Awe
mjuzi wa maadiko yaani msomaji hodari wa Biblia . ndio maana wengine wanasema
kiongozi wa shule ya sabato ni mzee wa kanisa kubwa ndani ya kanisa dogo; yaani
kanisa hili lenye idadi kujumisha idadi kubwa ya waumini ndani ya kanisa husika
lenye idadi ndogo ya washiriki kitabuniwashiriki wake ni kila aiingiaye ndani
ya kanisa ni mshiriki wake. Kwanini? Kiongozi wa shule ya sabato ni mtu
anayeongoza waumini na wasio waumini – wenye ushirika na wasio na ushirika; na
darasa la ubatizo na wale watoto wote ana mamlka nao. Wakati mzee wa
kanisa ni mzee anayewaongoza wale tu
waliobatizwa ndio alio na mamlaka nao. Hivyo shule ya sabat ni kitengo nyeti
maana ndio uhai wa kanisa. Kumbuka ni kuwa bado mzee wa kanisa ni mkuu wa idara zote ndani ya kanisa. Hivyo
kufanya kazi bega kwa bega kati ya
kiongozi wa shule ya sabato ni mzee wa kanisa kunaleta ufanisi wa kazi ya Mungu.
Kiongozi wa shule ya sabato
anapaswa kufanya yafuatayo:-
· Awe
ni mbunifu na mtu mwenye njozi ili aweze kuleta mvuto wa shule sabato.
· Aongoze
timu ya wasaidizi wake kuelewa majukumu yao. Itamuwia rahisi kuongoza kwa
ufanisi na mafanikio.
· Ahakikishe
kanisa limegawanywa katika madarasa ya watu 6-8. Mpango huu utasaidia
yafuatayo:- washiriki wawe watendaji sio watazamaji; wawe washuhudiaji;
wasaidiane katika shida mbalimbali; wapendane na kufahamiana zaidi; na
kupunguza uasi kwa wanaorudi nyuma kufahmika kwa haraka na utembeleaji wa
waumini wapya mara kwa mara. Na kuhakikisha kila mshriki ana lesoni yaani
kuhamasisha utoaji wa fedha ya lesson kila robo.
· Kuhamasisha sadaka za kanisa kila sabato;
sabato ya kwanza mni uinjilisti; ya pili ni sadaka ya kupata faida; ya tatu ni
washiriki; nay a nne ni shukrani ya kuzaliwa .
· Kusimamia
darasa la walimu au kupanga mtu wa
kusimamia na kupanga walimu kwa kushirikiana na baraza la shule ya sabato.
· Kuwa
mwenyekiti wa baraza la shule yaaaa sabato linalolatibu mipango yote ya SS.
· Atastawisha
na kuboresha mambo yote ya SS pamoja na sadaka zote za shule ya sabato. Siku
yake ya kusimamia shule ya sabato; ni
sabato ya nne kila mwezi.
Viongozi wa wasaidizi wa shule ya sabato na kazi zao:-
Ø Mkurugenzi wa SS- washiriki (watu
wazima)
o
Huyu anashughulika katika kumsaidia
mkurugenzi wa SS katika kuendesha program zote za SSS watu wazima. Hawa ni
miaka 19+++
o
Kupanga wa hudumu na kuona program
zilivyoendeshwa kwa utaratibu. Pia kumsaidia mkurugenzi kuhamasisha ununuzi wa
lesson za watu wazima.
o
Kuona watu wameketi katika madarasa ya
watu 6-8 na utaratibu wake wa muda umefuatwa.
o
Kubuni namna ya kuendesha shule ya
sabato yenye kuvutia. Hii itawezekana kwa kusimamia waendeshaji wa prodram
kanisani wanapata mbinu mbalimbali kwa kujifunza kwa maknisasa mengine.
o
Kuona kuwa kila msiriki, ameandikwa
kwenye makadi ya shule ya sabato. Kuhakikisha wote wanahudhuria katikaa shule
ya sabato.
o
Kuhakikisha kuwa wagojwa wasiojiweza-
wadhaifu wanaoorodheshwa majina yao. Kumpata mkuu wa SS utaandaji majina ya
wagonjwa na wadhaifu.
o
Kuhakikisha kwamba kila mshiriki anayo
lesson yake na kwamba anaisoma kila.
Kuorodhesha
majina katika makundi matatu:-
· Ashirki
wa ss ambao ni pia ni washiriki wa kanisa.
· Washiriki
wa ss ambao hawajabatizwa.
· Majina
ya washiriki waliorudi nyuma, na majina ya wale wanotazamiwa kubatizwa.
Ø Mkurugenzi wa shule ya sabato
–uinjilisiti
· Anamsaidia
mkurugenzi kuhamasisha swala la uinjilisti wa vikosi ndani ya madarasa ya SS.
Hii ni pamoja kugawa vijuzuu na masomo ya uguduzi/VOP/Biblia yasema.
· Kupanga
sabato za wangeni kupitia baraza la shule ya sabato. Kusimamia mipango yote ya
maadalizi ya sabato ya wageni na michango ya ufanikishaji.
· Kuhakikisha
kila sabot taarifa ya ushuhudiaji
imetolewa kwa kila darasa kwa kutembelea madarasa hayo na kutumia wahamasishaji
wa kila darasa kuhamasisha uinjilisti wa nyumba kwa nyumba.
· Kubuni
mikakati ya ufunguaji wa matawi ya shule
ya sabato mapya.
Mkurugenzi wa shule sabato –
utendaji
ü Kumsaidia
mkurugenzi kuwatia moyo wale ambao hawahudhurii shule sabato.
ü Pia
wale ambao wanafika wakiwa wamechelewakuwatia nguvu kuwahi.
ü Kuwasaidia
wale ambao hawanunui lesson waweze kununua.
ü Akisaidiana
na wanadarasa wakongwe, wagonjwa, na wenye shida ambao hawahudhuria SS.
Atawapelekea lesson zao, ikiwa walikwisha toa fedha, na kuchukua sadaka ya SS.
ü Wale
wasiofika kwa ajili shida mbalimbali anaweza pia kuwasiliana nao kwa njia ya
simu, kadi maalum(get wellsoon n.k);wale ambao hawa kufika kanisani siku hiyo.
Mkurugenzi wa shule ya sabato-
watoto (divisheni)
ü Anamsaidia
mkurugenzi katika usimamizi wa kugawanya kanisa katika divisheni ndogondogo
kutokana na umri wao.
ü Yeye
anasimamia watoto katika shule ya sabatowa umri kuanzai: 0-3 (crale); 4-6
(kindergarten); 7-9 (primary); 10-12 (teenage); 13-15 (Adolescent of eary
teen); 16 -18 (late teen or youth).
ü Achukue
idadi ya watoto walioko kanisani.
ü Atakuwa
msimamizi wa shule sabato ya watoto
ü Pia
atahamasisha wazazi kununua lesson za watoto.
ü Kutafuta
walimu watakaoweza kufundisha watoto katika mgawayo huo. Pia kutafuta masomo ya
hizo divisheni.
Mwimbishaji wa nyimbo za vitambuni
wa shule ya sabato:-
ü Ni
mtu muhimu katika shule ya sabato. Kipindi chake huanza saa 3:00 kila siku ya
sabato asubuhi.
ü Aachanguliwe
mtu wenye uwezo wa kujua nyimbo za vitambuni angalau robo tatu awe anazifahamu
ikiwezekana na noteni afahamu.
ü Nyimbo
zile zisizofahamika ndizo hutiliwa maanani kufundishwa.
ü Ataongoza
pia nyimbo zote wakati wa vipindi vya SS.
ü Daima
aonekane katika mavazi mazuri/ nadhifu na safi.
ü Atahimiza
watu waimbao kwa furaha na akili wakimsifu Mungu.
Karani wa shule sabato
ü Karani
wa SS ni katibu wa baraza la shule ya sabato.
ü Ndiye
mkusanyaji taarifa ya utendaji mzima ya mambo ya SS kanisani.
ü Anapaswa
kuwahi mapema zaidi pamoja na darasa la walimu kuchukua taarifa ya darasa hilo
na mahudhurio ya walimu.
ü Anapaswa
kuanda taarifa ya kusomwa kila sabato kwenye shule ya sabato.
ü Anapaswa
kusirikiana na karani wa huduma kupata taarifa ya huduma yangu kwa yesu.
ü Atatunza
makadi na kuwapa walimu kila juma.
ü Ataandika
kumbukumbu mbalimbali katika vikao vya baraza la SS.
ü Atatuma
taarifa ya kila robo kwa mchungaji wa mtaa.
ü Ataandika
majina ya madarasa yaliyopangwa 6-8, i- mtaa.
ü Atatunza
kumbukumbu muhimu za kila darasa.
ü Hesabu
ya waliotembelewa, hudumiwa n.k.
ü Mahudhurio
ya wanadarasa kila mwezi.
ü Idadi
ya misaa iliyotolewa na wana darasa.
Karani wa sadaka ya kupata faida
ü Atafundisha
watu namna ya kupata/ kutoa sadaka hiyo k.m kwa njia ya kuuza magazeti,
matunda, karanga, kuku,au kutenga mshahara wa siku moja.
Kiongozi wa upokeaji – Bawabu.
ü Wawe
wachangamfu wajue lugha vizuri. Awe na uso wa machungwa sio malimao. Wageni
wakaribishwe vizuri.
ü Bawabu
asichanguliwe aliye na kasoro ya viungo, kiziwi, killema au bubu.
ü Wahamasishe
washiriki kuwakaribisha wageni nyumbani, tufahamiane zaidi nao na kula nao.
ü Karibisha
watu wote kwa furaha wenyeji na wangeni bila kuwabangua kuwa huyu ni mgeni wa
kumkaribisha mwenyeji hapana.
Kiongozi
wa vbs – (vocational bible school)
Ni
kitengo ndani ya idara ya shule sabato. Ni shule ya Biblia wakati wa likizo.
Shule hii imekusudiwa kuwasaidia wanafunzi wakati wakiwa wapo likizo ili kuweza
kujishughulisha na mambo ya kiroho ili kuepuka mambo maovu na anasa.
Kitengo
hiki ni sehemu ya uinjilisti kanisani kwa kuwa watoto hao wanaalika watoto ambao
sio wa imani yetu ili kujifunza mambo mazuri.
Mambo
ambayo yanapaswa kutendwa wakati huo wa likizo na watoto chini ya usimamizi wa
kiongozi wa VBS na walimu wao ni kama ifuatavyo:=
· Utaratibu
wa program unaanza kwa kupandisha bebdera ya Taifa kisha wimbo wa Taifa
unaimbwa
· Nyimbo
na mafungu ya biblia
· Watoto
wanajifunza yafuatayo:-
i) Mashujaa
wa Biblia
ii) Kisa
au hadithi.
· Walimu
kuita ya wanafunzi na kurundisha bahasha kwa wanafunzi.
· Kucheza
michezo mbalimbali kati ya walimu pamoja na watoto.
· Kujinfuza
juu ya maisha :- a. wanyama – nature b.
afya ya mwili.
· Kupaka
rangi picha zilizochorwa tayari.
· Kurudisha
vifaa- bahasha ya rangi.
· Kuimba
na kuomba kisha kutawanyika – kwaheri.
Waalimu wa shule ya sabato
Ø Wameitwa
kwa ajili ya kazi kubwa ya kulea kiroho washiriki wa SS
Ø Daima
wanatakiwa kuwa mfano mzuri katika hali ya kiroho kwa wale wanao waongoza.
Ø Waweze
wao wenyewe kuwa wanafunzi wazuri wa Biblia.
Ø Wawe
wasomaji wa lesson zao kila siku; na kuadaa hadidu za kurejea fupi/ ktk mada ya
kufundishwa juma husika.
Ø Waweze
kufahamu wanafunzi wao; kitabia/ mwenendo, uwezo wa uelewa, wanakoishi
(mtaani).
Ø Waendeshe
darasa la lesson kama wahubiri.
Ø Wajue
kuhusianisha somo la juma hudika na maisha ya wakati wanaoishi washiriki.
Ø Waweze
kuonyesha namna ya ibada ya majadiliano yenye kicho, katika darasa.
Kazi
za walimu wa shule ya sabato
Ø Kazi
yao ni kuleta ushirikiano kiroho
Ø Kuhimiza
washiriki kutoka katika ulegevu/uvivu wa mambo ya kiroho.
Ø Mwalimu
asiwe mwimbaji bali mwibishaji yaani awe mwenyekiti wa mjadala sio mhubiri.
Ø Kuhakikisha
kwamba kila mwanadarasa anacho kitabu cha masomo ya kasha la asubuhi, na kwamba
anakisoma.
Ø Kuona
kwamba wanadarasa wanatembeleana angalau
mara moja kwa juma; ili kupanga mipango ya kushuhudia majirani zao.
Ø Kuhakikisha
kuwa kila mwana darasa anaelewa wajibu wake wa kuleta uhai wa darasa.
Ø Mwalimu
n mwenyekiti wa darasa hivyo awe na katibu watakaye saidiana kuratibu
uboreshaji wa mipango. Kutembleana wana darasa.
Darasa la walimu
Ø Darasa
la walimu huanza saa 2:00 asubuhi. Kama ilivyodesturi ya nchi yetu ya Tanzania.
Linashuriliwa kuwa lifanyike kabla ya sabato ili kwamba lisihalakishwe siku ya
sabato asubuhi wanapokutana walimu kukamilisha mambo machache.
Ø Kadhalika
kuligana na kanuni ya kanisa, sura ya 9, uk 14 toleo la 17 mwaka 2005;
inashauriliwa kukutana katikati ya juma ili kujifunza/kujadili lesson na kuweka
hadidu za rejea za somo la juma hilo.
Ø Darasa
la walimu linapangwa ili kuhudumia vizuri, matakwa ya kiini cha somo la juma
husika.
Ø Waalimu
wana takiwa kujifunza lesson kwa jinsi ya kufaidika na muktadha somo.
Ø Wanatakiwa wachangue maswali angalau matatu au manne,
yaliyo kiini cha lesson amabyo yatapelekwa kwenye mjadala wa madarasani.
Ø Kiongozi
wa SS anasimamia mjadala au kupanga mtu mwingine aendeshe darasa.
Ø Mzee
wa kanisa anapaswa kuhudhuria ili kusaidia mahali penye utata juu ya mafundisho
yetu makuu.
Vipengele 7 vya funguo za mafanikio
ya vikosi vya shule ya sabato.
i) Namna
ya uendeshaji wa darasa.
ii) Kujali
washiriki wa darasa wanaokosekana
iii) Mratibu
wa kutunza muda.
· Kupeana
uzoefu wa kufundishana
· Kuomba,
kuhamasisha, na kutembeleana.
iv) Matumizi
ya lesson maishani
v) Tathimini/
mashuri ya kiongozi
vi) Ushirikiano
wa karibu (corporate sharing)
vii)
Mahusiano ya nyumbani/ tathmini.
Uendeshaji
wa darasa.
i) Kiongozi
wa mjalada. (anatumia dk 5)
· Kuangalia
wale ambao wanakikosi ambao wamekosekana.
ii) Mratibu
wa uinjilisti (Dk. Care coordinator)
· Kutoa
uzoefu unaohusiana na mpango wa darasa.
· Kutoa
mafunzo kulingana na uzoefu uliotolewa.
· Kupanga
mipango ya utembeleaji
· Kuhamasisha
mipngo ya darasa
· Kuendesha
huduma ya maombi kwa kikosi.
iii) Msimamizi
wa mjadala – kiongozi wa kwaya na sio solo(Dk. 35)
· Kupitia
mada za muhimu sana ndani ya lesson
· Uliza
maswali 3 au 4.
· Hakikisha
kila mtu anashiriki kutoa mchango.
· Litumie
somo katika maisha ya juma hili.
Mahitaji ya darasa
i) Ukubwa
wa darasa la watu 6-8
ii) Kiongozi
wa ushuhudiaji.
iii) Mipango
ya ushuhudiaji
iv) Muda
(dakika 25)
Makusudi
ya shule ya sabato yazingatiwe:
i) Malezi
ya kiroho.
ii) Usirikiano
(mahusiano)
iii) Ushuhudiaji
kwa jamii
iv) Utume
ulimwenguni.
A.
IDARA
YA VIJANA (ADVENTIST YOUTH – AY)
Idara hii ilianzishwa mahsusi kwa ajili
ya kutumia nguvu ya vijana iliyopo kanisani,
kwa ajili ya wokovu wa wengine. Inaunganishwa vijana wote wenye umri wa miaka 6
mpaka 35 ndani ya kanisa. Nabii wa Mungu alionyesha kuwa kazi ya injili
itafungwa kwa nguvu ya vijana watakapoungana na wazee katika kutekeleza utume wa kanisa. Biblia inaeleza
katika YOELI 2:28- 32. “Hata itakuwa, baada ya hayo, ya kwamba
alitaminiwa robo yangu juu ya wote wenye mwili; na wana wenu wataona maono;
tena juu ya watumishi wenu wanaume kwa wanawake, katika siku zile, nitaminiwa
roho yangu…….”
Vijana wanapaswa kujitambua kuwa wao wapo
kanisani kwa ajili ya kutumika na kuokoa. Hili litawasaidia kujua baada ya wao
kuokolewa basi wanajkukumu la kuongoa vijana wezao walio ndani ya kanisa na walio nje ya kanisa.
Chimbuko la idara ya vijana
Mapema katika historia ya waadvetista wasabto
idra ya shuleeeee ya sabato ndiyo iliyoanza mapema mwaka 1852. Makusudi yake
yalikuwa kutunza maisha ya kiroho ya watoto na vijana. Somo kuhusu vijana
liliandaliwa na ndugu james white na kuchapwa mwaka huo 1852.
Wito
ulikuwa mara kwa mara ka nia ya maadishi ya Ellen G. white ya kutaka
kuwaunganisha vijana wote katika jeshi kusaidia kumaliza kazi kubwa ya kuchukua
ujumbe wa marejeo ulimwenguni. “Nabii alitangaza kwamba kila kijana kila mtoto,
ana kazi ya kufanya kwa ajili ya utukufu wa mungu.” (Ed. Uk. 58)
Mwaka
1879 Harry Ferner (miaka 16) na Luther warren (miaka 14) walipata wazo la kuona
kuwa vijana angekuwa na umoja Fulani ambao ugewaunganisha vijana na kuleta
ufanisi wa kazi ya mungu katika kanisa. Vijana hawa waliishi USA,
michigani kitongoji cha Hazzeeton. Siku
moja waliandaa mkutano kwa ajili ya
wavulana tu katika chumba kidogo cha luther katika nyumba ya wazazi wake. Lengo
lake ilikuwa kuhamasisha kazi ya umishenari na vitabu na baadae mambo ya afya
ya wazi.baadae wasichana walikaribishwa kujiunga. Baadae mkutano uliendelea
kupanuka ukawa mkubwa sana hata wazima katika familia ile wakahudhuria.
Agenda
ya namna ya kuwasaidia vijana ililetwa kanisani kupitia wazazi wa wale vijana.
Ferner na wenzake waliombwa kuendele kuwatia moyo vijana wenzao wavulana
na wasichana. Kadri mpango huu ulivyoendelea kuimarika hatimaye
ulikubarika na general conference. 1889
G.C ikaita umoja huu kwa jina la “Christan Volunteers.”
Mwaka
1901 idara ya shule ya sabato iliunganishwa na idara ya vijana ili kuendesha
shughuli zao vizuri. Mwaka 1907 idara hizi mbili zikatenganishwa mwaka 1907
idara ya vijana ilipewa jina lililokubarika katika general conference nalo ni
missionary volunteers (M.V) yaani wafanya kazi ya umisheonari kwa kujitolea.
Mkurugenzi alikuwa mchungaji M.E Kern. Vita ya kwanza ya dunia iliathiri sana
shughuli za idara hii ya vijana. Lakini mambo kama hiking, michezo, kusimulia
hadith, sanaa, ufundi, na kambi za moto ili kukithi mahitaji ya vijana
yaliendelea kufanyika. Baadaye chama kiliendelea kuimarika. Mwaka 1926 kambi la
kwanza la vijana lilifanyika huko Michigan, USA, ilikuwa lenye mvuto mkubwa
sana kwa vijana.
Historia ya AJY (Advenist junior
youth) vijana wadogo.
Mwaka
1919 ndugu A. W spalding alianzisha chama cha skauti cha kimishenari cha vijana
wadogo huko madson, Tannessee, chama hiki kilikuwa cha vijana wadogo wa kime na
vijana wa rafiki za vijana hao. Mambo yaliyosisitizwa yalikuwa ufundi wa kazi
ya uselemala na ukabikaji. Walijiwekea sheria, ahadi na kusudi ambayo baadaye
wana M.V walifuatisha.
Mwaka 1920 baraza la general
conference lilikutana na kupitisha ndugu hot kuwa katika idara ya vijana kama
msaidizi wa katibu wa M. V ili yeye ahamishe watoto ambao walijulikana katika
mwaka huo kuwa J.M.V (junior missionary volunteer) vijana wadogo wa kimishenari
wa kujitolea.
Mwaka huo huo 1920 madarasa ya vijana
wadogo yalianzishwa. Mwaka 1928 mafunzo
ya uongozi yalianzishwa kufundisha viongozi waliojulikana kama master
comrades (baadaye waliitwa master Guides).
Mwaka
1946 chama cha watafuta njia kiliazishw ahuko California ya kusini na ndugu
juhn Hancock. Tangu mwaka 1947 – 1940 program za watafuta nija ziliendelea
kukua. Ilipofika mwaka 1950 baraza la general conference lilianzisha chama cha
watafuta njia.
Mwaka 1978 jina lilibadisha kutoka M.V
(missionary volunteer) na kuwa A.Y( Adventist youth) yaani kijana wa
kiadvetista.
Kwa kuzingatia vipawa mbalimbali
walivyonavyo vijana, viongozi waliazisha
shughuli za madarasa mbalimbali yakiwepo yale ya kujifunza Biblia, viumbe
vya asili, ujuzi wa nyumbani, shughuli za kambi, huduma ya kwanza, afya ya
nyumbani, mazoezi ya viungo, huduma za jamii na shughuli nyingine za kushuhudia.
Mwaka 1927 Baraza la General
conference liliazisha madarasa mabalimbali ya mafunzo yaliyoitwa rafiki, mwenzi, na comrade kwa ajili ya vijana
wadogo na daras moja la watu wazima.
Mwaka 1928 nishani mbalimbali
ziliznazishwa na darasa la master comrade liliendelea kuimarishwa, ambalo
baadae liliitwa master Guide. Wahitimu wa kwanza wa master guide walivikwa pini
za o mwaka 1931.
Madarasa ya MV na JMV ambayo baadaye
yameitwa AY yamebuniwa ili kuwasaidia vijana kukua kimwili, kiakili, kiroho na
kijamii.yamethibitishwa kuwa yanafaa kujenga tabia, na yamekuwa mbaraka kwa
maisha ya maelfu ya vijana.
Chama cha wafumbuzi (Advenist
Adventurer club) kiliazishwa na general conference maka 1979.
A. Ufafanuzi
wa vyama vya idara ya vijana.
I.
A. Y Advetista Youth ( vijana wa
kiadventista) miaka 6-35. Hii ni idara inayounganisha vijana wote wa vyama vitatu vinavyounda idara ya
vijana navyo ni:-
1.
Adventist Adventurer club (chama cha wafumbuzi) kinchochukua watoto wote wa
miaka 6- 9 (A.C)
2.
Advetist pathfinder club ( chama cha watafuta njia ) kinachukua watoto wote wa miaka
6-9 ( A.C)
3.
Advestist senior Youth ( chama cha watafuta njia ). Kinachukua watoto wote wa
miaka 16-35 (A.Y )kiufupi chake
kinafanana na kile cha Advest youth ( jina la idara).
II.
A.J.Y – Adventist junior youth (vijana
wadogo wa kiadvetista.)
(miaka
6-15). AJY ina unganisha vyama viwili A.C na P.F.C .
i) A.C
– chama hiki kina madarasa manne kuligana na umri wao.
Miaka
6 darasa la nyuki wa shughuli {busy bee)
Miaka
7 darasa la mwali wa jua (sun beam)
Miaka
8 darasa la mjenzi (Builder )
Miaka
9 darasa la mkono wa msaada (helping hand)
ii) PFC
Chama hiki kina madarasa sita kuligana
na umri wao
Miaka
kumi darasa la rafiki (friend)
Miaka
11 darasa la mwezi (companion)
Miaka
12 darasa la mgunduzi (Explorer)
Miaka
13 darasa la msimamizi (ranger)
Miaka
14 darasa la msafiri (voyager)
Miaka
15 darasa la kiongozi (guide)
III.
A.Y.S (Advetist youth services) hawa ni
vijana ambao wameamua kufanya huduma mbalimbali za kanisa kwa njia ya kujitolea
na kwa gharama zao. Mpaka sasa kuna wanachama
4,000 tu duniani. Tanzania hatujapata ata mmoja .
B. Adventist
senior Youth (A. Y) Chama cha vijana wakubwa.
Madhumuni:-
Katika
roho ya unabii kumeelezwa madhumuni ya chama cha vijana wakubwa kama
ifuatavyo:-
i) Kuwaelimisha
vijana kufanya kazi kwa ajili ya vijana wenzao.
ii) Kuwaandaa
vijana kusaidia kanisa lao na wale watunzao sabato.
iii) Kufanya
kazi kwa ajili ya wale wasio na imani yetu (sign of the times, may 29, 1893).
Katika kutimiza madhumuni haya
vijana
· Wataomba
pamoja
· Watajifunza
neno la mungu pamoja
· Watashirikiana
pamoja katika maburudid\sho ya kikrsto.
· Kushuhudia
pamoja katika vikundi vidogo vidogo.
· Kukuza
mbinu, ujuzi na talanta katika huduma ya bwana wetu.
· Kutia
ndugu kila mmoja kila mmoja wetu katika kukua
kiroho.
Kanisa
linfanya kazi zake mbalimbali kupitia chama hiki cha vijana wakubwa wa
kiadvetista. Katika mipango yote ya kanisa program za Vijana zisitengwe na shughuli nyingi za kanisa
vijana wahusishwe katika majukumu ya
kanisa ya uongozi na program zote za
kanisa zima.kunapaswa kuwe na wazee wa kanisa vijana, mashemasi vijana wa kike
na wa kiume, n.k huku wakifanya kazi na
maofisa wenye uzoefu katika kona zote za
kanisani. Vijana wanapaswa kuwa moto.
Madondoo ya Roho ya unabii:
Chama
cha vijana ndicho pekee kinachoweza kuwafanya vijana wajisikie kuwa na furaha
wanaposhiriki shughuli za kanisa kwa pamoja. Umuhimu wake umeridhika baada ya
kuchunguza madhumuni yake ambayo ni:-
· Kutunza
changamoto ya kusundi, moto na ahadi mbele ya chama,
· Kumfanya
kila mmoja awe na moyo wake ujitoao ndani ya chama.
· Kuhamasisha
sura ya chama cha AY na shughuli za kivikosi katika kufikiri na maisha ya
chama.
· Kuwaunganisha
vijana na kanisa na wana AY wote ulimwenguni
· Kumpa
kila mwanachama uzoefu wa kuzungumza
mbele ya watu,kufanya kazi pamoja, kuomba pamoja, kujifunza pamoja na kupanga
pamoja.
· Kuwafundisha
vijana kanuni ya maisha ya kikristo na kuwasaidia vijana kupata suluhisho la
matatizo yao.
· Kujifunza
mbinu mbalimbali zilizo bora za huduma za kikristo na vijana kuwa na vikosi vya
kushuhudia.
· Kutoa
mvuto bora wa kushiriki wa kikiristo kwa vijana wa kanisa .
C.
Kijana
mwadvetista afanye vipi.
Mawazo ya kijana mwadvetista yameelezwa
katika KUSUDI, MOTTO, AHADI na SHERIA.
i) Mdhumuni
ya mwana A.Y
“Kutoka
dhabini na kuwaogoza katika utumishi.” Kupata wokovu katika maisha ya vijana ni
muhimu sana. Wafundishwe mamfundisho ya imani yetu na waweza kujitoa kwa kristo. Kisha washirikishwe
katika shughuli za kanisa. Kwa kuwa shughulika tunawaandaa kuwa watumishi bora
na kwa njia hiyo wanalindwa na uovu.
· Vijana
wenzao (MYP. UK 208,204,207)
· Kanisa
lao (Ed. Uk 269, MYP uk. 220, FCE. Uk. 488)
Madhumuni
hayo matatu ndiyo ambayo Mungu ametupa katika kuifanya kazi yake.
ii) Kusudi
la mwana A.Y
“Ujumbe
wa mrejesho katika ulimwengu wote wa kikazi hiki.” Ujumbe injili ambayo vijana
wataibeba ulimwenguni mwote – maneno mbalimbali ambayo vijana watapeleka ujumbe
huu katika kizazi hiki. Vijana hapaswi kujua ujumbe tu wa kiadvetista, bali
kwamba yesu atarudi upesi na maisha yao yaonyeshe kwamba kwa katika wanaamini
hivyo.
iii) Moto wa chama cha AY
“upendo
wa kikristo watubidisha” 11 kor. 5:14 bila upendo wa kikristo kutakuwa na kushindwa
njiani, kwa upendo wa yesu mafanikio ni ya hakika.
iv) Ahadi
ya chama cha AY
“nikimpenda
bwana Yesu, naahidi kuchukua sehemu ya juhudi yangu katika kazi za chama cha
vijana waliojitolea kumtumikia kristo, kufanya yote niwezayo kuwasaidia wengine
na kuimaliza kazi ya injili kwa ulimwengu wote.”
Vijana
wa kiadvetista wanaweza kufanya mambo manne ili kumaliza kazi:-
· Kuishi
maisha ya kujitolea.
· Kuwafanya
wapatikane katika kila nafasi ya kuokoa.
· Kuombea
kazi ya Mungu kanisani na ulimwenguni.
· Kujitolea
kwa hali na mali katika kuendekeza na kumaliza kazi ya injili. Kwa kufanya
hivyo watakuwa wameingia katika uwakili wakatoa muda wao, vipawa vyao, fedha
zao, na wao wenyewe.
D.
Maofisa
wa chama cha AY
i) Maofisa
wanaochanguliwa na kibaraza cha uchanguzi wa kanisa
o
Kongozi
o
Kiongozi msaidizi
o
Katibu/mhazini
o
Katibu /mhazini msaidizi
o
Mshauri
ii) Wengine
wanachanguliwa na wanachama wenyewe wa A.Y
o
Kiongozi wa nyimbo
o
Kiongozi wa mawasiliano
o
Kiongozi wa nidhamu
o
Kiongozi wa elimu
o
Kiongozi wa mambo ya ushirika
(fellowship)
o
Viongozi wa vikosi;-kikundi cha maombi
na kazi za binafsi
· Kikundi
cha kusaidia cha kikristo (washiriki)
· Kikundi
cha uinjilisti
· Kikundi
cha uimbaji n.k
· Vikundi
hivi vikishaundwa vitadumu kwa miezi
mitatu au miezi sita ili kutoa uzoefu kwa vijana wote kushiriki kwenye vyote
Wanaounda baraza la chama cha A.Y
· Kiongozi -
mwenyekiti
· Kiongozi
msaidizi -mjumbe
· Katibu
mhazini -mwandishi
wa baraza
· Katibu
mhazini
mjumbe
· Mshauri -mjumbe
· Kiongozi
wa mawasiliano mjumbe
· Kiongozi
wa nyimbo -mjumbe
· Mkuu
wa nidhamu -mjumbe
· Kiongozi
wa elimu(mkutubi) -mjumbe
· Kiongozi
wa ushirika -mjumbe
· Viongozi
wa vikosi -wajumbe
· Mkurungezi
wa (PF) -mjumbe,
mwalikwa
· Kurugenzi
wa huduma za kanisa -mjumbe,mwalikwa
· Mzee
wa kanisa au mchungaji aua wote -wajumbe,
mwalikwa.
Maofisa
wote ni wajumbe wa baraza.
Vikao vya mwezi: kutakuwa
na vikao vya kila mwezi (angalau kila mwezi) ili kujifunza na kupanga pamoja.
Vikao vya juma:
kuwe na vikao vya muda mfupi kila jumakwaajili ya kuomba pamoja na kushauriana
kuhusiana na yaliyopo pamoja na kujadili mambo ya dharura yanayojitokeza.
E.
Wajibu
wa wana baraza wa A.Y
1. Wataomba
pamoja kama tmu ya maofisa
· Watachukua
mizigo war oho za vijana wote kanisani.
· Watakuwa
na orodha ya vijana wote (miaka 16-35)
· Wawaone
vijana waliokata tama na wengine wasioogoka.
· Wawatie
moyo kuhudhuria kanisani na kufanya shughuli za kanisa.
2. Wawe
wajuzi wa mafundisho yote ya AY
· Wajifunze
kitabu cha “messages to young people .” Youth Ministry, Training Course na
maarifa mengine ya vijana kwa kadri yanavyowez kupatikana.
3. Kupanga
mikutano ya A.Y “Yule anayeshindwa kuanzaa, anajiandaa kushindwa.
4. Kutathimimi
taarifa za chama
5. Kuchunguza
kumbukumbu za chama kila mwisho wa mwezi na kwamba taarifa zitumwe
field/conference kila roho.
6. Kuchunguza
mahitaji ya pesa na matumizi yake.
7. Kupanga
shughuli 1 za maburudisho yale ya kikristo na shughuli za ushirika.
8. Kupanga
mipango ya juma la maombi la vijana.
9. Kuhamasisha
haja ya elimu ya kikristo.
10.Kudhamini
master Guide club na A.Y club.
11.Kukuza
moyo wa utii kwa vijana utakao waongoza.
12.Kushiriki
huduma za kiroho za kila juma.
13.Kurudisha
kwa uaminifu zaka na sadaka.
14.Kusisitiza
majuma ya maombi na maombi kwa ujumla.
15.Kujaza
nafasi za uongozi pale ambapo pana pengo la viongozi.
16.
Kuendelea kupokea wanachama wapya.
F.
Kazi
za kila ofisi wa AY
I.
Kiongozi
wa AY
· Aelewe
vizuri mipango ya chama
· Awe
karibu na mkurugenzi wa field
· Kupanga
ratiba ya baraza la A.Y
· Atakuwa
karibu na mshauri wa vijana
· Atawapa
madaraka viongozi wengine kwa kadri uwezavyo.
· Mwenyekiti
wa baraza la A.Y
II.
Kiongozi
msaidizi wa A.Y (Kazi zake)
· Atafanya
shughuli za kiongozi wa AY (watasaidiana)
· Atasaidiana
na kiongozi kujulisha baraza la kanisa mahitaji ya vijana kwa ujumla.
III.
Kazi
za mshauri au mdhamini wa vijana
· Mjumbe
wa baraza la chama na baraza la kanisa
· Ayajue
madhumuni ya chama na njia za kuendesha program
· Yeye
ni mshauri na kiongozi wa kiongozi wa chama na maofisa wake
· Ni
mshauri wa matatiz ya vijana binfsi.
· Atasaidiana
na kiongozi kuwasilisha mahitaji ya vijana kwenye baraza la kanisa
IV.
Katibu mtunza hazina (kazi zake)
· Mjumbe
wa baraza la vijana na mwadishi wa miniti na mtunza warekodi za yale
yaliyoamuriwa na baraza.
· Kutunza
majina ya wanachama wote na anuani zao katika kitabu
· Atatoa
taarifa za maendeleo ya chama.
· Atawaelimisha
vijana taarifa za kazi zao kila robo
· Atatunza
majina na anuani za viongozi wa chama
· Atatunza
orodha ya wale wanaochukua kozi ya uongozi wa watafuta njia ( master Guide) na
wale wanaochukua kozi ya kiongozi mwadvestista.
· Atapeleka
taarifa za kuhitimukwao kwa mkurugenzi wa vijana wa fied, pini zitolewazo na
vyeti
· Atapokea
fedha na kuzitunza hazina kwa mtunza hazina wa kanisa akiambatanisha risiti
yake
· Atatoa
taarifa ya fedha kila mwezi kuonyesha mapato na matumizi yake
· Ataangiza
vifaa vya chama kutoka ofisini ya field kwa kadri atakavyo ruhusiwa na baraza
la chama.
V.
Kazi za katibu mhazini msaidizi
· Mjumbe
wa baraza la chama cha AY
· Atafanya
majukumu yote ya katibu mhazini wa chama.
VI.
Kazi za kiongozi wa nyimbo wa wa nyimbo
wa chama
· Mjumbe
wa baraza la chama
· Atawajibika
na shughuli zote za nyimbo za chama
· Atashauriana
na viongozi ili ili nyimbo ziende sambamba na mtoa mada kuhamasisha uimbaji
bora kwa vijana
VII.
Kazi za kiongozi wa mambo ya kiroho
· Mjumbe
wa baraza la AY
· Atashauriana
na wanabaraza kuunda vikosi vya maombi
· Atawashauri
wanachama kujenga moyo wa kujitoa wakfu katika mikutano ya chama na shughuli za
kanisa
· Program
za maombi kwenyekwenye vikosi zifanyike
· Atakuwa
mwanafunzi wa Biblia na kupata orodha ya wale wote wanaosoma Biblia kwa mwaka
na kasha la asubuh
· Atawaelimisha
vijana namna ya kutunza Biblia na kila mmoja kwa nayo ya kwake na kuja nazo
kanisani
· Kutoa
taarifa kwa katibu wa chama juu ya wale walihitimu usomaji wa biblia kwa mpango
na kutumwa kwa mkurugenzi wa field/ conference
· Atasimamia
masomo ya juma la maombi la vijana na kupanga ratiba ya wahudumu.
· Atawatia
moyo vijana kusoma vitabu vya robo ya unabii.
VIII.
Kazi
ya kiongozi wa elimu- mkutubi
· Mjumbe
wa baraza la AY
· Atakuwa
na orodha ya majina ya wanachama
· Atakuwa
na orodha ya wale wanaosoma vitabu vilivyopangwa
· Kila
mwezi atapeleka majina ya wale waliohitimu kusoma vitabu vilivyopangwa kwa
katibu ili majina hayo yatumwe kwa mkuruugenzi wa field/conference
· Atawahamasisha
vijana kuanzisha maktaba zao
· Atawahamasisha
vijana kusoma vitabu mabalmbali
IX.
Kazi
za kiongozi wa mawasiliano
· Mjumbe
wa baraza la chama
· Afahamu
mipango ya chama ili aandae matangazo, mada zitakazofundishwa na matukio
maalumu kwa mujibu wa kalenda ya chama
· Kupeleka
matangazo ya chama kwa uongozi wa kanisa ili yatangazwe
· Anaweza
kuwa na kamera kwa ajili ya kumbukumbu za matukio ya matendo ya vijana na
kuyabandika kwenye ubao wa matangazo
X.
Kazi ya kiongozi wa maburudisho
a. Mjumbe
wa baraza la chama
b. Atahusiana
na wanabaraza juu ya maburudisho yafuatayo kwa mujibu wa roho ya unabii na
Biblia
Ataongoza katika
kupanga shughuli za ushirika
a. Atawakaribisha
wageni wote wanohudhria mikutano ya chama
II.
Kazi za kiongozi wa kikosi
a. Mjumbe
wa baraza la chama
b. Atawajibika
katika shughuli za kushuhudia za kikosi
c. Atakuwa
na karani wa kikosi ambaye atatunza yafuatayo
i. Nini
kifanyike
ii. Wapi
kifanyike
iii. Nani
ameshiriki katika kazi
iv. Atatoa
taarifa ya kikosi
III.
Kazi za mabawabu
a. Watahakikisha
kuwa viti vya mbele vipo sawa
b. Watafunga
madirisha au kuwasha taa na feni
c. Watahakikisha
chumba kimepangwa vizuri kabla ya mkutano kuanza
d. Watachukua
sakaka na kumkabidhi katibu mhazini
IV.
Uanachama
Vijana wa miaka 16 – 35 wanapojiunga na
chama wanapaswa kukubali ahadi hii,
“yesu, naahidi kuchukua sehemu ya juhudi yangu katika kazi za vijana
wajitoleao kumtumikia kristo na kufanya yote niwezayo kuwasaidia wengine, na
kuimaliza kazi y ainjili katika ulimwengu wote.
Kuna
aina tatu za uanachama
1. Wanachama
wa kawaida -(miaka 16-35) ambao ni
waadvetista wasabato wanaopenda kumtumikia bwana wao
2. Wanachama
wachagamana – hawa ni vijana ambao hawajaamua kuwa waadvetista wasabato lakini
wanapenda program zetu.
3. Wanachama
wa heshima- hawa ni watu wazima walio pita umri
wa miaka 35 lakini wao wanapenda kuendelea kushiriki za vijana.
· NB:
kijana anayekubari ahadi, moto na kusudi na kuwa mwanachama pia anakubali
changamoto kuwa na sehemu ya kumaliza kazi ya injili.
V.
SARE
ZA AY
Sare ni sehemu ya utambulisho wetu. Kwa
mjibu wa idara ya vijana kanda ya mashariki mwa Africa ilipitishwa kuwa sare AY
itakuwa kama ifuatavyo:-
· Sketi/suruali -kijivu
· Shati/blouse -light blue au nyeupe
· Tai -damu ya mzee
· Kiatu -nyeusi
· Koti - Nevy blue
Kadri
ambavyo mmeamua kuchangua aina Fulani ya kijivu katika kanisa lenu kila mmoja
ajitahidi ya aina hiyo. Kwani kijivu kimegawanyika katika aina mbalimbali.
Sare ya AY imeandaliwa au kubuniwa
rasmi kwa huduma za ibada na mafundisho mbalimbali ndaniya kanisa.
Sare ivaliwe wakati wa matukio ya
program za wana A.Y.
Ikubukwe kuwa namna ya kuwa mwanachama
wa chama hiki ni kwa hiari ya kila kijana. Na kipimo cha kijana hai AY ni
kujiandikisha kila mwaka na kuwa na pia kutoa michango ya chama au ada, na pia
kushiriki katika shughuli mbalimbali za chama.
Majukumu mengine ya idara ya vijana
wakubwa
Kiongozi
wa AY anapaswa kufanya mambo yafatayo:-
Ø Kiongozi wa AY anapaswa awe ni mtu aliyepitia kozi ya
kiongozi mkuu yaani ‘masterguide’.
Ø Kuongoza
vijana kuunda vikundi vidogo vidogo vya kushuhudia na kujifunza pamoja neno la
mungu.
Ø Vijana
waweza kuomba pamoja na kutembeleana kwa ajili ya kutiana moyo.
Ø Kushirikiana
pamoja katika maburudisho mbalimbali kama vile Bible conference, picknick, na kutazama
viumbe vya asili, n.k
Ø Kupanga
na kuhamasisha vijana kuhudhuria makambi mbalimbali.
Ø Kufundisha
miongozo mbalimbali na mafunzo yahusuyo vijana na pia kutafuta wakufunzi
waliofaulu katika mambo ya vijana.
Ø Kuendeleza
talanta na vipawa walivyonavyo vijana kwa kushirikisha vijana katika program
mbalimbali.
Ø Kuongoza
vijana wajue namna ya kushuhudia kwa ajili ya vijana wasio wa imani yetu na pia
kuamsha vijana ambao wamepoa ndani ya kanisa.
Ø Kuhakikisha
kanisa linatumia vijana ambao wamepoa ndani ya kanisa.uongozi kanisani. Hii ni
katika kuwapangia kazi za kufanya ili wawe sehemu ya kanisa. Kwani kanisa
lolote linajengwa na asilimia 80 litazuia kwa kiasi kikubwa uasi kanisani. Kisa
cha malangali: kanisa lote ni vijana chini ya miaka 35 kasoro watu wawili tu.
Ø Kuandaa
mataala wa kozi ya kiongozi mkuu ili kijana ajifunze kozi hiyo. Hili litawandaa
vijana kuwa viongozi bora kwa kupitia kozi hii.
HUDUMA ZA CHAMA CHA MABALOZI
Nembo
ya kwanza ina jina la Ambassadors. Wengine wanatumia hii isiyo na maandishi.
Hivyo chama hiki kina nembo yake ambayo ni rasmi kwa kanisa la ulimwengu. Hiki
ni chama kipya ndani ya kanisa ambacho kimeanza mwaka 2009. Chama hiki ni cha
vijana wenye umri ambao ni wa miaka 16-21 wanaojulikana kama ‘late
adolesencent’ (rika la vijana wakubwa waliobalehe)
Tangu huduma za idara ya vijana
zilipoanzishwa kanisa la waadvetista
wasabato, idara ya vijana katika divisheni mbalimbali likagudua kwamba
vijana wanaomaliza matakwa wa chama cha watafuta njia wanaachwa bila kuwa na
program zinzokidhi mahitaji yao.
wanatamani kuendelea katika chama cha watafuta njia, na wakati huohuo
wanajikuta kwamba hawako tayari kujiunga na chama cha vijana wakubwa katika
kikao cha mwaka 2001 na uongozi wa vijana ulimwenguni kilichofanyika huko
Brazil, kilichukua azimio muhimu kwa kuita idara ya vitini kwa ajili ya kundi
la vijana wa miaka 16-21, ili kukidhi mahitaji yao ndani ya kanisa la waadvetista wasabato. Mtaala wa
mabalozi ni matokeo ya mazimiano hayo.
Kumbuka kwamba, chama cha mabalozi sio
mbadala wa chama cha vijana wakubwa, baada yake kitawaimarisha vijana hawa
wakubwa wa miaka 16-21 katika kanisa letu. Hatua hii mpya imekusudiwa
kutengeneza muundo na kuandaa njia ambazo vijana hawa wa miaka 16-21 watakuwa
hai katika kulitumikia kanisa, kanisa mahalia na ulimwengu kwa ujumla.
Tamko la utume.
Chama
cha wavumbuzi ni chama katika kanisa la waadvetista wasabato kilichowekwa wakfu
kukidhi mahitaji ya kiroho, kijamii, na mtindo wa maisha kwa vijana wa umri wa
miaka 16-21 kwa kuwaptia changamoto ya uzoefu, na kuwashirikisha wengine juu ya
uhusiano binafsi na yesu kristo, kukuza mtindo wa maisha utakaokidhi mahitaji
ya imani yao, na matamanio yao, na
kuwapatia fursa bora za ukuaji wa ujumla wa urafiki unaodumu.
Kusudi.
Ujumbe wa marejeo katika ulimwengu
wote wa kizazi chnagu. Uhusiano wangu na yesu kikristo wa asili ya moyoni, na
ndio unaonisukuma kumshirikisha yeyote aliyetayari kuupokea, injili- bahari
njema za kuja kwa yesu upesi.
Motto
Upendo
wa kirsto wanibidisha. Nimesongezwa kwake kwa mfano wa maisha yake, kwa tukio la kusulubiwa kwake, ushindi
wake, na kwa ahadi yake ya kuifanya dunia upya katika muktadha wa jinsi
ilivyokuwa wakatia wa uumbaji. Kwa kadri ninavyokuwa karibu naye, ndivyo ninavyojisikia
kuwa karibu na mahitaji ya binadamu wezangu.
Chama cha watafuta njia-(pathfinder
club).
Chama hiki kinawaandaa watoto
kutafuata njia ya kuelekea ukubwani kwa
kuachana na mivuto mibaya ya dunia. EFESO
6:1-4.
wanachama wake ni umri kuanzia miaka
10 had 15. na pia wanachama wake ni watoto wa washiriki, washiriki wenyewe
{waliobatizwa), na wale ambao watoto au wazazi wao sio wa imani yetu.
Kanisa
liandae masomo yao au mitaala yao kwa kumsaidia mwalimu.sehmu kubwa wao wawe ni
wale ambao nia masterguide mafunzoni kama sehemu ya kukamilisha matakwa ya kozi
yao ya masterguide.
Ni
kipindi kibaya cha umri maana wengi wao ni umri wa kubalehe. Hivyo inahitajika
umakini zaidi katika kuwafundisha .
Nembo
ya chama ina pembe tatu.
Kiongozi wa PF anapaswa kufanya
mambo yafuatayo:-
Ø Kiongozi
ahakikishe watoto hawa wafundishwe katika makundi mawili;wale wa umri miaka
10-12 na wale wa miaka 13-15 wasichanganywe mara kwa mara katika mafundisho
yao.
Ø Kiongozi
anapaswa kuandaa camporee yao kila mwaka ambapo watajifunza mambo mbalimbali.
Ø Wafundishwe
namna ya kuwaogoa watoto wenzao kwa uundaji wa vikosi vya kushuhudia na ugawaji
wa vijizuu na mialiko kwa watotowenzao kanisani.
Ø Kuwafundisha
masomo ya ufudi wa kazi ya mikono.
Ø Kujifunza
Biblia hasa mafundisho makuu ya kanisa. Kukariri kusiwe sehemu kubwa tena. Bali
wajue namna ya kufundiasha Biblia.
Ø Kuwe
na matembezi mashambani ili wajifunze viumbe vya asili kwa vitendo na matembezi
ya kuapnda milima.
Ø Wafundishwe
namna ya kutunza uniform zao. Wajue wakati gani wa kuvaa na usio wa kuvaa
uniform.
Ø Wafundishwe
namna ya kutengeneza mahema yao na namna ya kukambika kwa kuweka kambi mbali na
nyumbani.
Ø Kuhamasisha
wazazi kununua uniforma zao. Uniform ni
uinjilisiti tosha kwa chama
Chama
cha wavumbuzi –(Adveturer Club).
Chama ambacho kimeazishwa mahsusi kwa watoto
wadogo. Hasa kwa kusaidia watoto wale ambao wako kanisani lakini hawasomi
katika shule zetu za ki-advetista. Hivyo ikiwa kanisa linaprogram madhubuti
katika chama hiki, basi ni hakika watoto wetu wataokolewa kutoka katika
maagamizi ya mafundisho yaliyopo katika dunia hasa katika mashule yasiyo ya
kanisa.
Watoto wanaitwa
wavumbuzi maana umri wao upo katika shule za msingi hivyo ni wadadisi kwa mambo
mengi. Ni watoto ambao sehemu ya ubogo haijajaa bado inahitaji kunasa mambo
mengi. Ubongo unanasa kila kitu chema au kibaya.
Wanachama wake ni wa
umri kuanzia miaka 6 hadi 9. Chama hiki kinajumuisha wanachama wale ambao ni
watoto wa washiriki na pia ambao wazazi wao washiriki.
Walimu wanapaswa kuwa
wavumilivu maana umri huu ni wasumbufu kwa kuchokozana, kucheza kwingi, kudeka,
na ujeuri.
Kanisa linapaswa kuhakikisha kuwa
chama kinakuwa na miogoni yao ambayo inapatikana kwenye ofisi ya idara ya
vijana field au konferensi.
Kazi ya kiongozi wa chama hiki ni
kufanya haya:
§ Kiongozi
anapaswa kutumia mitaala yetu kwa ajili kuwaandaa watoto hawa kujiunga na
mafunzo mengine baadaye katika chama cha watafuta njia- P.F.
§ Kuwatafuta
walimu wenye wito kwa watoto na wenye kupenda watoto na aliueogoka kwelikweli
kisha wapitishwe kwenye baraza la kanisa.
§ Kufundisha
watoto mafundisho yanayohusiana na kanisa letu kwa kujenga msingi uliobora kwa
ajili ya maisha ya ukubwani.
§ Kuhakikisha
watoto wanapitia madarasa yao kama ifuatavyo:- Rafiki,mwenzi, mvumbuzi, na
msimamizi
§ Kiongozi
awafundishe usanii,ustadi wa magari, namna ya utengenezaji wa mahema, na viumbe
vya asili.
§ Kufundishwe
kukariri mafungu ya Biblia kwa kuanza na mafungu mafupi mafupi ili wazoee
kuhariri na pia wajifunze kwa njia ya picha wataelewa zaidi.
§ Kiongozi
ahakikishe wanachama wawe na uniform. Hata wale wazazi sio waadvetista au ni
maskini basi kanisa liandae urtaratibu wa kuwashonea maana si vyema wengine
wawe nazo na wengine wasiwe nazo. Jambo hili linawaumiza watoto kisaikolojia.
A.
KWAYA YA KANISA NA VIKUNDI VYA
UIMBAJI
Zamani na kwa
miaka mingi ilijulikana kuwa kwaya ni kitengo ndani ya idara ya vijana. Kumbe
sivyo ilivyo. Kwaya ni kitengo ambacho ni mali ya kanisa lote. Ipo chini ya
mchungaji na wazee wa kanisa. Ipo chini ya utawala wa kanisa. Kumbuka idara ya
vijana inaweza kwa na kwaya yake na itaitwa kwaya ya kanisa ya idara ya vijana.
Kwaya ya kanisa ni chombo kinachotumika kutoa muziki wa
kikristo. Kwa sababu muziki unamvuto mkubwa katika mema na mabaya, basi
uchanguzi wa makini utumike katika kupata waimbaji bora. Ijulikane kuwa kwaya
ina kiongozi wa kwaya na sio mwenyekiti wa kwaya. Mwenyekiti wa kwaya ni
mchungaji au mzee wa kanisa.
Ø Kanisa lapaswa kuwa makini kupata
viongozi bora kwaya. Hili litaepusha migogoro inayoletwa na viongozi ambao
wanatumia kikundi cha kwaya kwa manufaa yao kwa kuanzisha malumbano ndani ya kanisa.
Ø Viongozi wa kwaya watende kazi kwa
ushirikiano wa karibu na mchungaji na wazee wa kanisa. Hili litawezesha malezi
ya kiroho kwa waimbaji na wanakwaya kwa ujumla kufanikiwa.
Ø Kanisa lapaswakusajili vkundi vyote
vya uimbaji kwa majina yao na wanachama
wao ili kuthibiti mwenendo na maadili mabaya yasipitie katika vikundi
hivyo vya uimbaji.
Ø Viongozi wa vikundi vya uimbaji
wanapochanguliwa basi wajulikane kwa
kanisa kwa mawasiliano ya karibu na kupata maelekezo mbalimbali au kutumika
ndani ya kanisa.
Sifa za kiongozi wa kwaya na waimbaji
wa kwaya
Ø Kiongozi wa kwaya kuwa mshiriki wa
kanisa mwenye msimamo mzuri.
Ø Kiogozi wa kwaya awe ni mtu aliyeongoka
vyema kani anaweza kuleta uasi kwa sababu ni kikundi chenye mvuto sana ndani ya
kanisa.
Ø Kiongozi wa kwaya anapaswa asimamie na
kuzielewa taratibu na kanuni za kanisa vyema. Hivyo aongoze kwaya chini ya
taratibu hizo.
Ø Waimbaji wa kwaya wawe ni waumini
wenye msimamo mzuri ndani ya kanisa.
Ø Waimbaji wa kwaya wawe ni washiriki
wa kanisa au wa shule ya sabato au wanachama wa idara ya vijana.
Ø Muimbaji au waimbaji wasiwe ni watu
waliochukuliwa hatua za kinidhamu za kanisa kama vile kalipio aua kuondolewa
ushirika.hawaruhusiwe kuimba wanapokuwa katika kipindi hicho cha hatua za
kinidhamu.
Ø Tabia zao ziendane na zipatane na
mwenedo wa mkristo katika mavazi na muonekano wan je na ndani.
Sifa za kwaya za kanisa.
Kwaya ya kanisa ni watu wanaofuatana
utaratibu wa kaisa la waadvetista wasabato. Kanisa linaweza kuwa na kwaya zaidi
ya moja. “Makanisa yanaweza kuwa na kwaya zaidi ya moja. Kwaya ya watoto ni
njia ya malezi ya kiroho, ikiwafungamanisha familia ya kanisa na uinjilisti.”
Kwaya hizi zinweza kutokana na idara
mbalimbali tulizonazo ndani ya kanisa. Kama vile idara ya vijana, chama cha
dorkasi, idara ya wanawake,chama cha watafuta njia, chama cha mambolezi, na
kadhalika. Lakini kwaya zote hizi zinawajibika moja kwa moja kwa kanisa sio
mali ya mtu Fulani au kikundi cha watu Fulani. Maadili yake ni yale yale
yameorodheshwa kwa kanisa lenye kwaya moja au zaidi. Kiongozi wa kwaya husika atafanya
kazi kwa karibu zaidi na mchungaji au mzee wa kanisa husika.
Mjukumu ya kwaya ya kanisa na uongozi
wake
Ø Wana kwaya wanapaswa kuelewa kuwa
mziki ni ibada kamili yaani neno, kusifu na maombi yapo ndani ya uimbaji. Hebu
sauti ziinuliwe vyema katika nyimbo za kusifu na ibada.
Ø Wanakwaya wanapaswa kutoa huduma za
uimbaji katika ibada zote za kanisa- ibada kanisani, mazishi, ndoa, na
kadhalika, mikutano ya kanisa.
Ø Uimbaji sio sifa pekee ya kuwa
mwanakwaya bali sifa nyingine ni tabia ya uimbaji anayefaa na pia kumpitisha
katika kujiunga na kwaya sio kwaya au mzee wa kanisa.
Viongozi wa kwaya na waimbaji
wanapaswa kujua:
Ø Kiongozi wa kwaya ya kanisa sio
kiongozi wa vikundi vyote vya uimbaji au kwaya za makundi za kansia. Yeye ni
kiongozi wa kwaya moja tu ya kanisa.
Ø Hatuna kiongozi wa kwaya zote
isipokuwa mchungaji wa kanisa/ mtaa au wazee wa kanisa kwa kuwa ni wasaidizi wa
wachungaji.
Ø Kiongozi au waimbaji wanapaswa kujua
wao ni kwaya ya kanisa moja na sio makanisa mengi. Hivyo waheshimu taratibu iwe
ni kwa ruhusa kwenda kanisa lingine inyofuata utaratibu wa kanisa kwenda
kuhudumu eneo jingine.
Mambo ambayo kwaya hairushusiwi
kutenda bila idhini;
Ø Kanuni zote zinazohusu masharti ya
kujiunga na kwaya lazima yapitishwe na kanisa. Sio kwaya peke yao tu, bali wao
kama timu wanaweza kuunda katiba yao na kupeleka mapendekezo kwa baraza la
kanisa kisha mashauri ya kanisa.
Ø Wanaweza kukaa kama kikundi na
kupanga muda wao wa mazoezi na taratibu zao kisha kuleta mapendekezo kwa baraza
la kanisa ili yapate kupitishwa kwa kuchunguzwa vyema. (kisa cha kutaka waimbaji
wote wanyoe nywele size moja).
Ø Unoforma zao lazima zipitishwe na
washiriki maana ni mali ya kanisa. Hairuhusiwi waimbaji kushona uniform yeyote
bila makubaliano ya kanisa maana uniform ina mvuto mkubwa kwa wema na uovu kwa
njisi ishonwavyo K.K uk 1995.
Ø Waimbaji hawaruhusiwi kufanya
reconding yeyote kabla ya nyimbo hizo kupitishwa na washiriki wa kanisa kuwa
zinakubaliana na msingi ya mafundisho yetu makuu au la. Ikiwa itangudulika
kukiuka taratibu hizo kanisa litawajibika viongozi na wanakwaya wote kwa ukaidi
na kisha kuharibu hiyo master record.
Ø Kwaya hairuhusiwi kusafiri safari
yeyote bila idhini ya kanisa.
Ø Kwaya hairuhusiwi kufanya changizo
lolote kwa kusudi lolote bila uongozi wa kanisa kuridhia michango hiyo. Iwe ni
ndani ya kwaya au nje ya kwaya. Hili litasaidia usimamizi wa matumizi ya fedha
za kwaya na pia kuepuka ubadhirifu kwa kutumia jina la kwaya la kwaya ya kanisa.
Ø Fedha zote za kwaya
hazifunguliwiakaunti yake bali zitatuzwa na mhazini wakanisa hilo kama fedha za
amana za idara nyingine. Zitakuwa risiti kilakinachoingia kwenye mapato yake.
F. MUZIKI WA KIKRISTO
Leo kanisa limeona umuhimu mkubwa wa
kuwa na mtu ambaye anahusika na usimamizi wa mziki kanisani ili kudumisha usafi
na utaratibu mzuri wa usimamizi wa muziki wa kikristo. Kiongozi wa muziki
kanisani anajulikana kama mratibu wa muziki (music coordinator) . hivyo kazi
yake kuu ni kuratibu muziki wa kikristo kuwa uibwe na kuchanguliwa muziki
unaoendana na maadili ya kanisa na kufuata msimamo wa mafundisho makuu ya
kanisa la waadvetista wasabato.
Sifa na kazi kiongozi au viongozi
(waratibu)wa muziki kanisani.
Kiongozi huyu anapaswa awe ni mtu
anayeuelewa vyema muziki wa kikristo.
1. Mratibu awe ni mtu alijitoa maisha
yake kwa yesu ili kulipatia kanisa muziki ambao unaenda sambasamba na maadili
ya kikristo.
2. Mratibu atafanya kazi kwa karibu na
mchungaji au wazee wa kanisa ili uchanguzi wa muziki uende sambamba na mada na
hubiri.
3. Mratibu atafanya kazi chini ya
uongozi wa mchungaji au wazee wa kanisa na sio kama apendavyo.
4. Kiongozi huyu atashirikiana na
uongozi wa kanisa (mchungaji wa wazee) katika swala la uchanguzi wa waimbaji na
wapiga muziki kanisani.
5. Mratibu wa muziki anapaswa kuwa mtu
makini kutoruhusu muziki wa kidunia au
ule uletao mashaka kwa namna ulivyo kuingizwa katika ibada zetu ndani ya kanisa
au matukio yote mikutano ya kanisa.
6. Mratibu wa muziki anaweza kuwa
mshauri wa mtunzi wa nyimbo na aina ya upigaji
wa muziki kwa waimbaji na kwaya zetu bila kuwaamulia aina gani ya utunzi ama upigaji. Atawaongoza
kujiepusha na upigaji wa kidunia wenye mvuto mbaya.
G. IDARA YA ELIMU:
Kanisa la Waadvetista Wasabto
linawajali binadamu wote katika malezi ya kiroho, kiakili, kimwili na hata
kijamii . hivyo linashirikiana na serikali za dunia katika kuelimisha jamii
kupitia taasis zote yaani shule ya awali mpaka chuo kikuu. Kanisa huendesha
utaratibu wa shule ili kuhakikisha kwamba vijana wake wanapokea elimu yenye
uwiano wa Nyanja nne nilizotaja hapo juu .
Sifa za kiongozi au katibu wa elimu.
1. Kiongozi au katibu wa elimu ni mtu
anayepaswa kuwa na mipango kwa ajili ya kuendekeza elimu ya kikristo.
2. Elimu ya kikristo ni elimu itolewayo
kwa ajili ya kumwinua mwanadamu katika hali yake ya maisha ya kiroho, kiakili,
na kimwili.
3. Awe ni mtu mwenye elimu pana juu ya
maadili ya kanisa na mipango yake katika kumwedeleza binadamu.
4.
Awe ni mtu mwenye mwamko wa elimu binafsi na ambye ataweza kuhamasisha
wazazi kuwa na mwamko wa elimu pia.
Wajibu na mjukumu ya kiongozi wa
elimu.
Ø Kutia mkazo juu ya swala la Elimu ya
kikristo.
Ø Kuhamasisha wazazi kupeleka watot
katika shule zetu za kiadvetista – msingi, sekondari, na vyuo. Pia kuwatia
nguvu wazazi kuelewa namna ya kupata ya fedha za masomo.
Ø Mahali ambapo hatuna shule zetu basi
kiongozi wa elimu ahamasishe kanisa litoe elimu yetu katika eneo hilo.
Mf.Kupitia vipindi vya dini katika shule za binafsi na serikali
Ø Kuhakikisha anakuwa na mawasiliano ya
karibu na wanafunzi /watoto wetu ambao wanasoma katika shule zilizo karibu na
zilizo mbali.
Ø Kuhamasisha wazazi ambao watot wao
bado si wa umri wa kwenda shule waweze kutiwa moyo kusaidia wanafunzi
waadvetista wenye shida za kusindwa kulipa ada.
Ø Kudumisha hesabu sahihi za watoto
wote na vijana walio n aumri wa kwenda
shule.
Ø Kuweka mipango kwa kanisa lake
kuazisha shule za chekechea, msingi na hatimaye sekondari.
H. IDARA YA HUDUMA ZA AFYA.
Idara hii iliazishwa mahususi katika
kutoa ufahamu wa mwanadamu katika kufahamu mwili wake na mazingira
yanayomzukuka kisha ufahamu mpango na makusudi ya mungu kwa ajili ya afya zetu.
Biblia inaeleza makusudi hayo katika e
yohana 1:2 “Mpenzi
naomba ufanikiwe katika mambo yote na kuwa na afya yako, kama vile roho
ifanikiwavyo.”
Hii ni idara nyeti sana maana afya ya
kanisa kimwili, kiakili na kiroho
inategemea sana jinsi kiongozi alivyojitoa wakfu kwa kufanya kazi yake na
majukumu ya idara hii. Washiriki wanapokuwa wangojwa katika nyaja mojawapo ya
afya yaani kimili, kiroho, na kiakili- moja kwa moja ibada za kanisa lazima
zitaadhirika kwa kiwango cha juu sana. Soma
Mithali 14:30.
· KIROHO:
Usomaji hakuna, kazi ya Mungu haifanyiki, uchelewaji wa saa za ibada kwa
kiwango cha juu, kupoa kiroho, n.k
· KIAKILI:-Hakuna
utambuzi wa mambo matakatifu, ugomvi ndani ya kanisa na familia na kaya,
mabaraza ya kanisa kuwa na maamuzi yasiyo ya busara, n.k.
· KIMWILI:-
Kanisa kuwa na wagonjwa wengi, umaskini, uzembe, na afya mabya, n.k
Wajibu na majukumu ya kiongozi wa idara hii.
Ø Ili kutatua matatizo yote haya,
kiongozi wa afya na kiasi anapaswa awe na baraza madhubuti ambalo litawahudumia
washirikikwa kusaidia wale ambao ni wangonjwa kimwili na kiakili, na pia mutoa elimu madhubuti ya maswala ya afya.
Ellen White anasema.. “siku zote aliye mgonjwa kimwili atakuwa atakuwa mgonjwa
kiroho, na aliye mgonjwa kiroho atakuwa mgonjwa kimwili”.
Ø Hivyo kiongozi anapaswa kufanya mambo
yafuatayo kulisaidia kanisa kukua katika afya kisha wawe na kiasi katika mambo
yote ni haya yafuatayo:
1. Kiongozi apange program za mwaka mzima akishauriana na
mchungaji na mzee wa kanisa ambazo zitasisitiza afya na kiasi kwa kanisa na
jamii.
2. Kutoa elimu juu ya vitu vinavyodhuru
mwili na akili na mambo ya kiroho kama tumbaku, pombe chai, kahawa, madawa ya
kulevya,kazi nyingi, kutokupata pumziko, n.k hata kama huna utalaamu huo
haikisha unapatamtu mwenye huruma juu ya mambo hayo kisha apewe nafasi ya
kufundisha kwa idhini ya mchungaji wa kanisa.
3. Kukuza mahusiano ya karibu sana na
mashirika ya afya kisha tuwatumie kwa zile mada ngumu kama vile magonjwa ya
kutisha,vifo visivyo vya lazima, uchafunzi wa mazingira n.k
4. Kiongozi anapaswa awe mwanfunzi
hodari wa Biblia na Roho ya unabii juu ya mafundisho ya afya.
5. Kiongozi lazima apange ratiba ambazo
ainangusa maisha ya jamii kwa ujumla sio kwa mtizamomtu wa kiadvetista. Nina
maana usije ukaacha kufundisha swala la tumbaku au pombe ukidhani kuwa walevi
au wavutaji hawapo ndani ya kanisa. Tambua wapo wanfanya kwa siri au
watakaojaribiwa na dhambai kama hizo.
6. Unapoandaa semina kama hizo, ratiba
yako ijumuishe mambo yafuatayo:-
a) Namna ya kuacha uvutaji wa tumbaku au
pombe –kisha toa matangazo kwa njia ya radio au mabango juu ya mada za uvutaji
wa tumbaku au ulevi-mf semina ya namna kuacha ulevi wa tumbaku; kisha tafuta
wakufunzi ndani ya kanisa au nje ya kanisa . zaidi ya yote tafuta ndani ya
kanisa watu watakaotoa ushuhuda wake njisi alivyoshida mazoezi mabaya.
b) Onyesha juu ya mafunzo ya mapishi-
familia nyingi hawajui namna namna ya upangaji wa ratiba ya chakula mfano
maembe + mchicha= kimoja. Nyama +maharange = protini.
c) Program za kuthibiti misongo ya
mawazo- wapo wanaokuja kanisani lakini ana msongo wa mawazo.
d) Madarasa ya afya – namna ya kuzuia
magonjwa ya luambukiza, usafi wa mazingira, dawa na miti shamba, kutambua
‘first aid’ – huduma ya kwanza.
e) Kuonyesha jinsi mtu anavyoweza kuwa
na kiasi katika upangaji wa kazi na majukumu mengine na muda wa kupumzika.
f) Namna ya kulea watoto wakiwa na afya
bora. Hili litahusu kufundisha uandaaji wa chakula bora cha watoto wadogo.
g) Kufundisha namna ya kuhifadhi chakula
katika mazingira safi na pia swala la ujenzi bora kwa afya bora. Siyo nyumba za
madirisha ya kuziba na nguo, isiyoingiza hewa ya kutosha.
I. IDARA YA HUDUMA ZA FAMILIA
Kanisa
la waadvetista wasabato linajali msingi wa kwanza wa kanisa ni yesu Kirsto. Kwa
kanisa ni mwili wa kirsto. Basi kanisa halizuki angani bila kuwa mawe
yanayoweza kulijenga kanisa.familia
imejulikana kuwa ni jiwe la pembeni katika kujenga jingo imara la kanisa. Kuwa
na familia.idara ya huduma za familia inajumuisha kwa kuanza na mtu mmoja, mume
na mke, mzazi mmoja, wazazi n awatoto. Ndio maana Paulo anasema hivi katika
EFESO 6:1-4 KUWA;
“Enyi
watoto watiini wazazi wenu katika Bwana, maana hii ndiyo haki. Waheshimu baba
yako na mama yako; amri hii ndiyo amri
ya kwanza yenye ahadi, apate heri ukae siku nyingi katika dunia. Nayi akina
Baba, msiwachoke watoto wenu; bali waleeni katika adabu na maonyo ya Bwana.”
Kanuni za
kanisa zinaonyesha wazi kuwa kaya ni jiwe la pembeni la kanisa maana kristo ndiye mwasisi wa
familia zote duniani. Kanisa lililo bora linaazishwa na familia bora. Kanisa
bovu linaazishwa na familia mbovu. Ni muhimu sana kanisa lolote kuimarisha familia
zetu ili tuwe na kanisa imara lenye msingi imara kutoka kwa Yesu Kirsto. Hivyo
ni wajibu wa kiongozi wa idara kukanzia maombia ya familia na ibada ili familia
hizi zifunikwe na mapenzi ya Mungu.” Hebu angalia kanuni za kanisa, sura 13,
uk.4
“kaya
ni jiwe la pembeni la kanisa, na kaya ya
kikristo ni nyumba ya sala.”Baba na mama” inasema Roho ya unabii. “ijapokuwa
shughuli zenu ziwe nyingi kiasi gani, msishindwe kukusanya familia yenu
kuizunguka madhahabu ya Mungi…. Wale wanaoishi maisha ya uvumilivu, upendo na
furaha, hawana budi kuomb.” Ministry of Healing uk. 393.
Utendaji wa idara ya huduma za
familia kanisani mahalia
Ø Idara hii ipo kanisani katika
kufundisha kanisa kuwa linapaswa kuwa na familia ambazo ni mbigu ndogo katika
familia kubwa ya kanisa.
Ø Kanisa kama familia kubwa ulimwenguni
inapaswa kujengwa na familia ambazo zimemtambua Yesu kama kichwa cha familia
kubwa- kanisa na hivyo kumwiga Kirsto.
Ø Idara hii husaidia kanisa kuelewa
unyonge unaopitiwa na watu binfsi na familia katika ulimwengu ulioanguka na
kuwezesha familia kupiga hatua kuelekea malengo ya kimbigu.
Ø Idara hii hulenga watu wenye uhusiano
kwa kuhusika na mahitaji ya waliooa, wazazi na watoto, mahitaji ya kifamilia
kwa waseja na pia kwa wazazi wa upande mmoja (single parents).
Ø Pia idara hii hueneza tumaini na
kutoa msaada wa hali zote kwa wale ambao wamejeruhiwa na kuumizwa na dhuluma,
mmonyoko wa familia, kuvujika kwa mahusiano, n.k.
Ø Pia kwa upande mwingine hutoa ushauri
wa kukuza mahusiano na kutoa elimu ya kunufaisha maisha ya familia-katika
kujikwamua kimaisha.
Ø Ni kazi ya idara kufanya tathimini
kujua familia zenye mahitaji maalum ili idara iweze kuwakwamua, mf, kushindwa
kusomesha mtoto aliyefaulu kwa ajili ya uwezo mdogo, au mmoja wa wanafamilia
kuugua kwa muda mrefu na hivyo familia kuadhirika kiuchumi,n.k
Majukumu na wajibu wa kiongozi wa
familia
· Ni jukumu la kiongozi huyu kuona
familia zinaishi kwa amani na upendo hasa kwa kujenga familia zenye maadili ya
Kirstin a yenye kuishi kwa kufuata haki za msingi za mwandamu. Mfano/; watoto
waende shule, wawe na afya bora, kupiga ukadamizaji, n.k
· Kiongozi ni muhimu kutambua kaya
ngapi ambazo wazazi waliopo ndani ya kanisa wamefunga ndoa na pia kuhamasisha
wale wasio na ndoa kutengeneza ndoa zao.
· Kiongozi anaweza kuanda sabato maalum
kwa ajili ya kuendesha huduma za kaya na familia hata kwa kualika familia
ambzao sia za kiadvetista. Ni jambo la msingi kuwepo na sabato za wangeni
ambazo zitaendeshwa na idara hii kwa kuandaa mkufunzi mzuri wa mambo ya kaya na
familia.
kama kiongozi uapnge mambo
yafuatayo:-
· Kiongozi uwe na kamati madhubuti ya
kaya na familia itakayoratibu mahitaji makuu ya familai. Kamati hiyo ijumuishe
waseja, wanadoa, mzazi mmoja zu zaidi, na mwakilishi anayejumuisha makundi ya
rika mbalimbali kanisani.
· Andaa semina kwa kutumia miongozo kwa
wenzi kabla ya ndoa ili kusaidia na kujenga ndoa imara.
· Andaa semina zinazoimarisha ndoa
change na za muda mrefu ambazo zinakabiliana na wawimbi ya maisha.
· Toa mafuzo kwa wazazi namna ya uleaji
wa familia zao kwa mahusiano yenye mvuto wa kikristo.
· Toa mbinu mbalimbali namna mzazi
mmoja anavyoweza kukabiliana na changamoto za maisha na upweke na pia wale
ambao wanaishia na watoto wa kambo namna ya kuwatunza katika upendo wa kweli.
· Toa mafunzo kwa familia zetu kufanya
uinjilisti wa familia kwa familia. Mf. Chakula cha pamoja siku ya sabato au
ijumaa jioni. N.k
· Hakikisha nakusanya takwimu sahihi za
idadi ya familia ndani ya kanisa na pia jamii inayolizunguka kanisa ambao ni
walengwa wetu wa injili.
· Kukuza hali ya joto la ushirikiano,
ili kuleta maana ya “ufamilia” kanisani mwetu na robo ya ukombozi na wale
wanaohitaji msaada.
· Kuweka mikakati ya kuwa na vipindi
vya mchana au sabato maalumu ya kaya na familia ambayo itakuwa na shuhuda za
baadhi ya familia namna walivyopita maisha yao ili kuwatia nguvu ndoa changa
kuwa ndoa sio lelemama; hivyo wakaze mwendo.
J. IDARA YA UWAKILI NA MAENDELEO.
Idara
ya uwakili ilianzishwa kuwasaidia
washiriki wawewe kuwa mawakili dhabiti na kusaidia katika utekelezaji wa mpango
wa Mungu wa mfumo wa ukarimu wa kanisa lote. Jambo hili linajumuisha usimamizi
sahihi wa maisha yote, dhana za uwakili kuhimiza ungalizi na matumizi sahihi wa
hekalu la mwili, wakati, uwezo na mali. Hapo mwanzo idara idara hii ilijulikana
kama uwakili na maendeleo. Lakini kanuni za kanisa za mwaka 2005 na 2010
kipengele hicho kimeondolewa. Hivyo inajulikana kama idara ya uwakili.
Swala la
uwakili ni jambo nyeti na pan asana katika Nyanja zote za maisha ya mwanadamu.
Uwakili unahusu ujumla wa binadamu kwa maisha yake yote (wholesome or whole being).
Biblia inasema tuwe mawakili waamiinifu. Unaweza kuwa wakili lakini siyo wakili
mwaminifu.
Uwakili
katika tafsiri ya maisha ya mkristo ninajaribu kuigawa katika vipengele vikuu
vinne. Vipengele hivyo vitatu vinajulikana sana na kukubalika na wakristo wengi
lakini kimoja wapo baadhi wanakubali na wengine hawakubalikipengele hiki cha
mwili kuwa hekalu la mwili. Ijapokuwa kanuni za kanisa kinatambua kipengele
hiki cha hekalu la mwili. Kuwa na mojawapo ya swala la uwakili wa mwanadamu kwa
mungu wake. Vipengele hivyo ni kama ifuatavyo;-
1. Uwakili wa muda(wakati)
2. Uwakili wa mwili(miili)
3.
Uwakili wa talanta(vipawa/karama au
uwezo wetu)
4. Uwakili wa mali(amana au vyote
tunavyovimiliki).
Biblia inasema kuwa tunaweza kujiita mawakili, lakini wale watakaookolewa
ni wale ambao wamekuwa mawakili waaminifu wa kweli.paulo anasema hivi katika 1wakorintho 4:1,2 “mtu na na atuhesabu hivi, kuwa tu watumishi wa kirsto, na mawakili wa
siri za Mungu. Hapa tena inahitajiwa katika mawakili, ndiyo mtu aonekane kuwa
mwaninifu.”
Sifa za kiongozi wa uwakili
· Kingozi wa uwakili awe ni mtu ambaye
ni mfano bora kwa kanisa.
· Kiongozi wa kiroho
· Kiongozi anayetekeleza kanuni za
uwakili wa kikristo.
· Kiongozi anayepaswa awe na ufahamu wa
kiroho wa program za uwakili na za uwakili wa kifedha.
· Kiongozi awe tayari kutoa muda
unaohitajika kupanga, akuasisi, na kuongoza katika maeneo yaliyotengwa ya
majukumu kwa ushirikiano na mkurugenzi wa conference au fild.
Wajibu na majukumu ya
kiongozi au taratibu wa uwakili
· Katibu afundishe kanisani namna ya
kuwa mawakili kwa mali zao na namna ya kupanga bajeti zao kwa maendeleo ya
familia za.
· Kiongozi aelewe program za fedha zote
yaani sadaka zote namna zinavyotumika kisha wafundishe washiriki umuhimu wa
utoaji wa sadaka hizo.
· Kiongozi atumie dakiki zake 10 kwa siku
za sabato kuhamasisha swala la utoaji zaka na sadaka. Pia uwakili wa washiriki
katika kila jambo.
· Kujaza taarifa yake kila mwezi ili
itumwe kwa mkurugenzi wa uwakili field sambamba na taarifa ya mhazini.
· Kusimamia na kuendesha prgramu zote
za uwakili na uendeshaji wa majuma ya uamsho na semina mbalimbali juu ya
uwakili mf. Kualika ata wahubiri wazuri kwa maswala ya uwakili ili kuliamsha
kanisa katika uwakili.
Kamati ya uwakili ina wajumbe
wafuatao:-
1. Mwenyekiti
2. Katibu wa uwakili
3. Mhazini wa kanisa
4. Mzee wa kanisa
5. Shemasi mkuu wa kike na kiume
6. Karani wakanisa
7. Wajumbe wawili wa kuteuliwa- kutoka
kwa washiriki wa kanisa wa kawaida.
# idadi inaweza kuongezeka bali itatengemea ukubwa wa kanisa.
Majukumu ya kamati ya uwakili ni
haya:
1. Upangaji wa budget za kanisa.
2. Usimamizi wa bajeti ya knaisa kwa
maidara yote.
3. Uelimishaji wa maendeleo ya kanisa
katika Nyanja zote za maisha; hili ni pamoja na kutoa eleimu ya kujitegemea kwa
kuinua kipato cha washiriki na pia utambuaji wa karama.
4. Usimamizi wa uendeshaji wa taratibu za
vikao na shughuli za kanisa kuona kuwa unafuatwa kama ipasavyo; na kurekebisha
kama kuna kasoro yoyote kwa kingozi yoyote.
5. Kamati hii inapaswa kukutana kila
mwezi au muda watakaokubaliwa kulingana uzito wa majukumu ili kufanya tathimini
ya maendeleo ya kanisa lao.
K: IDARA YA MAMBO YA
UMMA NA UHURU WA DINI.
Kanisa linatambua
mamlaka zilizowekwa na wanadamu zote zimepita kibali kutoka kwa Mungu. Paulo anasema
katika WARUMI 13:1 wazi kuwa “kila mtu na aiitii mamlaka iliyo kuu; kwa maana
hakuna mamlaka isiyoyopo imeamriwa na Mungu.”lakini upande wa pili wa shilingi
ni kuwa dunia hii imejaa uovu wa kila namna .Uongozi wa dunia unaweza kupingana
na mungu ,hapo ndipo kama Kanisa tunapaswa kusimama chini ya bendera ya kristo
na kusema kuwa”Petro na mitume wakajibu, wakisema,Imetupasa kumtii Mungu kuliko
wanadamu.”MATENDO 5:29.
Wajibu na majukumu ya
idara hii.
· Kanisa la Mungu lingali bado
duniani;mahali ambapo dhuluma na ufisadi vinatawala.Hakuna hofu ya mambo ya
Mungu.Hivyo idara hii iko kanisani kwa lengo maalumu kutetea haki na maslahi ya
washiriki na Kanisa kwa ujumla.
· Hili linagusa swala la uhuru wa dini
kwa mkazo juu ya uhuru wa dhamili ya mtu binafsi. Uhuru wa dini hujumuisha
uhuru wake wa kuabudu,au kuchagua dini au kuchagua dini aipendayo;kubadili
imani yake pia kudhihirisha dini yake binafsi au katika jamii pamoja na waumini
wenzake katika ibada,kuadhimisha mambo ya dini,desturi,ushuhuda, na mafundisho
kulingana na heshima yake kwa haki za watu wengine.
· Idara hii katika swala la mambo ya
kuadhimisha inatetea haki ya siku ya kuabudu kwa waumini wake kama msingi wa
Biblia.Pia husimamia katika ufafanuzi wa matukio ya duniani ambayo yanaweza
kudhihirisha mambo ya unabii.Mf, Jumapili ni alama ya mnyama,papa ndiye mnyama
wa ufunuo 13 au pembe ndogo ya Danieli 7,n.k.
· Idara hii inasimamia haki za dini na
kutangaza imani yake na mafundisho yake wazi wazi pasipo kuingiliwa na serikali
kwa shinikizo la kundi la watu fulani ya watu wa imani nyingine.
· Ili kupata nguvu idara hii
inashirikiana na chama cha kimataifa cha kutetea Uhuru wa Dini na vyama shiriki
ulimwenguni kote.
zingatia hili lifuatalo:-Kila kanisa linachukuliwa kama chama cha kutetea Uhuru
wa Dini kisicho rasmi. Na kwa sababu hiyo kila mshiriki ni mwanachama wa chama
hicho.
o
Hivyo
mchungajiau mzee wa kanisa ni mwenyekiti wa chama katika kila kanisa
o
Kanisa
linaweza pia kuchangua mtu mwingine badala ya nafasi hizo hapo juu kutokana na
majukumu.lakini anapaswa awe ni mtu wenye mvuto na mwenye kufanya kazi karibu
sana na mchungaji. Anajulikana kwa jina la kiongozi wa chama cha kutetea uhuru
wa dini kanisani.
o
Kiongozi
huyu anapaswa awe na uhusiano na umma na mwenye kufahamu taratibu za nchi au
umma; na pia mwenye kudumisha uhuru wa watu wa Mungu ili waweze kutekeleza kazi
ya Mungu
Kazi na majukumu muhimu ya kiongozi
huyu:-
· Kukuza usambazaji wa magazeti
yanayotetea uhuru na makala mengine yanayotolewa au kukubaliana na kanisa
katika ulimwengu.
· Kutoa semina juu ya uhuru wa dini kwa washiriki. Hili ni
pamoja program, mikutano au makongamano yanayozungumzia uhuru wa dini.
· Kutetea wanafunzi wetu katika shule
ya vyuo wanapolazimishwa kufanya kinyume na uhuru wao wa kuabudi. K.m kufanya
mitihani au kusoma siku za sabato, au kutopewa ruhusa ya kuadhimisha desturi
zao kama vile makambi, n.k
· Kuliwezesha kanisa kufahamu taratibu
za nchi yao na haki zao za uraia kwa kufundisha katiba ya nchi, au kujua
maswala ya mirathi, uadikaji wa wosia, na mambo mbalimbali kama taratibu za
kisheria, n.k.
· Kiongozi huyu anatoa ushirikiano wa
karibu pale kanisa linapodhulumiwa mali zao au linapohitaji kuingia mikataba ya
kisheria kwa kutafuta vyombo husika katika ushughulikiaji mfano kupata mwanasheria mzuri.
L: IDARA YA
MAWASILIANO.
Idara hii ni mpya
katika makanisa mengi lakini ipo siku nyingi bila kueleweka vyema. Na kama
makanisa yagelifahamu kwa hakika, basi waadvetista wasabato tugekuwa na mtandao
wa mawasiliano ambao ungetufanya tuwe watu wanaokwenda na wakati siku zote(upto
date) kanisa ligefahamika vyema kwa waulimwengu kwa njia ya matangazo. Ukuaji
wa kanisa kwa nyakati hizi inatengemea sana idra ya mawasiliano namna
inavyotenda kazi yake ndani ya kanisa.
Wengine kwa kushindwa kuelewa idara
hii wamelaumu kanisa kwa kutumia mamilioni ya fedha kwa usambazaji wa injili
kwa mahubiri ya satellite. Nadhani watu hawa hawajawahi kusoma roho ya unabii
tunapaswa kutumia kila njia halali ili kufikisha nuru mbele za watu….. hebu
uchapishaji utumiwe na kila wakala wa utangazaji ambao watatangaza kazi za
injili utumiwe.”- 6 Tuk. 36. “njia za kuwezesha kufikia mioyo ya watu zibuniwe.
Baadhi ya mbinu zinazotumika katika kazi hii zitakuwa tofauti na mbinu
zilizotumiwa kazini katika siku za nyuma……….” Evangelism, uk.105.
Ø Idara hii inahusika katika
kuhamasisha kanisa kutumia Nyanja zote za mawasiliano katika kupashia habari
kwa kutangaza injili.
Ø Ni kazi ya idara hii kutoa habari za
program kwa jamii kwa njia ya matangazo yaliyoandaliwa vyema na kupimwa na
kamati ya mawasiliano ili kanisa lijulikane kwa jamii yote. Tangaza mambo
yanayotedwa na kanisa kwa njia ya mabango, redio, televisheni, magari, sticker,
vipeperushi, n.k mfano sabato za wageni, efoti, siku maalimu za vijana,
watafuta njia, n.k.
Ø Hivyo ili kila kanisa kutimiza agizo
la mbingu la utangazaji injili milele kwa njia ya kisasa, inapasa kila kanisa
kuchangua katibu wa mawasiliano na ikiwezekana na kamati ya mawasiliano.
Kamati ya mawasiliano ina wajumbe
wafuatao :-katibu wa mawasiliano kama mwenyekiti wake, na wajumbe ambao wana
ujuzi katika Nyanja za mawasiliano kama magazet, radio, televisheni , huduma ya masomo kwa njia ya posta na pia
vyombo vya mawasiliano ndani ya kanisa.
Mnaweza kumwalika mmoja wa wafanyakazi wa chombo kilicho karibu cha mawasiliano
cha kanisa kuwa pia mjumbe wa kamati.
Kazi ya katibu wa mawasiliano.
Ø Anahusika katika ukusanyaji na
usambazaji wa habari.
Ø Anapaswa kuwa karibu na wanahabari
ili kutoa habari sahihi za utendaji wa kanisa. Kwa kutoa mtangazo ya kanisa kwa
njia ya redio au magazeti kama vile mikutano, effort, kongamano, n.k pia
upokeaji wa habari sahihi.
Ø Anapaswa kuanzisha huduma za masomo
ya Biblia kwa njia ya posta.
Ø Anapaswa kuhimiza sadaka ya radio na
televisheni; na piakushiriki kugawa vijizuu vya redio na televisheni kwa na
masomo ya Biblia kwa njia ya posta.
Ø Utoaj wa taarifa za mipango ya
field/conference katika mikutano wa mashuri katika kanisa lake na namna ya
kutekeleza mipango hiyo.
Ø Kuhakikisha kanisa lake limeweka
kibao kinchotambulisha uwepo wa kanisa mahali hapo (sign board).
Ø Kuchukua matukio muhimu ya mikutano na shuhuda mbalimbali kwa
kuhifadhi kumbukumbu kwa njia ya kamera, maadishi kurekodi,n.k
· Upangaji
wa matukio yanayoangukia kalenda ya kanisa ulimwenguni kwa kumpatia taarifa
kiongozi wa idara husika juu ya tukio lake linalotokea
· Kupeleka
katika maktaba na vituo vingine vya habari, habari zinazohusu kanisa la
waadventista wasabato mf. Magazeti yetu, shughuli zetu, n.k
· Kuhamasisha
washiriki katika swalla la uandishi wa habari kwa kutuma katika magazeti yetu
kama maranatha, outlook, n.k.
· Kuratibu
program zote za mahubiri ya satellite kwa kutoa parameters na pia kutuma
shuhuda mbalimbali kwa kiongozi wa mawasiliano field.
· Utengenezaji
wa mabango mbalimbali yanayoeleza mada mbalimbali wakati wa semina maalumu za
kanisa au effort au mahubiri ya satellite na miamsho
M.
IDARA YA HUDUMA ZA WATOTO
Kanisa
la waadventista wasabato linathamini sana watoto na vijana kwani ndio nguzo ya
kanisa. Watoto wanapolelewa vema tunakuwa na kanisa bora la baadaye na umilele
wake. Idara ya huduma za watoto ipo ili kukuza Imani ya watoto toka kuzaliwa
hadi umri wa miaka kumi na nne
UTUME:
utume wa idara ya huduma za watoto ni kuwalea watoto katika uhusiano wa upendo
na utumishi pamoja na yesu.
Wajibu na majukumu ya
idara ya huduma za watoto
· Idara
hii ilianzishwa kanisani kwa makusudi ya kusaidia malezi ya watoto na pia
kusaidia kanisa kujua mahitaji ya msingi ya watoto kwa swala zima la ibada
kanisani
· Idara
inakusudia kuanzisha huduma nyingi zitakazowavuta watoto kwa yesu na kuwafanya
kuwa wanafunzi wake katika kazi zao za kila siku.
· Idara
hii inakuza Imani ya watoto wadogo kuanzia umri wa kuzaliwa mpaka anapofikia
umri wa miaka kumi na nne au na tano ili hatimaye aweze kujiunga katika kanisa
la Mungu.
· Idara
hii inafanya kazi kwa karibu sana na idara ya shule ya sabato kitengo cha
watoto na pia idara nyingine kama vile vijana, kaya na familia, wanawake, na
vyama mbalimbali kama watafuta njia, wavumbuzi, n.k.
· Idara
inapaswa kufanya kazi kama kitengo cha wainjilisti kwa kuwatumia watoto
kufikisha ujumbe kwa watoto wenzao na hatimaye kwa wazazi ambao si waumini wetu
na kupewa mafunzo mbalimbali wakati wa likizo
Wajibu
na majukumu ya kiongozi wa idara ya watoto
· Kiongozi
wa idara hii anapaswa kuhakikisha watoto wanapewa haki zao za kiibada badala ya
kuwaacha wakiwa wamezagaa huko nje wakati ibada ikiendelea kwa watu wazima.
Kiongozi anapaswa kwa kushirikiana na mashemasi kuona utulivu waibada kanisani
· Kiongozi
awasiliane na mchungaji au mzee waw kanisa kuona ibada ya watoto inafanyika
kila siku kwa kupewa wahudumu: kwa makanisa yasiyo na jengo basi muhubiri akumbushwe kona ya
watoto
· Kila
kanisa ambalo halina jengo yawapaswa kupanga wahubiri wawili kila juma. Wa
kwanza ataanza na watoto kwa dakika 7 hadi 10 kisha muhubiri mwingine
atamalizia muda uliosalia
· Kama
kiongozi weka mikakati kwa kushirikiana na mkuu wa majengo kupata jengo la
kuabudia watoto – kwa uendeshaji wa shule ya sabato ya watoto na ibada yao kuu.
· Kama
kiongozi washirikishe watoto kwwa kushirikiana na wazee wa kanisa kuona vipawa
vya watoto mapema na kuwapa majukumu yakanisa mapema ili waanze kulipenda
kanisa tangu utotoni. Mfano kuendesha shule ya sabato, kuhubiri siku zao
maalumu, program za mchana za watoto, n.k
· Kiongozi
afanye jitihada ya kuwaingiza watoto katika uinjilisti wangali bado wadogo.
Kuandaliwa efoti za wiki moja au sikua nane ambazo zitaendeshwa na watoto.
Mahubiri yao maalumu na miongozo ya kufundisha vipindi vya afya. Imegudulika
program hizi zimeleta wengi kanisani wakubwa kwa wadogo katika maeneo
zilipofanyika.
IDARA
YA MAJENGO YA KANISA
Hiki ni kitengo kilichomo ndani ya kanisa ambacho
kinahusika na ujenzi wa majengo ya kanisa. Kitengo hiki viongozi wake mara
nyingi wanatumika pale wanapohitajika
hususani kanisa linapokuwa na jengo tayari. Hivyo inaonekana umuhimu
wake haupo.
-kiongozi au mkuu wa majengo ya kanisa anachaguliwa wakati baraza la uchaguzi
au wakati wa baraza jipya la kanisa baada ya uchaguzi. Hili litatokana na umuhimu wa kiongozi huyu kwa kipindi
hicho.
· Kiongozi
huyu ataratibu mambo ya ujenzi wa
majengo ya kanisa akishirikiana na kamati yake ya ujenzi pamoja na baraza la
kanisa.
· Atawajibika
kusimamia ujenzi wa kanisa au majengo yote ya kanisa kama vile choo, ofisi na
kadhalika.
· Kiongozi
wa majengo atakuwa ni mtu ambaye anashauriana na kanisa kutafuata ramani
inayofaa nay a kupendeza kwa ujenzi wa majengo ya kanisa
· Kiongozi
huyu atashirikiana nakamati ya ujenzi kuhakikisha kuwa majengo yetu yanajengwa
katika viwango vinavyokubalika na kumtukuza Mungu
· Kiongozi
wa idara ya majengo atakuwa ni mwenyekiti wa kamati ya majengo ya kanisa
· Kiongozi
huyu ataleta bajeti ya jingo lolote kwa baraza la kanisa hatimaye kwa mkutano
wa kanisa
· Kongozi
wa majengo atahusika pia kutafuta viwanja vya kanisa na kuhakikishwa kuwa
vimepimwa na mamlaka husika ya kiserikali
· Kiongozi
ataratibu mipango ya upatikanaji wa fedha kwa ajili ya ujenzi au ununuzi wa viwanja
akishirikiana na idara nyingine katika swala la kupata ardhi kwa matumizi ya
kanisa.
· Wajumbe
wa kamati ya majengo mara nyingi inaundwa kulingana na busara ya kanisa
mahalia. Makanisa mengine yanakuwa na kamati kama ifuatavyo
a. Mkuu
wa majengo – mwenyekiti
b. Msaidizi
mkuu wa majengo – karani
c. Mchungaji
wa mtaa – mjumbe
d. Mzee
wa kanisa - mjumbe
e. Karani
wa kanisa – mjumbe
f. Mhazini
wa kanisa - mjumbe
g. Mashemasi
wakuu [kiume na kike]
h. Kiongozi
wa uwakili – mjumbe
i. Washiriki
wa uwakili – wajumbe
j. Wengineo
kwa busara za baraza la kanisa.
IDARA
YA UKAGUZI [AUDITOR]
Kitengo cha ukaguzi makanisa mengi sana wamepuuza
kumchagua kiongozi wake kwani anaonekana
kana kwamba sio mtu wa muhimu sana. Lakini kama kuna kitengo cha muhimu
sana na ambacho kinaweza kuwa na lawama nyingi sana wakati anapowajibika kwa
usahihi ni Mkaguzi wa kanisa
Mkaguzi anapochaguiwa ni mtu aliyesaidia kanisa
kutembea katika barabara iliyonyooka wakati wote. Mkaguzi wa kanisa anapokuwepo
ni jicho la kanisa kutazama utendaji bora wa kanisa. Kwani kila mmoja
anawajibika kwa uaminifu kuwa siku moja
atakaguliwa na taarifa yake itasomwa kwa wote waliomchagua
Sifa za mkaguzi wa kanisa
Awe ni mtu anayejua kutunza siri za watu hasa
anapokagua vitabu vya zaka na sadaka. Awe ni mtu mvumilivu na pia asiwe na
hasira kwani hatapendwa anapokagua na kutoa taarifa ya ukweli. Anaweza
kuchukiwa bila sababu ya kweli.
Asiwe mwepesi wa kuropoka ripoti yeyote
anayegunduakutoleta hali ya kukosa Imani kwa mhazini au kiongozi husika kwa
washiriki
Awe anajua kuandika na mahesabu vizuri ili kupitia
vitabu vya zaka na sadaka kwa usahihi Zaidi
Asiwe ni mjumbe wa baraza la kanisa ili awe nauwezo
wa kulikagua kwa uhuru
Awe ni mtu mwaminifu katika utendaji wake wa kazi.
Aliywe na hofu ya Mungu
Awe ni mtu asiye na chuki au kisasi kwa ajili ya
kutenda haki kwa wote.
Anapaswa awe na hekima na pia mwenye kushaurika na
mtu aliye mwanana na mplle (utii)
Anapaswa kutambua kuwa kitengo hiki cha muhimu kwani
kinalinda mali ya Bwana kwa wivu wa Bwana. Hivyo awe ni mzalendo kwa mali za
Mungu. Asiye muonea mungu haya yeyote yule
Asiwe ni mtu anayeridhiamaovu pia mwenye kuchukia
mapato ya udhalimu na aibu. Awe tayari kukemea maovu na roho ya kurekebisha
maovu
Majukumu
na wajibu wa mkaguzi wa kanisa
Kuhakiki na kukagua taarifa zote zinazohitajika
kutolewa kwa washiriki
Kusimamia na kudhibiti mali za Mungu zinazomilikiwa
na Kanisa mahalia ziweze kutumika vyema kama ilivyopitishwa na halmashauri ya
kanisa hilo
Kukagua fedha na matumizi yake kuendana na jinsi
ilivyopitishwa kwenye bajeti ya kanisa hilo
Kulijulisha kanisa usafi wa matumizi ya kanisa na michango mbalimbali inayotolewa na washiriki wa kanisa
hilio ili kujenga Imani kwa watoaji.
Kulisaidia baraza la kanisa kuona kuwa linaongoza
kanisa kulingana na mujibu wa kanuni na
taratibu za kanuni za kanisa hili. Ina maana mkaguzi anatakiwa kuangalia miniti
za vikao kuwa vinazingatia utaratibu wa kanisa
Kukagua mali za kanisa kama vile majengo, viti,
vitabu, vyombo vya meza ya bwana na ubatizo, vifaa vya mahubiri na kwaya, na
mali zote zinazomilikiwa na kanisa hilo kuwa vipo katika idadi ile ile kila mwaka
au kuna upotevu.
Mkaguzi atatoa ripoti yake kwa mchungaji ili
irekebishwe kabla ya kwenda kwa baraza
la kanisa kujadiliwa hatimaye ifae kwenda kusomwa kwa mashauri ya
kanisa.
Kumsaidia mhazini wa kanisa kuona kuwa mapato ya
kanisa kutoka makundini na matawini yanamfikia sawa. Na pia kumkumbusha namna
anavyogawa matumizi ya kanisa bila kuendelea kitengo chochote ama kuonea
kitengo mojawapo bila kujali bajeti ya kanisa.