aliondoa kizuizi cha ubaguzi wa kijamii uliokuwepo. Sasa Petro anaweza kuwashuhudia wamataifa. Maono haya yanahusu ukweli kwamba kwa njia ya msalaba, ubaguzi wote miongoni mwa watu ulikuwa imeondolewa. Flp. 4:13 Yesu hupatia nguvu za kiroho ili kuyashinda mazoea ya kimwili. Ebr. 4:15-16 Yesu alijaribiwa kama sisi tunavyojaribiwa. Alifunga siku 40 na kushinda ili sisi pia tuweze kupokea nguvu zake zitakazotuwezesha kushinda.

HALI YA WAFU 


Yoh. 11:11-14 Yesu anafananisha kifo na usingizi. Biblia inafananisha kifo na usingizi mara 50. 1The.4:15-16 Wale waliolala katika Kristo watafufuliwa siku akija. Yoh. 5:28-29 Kuna ufufuo wa aina mbili (wa uzima na wa mauti). Mwa. 2:7 Mungu alimuumba mtu kwa mavumbi ya ardhi na kumpulizia puani pumzi ya uhai, na mtu akawa nafsi hai. Mungu hakuweka nafsi ndani mtu. Mhu.12:7 Mwili hayarudia mavumbi na roho humrudia Mungu. Biblia haisemi nafsi humrudia, bali roho. Ayu. 27:3 Roho ni sawa na pumzi au uweza wa Mungu uletao uhai. Zab. 146:3-4 Pumzi au roho inapomrudia Mungu mawazo yote hupotea. 1Tim. 6:16 Wanadamu hawana uzima wa milele, ni wa Mungu pekee asiyepatikana na mauti. Rum. 2:7 Sisi tunatafuta uzima wa milele. Biblia inalitumia neno "roho " mara 1600, lakini hakuna mahali inaposema "isiyokufa. 1Kor.15:51-54 Yesu atakaporudi ndipo tutakapovikwa kutokufa. Zab. 115:17 Watu hawamsifu Mungu. Mdo. 2:38 Daudi hakupanda mbinguni alipokufa, bali anangojea kuja kwa Yesu na ufufuo wa kwanza. Zab. 6:5 Katika kaburi watu hawamkumbuki Mungu. Mhu. 9:5 Wafu hawajui neno lolote. Ayu. 19:25-26 Wenye haki watafufuliwa ili wamone Mungu siku ya mwisho. Eze. 18:4 Roho (Mtu ) itendayo dhambi itakufa! Rum.6:23 Mshahara wa dhambi ni mauti. Mauti ni kutokuwa na uhai. Karama ya Mungu ni uzima wa milele. 2Tim. 4:7-8 Mtume Paulo alikuwa anangojea kuja kwa Bwana ili apate sawabu yake ya mwisho. Ufu. 22:12 Yesu atakuja na ujira wake wa uzima wa milele siku atakaporudi. 

MILENIA (MIAKA 1000 YA AMANI )
Yoh. 14:1-3 Ahadi ya Yesu juu kurudi kwake. Mdo. 1:9-11 Yesu huyu huyu mliemuona akienda mbinguni atakuja jinsi hiyo hiyo. 1The.4:16-17 Wenye haki waliokufa watafufuliwa ,ndipo wakiwa pamoja na wenye haki waliohai, watanyakuliwa kumlaki Bwana hewani. Yoh. 5:28-29 kutakuwa na ufufuo wa aina mbili, yaani, ufufuo wa uzima na ufufuo wa hukumu. 2Th.1:8 Waovu wataangamizwa Yesu atakaporudi. Uf. 19:11-21 Kama Mfalme aliyeshinda, akiyaongoza majeshi ya mbinguni, Yesu atawakomboa watu wake. Waovu au wasio haki wataangamizwa kwa mng'ao wa utukufu wake. Ufu. 20:1-2 Shetani atafungwa miaka 1000. 2Pet. Minyororo hiyo ni ya giza. Shetani atafungwa katika dunia iliyoharibiwa na kuwa ukiwa, ikiwa haina mtu wa kudanganya Uf. 20:1 Neno la Kiyunani linalotafsiliwa kuzimu lina maana ya "ukiwa, utupu, bila umbile "(Soma pia Mwa.1:2). Yer. 4:23-27 Nchi hii itabaki ukiwa (yaani, bila umbile na tupu ), ikiwa haina mtu ndani yake. Yer. 25:33 Waliouawa na Bwana hawatazikwa. Ufu. 20:4 Wenye haki watakaa pamoja na Mungu kule mbinguni kwa miaka 1000. Wakiketi katika viti vya enzi, watashiriki katika hukumu. 1Kor.6:2 Watakatifu watauhukumu ulimwengu. Ufu. 20:5(Sehemu ya kwanza ) ufufuo wa waovu kupokea thawabu ya mwisho utatokana baada ya hiyo miaka 1000. Ufu. 20:7 Shetani atafunguliwa atoke katika kifungo chake ili awaongoze waovu waliofufuliwa katika shambulio lake la mwisho zidi ya Mungu. Ufu. 20:9 Hatimaye shetani na majeshi yake ya waovu wanaangamizwa kabisa. Ufu. 21:1-3 Mungu atauumba nchi nzuri. 

HUDUMA ZA MAZISHI

Huduma ya Mazishi  (Mchungaji, mzee wa kanisa, au shemasi anaweza kufanya huduma hii). Ushauri umetolewa kwamba, kadiri inavyowezekana, maz...